Usahihi wa Historia Uislamu na Waislamu

Kimeandikwa na : Sayed Ali Asgher Razwy


YALIYOMO

Kuhusu Mwandishi. 2

Utangulizi . 4

Jografia ya Arabuni. 12

Ikolojia (uhusiano wa viumbe na mazingira) ya Arabia. 17

Arabia kabla ya Uislamu...19

Hali ya Ustawi wa Jamii ..24

Hali ya dini katika Arabia ya kabla ya Uislamu..26

Elimu miongoni mwa Waarabu kabla ya Uislamu.28

Hashim kabla ya kuzaliwa Uislamu ..32

Kuzaliwa kwa Muhammad na miaka ya mwanzo ya uhai wake...36

 

Ndoa ya Muhammad Mustafa na Khadij a ...40

Kuzaliwa kwa Ali Ibn Abi Talib....42

Kabla tu ya Tangazo la Ujumbe wake..46

Kuzaliwa kwa Uislamu..48

Waliosilimu mwanzoni na mateso kutoka kwa wapagani...60

Hijra mbili za Waislamu kwenda Abyssinia ( A.D.D. 615 - 616 )...73

Hamza aukubali Uislamu - A.D. 615...76

Kusilimu kwa Umar- A.D. 616 ...79

Kususiwa kiuchumi na kijamii kwa Bani Hashim.84

Vifo vya Khadija na Abu Talib - 616A.D...94

Safari ya Muhammad kwenda Taif..99

Maeneo Mapya ya Uislamu..103

Hajira (Kuhama)...105

Mwaka wa kwanza wa Hijiria .112

Vita vya Kiislamu ....124

Mwaka wa pili wa Hijiria.126

Vita vya Badr ....128

 

 

Ndoa ya Fatima Zahra na Ali Ibn Abi Talib..137Vita vya Uhud .. 141

Kuzaliwa kwa Hasan na Husein ...157

Vita vya Khandaq.160

Waislamu na Wayahudi..168

Mkataba wa Hudaybiyya.171

Ushindi wa Khaybar....183

Vita vya Mu'utah..197

Mapambano ya Dhat es - Salasil.205

Kutekwa kwa Makka..208

Vita vya Hunain.226

Vita vya Tabuk...238

Kutangazwa kwa Surat Bara'ah (At- Taubah)..242

Msafara wa mwisho....249

Hija ya Muago...251

Jeshi la Usamah.268

Abu Bakr kama Kiongozi katika Swala.277

Wosia Usioandikwa wa Mtume wa Allah (s.a.w.)..282

Wake zake Muhammad (s.a.w.) Mtume wa Allah (s.w.t)..288

Kifo cha Muhammad (s.a.w.) Mtume wa Allah 295.295

 

 

Hisia za Familia na za masahaba wa Muhammad Mustafa (s.a.w.)

Juu ya kofo chake....306

Kifo cha Muhammad Mustafa (s.a.w.) na Umma wake...308Muhammad Mustafa (s.a.w) na Urithi wake..309

Nadharia ya Kisunni juu ya Serikali .319

Kugombea madaraka (1).327

Kugombea madaraka (2).334

Kugombea madaraka (3).337

Kugombea madaraka (4).346

Tahakiki ya Saqifah....352

Saqifah na mantiki ya Historia ...364

Saad Ibn Ubadah, Ansari - Mgombea wa Ukhalifa..387

Abu Bakr; Khalifa wa kwanza wa Waislamu.389

Matukio Muhimu ya Ukhalifa wa Abu Bakr..392

Demokrasia na Waislamu..414

Umar bin al-Khattab, Khalifa a pili wa Waislamu.419

Uthmani Khalifa wa Tatu wa Waislam .. 455

 

 

Ali Ibn Talib, Khalifa wanne wa Waislam.506Utangulizi wa Vita.529

Vita vya Basra (Vita vya ngamia)..540

Kubadilisha Makao Makuu kutoka

Madina kwenda Kufa..569

Ufufukaji wa Bani Umayyah .579

Vita vya Siffin. 600

Kuuawa kwa Ali ..628

Baadhi ya yaliyoakisi katika Ukhalifa wa Ali..634

Sera ya Ali (a.s.), ya Ndani na ya Nje ...636

Ali (a.s) kama Mjumbe wa Amani ..648

Ali na mifano bora ya Uhuru na Fursa... 658

Orodha ya "Watu wa kwanza" katika Uislamu...663

"Mgawanyo wa lazima" wa Uislamu..667

Mihanga ya Muhammad kwa ajili ya Uislamu...672

Kushindwa kukubwa kwa Abu Bakr na Umar ...675

Ni nani aliyeandika historia ya Uislamu na vipi?..682
 

 


 

The .HTML version of this book is taken from
www.al-islam.org and ebooked by www.ShiaLibrary.com and www.islamkutuphanesi.com . May Allah be pleased with all.


 

Kimetarjumiwa na : Al-Akh Ramadhan Kanju Shemahimbo

P. O. Box 19701 Dar-es-Salaam

©Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 9987-427-20-0

Kimeandikwa na: Sayed Ali Asgher Razwy

Kimetarjumiwa na: Ramadhani Kanju Shemahimbo

P.O. Box 19701, Dar es Salaam/Tanzania.

Kimehaririwa na: Dr. M. S. Kanju

na Ustadh Abdallah Mohamed

Email: mokanju2000@yahoo.com

P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania

Simu: +255 22 2110640

Kupangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab.

Toleo la kwanza: Novemba 2005 Nakala:1000

Kimetolewa na kuchapishwa na: AFItrah Foundation

PO Box 19701, Daressalaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Fax: +255 22 2113107 Email: info@alitrah.org Website: www.alitrah.org

NENO LA MCHAPISHAJI USAHIHI WA HISTORIA YA UISLAMU

Hii ni historia ya vuguvugu la Uislamu ambalo lilianzishwa na Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) mnamo mwaka 610 A.D. huko Makka, na kuendelea alipohamia Madina mpaka alipofarika. Inahusisha kipindi cha miaka tisini kuanzia 570 A.D. wakati yeye Muhammad alipozaliwa huko Makka, hadi mwaka 661 wakati mrithi wake, Ali ibn Abi Talib, alipouawa huko mjini Kufah.

Historia zisizo na idadi zimeandikwa huko nyuma na zitaandikwa wakati ujao. Maendeleo ya kuvutia ya Uislamu katika nyanja ya ulinganiaji katika nyakati zetu wenyewe; kufufu-ka upya kwa mataifa ya Kiislamu baada ya karne nyingi za usingizi mzito; kujidukiza kwa mafuta kama wakala mpya katika siasa za kidunia katika karne hii; bali juu ya yote na hivi karibuni kabisa, yale mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu ndani ya Iran, yote haya yanakuwa, kote Mashariki na Magharibi, kama vichocheo vya shauku mpya katika Uislamu. Mapinduzi ndani ya Iran yamechokonoa mlipuko wa dunia nzima wa mvuto katika Uislamu, na vitabu vingi vipya vinaandikwa juu ya somo hilo - na wote, Waislamu na wasiokuwa Waislamu.

Hili tena ni jaribio letu kubwa la kutoa kitabu kikubwa kinachohusu historia ya Uislamu na waislamu kwa luhga ya Kiswahili. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwon-go, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu.

Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

Tunamshukuru ndugu yetu, Al-Akh Ramadhani Kanju Shemahimbo kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu katika dini.

Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam.

 

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

KUHUSU MWANDISHI

Sayyed Ali Asghar Razwy (1925-1996)

Marehemu Seyyid Ali Asghar Razwy anakumbukwa sana kama mwanachuoni wa Kiislamu mwenye maneno mazuri, ambaye haiba yake njema na moyo wa uchangamfu vililmpendezesha kwa wote waliokuwa na bahati nzuri ya kukutana naye. Wakati wote wale waliozungumza naye waliondoka wakiwa wameathirika sana kifikra, wakiwa wame-jifunza kitu kutoka kwa mtaalamu huyu mwenye mvuto.

Seyyid Ali Asghar alizaliwa huko Simla, India mnamo mwaka 1925. Baba yake, Agha Seyyid Muhammad Shah alikuwa amehamia hapo zamani kutoka Baluchistan. Agha Seyyid Muhammad Shah alikuwa, yeye mwenyewe ni Aalim, aliyepata elimu yake huko Najaf na Qum, na alikuwa ndiye mwakilishi wa Marehemu Ayatullah Seyyid Abul Hassan Al-Isfahani (R.A.).

Seyyid Ali Asghar Razwy alijiunga katika utumishi wa serikali ya India mara baada ya kuhitimu Shahada ya B.A. Hons kutoka Chuo Kikuu cha Kashmir. Baadaye alishiriki kikamilifu katika vuguvugu la kuunda Pakistani na mwishowe akahamia Pakistani ambako alijiunga na Idara ya mambo ya nje.

Mnamo mwaka 1950, alikwenda Washington D.C. kama mjumbe wa ujumbe wa Kibalozi wa Pakistani. Mnamo mwaka 1954, alihamishiwa Kabul na mwaka mmoja baadaye Seyyid Ali Asghar akahamia Canada na halafu Marekani mnamo mwaka 1960 ambako alifanya kazi na shirika moja la kibiashara.

Akiwa mfanyakazi wa huduma za kijamii, alijiunga na The Muslim World League na kwa miaka mingi akawa ni chimbuko la uongozi kwa iliyokuwa jumuiya changa ya Kishia katika Marekani ya Kaskazini. Anayo sifa ya kipekee ya kuwa mzungumzaji wa kwanza, katika Marekani ya Kaskazini, kuhutubia jamaa ya waumini kwa Kiingereza.

Miongoni mwa kazi zake za maandishi za awali ni wasifu - The Biograpy of Seyyidati Khadijatul-Kubra na Salman Far si. Seyyid Ali Asghar pia aliandika idadi ya vijitabu na majarida ya kidini juu ya mada mbalimbali. Muswada huu wenye sifa daima, A Restatement of The History of Islam and Muslims ulikubaliwa kuchapishwa (kama kitabu) na Mulla Asgharali M. M. Jaffer, aliyekuwa Raisi wa The World Federation mnamo Julai, mwaka 1996.

2

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kwa kuchapishwa kwa kitabu hiki, ambacho Marehemu alikifanyia kazi kwa kipindi cha miongo ya miaka, miezi minane tu baada ya kifo chake cha kuhuzunisha, mnamo Septemba, 15, mwaka 1996 kwenye hospitali ya Calvalry huko New York, yeye ameacha urithi wa kudumu wa maarifa na elimu yake na hivyo kujihakikishia mwenyewe thawab-l 'jari - thawabu zenye kuendelea

Wasomaji wanaombwa kusoma Surat al-Fatiha kwa ajili ya kumbukumbu yake.

3

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

UTANGULIZI

HII NI HISTORIA MPYA YA UISLAMU. Ni historia ya vuguvugu la Uislamu ambalo lilianzishwa na Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) mnamo mwaka 610 A.D. huko Makka, na ulikamilishwa kwa msaada wa binamu yake, mshiriki na mshikamakamu wake, Ali ibn Abi Talib, mnamo mwaka 632 A.D. hapo Madina. Inahusisha kipindi cha miaka tisini kuanzia 570 A.D. wakati yeye Muhammad alipozaliwa huko Makka, hadi mwaka 661 wakati mrithi wake, Ali ibn Abi Talib, alipouawa huko mjini Kufah.

Historia zisizo na idadi zimeandikwa huko nyuma na zitaandikwa wakati ujao. Maendeleo ya kuvutia ya Uislamu katika nyanja ya ulinganiaji katika nyakati zetu wenyewe; kufufu-ka upya kwa mataifa ya Kiislamu baada ya karne nyingi za usingizi mzito; kujidukiza kwa mafuta kama wakala mpya katika siasa za kidunia katika karne hii; bali juu ya yote na hivi karibuni kabisa, yale mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu ndani ya Iran, yote Haya yanakuwa, kote Mashariki na Magharibi, kama vichocheo vya shauku mpya katika Uislamu. Mapinduzi ndani ya Iran yamechokonoa mlipuko wa dunia nzima wa mvuto katika Uislamu, na vitabu vingi vipya vinaandikwa juu ya somo hilo - na wote, Waislamu na wasiokuwa Waislamu.

Siku hizi wakati viongozi wa dunia ya Kikristo wanapofanya kazi kimyakimya ili kufanik-isha ndoto ya siku nyingi ya imani ya umoja wa Kikristo, Waislamu wengi pia wanaangalia nyuma kwa hamu kubwa kwenye lile taifa bora wakati Uislamu ulipokuwa mfumo wa mawazo ya aina moja. Uislam, hata hivyo, ulikuwa mfumo wa mawazo ya aina moja tu wakati wa uhai wa Mtume wake, Muhammad aliyebarikiwa. Mara tu alipofariki, ufa wa kwanza ulijitokeza katika ile "nguzo imara" ya Uislamu. Wafuasi wake - Waislamu -walikingamizwa kwenye makundi mawili. Katika kingamizo hili, wengi wa maswahaba zake walikuwa upande mmoja na watu wa nyumbani kwake kwa upande mwingine. Wakati watu wa nyumbani kwake wakiwa wameshughulishwa na mazishi yake, baadhi ya maswahaba zake walishughulika katika "kuchagua" kiongozi mpya wa kumrithi Mtume.

Katika ule mwanya kati ya kifo na mazishi yake, hili kundi la mwisho (la maswahaba) lil-ijikusanya katika banda la Saqifah hapo Madina, na likamchagua mmoja kati yao wenyewe kama mkuu mpya wa umma wa Waislamu. Wao, kisha wakawakabili watu wa ile familia iliyoondokewa kwa jambo lililokwisha fanywa na kuthibitishwa. Mkabiliano huu, kwa bahati mbaya sana, ukawa Sura ya kudumu ya historia ya Waislamu.

Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t,), Rehma na amani juu yake na juu ya Ahlul-Bayt wake, alitokana na ukoo wa Bani Hashim. Baada ya kifo chake mwaka632 A.D., binamu

4

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

yake, mkwe wake na mrithi mstahiki wake, Ali ibn Abi Talib, alimfuatia yeye kama mkuu mpya wa Bani Hashim. Wengi wa maswahaba wa Muhammad, Mtume wa Uislamu, walikuwa wamelea uadui wa siri juu yake. Hawakuweza kumuonyesha uadui wao wakati wa uhai wake Mtume lakini mara walipokuwa na amri juu ya serikali yake hapo Madina, walikuwa wameazimia, kutoiachia, kwa kukosea kwa namna yoyote ile, iangukie kwenye mikono ya Ali ibn Abi Talib. Watu wa nyumba ya Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) hivyo walizuiwa, kwa nguvu kubwa ya wanadamu, sio tu kwenye urithi wa moja kwa moja bali pia kwenye nafasi zote za mamlaka na madaraka katika serikali za wafuasi wake zilizofuatia.

Marafiki, wafuasi na wanaounga mkono nyumba ya Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.w.t.) wamekuwa kihistoria wakiitwa Shia; na marafiki, wafuasi na wanaowaunga mkono maswahaba, yaani, lile kundi lililofanikiwa kutwaa madaraka hapo Madina, limekuwa likiitwa Sunni. Nitayatofautisha pia makundi haya mawili kwa majina haya.

M. Shibli, mwanahistoria mashuhuri wa Kihindi wa Uislamu, anasema kwamba takriban historia zote za Uislamu zimeandikwa na wanahistoria wa Sunni. Kauli hii inamaanisha kwamba wanazuoni wa Shia hawakuandika historia yoyote ya Uislamu. Kwa nini hawakuandika? Hawakuandika historia kwa sababu ya wazi. Makhalifa wote, masultani na wafalme, wote walikuwa Sunni. Aliyekuwa Shia hakuweza kuchapisha ufafanuzi wa historia ya Kiislamu ambao ulikuwa unatofautiana na ule ufafanuzi wa kiserikali, na hakuwa na haja ya kuendeleza kile alichoamini kuwa ni upotoshaji wa ukweli. Yeye, kwa hiyo, aliamua kutoandika historia yoyote kabisa.

Kwa namna hii, yalikuwa ni yale "maelezo" ya kiserikali ya historia ya siku za mwanzo za Uislamu ambayo yalipata kuenea na yakapata kukubalika. Lilikuwa ni jambo la kimantiki kabisa la kufanya kwa serikali za karne za mwanzoni za Uislamu kuingiza kwenye mzun-guko, ile hekaya tu, ambayo ilikuwa inakubaliana na itikadi ya kundi lao. Ilikuwa pia na mantiki kabisa kwa wafuasi wa sera za serikali hizo tunazozizungumzia, kutii itikadi hiyo. Na katika kutii itikadi hiyo ya kundi, kama walihisi kwamba ni muhimu kufunika ukweli, au kwa kiwango chochote, kufunika ule upande mwingine wa Hadith hiyo, ilikuwa na mantiki kabisa kufanya hivyo.

Hakuna jambo lolote la ajabu, la kushangaza au kushitusha katika mwenendo wa wanahistoria wa Sunni. Kitu chenye mantiki kabisa kwao kukifanya kilikuwa, na bado ni, kutetea uhalali wa matukio ambayo yalitukia ndani ya Saqifah, ambamo baadhi ya maswahaba, katika shambulizi la kuwahi kabla ya wengine, walitwaa serikali ya Muhammad, kiongozi wa Arabia.

Kile ambacho hata hivyo ni cha kushangaza na cha kushitusha, ni kwamba wanahistoria wa kimagharibi, yaani, wale Mustashriq, wamemeza, kama jambo la kweli kabisa, kila

5

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ambalo wanahistoria wa "baraza" la Kiislamu limewachotea wao kama "ukweli." Hawa Mustashriq wanadhaniwa kwamba hawana upendeleo, sio wafuasi, na wasiohusika kwa jazba kwa hali yoyote ile. Matokeo ya mashindano fulani katika zama za kale za Uislamu, kwa njia moja au nyingine, yasingeweza kuleta tofauti yoyote kwao. Na bado, vitabu vya wengi wao vinaonyesha, sio ukweli bali ufafanuzi na propaganda za kundi lililokuwa madarakani. Kwa maana hii, kazi zao ni uigaji wa vile vitabu "vilivyotiwa msukumo" na kile Wakomunisti wanachokiita "jamii inayotawala" ya Waislamu.

Vitabu vya Mustashriq vinaweza kuwa na maana ya kisayansi tu kama watachukua ushau-ri wa mwanahistoria mashuhuri wa Hispania ya Kiislamu, Dr. J. A. Conde. Yeye anasema: "Namna ya msiba unaojiingiza wenyewe kwenye mambo ya wanadamu unaweza kuelekea kudai kwamba katika uhusiano wa matukio ya kihistoria, yale yenye umuhimu wa hali ya juu kabisa, yashuke kuvifikia vizazi vijavyo kupitia kwenye njia zinazotiliwa mashaka kwa haki kabisa, za simulizi zilizoandikwa na makundi yanayoshinda. Mabadiliko ya falme, mapinduzi ya maana kabisa na kuangushwa kwa falme maarufu za kiukoo yote hay a yanaelekea kuwajibika na kasoro hii.

Ilikuwa ni kutokana na Warumi kwamba historia ya kujitwalia kwao wenyewe iliandikwa; simulizi za upinzani wao na vita vya umwagaji damu dhidi ya wa-Carthaginia zimetufikia sisi kutoka kwao wenyewe; au kama waandishi wa Kigiriki nao pia wamelijadili suala hili, watu hawa walikuwa ni walipa kodi na wategemezi wa Roma, wala hawakuzificha zile sifa zisizostahili zilizokusudiwa kuunga mkono fadhila yake. Scipio kwa hiyo anaonekana kwetu kama mtu anayevutia sana kati ya mashujaa, lakini je, sio kwamba kwa kiasi fulani hivi, ni kwa sababu historia ya maisha yake ni kazi ya mashabiki na wasifiaji wake?

Ni kweli kwamba yule Hannibal mwenye daraja kubwa na maarufu hawezi kuonekana vinginevyo zaidi ya mashuhuri na kwenye heshima hata katika masimulizi ya maadui zake wabAya kabisa, lakini kama ile chuki isiyotulizika na sera za uchokozi za Roma zisingeamuru kuteketezwa kwa zile kumbukumbu za kisaliti (za wa-Carthaginia), jenerali huyu maarufu bila shaka angetokezea kwetu kwa sifa inay-otofautiana sana na ile iliyowasilishwa na yule mshenzi katili, aliye elezewa na Livy na kukubaliwa na wasomaji wake kama ndio taswira ya Hannibal.

Kwa hiyo utambuzi thabiti na wa haki unatukataza sisi kutosheka wenyewe na ushahidi wa upande mmoja tu. Hii inahitaji kwamba tulinganishe mahusiano ya makundi yote kwa uadilifu makini, na inatutaka sisi kuyaonyesha bila ya lengo jingine zaidi ya lile la kuugundua ukweli."

(History of the Dominion of the Arabs in Spain - kilichotafsiriwa kutoka kwenye ki-Hispania na Mrs. J. Foster, Juz. I, uk. 1)

 

6

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Haiwezi kupingika kwamba Mustashriq wengi wametoa michango isiyofaa kabisa kwenye uchunguzi, elimu na ufahamu wa Uislamu. Ni kutokana tu na jitihada zao kwamba hazina nyingi zisizo na thamani, za historia, fani na fasihi za Kiislamu zimeokolewa kutokana na kusahaulika, na zimekuwa zimehifadhiwa. Inawezekana kabisa kwamba hazina nyingi kama hizo zingeweza kupotea daima kama isingekuwa kwa juhudi zao za kuziokoa. Miongoni mwao kuna watu ambao wana ufahamu wa kushangaza wa kina wa mafunzo ya Kiislamu, na ambao elimu zao ni za ki-ensaiklopidia kwa upana. Wamesoma na kupata viwango vikubwa vya maelezo, na kisha wameyafupisha, wakayapanga na kuyahariri kati-ka uchambuzi wa kistadi na wa ukosoaji. Wengine wao wamejitolea maisha yao na mali zao kwenye uchunguzi wa Uislamu, na k wao wao ulimwengu wa Kiislamu una deni kubwa la shukurani.

Lakini licha ya mapenzi na hamu ya elimu, na kujifunga kwenye ukweli kwa wanafunzi wa Magharibi, inaonekana kwamba wakati wengi wao wanapoufafanua Uislamu, historia yake na sheria zake, jambo fulani huenda kombo. Ni vigumu kuamini lakini ni kweli kwamba baadhi yao wanaonyesha kushindwa kwa ajabu kupenyeza kwenye mwonekano wa kawaida na usiobadilika wa matukio kwenye mambo na nguvu, na ukweli ulio dhahiri ambavyo wakati mwingine vimefichwa kwa makusudi. Na baadhi yao wanashindwa hata kuona yaliyo dhahiri.

Nimenukuu hapo juu utaratibu wa kuandika historia ya kisa yansi na isiyo na upendeleo kama ulivyoelezwa na Dr. J. A. Conde, ambaye yeye mwenyewe ni Mustashriq maarufu sana. Kanuni hii, yaani ile ya, hakuna ubigwa wa hukumu na maamuzi katika historia, inat-ulia katika akili ya kwaida, na hauna kitu cha ajabu juu yake. Na bado, wengi wa Mustashriq wameyakubali, kwa wepesi wa kusadiki ambao ni wa kipumbavu, yale maelezo ya matukio yaliyotokea punde tu kufuatia kifo cha Muhammad (s.a.w.), kama yalivy-otolewa na lile kundi lililofanikiwa katika kujitwalia lenyewe utawala wake (Muhammad s.a.w.).

Mfano wa dhahiri wa uzuzu huo, na msingi wa kutotambua wa hawa Mustashriq, kuhusu suala hili, ni kule kukubaliwa na wao, kama "ukweli" wa kihistoria wa ile taarifa ya uwon-go kwamba Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) alifariki bila ya kumteua mtu yeyote kama mrithi wake, na kwamba aliliacha suala la kumtafuta kiongozi wa umma wa Waislamu kwenye hiari ya wafuasi wake wenyewe.

Hakuna Mustashriq aliyesita na kufikiria, kwa kiasi ninavyotambua mimi, ili kuchunguza kama hili ni kweli au kama ni lenye uwezekano wa kuwa kweli kwamba Muhammad ali-watelekeza Waislamu bila ya kiongozi, na ikawabidi kumpata kiongozi katika mfumo usio na mipaka na unaoruhusu kila mbinu, wa kikatili, huru kwa wote na kushindana kwa ajili ya madaraka. Ili kuepukana na kazi ngumu ya kutafuta ukweli, Mustashriq wamekubaliana tu na wanahistoria wa Sunni kwamba Muhammad, Mtume wa Uislamu, hakuwa na chaguo

7

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

au upendeleo katika suala la urithi wake mwenyewe; na lolote lililotokea ndani ya Saqifah kwa hiyo, lilikuwa ni sawa na halali, na pia lilikuwa kwa faida kubwa ya umma wa Waislamu.

Huu muegemeo wa uungaji mkono Saqifah wa Mustashriq umewaingiza kwenye njia ya upofu ambamo hawawezi kupata majibu ya maswali ya msingi katika historia ya Uislamu, na wanajikuta wenyewe wamenasa, kama walivyonasa wanahistoria wa Sunni, kwenye nyavu za ukweli wenye mashaka na hitilafu nyingi.

Wanahistoria wengi wa Sunni na wengi miongoni mwa Mustashriq wamefanya majaribio ya makusudi ya kuipunguza nafasi iliyochukuliwa na Ali ibn Abi Talib katika historia ya Uislamu. Wao, bila shaka, wanastahiki kwenye maoni na dhana zao hata kama hizi hazikuthibitishwa na ukweli. Katika uwasilishaji wangu, nimejitahidi kuweka mkazo juu ya ukweli. Kwa kufanya hivyo, imekuwa ni matumaini yangu kwamba ukweli wenyewe utachukua nafasi kama "muamuzi." Kwa vile ukweli ni "muamuzi" asiyekuwa na upendeleo, anaweza kutegemewa kurudisha uwiano kwenye uchambuzi wa nafasi zili-zochukuliwa na wahusika wakuu katika historia ya Uislamu mchanga. Nimeuchagua (ukweli) na nimeutunga pamoja, kama lulu, kwenye "mkufu", ili kwamba wingi wa ukweli huo uweze kuonekana mahali pamoja.

Historia haina mahakama ya juu inayotoa fatwa; inao waandika tarikh tu, wenye kuweza kukosea. Na bado, historia inaweza kupata mahakama yake ya juu yenyewe au mahakama isiyopendelea, kwenye mantiki ya ukweli.

Ninayo sababu nyingine na ya mawazo yakinifu ya kutegemea juu ya ukweli. Kwa kuandi-ka Hadith ya siku za mwanzoni za Uislamu, vipo vyanzo vikuu vitatu, navyo ni, Qur'an Tukufu (kitabu cha Uislamu kilichoteremshwa); Hadithi (kumbukumbu za matendo na maneno matukufu ya Muhammad, kama yalivyosimuliwa kwa sanad ya watoa habari au wasimulizi); na matukio kama yalivyoandikwa na wanahistoria wa Kiarabu. Kati ya vitatu hivi, kile cha kwanza, yaani, Qur'an, inakubaliwa na Waislamu wote kuwa ni takatifu kiasili. Kama mwislamu anapinga maandiko ya Qur'an, papo hapo anakuwa kafiri. Lakini wakati ambapo maandikoko ya Qur'an, kwa kadiri Waislamu wanavyohusika, Hayakuvunjwa, Aya zake ni zenye kupatwa mara kwa mara na hitilafu na wakati mwingine (na) tafsiri zinazopingana, na hakuna kitu kama makubaliano ambamo, au ambayo tafsiri zake ni sawasawa. Hadithi vilevile zinapatwa na kikwazo; nyingi sana kati ya hizo ni za bandia ingawa kuna baadhi ambazo zinakubaliwa na wote, Sunni na Shia kuwa ni sahihi. Nimejaribu kwa hiyo, kuwa mchaguzi katika kuzidondoa zile Aya tu za Qur'an na zile Hadithi (maneno ya Mtume) zenye maelezo ambayo tofauti kati ya Sunni na Shia ni ndogo sana. Lakini ukweli wa kihistoria ni eneo ambamo hakuna nafasi kubwa ya mfarakano. Nimefanya udondozi wa mara kwa mara sana, kutoka kote, kwa wanahistoria wa zamani na wa kisasa, katika kitabu hiki, mara nyingi juu ya suala au tukio hilohilo. Nimefanya

8

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

hivyo ili kuwasilisha kwa msomaji zaidi ya hoja moja ya maoni au tafsiri zaidi ya moja ya matukio yenye umuhimu zaidi. Tukio hilohilo likiangaliwa kwa mitazamo tofauti huonekana tofauti kwa watazamaji mbalimbali na kwa hiyo, ni yenye kupatwa na tafsiri mbali mbali. Ni katika matumaini kwamba msomaji atashiriki katika maoni Haya ambayo nimejaribu, kwenye matukio mengi, kuacha zaidi ya mwanahistoria mmoja kuelezea kisa hicho hicho. "Wacha wataalamu waifanye kazi hiyo," umekuwa ndio wito wangu katika kutafsiri upya mambo muhimu ya historia ya Uislamu.

Sababu nyingine ya kwa nini nimewasilisha ushahidi wa wanahistoria kwa kiwango kikub-wa hivyo, ni kutegemeza tasnifu yangu na ushahidi, kiasi kwamba msomaji, kama akipen-da, aweze kurejea kwenye vyanzo ambavyo anaweza kuviona kama ni vya kuaminika kabisa.

Imesemekana kwamba kujasiri, kama kulivyo, katika kuchunguza yale yasiyojulikana, kupita kiasi, ni kutilia shaka yanayojulikana. Mengi ya yale yanayoitwa "mambo yanay-ofahamika" katika historia ya Uislam mchanga, ni dhana hasa za uchamungu au hata matakwa ya uchamungu ambayo kutokana na kung'ang'ania kurudiwa rudiwa na mlolon-go mrefu wa vizazi vya Waislamu, yamepata "mng'ao kama sio hadhi ya "masharti ya imani". Nilipozihoji baadhi ya dhana za Waislamu nyingi ambazo zinatambulika kama "ukweli" wa kihistoria, niligundua kwamba haziwezi kuhimili uchunguzi makini wa uchambuzi wa kukosoa. Msomaji mwenyewe anaweza kwa hiyo, kuamua kama atazishik-ilia hizo au atakubali ukweli ambao baadhi yake atauona ni mchungu sana na mkali. Kuna wale watu ambao huwa wanauogopa ukweli. Ukweli unatishia njozi zao, visa vyao wanavyopendelea, na dhana zao. Hivi (vilivyotajwa) vya mwisho, kutokana na ufananaji (wa mawazo) wa siku nyingi, vimezoeleka sana kwao kiasi kwamba wanahisi ni salama na vinatosha kuishi navyo bila ya "udukizi" wa ukweli. Wanalinganisha ukweli na "ukosefu wa usalama."

Hata hivyo, ukweli pekee ndio unaoweza kuwaletea wao usalama wa kweli. Ukweli ni laz-ima utetewe kwa gharama yoyoye ile, na watu wote, lakini hususan na wanahistoria. Ukweli lazima ukubaliwe hata kama unamuumiza rafiki na kumnufaisha adui. Uaminifu wa kwanza wa mwanahistoria lazima uwe ni ukweli, na lolote lile liwalo lazima lisimpo-toshe katika kuutafuta huo ukweli.

Vita vya mawazo na mgongano wa maoni unakuwa wa kuvutia sana pale ambapo mwenge wa uchunguzi unapogeuziwa mbali kutoka kwenye dhana za kifalsafa na itikadi dhahania za kisiasa kwenda kwenye tabia na mienendo ya (watu) shaksia ambayo ilifanya kazi muhimu katika matukio ambayo tunayachunguza. Historia huchimbuka kwenye uhai na uumbaji wa mhusika; inakuwa yenye kutikisika pamoja na watu wa kusawarika ambao "hufanya" matukio au kuyashughulikia au kuyapinga. (Wanaipamba) wanaiwekeza historia pamoja na elementi za "maslahi ya wanadamu", na mguso wa mfululizo wa mambo.

9

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Vyovyote vile historia iwavyo - ajali au vifo visivyozuilika, au shinikizo la hali ya maa-muzi ya kiuchumi, au vitendo vya viongozi wenye nguvu, au matokeo ya nguvu ambazo hakuna anayezijua, au matumaini ya pamoja ya watu - vyovyote historia iwavyo, Waarabu wenyewe wanaiona na kuitafsiri historia yao wenyewe zaidi kwa kigezo cha utendaji binafsi, kuliko kitu kingine chochote. Na wanaweza wakawa sahihi. Hata hivyo, kama ilivyo katika kila jitihada, historia inatengenezwa na wale wanaotenda. Inategemea, katika mwingiliano wake, sio wa nguvu zisizoeleweka bali wa wanadamu. Migongano ya historia sio ya kati ya dhahania za falsafa, uchumi au elimujamii, bali kati ya wanadamu. Imesemekana kwamba hata katika nyakati zake za kisosholojia, historia haiwezi kupuuza kipengele cha shaksia ya mwanadamu. Historia ya miaka 23 ya awali ya kazi ya Uislamu ambayo inajumuisha ujumbe wote wa Muhammad kama Mtume wa Allah (s.w.t.) imeten-genezwa kwa sehemu kubwa, karibu na yeye mwenyewe, na vitendo vya mshirika wake, Ali ibn Abi Talib.

Huu ndio ushahidi wa historia. Lakini ni ushahidi ambao wanahistoria wengi kwa kawai-da wamejaribu kuuficha. Ni kwenye ushahidi huu ambako nimejaribu kuvuta mazingatio ya wasomaji wa kitabu hiki.

Lakini licha ya kwenda upande kwa wakati uliopita na wakati wa sasa kwa uandishi wa historia wa kimagharibi juu ya Uislamu, kuna matumaini mapya kwamba wanahistoria wa wakati ujao watafanya marekebisho kwa ajili ya yaliyoachwa na mapungufu ya wanahistoria wa zamani. Wanachotakiwa kufanya tu ni kutokuwa na upendeleo, na kutokuyakubali kibubusa yale maelezo na maamuzi ambayo yamekuwa ni istiari iliyochakaa ya historia ya Uislamu, bali kuugundua upya ukweli wao wenyewe kupitia ulinganisho na uchunguzi wa ushahidi.

Katika utangulizi wa Cambridge History of Islamu, Juz. I, kilichochapishwa na University Press, Cambridge (1970), P.M. Holt anaandika hivi:

"Uchunguzi wa historia ya Uislamu sasa unapanuka, uhakika mwingi wa dhahiri wa uandishi wa zamani wa historia wa kimagharibi (mara nyingi unaoonyesha utetezi na maelezo ya wanahistoria wa mapokezi wa Waislamu) umepotea, na ni polepole kupitia utafiti wa kina ambapo ufahamu wa kweli zaidi wa mambo ya zamani unaweza kupatikana."

Uhakika wa uandishi wa zamani wa historia wa Kimagharibi unaoakisi utetezi na tafsiri ya wanahistoria wa mapokezi wa Waislamu haujapotea bado lakini natutegemee kwamba utapotea, na ufahamu wa kweli zaidi wa mambo ya zamani utapatikana kadiri siku zinavyokwenda.

Jitihada ya kuitafsiri historia ya Uislamu, hususan ile historia ya karne yake ya kwanza, ni kama kuingia kwenye eneo lililotegwa mabomu; kuchemka kwake na migogoro, lawama

10

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kali na ubishani, na mtu anaweza kulisogelea tu kwa tahadhari sana. Hata hivyo, tafsiri inabakia ya msingi kwa kuielewa historia. Bila ya tafsiri, historia inakuwa ni rundo la habari zisizoratibiwa na ni orodha ya matukio "yaliyokufa" na tarehe zisizo na uhusiano na kila mojawapo. Bado haya matukio "yaliyokufa" yanajirudisha nyuma kwenye maisha wakati athari zinapohusishwa na sababu, na uunganishaji wa mambo unapoanzishwa. Jambo linalohusiana na mambo mengine linakuwa na maana ya kihistoria; katika kuliten-ga kwake, linaweza kuwa halina maana kabisa.

Hata Nadharia ya Einstein ni kule kuielewa dunia sio kama mfululizo wa matukio bali kama mahusiano.

Kama ilivyoelezwa hapo juu, kuna vitabu vingi kupita kiasi juu ya Uislamu lakini vingi ya hivyo ni tafsiri zilizokaririwa za kisa cha kuzaliwa na kukua kwake, na uzoefu wake wa kidini, kama kilivyokabidhiwa kwa waandishi wake na wanahistoria wa baraza wa serikali ambayo ilizaliwa pale Saqifah, na serikali zake zilizofuatia - zile serikali za Damascus na Baghdad. Kisa hicho, hata hivyo, kina upande mwingine pia.

Kanuni ya sheria ya zamani ya Kirumi ilikuwa ni audi alteram partem - (katika mgogoro wowote ule, sikiliza na ule upande mwingine); au audiatur et alter a pars - (acha na ule upande mwingine usikilizwe). Tendo la pamoja la wanadamu - ambalo linaitwa siasa -limejaa misiba mingi, yenye kuvunja moyo ambayo imeyaharibu maisha ya kila mtu duni-ani. Mingi ingeweza kuepukwa kama sheria hii ingetiiwa na wote.

Utaratibu huu kwamba katika mgogoro wowote ule, pande zote katika suala hilo zina-paswa kusikilizwa - umefanywa ni kifungu madhubuti katika mifumo ya sheria ya mataifa mengi, lakini zaidi hasa katika ile ya Marekani na Ulaya Magharibi. Thomas Jefferson alikuwa akifafanua tu utaratibu huu, ambao bila ya huo hapawezi kuwepo na haki yoyote, wakati alipotamka kwa mshangao: "Tafadhalini sana, natusikilize kila upande kwa uhuru kabisa." Wanafunzi wa Uislam, wa Kimarekani na wa Ulaya, katika masuala mengi, wamesikia tu upande mmoja wa Hadith; kitabu hiki ni jitihada ya kuwasilisha ule upande mwingine. Ni pamoja na dhamira hii kwamba nikitoe kwa ajili ya uamuzi wa wasomaji wenyewe.

Kutoka kwenye woga unaonywea kwenye ukweli mpya; Kutoka kwenye uzembe ambao unaridhika na nusu-ukweli; Kutoka kwenye kiburi kinachodhani kinajua ukweli wote; Ewe Mungu wa Ukweli utuokoe!

11

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

JOGRAFIA YA ARABUNI

Ni makubaliano ya wanahistoria kuanza historia ya eneo kwa jografia yake. Wanafanya hivyo kwanza kwa sababu tamthiliya ya historia inaonyeshwa kwenye "uwanja" wa pazia lake la ki-jografia; na halafu tena kwa sababu ya kipengele kinachojulikana katika siasa za kijografia kama "utambuaji wa jografia". Imesemekana kwamba sio desturi nyingi nyingine zinaungana kuunda athari ambazo zikitendekea kupitia vizazi vinavyofuatana, hutengeneza tabia ya watu na dola, na tabia huchukua sehemu muhimu katika kuunda historia yao.

Peninsula (rasi) ya Arabia ndio chanzo cha Uislamu. Uislamu "umezaliwa" ndani yake humo, na "ukakua" ndani yake, na ulikuwa tayari "umekomaa" ulipotoka ndani yake.

Ilikuwa katika miji ya Kiarabu ya Makka na Madina ambamo utambulisho wa Uislamu fasaha ulikuzwa, na Uislamu kwa kweli "ulitengemaa." Ufahamu wa jografia ya Arabia, kwa hiyo ni muhimu sana kwa ajili ya kuelewa mkondo wa historia yake.

Ufuatao ni mukhtasari wa jografia ya peninsula ya Arabia: Arabia, kama eneo lolote jingine, ina namna ya mandhari inayonyoosha na kuwabadili wale wanaoishi ndani yake na wanaopita humo. Ni ardhi kavu, nzito isiyokalika, na iko au ilikuwa, mpaka kupatikana kwa mafuta, ni kikwazo cha kudumu cha uhai kwa umahiri wa mwanadamu.

Uhai wake humo ulitegemea uwezo wake wa kukubaliana nayo.

Kinyume na fikra za watu wengi, Arabia sio kwamba yote ni nyika ya mchanga. Ina sehemu kubwa tofauti katika umbo juu ya usawa wake wa ardhi, sehemu zake muhimu zikiwa ni mchanga wenye joto kali, milima yenye rangi ya urujuari, mabonde membamba yaliyo katikati, vilele vyake vya ajabu vinavyochoma kwenye anga ya shaba, mawe yenye kupukutika, nyanda ngumu, maumbile ya kushtusha ya miamba ya ki-jiometria na yenye umbo la pia, vichuguu vya mchanga vinavyohamahama daima na chemchemi na mazingi-ra ya maziwa, vijito na bustani.

Ingawa karibu sehemu kubwa ya usawa wa ardhi ya jangwani ni wazi na kame, Arabia ina sehemu nyingi ambazo zinaonekana vizuri kwenye mwanga wa picha. Zina mandhari nzuri za ajabu zenye mahadhi nzuri, zenye kutawala mawazo zenye kupumbaza na kuhadaa - uzuri wa mchanga laini, ambao kama mawimbi ya bahari, daima uko unatembea. Uzuri huu unafi-fia haraka zaidi kuliko uzuri wa nakshi za mti usio na maua na wenye manyoya kwenye ukungu, na hata zaidi ya theluji iliyodondoka mara. Mawimbi ya mchanga yamerefuka kufikia upeo wa macho na zaidi, katika dunia ya ukimya na utupu. Jua linaweka mabaka

12

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

yenye mwanga mkali juu ya mchanga, na upepo unafanya michoro ya kisanii ndani yake na kuifuta punde kidogo baadae. Hivyo upepo wakati wote unaumba, unaharibu na kuumba tena mandhari. Na mandhari haya, katika tash'bihi zake zisizo na ukomo yamezaliwa kutia nuru na kutoonekana katika hewa ya jangwani, na kuyeyuka bila kutambuliwa, Sura ya nchi inakuwa ikibadilika na kupata daima Sura mpya nyingi za ajabu, na inakuwa ikisogea bila kutabirika toka sehemu moja kwenda nyingine. Mchanga unaweza kurundikwa kuwa chuguu kubwa linaloweza kufikia zaidi ya mita 150 juu ya msingi wa mwamba. Kutegemea mwelekeo na nguvu ya upepo, vichuguu hivyo huchukua namna nyingi za maumbo kama mwezi muandamo wa sherehe au migongo mirefu iliyosambamba au mkusanyiko mkubwa wa milima kama piramidi ambayo inaweza kuitwa milima ya mchanga.

Ikiwa kama jangwa hilo linazo Sura nyingi, pia inazo hali nyingi, na nyingi zao hazitabiri-ki. Kitambo kimoja inaweza kuwa ya udanganyifu unaofaa na utulivu lakini kitambo kidogo tu kinachofuatia, inaweza kuwa na ghasia mbaya, rahisi kubadilika, yenye kuogofya na kutoaminika kama bahari iliyochafuka. Misafara mizima ya watu ngamia na farasi, inase-mekana kupotea ndani yake, imemezwa, kama kwamba na michanga katili yenye njaa.

Katika dhoruba ya mchanga ambayo inaweza kudumu kwa masiku kidogo, jua mwezi, nyota, kontua za Sura ya nchi na peo za macho vimefutiliwa mbali, na safu za mchanga zenye hasira zinazunguka ovyo ovyo, na kutoa vivuli vya kisanii (surreal) juu ya usawa wa jangwa linaloghadhibika. Katika kiangazi, jua la wima linatoa tufani ya joto ambayo huchoma ardhi kama iliyochomwa na mwenge wa moto, jangwa linakuwa lenye mgawanyiko wa element mbili - joto na mchanga. Wakati mwingine wimbi la vumbi lina-fuatiwa na manyunyu yenye baridi na upepo yanayoonyesha "pinde mbili" za mvua -upinde mkubwa ukiwa na mdogo zaidi kati yake. Hivyo kitisho na uzuri vyote vinapatana kwenye mzunguko wa maisha ya jangwani.

Lakini kuanzia upande mmoja hadi mwingine na daima, hilo jangwa linabakia kutengwa, kimya, baya, lisilostaarabika la kutisha na kuogofya; na linabakia limefunikwa katika hofu yake kuu na upweke. Baadhi ya watu wanaamini kwamba hili jangwa lenye mkanganyiko lina "muujiza" wake ambao kwa kina sana huwagusa watu. Ni kwa kuegemea kwenye pazia hili kwamba, Mwarabu - mtoto wa jangwa - alifikia kilele cha maisha yake.

Arabia ndio peninsula (rasi) kubwa duniani lakini Waarabu wenyewe wanaiita Jazirat-ul-Arab (kisiwa cha Arabia), ambayo kwa namna nyingine ndicho. Ikipakana upande wa Mashariki na Ghuba ya Uajemi, Kusini na bahari ya Arabia, na upande wa kaskazini na "bahari kuu ya mchanga" ya jangwa la Syria. Ki-umbo, Arabia ni ya pembe nne yenye eneo la maili mraba milioni 1.2. Pwani ya Bahari nyekundu kutoka Ghuba ya Aghaba upande wa kaskazini mpaka Bab-el-Mendeb upande wa Kusini, ina urefu wa maili 1,200; na kutoka Bab-el-Mendeb upande wa Magharibi hadi Ras-el-Hadd upande wa Mashariki ni karibu urefu huohuo.

13

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kwa Sura, Arabia ni uwanda wa juu, mkubwa unaonyanyuka taratibu kutoka Mashariki kwenda Magharibi.

Mbali na Yemem na mabonde yaliyotawanyika katika safu za milima ya Magharibi nchi yote ni ya mchanga na mawe, na kavu na iliyochakaa.

Ifuatayo ni migawanyiko ya Kisiasa ya peninsula ya Arabia (1992)

1. Falme ya Saudia.

2. Jamhuri ya Yemen

3. Usultani wa Oman

4. Umoja wa Falme za Kiarabu

5. Qatar

6. Bahrain

7. Kuwait.

Yafuatayo ni maelezo mafupi ya kila moja ya maeneo haya saba ya kisiasa:

1. Falme ya Saudia

Hii Falme ya Saudia inachukua maili za mraba 850,000 za peninsula ya Arabia. Idadi ya watu wake inakisiwa kuwa milioni kumi, na mji wake mkuu ni Riyadh.

Majimbo yake ya "Pwani" ni Hijaz na Asir kwenye bahari ya Red Sea. Uwanda mfinyu wa Pwani ya Tihama unakwenda sambamba na bahari nyekundu (Red Sea).

Miji pacha ya Makka na Madina iko mwenye jimbo la Hijaz. Hijaz kwa hiyo, ndio nchi takatifu ya Uislamu. Hesabu ya watu wa Hijaz inakadiriwa kuwa milioni mbili, na eneo lake ni maili mraba 135,000. Miji mikuu na miji ya kawaida ya Hijazi ni Jeddah, bandari ya Makka, na sehemu kuu ya kibiashara ya nchi hiyo; Yanbu, Bandari ya Madina; Ta-if, kituo cha mlimani kilichoko Kusini Mashariki ya Makka, na mji mkuu wa kiangazi wa falme hiyo; Khaybar, Tabuk na Tayma. Huu "Mpango kabambe" wa Uislamu ulikamilishiwa Hijaz, na historia ya kuzaliwa na kukua kwake kumefungamana bila kutengeka na jimbo hili kunakolifanya kitovu cha ulimwengu wa Kiislamu.

Asir ndio ukanda wenye rutuba kiasi wa nyanda za Pwani na milima upande wa Kusini Magharibi, Kaskazini mwa Yemen, wenye vilele vinavyonyanyuka kufikia futi 10,000, na mvua za kutosha kufanya kilimo cha matuta ya mkingamo. Kile kituo maarufu cha mlimani cha Abha na makazi muhimu ya kilimo ya Jizan yako Asir. Jizan ndio bandari ya Asir.

14

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Najd ni nyanda za juu za katikati ya Arabia yenye muinuko wa wastani wa futi 3,000. Hali inayotawala ya topografia (mandhari) yake ni ule mfumo wa milima uitwao Tuwayq. Riyadh, mji mkuu wa falme hii, upo Najd. Chemchemi za Buraydah na Hayil ziko sehemu ya Kaskazini ya Najd.

Al-Hasa au jimbo la Mashariki liko kwenye Ghuba ya Uajemi. Mafuta yote na gesi ya falme hii zipatikana katika jimbo hili. Linazo pia zile chemchemi maarufu za Hofuf na Qatif. Vituo vya kibiashara vinavyoongoza jimboni humu ni Al-Khobar na mji wa bandari wa Dammam. Miji mingine maarufu ni Dhahran na Ras Tanura.

Ruba'-al-Khali (upande wa wazi) ulioko Kusini ndio bonge kubwa la mchanga duniani linaloendelea, na linachukuwa eneo la maili mraba 250,000. Kwa Waarabu linajulikana tu kama "Ar-Ramal" (michanga). Kwa jumla ni jangwa lisilo na uhai, na ni moja kati ya sehemu ambazo ni pweke mno na kame za dunia. An-Nufud kaskazini mwa peninsula hii ndio jangwa kuu la pili katika Arabia. Lina eneo la maili mraba 30,000.

2. Jamhuri ya Yemen

Jamhuri ya Yemen iko Kusini na Kusini Magharibi ya peninsula ya Arabia, na idadi ya watu ya milioni kumi na moja na eneo la maili mraba 190,000. Ndio eneo pekee la peninsula hii linalopata mvua za monsuni, na kuifanya sehemu yenye rutba sana na yenye watu wengi. Mlima mrefu sana wa Arabia, an-Nabi Shu'aib, uko Yemen na unafikia urefu wa futi 12,350. Sana'a ndio makao makuu na mji mkubwa zaidi katika nchi hii. Upo katika muinuko wa futi 7200, na unafahamika kwa hali yake ya hewa ya kiafya nzuri. Aden ndio mji mkuu wa kibiashara. Al-Mocha, Al-Huhaydah, Ta'izz na Mukalla ni miji mingine mikuu. Sayun na Shibam ni miji ambayo ni maarufu kwa magorofa yake marefu.

3.   Falme ya Oman

Falme ya Oman inachukua pembe ya Kusini Mashariki ya peninsula ya Arabia na ina majimbo ya Oman na Dhafar. Ina idadi ya watu milioni moja na eneo la maili mraba 90,000. Muscat ndio makao makuu na Matrak ndio mji mkubwa zaidi.

4.Umoja wa Famle za Kiarabu (Imarati)

Jamhuri ya Falme za kiarabu inaudwa na nchi saba:

Abu Dhabi, Dubai, Ajman, Sharjah, Fujaira, Ras-el-Khaimah, na Ummul-Qawain. Zina jumla ya maili mraba 32,000 na idadi ya watu 500,000. Makao makuu ya umoja huo ni Abu Dhabi ambayo pia ndio kubwa zaidi na mji maarufu zaidi wa falme hizo.

15

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

5. Dola ya Qatar

Qatar ina eneo la maili mraba 4,250 na idadi ya watu 200,000. Makao makuu yake ni Doha. Qatar ina idadi ndogo zaidi ya watu katika dola yote ya Kiarabu.

6. Dola ya Bahrain

Bahrain ni mkusanyiko wa visiwa 30, vyenye eneo la maili mraba 240 kwa jumla, na idadi ya watu 300,000. Manama, mji mkuu wa dola hii, upo kwenye kisiwa cha Bahrain, na Muharraq ndio mji mkuu wa pili katika mkusanyiko huu wa visiwa.

7. Dola ya Kuwait

Kuwait ina maili mraba 6,200 kwa eneo na inayo idadi ya watu milioni 1.5. mji wa Kuwait ndio makao makuu.

Hali ya nchi

Ingawa Tropik ya Kansa inapita katikati ya peninsula ya Arabia, nchi hiyo sio ya joto jingi. Kiangazi chake ni kirefu na chenye joto jingi, chenye halijoto linalopanda hadi kufikia nyuzi joto 130 Farenhaiti katika sehemu nyingi. Vipupwe vyake ni vifupi na vyenye baridi. Mvua ni haba, zenye wastani wa inchi nne kwa mwaka. Pembe yake ya Kusini-Magharibi; hatahivyo, hupata mvua kubwa kiasi, kwa kadiri ya inchi ishirini.

Uotaji wa Mimea

Uotaji mimea kwa jumla umetawanyika sana kutokana na kukosekana mvua na kwa sababu ya kuwepo chumvi nyingi kwenye udongo. Miti halisi ni adimu sana na vichaka ni vya kawaida. Mimea yote imebidi ijitohoe yenyewe ili kukubaliana na hali ya kuwepo jangwa.

Mtende huota kila penye maji. Ndio mti maarufu unaopandwa sana katika peninsula yote. Matunda ya tende ndio zao kuu la Waarabu wengi, na mti wake unatoa mbao yenye thamani na mazao mengineyo. Miti aina ya Tamarisk na Acacia pia inapatikana katika sehemu nyingi za nchi hii.

Nafaka

Nafaka kuu za Arabia ni ngano, shairi, mahindi na ulezi. Kahawa inalimwa Yemen; na pamba kwa viwango tofauti huko Yemen na Oman. Matunda ya maembe yamelimwa kwa mafanikio katika Oasisi za jimbo la Al-Hasa la Saudi Arabia, na minazi inakua huko Oman. Misitu kama iliyopo Saudi Arabia, ni vikundi vichache vya miti ya mirende (junipers) katika nyanda za juu za Yemen.

16

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

IKOLOJIA (UHUSIANO WA VIUMBE NA MAZINGIRA) YA ARABIA

Sehemu muhimu ya Ikolojia ya peninsula ya Arabia ni maji.

Kuwepo au kutokuwepo kwake kumeiunda historia yake kwa kiwango kikubwa. Wakazi walivutiwa na eneo la Makka huko Hijazi kwa kuwepo kwa chemchemi iliyogunduliwa na Hajra, mke wa Nabii Ibrahim (a.s.) mama yake Ismail (a.s.) na aliiita kwa jina la "Zamzam".

Kwa kuhakikishiwa kupatikana kwa maji yake mazuri kwa misimu yote, waliujenga mji wa Makka kuizunguka hiyo chemchemi. Eneo la maji la jimbo hili linahusisha visima, mabubujiko na mibubujiko ya kasi. Eneo lote halina mito na vijito mbali na ule Hajat wenye urefu wa maili sitini ulioko Jamhuri ya Yemen. Lakini hata hiki sio kijito cha kudu-mu; kinakuwa kijito tu wakati mvua nyingi zinaponyesha kwenye bonde lake.

Kipengele kipya na chenye sehemu nyingi zenye umuhimu mkubwa katika siasa ya uchu-mi ni kuwepo kwa hazina kubwa ya mafuta katika peninsula ya Arabia. Mnamo 1900 peninsula yote ilikuwa na watu wachache, na ilikuwa kame, iliyokumbwa na umasikini na iliyotengwa.

Ilikuwa ni moja ya majimbo machache ulimwenguni takriban iliyokuwa haijaguswa na athari za Magharibi. Ndipo yalipokuja mafuta na kila kitu kikabadilika. Saudi Arabia ili-uza shehena yake ya kwanza mwaka 1923, na kisima chake cha kwanza cha mafuta kilichimbwa mwaka 1938. Ndani ya miaka michache, mapato ya mwaka kutokana na mafuta yalivuka dola milioni moja. Falme hiyo ilivuka kiwango cha dola bilioni moja mwaka 1970; dola bilioni 100 mwaka 1980.

Maisha ndani ya Saudi Arabia na katika ghuba ya Uajemi yalibadilishwa na athari za uta-jiri mpya mali za kustaajabisha, maendeleo ya haraka ya kiuchumi, kuwasili kwa wafanyakazi wa kigeni, ushawishi wa kimataifa pengine kimsingi zaidi kuliko maisha yamebadilika penginepo popote kwa wakati wowote katika uzoefu wa mwanadamu.

Utajiri wa mafuta unabadilisha Sura ya nchi katika sehemu nyingi za Saudi Arabia na nchi za Ki-sheikh za ghuba. Umefanya iwezekane kupata tekinologia ya kisasa ya kuvuta maji kutoka kwenye vina vikuu au kubadili maji ya bahari kwa kuyaondoa chumvi, na kuifanya ardhi kame kuwa ya kilimo kwa kutumia umwagiliaji. Kuigeuza ardhi kuwa ya kilimo pia kunabadilisha hali ya takwimu ya idadi ya watu, vifo na maradhi (demografia) ya peninsula hii. Makabila ya kuhamahama yanapata mizizi katika makazi ya kudumu popote

17

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

upatikanaji wa maji unapokuwa wa hakika. Mbinu za kisasa zaidi zinatumika katika kujaribu kudhibiti mwondoko wa mchanga na kuondoa hali mbaya ya mazingira.

Myama maarufu sana huko Arabia alikuwa ni ngamia. Ngamia wa kiarabu ni yule wa aina ya nundu moja, mbali na yule wa Asia ya kati mwenye nundu mbili (Bactrian). Huyu mwenye nundu moja (Dromedary) ana kwato bapa, pana zenye wayo nene yenye vidole ambazo hazizami kwenye mchanga, na anaweza kusafiri masafa marefu jangwani. Maziwa ya ngamia yalifanya sehemu muhimu ya mlo wa Waarabu wa jangwani, na manyoya yake waliyatumia kutengenezea mahema yao.

Ngamia, kwa hiyo, alikuwa na umuhimu wa lazima kwa uhai katika jangwa.

Lakini cha kushangaza na kustaajabisha, ngamia takriban ametoweka kutoka Saudi Arabia na nchi zote za Ki-sheikh za Ghuba ya Uajemi. William J. Polk anaandika kwenye kitabu chake, "Passing Brave" kilichochapishwa na Alfred A. Knopf, New York, mwaka 1973, hivi:

"Punde kabla ya kifo chake mwaka 1960, yule mchunguzi mkuu wa Kiingereza juu ya majangwa, St. John Philby, alibashiri kuwa ndani ya miaka thelathini, Arabia itakuwa haina ngamia. Alichekwa wakati huo, lakini leo inaonyesha ubashiri wake ungekuwa mkubwa mno. Ngamia na mtegemezi wake, yule mhamajihamaji, takriban wametoweka kutoka Arabia. Hivyo enzi hiyo iliyoanza karibu miaka 3,000 iliyopita pamoja na ufugaji wa ngamia, inaisha. Ngamia amefanya jukumu muhimu katika kuibuka kwa ustaarabu."

Magari makubwa ya dizeli, magari moshi na ndege za Jeti vimechukua nafasi ya ngamia na misafara yake imekuwa "haifai" katika Arabia.

18

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ARABIA KABLA YA UISLAMU

Katika kuandika historia ya Uislamu, ni kawaida kuanza na ukaguzi wa hali ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na ya kidini ya Arabia kabla tu ya tangazo la Muhammad (s.a.w.) la ujumbe wake kama Mtume wa Allah (s.w.t.)

Ndio mapatano ya pili ya wanahistoria (ya kwanza likiwa ni kutoa maelezo ya ki-jogografia ya eneo hilo). Nitazingatia mapatano haya, na nitachambua kwa ufupi, hali ya kijumla katika Arabia katika mwisho wa karne ya sita na mwanzo wa karne ya saba A.D.

Hali ya Kisiasa katika Arabia.

Sura inayoonekana sana ya maisha ya kisiasa ya Arabia kabla ya Uislamu ilikuwa ni kutokuwepo kabisa kwa mfumo wa kisiasa katika muundo wowote ule. Ukiiondoa Yemen iliyoko Kusini Magharibi, hakuna sehemu ya peninsula ya Arabia iliyokuwa na serikali kwa wakati wowote ule, na Waarabu kamwe hawakutambua mamlaka yoyote ile mbali na mamlaka ya machifu wao wa makabila yao. Haya mamlaka ya machifu wa kikabila hata hivyo, yaliegama, kwa namna nyingi, juu ya tabia na nafasi zao, na yalikuwa ya uungwana kuliko kisiasa.

Mwanafunzi wa kisasa wa historia anaona mshangao kwamba Waarabu wameishi, kizazi baada ya kizazi, karne baada ya karne, bila ya serikali ya aina yoyote ile. Kwa vile hapakuwa na serikali, hapakuwa na sheria na utulivu. Kanuni pekee ya nchi ilikuwa ni hali ya uhalifu. Kama inavyotokea, inapofanyika jinai, upande uliodhuriwa ulichukua hatua mikononi mwao, na ukajabiru kupitisha 'hukumu' kwa yule mwovu. Mtindo huu ulis-ababisha mara nyingi matendo ya ukatili wa kuogofya.

Kama Waarabu walifanya kiasi kidogo cha kujizuia, haikuwa ni kwa sababu ya wepesi wa hisia alizokuwa nazo juu ya maswali ya kweli na batili lakini ni kwa sababu ya kuhofia kuchochea visasi na mauaji ya kurithi kisasi. Mauaji ya kisasi cha kurithi yalimaliza vizazi vizima vya Waarabu. Kwa vile hakukuwepo na vitu kama polisi, mahakama au majaji, ulinzi pekee mtu alioweza kuupata kutokana na maadui zake, ulikuwa katika kabila lake mwenyewe.

Kabila lilikuwa na jukumu la kulinda watu wake hata kama walitenda maovu. Ukabila au 'asabiyya' (moyo wa kiukoo) ulichukua nafasi ya kwanza kabla ya maadili. Kabila lililoshindwa kulinda watu wake kutokana na maadui zao lilijihatarisha kwenye kebehi, kashfa na dharau. Maadili, kwa kweli hayakuingia kwenye picha mahali popote pale. Kwa vile Arabia haikuwa na serikali; na kwa vile waarabu walikuwa na utawala huria kwa

19

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

silika yao, walifungana katika mapigano yasiyokwisha. Vita ilikuwa ni desturi ya kudumu ya jamii ya kiarabu. Jangwa liliweza kuchukua idadi ndogo tu ya watu, na hali ya vita vya kikabila ilidumisha uthibiti mkali juu ya ongezeko la watu. Lakini Waarabu wenyewe hawakuiona vita katika mwanga huu. Kwao wao, vita vilikuwa burudani au kiasi mchezo wa hatari, au aina ya tamthiliya ya kikabila, iliyofanywa na wenye weledi (ubingwa), kwa mujibu wa mfumo wa kanuni za zamani na ushujaa, ambapo "watazamaji" walishangilia.

Amani ya kudumu haikuwa na mvuto kwao na vita vilitoa fursa ya kukwepa kazi ngumu na kutokubadilika kwa mwenendo wa maisha katika jangwa. Wao kwa hiyo walichochea msisimko wa mapambano ya silaha. Vita viliwapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao katika kutupa mishale, ufundi wa kurusha panga na upandaji wa farasi, na pia, katika vita, wangeweza kujipatia sifa kwa ushujaa wao na wakati huohuo kuleta fahari na heshima kwa makabila yao. Kwa mara nyingi, Waarabu walipigana ili kupigana tu, ama iwepo au isiwepo sababu ya kuchochea vita.

Anasema G.E.Grunebaum:

"Katika karne ya kabla ya kuja Uislamu makabila yalitawanya nguvu zao zote katika vita vya kuviziana, wote dhidi ya wote."

(Classical Islam - A History 600-1258-1970)

Yale makabila ya wahamaji yalizunguka kwenye peninsula yote na kupora misafara na makazi madogomadogo. Misafara mingi na vijiji vilinunua kinga ya mashambulizi Haya kwa kulipa kiwango maalum cha fedha kwa watekanyara wa wahamaji.

Ni muhimu kuzingatia ule ukweli katika usiku wa kuzaliwa Uislamu hakukuwa na serikali katika ngazi yoyote katika Arabia, na ukweli huu unawezakuwa umeathiri kuinukia kwa Uislamu wenyewe. Ukosekanaji mzima wa serikali, hata katika hali ya kuanzishwa tu, ni kitu kisichokuwa cha kawaida kabisa kwamba kimeonwa na kutolewa maoni na mus-tashirik wengi, miongoni mwao ni:

D.S. Margoliouth:

"Arabia ingebakia ya kipagani angekuwapo mtu katika Makka ambaye angeweza kutoa pigo; ambaye angeweza kutenda. Lakini wengi wao, kama walivyokuwa wabaya wa Moham med, hapakuwa na mmoja wao aliyekuwa na ujasiri wa namna hii; na (kama ilivyoonekana) hapakuwepo na mahakimu kwa ujumla ambao kwao angeweza kushitakiwa."

(Mohammed and the Rise of Islam, 1971).

20

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Naye Maxime Rodinson asema:

"Mauaji ya halaiki yalibeba adhabu kubwa kwa mujibu wa sheria zisizoandikwa za jangwani. Katika utendaji waarabu huru walikuwa hawakufungwa na kanuni ya sheria zake kwa msaada wa jeshi la polisi. Ulinzi pekee wa maisha ya mtu ni ile hakika iliyowekwa na mila na desturi, ambayo ingenunuliwa kwa gharama kubwa. damu kwa damu na uhai kwa uhai. Kisasi cha kurithi, tha 'r, kwa kiarabu, ni moja ya misin-gi ya jamii ya kibedui."

(Mohammed, 1971) Asema Herbert J. Muller:

"Katika Arabia ya Mohammed hakukuwa na dola kulikuwa tu na makabila huru yaliyotangaa na miji. Huyu Mtume (s.a.w.) aliunda dola yake mwenyewe, na aliipa sheria tukufu iliyoandikwa na Allah (s.w.t.)"

(The Loom of History, 1958)

Watu wa Arabia walitokana na makundi mawili, wenye maskani na wahamiaji. Hijazi na Arabia ya Kusini ilitapakaa miji mingi midogo na mikubwa michache. Nchi yote iliy-obakia illikuwa na watu waliotapakaa wakitokana na Mabedui. Walikuwa nyuma katika dhana ya uraia na siasa lakini pia walikuwa ni chanzo cha wasiwasi na hofu kwa wale wenye maskani. Waliishi kama maharamia wa jangwani, na walikuwa na sifa mbaya kwa ubinafsi wao usiozuilika na vurugu zao za upambanuzi wa kikabila.

Yale makabila maarufu zaidi yalitumia kiwango maalum cha mamlaka katika maeneo yao husika. Katika Makka kabila lenye nguvu lilikuwa la Quraishi, katika Yathrib, makabila yenye nguvu yalikuwa ni yale makabila ya Kiarabu ya Aus na Khazraji, na makabila ya kiyahudi ya Nadhir, Qaynuqa'a na Quraydha. Maquraishi wa Makka walijiona wenye we ni bora kuliko Mabedui lakini hawa Mabedui walikuwa na dharau tu juu ya hawa watu wa mjini ambao kwao wao walikuwa ni "Taifa la wauza maduka tu".

Waarabu wote walikuwa na sifa mbaya kwa namna fulani ya tabia kama vile majivuno, kiburi na majisifu, ulipizaji kisasi na kupenda kwingi uporaji. Kiburi chao kilihusika kwa namna fulani na kushindwa kwao kuanzisha dola yao wenyewe. Walikosa nidhamu ya kisi-asa, na mpaka kuja kwa Uislamu, hawakutambua mamlaka yoyote kama ni yenye umuhimu mkubwa katika Arabia.

Walitambua mamlaka ya mtu aliyewaongoza kwenye uvamizi lakini angeweza kulaz-imisha utii wao ikiwa tu walikuwa na uhakika wa kupata mgao mzuri wa ngawira, na mamlaka yake yaliisha mara tu shughuli hiyo ilipokwisha.

21

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hali ya kiuchumi

Kiuchumi, Wayahudi ndio waliokuwa viongozi wa Arabia. Walikuwa ndio wenye ardhi nzuri yenye kulimika katika Hijazi, na walikuwa wakulima wazuri zaidi nchini humo. Walikuwa pia ndio wawekezaji wa vile viwanda vilivyokuwepo katika Arabia wakati huo, na walikamata ukiritimba wa utengenezaji wa zana za kivita.

Utumwa ulikuwa ni asisi ya kiuchumi ya Waarabu. Watumwa wa kiume na wa kike wali-uzwa na kununuliwa kama wanyama, na waliunda tabaka la waliokandamizwa zaidi katika jamii ya kiarabu.

Tabaka lenye nguvu zaidi, la waarabu, liliundwa na mabepari na wakopeshaji fedha. Viwango vya riba walivyotoza kwenye mikopo vilikuwa vikubwa mno, na viliundwa maalum kuwafanya matajiri zaidi na zaidi, na wale wakopaji kuwa masikini zaidi.

Vituo maarufu zaidi vya mjini katika Arabia vilikuwa Makka na Yathrib, vyote katika Hijazi. Wakazi wa Makka zaidi walikuwa ni wafanyabiashara, wachuuzi na wakopeshaji wa fedha.

Misafara yao ilisafiri wakati wa kiangazi kwenda Syria na wakati wa kipupwe kwenda Yemen. Walisafiri pia kwenda Bahrain upande wa Mashariki na Iraq upande wa Kaskazini Mashariki. Misafara ya biashara ilikuwa msingi wa uchumi wa Makka, na kuiendesha kwake kulihitaji ujuzi, uzoefu na uwezo.

R.V.C. Bodley asema:

"Kuwasili na kuondoka kwa misafara kulikuwa ni matukio muhimu katika maisha ya watu wa Makka. Karibu kila mmoja ndani ya Makka alikuwa na namna ya kitega uchumi katika ile mali ya maelfu ya ngamia, mamia ya watu, farasi na punda walioon-doka na ngozi za wanyama, zabibu kavu na minara ya fedha na kurudi na mafuta, manukato na bidhaa mbalimbali kutoka Syria, Misri na Fursi (Persia), na viungo na dhahabu kutoka upande wa Kusini."

(The Messenger, 1946, Uk. 31)

Huko Yathrib, Waarabu waliendesha maisha yao kwa kilimo na Wayahudi waliendesha maisha yao kama wafanyabiashara na wanaviwanda. Lakini Wayahudi hawakuwa wafanyabiashara tu na viwanda; miongoni mwao pia walikuwepo wakulima wengi, na wameileta ardhi nyingi mbovu kwenye kulimika. Kiuchumi, kijamii na kisiasa, Hijazi ilikuwa ndio sehemu mashuhuri zaidi katika Arabia mwanzoni mwa karne ya saba.

22

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Francesco Gabrielli anasema:

"Katika mkesha wa Uislamu, watu wenye kujishughulisha mno na walioendelea wa Arabia waliishi katika mji wa Maquraish. Wakati wa himaya za Arabu ya Kusini za Petra na Palmyra ulikuwa umepita kwa muda kiasi katika historia ya Arabia. Sasa hali ya baadae ilikuwa inaandaliwa hapo katika Hijazi."

(The Arabs - A Compact History-1963)

Waarabu na Wayahudi wote walikula riba. Wengi miongoni mwao walikuwa wala riba wajuzi; waliishi kwa riba waliyotoza kwenye mikopo yao.

E.A.Belyaev anaeleza:

"Riba ilitumika sana Makka, kwani ili kushiriki katika msafara wenye faida, watu wa Makka wengi waliokuwa na kipato cha wastani walikimbilia kwa wala riba; mbali na riba kubwa, angeweza kutegemea kupata faida baada ya kurudi salama kwa msafara. Wafanyabiashara matajiri zaidi walikuwa wachuuzi na wala riba.

Wakopeshaji fedha kwa kawaida walichukua dinari kwa dinari, dirham kwa dirham, kwa maneno mengine, asilimia mia moja ya riba. Katika Qur'an 3:125, Allah (s.w.t.) akiwaambia waumini, alisema: 'Msile riba mara mbili maradufu.' Hii ingeweza kumaanisha kwamba riba ya asilimia mia mbili au hata mia nne ilidaiwa.

Nyavu za riba ya Makka hazikuwakamata wakazi wenzao tu na wa makabila yao bali pia watu wa makabila ya Ki-Bedui ya Hijazi walioshugulika katika biashara ya Makka. Kama katika Athens ya zamani "njia kuu za kukandamiza uhuru wa watu zilikuwa ni pesa."

(Arabs, Islamu and the Arab Caliphate in Early Middle Ages, 1969)

23

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

HALI YA USTAWI WA JAMII

Arabia ilikuwa ni jamii iliyoshikiliwa na wanaume. Wanawake hawakuwa na hadhi ya aina yoyote zaidi ya kuwa bidhaa za ngono. Idadi ya wanawake mtu anayoweza kuoa haikukadiriwa. Mwanaume alipokufa, mwanae 'alirithi' wake zake wote isipokuwa mama yake mzazi tu.Tabia ya kikatili ya Waarabu ilikuwa ni kuwazika watoto wao wa kike wachanga wakiwa hai. Hata kama Mwarabu hakutaka kumzika binti yake akiwa hai, alikuwa bado lazima adumishe mila hii ya 'heshima' kwa vile hana uwezo wa kuhimili shinikizo la jamii.

Ulevi ullikuwa ni mazoea mabaya ya kawaida ya Waarabu. Ulevi wao ulifuatana na uchezaji kamari wao. Walikuwa walevi waliokithri na wacheza kamari waliokubuhu. Mahusiano ya jinsia zao yalikuwa yamelegea sana. Wanawake wengi waliuza mapenzi kupata maisha yao kwa vile kulikuwa na kidogo sana kingine ambacho wangeweza kufanya. Wanawake hawa walipeperusha bendera kwenye nyumba zao na waliitwa "mabibi wa bendera" Dhaat-ur-rayyat).

Sayyid Qutb wa Misri katika kitabu chake, Milestone kilichochapishwa na International Islamuic Federation of student organizations, Salimiah, Kuwait mnamo 1978 (uk; 48,49), amemnukuu yule mpokezi wa Hadithi mashuhuri, Imam Bukhari, juu ya desturi ya ndoa katika Arabia kabla ya Uislamu kama ifuatavyo:

"Shihab (az-Suhri) amesema: 'Urwah b. az-Zubayt alimfahamisha yeye kwamba Aisha, mke wa Mtume (s.a.w.) alimjulisha kwamba ndoa wakati wa Ujahilia zilikuwa za aina nne:

1.        Moja ilikuwa ni ndoa ya watu kama ilivyo hivi sasa, ambapo mtu anamfungia uchumba mtoto wa kulea au binti yake kwa mtu mwingine, na huyu mwingine anatoa mahari kwa binti kisha anamuoa.

2.        Aina nyingine ilikuwa pale ambapo mtu alimwambia mkewe akiwa ametakasika kutokana na hedhi, 'Nenda kwa N. (yaani fulani) na muombe kufanya ngono naye;' kisha mumewe anakaa mbali naye na hamgusi kabisa mpaka iwe wazi kwamba ana mimba kutoka kwa mwanaume mwingine aliyefanya naye ngono.

Inapodhihirika kwamba anayo mimba, mumewe anafanya naye ngono kama akipen-da. Anafanya hivyo kwa sababu tu ya kutaka kupata mtoto mwenye daraja (mwema). Aina hii ya ndoa ilijulikana kama nikah al-Istibda (ndoa ya kutafuta ngono).

24

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

3.  Aina nyingine ilikuwa pale ambapo kikundi cha wanaume chini ya kumi (raht) walipomtembelea mwanamke huyo huyo na wote wakawa wamefanya ngono naye. Kama alipata ujauzito na kuzaa mtoto, wakati mausiku kadhaa yalipopita baada ya kumzaa, aliwaita wote, na hakuna mmoja wao angeweza kukataa. Walipofika wote mbele yake, huwaambia 'Ninyi' mnajua matokeo ya matendo yenu; nimezaa mtoto na ni mwanao wewe, akimtaja anayemtaka kwa jina lake. Mtoto wake anaambatanishwa kwa mwanaume huyo, naye hangeweza kukataa.

4.  Aina ya nne ni wakati ambapo wanaume wengi wanapomuendea mwanamke mmoja mara kwa mara, na haepukani na yoyote anayemjia. Wanawake hawa ni malaya (baghaya). Walitumia kuweka mabango milangoni kwao kama ishara. Yeyote aliye-wataka wao aliwaingilia.

Kama mmoja wao alishika mimba na akazaa mtoto, walijikusanya (wanaume) wote kwake na kumuita mtaalamu wa utambuzi wa Sura (physiognomist). Kisha wal-imuambatanisha mtoto huyo kwa mwanaume ambaye wamemfikiria ndio baba, na mtoto alibakia ameambatanishwa kwake na aliitwa mwanae, hakuna pingamizi lolote kwa mwenendo huu lililoweza kufanyika.

Alipokuja Muhammad (s.a.w.w) kuhubiri haki alivunja aina zote za ndoa za ujahilia isipokuwa ile watu wanayotumia leo.

25

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

HALI YA DINI KATIKA ARABIA YA KABLA YA UISLAMU

Kipindi katika historia ya Arabia kilichotangulia kuzaliwa kwa Uislamu kinajulikana kama Wakati wa Ujahilia. Kuamua kutokana na zile imani na matendo ya wapagani wa Kiarabu, inaonekana kwamba lilikuwa ndio jina linalostahili. Waarabu walikuwa wafuasi wa "dini" mbalimbali ambazo zinaweza kupangwa katika makundi yafuatayo:

1. Waabudu-Masanamu au Washirikina

Waarabu wengi walikuwa wakiabudu masanamu. Waliabudu masanamu mengi na kila kabila lilikuwa na lakwao sanamu au masanamu na miungu yao. Al-Kaaba huko Makka, ambayo kutokana na Hadith, ilijengwa na Nabii Ibrahim (a.s) na mwanae, Ismail (a.s) na wao waliitoa Wakfu kwa ibada za Mungu Mmoja, wameigeuza kuwa hekalu la mapagani na dini zote, likihifadhi masanamu 360 ya mawe na miti.

2.   Walahidi (Atheists)

Kundi hili lilikuwa limeundwa na wayakinifu nao waliamini kwamba dunia ilikuwa ya milele.

3. Wazandiki

Waliathiriwa na imani ya Kiajemi ya upili katika desturi. Waliamini kwamba kuna miungu wawili wanaoziwakilisha zile nguvu pacha za wema na uovu au mwanga na giza, na wote wamefungwa katika vita isiokwisha ya ukubwa.

4.Wa-Sabai

Waliabudu nyota

5. Wayahudi

Warumi walipoibomoa Jerusalem mwaka 70 A.D. na kuwatoa Wayahudi nje ya Palestana na Syria, wengi wao walipata makazi mapya huko Hijazi Arabia. Chini ya athari zao, waarabu wengi pia walikujageuka kuwa kwenye dini ya uyahudi. Vituo vyao vyenye nguvu vilikuwa katika miji ya Yathrib, Khaybar, Fadak na Ummu-ul-Qura.

26

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

6. Wakristo

Warumi waliwageuza kabila la Ghassan la Arabia ya Kaskazini kuwa wakristo. Baadhi ya koo za Ghassan zilihamia na kufanya makazi huko Hijazi. Huko Kusini, kulikuwa na wakristo wengi ndani ya Yemen ambapo imani hii ililetwa mwanzoni na wavamizi wa Ethiopia. Kituo chao chenye nguvu kilikuwa mji wa Najran.

7.Waamini Mungu Mmoja

Kulikuwa na kikundi kidogo cha waaminio Mungu mmoja kilichokuwepo Arabia katika usiku wa kuchomoza Uislamu. Wanachama wake hawakuabu-dia masanamu, na walikuwa wafuasi wa Nabii Ibrahimu (a.s). Watu wa famil-ia ya Muhammad (s.a.w.), Mtume wa baadae, na Ali bin Abi Twalib, Khalifa wa baadae, na watu wengi zaidi wa ukoo wao - Bani Hashim - walikuwa kwenye kundi hili.

27

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ELIMU MIONGONI MWA WAARABU KABLA YA UISLAMU

Miongoni mwa Waarabu walikuweko watu wachache sana walioweza kusoma na kuandi-ka. Wengi wao hawakuwa na shauku sana ya kujifunza fani hizi. Baadhi ya wanahistoria wana maoni kwamba elimu ya watu ya wakati ule takriban ilikuwa ya simulizi tu. Wayahudi na Wakristo walikuwa ndio watunzaji wa elimu kama hiyo ambayo Arabia ilikuwa nayo.

Elimu ya taaluma kubwa kamilifu ya wapagani wa Kiarabu ilikuwa ni ushairi wao. Walidai kwamba Mungu alijaalia Ubora usiokifani, wa kichwa, juu ya Wagiriki (ushahidi wake ni sayansi na falsafa yao); wa mikono, juu ya Wachina (ushahidi wake ni ufundista-di wao); na wa ulimi kwa Waarabu (ushahidi wake ni ufasaha wao). Fahari yao kubwa, nyakati zote kabla na baada ya Uislamu, ilikuwa ni ule ufasaha wao katika ushairi. Umuhimu wa mashairi unatathminiwa kama ifuatavyo:

Amesema D.S. Margoliouth:

"Katika Arabia ya kuhamahama, washairi walikuwa sehemu ya zana za kivita kwa kabila lao; walitetea kabila lao, na kuponda yale makabila ya maadui kwa kutumia nguvu iliyopaswa hasa kufanya kazi kiajabu, lakini ambayo kwa kweli ilitokana na kutunga vifungu mahiri vya namna ambayo ingeweza kuvutia uhakiki, na hivyo ingeweza kuenea na kukumbukwa sana.

(Mohammad na Kuchomoza Uislamu, 1931) E.A. Belyaev naye asema:

"Taarifa nyingi juu ya hali ya uchumi, utawala wa jamii na mengi ya Waarabu katika karne ya tano na ya sita A.D., zinatokana na mashairi ya kale au kabla ya Uislamu, yanayojulikana kwa 'uaminifu wa kipicha' kwa Sura zote za maisha ya kikabila ya Arabia na mazingira yake. Wataalam kwa hiyo, wanaukubali ushairi huu kama 'muhimu sana na chanzo cha kuaminika kwa kuelezea Waarabu na desturi zao katika kipindi hiki."

(Arabs, Islam and the Arab Caliphate in the Early Middle Ages, 1969)

28

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mashairi ya Kiarabu yalikuwa na utajiri katika ufasaha na matumizi ya tamathali za usemi katika mazungumzo au maandishi, lakini yalikuwa na ukomo wa masafa, na yalikuwa na upungufu wa maana. Maneno yaliyomo yaweza kuwa ya kuvutia lakini yalikuwa chapwa! Kazi bora za mashairi yao takribani hufuatia kabisa utaratibu uleule wa fikira na mawazo. Hata hivyo yalikuwa ni kioo cha uaminifu katika maisha ya zamani ya uarabuni. Vile vile katika kuchimbua sanaa ya ushairi, washairi wa kiarabu kwa hadhari walikuwa wakien-deleza moja ya sanaa kubwa za binadamu - lugha ya Kiarabu.

Utungaji mkubwa wa mapagani wa Kiarabu ni ule ulioitwa "Golden Odes", mkusanyiko wa mashairi saba, yakidhaniwa ya ubora usiopitwa, yenye nguvu na ufasaha. Yalitundikwa ndani ya Al-Kaaba kama changamoto kwa yeyote mwenye kutamani kuyapita au kulin-gana nayo. Sir William Muir anaandika kuhusu mashairi Haya kama ifuatavyo:

"Mashairi saba yaliyotundikwa yalikuwa hai kuanzia hata kipindi kilichomtangulia Muhammad, kielelezo cha kushangaza cha ufasaha usio hila. Uzuri wa lugha na utajiri wa kuenea haraka wa matumizi ya tamathali za usemi katika mazungumzo na maandishi unakubaliwa na wasomaji wa ulaya, lakini somo la mshairi liliwekewa ukomo, na yale yasiyo ya kawaida yalikengeukwa.

Haiba ya kimada wake, baka la kuonewa wivu lililowekwa na dalili za karibuni za kambi yake, na upweke wa makazi yake (huyu kimada) yaliyotelekezwa, ukarimu na ushujaa (wa mwenye kimada), heshima isiyo na upinzani wa kabila lake, sifa nzuri za ngamia wake - hizi zilikuwa ndio mada ambazo, pamoja na tofauti ndogo katika uten-daji, na bila hila yoyote ya njama au Hadith, zilitawala ndoto za Mwarabu - na baad-hi ya hizo ziliongeza mafuta kwenye mazoea mabaya ya kudumu ya watu, makuu, uhasidi, kisasi na majivuno."

(The life of Mohammed, 1877)

Pamoja na kutokeza kwa Uislamu, msisitizo ulihamishwa kwa muda, kutoka ushairi kwen-da nathari na ushairi ukapoteza nafasi yake ya ukubwa na hadhi kama vile "Malikia" wa sanaa za Arabuni. "Utungaji" mkubwa wa Uislamu ulikuwa ni Qura'n Tukufu, Kitabu cha Uislamu na kilikuwa katika nathari. Waislamu huamini kwamba Qur'an "iliandikwa" Mbingnii kabla ya kuteremshwa kwa Muhammad, Mjumbe wa Mungu.

Wanaamini kwamba kipaji cha mwanadamu kamwe hakiwezi kutoa kitu chochote amba-cho kinaweza kulingana na mtindo wake au yaliyomo ndani yake. Kwa vizazi kumi na tano vilivyopita, imekuwa kwao mtindo wa maandishi, filosofia, theologia, sheria, metafisikia na mawazo ya kimafumbo.

29

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Jaribio limefanyika katika kurasa zilizopita kufafanua hali ya kawaida ya Arabia na aina ya maisha ya Waarabu kabla ya Uislamu. "Taaswira" hii ni halisi kama ilivyochorwa kutoka kwenye "nyaraka" za Waarabu wenyewe wa kabla ya Uislamu.

Tukiamua kutokana na Taaswira hii, inaonyesha kwamba Arabia kabla ya Uislamu ilikuwa haina vistawishi vya kijamii au historia ya kina, na Waarabu waliishi katika taflisi ya maadili na utumwa wa kiroho. Maisha kwao yalikuwa hayana maana, lengo na mwelekeo. Moyo wa ubinaadamu ulikuwa kwenye minyororo, na ulikuwa ukisubiri, kama ilivyokuwa, ishara ya kufanya jitihada kubwa mno, ya kujinasua na kuwa huru.

Ishara hiyo ilitolewa mwaka 610 A.D. na Muhammad, mwana wa Abdillah, katika mji wa Makka, alipotangaza ujumbe wake wa Utume, na akaanzisha harakati iliyoitwa Uslamu katika kazi yake ya kuzunguka dunia.

Uislamu ulikuwa ndio neema kubwa kwa mwanadamu daima uliwaweka huru wanaume na wanawake, kupitia utu kwa Muumba wao, kutokana na utumwa katika udhahiri wowote. Muhammad, Mtume (s.a.w.) wa Allah. (s.w.t.) alikuwa ndio mkombozi mkuu wa wanadamu. Yeye alimnasua mwanadamu kutoka kwenye "Mashimo ya Maisha"

Peninsula ya Arabia ki-jiogorafia ilikuwa pembezoni na kisiasa, eneo lisilojulikana mpaka mwanzoni mwa karne ya saba A.D. Ni wakati huo ambapo Muhammad (s.a.w.) alipoiwe-ka kwenye ramani ya kisiasa ya dunia kwa kuifanya uwanja wa matukio ya maana sana ya historia.

Kabla ya Uislamu, Waarabu walishika nafasi ya pembeni tu katika historia ya Mashariki ya kati, na wangebaki daima taifa la watu wanaodhani kila kitu kina roho, na wachunga kondoo kama Muhammad (s.a.w.) asigewapatia kiini na kichocheo kilichoyaunganisha makabila yao ya kihamajihamaji yaliyokuwa yametawanyika, kwa nguvu yenye kujiende-sha, yenye lengo maalum. Alitengeneza "taifa" kutoka kwenye bonge lenye mashimoshi-mo lisilokuwa na umbo la msingi. Aliwapamba Waarabu na nguvu mpya, udhanifu na kipaji cha ubunifu, na walibadili mwelekeo wa historia.

Alianzisha elimu ya viumbe na mazingira ya akili na falsafa mpya kabisa, na kazi yake ili-weka kipindi cha waziwazi kaitka historia ya ulimwengu; na ilikuwa ni mwisho wa enzi moja na mwanzo wa nyigine.

Akiandika kuhusu njiapanda hii katika historia, Francesco Gabrieli anasema katika kitabu chake, The Arabs - A Compact History, (1963):

"Ndivyo ilivyokoma dibaji ya kipagani katika historia ya watu wa Arabia. Yeyote anayeilinganisha na yaliyofuata, yaliyowapa Waarabu nafasi ya msingi katika jukwaa

30

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

la dunia, na kutia msukumo mawazo makubwa na kazi kubwa, sio tu kwa mtu asiye wa kawaida aliyeibuka kutoka miongoni mwao, bali kwa tabaka la wasomi wote, ambalo kwa vizazi vingi lilikusanyika na kutangaza neno lake, (mtu) hawezi ila kutambua mruko wa majaaliwa ya watu hawa unavyoanza hapa. mpaka hapo utarat-ibu wa maisha yake, ya udhaifu na yaliotawanyika, yalipata umoja, kituo cha kusuku-ma mbele, lengo na yote Haya chini ya ishara ya imani ya dini.

Hakuna upendo wa ajabu wa mambo ya kale unaoweza kutufanya tushindwe kutambua kwamba bila ya Muhammad (s.a.w.) na Uislamu, yumkini huenda wangebakia bila akili kama mimea kwa karne nyingi humo jangwani, wakijiangamiza wenyewe katika utoaji damu wa vita zao zenye kuleta madhara kwa pande zote, wakiwaangalia Byzantium, Ctesiphon na hata Axum kama mianga mikubwa ya kujulisha habari za ustaarabu iliyoko nje kabisa ya uwezo wao."

31

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

HASHIM - KABLA YA KUZALIWA UISLAMU

Katika karne ya tano (A.D). mtu aliyeitwa Qusay, alizaliwa katika kabila la Quraish. Alipatia heshima kubwa na umaarufu kwa kabila lake kwa ajili ya hekima zake. Aliijenga upya Al-Kaaba iliyokuwa katika hali ya kukatisha tamaa, na aliwaamuru Waarabu kujen-ga nyumba zao kuizunguka. Alijenga pia "ukumbi wa mji" wa Makka, wa kwanza katika Arabia. Viongozi wa koo mbalimbali walikusanyika katika ukumbi huu kutafakari juu ya maswala yao ya kijamii, kibiashara, kiutamaduni na kisiasa. Qusay aliunda sheria juu ya kugawa chakula na maji kwa Mahujaji waliokuja Makka, na aliwashawishi Waarabu kuli-pa kodi kwa ajili ya msaada wa huduma zao.

Edward Gibbon anasema:

"Qusay, aliyezaliwa takriban A.D. 400, ni babu yake mkubwa Abdul-Muttalib, na hivyo wa tano katika kizazi cha kupanda toka Muhammad, alipata mamlaka makub-wa huko Makka.

(The decline and Fall of the Roman Empire)

Qusay alifariki mwaka 480 A.D., na mwanae, Abd Manaf, alitwaa madaraka ya kazi zake. Na yeye pia alijipatia sifa kutokana na uwezo wake. Alitambulika kwa ukarimu wake na maamuzi yake mazuri. Alifuatiwa na mwanae Hashim. Ni huyu Hashim aliyeupa ukoo wake jina lake uliokuja kuwa maarufu katika historia kama Bani Hashim. Hashim alikuwa ni mtu wa namna ya pekee. Alikuwa ni yeye aliyewafanya Maquraishi kuwa wafanyabi-ashara na wakawa wafanyabiashara bora. Alikuwa ndiye mtu wa kwanza kuanzisha zile safari mbili za misafara ya Maquraish, ya kiangazi na kipupwe, na wa kwanza kuandaa tharid (mchuzi) kwa Waarabu. Lakini kwake yeye, Waarabu wangeweza kubakia wachun-ga kondoo daima.

Uongozi wa uongofu na wema na ukarimu zilikuwa ni mbili tu kati ya sifa nyingi ambazo Muhammad, nabii wa baadaye, "alizorithi" toka kwa mababu zake. Hashim alioa mwanamke wa Yathrib na kutokana naye alipata mtoto wa kiume - Abdul-Muttalib. Kwa wakati upasao, Abdul Muttalib alikuwa amrithi baba yake kama mkuu wa ukoo wa Hashim.

32

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Edward Gibbon:

"Huyu babu yake Muhammad (Abdul Muttalib), na nasaba yake ya jadi, wanaonekana katika kumbukumbu za kigeni na za ndani kama mabwana (wafalme) wa nchi yao; lakini walitawala, kama Percales huko Athens, au Medics huko Florence, kwa maoni ya hekima zao na msimamo; athari zao ziligawanyika pamoja na urithi wao. Kabila la Kuraish, kwa udanganyifu au nguvu (sic), walijipatia usi-mamizi wa Al-Kaaba; ile ofisi ya kikasisi iliyoendelezwa kupitia mishuko minne ya nasaba hadi kwa babu yake Muhammad; na ukoo wa Hashim, kutoka pale alipochipukia, lilikuwa ndio liliheshimiwa sana na tukufu kwenye macho ya nchi yao.

Mshuko wa Muhammad kutoka kwa Ismail ulikuwa ni hadhi ya taifa au hekaya (sic), lakini kama hatua za mwanzo za jadi hii ni za giza na mashaka (sic), angeweza kutoa vizazi vingi vya uungwana (usharifu) safi na halisi; alichipukia kutoka kwenye kabi-la ya Quraish na ukoo wa Hashim ulio maarufu sana wa Waarabu, mabwana wa Makka, wasimamizi warithi wa Al-Kaaba.

(The Decline and Fall of the Roman Empire)

Hashim alikuwa na ndugu yake mdogo alikuwa akiitwa Al-Muttalib, mtoto wa Abd Manafi. Kwa kipindi, alikuwa ndiye mkuu wa ukoo huo, na alipofariki mpawe - Abdul Muttalib - mtoto wa Hashim, alimfuatia yeye kama mkuu mpya wa ukoo huo. Abdul Muttalib alidhihirisha sifa zote zilizoyafanya majina ya baba na babu yake kuwa makub-wa na maarufu.

Kama ilivyoonekana kabla, mji wa Makka kama Arabia yote, ulikuwa hauna serikali wala mtawala, lakini ulimilikiwa na kabila la Quraish. Quraish ilitokana na koo kumi na mbili, na Banu Hashim ulikuwa mmoja wao. Kwa kupinga uharibifu wa tabia wa nyakati; watu wa ukoo wa Banu Hashim, walikumbuka, nusu karne kabla ya kuzaliwa Muhammad, kufanya juhudi za kujaribu kuzuia kuanguka kwa maadili ya Waarabu na kuimarisha hali ya kijamii, kiuchumi na ukuzi wa akili ya nchi hiyo. Wao, kwa hiyo, walibuni au kuunda 'shirikisho la wenye maadili.' Malengo makuu ya shirikisho yalikuwa kuzuia vita kutokana na kugawanyika na kuwalinda wanyonge na wasio na ulinzi kutoka kwa maadui.

Hawa Banu Hashim vilevile walijishughulisha katika ustawi wa uchumi wa Waarabu na walianzisha mfumo wa biashara na nchi majirani kwa kutuma misafara kwenda Syria wakati wa kiangazi na Yemen wakati wa kipupwe, kama ilivyoelezwa kabla. Misafara iliondoka Makka ikiwa imebebeshwa bidhaa kama matunda ya tende, lijamu na hatamu za farasi na ngamia, mablanketi yaliyotengenezwa kwa sufi au manyoya ya ngamia; manuka-to na mimea yenye kunukia uzuri, viungo, ubani, pembe na ngozi za wanyama wa jang-

33

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

wani, na farasi wa ukoo safu. Walirudi na nguo, mafuta ya zeituni, silaha, kahawa, matun-da na nafaka.

Yote haya, shirikisho la wenye maadili na biashara ya misafara yalikuwa, bila ya ubishi, ni zawadi kubwa ya Bani Hashim kwa Waarabu. Lakini zawadi kubwa mno sio tu kwa Waarabu, bali kwa dunia nzima, ilikuwa iwe ni yule mtoto aliyekuwa aitwe Muhammad mwana wa Abdullah ibn Abdul Muttalib na Amina binti Wahab, alikuwa aje kuwa mfadhili mkuu, sio tu kwa Waarabu bali kwa wanadamu wote. Moj a ya matukio maarufu lilitokea wakati wa waj ibu wa Abdul Muttalib kama msimamizi wa Al-Kaaba, lilikuwa ni uvamizi wa Makka toka kwa jeshi la Ki-habeshi likiongozwa na yule jemadari wa Kikristo, Abraha. Hilo jaribio la kuiteka Makka lilishindwa kama ilivyoelezwa katika Aya ya Qur'an Tukufu ifuatayo:

Usahihi-2.jpg

"...Na akawapelekea juu yao, ndege makundi makundi, wakawatupia mawe ya udongo mkavu. Na akawafanya kama majani yaliyotafunwa tafunwa." (Sura ya 105: 3-5 )

Kawa vile wavamizi walikuja na tembo(ndovu), ule mwaka wa kampeini yao ulikuja kuju-likana kama "Mwaka wa Tembo". Huu mwaka wa Tembo uko sawia na mwaka 570 A.D. ambao pia umetokea kuwa ndio mwaka wa kuzaliwa Muhammad, nabii wa wakati ujao. Lile jeshi la uvamizi liliondoka Makka, na masharti ya makubaliano ya kusimamisha vita yakajadiliwa, kwa niaba ya mji wa Makka, na Abdul Muttalib.

Sir John Glubb:

"Mnamo mwaka 570 A.D. Abraha, kaimu mfalme wa Kikristo wa Uhabeshi wa huko Yemen aliingia Makka. Makuraish walikuwa waoga sana au wanyonge mno wa kulipinga jeshi hilo la Kihabeshi na Abdul Muttalib, akiongoza ujumbe, alitoka kwen-da kujadiliana na Abraha.

(The Great Arab Conquest, 1963)

Mmoja wa binamu wa mbali wa Hashim, alikuwa ni Abd Shams. Umayya fulani aliyedai kuwa ni mtoto wake, alimwonea wivu Abdul Muttalib juu ya mamlaka na hadhi yake kubwa. Wakati mmoja, alifanya jaribio la kumnyang'anya uwezo na mamlaka yake lakini alishindwa. Kushindwa huko kulimkereketa sana moyoni mwake. Aliweka chuki dhidi ya Abdul Muttalib na watoto wake, na akairithisha kwa wanae mwenyewe na wajukuu zake waliokuja kujulikana kama Bani Umayya.

34

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Lakini kulikuwa na kitu zaidi ya wivu wa kikabila katika uadui wa Bani Umayya kwa Bani Hashim. Koo hizi mbili zilikuwa na tofauti kati yao katika tabia na mwenendo, na katika mtazamo wao na mwelekeo kwenye maisha, kama matukio yalivyokuwa yaje kubainisha mara, wakati Bani Umayya walipoongoza genge katika kuupinga Uislamu.

Bani Hashim walikusudia kuwa ngao ya Uislamu. Allah (s.w.t.) mwenyewe aliwachangua wao kwa ajili ya kusudio hili tukufu. Ibn Khaldun, mwanahistoria mashuhuri na mwana-elimujamii, anaandika katika kitabu chake kiitwacho Muqaddimah (Dibaji) kwamba Mitume wote wa haki lazima wapate kuungwa mkono na kundi fulani lenye nguvu. Msaada huu, anasema, ni muhimu, kwa sababu unasimama kama kinga ambayo inawalin-da wao dhidi ya maadui zao na inawapa wao kiwango cha ulinzi, bila hicho hawawezi kutekeleza ujumbe wao Mtukufu.

Katika suala la Muhammad, Mtume wa Uislamu, hawa Bani Hashim walifanya hilo "kundi lenye nguvu" lililomlinda yeye kutokana na nia mbaya ya Bani Umayya, wakampatia usalama na wakamuwezesha kutekeleza ujumbe wake Mtukufu. Abdul Muttalib alikuwa na watoto wa kiume kumi. Wanne wao walikuwa maarufu katika historia. Hawa walikuwa: -

1. Abdullah, baba yake Muhammad

2. Abu Talib, baba yake Ali

3. Hamza, yule shahidi -shujaa wa vita vya Uhud.

4. Abbas, mhenga wa Makhalifa wa Bani Abbas wa Baghdad.

Abdullah na Abu Talib walikuwa watoto wa mama mmoja ambapo hawa watoto wengine nane wa Abdul Muttalib walizaliwa na wake zake wengine.

35

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

KUZALIWA KWA MUHAMMAD NA MIAKA YA MWANZO YA UHAI WAKE

Abdullah alikuwa ndiye mtoto kipenzi cha Abdul Muttalib.

Alipokuwa na umri wa miaka kumi na saba, alimuoa Amina, bibi wa uzao bora wa Yathrib, mji ulioko Kaskazini ya Makka. Hakuwa hata hivyo, amekadiriwa kuishi muda mrefu, na akafa miezi saba tu baada ya ndoa yake.

Muhammad, Mtume wa Mungu wa wakati ujao, alikuwa bado mimbani. Sheikh Muhammad el-Khidhri Buck, profesa wa historia ya Kiislamu, chuo kikuu cha Misri, Cairo, anasema katika kitabu chake, Nur-ul-Yaqin fi-sirat Sayyid al-Murasalin (1953) hivi:

"Yeye (Muhammad Ibn Abdullah) alizaliwa katika nyumba ya ami yake, Abu Talib, katika "mtaa wa Bani Hashim" huko Makka, tarehe 12 Rabil-awal ya ule Mwaka wa Tembo, tarehe ambayo inaoana na tarehe 8 Juni 570. Mkunga wake alikuwa ni mama yake Abdur Rahmani Ibn Auf. Mama yake, Amina, alituma habari za uzazi huu wa kheri kwa babu yake, Abdul Muttalib, ambaye alikuja, akamchukuwa mikononi mwake, na akampa jina hili la Muhammad."

Mgao wa Muhammad katika urithi wake ulikuwa ni mtumwa mmoja wa kike, Ummu Ayman; ngamia watano na kondoo kumi. Huu ni ushahidi kwamba Mitume wanaweza kurithi mali, na kama wanaweza kurithi mali toka kwa wazazi wao, wanaweza pia kurithisha mali kwa watoto wao wenyewe. Kuwa mitume hakuwabatilishii wao katika kupokea urithi wao wenyewe wala hakuwabatilishii watoto wao kupokea wa kwao. Kauli hii inaweza kuonekana kama isiyofuata mantiki katika muktadha huu lakini sio. Muhammad, Mtume wa Uislamu, alitoa kwa mwanae, Fatima kama zawadi, shamba la Fadak.

Lakini alipofariki; Abu Bakr, aliyekuwa Khalifa, na Umar, Mshauri wake, walilikamata shamba hilo kwa kisingizio kwamba Mitume hawarithishi mali yoyote kwa watoto wao wenyewe, na mali yeyote wanayomiliki, inahusika baada ya kifo chao, sio kwa watoto wao, bali kwa umma wao. Ni faini kali ambayo mtu anapaswa kulipa katika Uislamu kwa kuwa tu mtoto au binti wa Mtume wake. Mtu mwingine yoyote katika umma huu anayo haki ya kurithi utajiri au mali ya baba yake lakini sio binti wa Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.)!

Ilikuwa ni desturi miongoni mwa Maquraish kuwapeleka watoto wao jangwani kupitisha miaka yao ya mwanzo katika hali ya hewa ambayo ilikuwa ni yenye kutia afya kuliko ile ya Makka. Watoto walijenga miili yenye nguvu zaidi katika maeneo ya wazi na hewa safi

36

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ya jangwani kuliko ambavyo wangekuwa katika hewa ya mjini yenye kusonga na kukirihi.

Kulikuwa na sababu nyingine moja zaidi ya kwanini Waarabu wa koo bora waliwapeleka watoto wao kuishi jangwani. Walikuwa wanasisitiza ufasaha katika kuongea na walikuwa "washabiki" wakubwa wa maneno. Walivutiwa na lugha ya Kiarabu, maneno yake, maana zao na tofauti ndogo ndogo katika maana zao; na walijivunia sana katika ufasaha wao binafsi. Kwa kweli, matabaka ya juu katika Makka walipata mamlaka yao juu ya uwezo wao wa balagha. Makka ilikuwa ndio sehemu ya makutano ya misafara mingi na Kiarabu chake kilikuwa kimechafuliwa na kuwa "Kiarabu pijini" (chenye maneno mchanganyiko).

Waarabu wa koo bora hawakutaka watoto wao kujifunza na kuongea kiarabu pijini cha Makka; waliwataka wazungumze tu lugha safi na isiyochanganywa ya jangwani. Wao, kwa hiyo, waliwapeleka watoto wao mbali na Makka ili kuwakinga kutokana na athari zote haribifu kama hizi katika miaka yao ya awali ya maisha yao.

Amina alimtoa mwanae, Muhammad, kwa Halima, mwanamke wa kabila la Banu Asad, aliyekuwa akiishi Mashariki ya Makka, kwa ajili ya malezi. Mtoto mchanga huyu, Muhammad aliishi miaka yake minne ya kwanza ya maisha yake huko jangwani na mama mnyonyeshaji wake. Wakati fulani katika mwaka wake wa tano wa maisha yake, mama huyu anasemekana alimrudhisha kwa mama yake huko Makka.

Muhammad alikuwa na umri wa miaka sita wakati Amina, mama yake, alipofariki. Alichukuliwa baadae na Abdul Muttalib, babu yake, mpaka nyumbani kwake. Lakini miaka miwili tu ilipita wakati Abdul Muttalib naye alipofariki.

Kabla tu ya kifo chake, Abdul Muttalib aliwaita watoto wake wote pamoja, na akawaam-bia kwamba anaacha "urithi" namna mbili kwao; mmoja ulikuwa uongozi wa ukoo wa Bani Hashim, na mwingine ulikuwa ni Muhammad Ibn Abdullah, mpwa wao, yatima wa miaka nane. Kisha akawauliza ni nani miongoni mwao alitaka uwezo wake na mamlaka kama kiongozi wa kabila hilo, na ninani miongoni mwao atachukuwa dhima ya kijana huyo ambaye amepoteza shauku kubwa ya kufanywa kiongozi wa kabila lakini hata mmoja hakujitolea kuchukua dhima juu ya Muhammad.

Kama Abdul Muttalib alivyolitazama kusanyiko hilo na kutafakari maisha ya baadaye ya kijana huyo, Muhammad, ukimya wa wasiwasi ukatanda mahali hapo. Lakini haukuchukua muda mrefu. Abu Talib, mmoja wa watoto wake, alijitokeza mbele na akase-ma kwamba alimtaka yule mwana wa marehemu kaka yake, Abdullah, na kwamba hakuwa na haja yoyote ya mamlaka na madaraka.

37

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Tamko hili la wazi la Abu Talib lilikamilisha suala hilo kwa Abdul Muttalib. Aliamua kum-fanya Abu Talib sio tu mlezi wa Muhammad bali pia mlezi wa ukoo wa Bani Hashim.

Abdul Muttalib alitangaza, alipokaribaia kufariki, kwamba mwanae, Abu Talib, atamfuatia yeye kama kiongozi mpya wa Bani Hashim, na kwamba atakuwa pia mlezi wa Muhammad. Kisha akaliamuru kusanyiko hilo kumtambua Abu Talib kama kiongozi mpya wa Bani Hashim. Wao wakakubaliana, na akawaruhusu kuondoka.

Historia ilithibitisha uamuzi wa Abdul Muttalib. Mwanae na mirthi wake, Abu Talib, alitekeleza kazi zote kwa heshima sana.

Sir John Glubb:

"Katika mwaka wa 578 Abdul Muttalib alifariki. Kabla ya kifo chake, alimkabidhisha mwanawe, Abu Talib, kumuangalia Muhammad. Abdullah, baba yake Muhammad, alikuwa ndugu wa Abu Talib kwa baba na mama yao. Watoto wengine wa Abdul Muttalib ni dhahiri walitokana na wake wengine tofauti.

(The life and Times of Muhammad, 1970)

Abu Talib na mkewe walifurahi sana na kumpokea Muhammad kwenye familia yao. Hawakumchukua nyumbani kwao tu, bali mioyoni mwao pia, na walimpenda zaidi ya walivyowapenda watoto wao wenyewe.

Abu Talib alikuwa ni mtu mwenye hadhi kubwa na mwenye kuheshimika. Wakati wa wajibu wake kama kiongozi wa Bani Hashim alibeba vyeo vya "Bwana wa Quraish," na "Kiongozi wa bonde". Kama watu wengine wa kabila lake alikuwa pia ni mfanyabiashara, na misafara yake ilisafiri kwenda na kurudi hadi Syria na Yemen.

Katika kila msimu, misafara ya Abu Talib iliondoka Makka kwenda vituo mbalimbali. Mara chache, yeye mwenyewe aliandamana na msafara kusimamia mauzo na ununuzi wa bidhaa katika masoko ya kigeni. Muhammad akiwa bado mdogo anasemekana kasafiri naye kwenda Syria pamoja na msafara mmojawapo alipokuwa na miaka kumi na miwili.

Mapema katika maisha, Muhammad, nabii wa baadae alijenga sifa ya ukweli, uaminifu na maamuzi yenye busara. Kwa vile hakukuwa na mabenki siku zile, alikuja kuwa "benki" ya watu wa Makka. Walileta fedha zao, mapambo ya vito, na vitu vinginevyo vya thamani kwake kwa uhifadhi wa salama, na wakati wowote walipotaka kurudishiwa kitu chochote, aliwarudishia. Walimuita yeye al-Amin (Mwaminifu) na as-Sadiq (Mkweli).

38

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Sir William Muir:

"Kwa kujaaliwa na akili safi adilifu na tamaa dhaifu, mkimya na mwenye mazinga-tio, yeye (Muhammad) aliishi zaidi kiupweke, na tafakari ya moyoni mwake ilimpa-tia shughuli kwa masaa ya mapumziko yaliyotumiwa na watu wenye tabia duni katika michezo ya kikatili na ufisadi. Tabia njema na muelekeo wa heshima wa kijana huyu asiyejionyesha vilimletea kukubalika kwa wananchi wenzie; na alipata lile jina, kwa kuafikiana kwa jumla, la Al-Amin, 'mwaminifu.' Hivyo aliheshimiwa na kutukuzwa, Muhammad aliishi maisha ya utulivu na ya kitawa katika familia ya Abu Talib."

(The life of Muhammad 1887, uk 20)

Wakati Muhammad alipokuwa na umri wa miaka ishirini, ilizuka vita miongoni mwa Maquraish, kabila lake, na kabila la Hawazin. Ingawa alikuwapo katika kampeni za vita hii, hakushiriki kwenye nafasi yoyote katika mapigano. Hakuua au kujeruhi mtu yoyote, hivyo kuonyesha katika kipindi hiki cha mwanzo cha maisha yake, kuchukia kwake umwa-gaji wa damu. Anasemekana, hata hivyo, kuwahi kuokota mishale kutoka uwanjani, na kuitoa kwa ami zake ambao walikuwa wanapigana.

Miaka michache baadae, Muhammad aliingizwa kama mwanachama wa lile Shirikisho la Wenye Maadili. Kama ilivyotajwa mapema, hili Shirikisho limejiapia lenyewe kuwalinda wayonge, kuwapinga madhalimu na waonevu, kukomesha unyonyaji wa namna yoyote ile.

Ikumbukwe kwamba ulikuwa ni ukoo wa Bani Hashim, ambao Muhammad nabii wa baadae alitokana nao, ambao ndio ulioanzisha lile Shirikisho la Wenye Maadili. Lilikuwa ni jambo lililotukia tu! Hakuna njia ya kujibu swali hili. Lakini kwa taratibu zao za kisi-asa, Bani Hashim walikwishatangaza vita juu ya udhalimu na dhulma. Waliweka wazi kwamba hawatakula njama na wenye nguvu dhidi ya wanyonge; wala hawangeridhia katika unyonyaji wa maskini kwa Maquraishi wa Makka.

Sio miaka mingi baadae, Muhammad alikuwa aanzishe utaratibu wa ujenzi upya wa jamii ya wanadamu, sehemu ya uchumi ambayo itatambua wazi uharibifu wa unyonyaji. Angezichukua zile "fursa" za Maquraishi na "haki " zao za kunyonya maskini na wanyonge, kutoka kwao.

Montgomery Watt:

"Lile Shirikisho la Wenye Maadili linaelekea kuchukua sehemu muhimu sana katika maisha ya Makka, na kwa sehemu kubwa kuelekezwa kwa watu na sera ambazo baadae Muhammad alijikuta anapingana nazo. Hususan ukoo wake wa Bani Hashim ulikuja kuwa na wajibu mkubwa katika Shirikisho la Wenye Maadili."

(Muhammad, Prophet and Statesman, 1961)

39

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

NDOA YA MUHAMMAD MUSTAFA NA KHADIJA

Khadija, binti ya Khuwaylid, alikuwa mkazi wa Makka. Naye pia alikuwa wa kabila la Quraishi. Aliheshimiwa sana na watu wa Makka kwa sababu ya tabia yake ya mfano na uwezo wake wa kupanga. Kama vile watu wa Makka walivyomuita Muhammad 'Sadiq' na 'Amin', walimuita Khadija 'Tahira', yenye maana ya "Aliye safi." Alikuwa akijulikana pia miongoni mwa Waarabu kama 'Malkia wa Wafanya biashara.' Wakati wote misafara ilipoondoka Makka au kurudi Makka, waliona kwamba mzigo wake ulikuwa mkubwa kwa ujazo kuliko mizigo yote ya wafanyabiashara wa Makka ikichanganya pamoja.

Muhammad alipokuwa na umri wa miaka 25, ami yake na mlezi wake, Abu Talib, alimshauri Khadija, na kuelewa kwake kwa kimya, kwamba amchague yeye kama wakala wake katika mmoja wa misafara yake, uliokuwa uondoke kwenda Syria punde tu, mara.

Khadija kwa kweli alikuwa akihitaji wakala kwa wakati ule hasa. Alikubali kumchagua Muhammad kama wakala wake. Alichukua madaraka ya bidhaa za Khadija, na msafara ukatoka kwenda Syria. Mtumwa wa Khadija, Maisara, pia alifuatana naye na akamsaidia kama msaidizi wake.

Safari hii ya kibiashara kwenda Syria ilifanikiwa kupita matarajio, na Khadija alivutiwa sana na uwezo wa wakala wake na uaminifu wake kiasi kwamba aliamua kumpa madaraka ya shughuli zote za biashara zijazo baadae. Safari hii pia ilithibitisha kuwa mwanzo wa ndoa yao.

Edward Gibbon:

"Nyumbani au ugenini, kwenye amani au vita, Abu Talib, ami yake Muhammad aliye-heshimiwa sana kuliko ami zake wengine, alikuwa ndiye kiongozi na mlezi wa ujana wake; katika mwaka wake wa 25 aliingia kwenye huduma za Khadija, mjane aliyekuwa tajiri na mwadilifu wa Makka, ambaye mara tu alimtunza uaminifu wake kwa zawadi ya uchumba na mali.

Makubaliano ya ndoa, katika mfumo rahisi wa kizamani, yanaonyesha kupendana kwa Muhammad na Khadija; yanamuelezea yeye Muhammad kama mtu hodari zaidi wa kabila la Quraish; na anatamka mahari ya wakia kumi na mbili za dhahabu na ngamia ishirini, ambayo ilitolewa kwa ufadhili wa ami yake.

(Decline and Fall of the Roman Empire) 40

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Abu Talib alisoma khutba ya ndoa ya Muhammad na Khadija, na hotuba yake au waadhi unathibitisha bila shaka yoyote kwamba alikuwa akiabudu Mungu mmoja.

Alianza hotuba yake katika mfumo wa "Kiislam" kwa kutoa sifa na shukrani kwa Allah (s.w.t.) kwa rehma zake na baraka zisizoidadi na neema, na alimalizia kwa kumuomba Rehma na neema Zake juu ya maharusi wapya hao.

Ndoa ya Muhammad na Khadija ilifanikiwa sana. Imebarikiwa na furaha kuu isiyo na kifani kwa wote, mume na mke. Khadija alijitolea maisha yake kwenye huduma kwa mumewe na Uislamu. Alitumia utajiri wake mkubwa wote kwa kuimarisha Uislamu, na katika ustawi wa Waislamu.

Khadija alikuwa na hisia za ujumbe kama zile zile alizokuwa nazo Muhammad, na alikuwa na shauku kama aliyokuwa nayo ya kuona Uislamu unaushinda upagani. Kwa shauku yake ya kuuona ushindi wa Uislamu, aliongeza uwajibikaji na uwezo. Alimuondoa mumewe katika ulazima wa kutafuta maisha, na hivyo kumuwezesha kutoa muda wake wote katika ulazima wa kutafuta kujiandaa kwa kazi kubwa iliyokuwa imelala mbele yake.

Huu ndio mchango wa maana sana alioutoa kwenye kazi ya mumewe kama Mtume wa Mungu. Alikuwa ndio egemeo ambalo Muhammad alilihitaji katika miaka yote ya maan-dalizi kwa ajili ya Utume.

Ndoa ya Muhammad na Khadija ilibarikiwa pia na kuzaliwa kwa binti yao, Fatima Zahra. Ingawa neema ambazo Mungu amewajaalia juu yao zilikuwa nyingi, hapakuwa na yoyote waliyoithamini zaidi ya binti yao, Fatima Zahra. Alikuwa ni mboni ya macho ya baba yake, na "Bibi wa Peponi" wa baadae. Baba na Mama walitoa kwa wingi mno mapenzi yao juu yake, na alileta matumaini ndani ya nyumba yao.

41

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

KUZALIWA KWA ALI IBN ABI TALIB

Ali alizaliwa tarehe 13 Rajab ya mwaka wa thelathini wa Tembo (A.D. 600). Binamu yake, Muhammad, alikuwa ana miaka thelathini wakti huo. Wazazi wa Ali walikuwa ni Abu Talib Ibn Abdul Muttalib, na Fatima, binti Asad, wote wa ukoo wa Bani Hashim.

Ali alizaliwa ndani ya Al-Kaaba huko Makka.Yule mwanahistoria maarufu, Masud, Herodotus wa Waarabu anaandika kwenye ukurasa wa 76 wa juzuu ya 2 ya kitabu chake, Murujudh-Dhahab kwamba moja ya ubora ambao Ali alikuwa nao ulikuwa kwamba alizaliwa ndani ya Nyumba ya Allah (s.w.t.) Baadhi ya mabingwa wengine ambao wathibitisha kuzaliwa kwa Ali ndani ya Al-Kaaba, ni :-

1.   Muhammad Ibn Talha Shafii katika Matalibul-usul uk 11.

2.  Hakim katikaMustadrak, uk. 483, Juz. 111.

3.  Al- Umari katika Sharh Ainia uk. 15.

4.  Halabi katika Sira, uk. 165, Juz. 1.

5.   Sibt Ibnul- Jauzi katika Tadhkira Khawaisil Umma, uk.7.

6.   Ibn Sabagh Malik katika Fusuulul Muhimma uk. 14

7.   Muhammad Ibn Yusuf Shafi'i katika KifAyatut-Talib uk. 261.

8.   Shablanji katika Nurul Absar, uk. 76.

9.    Ibn Zahra katika Ghiyathul Ikhtisar, uk.97.

10.   Edvi katika Nafahatul Qudsia uk. 41.

Miongoni mwa wanahistoria wa kisasa, Abbas Mahmud al-Akkad wa Misri anaandika katika kitabu chake Al-Abqariyat ul-Imam Ali, (Cairo, 1970) kwamba Ali Ibn Abi Talib alizaliwa ndani ya Al-Kaaba.

Mwanahistoria mwingine wa sasa, Mahmud Said at-Tantawi, wa Supreme council of Islamic Affairs (Baraza la juu la Mashauri ya Kiislamu), Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, anaandika katika ukurasa wa 186 wa kitabu chake kiitwacho Min Fadha-il al-Ashrat al-Mubashirina bil-Janna, kilichochapishwa mwaka 1976 na Matab'a al-Ahram at-Tijariyya, Cairo, Misri hivi:-

"Rehma za Allah (s.w.t.) ziwe juu ya Ali Ibn Abi Talib. Alizaliwa ndani ya Al-Kaaba. Alishuhudia kuchipuka kwa Uislamu; alishuhudia Da'wa ya Muhammad na alikuwa ni shahidi wa Wahyi (kushuka kwa Qur'an al-Majid). Mara moja tu aliukubali Uislamu ingawa alikuwa bado mtoto, na alipigana maisha yake yote ili kwamba Neno la Mungu liwe juu kabisa."

42

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mshairi wa Kiarabu alitunga ubeti ufuatao juu ya kuzaliwa kwa Ali:

Yeye (Ali) ndiye yule ambaye ile Nyumba ya Allah (s.w.t.),

iligeuzwa kuwa wodi ya wazazi;

Na yeye ndiye aliyeyatupa masanamu nje ya Nyumba hiyo; Ali alikuwa mtoto wa kwanza na wa mwisho,

daima kuzaliwa ndani ya Al-Kaaba.

Ilikuwa ni desturi ya Waarabu kwamba wakati mtoto anapozaliwa, aliwekwa chini ya miguu ya sanamu au masanamu ya ukoo huo, hivyo kuashiria "kumkabidhi" kwa huyo mungu wa kipagani. Watoto wote wa Kiarabu "walitolewa" kwa masanamu isipokuwa Ali Ibn Abu Talib. Wakati watoto wengine wa Kiarabu walipozaliwa, mmoja wa waabudu sanamu alikuja kuwasalimia na kuwabeba mikononi mwake.

Lakini Ali alipozaliwa, Muhammad, mjumbe wa baadae wa Allah (s.w.t.) alikuja kwenye eneo la Al-Kaaba kumsalimia. Alimbeba mtoto huyo mikononi mwake, na kumtoa kwenye kumtumikia Allah (s.w.t.) Mtume huyu wa baadae lazima awe alikwishajua kwamba yule mtoto aliyekuwa mikononi mwake siku moja atakujakuwa adui asiyeshindika wa wanaoabudu masanamu wote na washirikina na wa miungu yao na miungu ya kike. Wakati Ali alipokua, aling'oa uabudu masanamu na ushirikina kutoka Arabia kwa upanga wake.

Kuzaliwa ndani ya Al-Kaaba kulikuwa ni moja kati ya sifa nyingi ambazo Mungu amez-ijaalia juu ya Ali. Sifa nyingine aliyokuwa nayo ni kwamba kamwe hakuabudu masanamu. Hii nayo inamfanya awe wa kipekee kwa vile Waarabu wote waliabudu masanamu kwa miaka na miaka kabla ya kukana uabudu masanamu na kuukubali Uislamu. Ni kwa sababu hii ambapo anaitwa, "Karama llahu waj-hahu" ("Ambaye Allah (s.w.t.) ameutukuza uso wake.")

Uso wake ulitukuzwa hasa na Allah (s.w.t.) kwani ulikuwa ndio uso pekee katika maswa-haba ambao kamwe haukuinama mbele ya Sanamu lolote.

Ali alikuwa ndiye mtoto mdogo kabisa katika familia hiyo. Kati ya kaka zake watatu, Talib na Aqil, walikuwa wakubwa kwa miaka kumi zaidi yake.

Kuzaliwa kwa Ali kuliujaza moyo wa nabii wa baadaye furaha isiyo kifani. Mtoto huyu alikuwa ni mtu mmoja "maalum" kwake yeye. Ingawaje Muhammad alikuwa na binamu wengi wengine na walikuwa na watoto wao mwenyewe, na Ali mwenyewe alikuwa na kaka zake wakubwa watatu; lakini hakuonyesha mvuto wowote juu ya yeyote kati yao. Ali, na Ali peke yake ndiye alikuwa kitovu cha mvuto wake na mapenzi.

43

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Wakati Ali alipokuwa na miaka mitano, Muhammad alimchukua kama mtoto wake wa kupanga, na kuanzia hapo tena hawakutengana tena daima. Kuna Hadith kwamba wakati mmoja kulitokea njaa huko Makka, na maeneo yanayoizunguka, na Abu Talib, akiwa kati-ka dhiki kubwa wakati huo, alikuwa akiona ugumu kutunza kundi kubwa la watu. Ilimjia Muhammad kwamba alipashwa kujaribu kupunguza baadhi ya uzito wa majukumu ya ami yake, na alishawishika kwa hiyo, kumchukua Ali.

Ni kweli kwamba Muhammad alimchukuwa Ali lakini sio kwa sababu iliyoelezwa hapo juu. Katika nafasi ya kwanza kabisa, Abu Talib hakuwa kwenye hali ya dhiki kubwa kiasi kwamba hakuweza kumlisha mtoto wa miaka mitano; alikuwa ni mtu mwenye hadhi na uwezo, na misafara yake ilikwenda na kurudi kati ya Hijaz na Syria au kati ya Hijaz na Yemen. Katika nafasi ya pili, kulisha mtoto wa miaka mitano kungekuwa vigumu kuleta tofauti yoyote kwa mtu ambaye alilisha hata wageni kama wangekuwa na njaa.

Muhammad na Khadija walimchukua Ali baada ya kufa kwa watoto wao wenyewe wa kiume. Ali kwa hiyo aliziba uwazi katika maisha yao. Lakini Muhammad, Mtume wa baadae, pia alikuwa na sababu nyingine ya kumchukua Ali. Alimchagua Ali kumlea, kumuelimisha na kumuandaa kwa ajili ya takdir kubwa iliyokuwa ikimngojea katika nyakati zijazo.

Dr. Taha Hussein wa Mirsi anasema kwamba Mtume wa Allah (s.w.t.) mwenyewe alikuwa kiongozi wa Ali, mwalimu na mwelekezaji, na hii ni sifa moja nyingine zaidi ambayo anayo Ali, na ambayo hakuna mwingine yeyote anayeshirikiana naye kwayo.

Kuhusu Uislamu imesemekana kwamba kati ya dini zote za dunia, ni hii moja pekee iliyokuwa katika mwanga wa historia, na hakuna sehemu ya Hadith yake iliyoko gizani.

Bernard Lewis asema:

"Katika insha juu ya Muhammad na chanzo cha Uislamu, Ernest Renan anazungumzia kwamba, tofauti na dini zingine ambazo zilianzishwa kwa usirisiri, Uislamu ulizaliwa katika mwanga kamili wa historia. "Mizizi yake iko kwenye usawa wa ardhi, na maisha ya Mwanzilishi wake yanafahamika vema kwetu sisi kama ya wale waleta mabadiliko wa karne ya kumi na sita .

(The Arabs in History, 1960) G. E. Von Grunebaum:

"Uislamu unaweka tamasha la maendeleo ya dini ya ulimwengu katika mwanga wa historia."

(Uislamu, 1969)

44

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kadhalika, inaweza kusemwa kwamba kati ya marafiki na Masahaba wote wa Muhammad, Mtume wa Uislamu, Ali ndiye pekee aliyekua katika mwanga kamili wa historia. Hakuna sehemu ya maisha yake, ama katika uchanga wake, utoto wake, uvulana wake ujana wake, uanaume wake au kupevuka, ambayo imefichikana kutoka kwenye mwangaza wa historia. Alikuwa ndio kivutio kikuu cha macho yote tangu kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake. Kwa upande mwingine maswahaba waliobakia wa Mtume (s.a.w.) wanakuja kwenye mvuto wa nadhari ya mwanafunzi wa historia baada tu walivyokubali Uislamu, na kidogo, kama kipo, kinajulikana mpaka kufikia hapo.

Ali alijaaliwa kuwa mkono wa kuume wa Uislamu, na ngao na kingio la Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) Takdira au maajaliwa yake yalikuwa kiungo kisichotenganishwa na takdira ya Uislamu, na maisha ya Mtume wake. Alikuwepo katika kila hali ya mambo katika historia ya harakati hii mpya, na alishika nafasi ya kuwa nyota ndani yake. Ilikuwa, kwa dharura, ni nafasi ambayo yeye pekee ndiye angeweza kuishika. Aliakisi "taswira" ya Muhammad. Kitabu cha Allah (s.w.t.) chenyewe kimemuita "nafsi" au mwandani (nafsi ya pili) ya Muhammad katika Aya ya 61 ya Sura ya tatu, na alionyesha jina lake maarufu toka upande mmoja hadi mwengine, wa historia.

Katika miaka ijayo, muundo wa ufanyaji kazi pamoja wa Muhammad na Ali - amir na mfuasi - utakuja kuweka "Ufalme wa Mbingnii" katika ramani ya dunia.

45

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

KABLA TU YA TANGAZO LA UJUMBE WAKE

Licha ya ukweli kwamba Arabia ilikuwa ni shimo la uovu na ngome ya ibada ya masamu na ushirikina, Muhammad mwenyewe hakuwa kamwe amechafuliwa na inda au dhambi yoyote, na kamwe hakuinama mbele ya sanamu lolote. Hata kabla hajatangaza kwamba amekuja kusimamisha ufalme wa Mbingnii hapa duniani, tabia yake na mwenendo wake mwenyewe vilikuwa ni kiakisi (picha) cha Qur'an Tukufu. Hata wakosoaji wake hawakuweza kuonyesha tofauti kati ya tabia yake na maagizo ya Qur'an wakati wowote, kabla na baada ya Tangazo.

Baada ya Tangazo la ujumbe wake kama Mtume wa Mungu, aliziweka mila na desturi za kipagani chini ya amri ya kupigwa marufuku, lakini hakuna ushahidi kwamba kabla ya kufanya hivyo, yeye mwenyewe aliwahi kutenda jambo la kipagani, au hasa tendo lolote lenye kukinzana na Qur'an.

Inaonekana kwamba, Qur'an, kitabu cha Mungu kilikuwa kimegandamizwa kwenye moyo wa Muhammad tokea mwanzo, na pia inaonyesha kwamba "alihubiri" Uislamu hata kabla ya kubaathiwa, bali tu kupitia matendo yake na sio kwa maneno. Matendo yake yalikuwa fasaha sawa kama ilivyokuwa hotuba zake, na yaliutangazia ulimwengu ni vipi alivyokuwa mtu wa adabu. Hata hivyo walikuwa ni wale mapagani waliomwitaAmin (mwaminifu) na Sadiq (mkweli), na walikuwa ni watu haohao ambao, katika miaka ya baadae, walimsum-bua, wakamuwinda, wakamfukuza, na kuweka na kutangaza malipo juu ya kupatikana kichwa chake.

Pamoja na kupotoka na ukorofi, kama mapagani wa Kiarabu walivyokuwa, bado walivu-tiwa na ukweli; hata ukiwa kwa adui. Bado kupendezewa kwao na ukweli wa Muhammad hakukuwazuia kutafuta kumuangamiza aliposhutumu ibada yao ya masanamu na ushirikina wao. Walishikwa na kiu juu ya damu yake tangu pale alipowaita kwenye Uislamu lakini hawakujiuliza kuhusu kuwa kwake mkweli. Juu ya hoja hii hapawezi kuwepo na ushahidi wa kuaminika kabisa hasa zaidi ya wao.

Wenyeji wa Makka walipendezewa sio tu na uadilifu wa Muhammad, bali pia na maamuzi yake. Wakati mmoja, Maquraish walikuwa wanajenga upya Al-Kaaba, na katika ukuta mmoja wapo walikuwa waweke lile Jiwe Jeusi. Mtu alikuwa alilete lile Jiwe Jeusi kwenye eneo la ujenzi, alinyanyue kutoka ardhini, na aliweke katika sehemu yake juu ya ukuta huo. Ni nani alikuwa alifanye hili?

46

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kila ukoo uliidai heshima hiyo iwe juu yao wenyewe, lakini zile koo nyingine hazikuwa tayari kumkubalia yeyote katika jambo hili. Kutokubaliana huku kulisababisha maneno makali, na wakaidi wakatishia kuamua kwa upanga, ni nani angeweka lile Jiwe Jeusi mahali pake katika ule ukuta.

Wakati ule, mzee mmoja wa Kiarabu akaingilia kati, na akashauri kwamba badala ya kupi-gana na kuuana, wakuu wa koo zile wangepaswa wasubiri na kuona ni nani atakuwa mtu wa kwanza kuingia katika maeneo ya Al-Kaaba asubuhi itakayofuatia, na kisha kulikabid-hi suala hilo kwake kulitolea hukumu.

Ulikuwa ni ushauri wa busara, na wale wakuu wakaukubali kwa busara. Asubuhi iliyofu-ata ule mlango wa Al-Kaaba ulipofunguliwa, walimuona Muhammad akiingia kupitia hapo. Wote walifurahi kwamba alikuwa ni yeye, na wakakubali wote kurufaisha mgogoro wao kwake, na kukubali uamuzi wake.

Muhammad aliagizia kipande cha nguo kiletwe, na kitandazwe pale chini. Kisha yeye akaliweka lile Jiwe juu yake, na akamwambia kila chifu kunyanyua moja ya pembe zake na kulibeba mpaka chini ya ule ukuta wa Al-Kaaba. Ilipokwisha fanywa hivyo, yeye mwenyewe alilinyanyua lile Jiwe na kuliweka kwenye nafasi yake.

Uamuzi wa Muhammad ulimridhisha kila mmoja. Kwa hekima zake, ameziokoa zile nyuso na ameepusha umwagaji wa damu. Tukio hili pia lilithibitisha kwamba nyakati za migogoro, Waarabu waliheshimu maoni yake. Alikuwa kiongozi wa watu mwenye kipaji.

47

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

KUZALIWA KWA UISLAMU

Tangazo la Muhammad la Ujumbe wake

Wakati Muhammad alipokuwa na umri wa miaka 40, aliamriwa na Allah (s.w.t.) kupitia Malaika Wake Jibril, kutangaza Upweke Wake Allah (s.w.t.) kwa waabudu masanamu na washirikina wa dunia nzima, na kutoa ujumbe wa amani kwa wanadamu waliokaa kivita. Kwa mwitiko wa amri hii ya Mbingnii, Muhammad alianzisha programu nzito sana iit-wayo Uislamu ambayo ilikuwa ibadili mwisho wa mwanadamu daima.

Kabla ya Mwito huo kumjia wa kutangaza Upweke wa Muumba, Muhammad alikuwa na tabia ya kutumia muda wake mwingi katika taamuli na tafakari. Ili kujikinga na kuingili-wa kati na wasiwasi usio na lazima, alikwenda mara kwa mara kwenye pango la mlimani liitwalo Hira, maili tatu kaskazini-Mashariki ya Makka, na kutumia zile siku nyingi za kiangazi pale.

Alikuwa huko Hira pale siku moja yule Malaika Mkuu Jibril alipotokea mbele yake, na kumletea zile habari njema kwamba Mungu amemchagua yeye kuwa Mtume Wake wa Mwisho kwa ulimwengu, na ameweka juu yake jukumu la kuwaongoza wanadamu kuto-ka kwenye msukosuko wa dhambi, makosa na ujinga, kwenda kwenye mwanga wa uon-gofu, Haki na Ujuzi. Jibril kisha akamwambia Muhammad "soma" Aya zifuatazo:

"Soma kwa jina la Mola Wako Aliyeumba. Amemuumba mwanadamu katika pande la damu! Soma, na Mola Wako ni Mtukufu mno. Ambaye Amemfunza

(kuandika) kwa kalamu.

Amemfunza mwanadamu Me asilolijua.

Aya hizi tano zilikuwa ndio wahyi wa mwanzoni kabisa, na zilikuja kwa Muhammad katika "Usiku wa Cheo" au "Usiku Uliobarikiwa" ndani ya mwezi wa Ramadhani (mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislam) wa mwaka wa 40 wa Tembo. Zipo mwanzoni mwa Sura ya 96 ya Qur'an Tukufu. Jina la Sura hiyo ni Iqra'a (soma) au 'Alaq (Pande la damu Iililoganda).

Huu Usiku wa Cheo au Usiku Uliobarikiwa hutokea, kwa mujibu wa Hadith, wakati wa kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhani, na inaweza ikawa mwezi 21, 23,25, au 27 ya mwezi huo.

Katika maelezo yao husika ya mapokezi ya Muhammad ya Wahyi wa Kwanza, Waislamu wa Sunni na Shia hawakubaliani. Kwa mujibu wa Hadith za Sunni, kule kutokea kwa Jibril

48

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kulimshutukiza Muhammad, na alipomwambia Soma, Muhammad alisema, "Siwezi kusoma." Hili lilitokea mara tatu, na kila mara Muhammad alipotamka kutojua kusoma kwake, Malaika huyo alimbana kwa nguvu kwenye kifua chake. Mwishowe, aliweza kurudia Aya hizo tano ambapo Malaika huyo alimwachia na akatoweka.

Pale Malaika Mkuu Jibril alipotoweka, Muhammad, ambaye sasa alikuwa 'amefanywa" Mtume wa Allah (s.w.t.) alishuka kutoka kwenye majabali hayo ya Hira, na akaenda nyum-bani kwake katika hali ya hofu kubwa. Alikuwa anatetemeka kwa baridi, na alipoingia nyumbani kwake, alimuomba mke wake, Khadija, amfunike na blanketi ambavyo alifanya. Alipopata nafuu sawasawa kutokana na mshituko huo, alimwelezea mke wake ile Hadith ya mkutano wake wa ajabu na Malaika Mkuu Jibril ndani ya pango la Hira.

Maelezo ya Hadith ya Sunni juu ya tukio hili yametolewa katika makala iliyoandikwa na Sheikh Ahmad Zaki Hammad, Ph.D, yenye kichwa cha habari Be hopeful, iliyochapishwa kwenye jarida la kila mwezi, Islamic Horizons la Jamii ya Kiislam ya Amerika Kaskazini, Plainfield, Indiana, la Mei-Juni 1987, kama ifuatavyo:

"Mtume (s.a.w.) katika hatua za mwanzo huko Makka, alihofia kwamba ile hali ya Wahyi ilikuwa ni mguso wa uovu uliokuwa ukimuwinda, ukimchezea kiakili, kutibua utulivu wake na amani ya mawazo. Alihofia kwamba huenda moja ya majini limemgusa. Alilieleza hili kwa Khadija. Hofu yake ilizidi kufikia kiasi kwamba - na tafadhali usishangazwe na Hadith sahihi ndani ya Bukhari - Mtume (s.a.w.) alitamani kuua nafsi yake kuliko kuguswa na uovu, kuchezewa, kupotoshwa, au kuchafuliwa."

Lakini kulingana na maelezo ya Waislamu wa Shia, Muhammad Mustafa, kinyume na kushutushwa au kuhofishwa na kutokea kwa Jibril, alimkaribisha kama aliyekuwa akim-tarajia. Jibril alimletea zile habari njema kwamba Allah (s.w.t.) amemchagua yeye kuwa Mtume Wake wa mwisho kwa wanadamu na akampongeza kwa kuteuliwa kuwa mpokea-ji wa heshima kubwa kuliko zote kwa mwanadamu katika dunia hii.

Muhammad hakusita katika kuupokea ujumbe wa Utume wala hakuwa na ugumu wowote katika kurudia zile Aya za Wahyi wa mwanzo. Alizisoma au kuzirudia bila ya taabu yoy-ote, mwenyewe. Jibril, kwa kweli, hakuwa mgeni kwake, na alijua pia kwamba sababu ya kuwepo kwake mwenyewe ilikuwa ni kutekeleza ujumbe uliowekwa juu yake na Allah (s.w.t.) kama Mtume Wake. Alikuwa "mwenye kuuelewa ujumbe" hata kabla ya kufika kwa Jibril. Yeye Jibril alimpa tu ishara ya kuanza.

Waislamu wa Shia pia wanasema kwamba kitu kimoja ambacho Jibril hakuwa akifanye, kilikuwa ni kutumia nguvu za kimwili juu ya Muhammad kusoma. Kama alifanya, itakuwa kwa kweli ni mtindo wa ajabu wa kumpa Muhammad huo uwezo wa kusoma - kwa kum-minya au kumkaba. Wanasisitiza zaidi kwamba Muhammad Mustafa hakuazimia kujiuwa

49

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

katika wakati wowote wa maisha yake, sio hata katika nyakati za huzuni sana; na kwam-ba haijawahi kumjia kwamba angeweza kamwe kuguswa na "uovu" au kwamba angeweza "kupotoshwa" au "kuchafuliwa."

Hata hivyo, Muhammad alihisi wasiwasi juu ya ukubwa wa jukumu lililo mbele yake. Alitambua kwamba katika utekelezaji wa kazi yake, atakuja kukabiliwa na upinzani mkub-wa, mgumu, na uliodhamiriwa wa mapagani wa dunia nzima. Ile hali ya wasiwasi wake ilikuwa karibu kudhihirika. Alikuwa, kwa hiyo, kwenye hali ya uzito wa mawazo alipoon-doka pale pangoni kurudi nyumbani. Na alimuomba Khadija kumfunika ndani ya blanketi wakati akikaa chini kumuelezea yale matukio ya kule Hira.

Khadija alipoisikia Hadith aliyomwambia Muhammad, alimliwaza na kumpa moyo kwa kusema, "Ewe mwana wa ami yangu, kuwa mwenye furaha nzuri, Allah (s.w.t.) amekuch-agua we we kuwa Mtume Wake. Wewe siku zote ni mpole kwa majirani zako, mwenye msaada kwa jamaa zako, mkarimu kwa mayatima, wajane na masikini, na mwenye upen-do kwa wageni. Allah (s.w.t.) kamwe hatakuacha wewe peke yako."

Inawezekana kwamba Muhammad alizidiwa kwa muda kidogo na mawazo juu ya uwa-jibikaji wake kwa Allah (s.w.t.) katika kuubeba mzigo mzito wa jukumu lake jipya, lakini pale aliposikia maneno ya kuliwaza ya Khadija, mara moja alijisikia zile fadhaa zote ndani yake zikipungua. Alimtuliza na kumpa moyo kwamba pamoja na Mkono wa Allah (s.w.t.) juu ya bega lake, atasimama sawia na majukumu yake na ataweza kushinda vikwazo vyote. Baada ya kipindi kifupi, Jibril alitokea tena mbele ya Muhammad wakati alipokuwa ndani ya pango la Hira, na akawasilisha kwake wahyi wa pili:

"Ewe uliyejifunika (shuka). Simama na uonye. Na Mola wako mtukuze. (Sura ya 74; Aya ya 1-3)

Hii amri kutoka Mbinguni ya "simama na uonye" ilikuwa ni ishara kwa Muhammad (aliye-funikwa na shuka) kuanza kazi yake. Jibril alimweleza yeye kazi zake mpya ya kwanza kabisa ilikuwa ni kuangamiza ibada ya miungu ya uongo, na kusimamisha beramu ya Tawhid - imani ya Upweke wa Muumba - ulimwenguni; na alikuwa awaite wanadamu kwenye dini ya Haki - Uislamu. Uislamu maana yake ni kunyenyekea kwa Allah (s.w.t.) na kumkubali Muhammad kama mja na Mtume Wake.

Jioni ile Muhammad alirudi nyumbani mwenye fahamu na dhamira juu ya kazi yake mpya kwamba alikuwa anapaswa kuutangaza Uislamu, na kwamba alikuwa aanzie kutoka nyumbani kwake mwenyewe - kwa kuutangaza kwa mkewe.

50

Usahihi-3.jpg

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Muhammad alimweleza Khadija juu ya kutembelewa kwa mara ya pili na Jibril, na wajibu uliowekwa juu yake na Allah (s.w.t.) wa kumwita yeye Khadija kwenye Uislamu. Kwa Khadija, historia na ukamilifu wa uadilifu wa mume wake vilikuwa ni uthibitisho usiopingika kwamba alikuwa ni mjumbe wa ki-ungu, na aliukubali Uislamu bila kusita. Kwa kweli, kati yake na Uislamu, kulikuwa na "uhusiano wa kiitikadi" fulani uliokuwepo kabla. Kwa hiyo, wakati Muhammad Mustafa alipoleta Uislamu kwake, Khadija "aliutam-bua" mara moja, na akaufuata kwa matumaini. Aliamini kwamba Muumba ni Mmoja, na kwamba Muhammad alikuwa ni Mtume Wake, naye akatamka:

"Nashuhudia kwamba hakuna mungu ila Allah (s.w.t.); na ninashuhudia kwamba Muhammad ni mtumwa na Mtume Wake."

Muhammad; huyu Mtume mpya wa Mungu, alijishindia mfuasi wake wa kwanza - Khadija - mke wake. Alikuwa ndiye wa kwanza, wa kwanza kabisa kuthibitisha imani yake katika Tawhid (Upweke wa Muumba), na alikuwa ndiye wa kwanza kabisa kumkubali Muhammad kama Mtume wa Allah (s.w.t.) kwa wanadamu wote. Alikuwa ndio Mwislamu mwanamke wa kwanza.

Muhammad "aliutambulisha" Uislamu kwa Khadija. Alimuelezea maana yake, na aka-muingiza kwenye Uislamu.

Heshima ya kuwa mtu wa kwanza katika ulimwengu mzima kushuhudia Upweke wa Allah (s.w.t.) na kuukubali utume wa Muhammad, ni ya Khadija kwa wakati wote.

F.E. Peters anasema:

"Yeye (Khadija) alikuwa wa kwanza kuukubali ukweli wake wa wahyi wake (Muhammad), mwislamu wa kwanza baada ya Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Alimtia moyo na kumsaidia Muhammad wakati wa miaka migumu ya mwanzo ya mahubiri yake ya hadhara, na katika miaka ishirini na tano ya ndoa yao hakuoa mke mwingine. Ndoa yao ilikuwa, kwa kiwango chochote cha akili cha kuamua, ni uwiano wa mapenzi na vilevile ubia wa ushirikiano.

(Allah (s.w.t.) 's Commonwealth, New York)

Kama ilivyoonyeshwa kabla, Ali Ibn Abi Talib, alikuwa akiishi wakati huu na walezi wake, Muhammad na Khadija. Wale vijana wawili wa Muhammad na Khadija - Qasim na Abdullah walikwisha kufa katika uchanga wao. Baada ya kifo chao, walimchukua Ali kama mtoto wao. Ali alikuwa na umri wa miaka mitano alipokuja nyumbani kwao, na alikuwa na miaka kumi pale Muhammad alipofanywa Mtume wa Allah (s.w.t.) Muhammad na Khadija walimlea na kumsomesha. Katika miaka iliyofuatia, alijionyesha

51

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

mwenyewe kuwa ni "matokeo" bora sana ya malezi na elimu ile Muhammad na Khadija waliyompa.

Sir William Muir:

'Mara tu baada ya kuijenga upya Al-Kaaba, Muhammad alijiliwaza mwenyewe kwa kupotea kwa mwanae mdogo Qasim kwa kumchukua Ali, mtoto wa rafiki yake na mlezi wake aliyetangulia, Abu Talib. Ali, wakati huu akiwa sio zaidi ya miaka mitano au sita ya umri, alibaki daima baadaye na Muhammad, na walionyeshana upendo wa baba na mwana.'

(The life of Muhammad, London, 1877)

Kwa kuwa Ali alikuwa mmoja wa familia ya Mtume (s.a.w.) mwenyewe, alikuwa bila ya kukwepa, wa kwanza miongoni mwa wanaume kuupokea ujumbe wa Uislamu. Alishuhudia kwamba Mungu ni Mmoja, na kwamba Muhammad alikuwa Mtume Wake. Na alikuwa na shauku ya kusimama nyuma ya Muhammad Mustafa kuswali. Kwa vile Muhammad hakuonekana kamwe kwenye Swala isipokuwa pale Ali alipokuwa pamoja naye.

Mvulana huyu pia alihifadhi Aya za Qur'an Tukufu kila pale ziliposhushwa kwa Muhammad. Kwa namna hii, alikua hasa na Qur'an. Kwa kweli, Ali na Qur'an "vilikua" pamoja kama "mapacha" ndani ya nyumba ya Muhammad Mustafa na Khadija-tul-Kubra. Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.w.t.) alikwishapata mwislamu wa kike wa kwanza kwa Khadija, na mwislamu wa kwanza wa kiume kwa Ali Ibn Abi Talib.

Muhammad Ibn Is'haq anatuambia:

"Ali alikuwa ndiye mwislamu wa kwanza kumwamini Mtume wa Allah (s.w.t.) kuswali naye na kuuamini ujumbe wake mtukufu, alipokuwa ni mvulana wa miaka kumi. Mungu alimpendelea kwa vile alilelewa katika uangalizi wa Mtume (s.a.w.) kabla Uislamu kuanza."

(The life of the Messenger of God)

Muhammad Husein Haykal naye asema:

"Hivyo basi Ali alikuwa ndio kijana wa kwanza kuingia Uislamu. Alifuatiwa na Zayd ibn Harithah, mtumwa wake Muhammad. Uislamu ulibakia umefungiwa ndani ya kuta nne za nyumba moja. mbali na Muhammad mwenyewe, wafuasi wa dini mpya walikuwa ni mkewe, binamu yake, na mtumwa wake."

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

52

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Marmaduke Pickhtalls:

"Wa mwanzo kati ya wafuasi wake (Muhammad) alikuwa ni mke wake, Khadija; wa pili binamu yake wa kwanza Ali, ambaye alimtwaa (kumlea); wa tatu mtumishi wake Zaid, aliyekuwa mtumwa hapo awali."

(Introduction to the Translation of Holy Qur 'an, Lahore, Pakistan, 1975)

Shahidi wa tatu kuukubali Uislamu, alikuwa Zayd ibn Harithah, huria wa Muhammad, na mtu wa nyumba yake.

Tor Andre:

"Zayd alikuwa mmoja wa watu wa mwanzo kuukubali Uislamu, kwa kweli alikuwa wa tatu, baada ya Khadija na Ali."

(Muhammad, the Man and his Faith, 1960)

Ali ibn Abi Talib alikuwa ndio mwanaume wa kwanza kukubali Uislamu, na kutangulia kwake hakuna shaka yoyote. Allama Muhammad Iqbal, yule mshairi-mwanafalsafa wa Indo-Pakistan, anamwita yeye, sio wa kwanza, bali "mwislamu wa mwanzo kabisa."

Ibn Ishaq:

"Kutoka kwa Yahya ibn al-Ash'ath ibn Qays al-Kindi kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake Afiif: Al-Abbas ibn Abdul Muttalib alikuwa rafiki yangu aliyekuwa akienda mara kwa mara Yemen kununua manukato na kuyauza wakati wa maonyesho. Nilikuwa pamoja naye huko Mina, alikuja mtu katika ujana wa maisha yake na akatekeleza kanuni zote za wudhu 'u na kisha akasimama na kuswali. Kisha akatoka mwanamke akachukua wudhu 'u na akasimama na kuswali. Kisha akatoka kijana anayekaribia utu uzima, akachukua wudhu 'u, kisha akasimama na akasali kando yake.

Nilipomuuliza Al-Abbas ni nini kilikuwa kinaendelea, akasema kwamba alikuwa ni mpwa wake Muhammad Ibn Abdullah Ibn Abdul Muttalib, anayedai kwamba Allah (s.w.t.) amemtuma kama Mtume; yule mwingine ni mtoto wa ndugu yangu, Ali Ibn Abi Talib, ambaye amemfuata katika dini yake; yule wa tatu ni mke wake, Khadija binti ya Khuwaylid ambaye pia anamfuata katika dini yake. Afiif alisema baada ya kuwa amekuwa mwislamu na Uislamu ukiwa umejengeka imara moyoni mwake, 'Laiti mimi ningekuwa wa nne!'

(The Life of the Messenger of God)

53

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Shahidi wa nne aliyeukubali Uislamu, ni Abu Bakr, mfanyibiashara wa Makka.

Hapo mwanzoni, Muhammad alihubiri Uislamu kwa siri kwa hofu ya kuamsha uhasama wa waabudu masanamu. Aliwaita tu wale watu kwenye Uislamu ambao alijuana nao yeye binafsi. Inasemekana kwamba kwa juhudi za Abu Bakr, huyu mwislamu wa nne, watu wengine wachache wa Makka pia waliukubali Uislamu. Miongoni mwao walikuwa Uthman bin Affan, Khalifa wa baadae wa Waislamu; Talha, Zubayr, Abdur Rahman bin Auf, Saad bin Abi Waqqas, na Ubaidullah ibn al-Jarrah.

Kwa muda mrefu Waislamu walikuwa wachache kwa idadi na hawakuthubutu kuendesha Swala zao hadharani. Mmoja wa wafuasi wa mwanzo wa Uislamu alikuwa ni Arqam bin Abi al-Arqam, kijana wa ukoo wa Makhzuum. Alikuwa tajiri na akiishi katika nyumba yenye nafasi kubwa katika bonde la Safa. Waislamu walikusanyika kwenye nyumba yake kuswali Swala zao za jamaa. Miaka mitatu ikapita kwa namna hii. Kisha katika mwaka wa nne, Muhammad aliamriwa na Allah (s.w.t.) kuwaita jamaa zake mwenyewe kwenye Uislamu waziwazi.

Usahihi-4.jpg

"Na waonye jamaa zako wa karibu." Sura ya 26; Aya ya 214)

Jamaa zake Muhammad walihusisha watu wote wa Bani Hashim na Bani al-Muttalib. Alimuamuru binamu yake mdogo, Ali, kuwaita wakubwa wao wote kwenye dhifa - watu arobaini.

Wakati wageni wote walipokuwa wamekusanyika kwenye ukumbi katika nyumba ya Abu Talib, na wameshiriki katika mlo wao, Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) akasimama kuongea nao. Mmoja wa wageni hao alikuwa ni Abu Lahab, ami yake Mtume (s.a.w.) kwa upande wa baba yake. Alikuwa amesikia minong'ono ya nini mpwa wake alichokuwa akifanya hapo Makka kwa siri, na yumkini akahisi sababu ya kwa nini amewaalika Bani Hashim kwenye karamu. Mtume (s.a.w.) alikuwa ameanza tu kuongea pale aliposimama; kifidhuli akamkatiza, na yeye mwenyewe akahutubia ule mkusanyiko, akisema:

"Ami zangu, kaka zangu na binamu zangu! Msimsikilize huyu "msaliti," na msiitupe dini ya mababu zenu kama akiwaiteni kutwaa dini mpya. Kama mtafanya hivyo, basi kum-bukeni kwamba mtaamsha ghadhabu za Waarabu wote dhidi yenu. Hamna nguvu za kupi-gana dhidi yao wote. Kwanza kabisa, sisi ni wachache mno. Kwa hiyo, ni kwa faida yenu kuwa imara katika dini yenu ya jadi."

54

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Abu Lahab, kwa hotuba yake, alifanikiwa kuzua mtafaruku na vurugu kwenye mkutano huo hivyo kwamba kila mtu alisimama na kuzunguka na kusukumana. Kisha wakaanza kuondoka, na mara ukumbi ukawa mtupu.

Muhammad, jaribio lake la kwanza la kugeuza kabila lake mwenyewe likashindwa. Lakini bila kuhangaishwa na kizuizi hiki cha kwanza, alimuamuru binamu yake, Ali, kuwaalika wageni walewale kwa mara ya pili.

Siku chache baadae wageni wale wakaja, na walipokwisha kula chakula cha jioni, Muhammad alisimama na kuzungumza nao kama ifuatavyo:

"Ninamshukuru Allah (s.w.t.) kwa rehma zake. Namhimidi Allah (s.w.t.) na ninaom-ba mwongozo wake. Ninamuamini Yeye na ninaweka dhamana yangu Kwake. Ninashuhudia kwamba hakuna mungu ila Allah (s.w.t.); Hana mshirika; na mimi ni Mtume Wake. Allah (s.w.t.) ameniamuru mimi niwaiteni ninyi kwenye dini Yake kwa kusema: "Waonye jamaa zako wa karibu'. Mimi, kwa hiyo, ninawaonya, na kuwatak-eni ninyi mkiri kwamba hakuna mungu ila Allah (s.w.t.) na kwamba mimi ni Mtume Wake.

"Enyi wana wa Abdul Muttalib! hakuna yeyote aliyewahi kuja kwenu kabla na kitu chochote bora kuliko kile nilichokuleteeni mimi. Kwa kukikubali kwenu, mambo yenu yatahakikishwa hapa duniani na kesho Akhera. Ni nani kati yenu atanisaidia katika kutekeleza kazi hii muhimu? Nani miongoni mwenu atasaidiana pamoja nami katika kutekeleza kazi hii nzito? Nani ataitikia mwito wangu? Ambaye atakuwa khalifa wangu, makamu wangu na waziri wangu?"

Walikuwepo wageni arobaini katika ukumbi huo. Muhammad alisita kidogo kuacha uzito wa maneno yake uingie kwenye mawazo yao lakini hakuna mtu kati yao aliyejibu. Mwishowe kimya kilipokuwa kizito mno, kijana Ali akasimama na kusema kwamba atam-saidia Mtume wa Allah (s.w.t.); angeshiriki katika uzito wa kazi yake; na angekuwa Khalifa wake, makamu na waziri wake. Lakini Muhammad alimuashiria akae chini, na akasema: "Subiri! Pengine mtu mzima kuliko wewe ataitika mwito wangu."

Muhammad alirudia mwaliko wake lakini bado hakuna hata mmoja aliyeelekea kushtuka, na alikaribishwa tu na kimya chenye wasiwasi. Kwa mara nyingine tena, Ali akajitolea msaada wake lakini Mtume (s.a.w.) bado akitaka kwamba mtu mzima wa ukoo wake angeweza kukubali mwaliko wake, na akamuomba Ali asubiri. Yeye tena akatoa ombi hilo kwa ukoo wake kwa mara ya tatu kufikiria mwaliko wake, na yakatokea yaleyale. Hakuna mtu katika mkutano ule aliyeonyesha shauku. Alilichunguza lile kundi na kumtupia macho kila mmoja kati yao lakini hakuna aliyetikisika. Baada ya muda mrefu akauona mwili pekee wa Ali akinyanyuka kwenye mkutano ule wa watu wakimya, kujitolea msaada wake kwake. Safari hii Muhammad alikubali kujitolea kwa Ali. Alimvuta karibu, akamkumbat-

55

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ia kifuani kwake, na akauambia mkutano: "Huyu ni waziri wangu, mrithi wangu na Khalifa wangu. Msikilizeni na mtii amri zake."

Edward Gibbon:

"Miaka mitatu ilitumika kimya kimya katika ubadilishaji wa watu kumi na nne waliobadili dini, matunda ya awali ya ujumbe wake Muhammad; Lakini katika mwaka wa nne alirudia tena kazi yake ya utume, na kwa kuazimia kuwapa familia yake ule mwanga wa haki tukufu, alitayarisha karamu ya kuwakaribisha wageni arobaini wa kizazi cha Hashim. 'Marafiki na ndugu zangu,' Muhammad aliuambia mkusanyiko huo, 'Ninakupeni ninyi, na ni mimi pekee ninayeweza kuwapeni, zawa-di iliyo bora sana, hazina za dunia hii na ijayo. Allah (s.w.t.)ameniamuru niwaiteni kwenye utumishi Wake. Nani miongoni mwenu atanisaidia katika kazi hii? Ni nani kati yenu atakayekuwa mwenzangu na waziri wangu?'

Hakuna jibu lililorudishwa, mpaka kimya cha kushangaza na mashaka, na aibu baada ya muda mrefu ilivunjwa na ujasiri wa haraka wa Ali, kijana aliyekuwa katika mwaka wa kumi na nne wa umri wake. 'Ewe Mtume' alisema, 'Mimi ndimi. Yeyote atakayes-imama dhidi yako, nitayang'oa meno yake, nitayapasua macho yake, nitavunja miguu yake, nitararua tumbo lake. Ewe Mtume, mimi nitakuwa waziri wako juu yao.' Muhammad alikubali ahadi yake kwa furaha, na Abu Talib kwa kejeli sana alishauri-wa kuheshimu hadhi ya juu ya mwanae."

(Decline and Fall of the Roman Empire) Washington Irving:

Enyi wana wa Abd al-Muttalib,' aliita Muhammad kwa shauku, 'kwenu ninyi, kati ya watu wote, Allah (s.w.t.) ametoa zawadi hizi zenye thamani kubwa. Kwa Jina Lake ninakupeni neema za dunia hii, na furaha ya milele ya Akhera. Nani kati yenu atashirikiana nami katika uzito wa ahadi yangu? Nani atakuwa ndugu yangu, msaidizi wangu na waziri wangu?'Wote walibakia kimya; wengine wakistaajabu; wengine wakitabasamu kwa mshangao na dhihaka.

Mwishowe Ali, akianza kwa ghera ya ujana, alijitolea binafsi kumtumikia Mtume ingawa kwa wastani akitambua ujana wake na udhaifu wake wa kimwili. Muhammad akatupa mikono yake kumzunguka kijana huyu mkarimu, na kumkumbatia kifuani mwake. 'Muoneni ndugu yangu, waziri wangu, khalifa wangu' aliguta, 'Wote msikie maneno yake, na mumtii.' ".

(The Life of Muhammad)

56

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Sir Richard Burton:

"Baada ya muda mrefu wa kutafakari, kwa kuchochewa na hasira za ushupavu wa kipumbavu wa Wayahudi, ushirikina wa Wasyria na Wakristo wa Kiarabu, na kule kuabudu masanamu kunakochukiza kwa watu wasioamini wa nchi yake, mwenye shauku pia - na ni moyo gani mkuu usiokuwa na shauku? - Yeye (Muhammad) alid-hamiria kurekebisha maovu yale ambayo yalisaidia wahyi kudharaulika kwa wasomi na wenye madhara kwa washenzi. Alijitambulisha kama aliyejaaliwa katika ujumla wa jamaa zake na wenzake katika ukoo. Hatua hiyo ilishindwa, isipokuwa kwamba ilimpatia mtu aliyesilimu mwenye thamani ya askari wa farasi elfu moja ambaye ni Ali, mwana wa Abu Talib."

(The Jew the Gypsy and El Islamu, San Francisco, 1898)

Ali amejitolea huduma zake kwa Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) na Mtume (s.a.w.) alimkubali. Kwa watu wazima wa kabila hilo, tabia ya Ali ingeweza kuonekana ya pupa na yenye kushupaa lakini mara alithibitisha kwamba alikuwa na ujasiri na uvumilivu wa kutimiza, mkubwa zaidi kuliko waliokuwa nao wengine, ushujaa huo hata kuota. Mtume wa Allah (s.w.t.) kwa upande wake, aliupokea msaada huo sio tu na muonekano wa shukrani na furaha bali pia alitamka kwamba Ali alikuwa, kutoka muda ule, Khalifa wake.

Tamko la Muhammad lilikuwa la wazi na lisilo na mashaka. Ni upuuzi kubishana, kama watu wengine wanavyofanya, kwamba ukhalifa wa Ali kwa Muhammad, ulikomea kwenye kabila la Bani Hashim. Lakini Muhammad mwenyewe hakuuwekea mipaka ukhalifa wa Ali kwa Bani-Hashim. Ali alikuwa Khalifa wake kwa Waislamu wote na kwa wakati wote.

Ile karamu ambayo Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) alimtangaza Ali kama mrithi wake, ni maarufu katika historia kwa jina la karamu ya Dhul- 'Ashiir - "karamu ya jamaa wa karibu." Jina hili limetoka kwenye Qur'an tukufu yenyewe (Sura ya 26; Aya ya 214). Ajabu, Sir William Muir ameliita tukio hili la kihistoria "lisiyothibitishwa." Lakini ni nini "kisichothibitishwa" au kisicho yamkini kiasi hicho kuhusiana na hilo? Kuna kitu kinaweza kuwa na mantiki zaidi kwa Mtume wa Allah (s.a.w.) kuliko kuanza kazi yake ya kuhubiri Uislamu nyumbani kwake mwenyewe, na watu wa familia yake mwenyewe na ukoo wake mwenyewe, hasa baada ya kuamriwa kwa dhati na Allah (s.w.t.) kuwaonya jamaa zake wa karibu?

Ile karamu ya Dhul- 'Ashiir ambayo Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) alimteua Ali ibn Abi Talib, kama mrithi wake, ni tukio la kihistoria, na usahihi wake umethibitishwa, mion-goni mwa wengine, na wanahistoria wa Kiarabu wafuatao:

57

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

1. Tabari, Tarikh, juz. 2, uk. 217

2. Kamil ibn Athir, Tarikh, juz. 2, uk. 22

3. Abul Fida, Tarikh, juz.1, uk.116

Sir William Muir:

"Binamu yake (Muhammad), Ali, sasa akiwa na umri wa miaka 13 au 14, tayari ali-toa dalili za hekima na uamuzi ambao ulimbainisha yeye katika maisha ya baadae. Ingawa alikuwa ana juhudi isiyoshindika, alikosa nguvu ya msukumo ambayo ingem-fanya kuwa mhubiri wa Uislamu mwenye kufaa sana. Alikua tangu utotoni katika dini ya Muhammad, na uhusiano wake wa mapema uliimarisha misimamo ya miaka ya ukubwani."

(The Life of Muhammad, London, 1877)

Tunayo mashaka mengi sana kuhusu kauli ya Sir William Muir kwamba Ali "alikosa nguvu ya msukumo ambayo ingemfanya yeye kuwa mhubiri wa kufaa sana wa Uislamu." Ali hakukosa nguvu wala kitu kingine chochote. Katika upeo wa migogoro yote ya Uislamu, alichaguliwa kutekeleza yale majukumu ya hatari kabisa, na kila wakati aliya-timiza.

Kama mhubiri, vilevile Ali alikuwa bila kifani. Hakukuwa na yeyote kati ya maswahaba wote wa Mtume (s.a.w.) aliyekuwa mhubiri mwenye nguvu kuliko yeye. Alizitangaza rasmi zile Aya 40 za mwanzo za Surat Bara'a (Tawba), ile Sura ya tisa ya Qur'an Tukufu, kwa mapagani huko Makka, kama mhubiri wa kwanza wa Uislamu, na kama mtu anayemuwakilisha Mtume wa Allah (s.a.w.) binafsi. Na alikuwa ni Ali aliyeyaingiza mak-abila yote ya Yemen katika Uislamu.

Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) , alimlelea Ali kama mtoto wake mwenyewe, na kama Ali alikosa chochote, yeye Mtume (s.a.w.) angekijua. Alimtangaza Ali kuwa waziri wake, mrithi wake na Khalifa wake katika wakati ambao hakuna ambaye angeweza kubashiri ile hali ya baadae ya Uislamu. Hii inaonyesha tu uhakika usio na kikomo ambao Mtume wa Uislamu aliokuwa nao juu ya mvulana huyu wa miaka kumi na minne.

Ali aliashiria matarajio na matumaini ya Uislamu. Katika mapinduzi makubwa ambayo Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliyaanzisha pale kwenye karamu ya Dhul- 'Ashiira, alihamasisha ule uwezo, udhanifu, na ari na juhudi za ujana; Ali alikuwa mfano wa yote haya.

Mambo mawili yalitokea pale kwenye Karamu. Moja lilikuwa kwamba Mtume (s.a.w.) ali-utoa nje Uislamu kwenye uwazi. Uislamu haukuwa tena harakati ya "siri"; ulikuwa

58

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

"umeibuka." Kwenye karamu ya jamaa zake wa karibu, Muhammad alikuwa "amejiingiza katika jambo" na sasa hakungeweza kuwa na kugeuka nyuma. Wakati ulikuwa umek-wishafika wa kuutoa ujumbe wa Uislamu nje ya ukoo wake mwenyewe, kwanza kwa Maquraishi wa Makka, kisha kwa Waarabu wote, na hatimae, kwa dunia yote iliyobakia. Jingine lilikuwa kwamba alimpata Ali ambaye alikuwa ndiye mfano halisi wa shauku, kuji-tolea na ushupavu, na alikuwa na thamani kubwa zaidi kuliko askari wa farasi elfu moja.

Imeelezwa kwamba siku kadhaa baada ya ile karamu ya Dhul- 'Ashiira ya pili, Muhammad alipanda kile kilima cha Safa karibu na Al-Kaaba, na akaita: "Enyi wana wa Fihr, Enyi wana wa Lui, Enyi wana wa Adi, na Quraishi wote waliobakia! Njooni hapa, na munisik-ilize. Nina kitu muhimu sana cha kuwaambieni ninyi."

Wengi wa watu wale wa Makka waliosikia sauti yake, walikuja kumsikiliza. Akiwahutubia, alisema: "Mtaniamini kama ingekuwa niwaambie kwamba kuna jeshi lime-jificha nyuma ya vilima vile, na lilikuwa likiwatazameni ili kuwashambulieni mara tu litakapowaona tu hamkujilinda?" Walisema wangemuamini kwa sababu hawajamsikia akisema uongo.

"Kama hivyo ndivyo," alisema Muhammad, "basi sikilizeni hili kwa makini. Mola wa Mbingu na Ardhi ameniamuru mimi kuwaonyeni ninyi juu ya wakati wa kuogopesha sana unaokuja. Lakini kama mtakuwa wasikivu, mtaweza kujiokoa wenyewe na laana ya milele..." Alikuwa amefikia hapo tu wakati Abu Lahab, ambaye alikuwepo miongoni mwa wasikilizaji hao, alipomuingilia kati tena kwa kusema: "Kifo juu yako! Umepoteza muda wetu kutuambia hili tu? Hatutaki kukusikia. Usituite tena."

Kuanzia hapo Abu Lahab akafanya ni mazoea ya kumfuata Mtume (s.a.w.) kila alipokwen-da. Kama alianza kusoma Qur'an au kusema kitu kingine, yeye Abu Lahab alimkatiza au alianza kumsumbua. Chuki ya Abu Lahab kwa Muhammad na Uislamu aliichangia na mkewe, Ummu Jameel. Wote walikuwa wenye kulaaniwa na Allah (s.w.t.) ndani ya Qur'an Tukufu (Sura ya 111).

59

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

WALIOSILIMU MWANZONI NA MATESO KUTOKA KWA WAPAGANI

Ingawa Abu Lahabi mara nyingi alifanikiwa katika kuyatawanyisha yale makundi yaliyokusanyika kusikiliza waadhi za Mtume, habari hata hivyo zilienea Makka kuhusu mawaidha hayo. Baadhi ya watu walizungumza kuhusu ujumbe wa Uislamu. Wale wenye fikra miongoni mwao waliuliza hili swali: "Ni dini gani hii ambayo Muhammad anatuitia sisi?" Swali hili lilionyesha udadisi kwa upande wao kuhusu huu ujumbe wa Uislamu, na wachache miongoni mwao walitaka kujua zaidi juu yake.

Katika siku zilizofuata, Muhammad alifanya majaribio mengi ya kuwahubiria watu wa Makka. Abu Lahab na mshirika wake, Abu Jahal, walifanya kila walichoweza kuihujumu kazi yake lakini hawakuweza kumkengeusha kutoka kwenye shabaha yake.

Muhammad, rehma na amani ziwe juu yake na kizazi chake, alitambua kwamba kazi yake haitakuwa rahisi. Alijua kwamba atakumbana na vikwazo vingi, na kwamba atakuwa apambane na upinzani mkali na wa kudumu wa waabudu masanamu. Lakini alitegemea rehma za Mungu kumuwezesha kuushinda upinzani.

Ulikuwa ni ujumbe wa ajabu ambao Muhammad alileta kwa Waarabu, na ulikuwa wa kipekee. Hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kusikia kitu kama hicho kabla. Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) aliwaambia Waarabu wasiabudu kundi la vitu visivyo na uhai vilivyotengenezwa kwa mawe au magogo (miti) ambavyo wameviunda wenyewe, na ambavyo havikuwa na uwezo wa ama kuwapa wao chochote au kuchukua chochote kutoka kwao. Badala yake, aliwaambia, wanapaswa kutoa utii wao kwa Allah (s.w.t.) Mola wa ulimwengu wote. Aliwaambia pia kwamba katika macho Yake, katika macho ya Muumba wao, wote walikuwa sawa, na kama watakuwa Waislamu, watakuwa wote ni ndugu wa kila mmoja wao.

Muhammad pia alipenda kuirekebisha jamii ya Kiarabu. Hii sheria mpya ambayo ameiwe-ka mbele kwa ajili ya madhumuni Haya, ilifanya Imani badala ya damu, kuwa kiungo maalum cha jamii hiyo. Lakini Waarabu hao wamezaliwa katika mfumo wa mila na des-turi za kipagani; waliamini katika msingi wa miundo ya kikabila na udugu. Kwao wao "damu" ilikuwa tu ni kigezo cha mpangilio wa kijamii. Katika mawazo yao, kama dini ingeruhusiwa kuchukua nafasi ya damu katika mgawanyo huu, ingeweza kuvuruga muun-do wote wa jamii ya Kiarabu.

Muhammad pia aliwataka wale Waarabu matajiri kugawana utajiri wao na masikini na wale wenye kipato cha chini. Wale masikini, alisema, walikuwa na haki ya kupokea fungu

60

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

lao kutoka kwenye mali ya matajiri. Ugawanaji huo, aliendelea kusema, utahakikisha ugawaji wa haki wa mali katika jamii.

Wengi wa Waarabu matajiri walikuwa wakopesha-fedha; ama hasa, walikuwa "wala riba wakubwa." Wamekuwa matajiri kwa kukopesha fedha kwa watu masikini kwa viwango vikubwa sana vya riba. Wale masikini hawakuweza kamwe kulipa madeni yao, na kwa hiyo wakanasa katika utumwa wa kiuchumi milele. Kugawana mali yao ya haramu na watu walewale waliokuwa wakiwanyonya, ilikuwa kwao ni sawa na "kufuru." Kwa kuwapen-dekezea kwamba wagawane mali yao na masikini, Muhammad alichezea kiota cha nyigu!

Kwa Waarabu, yote haya yalikuwa mambo mapya na yasiyojulikana; kwa kweli yalikuwa ya kimapinduzi. Kwa kuhubiri mambo ya kimapinduzi kama haya, Muhammad ali-wakasirisha wale wenye madaraka tangu zamani. Waliokasirika sana miongoni mwao ni ule ukoo wa Umayya wa Maquraish. Watu wake ndio waliokuwa wala-riba wanaoongoza na mabepari wa Makka, na walikuwa ndio makuhani wakuu wa hekalu la wapagani. Ndani ya Muhammad na huo ujumbe wa Uislamu, waliona tishio kwenye utaratibu wao wa kijamii ambao uliegama kwenye heshima na nguvu.

Wao, kwa hiyo, waliamua kudumisha hali kama ilivyo. Katika miaka iliyokuja, walikuwa waunde kikosi cha vita visivyotulizika dhidi ya Uislamu, na upinzani wa kufa baada ya mapambano na Muhammad.

Lakini walikuwepo pia watu wachache walioona mvuto wenye nguvu katika yale mawazo mapya ambayo Muhammad alikuwa anayaanzisha, kwa ujumla yakiitwa Uislamu. Kwa kweli, waliyaona ni yasiyokanika, na kwamba waliyakubali.

Miongoni mwa waliosilimu mwanzo kwenye Uislamu walikuwa Yasir; mke wake, Sumayya; na mtoto wao wa kiume, Ammar. Walikuwa ndio ukoo wa kwanza ambao watu wake wote waliukubali Uislamu sawia, hivyo kuwa Familia ya Kiislam ya Kwanza.

Uislamu ulikuwa na mvuto maalum kwa matabaka ya waliokandamizwa hapo Makka. Pale watu wa matabaka haya walipokuwa Waislamu, walitambua pia kwamba kama wapagani, walidharauliwa na kutengwa na tabaka la juu la wenye kujali tabaka na wenye kujali utaifa wa hali ya juu wa Makka lakini Uislamu uliwapa kujiheshimu kupya. Kama Waislamu waliona fahari mpya ndani yao wenyewe.

Wengi wa waliosilimu mwanzo walikuwa "masikini na wanyonge." Lakini walikuwepo Waislamu wachache matajiri pia kama Hudhayfa bin Utba na Arqam bin Abil-Arqam. Na wale watu wote ambao Abu Bakr aliwaleta kwenye Uislamu - Uthman, Talha, Zubayr, Abdur Rahman ibn Auf, Saad ibn Abi Waqqas na Abu Ubaidah ibn al-Jarrah - walikuwa pia ni matajiri na wenye nguvu. Walikuwa ni watu wa koo mbalimbali za Kiquraish.

61

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Tunaweza kuchukulia kwamba pale mwanzoni, lile tabaka la juu la wapagani wa Makka lilishuhudia zile juhudi za Uislamu za kutaka kupata kutambuliwa zaidi kwa burudani kuliko kwa kero, bila ya kuzungumzia zile chuki na mpagao uliowashika baadae kidogo. Lakini jinsi harakati hii mpya ilivyoanza kushika kasi, walihisi kwamba yale mawazo ambayo Muhammad alikuwa akiyatangaza, yalikuwa kwa kweli ni "hatari," na hayakuwa na chochote cha kichekesho juu yake. Walihoji kwamba mababu zao wameabudu masana-mu kwa vizazi visivyo na idadi, kwa hiyo ibada ya masanamu ilikuwa ni sawa; na hawakuweza kumruhusu Muhammad kucheza na mtindo wao wa ibada.

Lakini Muhammad hakuridhika tu kukanusha ibada ya masanamu. Ya hatari zaidi na ya kutisha kwa Bani Umayya wenye-uchu wa mali ilikuwa ni mawazo yake ya haki za kiuchumi na jamii yaliyotishia kuangusha ngome yao ya heshima; muundo wa zamani wa madaraka na kundi la watu wenye madaraka; na taasisi zote za zamani zilizopitwa na wakati. Waliweka wazi, kwa hiyo, kwamba heshima ilikuwa ni kitu ambacho hawatakiacha - kwa gharama yoyote ile - iwe jahannam au maji marefu.

Lakini wazo moja ambalo lile tabaka la juu lililojichagua lenyewe la Quraish, lililoliona la kufedhehesha zaidi, lilikuwa ni ile "dhana" iliyopangwa na Muhammad, kwamba wale watu wa matabaka ya waliokandamizwa, waliodharauliwa, walionyonywa, wengi wao wakiwa watumwa wao, ambao sasa wamesilimu, wamekuwa wanaolingana - walinganao na Maquraish wakubwa na wenye nguvu! Dhana yao kuu ya maisha ilikuwa ni majigam-bo na makuu, na usawa na watumwa wao wenyewe, walio achwa-huru na watumishi, ulikuwa kwao hauwaziki kabisa. Walikuwa wamejawa na ghiliba ya "ubora" wao binafsi kuliko wanadamu wote.

Kwa kutangaza rasmi hii kanuni ya "kinyume" ya usawa - usawa wa bwana na mtumwa, tajiri na masikini; na Mwarabu na asiyekuwa Mwarabu; kwa kukana madai ya ubora wa ukoo, na kufundisha kwamba mbele ya Allah (s.w.t.) hali ya muumini ilikuwa ya juu sana kuliko hali ya wasioamini wote katika dunia, Muhammad alitenda "uhaini" dhidi ya Maquraish!

Maquraish waliabudu masanamu mengi sana, na utaifa ilikuwa mojawapo.

Lakini kujivunia utaifa hakuthaminiwi katika Uislamu. Kwa mujibu wa Qur'an Tukufu, watu wote wametokana na Adam, na Adam alikuwa ni udongo. Ibilisi (Shetani) alilaaniwa kabisa kwa sababu alihoji ubora wa kile alichodhania kuwa asili yake ni ya juu kama kinyume na alichokiona kuwa uchini sana wa asili ya mwanadamu. "Mwanadamu," alise-ma, "ameumbwa kwa udongo ambapo mimi nimeumbwa kutokana na moto." Hisia kama hizi za utenganishaji ambazo huja pia kwa wanadamu hasa kwa nia ya kudai hadhi bora ya damu katika utu wao, zimekataliwa na Uislamu kwa nguvu kabisa. Uislamu umeangusha chini umaarufu wa utaifa, rangi na heshima, na umewakataza Waislamu

62

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kuwagawa watu katika makundi kwa misingi ya damu na/au ujirani wa kijografia au hadhi maalum ambazo wanaweza kuzidai juu yao wenyewe.

Machoni mwa Qur'an, mtu aliye bora sana ni yule muttaqi - yaani, mtu ambaye anampen-da na kumtii Allah (s.w.t.) wakati wote. Katika Uislamu, kipimo pekee cha ubora wa mtu, ni mapenzi yake kwa Muumba. Mitihani mingine yote ya maisha binafsi haina maana yoy-ote.

Lakini kama ilivyoelezwa hapo juu, Maquraish hawakuwa katika hali ya kupokea mawa-zo haya. Pengine walikuwa kiufahamu hawawezi kuyazingatia haya. Waliyaona kama ni kufuru ya daraja, na kwa hiyo, yasiyoweza kuvumilika kabisa. Ulikuwa ni wakati huo basi pale walipoamua sio tu kumpinga Muhammad, Mtume wa Uislamu, bali pia kuangamiza huo "uasi" ulioitwa Uislamu wenyewe kabla haujaota mizizi na kuwa wenye kuji-tosheleza.Walisukumwa na Kiburi - majivuno yanayojijaza yenyewe kuzidi kipimo cha mwanadamu - na kwa tamaa ya madaraka kufanya uamuzi kama huo dhidi ya Muhammad na Uislamu.

Wakiwa na uamuzo huu, Maquraish walitangaza nia yao ya kupigana katika kulinda masanamu yao na miungu yao na vilevile katika ulinzi wa mfumo wao wa kiuchumi na kijamii.

Makka ilikuwa katika hali ya kivita!

Maquraish walifungua mapambano dhidi ya Uislamu kwa kuwabughudhi na kuwatesa Waislamu. Mwanzoni, mateso yaliishia kwenye kuzomea na kebehi na matusi. Lakini kiasi muda ulivyoendelea mbele, makafiri hao walitoka kwenye ukali wa maneno kwenda kwenye ukali wa matendo. Walijizuia kuumiza majeraha ya mwili juu ya Muhammad mwenyewe kwa hofu ya kuchochea visasi; lakini hawakuwa na kusita katika kuwaumiza Waislamu, askari wa kawaida. Kwa muda mrefu, walikuwa ni hawa askari wa kawaida waliobeba sehemu kubwa ya ghadhabu za Maquraish.

Ibn Ishaq:

"Kisha Maquraish wakawachochea watu dhidi ya maswahaba wa Mtume (s.a.w.) ambao wamekuwa Waislamu. Kila kabila liliwashambulia Waislamu miongoni mwao, wakiwapiga na kuwashawishi kutoka kwenye dini yao. Mungu alimkinga Mtume wake kutokana nao kupitia ami yake (Abu Talib), ambaye, alipoona kile Maquraish walichokuwa wakikifanya, aliwaita Bani Hashim na Bani Muttalib kusi-mama naye katika kumkinga Mtume. Hili walikubaliana kulifanya, isipokuwa Abu Lahab."

(The Life of the Messenger of God)

63

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Baadhi ya waathirika wa mateso:

Bilal, yule aliyekuwa mtumwa wa Kihabeshi wa Umayya bin Khalaf. Umayya na makafiri wengine walimtesa katika mwanga mkali wa jua la moto sana la Makka, na wakamtesa kupita kiasi cha uvumilivu wa binadamu. Lakini aliimarishwa na asili ya nguvu za ndani na ujasiri ambavyo kamwe havikumvunja moyo. Kumpenda Allah (s.w.t.) na mapenzi kwa Mtume Wake vilimuwezesha kuyavumilia mateso kwa furaha. Abu Bakr akamnunua kuto-ka kwa bwana wake na akamwacha huru. Mtume (s.a.w.) alipohamia Madina, alimteua Bilal kuwa Muadhini wa kwanza wa Uislamu. Sauti yake kubwa yenye kuvuma ilisikika kwenye anga la Madina kwa ukelele wa Allah-u-Akbar (Mungu ni Mkubwa).

Katika miaka ya baadae, wakati utekaji wa peninsula ulipokamilika, Mtume wa Allah (s.w.t.) alimchagua Bilal kuwa katibu wake wa hazina.

Khabab ibn el-Arat. alikuwa ni kijana wa miaka ishirini aliposilimu. Alikuwa mtegemezi wa Banu Zuhra. Maquraish walimtesa siku baada ya siku. Alihama pamoja na Mtume (s.a.w.) kwenda Madina.

Suhaib bin Sinan, alikuwa ametekwa na kuuzwa kama mtumwa na Wagiriki. Alipokuja kuwa mwislamu, Maquraish walimpiga kikatili sana lakini hawakuweza kuitingisha imani yake.

Abu Fukaiha, alikuwa mtumwa wa Safwan bin Umayya. Alisilimu katika wakati mmoja na Bilal. Kama Bilal, aliburuzwa pia na bwana wake katika mchanga wa moto akiwa ame-fungwa kamba miguuni mwake. Abu Bakr alimnunua na kumpa uhuru. Alihamia Madina na Mtume (s.a.w.) lakini akafa kabla ya vita vya Badr.

Lubina, alikuwa mtumwa wa kike wa Mumil bin Habib. Amin Dawidar anaandika katika kitabu chake, Pictures From the Life of the Prophet (Cairo, Egypt, 1968), kwamba Umar bin al-Khattab, khalifa wa baadae wa Waislamu, alimtesa, na kila alipopumzika, alisema: "Sikuacha kukupiga kwa sababu ya huruma. Nimesimama kwa sababu nimechoka." Alirudia kumpiga baada ya kupumzika. Abu Bakr alimnunua na akamuacha huru.

Zunayra, alikuwa mtumwa mwingine wa kike. Alipotangaza imani yake katika Uislamu, Umar ibn al-Khattab, na Abu Jahl, walipokezana katika kumtesa mpaka akawa kipofu. Amin Dawidar anaeleza kwamba miaka mingi baaadae alirudia kuona tena, na Maquraish wakakuhusisha kupona huku na "uchawi" wa Muhammad. Abu Bakr akamnunua na kumwacha huru.

Nahdiyya na Ummu Unays walikuwa ni watumwa wengine wawili wa kike ambao walikuja kuwa Waislamu. Mabwana zao waliwatesa kwa kuukubali Uislamu. Abu Bakr aliwanunua na akawapa uhuru wao.

64

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Walikuwepo Waislamu wengine ambao hawakuwa watumwa bali walikuwa "masikini na wanyonge." Wao pia walipata mateso. Miongoni mwao walikuwa ni Ammar ibn Yasir na wazazi wake. Mtu mwingine wa kundi hili alikuwa ni Abdullah ibn Masud, kijana wa Kiislam. Alitambulikana miongoni mwa maswahaba wa Mtume (s.a.w.) kwa elimu yake na maarifa, na alikuwa mmoja wa mahafidh (wa Qur'an kwa kichwa) wa mwanzoni katika Uislamu, kila Aya mpya ilipoteremshwa, aliisikia kutoka kwa Mtume (s.a.w.) na akaikariri.

Imeelezwa kwamba wakati Surat Rahman (Sura ya 55) iliposhuka, Mtume wa Allah (s.w.t.) aliwauliza maswahaba zake, ni nani miongoni mwao angekwenda kwenye Al-Kaaba na kuisoma mbele ya makafiri. Masahaba wengine walirudi nyuma lakini Abdullah ibn Masud akajitolea kwenda. Alikwenda kwenye Al-Kaaba na akaisoma Sura hiyo mpya kwa sauti kubwa. Baada ya Mtume (s.a.w.) mwenyewe, Abdullah ibn Masoud alikuwa ndiye mtu wa kwanza kusoma Qur'an ndani ya Al-Kaaba mbele ya kundi lenye uhasama la makafiri. Hawa makafiri walimponda mara kwa mara lakini hawakuweza kumtishia kuwa kimya.

Ibn Ishaq anasema:

"Yahya ibn Urwa ibn al-Zubayr aliniambia, kama kutoka kwa baba yake kwamba mtu wa kwanza kusoma Qur'an kwa sauti hapo Makka, baada ya Mtume (s.a.w.) mwenyewe alikuwa ni Abdullah ibn Masud."

(The Life of the Messenger of God)

Mwanachama mwingine wa kundi hili alikuwa Abu Dharr al-Ghiffari. Alikuwa wa kabi-la la Ghiffar ambalo liliishi maisha yao kwa unyang'anyi. Kutoka kwa wasafiri alisikia kwamba ametokea Mtume (s.a.w.) hapo Makka ambaye amewashauri Waarabu kutupilia mbali ibada ya masanamu, na kumuabudu Allah (s.w.t.) peke yake, kutosema chochote ila kweli tupu, na kutowazika mabinti zao wakiwa hai. Alijihisi kwamba amevutiwa sana na Mtume huyu, na akasafiri kwenda Makka kuthibitisha ukweli wa taarifa alizozisikia kuhusu yeye.

Huko Makka alikuwa mgeni. Alikwisha kusikia kwamba Muhammad amekwishajifanyia maadui wengi mwenyewe kwa kuhubiri kinyume na ushirikina wa Kiarabu. Yeye, kwa hiyo, alisita kumuuliza mtu yeyote kumhusu Muhammad. Aliitumia siku nzima kwenye kivuli cha Al-Kaaba kuangalia wapita njia. Wakati wa jioni, Ali ibn Abi Talib alibahatika kupita hapo alipokuwa. Ali aligundua kwamba Abu Dharr alikuwa mgeni pale mjini, na akamkaribisha nyumbani kwake kwa ajili ya chakula cha jioni.

Abu Dharr akaukubali mwaliko huo, na baadae alimwelezea Ali juu ya madhumuni ya kutembelea kwake Makka. Ali, kwa kweli, alifurahi sana kumuelekeza mgeni wake mbele

65

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ya bwana wake, Muhammad Mustafa. Abu Dharr alijifunza kutoka kwa Mtume wa Allah (s.w.t.) maana ya ujumbe wa Uislamu. Aliona vyote, Mtume (s.a.w.) na ujumbe wake havikataliki. Alivutiwa na ile nguvu ya mvuto ya Uislamu. Baada ya kusilimu, kitu cha kwanza kabisa ambacho alitaka kufanya ni kuwakataa katakata makafiri. Alikwenda kwenye Al-Kaaba na kusema kwa sauti kubwa:

"Hapana mungu ila Allah (s.w.t.), na Muhammad ni Mtume Wake."

Kama ilivyotarajiwa, makafiri hao wakamvamia, na wakaanza kumuangushia vipigo juu yake. Kutoka kwenye ghasia hizi aliokolewa na Abbas ibn Abdul Muttalib, ami yake Mtume. Aliwaambia wale watu wa Makka kwamba Abu Dharr alikuwa wa kabila la Ghiffar ambao eneo lao limelala kutagaa zile njia za misafara kwenda kaskazini, na kama watamfanyia madhara yoyote, watu wa kabila lake watazuia upitaji wa misafara yao ya biashara kwenda Syria.

Abu Dharr al-Ghiffari ni mmoja wa watu maarufu kwenye historia ya Uislamu. Alikuwa ndiye mtu asiyekuwa na woga kabisa na asiyeogopa kusema kweli miongoni mwa maswa-haba wote wa Muhammad Mustafa ambaye wakati mmoja alisema "Mbingu haijawahi kutandaza mwamvuli wake juu ya mtu yeyote aliyekuwa mkweli kuliko Abu Dharr."

Woga wa vurugu za Maquraishi haukuzizuia nyoyo hizi za kishujaa na adilifu kuukubali Uislamu, na kila mmoja wao aliacha alama juu yake kwa kujitolea mhanga kwake.

Pia mtu mashuhuri miongoni mwa Waislamu wa awali alikuwa ni Mas'ab ibn Umayr, binamu ya baba yake Muhammad. Miaka mingi baadae, katika Kiapo cha Kwanza cha Akaba, wananchi wa Yathrib walimuomba Mtume (s.a.w.) kuwarudisha pamoja nao mwal-imu wa Qur'an, na bahati ikaangukia juu yake. Hii ilimfanya awe mtumishi wa kwanza katika Uislamu. Alikuwa pia ndiye mshika bendera wa jeshi la Waislamu katika vita vya Uhud lakini akauawa kwenye mapigano.

Kama jamaa wa familia ya Makka alikubali Uislamu, alitenganishwa nao kwa wakati wote, bila ya matumaini yoyote juu yake ya kurejesheana uhusiano. Watu wa Makkah wengi wal-iuona Uislamu kama "nguvu yenye kutenganisha" iliyokuwa ikivunja familia zao, na baad-hi yao walidhani kwamba walipaswa kuzuia "utenganishaji" huu usienee. Lakini mbali na tishio la kutumia nguvu kukomesha harakati hii mpya, hawakuweza kufikiria kitu kingine chochote ambacho kingeweza kuonekana chenye matokeo mazuri zaidi katika kusi-mamisha maendeleo yake. Walifikiria pia kwamba kama hawatafanya haraka na kwa uthabiti wa kutosha, haikuelekea kutowezekana kwamba kila nyumba hapo Makka kuwa uwanja wa vita ambamo wahusika wakuu wa ile imani ya zamani na hii mpya wangejiin-giza kwenye mapambano ya umwagaji damu mkubwa dhidi ya kila mmoja wao.

66

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Walikuwepo baadhi ya wengine miongoni mwa wapagani waliodhania kwamba Muhammad alishawishiwa na lengo la kukataa mtindo wao wa jadi wa ibada na masana-mu yao. Wote waliweka vichwa vyao pamoja na wakajaribu kufikiria juu ya ufumbuzi usio wa kawaida wa tatizo hilo. Baada ya mjadala mrefu, waliamua kumtuma Utba, mmoja wa wakuu wa Maquraish, kuonana na Muhammad, na kujaribu kumshawishi kuacha kazi yake hiyo. Utba alijulikana kwa uwezo wake wa kushawishi.

Alimwendea Mtume wa Allah (s.a.w.) na akasema: "Ewe Muhammad! Usipande mbegu ya mfarakano na kutoelewana miongoni mwa Waarabu, na usiilaani miungu ya kiume na ya kike, mababu zetu waliyoabudu kwa karne nyingi, na tunaiabudia leo. Kama nia yako katika kufanya hivyo ni kuwa kiongozi wa kisiasa, tuko tayari kukukubali kama mkuu wa Makka. Kama unataka mali, ni kiasi cha kusema tu, na tutakupatia kila tutakachoweza. Na kama umwenye kutaka kuoa katika ukoo bora, wewe utaje tu, nasi tutaandaa hilo kwa ajili yako."

Muhammad aliyasikia yote aliyoyasema Utba lakini badala ya kuonyesha tamaa yoyote ya cheo au mali au urembo, alisoma mbele yake Surat Sajda, (Sura ya 32 ya Qur'an), ule wahyi mpya kabisa kutoka Mbinguni. Kusoma kulipokwisha, Utba alirudi kwa Maquraish na kuwashauri wamwache Muhammad na wasimuingilie tena. Aliwaambia pia kwamba kama Muhammad akishindwa katika kazi yake, basi wao (Maquraish) hawatapoteza cho-chote; lakini kama atafanikiwa katika hilo, basi watashiriki katika mamlaka yake yote na utukufu.

Lakini Maquraish hawakuukubali ushauri wa Utba wa kujizuia katika kumshughulikia Muhammad na wafuasi wake. Waliendelea kuwatesa Waislamu kama mwanzoni na wakabaki kufikiria juu ya mkunjo mpya utakaoleta matokeo bora katika kusimamisha maendeleo ya Uislamu kuliko ukatili wao wote ulivyokwishafanya mpaka hapo.

Muhammad alilindwa na ami na mlezi wake, Abu Talib. Kwa wakati wote Abu Talib alipokuwa hai, wapagani hao hawakuweza kumsumbua mpwa wake. Iliwajia baadhi yao kwamba wangepaswa pengine kumshawishi Abu Talib mwenyewe, kutotilia maanani ulinzi wake juu ya Muhammad kwa niaba ya mshikamano wa kikabila. Kwanza, mshika-mano wa kabila ulikuwa ni kitu chenye umuhimu zaidi kulichukulia kwa purukushani hata na Abu Talib, licha ya mapenzi yake yote kwa mpwawe.

Maquraish waliamua kutuma ujumbe, unaotokana na watu mashuhuri wa kabila hilo, kwa Abu Talib. Ujumbe huo ulimwendea, na ukamsihi kwa niaba ya mshikamano wa kikabila wa Maquraish kupuuza ulinzi wake kwa Muhammad ambaye alikuwa "anauvuruga" vibaya sana.

67

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Abu Talib, kwa kweli, hakuwa na nia ya kupuuza ulinzi wake kwa Muhammad. Bali aliwaridhisha wale wajumbe wa Maquraish kwa maelezo ya kiuchamungu na maneno yenye kutuliza, na wakarudi majumbani kwao "mikono mitupu."

Wajumbe hao pia waligundua kwamba wamerudi nyumbani kutoka kwenye "kufukuza-zimwi;" lakini hawakushituliwa na kushindwa kwao, na wakati fulani baadae, walifanya jaribio jingine la kuvunja "ushirikiano" wa Abu Talib na Muhammad. Ujumbe mpya ukaenda kumuona Abu Talib, na safari hii, wajumbe wake walichukua pamoja nao kijana mmoja mwenye sura nzuri, Ammarra ibn Walid, ambaye walimtoa kwa Abu Talib kama "mwana" kama angewapa wao Muhammad.

Abu Talib atakuwa ameucheka sana huu mwanzo wa jambo hili la Maquraish. Hivi kweli waliamini kwamba angewapa mwanae mwenyewe wamuue, na kwamba angelea mmoja wa watoto wao kama mwanae hasa? Jambo lenyewe lilikuwa la kipumbavu. Lakini kwa mara nyingine tena, Abu Talib aliishughulikia hali hiyo kwa desturi yake ya maarifa na upole, na wakarudi.

Hili jaribio la pili la Maquraish la kumbembeleza Abu Talib kumtoa Muhammad, pia lil-ishindwa. Pale maana ya kushindwa huku ilipozama akilini mwao, walitambua kwamba majaribio ya amani ya kulitatua tatizo hili yote Hayakuzaa matunda. Waliamua kujaribu kitu chenye matokeo ya haraka zaidi.

Kwa ajili ya maudhi tu na kuvunja moyo, watunga-sera wa Maquraish walichukuwa msimamo mgumu na wakatuma ujumbe wao wa tatu na wa mwisho kwa Abu Talib. Jukumu lake lilikuwa ni kumshurtisha kumsalimisha Muhammad kwao. Viongozi wa ujumbe huo waliwasilisha kauli ya mwisho kwa Abu Talib: ama alikuwa amsalimishe Muhammad kwao, vinginevyo atakabiliana na matokeo ya kukataa kwake kufanya hivyo.

Abu Talib alikuwa mtu mwenye moyo wa furaha na tabia ya uchangamfu, lakini ilikuwa siku nzito katika maisha yake. Maquraish hao, alijua, hawakuwa wakiganganya. Kwa hiyo alimwita Muhammad na kumjulisha juu ya madhumuni ya uwakilishi wa Maquraishi, na kisha akaongeza : "Oh maisha ya ami yako! Usinitwishe mzigo juu yangu ambao nitauona ni zaidi ya nguvu zangu kuubeba."

Muhammad akajibu: "Ewe ami yangu! Kama Maquraishi wataliweka jua kwenye mkono wangu wa kulia na mwezi kwenye mkono wa kushoto, mimi sitaacha kutangaza Upweke wa Allah (s.w.t.) katika kutekeleza wajibu huu, ama nitafanikiwa na Uislamu utaenea; au, kama nitashindwa, nitachakaa katika jaribio hilo."

Abu Talib hakuwa mtu wa kumshawishi Muhammad asihubiri Uislamu. Bali alikuwa anajaribu ushupavu wake. Jibu la wazi la Muhammad lilimvutia na kumridhisha kwamba

68

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

hatasita, na akasema: "Nenda mwanangu, na fanya chochote unachotaka. Hakuna atakayethubutu kukufanyia madhara yoyote." Sir William Muir:

". lakini wazo la kutelekezwa na mlinzi wake mpole (Abu Talib) lilimlemea Muhammad. Alibubujikwa na machozi, na akageuka ili kuondoka. Ndipo Abu Talib akaita kwa sauti kubwa: "Mtoto wa ndugu yangu! Rudi." Hivyo akarudi. Na Abu Talib akasema: "Nenda kwa amani, mpwa wangu, na sema lolote unalotaka. Kwani Wallah, kwa namna yoyote ile, sitakuacha kamwe."

(The Life of Muhammad, 1877) Muhammad Husein Haykal:

"Abu Talib akasema: "Endelea, mpwa wangu, na sema utakalo. Wallah. ninaapa kamwe sitakusaliti kwa maadui zako."

Abu Talib aliwasilisha uamuzi wake kwa Bani Hashim na Bani al-Muttalib na akaongea nao kuhusu mpwa wake kwa mvuto mkubwa sana na kuzingatia kwa undani utukufu wa cheo cha Muhammad. Aliwataka wote kumlinda Muhammad dhidi ya Maquraishi. Wote waliahidi kufanya hivyo isipokuwa Abu Lahab aliyetam-ka wazi uadui wake kwake na kujitoa kwake kwenda kambi ya upinzani.

"...Maquraish waliwasababishia maswahaba wa Muhammad kila aina ya madhara ambayo kutokana nayo aliokolewa tu kupitia ulinzi wa Abu Talib, Bani Hashim, na Bani al-Muttalib."

(The Life of Muhammad)

Kukwamishwa na kuzuiwa kwa kurudiwa rudiwa kwa namna hii na Abu Talib, uvumilivu wa waabadu masanamu ulifikia mahali pa kuvunjika. Baada ya kushindwa kwa ubalozi wao wa mara ya tatu kwa Abu Talib, waliamua kutupia ukatishwaji tamaa wote na hasira walizoficha mioyoni juu ya wale Waislamu wasiokuwa na ulinzi. Walitumaini kuivunja ile dini mpya kwa vitisho na ukatili.

Waathirika wa kwanza wa msuguano na ushari wa wapagani walikuwa ni wale Waislamu wasiokuwa na ushirikishwaji wa kikabila hapo Makka. Yasir na mke wake, Sumayya, na mtoto wao, Ammar, hawakuwa na ushirikishwaji wa kikabila. Hapo Makka walikuwa ni "wageni" na hapakuwa na wa kuwalinda. Wote watatu waliteswa kikatili sana na Abu Jahl na makafiri wengine. Sumayya, mkewe Yasir, alikufa wakati akiwa anateswa. Yeye kwa hiyo akawa Shahidi wa Kwanza katika Uislamu. Baadae kidogo, mumewe, Yasir, aliteswa pia hadi kufa, naye akawa Shahidi wa Pili katika Uislamu.

69

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Maquraishi walichafua mikono yao kwa damu isiyokuwa na hatia! Katika orodha ya mashahidi, Sumayya na mume wake Yasir, wanashika nafasi miongoni mwa wale wa juu kabisa.Waliuawa bila ya sababu yoyote mbali na kumcha kwao Mungu na mapenzi yao kwa Uislamu na Muhammad Mustafa. Wale Waislamu waliouawa kwenye vita vya Badr na Uhud, walikuwa na jeshi la kuwalinda na kuwasaidia. Lakini Yasir na mke wake hawakuwa na mtu yoyote wa kuwalinda; hawakuwa wameshika silaha yoyote, na walikuwa ndio wasiokuwa na ulinzi kabisa kati ya mashahidi wote wa Kiislamu. Kwa kuji-tolea mhanga maisha yao, walidhihirisha ukweli wa Uislamu, na walitia nguvu katika muundo wake. Waliifanya desturi ya muhanga na kufa kishahidi kuwa sehemu muhimu ya maadili ya Uislamu.

Bilal, Khabab ibn el-Arat, Suhaib Rumi, na Waislamu wengine masikini na wasio na ulinzi walifanywa wasimame kwenye jua kali, na wakapigwa viboko na makafiri. Walinyimwa chakula na maji kwa matumaini matupu kwamba njaa na kiu vitawalazimisha kumtupa Muhammad na Uislamu.

Pale Maquraish walipomuona Muhammad peke yake, waliichukua fursa hiyo kumuudhi yeye. Wao kwa kweli walipenda kumuua lakini walilazimika kuizuia tamaa hii. Kama wangemuua, wangesababisha kisasi au hata vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Wakati mmoja, Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliingia kwenye Al-Kaaba kusoma Qur'an Tukufu. Alikuwa anasoma Qur'an wakati ghafla alipozungukwa na waabudu sana-mu. Walimsongasonga, na wangeweza kumfanyia madhara makubwa lakini walishindwa kwa kuingiliwa kati na Harith ibn Abi Hala, mpwa na mtoto wa kulea wa Khadija, aliye-bahatika kutokea kwenye tukio hilo wakati huohuo. Alijitosa kwenye ghasia hiyo kumuokoa Mtume wa Allah (s.a.w.) kutokana na vurugu hizo za washirikina wa Makka.

Harith ibn Abi Hala aliwapiga mateke na kupigana kwa ngumi zake. Inawezekana kabisa, yeye pia alikuwa amebeba upanga kama Waarabu wote walivyofanya lakini hakutaka kuu-toa, na kusababisha umwagaji damu ndani ya maeneo ya Al-Kaaba. Lakini katika tafrani hiyo, mmoja wa waabudu masanamu hao aliuchomoa upanga wake, na kumchoma kwa kurudiarudia. Alianguka kwenye dimbwi la damu yake mwenyewe, na akafa kwa majeraha mengi katika kifua chake, mabega na paji la uso. Alikuwa Mwislamu wa kwanza kuawa ndani ya maeneo ya Al-Kaaba. Harith alikuwa kijana wa miaka kumi na saba, na aliyafanya maisha yake kuwa dhabihu kwa ajili ya Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.). Alikuwa ndiye muathirika kijana mdogo wa vurugu zenye kuzunguka na kuongezeka za makafiri. Alijipatia taji la kufa kishahidi na kuwa Shahidi wa tatu katika Uislamu. Kifo chake, mapema sana katika uhai wake, kilimfanya Mtume (s.a.w.) kuwa mwenye huzuni sana.

Wanahistoria wa Kiarabu wako kimya kuhusu suala hili lakini mapigano mabaya zaidi laz-ima yawe yalitokea ndani ya Makka kati ya Waislamu na waabudu masanamu katika miaka

70

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ya kabla ya kuhama kwa Mtume (s.a.w.) kwenda Madina. Abu Talib alimlinda mpwa wake wakati wote alipokuwa hai. Baada ya kifo chake, wajibu huu ulirithiwa na mwanae, Ali.

Ali alikuwa bado ni kijana wakati alipojiteua mwenyewe kuwa mlinzi wa Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.). Baada ya mauaji yale, ndani ya Al-Kaaba, ya Harith ibn Abi Hala, Ali alifuatana na bwana wake wakati wowote alipotoka nje ya nyumba yake, na alisi-mama kati yake na maadui zake. Kama mtu mshari alimwendea Muhammad kwa kumkamia, Ali mara moja alimpa changamoto, na akapambana naye.

D.S.Margoliouth:

"Wale watu ambao kuingia kwao katika Uislamu kulikaribishwa sana walikuwa watu wenye nguvu za kimwili, na upiganaji mwingi wa dhati lazima uwe ulitokea hapo Makka kabla ya Hijra; vinginevyo ile hali ya kuwa tayari ambayo kwayo Waislam baada ya Hijra waliweza kuonyesha kutokana na idadi yao ya mashujaa waliojaribi-wa, ingekuwa isiyoelezeka. Shujaa aliyejaribiwa lazima awe amejaribiwa mahali fulani; na hakuna mapigano ya nje yaliyotajwa au ambayo angalau ni jambo la doke-zo kwa wakati huu."

(Muhammad and the Rise of Islamu, London, 1931)

Hakukuwa na mapigano ya nje hapo Makka kabla ya Hijra ya Mtume (s.a.w.) kwenda Madina, lakini kulikuwa na mapigano mengi sana mitaani na kwenye sehemu za wazi za mji huo. Ilikuwa ni katika "viwanja vya vita" hivi ambavyo Ali, yule simba kijana, alimopata umahiri wote huu wa kivita. Haya "mapigano" hapo Makka yalikuwa ni "mazoezi ya mwisho" ya dhima aliyotakiwa kuchukua miaka michache baadae huko Madina katika mapambano ya silaha kati ya Uislamu na upagani. Ilikuwa pia katika siku hizi za mwanzoni, kabla ya Hijra ya Mtume (s.a.w.) kwenda Madina, ambayo Ali alikuwa "msitari wa kwanza wa ulinzi wa Uislamu." Kwa kweli, alikuwa pia, kwa wakati huohuo, msitari wa pili na wa mwisho wa ulinzi wa Uislamu. Hili yeye, na yeye peke yake, lilikuwa lidumu kwa maisha yake yote yaliyobakia.

Maquraish waliitesa miili ya Waislamu wasiokuwa na ulinzi huko Makka kwa matumaini kwamba watawalazimisha kuuacha Uislamu, lakini walishindwa. Hakuna hata mmoja kati ya hawa Waislamu "masikini na wanyonge" aliyeukana Uislamu kamwe. Mazingira mabaya yanaweza kushirikiana kumvunja hata yule mtu mwenye nguvu sana, na kwa Waislamu, mazingira hayo hayakuweza kuwa mabaya zaidi. Lakini mazingira yale hayakuweza kuwavunja. Uislamu uliwaweka pamoja.

Kwa hawa Waislamu "masikini na wanyonge", Uislamu ulikuwa ni desturi "inayotia nguvu". Umeyavuta maisha pamoja kwa ajili yao; umeyawekea maana ndani yake,

71

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

umeyaendesha malengo kupitia humo, na umeweka upeo pande zote. Wao, kwa hiyo, walitupilia mbali usalama, starehe na anasa za maisha; na baadhi miongoni mwao kama Sumayya na mume wake, Yasir, waliyapuuzilia mbali maisha yenyewe; lakini walithibitisha Imani yao. Walikufa lakini hawakuafikiana na Upotofu.

Allah (s.w.t.) awe radhi na nafsi hizi za kishujaa na tukufu na azirehemu. Imani na uadili-fu wao vilikuwa, kama Maquraishi walivyogundua, visivyoshindika kwa kiasi kama isivyoshindika imani na uadilifu wa bwana na kiongozi wao, Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.w.t.) Walikuwa ni almasi ambazo Muhammad alizipata kwenye mawe ya dunia. Walikuwa wachache kwa idadi lakini wasio na bei kwa tathmini; ya kuweza kuelezeka, sio kwa wingi bali kwa ubora tu, na ubora huo ulikuwa adhimu sana.

72

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hijra mbili za Waislamu kwenda Abyssinia (A.D.D 615-616)

Muhammad Mustafa (rehma na amani juu yake na Ahlul-Bait wake), alishirikiana katika huzuni zote na madhara ya wafuasi wake walioteswa kwa kuamini kwamba "Mungu ni Mmoja", lakini hakuwa na njia ya kuwalinda. Pale vurugu za washirikina dhidi ya Waislamu zilipokuwa hazionyeshi dalili yoyote ya kutoshadidi, aliwashauri waondoke Makka na kutafuta hifadhi huko Abyssinia (Ethiopia) ambayo wakati huo ikitawaliwa na mfalme wa Kikristo, anayefahamika sana kuwa ni mtu muadilifu na mcha-Mungu.

Kwa kuitikia ushauri huu, kikundi cha Waislamu, chenye wanaume kumi na mmoja na wanawake wanne, kiliondoka Makka na kwenda Abyssinia. Kikundi hicho kilimhusisha Uthman bin Affan, khalifa wa baadae wa Waislamu; mke wake, Ruqayya; na Zubayr bin al-Awwam, binamu yake Mtume. Mtukufu Mtume (s.a.w.) alimteua Uthman bin Mazun, mmoja wa maswahaba wake wakuu, kama kiongozi wa kikundi hiki.

Ibn Ishaq:

"Wakati Mtume (s.a.w.) alipoyaona madhara ya maswahaba wake na kwamba ingawa ameweza kuyaepuka kutokana na kusimama na Allah (s.w.t.) na ami yake, Abu Talib, hakuweza kuwalinda, aliwaambia: 'Kama mngekwenda Abyssinia (ingekuwa bora kwenu), kwani huyo mfalme (huko) hatavumilia dhulma na ni nchi ya kirafiki, mpaka wakati huo ambapo Allah (s.w.t.) atakapowatoeni kwenye dhiki yenu.' Hapo maswahaba wake wakaenda Abyssinia, wakiogopa kuasi na kukimbilia kwa Allah (s.w.t.) pamoja na dini yao. Hii ilikuwa Hijra ya kwanza katika Uislamu.

(The Life of the Messenger of God) Hijra ya kwanza ilifanyika katika mwaka wa tano wa tangazo la Uislamu - 615. A.D.

Mfalme wa Abyssinia aliwakaribisha wakimbizi hao wa Kiislam kutoka Makka kwenye falme yake. Aliwapatia hifadhi, na walifurahia amani, usalama na uhuru wa kuabudu chini ya himaya yake. Kama mwaka mmoja baadae, Waislamu hao huko Abyssinia walisikia minong'ono kwamba Maquraishi huko Makka wameupokea Uislamu. Kama ilikuwa kweli basi hakukuwa na sababu ya wao kuishi uhamishoni. Walikuwa na hamu ya nyumbani, na waliamua kurudi Makka.

Lakini walipowasili Makka, waligundua kwamba sio tu kwamba ile minong'ono waliy-oisikia ilikuwa ya uongo, bali pia kwamba Maquraishi wameongeza mateso ya Waislamu.

73

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Wao, kwa hiyo, wakaondoka Makka kwa mara nyingine. Waislamu wengine wengi pia walifuatana nao. Kundi hili jipya lilikuwa na wanaume 83 na wanawake 18. Muhammad Mustafa akamteua binamu yake wa kwanza, Jafar ibn Abi Talib, kaka yake mkubwa Ali, kama kiongozi wa kikundi hiki.

Hajra hii ya pili ya Waislamu kwenda Abyssinia, ilitokea katika mwaka wa sita wa kutangazwa Uslamu, unawafikiana na mwaka wa 616. A.D.

Hijra hii ya Waislamu kwenda Abyssinia, na kupokewa kwao katika baraza la kirafiki la nchi ile, kuliwaogofya Maquraishi. Waliichukulia hofu ile kwamba Waislamu wanaweza kuongezeka nguvu, au kupata washirika wapya, na kisha, siku yoyote, wanaweza kurudi Makka kushindana nao. Ili kubadili mwelekeo wa tishio hili linalowezekana, kama walivy-oliona, waliamua kutuma ujumbe kwenye baraza la mfalme wa Abyssinia kumshawishi kuwahamishia (kwa kuwakabidhi) Waislamu hao Makka.

Wakimbizi hao wa Kiislamu ambao walitarajia kuachwa katika amani, walishangazwa na kuwasili, katika mji mkuu wa Abyssinia, kwa ujumbe kutoka Makka, ukiongozwa na Amr bin Al-Aas. Amr alileta zawadi nono kwa ajili ya mfalme na watumishi wake ili kujipen-dekeza kwao.

Pale mfalme alipokutana na wajumbe wa Maquraishi, Amr alisema kwamba Waislamu wale walioko Abyssinia hawakuwa wakimbizi kutokana na mateso bali walikuwa watoro wa haki na sheria, na akamuomba kuwahamishia Makka. Mfalme, hata hivyo, akataka kusikia upande wa pili wa Hadith pia kabla ya kutoa uamuzi, na akamwita Jafar ibn Abi Talib kwenye baraza kujibu mashtaka yale dhidi ya Waislamu.

Jafar alitoa utetezi kabambe kabisa. Ufuatao ni mukhtasari wa hotuba yake ndani ya baraza la Abyssinia katika kujibu maswali yaliyotolewa na yule mfalme wa Kikristo.

"Ewe Mfalme! Tulikuwa tu watu wajinga na tuliishi kama wanyama wa porini. Wale wenye nguvu kati yetu waliishi kwa kuwinda wanyonge. Hatukutii sheria yoyote na hatukukubali mamlaka yoyote mbali na ile nguvu ya kinyama. Tuliabudu masanamu yaliyotengenezwa kwa mawe au magogo ya miti, na hatukujua chochote cha heshima ya utu. Na kisha Allah (s.w.t.) kwa Rehma Zake, akatutumia Mtume Wake ambaye alikuwa mwenyewe ni mmoja wetu. Tulijua juu ya ukweli wake na uaminifu wake. Tabia yake ilikuwa nzuri sana, na alikuwa wa ukoo-bora sana wa Waarabu. Alituita sisi kwenye ibada ya Mungu Mmoja, na akatukataza kuabudu masanamu. Alitusihi tuseme kweli, na kuwatetea wanyonge, maskini, watu wa chini, wajane na mayatima. Alituamuru tuwaheshimu wanawake, na kutowakashifu kamwe. Tulimtii na kufuata mafundisho yake. Watu wengi katika nchi yetu ni washirikina bado, na walichukia kusilimu kwetu kwenye hiyo dini mpya ambayo inaitwa Uislam. Walianza

74

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kututesa sisi na ilikuwa ili kuepukana na mateso kutoka kwao kwamba tulitafuta na kupata hifadhi katika himaya yako."

Wakati Jafar alipomaliza hotuba yake, mfalme alimuomba asome baadhi ya Aya zili-zoshushwa kwa Mtume wa Waislamu. Jafar akasoma Aya chache kutoka kwenye Surat Maryam, Sura ya 19 ya Qur'an Tukufu. Mfalme aliposikia Aya hizi, alisema kwamba asili yake Aya hizo, ilikuwa ni sawasawa na ile ya Injili. Ndipo basi akatamka kwamba amerid-hika na ukweli wake, na akaongeza, kwenye huzuni kubwa ya Amr bin Al-Aas, kwamba Waislamu wale wako huru kuishi kwenye himaya yake kwa kiasi cha muda wowote wau-takao.

Lakini Amr bin Al-Aas alijishauri mwenyewe juu ya mkakati mpya, ambao, aliamini, ungeshambulia vile vigezo dhidi ya Jafar. Siku iliyofuata, kwa hiyo, alirudi kwenye baraza hilo na alimwambia mfalme kuwa yeye mfalme alipaswa kupuuza madai ya ulinzi wake kwa Waislamu hao kwa sababu waliikana jinsia-asili tukufu ya Kristo, na wao wakadai kwamba alikuwa ni binadamu kama watu wengine.

Alipoulizwa na mfalme juu ya suala hili, Jafar alisema: "Ufahamu wetu juu ya Yesu ni kama ule wa Allah (s.w.t.) na Mtume Wake (s.a.w.), yaani, Yesu ni mja wa Allah (s.w.t.) Mtume Wake, Roho Wake, na Amri Yake iliyotolewa kwa Maryam, yule bikra maasuma."

Mfalme akasema: “Yesu yu kama vile tu ulivyomuelezea alivyo, na si kingine zaidi ya hayo." Kisha akizungumza na wale Waislamu, akasema: "Nendeni majumbani kwenu na mkaishi kwa amani. Sitawatoa kamwe kwa maadui zenu." Alikataa kuwahamisha wale Waislamu, akarudisha zile zawadi ambazo Amr bin Al-Aas alizileta, na akaufukuza ule ujumbe wake.

Washington Irving

"Miongoni mwa wale waliokimbilia Abyssinia, alikuwemo Jafar, mtoto wa Abi Talib, ambaye ni nduguye Ali, hivyo ni binamu wa Muhammad. Alikuwa ni mtu wa ufasa-ha wenye mvuto na umbo la kupendeza mno. Alisimama na kujitokeza mbele ya mfalme wa Abyssinia, na akazifasili imani za Kiislamu kwa ghera na uwezo.

Mfalme ambaye alikuwa Mkristo wa Nestoria, aliziona imani hizi zenye kufanana sana kwa namna nyingi na zile za madhehebu yake na zenye kupingana sana na zile za ibada nzito ya masanamu ya Maquraishi, kwamba mbali sana na kuwakabidhi wale wakimbizi, aliwachukua zaidi mahsusi kwenye upendeleo na ulinzi, na kuzirudisha kwa Amr bin Al-Aas na Abdullah, zile zawadi walizozileta, na kuwatoa kutoka kwenye baraza lake.

(Life of Mohammed)

75

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Waislamu walikaa miaka mingi huko Abyssinia na waliishi kwa amani. Miaka kumi na tatu baadae - katika mwaka wa 7 A.H. (A.D. 628) - walirejea, sio kwenda Makka bali Madina. Kuwasili kwao kulifuatana na kutekwa kwa Khaibar na Waislamu.

Jafar ibn Abi Talib alikuwa ndio kiongozi wa Waislamu wote waliokuwa wamehamia Abyssinia katika mwaka wa 615 na 616. Anaonekana kama ndio alikuwa mtu pekee wa ukoo wa Bani Hashim kuondoka kwenda Abyssinia pamoja na wale wakimbizi wengine. Watu wengine wote wa Bani Hashim walibakia Makka.

Montegomery Watt:

"Mbali na watu wawili wa pekee Waislamu wote wa mwanzo waliobakia Makka (na hawakwenda Abyssinia) walitokana na kikundi cha koo tano, kikiongozwa na ukoo wa Muhammad wa Bani Hashim. Kikundi hiki kinaelekea kuwa ni namna ya Umoja wa Waadilifu ulioundwa upya. Kwa hiyo ndio kiini cha upinzani kwa wale wafanya biashara wakubwa pamoja na tabia yao ya ukirikimba."

(Muhammad, Prophet and Statesman, 1961)

76

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

HAMZA AUKUBALI UISLAMU - A.D. 615

Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) ingawa yuko salama chini ya ulinzi wa ami yake, Abu Talib, hakusalimika na bughudha za washirikina. Wakati wowote walipopata mwanya wa kumuudhi, hawakuupoteza. Wakati mmoja Abu Jahal alimkuta akiwa peke yake, na akatumia lugha ya kishenzi na ya kuchukiza sana juu yake Muhammad. Jioni hiyo hiyo wakati ami yake, Hamza ibn Abdul Muttalib alivyorudi nyumbani kutoka safari ya mawin-doni, mtumwa wake wa kike alimuelezea kile kisa cha fedhuli isiyo na sababu ya Abu Jahal kwa Muhammad na ustahimilifu wa Muhammad, ambao yeye alikuwa shahidi.

Hamza alikuwa mpiganaji, mwindaji na mwanamichezo, na alikuwa hana habari sana na mambo ya kila siku ya mjini hapo. Lakini tabia ya Abu Jahal kwa mpwa wake ilimpan-disha sana hasira kiasi kwamba alichukua upinde wake, na akaingia kwenye mkutano wa Maquraish ambamo yeye Abu Jahal alikuwemo akiwachambulia wenzie matukio ya siku ile.

Hamza akampiga kichwani mwake na upinde wake, na kumsababishia atokwe na damu, na akasema: "Na mimi pia nimekuwa Mwislamu."

Huu ulikuwa ni mtihani kwa Abu Jahal lakini aliona kwamba kimya kilikuwa ni sehemu bora ya ujasiri, na hakugombana na Hamza, pia akawazuia rafiki zake ambao walitaka kusimama kumtetea.

Betty Kelen:

"Ami yake Muhammad, Hamza, mtu wa umri wake mwenyewe, alisifika kuwa mwenye nguvu sana na uwezo kati ya Maquraish, shujaa wao katika vita na michezo. Alitumia muda wake mwingi kwa kuwinda vilimani. Siku moja alipokuwa anarudi kutoka kwenye msako na uta wake ukinin'ginia kwenye bega lake, mtumwa wake wa kike alimweleza jinsi Abu Jahal alivyomrundikia matusi mpwa wake.

Hamza alijikuta mwisho kabisa wa uvumilivu wote. Alimpenda Muhammad, ingawa alikuwa hamuelewi (japo kwa makosa, sio kweli). Alikimbilia Msikitini, ambako alimuona Abu Jahal akiwa amekaa miongoni mwa marafiki zake. Akanyanyua uta wake mzito na akampiga nao pigo kubwa sana kichwani mwake. "Utamtukana tena nitakapojiunga na dini yake?" alipiga kelele, akinyoosha misuli yake mikubwa mbele ya Maquraish.

Hamza akawa Mwislamu, na hili lilitia nguvu kwenye imani hiyo. Baadhi ya Maquraish walikuwa waangalifu zaidi juu ya kumwita Muhammad mshairi.

(Muhammad, the Messenger of God, 1975) 11

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hamza akawa mwislamu mcha-mungu na shujaa wa Uislamu. Alikuwa ndiye askari-mwenza wa mpwawe mwingine, Ali, na ilikuwa ni wao wote waliowauwa wengi wa vion-gozi wa Maquraish katika vita vya Badr, vilivyokuwa vipiganwe miaka michache baadae.

Katika vita vya Uhud, Hamza alimuua mshika-bendera wa pili wa wapagani, na pale wali-poshambulia mstari wa Waislamu, alijItosa kati yao. Alikuwa akipasua njia yake kupitia kwenye safu zao pale alipopigwa na mkuki uliotupwa na Wahshi, mtumwa wa kihabeshi. Wahshi alipangwa kwa ajili ya kazi hii hasa, na Hindu, mke wa Abu Sufyan na mama yake Muawiya; na muabudu sanamu mwingine wa Makka. Hamza alianguka chini na akafa mara moja.

Baada ya kusambaratika kwa Waislamu siku ile, Hindu na wanawake wengine makatili kutoka Makka, walikatakata viungo vya miili ya Waislamu waliouawa. Alipasua tumbo la Hamza, akalin'goa ini lake, na akalitafuna. Alimkata pia pua yake, masikio, mikono na miguu, akavitunga kama "mkufu," na kuingia Makka ameuvaa kama tuzo la vita.

Muhammad Mustafa alisikitishwa sana na kifo na kukatwakatwa kwa mwili wa muumini hodari wa Uislamu kama Hamza. Alitoa majina ya "Simba wa Mungu", na "Kiongozi wa Mashahidi" juu yake.

Hamza aliukubali Uislamu katika mwaka wa tano wa kutangazwa Uislamu.

78

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

KUSILIMU KWA UMAR - A.D. 616

Tukio maarufu la mwaka wa sita wa Tangazo la Uislamu lilikuwa ni kusilimu kwa Umar bin Khatab, khalifa wa baadae wa Waislamu. Alikuwa mmoja wa maadui wakali sana wa Uislamu na Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) na alikuwa mtesaji mkubwa wa Waislamu. Yule mwanahistoria wa kisasa wa Kimisri, Amin Dawidar, anasema kwamba chuki ya Umar kwa Uislamu, na uhasama wake kwa Muhammad, vilifanana tu na chuki na uhasama kwavyo wa ami (mjomba) wake wa upande wa kikeni, Abu Jahl.

Inasemekana kwamba siku moja kwa maudhi tu, Umar alikusudia kumuua Muhammad, na hivyo kuuzima mwale wenyewe wa Uislamu. Aliondoka nyumbani kwake akiwa na nia hii.

Kama ilivyokwisha elezwa, Waislamu kwa wakati huu (siku za mwisho za mwaka wa sita) walikuwa bado wanajikusanya katika nyumba ya Arqam bin Abi Arqam kuswali Swala zao za jamaa. Walikuwa wanaanza kujikusanya wakati mmoja wao, akitazama nje ya dirisha, akamwona Umar akija kuelekea nyumbani hapo na upanga uliochomolewa. Katika hali ya wasiwasi kiasi, aliwaambia wale watu wengine wa jamaa ile kile alichokiona. Labda, na wao pia walikuwa na wasiwasi. Lakini Hamza, ambaye pia alikuwemo ndani ya nyumba hiyo ya Arqam, aliwatuliza, na akasema kwamba kama Umar alikuwa anakuja na nia nzuri, basi ilikuwa ni sawa sawa; lakini kama sivyo, basi yeye Hamza atamchoma kwa upanga wake Umar mwenyewe. Lakini ilitokea kwamba Umar alikuja kwa nia ya kusilimu, na akafanya hivyo.

Hadithi inaelezwa kwamba Umar alikuwa anakwenda kuelekea Dar-ul-Arqam kwa nia ya kumuua Muhammad wakati mpita njia alipomsimamisha, na kumjulisha yeye kwamba dada yake mwenyewe na mumewe wamekuwa Waislamu, na akamshauri kuiweka nyumba yake mwenyewe sawa kabla ya kuanza mpango mwingine wowote mkubwa wa kubuni-wa tu.

Muhammad Husein Haykal:

"Umar alikwenda pale (Dar-ul-Arqam) - kwenye nyumba ya Arqam, akiwa amekusu-dia kumuua Muhammad na hivyo kuwaondolea Maquraish mzigo, na kusimamisha upya heshima ya ile miungu ambayo Muhammad aliipinga. Akiwa njiani kuelekea Makka alikutana na Nu'aym ibn Abdullah. Baada ya kujua nia ya Umar, Nu'aym akasema, "Wallahi umejidanganya mwenyewe, ewe Umar! Unadhani Bani Abd Manaf watakuacha utembee ukiwa hai pindi utakapokuwa umemuua mtoto wao Muhammad? Kwa nini usirudi nyumbani kwako mwenyewe na angalau

ukakuweka sawa?"

(T he Life of Muhammad)

79

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Umar alikasirika kusikia kwamba dada yake na mumewe wamekuwa Waislamu. Mara moja akabadili njia kutoka ile ya kwenda kwenye nyumba ya Arqam na kuchukua ya kwenda nyumbani kwa dada yake kuchunguza madai yale. Kwa majibu ya maswali yake, dada yake alimpa jibu makinifu lakini la ukwepaji.

Ibn Ishaq:

"Umar alifika kwenye mlango (wa nyumba ya dada yake) wakati Khabbab (sahaba wa Mtume) alikuwa akisoma chini ya uongozi wake ile Sura ya Taha na pia "Jua litakapokunjwa" (81:1). Washirikina walikuwa wakikiita kisomo hiki "takataka". Umar alipoingia, dada yake aliona kwamba alikusudia madhara na akaficha zile karatasi ambazo walikuwa wakisoma. Khabbab akatorokea ndani ya nyumba. Umar akauliza ni upuuzi gani aliokuwa akisikia, ambapo dada yake akamjibu kwamba yalikuwa ni mazungumzo tu kati yao..."

(The Life of the Messenger of God)

Umar alihamaki kwa kile alichoamini kuwa ni uongo, na akampiga dada yake usoni. Pigo hilo lilisababisha mdomo wake kutokwa na damu. Alikuwa ampige tena lakini kule kuona damu kulimfanya asite. Ghafla alionekana kupunguza ukali, na kisha kwa sauti iliyobadi-lika akamuomba amuonyeshe kile alichokuwa akisoma. Alimhisi amebadilika lakini akase-ma: "Wewe ni muabudu masanamu mchafu, na siwezi kukuruhusu kugusa Neno la Allah (s.w.t.)"

Umar mara moja aliondoka zake, akaoga, akarudi nyumbani kwa dada yake, akasoma yale maandishi ya Qur'an, na kisha akaenda kwenye nyumba ya Arqam ambako alisilimu rasmi.

Sir William Muir anasema kwamba kusilimu kwa Umar kulitokea mwishoni mwa mwaka wa sita wa ujumbe wa Mtume. Anaongezea tanbihi ifuatayo chini ya kurasa:

"Kusilimu kwa Umar kulitokea ndani ya Dhil-Hajj, mwezi wa mwisho wa mwaka. Waumini wanasemekana sasa kufikia kwa jumla watu 40 wanaume na wanawake; au kwa hesabu zingine, wanaume 45 na wanawake kumi na moja."

(The Life of Muhammad, 1877, uk. 95)

80

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Umar alikuwa na miaka kama 35 wakati aliposilimu.

Muhammad Husein Haykal:

"Kwa wakati ule, (aliposilimu) Umar ibn al Khattab alikuwa mtu mzima wa miaka thelathini na tano kwa umri."

(The Life of Muhammad)

Waislamu wengi wanadai kwamba kwa kusilimu kwa Umar, Uislamu ulipata nguvu mpya, na Waislamu walikuwa sasa wametiwa moyo kuwapinga wapagani. Waliweza sasa, kulingana na madai haya, kutoka nje ya sehemu zao za kujifichia, na kuswali waziwazi kwenye maeneo ya Al-Kaaba, ama hasa, alikuwa ni Umar mwenyewe aliyewatoa kwenye sehemu zao za kujifichia, na hawakuwa sasa wakimuogopa Abu Jahl au mtu mwingine yeyote.

Muhammad Husein Haykal:

"Waislamu waliorudi kutoka Abyssinia walifanya hivyo kwa sababu mbili. Kwanza, Umar ibn al Khattab alisilimu mara tu baada ya Hajira yao. Pamoja naye, alileta kwenye kambi ya Waislamu ukakamavu , dhamiri, na msimamo ule ule wa kikabila ambao alikuwa akipiga nao Waislamu kabla. Hakuficha kamwe kusilimu kwake wala kamwe hakuwakwepa wale wapinzani wa Kiquraishi. Badala yake, alitangaza kusilimu kwake hadharani na aliwapinga Maquraishi wazi wazi.

Hakuridhika na kujificha kwa Waislamu wenyewe, mienendo yao ya siri kutoka upande mmoja wa Makka hadi mwingine, na kusimamisha kwao Swala kwenye umbali wenye usalama kutokana na mashambulizi yoyote ya Maquraishi. Umar alian-za kupigana na Maquraishi mara tu alipoingia kwenye imani ya Uislamu, daima akishinikiza njia yake karibu na Al-Kaaba, na akasimamisha Swala yake pale pamoja na Waislamu wowote walioamua kujiunga naye."

(The Life of Muhammad)

Lakini madai haya ya ajabu yanapata nguvu ndogo katika ushahidi. Na kama ushahidi huo una maana yoyote, unaelekea kupingana na madai yenyewe.

Madai mengine ni ya ubadhilifu sana. Kwa mfano, yule mwanahistoria wa Kimisri, Amin Dawidar, anasema ndani ya kitabu chake, Pictures From the Life of the Messenger of God kwamba kusilimu kwa Umar kulikuwa ni pigo la kifo kwa Maquraishi.

Kilichotokea hasa ni kwamba kusilimu kwa Umar kulioana na wimbi jipya na ambalo halijawahi kutokea, la hofu kuu lililotojikeza juu ya Waislamu. Ambapo kabla ya kusilimu kwake ni Waislamu wale tu walioathirika na mateso ambao hawakuwa na wakuwalinda,

81

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

sasa hakuna mwislamu, sio hata Muhammad Mustafa mwenyewe, aliyekuwa salama kutokana na nia mbaya za washirikina.

Muhammad Husyn Haykal:

"Huko uhamishoni kwao (nchini Abyssinia) walisikia kwamba kwa kusilimu Umar Maquraishi wamesimamisha mateso yao juu Muhammad na wafuasi wake. Kwa mujibu wa Hadith moja baadhi yao walirudi Makka, kwa mujibu wa nyingine, waliru-di wote. Walipofika Makka waligundua kwamba Maquraishi wamerudia mateso ya Waislamu kwa chuki zaidi na nguvu mpya. Kwa kushindwa kuhimili, baadhi yao walirudi Abyssinia wakati wengine waliingia Makka chini ya ulinzi wa kiza cha usiku na wakajificha kabisa."

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Lakini hii haikuwa ndio basi. Mengine mengi yalikuwa bado yatokee. Sasa Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) hakuweza walau kuishi Makka. Kwa kweli, zaidi kido-go ya wiki ilikuwa imepita tangu kusilimu kwa Umar, wakati Muhammad na watu wote wa familia na ukoo wake, walikuwa waondoke Makka, na waende uhamishoni. Kwa hiyo, ile dhana kwamba kusilimu kwa Umar kuliwafanya Waislamu kuacha tahadhari zao na mkao wa kiulinzi, na kutowaogopa makafiri, moja kwa moja hailingani na mambo.

S. Margoliouth:

"...hatuna kumbukumbu yoyote ya tukio lolote ambalo juu yake Umar alionyesha ujasiri mkubwa wa kuonekana, ingawa mifano mingi inapatikana juu ya ukatili wake na hamu ya kuua; katika vita vya Hunain alikimbia, na kwenye tukio jingine aliokole-wa maisha yake kwa utu wema wa adui."

(Muhammad and the Rise of Islam, 1931)

Profesa Margoliouth amefanya marejeo kwenye lile tukio ambapo adui mwenye utu mwema alinusuru maisha ya Umar. Atakuwa lazima anarejea ile vita ya Handaki au kule kuzingirwa kwa Madina (627 A.D). Katika vita vile, Ali ibn Abi Talib alimuua yule jemadari wa Makka, Amr ibn Abd Wudd, ambapo maaskari-wenza wake walikimbia kwa haraka kuvuka lile Handaki. Walipokuwa wakikimbia, Umar alijaribu kumpita mmoja wao. Shujaa huyu aliyekuwa akirudi nyuma, alikwisha wahi kusikia kwamba Ali kamwe alikuwa hamuandami adui anayekimbia.

Yeye, kwa hiyo, alitambua kwamba yoyote huyo anayemfukuzia basi, hawezi kuwa ni Ali. Kwa upekuzi tu, aliibia kutazama nyuma na akagundua kwamba alikuwa ni Umar aliyekuwa akimjia kwa vitisho. Alipomuona Umar, mara moja aligeuza hatamu za farasi wake kumkabili, na hili lilimfanya Umar asimame. Shujaa huyu aliyemjua Umar,

82

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

akamwambia: "Kama mama yangu asingenifanya niapie kwamba kamwe sitamuua Quraishi, ungekuwa maiti sasa hivi. Mshukuru yeye (mama), na usisahau kwamba nimeyasalimisha maisha yako."

Ifahamike kwamba Hamza alisilimu mwaka mmoja kabla Umar hajawa mwislamu, na ameadhimisha kusilimu kwake kwa kumshambulia Abu Jahl, ami (mjomba) wa kikeni wa Umar, kwa upinde wake. Mtu hawezi kumtegemea Umar kuigiza mfano wa Hamza kwa kumshambulia ami yake mwenyewe, lakini hakuna kumbukumbu yoyote kwamba alishambulia muabudu sanamu mwingine yoyote kwa kuonyesha fidhuli kwa Mtume wa Allah (s.a.w.). Zaidi ya hayo, pale Hamza alipokubali Uislamu na akaitoa damu pua ya Abu Jahl, Umar mwenyewe alikuwa muabudu sanamu.

Ilikuwa ni wajibu wake, kwa jina la "mshikamano wa kikabila," kushindana na Hamza, na kulinda heshima ya kaka wa mama yake. Hata hivyo, kwa mujibu wa madai mengi yaliyosambaa, alikuwa ndiye mtu shupavu sana, anayetisha sana, mwenye hasira kali, na mkaidi sana hapo Makka. Na ni nani isipokuwa Umar angeweza kuthubutu kumtia chang-amoto Hamza? Lakini changamoto hiyo haikutokea kamwe.

83

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kususiwa kiuchumi na kijamii kwa Bani Hashim

Mwaka wa sita wa Tangazo ulikuwa unakaribia. Wapagani walikuwa tayari wamemaliza miaka mitatu kupiga kampeni dhidi ya Uislamu. Wamezalisha uchungu mwingi na uhasama dhidi ya Waislamu katika miaka hii mitatu, lakini walikuwa na kidogo sana, kama kilikuwapo chochote, cha kuonyesha kwa ajili ya juhudi zao. Walitumia kila silaha dhidi ya Waislamu kuanzia vivutio mpaka ushawishi, hadi matusi mpaka kebehi, na dhihaka mpaka vitisho vya kutumia nguvu na utumiaji hasa wa nguvu zenyewe, lakini bila mafanikio. Ile nguvu ya imani ya Waislamu iliwakanganya.

Kutofaulu kwao kwa mara kwa mara kuliwalazimu Maquraish kutathimini upya ile hali ana kwa ana, Muhammad na Uislamu, na baadhi yao walijaribu kuliangalia tatizo lao kwa namna nyingine mpya. Katika kutafuta kwao ufumbuzi wa tatizo hili linalichusha, alianza taratibu kuwapambanukia juu yao kwamba adui yao hakuwa kile kikundi cha wale Waislamu wasio na mizizi na waliokumbwa na umasikini walioko pale Makka. Adui wa kweli - adui wa waabudu masanamu na washirikina - walimtambua alikuwa ni Abu Talib! Hata hivyo alikuwa ni Abu Talib aliyekuwa akimlinda Muhammad na Uislamu kwa uaminifu na msimamo thabiti. Waislamu, kwa upande mwingine, hawakuwa na uwezo wa kumlinda Muhammad. Kwa kweli, walikuwa wao wenyewe katika haja kubwa ya ulinzi. Mafanikio haya katika "kumtambua adui" yalikuwa na uzito wa udhihirisho kwa viongozi wa Maquraishi katika harakati zao dhidi ya Uislamu, na yamewawezesha kupanga mkakati mpya.

Abd-al-Rahman 'Azzam:

"Mwishowe, ule utawala wa wachache wa pale Makka uliamua kwa wasiwasi mkub-wa kuchukua hatua dhidi ya Abu Talib. Kwa mawazo yao, yeye ndiye aliyekuwa mlinzi hasa wa kufuru hii, ingawa bado alikuwa ni mtetezi wa kuheshimika wa mila za Makka na hajasilimu kwenye dini ya Muhammad (sic - japo sio kweli). Walikubaliana kumpelekea masharti ya mwisho...

(The Eternal Message of Muhammad, London, 1964)

Huko nyuma, Maquraish walikwishawahi kufanya majaribio ya "kumtenga" Muhammad kutoka kwenye ukoo wake, na walitegemea kwamba wangeweza ama kumchombeza au kumhadaa Abu Talib katika kutotilia maanani msaada wake na ulinzi kwa mpwa wake na Uislamu. Kama wangemtenganisha Muhammad na ukoo wake, walitumaini, wangeweza kutatua hilo tatizo gumu na sumbuvu kwa njia rahisi ya "kumfilisi" yeye.

84

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Lakini Abu Talib hakuwaacha Maquraishi "kumtenga" Muhammad. Sio tu yeye mwenyewe aliyekuwa akimlinda mpwa wake, alikusanya pia ukoo wote wa Bani Hashim nyuma yake. Huu ukoo wa Bani Hashim ulikuwa imara katika msaada wake kwa Muhammad, na wakuu wa Maquraish walijikuta wanyonge mbele yake.

Baada ya mashauriano marefu na mjadala, Maquraishi walikubali kwamba "ukaidi" wa Bani Hashim ulihitaji hatua madhubuti, na waliamua kumtenga na kumfukuza sio tu Muhammad bali walinzi wake wote pia, yaani, ule ukoo wa Bani Hashim wote.

Ilitarajiwa kwamba jaribio lolote la kuwafukuza Bani Hashim lingepelekea kwenye kingamizo la vikundi hapo Makka. Kila mmoja hapo Makka angekuwa ajitangaze mwenyewe kuwapendelea au kuwapinga Bani Hashim. Lakini mara ikaja kuwa dhahiri kwamba katika mkabala huu, Bani Hashim watakuta Arabia yote imejipanga dhidi yao.

Muhammad Husein Haykal:

"Ni kama haiwezekani kwa sisi kufikiria nguvu na kiasi cha jitihada ambazo Maquraishi walitumia katika mapambano dhidi ya Muhammad, au uvumilivu wake katika miaka mingi mirefu ya mapambano hayo. Maquraishi walimtishia Muhammad na jamaa zake, hususan ami zake. walimdhihaki yeye na ujumbe wake, na walimtusi yeye vilevile na wafuasi wake. Waliwaagiza washairi wake kumtukana yeye kwa uho-dari wao makini sana na kuelekeza utani wao mkali dhidi ya mahubiri yake. Walimpa madhara na maumivu kwenye nafsi yake na kwenye nafsi za wafuasi wake.

Walimuahidi hongo za pesa, za hadhi ya kifalme na mamlaka, za vyote vile vinavy-omridhisha mtu aliye mgumu kabisa wa kuridhisha miongoni mwa watu. Hawakuwafukuza tu na kuwatawanya wafuasi wake kutoka kwenye nchi yao wenyewe, bali waliwadhuru katika uchuuzi na biashara zao wakati ikiwafukarisha. Ilimtahadharisha yeye na wafuasi wake kwamba vita pamoja na masaibu yake inge-waangukia juu yao. Mambo yote yaliposhindikana, walianza msusio juu yao uliopangwa kuwaua kwa njaa."

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Siku chache kabla ya mwanzo wa mwaka wa 7, wakuu wa koo mbali mbali za Quraishi walikutana katika kikao kizito cha faragha ndani ya "baraza la mji" la Makka, na pale, kwa makubaliano, walirasimu na kutia sahihi waraka unaotamka kwamba ila tu, kama huo ukoo wa Bani Hashim utamkabidhi Muhammad kwao, utafanyiwa mgomo wa kiuchumi na kijamii. Wakajiapiza wenyewe kutonunua chochote, wala kuuza chochote, kwa watu wa ukoo wa Bani Hashim, na waliweka marufuku kuoana kati yao na wao.

85

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mkataba huu ulipelekwa kwenye makabila mengine kwa ajili ya kuidhinishwa. Walipokwishaidhinisha, ukatundikwa kwa taadhima kwenye ukuta wa Al-Kaaba. Kuidhinishwa kwa mkataba huo kulikuwa ni kitendo cha uchokozi!

Abu Talib aliweza kuona dhahiri kwamba mfumo wa wasiwasi ulikuwa unaelekea kwa Bani Hashim. Hali ya Makka imekuwa ya mlipuko kiasi kwamba ukoo wa Bani Hashim ulijikuta kwenye hatari kubwa. Abu Talib alitambua kwamba haitakuwa busara kuishi kati-ka mji, wakati wowote adui anaweza kuzichoma moto nyumba zao. Kwa maslahi ya usala-ma wa ukoo huo, yeye, kwa hiyo, akaamua kuondoka Makka, na kutafuta usalama wa ukoo huo katika bonde karibu ya Makka ambalo baadae lilikuja kujulikana kama Sh'ib Abu Talib. Bonde hilo lilikuwa na namna ya ulinzi wa asili, na lilikuwa kwa hali yoyote lenye usalama wa kuishi kuliko kuishi kwenye nyumba zao mjini hapo ambazo zilikuwa sio sala-ma kwa mashambulizi.

Katika siku ya kwanza ya mwaka wa 7 wa Tangazo la Uislamu, kwa hiyo, zile koo mbili za Bani Hashim na Bani al-Muttalib ziliondoka Makka na zikachukua makao kwenye bonde. Koo hizo zilikuwa katika hali ya kuzingirwa (karantini). Ilikuwa iwe karantini ndefu!

Muhammad Husein Haykal:

"Ule mkataba ambao koo za Quraishi ziliuingia wa kumgomea Muhammad na kuwazingira Waislamu uliendelea kutekelezwa kwa miaka mitatu mfululizo."

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Marmaduke Pickthall:

"Kwa miaka mitatu, Mtume (s.a.w.) alikuwa amefungiwa pamoja na jamaa zake wote katika ngome yao ambayo ilikuwa katika moja ya mabonde linalokwenda hadi Makka."

(Introduction to the Translation of Holly Qur 'an,1975)

Hadithi ya karantini ya Bani Hashim ni mlango wa kusisimua katika utenzi wa Kiislam, na umesimuliwa na kila mwanahistoria wa somo hilo, miongoni mwao:

Sir William Muir:

"...Maquraishi walifanya muungano dhidi ya Bani Hashim - kwamba hawatawaoa wanawake zao, wala kuwaoza wanawake kwao; kwamba hawatauza chochote kwao, wala kununua kitu chochote kutoka kwao; na kwamba kuhusiana nao kwa aina yoyote ile kukome.

86

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Amri ya kupigwa marufuku huko iliwekwa kwa maandishi kwa uangalifu, na yaka-fungwa kwa mihuri mitatu. Pale wote walipojifunga wenyewe kwenye mkataba huo, kumbukumbu hiyo ikatundikwa kwenye ukuta wa Al-Kaaba, na hivyo kibali cha kidi-ni kikatolewa kwenye mahitaji yake.

Bani Hashim hawakuweza kuhimili mwelekeo wa maoni ya umma ambayo yamepa-ta nguvu kali hivyo dhidi yao, na yenye wasiwasi kwamba yanaweza kuwa ni utan-gulizi tu wa mashambulizi ya wazi, au wa mapigo ya gizani ambayo bado ni mabaya zaidi, walijitenga kwenye nafasi ya mji iliyojitenga inayojulikana kama Sh'ib Abi Talib. Imeundwa na moja ya mabonde mikatiko ya milima, ambamo yale mawe yanayochomoza ya Abu Qubais yamelemea kwenye viunga vya Mashariki ya Makka. Iliingiliwa kwenye upande wa mji kwa njia ya chini yenye lango, kwa njia hiyo ngamia alipita kwa taabu. Kwenye pande nyingine zote ilitengwa na mji kwa maja-bali na majengo.

Katika usiku wa kwanza wa mwezi wa kwanza wa mwaka wa saba wa ujumbe wa Muhammad, hawa Bani Hashim, pamoja na Mtume (s.a.w.) na familia yake, walijitenga kwenye kambi ya Abu Talib; na pamoja nao kilifuata pia kizazi cha Al-Muttalib, ndugu yake Hashim. Amri ya utenganisho ilitumiliwa kwa ukali kabisa. Hawa Bani Hashim mara wakajikuta wamekatwa kwenye njia yao ya kupatia nafaka na mahitaji yao mengine ya maisha; na uhaba mkubwa ukajitokeza kwa sababu hiyo ... akiba hiyo ya Bani Hashim isiyotosheleza iliyojalizwa tena kwa majaribio ya nadra na ya siri, iliwaweka kwenye upungufu na dhiki. Raia waliweza kusikia uliaji wa watoto wanaoteseka kwa njaa ndani ya bonde hilo ... miongoni mwa ndugu wa kundi hili lililotengwa, walipatikana waliojaribu, mbali na vitisho vya Maquraishi, kupitisha mara kwa mara mahitaji kwa hila wakati wa usiku, kwenye kambi ya Abu Talib. Hakim, mjukuu wa Khuwalid, alikuwa, japo jaribio lenyewe wakati mwingine lilikuwa hatari, akibeba mahitaji kumpelekea shangazi yake Khadija.

(The Life of Muhammad, London, 1877)

Mwanzoni mwa karantini hiyo, Ali alikuwa na umri wa miaka 16, na alibebeshwa kazi ngumu na ya hatari ya kuwapatia chakula ukoo mzima. Alitekeleza kazi hii kwa kuhatar-isha sana maisha yake na alileta maji na nafaka wakati wowote alipopata chochote kile. Kwa mfuko mmoja wa ngozi ya mbuzi wa maji, ilimbidi alipie kipande kimoja cha dha-habu, na alijiona mwenye bahati kama alifanikiwa kuufikisha kule kwenye bonde. Juhudi zake, hata hivyo, zilileta nafuu ya kiasi tu kwenye kabila hilo lililozingirwa.

Abu Talib mwenyewe hakuwa akilala usiku. Kwake yeye usalama wa kimwili wa mpwa wake ulipewa umuhimu wa kwanza kuliko kitu kingine chochote. Wakati Muhammad ali-poshikwa na usingizi, Abu Talib alimuamsha na kumwambia alale katika kitanda cha

87

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

mmojawapo kati ya wanawe wanne, na alimuamuru mwanae kulala kwenye kitanda cha Muhammad. Baadae kidogo, atamuamsha mpwa wake tena, na kumwambia aende kwenye kitanda cha mwanae mwingine.

Aliutumia usiku wote katika kumhamisha Muhammad kutoka kwenye kitanda kimoja na kumuweka kwenye kingine. Hakudanganyika juu ya maadui zake; walikuwa wang'ang'an-ifu, wadanganyifu, mafisadi na wasiosamehe. Yeye, kwa hiyo, hakuwatweza. Kama mmoja wao angenyemelea ndani ya bonde hilo kwa nia ya kumuua Muhammad, yumkini kabisa, angemuua mmoja wa watoto wa Abu Talib. Yeye Abu Talib na mkewe daima walikuwa tayari kuwatoa mhanga watoto wao kwa ajili ya Muhammad.

Kulikuwa na nyakati ambapo Ali, licha ya ujasiri na uwezo wake mkubwa, alishindwa kupata mahitaji yoyote, na watoto (na watu wazima pia) waliishi kwa njaa. Lakini kuishi kwa njaa na kiu kulikuwa ni kawaida ndani ya bonde hilo. Wakati maji yakiwepo, akina mama walichemsha majani makavu ndani yake ili kuwaliwaza watoto wao wanaolia. Kilio cha watoto wenye njaa kiliweza kusikika nje ya bonde hilo, na Abu Jahl na Bani Umayya walikipokea kwa kicheko cha dhihaka. Walichekelea "ushindi" wao wa kuwafanya watoto wa Bani Hashim kulilia maji na chakula.

Zawadi ya thamani sana kwa hizi koo zilizotengwa katika miaka hii mitatu, ilikuwa ni maji. Maji yalikuwa ni zawadi ya maisha, na koo mbili hizi ziliyapokea kutoka kwa Khadija. Yeye alimpa Ali vile vipande vya dhahabu ambavyo alinunulia maji. Masikitiko yake juu ya wale waliomzunguka yalijionyesha kwa njia nyingi. Aliswali na kuomba rehma za Allah (s.w.t.) juu ya waliotengwa. Swala ilikuwa ndio "mkakati" wake wa kushughulikia shida. Ilikuwa, alivyouona, ni mkakati rahisi lakini wenye nguvu.

Mara chache, wale marafiki wachache ambao Bani Hashim walikuwa nao huko Makka, walijaribu kuingiza chakula kwa magendo ndani ya bonde hilo, lakini kama hao mapagani walikikamata, walikichukua.

Mmoja wa marafiki wa Bani Hashim aliyekuwako Makka alikuwa ni Hisham ibn Amr al-Aamiri. Aliwaletea chakula na maji kila mara kiasi alivyoweza. Muda aliouchagua wa kupeleka hayo mahitaji kwenye bonde hilo, ulikuwa ni masaa machache kabla ya kucha; lakini hatimae Maquraishi walimkamata, na walitishia kumuua kama angeng'ang'nia kule-ta ngamia wake waliosheheni bondeni hapo kwa ajili ya Bani Hashim. Rafiki mwingine wa siri wa Bani Hashim alikuwa ni Hakim ibn Hizam, mpwawe Khadija. Yeye na mtumwa wake walibeba chakula na maji kumpelekea Khadija ambayo mara moja aliyatoa kwa watoto.

Abul Bukhtari alikuwa mmoja wa marafiki wa Hakim. Yeye pia alileta mahitaji ya lazima kwa Bani Hashim. Usiku mmoja yeye na Hakim walikuwa wamepanda ngamia kwenda

88

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

huko kwenye bonde wakati waliposhitukizwa na Abu Jahl. Aliwaambia kwamba atawanyang'anya zile bidhaa na ngamia. Mwanzoni, Abul Bukhtari akajaribu kuelewana naye kwa maneno lakini hakutaka kusikiliza kitu chochote. Alizuia ile njia ya kwendea kwenye bonde na akakataa kuwapisha wapite.

Abul Bukhtari alijaribu kulazimisha kumpita Abu Jahl, na hili lilisababisha ugomvi mkali wa ngumi kati yao. Mizozo kama hii ilizuka mara kwa mara karibu na bonde hilo lakini wale marafiki wachache ambao ukoo wa Bani Hashim waliokuwa nao hapo mjini, hawakuvunjika moyo, na walifanya kila kitu walichoweza kuwaletea msaada.

Hisham bin Amr al-Aamiri, Hakim bin Hizam, na Abul Bukhtari, hawakuwa Waislamu lakini hawakutaka kuona mtoto yeyote au hata mtumwa wa Bani Hashim akifa kwa njaa, na wakahatarisha maisha yao wenyewe mara kwa mara katika kuleta chakula na maji kwenye Sh'ib Abu Talib. Walikuwa vilevile wakifurahia kulipia madeni ya huduma za msaada kama hizo kwa miaka mitatu, na chote walichokitafuta kama malipo yao kilikuwa ni usalama wa zile koo zilizotengwa.

Haina budi ionyeshwe hapa kwamba ile chuki na hasira ya Bani Umayya ya Quraishi ilielekezwa sio dhidi ya Waislamu bali dhidi ya ukoo wa Bani Hashim. Nia yao ilikuwa ni kuuangamiza Uislamu. Lakini hawangeweza kuangamiza Uislamu bila ya kumuua Muhammad. Walifanya idadi kubwa ya majaribio ya kumuua lakini walishindwa kwa sababu hawakuweza kumfikia. Alikuwa salama na shwari katika "ngome" ambayo Abu Talib na Bani Hashim wameijenga kwa ajili yake.

Bani Umayya waliwalenga kwa usawa kabisa Bani Hashim kama wahusika wa kushindwa kwao kote na kukatishwa tamaa katika vita vyao juu ya Uislamu, na kamwe hawakuipu-uza ili kuwashinda katika mapambano yao marefu na magumu dhidi yake.

Na kwa Waislamu ambao hawakutokana na ukoo wa Bani Hashim, walikuwepo wengi, na wote walikuweko Makka. Hawakwenda Sh'ib Abu Talib pamoja na Bani Hashim. Wengine miongoni mwao wanasemekana walikuwa matajiri, wenye uwezo na mashuhuri, na wote walidai kwamba walikuwa wakimpenda Mtume wao; lakini cha kushangaza, hakuna hata mmoja wao aliyekuja kumuona sembuse kumletea msaada wowote, wakati wa miaka mitatu ya karantini. Walifurahia starehe na usalama wa majumbani mwao hapo mjini kwa miaka mitatu wakati Mtume wao, Muhammad Mustafa, akiishi kwenye ncha ya upanga, akizungukwa na maadui wenye kiu na damu yake, na katika hali ya wasiwasi kamili akiwa hajui kamwe ni matata gani mchana au usiku unaokuja utamletea yeye na kwa ukoo wake.

Karantini hii ya Bani Hashim iliondolewa miaka mitatu baadae, mwaka wa A.D. 619, na ukoo huo ukarudi mjini. Miaka kumi imepita tangu Muhammad, rehma na amani ziwe juu yake na Ahlul-Bait wake, alipotangaza kwa mara ya kwanza ujumbe wake. Mgomo wa

89

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Maquraishi umeshindwa kuzaa matokeo yaliyotarajiwa. Watu wa Bani Hashim walikuwa majasiri, na murua wao ulikuwa juu. Ilikuwa haiwaziki kwao vilevile, hapo mwishoni mwa karantini, kama ilivyokuwa hapo mwanzoni, kumtoa Muhammad, mpendwa wao, kwa maadui wake.

Bani Hashim na Bani Al-Muttalib walirejea majumbani kwao huko Makka baada ya miaka mitatu. Muda wote wa miaka hii mitatu, utajiri wote wa Khadija na Abu Talib ulikwisha. Walikuwa waanze, kama ilivyokuwa, mwanzo mpya katika maisha, kwa kuweka matofali yao kwenye nafasi zao - moja moja.

Kama wakuu wa Maquraishi waliiondoa karantini, haikuwa kwa sababu kulikuwa na "mabadiliko ya moyo" yoyote kwa upande wao. Waliiacha karantini hiyo kwa sababu kulikuwa na nguvu nyingine zilizokuwa zikifanya kazi dhidi yake. Yafuatayo ni maelezo yaliyotolewa katika chanzo cha mapema sana kinachopatikana hadi leo, ‘Wasifu wa Mtukufu Mtume wa Uislamu' cha Muhammad ibn Ishaq, cha matukio yaliyofikia kilele katika kurudi Makka kwa koo za Bani Hashim na Bani al-Muttalib kutoka Sh'ib Abu Talib, baada ya miaka mitatu.

Kutanguka kwa mgomo

"Bani Hashim na Bani al-Muttalib walikuwa katika bonde (maficho ya mlimani) la Sh'ib kwa vile Maquraishi waliweka ahadi ya kuwatenganisha. Kisha baadhi ya watu wa kabila la Quraishi lenyewe walichukua hatua za kuutangua mgomo huo dhidi yao. Hakuna aliyehangaika sana na hili kuliko Hisham ibn Amr ... kwa sababu ya kwam-ba alikuwa mtoto wa ndugu ya Nadla bin Hashim bin Abd Manafi kwa mama yake na alihusiana kwa karibu sana na Bani Hashim. Aliheshimiwa sana na watu wake. Nimesikia kwamba wakati koo hizi mbili zilipokuwa kwenye bonde lao, alikuwa akipeleka ngamia aliyesheheni chakula usiku na kisha, alipokuwa amemfikisha kwenye mlango wa njia, alimuondolea hatamu yake, akampiga kwa kishindo ubavu-ni, na akamfanya akimbie ndani ya uchochoro wa njia inayoelekea kwao. Atafanya vivyo hivyo safari nyingine, akiwaletea nguo.

Akaenda kwa Zubayr bin Abu Umayya bin Al-Mughira ambaye mama yake alikuwa ni Atika binti ya Abdul Muttalib na akasema: 'Unaridhika kula chakula na maji na kuvaa nguo wakati ukijua hali ya ami zako wa kikeni? Hawawezi kununua au kuuza au kuchanganya damu. Wallahi kama wangekuwa ami za Abu'l-Hakam bin Hisham (Abu Jahl), na ukamtaka afanye alivyokutaka wewe ufanye, asingelikubali hilo kamwe.' Yeye (Zubayr) akasema, 'Unanishangaza wewe Hisham, mimi nitafanya nini? Nipo mtu mmoja tu. Wallahi, kama ningekuwa na mtu mwingine wa kuniunga mkono mimi, ningeutangua mapema sana.' Akasema, 'Nimepata mtu - mimi mwenyewe.' 'Tafuta mwingine,' akasema. Hivyo Hisham akaenda kwa Al-Mutim bin

90

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Adiy na akasema, 'unaridhika kwamba koo mbili za Bani Abd Manafi ziangamie huku ukiona ukiwaafiki kuwafuata Maquraishi? Utaona kwamba hivi karibuni watak-ufanyia vivyo hivyo na wewe.' Mutim akatoa jibu kama lile la Zibayr na akataka mtu wa nne.

Hivyo Hisham akaenda kwa Abu'l Bukhtari bin Hisham ambaye alitaka mtu wa tano, na kisha kwa Zama'a bin Al-Aswad bin Al-Muttalib, ambaye aliomba mtu wa sita, na akamkumbusha udugu na wajibu wao. Aliuliza endapo wengine walikuwa tayari kushirikiana kwenye kazi hii. Akampa majina ya wale wengine. Wakakubaliana wote kukutana usiku karibu na Hujun, juu ya Makka, na walipokutana, walijifunga kulichukulia swala la ile hati hadi wamepata utanguzi wake.

Siku iliyofuata, wakati watu walipokusanyika pamoja, Zubayr alivaa joho, akazungu-ka Al-Kaaba mara saba; kisha akaja mbele na kusema: 'Enyi watu wa Makka, hivi sisi tule na kujivisha wenyewe wakati Banu Hashim wanaangamia, wakiwa hawawezi kununua wala kuuza? Wallahi sintapumzika hadi pale hati hii ya mgomo muovu itakapopasuliwa!

Abu Jahal akapaza sauti: 'Unajidanganya. Haitapasuliwa.'

Zama'a akasema: "Wewe ni muongo mkubwa; hatukuipenda hati hii hata pale mwan-zo iliporasimiwa na kutiwa saini."Abu'l Bukhtari akasema, 'Zama'a anasema kweli. Hatukuridhika na hati hii ilipokuwa inaandikwa, na haturidhiki nayo sasa hivi.'

Al-Mutim akaongeza: "Wote mnasema kweli, na yeyote anayesema vinginevyo, huyo ni muongo. Tunamuomba Allah ashuhudie kwamba tunajitoa kwenye wazo zima na kile kilichoandikwa kwenye hati hiyo." Hisham akaongea kwa maana hiyo hiyo, na akawaunga mkono marafiki zake.

Kisha Al-Mutim akaiendea ile hati na kuichana vipande vipande. Aligundua kwamba wadudu walikwisha itafuna isipokuwa yale maneno, "Kwa Jina lako Ewe Allah (s.w.t.)" Hii ni kanuni iliyozoeleka ya Maquraishi ya kuanzia maandishi yao. Mwandishi wa hati hii alikuwa ni Mansur bin Ikrima."

Mutim ibn Adiy akachana ile hati ya fedheha ya Maquraishi katika vipande vipande. Vile vipande vikapeperushwa na upepo, na hakuna sazo lililoachwa. Ni kitendo kilichohitaji msimamo na ujasiri - msimamo kwamba Bani Hashim walikuwa waathirika wa udhalimu, ukatili na majuto, wasio na hatia; na ujasiri kuwakaidi Maquraishi. Kitendo chake imara kilikuwa ni ishara kwamba ile karantini ya Bani Hashim imekwisha, na kwamba watu wake sasa wanaweza kurejea mjini. Mutim mwenyewe na wapiganaji vijana wa ukoo wake walikwenda kwa vipando vyao wakiwa katika mavazi kamili ya kivita, kwenye bonde hilo

91

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

na kumsindikiza Muhammad Mustafa na watu wote wa koo mbili za Bani Hashim na Bani al-Muttalib, kurudi Makka na majumbani kwao.

Dr. Muhammad Hamidullah anaandika kwenye ukurasa wa 10 wa kitabu chake, Introduction to Uislamu, kilichochapishwa na International Islamuic Federation of Student Organizations, Salimiah, Kuwait (1977):

Baada ya miaka mitatu, watu wanne au watano wasiokuwa Waislamu, wenye ubinaadamu zaidi kuliko wote waliobakia na wanaotokana na koo tofauti, walitangaza bayana shutuma zao za ule mgomo wa kiuonevu.

Dr. Hamidullah amedhania kwamba kushindwa kwa mgomo huu ni matokeo ya ubi-nadamu wa "watu wanne au watano wasiokuwa Waislamu." Walikuwa, anasema, 'wenye ubinadamu zaidi kuliko wengine waliobaki.' Ana haki. Lakini walikuwa na ubinadamu zaidi hata ya waleWaislamu waliokuwa wakiishi Makka?

Kwa mshangao, cha ajabu, jibu la swali hili lenye kughasi ni la kukubali. Hata hivyo, mbali na hawa mashujaa watano - wasiokuwa Waislamu, wote - ubinadamu haukumsukuma mtu mwingine yeyote hapo Makka - asiyekuwa mwislamu au mwislamu - kuwakaidi Maquraishi na kutenda katika ulinzi wa Bani Hashim.

Kuna swali jingine moja, yaani, kwa nini Zubayr alijiona yuko yeye peke yake?

Wakati Hisham alipolijulisha kwa mara ya kwanza hili suala la kutangua huu Mkataba wa washirikina wa kuwagomea hawa Bani Hashim, kwa rafiki yake Zubayr, na akamsuta kwa kutokuwa na hisia juu ya mateso ya Bani Hashim, na kwa kushindwa kwake kushughuli-ka kuyamaliza mateso yale, Zubayr akasema, "Unanishangaza ewe Hisham, mimi nifanye nini? Mimi ni mtu mmoja pekee. Wallahi, kama ningekuwa na mtu mwingine wa kuniun-ga mkono, ningeutangua mapema tu."

Jibu la Zubayr ni la fumbo. Kwa nini alijiona yuko peke yake? Kwa nini asijaribu kuorod-hesha uungaji mkono wa Waislamu ambao walikuwa wengi hapo Makka? Kwa mujibu wa wanahistoria, baadhi ya Waislamu hapo Makka walikuwa ni watu wenye hadhi na wenye mali, na walikuwa na ushawishi wa kutosha kwa washirikina. Lakini kwa sababu za kisirisiri, haikuwajia ama kwa Zubayr mwenyewe au kwa rafiki yake yoyote, kuwaku-sanya Waislamu hawa kwenye kundi moja - "timu" - ambalo lilimaliza huu mgomo kwa Bani Hashim.

Zubayr na rafiki zake walifanikiwa katika juhudi zao za kuwarudisha Bani Hashim hapo mjini. Lakini kwa kitendo chao hiki, wamedhihirisha kwamba wale Waislamu ambao walikuwa wanaishi Makka, hawakuwa "wenye lazima" kwa Muhammad au kwa Uislamu.

92

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ni mojawapo ya ukweli mkubwa kabisa unaofanana na uongo katika historia ya Uislamu kwamba ule mkono uliofikia na kuchana vipande vipande, ule mkataba wa washirikina wa kuutenga na kuuhamisha ule ukoo wa Bani Hashim, ulitokana, sio kwa "mu'min" bali kwa "asiyeamini" Mutim ibn Adiy! Sio Mutim wala yeyote kati ya marafiki zake wanne, yaani, Hisham ibn Amr, Zubayr ibn Abu Umayya, Abu'l Bukhtari ibn Hisham, na Zama'a ibn Al-Aswad, aliyekuwa mwislamu. Lakini wote watano walikuwa mashujaa wenye maadili, na hawakuridhia katika dhulma iliyokuwa ikifanywa kwa Bani Hashim. Hawakutulia mpaka waliporejesha haki ndani ya Makka.

Kusema kweli, hawa mashujaa watano hawakuwa Waislamu. Lakini wao na wao wenyewe tu walikuwa na ujasiri na busara ya kutetea kanuni ambayo ni ya Kiislam, yaani, ile Kanuni ya Haki. Walitetea haki, na kitendo chao cha kishujaa, kiliwaletea sifa njema ya kudumu katika kisa kirefu cha historia ya Uislamu.

Waislamu, kwa upande mwingine, sio tu hawakushughulika; hawakuupinga walau, ule ubeuzi na uonevu wa Maquraishi katika kuwafukuza Bani Hashim kutoka Makka. Walidumisha, kwa miaka mitatu, upweke wenye hadhari na ukimya usioaminika. Matendo yao, inavyoonekana, yalitawaliwa na busara. Kwa hiyo, yote yale waliyofanya, ilikuwa ni kupitisha muda, na kuangalia mwelekeo wa matukio, kama watazamaji wasiojali.

93

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Vifo vya Khadija na Abu Talib

Shukrani kwa uungwana na ujasiri wa wale mashujaa watano wa Makka, kwa vile watu wa ukoo wa Bani Hashim wamewewza sasa kuishi majumbani mwao tena. Lakini walikuwa hata hawajaweza kupata nafuu vizuri kutokana na uchovu wa kuishi kwenye maficho ya mlimani kwa miaka mitatu, wakati Khadija, yule mke, rafiki na sahaba wa Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.w.t.), na yule mfadhili wa Uislamu na Waislamu, alipougua na kufa. Maisha yake yote aliishi katikati ya starehe na wingi wa anasa lakini miaka ile mitatu ya uhamishoni ilikuwa ni wakati wa ugumu uliozidi kiasi kwake ambao bila ya kuk-wepa ulimuua.

Kama ilivyoonyeshwa kabla, Khadija alikuwa ndiye mwanamke wa kwanza hasa katika dunia nzima kutamka kwamba Mungu ni Mmoja, na Muhammad alikuwa ni Mtume Wake kwa wanadamu wote. Heshima na sifa ya kuwa Muumini wa Kwanza katika dunia nzima ni yake milele. Alijitolea raha zake, mali yake, na nyumba yake kwa ajili ya Uislamu; na sasa itaonekana kama amejitoa mhanga maisha yake pia. Bila ya shaka, kama angeishi katika nyumba yake yenye nafasi na anasa hapo Makka, akiwa amezungukwa na watu-mishi wake wa kike, angeweza kuishi kwa miaka mingi zaidi. Lakini alipendelea kusima-ma na mume wake na ukoo wake, na kushiriki machungu ya maisha pamoja nao. Katika wakati wa karantini, ilimbidi avumilie sio tu makali ya njaa na kiu bali pia na vipeo vya juu vya joto katika kiangazi na baridi wakati wa kipupwe, na bado hakuna aliyesikia kamwe neno la kulalamika kutoka kwake, na kamwe hakupoteza utulivu wake. Kama nyakati zilikuwa nzuri au mbaya, ama alikuwa na kitu kwa wingi au alikuwa hana cho-chote, daima alikuwa mwenye furaha hata kule uhamishoni. Kukoseshwa na ugumu kamwe havikuuchukiza moyo wake. Ulikuwa ni moyo wake uliokuwa chanzo cha nguvu isiyoshindika, faraja na ujasiri kwa mume wake katika nyakati unyonge uliokithiri za maisha yake.

Katika ile miaka ya karantini, Khadija alitumia mali yake nyingi sana kwa kununulia mahi-taji muhimu ya maisha kama maji, chakula na nguo kwa ajili ya ukoo huo na mumewe. Aliporudi kwenye nyumba yake, senti yake ya mwisho ilikuwa imekwenda; na alipokufa, hamkuwa na pesa ya kutosha humo ndani ya nyumba ya kununulia sanda. Shuka la mumewe lilitumika kama sanda yake, na alizikwa ndani yake.

Muhammad Mustafa kamwe hakuoa mke mwingine wakati Khadija alivyokuwa hai, na kama asingekufa, inawezekana kabisa kwamba asingeoa mwanamke mwingine yeyote.

94

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Edward Gibbon

"Katika miaka 24 ya ndoa yao, mumewe Khadija aliyekuwa kijana alijinyima haki ya kuoa wake wengi, na fahari au upendo wa mke huyu mwenye kuheshimika ulikuwa bado haujafedheheshwa na jamii ya upinzani. Baada ya kifo chake, Mtume (s.a.w.) alimuweka katika cheo cha wanawake wanne wema, pamoja na dada yake Musa, mama yake Isa (Yesu), na Fatima, mpendwa bora wa mabinti zake.

(The Decline and Fall of the Roman Empire) Sir John Glubb

"Khadija alikuwa mfuasi wa kwanza wa Muhammad. Kutoka wakati wa mwito wake wa kwanza, mpaka kifo chake miaka tisa baadae, Khadija hakuyumba kamwe. Wakati wowote Mtume (s.a.w.) alipokabiliana na dhihaka au hitilafu, alikuwa na uhakika, pale atakaporudi nyumbani jioni, wa kumpata mliwazaji mcheshi na mwenye upendo. Alikuwa tayari wakati wote kwa akili yake timamu kuhifadhi ujasiri wake na kumpunguzia mzigo wa hofu zake."

(The Life and Times of Muhammad, New York, 1970)

Ibn Ishaq, yule mwandishi wa wasifu wa Mtume, anasema kwamba kulipokuwa na kuanza tena kushuka kwa Wahyi baada ya kusimama kwake kufuatia kushuka kwa awali, Khadija alipokea Heshima Tukufu na salamu ya amani kutoka kwa Allah (s.w.t.) Ujumbe huo ulifik-ishwa kwa Muhammad na Jibril, naye alipoufikisha kwa Khadija, akasema Khadija: "Allah (s.w.t.) ni Amani (as-Salam), na kutoka Kwake ni Amani tupu, na amani iwe juu ya Jibril."

Muhammad Mustafa daima alimkumbuka Khadija kwa mapenzi, upendo na shukurani. Wakati wa maradhi yake mafupi, alikesha usiku mzima akimuuguza, kumliwaza na kumuombea. Alimwambia kwamba Allah (s.w.t.) amemjengea kasiri la lulu ndani ya Pepo. Kifo chake kiliujaza moyo wake huzuni nzito.

Khadija alikufa mwezi 10 ya Ramadhani ya mwaka wa kumi wa Tangazo la Uislamu. Alizikwa huko Hujun juu ya Makka. Baada ya mazishi, Mtume (s.a.w.) mwenyewe alisawazisha udongo wa kaburi lake.

Mwezi mmoja baada ya kifo cha Khadija, Mtume (s.a.w.) alipata mshituko mwingine katika kifo cha Abu Talib, ami yake na mlezi wake. Abu Talib alikuwa ndio ngao ya Uislamu tangu kuanzishwa kwake. Vifo vya marafiki hawa wawili, Khadija na Abu Talib, vilikuwa ndio mshituko mkubwa na huzuni ambavyo ilimbidi avivumilie katika miaka hamsini ya maisha yake. Aliuita ule mwaka wa vifo vyao "Mwaka wa Huzuni."

95

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ule mwaka wa 619 uligeuka kuwa mwaka wa huzuni kwa Muhammad Mustafa kwa maana zaidi ya moja. Kifo cha mpenzi wa mtu kwa kawaida ni chanzo cha huzuni. Lakini kwa upande wake yeye, vifo vya hawa marafiki wawili havikuwa tukio la kinafsi tu. Mara tu, alifahamishwa maana ya vifo vyao kwa mfululizo wa matukio yasiyofungamana.

Ibn Ishaq

Khadija na Abu Talib walikufa mwaka mmoja, na kwa kifo chake Khadija matatizo yalifuatia haraka nyuma ya kila mtu, kwani alikuwa mtoaji msaada mkubwa kwake katika Uislamu, na alikuwa akimwelezea matatizo yake. Kwa kifo cha Abu Talib, alipoteza nguvu na tegemeo katika maisha yake binafsi na ulinzi na kinga dhidi ya kabila lake. Abu Talib alikufa miaka mitatu kabla ya yeye (Muhammad) kuhamia Madina, na ilikuwa hapo ambapo kwamba Maquraishi walimshughulikia kwa njia ya maonevu ambayo wasingeweza kuthubutu kuifuata katika uhai wa ami yake. Baradhuli mdogo kwa kweli alimtupia vumbi kichwani mwake.

Hisham kutoka kwa baba yake, Urwa, aliniambia kwamba Mtume (s.a.w.) aliingia ndani ya nyumba yake, na alikuwa amesema, "Maquraishi kamwe hawakunitendea hivi wakati Abu Talib alipokuwa hai."

(The Life of the Messenger of God) Washington Irving

"Muhammad mara akatambua kupotelewa alikokupata katika kifo cha Abu Talib ambaye alikuwa sio tu ndugu mpendwa, bali mlinzi imara na mwenye madaraka, kutokana na umaarufu wake hapo Makka. Kwa kufa kwake hapakuwa na mtu yeyote wa kusimamisha na kukinza uhasama wa Abu Sufyan na Abu Jahl."

Bahati ya Muhammad ikawa inakuwa mbaya na mbaya zaidi katika mahali pake pa asili. Khadija, mfadhili wake wa awali, yule sahaba mwaminifu wa faragha yake na upweke, yule muumini mwenye shauku kwenye mafundisho yake, alikuwa amekufa; vilevile na Abu Talib, wakati fulani aliyekuwa mhifadhi mwaminifu na madhubuti. Akinyimwa uzoefu wa ulinzi wa Abu Talib, Muhammad amekuwa kwa namna fulani, aliyetengwa na jamii hapo Makka, akilazimika kujificha na kubakia kuwa mzigo juu ya ukarimu wa wale ambao mafundisho yake mwenyewe yamewaingiza kwenye mateso (sic-japo kwa makosa). Kama manufaa ya dunia yangekuwa ndio lengo lake, yamepatikana vipi?

(Life of Muhammad)

Katika kusema kwamba Muhammad aligeuka kuwa "mzigo juu ya ukarimu wa wale ambao mafundisho yake mwenyewe yamewaingiza kwenye mateso," yule mwanahis-toria aliyetajwa hapo juu, ameelezea dhana ambayo kwamba hatuwezi kukubaliana nayo. Muhammad kamwe hakuwa mzigo kwa mtu yeyote kwa wakati wowote. Watu

96

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

wa ukoo wake, hawa Bani Hashim, waliona kama ni upendeleo na heshima kumkinga na kumlinda yeye dhidi ya maadui zake.

Sir William Muir:

"Kujitolea ambako Abu Talib alijitokeza yeye binafsi na familia yake kwa ajili ya mpwa wake, ambapo bado alikuwa haamini ujumbe wake (sic. - hii sio kweli), kulithibitisha tabia yake kama ya utukufu wa kipekee na asiye na choyo. Kunatoa kwa wakati huo huo uthibitisho mzito wa uaminifu wa Muhammad. Abu Talib asingeweza kufanya hivyo kama mdanganyifu anayejipendeza; na alikuwa na uwezo wa kutosha kufanya uchunguzi."

Wakati mkuu wa familia alipoona maisha yanadhoofika, aliwaita ndugu zake, wana wa Abd al-Muttalib, kuzunguka kitinda chake, akamuweka mpwa wake mikononi mwao kumlinda; na, akapokelewa dhamana hiyo, akafa kwa amani, na akazikwa sio mbali sana na kaburi la Khadija. Muhammad alimlilia kwa uchungu sana ami yake; na sio bila sababu. Kwa miaka arobaini amekuwa ni rafiki yake mwaminifu - nguzo ya utotoni mwake, mlezi wa ujana wake, na katika maisha ya baadae, aliyemtegemea kwa ulinzi. Kutokuamini kwake hasa (sic - hii sio kweli) kulifanya athari zake kuwa na nguvu zaidi. Kwa kiasi cha muda alipokuwa hai, Muhammad hakuwa na haja ya kuogopa vurugu au mashambulizi. Lakini hapakuwa na mkono (mtu) wenye nguvu sasa ya kumlinda kutokana na maadui zake. Khadija wa pili anaweza kupatikana, lakini sio Abu Talib wa pili.

(The Life of Muhammad, London, 1877) Sir John Glubb:

"Mtume (s.a.w.) alifanya juhudi kubwa sana kumshawishi Abu Talib kurudia ile sha-hada ya imani ya Kiislam, lakini alilala kimya bila ya kujibu, mpaka alipokufa (sic. hii sio kweli). Abu Talib kwetu sisi anaelekea kuwa mtu wa kuvutia. Msema kweli, mwaminifu na mwenye huruma, alivumilia mashaka mengi, hasara na hitilafu ili kumlinda mpwa wake, ingawa hakuwa akiamini mafundisho yake (sic. - hii sio kweli). Huchukuliwa kama shujaa na Waislamu, kwani alikufa katika ukafiri (sic. -hii sio kweli). Hata hivyo, kama isingekuwa kwa ujasiri imara ambao kwawo alisi-mama nao kwa mpwa wake, Uislamu ungekufa katika chimbuko lake.

(The Life and Times of Muhammad, New York, 1970)

Nimewanukuu hapo juu Sir William Muir na Sir John Glubb neno kwa neno. Wamepiga vijembe kwamba Abu Talib alikufa katika ukafiri. Kama watapewa changamoto ya kutoa rejea ya maelezo hayo, watamtaja Bukhari. Bukhari anasema kwamba Abu Talib

97

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

alipokuwa kwenye kitanda chake cha umauti, Mtume (s.a.w.) alimsisitiza awe mwislamu lakini akasema kwamba kufanya hivyo kutamfedhehesha kwa marafiki zake wa kiquraishi.

Waandishi wa "Hadith" hii walisahau kitu kimoja. Abu Talib alikuwa anakufa, na akijua kwamba hatawaona "marafiki" zake Maquraishi tena. Alijua kwamba anakwenda mbele kwa Muumba wake. Kwa muda kama huu asingelijali sana juu ya Quraishi. Shauku yake wakati wote ilikuwa ni kupata radhi za Allah (s.w.t.) na alithibitisha kwa matendo yake zaidi kuliko ambavyo mtu mwingine yeyote angeweza kuthibitisha kwa maneno yake, kwamba imani yake katika Tawhid ya Allah (s.w.t.) na katika ujumbe wa Muhammad kama Mtume Wake, ilikuwa kama jiwe na haitikisiki.

Abu Talib alikuwa mu'min mwenye moyo wa bidii katika Uislamu. Kujiambatanisha kwake kwenye Uislamu kunadhihirishwa na msimamo wake na mantiki ya mambo.

Hakuna mtu anayeweza kumpenda Muhammad na uabudu masanamu kwa wakati mmoja; mapenzi mawili hayo yote yanajitenga. Na hakuna mtu anayeweza kumpenda Muhammad na bado auchukie Uislamu. Upendo kwa Muhammad na chuki kwa Uislamu haviwezi kuwa pamoja. Mwenye kumpenda Muhammad, ni lazima, bila kukwepa, aupende Uislamu. Wala hawezi mtu akamchukia Muhammad na akaupenda Uislamu. Dhana kama hiyo itakuwa kichekesho kikubwa sana.

Kama kuna kitu kimoja chochote kisicho na shaka yoyote ile katika historia ya Uislamu, ni mapenzi ya Abu Talib kwa Muhammad. Kama ilivyoonyeshwa kabla, Abu Talib na mkewe, Fatima bint Asad, walimpenda Muhammad zaidi ya walivyowapenda watoto wao wenyewe. Wote mume na mke walikuwa tayari daima kuwatoa watoto wao muhanga kwa ajili ya Muhammad. Mapenzi kama hayo yangeweza tu kuwa na kiini kimoja tu, kile cha imani juu ya Muhammad na Uislamu. Mkewe Abu Talib, Fatima bint Asad, yule mama wa kunyonya wa Muhammad, alikuwa ndiye mwanamke wa pili kuingia Uislamu, wa kwan-za akiwa ni Khadija.

Abu Talib alikuwa na fahari kwamba Allah (s.w.t.) amemchagua Muhammad, mwana wa kaka yake, Abdullah, katika viumbe wote, kuwa Mtume Wake wa Mwisho kwa wanadamu. Muhammad alikuwa ni kipenzi mkubwa na fahari kuu ya ami yake, Abu Talib.

Vitendo vitukufu vya Abu Talib ni sehemu muhimu sana katika Hadith ya Uislamu. Hakuna Hadith ya Uislamu ambayo ama itakuwa imekamilika au kuwa ya kweli kama haikuingiza maelezo ya jukumu lake kama mlinzi wa Muhammad na ngao ya Uislamu. Matendo yake ndio uthibitisho fasaha wa imani yake juu ya Allah (s.w.t.) na Mtume Wake. Allah (s.w.t.) awarehemu waja wake watiifu, Khadija; Abu Talib na mke wake, Fatima binti Asad. Wote watatu walikuwa ndio "vyombo" ambavyo kwavyo Ameuimarisha Uislamu, na kuuwezesha kuwepo.

98

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Safari ya Muhammad kwenda Taif

Zaidi ya miaka kumi imepita tangu muhammad, rehma na amani juu yake na Ahlul-Bait wake, alipoanza kutangaza Uislamu. Mafanikio yake katika miaka hii kumi yamekuwa kidogo ni ya wastani, yakiishia kama ilivyokuwa, kwenye kusilimisha chini ya watu 170 wake kwa waume hapo Makka. Lakini baada ya kifo cha mke wake, Khadija, na ami yake, Abu Talib, ilionekana kwamba Maquraishi wangemnyang'anya hata yale mafanikio mado-go kutoka mikononi mwake. Makka ilithibitika kuwa isiyokalika kwa Waislamu na iliji-tokeza kwa Mtume (s.a.w.) kwamba alipaswa, pengine kujaribu kuilingania hii imani mpya kwenye mji mwingine. Mji wa karibu sana ulikuwa ni Taif, maili 70 upande wa Kusini-Mashariki ya Makka, na alikwenda huko mwishoni mwa mwaka 619. Alifuatana pamoja na Zayd bin Haritha.

Akiwa huko Taif, Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) aliwatembelea wakuu watatu wa makabila ya wenyeji wa hapo, na akawalingania waache uabudu masanamu wao mbaya, na kukubali Tawhid ya Allah (s.w.t.) kukana heshima zilizoundwa na watu za jamii yote, na kuamini katika usawa na udugu wa watu wote.

Wale wakuu wa Taif walikuwa watu wa majivuno na kiburi, na hawakutaka hata kumsik-iliza Muhammad. Walimkaribisha kwa dhihaka na kebehi na wakamshakizia wale watu wazembe na mabaradhuri wa mji huo. Walimshambulia yeye na Zayd kwa kuwatupia madongo na mawe. Akiwa amejeruhiwa na kufunikwa na damu, Muhammad aliyum-bayumba kutoka nje ya Taif. Mara alipofika nje ya kuta za mji, karibu azirai lakini mkuli-ma wa bustani mmoja alimchukua nyumbani kwake, akamfunga majeraha yake, na akamwacha apumzike na kurudisha nguvu, mpaka alipojisikia mwenye nguvu za kutosha kuanza tena safari yake kuvuka nchi ngumu kati ya Taif na Makka.

Lakini Muhammad alipowasili kwenye viunga vya Makka, alihisi kwamba hangeweza kuingia tena kwenye mji wake wa asili sasa kwa vile ami yake, Abu Talib, hakuwepo pale kumlinda. Uhasama wa wapagani juu yake umefikia kiwango cha hatari. Alitambua kwamba kama ataingia Makka, anaweza kuuawa. Muhammad hakuweza kuingia mji wake wa nyumbani, na hapakuwa na sehemu nyingine ya kwenda. Je, angefanya nini?

Katika hali hii mbaya, Muhammad alituma habari kwa mabwana wakubwa watatu wa hapo mjini akiwaomba kila mmoja wao amchukue chini ya ulinzi wake. Wawili wao walikataa lakini yuke wa tatu - yule muungwana Mutim ibm Adiy - aliijibu ile ishara yake ya wasi-wasi. Alikuwa ni Mutim yuleyule, ambaye hapo mwanzoni, aliwaasi wale wakubwa wa Maquraishi kwa kuchanachana ule mkataba wa kuwagomea Bani Hashim, na alizirudisha

99

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

zile koo mbili za Bani Hashim na Bani al-Muttalib kutoka Sh'ib Abu Talib kuja mjini. Mutim aliamuru wanae, wapwa zake na vijana wengine wa ukoo wake kuvaa mavazi yao ya kivita. Kisha yeye akatoka, katika mavazi maridadi na kamili ya kivita, akiwa mbele yao, kwenda nje ya mji. Alimleta Muhammad Mustafa pamoja naye, kwanza kwenye mae-neo ya Al-Kaaba ambako Muhammad alifanya ile mizunguko saba ya desturi, na kisha akamsindikiza nyumbani kwake.

Abd-al-Rahman 'Azzam:

"Hakuna hata mmoja kati ya machifu wa Makka ambao Muhammad aliomba kwao ulinzi kwa ajili ya kuingia kwa salama hapo mjini aliyeweza kumtolea msaada; laki-ni chifu mmoja muungwana wa kipagani, al-Mutim ibn Adiy, alimchukua chini ya ulinzi wake na kumrudisha nyumbani. Hivyo ndivyo Muhammad alivyoingia tena Makka - akilindwa na mshirikina!"

(The Eternal Message of Muhammad, chapa ya New English Library, London, 1964) Sir John Glubb:

"Huko Taif Mtume (s.a.w.) alipigwa mawe na kufukuzwa. Akiogopa kurudi Makka sasa kwa vile hakufaidi tena ulinzi wa Abu Talib, alituma ujumbe kwa baadhi ya waabudu masanamu wakuu, akiwaomba ulinzi wao. Wawili walikataa lakini hatimae Mutim ibn Adiy, mkuu wa ukoo wa Nufal wa Quraishi, alikubali kumlinda. Asubuhi iliyofuata, yeye, wanae na wapwa zake walitoka na silaha kamili kwenda kwenye uwanja wa hadhara wa Al-Kaaba, na kutangaza kwamba Muhammad alikuwa chini ya ulinzi wao. Ulinzi huu wa Mutim ibn Adiy ulimuwezesha Mtume (s.a.w.) kurudi Makka.

(The Life and Times of Muhammad, New York, 1970)

Maombi ya Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.w.t.) wakati wa kurudi kwake kutoka Taif, kwa Mutim ibn Adiy, asiyekuwa mwislamu kuomba ulinzi wake, yanaleta tena, swali baya sana, katika namna iliyolenga sana, kwenye msimamo na tabia ya Waislamu. Kwa nini Mtume (s.a.w.) hakumuomba yeyote kati yao kumchukua kwenye ulinzi wake ingawaje baadhi yao walisemekana kuwa matajiri na maarufu, na wengine wao wali-tangazwa kuwa ndio tishio la wapagani? Kwa nini ikawa kwamba Mtume (s.a.w.) alitafu-ta ulinzi wa asiyekuwa mwislamu lakini hakujidhalilisha japo kwa kuwajulisha hao Waislamu kwamba alitaka kuingia tena Makka na alikuwa akihitaji ulinzi?

Au swali jingine! Kwa nini hao Waislamu wenyewe hawakwenda kwenye lango la mji na kumsindikiza Mtume wao nyumbani kwake? Hapa walikuwa na fursa nzuri ya kumuonye-sha yeye kwamba wanastahili kuaminiwa naye hata kama aliwaona hawafai. Lakini wali-

100

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ikosa fursa hiyo. Hawakufanya kitu chochote ambacho kingeweza kuonyesha kwamba wana shauku yoyote juu ya usalama wake binafsi.

Arabia ya kipagani, hata hivyo, haikukosa sehemu yake ya uungwana na ushujaa. Sifa hizi zilionyeshwa na Mutim ibn Adiy, Abul Bukhtari na wengine wachache. Walikuwa ndio mashujaa wa Arabia, na ilikuwa ni uungwana wao ulioifanya nchi yao kuwa maarufu katika karne za baadae. Arabia ya kipagani kamwe haikutoa watu waungwana zaidi kuliko hawa. Hata Waislamu wanapaswa kutambua deni lao la shukurani kwao. Hata hivyo ilikuwa ni wao walioweza kuwapa changamoto Maquraishi katika baadhi ya nyakati ngumu sana za maisha ya Mtume wa Uislamu. Kwa kufanya hivyo, walishinikizwa tu na mawazo yao binafsi ya uungwana. Walichukulia kuwa ni wajibu wao kuwalinda wale wasio na ulinzi.

Kushindwa kule kwa Taif kulikuwa ni kwa kuvunja moyo sana kwa Mtume, na alijua kwamba bila ule uingiliaji kati wa kishujaa wa Mutim ibn Adiy, asingeweza kabisa kuin-gia Makka. Kwa mtazamaji wa kawaida inaweza kuonekana kwamba Mtume (s.a.w.) ali-fikia kilele cha uvumilivu wa kibinadamu na subira. Maendeleo ya Uislamu yamesimama, na mtazamo wa baadae haukuweza kuonekana wazi zaidi.

Lakini je, Muhammad alikubali kukata tamaa mbele ya kushindwa kwa mfululizo na mbele ya makabiliano makali na washirikina? Ingekuwa ni kawaida tu kama angekubali. Lakini hakukubali. Hakukatia tamaa kamwe rehma za Allah (s.w.t.) zisizo na mpaka. Alijua kwamba anafanya kazi ya Allah (s.w.t.) na hakuwa na shaka yoyote kwamba ange-muongoza kumtoa kwenye giza la ukosaji matumaini na msaada kwenda mahali pa ushin-di na baraka.

Ilikuwa ni katika moja ya nyakati za kiza kikuu na huzuni kubwa za maisha yake ambapo Muhammad, Mtume wa Uislamu, alinyanyuliwa na Allah (s.w.t.) kwenda mbingu ya juu kabisa, huenda ni katika kutambua kukataa kwake kukubali kushindwa na kutokuwa imara katika mpangilio wa kazi. Allah (s.w.t.) alimtunuku Mtume wake na Isra' na Mi'raj. Isra' ni ile safari yake ya usiku kutoka "Msikiti mtukufu" kwenda "Msikiti wa Mbali" (Masjid al-Aqsa); na Mi'raj ni kule kupanda kwenda Mbingnii. Isra' na Mi'raj ziliashiria matukio makubwa na ya kihistoria ambayo tayari yalikuwa yametawala mawazoni, ingawa kwa wakati huo hapakuwa na uwezo wa kuyatambua.

Maana ya kimuujiza ya Mi'raj inahusika kwenye juhudi za kudumu za nafsi binafsi dhidi ya maovu. Ina vipingamizi vyake na madhaifu yake. Lakini kama ina ukweli kwake yenyewe, na kweli katika Imani juu ya Allah (s.w.t.), Yeye ataipa ushindi dhidi ya maovu. Hadithi ya Mi'raj, kwa hiyo, ni mwanzo unaofaa kwenye safari ya nafsi ya mwanadamu katika maisha. Hatua ya kwanza juu ya safari hii ni ya kuchukuliwa kupitia mwenendo wa utashi - hisia ya wajibu binafsi kwa ajili ya ustawi wa wanadamu wenzie, utumishi kwa

101

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Allah (s.w.t.), kupitia kutumikia viumbe Vyake, na utambuzi wa kuwepo Kwake nasi nyakati zote.

Isra' imetajwa katika Aya ya kwanza ya Sura ya 17 ya Qur'an Tukufu kama ifuatavyo:

Ametakasika aliyemchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa mbali, ambao tumevibariki vilivyouzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.

Isra' na Mi'raj zilitokea katika usiku wa tarehe 27 ya Rajab (mwezi wa saba wa kalenda ya Kiislam) wa mwaka wa kumi na mbili wa Tangazo la Uislamu, yaani, mwaka mmoja kabla ya Hijira ya Mtume (s.a.w.) kutoka Makka kwenda Madina.

102

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Maeneo Mapya ya Uislamu

Yathrib ulikuwa ni mji kwenye chemchem karibu maili 250 kaskazini ya Makka. Mnamo mwaka wa 620 A.D., watu sita wa Yathrib walitembelea Makka kwa ajili ya Hija. Kukutana kwao kwa bahati na Muhammad kulisababisha kuingia kwao kwenye Uislamu. Walimwambia yeye kuwa waliiacha Yathrib katika hali ya kutokota na kwamba inaweza kulipuka wakati wowote kwenye vita. Lakini walionyesha matumaini kwamba Allah (s.w.t.) atairudisha amani kwenye mji wao kupitia kwa Mtume Wake. Waliahidi pia kuru-di Makka na kukutana naye mwaka unaofuata.

Huu ulikuwa ndio mwanzo wa Uislamu huko Yathrib.

Wakati hawa Waislamu wapya sita waliporejea Yathrib, waliongea na jamaa zao na marafi-ki kuhusu Uislamu, na wakawaona wanaridhia, hata kuwa na shauku ya kusikiliza. Mwaka mmoja baadae, wakati msimu wa hija ulipofika, wenyeji kumi na wawili wa Yathrib, pamoja na wale sita wa mwanzo, walitembelea Makka. Miongoni mwao walikuwemo wanawake wawili pia. Walikutana na Mtume wa Allah (s.w.t.) huko Aghaba. Aliwaelezea juu ya Shuruti za Imani katika Uislamu, na wote wakaukubali Uislamu. Wakati huo huo, walimpa pia kiapo chao cha utii. Hiki kinaitwa Kiapo cha Kwanza cha Aghaba.

Waislamu hawa walimhakikishia kwa dhati Mtume wa Allah (s.w.t.) kwamba:

Hawatamshirikisha Allah (s.w.t.) kamwe na yeyote, hawatamuabudu yeyote isipokuwa Allah (s.w.t.); hawatanyang'anya na kuiba kamwe; hawatawaua kamwe watoto wao wachanga wa kike; hawatawatukana watu wengine kamwe; hawatawakashifu tena wanawake; watakuwa sahihi na safi daima; watamtii Allah (s.w.t.) na Mtume Wake; na watakuwa waaminifu kwake wakati wote.

Hawa waumini wapya walimuomba Mtume (s.a.w.) kuwapa mwalimu wa kwenda naye Yathrib kuwafundisha Qur'an na maadili ya Uislamu. Alimtuma Mas'ab ibn Umayr, mmoja wa ami zake (Mas'ab alikuwa binamu ya baba yake), pamoja na kikundi hicho kwenda kuutangaza Uislamu huko Yathrib. Ujumbe wa Mas'ab ulifanikiwa, na familia nyingi huko Yathrib ziliukubali Uislamu.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Muhammad kuchagua mtumishi. Profesa Margliouth anasema kwamba Mas'ab ibn Umayr alikuwa chaguo la kwanza la mtumishi katika Uislamu.

103

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kiapo cha pili cha Aghaba

Mwaka 622 A.D., wenyeji wa Yathrib sabini na watano walikuja Makka katika msimu wa hija. Mtume (s.a.w.) alikutana nao mahali palepale huko Aghaba ambako alikutana na lile kundi la watu kumi na wawili mwaka uliopita. Watu hawa 75 waume kwa wake pia wal-iukubali Uislamu. Walimpa kiapo chao cha utii, na wakamkaribisha Yathrib.

Ami yake Mtume, Abbas ibn Abdul Muttalib, alikuwa pamoja naye safari hii. Anasemekana kwamba aliwaambia wale "wenyeji" kutoka Yathrib kuwa: "Muhammad anatukuzwa sana na watu wake mwenyewe. Kama mtaweza kusimama naye kwa heri na shari, mchukueni mwende naye Yathrib; la sivyo, basi liacheni suala zima."

Mmoja wa viongozi wa watu wa Yathrib alikuwa ni Bira'a ibn Ma'ruur. Alisema: "Tulipokuwa watoto, wanasesere wetu tuliokuwa tukiwapenda sana walikuwa ni panga na mikuki." Mkuu mwingine, Abul Haithum, alimkatisha, na akasema: "Ewe Mjumbe wa Allah (s.w.t.)! Kitatokea nini wakati Uislamu utakapokuwa mkubwa na wenye nguvu? Hapo tena wewe utaondoka Yathrib na kurejea Makka?"

Muhammad Mustafa akatabasamu na kusema: "La hasha. damu yenu ni damu yangu na damu yangu ni damu yenu. Tokea siku ya leo ninyi ni wangu na mimi ni wenu, na sitaten-gana nanyi kamwe."

Waislamu wale wa Yathrib waliridhika na uhakikisho waliopewa na Muhammad Mustafa, na wakarudi Yathrib kuueneza Uislamu miongoni mwa jamaa zao. Uislamu ukaanza kupa-ta maendeleo imara huko Yathrib. Ilipoonekana kwamba imani hii mpya imepata mahali pa usalama katika mji ule, Mtume (s.a.w.) aliwashauri wale waathirika wa mateso pale Makka kuhamia pale. Kwa kufuata ushauri wake, Waislamu wakaanza kuondoka Makka, katika vikundi vidogo vidogo, na kuanza makazi katika majumba yao mapya hapo Yathrib.

Kile Kiapo cha Pili cha Aghaba ni tukio muhimu katika historia ya Uislamu. Kilikuwa ndio nanga ambayo juu yake kile chombo dhaifu kilikuja kupumzika mwishoe, baada ya kurushwa huku na kule kwa miaka kumi na tatu katika bahari zisizodhibitika za upagani ndani ya Arabia.

104

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hajira (Kuhama)

Wakati wengi wa Waislamu walipoondoka Makkah na kufanya makazi huko Yathrib, ilionekana kwa waabudu masanamu kwamba kama Uislamu utapata mizizi katika ile Nchi ya CHEMCHEM iliyopo kaskzini mwao, na ukaweza kujitegemea, itakujaleta tishio kwenye maslahi yao ya kibiashara huko Syria. Waliuona Uislamu kama "hatari kubwa" mpya inayonyanyua kichwa chake huko kaskazini. Kwa hiyo, waliitisha mkutano katika ukumbi wao wa jiji ambamo walifikiria njia yenye kufaa zaidi ya kuivuruga mapema hii "hatari kubwa". Baada ya majadiliano kiasi, walikubaliana, kwa pamoja, kwamba njia ya pekee ya kuizuia hii hatari kubwa mpya, ni kwa kumuua mwanzilishi wake - Muhammad mwenyewe - akiwa angali bado yupo Makka. Uamuzi huu ukazua maswali mengine machache kama vile ni nani atakayemuua, vipi, lini na wapi. Wakayajadili zaidi maswali haya, wakafikiria uwezekano wa namna nyingi, na hatimae wakaamua, kwa pamoja tena, kwamba mpiganaji mmoja kutoka kila ukoo wa kila kabila linaloishi Makka na viunga vyake, atachaguliwa; wote watashambulia nyumba ya Muhammad kwa wakati mmoja, na watamuua, kabla tu ya alfajiri ya siku inayofuatia. Tendo lililofanywa kwa pamoja kama hilo, waliamini, "lingewakwamisha" Bani Hashim ambao hawangeweza kuwa na uwezo wa kupigana dhidi ya koo zote hizo kwa wakati mmoja kwa kulipiza kisasi cha kuuawa kwa Muhammad.

Mtume, hata hivyo, alikuwa tayari kukutana na dharura kama hii. Kwa kuarifiwa wakati wa mpango wa Maquraishi wa kumuua, na mtu aliyesilimu kwa siri. Alimwita binamu yake mpendwa, Ali ibn Abi Talib, akamfahamisha ule mpango wa Maquraishi, na wa kwake mpango wa kuwazidi maarifa. Mpango wake ulikuwa ni kumuweka Ali kwenye kitanda chake yeye mwenyewe, na kisha kutoroka nje ya nyumba hiyo wakati wowote wenye fursa. Hao Maquraishi, kwa kumuona Ali akiwa amefunikwa na shuka, watadhania kwamba Muhammad alikuwa amelala, alimueleza. Alimuomba Ali pia kurudisha dhamana zote za wapagani kwa wenyewe, na kisha kuondoka Makka na kumkuta yeye huko Yathrib. Ali alielewa kila kitu, na Mtume (s.a.w.) akamdhamini kwenye ulinzi wa Allah (s.w.t.)

Muhammad Husein Haykal

Wale vijana ambao Maquraishi waliwaandaa kwa ajili ya kutekeleza mauaji ya Muhammad walikuwa wamezingira nyumba yake wakati wa usiku ili asije akatoro-ka. Katika huo usiku wa Hajira, Muhammad alitoa siri ya mpango wake kwa Ali ibn Abi Talib na akamuomba ajifunike shuka la kijani la Mtume, na alale kwenye kitanda cha Mtume. Alimuomba tena akae hapo Makka mpaka atakapokuwa amerudisha vitu vyote vya thamani vilivyokuwa vimewekwa kwa Muhammad, kwa wenyewe.

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

105

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Marmaduke Pickthall:

"Wauaji walikuwa mbele ya nyumba yake (Muhammad). Alitoa shuka lake kwa Ali, akimtaka alale kwenye kitanda hicho ili kwamba yeyote atakayekuwa anatazama ndani angefikiria kwamba Muhammad amelala pale.

(Introduction to the Translation of Holy Qur'an, Lahore, 1975)

Washirikina waliizunguka nyumba ya Muhammad. Walichungulia ndani wakaona mtu aliyelala amefunikwa na blanketi, na wakaridhika kwamba "windo" lao liko salama. Ule wasaa wa fursa kwa ajili ya Mtume (s.a.w.) kutoroka ulifika muda baada ya usiku wa man-ane wakati ambapo wale askari wa doria wamesinzia. Alitembea kimya kimya na kuwapi-ta na kutoka nje ya maeneo ya nyumba yake.

Wale askari wa doria wa kipagani walikutwa wamejisahau, na Mtume wa Allah (s.w.t.) ali-fanikiwa katika kuukwepa kwa hila uchunguzi wao!

Ali alilala kwenye kitanda cha Mtume (s.a.w.) usiku mzima. Kabla tu ya mapambazuko, wale wauaji wa kipagani wenye kuhifadhi vichwa vya maadui, walivamia ndani ya nyumba panga zikiwa zimechomolewa kwenda kumuua Mtume. Lakini mshangao wao na mfad-haiko havikuwa na mipaka pale walipotambua kwamba alikuwa ni Ali na sio Muhammad ambaye alikuwa amelala pale kitandani. Wakamkamata Ali kwa kumhoji na pengine kwa kumtesa. Lakini mkuu wa wale askari wa doria akawaambia kwamba Muhammad hawezi kuwa amekwenda mbali sana, na kwamba wanaweza bado kumkamata kama hawatapoteza muda wao wenye thamani katika kumhoji Ali, hapo ndipo wakamuachia. Tukio hili linait-wa katika historia ya Kiislam Hajira au Kuhama.

M. Shibli, mwanahistoria ya Kiislam mashuhuri wa Kihindi, anaandika katika wasifa juu ya Mtume wa Allah (s.a.w.):

"Wapagani wa Makka walimchukia Muhammad, na bado walimuamini. Yeyote aliyekuwa na vitu vya thamani, alivileta na kuvihifadhi kwake. Alikuwa ndiye "mwenye-benki" wao. Alitambua juu ya mpango wa Maquraishi wa kumuua yeye. Kwa hiyo, yeye, akamwita Ali na akasema: "Allah (s.w.t.) ameniamuru mimi kwenda Yathrib. Wewe utalala kwenye kitanda changu na kesho urudishe amana za watu wa Makka kwa wenyewe." Hii ilikuwa ni hali yenye kuleta maafa na yenye hatari mbaya sana. Ali pia alijua kwamba Quraishi wamekusudia kumuua Mtume wa Allah (s.a.w.) usiku ule, na kwamba kulala kwenye kitanda chake ni kulala katika meno ya kifo. Lakini ni lini ambapo Ali alikiogopa kifo? Yule shujaa wa Khaibar akalala kwenye meno ya kifo usingizi mzito ambao hajawahi kuulala maishani mwake mwote.

(Life of the Apostle of God, Azamgarh, India, 1976)

106

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mtume (s.a.w.) hakuwa na muda wa kumwelezea Ali kwa kinaganaga ni amana ngapi alikuwa nazo na zilikuwa zikadhiwe kwa nani. Ilitosha kwake yeye kumwambia Ali arud-ishe amana zote kwa (wapagani) wenye mali zao, na yeye (Ali) akafanya hivyo. Ilikuwa kama vile tu kwenye karamu ya Dhul-Ashiira wakati kile ambacho Mtume (s.a.w.) alikuwa afanye, kilikuwa ni kumwambia tu Ali awakaribishe kwenye chakula watu wazima wote wa ukoo wa Bani Hashim. Hakukuwa na maelekezo ya kina yaliyokuwa lazima. Ali bila ya kufikiri alielewa nini bwana wake alichokitegemea kutoka kwake. Kule kukabidhiwa kurudisha zile amana za watu wa Makka kwao, ni ushahidi tosha kwamba Ali alikuwa msiri na "mwandishi binafsi" wa Mtume wa Uislamu hata kabla ya kule Kuhama kwenda Yathrib.

Ikiwa Hajira inasisitiza uaminifu wa Ali usio na mjadala kwa bwana wake, Muhammad, inaonyesha pia ujasiri wake wa ajabu. Wale askari wa doria wa maadui wangeweza kumuua ama kwa kuamini kwamba alikuwa ni Muhammad, au katika kugundua kwamba siye, kwa kuvunjika moyo tu. Alilijua hili vizuri sana, lakini kwake yeye hakuna hatari iliyokuwa kubwa sana kama angeweza kuokoa maisha ya Mtume wa Allah (s.a.w.) . Ilikuwa ni kujitolea huku na ujasiri huu kuliko mpatia ushindi yeye wa sifa nyingi za Qur'an Tukufu. Qur'an imetoa sifa kwenye uaminifu wake na ujasiri wake alioonyesha katika usiku ule wa majaaliwa wa Hajira (Kuhama) kama ifuatavyo:

Usahihi-5.jpg

"Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Allah. Allah ni mpole kwa waja wake."(Sura ya 2; Aya ya 207)

Razi, yule mfasiri maarufu wa Qur'an, anasema ndani ya Tafsir Kabir yake (juz. 2,uk. 189) kwamba Aya hii ilishuka hasa kwa kutambua kazi kubwa na tukufu ya Ali katika usiku wa Hijiria alipomuwezesha Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) kuondoka Makka. Kwa sababu ya Ali, aliweza kuondoka kwa usalama.

Katika usiku ule wa kihistoria, ilifanyika shughuli ya kibiashara ya ajabu na ya kimuujiza, ya kwanza na ya mwisho ya aina yake katika historia nzima ya Maumbile. Yalikuwa ni mapatano ya kuuza-na-kununua kati ya Allah (s.w.t.) na mmoja wa waja Wake. Mja aliyehusika hapa ni Ali ibn Abi Talib.

Katika usiku mkimya na usio na mbaramwezi, Allah (s.w.t.) alikuja kwenye "soko" kama "Mteja." Alikuja kununua bidhaa maalum. Mja Wake, Ali, alikuja kwenye "soko" kama "mfanyabiashara." Shughuli yake: kuuza ile bidhaa ambayo Allah (s.w.t.) alikuwa anaitafuta. Hiyo "bidhaa" ilikuwa ni roho yake, maisha yake!

Allah (s.w.t.) huyo "Mteja" aliangalia sana sifa ya "bidhaa" hiyo, na akaiona ni bora sana. Yeye, kwa hiyo, aliamua kuinunua papo hapo. Alilipa "thamani" yake kwa huyo

107

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

"mfanyabiashara," na bidhaa ikabadilishanwa, sawasawa kama kwenye mapatano ya biashara nyingineyo ile. Kutokea muda ule, ile "bidhaa" - maisha ya Ali - ikakoma kuwa yake, na ikawa mali pekee ya Allah (s.w.t.) Yale mapatano ya kuuza na kununua kati ya Bwana na mtumwa kwa hiyo yakakamilika, kwa ridhaa kamili ya pande zote.

Walikuwepo "mashahidi" pia wa mapatano haya. Walikuwa ni Malaika na nyota - wengi mno - wakiangalia kutoka kwenye "majumba yao ya kisanii" ya mbinguni. Walitazama kwa kimya cha mshangao na kimya cha uvutiwaji vile Ali alivyouza maisha yake kwa Allah (s.w.t.) Qur'an Tukufu ikawa ndio "msemaji" wao kwa watu wa dunia hii, na ikaandika kile wao - hao mashahidi - walichokiona katika usiku ule wa kukumbukwa.

"Kumbukumbu" ya mapatano haya, kama ilivyohifadhiwa na Qur'an, tunayo hivi sasa, na ni ya kudumu na isiyoweza kuharibiwa. Itadumu kwenye dunia hii kwa muda ambao wale Malaika na zile nyota - "wale mashahidi" wa mapatano hayo - watakavyodumu huko Mbinguni!

Ali aliuza ile "bidhaa" kwa Allah (s.w.t.) Sasa akiwa ameondokana na ule "wasiwasi" kwa ajili ya usalama wa ile "bidhaa," angeweza kulala, na akaenda kulala - kwenye kitanda cha Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.). Katika Usiku ule wa Majaaliwa, alilala fofofo. Wakati wa alfajiri, alipoamka, au kwa usahihi zaidi, alipoamshwa na sauti kubwa na mgongano wa mikuki na panga za wale wauaji wenye kuhifadhi vichwa vya maadui, waliotumwa na Maquraishi, kumuua Muhammad, alikwishapata uzima!

Katika waja Wake wote, Allah (s.w.t.) alimchagua Ali kutekeleza Mpango Wake. Mpango ule ulikuwa ni kumlinda Mtume Wake, kutokana na maadui zake. Hawa maadui walik-wishaandaa mpango kwa ajili ya kuangamiza Uislamu. Waliamini kwamba kama wange-muua Muhammad, Uislamu ungeangamia. Wao, kwa hiyo, wakapanga na kula njama za kumuua Muhammad. Bali hawakujua kwamba Allah (s.w.t.) alikuwa na mpango wake mwenyewe - Mpango-Tibuzi (wenye kutibua) - tayari kwa ajili ya tukio hili.Ulikuwa ni Mpango-Tibuzi wa Allah (s.w.t.) ambao ulikuwa uje kuwakwamisha Maquraishi kwa kuokoa maisha ya Mtume Wake. Rejea ya Qur'an kwenye Mpango-Tibuzi wa Allah (s.w.t.) inapatikana kwenye Aya ifuatayo:

Usahihi-6.jpg

"Na makafiri walipanga mipango na Allah akapamnga mipango, na Allah ndiye mbora wa wenye kupanga." (Qur'an; 3: 54

108

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ali ibn Abi Talib alikuwa ndiye "kiungo muhimu" katika Mpango-Tibuzi wa Allah (s.w.t.) Jukumu la Ali lilihakikisha mafanikio ya Hajira (Kuhama) ya Muhammad, na mafanikio hayo ya Hijira peke yake yalifanya kuanzishwa kwa dola ya kisiasa ya Madina kuwezekana. Kama Hajira ingeshindwa, hiyo Dola ya Madina kamwe isingekuja kuwepo. Hiyo Dola ya Madina ndio lilkuwa chombo cha kimaada cha Utawala wa Mbinguni wa mwanzo na wa mwisho Duniani. Allah (s.w.t.) alimfanya mja Wake, Ali ibn Abi Talib, kuwa chombo ambacho kupitia hicho Aliuweka ule Utawala katika dunia hii.

Wakati Muhammad alipokuwa ametoka nje ya mzingo wa nyumba yake, alikwenda kwenye nyumba ya Abu Bakr, na akamwambia kwamba Allah (s.w.t.) amemuamuru kuon-doka Makka usiku uleule. Kwa vile hawakuwa na muda wa kusita, waliuondoka mji mara moja, na wakaenda kwenye pango linaloitwa Thaur Kusini ya Makka. Walilifikia pango hilo na wakaingia kukiwa bado kuna giza.

Walikuwa wamejificha ndani ya pango hilo wakati, masaa machache baadae, wale wauaji walipotokea pia katika ufukuzaji wao. Kwa mujibu wa Hadith, buibui alitanda utando kwenye mlango wa pango, na ndege alitaga yai hapo mlangoni. Wale wauaji walihoji kwamba kama mtu yeyote angeingia ndani ya pango, ule utando na yai vingevunjika, laki-ni kwa vile vyote ni vizima, hakuna aliyeingia humo. Hivyo kwa kuridhika kwamba wale watoro hawakuwa ndani ya pango lile, waliacha msako wao na wakarudi Makka.

Wakati wale wauaji wakiwa wanajadili ile hoja ya kama waingie au wasiingie kule pango-ni kuwakamata hao watoro ambao wanaweza kuwa wamejificha ndani yake, Abu Bakr alishikwa na hofu, na akamwambia Mtume: "Sisi tupo wawili tu na maadui zetu ni wengi sana. Tuna nafasi gani ya kuokoa maisha yetu kama wataingia hapa pangoni?" Mtume (s.a.w.) akasema: "Hapana. Hatupo wawili. Yupo Wa Tatu pamoja nasi, naye ni Allah (s.w.t.)" Tukio hili limetajwa ndani ya Qur'an Tukufu kama ifuatavyo:

Usahihi-7.jpg

"Na Allah ali mnu suru Mtume Wake walipomtoa waliokufuru. Na walipokuwa pangoni, alimwambia sahibu yake: "usihuzunike. Hakika Allah yuko pamoja nasi." Na Allah akamteremshia utulivu juu yake (Mtume)." (Sura ya 9; Ay a ya 40)

Mtume (s.a.w.) pamoja na Abu Bakr walikaa kwa siku tatu ndani ya pango hilo. Huko Makka, kwa wakati huu, shauku ya kumkamata Mtume (s.a.w.) imepungua. Katika siku ya

109

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

nne, Abdullah, mtoto wa Abu Bakr, alikuja na ngamia wawili kwa ajili ya kupanda wao. Abu Bakr alimtoa mmoja wa ngamia hao kwa Mtume (s.a.w.) lakini akakataa kumpokea kama zawadi, na akalipa bei yake kabla ya kumpanda. Yeye na Abu Bakr ndipo wakapan-da ngamia hawa, na wakiiambaa Makka kuelekea kaskazini na Mashariki, walisafiri kuelekea Yathrib upande wa kaskazini.

Muhammad ibn Ishaq:

"Pale Abu Bakr alipoleta wale ngamia wawili kwa Mtume, alimtoa yule mbora zaidi kwake na akamuomba ampande. Lakini Mtume (s.a.w.) alikataa kumpanda mnyama ambae hakuwa wake binafsi, na wakati Abu Bakr alipotaka kumpa ngamia huyo, ali-taka kujua alichokuwa amelipa kumnunua, na akamnunua kutoka kwake."

(Life of the Messenger of God)

Wasafiri hawa wawili wakatembea umbali kati ya Makka na Yathrib kwa siku tisa, na siku ya kumi wakafika Quba, mahali palipo maili mbili Kusini ya Yathrib ambapo walikaa kati-ka nyumba ya Kulthum bin Hind, kama wageni wake. Mtume (s.a.w.) aliamua kusubiri kuwasili kwa Ali kutoka Makka kabla ya kuingia Yathrib. Katika wakati huo, alijenga msingi wa Msikiti hapo Quba. Lilikuwa ni jengo lisilokamilika ambalo kwisha kwake kunasemekana kulichukua siku kumi na nne.

Mtume wa Allah (s.a.w.) alifika Quba siku ya Jumatatu. Siku ya Alhamisi Ali naye akawasili. Alikuwa amekwisha rudisha fedha na vito, nyaraka na vitu vingine vya thamani vya watu wa Makka kwao wenyewe. Bwana wake alifurahi sana kumuona yeye, na akamshukuru Allah (s.w.t.) Ambaye alimtoa salama kwenye mji wa Makka.

Muhammad ibn Ishaq:

"Ali alibakia Makka kwa siku tatu, usiku na mchana mpaka akawa amerudisha zile amana ambazo Mtume (s.a.w.) alikuwa amezishikilia. Hili lilipokwisha kutendeka, alijiunga na Mtume, na akakaa naye katika nyumba ya Kulthum."

(The Life of the Messenger of God)

S. Margoliouth:

"Siku ya Jumatatu tarehe 8 ya mwezi wa Rabi ul Awwal wa mwaka wa 1 H.A., kulin-gana na Septemba 20 ya mwaka 622 A.D, Mtume (s.a.w.) alifika Quba, hivi sasa ikiwa ni mahali pakubwa kwa bustani na miti ya matunda. Ukarimu ulitolewa na mfuasi mmoja mtu mzima, Kulthum ibn Hind, jina la ambaye "mafanikio" ya utumwa wake yalielekea kwa Mtume (s.a.w.) kuwa ya ishara njema (Isabah, iii, 1138). Ulikubalika, ingawa kwa mapokezi ya wageni nyumba ya mfuasi mwingine ilionekana kuwa yenye kufaa zaidi. Hapo Quba, Mtume (s.a.w.) aliamua kubaki

110

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

mpaka Ali atakapojiunga naye ambapo ilitokea siku ya Alhamisi; pamoja naye alikuwepo Suhaib ibn Sinan, ambaye alilazimishwa kukabidhi akiba zake kwa Maquraishi. Siku ya Ijumaa, Mtume (s.a.w.) alisafiri kutoka Quba kuelekea Yathrib, na anasemekana alifanya ibada ndani ya Wadi Ra'unah.

(Muhammad and the Rise of Islam, London, 1931)

Njia ilikuwa imejipanga kundi kubwa lenye furaha la watu wa Yathrib waliokuwa wamevaa mavazi yao ya sikukuu. Wanawake na watoto walikuwa wakiimba nyimbo za makaribisho kutoka kwenye mapaa ya nyumba zao. Yalikuwa ni mandhari ambayo ni vigu-mu sana kuweza kuwa yamebuniwa katika njozi. Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) lazima awe alivutiwa sana na mapokezi ya namna ile.

Kila mkazi (wa Kiarabu) wa Yathrib alikuwa na shauku ya kuwa mwenyeji wa Mtume wa Uislamu ambaye alikuwa anaingia mjini kwake kama mgeni. Lakini kwa kutokutaka kumkatisha tamaa hata yule mkazi mnyonge zaidi, alishusha hatamu za yule ngamia-jike, na akatangaza kwamba angekaa popote pale atakaposimama. Yule ngamia-jike akatembea polepole kupita nyumba nyingi, na kisha akasimama mbele ya nyumba ya Abu Ayyub, baadae akawa ndiye mwenyeji mwenye fahari wa Mtume wa Allah (s.a.w.), Abu Ayyub alikuwa mwenyeji maarufu wa Yathrib, na alitokana na ukoo wa Bani Najjar. Wote Amina, mama yake Mtume, na mama wa babu yake, Abdul Muttalib, walitokana na ukoo huu.

111

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mwaka wa Kwanza wa Hijiria

Kulingana na uchunguzi wa marehemu Mahmud Pasha al-Falaki wa Misri, siku ambapo Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Allah (s.a.w.) , aliyofika Quba ilikuwa ni Jumatatu, tare-he 8 ya mwezi wa Rabi ul Awwal wa mwaka wa 13 wa Tangazo la Utume, tarehe ambayo inafikiana na tarehe 20, Septemba 622 A.D.

Katika Ijumaa iliyofuata, 12 Rabi ul Awwal (Septemba, 24), Mtume wa Allah (s.a.w.) aliondoka Quba, na akaingia Yathrib. Alifikia kwenye nyumba ya Abu Ayyub, kama ilivy-oelezwa tayari.

Ujenzi wa Msikiti hapo Yathrib

Tendo la kwanza la Muhammad Mustafa, Allah (s.w.t.) ampe amani yeye na Ahlu-Bait wake, wakati alipofika Yathrib, lilikuwa ni kujenga Msikiti wa kumuabudia Allah (s.w.t.) ndani yake. Mbele ya nyumba ya Abu Ayyub palikuwa na eneo la wazi mali ya mAyatima wawili. Mtume (s.a.w.) aliwaita wao na walezi wao, na akawaambia kwamba alikuwa anataka kununua ardhi ile. Wakamwambia kwamba wangefurahi sana kuifanya ardhi ile zawadi kwake. Lakini alikataa kuipokea kama zawadi, na akasisitiza kuilipia kwa bei yake. Hatimae walikubali kupokea malipo kwa ajili ya ardhi yao. Malipo yakafanywa na uchim-baji wa kiwanja ukaanza mara moja.

Akielezea sababu kwa nini Mtume (s.a.w.) hakuipokea ile ardhi kama zawadi, M. Abul Kalam Azad anasema katika kitabu chake, Rasul-e- Rahmat (Mtume wa Rehma), (Lahore, Pakistan, 1970):

Mtukufu Mtume (s.a.w.) hakutaka kuchukua wajibu wa mtu yeyote. Ni nani anayeweza kudai kuwa muaminifu zaidi kwake kuliko Abu Bakr? Na yeye mwenyewe alisema kwamba anamshukuru sana Abu Bakr kwa msaada wake wa utu na mali kuliko mtu mwingine yeyote. Na tena, pale Abu Bakr alipotaka kumpa zawadi ya ngamia kwenye usiku wa kuon-doka Makka kwenda Yathrib, yeye hakuikubali mpaka alipokuwa amemlipa Abu Bakr bei yake. Vivyo hivyo, huko Yathrib, alipotaka kununua ardhi kwa ajili ya kujenga Msikiti juu yake, wamiliki wake waliitoa kwake kama zawadi. Lakini alikataa kuipokea kama zawadi. Ardhi hiyo ilichukuliwa tu pale wamiliki wake walipokubali kupokea bei yake kutoka kwake ambayo aliilipa.

Huu Msikiti wa Yathrib ulikuwa ndio bora sana katika urahisi wa dhana na usanii muun-do. Vifaa vilivyotumika katika ujenzi wake vilikuwa ni matofali yasiyochomwa na mota kwa ajili ya kuta, na makuti ya mtende yaliyozuiliwa na magongo ya minazi. Shubaka la

112

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Msikiti huo lilielekea upande wa Jerusalem upande wa kaskazini. Kila moja kati ya pande zile nyingine tatu ulitobolewa na lango. Sakafu ya Msikiti haikuwa na matandiko hapo mwanzoni, hata angalau mikeka iliyochakaa. Vibanda viwili pia vilijengwa kwenye ukuta wa nje, kimoja cha Sauda binti ya Zama'a; na kingine kwa ajili ya Aishah, binti ya Abu Bakr, wale wakeze wawili Mtume (s.a.w.) kwa wakati huo.

Vibanda vipya vilijengwa kwa ajili ya wake wapya kama walivyoingia katika miaka ya baadae. Ilikuwa ni mara ya kwanza ambapo Waislamu walifanya kazi kama timu moja katika mradi wa jamii. Katika miaka iliyofuatia, timu hii ilikuwa ijenge jengo kubwa la Kiislam.

Kwa kuhamasishwa na kuwepo kwa Mtume wa Allah (s.a.w.), kila mmoja wa Masahaba alikuwa anachuana ili kuwashinda wengine. Miongoni mwa Masahaba hao alikuwa ni Ammar ibn Yasir, ambaye, kwa mujibu wa Ibn Ishaq, alikuwa ndiye mtu wa kwanza katika Uislamu kujenga Msikiti. Ibn Ishaq hakutaja bayana ni Msikiti upi ambao Ammar ali-jenga. Lakini Dr. Taha Husain wa Misri anasema kwamba Ammar alijenga Msikiti huko Makka kwenyewe na aliswali ndani yake, nyuma kabisa kabla hajahamia Yathrib.

Wakati Msikiti ulipokuwa unajengwa, lilitokea tukio ambalo Ibn Ishaq ameliandika kama ifuatavyo:

"Ammar b. Yasir aliingia ndani wakati wakiwa wamemzidishia mzigo wa matofali, akisema, "Wananiua. Wananitwisha mimi mizigo wasiyoweza kuibeba wao wenyewe." Ummu Salma, mkewe Mtume (s.a.w.) akasema: "Nilimuona Mtume (s.a.w.) akipitisha mkono wake kwenye nywele zake (Ammar) - kwani alikuwa ni mwenye nywele zenye mawimbi - na akasema, "Wapi, ibn Sumayya! Sio hao watakaokuua wewe, bali ni kundi la watu waovu."

(Ubashiri huu unasemekana ulikuja kutimizwa wakati Ammar alipouawa huko Siffin - Suhayli, ii, uk. 3)

Ali alitunga shairi la rajaza siku hiyo (Msikiti ulipokuwa unajengwa):

Yupo mmoja anayejitahidi usiku na mchana Kutujengea sisi Msikiti wa tofali na ufinyanzi Na mtu anayekimbia mavumbi mbali.

Ammar alilikariri na kuanza kulighani.

Alipolishikilia sana, mmoja wa Masahaba wa Mtume (s.a.w.) alidhani ni yeye aliyeleng-wa ndani yake, kwa mujibu wa kile Ziyad b. Abdullah el-Bakkai alivyoniambia mimi kutoka kwa Ibn Ishaq. Huyu wa baadae (ibn Ishaq) kwa kweli alimtaja mtu mwenyewe.

113

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Alisema: "Nimesikia ulichokuwa ukisema kwa muda mrefu, Ewe Ibn Sumayya, na Wallahi nafikiri, nitakupiga kwenye pua!" Sasa alikuwa na fimbo mkononi mwake, na Mtume (s.a.w.) alikasirika sana na akasema: "Kuna nini kati yao na Ammar? Anawakaribisha wao Peponi ambapo wao wanamkaribisha motoni. Ammar ana thamani kwangu kama uso wangu mwenyewe. Kama mtu atakuwa na tabia namna hii hatasamehewa, hivyo muepuke."

Sufyan b. Uyana ametaja kutoka kwa Zakariya kutoka kwa al-Shabi kwamba mtu wa kwanza kujenga Msikiti alikuwa ni Ammar bin Yasir.

(Suhayli anasema: Ibn Ishaq alimtaja mtu huyo, lakini Ibn Hisham alipendelea asi-fanye hivyo, kama kutomtaja mmoja wa maswahaba wa Mtume (s.a.w.) katika mazin-gira yanayoaibisha. Kwa hiyo haitakuwa haki kamwe kutafuta kumjua. Abu Dharr anasema: Ibn Ishaq alimtaja mtu huyo na akasema,: "Mtu huyu alikuwa ni Uthman b. Affan." Wahariri wa Cairo wanasema kwamba katika ile Mawahib al-Laduniya, al-Qastalani, (kafa A.D. 1517), amesema kwamba mtu huyo anasemekana kuwa alikuwa ni Uthman b. Mazun. Huyu mwandishi wa mwisho anaweza kupuuzwa kwa usalama katika nukta hii.)"

Katika eneo la ujenzi wa Msikiti huo, mtu anaweza kushuhudia vituko vyenye kuumiza sana katika Hadith ya siku za mwanzo za Uislamu - Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Allah (s.a.w.) akiondoa vumbi, kwa mikono yake mwenyewe, kutoka kwenye kichwa na uso wa Ammar ibn Yasir. Hakumpendelea sahaba mwingine yoyote kwa dalili za mguso, upendo na huruma.

Wakati Mtume wa Allah (s.a.w.) alipowalaumu maswahaba zake kwa kumwingilia Ammar, na akasema kwamba yeye (Ammar) alikuwa anawakaribisha peponi ambapo wao walikuwa wanamkaribisha motoni, yeye (Mtume) alikuwa, yumkini kabisa, anafasiri ile Aya ya 41 ya Sura ya 40 (Sura-tul-Mu'min) iliyoko ndani ya Qur'an ambayo inasomeka kama ifuatavyo:

"Na enyi watu wangu! Kwa nini mimi nakuiteni kwenye uokovu, nanyi mnaniita kwenye moto?"

Akitoa maelezo juu ya Aya hii, Abdullah Yusuf Ali, yule mfasiri wa Qur'an Tukufu anasema:

"Inaweza kuonekana ni ajabu kwa mujibu wa sheria za dunia hii kwamba angekuwa anawatafutia wao wema, ambapo wao wanamtafutia maangamio yake; lakini huo ni upeo wa Imani."

114

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Yule sahaba aliyezozana na Ammar ibn Yasir wakati Msikiti wa Yathrib ulipokuwa unaj engwa, hakuwa mwingine zaidi ya Uthman bin Affan, mmoja wa makhalifa wa baadae wa Waislamu. Alichukizwa na kufanya kazi kwenye vumbi na matope, na kufanya nguo zake kuingia tope. Wakati Mtume wa Allah (s.w.t.) alipomuonyesha kutoridhika kwake, ilibidi anyamaze kimya lakini tukio hilo lilimkereketa moyoni mwake, na hakulisahau kamwe. Miaka mingi baadae alipokuwa khalifa, na kuwa na mamlaka mikononi mwake, aliwaamuru watumwa wake kumuangusha chini Ammar ibn Yasir na kumpiga - mtu ambaye alikuwa na thamani kwa Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.w.t.) kama uso wake (Mtume) mwenyewe.

Madai kwamba hakuwa Uthman bin Affan bali alikuwa ni Uthman bin Mazun au mtu mwingine yoyote yule, ambaye, kwa kumtisha Ammar ibn Yasir, aliamsha hasira za Mtume wa Allah (s.w.t.), ni jaribio tu la kujionyesha kwa wanahistoria "wanaojipen-dekeza" wa nyakati zilizofuata baadae.

Kwa wakati huu, Ammar ibn Yasir tayari alikwishapata sifa bora nne ambazo lazima ziwe zimemfanya yeye kuwa husuda wa maswahaba wengine wote wa Muhammad, Mjumbe wa Allah (s.a.w.). Sifa hizo zilikuwa ni:

1.  Alitokana na familia ya kwanza ya Kiislam.

2.  Alikuwa mtoto wa Mashahidi wa Kwanza na wa Pili wa Uislamu. Mama yake, Sumayya, alikuwa wa kwanza, na baba yake, Yasir, alikuwa shahidi wa pili katika Uislamu. Ilikuwa ni heshima ambayo haikupatwa na sahaba mwingine yoyote wa Muhammad Mustafa.

3.   Alikuwa ndio mjenzi wa Msikiti wa kwanza.

4.   Alikuwa ni kipenzi cha Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Allah (s.a.w.) . Allah (s.w.t.) awape rehemu Ammar ibn Yasir na wazazi wake.

Adhana na Swala

Ilikuwa ni amri kwa Waislamu kuswali mara tano kwa siku. Walipaswa kusimamisha shughuli za kazi zao za siku, na kutekeleza wajibu huu. Lakini hapakuwa na njia ya kuwatahadharisha kwamba wakati umefika kwa ajili ya kuswali.

Kwa mujibu wa Hadith za Sunni, sahaba mmoja alimshauri Mtume (s.a.w.) kwamba lingepulizwa tarumbeta au kengele ingegongwa kuwatahadharisha Waislamu kabla ya wakati wa kila Swala. Mtume (s.a.w.) hakukubali ushauri huu, kama alivyosema kwamba hakutaka kuchukua desturi za Kiyahudi au Kikristo.

115

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Abdillah bin Ziyad alikuwa mwenyeji wa Yathrib. Alikuja kumuona Mtume, na akasema kwamba alipokuwa nusu-macho au nusu-usingizini, mtu alitokea mbele yake na kumwambia kwamba sauti ya mwanadamu ingetumika kuwaita waumini kwenye Swala; na pia alimfundisha hiyo Adhana (mwito wa Swala), na namna ya kuisoma.

Wanahistoria wa Sunni wanasema kwamba wazo hilo lilikubalika kwa Mtume, na akalichukua papo hapo. Yeye ndipo akamwita Bilal, akamfundisha jinsi ya kuwaita Waislamu kwenye Swala; na akamchagua kuwa Muadhini wa kwanza wa Uislamu.

Hadithi hizi hazifuatwi na Waislamu wa Shia. Wao wanasema kwamba kama vile Qur'an Tukufu ilivyoshushwa kwa Muhammad Mustafa, na Adhana ilikuwa vivyo hivyo.

Wanatetea kwa dhati kwamba ile namna ya kuwaita waumini kwenye Swala haingeweza kuachwa kwenye ndoto au ruya za Mwarabu fulani. Wanaendelea kusema kwamba kama Mtume (s.a.w.) ameweza kuwafundisha Waislamu jinsi ya kuchukua udhuu, na ni vipi, lini na nini cha kusema katika kila Swala, angeweza pia kuwafundisha jinsi na wakati gani wa kuwatahadharisha wengine kabla ya wakati wa kila Swala.

Kwa muj ibu wa Hadith za Shia, yule Malaika aliyemfundisha Mtume wa Allah (s .w.t.) j insi ya kuchukua udhuu kujiandaa kwa Swala, na jinsi ya kuswali, pia alimfundisha namna ya kuwaita wengine kwenye Swala.

Yathrib yawa Madina

Hili jina "Yathrib" mara likawa halifai. Watu wakaanza kuuita mji huo "Madina-tun-Nabi," - Mji wa Mtume. Kiasi muda ulivyopita, matumizi yakafanya ufupisho wa jina hili utwaliwe kirahisi kama "Madina" - "Mji," na hivyo ndivyo jina la mji wa Mtume wa Uislamu lilivyobakia tangu hapo.

Makundi ndani ya Madina

Wakati Mtume (s.a.w.) na wale wahamiaji kutoka Makka walipofika Yathrib (sasa Madina), waliyakuta makabila matatu ya Kiyahudi, yaani, Quainuqa, Nadhir na Quraydha, na makabila mawili ya Kiarabu, yaani, Aus na Khazraj, yakiishi kwenye mji huo.

E.A.Belyaev:

"Idadi ya watu wa asili ya Madina ilijumlisha makabila yake matatu ya Kiyahudi, Quainuqa, Qurayza na Nadhir; na ya makabila mawili ya Kiarabu, Aus na Khazraj.

(Arabs, Islam and the Arab Caliphate in the Early Middle Ages. 1969)

116

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hao Wayahudi walikuwa wakulima, wachuuzi, wafanyabiashara, wakopesha-fedha, wami-liki-ardhi na wenye viwanda. Wamekuwa matajiri kupitia matumizi ya riba na walitawala ukiritimba wa viwanda vya zana za vita katika Arabia.

Haya makabila mawili ya Kiarabu ya Madina, Aus na Khazraj, yaliishi kwa kilimo. Kabla ya kuwasili kwa Mtume, walikuwa wamefungana kwenye vita dhidi yao wenyewe vilivy-odumu kwa zaidi ya vizazi vitano. Walipigana vita vyao vya mwisho miaka minne tu iliy-opita, yaani, mnamo 618 A.D., na iliwaacha wachovu sana na walegevu.

Walikuwepo pia Wakristo wachache wanaoishi Madina. Hawakukubaliana na Mtume wa Uislamu kwa sababu aliikana ile imani ya Utatu, na akahubiri Tawhiid ya Muumba.

Kundi la nne ndani ya Madina lilikuwa lichomoze baadae kidogo, likiundwa na "wanafi-ki" au "waliokosa imani." Wakati wa ujumbe wa Mtume (s.a.w.) huko Makka, walikuwepo Waislamu wengi ambao walikuwa wafiche imani yao ya kweli kwa kuhofia mateso. Hapo Madina, hali iligeuka. Watu hawa (wanafiki) walikuwa Waislamu jina; usoni wali-tangaza Uislamu lakini hawakuwa wakweli. Walikuwa chanzo cha nguvu isiyodhihirika ya uchochezi, hujuma na uasi.

Mkataba au Katiba ya Madina

Raia wa Yathrib walimtambua Muhammad kama mtawala wao, na akawapa "Mkataba wa Uraia" ambao unaaminika kuwa ndio waraka wa kwanza ulioandikwa katika Uislamu (mbali na Qur'an). Mkataba wa asili kama ulivyohifadhiwa na Ibn Ishaq, una masharti arobaini na saba (47). Yafuatavyo ni yale ambayo ni muhimu zaidi kati ya hayo:

*   Migogoro yote kati ya pande zozote mbili ndani ya Yathrib itapelekwa kwa Muhammad kwa uamuzi wake juu yake.

*  Waislamu na Wayahudi watakuwa na haki sawa.

*    Kila kundi ndani ya Yathrib litafuata imani yao, na hakuna kundi lolote litakaloingilia katika mambo ya kundi jingine lolote.

*    Katika tukio la shambulio lolote la nje juu ya Yathrib, makundi yote, yaani, Waislamu na Wayahudi, yataulinda mji.

*    Makundi yote yatajiepusha na kumwaga damu ndani ya mji.

*   Waislamu hawatakwenda vitani dhidi ya Waislamu wengine kwa faida ya wasiokuwa Waislamu.

117

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

R.V.C. Bodley:

"Muhammad alitengeneza mkataba na Wayahudi ambamo, miongoni mwa mambo mengine, iliainishwa kwamba Wayahudi na Waislamu wasaidiane pamoja katika mambo yote yanayohusu mji huo. Walikuwa wawe washirika dhidi ya maadui wote wa kawaida, na hili bila ya wajibu wa pande mbili kwa Uislamu au Uyahudi. Sharti muhimu la mkataba huu linasomeka kama ifuatavyo: Wayahudi wanaojiunga wenyewe kwenye umoja wetu watakuwa na haki sawa na watu wetu wenyewe kwenye msaada wetu na madaraka yetu mazuri. Wale Wayahudi wa matawi tofauti wanaoishi Yathrib wataunda pamoja na Waislamu dola moja ya pamoja. Watafuata dini yao kwa uhuru kama Waislamu. Watumishi na washirika wa Wayahudi watanu-faika kwa usalama na uhuru huo huo.

(The Messenger, the Life of Muhammad, New York, 1946)

Muhajirina na Ansari

Muhammad alibadili majina ya makundi yale mawili ya Waislamu ambao sasa walikuwa wanaishi Madina. Aliwaita wale wakimbizi kutoka Makka "Muhajirin" (Wahamiaji); na akawaita wale wenyeji wa Yathrib ambao waliwakaribisha wao, "Ansar" (Wasaidizi). Makundi haya mawili yalijulikana kwa majina haya daima baadae.

Hali ya kiuchumi hapo Madina

Utajiri wa Madina ulikuwa karibu wote umekusanyika katika mikono ya Mayahudi. Hao Waarabu (sasa Ma-ansari) waliishi kwenye umasikini na dhiki ya kudumu. Sababu moja ya kwa nini walikuwa masikini sugu, ilikuwa ni viwango vikubwa vya riba walivyokuwa wakilipa kwa Mayahudi kwenye mikopo yao.

D.S. Margoliouth:

"Ingawa tunasikia majina ya mmoja au wawili wa matajiri wa Yathrib, wengi wao wanaonekana walikuwa masikini. Hapo Yathrib wakati wa Mtume, kulikuwa na vazi moja tu la harusi; mapambo yalikuwa yakiazimwa kutoka kwa Wayahudi. Umasikini huu ulikuwa hasa ukikuzwa na ukopeshaji-pesa wa Kiyahudi."

(Muhammad and the Rise of Islam, Londln, 1931)

Lakini kama Maansari walikuwa masikini, Muhajirin walikuwa masikini zaidi. Katika kukimbia kutoka Makka, waliacha kila kitu walichokuwa wakikimiliki, na walipokuja Yathrib kutafuta hifadhi, walikuwa hawana kitu. Kwa kifupi, hali yao iligeuka kuwa ya

118

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kukatisha tamaa. Walikuwa wafanye kitu ili wapate kuishi. Lakini kwa vile hawakujua kitu kuhusu kilimo, cha maana walichoweza kufanya kilikuwa ni kufanya kazi kama vibarua wasio na ujuzi katika mashamba na bustani za Wayahudi na Ansari.

D.S. Margoliouth:

"Ilikuwa mwanzoni imepangwa kuwa wale Wakimbizi wawasaidie Wasaidizi (Ansar) katika kazi zao za nje; lakini kwa kutokujua chochote cha utunzaji wa mitende, wali-weza tu kufanya zile kazi za kitumishi zaidi; hivyo wengine hasa walikata kuni na kuchota maji; wengine waliajiriwa kwenye kunywesha mitende, wakibeba mifuko ya ngozi migongoni mwao; na Ali, angalau wakati mmoja, alipokea tende kumi na sita kwa kujaza ndoo na maji, na kuzimwaga juu ya udongo kwa ajili ya kutengeneza matofali kwa kiwango cha tende moja kwa ndoo moja; ambacho kwa shida kilimpa-tia mlo aliokula pamoja na Mtume."

(Muhammad and the Rise of Islam, London, 1931)

Kuwafungamanisha Muhajirina kwenye maisha ya kiuchumi ya Madina, lilikuwa ni tatizo gumu sana, na lilielemea ubunifu wote wa Mtume. Hakutaka mtu yoyote wa jamii ya Kiislamu, sana sana wale Muhajirina, awe mzigo kwa mtu mwingine yeyote, na alifanya kila lile aliloweza kufanya kupunguza utegemezi wao juu ya Ansari.

Udugu wa Muhajirina na Ansari

Moja ya shughuli za mwanzo za Mtume (s.a.w.) za kuwajenga upya wale Muhajirina wasio na makazi pale Madina, na kuwafungamanisha katika maisha ya kiuchumi na kijamii ya mji huo, ilikuwa ni kuwafanya wawe "ndugu" wa Ansari. Miezi michache baada ya kuwasili kwake hapo Madina, aliwaambia Muhajirina na Ansari kwamba walipaswa kuishi kama "ndugu" wa kila mmoja wao, na akawaunganisha wawili wawili kama ifuatavyo:

Muhajir                                  ndugu ya                                 Ansari

Ammar ibn Yasir                            "                                     Hudhayfa al-Yamani

Abu Bakr Siddiq                             "                                     Kharja bin Zayd

Umar bin Khattab                           "                                     Utba bin Malik

Uthman bin Affan                           "                                     Aus bin Thabit

Abu Dharr al-Ghiffari                     "                                     Al-Mundhir b. Amr

Mas'ab ibn Umayr                          "                                     Abu Ayyub

Abu Ubaidah Aamer al-Jarrah          "                                     Saad ibn Maadh

Zubayr ibn al-Awwam                     "                                     Salama bin Waqsh

Abdul Rahman bin Auf                   "                                     Saad ibn Rabi

Talha ibn Ubaidullah                       "                                     Ka'ab ibn Malik

119

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ali ibn Abi Talib pekee ndiye aliyeachwa bila ya "ndugu." Alikuwa anastaajabu kwa nini wakati Mtume wa Allah (s.a.w.) alimshikilia mikononi mwake na akamwambia: "Wewe ni ndugu yangu katika dunia hii na katika akhera."

Muhammad ibn Ishaq:

"Mtume (s.a.w.) mwenyewe alimshika Ali mkononi na kusema: "Huyu ni ndugu yangu." Hivyo Mtume wa Allah (s.a.w.) Bwana wa waliotumwa, na kiongozi wa Wacha-Mungu, Mtume wa Mola wa mbingu na ardhi, asiye na mshirika wala asiyelingana na yoyote, na Ali ibn Abi Talib wakawa ndugu."

(The Life of the Messenger of God) Edward Gibbon:

"Baada ya safari ya hatari na ya haraka kandoni mwa mwambao wa bahari, Muhammad alisimama hapo Kuba, maili mbili kutoka mjini, na akafanya kuingia kwake kwa uwazi ndani ya Madina siku kumi na sita baada ya kukimbia kwake toka Makka. Wafuasi wake shupavu sana walikusanyika kumzunguka yeye; na walio sawa, ingawa sifa mbali mbali za Waislamu zilitambulikana kwa majina ya Muhajirina na Ansari, wakimbizi wa Makka na wasaidizi wa Madina.

Kufutilia mbali mbegu za wivu, Muhammad kwa hekima na busara akawaunganisha wawili wawili wale wafuasi wake wakuu kwa haki na wajibu wa udugu; ambapo Ali alijikuta binafsi bila mwenza, na Mtume (s.a.w.) kwa upendo mwingi akatamka kwamba yeye atakuwa sahiba na ndugu wa yule kijana mtukufu.

.(The Decline and Fall of the Roman Empire) Muhammad Husein Haykal:

"Wazo la kwanza kumjia yeye (Muhammad) lilikuwa lile la kupanga upya safu za Waislamu ili kuunganisha umoja wao na kufuta kila uwezekano wa kuibuka tena kwa mgawanyiko na uhasama. Kwa kulitambua lengo hili, aliwataka Waislamu kusuhu-biana wao kwa wao kwa ajili ya Allah (s.w.t.) na kujifunga wenyewe wawili wawili. Alieleza jinsi yeye na Ali ibn Abi Talib walivyokuwa ndugu..."

(The Life of Muhammad, 1935)

Muhammad, Allah (s.w.t.) ampe rehma na Ahlul-Bait wake, aliwafanya Muhajirina na Ansari kuwa "ndugu" wa kila mmoja wao. Lakini Ali, kama yeye mwenyewe, alikuwa Muhajir (mhamiaji), na bado yeye (Muhammad) alimchagua yeye kuwa ndugu yake. Kwa kufanya hivyo, alikuwa akibainisha kile cheo cha kipekee na hadhi maalum ya Ali katika

120

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Uislamu. Ali, ingawa bado kijana, tayari alikuwa amemzidi kwa cheo kila mtu katika kutu-mikia Uislamu bidii ya wajibu kwa Allah (s.w.t.) na Mtume Wake. Alikipata cheo hiki kikubwa kwa kutumia uwezo wake na tabia.

Hii haikuwa, hata hivyo, mara ya kwanza ambapo Mtume wa Allah (s.a.w.) alimtangaza Ali kuwa ndugu yake. Mapema, wakati akiwa bado yuko Makka, aliwafanya maswahaba zake wakuu kuwa "ndugu" wa kila mmoja. Jozi hizo za "udugu" zilikuwa za Abu Bakr na Umar; Uthman bin Affan na Abdur Rahman bin Auf; Talha na Zubair; Hamza na Zayd bin Haritha; na Muhammad Mustafa ibn Abdullah na Ali ibn Abi Talib.

Imam Nuurdin Ali ibn Ibrahim al-Shafi'i amemnukuu Mtume wa Allah (s.a.w.) katika kitabu chake Siirat Halabia (juz. 2, uk.120) alisema: "Ali ni ndugu yangu katika dunia hii na vile vile katika dunia ya Akhera."

Makadirio ya wajibu wa Muhajirina na wa Ansari

Hawa Muhajirina walikwisha poteza mali walizokuwa nazo huko Makka, na wote waliin-gia Madina wakiwa mikono mitupu. Walitokana na vikundi vya wilaya mbili. Kikundi kimoja kilikuwa ni cha wale watu waliokuwa wachuuzi na wafanyabiashara kitaaluma, na walikuwa matajiri sana. Walipokwenda Madina, waliingia kwenye biashara, wakafanikiwa kwayo, na wakawa matajiri tena.

Kundi jingine lilitokana na "watawa" wa Kiislam. Walikuwa masikini huko Makka, na walipohamia Madina, bado walichagua kuwa masikini. Walibeua utajiri wa kidunia, na hawakuchukua mamlaka ya kiuchumi mikononi mwao wakati wowote ule.Wawakilishi wa kundi hili walikuwa watu kama Abu Dharr al-Ghiffari; Ammar ibn Yasir na Miqdad ibn al-Aswad. Allah (s.w.t.) aliwasifia katika Kitabu Chake kama ifuatavyo:

Usahihi-8.jpg

"(Sehemu yake) wapewe mafakiri Muhajirina waliotolewa majumbani mwao na mali yao kwa ajili ya kutafuta fadhila kutoka kwa Allah na radhi zake, na wanamsaidia Allah na Mtume Wake. Hao kwa hakika ndio wakweli." (Sura ya 59 Aya ya 8)

Maansari waliwafanyia wema mhajirina kutoka Makka kuliko vile ndugu za hawa Muhajir wenyewe ambavyo wangeweza kuwafanyia. Waliwaweka katika nyumba zao wenyewe, wakawapa vifaa vya matumizi ya nyumbani; wakawafanya washirika katika kilimo, au wakawapa nusu ya ardhi yao. Wale Ansari waliokuwa kwenye biashara, wakawafanya

121

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

hawa Muhajir washirika katika biashara. Historia haiwezi kuonyesha ukarimu unaolingana na wa hawa Ansari. Walikuwa ni "wenyeji" sio tu kwa wale Muhajirina wasiokuwa na makazi na mafukara peke yake bali pia na kwa Uislamu wenyewe, uliong'olewa Makka, ukaota mizizi mipya hapo Madina, ukachipua na mara ukawa na uwezo.

Hawa Ansari walikuwa wa lazima kwa ajili ya kudumu kihakika kwa Uislamu. Wapi ungekuwa Uislamu uwe, na wapi wangekuwepo Muhajirina kama Ansari wasingewapa hifadhi? Wakati uhasama na waabudu masanamu ulipoanza, walikuwa ni Ansari, na wala sio Muhajirina, waliochukua sehemu kubwa ya mapigano. Bila ya msaada mkubwa na imara ambao waliutoa kwa Mtume, vile vita vya Waislamu visingepiganwa, mbali na ushindi uliopatikana. Walikuwa pia wapokeaji wa sifa na utambulikanaji wa Mbingnii, kama tunavyosoma kwenye Aya ya Qur'an Tukufu ifuatayo:

Usahihi-9.jpg

"Lakini wale ambao, kabla yao, walikuwa na makazi (huko Madina) na walikuwa wameami-ni, wakaonyesha mapenzi yao kwa wale waliohamia kwao, wala hawaoni choyo vifuani mwao kwa vile walivyopewa (Muhajirina), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushiwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa." (Sura ya 59; Aya ya 9).

Hawa Muhajirin, mwanzoni, hawakuwa na jinsi ya kuwalipa hao Ansari kwa ukarimu na wema wao. Lakini je waliwahi kutoa shukurani zao? Inaonekana kwamba ukiwaondoa Muhajirin wawili, hakuna aliyeshukuru. Hawa wawili wa kuwaondoa walikuwa ni Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) na Ali, mshika makamu wake. Walikiri deni lao la shukurani kwa Ansari kwa maneno na vitendo pia, na kamwe hawakuipoteza nafasi ya kufanya hivyo. Hata hivyo, wote Muhammad na Ali, kama walezi pekee wa maadili ya Uislamu, walitambua kwamba Uislamu umepata mahali pa usalama hapo Madina pamoja na Ansari. Hawa Ansari kwa hiyo, walishika nafasi maalum katika mioyo yao.

Muhajirin waliobakia, yaani, wale matajiri miongoni mwao, hawakushiriki katika wasi-wasi wa Muhammad na Ali kwa ajili ya Ansari. Wakati madaraka yalipoingia mikononi mwao, waliwasukuma wale Ansari nyuma, na wakawashusha wahusike na dhima ndogo ndogo tu. Mwanzoni, waliwapuuza kabisa Ansari. Lakini kupuuzwa hakukuwa kubaya sana kulinganishwa na kile kilichokuwa kiwafike katika nyakati za baadae.

122

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

(Kati ya kipindi kilichoshughulikiwa na Sira na kuhaririwa kwa kitabu chenyewe inatishia misiba mikubwa miwili ya Karbala, wakati Husein na wafuasi wake walipouawa katika mwaka wa 61 H.A., na kilio cha Madina mnamo mwaka 63 H.A. wakati Ansari kama elfu kumi wakiwemo maswahaba wa Mtume (s.a.w.) wasiopungua themanini walipouawa. Imenukuliwa katika - Introduction to the biography of the Prophet by Ibn Ishaq).

Muhajirin waliwaghilibu watetezi wa wapagani wa Makka - Banu Umayya - juu yao. Banu Umayya walikuwa maadui wakubwa wa Ansari. Kama ukarimu wa Ansari kwa Muhajirin hauna kifani katika historia, utomvu wa shukurani wa hawa Muhajirin kwa wahisani wao pia hauna kifani. Wakati Muhajirina walipokuja Madina, Maansari ndio waliokuwa mabwana wa Madina. Ilikuwa tu ni kwa uungwana wa Ansari kwamba Muhajirin waliweza kuingia na kuishi Madina. Lakini mara tu Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) na rafiki na mlezi wa Ansari, alipokufa, wakakoma kuwa mabwana nyumbani kwao wenyewe. Kifo chake kilikuwa ndio ishara ya mgeuko wa ghafla katika ustawi wao.

123

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Vita vya Kiislamu

Muhammad Mustafa, Mtume Wa Allah (s.a.w.) ilibidi apigane mfululizo wa vita katika kuutetea Uislamu kutoka kwenye makazi yake mapya hapo Madina. Vile vita ambavyo aliongoza jeshi la Kiislam yeye mwenyewe, vinaitwa "Ghaz'wa" na ile misafara ambayo aliyotuma kutoka Madina chini ya amri ya mmojawapo wa maswahaba wake, inaitwa "Sariyya".

Kwa kukisia, Mtume (s.a.w.) alizindua kampeni za kijeshi 80 katika ile miaka kumi tangu kuhama kwake mwaka 622 A.D. mpaka kufa kwake mwaka 632 A.D. Baadhi ya kampeni hizi hazikuwa chochote zaidi ya ujumbe wa upelelezi. Idadi iliyohusika ndani yake ilikuwa ndogo sana, na hasa walichokifanya kilikuwa ni kuangalia mienendo ya koo au kabila fulani. Zingine zilikuwa ni misafara ya ki-tablighi. Nyingine nyingi zilikuwa ni za mik-waruzano midogodogo tu. Bado nyingine zilikuwa ni za udadisi tu kwa sababu ya tukio maalum lililohusiana nazo. Nitatoa maelezo ya juu juu ya kampeni hizo ndogo, na nitawe-ka msisitizo hasa kwenye yale mapambano makubwa ya Uislamu.

Hapo nyuma kabisa kabla ya Uislamu, Wagiriki na Warumi waligundua kwamba vita vinaweza kubadili hatma za mataifa. Miongoni mwa kampeni za Mtume, kuna vita vitano ambavyo vinaweza kusemekana kwamba vimebadili hatma za mataifa. Navyo ni vita vya Badr, Uhud, Khandaq, Khaybar na Hunayn.

Vita hivi vilikuwa haviepukiki. Maquraishi wa Makka waliamini kwamba kama Waarabu wote wataukubali Uislamu, itakuwa na maana kwao (Maquraishi) ya kupoteza mapato yote ya Hijja, na kupotea kwa heshima waliyokuwa nayo kama walezi wa masanamu. Mafanikio ya Uislamu waliyabashiri kwa usawa kabisa kama pigo la kifo cha heshima. Ilikuwa ni hofu hii, hofu ya kupoteza mamlaka ya kiuchumi na kisiasa na hadhi ambayo iliharakisha vita kati yao na Waislamu.

Tangu kule kuhama kwa Waislamu toka Makka, hali ya kivita isiyopingika ilijitokeza kati yao na Maquraishi. Katika siku za mwanzoni hapo Madina, Waislamu hawakuthubutu kusogeza silaha zao wakati wowote. Askari wa doria waliwekwa mjini kote kila usiku kuwatahadharisha wakazi endapo adui atafanya shambulizi la ghafla. Mtume (s.a.w.) hakuweza kulala usiku akihofia mashambulizi wakati wowote. Ilikuwa ni katika mazingi-ra kama Haya ambapo ilikuwa achukue hatua za maksudi kwa ajili ya usalama wa Madina. Kama mkuu wa dola inayoondokea, usalama wa dola hiyo ulikuwa ndio wajibu wake wa kwanza.

124

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kwa manufaa ya usalama, Waislamu iliwabidi kutupia macho nyendo za adui, marafiki zake adui na wasaidizi wao.

Mtume (s.a.w.) alituma msafara wa kwanza mnamo mwezi wa tisa wa mwaka wa kwanza wa Hijiria, chini ya uongozi wa ami yake, Hamza ibn Abdul Muttalib. Muhajirina thelathi-ni walishiriki ndani yake. Makusudio yao yalikuwa ni kuzuia msafara wa kibiashara wa Maquraishi. Lakini kabila moja, lenye urafiki kwa pande zote, likasuluhisha kati yao. Hapakuwa na mapigano, na msafara ule ukarudi Madina.

Katika mwezi uliofuatia, Mtume (s.a.w.) aliwatuma Muhajirina sitini chini ya uongozi wa binamu yake, Ubaida ibn al-Harith, kwenda Raghib, karibu na Red Sea (bahari nyekundu). Walikabiliana na msafara wa Maquraishi. Pande zote mbili zilirushiana mishale michache lakini hapakuwa na majeruhi. Wafanyibiashara wawili wa Makka waliuacha msafara wao, wakaja upande wa Waislamu, wakasilimu, na wakafuatana na msafara ule wakati ulipore-jea Madina.

Ubaida ibn al-Harith anasemekana alirusha mshale kwa adui. Ulikuwa ndio mshale wa kwanza kurushwa kwa ajili ya Uislamu.

Sir William Muir:

"Ubaida anajulikana katika Hadith kama ni yeye ambaye katika tukio hili, "alirusha mshale wa kwanza kwa ajili ya Uislamu."

(The Life of Mohammed, London, 1877)

Hapakuwa na kampeni nyingine za kivita katika muda uliobakia wa mwaka wa kwanza wa Hijiria.

125

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mwaka wa pili wa Hijiria

Msafara wa kwanza ambao Muhammad Mustafa aliuongoza yeye mwenyewe, ulikuwa ni ile Ghaz'wa (kampeni) ya Waddan. Alimteua Saad ibn Ubadah kama gavana wa Madina, na akachukua kikundi cha wafuasi wake kwenda Waddan, kijiji kati ya Madina na Makka. Msafara wa Maquraishi ulielezewa kwamba ulisimama pale. Lakini msafara huo uliondo-ka Waddan kabla ya kuwasili kwa Waislamu. Wao, kwa hiyo, walipumzika kwa siku chache na kisha wakarudi Madina.

Mnamo mwezi wa saba (Rajab) wa mwaka wa pili wa Hijiria, yaani, miezi kumi na tano baada ya kuhamia Makka, Mtume (s.a.w.) alituma watu saba chini ya uongozi wa binamu yake Abdullah ibn Jahash, kwenda Nakhla, oasis iliyoko Kusini, ambako walikuwa wachunguze mienendo ya msafara fulani wa Maquraishi.

Huko Nakhla, Abdullah aliuona msafara mdogo wa Maquraishi uliokuwa ukirejea Makka. Wenye msafara huo walikuwa ni Amr bin al-Hadhrami, Uthman bin Abdullah bin al-Mughira, na kaka yake, Naufal, na Hakam bin Kaisan. Abdullah akawashambulia na kuka-mata mizigo yao. Amr bin al-Hadhrami aliuawa; Uthman na Hakam wakatekwa; na Naufal akafanikiwa katika kutoroka.

Msafara huu unachukuliwa kwamba ni muhimu kwa sababu ilikuwa ni mara ya kwanza ambapo palikuwa na mapambano kati ya Waislamu na wapagani. Ilikuwa pia ni mara ya kwanza ambapo palikuwa na umwagaji wa damu kati yao, na Waislamu walikamata ngawira kutoka kwao.

Abdullah bin Jahash na kundi lake wakarudi Madina pamoja na wafungwa wao na ngawira za vita. Kati ya wafungwa wawili hao, Hakam bin Kaisan alisilimu na akaishi Madina. Uthman bin Abdullah alikombolewa na ndugu zake, na akaenda Makka.

Kubadilishwa kwa Qibla - February 11, A.D. 624.

Katika miezi kumi na sita ya kwanza baada ya Hajira, Qibla cha Waislamu kwa ajili ya Swala kilikuwa Jerusalem (walielekea Jerusalem wakati walipokuwa wakiswali). Kisha Mtume wa Allah (s.a.w.) akapokea wahy (ufunuo) ukimuamuru kubadilisha sehemu ya mwelekeo kutoka Jerusalem upande wa kaskazini kwenda Makka upande wa Kusini.

Dr. Montgomery Watt na John Christopher wametoa "sababu" zao juu ya kubadilika kwa muelekeo wa Qibla. Wanasema kwamba, hapo mwanzoni. Mtume (s.a.w.) alitegemea kwamba kuelekea Jerusalem wakati wa kuswali, kungefanya nyoyo za Wayahudi wa Yathrib kumnyenyekea yeye, na wangemkubali kama Mjumbe wa Allah (s.a.w.). Lakini

126

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

aligundua, wanaendelea kusema kwamba, ingawa alielekea Jerusalem, wakati alipokuwa akiswali, wale Wayahudi walibakia wenye kushuku ukweli na uaminifu wake. Kisha wanaongeza kwamba baada ya miezi kumi na sita, Mtume (s.a.w.) alikata tamaa ya kuwaingiza Wayahudi wale kwenye Uislamu.

Kwa mujibu wa Dr. Montgomery Watt na John Christopher na baadhi ya mustashirki wa Magharibi, mara Mtume (s.a.w.) alipopoteza matumaini ya kuwapata wale Wayahudi kwenye Uislamu, aliondoa shauku juu yao, na akaamua kuweka dhamira yake kwa Waarabu. Huku kubadilika kwa Qibla, wanadai, kulikuwa ni tendo la hisia za kuwaridhisha Waarabu.

Hatujui kama Wayahudi hawa walikasirika ama kama Waarabu hawa walifurahishwa na kubadilika kwa Qibla. Sisi, kwa kweli, wala hatujui ni Waarabu wa wapi, kwa mujibu wa Dr.Watt, ambao Mtume (s.a.w.) alikuwa anajaribu kuwafurahisha - ni Waarabu wa Madina ama Waarabu wa Makka!

Waarabu wa Madina walikuwa wameukubali Uislamu na walimtii Mtume. Kwao wao kitu muhimu kilikuwa ni kumtii yeye Mtume (s.a.w.) kwa vile alikuwa ndiye mfasili wa ujumbe wa Allah (s.w.t) kwa wanadamu. Walielekea Makka walipokuwa wanaswali na hawakuuliza maswali yoyote ya kwa nini Qibla kilibadilishwa.

Waarabu wa Makka walikuwa bado ni waabudu masanamu. Na wao pia walisikia habari za kubadilika kwa Qibla kutoka Jerusalem kwenda Makka. Lakini hakuna ushahidi wowote kwamba mmoja wao yeyote, kwa kuridhishwa na kufurahishwa na mabadiliko haya, alikuja Madina na kujitolea kuwa mwislamu. Walibakia walivyokuwa, ama Qibla kilikuwa Jerusalem au Makka, kwao haikuonyesha tofauti yoyote.

Maelezo ya Waislamu ni rahisi na yenye mantiki; Allah (s.w.t.) amemuamuru mja Wake, Muhammad, kubadili Qibla, na alitii. Hii amri ya kubadili Qibla ilitolewa ndani ya Aya ya 44 ya Sura ya pili ya Qur'an Tukufu.

Katika mwezi wa Shaban (mwezi wa nane), mwaka wa pili wa Hijiria, kufunga katika mwezi wa Ramadhani (mwezi wa tisa) kulifanywa ni amri ya lazima kwa Waislamu. Wao, kwa hiyo, walifunga katika mwezi uliofuata (yaani, mwezi wa Ramadhani). Mwisho wa mwezi wa kufunga, walitakiwa kutoa Zaka-ul-Fitr, Zaka maalum.

Katika mwaka huo huo, kodi nyingine, Zaka-ul-Mal, iliwekwa juu ya Waislamu. Kodi hii inakadiriwa katika kiwango cha asilimia 2.5 ya mali ya mwislamu. Katika nyakati za Mtume, kodi hii ilikuwa ikilipwa kwenye Bayt-ul-Mal au hazina ya umma, na ilitumika katika ustawi wa masikini na watu wagonjwa katika jamii. Lakini kama hakuna Bayt-ul-Mal, Waislamu lazima wailipe kwa masikini wanaostahiki, wajane, mayatima na wale watu katika jamii ambao hawana uwezo wa kujikimu wenyewe

127

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Vita vya Badr

Vita vya kuvunja moyo kati ya Maquraishi na Waislamu vingeshadidisha kwenye uhasama wa dhahiri wakati wowote. Abu Jahl alikuwa mmoja wa "wachuuzi" katika Makka ambaye aliyeendeleza vita-visivyokoma vya kisirisiri dhidi ya Muhammad Mustafa na wafuasi wake. Ushari wake wa kiuzalendo uliiweka Makka katika hali ya wasiwasi wa kudumu.

V.C.Bodley:

"Wazimu wa Abu Jahl juu ya Muhammad ulibakia katika kiwango cha kuchemka. Aliweka vikundi vya mashambulizi daima kwenye hali ya kuendelea kushambulia, vikishambulia makundi yoyote ya Waislamu yaliyo pembeni ambayo yangeweza kushambuliwa kwa ghafla. Alifanya uvamizi kwenye vitongoji vya Madina na kuharibu mazao na bustani. Alimfanya Muhammad aone kwamba hisia zake hazi-jabadilika, kwamba makusudio yake bado ni ya kimauaji."

(The Messenger, the Life of Mohammed, New York. 1946)

Mapema mwezi March, 624, habari zilipokelewa Madina kwamba msafara wa Maquraishi ulikuwa ukirejea Makka kutoka Syria. Msafara huo haukuwa umebeba bidhaa tu bali pia na silaha. Ilikadiriwa kuwa msafara huo ulitengeneza faida ya dinari 50,000 (vipande vya dhahabu). Silaha hizo na utajiri mpya uliopatikana vilikuwa vitumike, kwa mujibu wa habari hizohizo, kuandaa jeshi la kupigana dhidi ya Waislamu. Msafara huo uliongozwa na Abu Sufyan, mkuu wa ukoo wa Banu Umayya.

Muhammad Mustafa aliamua kuuzuia msafara huo wa Makka. Alimteua Abu Lababa kama gavana wa Madina, na akaondoka mjini hapo na kikosi cha watu 313. Kati ya hawa, 80 walikuwa Muhajir, na 233 walikuwa Ansari. Mwisho wa safari yao ulikuwa ni Badr, kijiji Kusini-Magharibi ya Madina ambako wakitegemea kukutana na huo msafara wa Makka.

Waislamu hawakulijua hilo bado kwamba hawangeuona kamwe msafara wa Maquraishi, na kwamba watakuwa, badala yake, wawe kwenye mapambano, kwenye uwanja wa vita, na jeshi la Maquraishi.

Wakati huohuo, wapelelezi wa Makka walimjulisha Abu Sufyan kwamba kundi la Waislamu limeondoka Madina, na lilikuwa likienda kwa haraka kuelekea kwenye msafara wake. Mara tu alivyosikia hivyo, aliiacha ile njia ya msafara ya kawaida, akauongoza ule

128

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

msafara wake kuelekea Magharibi kwenye pwani ya bahari ya Red Sea, na kisha akageukia upande wa Kusini kuelekea Makka, vile vile alituma ujumbe Makka kuomba msaada. Mjini Makka Abu Jahl alikuwa tayari akishughulika kuchochea ghadhabu za watu dhidi ya Waislamu, kufuatia tukio la Nakhla.

Aliitikia kwa shauku sana mwito wa Abu Sufyan, na akakiongoza nje ya Makka kikosi cha wapiganaji 1000 chenye wapanda farasi 100, dhidi ya Waislamu. Msururu wa ngamia 700 ulibeba vifaa kwa ajili ya vita na mahitaji mengineyo. Askari wa miguu walivaa ngao na deraya.

Muhammad Mustafa hakujua kwamba jeshi limeondoka Makka na lilikuwa likisonga mbele kuelekea Madina kuulinda msafara wa Maquraishi, na kuwapa changamoto Waislamu. Wakati Mtume (s.a.w.) alipowasili kwenye maeneo ya Badr, alimtuma Ali kuchunguza nchi iliyozunguka pale. Katika visima vya Badr, Ali aliwashitukiza baadhi ya wabeba maji. Katika majibu kwa maswali yake, walimwambia kwamba walikuwa wan-abeba maji kwa ajili ya jeshi ambalo lilikuja kutoka Makka, na ambalo lilipiga kambi upande wa pili wa vile vilima vya karibu.

Ali aliwapeleka wale wabeba maji mbele ya Mtume wa Uislamu. Kutoka kwao alijua kwamba ule msafara wa Maquraishi tayari ulikuwa umekwisha toroka, na kwamba Waislamu wale, katika muda ule ule, walikabiliwa na jeshi la Makka.

Sir William Muir:

"Katika kufika kwenye maeneo karibu na Badr, Muhammad alimtuma Ali, pamoja na wengine wachache, kuchunguza ile ardhi iliyoinuka juu ya chemchemu. Hapo wali-washitukiza wabeba-maji watatu wa maadui, wakiwa karibu na kujaza mifuko yao ya ngozi ya kondoo. Mmoja akatorokea kwa Maquraishi; na wale wengine wawili wakakamatwa na kupelekwa kwenye jeshi la Waislamu. Kutoka kwao Muhammad alitambua ukaribu wa adui zake. Walikuwepo watu 950; mara tatu zaidi ya idadi ya watu wa jeshi la Waislamu. Walikuwa wamepanda juu ya ngamia 700 na farasi 100, hawa wapanda farasi wakiwa wamefunikwa na ngao za chuma.

(The Life of Muhammad, London, 1877)

Taarifa hii muhimu ya kuhusu maadui ilipokelewa kupitia Ali ibn Abi Talib. Kitendo chake, kwa upande mmoja, kiliwatahadharisha Waislamu; na kwa upande mwingine, kili-wapora maadui ile fursa ya kuwashitukiza. Waislamu walikuwa tayari kuwakabili. Hata hivyo, kuwepo kwa adui hai, mshari na mwenye kutisha, badala ya msafara tajiri, ndani ya umbali wa jirani sana, kulibadilisha kabisa hali kamili kwa Waislamu, na iliwabi-di wafanye tathmini mpya ya hatari na uwezekano wa mkabiliano naye. Hawakuwa wame-

129

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

jiandaa vema, na walikuwa na farasi wawili tu na ngamia 70 pamoja nao.Wengine wao walikuwa na panga lakini hawakuwa na ngao na wengine walikuwa na ngao bali hawakuwa na panga. Mtume (s.a.w.) ambaye alivitambua vikwazo hivi vya dhahiri, aliitisha baraza la vita, na akalifikisha suala hili mbele ya maswahaba zake kwa tafakari na uamuzi.

Mtu wa kwanza aliyesimama na kuzungumza juu ya wakati huu mgumu, alikuwa ni Miqdad. Alizungumza hisia na mawazo ya Muhajirina aliposema: "Ewe Mtume wa Allah, fanya kile ambacho Allah (s.w.t.) amekuamuru kufanya. Tuko pamoja nawe, sasa na wakati wote; na hatutakuambia kile Wana wa Israeli walichomwambia Musa: 'Wewe na Mungu wako mwende mkapigane dhidi ya adui; na sisi, tutabaki hapa, na kukaa hapa.' Hapana, hatutawaiga wale Wana wa Israeli. Tutakufuata wewe na kuzitii amri zako."

Muhammad alitoa baraka zake kwa Miqdad. Lakini Miqdad alikuwa ni Muhajir, na Muhammad alikuwa na shauku ya kujua ni nini Ansari watafanya. Yeye aliona kwamba wale Ansari wangepigana katika kuilinda Madina yenyewe lakini wasingependa kupigana nje ya mji wao. Akihisi shauku yake, Saad ibn Muadh, mmoja wa viongozi wa Ansari, alisimama na kusema: "Tumeshuhudia kwamba wewe ni Mjumbe wa Allah. Tumekupa kiapo chetu cha kukutii wewe. Popote utakapokwenda, tutakwenda pamoja nawe. Kama kutakuwa na kuonyeshana dhamira na washirikina, tutasimama imara katika kukuunga mkono kwetu. Kwa vita na kwa amani, tutakuwa daima waaminifu kwako."

Matamshi Haya yenye msimamo wa wazi ya kuunga mkono ya kiongozi wa Ansari, yalimridhisha Mtume, na akaomba baraka za Allah (s.w.t.) juu yao wote. Yeye alijua kwamba sio vita vya Badr wala vita vyovyote vile vingeweza kupiganwa bila ya msaada wa Ansari. Hawa Ansari walikuwa, kwa hakika, wa muhimu sana kwa ajili ya mafanikio katika mapambano kati ya Uislamu na upagani, kama ilivyoonyeshwa kabla.

Kwa namna halisi na kwa kiasi, Waislamu walikuwa kwenye upungufu lakini kasoro hizi zilifutwa na hamasa zao. Walikuwa na imani na uongozi wa kimajaaliwa wa Muhammad. Na walikuwa wameungana. Muungano na umoja wao wa dhamira vilikuwa viwe chanzo cha nguvu kubwa kwao katika mapambano yajayo na jeshi la Makka.

Kwa kuhakikishiwa msaada wa Ansari, Muhammad Mustafa alichukua uamuzi wa kukubali changamoto ya Maquraishi. Yeye na askari wa kawaida wa jeshi la Madina wanaelekea kutambua wazi kwamba matokeo ya mapambano na adui siku itakayofuata, yatakuwa yamezidi katika athari zake.

130

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Sir William Muir:

"Muhammad alikuwa anayafahamu kabisa mazingira hayo magumu. Majaaliwa ya Uislamu yalitegemea juu ya matokeo ya mapambano yanayokuja."

(The Life of Mohammed, London, 1877)

Mtume (s.a.w.) aliwaamuru Waislamu kukita mahema yao juu ya ardhi ya pale waliposimama. Lakini kijana mmoja wa Ansari alionyesha faida za kuchagua sehemu nyingine ya kupiga kambi ambapo ardhi ilikuwa juu zaidi na imara, na pia alipendekeza kwamba Waislamu wachukue milki ya visima vyote vya Badr. Mapendekezo yake yalikubalika moja kwa moja.

S. Margoliouth:

"Hubab mtoto wa al-Mundhir, mdogo kwa Mtume (s.a.w.) kwa miaka ishirini, baada ya kuhakikisha kwamba walikuwa kwenye vita vya kawaida, na kule kuwa na ujuzi maalum wa vile visima vilivyoko jirani, alimshauri Mtume (s.a.w.) kukaa mbele ya vyote isipokuwa kimoja, ambacho katika mzunguko wake wangefanya hifadhi, ili kuwa na ugawaji wa maji wa kuaminika kwa ajili ya vikosi hivyo; kule kuwa na nguvu hii ya asili yenye thamani baadae kutasaidia. Mtume (s.a.w.) aliyakubali mapendekezo yake na akaliweka jeshi lake chini ya usimamizi wa Hubab.

(Mohammed and the Rise of Islam, London, 1931)

Matukio mara yakadhihirisha kwamba mapendekezo ya Hubab yalikuwa mazuri sana, na kukubaliwa kwake na Mtume (s.a.w.) kuliwapa Waislamu faida kubwa ya kimbinu juu ya maadui.

Vita hivi vya Badr vilipiganwa katika mwaka wa pili wa Hijiria, kwenye tarehe 17 ya mwezi wa Ramadhani, mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislam (March 15, A.D.624). Lile jeshi la Makka lilitoka nje ya kambi yao mapema asubuhi kukutana na Waislamu. Majeshi haya maw-ili yakajipanga katika mpango wa kivita. Mtume (s.a.w.) akachukua upinde mkononi mwake na akatembea kati ya mistari iliyopanga safu za Waislamu. Tendo lake la mwisho kabla ya vita kuanza, lillikuwa ni kumuomba Allah (s.w.t.) kutoa ushindi kwa waja Wake wanyenyekevu.

Vita vikaanza katika desturi ya Kiarabu ya taratibu za vita ambamo shujaa wa upande mmoja alipanda au kutoka nje ya msitari, na kuwapa changamoto mashujaa wa adui kukutana naye katika pambano la mtu mmoja mmoja.

Hii ilimpa fursa ya kujipatia sifa binafsi kwa kuonyesha ujasiri wake mwenyewe, nguvu zake na ujuzi katika upanda farasi. Majeshi hayo mawili yalifanya kama namna ya kibwa-gizo kwa ajili ya mapambano kati ya mashujaa wachache wanaojigamba. Baada ya Haya

131

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

mapambano ya awali, ilikuwa ni desturi kwa majeshi hayo mawili kushambuliana, na kuin-gia kwenye mapigano ya mkono kwa mkono.

Kutoka upande wa Makka, wapiganaji watatu, Utba mtoto wa Rabia; Shaiba, kaka yake; na Walid, mtoto wake; walitoka kwenye nafasi ya wazi kati ya majeshi hayo mawili, na wakawapa changamoto Waislamu. Changamoto yao ilichukuliwa na Hamza, ami yake Muhammad na Ali; Ubaida ibn al-Harith, binamu yake Muhammad na Ali; na Ali ibn Abi Talib.

Walid ibn Utba alikuwa mmoja wa wapiganaji wakali sana wa Makka. Ali alijikuta akika-biliana naye. Walikuwa ndio jozi ya vijana zaidi, na walikuwa wa kwanza kuingia kwenye kupigana. Zile jozi zingine mbili zikapumzika, kuwaangalia wale wapiganaji vijana waw-ili wakipambana. Vijana hawa wawili walitupiana mapigo machache, na kisha Ali akapiga pigo lake ambalo lilimuua Walid.

Mara baada ya Walid kuuawa, wale wapiganaji wengine nao wakashambuliana. Hamza akamuua Utba. Lakini Ubaida alijeruhiwa vibaya sana na Shaiba. Wakati Ali alipomuona Ubaida anaanguka chini, alimshambulia Shaiba, na akamuua pia. Kwa maadui zao wawili kufa, na hakuna mtu uwanjani, Ali na Hamza walimbeba Ubaida kumrudisha kwenye safu za Waislamu ambako alikufa kwa sababu ya majeraha yake. Alikuwa mwislamu wa kwanza kuuawa kwenye uwanja wa mapambano.

Sir William Muir:

"Ndugu hawa wawili, Shaiba na Utba, na Walid, mtoto wa Utba, walisonga mbele kwenye nafasi kati ya majeshi hayo, na wakawataka shari mashujaa watatu kutoka kwenye jeshi la Muhammad kupambana nao mmoja mmoja. Muhammad aki-wageukia jamaa zake, akasema: "Enyi wana wa Hashim! Amkeni na mpigane, kwa mujibu wa haki yenu." Ndipo Hamza, Ubaida na Ali, wale ami na binamuze Mtume, wakatoka mbele.

Hamza alivaa unyoya wa mbuni kifuani mwake, na nyoya jeupe lilitambulisha kofia ya vita ya Ali. Kisha Utba akamwita mwanae, Walid, "Simama na upigane." Hivyo Walid alitoka mbele na Ali akatoka dhidi yake. Walikuwa ndio vijana zaidi ya hao sita. Mapambano yalikuwa mafupi; Walid alianguka akiwa amejeruhiwa vibaya kwa upanga wa Ali.

(The Life of Mohammed, London, 1877) Sir John Glubb:

"Machifu watatu wa Makka, Utba, Shaiba na Walid, mtoto wa Utba, walijitokeza mbele ya msitari wa Maquraishi na kuwataka vita Waislamu watatu kukutana nao

132

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

katika pambano la mmoja mmoja. Muhammad akiwageukia Muhajir aliita: "Enyi Bani Hashim, simameni na mpigane." Watu watatu wakiwa wamefunikwa na ngao za chuma walitoka kwenye safu za Waislamu. Walikuwa ni Hamza, ami yake Mtume; Ali ibn Abi Talib, binamu yake, na mfuasi wa kwanza wa kiume; na Ubaida ibn Harith.

Ile jozi ya vijana zaidi ilishambuliana mwanzo, Ali akitoka mbele kukutana na Walid. Baada ya muda kidogo wa kucheza na panga, Walid aliangushwa na upanga wa adui yake mwislamu. Kisha Hamza akamshambulia Utba na akamkata na kumuangusha chini. Ubaida ibn Harith, shujaa wa tatu wa Kiislam, alipata jeraha baya sana kutoka kwa Shaiba. Ali na Hamza haraka sana wakamuua Shaiba, wakimbeba Utba kwenda kufia kwenye safu za Waislamu.

(The Great Arab Conquests, 1963)

Badr ilikuwa ndiyo pambano la kwanza, katika uwanja wa vita, kati ya Uislamu na Wapagani. Ilianzishwa upande wa Uislamu, na Ali ibn Abi Talib, simba kijana, na ushindi wake ulikuwa ni ishara ya mafanikio ya Uislamu. Vita nyingine zote za Kiislam zilifuata mkondo huohuo; Ali alikuwa ndiye mshindi katika kila moja yao.

Maquraishi walituma mashujaa watatu dhidi ya Waislamu, na wote watatu waliuawa. Abu Jahl, kwa hiyo, hakuwa na shauku ya kuchukua majaribio zaidi na Ali na Hamza, na akaa-muru majeshi yake kusonga mbele. Watu wa Makka waliwashambulia Waislamu lakini hawakuweza kuvunja mipangilio yao. Walishambulia tena na tena lakini safu za Waislamu zilibakia imara chini ya ukamanda wa Ali na Hamza.

Watu wa Makka walikuwa wakijikusanya kwa ajili ya mashambulizi mapya wakati Muhammad alipowaashiria Waislamu kusonga mbele. Ali na Hamza waliongoza mapam-bano ya kujibu shambulizi, na wote walileta mauji na fadhaa kwenye kundi kubwa la safu za adui. Wengi wa viongozi na maafisa wa Makka waliuawa, miongoni mwao Abu Jahl mwenyewe. Baada ya kifo chake, waabudu-masanamu hao hawakuweza kujikusanya, na walianza kurudi nyuma. Waislamu walishikilia fursa yao, na kule kurudi nyuma kwa watu wa Makka mara kukawa ni msambaratiko. Uislamu umepata ushindi wake wa kwanza na wa muhimu sana!

S. Margoliouth:

"Kwa hakika inaonekana kwamba kushinda kwa pambano hili muhimu kulikuwa katika kustahili kukubwa kwa ushujaa wa Ali na Hamza. Mtukufu Mtume (s.a.w.) anasemekana kutoa sifa maalum kwa ujasiri wa Simak ibn Kharashah; Sahl ibn Hunaif; al-Harith ibn al-Simmah; na Kais ibn al-Rabi; wote wakiwa ni watu wa Madina.

(Mohammed and the Rise of Islam, London, 1931) 133

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Tor Andre:

"Kufikia mchana vita vilikuwa vimekwisha. Watu arobaini na tisa wa adui walikuwa wameanguka na Ali aliuwa watu ishirini na wawili, ama peke yake au pamoja na msaada wa wengine. Idadi kama hiyo hiyo walitekwa. Waumini walipoteza watu kumi na wanne katika uwanja wa mapambano."

(Mohammad, the Man and his Faith, 1960)

Kama ilivyoonyeshwa hapo juu, Badr ndio vita muhimu sana katika historia nzima ya Uislamu, na moja kati ya zile maarufu katika historia ya ulimwengu. Ushindi ulihakikisha kuwepo kwa Uislamu, na uhai wa dhahiri wa jumuiya ya Waislamu ya Madina ambayo mpaka sasa imetokea, kwa vyovyote, kuwa ya hatari.

A.Nicholson:

"Lakini umuhimu wa mafanikio ya Muhammad (katika vita vya Badr) hayawezi kupimwa kwa uharibifu wa vitu aliousababisha (juu ya wapagani wa Makka). Tukitazama mambo ya maana sana yaliyohusika, ni lazima tukubali kwamba Badr, kama masafa marefu, ni moja ya vita vikubwa na vya kukumbukwa sana katika historia yote.

(A Literary History of the Arabs, 1969)

Ali ibn Abi Talib na vita vya Badr

Msanifu wa Ushindi wa Waislamu huko Badr, bila ya shaka yoyote, alikuwa ni Ali ibn Abi Talib. M. Shibili, yule mwanahistoria wa Kihindi aliyeandika vitabu vya kutegemewa vya wasifu kwa Ki-Urdu vya Umar bin Khattab na vya Mtume wa Uislamu, anasema katika kitabu chake Life of the Apostle, kwamba shujaa wa vita vya Badr ni Ali ibn Abi Talib.

F.E.Peters:

"Badr ilikuwa ni ushindi kwa Waislamu, kwa jumla kama ilivyokuwa haikutegeme-wa; Waislamu walipoteza watu kumi na wanne na Maquraishi watu 50 hadi 70, pamoja na kiongozi wao, Abu Jahl. Ulikuwa ni ushindi mkubwa sana wa kisaikolojia na kulikuwa na wingi wa ngawira kwa ajili ya wale Muhajir waliodhikika kiuchumi. Hili halikuwa shambulio la hivihivi tu, hata hivyo. Lilipambanisha Waislamu dhidi ya wasio-Waislamu katika Vita Tukufu (Jihad), na akina baba dhidi ya watoto wao katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Majeruhi wa Maquraishi walikuwa wengi mno, na kwa vile wengi wao walitokana miongoni mwa machifu wao, uongozi hapo Makka ulidhoofishwa kabisa daima.

(Allah s Commonwealth, 1973) 134

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Uongozi wa washirikana wa Makka kwa hakika ulidhoofishwa daima hapo Badr. Shujaa aliyehusika na hili alikuwa ni Ali. Yeye peke yake aliwauwa watu wa Makka 22, na kumi na wawili wao wakiwa ni wale watu maarufu wa ukoo wa Bani Umayya. Jeshi la Waislamu lililobakia liliuwa wapagani wengine 27.

Miongoni mwa ngawira za vita vya Badr ulikuwepo upanga ambao ulikuwa uje kuwa ndio upanga maarufu kabisa katika historia nzima ya Uislamu. Jina lake lilikuwa ni Dhul-Fiqar.

Washington Irving:

"Miongoni mwa ngawira za vita vya Badr ulikuwa ni upanga maarufu wenye hali ya kupendeza uitwao Dhul-Fiqar. Muhammad daima baadae aliushika akiwa vitani, na mkwe wake, Ali aliurithi baada ya kifo chake."

(The Life of Muhammad)

Abdullah Yusuf Ali, yule mtarjuma na mfasiri wa Qur'an Tukufu, anasema kwamba vile vita vya Badr vinaitwa Furqan katika elimu ya Kiislam, kwa sababu ilikuwa jaribio la kwanza la nguvu kwa njia ya vita, katika Uislamu, kati ya nguvu za wema na uovu. Furqan ina maana ya kibainishi kati ya ukweli na uongo; uamuzi kati ya nguvu za Imani na Ukafiri. Vita vya Badr vinaitwa kwa jina hili.

Wafungwa wa kivita

Waislamu walikamata wafungwa wa kivita hamsini. Waliletwa mbele ya Mtume (s.a.w.) ambaye alikuwa aamue wafanyiwe nini. Alishauriana na maswahaba zake katika jambo hilo. Umar allimshauri awauwe wote, lakini Abu Bakr akamshauri kuwaachia huru kwa fidia. Mtume (s.a.w.) akaukubali ushauri wa Abu Bakr.

Kwa vile hapakuwa na nyumba ya kizuizi hapo Madina, Mtume (s.a.w.) aliwagawanya wale wafungwa miongoni mwa familia za Waislamu. Familia hizi ziliwatendea wafungwa wao kama vile walikuwa wageni. Baadhi yao walilisha chakula chao wenyewe kwa "wageni" wao na wenyewe wakakaa na njaa. Kwa kweli waliwafedhehesha wafungwa wao kwa mashaka yao juu ya ustawi wao.

Wale wafungwa matajiri waliachiliwa kwa fidia. Wale wafungwa ambao hawakuweza kulipa fidia lakini waliweza kusoma na kuandika, walitakiwa kuzifundisha sanaa hizo kwa watoto wa Kiislam, na walipofanya hivyo, pia na wao waliachiliwa. Wale wafungwa waliokuwa mafukara sana, waliachiliwa bila ya fidia yoyote.

Matokeo ya vita vya Badr

Ushindi wa Badr uliwapa Waislamu heshima kubwa sana. Lile tishio kwa usalama wa Madina liligeuzwa, na Muhammad Mustafa aliweza sasa kuweka misingi ya Ufalme wa kwanza na wa mwisho wa Mbingnii hapa Duniani.

135

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

S. Margoliouth:

'Hakuna tukio katika historia ya Uislamu lililokuwa na umuhimu zaidi kuliko vita hii (ya Badr); Qur'an inaviita sawa kabisa - Siku ya Ukombozi, siku ambayo kabla yake Waislamu walikuwa wanyonge, baada yake wakawa wenye nguvu. Utajiri, umaaru-fu, heshima, mamlaka, vyote vilipatikana au kwa hali yoyote vililetwa karibu na hiyo - Siku ya Ukombozi."

(Mohammed and the Rise of Islam, London, 1931)

Tokeo moja la kusikitikia la vita vya Badr, hata hivyo, lilikuwa kwamba ushindi wa Uislamu uliwasha mioto mipya na mikali zaidi ya chuki na uhasama katika vifua vya Banu Umayya dhidi ya Muhammad Mustafa na Ali ibn Abi Talib. Chuki zao na wivu juu ya Bani Hashim ilidumu vizazi vingi. Lakini baada ya vita vya Badr, uhasama wao ulielekezwa kwa Ali na kwa watoto wa Muhammad Mustafa.

Kama kwa Waislamu, Ali alikuwa ndio alama ya ushindi wa Uislamu, kwa Banu Umayya, alikuwa ni alama ya kuangamia kwa ushirikina wao na heshima zao. Kwa hiyo, wao, vizazi vyao vilivyofuata, na marafiki zao na wanao waunga mkono, kamwe hawakumsamehe Ali kwa jukumu alilotekeleza hapo nyuma, wakati na baada ya vita vya Badr. Chuki yao inaeleweka. Alikuwa ni Ali, na ni Ali peke yake ambaye alishambulia, sio tu pale Badr, bali katika kila pambano, kwa mashambulizi makubwa, ile nguvu iliyolingana sawa na kumakinika ya upagani, na akaiangamiza.

136

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ndoa ya Fatima Zahra na Ali ibn Abi Talib

Allah swt. aliwapa ushindi Waislamu katika vita vya badr katika mwaka wa 2 wa Hijiria. Miezi miwili baada ya vita hivyo, Fatima Zahra, binti yake Muhammad Mustafa, na Ali, mwana wa Abi Talib walifunga ndoa.

Fatima Zahra alikuwa na miaka mitano tu wakati mama yake - Khadija (R.a.), alipofariki, na kuanzia hapo na kuendelea, baba yake, Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) alichukua wajibu wa kazi za mama pia kwa ajili yake. Kifo cha mama yake kilileta pengo katika maisha yake lakini baba yake alilijaza kwa upendo na huruma.

Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliweka uangalifu wa hali ya juu kwenye elimu na malezi ya binti yake. Kama alikuwa ndiye mfano bora kwa watu wote, binti yake alikuwa awe mfano bora kwa wanawake wote, na alikuwa hivyo. Alimfanya yeye kuwa mfano bora wa uwanauke katika Uislamu. Alikuwa ni mfano halisi wa ibada na utii kwa Muumba, na alikuwa ni mfano halisi wa usafi wa ki-ungu na utakatifu. Katika tabia na hulka, alikuwa na mfanano unaovutia sana kwa baba yake. Fatima, binti huyu, alikuwa ni picha ya Muhammad, baba yake.

Kwa kufanya utii na ibada kwa Allah (s.w.t.) Fatima Zahra alipanda kufikia cheo kikubwa mbele ya Allah (s.w.t.) kama ilivyoshuhudiwa na Qur'an Tukufu. Allah (s.w.t.) alimpa utukufu mkubwa sana juu yake, na Mtume wa Uislamu (s.a.w.), kwa upande wake, alim-wonyesha kiwango cha heshima ya juu sana, moja ambayo hakuionyesha kwa mwanaume au mwanamke mwingine yeyote yule katika wakati wowote wa maisha yake.

Wakati Fatima alipokuwa, maswahaba wawili wazee - wa kwanza na kisha baadae mwingine - walimuomba baba yake wamchumbie. Lakini aligeukia pembeni kwa kuchukia, na akasema:

"Hili suala la ndoa ya Fatima, binti yangu, liko mikononi mwa Allah (s.w.t.) Mwenyewe, na Yeye pekee ndiye atamchagulia yeye mchumba".

Allah (s.w.t.) alifanya uchaguzi Wake kama ipasavyo. Alimchagua mja Wake, Ali ibn Abi Talib, kuwa ndiye mchumba wa binti ya mja Wake mpendwa mno, Muhammad Mustafa. Alipenda kuwaona Fatima binti Muhammad na Ali ibn Abi Talib wakioana.

Miezi miwili baada ya vita vya Badr, yaani, katika mwezi wa Dhilqa'da (mwezi wa 11) wa mwaka wa 2 H.A., Ali alikwenda kwa Muhammad Mustafa, na akasema: "Ewe Mtume wa Allah, umenilea mimi kama mwanao mwenyewe. Ulinijaza na zawadi zako, ukarimu wako na wema wako. Ninawiwa nawe kila kitu katika maisha yangu. Sasa ninaomba wema mmoja zaidi kutoka kwako."

137

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mtume (s.a.w.) alielewa nini Ali alichokuwa akijaribu kukisema. Uso wake ulichangamka kwa tabasamu pana, na alimtaka Ali asubiri kwa muda kidogo mpaka apate majibu ya binti yake.

Aliingia ndani, akamwambia Fatima kwamba Ali alikuwa anaomba uchumba kwake, na akamuuliza ni lipi jibu lake. Akabakia kimya. Yeye Muhammad akatafsiri kimya chake kama idhini yake, akarudi kwa Ali, akamjulisha kwamba ombi lake limekubaliwa, na akamwambia afanye matayarisho ya harusi.

Katika siku ya mwisho ya Dhilqa'ada, Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) ali-wakaribisha Muhajirina na Ansari, kuhudhuri karamu, katika tukio la kuolewa kwa binti yake. Alikuwa ndiye mwenyeji wao. Wakati wageni wote walipofika, na wakawa wamek-wishakaa, alichukua, kwa mara nyingine tena, idhini ya kisheria ya binti yake kwa ajili ya ndoa na Ali ibn Abi Talib.

Muhammad Mustafa alimtukuza Allah (s.w.t.) na akamshukuru Yeye kwa ajili ya rehema Zake zote. Yeye kisha akasoma hotuba ya ndoa; akawatangaza Ali na Fatima kama mume na mke, na akaomba baraka za Allah (s.w.t.) ziwe juu yao wote. Wageni wote wakam-pongeza Mtume (s.a.w.) kwa tukio hili lenye baraka tele. Baada ya sherehe hii, wageni wale walikula karamu ya nyama ya kondoo, mkate, maji ya tende na maziwa.

Siku chache baadae, yaani, katika Dhil-Hajj (mwezi wa 12 wa kalenda ya Kiislam), Fatima Zahra ilibidi aiage nyumba yake ya kuzaliwa ili aweze kwenda kwenye nyumba ya mumewe. Baba yake alimsaidia katika kumpakia kwenye ngamia-jike wake (Muhammad). Madina ilivuma kwa sauti za Allah-u-Akbar. Salman Muajemi alishikilia hatamu za ngamia-jike huyo, na akatembea mbele yake, huku akisoma Qur'an Tukufu. Mtume wa Allah (s.a.w.) alitembea upande mmoja wa ngamia-jike huyo, na Hamza, Simba wa Mungu, upande mwingine.

Vijana wote wapanda farasi wa Bani Hashim walipanda kama wasindikizaji wa Bibi-harusi huyo, pamoja na panga zinazomeremeta zikiwa zimenyanyuliwa juu kabisa. Nyuma yao walikuwa ni wanawake Muhajira na Ansari, na nyuma yao hawa wakaja Muhajirina na Ansari wenyewe. Walikuwa wakisoma qaswida kutoka kwenye Qur'an Tukufu kumtukuza Allah (s.w.t.) Usomaji huo wa qaswida uliwekwa vituo vya mara kwa mara na mrindimo wa sauti za Allah -u-Akbar.

Maandamano haya ya kitukufu yaliuzunguuka Msikiti Mkubwa wa Madina, na kisha yakaishia kwenye ukomo wake - nyumba ya Bwana-harusi - Ali ibn Abi Talib. Muhammad Mustafa akamsaidia binti yake kushuka toka kwenye ngamia-jike. Akamshika mkono wake, na kwa ishara akauweka kwenye mkono wa mumewe, na kisha, akisimama kwenye kizingiti cha nyumba hiyo, akasoma du'a ifuatayo:

138

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

"Ewe Allah (s.w.t.)! Ninawaweka Ali na Fatima, waja wako wanyenyekevu, kwenye ulinzi wako. Uwe Wewe ndio Mlinzi wao. Wabariki hawa. Kuwa radhi nao, na uwape neema zako zisizo na mipaka, huruma, na fadhila Zako bora juu yao. Uifanye ndoa yao kuwa yenye matunda, na uwafanye wote imara katika upendo Wako, na ibada Zako."

Ilikuwa kwa kweli ni siku ya furaha katika maisha ya Muhammad Mustafa. Lakini ni vipi ambavyo angependa kwamba mke we mpendwa, Khadija, angekuwa pamoja naye ili wote kwa pamoja wakashuhudia ndoa ya binti yao.

Siku chache baadae, Mtume wa Allah (s.a.w.) alikwenda kwa binti yake, na akamuuliza kama alimuonaje mume wake. Binti akasema kwamba alimuona ni mwenza bora katika kufanya ibada na utii kwa Allah (s.w.t.) Baadae, alimuuliza Ali alimuona vipi mke wake, na akasema alimuona ni mwenza bora katika kumuabudu Muumba. Nyakati nzuri kabisa za maisha kwa wote mume na mke zilikuwa zile walipokuwa wamekwenda Mbele ya Mola wao, na wakazama katika kumuabudu Yeye.

Kati ya Ali na Fatima Zahrah, kulikuwa na utambulisho kamili wa manufaa. Wote walilele-wa na kufundishwa na Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) na Khadija-tul-Kubra. Wote kwa hiyo, walikuwa na ukamilifu wa wazazi wao. Wote waliweka ibada kwa Allah (s.w.t.) mbele ya kitu kingine chochote kile. Hapakuwepo na nafasi kabisa ya kutoelewana kati yao. Mawazo yao, maneno na matendo yao, yote "yalizoeshwa" na Qur'an Tukufu. Ndoa yao kwa hiyo, ilikuwa timilifu tu na ya furaha tu kama ile ndoa ya Muhammad na Khadija ilivyokuwa.

Kama ilivyoelezwa kabla, furaha kuu ya Fatima ilikuwa ni kuwa na subira juu ya Allah (s.w.t.) Alitumia muda wake mwingi katika Swala. Furaha yake kuu ya pili ilikuwa ni kutekeleza wajibu wake kwa familia yake. Allah (s.w.t.) aliridhia kumpa watoto wanne -kwanza wavulana wawili na kisha wasichana wawili. Alisaga nafaka katika kinu alichope-wa na baba yake kama sehemu ya mahari yake, na akawaokea mikate. Kusaga nafaka siku hadi siku kulisababisha malengelenge kutoka kwenye mikono yake lakini hakulalamika kamwe kwa mume wake au kwa baba yake juu ya malengelenge hayo, na alifanya kazi zake za nyumbani kwa furaha kabisa.

Hizi kazi za nyumbani zingeweza kuwa kama za kushurutisha sana kwa Fatima Zaharah lakini alipata furaha na nguvu katika kumkumbuka Allah (s.w.t.) Kitabu cha Allah (s.w.t.) kilikuwa ndio rafiki yake wa kudumu. Alisahau uchovu wa kazi vile alivyokuwa akisoma vifungu kutoka kwenye kitabu hicho. Na alipowalaza watoto wake katika kitanda chao, alisoma tena baadhi ya vifungu kutoka kwenye kitabu hicho hicho kama "nyimbo za kibembelezo" kwa ajili yao. Walikua huku wakiisikia Qur'an Tukufu toka utotoni mwao. Aliligandisha Neno la Allah (s.w.t.) juu ya mioyo yao michanga. Kwa kupitia

139

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

"mfyonzo" kama huu, Qur'an na watoto wa Fatima Zahrah vikawa havitenganishiki kwa wakati wote.

Katika mwaka huo huo, yaani, mwaka wa 2 H.A., Sala za hadhara kwenye sikukuu mbili kwa ajili ya Waislamu, yaani, Idd-el-Fitr na Idd-el-Udh-ha., zilifanywa kuwa sunnah (zenye kustahili) juu yao.

140

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Vita vya Uhud

Hivi vita vya uhud vilikuwa ni kisasi dhidi ya Waislamu kufuatia vile vita vya Badr. Baadhi ya watu mashuhuri wa Quraishi kama vile Abu Jahl, Utbah, Shaiba, Walild, Umayya bin Khalaf, na Hanzala bin Abu Sufyan, waliuawa kwenye vita vya Badr. Baada ya kifo cha Abu Jahl, uongozi wa watu wa Makka ulipitia kwa mwenza wake, Abu Sufyan, ambaye alikuwa mkuu wa ukoo wa Banu Umayya. Kulikuwa na huzuni nzito hapo Makka kwa kupotea kwa wakuu wengi lakini Abu Sufyan alizikataza zile familia zilizofiwa kulia na kuomboleza kuondokewa kwao. Machozi, alijua, yangeweza kusafisha uovu kutoka nyoy-oni. Lakini muda na machozi, alidai, havitaachiliwa kuponya majeraha yaliyoupata utawala wa kikabila wa Makka huko Badr. Yeye mwenyewe alikula kiapo kwamba atajie-pusha na kila anasa mpaka awe amewatendea Waislamu kama walivyomtendea. Yeye na wakuu wengine wa Maquraishi waliutumia mwaka mzima wa shughuli za msisimko ambamo waliandaa na kufundisha jeshi jipya.

Mwaka mmoja baada ya vita vya Badr, lile jeshi jipya la waabudu-masanamu wa Makka lilikuwa tayari kusimama uwanjani dhidi ya Waislamu. Mnamo Machi 625 Abu Sufyan aliondoka Makka akiongoza wapiganaji elfu tatu waliozoeshwa. Wengi wao walikuwa askari wa miguu lakini walisaidiwa na kikosi chenye nguvu cha wapanda farasi. Pia wakiandamana na jeshi hilo, walikuwa ni kundi la wanawake wenye kupenda vita. Kazi yao ilikuwa ni kuendeleza "vita vya kimawazo" dhidi ya Waislamu kwa kusoma mashairi na kuimba nyimbo za mapenzi ili kuhimiza ujasiri na shauku-ya-kupigana ya askari hao. Walijua kwamba hakuna kilichohofisha kwa Waarabu kiasi hicho kama dhihaka za wanawake kwa waoga, na vile vile walijua kwamba hakuna chenye kufaa zaidi kuwageuza kuwa wapiganaji wasiojali kabisa, kama ahadi ya mapenzi ya kimwili. Majikedume haya yalikuwa ni pamoja na wake za Abu Sufyan na Amr bin Al-As, na dada zake Khalid bin Walid.

D.S. Margoliouth:

"Abu Sufyan anaonekana kufanya juhudi zake zote, na, kama badala ya muziki wa kijeshi, alisababisha ama kuruhusu jeshi hilo kufuatiwa na kundi la wanawake, ambao, kwa kutishia na kuahidi, walikuwa waweke ujasiri wa vikosi hivyo kwenye kiwango sahihi; kwani hakuna chochote alichohofia aliyekimbia kutoka kwenye uwanja wa mapambano, zaidi kuliko kushutumiwa na wanawake wa kwao. Wanawake wa Kikuraishi walifanya kazi ya kipekee yenye uhakika. Mke wa Abu Sufyan alitoa ushauri kwamba mwili wa mama yake Muhammad ufukulliwe na kuwekwa kama mateka; lakini Maquraishi waliukataa ushauri huu (ambao kwamba uwezekano wake kwa kweli ulikuwa na mashaka) kwa kuhofia visasi."

(Muhammad and the Rise of Islam, 1931) 141

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kana kwamba vile vidokezo vya mapenzi vilivyotolewa na wale wanawake wa Kikuraishi havikutosheleza, Abu Sufyan aliweka kampeni yake kwenye "utakatifu wa kidini" vilevile. Kuondoa mashaka kabisa katika akili ya mtu yoyote kwamba alikuwa kwenye vita tukufu dhidi ya Waislamu, alimuweka Hubal, lile sanamu ambalo ukoo wa Banu Umayya walili-abudu kama mungu wao mkuu, juu ya ngamia, na akalibeba kwenda nalo ndani ya vita. Kazi ha Hubal ilikuwa ni kuzidisha hamasa ya waabudu-masanamu kwa kuwepo kwake kwenye uwanja wa vita.

Mapenzi ya kijinsia na dini vilikuwa ndio vitu viwili vipya vilivyoandaliwa na Maquraishi katika vita vyao dhidi ya Muhammad na Uislamu.

Betty Kelen:

"Katika kiti chenye mwamvuli (mgongoni mwa tembo) alipanda Hubal, kwenye mapumziko kutoka kwenye Al-Kaaba. Abu Sufyan alikuwa ameshikilia kabisa kwamba mbali kabisa na mawazo ya kisasi na njia za misafara, alikuwa ameingia kwenye vita vya jihad."

(Muhammad, the Messenger of God, 1975)

Muhammad Mustafa, Mtume wa Uislamu, pia alizisikia habari za uvamizi wa Madina unaokaribia kutoka kwa watu wa Makka, na yeye pia aliwaamuru wafuasi wake kujiandaa kwa ulinzi. Waislamu mia saba walikuwa tayari kumfuata kwenye vita.

Mtume (s.a.w.) aliliweka jeshi lake kwa mlima wa Uhud kuwa nyuma yake hivyo kwamba lilisimama kuelekea Madina. Wakati jeshi la watu wa Makka lilipokuja, lilichukua nafasi yake mbele ya Waislamu hivyo kwamba lilikuwa limesimama kati yao na Madina ambayo ilikuwa nyuma yao.

Sir William Muir:

"Abu Sufyan, kama kiongozi wa upagani, aliliteta jeshi la Makka; na wakielekea Uhud, akaliongoza mbele ya Muhammad. Bendera ilikuwa imeshikwa na Talha mtoto wa Abdal Uzza. Vikosi vya upande wa kulia viliongozwa na Khalid; na vya kushoto na Ikrima mtoto Abu Jahl. Amr bin Al-As alikuwa juu ya farasi wa Kiquraishi."

(The Life of Muhammad, 1877)

Sir John Glubb:

"Waislamu walisonga mbele na watu 700 dhidi ya wapiganaji 3000 kutoka Makka. Zaidi ya hayo, wakati Waislamu waliweza kukusanya nguvu ya watu mia moja tu wenye deraya, na bila ya farasi, Maquraishi na washirika wao walikuwa na watu 700 wenye deraya na wapanda farasi 200.

142

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Wakitaka kuziba nyuma yao kutokana na idadi yao ndogo, Waislamu walijipanga chini ya mlima Uhud. Upande wao wa kulia na nyuma vilifunikwa na milima, lakini upande wao wa kushoto ulikuwa kwenye uwanja wa wazi na kwa hiyo uliachwa kwenye shambulizi la askari wa farasi wa adui. Kujihami dhidi ya hili, Muhammad aliweka wapiga mishale hamsini kwenye upande huu, pamoja na amri ya kutoiacha nafasi yao kwa hali yoyote ile, ambapo kutokea hapo wanaweza kuulinda upande wa kushoto wa Waislamu kutokana na farasi wa Maquraishi.

Watu wa Makka waliweka safu yao kuwaelekea Waislamu kwa namna ambayo Waislamu, migongo yao ikielekea Uhud, walikuwa wakitazama kuelekea Madina, ambapo safu ya Maquraishi iliwakabili na Madina ikiwa nyuma yao, hapo wakiwa kati ya Waislamu na mji huo.

Maquraishi walikuwa wamekuja na wanawake wachache, wakiwa wamepanda kati-ka vitanda vya kubebwa na ngamia. Hawa sasa, wakati safu mbili hizo zilipokuwa zinasogeleana, waliendelea kuamsha shauku ya watu wa Makka, wakipiga vijingoma, wakisoma mashairi ya kivita na kushusha nywele zao ndefu."

(The Great Arab Conquests)

Vita vya Uhud vilianza kama vile tu vita vya Badr vilivyoanza, kwa mpiganaji wa Makka kuchomoza kutoka kwenye safu zao na kuwapa changamoto Waislamu kwa mapambano ya mtu mmoja mmoja.

Sir William Muir:

"Akipepea bendera ya Kikuraishi, Talha, yule mshika-bendera wa jeshi la Makka, alisonga mbele, na kuwapa changamoto maadui kwenye pambano la mtu mmoja mmoja. Ali alitoka mbele, na, akimvamia, kwa pigo moja la upanga wake alimuan-gusha chini. Muhammad, ambaye aliliangalia kwa makini pambano hilo la haraka, aliguta kwa mshangao, kwa sauti kubwa: "Allah-u-Akbar!" na mguto huo, ukirudiwa, ulipaa kwa sauti kubwa mno kutoka kwenye jeshi zima la Waislamu."

(The Life of Muhammad, London, 1877)

Muhammad Husein Haykal:

"Talha ibn Abu Talha, mshika bendera wa Makka, alichomoka mbele akiwataka Waislamu kupambana naye. Ali ibn Abu Talib alitoka mbele kupigana naye. Pambano hilo lilikwisha mara wakati Ali alipompiga adui yake dhoruba moja kali sana. Kwa furaha kuu, Mtume (s.a.w.) na Waislamu walipiga ukelele mkubwa, "Allah-u-Akbar."

(The Life of Muhammad, 1935, Cairo)

143

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

R.V.C.Bodley:

"Watu wa Makka, wakisaidiwa kwa ukarimu sana na wanawake ambao walileta vigo-ma vyao, walirusha matusi kwa Waislamu. Haya yalipokelewa na Hind, mke wa Abu Sufyan, ambaye aliongoza vipokeo vya shangwe alipokuwa akicheza kulizunguka lile sanamu lililokuwa limekaa juu ya ngamia.

Talha, yule mshika-bendera wa wapagani wa Kiquraishi, alikuwa ndiye mtoa chang-amoto wa kwanza wa watu wa Makka. Vile alipotoka kwenye safu za Abu Sufyan, Ali alitoka kwenye safu za Muhammad. Watu wawili hawa wakakutana katikati ya 'ardhi isiyo na mwenyewe.' Bila ya maneno au madoido ya kutangulia, pambano likaanza. Talha kamwe hakupata nafasi. Jambia la Ali liliwaka katika lile jua la asubuhi na kich-wa cha mshika-bendera huyo kiliruka kutoka kwenye mabega yake na kikabingirika kwenye mchanga.

'Allah-u-Akbar! aliguta Muhammad. 'Allah-u-Akbar!' 'Allah-u-Akbar!' ilirudiwa kutoka kwa Waislamu waliokuwa wakiangalia kwa shauku."

(The Messenger, the Life of Muhammad, New York, 1946)

Sir John Glubb:

"Zile safu mbili zilisogea kutoka kila upande. Talha ibn Abdul Uzza, wa Abdul Dar, akiungua kwa chuki juu ya dhihaka za Abu Sufyan, na akiwa amebeba bendera ya Maquraishi, alitoka nje mbele ya safu na akatoa changamoto kwa mwislamu yoyote kwenye pambano la mtu mmoja mmoja. Ali alichepuka mbele na akamuua kwa pigo moja la upanga wake, huku bendera ya Maquraishi ikidondoka chini. Kutoka kwenye safu za Waislamu ikatoka sauti kubwa, "Allah-u-Akbar, Mungu ni Mkuu."

(The Life and Times of Muhammad)

Hili ni moja ya maonyesho ya kuvutia katika historia ya Uislamu. Muhammad, Mjumbe wa Allah (s.w.t.) alikuwa akimwangalia binamu yake, Ali, akipambana, na alisisimuliwa na ushindi wake wa haraka. Wakati lile pigo zito la upanga wa Ali lilipomuua jenerali wa wapagani, Muhammad alipiga ukelele Allah-u-Akbar, na ukelele huo wa kivita ulifuatish-wa na jeshi zima la Uislamu.

Pigo la Ali lisilozuilika limesababisha bendera ya watu wa Makka, ile nembo ya uabudu masanamu na ushirikina, kuanguka chini kwenye vumbi. Alishinda raundi ya kwanza kwa Uislamu, na alikuwa ametoa pigo la kifo kwenye hamasa ya Maquraishi.

144

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Wakati Ali aliporudi kwenye safu zake, ndugu yake Talha, Uthman ibn Abu Talha, alifanya jaribio la kuipata tena ile bendera ya Makka. Lakini Hamza akatoka kwenye safu za Waislamu, na akamuua.

Muhammad Husein Haykal:

"Wakati Ali alipomuua yule mshika-bendera wa Makka, Talha ibn Abu Talha, ilinyanyuliwa mara moja tena na Uthman ibn Abu Talha. Na pale Uthman alipoanguka mikononi mwa Hamza, ilinyanyuliwa tena na Abu Sa'd ibn Abu Talha. Mara alipoinyanyua ile bendera ya Makka aliwakemea Waislamu: "Mnajidai kwamba mashahidi wenu wako peponi na wetu wako motoni? Wallahi, mnadanganya! Kama mmoja wenu kwa ukweli anaamini habari kama hiyo, naaje hapa mbele apigane na mimi." Changamoto yake ilimvuta Ali ambaye alimuua papo hapo. Hawa Banu Abd al Dar waliendelea kuishika bendera ya Makka mpaka wakapoteza watu tisa."

(The Life of Muhammad)

Ali, simba kijana, peke yake aliuwa washika bendera nane wa waabudu-masanamu wa Makka. Ibn Athir, yule mwanahistoria wa Kiarabu, anaandika katika Tarikh Kamil: "Mtu aliyewaua washika-bendera wa wapagani alikuwa ni Ali." Baada ya kifo cha mshika-bendera wake wa tisa, Abu Sufyan aliliamuru jeshi lake kusonga na kushambulia mipango ya Waislamu. Wakati Mtume (s.a.w.) alipoliona jeshi likisogea, yeye pia aliwatahadharisha Waislamu. Alishika upanga kwenye mkono wake, na akautoa kwa yeyote ambaye angeweza kuuletea heshima. Baadhi ya waliokuwa na matumaini walitokeza mbele yake kuuchukua lakini akawanyima.

Muhammad Ibn Ishaq :

"Mtume (s.a.w.) alivaa makoti mawili ya deraya katika siku ya vita vya Uhud, na alichukua upanga na akaupunga akisema: "Ni nani atauchukua upanga huu na haki yake?" (yaani, kuutumia kama ipasavyo na unavyostahili kutumiwa). Baadhi ya watu walisimama ili kuuchukua lakini aliuzuilia kuwapa mpaka Abu Dujana Simak bin Kharasha, ndugu yake B. Saida, aliposimama na kuuchukua.

Umar alisimama kuuchukua, akisema: "Nitauchukua pamoja na haki yake," lakini Mtume (s.a.w.) aligeukia pembeni na alikokuwa na akaupunga mara ya pili akitumia maneno yale yale. Kisha Zubayr bin al-Awwam akasimama naye pia akakataliwa, na wawili hawa wakawa wamefedheheka sana."

(The Life of the Messenger of God)

145

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mtume (s.a.w.) alimpa upanga huo Abu Dujana, mmoja wa Ansari. Aliuchukua na akautu-mia kama ulivyostahili kutumiwa. Alithibitisha ile imani bwana wake aliyokuwa amemuwekea. Wale wanawake wa Makka walikuwa wamekaa kitako juu ya ngamia wao na walikuwa wakiangalia lile tendo la haraka. Jeshi lao liliposonga mbele kushambulia Waislamu, na wao pia waliingia kazini. Walianza kuwachochea wapiganaji wao kuwaua Waislamu. Waliimba nyimbo ambazo zilikuwa zimejaa ukaribisho na dharau - ukaribisho kwa mashujaa wao na dharau kwa wale waoga. Kwa muziki wao na ushairi wao wenye ushawishi wa hali ya juu, waliwachochea watoto hao wa jangwani wenye pupa kwenye ghadhabu za kupigana.

Betty Kelen:

"Vikiwa vimejengwa juu kabisa ya ngamia wengi vilikuwa ni vibanda vidogo, au machela, ambamo walipanda kikosi cha wanawake waliofunzwa vyema na Hind kuimba tenzi za kivita ambazo zitawaweka wanaume wao katika msisimko au ghadhabu na kupinga woga.

Vita viliungwa. Hind na wanawake wenzie walisonga mbele pamoja na majeshi, wak-itawanyika uwanjani kwa karibu sana kiasi walivyoweza kuthubutu kuwafikia wale wanaume wanaopigana, huku wakipiga vigoma vyao kwa mpigo mkali na wakike-mea:

"Mabinti wa Nyota ya Asubuhi inayong'ara, Wakiwaangalieni kutoka kwenye vitanda vyenye hariri ni sisi, Wacharazeni! Katika mikono yetu tutawakumbatia; Kimbieni, na kamwe tena hatutawashikeni."

(Muhammad, the Messenger of God)

Muhammad Husein Haykal:

"Hapo kabla wanawake wa Kiislam (huko Arabuni) walikuwa wakijionyesha sio tu kwa waume zao bali kwa wanaume wengine wowote waliowataka. Walikuwa waki-toka nje kwenye sehemu za wazi mmoja mmoja au katika vikundi na kukutana na wanaume na vijana bila ya kizuizi au hisia ya aibu. Waliangaliana kwa hisia kali na vidhihirisho vya mapenzi na tamaa. Hili lilifanyika kwa ukweli wa wazi na ukosefu wa aibu kwamba Hindi, mke wa Abu Sufyan, hakuwa na haya yoyote juu ya kuimba katika wakati wa hadhara na wa hatari kama Siku ya Uhud.

"Songeni mbele nasi tutawapiga pambaja nyie! Songeni mbele na sisi tutatandaza mabusati kwa ajili yenu! Geuzeni migongo yenu nasi tutawaepuka ninyi! Geuzeni migongo yenu nasi kamwe hatutawajieni ninyi."

146

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Miongoni mwa idadi ya makabila, uzinzi haukuonekana kamwe kama ni kosa kubwa. Kucheza kimapenzi na kufanya urafiki na mwanamke vilikuwa ni matendo ya kawai-da. Mbali na cheo maarufu cha Abu Sufyan na jamii yake, wana tarikh wanasimulia, kuhusu mke wake, Hadith nyingi mno za mapenzi na hisia kali na wanaume wengine bila ya kuweka doa lolote juu ya heshima yake".

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Watu wa Makka walijiandaa vema na walikuwa wengi zaidi kuliko Waislamu. Zaidi ya hayo, kuwepo katika uwanja wa vita, kwa mungu wao, Hubal, na wanawake wao, ulikuwa ni uhakikisho kwamba hamasa yao haitalegea, hususan, baada ya hawa wanawake kuwa wameingiza kwenye mapambano, kisaidizi kipya na cha kuhatarisha cha kishawishi.

Lakini licha ya manufaa haya ya dhahiri na yasiyo dhahiri, hawa watu wa Makka walikuwa wakifanya maendeleo, kidogo, kama yalikuwepo. Kwa kweli, hapo mwanzoni, vita vilielekea kwenda dhidi yao.

D.S.Margoliouth:

"Inaelekea pia kwamba katika kuanza mambo yalikuwa yakienda kama vile Mtume (s.a.w.) alivyodhania. Wale mashujaa wa Badr, Ali na Hamza, walisababisha vifo bila kizuizi kama hapo kabla; ujasiri wa Kiquraishi ulilazimika kukutana na mashujaa hawa katika mwandamano wa mapambano ya mtu mmoja mmoja, ambamo mashujaa wao wenyewe waliuawa, na kuangushwa kwao kulieneza mfadhaiko na hofu."

(Muhammad and the Rise of Uislamu, London, 1931)

Shambulizi la Ali, Hamza na Abu Dujana lilieneza hofu na fadhaa katika safu za Makka, na wakaanza kuyumba. Waislamu wakaendeleza fursa yao.

Sir John Glubb:

"Ali ibn Abi Talib aliendelea bila hofu kwenye safu za adui - ilikuwa ni Badr tena; Waislamu walikuwa wasioshindika."

(The Great Arab Conquest, 1963)

Ali alizivunja safu za Maquraishi, na alikuwa tayari yuko ndani kabisa ya safu zao. Wakishindwa kuhimili shambulizi lake, walianza kuachia uwanja. Akiwa hayuko mbali naye, ami yake, Hamza, alikuwa akishughulika kukata njia yake kati ya kundi kubwa la maadui. Kati yao, walikuwa wakilisaga jeshi la Maquraishi.

147

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ilikuwa ni katika wakati huu ambapo matukio mawili yalitokea ambayo yalisababisha mpinduko katika mafanikio ya Waislamu, na ambayo yaliwanyang'anya ushindi kutoka mikononi mwao. La kwanza lake likiwa ni kifo cha Hamza.

Hinda, mke wa Abu Sufyan, alikuwa amekuja kutoka Makka na mtu mmoja, Wahshi, mtumwa wa Kihabeshi, kuja kumuua Hamza, na alikuwa amemuahidi kumpa sio tu uhuru wake bali pia na dhahabu nyingi, madini ya fedha na hariri katika kufanikiwa kwake. Alikuwa anafahamika kwa ustadi wake katika kutumia silaha ya "taifa lake", mkuki.

Wahshi alijificha nyuma ya jiwe akingojea wasaa wa fursa, na mara ukatokea. Pale tu Hamza alipomuua muabudu-sanamu mmoja, na akamrukia mwingine, Wahshi akasimama, akachukua shabaha kali, na akairusha ile silaha ya kombora ambayo kwayo hapakuwa na kinga dhidi yake. Mkuki huo ukampata Hamza kwenye kinena. Alianguka chini na akafa karibu mara moja.

Tukio jingine lilihusisha sehemu kuu ya jeshi la Madina. Kutetereka na kuchanganyikiwa kwa jeshi la Makka kulikuwa kunaonekana wazi kabisa kwa muda huu, na Waislamu walichukulia kwamba tayari wamekwishapata ushindi. Kwa shauku kubwa ya kutokosa fursa ya kumpora adui, walisahau nidhamu yao. Hila hii iligunduliwa na wale wapiga mishale waliokuwa wamewekwa na Mtume (s.a.w.) pale katika kijinjia muhimu cha mlimani. Wao pia walidhania kwamba adui alikuwa amekwisha shindwa, na alikuwa anakimbia. Walifikiri kwamba kama wenzao kule kwenye uwanja wa vita watakamata mizigo ya adui, basi wao wenyewe watapoteza sehemu yao ya ngawira. Hofu hii iliwachochea wao kushuka kule chini bondeni dhidi ya amri halisi ya Mtume. Kapteni wao, Abdullah ibn Jubayr, aliwasihi wasiache kile kijinjia lakini hawakumsikiliza, na wakaenea ndani ya bonde. Tamaa yao ya ngawira iliwanyima Waislamu ushindi katika vita vya Uhud!

Sasa, jenerali mmoja wa Makka, Khalid bin al-Walid, akagundua kwamba kile kijinjia muhimu upande wa kushoto wa jeshi la Madina hakikuwa na ulinzi. Yeye haraka sana akaichukua fursa hiyo kuwashambulia askari doria wachache waliokuwa bado wapo pale kwenye kinjia kile, kwa wapanda farasi wake. Wale doria walipigana kishujaa lakini wote pamoja na Abdullah ibn Jubayr, walizidiwa nguvu, na wakauawa. Mara moja Khalid akakiteka kinjia kile, akalishambulia lile jeshi la Madina kwa kutokea nyuma.

Lile jeshi la Madina lilikuwa linashughulika kukusanya ngawira, bila kuelewa kabisa kitu kingine chochote kile. Ghafla, lilishitukizwa na shambulio la lile jeshi la farasi la Makka nyuma yao. Abu Sufyan pia aliigundua hila ya Khalid, na ule mkanganyiko wa Waislamu. Alikusanya upya vikosi vyake, akarudi kwenye uwanja wa mapambano na kuanzisha mashambulizi ya mbele juu yao. Sasa wakajikuta wameshikwa katika mashambulizi ya mbele na nyuma ya maadui, na wakahofu. Ilikuwa sasa ni zamu yao kushindwa. Walianza

148

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kukimbia lakini bila kujua ni upande gani wa kukimbilia, na kila mmoja alikimbia na njia yake.

Mshangao haukuishia kwa askari wa kawaida wa jeshi la Waislamu tu; ulikuwa ni wa jumla. Baadhi ya maswahaba wakuu wa Mtume (s.a.w.) walikumbwa pamoja na wengine kabla ya shambulizi la adui. Miongoni mwa waliokimbia walikuwa wote Abu Bakr na Umar. Inasimuliwa na Anas bin Nadhr, ami yake Anas bin Malik, kwamba Abu Bakr alisema katika nyakati za baadae kwamba pale Waislamu walipokimbia kutoka kwenye vita vya Uhud, na wakamuacha Mtume wa Allah (s.a.w.) yeye alikuwa wa kwanza kurudi kwake. Umar mara nyingi alisema kwamba wakati Waislamu waliposhindwa huko Uhud, alikimbia na kupanda kwenye kilima (Tarikh Tabari, juz. IV, uk. 96). Baadhi ya maswahaba waliweza kufika Madina na wengine walitafuta hifadhi kwenye mapango na makorongo ya mlima.

Uthman bin Affan, khalifa wa tatu wa Waislamu baadae, hakushiriki katika vita vya Badr lakini alikuwepo Uhud. Hata hivyo, aliiona milio ya migongano ya panga na mikuki imezi-di kiasi kidogo katika ujasiri wake, na alikuwa miongoni mwa wakimbizi wa mwanzo. Sheikh Muhammad Khidhri Buck anasema katika kitabu chake cha wasifu wa Mtume (s.a.w.) kwamba Uthman alikuwa mtu mwenye aibu sana, na kwamba ingawa alikimbia kutoka kwenye uwanja wa vita, hakuingia Madina. Kuwa na aibu kwake kulimzuia kufanya hivyo.

Pale Waislamu walipokuwa wanakimbia kupita alipokuwapo Mtume, alijaribu kuwazuia lakini hakuna hata mmoja aliyejaribu kumsikiliza. Katika muda mfupi mambo yali-wageukia, na ushindi ukakwapuliwa kutoka mikononi mwao. Ilikuwa ni gharama iliyokuwa wailipe kutokana na kukosa utii kwa Mtume wao, na kwa shauku ya wasiwasi juu ya kukusanya ngawira.

Ufuatao ni ushuhuda wa Qur'an Tukufu juu ya mwenendo wa Waislamu katika vita vya Uhud

Usahihi-10.jpg

"Tazama! Mlikuwa mnapanda juu ya mlima, Bila ya kutupa jicho la pembeni kumuangalia yeyote yule, Na Mtume akiwa nyuma yenu anawaiteni mrudi. Hapo Allah akawapeni dhiki baada ya dhiki kwa njia ya kukulipisheni, kuwafundisha msisikitikie ngawira iliyowakoseni, na kwa (madhara) yaliyokufikeni. Kwani Allah ni Mwenye kujua yote mnayoyafanya." (Sura 3: Aya ya 153)

149

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mtume (s.a.w.) alikuwa amempa bendera ya Uislamu ami yake, Masaab ibn Umayr, kati-ka vita vya Uhud. Aliuawa na adui, na ile bendera ya Uislamu ikaanguka chini. Wakati Ali alipoona ile bendera inaanguka chini, alikurupuka mbele, akaisimamisha, na akainyanyua juu mara nyingine tena.

Washington Irving:

"Hamza alichomwa na mkuki wa Wahshi, yule mtumwa wa Kihabeshi, aliyekuwa ameahidiwa uhuru wake kama angemuua Hamza. Musaab ibn Umayr, pia, aliyekuwa amebeba bendera ya Muhammad, aliangushwa chini, lakini Ali aliikamata ile bendera tukufu, na akainyanyua juu sana katikati ya wimbi la vita.

Kwa vile Musaab alifanana sana na Mtume (s.a.w.) mwenyewe, ukelele ulitolewa na adui kwamba Muhammad ameuawa. Maquraishi walitiwa moyo na hamasa maradu-fu kwa kusikia sauti hiyo; Waislamu wakakimbia kwa kukata tamaa, wakiwa wame-wabeba pamoja nao Abu Bakr na Umar, ambao walikuwa wamejeruhiwa."

(The Life of Muhammad) Muhammad Husein Haykal:

"Wale waliodhania kwamba Muhammad alikuwa amekufa, ikiwa ni pamoja na Abu Bakr na Umar, walikwenda kuelekea mlimani na wakakaa chini. Wakati Anas ibn al-Nadr alipouliza ni kwa nini wanakata tamaa mapema hivyo, na akaambiwa kwamba Mtume wa Allah (s.a.w.) alikuwa ameuawa, akajibu kwa ukali: "Na mtajifanyia nini nyie wenyewe na maisha yenu baada ya Muhammad kufa? Simameni, na mfe kama alivyokufa yeye." Akageuka, akashambulia dhidi ya adui, na alipigana kwa ushujaa sana (mpaka akauawa)."

(The Life of Muhammad, 1935, Cairo)

Waislamu wengi walikuwa wamekimbia kutoka kwenye uwanja wa vita lakini Ali alikuwa bado anapigana. Alikuwa amebeba bendera ya Uislamu kwenye mkono mmoja, na upanga katika ule mwingine. Yeye pia aliusikia ule ukelele "Muhammad amekufa." Lakini ulim-fanya kutojali sana juu ya maisha yake mwenyewe.

Mtume, hata hivyo, alikuwa kwenye sehemu nyingine ya uwanja wa mapambano. Alikuwa amejeruhiwa, na kichwa chake na uso ulikuwa unatoka damu. Waislamu wachache, zaidi hasa Ansari, walikuwa wakimlinda. Lilikuwa ni kundi hili dogo, na kelele zao za kivita ndivyo vilivyovuta nadhari ya Ali. Alipasua njia yake katikati ya mistari ya adui na akawafikia wapiganaji wenzie. Walikuwa wamesimama kumzunguka Mtume, na wakion-gozwa na Abu Dujana, walikuwa wakifanya kila walichoweza kumkinga Muhammad

150

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kutokana na silaha za makombora za adui. Ali alisisimka kumwona bwana wake akiwa hai bado lakini hakuwa na muda wa kuswalimiana. Wale waabudu-sanamu walikuwa wamean-za upya mashambulizi yao, na sasa ilikuwa ni Ali ambaye alipaswa kuwapiga kuwarudisha nyuma. Walishambulia kwa marudio lakini aliwakwamisha kila mara.

Muhammad Husein Haykal:

".. wakati mtu mmoja alipokemea kwamba Muhammad ameuawa, vurugu zilichukua madaraka kamili, hamasa ya Waislamu ilishuka chini na wapiganaji wa Kiislamu walipigana kwa mtawanyiko na bila ya lengo. Vurugu hizi zilihusika na kumuua kwao Husayl ibn Jabir Abu Hudhayfah kwa makosa, kwani kila mtu alitafuta kuokoa maisha yake mwenyewe kwa kukimbia isipokuwa watu kama Ali ibn Abi Talib ambaye Allah (s.w.t.) alimuongoza na kumlinda."

(The Life of Muhammad, 1935, Cairo)

Katika vita vya Uhud, wengi wa maswahaba waliotangazwa kuwa majasiri sana na waaminifu, waliwageuzia migongo maadui, na wakakimbilia kujificha. Lakini walikuwe-po wachache ambao hawakukimbia. Mmoja wao alikuwa ni Ummu Ammarra Ansariyya, bibi kutoka Madina. Alikuwa muumini asiyekuwa na hofu, na Waislamu wote wanaweza kwa haki kabisa kujivunia ujasiri wake. Alitambulikana kwa ujuzi wake kama daktari na muuguzi, na alikuja Uhud pamoja na jeshi la Madina.

Mwanzoni mwa vita hivyo, Ummu Ammarra Ansariya alileta maji kwa ajili ya wapiganaji hao au aliwahudumia kama walikuwa wamejeruhiwa. Lakini Waislamu waliposhindwa na wakakimbia kutoka kwenye uwanja wa vita, wajibu wake ulibadilika kutoka ule wa muuguzi kuwa wa mpiganaji. Wakati mmoja maadui walileta watupa mishale ili kumrushia mishale Mtume. Ummu Ammarra alichukua ngao kubwa na akaishikilia mbele yake kumlinda kutokana na yale makombora yanayoruka.

Muda mfupi baadae, watu wa Makka wakashambulia kwa panga na mikuki ambapo Ummu Ammarra alitupa ile ngao, na akawashambulia kwa upanga. Muabudu-sanamu mmoja akaja kwa hatari karibu sana na Mtume (s.a.w.) lakini Ummu Ammarra akaja mbele yake, na wakati yule muabudu-sanamu alipotupa dhoruba, pigo hilo liliangukia begani mwake. Ingawa Ummu Ammarra alikuwa amejeruhiwa, hakuingiwa na hofu, na kwa dhamiri kabisa akasimama kati ya Mtume (s.a.w.) na maadui zake, akiwadharau wao na kutoogopa kifo.

Wakati huo kulikuwa na utulivu wa muda katika mapigano. Kwa kuchukua fursa hiyo, Ali alimtoa Mtume (s.a.w.) kutoka kwenye ile sehemu ya hatari mpaka kwenye pango ambako angeweza kupata mapumziko kidogo, na ambako majeraha yake yangeweza kufungwa.

151

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

D.S.Margoliouth:

"Yule shujaa Ali pamoja na (baadhi) watu wengine majasiri walipomuona (Mtume) walimbanisha faraghani kwenye pango ambako angeweza kuuguzwa."

(Muhammad and the Rise of Islam)

Fatmah Zahra, binti ya Mtume, alikuja kutoka mjini pamoja na kikundi cha wanawake wa Kiislam aliposikia habari za kushindwa kwa Waislamu. Ali alileta maji katika mbonyeo wa ngao yake, na Fatmah Zahra akaiosha damu kutoka kwenye uso wa baba yake, na akam-funga majeraha yake.

Wajibu wa wale Wanawake wa Makka

Kufukuzwa kwa Waislamu kutoka kwenye uwanja wa vita kulikuwa ni mwaliko kwa wale wanawake kutoka Makka kutafuta na kupata kutosheleza hamu yao ya kuua juu ya miili ya wale mashahidi. Walikata pua zao, masikio, mikono na miguu, na waliwapasua matumbo yao, wakatoa viungo, na wakavifanya mikufu kama mashada ya ushindi wa vita.

Muhammad ibn Ishaq:

"Saleh bin Kaysan aliniambia kwamba Hind, binti ya Utba, na wale wanawake aliokuwa nao, waliwakatakata maswahaba wa Mtume (s.a.w.) waliokufa. Waliwakata masikio yao na puazao na Hind akatengeneza kutokana navyo bangili za miguuni na skafu na akatoa bangili (zake mwenyewe) na skafu na vidani kwa Wahshi, yule mtumwa wa Jubayr bin Mutim. Alikata ini la Hamza na akalitafuna, lakini hakuweza kulimeza na akalitupilia mbali.

Al-Hubab bin Zabban, kaka yake B. Harith bin Abdu Manat, ambaye wakati huo alikuwa ndiye mkuu wa vile vikosi vya watu weusi, alipita karibu na Abu Sufyan alipokuwa anaichoma pembe ya mdomo wa Hamza kwa ncha ya mkuki wake, akise-ma: "Onja hiyo, wewe muasi." Hulays aliguta kwa mshangao, "Oh! Banu Kinana, hivi huyu ndiye mkuu wa Maquraishi anayefanya hivyo kwa binamu yake aliyekufa kama mnavyoona?"

(The Life of the Messenger of God)

Waislamu Sabini na tano waliuawa kwenye vita vya Uhud, na miili ya wengi wao ilikat-wakatwa na Hinda na wale wanawake makatili wengine kutoka Makka.

Chuki juu ya Muhammad, Ali na Hamza ilikuwa ni moto ambao ulimmeza Hinda. Ingawa Hamza peke yake alikuwa ndio muathirika wa uchu wa ula-binadamu wa Hinda katika vita

152

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

vya Uhud, Muhammad na Ali hawangetegemea kutendewa kwa tofauti yoyote kutoka kwake kama wangeangukia mikononi mwake. Aliirithisha chuki yake juu ya Muhammad na Ali kwa wanae na wajukuu zake, na vizazi vitakavyofuatia.

Kuondoka kwa Jeshi la Makka.

Baada ya mshituko wa kwanza wa kushindwa ulipopita, baadhi ya Waislamu walirudi kwenye uwanja wa mapambano. Abu Bakr na Umar walikuwa miongoni mwao. Wao pia waliingia kule kwenye pango ambako Ali alimpeleka Mtume.

Kwa wakati huu, Abu Sufyan ambaye alikuwa tayari kurudi Makka, anaelezwa kuwa alikuja karibu na lile pango. Akiwa amesimama chini ya vile vilima, alibishana kidogo na Umar.

Sir John Glubb:

"...Maquraishi wangeweza kuupanda Mlima Uhud kwa gharama ya majeruhi wachache na kuweza kumuua Mtume wa Allah (s.a.w.) na kile kikundi kidogo cha wafuasi waliojitoa ambao walibakia pamoja naye. Pale Abu Sufyan alipomuuliza Umar ibn al-Khatab kama Muhammad alikuwa amekufa, alimjibu, "Hapana, Wallahi, anakusikia unavyoongea." Lakini haikumjia Abu Sufyan kuchukua fursa hiyo ya uvunjaji hatari wa usalama.

Ukatili wa kinyama wa mauaji hay a (katika vita vya Uhud) unafafanua kwa mara nyingine tena ile tofauti ya kipekee kati ya mapigano rahisi na mara nyingi ushujaa ya Waarabu na unyama wa uadui baina ya koo mbili. Abu Sufyan anazungumza kwa maelewano na Umar ibn al-Khatab kwenye uwanja wa vita wa Uhud, kwani hakuna kati yao aliyeua ndugu wa mwenzie. Lakini mke wa Abu Sufyan, Hinda, binti ya Utba ibn Rabia, anaikatakata maiti ya Hamza, aliyemuua baba yake."

(The Life and Times of Muhammad)

Maquraishi walidhania wamemaliza kazi yao. Walikuwa wamewashinda Waislamu na wameokoa heshima yao. Hivyo wenyewe wakiwa wameridhika, waliondoka kwenye uwanja wa vita na wakaelekea kwenye mji wao wa nyumbani upande wa Kusini. Lakini Mtume, akiwa bado hana uhakika na nia zao, alimtuma Ali kwenda kuwaangalia kwa mbali na kumpa taarifa za mienendo yao.

Ali alirudi na kukmfahamisha Mtume (s.a.w.) kwamba Maquraishi wameshaipita Madina, na walikuwa wakienda kuelekea Makka. Hii ilimhakikishia Mtume. Waislamu ndipo wakashuka kutoka mlimani, wakawaswalia maiti wao, na wakawazika.

153

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ali na Vita vya Uhud

Katika vita vya Uhud, Ali alimuua mshika-bendera wa kwanza wa jeshi la wapagani. Wakati mshika-bendera huyo alipoanguka chini, na bendera pia ilianguka chini pamoja naye. Ali kwa hiyo aliiangusha nembo ya upagani.

Baadae, vita vilipokuwa vinachachamaa, wapagani walimuua Musaab ibn Umayr, mshika-bendera wa jeshi la Waislamu. Musaab alianguka chini, na bendera pia ikaanguka pamoja naye. Lakini muda uliofuata tu, Ali akatokea; aliinyanyua ile bendera iliyoanguka kutoka ardhini, na akaikunjua kwa mara nyingine. Alikuwa kwa hiyo sawasawa kama ishara ya kuangamia kwa uabudu-sanamu na ushirikina kama alivyokuwa ishara ya kunyanyuka na kuzaliwa-upya kwa Uislamu. Hapo Uhud, rafiki na adui wote waliona kwa macho yao yale matendo ya ajabu ya ushujaa na ujasiri wa Ali, na kujitolea kwake kwa bwana wake, Muhammad, Mtume wa Allah (saw) Ali alipigana vile vita vya Uhud kwa ule upanga mashuhuri, Dhu'l-Fiqar.

Muhammad ibn Ishaq:

"Upanga wa Mtume (s.a.w.) ulikuwa unaitwa Dhu 'l-Fiqar. Muhadithin mmoja alinieleza kwamba Abu Najih alisema, 'Mtu mmoja aliguta katika vita vya Uhud:

'Hakuna upanga ila Dhu 'l-Fiqar Na hakuna shujaa kama Ali. "

(The Life of the Messenger of God)

Katika mikono ya Ali, Dhu'l-Fiqar ulikuwa ni radi iliyoshambulia na kuumaliza upagani, uabudu masanamu na ushirikina. Lakini kwa Uislamu, ulikuwa ndio mletaji wa matumai-ni, nguvu mpya, maisha mapya, na heshima, utukufu na ushindi. Akielezea juu ya matukio ya Uhud, kufuatia kutimuliwa kwa Waislamu wakati Mtume (s.a.w.) alipokuwa amesham-buliwa na maadui zake, M. Shibli, yule mwanahistoria wa Kihindi, anasema:

Ilikuwa ni wakati mbaya sana katika historia ya Uislamu. Waabudu-masanamu wal-imshambulia Mtume wa Allah (s.a.w.) kama miungu ya ghadhabu ya hadithini lakini kila mara walizuiwa kwa ncha ya Dhu'l-Fiqar.

Shibli anaendelea kusema kwamba hao waabudu-masanamu walikuja kama "mawingu meusi na ya kutisha, tayari kuwapasukia Waislamu." Kama Ali asingeyapunguza nguvu mashambulizi ya watu wa Makka, basi kupasuka kwa wingu huku kungeikumba Madina, na Uislamu ungesombwa katika mafuriko ya uabudu-masanamu. Kama Ali pia angeshind-wa katika wajibu wake kama wengine wengi walivyoshindwa, waabudu-masanamu hawa wangemuua Mtume wa Allah (s.a.w.) na wangeuzima mwanga wa Uislamu. Lakini Ali na

154

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Waislamu wengine wachache, wakiwa ni pamoja na Abu Dujana na Ummu Ammarra Ansariyya, walilizuia balaa hili. Katika vita hivi vya kuhuzunisha, Waislamu 75 waliuawa. Kati yao wanne walikuwa ni Muhajir, na waliobakia walikuwa ni Ansari.

Mashahidi wa Uhud

Tukio la kusikitisha sana kati ya matukio ya vita vya Uhud lilikuwa ni kifo cha Hamza na kuharibiwa kwa mwili wake. Baada ya kuondoka kwa watu wa Makka, Mtume (s.a.w.) alikwenda kuona maiti ya ami yake.

Masikio na pua vilikuwa vimekatwa; tumbo limepasuliwa, na viungo vyake vilikuwa vimeondolewa. Alijawa na huzuni kwa kuuona mwili ule wa shahidi katika hali ile, na akaamuru ufunikwe.

Hinda, mke wa Abu Sufyan, na mama yake Mu'awiyyah, anaitwa "mla-ini" katika historia ya Uislamu. Ibn Ishaq anasema kwamba alilitafuna ini la Hamza lakini hakuweza kulimeza. Lakini Ibn Abdul Birr anasema katika kitabu chake, Al-Isti 'aab, kwamba kwa kweli alitengeneza moto katika uwanja wa vita hivyo, akalichoma ini la Hamza kwenye moto huo, na akalila!

Wakati Mtume (s.a.w.) aliporudi Madina, alivisikia vilio vya huzuni vya watu wa zile familia zilizoondokewa. Ndugu na jamaa wa mashahidi wa Uhud walikuwa wanawaom-boleza watu wao waliokufa.

Alimaka kwa mshangao: "Wapi! Hakuna hata mtu wa kuomboleza kifo cha ami yangu, Hamza." Viongozi wa Ansari kusikia kauli hii, wakaenda majumbani kwao, na wakawaa-muru wanawake zao kwenda kwenye nyumba ya Mtume, na kuomboleza kifo cha ami yake.

Wakati huo kundi la wanawake wa Madina likakusanyika katika nyumba ya Muhammad, na wote walikililia kifo cha huzuni cha Hamza, shujaa wa Uislamu.Mtume (s.a.w.) akaom-ba baraka za Allah (s.w.t.) juu yao wote. Baada ya hapo ikawa ni desturi hapo Madina kwamba wakati wo wote mtu yoyote akifa, waombolezaji wake walianza vilio vyao kwa nyimbo za maombolezo ya Hamza.

Watu wa Madina walianza kwanza kumuombeleza Hamza kisha wakawaombolezea watu wao wenyewe waliokufa.

155

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Muhammad Ibn Ishaq:

"Mtume (s.a.w.) alipita kwenye makazi ya Banu Abdul Ashal na Zafar na akawasikia wakilia kwa ajili ya wafu wao. Macho yake yalijawa na machozi na akasema: "Lakini hakuna wanawake wanaolia kwa ajili ya Hamza." Wakati Sa'd bin Mu'adh na Usayd bin Hudayr waliporudi majumbani kwao, waliwaamuru wanawake zao kujitayarisha na kwenda kulia kwa ajili ya ami yake Mtume (s.a.w.)

(The Life of the Messenger of God)

Mbali na Hamza, Muhajirina wengine watatu walipata taji la kufa kishahidi katika vita vya Uhud. Walikuwa ni Abdullah ibn Jahash, binamu yake Mtume; Masaab ibn Umayr, ami yake Mtume; na Shams ibn Uthman. Hasara kwa Ma-Ansari ilikuwa kubwa sana. Waliacha maiti sabini na moja hapo uwanjani, na wengine wengi waliojeruhiwa. Allah (s.w.t.) awape rehema hao wote.

Vita vya Uhud vilikuwa ni wakati wa majira ya upinzani wa kipagani kwa Uislamu. Ingawa walikuwa washindi kwenye vita, Maquraishi hawakuweza kufuatilia na kufaidi ushindi wao, na mafanikio yao yalibadhirika mara tu.

156

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kuzaliwa kwa Hasan na Husein

Mnamo tarehe 15 ya mwezi wa Ramadhani ya mwaka wa 3 H.A. (Machi, 625), Allah (s.w.t.) aliridhia kumbariki binti ya Mtume Wake, Muhammad, kwa kuzaa mtoto wake wa kwanza. Muhammad Mustafa alikuja akionyesha furaha; alimchukua mtoto mchanga huyo mikononi mwake, akambusu, akamsomea adhana kwenye sikio lake la kulia, na iqamah kwenye sikio lake la kushoto; na akamwita Hasan.

Mwaka mmoja baadae, yaani, mnamo tarehe 3 Shaaban ya mwaka wa 4 H.A. (Februari, 626), Allah (s.w.t.) aliridhia kumpa binti ya Mtume Wake, mwanae wa pili. Mtume (s.a.w.) akaja, mwenye tabasamu na furaha, akamchukua mtoto huyo mikononi mwake, akambusu, akamsomea adhana kwenye sikio lake la kulia, na iqamah kwenye sikio lake la kushoto, na akamwita Husein.

Kuzaliwa kwa kila mmoja wa mabwana hawa kulikuwa ni tukio la kufurahia kwa Muhammad. Aliwachukulia kama miongoni mwa baraka kubwa za Allah (s.w.t.) na akamshukuru Yeye kwa ajili yao. Katika kuzaliwa kwa kila mmoja wao, Waislamu walim-iminika kwenye ule Msikiti Mkubwa na kumpongeza yeye. Aliwapokea kwa tabasamu na shukurani, na akashirikiana furaha yake pamoja nao.

Hapakuwa kamwe na siku ambayo Mtume (s.a.w.) hakutembelea nyumba ya binti yake kuwaona watoto wake. Alipendelea kuwaona wao wakitabasamu, hivyo aliwachekesha na kuwarusharusha; Aliwakumbatia na kuwadekeza, na alichukulia kila hatua yao na kila neno kama shani.

Wakati mabwana hawa wawili walipokua kidogo, na wakawa wanaweza kutembea hapa na pale, mara nyingi sana walitoka nje ya nyumba yao kuingia Msikitini. Kama babu yao alikuwa katikati ya hotuba, aliacha mara moja, akateremka kutoka kwenye mimbari, akawachukua mikononi mwake, akawabeba na kurudi nao, akawakalisha karibu naye mwenyewe juu ya mimbari, na kisha akaendelea na hotuba yake. Kama alikuwa anaongoza Swala ya jamaa, na alikuwa kwenye sijdah, watoto hawa wote, mara kwa mara, walipan-da juu ya shingo na mgongo wake. Alipendelea kurefusha sijdah hiyo kuliko kuwavuruga, na kunyanyuka kutoka kwenye sajdah pale tu waliposhuka kutoka kwenye shingo au mgongo wake kwa hiari yao. Kama alitoka nje ya nyumba yake au Msikitini, walipanda mabegani mwake. Watu wa Madina waliwaita "Wapandaji wa Mabega ya Mtume wa Allah (s.a.w.)," walikuwa wamemganda sana yeye kuliko walivyowaganda wazazi wao wenyewe.

157

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Muhammad, Mtume wa Uislamu, kamwe hakuwa na furaha zaidi kuliko alipokuwa na Hasan na Husein. Walikuwa ni matunda ya macho yake, na furaha ya moyo wake, na kati-ka kuwa pamoja nao peke yao yeye alipata burudani ya kweli na kamilifu. Alicheza pamo-ja nao mchezo wa kujificha na kutafutana, na kama walikuwa wanacheza na watoto wengine, alikaa karibu nao kiasi tu cha kusikia uzuri wa sauti ya kicheko chao. Kwa ajili yao, aliweza kuacha hata mambo muhimu ya nchi. Walipotabasamu, alisahau usumbufu na wasiwasi wote wa nchi na serikali. Alipenda kusoma kila ujumbe ambao walimwandikia katika tabasamu zao za kimalaika.

Mwanzoni, Mtume wa Allah (s.a.w.) alimlea binti yake mwenyewe, Fatima Zahrah, ambaye alimwita Bibi wa Peponi. Sasa alichukua wajibu wa kuwalea watoto wake wawili - Hasan na Husein - ambao aliwaita Mabwana wa Vijana wa Peponi. Kwake yeye elimu yao ilikuwa ni jambo lenye umuhimu mkubwa, na yeye mwenyewe alishughulikia kila jambo ndani yake. Lengo lake lilikuwa wazi: aliwataka wao kuwa mazao bora kabisa ya Uislamu, na walikuwa hivyo. Aliijenga tabia yake mwenyewe kwenye tabia zao, na akawafanya kuwa mfano kwa umma wake ambao ulikuwa uigize mpaka mwisho wa wakati wenyewe.

Ali na Fatmah Zahrah pia walikuwa na mabinti wawili - Zainab na Ummu Kulthum. Walipokua, waliolewa na binamu zao - watoto wa Jafar ibn Abi Talib, yule Shahidi mwenye Mbawa (Tayaar) wa Uislamu. Zainab aliolewa na Abdullah ibn Jafar, na Ummu Kulthum aliolewa na Muhammad ibn Jafar.

Hasan, Husain, Zainab na Ummu Kulthum, watoto wote wanne walistareheshwa na babu yao, Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) na siku za furaha sana katika maisha yao wote watano ni zile walizokuwa pamoja.

Kifo cha Fatima binti Asad, Mama yake Ali ibn Abi Talib

Katika mwaka wa 4 A.H (626 A.D.) Fatima binti Asad, mjane wa Abu Talib na mama yake Ali, alifariki hapo Madina. Alimlea Muhammad, Mtume (s.a.w.) wa baadae, kama mwanae mwenyewe, naye Muhammad alimwita yeye mama yake. Alikuwa ndiye mwanamke wa pili katika Arabia kuukubali Uislamu, wa kwanza akiwa ni Khadija, mke wa Mtume.

Muhammad alimkosa mama yake mapema sana maishani lakini mara akapata mama wa pili kwa Fatima binti Asad. Yeye, kwa hiyo, hakukosa mapenzi na upendo ambavyo ni mama peke yake anayeweza kuvitoa. Wakati mama yake wa kunyonya alipofariki, alihud-huria mazishi, na akasema: "Allah (s.w.t.) airehemu roho yako tukufu. Ulikuwa kwangu mimi kama mama yangu mwenyewe. Ulinilisha mimi wakati wewe mwenyewe ukikaa na njaa. Lengo lako katika kufanya hivyo lilikuwa ni kumridhisha Allah (s.w.t.) kwa maten-do yako." Alitoa shuka lake mwenyewe kwa ajili ya sanda yake, na alizikwa nalo. Alikuwa

158

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

mara kwa mara akisema, "Nilikuwa yatima na akanifanya mimi ni mwanae. Alikuwa ndiye mtu mpole sana kwangu baada ya Abu Talib."

Kaburi lilipochimbwa tayari, Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliliingia; alilala ndani yake, na akasema: "Ewe Allah! Uhai na mauti viko mikononi Mwako. Wewe peke yako ndiye hutakufa kamwe. Mrehemu mama yangu, Fatima binti Asad, na umpe jumba kubwa huko Peponi. Wewe ni Mwingi wa Rehema."

Wakati Fatima binti Asad alipozikwa, Muhammad Mustafa alirudia Allah-u-Akbar mara arobaini, na akaomba: "Ewe Allah! Muweke kwenye Nuru, na ujaze moyo wake na Nuru."

Muhammad Mustafa alikuwa ndiye Mtekelezaji wa hati ya wosia ya Fatima binti Asad.

Fatima binti Asad alikuwa ni mwanamke wa kipekee sana kwa vile watoto wawili kati ya watoto aliowakuza, Muhammad, na Ali, walitokea kuwa watu wa kipekee katika historia ya Uislamu. Nyumbani kwake ndipo chimbuko halisi la Uislamu. Wote Muhammad, Mtume (s.a.w.) wa baadae wa Uislamu, na Ali, shujaa wa baadae wa Uislamu, walizaliwa katika nyumba yake, na walikulia ndani yake. Wote walikuwa "Matunda" ya elimu yake.

Fatima binti Asad pia ni mama yake Jafar, yule shujaa wa vita vya Muutah, na Shahidi mwenye Mbawa (Tayaar) wa Uislamu. Hili jina la mumewe, Abu Talib, linajitokeza kwenye historia kama mfadhili mkubwa sana wa Uislamu, lakini nafasi yake Fatima katika Uislamu si ya umuhimu wa chini kuliko ya mumewe. Anachangia sifa hiyo pamoja naye ya kumlea na kumsomesha Muhammad, Mtume (s.a.w.) wa baadae wa Allah (s.w.t.) Kama mumewe alimlinda Muhammad kutokana na maadui zake huko nje, yeye Fatima alimpa upendo, faraja na usalama huko nyumbani. Ilikuwa ni ndani ya nyumba yake ambamo Muhammad alipata usalama wa kihisia na ukaribu wa hisia wa familia.

Kama Khadija alikuwa ndiye mwanamke wa kwanza mwislamu na mfadhili mkubwa sana (mwanamke) wa Uislamu, Fatima binti Asad alikuwa mwanamke wa pili mwislamu, na mfadhili wa pili (mwanamke) mkubwa sana wa Uislamu. Allah (s.w.t.) awawie radhi waja Wake, Khadija na Fatima binti Asad, na Awarehemu hao.

159

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Vita vya Khandaq

Baada ya vita vya Uhud, Abu Sufyan na wale viongozi wengine wa wapagani waligundua kwamba walipigana vita visivyo na uamuzi, na kwamba ushindi wao haukuwazalia matun-da yoyote. Uislamu ulikuwa, kwa kweli, umeimarika kutoka kinyume chake pale Uhud, na katika muda mfupi wa kustaajabisha, umerejesha mamlaka yake hapo Madina na maeneo yanayoizunguka.

Wapagani waliuona Uislamu ni tishio kwenye usalama wao wa kiuchumi na mamlaka ya kisiasa katika Arabia, na hawangeweza kamwe kukubaliana na kuwepo kwake. Walijua kwamba kama wangeweza kumuua Muhammad, maslahi yao yangepata ulinzi, na mamlaka yao juu ya wengine yangedumishwa katika Arabia. Wakiwa na lengo hili waliamua kushusha shambulizi la mwisho na la kuvunja nguvu juu ya Madina na kuangamiza Waislamu wote.

Montgomery

Lengo la mkakati la watu wa Makka halikuwa ni chochote pungufu zaidi ya kuiangamiza jamii ya Waislamu kama hivyo, au - kile kinacholingana na jambo hilo hilo - kumuondoa Muhammad kutoka kwenye nafasi yake ya mamlaka.

(Muhammad, Prophet and Statesman)

Wakisukumwa na lengo hili, na kwa nguvu ya shauku ya kufanya fidia kwa ajili ya kushindwa kwa siku zilizopita, hawa viongozi wa Makka walianza maandalizi kwa ajili ya vita vya juhudi zote; vita ambavyo vitakuwa ni mwisho wa vita nyingine zote kwa kuuteketeza kabisa Uislamu!

Ndani ya miaka miwili Maquraishi waliunda jeshi la mapambano la wapiganaji elfu kumi. Hili lilikuwa ndio jeshi kubwa kabisa lililowahi kukusanywa na Waarabu mpaka wakati huo. Pamoja na shangwe kubwa na kujiamini, jeshi hili la kutisha liliondoka Makka mwezi wa Februari, 627A.D. kwenda kuiteka Madina na kufutilia mbali Uislamu.

Muhammad Husein Haykal

Wakati habari za uhamasishaji huu mkubwa mno zilipomfikia Muhammad na Waislamu huko Madina, ziliwatia wote wasiwasi. Uhamasishaji wa Arabia yote dhidi yao uliingiza hofu ndani ya mioyo yao kwani walikuwa wanakabiliwa na matarajio sio tu ya kushindwa bali kuteketezwa kabisa. Uzito halisi wa hali hiyo ulikuwa dhahiri katika ukweli kwamba lile jeshi ambalo makabila ya Kiarabu sasa walikuwa wameliunda lilikuwa limezidi katika idadi na zana, kitu chochote ambacho Peninsula hiyo imewahi kushuhudia kabla.

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

160

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mtume (s.a.w.) aliitisha mkutano wa dharura wa maswahaba wake wakuu kushauriana nao katika suala la kuulinda mji. Kitu kimoja kilikuwa wazi. Waislamu walikuwa wachache sana kwa idadi na wadhaifu sana katika zana kwamba walikuwa hawawezi kukutana na lile jeshi linalovamia kwenye ardhi ya wazi. Madina ilikuwa ilindwe kutoka ndani yake. Lakini vipi? Vipi askari wa ulinzi wachache wa Waislamu wataweza kulizuia jeshi la Makka kutokana na kuivamia na kuizagaa Madina ambayo ingekuwa imejaa idadi ya watu wasio-fuzu, lilikuwa ndio swali katika akili ya kila mtu.

Mmoja wa marafiki wa karibu wa Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) alikuwa ni Salman yule Muajemi. Alizaliwa na kukulia huko Uajemi (Iran) lakini aliishi kwa miaka mingi huko Syria na Palestina, na alikuwa na uzoefu wa vita na operesheni za kuzingira za wote, Waajemi na Warumi. Madina ilikuwa na ulinzi wa asili au uliotengenezwa na watu katika pande tatu lakini ilikuwa wazi katika upande mmoja, yaani, ule upande wa kaskazi-ni. Salman alimwambia Mtume (s.a.w.) kwamba kama handaki lingechimbwa katika upande wa kaskazini, mji ule pengine ungeweza kulindwa kwa mafanikio.

Wazo hili, ingawa ni geni na lisilo la kawaida katika Arabia, lilimvutia Mtume. Akalikubali na kuwaamuru Waislamu kulichimba handaki hilo.

Muhammad Husein Haykal

Salman al-Farsi, aliyejua vizuri zaidi juu ya mbinu za vita kuliko ilivyokuwa kawaida hapo katika Peninsula. Alishauri kuchimbwa kwa handaki kavu kuzunguka Madina na kuimarisha kwa majengo yaliyomo ndani yake. Waislamu waliharakisha kutekeleza ushauri huo. Handaki lilichimbwa na Mtume - rehema na amani za Allah (s.w.t.) ziwe juu yake - alifanya kazi kwa mikono yake sambamba na maswahaba zake kutoa uchafu, kuwatia moyo wale Waislamu wanaofanya kazi, na kumshawishi kila mtu kuongeza juhudi zake.

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Kwa kuwa lile jeshi la Makka lilijulikana kwamba linasogelea Madina kwa haraka, hapakuwa na muda wa kupoteza, na Waislamu walifanya kazi kwa harakati kubwa - kwa kupokezana. Ndani ya siku sita handaki hilo likawa limechimbwa, mapema tu kuwazuia wavamizi kuuchukua mji kwa uvamizi.

Kikosi cha wapanda farasi wa Makka kilikuja kama kimbunga lakini ghafla kikazuiwa, katika kasi yake, na handaki hilo. Wapanda farasi hao waliwasimamisha farasi wao kwenye ukingo wake. Mkakati wao mkuu ulikuwa ni kuiteka kwa nguvu Madina kwa masaa machache lakini sasa ilionekana kwao kwamba hawawezi kufanya hivyo. Hapa kulikuwa na handaki, kikwazo kipya ambacho hawakuweza kukipita. Limeingia vipi kwenye mkakati wao? Waliduwazwa kabisa na handaki hilo.

161

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hatimae, na baada ya majadiliano marefu, makamanda wa Makka waliamua kuizingira Madina, na kuwalazimisha Waislamu kuswalimu amri, kwa msuguano (kuwadhoofisha). Walifunga njia zote za kutoka nje ya Madina, na kuwazunguka Waislamu. Madina ilikuwa katika hali ya kuzingirwa!

Ingawa alikuwa ni Abu Sufyan ambaye aliongoza kampeni hiyo nzima, na alikuwa ndiye mkurugenzi wake wa utendaji, hakuwa mtu mpiganaji yeye mwenyewe. Mpiganaji wa jeshi lake alikuwa ni Amr ibn Abd Wudd, mkali zaidi kati ya wapiganaji wa wapagani wa Arabia. Matumaini ya Abu Sufyan ya ushindi wa haraka na wenye uamuzi juu ya Waislamu yalikuwa juu yake huyu. M. Shibli, yule mwanahistoria wa kihindi, na Abbas Mahmud Al-Akkad, yule mwanahistoria wa Misri, wanasema kwamba Amr ibn Abd Wudd alihesabiwa, na Waarabu wa wakati huo, kuwa zaidi ya usawa na askari wa farasi elfu moja.

Amr ibn Abd Wudd hakuwa akipendezewa na vita tulivu au mzingiro (karantini). Alitweta kwa kutaka vitendo. Wakati siku chache zilipokuwa zimepita, na hakuna chochote kili-chotokea, alipoteza subira, na akaamua kuiteka Madina kwa vitendo vyake mwenyewe. Siku moja, akiranda kuzunguka Madina kwa kuvizia, yeye pamoja na mashujaa wengine watatu wa Makka waligundua sehemu yenye mawemawe ambapo lile handaki halikuwa pana sana. Waliwatia chonjo farasi wao kutoka kwenye sehemu hiyo, na wakafanikiwa katika kulivuka lile handaki!

Sasa Amr alikuwa ndani ya mzingo wa Madina. Kwa ujasiri kabisa akasonga mbele kwenye kambi ya Waislamu, na kuwapa changamoto mashujaa wa Kiislam kutoka na kupi-gana dhidi yake katika desturi ya jadi ya Kiarabu ya mapambano ya watu wawili wawili.

Changamoto ya kwanza ya Amr ilipita bila kujibiwa kwa hiyo akairudia lakini bado haku-pata jibu. Hiyo ndiyo fahari kuu ya jina lake kwamba hakuna yeyote katika kambi ya Waislamu aliyethubutu kukabiliana naye katika kupimana nguvu. Kama waabudu masana-mu waliyaona kwake matumaini ya ushindi, Waislamu waliona katika changamoto yake hukumu ya kifo chao.

Amr ibn Abd Wudd alitoa changamoto yake yenye dharau kwa mara ya tatu na akawadhi-haki Waislamu wakati huo huo kwa woga wao.

Kwa Amr lazima itakuwa imeelekea kwamba Waislamu walikuwa wameishiwa na nguvu kwa woga, ambavyo wengi wao, kwa kweli, walikuwa hivyo. Qur'an Tukufu pia imecho-ra picha ya hali ya Waislamu katika kuzingirwa Madina katika Aya zifatazo:

162

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Usahihi-11.jpg

"Tazama! Walikujieni kutoka juu yenu, na kutoka chini yenu, na tazama; macho yalipofifia, na nyoyo zikapanda kooni, nanyi mkamdhania Allah dhana mbalimbali." (Sura ya 33; Aya ya 10)

Usahihi-12.jpg

"Tazama! Na kundi moja kati yao likasema: 'Enyi watu wa Yathrib! Hamuwezi kuhimili (shambulizi). Hivyo rudini' na kundi jingine kati yao likaomba ruhusa kwa Mtume (s.a.w.) likisema: 'Hakika nyumba zetu ni tupu na wazi' Wala hazikuwa wazi; hawakutaka chochote ila kukimbia tu." (Sura ya 33; Aya ya 13)

Amr ibn Abd Wudd pia alionyesha mshangao kwamba wale Waislamu hawakuwa wakionyesha shauku yoyote ya kuingia peponi ambako alikuwa tayari kuwapeleka.

Ni kweli kwamba wengi wa Waislamu walikuwa wamekumbwa na hofu lakini alikuwepo mmoja kati yao ambaye hakuwa hivyo. Alikuwa, kwa kweli, amejitolea kuikubali chang-amoto ya kwanza kabisa ya Amr lakini Mtume (s.a.w.) alimzuia, akitegemea kwamba mtu mwingine yeyote angependa kumkabili Amr. Lakini aliweza kuona kwamba hakuna hata mmoja aliyethubutu kunyoosheana panga naye.

Huyu kijana mdogo aliyekuwa tayari kuipokea changamoto ya Amr hakuwa mwingine yoyote mbali na Ali ibn Abi Talib, yule shujaa wa Uislamu. Pale Amr alipotupa changamoto yake ya tatu, na hapakuwa na mtu aliyemjibu, Ali alisimama na kuomba ruhusa ya Mtume (s.a.w.) ya kutoka na kupigana dhidi yake.

Mtume wa Uislamu hakuwa na budi tena sasa ila kumruhusu binamu yake, Ali, yule Simba wa Uislamu, kwenda na kunyamazisha zile dhihaka na kejeli za Amr Ibn Abd Wudd.

Ali alivaa lile vazi la vita la Mtume wa Uislamu. Mtume (s.a.w.) mwenyewe akaning'inizia Dhu'l-Fiqar (upanga wake) pembeni mwake, na kumuombea kwa ajili ya ushindi wake, akisema: "Ewe Allah! Ulimwita kwenye huduma yako, Ubaida ibn al-Harith, ile siku ambayo vita vya Badr vilipopiganwa, na Hamza ibn Abdul-Muttalib, siku ambayo vita vya Uhud vilipopiganwa. Sasa ni Ali pekee aliyebakia nami. Kuwa Wewe Mlinzi wake, mpatie yeye ushindi, na mrudishe salama kwangu."

163

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Wakati Mtume (s.a.w.) alipomwona Ali akienda kuelekea kwa adui yake, alisema: "Yeye ndiye tashihisi wa Imani yote ambaye anakwenda kupambana na tashihisi ya Ukafiri wote."

Muda mchache baadae, Ali alikuwa amesimama mbele ya Amr. Mashujaa wawili hawa wakatambulishana, na wakapimana. Ali alikuwa na seti ya kanuni ambazo alizitumia katika hali zote ama za vita au za amani. Kwenye vita vya handaki, Waislamu na wapagani waliona maonyesho ya matumizi ya kanuni hizo. Wakati wowote alipokabiliana na adui, alimpa hiari ya kuchagua kati mambo matatu. Nayo yalikuwa ni:

1.  Ali aliutambulisha rasmi Uislamu kwa adui yake. Alimualika kuacha uabudu-sanamu na kuukubali Uislamu. Mwaliko huu ulimfanya Ali muba-ligh wa Uislamu katika uwanja wa vita wenyewe.

2.  Kama adui huyo hakuukubali mwaliko wa Ali wa kuukubali Uislamu, alimshauri yeye kujiondoa kutoka kwenye vita, na asipigane dhidi ya Allah (s.w.t.) na Mtume wake. Kupigana dhidi yao, alimuonya, kutamletea tu laana ya milele juu yake katika dunia zote mbili.

3. Kama adui huyo hakukubali chaguo hili la pili pia, na akakataa kujiondoa kwenye vita, basi Ali alimkaribisha kutupa dhoruba ya kwanza. Ali mwenyewe kamwe hakuwa wa kwanza kushambulia adui.

Amr ibn Abd Wudd alidharau hata kufikiria lile chaguo la kwanza na la pili lakini akakubali hili la tatu, na akapiga dhoruba kubwa kwa upanga wake mkubwa sana ambao ulikata kupita kwenye ngao, kofia ya chuma na kilemba cha Ali, na kufanya jeraha kubwa sana kwenye paji lake la uso. Damu iliruka kutoka kwenye jeraha hilo katika mchirizi lakini Ali hakuvunjika moyo. Alipata nguvu, na kisha akatupa pigo la kujibu kwa upanga ule maarufu Dhu'l-Fiqar, na ukampasua yule mpiganaji wa kutisha wa Arabia katika vipande viwili!

Wakati Amr alipouawa, wale mashujaa watatu katika msafara wake waligeuka na kuwatia chonjo farasi wao kukimbia. Ali akawaacha wakimbie. Ilikuwa ni moja ya kanuni zake kutomfukuza adui anayekimbia. Yeyote yule aliyetaka kuokoa maisha yake, Ali alimwacha ayaokoe.

Kifo cha Amr ibn Abd Wudd kilivunja mgongo wa mashambulizi ya Makka dhidi ya Uislamu, na kuvunja hamasa yao. Nguvu za asili pia zilitangaza vita dhidi yao. Joto lilishu-ka kufikia kiwango cha kuganda, na wingu la vumbi lilinyanyuka ambalo lilivuma kwenye nyuso zao. Wakiwa wamekata tamaa na kuvunjika moyo, wale jamaa wa makabila wenye kigeugeu walianza kuwaacha marafiki zao wa Makka, kwanza mmoja mmoja na wawili

164

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

wawili na watatu watatu, na kisha kwa makumi na ishirini ishirini, na baadae kidogo, kwa mamia. Ule muungano ukaanza kutoweka polepole kwa uwazi kabisa. Abu Sufyan alilaz-imika kuacha kuzingira, na akatoa ishara kwa jeshi lake kurudi nyuma kutoka Madina. Jeshi lake lilitawanyika, na kampeni yake ilikuwa imeshindwa vibaya. Madina ilikuwa imeokolewa.

Kushindwa kwa mzingiro (karantini) wa Madina kwa waabudu-masanamu wa Makka lilikuwa ni tukio muhimu sana katika historia ya Arabia. Ilimaanisha kwamba watakuwa hawawezi kamwe kuandaa uvamizi mwingine wa Madina. Baada ya vile vita vya handa-ki, uamuzi ukahama, hatimae na kwa dhahiri kabisa, kutoka kwa waabudu-sanamu wa Makka kwenda kwa Waislamu wa Madina.

Madina na Uislamu viliokolewa na wazo na shujaa. Wazo lilikuwa ni lile handaki ambalo liliwazuia askari wa farasi wa Makka. Ilikuwa ni fikra mpya kabisa katika vita vya Uarabuni, na Waarabu hawakuwa na uzoefu nayo. Bila ya hilo handaki, wale watu elfu kumi wa kabila la majambazi wangeweza kuivamia na kuizagaa Madina, na wangemuua kila mtu humo. Heshima ya kuiokoa Madina-tun-Nabi, mji wa Mtume, na makao makuu ya Uislamu, inakwenda kwa Salman yule Muajemi, na kwa bwana wake, Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Huyu wa kwanza alianzisha wazo jipya katika kanuni za kijeshi; na huyu mwingine alionekana tayari ni mwenye kulisikiliza, na papo hapo akalitekeleza.

Kila mmoja hapo Madina alidai kuwa ni rafiki au sahaba wa Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) Mji huo ulikuwa na fungu lake wenyewe la watu wenye kutafuta umaarufu. Lakini walikuwepo wachache, kwa kweli wachache sana, watu ambao Muhammad mwenyewe amewakiri kama marafiki zake. Salman, yule Muajemi alihusika kwenye kundi hili teule, ule mzunguko wa ndani kabisa wa marafiki wa Mtume wa Allah (s.a.w.)

Salman alikuwa mtu wa kimo kirefu sana na nguvu za kimwili nyingi mno. Wakati handaki lilipokuwa linachimbwa, alifanya kazi kama ya watu sita wengine. Hili lilimshawishi mmoja wa Muhajirina kutangaza kwamba Salman alikuwa mmoja wao, yaani alikuwa Muhajirina. Lakini alipingwa mara moja na Ansari ambao mmoja wao alisema kwamba Salman alikuwa ni Ansari na sio Muhajir. Makundi mawili hayo yalikuwa bado yanabishana wakati Mtume (s.a.w.) alipowasili hapo kwenye tukio. Yeye pia aliyasikia madai ya pande zote mbili na ali-furahishwa nayo. Lakini aliyakatisha mabishano hayo kwa kutoa "fatwa" yake binafsi. Alisema kwamba Salman hakuwa Muhajir wala Ansari bali alikuwa ni mtu wa nyumba yake mwenyewe - ni Ahlul-Bayt - mtu wa nyumba ya Muhammad Mustafa mwenyewe!

Yule mwanahistoria wa Kiarabu, Ibn Athir, amemnukuu Mtume (s.a.w.) ndani ya kitabu chake, Tarikh Kamil, juz. 2, uk.122, kwamba alisema: "Salman ni mmoja wetu. Yeye ni mtu wa Nyumba yetu." Hii ndio heshima kubwa kabisa ambayo kamwe haijawahi kutole-wa kwa sahaba wake yeyote na Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.)

165

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Salman alikuwa ni mkristo aliyekuwa akiishi huko Ammuria-Asia Ndogo, wakati ali-posikia kwa mara ya kwanza habari zisizokuwa na yakini za kutokea kwa Mtume (s.a.w.) huko Hijazi. Ili kuhakikisha habari hizi, alikuja Madina. Wakati alipouangalia kwa mara ya kwanza uso wa Mtume, aliguta kwa mshangao: "Huu hauwezi kuwa uso wa mtu ambaye amewahi kamwe kusema uongo," na papo hapo akasilimu.

Uislamu ulimkubali Salman kama vile yeye "alivyoukubali" Uislamu. Uislamu ukawa ni kiunganisho cha hisia zake, naye akawa ni sehemu yake ya "mtiririko wa damu." Huko Madina, safari moja mgeni mmoja akamuuliza yeye jina la baba yake. Jibu lake lilikuwa ni: "Uislamu! Jina la baba yangu ni Uislamu. Mimi ni Salman mtoto wa Uislamu." Salman "alichanganyika" kwenye Uislamu kwelikweli kiasi kwamba alikuwa hatofautishiki nao.

Tishio kwenye usalama wa Madina, hata hivyo, halikwisha kwa kuchimbwa kwa hilo han-daki. Madini ilikuwa bado sio salama. Kwenye sehemu ambayo lile handaki lilikuwa jem-bamba, yule jenerali wa jeshi la Makka na mashujaa wengine watatu, waliweza kuruka juu yake na kwenda (kwa farasi) kwenye kambi ya Waislamu. Kama walifanikiwa kuanzisha daraja ya kuvukia juu ya handaki hilo, jeshi la farasi lote la Makka na askari wa miguu, na maharamia wasiotabirika wangeweza kuingia mjini humo na kuuteka. Lakini Ali aliwazuia na kuwashinda kabisa. Hivyo werevu wa Salman, busara za Muhammad na upanga wa Ali vilithubutu kuwa ulinzi bora wa Uislamu dhidi ya muungano wa kutisha wa washirikina katika historia ya Uarabuni.

Ilikuwa ni desturi katika vita za Kiarabu kumpora adui aliyeshindwa silaha zake, mavazi ya chuma - deraya na farasi wake. Katika kuizingira Madina, Amr alikuwa amevaa deraya nzuri sana katika Arabuni yote. Ali alimuua lakini hakugusa kitu chochote ambacho kilikuwa mali yake, kwa mshangao mkubwa sana wa Umar ibn al-Khattab. Baadae, wakati dada yake Amr alipokuja kwenye maiti yake kumlilia kifo chake, yeye pia alishangaa kugundua kwamba silaha zake na mavazi viko salama. Alipoambiwa kwamba alikuwa ni Ali aliyemuua, alitunga beti kadhaa za kumsifia yeye (Ali). Beti hizi zimenakiliwa na yule mwanahistoria wa Misri, Abbas Mahmud Al-Akkad, katika kitabu chake, Al-Abqariyyat Imam Ali (kipaji cha Imam Ali), na zinaweza kutarjumiwa kijuujuu kama ifuatavyo:

"Kama mtu mwingine mbali na Ali angemuua Amr, Ningehuzunikia kifo chake maisha yangu yote. Lakini mtu aliyemuua yeye ni shujaa na hana kifani. Baba yake pia alikuwa ni muungwana."

Akitoa maelezo juu ya mistari hii, Abbas Mahmud Al-Akkad anasema kwamba kabila halikuchukulia kuwa ni fedheha kama mmojawapo wa mashujaa wao aliuawa na Ali. Ali alikuwa ndiye jasiri zaidi na muungwana zaidi kwa maadui, na pia alikuwa asiyeshindika. Baada ya kushindwa kwa kule kuizingira Madina, yale makabila yote kati ya Madina na

166

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Bahari Nyekundu na kati ya Madina na Yammama kwa upande wa Mashariki, yaliweka saini mikataba ya amani na Mtume wa Uislamu.

Katika mwaka huo huo, yaani mwaka wa 5 H.A. (627 A.D.), Hajj (kwenda kuhiji Makka) ilifanywa ni lazima kwa wale Waislamu wote waliokuwa na hali nzuri ya kifedha na walio na afya njema.

167

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Waislamu na Wayahudi

Mnamo mwaka wa 70 A.D. Yule jenerali wa Kirumi, Titus, aliiteka Jerusalem na akakome-sha utawala wa Kiyahudi wa Palestina. Kufuatia utekaji nyara wa Warumi, Wayahudi wengi waliondoka kwenye nchi yao na wakatangatanga kwenye nchi nyingine. Baadhi ya makabila ya Kiyahudi yalivuka jangwa la Syria na kuingia kwenye peninsula ya Arabia ambako waliweka makazi yao huko Hijazi. Baada ya kupita muda walijenga makoloni mengi huko Madina na kati ya Madina na Syria. Wanasemekana pia kwamba waliwabadili Waarabu wengi na kuwaingiza kwenye Ujuda (dini ya Wayahudi).

Mwanzoni mwa karne ya saba A.D., kulikuwa na makabila matatu ya Kiyahudi yaliyokuwa yanaishi Madina (Yathrib). Haya yalikuwa ni Banu Qainuka'a, Banu Nadhir na Banu Qurayza. Makabila yote matatu yalikuwa matajiri na yenye nguvu, na pia, yalikuwa yamestaarabika zaidi kuliko hao Waarabu. Wakati ambapo Waarabu walikuwa wote ni wakulima, hawa Wayahudi walikuwa wawekezaji mali wa viwanda, biashara na uchuuzi katika Arabia, na walisimamia maisha ya kiuchumi ya Madina (Yathrib). Yale makabila mawili ya Kiarabu - Aus na Khazraj - walikuwa wamejawa na madeni kwa Wayahudi daima.

Mbali na Madina, vituo vizito vya Wayahudi katika Hijazi vilikuwa Khaibar, Fadak na Wadi-ul-Qura. Ardhi katika mabonde haya ilikuwa ndio yenye rutuba zaidi katika Arabia yote, na wakulima wake wa Kiyahudi walikuwa ndio wakulima wazuri zaidi katika nchi hiyo.

Kule kuhama kwa Muhammad, Mtume wa Uislamu, kutoka Makka kwenda Madina (wakati huo Yathrib) kulimkutanisha na Wayahudi kwa mara ya kwanza. Hapo mwanzoni walikuwa na urafiki naye. Aliwapa ule mkataba maarufu wa Madina, na wakamtambua yeye kama mtawala wa mji wao, na wakakubali kufuata uamuzi wake katika migogoro yote. Walikubali pia kuulinda mji huo katika kitendo cha kuvamiwa na adui.

Lakini, kwa bahati mbaya, urafiki huu haukudumu kwa muda mrefu. Mara moja ikaonekana wazi kwamba hao Wayahudi walitoa urafiki wao kwa Muhammad kwa masha-ka mengi. Kwa maslahi yao binafsi, walipaswa kutekeleza wajibu wao wa makubaliano kwa uaminifu lakini hawakufanya hivyo. Kwa mabadiliko haya katika tabia zao, kulikuwa na sababu nyingi, miongoni mwao zikiwa:

1. Wakati Muhammad alipowasili Madina, alirekebisha maisha ya Waarabu au yeyote yule aliyeingia Uislamu. Aliwafundisha wao kuwa na msimamo

168

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

wa kadiri na wastani katika kila jambo na akawafundisha thamani ya nid-hamu katika maisha. Waliacha kunywa pombe na kucheza na kamari vyote ambavyo vilikuwa ndio vyanzo vya kuharibikiwa kwao huko nyuma; na waliacha kuchukua mikopo kwa viwango vya juu vya riba kutoka kwa Wayahudi. Pale Waarabu walipoacha kuchukua mikopo na kuitolea riba juu yake, chanzo kikubwa cha mapato kwa Wayahudi ghafla kikakauka, na walilikasirikia sana hili. Waliweza kuona sasa kwamba nguvu yao katika maisha ya kiuchumi ya Madina ilikuwa inaanza kulegea.

2.   Wayahudi pia walitambua kwamba Uislamu ulikuwa ni adui wa mfumo wao wa unyonyaji, na mfumo wa kibepari. Walianza kuuona Uislamu kama ni tishio kwa maslahi yao ya kiuchumi.

3.    Makuhani wa Kiyahudi walimchukia Muhammad kama vile walivyom-chukia wakopesha fedha. Alikuwa amewaonyesha Wayahudi jinsi makuhani wao walivyofuata tafsiri potovu ya maandiko yao, na jinsi walivyochafua vitabu vyao. Makuhani hao, kwa upande wao, walijaribu kuwashawishi waumini wao kwamba Muhammad hakuwa na elimu ya maandiko yao, na walijaribu kuwaonyesha wao "makosa" katika Qur'an

Wayahudi hao pia waliamini kuwa walikuwa salama tu mradi yale makabila mawili ya Madina, Aus na Khazraj, yalikuwa yanapigana yenyewe kwa yenyewe. Amani kati ya Aus na Khazraj, walidhania, italeta tishio kwa maisha yao katika Arabia. Kwa sababu hii, walikuwa daima wakichochea ugomvi kati yao.

Kati ya makabila matatu ya Kiyahudi ya Madina, hawa Banu Qainuka na Banu Nadhir yalikuwa tayari yamefukuzwa baada ya vita vya Badr na Uhud kwa mfuatano wake, na walikuwa wameondoka na mizigo yao, na makundi ya wanyama, na wamefanya makazi huko Khaibar.

Hili kabila la tatu na la mwisho la Wayahudi wa Madina lilikuwa la Banu Qurayza. Kwa mujibu wa masharti ya ule Mkataba wa Madina, ilikuwa ni wajibu wao kuchukua sehemu muhimu katika kuulinda mji huo wakati wa kule kuzingirwa kwa mwaka 627 A.D. Lakini sio tu hawakutoa mtu yeyote au vifaa wakati wa mzingiro bali walikamatwa wakila njama na maadui kuwekea mzingo maangamizi ya Waislamu. Baadhi ya Wayahudi pia walisham-bulia nyumba moja ambayo ndani yake wanawake wengi wa Kiislam na watoto walichukua hifadhi kama ilivyodhaniwa kuwa ni sehemu yenye usalama kwao kuliko kwenye nyumba zao wenyewe. Kama Amr ibn Abd Wudd angeushinda upinzani wa Waislamu, hawa Wayahudi wangewashambulia kwa nyuma. Katikati ya wapagani wa Makka na Wayahudi wa Madina, Waislamu wangeuawa kwa halaiki. Ilikuwa ni kuwepo kwa akili ya Muhammad na kujasiri kwa Ali ambako kulizuia maafa kama haya..

169

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

R.V.C.Bodley

Wale Wayahudi mwanzoni hawakuelekea kulisikiliza pendekezo la Abu Sufyan (la kuwashambulia Waislamu kutokea nyuma), lakini baada ya muda walielewana na wakakubali kuwasaliti Waislamu pale muda utakapoelekea kuwa muafaka.

(The Messenger - the Life of Muhammad)

Tabia ya Wayahudi wakati ule wa mzingiro wa Madina ilikuwa ni uhaini mkubwa dhidi ya Nchi. Kwa hiyo, wakati lile jeshi la muungano lilipovunjika na ile hatari ya Madina ikawa imezuiwa, Waislamu wakaguezia macho yao kwao.

Wale Wayahudi wakajifungia kwenya ngome zao na Waislamu wakawazingira. Lakini siku kadhaa baadae, walimuomba Mtume (s.a.w.) kuondoa mzingiro ule, na wakakubali kupele-ka mgogoro huo kwenye usuluhishi.

Mtume (s.a.w.) aliwaruhusu wale Wayahudi kuchagua msuluhishi wao wenyewe. Hapa walifanya kosa lililowagharimu sana. Wangemchagua Muhammad mwenyewe - aliye mfano halisi wa msamaha - awe hakimu wao. Kama wangefanya hivyo, angeweza kuwaruhusu waondoke Madina na mizigo na wanyama wao, na kadhia hiyo ingefikia mwisho.

Lakini Wayahudi wale hawakumchagua Muhammad kama hakimu wao. Badala yake, wal-imchagua Sa'ad ibn Muadh, kiongozi wa washirika wao wa awali, wale Aus. Sa'ad alikuwa ni mtu asiyejali kabisa maisha yake mwenyewe na ya wengine vilevile.

Sa'ad alipata jeraha baya sana wakati wa vita vya Handaki, na kwa kweli alikufa baada ya kutoa hukumu juu ya majaaliwa ya wale Wayahudi. Aliutaja uhaini kwamba ni kosa lisilosameheka, na hukumu yake ilikuwa kali. Aliitekeleza Taurati, lile andiko la Wayahudi, na akawahukumu wanaume wote kifo, na wanawake na watoto kuwa watumwa. Hukumu yake ilitekelezwa papo hapo.

Wale Wayahudi wa kabila la Qurayza waliuawa kwenye majira ya kuchipua ya mwaka wa 627 A.D. Kutoka tarehe hii, Wayahudi wakakoma kuwa nguvu hai katika maisha ya kiuchumi na kisiasa ya Madina.

170

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mkataba wa Hudaybiyya

Kwa mujibu wa Hadith za Kiislam, ile Al-Kaaba ya Makka ilijengwa na Mitume Ibrahim na mwanae, Ismail. Waliitoa Waqfu kama kituo cha kiroho cha dunia ya waabudu Mungu mmoj a. Na sasa Al-Kaaba ilikuwa ndio "Qibla " cha Waislamu ambacho ina maana kwamba walikuwa wageukie kukielekea wakati wanaposali Swala zao. Lakini walezi wa hiyo Al-Kaaba walikuwa ni wale waabudu masanamu wa Makka, na walikuwa wakiitumia kama hekalu la kitaifa la ushirikina, wakiweka ndani yake masanamu 360 ya makabila yao.

Kwa desturi za kijadi za Kiarabu, kila mmoja alikuwa huru kuitembelea hiyo Al-Kaaba -bila ya silaha. Pia, kwa desturi za jadi, mapigano ya aina yoyote yalikatazwa wakati wa miezi minne mitukufu ya mwaka. Moja ya miezi hii ulikuwa ni Dhilqa'ada, mwezi wa 11 wa kalenda ya Kiislamu.

Waislamu walitamani kuona ilikuwa ni nini kwao, ile Nyumba ya Allah (s.w.t.) Kwa hiyo, katika Dhilqa 'ada ya mwaka wa sita wa Hijiria, Mtume wao alitaarifu kwamba atatembe-lea Makka kufanya Umra au Hija Ndogo - bila ya kuwa na silaha lakini akiwa na wafuasi wake. Kwa dhamira hii, aliondoka Madina mwishoni mwa Februari 628 A.D., pamoja na idadi ya wafuasi wake 1,400. Walichukua ngamia na wanyama wengine kwa ajili ya kafara lakini hawakuwa na silaha yoyote isipokuwa panga zao.

Wakati msafara huu wa mahujaji ulipofika kwenye viunga vya Makka, Mtume (s.a.w.) ali-julishwa kwamba wale waabudu-sanamu hawatamruhusu yeye kuuingia mji huo, na kwamba, watatumia nguvu kumzuia asifanye hivyo. Taarifa hii ilisababisha wasiwasi mkubwa miongoni mwa Waislamu. Walisimama karibu na kisima mahali panapoitwa Hudaybiyya kaskazini ya Makka. Mtume (s.a.w.) alituma ujumbe kwa Maquraishi kwamba alitaka afanye tu ile mizunguko ya kidesturi saba, ya Al-Kaaba, kutoa kafara wanyama wao, na kisha warudi Madina na wafuasi wake. Maquraishi hawakukubali. Ujumbe mwin-gi tena ulitumwa lakini Maquraishi walisema kwamba hawatawaruhusu Waislamu kuingia Makka.

Hatimae, Mtume (s.a.w.) alimuamuru Umar ibn al-Khattab kwenda Makka kuwaelezea wale waabudu-masanamu madhumuni ya safari ile ya Waislamu, kuwahakikishia wao kwamba Waislamu hawakuwa na nia ya kupigana dhidi ya mtu yoyote yule, na kuwapa ahadi kwamba baada ya kufanya taratibu (ibada) za Umra wataondoka Makka mara moja na watarudi Madina.

Lakini Umar alikataa kwenda. Alisema hakuna mtu huko Makka wa kumlinda yeye. Alishauri, hata hivyo, kwamba Mtume (s.a.w.) angemtuma Uthman bin Affan na ujumbe wake kwenda Makka kwa vile wale waabudu masanamu hawatamfanyia madhara yoyote.

171

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Sir William Muir

Mjumbe wa kwanza kutoka kambi ya Waislamu kwenda Makka, mtu aliyesilimu kutoka kabila la Bani Khuzaa, Maquraishi walimkamata na kumfanyia ukatili; wakamtia kilema ngamia wa Mtume (s.a.w.) ambaye alikuwa amempanda, na hata kumtishia maisha yake. Lakini hasira sasa zilikuwa zimetulia zaidi, na Muhammad alitaka Umar aende Makka kama balozi wake. Umar alijipa udhuru mwenyewe kwa sababu ya uadui binafsi wa Maquraishi juu yake; alikuwa, zaidi ya hayo, hana ndugu wenye uwezo hapo mjini ambao wangeweza kumkinga kutokana na hatari; na alielekeza kwa Uthman kama mjumbe anayefaa zaidi.

(The Life of Muhammad, 1877) S. Margoliouth.

Wakati huu ilikusudiwa kutuma mwakilishi kwenda Makka, lakini ule utambuzi kwamba wengi wa Waislamu walikuwa na madoa ya damu ya Makka, uliwafanya wale mashujaa wa Uislamu wasiwe tayari kuhatarisha maisha yao kwenye safari hii fupi; hata Umar, ambaye kwa kawaida alikuwa tayari kabisa na upanga wake, alirudi nyuma. Hatimae mkwewe Mtume, Uthman bin Affan, ambaye alichagua kumuuguza mkewe badala ya kupigana huko Badr, alitumwa kama mjumbe anayekubalika humo...

(Muhammad and the Rise of Islam, 1931)

Ni ajabu kabisa kwamba Umar hakuwa tayari kuhatarisha maisha yake kwa kutembelea Makka. Hapakuwa na hatari yoyote iliyohusika juu yake kwa sababu hakuwa mmojawapo wa wale Waislamu ambao "walitiwa doa na damu ya Makka." Kwa vile Umar hakuua mtu yeyote wa Makka, atakuwa ni mtu anayekubalika kwa hawa waabudu masanamu kwa nyakati zote. Kukataa kwake kutii amri ya Mtume wa Allah (s.a.w.) kwa hiyo, hakuelewe-ki.

Umar hakwenda Makka. Hata hivyo, alilitatua tatizo hilo kwa kumtoa mshika nafasi yake, Uthman bin Affan. Badala yake, kwa hiyo, Uthman alitumwa Makka kufanya mazungum-zo na Maquraishi. Kama Umar mwenyewe, Uthman pia hakuwa na doa la damu ya pagani yeyote.

Waabudu masanamu hao walimkaribisha Uthman na wakamwambia yeye kwamba alikuwa huru kufanya hiyo Umra. Lakini alisema kwamba yeye peke yake hataweza kufanya Umra, na kwamba walikuwa wamruhusu Mtume (s.a.w.) na Waislamu wote waliokuwa pamoja naye, kuingia mjini humo. Hili halikukubaliwa na Maquraishi, na ilielezwa kwamba walimkamata yeye. Ilinong'onwa pia kwamba walimuua.

172

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Wakati tetesi la kuuawa kwa Uthman zilipomfikia Mtume, alikitafsiri kitendo hicho cha Maquraishi kama makataa (kauli ya mwisho), na akawataka Waislamu kutoa upya kiapo chao cha utii kwake. Waislamu wote wakatoa kiapo chao cha utii kwa Mtume wa Allah (s.a.w.) bila kujali matukio yanayoweza kutokea baada ya hapo.

Kiapo hiki kinaitwa "Kiapo cha Ridhwan" au "Mkataba wa Uaminifu," na wale Waislamu waliokitoa, wanaitwa "Masahaba wa chini ya mti," kwa sababu Mtume (s.a.w.) alisimama chini ya mti walipokuwa wakipita kwa safu mbele yake wakitoa upya kiapo chao cha utii kwake. Idadi yao imetajwa kuwa 1,400.

Uamuzi huu wa Waislamu wa kujasiri matokeo unaonekana kuwaweka Maquraishi katika hali ya akili ya kutosha, kwa vile walivyotambua kwamba ukaidi wao unaweza kus-ababisha umwagaji damu usio wa lazima. Uthman, ilitokea kwamba, hakuwa ameuawa kama ilivyotetwa bali alikuwa amekamatwa tu, na sasa wakamuachilia - kitendo kinacho onyesha mabadiliko katika msimamo wao. Pia kuonyesha mabadiliko haya kulikuwa ni ule uchaguzi wao mtu mmoja, Suhayl bin Amr, ambaye walimtuma kwenye kambi ya Waislamu kukamilisha mkataba na Mtume wa Uislamu. Suhayl alikuwa ni mtu aliyeju-likana kama mpatanishi hodari lakini hakuwa madhubuti.

Suhayl aliwasili Hudaybiyya na kufungua majadiliano na Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) Baada ya mazungumzo marefu na mjadala wenye kuchosha walifanikiwa katika kufikia mkataba, ambao masharti yake muhimu sana yalikuwa kama yafuatayo:

1. Muhammad na wafuasi wake watarudi Madina bila ya kutekeleza Umra (Hija Ndogo) ya mwaka ule.

2.  Kutakuwa na amani kati ya Waislamu na Maquraishi kwa kipindi cha miaka kumi kutoka tarehe ya kusaini mkataba huo.

3. Kama mtu yeyote wa Makka ataukubali Uislamu na kutafuta hifadhi kwa Waislamu huko Madina, watamrejesha Makka. Lakini kama mwislamu, aliyekimbia kutoka Madina, akitafuta hifadhi kwa wapagani wa Makka, hawatamrejesha.

4. Makabila yote ya Arabia yatakuwa huru kuingia kwenye mahusiano ya mkataba na kundi lolote - Waislamu ama Maquraishi.

5. Waislamu watatembelea Makka kufanya hijja katika mwaka unaofuata lakini hawatakaa katika mji huo kwa zaidi ya siku tatu, na silaha pekee ambazo wataruhusiwa kuja nazo, zitakuwa ni panga zao ndani ya ala zao.

173

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mkataba huu unaitwa Mkataba wa Hudaybiyya. Ndio nyaraka ya kisiasa maarufu sana katika historia ya Uislamu. Katibu aliyechaguliwa kuandika masharti yake alikuwa ni Ali ibn Abi Talib.

Wakati Mkataba wa Hudaybiyya ulipokuwa unaandikwa, lilitokea tukio ambalo linatoa kiangaza kinachofichua juu ya tabia za baadhi ya waongozaji waliohusika katika kurasimu masharti yake.

Akitoa imla kwa Ali, Mtume (s.a.w.) alisema: "Andika, Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu." Suhayl, yule mjumbe wa Makka, mara moja akatoa pingamizi, na akasema, "Usiandike hivyo. Badala yake, andika, 'Kwa Jina Lako Ewe Allah'" Mtume (s.a.w.) akakubaliana na madai haya.

Mtume (s.a.w.) tena akamwambia Ali aandike: "Huu ni mkataba wa amani kati ya

Muhammad, Mtume wa Allah na Maquraishi.." Suhayl tena akapinga, na akasema:

"Kama tumekukubali wewe kama mjumbe wa Allah kwa nini tuwe tunapigana dhidi yako? Kwa hiyo, usiandike hayo maneno, 'Mtume wa Allah' na andika jina lako mwenyewe tu na jina la baba yako."

Mtume (s.a.w.) alikuwa ameridhia kukubaliana na dai hili pia lakini Ali alikuwa amek-wisha andika tayari maneno haya, "Muhammad ni Mtume wa Allah." na alikataa kuyafu-ta. Alimwambia bwana wake: "Hiki cheo cha juu kimewekwa juu yako na Allah (s.w.t.) Mwenyewe, na sitayafuta kamwe haya maneno 'Mtume wa Allah (s.a.w.) .' kwa mkono wangu." Kwa sababu hiyo, Mtume (s.a.w.) akaichukua ile kalamu mkononi mwake mwenyewe, na akayafuta yale maneno ambayo yalikuwa ni yenye kuchukiza kwa wale waabudu masanamu.

Huu Mkataba wa Hudaybiyya ulisainiwa katika nakala mbili, moja kwa kila upande. R.V.C.Bodley

Ile karatasi ya awali ya Mkataba wa Hudaybiyya ilibakia na Muhammad ambapo nakala yake ilikabidhiwa kwa Suhayl kwa uhifadhi wa salama katika hifadhi ya nyaraka ya Makka.

(The Messenger - the Life of Muhammad, 1946)

Huko Makka viongozi wa Maquraishi waliukaribisha ule Mkataba wa Hudaybiyya kama ushindi wa werevu wao. Walichukulia kwamba Muhammad ameshindwa ujanja na kwam-ba mkataba huo ulikuwa ni sawa na, hata kama sio tangazo rasmi la, "kusalimu amri." Maquraishi walifurahia sana juu ya kile walichofikiria ni kusalimu amri kwa adui lakini matukio yalikuwa mara tu yaonyeshe kwamba walikuwa wamekosea. Mbali kabisa na

174

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kuwa ni kusalimu amri, ule Mkataba wa Hudaybiyya ulikuwa ni mmojawapo kati ya ushin-di mkubwa sana wa Uislamu.

Miongoni mwa wafuasi wa Mtume, hata hivyo, ule Mkataba wa Hudaybiyya ulikuwa uzae hisia zenye mzozo mkali sana. Kwa namna ya kipekee. Kama vile walivyokuwa wale wapagani wa Makka, wale "wazalendo wapofu" katika kambi ya Waislamu pia waliulin-ganisha na "kusalimu amri." Waliongozwa na Umar ibn al-Khattab. Aliyaona masharti yake ni "yenye kufedhehesha," na alikuwa amesikitishwa sana nayo kiasi kwamba alimgeukia Abu Bakr kwa majibu ya maswali yake, na mahojiano yafuatayo yalifanyika kati yao:

Umar: Hivi yeye (Muhammad) ni Mtume au sio Mtume wa Allah? Abu Bakr: Ndio. Yeye ni Mtume wa Allah. Umar: Sisi ni Waislamu au sio Waislamu? Abu Bakr: Ndio. Sisi ni Waislamu.

Umar: Kama sisi ni Waislamu, basi ni kwa nini tunasalimu amri kwa wapagani katika jambo linalohusu imani yetu?

Abu Bakr: Yeye ni Mtume wa Allah. na wewe usiingilie katika jambo hili.

Ufidhuli wa Umar ulishadidi kwa kiwango cha juu baada ya kuaswa na Abu Bakr, na akaenda kumuona Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Baadae alisema: "Nilikwenda mbele ya Mtume, na nikamuuliza: 'Wewe sio Mtume wa Allah?' akanijibu, 'Ndio, mimi ndimi.' Nikauliza tena: 'Sisi Waislamu hatuko sahihi, na wale washirikina hawako kwenye makosa?' Akajibu, 'Ndio, hivyo ndivyo.' Niliuliza zaidi: 'Basi ni kwa nini tunaonyesha unyonge zaidi kwao? Hata hivyo sisi tunalo jeshi. Kwa nini tunafanya amani nao?' Akasema: 'Mimi ni Mtume wa Allah (s.w.t.) na ninafanya kile tu Anachoniamrisha kufanya."

Lakini inaonekana Umar hakuridhika hata na majibu ya Mtume (s.a.w.) mwenyewe kwa maswali yake. Yale masharti ya Mkataba wa Hudaybiyya yamesababisha wasiwasi mkubwa katika akili yake, hivyo alisema: "Nilirudia rudia kumuuliza Mtume (s.a.w.) kuhusu yale masharti ya mkataba huu, na sijawahi kamwe kuongea naye kwa namna hii."

Sir John Glubb.

Wengi wa Waislamu walivunjwa moyo na matokeo ya Hudaybiyya, wakiwa walitara-jia uingiaji kwa ushindi ndani ya Makka. Umar ibn al-Khattab, kama kawaida, alita-

175

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

mka hasira zake, 'Huyu siye Mtume wa Allah, na sisi sio Waislamu na wao sio washirikina?' alitaka kujua kwa hasira kutoka kwa Abu Bakr mpole na mwaminifu. 'Kwa nini tusipigane nao; kwa nini tuafikiane hivyo?'

(The Great Arab Conquests)

Tor Andre

Umar aligeukia kwa taharuki kwa Abu Bakr na viongozi wengine waliokuwa karibu na Mtume (s.a.w.) kuhakikisha kama kweli walidhamiria kuridhia fedheha hii (ingawa sio kweli). Alitamka baadae kwamba kamwe kabla ya hapo hajawahi kuwa na mashaka kuhusu ukweli wa Muhammad, na kama angepata angalau watu mia moja wenye mawazo kama hayo, angejiuzulu kwenye umma wa Kiislam.

(Muhammad - the Man and his Faith)

Maxime Rodinson

Umar na baadhi ya wengine walikasirikia lile wazo la kufanya maafikiano na hawa wapagani. Huyu khalifa wa baadae alikuja kumlaumu Mtume. Alitamka baadae kwamba kama angekuwa na watu mia moja upande wake, angejitoa. Lakini Muhammad alikuwa hatingishiki.

(Muhammad, kilichotafsirwa na Anne Carter)

R.V.C.Bodley

Wengi wa wale mahujaji, na Umar hasa, waliaibika sana kwamba Muhammad ame-wakubalia Maquraishi katika karibu kila jambo. Ilionekana ni ajabu kwao kwamba, baada ya kuletwa umbali wote huu na kiongozi wao ambaye hakuwa na woga wa kumuandama adui ambaye alimshinda yeye, wasimamishwe nje ya lengo lao. Ilielekea kushangaza zaidi kwamba amejishusha mwenyewe mbele ya yule mjumbe wa Makka kwa kiasi cha ama kumwita Mola wake kwa jina Lake halali wala kutumia cheo chake mwenyewe, kwa sababu tu yule kafiri amedai hivyo. Umar alifikia kiasi cha kuuliza: "Wewe kweli ni Mtume wa Allah?" Umar alikwenda kuona ni nini Waislamu wengine walichohisi. Aliwakuta wao katika hali hiyo hiyo ya mawazo kama aliyokuwa nayo. Kwa mara ya kwanza tangu Uislamu uanze, kulikuwa na dalili za uasi.

(The Messenger - The Life of Muhammad)

Umar alitamka baadae kwamba tangu aliposilimu, hajawahi kuwa na mashaka kama hayo juu ya ukweli wa Muhammad kama aliyokuwa nayo ile siku Mkataba wa Hudaybiyya uli-posainiwa.

176

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hii ina maana kwamba Umar alikuwa akisumbuliwa na mashaka ya mara kwa mara kuhusu ukweli wa Muhammad na ujumbe wake wa Utume. Yumkini alikuwa akiyazuia kila wakati yalipojitokeza. Lakini kwenye kigezo cha kuthibitisha uasili wake cha Mkataba wa Hudaybiyya, mashaka yake sugu yaliibuka kwa nguvu kali mno kiasi kwamba hakuweza kuyazima. Akitawaliwa na mashaka yake, yeye kwa kweli alifikiria kuuacha udugu wa Kiislamu wenyewe lakini hakuweza kumpata mtu yoyote kwenye kambi hiyo ambaye angeweza kumsaidia kumuunga mkono katika "ujasiri" wake.

Mwelekeo wa mapokezi ya Sunni umekuwa kwamba katika kuonyesha ufedhuli na dharau kwa Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (rehma na amani juu yake na Ahlul-Bait wake), Umar alichochewa na mapenzi yake kwa Uislamu. Kwa mujibu wao, aliupenda sana Uislamu kiasi kwamba "alijisahau." Mwanzoni, alikataa kutii amri ya Mtume (s.a.w.) ya kupeleka ujumbe kwa Maquraishi huko Makka. Kukataa kule, yumkini, kulichochewa na mapenzi hayo hayo.

Wale watu wanaohusisha unafiki wa Umar na mapenzi yake kwa Uislamu, kwa kweli, wanamaanisha kwamba yeye aliupenda Uislamu zaidi kuliko Muhammad, Mtume wa Uislamu mwenyewe alivyoupenda! Pia, kwa tabia yake, alikuwa anamaanisha kwamba Mtume wa Allah (s.a.w.) alikuwa anakosea katika kutafuta amani na Maquraishi lakini yeye mwenyewe alikuwa sahihi, na kwamba ilikuwa ni wajibu wake "kumsahihisha" yeye Muhammad Mustafa.

Kama siku moja hivi kabla, Umar alitoa kiapo cha "kumtii Mtume wa Allah (s.a.w.)" katika hali yoyote ile, kwenye amani na kwenye vita, kwenye neema na kwenye dhiki. Ilikuwa pengine ni kiapo hiki kilichomsukuma kujionyesha yeye binafsi kuwa ni "mfuasi" bora zaidi (wa Uislamu) kuliko "mfalme" mwenyewe (Mtume)!

Kama ni sadfa kwamba wote, Maquraishi wa Makka, na Umar na wafuasi wake katika kambi ya Waislamu, walisoma, "kusalimu amri" kwa Waislamu, katika Mkataba ule wa Hudaybiyya, basi kweli ilikuwa ni ajabu. Lakini kama vitisho vya kijeshi vya Umar vingeishia kwenye kuonyeshana nguvu na Maquraishi, basi mtu anaweza kukisia ni sehe-mu gani angeishughulikia ndani yake, akimpima kutokana na "kumbu kumbu ya matendo" yake mwenyewe, ya kabla na baada.

Akiandika juu ya huu Mkataba wa Hudaybiyya, Lt. Jenerali, Sir John Glubb anasema katika kitabu chake, "The Life and Times of Muhammad":

Madukuduku yaliyovumiliwa na Waislamu pale Hudaybiyya yanadhihirishwa na namna ambavyo zile siku za wasiwasi zilivyobakia zimeganda kwenye kumbukumbu zao. Miaka mingi baadae, wakati majeshi ya Waislamu yalipokuwa tayari yamejenga himaya kubwa, wakati marafiki wakongwe wakizungumzia zile siku za mwanzoni,

177

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

heshima kubwa kabisa ilionyeshwa daima kwa wale watu ambao walipigana kule Badr na kwa wale waliokula kiapo pale Hudaybiyya - ile migogoro miwili mizito ya mwanzo wa Uislamu.

(The Life and Times of Mohammed)

Hapakuwa na yeyote miongoni mwa maswahaba wote wa Muhammad Mustafa ambaye alikuwa na mwenendo wa kiheshima, kote katika vita vya Badr na pale Hudaybiyya, na kwa kweli, katika nyakati zote za hatari katika historia ya Kiislamu, kama Ali ibn Abi Talib. Huko nyuma, alijitokeza mwenyewe kuwa wa kwanza katika vita; huko Hudaybiyya kila mmoja aliona kwamba alikuwa pia wa kwanza katika amani. Amedhihirisha mara nyingi katika vita kwamba alikuwa na imani kamili juu ya Muhammad na ujumbe wake, na sasa alikuwa anadhihirisha katika amani kwamba hakuna chochote ambacho kinaweza kamwe kutingisha imani yake juu ya bwana wake.

Baada ya kuondoka kwa wale wajumbe wa Makka, Mtume (s.a.w.) aliwaamuru Waislamu kunyoa vichwa vyao na kuchinja wanyama wao kama kafara, kama kanuni za Umra. Lakini alishtuka kuona kwamba wengi wao walikuwa katika hali ya uasi na hawakutaka kutii amri zake.

Kilichotokea hasa ni kwamba, Umar alimdharau hadharani Mtume wa Allah (s.a.w.) na kwa mfano wake huo, amewatia moyo wafuasi wake pia kufanya vivyo hivyo. Mtume (s.a.w.) aliingia kwenye hema lake, na akamwambia mkewe kwamba Waislamu walikuwa wanakaidi amri zake. Mkewe akasema kwamba kama angewapuuza hao, na akatekeleza kazi hiyo yeye binafsi, watamfuatisha yeye.

S. Margoliouth

Waislamu walinuna kimya wakati walipoambiwa na Muhammad wanyoe vichwa vyao na kutoa makafara yao. Mwishowe (kwa ushauri wa mkewe, Ummu Salamah), alitekeleza wajibu huo yeye binafsi, na wafuasi wake wakafanya vivyo hivyo.

(Muhammad and the Rise of Uislamu)

Kazi yake ilipokamilika, Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliondoka Hudaybiyya na wale mahujaji, ili kurudi Madina. Alikuwa bado katika safari ya siku saba kutoka Madina, wakati wahy ufuatao ulipokuja kutoka Mbinguni:

178

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hakika tumekupa ushindi wa dhahiri (Sura ya 48; Aya ya 1)

Ulikuwa ni ule Mkataba wa Hudaybiyya ambao huu wahy mpya umeuita "Ushindi wa dhahiri." Amin Dawidar, yule mwanahistoria wa Kimisri, ameandika katika kitabu chake Pictures From the Life of the Prophet (Cairo, 1968 uk.465) kwamba wakati Mtume wa Allah (s.a.w.) alipotangaza rasmi huu wahy mpya unaoitwa "Ushindi," Umar ibn al-Khattab alikuja kumuona, na akauliza: "Huu ndio unaouita Ushindi wa Dhahiri?" "Ndio," akasema Mtume wa Allah (s.a.w.) "kwa Yule Ambaye mikononi Mwake yamo maisha yangu, huu ni Ushindi wa Dhahiri."

Mkataba wa Hudaybiyya ulikuwa kweli ni "Ushindi wa Dhahiri" kama maendeleo ya mfu-lulizo wa matukio ya historia yalivyokuwa yaonyeshe, licha ya ajizi juu yake ya Waislamu wengi katika kambi ya Mtume.

Muhammad Mustafa alikuwa ni Mtume wa amani. Kama angeruhusu mashinikizo ya wale "wazalendo wapofu" katika kambi yake kutumia mbinu za mabavu, ujumbe wake wote ungekuwa hatarini, na vizazi vya wakati ujao vingemshitaki rasmi kwa kupenda kwake "ugomvi." Lakini alikataa mashinikizo ya kuvutiwa kwenye usuluhishi wa silaha, na badala yake, alivutiwa na usuluhishi wa amani, na akapata matokeo ambayo hakuna ushindi wa kijeshi ambao ungeweza kuyapata.

Mkataba ya Hudaybiyya ulikuwa ni matunda ya ustadi wa utawala wa majaaliwa na kipa-ji cha kisiasa cha hali ya juu sana. Ulileta manufaa makubwa sana kwa Uislamu. Miongoni mwao:

1. Maquraishi wa Makka walimkubali Muhammad kuwa ni sawa na wao. Kabla ya hapo walimuona kama muasi na mkimbizi wa kisasi chao.

2. Kwa kuuweka saini mkataba huo, Maquraishi walitoa utambuzi wa kimya wa ile Dola ya Kiislam ya Madina inayochipukia.

3. Wale Waislamu waliokuweko Makka, walificha imani yao mbele ya waabudu masanamu kwa hofu ya mate so kutoka kwao. Lakini baada ya Mkataba wa Hudaybiyya, walianza kutekeleza Uislamu hadharani.

4. Hadi mwaka wa 6 A.H. Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) alikuwa amefungwa katika mapambano yasiyokwisha na wapagani wa Kiarabu na Wayahudi, na hapakuwa na fursa kwa ajili yao ya kuuona Uislamu katika

179

Usahihi-13.jpg

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

matendo. Baada ya Mkataba wa Hudaybiyya waliweza "kuutathmini" Uislamu kwa mara ya kwanza. "Tathmini" hii ilisababisha kusilimu kwa wengi wao, na Uislamu ukaanza kuenea kwa kasi sana. Mkataba wa Hudaybiyya ulifungua milango ya kubadilisha-dini.

5. Makabila mengi ya Kiarabu, ingawa bado wapagani, yalitaka kuingia mikataba ya uhusiano na Waislamu lakini yalijihisi kuzuiwa na upinzani wa Maquraishi. Sasa yaliachiwa uhuru wa kufanya ushirikiano na Waislamu.

6. Mkataba wa Hudaybiyya ni jibu zuri sana kwa wale wakosoaji wanaodai kwamba Uislamu ulienea kwa ncha ya upanga. Hakuna uthibitisho bora zaidi kuliko Mkataba wa ukataaji huu wa vita kwa Muhammad, kama chombo cha sera, na cha mapenzi yake halali ya amani. Wapagani wa Kiarabu walivutiwa sana na propaganda za Maquraishi kwamba Muhammad alitamani sana vita. Sasa waliweza kuona kwa macho yao wenyewe kwamba Muhammad alirudi Madina bila hata ya "kulipiza," ingawa alikuwa na jeshi pamoja naye, na ingawa aliwahi kuwashinda hao Maquraishi mara mbili - mnamo mwaka 624 na 627.

Huu Mkataba wa Hudaybiyya pia unaonyesha chuki ya Qur'an juu ya vita. Kabla ya mkataba, Waislamu walikuwa wamekwisha kushinda zile vita mbili za kihistoria za Badr na Ahzab (Handaki). Kama wangeshindwa katika yoyote kati ya hizo, Uislamu ungetowe-ka kabisa daima kutoka kwenye uso wa dunia. Ushindi katika vita vyote hivi viwili uli-hakikisha uhai wa kivitendo wa Uislamu. Machoni mwa Qur'an, miongoni mwa kampeni zote za Muhammad, ule Mkataba wa Hudaybiyya pekee ndio ulikuwa "Ushindi wa Dhahiri".

Mkataba wa Hudaybiyya ulikuwa ndio utangulizi wa kwenye ushindi wa Uislamu dhidi ya nguvu za upagani, ushirikina, uabudu masanamu, ujinga, dhulma na unyonyaji. Umar ibn al-Khattab alileta kiburi kwenye sharti la tatu la Mkataba huo kwa vile lilikuwa halikubaliani; lakini ilikuwa, kwa usahihi kabisa, ni sharti hili hasa lililowaweka Maquraishi kwenye kujihami mara moja tu, na walikuja kwa kuomba kwa Mtume (s.a.w.) alibatilishe.

Miezi kumi na nane baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa Hudaybiyya, Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliingia Makka, kama mshindi, na alifuatana na waumini elfu kumi. Kutekwa kwa Makka kulikuwa ni matokeo ya moja kwa moja ya Mkataba huu. Kwa sababu ya matokeo haya, wanahistoria wengi wameuita kwa usahihi kabisa huu Mkataba wa Hudaybiyya kama ubingwa wa ustadi wa utawala wa Muhammad.

180

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Marmaduke Pichthall.

Kulikuwa na mfazaiko miongoni mwa Waislamu juu ya masharti haya (ya Mkataba wa Hudaybiyya). Waliulizana wenyewe kwa wenyewe: 'Uko wapi huo ushindi ambao tuliahidiwa?' Ilikuwa ni wakati wa safari ya kurudi kutoka al-Hudaybiyya ambapo ile Sura inayoitwa ushindi iliteremshwa. Makubaliano haya (ya kusitisha vita) yalithibitika, kwa kweli, kuwa ndio ushindi mkubwa ambao Waislamu mpaka hapo walikuwa wameupata. Vita vilikuwa ni kipingamizi kati yao na waabudu masanamu, lakini sasa marafiki walikutana na kuongea pamoja, na dini hii mpya ikae-nea kwa haraka sana. Katika miaka miwili iliyopita kati ya kusainiwa kwa makubaliano hayo na kuanguka kwa Makka, idadi ya waliosilimu ilikuwa kubwa zaidi kuliko jumla ya idadi ya wote waliokuwa wamesilimu hapo kabla. Mtume (s.a.w.) alisafiri kwenda al-Hudaybiyya na watu 1400. Miaka miwili baadae, wakati watu wa Makka walipoyavunja makubaliano hayo, alikwenda dhidi yao pamoja na jeshi la watu 10,000.

Introduction to the translation of Holy Qur 'an, 1975)

Kanuni mbili muhimu za Kiislamu zinaweza kuonekana katika utekelezaji wake ndani ya Mkataba wa Hudaybiyya, yaani:

1. Vita lazima iepukwe kwa gharama yoyote ile, labda ikiwa haizuiliki kabisa. Ufumbuzi wa matatizo yote lazima utafutwe na kupatikana kwa njia za amani, kwa kweli bila kuzihatarisha kanuni za Kiislamu. Kwa wapagani na Waislamu wengi, ilionekana kwamba Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) , ametoa "mamlaka kamili" kwa Suhayl, yule mjumbe wa Makka, kwa hiyo kwamba yeye (Suhayl), kwa namna fulani, alitamka masharti yake mwenyewe. Licha ya kujitokeza kama huko, Mtume (s.a.w.) aliyakubali masharti yale. Bila shaka, hapakuwa na hatari kwenye kanuni yoyote. Ilikuwa haiwaziki kwamba Mtume wa Uislamu atapingana na kanuni yoyote ya Kiislamu.

2. Mtume wa Allah (s.a.w.) . hana lazima ya kukubali kushindwa (kwa kus-tahi) na maoni au matakwa ya wafuasi wake, au ya watu kwa jumla. Idadi kubwa sana ya maswahaba zake Muhammad walikuwa hawakubaliani na kutiwa saini kwa Mkataba wa Hudaybiyya. Lakini alipuuza upinzani wao, na akaendelea na kuusaini. Yeye, kwa kweli , wala hakutafuta hata ushauri wa hata mmoja wao katika suala hilo. Kutoka mwanzo mpaka mwisho, aliongozwa, sio na matakwa ya "watu" au matakwa ya "wingi" wa watu bali na amri za Allah (s.w.t.) zilizohifadhiwa katika Kitabu Chake, makhsusi kwenye Aya ifuatayo:

181

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Usahihi-14.jpg

Na wahukumu baina yao kwa aliyoyateremsha Allah, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyokuteremshia Allah. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Allah anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi wa watu ni wapotofu. (Sura ya 5; Aya ya 49)

182

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ushindi wa Khaybar

Khaybar ni mji ulioko maili 90 kaskazini ya Madina, ndani ya harra au eneo la volkano, lililo na maji mengi na chemchemu zinazotoka kwenye mawe yake meusi ya msingi ya volkano. Lina mfumo mzuri wa umwagiliaji na linatoa mavuno mengi ya tende na nafaka.

Nyuma kabisa kabla ya wakati wa Mtume wa Uislamu, bonde la Khaybar na mabonde mengine upande wa kaskazini na Kusini, yalikuwa chini ya ukoloni wa Wayahudi. Kama ilivyooneshwa kabla, Wayahudi hawa hawakuwa tu ndio wakulima wazuri wa nchi hiyo, walikuwa pia ni wenye kuongoza katika viwanda na biashara, na walimiliki ukiritimba wa viwanda vya silaha.

Katika nyakati za Mtume, viwanda vizuri vya zana za vita katika Arabia vilikuwa vyote vipo Khaybar. Wale Wayahudi ambao walifukuzwa kutoka Madina, walikuwa pia wameweka makazi huko Khaybar, na walikuwa wanatambulika kwa ustadi wao katika ufuaji-chuma.

Betty Kelen

Hawa Qaynuka walifukuzwa kutoka Madina. Aghalabu walikuwa ni wafuachuma, wakiwa wamejifunza ile sanaa ya kufua deraya bora na zenye kumeremeta, panga zenye umbo la mwezi na helimeti za kuzuia jua ambazo zilifaharisha vita humo jang-wani. Walitengeneza dereya nzuri za shaba nyeusi, zilizofuliwa na kung'arishwa, pamoja na helmeti za kufanana, na panga zinazomeremeta ambazo makato yake makali yanaweza kuifanya hewa kuvuma kwa mlio.

(Muhammad - the Messengeer of God)

Wayahudi wa Khaybar pia walisikia habari kuhusu huo Mkataba wa Hudaybiyya na masharti yake. Kama vile tu Maquraishi wa Makka na Umar bin al-Khattab na baadhi ya "wapenda vita" wengine miongoni mwa Waislamu kule Madina walivyoutafsiri huo mkataba kama "kusalimu amri" kwa Waislamu, ndivyo hivyo pia walivyouona wale Wayahudi wa Khaybar kama ni dalili ya mwanzo ya kuanguka kwa mamlaka ya Nchi ya Madina. Wakitegemea hii nadharia ya "kuanguka," walianza kuyashawishi yale makabila ya Waarabu kati ya Khaybar na Madina kuwashambulia Waislamu. Moja ya makabila haya lilikuwa lile la Ghatafan, marafiki wa Wayahudi wa Khaybar.

Walianza kupeleka misafara yao ya mashambulizi kule kwenye mbuga za malisho karibu na Madina. Moja ya malisho haya yalikuwa ni ya Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Katika safari moja, mtoto wa Abu Dharr al-Ghiffari alikuwa anachunga ngamia wa Mtume (s.a.w.)

183

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

wakati hawa Ghatafan waliposhambulia. Wakamuua, na kumteka mama yake ambaye alikuwa pamoja naye, na wakaliswaga pamoja nao lile kundi la ngamia. Waislamu, hata hivyo, waliweza, wakati ule ule tu, kuwakuta wale majambazi na kumuokoa mke wa Abu Dharr al-Ghiffari.

Muhammad aliamua kukomesha uchokozi huu usio na sababu. Alifikiria kwamba hau-takuwa uangalifu kungoja mpaka hao Wayahudi na washirika wao waweke mzingiro mwingine hapo Madina, na kwamba ingekuwa vizuri kuwawahi mapema. Yeye, kwa hiyo, aliwaamuru Waislamu kujikusanya na kuelekea Khaybar.

Mnamo Septemba 628 Mtume (s.a.w.) aliondoka Madina na askari 1600. Baadhi ya wanawake wa Kiislam pia waliandamana na jeshi hilo kwenda kufanya kazi kama wauguzi na kutoa huduma ya kwanza kwa wale walioumia na wagonjwa

Khaybar ilikuwa na ngome nane. Imara zaidi na mashuhuri zaidi ya zote ilikuwa ni ile ngome ya al-Qamus. Kapteni wa askari walinzi wake alikuwa ni shujaa maarufu aliyekuwa akiitwa Mehrab. Alikuwa na, chini ya uongozi wake, wale wapiganaji wazuri wa Khaybar, na walikuwa ni askari waliokuwa na silaha bora wa wakati huo katika Arabia yote.

Muhammad Husein Haykal

Vile vita vya Khaybar vilikuwa moja ya vita kubwa. Idadi kubwa ya Wayahudi waliokuwa wakiishi Khaybar walikuwa ndio wenye nguvu zaidi, matajiri zaidi, na waliojiandaa vizuri zaidi kwa vita kati ya watu wote wa Arabia.

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Waislamu, hata hivyo, waliweza kuzikamata ngome zote za Khaybar isipokuwa al-Qamus ambayo ilithibiti kuhimili mashambulizi. Muhammad alimpeleka Abu Bakr katika wakati mmoja, na Umar katika wakati mwingine, na wapiganaji waliochaguliwa, kujaribu uteka-ji wa al-Qamus. Wote walifanya hilo jaribio na wote walishindwa. Baadhi ya Makapteni wengine walijaribu pia kuiteka ngome hiyo lakini wao pia walishindwa. Huku kushindwa kwa marudio rudio kulianza kuhujumu ile hamasa ya jeshi hilo.

Muhammad alitambua kwamba jambo la kutia shauku lazima lifanyike ili kurudisha ile hamasa ya Waislamu inayonywea, na iwe mara moja. Na wakati jaribio jingine zaidi la kuiteka al-Qamus lilipoharibika pia, akili yake ilipata uamuzi, na akatangaza: "Kesho nita-toa bendera ya Uislamu kwa shujaa ambaye anampenda Allah (s.w.t.) na Mtume Wake, na ambaye Allah (s.w.t.) na Mtume Wake wanampenda yeye. Ni mtu anayemshambulia adui lakini hakimbii, na yeye ataiteka Khaybar."

Masahaba walijua kwamba utabiri wa Mtume wa Allah (s.a.w.) utatokea kuwa kweli, na

184

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kwamba Khaybar itatekwa katika siku inayofuata. Kila mmoja wao, kwa hiyo, aligeuka kuwa mgombea wa sifa na heshima ya kuiteka Khaybar. Wengi wao walikaa macho usiku mzima kwa tamaa ya kuwa "mpendwa wa Allah (s.w.t.) na Mtume Wake," na kuwa shujaa atakayeiteka Khaybar.

Asubuhi iliyofuata, maswahaba walijikusanya mbele ya hema la Mtume. Kila mmoja wao alikuwa amejipamba katika mavazi ya kijeshi, na alikuwa akichuana na wengine katika kuonekana mwenye kuvutia zaidi.

Wakati huo, Mtume wa Allah (s.a.w.) akatoka nje ya hema lake, na ule umati mkubwa ukaanza kuonyesha dalili za kutotulia. Kila sahaba alijaribu kujionyesha zaidi kuliko wengine kwa matumaini ya kuonwa na jicho la bwana. Lakini huyo bwana hakuonekana kumtambua yeyote kati yao ila alitoa swali moja tu: "Yuko wapi Ali?"

Ali wakati huu alikuwa kwenye hema lake (akiwa anumwa na macho na yamevimba). Alijua kwamba, kama alikuwa yeye ndiye "mpendwa wa Allah (s.w.t.) na Mtume Wake," basi ni yeye, na si mwingine yeyote yule, atakayeiteka ile ngome ya al-Qamus. Mtume (s.a.w.) aliagiza aitwe.

Ali alipokuja, Mtume (s.a.w.)(akamtemea mate machoni na yakapona) kisha yeye kwa taadhima kabisa akaiweka bendera ya Uislamu mikononi mwake. Alimuombea baraka za Allah (s.w.t.) ziwe juu yake, na akaomba kwa ajili ya ushindi, na akamuaga na kumtakia kila la kheri. Huyu kijana shujaa ndipo akasonga mbele na kuelekea kwenye ile ngome ngumu katika Arabia yote ambako wale mashujaa wakubwa wa wapiganaji wa Kiebrania walikuwa wanamngojea yeye. Alipigana dhidi yao wote, akawashinda wote, na akaisimi-ka ile bendera ya Kiislam kwenye mnara mkuu wa ngome hiyo.

Wakati yule mshindi aliporudi kule kambini, Mtume wa Allah (s.a.w.). alimpokea kwa tabasamu nyingi, mabusu na pambaja nyingi, na akamuomba Allah (s.w.t.) kuweka fadhi-la Zake njema juu ya simba Wake.

Ibn Ishaq

Burayda b. Sufyan b. Farwa al-Aslami alinisimulia kutoka kwa baba yake Sufyan b. Amr b. Al-Akwa: Mtume (s.a.w.) alimtuma Abu Bakr pamoja na bendera yake dhidi ya moja kati ya ngome za Khaybar. Alipigana lakini alirudi akiwa amepoteza watu na hakuichukua. Kesho yake alimtuma Umar na mambo yale yale yakatokea. Mtume (s.a.w.) akasema: "Kesho nitampa bendera mtu ambaye anampenda Allah (s.w.t.) na Mtume Wake. Allah (s.w.t.) ataiteka kwa hali yoyote ile. Yeye si mwenye kukimbia." Siku iliyofuatia akaitoa bendera kwa Ali.

(The life of the Messenger of God) 185

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Edward Gibbon

Kaskazini-Mashariki ya Madina, ule mji wa zamani na wa kitajiri wa Khaybar ulikuwa ndio makao ya mamlaka ya Wayahudi katika Arabia: eneo hilo, sehemu yenye rutuba humo jangwani, ilikuwa imejaa mashamba makubwa na ng'ombe, na ikilindwa na ngome nane, baadhi ya hizo zilikuwa zikisifiwa kuwa na nguvu zisizoshindika. Majeshi ya Muhammad yalikuwa ya wapanda farasi 200 na askari wa miguu 1400: katika ule mfuatano wa mizingiro (karantini) nane ya mara kwa mara na michungu, walikuwa kwenye hatari na uchovu, na njaa; na wale majasiri wakubwa kabisa walilikatia tamaa tukio hilo. Mtume (s.a.w.) alihuisha imani yao na moyo kwa mfano wa Ali, ambaye kwake alitoa jina la Simba wa Mungu, labda tunaweza kuamini kwamba shujaa wa Kiyunani wa kimo kikubwa sana alipasuliwa kwenye kifua kwa upanga wake usiozui-lika; lakini hatuwezi kusifia ile staha ya mapenzi, inayomuonyesha yeye kwamba alil-ing'oa kutoka kwenye bawaba zake lile lango la ngome na kuishika na kuitumia ile ngao nzito sana kwenye mkono wake wa kushoto (sic - japo kwa makosa).

(The decline and Fall of the Roman Empire) Washington Irving

Mji wa Khaybar ulikuwa umelindwa sana kwa maboma ya mbele, na ngome yake, Al-Qamus, iliyojengwa kwenye mwamba wa mporomoko, ilichukuliwa kuwa isiy-oingilika. Kuzingira mji huu kulikuwa ndio kazi muhimu sana ambayo Waislamu walikuwa bado hawajaifanya. Pale Muhammad alipoziona kuta zake imara na za kutisha, na ngome yake iliyojengwa kwa mawe, anasemekana aliomba msaada wa Allah (s.w.t.) katika kuiteka.

Kuizingira ile ngome kulichukua muda kiasi, na kukaushughulisha ujuzi na uvu-milivu wa Muhammad na vikosi vyake, kwani bado walikuwa na uzoefu mdogo katika mashambulizi ya sehemu zilizojengewa ngome. Muhammad aliongoza masham-bulizi yeye mwenyewe; wale wazingiraji walijilinda kwa mahandaki, na wakaja na magogo ya kuvunjia ili kuyapiga kwenye kuta hizo; upenyo baada ya muda uli-patikana, lakini kwa siku kadhaa jaribio la kuingia lilizuiwa kwa nguvu sana. Abu Bakr kwa wakati mmoja aliongoza mashambulizi, akiwa ameshika bendera ya Mtume; lakini, baada ya kupigana kwa ujasiri mkubwa, alilazimika kukimbia. Shambulizi lililofuata liliongozwa na Umar ibn al-Khattab, aliyepigana mpaka mwisho wa siku bila mafanikio yoyote ya maana.

Shambulizi la tatu liliongozwa na Ali, ambaye Muhammad alimpa upanga wake mwenyewe, unaoitwa Dhu 'l-Fiqar, au Mwenye Makali. Katika kuikabidhi mikononi mwake ile bendera tukufu, alimtangaza yeye kama "mtu aliyempenda Allah (s.w.t.) na Mtume Wake; na ambaye Allah (s.w.t.) na Mtume Wake wanampenda yeye; mtu ambaye alikuwa hajui woga, wala ambaye kamwe hajageuka nyuma mbele ya adui."

186

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Na hapa ingekuwa vizuri kutoa maelezo ya Hadith juu ya hali na tabia ya Ali. Alikuwa mwenye urefu wa kati, lakini mwenye afya na pande la mtu, na mwenye nguvu nyingi mno. Alikuwa na Sura ya tabasamu, mwekundu mno, mwenye ndevu nyingi. Alitambulikana kuwa mwenye tabia maridhawa, akili ya busara, na ari ya dini, na kutokana na moyo wake wa kijasiri, alipewa jina la Simba wa Mungu.

Waandishi wa Kiarabu wanaandika kwa kuutia chumvi nyingi ya upendo ule ujasiri wa Khaybar, wa huyu shujaa wao kipenzi. Alikuwa amefunikwa, wanasema, na fulana nyekundu, ambayo juu yake imefungwa deraya ya chuma. Akikwea na wafuasi wake juu ya rundo kubwa la mawe mbele ya ule upenyo, aliisimika ile bendera juu yake, akidhamiria kutorudi nyuma mpaka ile ngome iwe imechukuliwa. Wale Wayahudi walishambulia mbele ghafla kuwasukuma chini wale washambuliaji. Katika mapigano yaliyotokea, Ali alipigana mkono kwa mkono na yule kamanda wa Kiyahudi, Al-Harith, ambaye alimuua. Ndugu wa huyu aliyeuawa alisonga mbele kuja kulipa kisasi cha kifo chake. Alikuwa wa kimo kirefu; akiwa na deraya maradufu, vilemba viwili, aliyefunga helmeti ya kinga, ambayo mbele yake inameremeta almasi kubwa. Alikuwa na panga zilizofungwa kuning'inia pande zote mbili, na alikuwa anatikisa mkuki wenye ncha tatu, kama chusa cha ncha tatu. Wapiganaji hawa wakapimana kwa macho, na wakakabiliana kwa majigambo ya mtindo wa kiMashariki. "Mimi" akasema yule Myahudi, "ni Merhab, niliye na silaha sehemu zote, na mkali katika mapambano." " Na mimi ni Ali, ambaye mama yake, wakati wa kuzaliwa kwake, alimpa jina la Al-Haidarr (simba mwenye nguvu)."

Waandishi wa Kiislam wanafanya kazi fupi juu ya huyu shujaa wa Kiyahudi. Alimsonga Ali kwa mkuki wake wenye ncha tatu, lakini ulipanguliwa kwa ustadi sana, na kabla hajaweza kujiweka sawa mwenyewe, pigo kutoka kwenye upanga, Dhu'l-Fiqar lilipasua na kugawa ngao yake, likapita kwenye ile helmeti ya kinga, kupita vile vilemba viwili, na kwenye fuvu sugu, na kupasua kichwa chake mpaka kwenye meno yake. Lile umbo lake refu lilianguka kama gogo mpaka chini ardhini.

Wayahudi sasa wakarudi ndani ya ngome, na shambulizi kubwa likafanyika. Katika joto la harakati hizo ngao ya Ali ilidondoka kutoka mkononi mwake, ikiuacha mwili wake wazi; akivuta ghafla lango, hata hivyo, kutoka kwenye bawaba zake, alilitumia kama ngao katika sehemu ya mapambano iliyokuwa imebakia.

Abu Rafii, mtumishi wa Muhammad, alitoa ushuhuda wa jambo hili: "Mimi baadae," yeye anasema, "nilichunguza lango hili nikiwa pamoja na watu saba na sisi wote wanane tulijaribu bila mafanikio kulitumia hilo."

187

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

(Tendo hili gumu la kishujaa na la ajabu limeandikwa na yule mwanahistoria Abul Fida. "Abu Rafii," anahoji Gibbons, "alikuwa shahidi wa kuona kwa macho; lakini ni nani atakuwa shahidi wa Abu Rafii?" Tunaungana na mwanahistoria huyu maarufu katika shaka yake lakini kama tutahoji kwa hadhari sana uthibitisho wa shahidi wa macho, historia itakuwa nini?)

(The Life of Muhammad)

Sir William Muir

Wayahudi walikusanyika kumzunguka chifu wao Kinana na wakajipanga wenyewe mbele ya ile ngome Al-Qamus, wakiwa wameazimia juu ya mapambano ya mwisho kabisa. Baada ya majaribio yasiyo na mafanikio ya kuwaondoa, Muhammad alipan-ga shambulizi la mwisho. "Nitaiweka ile bendera," alisema - ile bendera kubwa nyeusi - "kwenye mikono ya yule anayempenda Allah (s.w.t.) na Mtume Wake , na ambaye anapendwa nao Allah (s.w.t.) na Mtume Wake; yeye atapata ushindi." Asubuhi iliyofuata ile bendera iliwekwa mikononi mwa Ali, na vikosi vikasonga mbele. Wakati huo, mpiganaji mmoja akatoka mbele kutoka kwenye msitari wa Wayahudi, na akatoa changamoto kwa maadui zake kwenye pambano la mmoja mmoja: "Mimi ni Merhab," alipiga ukelele, "Kama Khaybar yote inavyojua, mpiganaji aliyejawa na silaha, wakati vita inapopamba moto." Ndipo Ali akasonga mbele akisema: "Mimi ni yule ambaye mama yangu aliniita Simba; kama simba wa mvumo wa msituni. Ninawapima maadui zangu katika kipimo cha mapandikizi ya watu."

Wale wapiganaji wakaanza kupigana, na Ali akakipasua kichwa cha Mirhab vipande viwili. Ile safu ya Waislamu sasa ikafanya shambulizi la mwisho kabisa, na, baada ya mapigano makali, wakamrudisha nyuma yule adui. Katika vita hii, Ali alifanya mambo makubwa ya ajabu ya kishujaa. Akiwa amepoteza ngao yake, alikamata linta ya mlango, ambayo aliishika na kuitumia kwa mafankio sana badala yake. Hadithi, katika mwenedo wake mpana, imeibadilisha hii ngao ya papo kwa hapo kuwa mhim-ili mkubwa sana, na kumkuza shujaa huyu kuwa Samson wa pili. Ushindi huo ulikuwa wa wazi, kwani Wayahudi walipoteza watu 93; ambapo kwa Waislamu ni watu 19 tu waliouawa katika vita yote nzima.

(The Life of Muhammad. London, 1877) R.V.C.Bodley

Yeye (Muhammad) alianza vita (vya Khaybar) kwa kupunguza moja moja zile ngome ndogo ndogo. Hili lilipokamilika, alisonga mbele dhidi ya Al-Qamus, ile ngome kuu ya Khaybar. Ilikuwa ni sehemu inayoonekana kutisha na kuta zake ngumu zilizojeng-wa na mwamba wa asili. Njia zote zilikuwa zimelindwa sana, na karibu ya ngome hiyo palikuwa na walinzi walioandaliwa vyema na walio na mahitaji ya kutosha. Vita vya kuzingira havikuwa vimezoeleka kwa hawa wahamahamaji waliozoea uvamizi wa jangwani. Hata hivyo, Muhammad alikuwa na idadi ya zana za uzingira-

188

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ji wa papo kwa hapo zilizokuwa zimewekwa pamoja hapo mahali. Zilizokuwa za nguvu sana kati ya hizo ni magogo ya kuvunjia ya mitende ambayo, hatimae, yali-fanya upenyo mdogo katika hizo kuta.

Ndani ya hizi, Abu Bakr alifanya shambulizi la kishujaa, lakini alirudishwa nyuma. Kisha Umar akajaribu, lakini alipofikia mdomo wa ule mpenyo, ilimbidi arudi nyuma, akiwa amepoteza wengi wa watu wake. Mwishowe, Ali alijitokeza mbele ya ule ukuta, akiwa amebeba ile bendera nyeusi. Alivyokuwa anashambulia, alikariri: "Mimi ni Ali yule Simba; na kama simba anayenguruma msituni, ninawapima maadui zangu kwa kipimo cha mapandikizi ya watu."

Ali hakuwa pandikizi la mtu, lakini alifidia upungufu wake wa urefu kwa upana wake mkubwa na nguvu zake nyingi sana. Leo alikuwa anaogopesha ndani ya koti lisilo na mikono refu jekukudu ambalo juu yake amevaa deraya yake ya kifua na ya mgongo. Kichwani mwake iling'ara helmeti yenye njumu iliyopambwa kwa fedha. Kwenye mkono wake wa kulia alipunga upanga wa Muhammad mwenyewe, Dhu 'l-Fiqar, ambao aliukabidhiwa pamoja na ile bendera nyeusi.

Tena na tena askari wakongwe walimkurupukia Ali. Tena na tena walipepesuka kuto-ka kwake na mikono au vichwa vikiwa vimekatwa. Mwishowe, yule shujaa wa Wayunani wote, mtu aliyeitwa Merhab, aliyewapita uwezo askari wote, alijitokeza mwenyewe mbele ya Ali. Alikuwa amevaa deraya maradufu, na kuzunguka helimeti yake kilikuwa ni kilemba kinene kilichoshikiliwa na almasi kubwa. Alikuwa ame-fungwa mkanda wa dhahabu ambao ulining'inia panga mbili. Hakuzitumia panga hizi, hata hivyo, na aliua kushoto na kulia kwa mkuki wake mrefu wenye ncha tatu. Kwa muda kidogo pambano lilisimama na wapiganaji waliegemea kwenye silaha zao wakiangalia pambano. Merhab, kama Goliath wa Gath, na kamwe hajawahi kushind-wa. Ukubwa wake peke yake ulitishia maadui kabla hawajafika karibu naye. Mkuki wake wenye chembe uliwavunja moyo wale washika panga wastadi.

Mirhab alianza kushambulia kwanza, akimkusudia Ali kwa mkuki wake wenye vyembe vitatu. Kwa muda kidogo, Ali, akiwa hana mazoea na aina hii ya silaha, alizidiwa kidogo. Kisha akajiweka imara na akshindana kwa silaha na huyu Myunani. Kutishia na kupangua kuliupeperusha ule mkuki hewani. Kabla Merhab hajaweza kuchomoa moja ya panga zake, upanga wa Ali ulikwisha pasua kichwa chake kupitia helimet na kilemba chake hivyo kikaangukia pande zote za mabega yake.Wale Wayahudi, kumuona shujaa wao amekufa, wakakimbilia mjini. Muhammad akatoa ishara ya shambulio la jumla. Waislamu wakasonga mbele. Ali aliongoza mashambu-lizi hayo. Alikuwa amepoteza ngao yake wakati wa pambano na, kupata badala yake, aling'oa mlango kutoka kwenye bawaba zake, ambao aliunyanyua mbele yake.

(The Messenger - the Life of Muhammad, 1946) 189

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Muhammad Husein Haykal

Wakitambua kwamba hii ndio kambi yao ya mwisho katika Arabia, wale Wayahudi walipigana sana. Jinsi siku zilivyokwenda, Mtume (s.a.w.) alimtuma Abu Bakr pamo-ja na kikosi na bendera kwenye ngome ya Na 'im; lakini hakuweza kuishinda mbali na mapigano makali. Mtume (s.a.w.) tena akamtuma Umar bin al-Khattab katika siku iliyofuatia, lakini hakupata mafanikio yoyote bora zaidi ya Abu Bakr. Katika siku ya tatu, Mtume (s.a.w.) alimwita Ali ibn Abi Talib, na, akimtakia kheri, alimuamuru kuivamia ile ngome. Ali aliongoza majeshi yake na akapigana kijasiri sana. Katika mapambano hayo, alipoteza ngao yake na, akijilinda mwenyewe kwa lango alilolika-mata, aliendelea kupigana mpaka ile ngome ikavamiwa na vikosi vyake. Lango hilo hilo lilitumiwa na Ali kama daraja ndogo ya kuwawezesha wapiganaji wa Waislamu kuziingia zile nyumba zilizokuwa ndani ya ile ngome.

(The Life of Muhammad, Cairo,1935)

Matokeo ya Ushindi wa Khaybar

Ushindi wa Khaybar ni tukio muhimu katika historia ya Uislamu kwani ndio mwanzo wa Dola ya Kiislam na Milki. Mwanahistoria wa Kihindi, M. Shibli, anasema katika kitabu chake cha wasifa wa Mtume:

Khaybar ilikuwa ndio vita ya kwanza ambamo wasiokuwa Waislamu walifanywa raia wa Nchi ya Kiislam. Ilikuwa ndio mara ya kwanza kwamba kanuni za serikali katika Uislamu zilifafanuliwa na kutumika. Kwa hiyo, Khaybar ndio vita vya kwanza vya mafanikio ya Uislamu.

Hapo Khaybar, Dola ya Kiislamu changa ilipata raia wapya na maeneo mapya. Ulikuwa ni mwanzo, sio tu wa hiyo Dola la Kiislamu bali pia wa upanukaji wake. Kama ushindi wa Khaybar ndio mwanzo wa Dola ya Kiislam, basi Ali ibn Abi Talib, mtekaji wake, ndiye msanifu wake mkuu.

Kabla ya ushindi wa Khaybar, Waislamu walikuwa masikini sana au nusu-masikini. Khaybar mara ghafla ikawafanya kuwa matajiri. Imam Bukhari amemnukuu Abdullah bin Umar bin al-Khattab akisema: "Tulikuwa na njaa wakati wote mpaka kwenye ushindi wa Khaybar." Na mwandishi huyo huyo amemnukuu Aishah, mke wa Mtume, akisema: "Haikuwa mpaka wakati wa ushindi wa Khaybar ambapo niliweza kula tende mpaka kuridhika moyo wangu."

Muhajirina hapo Madina hawakuwa na njia ya kutengenezea maisha na kwa hiyo hawakuwa na kipato cha uhakika. Waliweza kuishi tu hivi hivi mpaka wakati wa ushindi

190

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

wa Khaybar. Mara tu Khaybar ilipokuwa imetekwa, kulikuwa na mabadiliko ya ghafla katika mali zao.

Montgomery Watt

Mpaka ilipotekwa Khaybar mapato ya jamii ya Kiislamu yalikuwa ya wasiwasi, na wale Muhajirina waliishi kwa kiasi fulani kutokana na misaada au ukarimu wa Maansari.

(Muhammad, Prophet and Statesman)

Khaybar ilionyesha tofauti kwa jamii ya Waislamu kati ya umasikini mkubwa sana na ulimbikizaji mali.

S. Margoliouth

Wakati Waislamu walipokuja kugawana ngawira zao waligundua kwamba ule ushindi wa Khaybar ulizidi kila faida nyingine ambayo Allah (s.w.t.) alitunuku juu ya Mtume wao.

(Mohammed and the Rise of Uislamu, 1931)

Ule ushindi wa Khaybar ulitunukia faida zisizo na mpaka kwa Waislamu; baadhi ya hizo zilikuwa:

1. Kiasi kikubwa cha dhahabu na fedha ambacho Wayahudi walikuwa wamekilimbikiza kwa vizazi vingi.

2. Maghala mazuri kabisa yenye silaha mpya kabisa za nyakati hizo kama panga, mikuki, marungu, ngao, deraya, pinde na mishale.

3. Makundi makubwa ya farasi, ngamia na ng'ombe, na makundi ya kondoo na mbuzi.

4.  Ardhi nzuri inayolimika yenye viunga vya mitende.

Sir John Glubb

Watu wa Khaybar, kama wale wa Madina, waliishi kwa kilimo, hasa cha mitende. Hata leo hii, makabila hayo yana methali isemayo, "Kupeleka tende Khaybar," ambayo ina maana kama ile ile ya usemi wetu, "Kupeleka makaa ya mawe Newcastle." Khaybar ilisemekana kuwa ndio oasis tajiri kabisa huko Hijazi.

(The Life and Times of Mohammed) 191

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Baada ya kushindwa Wayahudi huko Khaybar, Mtume (s.a.w.) ilimbidi afanye baadhi ya mipango mipya kwa ajili ya utawala wa yale maeneo mapya waliyoshinda.

S. Margoliouth

Sasa Muhammad alijishauri juu ya mpango ambao ulikuwa desturi ya kawaida inay-ojulikana ya Uislamu. Kuwaua au kuwafukuza wale wakazi wachapakazi wa Khaybar isingekuwa busara nzuri, kwani isingefaa kwamba Waislamu, ambao watakuwa wakati wote wakitakiwa jeshini, wakaishi mbali sana na Madina. Aidha, ujuzi wao kama wakulima hautalingana na ule wa wamiliki wa awali wa ardhi hiyo. Hivyo alia-mua kuwaacha wale Wayahudi katika kazi yao kwa malipo ya nusu ya mazao yao, yakikadiriwa na Abdullah mtoto wa Rawahah kuwa kama mizigo 200,000 ya tende.

(Mohammed and the Rise of Islam, 1931)

Pigo moja la nguvu la upanga wa Ali lilisuluhisha matatizo ya kiuchumi ya jamii ya Waislamu, na kuweka ukomo kwenye umasikini wake daima. Aliweka pia ukomo kwenye utegemezi wa Waislamu juu ya hali ya kigeugeu na nyepesi kubadilika, kuwalisha, mara atakapoitoa ile ardhi ya Khaybar yenye rutuba kwao.

Bado kuna maana nyingine ambamo hivi vita vya Khaybar vilikuwa vya umuhimu mkub-wa sio tu kwa Waislamu wa wakati wa Mtume (s.a.w.) bali pia kwa vizazi vya baadae. Ilikuwa ni kuondoka, kwa mara ya kwanza, kutoka kwenye desturi ya jadi ya vita vya Kiarabu. Mtindo wa Kiarabu wa mapigano ulikuwa mara nyingi ni wa kiungwana lakini mara nyingi sana ulikuwa usio na ufanisi. Waarabu walijua kidogo kuliko chochote juu ya mikakati, na kile walichojua wao kuhusu mbinu za kivita ni kupiga-na-kukimbia. Waliweka matumaini yao ya ushindi katika uwezo wao wa kuwakamata waathirika wao kwa kustukiza.

Kwa karne nyingi, wamepigana dhidi ya kila mmoja wao, na kwa kawaida walifuata mtindo ule ule wa asili wa kupiga-na-kukimbia, bila mabadiliko katika mbinu. Tumeona jinsi handaki lilivyozuia jeshi la wapiganaji elfu kumi, na kulisimamisha kabisa kwenye kuizin-gira Madina mnamo mwaka 627A.D. Wale majemedari wakubwa wa waabudu- masana-mu kama Khalid bin Walid na Ikrama bin Abu Jahl walikanganywa na lile handaki, na wakawa hawana msaada wowote mbele yake.

Yote hii ilikuwa ibadilike baada ya Khaybar. Ali ibn Abi Talib aliwafundisha Waislamu ustadi wa kuweka mzingiro, na kuteka sehemu zilizojengewa ngome. Aliwafundisha jinsi ya kupanga mikakati ya vita, na jinsi ya kupigana vita vilivyoandaliwa rasmi na vyenye uamuzi kama jeshi lenye nidhamu. Hapo Khaybar, Ali aliuweka ufunguo wa ushindi wa dunia nzima mikononi mwa Waislamu.

192

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Shamba la Fadak

Fadak ilikuwa ni makazi mengine ya Wayahudi karibu na Khaybar. Watu wa Fadak kwa hiari yao walituma wawakilishi wao kwa Mtume (s.a.w.) wakiahidi kujadiliana masharti ya kujisalimisha. Aliikubali ahadi yao ya kujisalimisha, na akawapa haki ya kukaa kwenye ardhi yao kama raia wa Dola ya Kiislam. Fadak ilipatikana kwa namna hii bila ya nguvu yoyote ile kwa upande wa jeshi la Waislamu. kwa hiyo, ilichukuliwa, kama mali binafsi ya Mtume (s.a.w.) .

Muhammad Husein Haykal

Utajiri wa Khaybar ulikuwa ugawanywe miongoni mwa watu wote wa jeshi la Waislamu kwa mujibu wa sheria kwa sababu walipigana ili kuupata. Utajiri wa Fadak, kwa upande mwingine, uliangukia kwa Muhammad, kwa vile hakuna mwis-lamu na hakukuwa na mapigano yoyote yaliyohusika katika kuupata kwake.

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Katika siku za mwanzo za historia ya Uislamu, Waislamu, walipokuwa bado wapo Makka, walikuwa masikini sana, na hawakuwa na njia yoyote ya kupatia maisha. Khadija, mke wa Mtume, aliwalisha na kuwapa makazi wengi wao. Alitumia utajiri wake wote juu yao hivyo kwamba alipokufa, hapakuwa na chochote ambacho angeweza kumuachia binti yake, Fatima Zahrah. Sasa wakati shamba la Fadak lilipochukuliwa na Mtume, yeye Mtume (s.a.w.) aliamua kulifanya zawadi kwa binti yake kama fidia kwa mihanga mikub-wa aliyofanya mama yake kwa Uislamu. Yeye, kwa hiyo, alilitoa lile shamba la Fadak kwa binti yake, na likawa mali yake.

Wale Mayahudi wa Wadi-ul-Qura na Tayma, oasis nyingine katika Hijazi, pia walikubali kujisalimisha kwa Mtume (s.a.w.) kwa masharti yale yale ya Khaybar na Fadak, na wakaishi kwenye ardhi zao.

Jafar ibn Abi Talib

Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) alikuwa bado yuko Khaybar wakati binamu yake, Jafar ibn Abi Talib, aliporudi kutoka Abyssinia baada ya kukosekana kwa karibu miaka kumi na nne. Wakati Jafar alipotambua huko Madina kwamba bwana wake alikuwa yuko Khaybar, alielekea huko mara moja. Kwa kutukiza, kuwasili kwake huko Khaybar, kulioana na kutekwa kwa ile ngome ya Al-Qamus na kaka yake, Ali. Muhammad alimpen-da Jafar kama mwanae mwenyewe. Alitupa mikono yake kumkumbatia na akasema: "Sikijui kinachonifanya niwe na furaha zaidi; huu ushindi wa Khaybar au kurudi kwa Jafar."

193

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Muhammad Husein Haykal

Muhammad alikuwa na faraha sana kwa kuungana tena na Jafar kiasi kwamba alise-ma hakuweza kueleza ni lipi lilikuwa kubwa zaidi: ushindi juu ya Khaybar au kuungana tena na Jafar.

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Umrah au Hijja Ndogo - A.D.629 (8 H.A.)

Mwaka mmoja baada ya Mkataba wa Hudaybiyyah, Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) alikwenda Makka kufanya hijja. Alifuatana na Waislamu elfu mbili. Kulingana na mashar-ti ya Mkataba huo, wale washirikina waliihama Makka kwa siku tatu. Waislamu waliuin-gia mji kutokea upande wa kaskazini, na hawakuwahi kumuona mtu yoyote wa Makka. Mtume wa Allah (s.a.w.) alimpanda ngamia-jike wake, al-Qas 'wa. Rafiki yake, Abdullah ibn Rawaha, alishikilia hatamu zake alipokuwa akiingia maeneo ya Al-Kaaba. Alikuwa anasoma Aya za ile Sura inayoitwa, Ushindi, kutoka kwenye Qur'an. Waislamu wengine walikuwa wakiitikia kwa kurudia "Tuko chini ya amri Yako, Ewe Allah (s.w.t.)! Tuko chini ya amri Yako, Ewe Allah (s.w.t.)!

Wakati Waislamu wote walipokuwa wamekusanyika ndani ya uwanja wa Al-Kaaba, Bilal alipanda juu ya jengo hilo na kupiga Adhana (mwito wa Waislamu kwenye Swala) - ya kwanza kabisa katika Nyumba ya Allah (s.w.t.) na watu elfu mbili wakaitika kwenye wito wake.

Washirikina walikuwa wakishuhudia mandhari hii kutoka kwenye vilele vya vilima vinavyozunguka lile bonde la Makka. Hawajawahi kuona nidhamu ya namna hiyo hapo kabla, wakati Waislamu wa uzao-bora walipokuwa wakitii bila ukaidi, wito wa mtumwa wa zamani wala hawajaona udhihirisho wa usawa na umoja. Lile kundi kubwa la Waislamu lilisogea kama mwili mmoja, na Maquraishi waliweza kuona kwa macho yao wenyewe kwamba ulikuwa ni mwili ambamo mlikuwa hamna utofautishaji kati ya matajiri na masikini, mabwana na watwana, weusi na weupe, na Waarabu na wasiokuwa Waarabu. Maquraishi pia waliweza kuona kwamba ule udugu, usawa na umoja wa watu ambao Uislamu ulikuwa unauendeleza haukuwa dhana ya kinadharia bali ulikuwa ni kweli tupu. Ilikuwa ni mandhari ya kuvutia sana na haingeweza kushindwa kugusa nyoyo hata za wale waabudu sanamu sugu kabisa.

Ule mwenendo wa Waislamu ulikuwa wa namna yake. Walikuwa na shauku sana ya kutok-ufanya kitu chochote kile ambacho kimekatazwa, na walikuwa na moyo wa kufanya kitu kimoja tu - kutii amri za Allah (s.w.t.)

Na bado udhihirishaji huu ndani ya Al-Kaaba wa nidhamu wa Waislamu, ulikuwa usio-fanyiwa mazoezi, uliojitokeza wenyewe kabisa. Si kwa chochote katika dunia hii ambacho

194

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mwarabu alikuwa na mzio (allergic) sana kuliko kwenye nidhamu; lakini alibadilishwa, ndani ya miaka michache, kwa muujiza wa Uislamu. Ule "mguso" wa Uislamu umem-fanya kuwa kiigizo cha nidhamu miongoni mwa mataifa ya dunia.

M. Shibli, yule mwana historia wa Kihindi, anaandika ndani ya kitabu chake Sira-tun-Nabi (Maisha ya Mtume), juz.1,uk.504, chapa ya 11 (1976), kilichochapishwa na Maarif Printing Press, Azamgarh, U.P., India, kwamba mwishoni mwa siku tatu, wakuu wa Maquraishi walimwendea Ali ibn Abi Talib, na wakamwambia: "Tafadhali mfahamishe Muhammad kwamba ule muda uliopangwa umepita na yeye na wafuasi wake, kwa hiyo, waondoke hapa Makka." Ali alitoa ujumbe huo kwa Mtume. Naye Mtume (s.a.w.) mara moja akatekeleza, na akawaamuru Waislamu kuondoka Makka ambapo waliondoka hapo na wakaanza safari yao ndefu kuelekea nyumbani.

Waislamu walifanya ile Umrah, na kisha wakarudi majumbani kwao huko Madina. Ilikuwa ni katika wakati huu ambapo Khalid ibn al-Walid na Amr bin Al-Aas walipoamua kusil-imu. Walikwenda Madina, wakasilimu na kujiunga na safu za Muhajirina. Wote hawa wal-ijaaliwa kuwa maarufu katika siku za baadae kama majenerali wa Abu Bakr na Umar ibn al-Khattab kwa mfuatano.

Barua za Mtume (s.a.w.) kwa Watawala wa Nchi Jirani

Mnamo Augasti 629, Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliandika barua kwa watawala wa nchi jirani akiwaita kwenye Uislamu.

E.Von Grunebaum

Mnamo mwaka 629, Muhammad alituma barua kwa watawala sita - mfalme wa Uajemi, mfalme wa Byzantine, Najashi wa Abyssinia, gavana wa Misri, mtoto wa mfalme wa Bani-Ghassan, na chifu wa Bani Hanifa huko Kusini-Mashariki ya Arabia, akiwalingania kwenye Uislamu.

(Classical Uislamu - A History 600 - 1258)

Muhammad alikuwa Mtume wa Allah (s.w.t.), sio tu kwa Waarabu bali kwa dunia nzima.

Ulikuwa ni wajibu wake kufikisha ujumbe wa mwisho wa Allah (s.w.t.) kwa wanadamu,

na alifanya hivyo. Profesa Margoliouth, hata hivyo, anazichukulia barua hizi kama mwan-

zo wa uchokozi na utekaji nyara. Anasema:

Karibu na wakati wa vita vya Khaybar, yeye (Muhammad) alitangaza mpango wake wa kuuteka ulimwengu kwa kutuma barua kwa watawala ambao umaarufu wao amekwisha usikia.

(Mohammed and the Rise of Islam, 1931)

Ni kweli kwamba ule mpango wa Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) ulikuwa ni mmoja wa "kuiteka-dunia," bali sio kwa nguvu ya silaha. Makusudio yake yalikuwa ni kuziteka

195

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

akili na nyoyo za wanaume na wanawake, ambayo Uislamu uliyafanya katika wakati wake, na bado unayafanya hadi leo.

Katika kuzituma barua hizi, Mtume (s.a.w.) alishawishiwa na shauku yake kwamba watu wote waishi katika utii wa amri na sheria za Allah (s.w.t.). Utii kwenye hizo amri na sheria peke yake ndio unaoweza kuhakikishia amani, furaha na ustawi wa mwanadamu katika dunia hii, na wokovu wake huko Akhera.

196

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

VITA VYA MU'UTAH

Mnamo mwaka 629, lile kabila la Kiarabu la kikristo la Banu Ghassan lilikuwa likitawali-wa na Shorhail, mtoto wa mfalme ambaye alikuwa ni mtwana wa mfalme wa Byzantine. Alikuwa mmoja wa wale watawala ambao walipokea barua kutoka kwa Muhammad Mustafa akiwataka kuingia Uislamu. Katika siku hizo alikuwa na baraza huko Muutah, mji uliokuwa Mashariki ya Bahari ya Chumvi. Wakati mwakilishi wa Mtume, Harith bin Umayr, alipowasili kwenye baraza lake akiwa na barua yake, aliamuru kuuawa kwake.

Kuuawa kwa Harith bin Umayr kilikuwa ni kitendo cha kikatili kisichosababishwa na uchokozi, na mauaji ya balozi yanachukuliwa kama kosa lisilosameheka katika mataifa mengi. Mtume (s.a.w.) aliamua kuchukua hatua ya kuadhibu. Aliandaa jeshi la watu 3000, na akalituma chini ya ukamanda wa rafiki yake na muachwa huru, Zayd bin Haritha, kwen-da Muutah, kudai fidia. Wakati huo huo, alifanya mkusanyiko wa ukamanda na madaraka. Kama akifa Zayd, amri ya jeshi hilo ilikuwa iende kwa Jafar ibn Abi Talib. Kama na yeye ikibidi auawe, basi jenerali wa tatu ilikuwa awe Abdullah ibn Rawaha.

Wakati Shorhail aliposikia kwamba kuna jeshi linaloelekea kwenye makao yake makuu kutoka Madina, yeye pia aliwakusanya watu wake, na mara akawa tayari kukutana nalo. Alipanga vikosi vyake upande wa Kusini, nje ya kuta za Muutah. Viliundwa na askari wal-inzi wa Kirumi wa Muutah, na makundi ya askari wa kikabila yaliyokusanywa wakati huo huo. Pale Waislamu walipowasili na kuitathmini hali halisi, walitambua kwamba yatakuwa ni mapigano yasiyolingana kwa jinsi walivyozidiwa idadi na maadui.

Viongozi wa Waislamu wakafanya baraza la kivita. Zayd bin Haritha akapendekeza kwamba watume mjumbe mara moja kwa Mtume (s.a.w.) kumuarifu yeye juu ya kutolingana katika nguvu za majeshi hayo mawili, na kumuomba atume askari wa nyongeza. Lakini Abdullah bin Rawaha akampinga, na akasema kwamba uamuzi wa kupigana au kutopigana haukuwa juu ya idadi yao, na kama wamezidiwa idadi na maadui, haikuwa na muhimu kwao. "Tunapigana ili kupata shahada ya kufa kishahidi, na sio heshima ya ushindi, na hii ni fursa yetu; tusiikose hii," alisema. Abdullah bin Rawaha aliushinda mjadala kwa hoja zake zenye nguvu, na Waislamu wakasonga mbele kukutana na maadui. Katika pambano la mwanzo kabisa la silaha, Zayd ibn Haritha, yule jenerali wa kwanza wa Waislamu, akauawa.

Betty Kelen

Zayd alibeba bendera ya Mtume (s.a.w.) na akauawa mara moja kabisa, Mwislamu wa kwanza kufa kwa ajili ya dini katika ardhi ya ugenini.

(Mohammed, Messenger of God) 197

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kisha kamandi ya jeshi ikaenda kwa Jafar ibn Abi Talib, kaka yake mkubwa Ali. Alipigana kishujaa na kwa muda mrefu, akiwaua maadui wengi kiasi kwamba miili yao ilijipanga kama kamba ya kuni kumzunguka yeye. Lakini baadae askari wa Kirumi alitambaa kuto-ka nyuma, bila ya kuonekana, na akampiga kwa upanga wake kwenye mkono wake wa kulia, na akaukata kabisa. Jafar hakuiachia bendera ianguke chini, na alizidi kumbana adui. Baadae kidogo, Mrumi mwingine akaja kutokea nyuma, na kwa pigo la upanga wake, akaukata mkono wa kushoto pia. Shujaa huyu, akiwa bado hajakata tamaa, aliishikilia bendera chini ya kidevu chake, na akaendelea kusonga mbele. Lakini kuondoka mikono yote miwili, hakuweza kujilinda mwenyewe, na katika muda mchache, Mrumi wa tatu alimso-gelea, na akamuua kwa rungu lake kichwani mwake. Baada ya kifo cha Jafar, Abdullah bin Rawaha alichukua uongozi wa jeshi hilo, naye pia alianguka akipigana dhidi ya upinzani mkali.

Washington Irving

Miongoni mwa ujumbe tofauti ambao Muhammad ameutuma nje ya mipaka ya Arabia kuwavuta watoto wa kifalme wa jirani kuingia kwenye Uislamu, ulikuwa ni mmoja kwa gavana wa Basra, soko kuu ndani ya mipaka ya Syria. Mwakilishi wake aliuawa huko Muutah na Mwarabu wa kabila la kikristo la Ghassan, na mtoto wa Shorhail, aliyekuwa gavana, aliyetawala Muutah kwa jina la Heraclius.

Muhammad alituma jeshi la watu 3000 dhidi ya mji huu wenye hatia. Ilikuwa ni safari ya maana sana, kama ambavyo ingeweza, kwa mara ya kwanza, kuleta silaha za Uislamu kupambana na zile za Himaya ya Kirumi. Ukamanda ulikabidhiwa kwa Zaid,mtumwa wake aliyemuacha huru. Baadhi ya maafisa waliochaguliwa waliun-ganishwa naye. Mmojawapo alikuwa binamu yake Muhammad, Jafar, huyo huyo ambaye, kwa ufasaha wake, alithibitisha uhalali wa mafundisho ya Uislamu mbele ya mfalme wa Abyssinia, na akamshinda yule balozi wa Kiquraishi. Alikuwa katika ujana wake sasa, na akitambulika kwa ujasiri na uzuri wake wa kidume.

(The Life of Mohammed)

Wakati Jafar alipokuwa anamshambulia adui, aliimba wimbo. Sir William Muir ametoa tafsiri ifuatayo ya wimbo wake huo:

Peponi! Oh Peponi! Mahali pazuri kiasi gani pa kupumzikia! Maji yake ni ya baridi pale, na kivuli kizuri.

Roma, Roma! Saa yako ya majonzi inakaribia. Wakati nitakapopambana naye, nita-mtupa chini ardhini.

198

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Pale Jafar alipouawa, mwili wake uliletwa kambini. Abdullah bin Umar bin al-Khattab, ambaye alikuwa pamoja na jeshi hilo, anasema kwamba aliyahesabu majeraha kwenye mwili wa shujaa huyu, na akayakuta zaidi ya hamsini, na yote yalikuwa mbele. Jafar alithubutu upanga na mkuki hata baada ya kupoteza mikono yake, lakini hakukwepa.

Wakati majenerali wote watatu waliochaguliwa na Mtume (s.a.w.) walipokuwa wameuawa, Waislamu waliachwa bila kiongozi kwa muda. Kisha Khalid bin al-Walid ambaye alikuwa akipigana kwenye safu, akaikamata ile bendera, na akamudu kuwaku-sanya wale Waislamu. Usiku majeshi yale yaliacha mapigano, na hii ilimpa fursa ya kupanga upya watu wake. Anasemekana kupigana vita vya kujihami katika siku iliyofuata lakini akitambua kwamba ilikuwa vigumu kupata ushindi, aliamuru kurudi nyuma kutoka Muutah, na akafanikiwa kufikisha mabaki ya lile jeshi Madina.

Pale wapiganaji hao walipoingia Madina, walipata "mapokezi" ambayo lazima yali-wafanya wao kusahau yale "mapokezi" ambayo Warumi waliwapa huko Muutah. Walikaribishwa na makundi yanayowazomea ambayo yaliwatupia mavumbi nyusoni mwao na takataka vichwani mwao, na kuwasuta wao kwa kumkimbia adui badala ya kufa kama wanaume kama sio kama mashujaa. Hatimae, Mtume (s.a.w.) mwenyewe alilazimi-ka kuingilia kati kwa niaba yao kuwaokoa kutokana na kuvunjiwa heshima na maudhi.

Sir Willam Muir

Safu za Waislamu tayari zilikuwa zimevunjika; na wale Warumi wakiwa katika ufukuzaji kamili walifanya maangamizi makubwa sana miongoni mwa wale wakim-bizi. Hivyo, tofauti kabisa, katika kitabu cha Wackidi. Baadhi ya maelezo yanadai kwamba Khalid alilikusanya jeshi, na ama aliigeuza siku dhidi ya Warumi, ama ali-ifanya kuwa vita isiyo na mshindi. Lakini mbali na kwamba kifupi cha maelezo yote ni ushahidi wa kutosha wa kinyume chake, mapokezi ya hilo jeshi wakati wa kurudi kwao Madina, yanakubaliana na uamuzi mmoja tu, yaani, kushindwa kabisa, kunakofedhehesha na kusikorekebishika.

(The Life of Mohammed, London, 1861)

Sir John Glubb

Katika vita vya Muutah, Jafar ibn Abu Talib, kaka yake Ali, aliichukua ile bendera kutoka kwa Zaid anayekufa na akainyanyua juu mara nyingine tena. Maadui wakam-zonga huyu shujaa Jafar, ambaye mara tu aligubikwa na majeraha. Hadithi inaelezea kwamba wakati mikono yake yote ilipokatwa ikiwa bado imeng'ang'ania ile bendera, bado alisimama imara, akiishikilia bendera hiyo kati ya vigutu vyake, mpaka askari wa ki-Byzantine alivyompiga pigo lililomsababishia kifo.

199

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Wakati wale Waislamu walioshindwa walipokaribia Madina, Mtume (s.a.w.) na watu wa pale mjini walitoka kuwalaki. Wale raia wakaanza kuwatupia uchafu wale askari wenye huzuni, wakiwapigia mayowe, "Nyie wakimbizi, mmeikimbia njia ya Allah (s.w.t.)!" Lakini Muhammad, kwa ule upole wa ubaba ambao alijua jinsi ya kuutumia vizuri, aliingilia kati kwa niaba yao.

Asubuhi iliyofuata huko Msikitini, Mtume (s.a.w.) alitangaza kwamba ameona, kati-ka ruiya, wale mashahidi wa Muutah huko peponi, wakiegemea katika makochi, lakini Jafar alikuwepo pale katika umbo la Malaika mwenye mbawa mbili, zilizotapakaa ile damu ya kifo cha ushahidi kwenye manyoya yao. Ilikuwa ni kwa matokeo ya ruiya hii kwamba shahidi huyu tangu hapo akijulikana kama Jafar Mwenye Kuruka, Jafar at-Tayyar.

(The Great Arab Conquests)

Betty Kelen

Pale lile jeshi lilipokuja likielekea nyumbani, yeye (Muhammad) alitoka kwenda kuwalaki, mtoto wa Jaafer akiwa juu ya mgongo wa farasi mbele yake. Kulikuwa ni kurudi nyumbani kunakohuzunisha kwa hawa watu ambao walirudi kutoka vitani wakiwa hai, wakimfuata Khalid, ambapo ndugu zake Mtume (s.a.w.) mwenyewe na maswahaba wapendwa wakiwa wameanguka. Watu wa Madina waliokota michanga na uchafu humo njiani kulirushia lile jeshi linalorudi, wakipiga makelele, "Waoga! Wakimbizi! Mumemkimbia Allah (s.w.t.)"

(Muhammad, the Messenger of God)

Baadhi ya wanahistoria wa Kiislamu wamefanya juhudi kubwa "kuthibitisha" kwamba Muutah ulikuwa ni ushindi wa Waislamu ambapo haukuwa. Haieleweki ni kwa nini kushindwa kunachukuliwa na wao kama ushindi. Hili jaribio la kuthibitisha kwamba Waislamu walishinda vita hiyo, kunaweza kuwa kumechochewa na shauku yao ya kuwatambulisha askari wa Waislamu kama wasioshindika. Lakini watauzima ukweli hivi hivi tu kuthibitisha kwamba Waislamu walikuwa hawashindiki. Hata hivyo, Waislamu wal-ishindwa katika vita vya Uhud!

Abul Kalam Azad, yule mwandishi wa Kihindi wa wasifa wa Mtume, anasema kwamba Waislamu walilazimisha kushindwa kwa kipigo kwa Warumi wa Muutah. Anahakiki yale mapokezi ambayo wenyeji wa Madina waliwapa wale "washindi" pale waliporudi nyumbani, lakini anayahusisha na "kutokujua" kwao, na anasema kwamba walipokea taarifa za uongo za matokeo ya vita hivyo.

200

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Lakini kama wenyeji hao walipokea taarifa za uongo, basi ni ajabu kwamba hakuna hata mmoja kati ya hao wapiganaji aliyejaribu kuwasahihisha. Hakuna hata mmoja kati yao, kwa mfano, aliyewaambia wenyeji hao kwamba: "Hii ndio namna yenu ya kuwapokea mashujaa wa Uislamu, kwa uchafu na takataka? Mnawalipa watetezi wa hii dini kwa kuwazomea na kuwakashifu?" Bali hawakuuliza swali lolote la namna hiyo.

Hata kama wenyeji wa Madina walipotoshwa kwamba Waislamu walishindwa huko Muutah, kama Azad anavyodai, basi ingewachukua muda kiasi gani kuweza kugundua huo ukweli? Katika nafasi ya kwanza, hao wapiganaji wenyewe hawakupinga pale wenyeji walipowafunika na takataka, kama ilivyokwisha onekana. Katika nafasi ya pili, baadhi yao walitahayari kabisa kutoka nje ya nyumba zao. Hawakutaka kuonekana hadharani kwa hofu ya kulaumiwa au hata kufanyiwa ukatili na wenyeji hao kwa woga wa kinyonge waliouonyesha mbele ya jeshi. Shauku yao kubwa ilikuwa ni kujificha wenyewe kwa kila mtu mwingine.

D. S.Margoliouth

Wale waliosalia kwenye mapigano Haya ya maafa makubwa ya (Muutah) walilakiwa na Waislamu kama watoro, na wengine walikuwa hata waoga wa kutokeza hadharani kwa kiasi cha muda. Watu wa Madina walikuwa wavumilivu kiasi hicho katika miaka yao nane ya hali ya vita.

(Mohammed and the Rise of Uislamu, 1931) Muhammad Husein Haykal

Mara tu Khalid na lile jeshi walipofika Madina, Muhammad na Waislamu walitoka kwenda kuwalaki, Muhammad akimbeba mkononi mwake, Abdullah, mtoto wa Jafar, kamanda wa pili wa jeshi la Waislamu. Baada ya kuzijua hizo habari, watu hao walirusha mavumbi kwenye nyuso za askari wa Kiislam na kuwashutuma kwa kukimbia mbele ya macho ya adui na kuiacha njia ya Allah (s.w.t.) Mtume wa Allah (s.a.w.) alihojiana na watu hao kwamba wale wapiganaji hawakukimbia bali wali-jiondoa tu ili, kwa mapenzi ya Allah (s.w.t.) kuja kushambulia tena. Mbali na uthibitisho huu kwa upande wa Muhammad wa lile jeshi la Waislamu, watu hao hawakuwa tayari kuwasamehe kujitoa kwao na kurudi. Salamah ibn Hisham, mmo-jawapo katika msafara huu, hakwenda ama Msikitini kuswali wala kujionyesha hadharani kwa kuepuka kuadhibiwa kutokana na kukimbia kutoka kwenye njia ya Allah (s.w.t.) Isingekuwa ule ukweli kwamba watu hawa hawa, hasa Khalid ibn al-Walid, walijipatia sifa kubwa katika vita dhidi ya adui huyo huyo, heshima yao ingebakia daima yenye madoa.

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

201

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

"Ushahidi" mwingine ambao Abul Kalam Azad ameupata wa huo "ushindi" wa Waislamu huko Muutah, ni kwamba hao Warumi hawakuwafukuza. Anasema kwamba kama hao Warumi wangeshinda hiyo vita vya Muutah, wangewafukuza hao Waislamu mpaka kwenye milango ya Madina yenyewe, na zaidi ya hapo.

Lakini hao Warumi wangeweza kuwa na sababu nyingine ya kutowafukuza hao Waislamu. Mojawapo ilikuwa kwamba kwa jeshi lao la farasi, wasingeweza kuwa na ujanja humo jangwani. Kwao jangwa lilikuwa kama bahari, na sio wao wala Wayunani waliokuwa na "meli" yoyote ya "kusafiria" ndani yake. Cha maana walichoweza kufanya, kilikuwa ni kutekeleza shughuli zao "ufukweni" kama "majeshi ya nchi kavu" ambayo wao, kwa kweli, ndiyo waliyokuwa, na katika kizuizi kilichoamuliwa kimkakati na ki-ustadi wa mbinu dhidi ya taifa la "Pwani" kama hao Waarabu.

Kama Waarabu walikimbilia jangwani mbele ya adui mkakamavu, usalama wao ulipata uhakiuka. Hakuwa tu ameandaliwa kupenya hilo jangwa. Matatizo ya lojistiki (mpangilio wa ugavi na usafirishaji wa watu na vitu) peke yake ya kuwashambulia kwenye asili yao wenyewe kulivunja nguvu ile mioyo yenye ujasiri mkubwa ya siku zile. Jangwa lilikuwa ndio "ngome" ambayo iliwalinda Waarabu kutokana na shauku za watekaji wote wa nyakati zilizopita, na kuwahakikishia uhuru wao na kujitegemea.

Sir John Glubb

Msingi wa operesheni zote za vita za mwanzoni, dhidi ya Uajemi na dhidi ya Syria kwa namna moja, ni kwamba wale Waajemi na Wabyzantium hawakuweza kutembea ndani ya jangwa, wakiwa wamepanda farasi. Waislamu walikuwa kama majeshi ya baharini, wakivinjari karibu na ufukweni ndani ya meli zao, ambapo Waajemi na Wabyzantium kwa kufanana waliweza kushika nafasi juu ya ufukwe tu (yaani, sehe-mu iliyolimwa) wasiweze kushuka "baharini" na kumshambulia adui ndani ya asili yake mwenyewe ya jangwa. Hali kadhalika hao Waarabu, kama vile wale maharamia wa Norway au Wadenishi walioshambulia Uingereza, walikuwa mwanzoni wanao-gopa kusogea ndani ya nchi mbali na "meli" zao. Wakishambulia maeneo yaliyokuwa "ufukweni" mwa hilo jangwa, waliharakisha kurudi kwenye asili yao wakati hatari ilipowatishia.

(The Great Arab Conquests, 1963)

202

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Joel Carmichael

Kuna kufanana kwa ajabu kati ya mkakati wa Mabedui na ule wa majeshi ya bahari-ni ya kisasa. Ikiangaliwa kutoka mahali pafaapo kuangalia mambo ya wahamaji hamaji, hilo jangwa, ambalo waliloweza kulitumia vizuri, lilikuwa kama bahari kubwa ambayo ndani yake walimiliki vile vyombo vilivyokuwepo. Mabedui wali-weza kulitumia kwa ugavi wa vifaa na mawasiliano - na kama kimbilio wanaposhind-wa. Waliweza kutokeza kutokea ndani yake kabisa wakati wowote walipopenda na kuchurupuka kurudi tena kwa hiari yao. Hii iliwapa usogeaji mkubwa sana na uimara, alimradi walikuwa wanasonga dhidi ya jamii zenye maskani.

(Shaping of the Arabs, 1967)

Vita hivyo vilipiganwa nje kidogo tu ya Muutah. Kama Waarabu wangewashinda Warumi na kuwafukuza, basi walifanya nini na mji huo ambao uliangukia miguuni kwao? Kama watekaji, iliwabidi waumiliki. Lakini hakuna mwanahistoria aliyedai kwamba Waislamu waliingia mji wa Muutah na wakaumiliki.

Waarabu walivuma kwa kupenda kwao ngawira. Huu ni ukweli unaojulikana kwa kila mwanafunzi wa historia yao, na wanahistoria kama Abul Kalam Azad hawawezi kutokuu-jua. Mwanahistoria huyu huyu anasema kwamba idadi ya Warumi na washirika wao ambao waliopigana hapo Muutah ilikuwa ni elfu mbili. Kama Waislamu waliwashinda hao Warumi, basi walipaswa wawe wameteka maelfu wa Warumi, na iliwabidi warudi Madina wakilemewa na nyara na hazina za Muutah. Lakini hawakufanya hivyo. Kumbukumbu za kihistoria ziko kimya juu ya jambo hili. Hakuna utajo wa ngawira yoyote au wafungwa wowote wa kivita katika maelezo ya hivyo vita vya Muutah. Ukimya huu ni ushahidi unao-jieleza wazi kwamba hao Waislamu hawakuwa ndio washindi. Kwa kweli, walijiona wao wenyewe ni wenye bahati kuweza kuwa wameondoka wakiwa hai kutoka kwenye uwanja wa vita.

Muhammad Husein Haykal

Baada ya vita vya Muutah, jeshi la Waislamu likiongozwa na Khalid ibn al-Walid, lilirudi Madina sio walioshinda wala walioshindwa, lakini wakifurahia kabisa kuweza kurudi.

(The Life of Muhammad,Cairo, 1935)

203

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Tunawapenda wale Waislamu ambao walijijua kwamba walionyesha woga katika vita vya Muutah, na waliuonea haya. Lakini walikuwepo Waislamu wengine, baadhi yao maswaha-ba wa Mtume, ambao walikimbia kutoka vitani, sio mara moja, bali mara nyingi, na hawakuwa na haya juu ya utendaji wao. Mtu anaweza akapendezewa nao kwa kujikausha kwao hata hivyo. Kuokoa maisha yao wenyewe ya thamani, waliweza kukimbia kutoka kwenye medani ya vita, na kisha kuirudia wakati mizani ilipoinamia upande wa Waislamu. Vita vya Muutah vilikuwa ni kushindwa kwa Waislamu. Na kwa Warumi, haikuwa cho-chote zaidi ya mikwaruzo midogo ya mpaka. Waliwasukuma Waarabu kuwarudisha jang-wani, na kwao wao tukio hilo lilifungwa.

204

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mapambano ya Dhat es-Salasil

Vita vya Muutah vilipiganwa mwezi wa Septemba 629. Katika mwezi uliofuata, Mtume (s.a.w.) alipokea taarifa kwamba watu wa kabila la Qadha'a walikuwa wakijikusanya huko kaskazini mwa Wadi-ul-Qura kwa nia ya kuvamia Madina. Haya yalikuwa ni matokeo ya moja kwa moja ya kule kushindwa kwa Waislamu kule Muutah. Makabila ya kipagani yaliamini kwamba uwezo wa Waislamu ulivunjika kule Muutah, na kwamba kama watashambulia Madina, hawakudhani wangekutana na upinzani wowote.

Ilimbidi Mtume (s.a.w.) kuchukua hatua-kinzani kuvuruga matembezi ya kikabila kuingia Madina. Yeye, kwa hiyo, alituma jeshi la askari mia tatu chini ya ukamanda wa Amr bin Al-Aas, kuwachunguza wale wa-Qadha'a katika nchi yao wenyewe, na kuwatawanya, ikibidi kuwa lazima.

Amr aliondoka Madina, na kusimama kaskazini mwa Wadi-ul-Qura, karibu na chem-chemii iliyokuwa ikiitwa Dhat es-Salasil. Alishtuka kuona makundi ya watu wa makabila wenye silaha wakizurura ndani ya hilo bonde na akatuma mjumbe kwa Mtume (s.a.w.) akimuomba askari wa ziada. Mtume (s.a.w.) mara moja alitekeleza, na akatuma watu wengine mia mbili chini ya ukamanda wa Abu Ubaidah ibn al-Jarrah. Kundi hili la pili walikuemo Abu Bakr na Umar.

Wakati Abu Ubaidah alipofika kwenye kambi ya Amr bin Al-Aas, alionyesha kwamba angetaka kuchukua uongozi wa vikosi vyote vya ziada. Lakini majibu ya Amr kwa pen-dekezo hili yalikuwa ni hapana yenye mkazo. Alifanya ieleweke wazi kwa Abu Ubaidah kwamba yeye (Amr) alikuwa ndiye kamanda mkuu wa vikosi vyote, cha kwake mwenyewe na vile vya ziada vile vile, ambavyo huyu wa baadae (Abu Ubaidah) alivyole-ta, watu mia tano wote.

Wakati wa usiku kulikuwa na kushuka kwa ghafla kwa hali ya joto, na hali ya hewa ikawa ya baridi isiyo ya kawaida. Wale askari wa farasi wakawasha mioto midogo midogo kwa ajili ya joto, na wakakaa kuizunguka. Amr, hata hivyo, aliwaamuru kuizima mioto hiyo. Wote wakatii isipokuwa Abu Bakr na Umar. Amr akarudia kutoa amri yake. Lakini bado wakabakia kimya ambapo Amr akatishia kuwatupa wote kwenye moto huo kama wataen-delea kutomtii yeye. Umar akamgeukia Abu Bakr na kumlalamikia juu ya tabia isiyo na adabu na ya ghafla ya Amr. Abu Bakr akamwambia kwamba Amr aliuelewa ujanja wa vita vizuri zaidi kuliko wao wanavyo zielewa, na kwa hiyo walipaswa kumtii. Ndipo wao wakauzima huo moto.

Katika siku iliyofuata kulikuwa na mapigano yasiyo na utaratibu lakini wale watu wa makabila walipigana bila mpango au nidhamu na walitawanywa mara moja. Waislamu walita-

205

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ka kuwafukuza kwenye vilima na mabonde lakini Amr aliwakataza kufanya hivyo. Watu hao wa makabila waliacha mizigo yao na Waislamu wakaikusanya. Waliteka vile vile ngamia wengi na kondoo, na kisha wakarudi Madina.

Wakati wa vita hiyo, na katika safari ya kurejea, Amr bin Al-Aas aliongoza vikosi vyake katika Swala. Kwa hiyo aliwadhihirishia kwamba alikuwa ni kiongozi wao katika nyanja zote - kivita na kidini. Abu Ubaidah, Abu Bakr na Umar, wote watatu, walipokea amri kutoka kwake, na waliswali Swala zao nyuma yake.

Pale msafara huo uliporudi Madina, Umar alilalamika kwa Mtume (s.a.w.) kuhusu ile tabia yake isiyo ya heshima na ya uonevu ambayo mkuu wake wa kikosi, Amr bin Al-Aas, aliy-omtendea yeye na Abu Bakr huko Dhat es-Salasil. Ilikuwa ni desturi ya Mtume (s.a.w.) kuwahoji Makapteni wake waliporudi kutoka kwenye msafara. Walikuwa wampe taarifa pana yenye kueleweka juu ya mwenendo wa vita hivyo.

Amr alikuwa tayari kutetea vitendo vyake. Alimwambia Mtume (s.a.w.) kwamba Waislamu walikuwa wachache sana, na ile mioto mikubwa ingeweza kufichua ukosefu wao wa idadi kubwa kwa maadui. Ilikuwa ni kwa maslahi ya usalama wao wenyewe, alise-ma, kwamba aliwaamuru wao kuizima. Aliendelea kusema zaidi kwamba ile sababu ya kwa nini aliwakataza watu wake kuwafukuza wale maadui ilikuwa kwamba hao maadui walikuwa kwenye nchi yao wenyewe, na wangeweza kujikusanya kirahisi na kuwasham-bulia wao. Hao Waislamu, alifafanua, walikuwa wakipigana kwenye nchi wasiyoizoea, na walikuwa, kwa hiyo, katika hali ngumu. Mtume (s.a.w.) aliridhika na maelezo ya Amr, na akayakataa malalamiko ya Umar.

Sir William Muir

Kule kurudishwa nyuma kwa majeshi yake kutoka Muutah kuliathiri vibaya ile hadhi kubwa ya Muhammad miongoni mwa makabila ya mpakani mwa Syria. Kulikuwa na minong'ono kwamba yale makabila ya kibedui ya maeneo yale yalikuwa yameku-sanya jeshi kubwa, na walikuwa hata wakitishia shambulio la ghafla juu ya Madina. Amr, yule mwislamu mpya, aliwekwa kwa hiyo kuwa kiongozi wa watu mia tatu pamoja na farasi thelathini, pamoja na maagizo ya kuyakomesha yale makabila yenye uadui na kuwashawishi wale aliowaona ni wepesi kukubali, na kushambulia mara kwa mara ule mpaka wa Syria.

Baada ya mwendo wa siku kumi aliweka kambi kwenye chemchemi karibu na mipa-ka ya Syria. Pale aliona kwamba maadui walikuwa wamekusanyika kwa idadi kubwa, na kwamba aliweza kutafuta msaada kidogo kutoka kwenye makabila ya kienyeji. Alisimama na kutuma mjumbe kwa ajili ya majeshi ya nyongeza. Muhammad mara moja akajibu, na akatuma watu mia mbili, ambao miongoni mwao walikuwemo Abu Bakr na Umar, chini ya uongozi wa Abu Ubaidah. Katika kujiunga na Amr, Abu Ubaidah alitaka achukue uongozi wa jeshi lote, au

206

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

angalau abakie kuwa kiongozi juu ya kikosi chake mwenyewe; lakini Amr, akitoa ahadi ya uamuzi na uimara ambao ulimtambulisha katika siku za baadae, alisisitiza katika kushika uongozi mzima. Abu Ubaidah, mtu mwenye tabia ya upole na mwenye kushawishika kirahisi, akashindwa. "Kama unakataa kukubali mamlaka yangu," alisema, "sina shauri bali kukutii wewe; kwani Mtume (s.a.w.) aliniagiza kabisa nisiruhusu mabishano, wala mgawanyiko wowote wa uongozi." Amr akajibu kwa sharti: "Mimi ni mkuu wako. Umeleta tu nyongeza kwenye jeshi langu." "Naiwe hivyo," alisema Abu Ubaidah. Amr kisha akaanza kuongoza vile vikosi vilivyoun-gana, na akaongoza Swala; kwani hapo mwanzoni utendaji wa kiroho katika Uislamu uliunganishwa na ule wa kisiasa na kijeshi.

(The Life of Mohammed, London, 1877) Muhammad Husein Haykal

Wiki chache baada ya kurudi kwa Khalid, Mtume (s.a.w.) alitafuta kufidia zile pengo katika heshima ya Waislamu katika sehemu za kaskazini za peninsula hiyo ambazo yale mapambano yaliyotangulia na wale Byzantium yalizosababisha. Yeye, kwa hiyo, alimwagiza Amr ibn al-Al-Aas kuwaamsha Waarabu watembee kuelekea al-Sham. Alimchagua Amr kwa kazi hii kwa sababu mama yake yeye huyu alitokana na mojawapo ya hayo makabila ya kaskazini, na alitegemea kwamba Amr ataweza kutu-mia kiungo hiki kurahisisha kazi yake. Wakati alipowasili kwenye chemchem iliyokuwa ikiitwa al-Salasil, katika nchi ya Judham, akihofia kwamba maadui wanaweza kumkuta, alituma ujumbe kwa Mtume (s.a.w.) akiomba askari wa ziada. Mtume (s.a.w.) alimtuma Abu Ubaidah ibn al Jarrah akiongoza kundi la Muhajirina

ambalo walikuwemo Abu Bakr na Umar...

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Amr bin Al-Aas alikuwa mwislamu mpya. Lakini mara alipokuwa mwislamu, alinyanyukia haraka sana kutoka askari wa kawaida mpaka jenerali katika jeshi la Madina. Ni dhahiri kabisa, alikuwa amejaaliwa na uwezo usiokuwa na kifani kote, kama jenerali na kama mtawala. Mtume, kwa hiyo, aliwaweka watu ambao walikuwa wakubwa kwa miaka mingi kuliko yeye, na ambao waliingia Uislamu muda mrefu zaidi kabla yake, chini ya uongozi wake.

Abu Ubaidah na Abu Bakr walikwisha kuwa Waislamu miaka ishirini kabla ya Amr, na hivyo wao waliwakilisha "shaba" ambapo Amr bin Al-Aas alikuwa "kajiwe" tu katika imani kwa wakati huu. Na bado Mtume (s.a.w.) alimuamuru Abu Ubaidah kutumika chini ya Amr.

Hii inathibitisha tu kwamba ilipofika wakati wa Mtume (s.a.w.) kuchagua mtu kushika uongozi katika shughuli fulani, alitilia maanani, sio umri wake, bali uwezo wake - uwezo wa kupata matokeo!

207

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kutekwa kwa Makka

Maquraishi walishindwa kutumia ushindi wao wenyewe juu ya Waislamu katika vita vya Uhud, lakini hawa Waislamu waliposhindwa katika vita vya Muutah na Wakristo, wali-jaribu kutumia ule ushindi wa Wakristo, na kurudisha ile hali ya kabla y a Hudaybiyya katika Arabia. Kushindwa kwa Waislamu kule Muutah kulichukua nafasi kubwa katika matukio yaliyotangulia kuanguka kwa Makka mnamo mwaka 630.

Muhammad Husein Haykal

Tunaweza kukumbuka kwamba mara tu Khalid na lile jeshi waliporudi Madina bila ya uthibitisho wa ushindi (katika vita vya Muutah), waliitwa wakimbizi. Askari wengi na makamanda walijihisi kuabika sana kiasi kwamba walikaa majumbani ili wasionekane na kudhalilishwa hadharani. Vile vita vya Muutah viliwapa Maquraishi ile picha kwamba Waislamu na nguvu zao sasa wameangamizwa na kwamba, hadhi yao na hofu ambavyo hapo kabla waliviingiza kwa wengine vyote vimetoweka. Hii iliwafanya Maquraishi kuegemea kwa nguvu sana kwenye hali zilivyokuwepo kabla ya Mkataba wa Hudaybiyya. Walidhani sasa wangeweza kuanzisha vita ambavyo dhidi yake Waislamu walikuwa hawawezi kujihami wenyewe, bila kuzungumzia juu ya kujibu mashambulizi au kulipiza kisasi.

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Kulingana na makubaliano ya ule Mkataba wa Hudaybiyya, yale makabila ya Waarabu yalikuwa huru kuingia kwenye mahusiano ya mkataba ama na Waislamu au hao Maquraishi. Kwa kuchukua fursa ya mapatano haya, lile kabila la Banu Khuza'a waliandi-ka mkataba wa urafiki na Mtume wa Uislamu, na kabila lingine - Banu Bakr - wakawa washirika wa Maquraishi. Uhasama ulidumu baina ya haya makabila mawili tangu nyakati za kabla ya Uislamu lakini sasa yote yalipaswa yafuate masharti ya ule Mkataba wa Hudaybiyya, na kuepuka kushambuliana.

Lakini miezi kumi na nane baada ya huo Mkataba wa Hudaybiyya kutiwa saini, kundi la wapiganaji la Banu Bakr ghafla likawashambulia Banu Khuza'a majumbani mwao wakati wa usiku. Wakati wa shambulio hili unatolewa kama ni mwishoni mwa Rajab ya mwaka wa 8 A.H. (Novemba 629). Banu Khuza'a hawakufanya chochote kuchochea shambulio hili. Walichukua hifadhi katika maeneo ya Al-Kaaba lakini maadui zao waliwafuatilia hata hapo, na wakawaua baadhi yao. Wengine waliokoa maisha yao kwa kutafuta ulinzi wa Budail bin Waraka na rafiki yake, Rafa'a, katika nyumba zao, hapo Makka.

208

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Muhammad Husein Haykal

Ule Mkataba wa Hudaybiyya uliandika kwamba mtu yoyote asiye wa Makka akitaka kujiunga na kambi ya Muhammad au ile ya Maquraishi anaweza kufanya hivyo bila ya kipingamizi. Kwa msingi wa kipengele hiki, lile kabila la Khuza'a lilijiunga na safu ya Muhammad, na lile la Banu Bakr likajiunga na Maquraishi. Kati ya Banu Khuza'a na Banu Bakr idadi ya migogoro ya zamani ambayo ilikuwa haijasuluhishwa ilibidi isimamishwe kwa sababu ya mipango mipya. Pamoja na Maquraishi kuamini kwamba (baada ya vita vya Muutah) uwezo wa Waislamu umevunjika, Banu al Dil, ukoo mmoja wa Banu Bakr, walidhani kwamba muda umefika wa kilipiza kisasi chao dhidi ya Khuza'a.

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Banu Bakr wasingeweza kuwashambulia Khuza'a bila ya kula njama na kutiwa moyo kama sio kuungwa mkono kwa uwazi na Maquraishi. Tabari, yule mwanahistoria, anase-ma kwamba Ikrima bin Abu Jahl, Safwan bin Umayya na Suhayl bin Amr, wote watu mashuhuri wa Quraishi, walijibadili wenyewe na kupigana kwenye upande wa Banu Bakr dhidi ya Khuza'a. Kati ya hawa watatu, huyu wa mwisho kutajwa ndiye mweka saini mkuu wa Maquraishi kwenye Mkataba wa Hudaybiyya.

Maxime Rodinson

Katika Rajabu ya mwaka wa 8 (Novemba 629), katika mfululizo wa kisasi cha kurithi baina ya koo ambacho kilikuwa kikiendelea kwa miongo kadhaa, baadhi ya wale waliotaharuki sana katika Maquraishi kule nyuma yao, walishambulia kikundi cha kabila la Khuza'a, washirika wa Muhammad, sio mbali sana kutoka Makka. Mtu mmoja aliuawa na waliobakia waliumizwa vibaya na kulazimishwa kukimbilia ndani ya eneo tukufu la Makka. Wakifuatiliwa hata huko walichukua hifadhi kwenye nyumba mbili za kirafiki. Kwa aibu sana hawa Banu Bakr waliweka mzingiro kwenye nyumba hizo. Kwa jumla watu ishirini wa Khuza'a waliuliwa.

(Mohammed, kilichotafsiriwa na Anne Carter)

Mmoja wa wakuu wa Khuza'a, Amr bin Salim, alikwenda Madina na kumsihi Mtume (s.a.w.) kuingilia kati. Mtume alishituka kusikia habari hizo za ufisadi. Kama mshirika wa hao Khuza'a, alipaswa kuwalinda kutokana na maadui zao. Lakini kabla ya kufikiria hatua za kijeshi, alijaribu kutumia njia za amani ili kupata marekebisho na haki. Alituma mjumbe kwa Maquraishi, na akashauri kwamba:

209

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

* Wale wateja wa Maquraishi, yaani, Banu Bakr, au Maquraishi wenyewe walipe fidia ya damu kwa Banu Khuza'a, au;

*  Maquraishi wabatilishe ulinzi wao wa Banu Bakr, au;

* Watangaze ule Mkataba wa Hudaybiyya kuwa umefutwa.

Zarqani anasema kwamba mtu aliyewajibia Maquraishi alikuwa ni Qurtaba bin Umar. Alimwambia mjumbe wa Mtume (s.a.w.) kwamba lile la mwisho tu kati ya masharti yale matatu ndio lililokuwa linakubalika kwao. Kwa maneno mengine, Maquraishi wal-imwambia kwamba ule Mkataba wa Hudaybiyya pamoja na makubaliano yake ya miaka kumi ya kusimamisha vita, tayari ni "kanuni isiyo na nguvu" kiasi wao walivyohusika.

Wale wakaidi wa Maquraishi walikuwa wepesi kuukana ule Mkataba wa Hudaybiyya laki-ni haraka sana wale viongozi wao wakweli zaidi na makinifu walitambua kwamba lile jibu walilopeleka Madina lilikuwa ni kosa la kijinga kwani lilitamkwa, sio kwa busara na heki-ma, bali kwa ufedhuli na ujinga. Na pale walipofikiria juu ya matokeo gani ya kitendo chao yatakayokuwa, waliamua kuchukua hatua haraka sana kuzuia maafa. Lakini vipi? Baada ya mjadiala wa kusisimua, walikubaliana kwamba Abu Sufyan aende Madina, na ajaribu kumshawishi Mtume (s.a.w.) kurudia upya ule Mkataba wa Hudaybiyya.

Wakati Abu Sufyan alipowasili Madina, alikwenda kwanza kumuona binti yake, Ummu Habiba - mmoja wa wake zake Mtume. Alipokuwa anataka kukaa juu ya zulia, binti yake akalivuta kutoka chini yake, na akasema: "Wewe ni muabudu masanamu usiye na tohara, na siwezi kukuruhusu kukalia zulia la Mtume wa Allah (s.a.w.)" Alimfanya kama mtu aliyetengwa na jamii, asiyegusika. Akishtushwa na mapokezi kama hayo, alimuacha na kuondoka na akaenda Msikitini akitegemea kumuona Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Lakini Mtume (s.a.w.) hakumpa fursa ya kuonana naye. Baadae aliomba msaada wa Abu Bakr, Umar na Ali lakini wote walimwambia kwamba hawawezi kumuombea yeye kwa Mtume, na akarudi Makka mikono mitupu.

Maquraishi waliuvunja ule mkataba, na wajumbe wa Khuza'a walikuwa bado wapo Madina, wakidai haki. Kama Mtume (s.a.w.) angesamehe lile kosa la Maquraishi, angeiabisha vibaya sana heshima yake machoni mwa Waarabu wote. Asingeweza kukubali hili litokee. Hatimae, Mtume (s.a.w.) aliamua kuiteka Makka, na aliwaamuru Waislamu wakusanyike.

Jeshi hilo la Uislamu liliondoka Madina mnamo mwezi kumi ya Ramadhini ya mwaka wa 8 H.A. (1 Feb.630). Habari kwamba kuna jeshi lililokuwa linaelekea upande wa Kusini, zilienea haraka sana humo jangwani, na hata zikafika Makka kwenyewe. Wale watu wa ukoo wa Bani Hashim ambao walikuwa bado wako Makka, wakaamua, baada ya kusikia habari hizi, kuondoka hapo mjini na kukutana na hilo jeshi linalokuja. Miongoni mwao

210

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

walikuwa ni Abbas bin Abdul Muttalib, yule ami yake Mtume; Aqiil bin Abi Talib, na Abu Sufyan bin al-Harith bin Abdul Muttalib, binamu zake. Walijiunga na jeshi hilo la Uislamu, na wakaingia tena Makka pamoja nalo.

Mnamo mchana wa mwezi 19 Ramadhan, jeshi hilo liliwasili Merr ad-Dharan kaskazini ya Makka, na likasimama hapo ili kuupitisha usiku huo. Usiku Mtume (s.a.w.) aliwaamuru wapi-ganaji wake kuwasha mioto midogo midogo, na uwanda wote ukamulikwa na maelfu ya mioto.

Abu Sufyan na Hakim bin Hizam walikuwa wameondoka pia Makka kwenda kuchunguza zile taarifa za uvamizi wa Waislamu. Wakielekea kaskazini kwenye njia iendayo Madina, wao pia waliwasili Merr ad-Dharan, na walipigwa na butwaa kuona mioto midogodogo isiyo na idadi ikiwaka ndani ya bonde hilo. Walipotambua kwamba wako kwenye kambi ya Waislamu, walipata taabu sana wasijue chakufanya kujiokoa wao wenyewe au mji wao.

Abbas bin Abdul Muttalib pia alikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya usalama wa watu wa Makka. Alihofia kwamba kama watatoa upinzani, watauawa kwa wingi. Alikuwa amem-panda yule farasi mweupe wa Mtume (s.a.w.) kupita mle kambini, ambapo katika mpaka wake wa Kusini, alikumbana ghafla na Abu Sufyan na Hakim bin Hizam. Aliwaambia kwamba wanaweza kuona ile idadi ya Waislamu, na kwamba Maquraishi hawakuwa na uwezo wa kushindana nao. Abu Sufyan alimuuliza ni nini yeye angepaswa kufanya . Abbas akamwambia afuate nyuma yake juu ya farasi wake mwenyewe, na kwamba atampeleka kwa Mtume, na atajaribu kupata hati ya usalama kwa ajili yake. Hakim bin Hizam akaru-di Makka kwenda kuelezea juu ya kile alichokiona na kusikia. Abbas na Abu Sufyan wali-wapanda farasi wao kuingia kwenye kambi ya Waislamu wakati huo huo, walipita karibu na hema la Umar, naye Umar akataka kujua ni akina nani hao wageni wawili.

Pale Umar alipomtambua Abu Sufyan, alisisimka, na akamwambia: "Ewe adui wa Allah (s.w.t.) hatimae uko kwenye mamlaka yangu, na sasa nitakuua." Lakini Abbas akamwambia kwamba yeye (Abu Sufyan) yuko chini ya ulinzi wake. Pale pale Umar alikimbia kwenda kumuona Mtume (s.a.w.) na kumuomba ruhusa yake ili amuue (Abu Sufyan). Lakini Mtume (s.a.w.) alimwambia tu Abbas amlete asubuhi itakayofuata.

Mapema sana asubuhi iliyofuata, Abbas, Abu Sufyan na Umar, wote watatu walitokea mbele ya hema la Mtume. Umar alikuwa na hamu ya kumuua Abu Sufyan lakini Mtume (s.a.w.) alimzuia, na akamualika Abu Sufyan kusilimu. Abu Sufyan hakuwa na moyo sana wa kuukubali Uislamu lakini Abbas alimwambia kama hakusilimu, basi Umar atamuua, na hatarudi kamwe Makka. Akikabiliwa na tishio la kifo, Abu Sufyan aliitamka Shahada ambayo ilimwingiza rasmi kwenye jamii ya Waislamu.

Abbas pia alimuomba Mtume (s.a.w.) kumpa Abu Sufyan upendeleo fulani ambao angeulinganisha na "heshima maalum." Mtume (s.a.w.) akasema wale watu wote wa

211

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Makka watakaoingia kwenye nyumba ya Abu Sufyan, au watakaokaa kwenye nyumba zao wenyewe, au watakaoingia kwenye maeneo ya Al-Kaaba, watakuwa salama kutokana na madhara yote. Abu Sufyan alijivuna sana kwamba Mtume (s.a.w.) ameitangaza nyumba yake kuwa kimbilio la waabudu masanamu wa Makka. Marafiki zake wa baadae na wapenzi wanaringia ile "heshima maalum" yake mpaka leo.

Ilikuwa ni Ijumaa, Ramadhan 20, 8 A.H. (Feb.11, 630) pale jeshi la Waislamu lilipovunja kambi pale Merr ad-Dharan, na kuelekea Makka. Abbas na Abu Sufyan walisimama juu ya ukingo wa kilima kuangalia vile vikosi vikipita mbele yao. Huyu Abu Sufyan alivutiwa sana na utaratibu huo, na nidhamu, ile idadi na moyo wa mshikamano wa mipangilio, na akamwambia Abbas:

"Mpwa wako kwa hakika amepata ufalme mkubwa na mamlaka makubwa." Abbas akamkaripia: "Ole wako! Huu ni Utume na sio ufalme." Abu Sufyan alikuwa hajawahi kuona mandhari ya kutisha kama hii hapo kabla, na kwa hisia zake za kipagani, na uono wake wenye kikomo kabisa, aliweza kuitafsiri tu katika istilahi za mamlaka yakinifu. Lakini alitambua kwamba mchezo wake na waabudu masanamu umekwisha hatimae, na kitu muhimu sasa kilikuwa ni kuokoa maisha yake na yao.

Abu Sufyan aliharakisha kurudi Makka, na akiingia kwenye maeneo ya Al-Kaaba, alike-mea kwa sauti kubwa: "Enyi watu wa Makka! Muhammad amewasili pamoja na jeshi lake, na hamna uwezo wa kumpinga yeye. Wale miongoni mwenu watakaoingia nyumbani kwangu, watakuwa salama kutokana na madhara yote, na sasa ni kusalimu amri kwenu tu bila ya masharti kutakakoweza kuwaokoeni na mauaji ya halaiki."

Mke wa Abu Sufyan, Hinda, aliusikia mwito wake huo. Alishikwa na hasira kali, akatoka kwa kasi nje ya nyumba yake, akamshika kwenye ndevu zake, na akapiga may owe: "Enyi watu wa Makka! Muueni huyu mpumbavu asiye na bahati. Ana upungufu wa akili. Muondoeni yeye na mlinde mji wenu kutokana na adui yenu."

Lakini ni nani anayeweza kuilinda Makka na vipi? Sasa hivi, Abu Sufyan alikuwa amezungukwa na raia wengine wa Makka, na mmoja wao akamuuliza: "Nyumba yako inaweza kuchukua watu wachache tu. Ni vipi watu wengi watakavyopata kimbilio ndani yake?" Akasema: "Wale wote watakaokaa ndani ya nyumba zao au watakaoingia kwenye viwanja vya Al-Kaaba, watakuwa pia salama." Amri hii ilikuwa na maana kwamba kile ambacho waabudu masanamu hao wanachoweza kufanya kuokoa maisha yao, kilikuwa ni kubaki ndani ya nyumba zao, na kuepuka kushindana na wale wavamizi.

Washington Irving

Muhammad aliandaa msafara wa siri wa kuishtukiza Makka. Njia zote zinazoelekea Makka zilifungwa kuzui taarifa zozote za harakati zake kubebwa na kupelekwa

212

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Makka. Lakini miongoni mwa wakimbizi kutoka Makka, alikuwepo mtu mmoja, Hatib, ambaye familia yake ilibakia nyuma, na walikuwa bila kiunganisho au marafi-ki wa kuweza kujali juu ya ustawi wao. Hatib sasa alifikiria kupata msaada kwa ajili yao miongoni mwa Maquraishi, kwa kuisaliti mipango ya Muhammad. Yeye kwa hiyo, aliandika barua inayofichua lile jambo kubwa lililokusudiwa, na akaitoa mikononi mwa mwanamke anayeimba, ambaye alijitolea kuipeleka Makka. Mwanamke huyo alikuwa tayari njiani wakati Muhammad alipofahamishwa juu ya usaliti huo. Ali na watu wengine watano, wenye vipando vizuri, walitumwa kum-fukuzia huyo mjumbe. Walimkuta mara moja, lakini wakampekua mwili mzima bila mafanikio. Wengi wao wangejiachia huo upekuzi na kurudi lakini Ali alikuwa na hakika kwamba Mtume wa Allah (s.a.w.) asingeweza kukosea wala kupewa taarifa za uongo. Akichomoa upanga wake, aliapia kumuua huyo mjumbe labda barua ikitole-wa. Tishio hilo lilileta athari. Aliitoa barua hiyo kutoka kati ya nywele zake.

Hatib, katika kulaumiwa kwa usaliti wake, aliukubali; lakini alikiri shauku ya kupata msaada kwa ajili ya familia yake masikini, na uhakika wake kwamba barua ile isingekuwa na madhara, na isiyo na mafanikio dhidi ya malengo ya Mtume wa Allah

(s.a.w.).

Umar alizikataa sababu hizo na angemkata kichwa chake; lakini Muhammad, akikumbuka kwamba Hatib alipigana kishujaa katika kuitetea dini katika vita vya Badr, alimsamehe.

Muhammad, ambaye alikuwa hajui ni upinzani gani atakaokutana nao, alifanya ugawaji wa uangalifu wa vikosi vyake alipokuwa akikaribia Makka. Wakati kikosi kikubwa kilisonga mbele moja kwa moja, vikosi imara vilisonga juu ya vilima kwenye pande zote. Kwa Ali ambaye aliongoza kikosi kikubwa cha wapanda farasi, alikabidhiwa ile bendera tukufu, ambayo ilikuwa aisimike juu ya Mlima Hadjun, na kuibakisha hapo mpaka Mtume (s.a.w.) atakapoungana naye. Amri dhahiri zilitolewa kwa majenerali wote kuwa wenye subira, na kwa namna yoyote ile wasiwe wa kwan-za kushambulia.

(The Life of Muhammad)

Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliingia Makka tokea upande wa kaskazini. Usamah, mtoto wa rafiki yake na shahidi wa Muutah, Zayd bin Haritha, alikuwa amepanda nyuma ya farasi pamoja naye. Kichwa cha Muhammad kilikuwa kimeinamishwa chini, na alikuwa akisoma ile Sura kutoka ndani ya Qur'an iitwayo "Ushindi"

Ali alibeba ile bendera ya Uislamu alivyokuwa juu ya farasi mbele ya kile kikosi cha wapanda farasi. Mtume (s.a.w.) alimuamuru Zubayr bin al-Awwam kuingia mjini hapo kutokea upande wa Magharibi, na Khalid bin al-Walid kutokea upande wa Kusini. Alitoa amri kali kwa jeshi lake wasimuue mtu yoyote isipokuwa katika kujihami. Alitamani siku

213

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

nyingi kuyaharibu yale masanamu ndani ya Al-Kaaba lakini alitaka kufanya hivyo bila ya umwagaji damu wowote. Amri zake zilikuwa wazi na dhahiri; hata hivyo, Khalid aliuwa watu wa Makka 28 kwenye lango la Kusini la mji huo. Alisema kwamba alikutana na upin-zani.

Sir John Glubb

Utwaaji wa Waislamu, wa Makka ulikuwa kwa kweli si wa kumwaga damu. Yule mwenye harara, Khalid bin al-Walid aliua watu wachache kwenye lango la Kusini na alikaripiwa vikali na Muhammad kwa kufanya hivyo.

(The Great Arab Conquests)

Miaka nane kabla Muhammad aliondoka Makka kama mkimbizi pamoja na kunadiwa kichwa chake, na sasa alikuwa anaingia mji huo huo kama mtekaji wake. Tabia yake, hata hivyo, haikuashiria kiburi au hata kushangilia sana bali shukrani na unyenyekevu -shukrani kwa Allah (s.w.t.) kwa neema zake katika kuweka mafanikio juu ya Mtumwa wake mnyenyekevu, na unyenyekevu katika kuzingatia kiburi cha fahari za kidunia, na kufifia kwa vitu vyote vya kibinadamu.

Mtume (s.a.w.) aliingia na ngamia wake ndani ya viwanja vya Al-Kaaba, akashuka kwenye ngamia wake, akamwita binamu yake, Ali ibn Abi Talib, na wote wakingia ndani ya Al-Kaaba, wakizitambua zile Amri Tukufu kwa wale Mitume, Ibrahim na Ismail:

Usahihi-15.jpg

"...na tuliagana na Ibrahim na Ismail kwamba itakaseni Nyumba Yangu ..." (Sura y a 2; Aya ya 125)

Mtume (s.a.w.) pamoja na Ali waliikuta ile Nyumba ya Allah (s.w.t.), (Al-Kaaba) katika hali ya unajisi; ilikuwa imegeuzwa kuwa hekalu la masanamu 360, na ilibidi itakaswe. Mtume (s.a.w.) aliangusha chini kila sanamu huku akisoma Aya ifuatayo kutoka kwenye Qur'an:

Usahihi-16.jpg

"Ukweli umefika, na uongo umetoweka. Hakika ya uongo(kwa asili yake) lazima utoweke."

(Sura ya 17; Aya ya 81)

Sanamu kubwa sana ndani ya hekalu hilo lilikuwa ni lile la Hubal, mungu wa kifamilia wa ukoo wa Banu Umayya. Abu Sufyan alikwenda nalo juu ya ngamia kwenye vita vya Uhud

214

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kuwatia moyo wale wapiganaji kwa kuwepo kwake. Hubal aliwekwa juu ya kiegemeo kirefu, na Mtume (s.a.w.) hakuweza kumfikia. Yeye, kwa hiyo, alimwamuru Ali kupanda juu ya mabega yake, na kuliangusha chini. Katika kutii ile amri ya Kitume, ilimbidi Ali kusimama juu ya mabega ya Mtume; alilenga pigo kwenye yule mungu mkuu wa waabudu masanamu, na akamvunja vipande vipande. Kwa pigo lile kubwa, Ali aliweka mwisho wa kudumu kwa uabudu masanamu ndani ya ile Al-Kaaba! Al-Kaaba, Nyumba ya Allah (s.w.t.) ikawa imetakaswa!

Abul Kalam Azad

Baadhi ya masanamu yalikuwa yamewekwa juu ya viegemeo virefu na Mtume (s.a.w.) hakuweza kuyakuta. Alimuamuru Ali kupanda juu ya mabega yake na kuyaangusha chini. Ali akapanda juu ya mabega ya Mtume, na akayaangusha chini yale masanamu. Yeye kwa hiyo aliondoa uchafu wa uabudu masanamu kutoka kwenye Al-Kaaba kwa zama zote.

(The Messenger of Mercy, Lahore, Pakistan, 1970)

Wakati masanamu yote yalipokuwa yameharibiwa, taswira zote zilikuwa zimefutwa, na dalili zote zilizobakia za ushirikina zilikuwa zimefutiliwa mbali kabisa. Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) alimtuma Bilal kupiga Adhana. Bilal alipiga Adhana na bonde la Makka likavuma kwa ile takbir yake yenye nguvu na ya kuvutia. Mtume (s.a.w.) ndipo akafanya mizunguko saba ya Al-Kaaba, na akaswali Swala ya kutoa shukruni kwa Muumba wake.

Wakati huo huo, Maquraishi walikuwa wamekusanyika katika baraza ya Al-Kaaba wakim-subiri Mtume. Walitegemea kwamba angeonana nao kabla ya kutoa fatwa juu ya hatima yao.

Hapo Mtume (s.a.w.) alitokea kwenye kizingiti cha Al-Kaaba. Alilitazama lile kundi la watu lililokuwa mbele yake na akawahutubia kama ifuatavyo:

"Hakuna mungu ila Allah (s.w.t.) Yeye ni Mmoja na Mpweke kabisa, na Yeye hana washirika. Sifa zote na shukrani ni Kwake. Yeye ametimiza ahadi Yake. Amemsaidia mja wake kupata ushindi, na Ameyatawanya makundi ya maadui zake.

'Enyi watu! Nisikilizeni! Kiburi chote, majisifu, majivuno, na madai yote ya damu ya Nyakati za Ujahiliya yako chini ya miguu yangu leo.

'Enyi Maquraishi! Allah (s.w.t.) amevunja kiburi cha Zama za Ujahilia, na Yeye ame-vunja majivuno ya ukabila. Watu wote ni wana wa Adam, na Adam alikuwa ni ukafi tu udongo."

215

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mtume (s.a.w.) kisha akasoma Aya ifuatayo kutoka kwenye Qur'an:

Usahihi-17.jpg

"Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumeku jaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mbora zaidi kati yenu mbele ya Allah ni yule mcha-mungu zaidi miongoni mwenu. Hakika Allah ni Mwenye kujua, Mwenye habari." (Sura ya 49; Aya ya 13)

Aya hii ndio waraka wa usawa na udugu wa watu wote katika Uislamu. Hapawezi kuwa na tofauti yoyote kati ya watu kwa misingi ya ukabila, rangi, utaifa, ukoo wala utajiri. Bali wakati ambapo Uislamu unavunja tofauti za aina nyingine zote, unatetea sifa yake ya kipekee, na hiyo ni sifa ya imani na tabia.

Muhammad ndipo akawauliza swali Maquraishi: "Mnafikiri nitawafanya nini sasa?" Wakasema: "Wewe ni ndugu mkarimu, na mtoto wa ndugu mkarimu. Tunategemea wema na msamaha tu kutoka kwako." Akasema: "Nitawaambia kile Yusufu alichowaambia ndugu zake, 'hakuna lawama juu yenu leo.' (Qur'an. Sura ya 12 Aya ya 92). Ondokeni sasa, nyote ni waachwa huru wangu."

Mtume (s.a.w.) alitangaza msamaha wa jumla hapo Makka. Msamaha huo uliwafikia na makafiri pia. Alilikataza jeshi lake kuteka nyara za mji huo au kuzuia kitu chochote kili-chokuwa mali ya Maquraishi. Hao Maquraishi hawakuacha kukamilisha kitu chochote kuzingira uharibifu wake, na uharibifu wa Uislamu; lakini katika saa yake ya ushindi alisamehe makosa yao yote na uhalifu wao.

Maquraishi, hapo mwanzoni, walikuwa hawasadiki. Hawakuweza kuamini masikio yao wenyewe. Vipi Muhammad anaweza kuzuia vishawishi vya kuwaua wote, baada ya yote yale ambayo wamemtendea kwa zaidi ya miongo miwili, na hasa sasa hivi ambapo alikuwa ana mamlaka makubwa kiasi hicho mikononi mwake? Kule kutokupenda kwake Muhammad kutumia madaraka yake kulikuwa ni kitu ambacho kabisa kilizipita akili-tam-buzi za washirikina wa Makka. Muda mwingi ulipita kabla ya maana ya dhamira ya Muhammad kuingia akilini mwao, na ule msamaha ukaanza kuonekana wenye kuwezekana na wa kweli kwao.

Nia ya Muhammad, Mtume wa Amani, ilikuwa ni kuiteka Makka bila ya umwagaji wa damu, na katika hili alifanikiwa. Ilikuwa ni hapa ambapo alijidhihirisha mwenyewe, kwa maneno ya Qur'an Tukufu "...rehma kwa wanadamu wote." Historia haiwezi kutoa

216

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

mfano wa uvumilivu kama huo. Sio kwamba wapagani hawakuangamizwa tu; sio tu kwamba hawakuwa walipe fidia yoyote kwa makosa yao ya wakati uliopita; hawakuingili-wa katika umiliki wa zile nyumba ambazo Muhajiriin waliziacha hapo Makka, na ambazo walizikalia.

Kutoka pale kwenye al-Al-Kaaba, Mtume (s.a.w.) alikwenda kwenye Mlima Safa, na watu wa Makka walikuja kumthibitisha kama mkuu wao katika hali zake mbili - kama Mtume wa Allah (s.w.t.) na kama mtawala wao wa kidunia. Watu wote walitoa kiapo cha uamini-fu kwa Muhammad kwa kuweka mikono yao juu ya mkono wake. Baadae ikaja zamu ya wanawake kutoa hicho kiapo cha uaminifu. Lakini hakutaka kugusa mkono wa mwanamke yeyote ambaye hakuwa mke wake,. Yeye, kwa hiyo, alimtuma Umar ibn al-Khattab kupokea hicho kiapo cha wanawake kwa niaba yake.

Sir John Glubb

Mtume (s.a.w.) kisha akamtuma Umar ibn al-Khattab kupokea hivyo viapo vya wanawake.

(The Great Arab Conquests)

Wakati kula viapo kulipokwisha, Mtume wa Allah (s.a.w.) alijishughulisha na yale masu-ala mapya ya kisiasa na kiutawala yaliyotokana na ule ushindi wa Makka.

Ile Hadith nzito ya kuvutia ambayo ilianza mnamo Februari 12, mwaka 610, katika pango la Hira, ilifikia kileleni mnamo Februari 11, mwaka 630, katika baraza ya Al-Kaaba. Ilikuwa ni siku ya hisia, ahadi na sherehe, na siku kubwa katika historia, yenye umuhimu na uashiriaji. Ile hamu iliyoelekea kutokuwa na matumaini mwaka 620 kule Taif, imekuwa jambo kamilifu mwaka 630 hapo Makka.

Maquraishi waliendeleza mapambano marefu na makali dhidi ya Uislamu kwa miaka ishirini lakini wengi miongoni mwao sasa waliweza kuona kwamba yale masanamu ambayo waliyaabudu kama miungu yao, yalikuwa ni vitu bure kabisa. Wao, kwa hiyo, wal-iukubali Uislamu. Miongoni mwao, kulikuwemo na aina zote za watu waliosilimu: wachache ambao waliridhika kwamba Muhammad alikuwa ndiye Mtume wa kweli wa Allah (s.w.t.) na walimkubali yeye kama hivyo. Lakini kulikuwa na wengine wengi ambao waliukubali Uislamu kwa sababu walikuwa na kidogo sana cha kuchagua kutokana nacho. Walitambua kwamba ilikuwa hakuna sababu ya kupingana na kundi la wengi, na vile vile waliona kwamba hayakuwa maafikiano mabaya hata hivyo kujitangaza kuwa Waislamu, na walifanya hivyo, kwa mashaka gani, lilikuwa ni swali la kujibiwa na hali yenyewe ya baadae.

Watu wote wa ukoo wa Banu Umayya, pamoja na Hinda, mke wa Abu Sufyan, yule mla watu wa Uhud, pia "waliukubali" Uislamu.

217

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hapa mtu anaweza kuweka kituo kutafakari juu ya "kuukubali" Uislamu kwa Banu Umayya. Mtu anaweza kujisalimisha kwa adui kwa sababu ya hofu, na hofu pia inaweza kuufunga mdomo wake. Hofu inaweza kufanya mambo mengi lakini kuna kitu kimoja hai-wezi kukifanya - haiwezi kubadilisha chuki kuwa upendo. Kwa miaka ishirini, Banu Umayya wameongoza upinzani wa mapagani kwa Uislamu. Walifanya vita vya kiuchumi, kisiasa, kijeshi na kisaikolojia dhidi ya Mtume Wake, na dhidi ya wafuasi wake. Sasa kufikiria kwamba onyesho moja la nguvu za kijeshi lililoonyeshwa na Muhammad "lili-waridhisha" wao kwamba yeye alikuwa ni Mtume wa kweli wa Allah (s.w.t.) litakuwa ni vigumu kulitegemea kutoka kwenye asili ya mwanadamu. Hilo onyesho moja la uwezo la Waislamu halikubadili ile chuki, kinyongo na uchungu wa Banu Umayya kuwa upendo na haiba, hususan katika wakati ambao Uislamu umewanyima wao sio tu yale masanamu waliokuwa wakiyaabudu kama miungu yao bali pia umewanyima hadhi yao, fursa, uluwa na mamlaka. Walikuwa, kwa hiyo, na hali ile ile ya mawazo ambayo kila taifa linaloshind-wa linakuwa nayo. Mioyo yao ilikuwa imejaa chuki, kinyongo na hisia za kulipa kisasi dhidi ya walezi wa Uislamu.

Hawa Bani Umayya waliukubali Uislamu kwa kujirejea katika kuogopa sana kuvunjika kwa juhudi zote za upagani hapo Makka. Juhudi zao za kuokoa kale yao, na mapambano ili kudumisha uhusiano wao na upagani kama wapagani yameshindwa lakini pengine wangeweza kufanya kitu hicho hicho kama Waislamu. Mabingwa wa hayo masanamu, kwa hiyo, waliingia kwenye safu za waumini wakijifanya kama ni Waislamu. Hili lili-wafanya wao kuwa hatari zaidi kuliko hapo kabla wakati upinzani wao kwa Uislamu ulipokuwa dhahiri. Wakati huu, hata hivyo, walikwenda "kichinichini" wakivuta muda kusubiri fursa ya kujitokeza watakapouvunja Uislamu, kama ikiwezekana; la sivyo, basi watazibadili sifa-bainifu zake zinazoutambulisha, na wangerudisha desturi nyingi za Zama za Ujahilia kiasi iwezekanavyo.

Bani Umayya hawakuweza kuuharibu Uislamu wakati wa uhai wa Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) kwa sababu alichukua tahadhari zenye nguvu dhidi ya kuzuka tena kwa upagani. Alikuwa macho wakati wote, na hawakuweza kutoa mshitukizo wa ghafla kwake. Yeye pia alichukua tahadhari ya kutowapa nafasi yoyote ya madaraka ambayo wangeweza kuitumia kama msingi wao wa kujiongezea wenyewe.

Baadhi ya wanahistoria wamedai kwamba Mtume (s.a.w.) alikuwa na shauku ya kuwain-giza Bani Umayya katika utumishi wa Uislamu kwa vile walikuwa na ujuzi mwingi adimu na vipaji. Von Grunebaum, kwa mfano, anaandika hivi:

Muhammad kwa upande wake alihitaji uzoefu wa tabaka la watawala wa Makka; upanuzi wa umma na zaidi ya yote mfumo wake wa asili usingeweza kuendeshwa bila ya msaada wa wale watu wa mji huo.

(Classical Islam - A History 600-1258,1970)

218

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hili ni moja ya yale madai ambayo hayawezi kuthibitika mbele ya uchunguzi makini. Hakuna ushahidi kama Mtume (s.a.w.) aliwahi kamwe kuweka "uzoefu" wa Bani Umayya kwenye kazi yoyote. Lisilo na maana kama hilo hilo ni lile dai kwamba upanuzi wa umma na mfumo wake wa asili usingeweza kuendeshwa bila wao. Kama hao Bani Umayya walikuwa na uwezo huo wanaohusishwa nao, kwa nini hawakuutumia katika vita vyao beuzi dhidi ya Muhammad na Uislamu, na kwa nini walishindwa? Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliunda na kuimarisha ile Dola ya Kiislamu kwenye meno ya upinzani wa Bani Umayya. Hiyo Dola ya Kiislamu isingeweza kuishi pamoja kwa amani na utawala wa wachache wa kipagani uliokuwa ukiongozwa na Bani Umayya, na ilimbidi auangamize. Hakuwa amevutiwa na huo "uzoefu" wao kabla au baada ya kuukubali Uislamu, na hakumchagua yeyote kati yao kama jenerali au kama mtawala au hakimu au chochote kile. Hii sehemu ya sera yake juu yao haingeweza kuwa wazi zaidi.

Baadhi ya wanahistoria wa ki-Sunni wameeleza kwamba Mtume (s.a.w.) alimteua Mu'awiyyah, mtoto wa Abu Sufyan na Hinda, kuwa "mwandishi" wake wa kuandika Aya za Qur'an. Mu'awiyyah anaweza kuwa ameandika baadhi ya Aya za Qur'an lakini haina maana kwamba hazingeweza kuandikwa bila yeye. Wapo waandishi wengi wanaopatikana kwa Mtume. Kwanza kabisa, wakati Mu'awiyyah alipoingia Uislamu, nyingi ya Aya za Qur'an zilikuwa tayari zimekwisha teremshwa, na kulikuwa na kidogo, kama kilikuwepo, kwa yeye kuandika. Katika nafasi ya pili, alikuwa ni mmoja tu kati ya waandishi wengi. Kama kuandika Aya za Qur'an ni "sifa" kwake, basi anashirikiana pamoja na wanakili wengine wengi. Hata hivyo, Abdullah bin Saad bin Abi Sarh, yule ndugu wa kunyonya wa Uthman bin Affan pia alikuwa mwandishi. Alizibadilisha Aya za Qur'an alipokuwa anaziandika. Mtume (s.a.w.) alimtangaza yeye kama kafiri. Alikuwa auwawe lakini aliokolewa na Uthman. Mtume (s.a.w.) alimfukuza kutoka Madina.

Ujuzi wa Mu'awiyyah kama mwandishi, kwa hiyo, haukuwa mmoja ambao ulikuwa na upungufu katika baraza la Madina. Wanahistoria wamehifadhi majina 29 ya waandishi wa Mtume.

Hata hivyo, yale maelezo ya Von Grunebaum yaliyonukuliwa hapo juu, yanaweza, kwa kweli, kuwa sahihi, kama yakifanyiwa marekebisho kidogo kusomeka kwamba haikuwa Mtume (s.a.w.) wa Uislamu bali ni Abu Bakr na Umar waliohitaji uzoefu na ubingwa wa Bani Umayya, walikuwa ni wote hao ambao hawakuweza kuiongoza hiyo dola mpya bila ya msaada wao. Hao Bani Umayya walikuwa wa muhimu sana kwa Abu Bakr na Umar. Hadithi ya kufufuka kwa Bani Umayya wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr na Umar inaelezewa kwenye mlango mwingine.

Mtume (s.a.w.) hata hivyo, alijaribu kuwaridhisha kwa vitulizo kwa matumaini kwamba wangevua uadui wao kwa Uislamu, na siku moja, wao wenyewe au watoto wao wangekuwa Waislamu waaminifu. Lakini juhudi zake hazikuzaa matunda. Hakuna ali-

219

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

chowafanyia wao, ambacho kamwe kililainisha nyoyo zao kuelekea kwenye Uislamu. Kamwe hawakupata akili ya utambulisho na Uislamu au kuutii. Walikuwa kihisia, kiasili na kiitikadi hawawezi kukubaliana nao. Kwa kushindwa tu kufikia malengo yao kwa upan-ga, ndipo walipouona ulazima na kukubali amri ya amani. Lakini kwao wao, ni njia tu ime-badilika, sio mwisho.

Hiyo siku Abu Sufyan; mke wake Hinda, mtoto wao Mu'awiyyah, na watu wengine wa ukoo wa Umayya walipoukubali Uislamu, Farasi mnafiki wa ushirikina pia aliingia kwenye ngome ya Uislamu. Ali ibn Abi Talib, yule mwana falsafa wa Uislamu, alitoa mukhtasari wa asili ya uingiaji kwenye Uislamu wa Bani Umayya kama ifuatavyo:

"Bani Umayya hawakuwa Waislamu wa kweli, walijisalimisha tu, kwenye nguvu kuu -iliyowazidi"

Katika kutoa fatwa hii juu ya kusilimu kwa Bani Umayya na kuwa Waislamu, Ali alikuwa anafasili Aya ifuatayo kutoka kwenye Kitabu cha Allah (s.w.t.):

Usahihi-18.jpg

Mabedui wanasema: 'Tumeamini'. Sema (uwaambie) "Ninyi bado hamjaamini, bali semeni, 'Tumesilimu', kwani imani haijaingia katika nyoyo zenu." (Sura ya 49; Aya ya 14)

Mtume (s.a.w.) wa Uislamu alitumia majuma mawili hapo Makka kuwaelimisha wale watu wapya wa Makka walioingia katika Uislamu, na katika kuanzisha serikali ya mji ule. Alikuwa amekwisha "twahirisha" ile Al-Kaaba, na Waislamu sasa walikuwa wanaumiliki huo mji ambao ulikuwa ndio kitovu cha kijamii, kisiasa, kiutamaduni, kibiashara na kidi-ni cha Arabia. Makabila yote ya Kiarabu sasa yaliyatambua mamlaka ya serikali yake kama yenye umuhimu mkubwa.

Mtume (s.a.w.) aliimarisha yale maeneo mapya yaliyopatikana kati ya Makka na Madina na sehemu zilizo karibu ya Makka. Ndipo yeye akaanza kazi ya kuitengeneza upya ile jamii ya Ki-Arabu. Huko nyuma, Waarabu walikuwa na uzoefu wa miundo ya asili ya uka-bila na ukoo tu katika mfumo wao wa kijamii lakini sasa wamekuwa "taifa" (umma) chini ya uongozi wake. Uwajibikaji wao kama Waislamu, haukuangalia asili ya rangi zao, ushirikishwaji wa kikabila, uhusiano wa kitaifa au kilugha au hata mipaka ya kijografia. Uwajibikaji wa Waislamu ulivuka vikwazo vyote vya asili na tofauti zilizowekwa na binadamu. Walipaswa kutoa uaminifu wao mpya kwenye Jumuiya ya Waumini ambayo ilimkiri Allah (s.w.t.) kwamba ni Mmoja, na Muhammad kama Mtume Wake.

220

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Makabila mengi karibu ya Makka yalikuwa bado ni wapagani, na Mtume (s.a.w.) alitaka kuwalingania kwenye Uislamu. Pia, yalikuwepo makabila mengine ambayo yalikuwa yameupokea Uislamu lakini yalikuwa bado Hayajalipa Zaka zao kwenye Hazina ya Umma, na alitaka awakumbushe kulipa madeni yao yale. Yeye, kwa hiyo, alituma wajumbe wakakusanye Zaka katika pande mbalimbali, pamoja na maagizo maalum juu ya kazi zao, wajibu na madaraka yao.

Mmoja wa hawa wakusanyaji wa Zaka alikuwa ni Khalid bin al-Walid. Mtume (s.a.w.) alimtuma kwa kabila la Banu Jadhima kukusanya Zaka zilizokuwa hazijalipwa lakini alivuka mipaka ya madaraka yake, na akaitia doa mikono yake kwa damu ya Waislamu wasio na hatia!

Muhammad ibn Ishaq

Msafara wa Khalid baada ya kutekwa Makka, kwa Bani Jadhima wa Kinana, na msa-fara wa Ali kusahihisha makosa ya Khalid.

Hakim aliniambia kwamba Mtume (s.a.w.) alimwita Ali na akamwambia aende kwa hawa watu na kuliangalia suala lao, na kukomesha vile vitendo vya zama za upagani. Hivyo Ali alikwenda kwao pamoja na fedha ambazo Mtume (s.a.w.) alizituma na akalipa fidia ya damu na akafidia hasara zao za kifedha. Wakati damu na mali vyote vilipokuwa vimekwisha kulipiwa bado alikuwa na pesa zilizobakia. Aliuliza kama kuna fidia yoyote ambayo ilikuwa haijalipiwa bado na waliposema hakuna, aliwapa zile pesa zilizobakia kwa niaba ya Mtume. Kisha alirudi na kutoa taarifa kwa Mtume (s.a.w.) alichokuwa amekifanya naye akamsifu. Kisha Mtume (s.a.w.) akasimama na akielekea Qibla, akanyanyua mikono yake juu, na akasema: Ewe Allah (s.w.t.)! Mimi sina hatia mbele Yako kwa aliyoyafanya Khalid. Haya ameyafanya mara tatu.

Khalid na Abdur Rahman ibn Auf walijibizana kwa maneno makali kuhusu jambo hili. Huyu Abdur Rahman akamwambia Khalid: "Umefanya kitendo cha kipagani katika Uislamu." Khalid akasema kwamba alikuwa amelipiza tu kisasi cha baba yake Abdur Rahman. Yeye akamjibu kwamba ni muongo kwa sababu yeye Abdur Rahman mwenyewe alimuua yule muuaji wa baba yake, lakini Khalid alilipiza kisasi cha ami yake hivyo kwamba kulikuwa na hisia mbaya kati yao.

Katika kuyasikia haya Mtume (s.a.w.) akamwambia Khalid: "Waache maswahaba wangu, kwani Wallahi kama ungekuwa na mlima wa dhahabu na ukautumia katika njia ya Allah (s.w.t.) usingeweza kukaribia sifa njema za maswahaba wangu."

(The Life of the Prophet)

221

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Washington Irving

Akiwa kwenye ujumbe maalum (akiwa njiani kuelekea Tehama) Khalid bin Walid ilimbidi apitie kwenye nchi ya kabila la Jadhima. Alikuwa na watu 350 pamoja naye na alikuwa amefuatana na Abdur Rahman, mmoja wa waliosilimu mapema sana. Maagizo yake kutoka kwa Mtume (s.a.w.) yalikuwa ni kuhubiri amani na mapenzi, kufundisha dini, na kujiepusha na vurugu, vinginevyo labda wakishambuliwa.

Sehemu kubwa ya hilo kabila la Jadhima walikuwa wameingia kwenye Uislamu lakini baadhi yao walikuwa bado ni wa dini ya Sabean. Katika wakati uliopita kabila hili lili-pora na kumuua ami yake Khalid, pia na baba wa Abdur Rahman, walipokuwa wakire-jea kutoka Arabia ya shangwe. Wakiogopa kwamba Khalid na jeshi lake wanaweza kulipiza kisasi kwa matendo yale mabaya, walijiandaa na silaha katika kuwasogelea kwao. Khalid kwa siri alifurahia katika kuwaona wakija (juu ya vipando vyao) kuwala-ki katika mpango huu wa kivita. Akiwasalimia kwa sauti ya haraka haraka, aliwauliza kama walikuwa Waislamu au makafiri. Walijibu kwa mkazo wa sauti ya kugugumia, "Waislamu." " Kwa nini basi mnakuja kutulaki mkiwa na silaha mkononi?" "Kwa sababu tunao maadui miongoni mwa makabila ambao wanaweza kutushambulia sisi kwa ghafla," walisema. Khalid kwa ukali kabisa aliwaamuru kushuka chini na kuweka silaha zao pembeni. Baadhi yao walikubali. Na mara moja walikamatwa na kufungwa kamba; wale waliobakia wakakimbia. Akichukulia kukimbia kwao kama kukiri makosa yao, aliwaandama kwa mauaji makubwa; akaiharibu nchi hiyo, na katika kuchemka kwa raghba yake aliwaua hata baadhi ya wale wafungwa.

Muhammad, wakati aliposikia juu ya hiki kitendo kiovu na cha kikatili, alinyanyua mikono yake juu mbinguni, na akamuomba Allah (s.w.t.) Ashuhudie kwamba yeye hakuwa na hatia juu ya hilo. Khalid wakati alipolaumiwa nalo wakati aliporudi, hakuwa na jibu akahamishia lawama zote kwa Abdur Rahman, lakini Muhammad akakataa kwa hasira tuhuma zozote dhidi ya mmoja wa wafuasi wake wa awali na mashuhuri. Yule Ali mkarimu alitumwa mara moja kwenda kurudisha kwa watu wa Judham kile ambacho Khalid alikinyang'anya kutoka kwao, na kufanya fidia ya kifedha kwa ndugu wa wale waliouawa.

Ilikuwa ni kazi inayoendana na tabia ya Ali, na aliitekeleza kwa uaminifu. Akiulizia juu ya hasara na mateso ya kila mtu mmoja, alimlipa mpaka akaridhika kabisa. Wakati kila hasara ilipokuwa imefidiwa, na damu yote kulipiwa, aligawanya zile pesa zili-zobakia miongoni mwa watu, akifurahisha kila moyo kwa ukarimu wake. Hivyo Ali alizipokea shukurani na sifa za Mtume, lakini huyu mlipiza kisasi Khalid alilaumiwa na hata wale aliofikiria kuwafurahisha. "Tazama" alimwambia Abdur Rahman, "Nimelipiza kisasi cha kifo cha baba yako." "Badala yake sema," huyu mwingine alimjibu kwa hasira, "umelipiza kifo cha ami yako. Umeifedhehesha dini kwa kitendo kinachomstahili muabudu sanamu."

(The Life of Muhammad)

222

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Sir John Glubb

Baada ya kuikalia Makka, wajumbe walitumwa kwa yale makabila yanayoizunguka kuwasisitiza wao wAyaharibu masanamu yao ya kienyeji na madhabahu ya kipagani. Kikundi kimoja kama hicho kiliongozwa na Khalid bin Walid, yule mshindi wa Uhud. Khalid alikuwa ni mpiganaji mwenye mafanikio makubwa lakini mtu mkaidi, mwenye vurugu na mwenye kiu ya damu. Alitumwa kwa Bani Jadhima, ukoo wa Banu Kinana, katika ukanda wa Pwani Kusini-Magharibi ya Makka.

Kwa majonzi yaliyoingiliana wakati mmoja, hawa Bani Jadhima walikuwa wamemuua ami yake Khalid miaka mingi kabla, wakati alipokuwa anarudi kutoka kwenye safari ya kibiashara ya Yemen. Mtume, ambaye yumkini alikuwa hajui kwamba Khalid ana ugomvi binafsi na wale watu aliotumwa kuwasilimisha, alimwambia aepuke umwagaji damu. Wakati alipowakuta. Bani Jadhima, Khalid ali-waambia waweke silaha zao chini kwani vita ilikuwa imekwisha na kila mmoja sasa ameukubali Uislamu. Wakati walipokuwa wamefanya hivyo, hata hivyo, yeye ghafla alikamata idadi kadhaa ya watu hao, akawafunga mikono yao nyuma ya migongo yao, na akatoa amri kwamba wakatwe vichwa vyao, kama kisasi kwa ajili ya kuuawa kwa ami yake.

Mpanda farasi mmoja wa Kiarabu aliyekuwa pamoja na jeshi la Khalid, baadaye alieleza jinsi kijana mmoja wa Bani Jadhima, mikono yake ikiwa imefungwa, alivy-omuomba yeye amruhusu kuongea na wanawake kadhaa waliokuwa wamesimama mbali kidogo. Yule mwislamu alikubali na akamuongoza yule mfungwa kuelekea kwa wale wanawake. "Kwa heri, Hubaisha," yule kijana alimwambia msichana mmoja miongoni mwao, " maisha yangu yako mwishoni sasa." Lakini msichana alip-iga kelele, "Hapana, hapana, maisha yako yarefushwe kwa miaka mingi ijayo." Yule mfungwa aliongozwa kurudishwa na mara moja akakatwa kichwa chake. Alipokuwa anaanguka, yule msichana alitoka kwenye lile kundi la wanawake na akamkimbilia. Akimuinamia, alimgubika na mabusu mengi, akikataa kumuachia mpaka walipomuua na yeye pia.

Mtume (s.a.w.) kwa kweli alishitushwa pale aliposikia juu ya kitendo cha Khalid. Akiwa amesimama kwenye uwanja wa Al-Kaaba, alinyanyua mikono yake juu ya kichwa chake na akakemea kwa sauti: " Ewe Allah! Mimi sina hatia mbele Yako kwa kile Khalid alichokifanya." Ali alitumwa mara moja pamoja na fungu kubwa la pesa kulipa fidia ya damu kwa ajili ya wale wote waliokuwa wameuawa, na fidia ya ukarimu kwa ajili ya hasara yoyote ya mali.

(The Life and Times of Muhammad, 1970, uk.320)

223

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Muhammad Husein Haykal

Muhammad alikaa Makka kwa siku kumi na tano wakati ambapo alisimamia mambo ya mji huo na akawaelekeza watu wake kwenye Uislamu. Katika kipindi hiki, alitu-ma wajumbe kuwalingania watu kwa amani kwenye Uislamu na kuharibu masanamu bila ya kumwaga damu yoyote. Khalid ibn al-Walid alitumwa huko Nakhlah kumharibu al-Uzza, mungu wa kike wa Banu Shayban. Kazi yake ilipokamilika, ibn al-Walid aliendelea kuelekea Jadhimah. Kule, hata hivyo, watu walikamata silaha wakati wa kukaribia kwake. Khalid aliwaambia waweke silaha zao chini kwani watu wote walikuwa wameukubali Uislamu. Mmoja wa wale watu wa kabila la Jadhima aliwaambia watu wake: "Ole wenu, Banu Jadhima! Ninyi hamjui kwamba huyu ni Khalid? Wallah hakuna kinachowangojeni ninyi mara mtakapokuwa mmeweka chini silaha zenu isipokuwa utekwaji, na mara mtakapokuwa mateka, msitegemee chochote bali kifo." Baadhi ya watu wake wakajibu: "Unatafuta kutufanya sisi wote tuuawe? Wewe hujui kwamba watu wengi wameingia kwenye Uislamu, kwamba vita vimek-wisha, na kwamba usalama umerudishwa tena?" Wale walioshikilia wazo hili walien-delea kuongea na watu wa kabila lao mpaka wakasalimisha silaha zao. Papo hapo, ibn al-Walid akaamuru wafungwe kamba, na akawauwa baadhi yao. Wakati alipozisikia habari hizi, Mtume (s.a.w.) alinyanyua mikono yake kuelekea juu mbinguni na akaomba: "Ewe Allah! Ninakishutumu kile Khalid ibn al-Walid alichokifanya."

Mtume (s.a.w.) alimpa pesa Ali ibn Abi Talib na akamtuma kwenda kuchunguza mambo ya kabila hili, na kumtahadharisha kupuuza desturi zote za kabla ya Uislamu. Alipofika, Ali alilipa fidia ya damu ya waathirika wote na akafidia wenye mali zao kwa kuharibiwa kwao.

Kabla ya kuondoka, alizitoa zile pesa zote ambazo Mtume (s.a.w.) alimpa kwa kabila hilo kiasi tu kwamba kama kulikuweko na hasara zozote zile ambazo zingeweza kukosa kuonekana kwa wakati ule.

(The Life of Muhammad, Cairo,1935)

Ule ujumbe wa kidiplomasia ambao Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) alio-ufanya kwa kabila la Jadhima, kupitia kwa Ali, ulikuwa wa muhimu kabisa, Khalid alikuwa ameua watu ambao hawakuwa ni Waislamu tu bali pia walikuwa hawana hatia ya kosa lolote. Kukosa kufanya marekebisho ya maovu yake kungeweza kuwapatia Waislamu sifa sio tu kwa ukatili usio na maana na matumizi mabaya tele ya madaraka, bali pia kwa usaliti. Wapagani na wale Waarabu ambao wangeweza kuitwa Waislamu, katika tarehe hizi za mwanzo, kwa heshima tu, wangeweza, bila kukwepa, kuunganisha vitendo viovu vya Khalid na Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Ilikuwepo hata hatari kwamba wataweza kuukana Uislamu na kurudi tena kwenye uabudu masanamu, kwa kumchukia Khalid tu. Mtume, kwa hiyo, aliingia ndani ya Al-Kaaba, na mara tatu akakikana hadharani kitendo cha Khalid, na akaiomba Mbingu iwe ni Shahidi kwamba hakuwa na lawama juu ya hilo.

224

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hawa Bani Jadhima waliachwa wamekongolewa na kuvunjwa kabisa na Khalid. Mtume (s.a.w.) alitaka sio kuwafariji tu na kuwajenga upya, bali pia kurudisha imani na mapenzi yao. Ilikuwa ni kazi ngumu na yenye kuhitaji uangalifu sana, na alimchagua Ali kuitekeleza. Khalid alikuwa ameharibu picha ya Uislamu, na Mtume (s.a.w.) alijua kwam-ba hakuna yoyote miongoni mwa maswahaba wake isipokuwa Ali aliyekuwa na uwezo wa kuirudishia mng'ao wake halisi.

Ali alithibitisha mara nyingine tena kwamba bwana wake asingeweza kumchagua mtu yeyote bora kuliko yeye kwa kazi hii nyeti, na alidhihirisha mara nyingine tena kwamba alikuwa wa kwanza katika vita, na alikuwa pia ni wa kwanza katika amani. Aliwashangaza na kuwavutia sana Bani Jadhima kwa uadilifu wake, ukarimu wake, wema wake, na kuji-husisha kwake juu ya furaha yao na ustawi wao.

Kwa ubora wake wa kuhutubia, Ali alizikamata tena nyoyo za Bani Jadhima kwa ajili ya bwana wake, Muhammad Mustafa, na kwa Uislamu. Huu ulikuwa ni wajibu ambao ulikuwa "unaafikiana" na yeye kuutimiza. Aliupenda wajibu huu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Alipenda kufunga vidonda vya kisaikolojia vya watu wengine, na alipenda kuleta furaha na faraja kwenye mioyo iliyo na majonzi. Alijaaliwa na kila kipawa maalum kutekeleza wajibu kama huu.

225

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Vita vya Hunain

Kule kutekwa kwa Makka kulichochea uingiaji kwa wingi wa Waarabu kwenye Uislamu katika sehemu nyingi za nchi hiyo. Lakini yalikuwepo baadhi ya makabila yaliyokuwa yakiishi Mashariki na Kusini-Mashariki ya Makka ambayo hayakutaka kuacha uabudu masanamu. Walitishiwa na maendeleo ya haraka ya Uislamu, na walifikiria kwamba kama utaendelea kuenea kwa kasi hiyo hiyo, watazungukwa na Waislamu hivi karibuni, na watakuwa wametengwa na makabila mengine ya wapagani.Viongozi wao waliwaza kwamba haitakuwa busara kuwaacha Waislamu waunganishe mafanikio yao ya hivi karibuni na kuwa na nguvu sana. Wao, kwa hiyo, waliamua kuchukua hatua mara moja kwa kuwashambulia Waislamu huko Makka na kuwaagamiza. Makabila makubwa miongoni mwao yalikuwa ni Thaqiif, Hawazin, Bani Sa 'ad na Banu Jashm, wote wapiganaji wakali, wenye wivu na uhuru wao na wenye fahari na mila zao za kivita. Walikuwa wamefahamu kwamba Makka imesalimu amri kwa Muhammad bila ya kufanya shambulio lolote lakini walihusisha kule kushindwa kwa watu wa Makka kukataa kuswalimu amri kwake na tabia yao ya kike. Na kwa upande wao wenyewe, walikuwa na imani kwamba walikuwa na uwezo zaidi katika uwanja wa mapambano kuliko wapiganaji wa Kiislam au wapiganaji wo wote wengine.

Mwishoni mwa Januari 630, Mtume (s.a.w.) alipokea taarifa kwamba kabila la Thaqiif na Hawazin walikuwa wameondoka kwenye kituo chao cha nyumbani, na walikuwa wanakwenda kuelekea Makka. Wakati habari hizi zilipothibitishwa, yeye pia aliagiza uku-sanyikaji wa jumla ndani ya ule mji uliotekwa hivi karibuni.

Mtume (s.a.w.) hakutaka Makka igeuke uwanja wa mapambano.Yeye, kwa hiyo, haraka sana akaondoka Makka mnamo Januari 26,630 akiongoza wapiganaji 12,000, kwenda kukutana na adui. Kutoka kwenye jeshi hili, watu elfu kumi walikuwa wanatoka Madina, na wale wengine elfu mbili walikuwa ni askari wapya kutoka watu wa Makka waliosilimu hivi karibuni.

Jeshi hili jipya lilikuwa ndio jeshi kubwa sana liliwahi kukusanywa katika Arabia mpaka wakati ule. Wakati mipangilio yake mbali mbali ilipokuwa inatoka nje ya lango la mji, katika mavazi maridadi ya kivita, Abu Bakr aliyekuwa anaangalia, alivutiwa sana, na akatam-ka ghafla: "Hatuwezi kushindwa safari hii kwa sababu ya kukosa wingi." Lakini mapema sana akathibitika kwamba amekosea. Waislamu walishindwa mwanzoni ingawa walikuwa mara tatu ya wingi wa adui. Qur'an yenyewe ilitaka tahadhari ya Waislamu, kwa uwazi hasa, kwamba wingi peke yake haukuwa hakikisho kwamba watakuwa washindi.

226

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Sir William Muir

Majuma manne yalikuwa yamepita tu tangu yeye (Muhammad) alipokuwa ametoka Madina, wakati aliposonga mbele kutoka Makka akiongoza vikosi vyake vyote, viki-wa vimetuna sasa, kwa kuongezeka kwa kikosi cha kuongeza nguvu kutoka Makka, kwenye idadi kubwa ya watu 12,000. Safwan, kwa maombi yake, alimpatia yeye suti mia moja za deraya na kibanda kizima cha silaha kamili na ngamia wengi kiasi. Ule mpango wa askari wa makabila, kila moja likiwa na bendera inayopepea mbele yake, ulikuwa wa kushangaza sana kiasi kwamba Abu Bakr alianza ghafla, wakati vile vikosi vilivyopangwa vilipopita, kwa ugutaji huu wa ghafla: "Leo hii hatutashindwa kwa sababu ya uchache wa idadi yetu."

(Life of Muhammad, London, 1861)

Wakati ile safu ya kwanza iliyokuwa na kikosi cha Waislamu, kikiongozwa na Khalid ibn al-Walid, kilipoingia kwenye bonde la Hunain upande wa Kusini-Mashariki ya Makka, adui tayari alikuwa amelala kwenye mavizio, tayari kukipokea kwa silaha zake za makombora. Mwanya ulikuwa mfinyu sana, njia ilikuwa mbaya sana, na Waislamu walikuwa wanasonga mbele dhahiri kwa kutotambua kuwepo kwa adui. Ilikuwa kabla tu ya mawio wakati kwa ghafla tu, Hawazin walipoanzisha shambulizi lao.

Fumanizi hili lilikuwa halikutegemewa kabisa na shambulizi la adui lilikuwa la haraka sana kiasi kwamba Waislamu hawakuweza kulihimili. Kikosi hicho, kilichoundwa na watu wa kabila la Banu Sulaym, kilivunjika na kikakimbia. Sehemu kubwa ya jeshi hilo ilikuwa nyuma kidogo tu. Safu ya Khalid ilipata pigo usoni mwake, na likatia hofu ndani ya watu wake hivyo kwamba wao pia waligeuzia migongo yao kwa adui. Na wakaanza kukimbia. Mara kila mtu katika jeshi hilo alikuwa anakimbia, na haikuchukua muda kabla Muhammad hajaachwa peke yake pamoja na wafuasi wake waaminifu wachache karibu yake.

Watu waliokuwa wakiongozwa na Khalid ndio wa kwanza kukimbia mbele ya maadui wanaoshambulia, na walifuatiwa na wale Umayya wa Makka waliosilimu hivi karibuni na marafiki zao na wafuasi wao. Nyuma yao walikuwa raia wa Madina. Waislamu wengi wal-iuawa katika kukimbia huko, na wengine wengi walijeruhiwa. Mtume (s.a.w.) aliwaita wale watoro lakini hakuna hata mtu mmoja aliyemsikiliza.

Jeshi la Waislamu lilikuwa katika msambaratiko wa kukimbia bila mpango na adui waki-wa kwenye kasi kali ya kuwafukuza. Mtume, kwa kweli, hakuondoka kwenye nafasi yake, na alisimama imara kama jiwe. Watu nane walikuwa bado wako naye, wote wakitazama kioja cha kukimbia kwa jeshi lao. Walikuwa ni:

227

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

1. Ali ibn Abi Talib

2. Abbas ibn Abdul Muttalib

3. Fadhil ibn Abbas

4. Abu Sufyan ibn al-Harith ibn Abdul Muttalib

5. Rabi'a, kaka yake Abu Sufyan ibn al-Harith

6. Abdullah ibn Masood

7. Usamah ibn Zayd ibn Haritha

8. Ayman ibn Ubaid

Kati ya hawa nane, watano wa mwanzo walikuwa ni wa ukoo wa Banu Hashim. Walikuwa ni ami zake na binamu zake Mtume.

Mtume (s.a.w.) alimwomba ami yake, Abbas ibn Abdul Muttalib, kuwaita wale Waislamu waliokuwa wanakimbia. Abbas alikuwa na sauti yenye nguvu sana, na akaguta: "Enyi Muhajirina na Enyi Ansari! Enyi washindi wa Badr na enyi watu wa Mti wa Kiapo! Mnakwenda wapi? Mtume wa Allah (s.a.w.) yuko hapa. Rudini kwake." Sauti ya Abbas ilivuma katika lile bonde finyu na karibu kila mtu aliisikia, na ilionekana kuwa na matokeo katika kusimamisha kukimbia kwa Waislamu.

Ansari walikuwa wa kwanza kusimama, na kurudi kwenye vita. Wakitiwa moyo na mfano wao, wengine pia walipata nguvu tena. Mara wakaweza kujikusanya tena. Mapambano makali yalitokea. Mwanzoni, matokeo yalionekana kutokuwa na uhakika lakini baadae Waislamu walianza kuwabana maadui. Mara tu waliporudisha hamasa zao, wakafanya mashambulizi. Adui bado alipigana kijasiri lakini wakazuiwa katika usogeaji wao na ile adadi kubwa ya wanawake na watoto aliokuja nao. Waislamu walizidi kusonga mbele na baadae ilikuwa ni Mabedui ambao walikuwa wanakimbia pande zote.

Sir William Muir ameielezea Hadith ya kushindwa na kupata nguvu tena kwa Waislamu katika vita vya Hunain kwa kirefu kiasi. Anaandika katika kitabu chake, The Life of Muhammad, (London, 1877) hivi:

Mapema sana wakati wa asubuhi, ambapo alfajiri ilikuwa bado ya rangi ya kijivu, na anga ikiwa imetanda mawingu, jeshi la Muhammad lilikuwa kwenye mwendo. Akiwa amevaa mavazi kamili ya kivita, kama kwenye siku ya Uhud, alipanda juu ya farasi wake mweupe, Duldul, nyuma ya vikosi vyake.

Kikosi kilichoundwa na Banu Sulaim na kikiongozwa na Khalid, walikuwa wakipan-da kwa msururu taratibu juu ya njia ya mlimani ya mteremko na nyembamba, wakati ghafla Hawazin walipochupa kutoka kwenye mavizio yao, na wakawashambulia kwa kasi. Wakibumbuazwa na uvamizi huu wa ghafla, Banu Sulaim walikatika na kurudi nyuma. Mshituko huu ulipita kutoka safu hadi safu. Wakikerwa na utusitusi wa saa

228

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

hizo, na wembamba na mikunjokunjo ya njia, hofu ikalishika jeshi lote; wote waligeuka na wakakimbia. Jinsi kikosi kwa kikosi walivyoharakisha kumpita yeye, Muhammad alikemea: "Mnakwenda wapi? Mtume wa Allah (s.w.t.) yuko hapa! Rudini! Rudini! - lakini maneno yake hayakuwa na athari yoyote, isipokuwa kikun-di cha marafiki na wafuasi waliojitolea walijikusanya karibu naye.

Kiwewe kiliongezeka, kundi la ngamia lilisukumana bila mpango mmoja dhidi ya mwingine; ilikuwa kelele tupu na ghasia, na sauti ya Muhammad ilipotea katikati ya mshindo huo. Mwishoe, walipoona zile safu za vikosi vya Madina vikiondoka katika kukimbia kwa pamoja, alimuambia ami yake, Abbas, aliyekuwa ameshikilia farasi wake, kuita kwa sauti kubwa: "Enyi watu wa Madina! Enyi wa Mti wa Kiapo! Enyi watu wa Surat Baqra !" Abbas alikuwa na sauti yenye nguvu sana, na alipoguta maneno haya tena na tena kwa sauti yake yote, yalisikika mbali na karibu. Mara moja yakagusa hisia katika nyoyo za watu wa Madina. Walizuiwa katika kukimbia kwao, na wakaharakisha kwa Muhammad, wakipiga kelele, "Ya Labeik! Sisi tuko hapa kwa mwito wako!" Watu mia moja kati ya hawa wafuasi watiifu, walijinasua kwa taabu kutoka kwenye wale ngamia waliokuwa wameziba ile njia finyu, wakajitupa juu ya adui aliyekuwa anasonga mbele na kusimamisha maendeleo yake. Lilipopata nafuu kutokana na shinikizo, lile jeshi lilipata nguvu polepole, na likarudi kwenye vita. Mapambano yalikuwa makali; na matokeo, kutoka na ubaya wa asili wa ardhi na kishindo cha Mabedui wakali, yalibakia kwa muda kiasi ya mashaka. Muhammad ali-panda kwenye kilima na akaangalia yale mapambano. Akitiwa nguvu na yale mand-hari, alianza kuguta kwa sauti kubwa; "Sasa ndio tanuru limepata moto: Mimi ni yule Mtume asiyesema uongo. Mimi ni kizazi cha Abdul Muttalib."

Kisha akimuagiza Abbas kumuokotea ukofi wa changarawe, aliutupa kuelekea kwa maadui, akisema, "Maangamizi yawakamate hao!" Walikuwa kwa kweli tayari wamekwishayumba. Uimara wa kikosi cha Madina, na shauku ya wale waliobakia wakati pale walipoitwa tena, ulikuwa umepata ushindi. Adui alikimbia, na ushindi ulikuwa kamili. Wengi waliuawa na kwa nguvu sana Waislamu waliendeleza mashambulizi, kiasi kwamba waliuwa miongoni mwa waliobakia, baadhi ya watoto wadogo - ukatili ambao Muhammad alikuwa ameukataza kabisa.

Betty Kelen

Waislamu waliweka kambi mbali na Bonde la Hunain na wakati wa alfajiri wakam-sogelea adui kupitia kwenye njia nyembamba. Mtoto wa Umar anaelezea kile kili-chotokea baadae:

"Tuliteremka kupitia kwenye korongo kavu la mto, pana na lenye mteremko tukishu-ka polepole katika mwanga hafifu wa asubuhi; lakini adui alikuwa pale kabla yetu na alikuwa amejificha katika vinjia vidogo, njia za pembeni na sehemu finyu. Walikuwa

229

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

katika jeshi, wakiwa na silaha kamili wakijua hasa ni nini cha kufanya, na Wallahi, tulikuwa na hofu wakati tuliposhuka na ghafla Hawazin walitushukia kama mtu mmoja!

Mabedui walishambulia kwa mawe, majabali, mishale, mikuki na panga. Kile kikosi cha Muhammad, chini ya jenerali Khalid, kilivunjika, ngamia wakasukumana na kugongana, wakilia kwa mikwaruzo na kusongamanisha miguu yao mirefu.

Yeye Muhammad aliona miongoni mwa wale watu wanaokimbia, wafuasi wake wapya kutoka Makka, na aliwaita wao kama mmoja wao wenyewe: 'Mnakwenda wapi enyi watu? Rudini! Njoni kwangu! Mimi ni Mtume wa Allah (s.w.t.) Mimi ni Muhammad, mtoto wa Abdullah!'

Sio hata mmoja aliyesikiliza, na kwa nini wasikilize? Alikuwepo mpiganaji wa Hawazin akiwafukuza akiwa juu ya ngamia wa rangi ya damu ya mzee, bendera yake ikipepea kutoka kwenye mkuki mrefu, na kila wakati alipoutumbukiza ubapa wa mkuki ule, ulichomoza upande mwingine wa kifua cha mtu. Sauti ya Mtume (s.a.w.) ilizama kwenye makelele ya watu, na milio ya ngamia. Alimuambia ami yake Abbas, mtu mwenye mapafu makubwa, kuchukua huo mwito, 'Enyi marafiki, ukumbukeni ule mti wa mkangazi...' Na Ali, akiwa kimya kabisa lakini katika mapambano kama jinni mkali, alirukaruka kiushindi karibu yake, akipigania kufika nyuma ya farasi wa yule kiongozi wa Hawazin na kumlemaza.

(Muhammad, Messenger of God) Muhammad Husein Haykal

Waislamu walifika Hunain wakati wa jioni na wakaweka kambi kwenye mlango wa bonde hilo mpaka alfajiri. Wakati wa alfajiri siku iliyofuata jeshi hilo lilianza kuon-doka, na Muhammad, akiwa amempanda farasi wake mweupe, alikuwa nyuma wakati Khalid ibn al-Walid, akiongoza kikundi cha askari kutoka Banu Sulaym, alikuwemo kwenye kikosi hicho.

Wakati Waislamu walipokuwa wanapita kwenye korongo la Hunain, Malik ibn Awf aliamuru jeshi lake kushambulia katika giza kabla ya alfajiri, kwanza kwa mishale na kisha kwa shambulizi la jumla. Safu za Waislamu zikavunjika na waliingiwa na hofu. Baadhi yao walikimbia kutoka nje ya korongo hilo haraka sana kama walivyoweza katika kutafuta usalama. Akishuhudia kile kilichowakuta Waislamu, Abu Sufyan hakuhisi kutokuwa na furaha hata ndogo kwa kushindwa maadui zake wa awali ambao mpaka sasa walikuwa wakisherehekea ushindi wao juu ya Makka. Alisema, "Waislamu hawatadhibitiwa mpaka wawe wametupwa ndani ya bahari."

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

230

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Makabila ya kipagani yalishindwa lakini yaliweza kujikusanya tena, na yanasemekana kuweza kurudi nyuma kwa mpango mzuri kutoka kwenye bonde la Hunain.

D.S.Margoliouth

Jenerali Malik, mtoto wa Auf, anasemekana kukusanya wapanda farasi wake wa kutosha kufanya waweze kusimama imara mpaka watu dhaifu wa kundi lao wawe wamekingwa, na kisha waweze kuwafikisha kwenye usalama kwenye kilima ambapo wanaweza kupata njia yao ya kwenda Taif. Pale ni dhahiri baadhi ya wanawake waliokolewa, ingawa wengine waliangukia kwenye mikono ya Waislamu. Khalid mtoto wa al-Walid, ambaye ukatili wake tayari ulikwishapata karipio kutoka kwa Mtume, alipata jingine kwa kufikiri kwamba ni kazi yake kuwaua hawa majikedume; kitendo ambacho kilikuwa kinyume kabisa na dhana za Mtume (s.a.w.) za ushujaa.

Kama vile tu alivyoona ni muhimu kuwakaripia wengine ambao walifikiria ni wajibu wao kuwaua watoto wa makafiri. "Ni nini kilicho bora chenu," aliuliza, "kama sio watoto wa makafiri?"

Mafanikio ya muhimu sana yalipatikana, na ubashiri wa Mtume (s.a.w.) ulithibitika kuwa thabiti katika wakati ambapo kinyume chake kingeweza kuwa na matokeo mabaya; kwani Abu Sufyan angeweza kuwa na uwezo wa kutumia fursa ya janga, ingawa lisiwe lenye nguvu sana, kuweza kusababisha jingine.

(Muhammad and the Rise of Islam, London, 1931)

Hunain ilikuwa ni vita iliyoongozwa binafsi na Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) mwenyewe. Vita vilianza na kushindwa kwa Waislamu, na walikimbia njia ya kila upande ili kuokoa maisha yao wenyewe, bila kutambua kabisa kuwepo, katika uwanja wa mapambano, kwa Mtume (s.a.w.) wao. Mwishoni, hata hivyo, walikuwa washindi, shukrani kwa ujasiri na ushupavu wa Mtume (s.a.w.) mwenyewe na wachache kati ya jamaa zake.

M. Shibli, mwanahistoria wa Kihindi, anaandika katika kitabu chake cha wasifu wa Mtume:

Badala ya ushindi (wa Waislamu) mtu anaweza kuona kushindwa kwao (katika vita vya Hunain). Mtume (s.a.w.) alitazama pote na hakuona mtu yeyote pamoja naye isipokuwa wachache wa marafiki zake. Abu Qatada, sahaba mmoja, ambaye alikuwe-po huko Hunain, anasema kwamba wakati jeshi lilipokuwa linakimbia, alimuona Umar ibn al-Khattab, na akamuuliza: "Ni hali gani ya mambo ya Waislamu?" Yeye akasema: "Hayo ni Mapenzi ya Allah (s.w.t.)"

(The Life of the Prophet {Siraatun-Nabi, juz. 1, uk. 535-536}, 1976, Azamgarh, India).

231

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Sir William Muir

Kinyume kilichopatikana mwanzoni mwa siku hiyo, kilihusishwa na Mtume (s.a.w.) na matumaini ya kujiona ambayo kwayo waumini walitegemea juu ya jeshi lao kubwa. Mafanikio ya baadae sawasawa yalipachikwa kwenye msaada wa wa jeshi lisiloonekana ambalo lilipigana dhidi ya adui yao. Shambulio hilo limegusiwa hivi kwenye Qur'an:"

Hakika Allah amewasaidieni kwenye medani za vita nyingi: na katika siku ya Hunain, wakati kwa kweli mlifurahia katika wingi wa jeshi lenu. Lakini idadi yao kubwa kwa namna yoyote ile haikukunufaisheni ninyi: ardhi ilikuwa finyu sana kwenu pamoja na upana wake wote. Kisha mligeuza migongo yenu na mkakimbia."

(The Life of Muhammad, London, 1877, uk.143)

"Majeshi yasiyoonekena" ambayo yaliwasaidia Waislamu, ina maana, katika muktadha huu, nguvu ya hali ya juu. Mwanzoni mwa vita hivyo, walishindwa na kufukuzwa. Lakini walitiwa moyo na mfano wa Mtume (s.a.w.) mwenyewe ambaye ujasiri wake uliwarud-ishia hamasa yao, na walimpiga adui kwa ari na nguvu mpya.

Vita vya Uhud vilianza kwa ushindi wa Waislamu na viliishia na kushindwa kwao; vita vya Hunain vilianza na kushindwa kwao na vikaishia na ushindi wao. Kulikuwa na mauaji makubwa kwa Waislamu wakati wa mwanzo ambayo yalisababishwa na hofu yao wenyewe na kukosa ushupavu.

Muhammad Husein Haykal

Ushindi haukupatikana kirahisi. Waislamu walilipa gharama kubwa sana. Wangeweza kuimudu kwa gharama ndogo kama wasingerudi nyuma hapo mwanzoni na kus-ababisha kauli ya dhihaka ya Abu Sufyan kwamba watakuwa watupwe baharini. Ingawa vitabu vya msingi wa rejea havikuorodhesha wale wote waliouawa katika vita hivyo, vimetaja kwamba makabila mawili ya Kiislam yalikuwa karibu yote yameangamizwa kabisa, na kwamba Mtume (s.a.w.) aliendesha Swala ya jeneza kwa ajili yao. Kufidia sehemu ya hii hasara kubwa ya maisha ya watu, ni yale mamlaka yasiyo na shaka ushindi uliyoyaleta kwa Waislamu. Zaidi ya hayo, ushindi ulileta mateka na ngawira zaidi kwa ajili yao kuliko walivyowahi kuona hapo kabla.

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935) Ali na vita vya Hunain

Shujaa wa vita vya Hunain alikuwa ni Ali ibn Abi Talib kama vile alivyokuwa shujaa wa vita vyote vilivyotangulia. Katika wakati ambapo maswahaba wote walikimbia kutoka kwenye medani ya vita, na watu wanane tu walikuwa wamebaki na Mtume, alikuwa ni Ali

232

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

aliyesimama kati yake na adui, na akamkinga yeye. Makabila yalishambulia kwa kurudia lakini aliyarudisha nyuma kila wakati sawa na alivyokwisha kufanya huko Uhud. Kwa wakati fulani, ilikuwa ni Uhud tena.

Mwishowe, Ali alifanikiwa katika kuugeuza mwelekeo wa vita hivyo. Kwanza alimsababisha Uthman bin Abdullah, mmoja wa viongozi wa adui, kuanguka kutoka kwenye ngamia wake, kuyumba, na kuuawa; na baadae, alimuua, katika pambano la mkono kwa mkono, Abu Jerdel, kiongozi wa Hawazin. Wakati majenerali hawa wawili walipokuwa wameuawa, adui alivunjika moyo, akashindwa vita.

M.Shibli

Banu Malik wa kabila la Thakiifwalipigana kwa ujasiri wa makusudi lakini pale kiongozi wao, Uthman ibn Abdullah, alipouawa, walianza kuyumba...

(The Life of the Prophet, Azamgarh, India, 1976)

Abu Sufyan, mkuu wa Bani Umayya, alikuweko kwenye kambi ya Waislamu, kama ilivy-oelezwa hapo juu. Ingawa alikwisha "kuukubali" Uislamu, alivutiwa na kusisimka kuona kule kukimbia kwa Waislamu, na akawa na matumaini kwamba watatupwa baharini. Wakati Hikda bin Umayya, "Mwislam" mwingine wa ukoo wa Bani Umayya, alipoona ukimbiaji wa Waislamu, pale mwanzoni mwa vita, alitamka: "Hatimae uchawi wa Muhammad umevunjika." Wote lazima watakuwa wamebuni, katika fikra zao, picha za kumrudisha Hubal, mungu wao wa jadi, kwenye kiti chake ndani ya Al-Kaaba.

Abu Sufyan na watu wengine wa ukoo wake, hawakuweza kuficha furaha zao wakati kwao wao ilionekana kana kwamba Waislamu walikuwa wameshindwa na watu wa makabila ya wapagani. Lakini furaha yao ilidhihirika kuwa ya kudumu kwa muda mfupi sana. Baadae kidogo kulikuwa na mabadiliko katika matokeo ya vita hivyo, na kisha ilikuwa ni hawa wapagani ambao mwishowe na kwa uwazi kabisa walioshindwa. Kinyume hiki lazima kiwe kilisababisha kijicho kikubwa sana kwa Abu Sufyan na jamaa wa ukoo wake vile walivyopoteza matumaini ya mwisho, mazuri kabisa waliyokuwa nayo ya kufufua "Zama za Ujahilia."

Jamaa wa kabila walikuwa wameacha mizigo yao yote na maelfu ya wanyama wao. Mtume (s.a.w.) aliamuru mizigo hiyo ikusanywe, wanyama hao wakusanywe na kupelek-wa Jirana, sehemu ya katikati baina ya Taif na Makka, na iwekwe hapo kusubiri kuwasili kwake yeye mwenyewe. Kwa wakati huo, aliamua kuiteka Taif ambayo bado iliendelea kubaki kama ngome ya mwisho ya makafiri, na akaamuru sehemu kubwa ya jeshi kutem-bea kuelekea kwenye mji huo. Wale watoro toka kwenye vita ile pia walikuwa wamepata hifadhi kwenye ngome ya Taif.

233

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Akiwa njiani kuelekea Taif, Mtume (s.a.w.) alipita kikundi kidogo cha watu waliokuwa wamesimama karibu na mwili wa mwanamke aliyeuawa. Katika kuuliza, aligundua kwamba aliuawa na Khalid bin al-Walid.

Muhammad ibn Ishaq

Mmoja wa maswahaba alituambia kwamba Mtume (s.a.w.) siku ile (mara baada ya vita vya Hunain) alipita karibu na mwanamke ambaye alikuwa amemuawa na Khalid bin al-Walid ambapo watu walikuwa wamekusanyika karibu yake. Wakati aliposikia yaliyotokea, alituma ujumbe kwa Khalid na kumkataza kuua mtoto, mwanamke au mtumwa aliyekodiwa.

(The Life of the Messenger of God)

Mtume (s.a.w.) alizingira Taif lakini haikufanikiwa na ikaachwa. Taif, hata hivyo, ilisalimu amri kwa hiari majuma kadhaa baadae.

Kutoka Taif, Mtume (s.a.w.) alikwenda Jirana kugawanya ngawira za vita ambazo ziliku-sanywa katika uwanja wa Hunain. Sehemu aliyompa Abu Sufyan na wanae, wakuu wa ukoo wa Bani Umayya, ilikuwa kubwa zaidi kuliko sehemu aliyompa mtu mwingine yoy-ote katika kambi ya Uislamu. Bani Umayya hawakuweza kuamini kwamba walikuwa na bahati nzuri kama hiyo. Abu Sufyan, ambae alikuwa na sababu nzuri ya kutarajia kidogo kuliko chochote, baada ya "utendaji" wake katika vita vya Hunain, aliguswa sana na ukarimu wa Mtume, na akaongea naye kwa shauku: "Wewe umkarimu katika vita sio chini ya ulivyo mkarimu kwenye amani."

Mustashriq wengine wamemaanisha kwamba ile sehemu ambayo Mtume (s.a.w.) aliyotoa kwa Abu Sufyan na wanae, ilikuwa kwa kweli ni hongo la kuwabakisha wawe Waislamu, na kwamba hapakuwa na njia nyingine yoyote ambayo angeweza kupatia utii wao. Wao wanasema zaidi kwamba Mtume (s.a.w.) kamwe hakusita kuwahonga waabudu masanamu kama alidhani kwamba wangeuza imani zao kwake kwa kubadilishana na ngamia, kondoo, na vipambo vidogodogo na vitu vizuri vyenye thamani ndogo.

Sisi hatukubaliani nao. Baada ya kutekwa Makka, Abu Sufyan, wanae na watu wengine wa ukoo wa Bani Umayya, walikuwa chini ya huruma ya Muhammad. Angeweza kuwaangamiza wote, na waabudu masanamu wote wa Arabia wasingeweza kufanya lolote kuwaokoa. Haikuwa lazima kwake kuwahonga wao au mtu mwingine yeyote katika kuukubali Uislamu. Kusilimu kwao kulikuwa na thamani ndogo kwa Uislamu vyovyote vile. Katika kutoa zawadi juu ya Abu Sufyan na wanae, Mtume (s.a.w.) wa Uislamu alikuwa akidhihirisha tu chaguo lake kutoka kwenye ulipizaji wa kisasi. Kwa Waarabu, itakumbukwa, ulipizaji wa kisasi ulikuwa ni tabia yao mbaya. Alijaribu kumaliza uadui wao kwa Uislamu kwa upole wake na ukarimu. Zawadi hizo zilikuwa ni ishara ya mfano

234

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

wa mwelekeo huu tu.

Abu Sufyan, watoto wake na watu wengine wa Bani Umayya - wapokeaji wa zawadi hizo, waliitwa, daima baadae Muallafa Qulubuhum - wale wenye kuimarishwa nyoyo zao. Mtume (s.a.w.) aliwapa maadui zake sehemu kubwa kutoka kwenye ngawira kwa ajili tu ya Taliif al-Qulub - kuimarisha nyoyo zao.

Dr. Muhammad Hamidullah anasema katika kitabu chake, Introduction to Islam, uk. 80, (1977):

Wale ambao nyoyo zao ni za kuimarishwa ni wa namna nyingi. Faqihi mkuu, Abu Ya'la al-Farra, anaonyesha: "Na kwa wale ambao nyoyo zao ni za kuimarishwa, wapo wa aina nne:

1.   Wale ambao nyoyo zao ni za kupatanishwa kwa kuja kwao kwenye msaada wa Waislamu;

2.   Wale ambao nyoyo zao ni za kuimarishwa ili kwamba wajiepushe na kufanya madhara kwa Waislamu;

3.    Wale wanaovutiwa kwenye Uislamu;

4.   Wale ambao kwa kuwatumia wao kuingia kwenye Uislamu kunakuwa na uwezekano kwa watu wa makabila yao.

Ni halali kunufaisha kila moja ya makundi haya ya 'wale ambao nyoyo zao ni za kuimarishwa' wawe Waislamu au washirikina." Abu Sufyan na ukoo wake walikuwa ni wa kundi lile la pili; nyoyo zao "zilikuwa ziimarishwe ili kwamba wataweza kujie-pusha kutokana na kufanya madhara kwa Waislamu."

Maansari na ngawira za Hunain

Baadhi ya vijana wa Ansari walikuwa hawakuridhika na kile walichokiona kuwa ni ugawaji "usio haki" wa ngawira za vita. Wachache miongoni mwao walinung'unika kwamba wakati ulipofika wa kugawa ngawira, Mtume (s.a.w.) alifanya "upendeleo" kwa Maquraishi. Wakati Mtume (s.a.w.) alipolisikia hili, aliamuru Ansari waku-sanyike katika hema, na akawahutubia hivi:

"Ni nini hiki ninachokisikia kutoka kwenu, Enyi Ansari, kuhusu ugawaji wa ngawira? Mmefadhaika kwa sababu nimetoa sehemu kubwa ya ngawira kwa watu wa Makka kuliko niliyowapeni ninyi? Lakini hebu niambieni hili: hivi sio kweli kwamba mli-abudu masanamu na Allah (s.w.t.) akawapeni mwongozo kupitia kwangu mimi? Hivi sio kweli kwamba mlitenganishwa na ugomvi wa wenyewe kwa wenyewe na Allah

235

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

(s.w.t.) akawaunganisha kupitia kwangu mimi? Sio kweli kwamba mlikuwa masikini na Allah (s.w.t.) akawafanyeni matajiri kupitia kwangu mimi?"

Katika kujibu kila swali, Ansari walisema: "Ndio, hivyo ndivyo ilivyo, na ni neema ya Allah (s.w.t.) na Mtume Wake (s.a.w.)."

Lakini maswali haya yalikuwa ni balagha tu - maswali yasiyohitaji majibu - na Mtume wa Allah (s.a.w.) mwenyewe aliyajibu.

Sir William Muir

"...Lakini nyie mngeweza kujibu (na mkajibu kwa dhati, kwani ningehakikisha hilo mimi mwenyewe) - ulikuja Madina ukiwa umekanwa kama mlaghai, na tukashuhu-dia ukweli wako; ulikuja kama mkimbizi asiye na msaada na tukakusaidia wewe; mtu aliyetengwa na jamii, nasi tukakupa hifadhi, ukiwa fukara, nasi tukakufariji wewe. Kwa nini mnachanganyikiwa akilini kwa sababu mambo ya maisha Haya, kwa hili nilitafuta kuelekeza nyoyo za watu hawa (Maquraishi wa Makka) kwenye Uislamu, ambapo ninyi tayari mko imara kwenye imani zenu? Hamridhiki ninyi kwamba wengine wapate hayo makundi ya mifugo na hao ngamia, ambapo ninyi mnamchukua Mtume wa Allah (s.w.t.) kurudi naye majumbani kwenu? Hapana, mimi sitawaacheni ninyi milele. Kama wanadamu wote wangekwenda njia moja, na watu wa Madina njia nyingine, hakika, ningekwenda ile njia ya watu wa Madina. Mola awe mwema juu yao, na awabariki wao, na watoto wao na watoto wa watoto wao milele."

(The Life of Muhammad, London, 1861)

Wakati Ansari waliposikia maneno haya, waligubikwa na machozi, na wakapaza sauti: "Waache wengine wachukue hao kondoo, ng'ombe na hao ngamia waondoke nao. Tunachokitaka sisi ni Muhammad, na sio kitu kingine chochote."

Ansari walipatwa pia na hofu kwamba Mtume (s.a.w.) angeweza kuamua kuishi hapo Makka, na kupafanya makao yake makuu. Lakini aliwahakikishia kwamba yeye kamwe hatawaacha wao au Madina, na kwamba yeye na wao hawatenganishiki milele.

Kutoka Jirana, Waislamu walirudi Makka ambako Mtume (s.a.w.) alifanya ile mizu guko saba ya Al-Kaaba, na akatekeleza ibada za Hijja Ndogo (Umra).

Vita vya Hunain vilikuwa ndio "limbuko" la mwisho la Arabia ya upagani. Wakati Waislamu walipopata ushindi, pazia hatimae likaanguka kwenye dibaji ya ushenzi na upagani, ya mfululizo wa matukio ya historia ya Arabuni. Lakini wapagani au kwa usahihi zaidi, watetezi wa siri wa upagani wa Kiarabu walikuwa bado wapigane mapigano, ya jeshi linalorudi nyuma, na askari, marefu na magumu, dhidi ya Uislamu.

236

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hapo Makka, Mtume (s.a.w.) alitoa maelekezo ya mwisho kwenye mambo yanayohusu uongozi na sera. Kabla ya kuondoka Makka kwenda Madina, alimteua Akib bin Usayd kama gavana wa mji huo. Huu ulikuwa ndio uteuzi wa kwanza wa kudumu wa kiserikali katika Uislamu. Yeye pia aliutangaza mji wa Makka kuwa makao makuu ya kidini ya Kiislam.

Baada ya kumaliza mwezi mzima wenye matukio mengi hapo Makka na viungani mwake, Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) na jeshi lake, walirudi Madina.

D. S. Margoliouth

Kwa kuipa himaya ya Kiislam makao makuu ya kidini, yasiyotumika wakati wowote kama makao makuu ya kisiasa, mwanzilishi aliyapatia makao hayo nguzo ambayo imelinda uendeleaji wa mfumo huo katikati ya misukosuko mikali kabisa.

Kutembelea Makka ambako kuliandamana na mabadiliko mengi sana kulisimamish-wa kwa Mtume (s.a.w.) kupitia kwenye taratibu za hijja ndogo. Baadae, Akib, mtoto wa Usaid, aliteuliwa kuwa gavana wa Makka kwa mshahara wa dirham moja kwa siku; huu ulikuwa ni uteuzi wa kwanza wa kudumu wa kiserikali kufanywa katika Uislamu; huko Khaibar, mji mwingine pekee wa muhimu ambao Waislamu walikuwa wameuteka, serikali ya (wenyeji wa) hapo ilibaki. Mbali na gavana, kiongozi wa kiro-ho aliachwa hapo, Mu'adh mtoto wa Jabal, mwenyeji wa Madina, ambaye katika uho-dari wake wa kufundisha hiyo dini mpya, Mtume (s.a.w.) alikuwa na imani nao. Mtume (s.a.w.) alirudi Madina pamoja na jeshi la Waislamu baada ya kutokuwepo kwa zaidi ya mwezi.

(Muhammad and the Rise of Islam, London, 1931)

237

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

VITA VYA TABUK

Vita vya Muutah ambavyo Waislamu walishindwa, vilipiganwa mnamo Septemba mwaka 629. Kushindwa kwao kulitafsiriwa katika jamii nyingi kama ni ishara ya kuanguka katika mamlaka ya Dola mpya ya Kiislamu. Maharamia wa Kiarabu lazima watakuwa wame-ona inatia hamu kushambulia Madina baada ya kuanguka huku kwa kubuniwa. Lakini katika kiangazi cha mwaka 630, minong'ono ilikuwa ikizunguka hapo Madina kwamba hayakuwa yale makabila ya Arabia ya kaskazini bali ni vikosi vya Kirumi ambavyo vilikuwa vinajikusanya katika mpaka wa Syria kwa ajili ya uvamizi wa Hijazi.

Muhammad, Mtume (s.a.w.) wa Uislalmu, aliamua kuchukua hatua za tahadhari kwa ajili ya ulinzi wa Madina, na akawaamuru wafuasi wake kujiandaa na mapambano marefu upande wa kaskazini.

Ilikuwa ni mwezi wa Septemba, na hali ya hewa ya Hijazi mwaka ule ilikuwa ni ya joto kupita kiasi. Zaidi ya hayo, ukame mrefu ulitishia jimbo hilo na hali ya nusu njaa. Majibu ya Waislamu, kwa hiyo, yalikuwa yamepooza sana. Hawakupenda kuondoka majumbani mwao kwa wakati kama huu.

Sir John Glubb

Mnamo Septemba au Oktoba 630, Mtume wa Allah (s.a.w.) alitoa amri ya kujiandaa kwa msafara wa kwenye mpaka wa Byzantium. Hali ya hewa ya Hijazi ilikuwa bado ni ya joto kali sana, maji na malisho yalikuwa adimu, na mizunguko ya jeshi kubwa kama hilo ingekuwa ni migumu sana. Huenda kumbukumbu za maafa ya Muutah zili-wakosesha watu wengi nia ya kupambana na Byzantium tena.

(The Life and Times of Muhammad)

Washirikina hapo Madina waliichukua fursa hii kupandikiza mfarakano katika vichwa vya waumini wapya katika Uislamu. Sio kwamba hawakushiriki tu katika vita bali pia wali-jaribu kuwageuza wengine mawazo kutofanya hivyo. Katika jaribio la kudhoofisha nia na makusudi ya Waislamu, walianza kueneza habari za wavumishaji wa mambo ya kutisha kwamba maadui safari hii hawakuwa wale askari wa kikabila wa kuchukuliwa kwa nguvu, masikini, wenye zana duni, wasiojiamini na wajinga waliopigana bila mpango na bila nid-hamu bali ni Warumi ambao walikuwa ndio dola iliyoendelea sana na yenye nguvu sana duniani, na ambao, kwa kweli, watawateketeza Waislamu.

238

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hata hivyo, Waislamu wengi waliitika kwenye mwito wa Mtume, na wakachukua silaha kuilinda dini. Wakati ilipochukuliwa idadi ya vichwa, walipatikana watu 30,000 walioji-tolea. Lilikuwa ndio jeshi kubwa sana lililowahi kukusanywa katika Arabia hadi hapo.

Mtume (s.a.w.) alimteua Ali ibn Abi Talib kama kaimu wake hapo Madina wakati wa kutokuwepo kwake yeye mwenyewe. Alimchagua Ali kuwa kaimu wake kwa sababu zifu-atazo:

Alitaka kuonyesha kwa dunia yote kwamba alimuona Ali kuwa mwenye sifa zinazostahili zaidi kuliko mtu mwingine yoyote za kuwa mtawala wa Waislamu wote, na kuwa mkuu wa Umma wa Kiislamu. Yeye, kwa hiyo, alimchagua kama mwakilishi wake katika makao yake makuu.

Wapiganaji wote walikuwa wanakwenda na msafara huo, wakiiacha Madina bila vikosi vyovyote. Kama litatokea shambulizi lolote juu ya mji huo kutoka kwa waporaji wa mak-abila ya kihamaji, Ali anaweza kutegemewa katika kuishughulikia hali hiyo kwa kutumia ushujaa na uwezo wake.

Wanafiki wengi walibaki nyuma hapo Madina, na wengine wengi walilikimbia jeshi na kurudi mjini. Walikuwa ni tishio linalowezekana kwa usalama wa makao makuu ya Uislamu. Mtume, kwa hiyo, alichagua mtu wa kutawala mahala pake ambaye alikuwa na uwezo wa kuikinga Madina dhidi ya shambulizi lolote la wapagani, ama kwa uchokozi kutoka nje au kupitia uchochezi wa ndani.

Kwa upande wa wanafiki hapakuwa na kitu kisichokubalika zaidi kuliko kumuona Ali kwenye mamlaka juu yao. Wakati jeshi lilipoondoka Madina, walianza kunong'ona kwamba Mtume (s.a.w.) alimuacha Ali hapo Madina kwa sababu alitaka kumuepuka. Ali alid-halilishwa kusikia kwamba bwana wake amemuona kama "mzigo." Yeye, kwa hiyo, upesi sana akalikimbilia lile jeshi na akalikuta hapo Jurf. Mtume (s.a.w.) alishangaa kumuona yeye lakini wakati Ali alipoeleza ni kwa nini alikuja, yeye Mtume (s.a.w.) alisema:

"Watu hawa ni waongo. Nilikuwacha Madina kuniwakilisha mimi kwa kutokuwepo kwangu. Huridhiki wewe kuwa kwangu kama Harun alivyokuwa kwa Musa isipokuwa kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu."

Washington Irving

Wengi wamefahamu kutokana na hayo yaliyoelezwa kwamba Muhammad alimkusu-dia Ali kama khalifa au mshikamakamu wake; kuwa ndio maana ya neno la Kiarabu lililotumika kuonyesha uhusiano wa Haruni kwa Musa.

(The Life of Muhammad)

239

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ali aliridhika kwa ule uhakika ambao Mtume (s.a.w.) alimpa, na akarudi Madina kuchukua dhima ya kazi yake kama khalifa.

Wakati Mtume (s.a.w.) alipokutana na kuzungumza na Ali katika kambi yake huko Jurf, baadhi ya maswahaba wake walikuwa pamoja naye. Mmoja wao alikuwa ni Saad bin Abi Waqqas, mshindi wa baadae wa vita vya Qadsiyya dhidi ya Waajemi. Alisimulia kwa Waislamu wengine kwamba ilikuwa ni mbele yake ambapo kwamba Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) alipomwambia Ali kwamba yeye (Ali) alikuwa kwake Muhammad ni kama vile alivyokuwa Harun kwa Musa, isipokuwa kwamba yeye Ali hakuwa Mtume. Baada ya matembezi magumu jeshi hilo lilifika kwenye mpaka wa Syria, na likasimama kwenye kitongoji kiitwacho Tabuk lakini Mtume (s.a.w.) hakuweza kuona dalili zozote za jeshi la Warumi au jeshi lingine lolote au adui. Mpaka huo ulikuwa na amani na ukimya. Habari alizozisikia huko Madina kuhusu uvamizi unaoweza kufanywa karibuni na Warumi, zilikuwa za uongo.

Amani na utulivu kwenye mpaka wa Syria ni uthibitisho mwingine kwamba Warumi waliviona vita vya Muutah kama si kingine chochote zaidi ya uvamizi wa kikundi cha Waarabu wa jangwani. Kama Muutah ingekuwa ni vita kubwa mno hivyo kama baadhi ya wanahistoria wa Kiislam wanavyodai ilikuwa, Warumi wangedumisha ngome yao kwenye mpaka huo. Lakini hawakudumisha hata doria seuze ngome!

Mtume wa Allah (s.a.w.) kisha akatafakari juu ya hatua inayofuatia ya kuchukuliwa hapo

Tabuk.

Washington Irving

Akiitisha baraza la vita, yeye (Muhammad) alitoa swali la ama waendelee mbele au la (kutoka Tabuk). Kwa hili Umar akajibu kimkato: "Kama unao wahy kutoka kwa Allah (s.w.t.) wa kuendelea mbele, fanya hivyo." "Kama ningekuwa na wahy kutoka kwa Allah (s.w.t.) wa kuendelea mbele," alijibu Muhammad, "nisingetaka ushauri wenu."

(The Life of Muhammad)

Mwishowe, Mtume (s.a.w.) aliamua kutokuendelea kwenda Syria bali kurudi Madina. Jeshi hilo lilikaa siku kumi hapo Tabuk. Ingawa halikuingia kwenye shughuli yoyote, kuwepo kwake pale mpakani kulikuwa na matokeo ya kufaa. Makabila mengi ya kaskazi-ni ya kibedui yaliingia Uislamu. Dauma-tul-Jandal, sehemu ya kimkakati kati ya Madina na Syria, ilipatikana kama eneo jipya.

240

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Punde tu kabla ya jeshi hilo kuondoka Tabuk, watawa wa nyumba kubwa ya utawa ya Mtakatifu Catherine katika bonde la Sinai, walikuja kumuona Mtume. Alikutana nao kwa mazungumzo, na akawapa mkataba ambao unalingana na Mkataba wa Madina ambao ali-wapa Mayahudi. Masharti yake makuu yalikuwa :

1.  Waislamu watayalinda makanisa na nyumba za watawa za Wakristo. Hawatavunja mali yoyote ya kanisa wala kujenga misikiti au kujenga nyumba kwa ajili ya Waislamu.

2. Mali zote za kanisa (za Wakristo) zitasamehewa kutokana na kodi yoyote ile.

3. Hakuna mtu yoyote mwenye mamlaka ya kikanisa atakayelazimishwa na Waislamu kuacha kazi yake.

4. Hakuna Mkristo atakayelazimishwa na Waislamu kusilimu na kuwa mwis-lamu.

5. Kama mwanamke wa kikristo ataolewa na mwislamu, atakuwa na uhuru kamili wa kufuata dini yake mwenye we.

Jeshi lilipata nguvu tena kutokana na kazi ngumu na uchovu wa ile safari ndefu, na Mtume (s.a.w.) alilipa ishara ya kurudi nyumbani. Aliwasili Madina baada ya kutokuwepo hapo kwa mwezi mmoja.

241

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kutangazwa kwa Surat Bara'ah ( At-Taubah)

Wakati msimu wa hijja ya mwaka wa 9 H.A. ulipowadia, Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) alikuwa na idadi kubwa ya kazi zilizombana ambazo zilihitaji uangalizi wake wa haraka kiasi kwamba alikuwa hawezi kuondoka Madina. Yeye, kwa hiyo, alimtuma Abu Bakr kwenda Makka kama kiongozi wa kundi la mahujaji mia tatu kwenda kuongoza ibada za Hijja.

Lilikuwa ni jukumu la uongozi halisi, mbele ya watu, la kwanza kabisa la Abu Bakr. Abu Bakr na mahujaji hao waliondoka Madina. Siku moja baada ya kuondoka kwao. Mtume (s.a.w.) alipokea kutoka Mbingnii wahy mpya uitwao Bara'a (At-Taubah) - Sura ya tisa ya Qur'an, na aliamriwa kwa dhati kabisa kuitangaza huko Makka ama yeye mwenyewe binafsi au kutoa mamlaka ya kufanya hivyo kwa mtu kutoka kwenye familia yake mwenyewe, lakini sio kwa mtu mwingine yeyote.

Kulingana na amri hii ya Mbingnii, Muhammad Mustafa alimwita binamu yake, Ali ibn Abi Talib, akampa kipando chake apande, na akamuamuru kupeleka ule wahy mpya Makka, na kuutangaza huko katika mkusanyiko wa mahujaji - Waislamu na mapagani.

Muhammad ibn Ishaq

Wakati At-Taubah iliposhuka kwa Mtume (s.a.w.) baada ya kuwa alikwishamtuma Abu Bakr kusimamia hijja, mtu mmoja alionyesha nia kwamba angeipeleka kwa Abu Bakr. Lakini akasema: "Hakuna mtu atakayeitangaza kutoka kwangu bali mtu wa nyumba yangu mwenyewe." Ndipo akamwita Ali na akasema: "Chukua sehemu hii kutoka mwanzo wa At-Taubah, na uitangaze kwa watu siku ya kafara wakati watakapokusanyika huko Mina."

(The Life of the Messenger of God) Washington Irving

Muhammad alimtuma Abu Bakr kama mkuu wa mahujaji kwenda Makka, yeye mwenyewe akiwa ameshikwa sana na shughuli za jamii na za nyumbani kiasi cha kumfanya asiweze kukosekana Madina.

Sio muda mrefu sana baadae Muhammad akamwita mkwe wake na Sahaba mtiifu,

242

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ali, na akimpandisha juu ya ngamia mwepesi sana kati ya ngamia wake, alimhimiza kufanya haraka kwa kasi yote kwenda Makka, huko akatangaze mbele ya umati wa mahujaji waliokusanyika kutoka sehemu zote, Sura muhimu ya Qur'an, aliyoipokea hivi punde kutoka mbingnii.

Ali alitekeleza kazi yake kwa moyo na usahihi wake uliozoeleka. Aliufikia huo mji mtukufu kileleni mwa tamasha hilo kubwa la kidini. Alisimama mbele ya umati mkubwa uliokusanyika kwenye kilima cha Al-Akaba, na akajitangaza yeye mwenyewe kama mjumbe kutoka kwa Mtume, akiwa amebeba wahy muhimu. Kisha yeye akasoma ile Sura ambayo yeye alikuwa mbebaji, ambayo ndani yake ile dini ya upanga (sic) ilitangazwa katika ugumu wake wote.

Wakati Abu Bakr na Ali waliporudi Madina, huyu Abu Bakr alionyesha mshangao na kutoridhika kwake kwamba hakufanywa kuwa mtangazaji wa wahy muhimu kama huo, kama ulivyoonyesha kuunganishwa na kazi yake ya awali, lakini alitulizwa kwa uhakikisho kwamba wahy mpya wote lazima utangazwe na Mtume (s.a.w.) mwenyewe, au na mtu kutoka kwenye familia yake wa karibu.

(The Life of Muhammad)

Sir William Muir

Kuelekea mwishoni mwa hijja, katika sikukuu ya kuchinja (kafara), pale mahali pa kutupia mawe karibu na Mina, Ali aliusomea kwa sauti ule umati mkubwa uliokusanyika karibu yake katika ile njia nyembamba, ile amri ya mbingnii.

Alipokuwa amemaliza kusoma kifungu hiki, Ali aliendelea: "Nimeamriwa kuwatangazieni kwamba hakuna asiyeamini atakayeingia peponi. Hakuna muabudu sanamu atakayefanya hijja baada ya mwaka huu; na hakuna mtu yoyote atakayefanya mzunguko wa Nyumba Tukufu akiwa uchi. Yeyote yule aliye na mkataba na Mtume, utaheshimiwa mpaka ukomo wake. Miezi minne imeruhusiwa kwa kila kabila kurudi kwenye nchi zao kwa usalama. Baada ya hapo wajibu wa Mtume (s.a.w.) unakoma."

Mkusanyiko mkubwa wa mahujaji ulisikiliza kwa utulivu mpaka Ali alipomaliza. Kisha wakatawanyika na kuondoka kila mtu kwenda nyumbani kwake, kutangaza kwa makabila yote ya peninsula nzima hii amri kali ambayo wameisikia kutoka kwenye midomo ya Ali.

(The Life of Muhammad, London, 1877)

Muhammad Husein Haykal

... Baada ya (Ali) kumaliza kisomo chake cha Qur'an, aliendelea kwa maneno yake mwenyewe: "Enyi watu, hakuna asiyeamini atakayeingia Peponi; hakuna mshirikina

243

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

atakayefanya hijja baada ya mwaka huu; na hakuna mtu aliyeko uchi atakayeruhusi-wa kuizunguka Al-Kaaba. Yeyote aliyeingia mkataba na Mtume wa Allah - rehema na amani ziwe juu yake - atatimiziwa mkataba wake mpaka kipindi chake kitakapokwisha." Ali alitangaza haya maagizo manne kwa wale watu na kisha akampa kila mtu miezi minne ya amani ya kawaida na msamaha ambayo ndani yake mtu yoyote anaweza kurudi nyumbani kwa usalama. Kuanzi wakati ule na kuendelea, hakuna muabudu sanamu aliyefanya hijja na hakuna mtu aliye uchi aliyefanya mizunguko ya Al-Kaaba. Kuanzia siku ile na kuendelea, Dola ya Kiislam ilianzishwa.

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Ali ibn Abi Talib "alizisoma tena zile Aya za Allah (s.w.t.)" huko Mina, akimuwakilisha Mtume wa Allah (s.a.w.). Hii lazima iwekwe akilini na msomaji kwamba "kusoma Aya za Allah (s.w.t.)" ni kitendo chenye madaraka makubwa. Ni kitendo, kwa kweli, muhimu sana kiasi kwamba Allah (s.w.t.) Mwenyewe alikitwaa. Tunasoma katika Qur'an:

Hizi ni Aya za Allah. Tunakusomeeni kwa haki, Hakika wewe ni miongoni mwa Mitume.

(Sura ya 2; Aya ya 252)

Haya tunayokusomea ni katika Aya na ukumbusho wenye hekima. (Sura ya 3; Aya ya 58) Hizi ni Aya za Allah. Tunakusomea kwa haki; Na Allah hapend i kuwadhulumu walimwengu. (Sura ya 3; Aya ya 108)

Kulingana na Aya hizi, Allah (s.w.t.) Mwenyewe Alizisoma Aya Zake kwa Muhammad, Mtume Wake, na baadae (mara alipokwisha kuzisikia) akazisoma kwa wanadamu wote. Kusoma Aya za Allah (s.w.t.) kulikuwa ni moja kati ya kazi zake muhimu. Umuhimu wa kazi hii unaakisiwa na Aya zifuatazo za Qur'an Tukufu:

Usahihi-19.jpg

Ewe Mola wapelekee miongoni mwao Mtume, anayetokana nao wenyewe. Atakayewasomea Aya Zako na awafundishe Kitabu na Hekima na awatakase; hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima. (Sura ya 2; Aya ya 129)

244

Usahihi-20.jpgUsahihi-21.jpg

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Usahihi-22.jpg

Kama tulivyotuma Mtume kwenu, anayetokana na ninyi, anayekusomeeni Aya Zetu na kuku-takaseni, na kukufudisheni Kitabu na Hekima, na kukufundisheni yale mliyokuwa hamyajui.

(Sura ya 2; Aya ya 151)

Usahihi-23.jpg

Hakika Allah aliwafanyia wema mkubwa Waumini, pale alipowapelekea Mtume aliyetoka miongoni mwao wenyewe, Aliyewasomea Aya Zake na kuwatakasa, na kuwafundisha Kitabu na Hekima, ambapo kabla ya hapo walikuwa katika upotovu uliowazi. (Sura ya 3; Aya ya 164)

Usahihi-24.jpg

Yeye ndiye aliyempeleka kwa watu wasiojua kusoma, Mtume anayetoka miongoni mwao, awasomee Aya Zake na awatakase, na awafundishe Kitabu na hekima, ingawa kabla ya hapo, alikuwa katika upotovu ulio dhahiri. (Sura ya 62; Aya ya 2)

Kulingana na Aya hizi, Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) alikuwa na kazi za kufanya zifuatazo:

1. Kusomea watu Aya za Allah (s.w.t.);

2. Kuwafundisha maandiko na hekima;

3. kuwatakasa;

4. Kuwafundisha katika elimu mpya.

Ya kwanza kutajwa katika kazi za utume ni, "kusoma Aya za Allah (s.w.t.)" Ni muhimu sana kwamba inachukua utangulizi juu ya kazi nyingine zote za Mtume.

245

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kusoma Aya za Allah (s.w.t.) kumetajwa pia pekee pekee katika Qur'an katika Aya zifu-atazo:

Usahihi-25.jpg

Hivyo tumekutuma kwenye umati ambao wamekwisha kupita kabla yao umati zingine, ili uwasomee haya tunayokufunulia kwa njia ya wahy. .. (Sura ya 13; Aya ya 30)

Usahihi-26.jpg

Ama mimi nimeamrishwa nimuabudu Allah, Mlezi wa mji huu, ...-na niisome Qur'an: na mwenye kuongoka, basi ameongoka kwa faida ya nafsi yake mwenyewe, na mwenye kupotea, basi sema: "Hakika mimi ni miongoni mwa waonyaji." (Sura ya 27; Aya ya 91 - 92)

Usahihi-27.jpg

...Hakika Allah amekuteremshieni ukumbusho, Mtume, anayekusomeeni Aya za Allah zina-zobainisha, Ili kuwatoa walioamini na wakatenda mema kutoka kwenye Giza, na kuwapele-ka kwenye Nuru... (Suraya 65; Ayaya 10-11)

Pia kuna onyo lifuatalo katika Qur'an Tukufu:

Usahihi-28.jpg

...Hakika wale waliozikanusha Aya za Allah, watakuwa na adhabu kali (katika Akhera). Na Allah ni Mwenye Nguvu na Mwenye kulipiza kisasi. (Sura ya 3; Aya ya 4)

Ilikuwa ni kazi hii - Kusoma Aya za Allah (s.w.t.) - ambayo Ali ibn Abi Talib alitakiwa aitekeleze.

246

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kama ilivyoelezwa hapo juu, katika Dhil-Hija ya mwaka wa 9 H.A., Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.), alikuwa na shughuli sana hivyo kutoweza kwenda Makka kutekeleza Hija, na kutangaza ile Surah ya Bara'a iliyoshuka karibuni. Kwa hiyo, kwa amri dhahiri ya Allah (s.w.t.), ilimbidi achague mtu mwingine wa kutekeleza kazi hii. Mtu aliyechaguliwa alikuwa ni Ali ibn Abi Talib.

Mnamo mwaka wa 8 H.A. (A.D. 630) wakati wa kutekwa Makka, Ali na bwana wake, Muhammad Mustafa waliitakasa Nyumba ya Allah (s.w.t.) (Al-Kaaba) kutokana na masanamu ya Waarabu. Ali aliyavunja masanamu yale vipande vipande, na akavitupa vipande hivyo nje ya Al-Kaaba. Mnamo mwaka wa 9 H.A. (A.D.631), aliitakasa Al-Kaaba kutokana na waabudu masanamu wenyewe kwa kuwatangazia kwamba hawataruhusiwa tena kamwe kuingia katika maeneo yake matukufu.

Msimu wa hija wa mwaka wa 9 H.A, ulikuwa ndio mkusanyiko wa mwisho wa waabudu masanamu wa Arabia katika maeneo ya Al-Kaaba au hapo Makka.

Allah (s.w.t.) alimchagua Ali ibn Abi Talib kuirudisha Nyumba Yake (Al-Kaaba) kwenye hali yake ya utakaso wake wa asili, na akatuma Agizo maalum kwa Muhammad Mustafa, Mtume Wake, kufanya kusudi Lake lieleweke kwake (Ali). Ali, mtumwa wa Allah (s.w.t.) aliirudisha ile Nyumba Tukufu na Iliyobarikiwa kwenye hali ileile ambayo Mtume Ibrahim na Ismail (A.S) waliyoiacha nayo karne nyingi nyuma.

Katika kutangaza hapo Mina katika mwaka wa 9 H.A., ile Sera ya Dola ya serikali ya Kiislam, Ali alikuwa ndiye "Chombo" cha Allah (s.w.t.), kama vile katika mwaka wa 7 H.A., alivyokuwa "Mkono" wa Allah (s.w.t.) ambao uliiteka Khaybar kwa ajili ya Uislamu, na akaweka msingi wa Ufalme wa Mbinguni juu ya Ardhi. Kisa cha ushukaji na utangazaji wa Sura ya Bara'a (Sura ya 9 ya Qur'an Tukufu), kinadhihirisha kwamba:

1. Ali ibn Abi Talib ni mtu wa familia ya Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliyebarikiwa.

2. Kazi za Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) zinaweza kufanywa, katika kutokuwepo kwake, na Ali tu, na sio na mtu mwingine yoyote.

3. Mwakilishi au mshikamakamu wa Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) anaweza kuchaguliwa na Allah (s.w.t.) Mwenyewe au na Mtume Wake, lakini sio na umma wa Kiislam.

4. Ali ndiye mtu mwenye sifa stahilifu zaidi za kumuwakilisha Mtume wa Allah (s.a.w.) na hakuna mtu mwingine mwenye sifa bora zaidi kuliko

yeye.

247

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

5. Kazi muhimu zaidi ya Mkuu wa Dola ya Kiislamu ni kutangaza Amri za Allah (s.w.t.) katika dunia hii. Ingawa Abu Bakr alikuwapo mahali hapo huko Makka, hakuruhusiwa kutangaza Amri za Allah (s.w.t.); bali Ali ibn Abi Talib ndiye aliyezitangaza.

Marmaduke Pickthall

Ingawa Makka ilikuwa imekwishatekwa na watu wake sasa walikuwa ni Waislamu, ile amri rasmi ya hija ilikuwa imebadilishwa; wapagani wa Kiarabu wakiifanya katika namna yao na Waislamu kwa namna yao. Ilikuwa ni baada tu ya msafara wa mahu-jaji ulipokuwa umeondoka Al-Madina katika mwaka wa tisa wa Hijiria, wakati Uislamu ulikuwa umetawala huko Arabia ya Kaskazini, ambapo lile Tangazo la Tauba, kama linavyoitwa, lilipoteremshwa. Mtume (s.a.w.) alituma nakala yake kwa Abu Bakr, kiongozi wa hija, pamoja na maagizo kwamba Ali alikuwa ndiye alisome Tangazo hilo kwenye mkusanyiko wa watu uliokuwako huko Makka. Madhumuni yake yalikuwa kwamba baada ya mwaka ule Waislamu tu, ndio wafanye hija, nafasi zikiwa zimetolewa tu kwa waabudu masanamu kama wale ambao walikuwa na mkataba na Waislamu na hawajawahi kuvunja mkataba wao wala hawa-jawahi kumsaidia yeyote aliyekuwa dhidi yao (Waislamu). Hao walikuwa watumie fursa ya mkataba wao kwa muda ule, lakini mkataba wao utakapokwisha watakuwa kama waabudu-masanamu wengine. Tangazo lile linaweka mwisho wa uabudu masanamu katika Arabia.

(Introduction to the Translation of Holy Qur 'an, Lahore, Pakistan, 1975)

Yalikuwa ni mapenzi yake Allah (s.w.t.) kwamba mja Wake mpendwa, Ali ibn Abi Talib, aweze, kwa kusoma Tangazo Lake, kukomesha uabudu masanamu katika Arabia daima.

248

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Msafara wa Mwisho

Baada ya kutekwa kwa Makka makabila mengi ya kipagani yalikuja kuwa Waislamu kwa hiari, ambapo kuna mengine ambayo yaliingia Uislamu wakati Mtume (s.a.w.) alipotuma mubaligh wake kwao kuwaelekeza kwenye kanuni na matendo ya dini. Mmoja wa muba-ligh wake alikuwa ni Ali ibn Abi Talib. Bwana wake alimtuma kwenda Yemen katika mwaka wa 10 H.A. kuyaalika makabila ya Yemen kwenye Uislamu.

Ingawa ule msafara wa mwisho ambao Mtume (s.a.w.) aliuandaa ulikuwa ni ule ambao ulikuwa utumwe kwenda kwenye mpaka na Syria chini ya uongozi wa Usama bin Zayd bin Haritha, haukuondoka kamwe Madina katika wakati wa uhai wake. Kwa hiyo, ule msafara wa Ramadhani ya mwaka wa 10 H.A. ambao aliutuma Yemen chini ya uongozi wa Ali, ulikuwa ndio wa mwisho ambao hasa uliondoka Madina alipokuwa bado yuko hai.

Ali aliwasili Yemen pamoja na wapanda farasi wake katikati ya kipupwe, na aliwalingania watu wa kabila la Madhhaj kuukubali Uislamu, lakini walimjibu kwa mfululizo wa mishale na mawe ambapo na yeye aliviashiria vikosi vyake vifanye mashambulizi. Waliwashambulia wale watu wa kabila na kuwashinda lakini hawakuwafukuza kwa sababu ujumbe wa Ali ulikuwa wa amani na sio wa vita. Amri zake kwa vikosi vyake zilikuwa ni kupigana tu katika kujihami wenyewe.

Madhhaj waliomba amani ambayo Ali bila kusita aliwapatia, na akatoa mwaliko wake upya kwao kuukubali Uislamu. Safari hii wao na pia kabila la Hamdan waliitikia mwito wake, na wakasilimu. Ujumbe wa Ali ulifanikiwa. Yemen yote wakawa Waislamu kwa kupitia juhudi zake. Alitekeleza ujumbe wake, kama kawaida, kwa ustadi mzuri sana na kujiamini, na akadhihirisha kwamba alikuwa ndiye mubaligh wa Uislamu kwa uwezo hal-isi.

M. Shibli

Kikundi chenye nguvu sana na chenye uwezo huko Yemen kilikuwa kiliundwa na jamaa wa kabila la Hamdan. Mwishoni mwa mwaka wa 8 H.A., Mtume (s.a.w.) alimtuma Khalid bin Walid kuwalingania kwenye Uislamu. Khalid alikaa miezi sita mion-goni mwao akihubiri Uislamu lakini hakuweza kupata wafuasi wapya wowote, na ujumbe wake ulishindwa. Alikuwa ni jenerali na mtekaji lakini sio mhubiri na mubaligh. Mwishowe Mtume (s.a.w.) alimwita arudi Madina, na badala yake, akamtuma Ali ibn Abi Talib.

Ali aliwakusanya watu wa kabila la Hamdan katika bonde, akasoma mbele yao ule ujumbe wa Mtume wa Allah (s.a.w.) na akawafikishia Uislamu. Safari hii waliitika -kwa kuukubali Uislamu. Kabila zima, wote wakawa Waislamu.

249

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ali alituma taarifa juu ya matokeo ya ujumbe wake kwa Mtume (s.a.w.) huko Madina. Wakati Mtume (s.a.w.) alipoisoma taarifa hiyo, alimshukuru Allah (s.w.t.) kwa Rehema Zake, na akinyanyua macho yake kuelekea juu Mbinguni, akaomba baraka juu ya kabila la Hamdan. Hili alilifanya mara mbili.

(Sira-tun-Nabi, Juz.11, (Toleo la 10) 1974, Chapa ya Ma'arif Printing Press, Azamgarh, India).

Katika miaka kumi ya mwisho ya maisha yake, Mtume (s.a.w.) wa Uislamu aliandaa mis-afara themanini ambayo iliondoka Madina kwa shughuli mbalimbali - mingine ya kivita na mingine ya amani. Msafara wa Ali kwenda Yemen ni wa manufaa maalum kwa sababu ulikuwa ni wa mwisho wa yote. Hakuna msafara mwingine ulioondoka Madina katika uhai wa Mtume.

Mwaka wa 10 H.A. (631A.D.) unaitwa 'Mwaka wa Wajumbe'. Makabila mengi ya Kiarabu yalituma wajumbe huko Madina kwa kuukubali Uislamu, na kumpa Muhammad Mustafa kiapo chao cha utii kama mtawala wao wa kidunia.

Katika mwaka wa kwanza wa Hijiria (A.D. 622) Madina ilikuwa na hadhi ya Serikali ya Jiji lakini kwa miaka kumi ilikuwa imechipuka kuwa makao makuu ya Serikali ya "Taifa". Peninsula yote ilikuwa imekubali mamlaka yake ya kiroho na kidunia. Muhammad Mustafa, (Rehema Allah (s.w.t.) ziwe juu yake na juu ya kizazi chake), alikuwa amesi-mamisha amani ya ndani katika nchi nzima, na alikuwa amechukua hatua zenye nguvu kulinda maslahi ya "Kitaifa" ya umma wa Kiislamu. Hakukuwa na tishio kwenye usalama wa Dola ya Kiislamu kutokana na uvamizi wowote wa nje.

Wayahudi na Wakristo walilkuwa wanalipa kodi au ushuru (Jizya). Walikuwa wanafaidika na haki zote za uraia wa Dola ya Kiislamu, na walikuwa wakifaidi uhuru kamili wa kidi-ni. Waarabu, wengi wao sasa wakiwa wamesilimu na kuwa Waislamu, walikuwa katika mkesha wa ufufukaji wa "Kitaifa" wenye nguvu. Kulikuwa na chache tu ya neema zisizo na idadi ambazo Uislamu ulizileta kwenye peninsula ya Arabia.

250

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hija ya Muago

Katika Dhil-Qaddah, (mwezi wa 11 wa kalenda ya Kiislam) ya mwaka wa 10 H.A., Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) alitangaza kwamba atatembelea Makka kufanya Hija. Habari hizo zikaenea nchi nzima na idadi kubwa ya Waislamu ilikusanyika Madina ili kuongozana naye kwenda Makka. Idadi yao inakadiriwa kuwa zaidi ya 100,000. Kabla ya kuondoka kwake, alimteua Abu Dujana Ansari kama gavana wa Madina wakati wa kutokuwepo kwake. Mnamo mwezi 25 Dhil- Qaddah, aliondoka Madina, akifuatana na wake zake wote.

Waislamu waliangalia kila hatua, kila tendo, na kila ishara ya Mtume (s.a.w.) kwenye safari hii, na kila kitu ambacho alikifanya, likawa ni mfano wa wakati wote, wa kuigwa na Waislamu wote.

Maxime Rodinson

Baada ya kuanguka kwa Makka, Muhammad alifanya (kwa mara ya pili tangu kuhama kwake) ibada ya Umra, ibada ya maandamano kuzunguka Al-Kaaba, na zile safari kati ya Safa na Marwa (utengano wa yadi 400). Lakini hakushiriki katika Hija... Anaweza kuwa alikuwa na wazo la kuirudisha kwenye upagani hiyo Hija. Baada ya kuiteka Makka, katika Dhil-Hijja iliyofuata, Attab, gavana ambaye Muhammad alikuwa amemuweka hapo Makka, aliendesha hiyo ibada; Waislamu na mapagani wote walishiriki. Mwaka uliofuatia, Dhil-Hijja ya mwaka wa 9 (March-April 631), Muhammad bado alibaki nyuma na kutojiunga na Hija. Alikuwa bado hajakamilisha mafundisho yake juu ya kila jambo moja moja la hija na alikuwa hayuko radhi kufanya ibada hiyo pamoja na mapagani. Alimtuma Abu Bakr kwenda kuongoza ibada hizo. Alikutwa humo njiani na Ali, ambaye alikuwa mbebaji wa wahy mpya kabisa kutoka juu ambao ilikuwa ni kazi yake kuona unatekelezwa. Wapagani kwa kawaida walikuwa wasishiriki tena baada ya hapo katika hija. Katika kumalizika kwa muda wa makubaliano matakatifu ya miezi minne, wote ambao walikuwa bado hawajasilimu au kufanya mapatano maalum na Muhammad, watachukuliwa kama maadui. Huu ndio ulikuwa mwaka wa mwisho kwa mapagani kuruhusiwa kujiunga na hija.

Mwaka mmoja baadae, katika Dhul-Hijja ya mwaka wa 10 (Machi 632) Mtume (s.a.w.) alitangaza kwamba ataongoza mwenyewe ibada hiyo, kwa sababu sasa hekalu na sehemu takatifu zote zimetakaswa na kuwepo kokote kwa upagani. Aliwasili Makka mnamo 5 Dhil- Hajji (3 Machi). Mnamo mwezi 8 Dhil-Hijja, ibada zilianza. Macho yote yalimtazama Mtume (s.a.w.) kwa sababu mwenendo wake wakati wa ibada hizo utakuwa ni sheria.

(Muhammad)

251

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Siku ya mwezi 9 Dhil-Hajj ya mwaka wa 10 H.A., Mtume (s.a.w.) alitoa hotuba ya kihis-toria katika bonde la Arafat ambayo ndani yake alitoa mukhtasari wa mambo muhimu katika mafundisho yake. Mtume (s.a.w.) kwanza alimshukuru Allah (s.w.t.) kwa neema na rehema zake zisizo na idadi, na kisha akasema:

"Enyi Waislamu! Nisikilizeni kwa makini. Hii inaweza kuwa safari yangu ya mwisho yakuwa pamoja nanyi, na ninaweza nisiwe hai kufanya hija nyingine.

Allah (s.w.t.) ni Mmoja na Yeye hana washirika. Msimshirikishe mtu yeyote au kitu chochote pamoja Naye. Muabuduni Yeye, muogopeni Yeye, mtiini na mumpende Yeye. Msizikose Swala zenu za wajibu. Tekelezeni kikamilifu ule mwezi wa mfungo. Toeni Zaka kwa desturi yake, na tembeleeni Nyumba ya Allah (s.w.t.) wakati wowote mtakapoweza.

Kumbukeni kwamba kila mmoja wenu anawajibika kwa Allah (s.w.t.) kwa kila kitu mnachofanya katika dunia hii, na hivi karibuni tu mtajikuta wenyewe mbele Yake.

Ninazifuta desturi zote, matendo na mila za Wakati wa Ujahilia. Ninakataa haki ya kulipiza kisasi kwa ajili ya damu ya binamu yangu, Ibn Rabi'a; na ninakataa riba kwenye mikopo iliyotolewa na ami yangu, Abbas ibn Abdul-Muttalib.

Ninawalinganieni wote kuonyesha heshima kwa utu, maisha na mali ya kila mmoja wenu kwa namna ileile kama mnavyoonyesha heshima kwa utukufu wa siku hii. Waumini wote ni ndugu kwa kila mmoja wao. Kama kitu ni mali ya mmoja wao, ni haramu kwa wengine kukichukua bila ya ruhusa yake.

Kuweni waaminifu katika maneno na vitendo vyenu, na kuweni waaminifu kwa kila mmoja wenu, na bakini mmeungana wakati wote.

Mnazo haki kuhusu wanawake; hivyo pia mnao wajibu juu yao. Watunzeni kwa mapenzi, upole, heshima na upendo.

Watumwa mlionao wao pia waliumbwa na Allah (s.w.t.). Msiwe wakali kwao. Kama wakikosea, wasameheni. Wapeni wale kile mnachokula ninyi na wapeni wavae namna ileile ya nguo mnazovaa nyie.

Watu wa familia yangu ni kama ile nyota ya kaskazini. Watawaongoza kwenye uon-gofu wale wote watakaowatii na kuwafuata wao. Ninawaachieni miongoni mwenu urithi wa vitu viwili - Kitabu cha Allah (s.w.t.) (Qur'an) na watu wa nyumba yangu. Vyote vinakamilishana na havitenganishiki. Kama mtavinyenyekea vyote hivi ham-tapotea kamwe.

252

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Na kumbukeni kwamba mimi ndiye wa mwisho wa Mitume wa Allah (s.w.t.) kwa wanadamu. Baada yangu mimi hakutakuwa na Mtume mwingine au mitume wa Allah

(s.w.t.)"

Muhammad Mustafa alimalizia hotuba yake kwa du'a nyingine fupi ya shukurani kwa Muumba wake, na akamuomba Yeye awe Shahidi kwamba ametekeleza kazi yake, ame-timiza wajibu wake, na amefikisha ujumbe wa Uislamu kwa watu wake.

Hotuba hii, kama hutuba nyingine zote za Mtume, inafahamika kwa uwazi wake na maar-ifa yake ya kawaida ya kiutendaji. Alifupisha ndani yake mafundisho yake ili yagande kwenye nyoyo na akili za wasikilizaji wake kwa wakati wote.

Mtume (s.a.w.) alikuwa ameonyesha kwa Waislamu jinsi ya kutekeleza taratibu za Hija, na alikuwa amefagilia mbali mabaki ya upagani.

Katika hotuba yake, Mtume (s.a.w.) pia alidokeza kwamba alikuwa pengine hana muda mrefu wa kuishi. Ilikuwa ni karibu na wakati huu ambapo ile Sura ya 110 ya Qur'an Tukufu inayoitwa "Msaada" (Suratun-Nasr), ilipoteremshwa, na ambayo inasomeka kama ifutavyo:

"Itakapokuja nusura ya Allah, na ushindi, Na ukawaona watu wanaingia katika dini ya Allah kwa makundi,

Zitukuze sifa za Mola wako, na umuombe msamaha; hakika Yeye ndiye mwenye kupokea toba. "

Imam Bukhari anasimulia kwamba wakati Sura hii iliposhuka, Umar ibn al-Khattab alimuuliza Abdullah ibn Abbas kama angeweza kumuelimisha yeye juu ya maana yake. Ibn Abbas akasema: "Aya hizi zina maana kwamba wakati wa Mtume (s.a.w.) wa kututo-ka sisi unakaribia."

Wanahistoria wengi wa siku za baadae wa Mashariki na Magharibi wamedai kwamba kifo cha Mtume (s.a.w.) kilikuwa cha ghafla na kisichokuwa kimetegemewa. Lakini kifo chake hakikuwa cha ghafla wala kisichotegemewa. Kwa kweli, alikuwa wa kwanza yeye mwenyewe kuzungumza juu ya jambo hilo, na wakati ile Sura inayoitwa "Msaada" (Nasr) ilipoteremshwa, mashaka madogo sana yalikuwa yamebaki katika akili za maswa-haba wakuu kwamba kazi yake ya kidunia ilikuwa inafikia mwisho. Taarifa za kifo ziko kwenye Aya ya tatu ambamo alilinganiwa "kuomba msamaha Wake," na watu wenye utambuzi walikuwa wepesi kuupata ujumbe huo.

253

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Marmaduke Pickthall

Ilikuwa ni wakati wa hija ya mwisho ambapo ile Sura inayoitwa an-Nasr ilipoteremshwa, ambayo yeye (Muhammad) aliipokea kama tangazo la kifo kina-chokaribia.

(Introduction to the translation of the Holy Qur 'an, Lahore, Pakistan, 1975)

254

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kutawazwa kwa Ali ibn Abi Talib kama Mtawala

wa Baadae wa Waislamu, na kama Kiongozi

wa Umma wa Kiislam

Hija ya mwisho ilikuwa imekwisha, na Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) na lile kundi kubwa la wafuasi wake, walikuwa sasa wako tayari kurudi majumbani kwao. Alitoa ishara na ile misafara ya mahujaji ikaanza kuondoka Makka.

Katika kipande kifupi upande wa kaskazini ya Makka, kuna bonde linaloitwa Khumm, na huko Khumm kulikuwa na kisima au bwawa la maji (Ghadiir). Khumm ipo katika maku-tano ya njia nyingi. Wakati Mtume (s.a.w.) alipowasili katika ujirani wa Ghadiir, alipokea ujumbe mpya - wahy unaofuata kutoka Mbinguni:

Usahihi-29.jpg

Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako. Na kama hutafanya hivyo, basi utakuwa kama hujafikisha ujumbe Wake wowote. Na Allah atakulinda na watu. Hakika Allah hawaongoi watu makafiri. (Sura ya 5; Aya ya 67)

Agizo la Mbinguni lilikuwa mara chache, kama ilikuwa, ni yenye kuamrisha hivyo, kama ilivyo kwenye Aya hii, na ilihusishwa, dhahiri kabisa, kwenye jambo lenye umuhimu sana ambalo Mtume (s.a.w.) ilimbidi ajieleze mwenyewe - hapo hapo. Yeye, kwa hiyo, aliamu-ru mwenyewe msafara wake usimame, na aliirudisha misafara yote ambayo ilikuwa imek-wenda ama mbele au imekwenda pande zingine tofauti tofauti. Yeye mwenyewe alisubiri mpaka msafara wa mwisho ambao ulikuwa umeondoka Makka, pia umewasili jirani na kisiwa cha Khumm.

Mahujaji walikuwa wakagawanyike hapo Khumm kwenye misafara yao tofauti na walikuwa wakatawanyike, kila mmoja akielekea aendako. Mtume (s.a.w.) alikuwa na tangazo muhimu sana la kutangaza kabla ya kutawanyika kwa mahujaji, na alikuwa na shauku sana kwamba idadi kubwa kabisa ya Waislamu walisikie kutoka kwake.

"Mimbari" ilitengenezwa kwa haraka bila vifaa maalum kwa matandiko ya ngamia, na Mtume (s.a.w.) akapanda juu yake ili kwamba kila mtu kwenye ule mkusanyiko mkubwa aweze kumuona yeye kwa macho yake mwenyewe. Binamu yake, Ali, alikuwa amesima-

255

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ma karibu yake.

Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) alikuwa sasa yuko tayari kutoa lile tanga-zo la kihistoria katika kutimiza lile agizo tukufu lililonukuliwa hapo juu. Alimshukuru Allah (s.w.t.) kwa ile Neema kubwa ya Uislamu, na kwa Rehema Zake na Wema Wake, na kisha akauliza swali hili kwa Waislamu:

"Je, ninayo haki au sina haki kubwa zaidi juu ya nafsi zenu kuliko ninyi wenyewe mliyonayo juu yake?"

Waislamu wakajibu kwa sauti moja: "Mtume wa Allah anayo haki kubwa juu ya nafsi zetu kuliko sisi wenyewe tuliyonayo juu yake (hiyo nafsi)." "Kama hivyo ndivyo," alisema, "basi ninao ujumbe muhimu sana wa kufikisha kwenu," na akauelewesha ujumbe huo kama ifuatavyo:

"Enyi Waislamu! Mimi ni binadamu kama ninyi, na ninaweza kuitwa hivi karibuni mbele ya Mola wangu. Urithi wangu wa thamani sana kwenu ni Kitabu cha Allah (s.w.t.) na watu wa Nyumbani kwangu, kama nilivyowaambieni kabla. Sasa sikilizeni hili kwa makini kwamba mimi ni Bwana (Maula) wenu ninyi wote - wa Waumini wote. Wale wanaume na wanawake wote wanaonikubali mimi kama Bwana wao, ninawataka wamkubali (hapa aliushika mkono wa Ali na akaunyanyua juu zaidi ya kichwa chake) Ali pia kama Bwana (Maula) wao. Ali ni Bwana wa wale wanaume na wanawake wote ambao mimi na Bwana wao."

Alipokwisha kuutoa ujumbe huu, Muhammad Mustafa alinyanyua mikono yake kuelekea juu mbinguni, na akasema:

"Ewe Allah sw! Kuwa Rafiki wa yule ambaye ni rafiki wa Ali, na kuwa ni Adui wa yule ambaye ni adui yake. Msaidie yule anayemsaidia Ali, na umtelekeze yule anayemtelekeza yeye Ali."

Uliopita ni mukhtasari wa yale ambayo Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliyoyase-ma hapo Khumm. Maneno halisi na muktadha wa hotuba yake yamehifadhiwa katika kile kitabu maarufu Taudih-ed-Dala'il kilichoandikwa na profesa mkubwa wa Kisunni, Allamah Shahab-ud-Diin Ahmed. Ufuatao ni ufupisho wa hotuba hiyo kama ilivyoandik-wa katika Taudih-ed-Dalai ’l:

Ninatoa sifa na shukurani kwa Allah (s.w.t.) kwa neema Zake zote. Nashuhudia kwamba hapana Mola ila Allah (s.w.t.) na Yeye ni Mmoja, Mwenye Nguvu zote, Mkamilifu. Wote tunamtegemea Yeye. Yeye hana mke, hana mtoto, hana washirika. Mimi ni mmoja wa waja Wake lakini Yeye amenichagua mimi kama Mtume Wake

256

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kwa ajili ya uongofu kwa wanadamu. Enyi watu! muogopeni Yeye katika nyakati zote na kamwe msimuasi Yeye. Msipigane ila kwa ajili ya Uislamu, na kumbukeni kwam-ba elimu ya Allah (s.w.t.) imekizunguka kila kitu.

Enyi Waislamu! tahadharini kwamba wakati nitakapokuwa nimeondoka, watatokea watu ambao watahusisha Hadith za uongo kwangu mimi na watakuwepo watu wengine watakaoziamini hizo. Lakini ninaomba ulinzi wa Allah (s.w.t.) kwamba nisi-je kamwe kusema kitu chochote bali Ukweli na kuwaiteni kwenye lolote ila kile Yeye alichoteremsha kwangu. Wale wanaovuka mipaka katika jambo hili, watapata adhabu.

Kufikia hapa sahaba mmoja, Ibada ibn Samit, alisimama na akauliza: "Ewe Mtume wa Allah (s.w.t.)! wakati huo utakapofika, ni nani tutakaye muangalia kwa ajili ya mwongo-zo?"

Mtume wa Allah (s.w.t.) alijibu kama ifuatavyo:

"Muwafuate na kuwatii 'Watu wa Nyumba yangu' (Ahlul-Bait)." Wao ndio warithi wa elimu yangu ya kinabii na utume. Watawaokoeni kutokana na upotovu, na watawaongozeni kwenye uongofu. Watawalinganieni kwenye Kitabu (Qur'an Tukufu) na Sunnah yangu. Wafuateni hao kwa sababu hawana shaka kamwe juu ya jambo lolote. Imani yao juu ya Allah (s.w.t.) haiyumbi. Wao ndio wale walioongozwa sawasawa; wao ndio wale Maimamu, na ni wao peke yao wanaoweza kuwaokoeni kutokana na ukafiri, uasi na uzushi.

Allah (s.w.t.) amekuamuruni kuwapenda Ahlul-Bait wangu. Utii kwao umefanywa ni lazima juu yenu (Qur'an Tukufu: Sura ya 42; Aya ya 23). Wao ndio wale walio-takaswa (Qur'an Tukufu Sura ya 33; Aya ya 33). Ndio wale waliopewa uadilifu na ubora ambao hakuna mtu mwingine yoyote aliyenao. Wao ndio Wateule wa Allah (s.w.t.) Mwenyewe.

Sasa nimeamriwa na Allah (s.w.t.) kutoa tangazo hili:

Hapa aliushika mkono wa Ali, akaunyanyua juu kabisa, na akasema: "Fahamuni ninyi wote, yeyote yule ambaye mimi ni Maula (Bwana) wake, Ali ni Maula (Bwana) wake. Ewe Allah! Kuwa Rafiki wa yule ambaye ni rafiki wa Ali, na kuwa Adui kwa yule ambaye ni adui wa Ali. Ewe Allah! Msaidie yule anayemsaidia Ali, na mtelekeze yule anayemtelekeza Ali."

Hotuba ilikwisha. Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.w.t.) alikuwa kiutaratibu na kirasmi amekwisha kumtangaza Ali ibn Abi Talib kuwa Mkuu wa Waislamu wote, na

257

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

amemteua kama kiongozi wa Dola na Serikali ya Kiislamu.

Mara tu baada ya kutolewa tangazo hili, Aya nyingine, Aya ya mwisho ya Qur'an Tukufu, iliteremshwa kwa Muhammad. Inasomeka kama ifuatavyo:

Usahihi-30.jpg

Leo hii nimekukamilishieni dini yenu, na Nimekutimizieni Neema Yangu, na Nimekuchagulieni Uislamu kuwa dini yenu. (Sura ya 5; Aya ya 3)

Ilikuwa ni siku ya 18 ya mwezi wa 12 wa mwaka wa 10 wa kalenda ya Kiislam (Machi 21, 632) wakati Aya ya mwisho ya Ufunuo ilipoteremshwa duniani hapa. Wahy ulikuwa umeanza mwaka 610 A.D., katika pango la Hira huko Makka, na ulifikishwa mwisho mwaka 632 A.D., katika bonde la Khumm kwa tangazo kwamba Ali ibn Abi Talib atakuwa ndiye Mtekelezaji Mkuu, baada ya Muhammad mwenyewe, wa Serikali ya Madina na Dola ya Kiislamu.

Ibn Hajar Asqalani anaandika katika Isaba kwamba baada ya kutoa tangazo hili, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliweka kilemba juu ya kichwa cha Ali ibn Abi Talib, na hivyo kukamil-isha kutawazwa kwake.

Masahaba wote walimpongeza Ali katika tukio hili tukufu wakati Mtume wa Allah (s.a.w.) mwenyewe alipomtawaza yeye na kumtangaza kama mshikamakamu na mrithi wake. Miongoni mwa wale ambao walimpongeza walikuwa Umar bin al-Khattab na wake za Mtume.

Hasan bin Thabit Ansari alikuwa ndiye mshairi wa baraza la Mtume, na alitungia mashairi matukio yote muhimu. Kutawazwa kwa Ali kulikuwa ni moja kati ya matukio ya kihisto-ria sana ambayo yalikitia changamoto kipawa chake cha ushairi. Alitunga wimbo wa sifa ambao aliutoa kwa heshima ya Ali.

Ifuatayo ni tarjuma ya haraka haraka ya beti zake:

Katika siku ya Ghadir Khumm, Mtume (s.a.w.) na Waislamu aliwaita, na nilimsikia wakati yeye aliposema:

"Ni nani Mola wenu, na ni nani Bwana wenu?" Wote wakasema: "Allah (s.w.t.)

ndiye Mola wetu, na wewe ndiye Bwana wetu, na hakuna yeyote kati yetu

anayeweza kukukaidi wewe."

Hivyo alimuomba Ali asimame. Wakati Ali aliposimama, aliushika mkono wake,

na akasema:

"Nakuchagua wewe kama kiongozi baada yangu. Kwa hiyo, yeyote yule ambaye

258

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Bwana wake ni mimi,

Ali ni Bwana wake pia. Kwa hiyo, nyote nyie muwe marafiki zake wa kweli na

wafuasi wake."

Mtume (s.a.w.) kisha akaomba, akisema: "Ewe Allah! kuwa Rafiki kwa wale

ambao ni marafiki wa Ali;

na kuwa Adui wa wale ambao ni maadui zake."

Mshairi mwingine ambaye alitunga mashairi katika tukio la kutawazwa kwa Ali, alikuwa ni Qays ibn Ubada Ansari. Alisema:

Wakati maadui walipoasi dhidi yetu, nilisema kwamba Mpaji wetu, Allah (s.w.t.) anatutosha sisi, na Ndiye Mlinzi bora tunayeweza kuwa naye.

Ali ni Bwana wetu na ni bwana wa waumini wote. Hili linathibitishwa na Qur'an Tukufu na ni hivyo tangu ile siku Mtume wa Allah (s.a.w.) aliposema: "Yeyote yule ambaye Bwana wake ni mimi, Ali ni Bwana wake pia" Hili kwa hakika lilikuwa ni tukio la kufahamika sana.

Chochote kile Mtume wa Allah (s.a.w.) alichokisema siku ile, ni mwisho; ndio neno la mwisho, na hakuna kabisa nafasi ya hoja yoyote ndani yake.

Kwa mshangao na kutosadikika, hata mtu kama Amr bin Al-Aas "alitiwa moyo" kutoa shairi kwa heshima ya Ali hapo Ghadir Khumm. Ifuatayo ni mistari miwili ya utunzi wake:

Pigo la upanga wa Ali ni kama kile kiapo cha utii ambacho kila mmoja ali-kichukua ile siku ya Ghadir, na ambacho kilimfanya kila mtu kusalimu amri mwenyewe mbele ya mamlaka yake (mapya).

Kama hizo Aya mbili za Qur'an zinazohusu kutawazwa kwa Ali, zitasomwa katika utarat-ibu wa mpango wake, na katika fuo lake la kihistoria, maana zao zitakuwa wazi. Nitazinukuu mara nyingine tena katika uchambuzi mfupi; na kwa wepesi wa rejea, nitazi-ita Aya ya kwanza na ya pili.

{1}. Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako.

Na kama hutafanya hivyo, basi utakuwa kama hujafikisha ujumbe Wake wowote. Na Allah atakulinda na watu. Hakika Allah hawaongoi makafiri.

{2} Leo hii Nimekukamilishieni dini yenu na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuchagulieni Uislamu kuwa dini yenu.

Kutawazwa kwa Ali kulitokea ndani ya mfumo wa Aya hizi mbili za Qur'an. Kutawazwa kwake kulikuwa ni jambo lenye mkazo kiasi kwamba Muhammad Mustafa, Mpokezi wa

259

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Wahy, aliamriwa, katika Aya ya kwanza, kusimamisha chochote alichokuwa anakifanya, na ashuhulishwe kwanza na hilo. Yeye, kwa hiyo, aliwaamuru mahujaji wote wakusanyike katika bonde la Khumm, na akawaambia kwamba Ali atawatawala wao kama mrithi wake katika Ufalme wa Mbinguni katika Ardhi.

Mara tu Mtume (s.a.w.) alipokwisha kufanya hivyo, kisha hii Aya ya pili ilishushwa kama ishara ya idhini ya Mbinguni ya kitendo chake. Kutangazwa kwa Ali kama mrithi wake kulikuwa ndio ukamilisho na kilele cha kazi ya maisha ya Muhammad. Kwa tangazo hili, kazi yake kama Mtume wa Allah (s.a.w.) ilikamilika. Alikuwa amemtangaza Ali kuwa mrithi wake kwenye matukio mengi wakati uliopita lakini pale Ghadir-Khumm, alimtawaza rasmi kama Kiongozi wa Umma wa Kiislamu wa baadae.

Kati ya Aya hizi mbili za Qur'an-moja yenye nguvu sana katika kudai kitendo na ile nyingine ikiwa dhahiri mno katika kuthibitisha kwake usimikwaji wa Ali kama mrithi wa Mtume (s.a.w.) - na kauli ya Mtume: "Ali ni Bwana wa wale wanaume na wanawake wote ambao mimi ni Bwana wao," kuna uwiano wa kimantiki na wa dhahiri.

Walaghai wengine wamejadili bila msingi hili neno Maula kama lilivyotumiwa na Mtume (s.a.w.) wakati aliposema: "Ali ni maula wa wale wanaume na wanawake ambao mimi ni maula wao. Wanakubali kwamba kauli hiyo ni halisi lakini wanalitafsiri neno maula sio kama "Bwana" bali ni kama "rafiki." Lakini hii haikuwa ndio dhimiri ya Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Hivi aliirudisha ile misafara yote na kuwaamuru wakusanyike katika lile bonde la Khum lisilo na kivuli kwa ajili tu ya kuwaambia kwamba Ali ni rafiki yao? Je, ilichukuliwa na maswahaba wakati ule kwamba Ali hakuwa rafiki yao, na Mtume (s.a.w.) ikambidi awahakikishie wao kwamba yeye (Ali) kwa kweli alikuwa ni rafiki yao?

Wale watu wanaolitafsiri hili neno maula kama "rafiki," labda wanasahau kwamba Mtume (s.a.w.) alilitumia kwa kujihusisha yeye mwenyewe kabla hajalitumia kumhusu Ali, na hili linaweza kuruhusu tu tafsiri moja sahihi, ndio kusema, kama Muhammad, Mtume, ndiye Bwana wa Waislamu wote, Ali pia ni Bwana wao.

Walaghai hao pia wanasahau kwamba kabla ya kumtangaza Ali kama mrithi wake na mkuu wa Waislamu wote, Mtume (s.a.w.) alikwisha kuwauliza swali lifuatalo:

"Ninayo au sinayo haki kubwa zaidi juu ya nafsi zenu kuliko mliyonayo ninyi wenyewe juu yenu?"

Jibu la Waislamu kwa swali hili lilikuwa ni "ndio" isiyo na kifani. Swali hili lilikuwa ni la utangulizi wa tangazo la Mtume (s.a.w.) kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi wake. Hilo swali na hilo tangazo vilikuwa ni sehemu ya muktadha huo huo, na kama vikisomwa pamoja, havitaacha shaka yoyote akilini mwa msomaji kwamba hili neno maula maana yake ni "Bwana" na sio "rafiki."

260

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Wengi wa wafasiri wa Ki-Sunni wamekubali kwamba ile amri ya Allah (s.w.t.) kwa Mtume Wake katika ile Aya ya kwanza inafungamana hasa na tangazo kwamba Ali ndiye Mkuu wa Waislamu wote. Baadhi ya wafasiri hawa ni:

Wahidi katika Asbab-un-Nuzuula

Suyuti katika Tafsir Durr al-Manthur

Ibn Kathir

Imam Ahmad bin Hanbal

Abu Ishaq Nishapuri

Ghazali katika Sirrul-Alamiin

Tabari katika Tarikh-ar-Rusul wal-Muluuk

Sheikh Abdul Haq Muhaddith wa Delhi, India

Hapa ni lazima pia ielezwe kwamba kabla ya kushushwa kwa Aya hiyo ya kwanza (5:67), amri zote zinazohusika na Shari 'ah (mfumo wa kanuni na taratibu za dini ya Kiislam), kama vile Sala za kila siku, Funga, Zaka, Hajj (kwenda Hija Makka), na Jihad - kwa haki-ka zile sheria zote kwa maisha ya mtu binafsi, kijamii, kiuchumi na kisiasa za Waislamu, zilikuwa tayari zimekwisha kutolewa kwa Muhammad. Alikuwa amekwisha zifikisha, na Waislamu walikuwa wakizifanyia kazi, na zimekuwa sehemu muhimu za maisha yao. Alikuwa amekwisha kutambulisha na kutekeleza kila sheria.

Kitu pekee ambacho Mtume (s.a.w.) alikuwa bado hajakifanya hadi kufikia wakati huo, kilikuwa ni kumtambulisha rasmi kwa umma wake, mrithi wake mwenyewe. Umma huo ulikuwa unayo haki ya kujua ni nani atakayekuwa mtawala wake baada ya kifo chake (yeye Mtume). Hiki ndicho alichokifanya wakati alipoamriwa "kufikisha ujumbe." Hii amri ya Allah (s.w.t.) ilikuwa na nguvu sana, na Mtume (s.a.w.) hakuweza kuahirisha utekelezaji wake kwa muda mwingine.

Lakini mara tu baada ya Mtume (s.a.w.) kutekeleza ile amri ya mbingnii, kwa uwazi kamili na kwa uamuzi wa mwisho kabisa, ile Aya ya pili (5:3) iliteremshwa, na iliweka muhuri wa uthibitisho juu ya kitendo chake.

Kwa usimikwaji rasmi wa Ali ibn Abi Talib kama mrithi wa Muhammad na kama kiongozi wa Waislamu wote, imeandikwa katika Aya za mwisho zilizoteremshwa kwenye Kitabu cha Allah (s.w.t.).

Aya ya mwisho ya Kitabu cha Allah (s.w.t.) ilishushwa na iliandikwa mnamo Machi 21, 632, kama ilivyoelezwa kabla, na mlango wa Wahy ukafungwa milele. Siku themanini baadae, yaani, mnamo Juni 8, 632, Muhammad Mustafa aliagana na umma wake, na akaenda mbele ya Mola wake. Hakuna kumbukumbu kwamba aliupa umma wake amri

261

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

mpya zozote au makatazo (Awamir au Nahawi), ya mafundisho au ya vitendo, katika muda wa hizi siku 80. Uislamu ulitangazwa kuwa umekamilika na kutimia mara tu baada ya Mtume Wake kumteua Ali ibn Abi Talib kuwa mrithi wake.

Allah (s.w.t.) awazidishie waja Wake, Muhammad na Ali, na watu wa familia zao, Fadhila Zake, na Neema na Baraka Zake.

Muhammad Mustafa angeweza sasa kuangalia nyuma kwa kuridhika juu ya kazi yake, na angeweza kuangalia mbele kwenye wakati ujao kwa matumaini mapya, kwa kujiamini na furaha. Kwa kumuweka Ali kama mrithi wake, aliuona uendeleaji wa ile kazi ambayo kwayo alitumika bila kujizuia kwa miaka 23, na ambayo ilikuwa imejaa vitisho na hatari nyingi. Kazi yake imehitaji mihanga isiyo na idadi kwa upande wake. Sasa ilionekana kwake kwamba zile suluba zake zote na ile mihanga mwishowe imezaa matunda, kwa vile alijua kwamba Ali atakiendesha chombo cha Uislamu kule kiendako kwa ustadi uleule kama yeye mwenyewe alivyofanya.

Muhammad hakumchagua Ali kuwa mrithi wake kwa sababu tu kwamba alikuwa binamu yake, mkwewe, na sahaba wake mpendwa; wala hakumchagua kwa sababu ya sifa binafsi zake yeye Ali. Muhammad alikuwa na kidogo sana cha kufanya na uchaguzi wake. Mpangilio wa muda wa kushuka kwa Aya hizi mbili za mwisho za Qur'an Tukufu (5:67 na 5:3), na matukio yaliyopita wakati wa muda baina ya wahy hizi mbili, na uwiano wao, vinamuongoza mfuatiliaji kwenye hatima moja tu, yaani, uchaguzi wa Ali kama mrithi wa Mtume (s.a.w.) wa Uislamu, ulifanyika Mbinguni. Allah (s.w.t.) Mwenyewe aliyemchagua Ali. Allah (s.w.t.) asingeweza kuchagua wa tatu au wa pili. Angeweza kuchagua tu yule msafi sana, mbora, wa kipekee kabisa, kama alivyokuwa Ali. Ali alikuwa ndio alama na kielelezo dhahiri cha Ukweli wa Uislamu, na alikuwa ndiye shahidi wa kwanza wa Ukweli wa Mtume (s.a.w.) wa Uislamu. Allah (s.w.t.) awabariki wao wote na familia zao.

Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) alitumia kila nafasi kutaka uangalifu wa Waislamu kwenye daraja tukufu ya Ali. Katika moja ya Hadithi zake mashuhuri (kauli, simulizi), alisema kwamba uhusiano wake na Ali ulikuwa ni sawa na ule wa watangulizi wake wa kinabii - Musa na Harun - pamoja na tofauti tu kwamba Ali hakuwa ni Mtume.

Hadithi hii ilisimuliwa na Saad bin Abi Waqqas, na imeandikwa na Imam Muslim katika Sahihi yake kama ifuatavyo:

Amir bin Sa'd bin Abi Waqqas amesimulia kutoka kwa baba yake kwamba Mtume wa Allah (s.w.t.) (amani iwe juu yake) akimwambia Ali alisema: "Unayo daraja ileile katika uhusiano na mimi kama Harun aliyokuwa nayo kwa Musa lakini pamoja (na tofauti hii ya wazi) kwamba hakuna nabii baada yangu." Sa'd akasema: "Nilikuwa na hamu kubwa ya kuisikia moja kwa moja kutoka kwa Sa'd, hivyo nilikutana naye na

262

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

nikamweleza kile ambacho Amir (mwanae) alikuwa amenisimulia, ndipo akasema: "Ndio, niliisikia." Mimi nikasema: "Uliisikia wewe mwenyewe?" Hapo akaweka vidole vyake juu ya masikio yake na akasema: "Ndio, na kama sivyo, basi masikio yangu yote nayazibe kabisa."

Sa'd bin Abi Waqqas amesimulia kwamba Mtume wa Allah (s.w.t.) (amani iwe juu yake) alimuacha Ali ibn Abi Talib nyuma yake alipokuwa anakwenda Tabuk, ambapo yeye (Ali) alisema: "Ewe Mtume wa Allah, unaniacha mimi hapa pamoja na wanawake na wato-to?" Hapo Mtume (s.a.w.) akasema: "Huridhiki wewe kuwa kwangu mimi kama alivyokuwa Harun kwa Musa bali kwa tofauti kwamba hakutakuwa na nabii baada yangu mimi?"

Hadithi hii imesimuliwa kutoka kwa Shu'ba kwa sanadi ileile ya wapokezi. Amir bin Sa'd bin Abi Waqqas amesimulia kutoka kwa baba yake kwamba Mu'awiyyah bin Abu Sufyan alimteua Sa'd kama gavana na akasema: "Ni nini kinachokuzuia kumtukana Abu Turab (Ali)?" Akasema: "Ni kwa sababu ya mambo matatu ambayo nilimsikia Mtume wa Allah (s.w.t.) akiyasema juu yake ambayo kwayo sintamtukana yeye, na kama ingekuwa nipate hata moja tu ya yale mambo matatu, lingekuwa na thamani sana kwangu kuliko ngamia wekundu. Nilimsikia Mtume wa Allah (s.w.t.) akisema kuhusu Ali pale alipomuacha yeye (huko Madina) wakati alipokuwa anakwenda kwenye msafara (Tabuk). Ali alimwambia: "Ewe Mtume wa Allah (s.w.t.) hivi unaniacha mimi hapa na wanawake na watoto.?" Hapo Mtume wa Allah (s.w.t.) akamwambia: 'Hivi huridhiki wewe kuwa kwangu mimi kama Haroun alivyokuwa kwa Musa bali pamoja na tofauti kwamba hakuna utume baada yangu?' Na mimi pia nilimsikia akisema ile Siku ya Khaibar: 'Nitampa bendera hii mtu ambaye anampenda Allah (s.w.t.) na Mtume Wake, na ambaye Allah (s.w.t.) na Mtume Wake wanampendwa.' Yeye (msimuliaji) akasema: Tulikuwa tunaisubiri kwa hamu sana wakati yeye (Mtume) aliposema: 'Mwiteni Ali.' Alikuja na macho yake yalikuwa yanawasha. Alimuweka mate kwenye macho yake na akampa ile bendera, na Allah (s.w.t.) akampa ushindi..

Safari ya tatu ilikuwa ni wakati Aya ifuatayo iliposhuka: "...Tuwaite watoto wetu na watoto wenu..."

Mtume wa Allah (s.a.w.) alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husein na akasema: "...EweAllah! Hawa ndio watu wafamiliayangu..."

Hadithi ya Mtume (s.a.w.) ambamo amesema kwamba Ali alikuwa kwake kama Harun alivyokuwa kwa Musa, inakubaliana na Aya za Qur'an Tukufu zifuatazo:

(Musa aliomba):

"Ewe Mola wangu! Nikunjulie kifua changu;

263

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Niwepesishie kazi yangu;

Na uniondolee vifundo kwenye ulimi wangu;

Wapate kuyaelewa maneno yangu;

Na unipe waziri katika familia yangu;

Harun, ndugu yangu,

Kwake yeye uniongezee nguvu zangu,

Na umshirikishe katika kazi yangu:

Ili tukutukuze sana;

Na tukukumbuke sana;

Hakika Wewe unatuona sisi."

(Allah (s.w.t.)) Akasema:

Usahihi-31.jpg

"Hakika umekubaliwa maombi yako, Ewe Musa!" Na hakika tulikwisha kukufanyia hisani juu yako mara nyingine kabla. (Sura ya 20; Ay a ya 25 hadi 37)

Nabii Musa (a.s.) alimuomba Allah (s.w.t.) ampatie Waziri kutoka kwenye familia yake mwenyewe. Hakutaka waziri kutoka miongoni mwa maswahaba na marafiki zake. Aliomba kwamba Harun, ndugu yake, awe ndiye Waziri wake, na angekuwa ni chanzo cha nguvu kwake.

Allah (s.w.t.) alijibu du'a ya Mtume Wake Musa, akampa ndugu yake, Harun, kama waziri wake, na akamfanya kuwa chanzo cha nguvu kwake.

Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Mwisho wa Allah, pia alichagua waziri wake kutoka kwenye familia yake mwenyewe. Chaguo lake lilikuwa ni Ali, ndugu yake. Ali aliongeza nguvu zake, na alishiriki kwenye kazi yake pamoja naye, kama vile ambavyo aliahidi kufanya, miaka mingi iliyopita, katika karamu ya Dhu ’l- 'Ashiira huko Makka katika mku-sanyiko wa wazee wa koo za Bani Hashim na Bani Muttalib.

Usahihi-32.jpg

(Kabla ya hapa) Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukamweka pamoja naye, nduguye Haroun, kuwa waziri. (Sura ya 25; Ay a ya 35)

Allah (s.w.t.) Mwenyewe alimchagua Harun kuwa Waziri. Haukuwa umma (watu) wake Musa ambao walimchagulia Waziri wake.

264

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Usahihi-33.jpg

Tulimuahidi Musa masiku thelathini, na tukayatimiza kwa kumi zaidi: Hivyo ikatimia ahadi ya Mola wake, masiku arobaini. Na Musa akamwambia ndugu yake Harun (kabla ya kuon-doka): Shika mahala pangu miongoni mwa watu wangu; ufanye haki na wala usifuate njia ya waharibifu. (Sura ya 7; Aya ya 142)

Musa alimweka ndugu yake, Harun, kwenye madaraka juu ya umma (watu) wake, na haku-uacha (huo umma) bila ya kiongozi ingawa alikuwa anaondoka kwa siku arobaini tu.

Muhammad Mustafa (rehma na amani ziwe juu yake na kizazi chake) hakukengeuka kwenye mwenendo huu wa manabii na mitume wa Allah (s.w.t.) Yeye pia hakuwaacha Waislamu bila ya kiongozi, na alimchagua ndugu yake, Ali, kama kiongozi na mtawala wao baada yake.

Musa aliomba:

Usahihi-34.jpg

"Ewe Mola wangu! Nisamehe mimi na ndugu yangu! Na utuingize katika Rehema Yako! Kwani Wewe ni Mwenye kurehemu kuliko wote wenye kurehemu. (Sura ya 7; Aya ya 151)

Musa hakujiombea yeye peke yake tu; alimuombea ndugu yake Harun pia. Muhammad Mustafa pia aliombea wote, yeye mwenyewe na ndugu yake, Ali. Aliomba rehema za Allah (s.w.t.) juu yao wote na familia zao.

Usahihi-35.jpg

Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Harun. Amani iwe juu ya Musa na Haroun. Hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa walio wema. Hakika wawili hao ni katika waja walioami-ni. (Sura y a 37; Ay a ya 114, 120, 121, 122)

265

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Allah (s.w.t.) aliweka Rehema Zake juu ya Musa na Harun, na aliweka Rehema Zake juu ya Muhammad na Ali, waja Wake walioamini. Wote wanne walitenda haki, na Allah (s.w.t.) akawalipa wao, na akashusha amani na salamu kwao.

Ingawa Harun alichaguliwa ki-mungu kuwa mrithi na msikamakamu wa Musa, alikufa katika uhai wake (Musa), hivyo kusababisha kuchaguliwa kwa kiongozi mpya. Kiongozi mpya alikuwa ni Yush'a bin Nun (Joshua). Kama Harun, yeye pia, aliteuliwa ki-mungu kuwa mshikamakamu wa Musa, na umma haukuwa na lolote la kufanya katika kuchaguliwa kwake.

Baada ya kifo cha Musa, mshikamakamu wake, Yush'a bin Nun, aliwaongoza Bani-Israil kwenye ushindi.

Vigezo vya hekima katika suala la kuchagua na kuweka kiongozi wa umma wa Kiislam, baada ya kifo cha Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.w.t.) vinaweza kuonekana wazi katika Aya za Qur'an zilizonukuliwa hapo juu. Ali alikuwa ndiye chaguo la Mbinguni. Chote alichokuwa afanye Muhammad, ni kule kutoa lile tangazo rasmi kwamba Ali atakuwa ndio kiongozi wa Waislamu baada ya kifo chake yeye mwenyewe. Ilikuwa ni kutoa Tangazo hili ambako aliwaamuru Waislamu kukusanyika kwenye bonde la Khumm.

Mwislamu wa kisasa anaweza kuchukulia kwamba hili Tangazo la kihistoria lililotolewa na Mtume, lazima lingefuatiliwa na sherehe ya kimataifa miongoni mwa Waislamu. Inaonekana kuwa ni ajabu kusema kwamba haikuwa hivyo. Walikuwepo Waislamu waliokuwa na furaha lakini walikuwepo wengine wengi ambao hawakufurahia. Hawa wengine waliwazia mategemeo mengine, na walijali tamaa nyingine, na mategemeo na tamaa zao havikubadilisha mwelekeo wa tangazo la Mtume (s.a.w.) pale Ghadir-Khumm. Tangazo lake, la wazi kabisa na lisilo na mashaka, ilivuruga matumaini na tamaa zao.

Lakini hawakuvunjika moyo. Walitunga jambo jingine. Walianza kunon'gona kwenye masikio ya Waarabu kwamba uteuzi wa Ali kama Mkuu wa Waislamu wote kulikuwa ni kitendo kilichochochewa na tamaa ya Mtume (s.a.w.) ya kuhodhi mamlaka ya kisiasa katika familia yake mwenyewe - katika ukoo wa Bani Hashim - na kuwaondoa wengine wote, na kwamba haikuwa na uhusiano wowote na Wahy. Walitegemea kwamba ikiwa "hoja" yao itawavutia Waarabu, basi watakuwa na uwezo wa kuwaingiza kwenye kugombania madaraka ambamo wao wenyewe wanaweza wakawa wa juu. Tokea muda huo, Kwa hiyo, walianza kufanya kazi ya kujipangia mkakati mpya wa kupambana na hali hiyo mpya.

Walikuwa ni akina nani watu hawa? Hawakuainishwa kwa majina yao lakini kuwepo kwao na uwezo wao katika fitna vinaonekana katika ile Aya ya kwanza (5:67). Mtume, ni dhahiri, alikuwa anasita kuchukua hatua, akiwa anajua upinzani mkubwa wa Waarabu wengi kwenye kuchaguliwa kwa Ali kama kiongozi wa baadae wa Dola ya Kiislam. Lakini

266

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

alihakikishiwa kwamba Allah (s.w.t.) atamlinda kutokana nao hao; kwamba akushinde kusitasita kwake, na autangaze ushika-makamu wa Ali ibn Abi Talib.

Kupinga lile Tangazo la kihistoria pale Ghadir-Khumm kulikuwa ni kumpinga mwenyewe. Upinzani juu yake, mpaka wakati wa Tangazo lile, hata hivyo, ulikuwa umejificha na kuto-jionyesha; lakini muda si mrefu ulikuwa utokeze kichwa chake cha husuda katika wakati wa uhai wake yeye mwenyewe. Suala hili limeshughulikiwa katika Sura ya 39.

Kule kuteuliwa, na Muhammad Mustafa, pale Ghadir-Khumm, kwa Ali ibn Abi Talib kama mrithi wake, kumesimuliwa na maswahaba wake wafuatao:

Khuzayma bin Thabit

Sahl bin Sa'ad

Adiy bin Hatim

Aqba bin Aamir

Abu Ayyub Ansari

Abul-Haithum bin Taihan

Abdullah bin Thabit

Abu Ya'la Ansari

Nu'man bin Ajlan Ansari

Thabit bin Wadee'a Ansari

Abu Fadhala Ansari

Abdur Rahman bin Abd Rabb

Junaida bin Janada

Zayd bin Arqam

Zayd bin Sherheel

Jabir bin Abdullah

Abdullah bin Abbas

Abu Said al-Khudri

Abu Dharr al-Ghiffari

Salman el-Farsi

Jubayr bin Mutim

Hudhayfa bin Yaman

Hudhayfa bin Usayd

Miongoni mwa wanahistoria ambao wameandika matukio ya Ghadir-Khumm ni Athiir-ud-Diin ndani ya kitabu chake Usudul-Ghaba; Halabi katika kitabu chake Siira-tul-Halabiyya; na Ibn Hajar katika kitabu chake al-Sawa 'iq-al-Muhriqa.

Wapokezi wa Hadith waliotaja matukio ya Ghadir-Khumm ni akina Muslim, Nasai, Tirmidhi, Ibn Majah; Ahmad Hanbal na Hakim.

267

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Jeshi la Usamah

Zayd bin Haritha alikuwa ni mtumwa aliyeachwa huru na rafiki wa Muhammad Mustafa. Aliuawa katika vita vya Muutah mnamo A.D.629 ambavyo aliongoza Waislamu dhidi ya Warumi. Waislamu walishindwa katika vita hivyo, na walikimbilia Hijazi.

Mtume (s.a.w.) wa Uislamu alitaka kufutilia mbali ile kumbukumbu ya kushindwa kule lakini alikuwa akisubiria muda unaofaa kwa kufanya hivyo. Tangu wakati ule Mtume, rehema na amani juu yake na Ahlul-Bait wake, alipohamia Yathrib (Madina) mnamo mwaka 622, alifanya kazi kwa bidii sana. Alikuwa amebeba mzigo wa majukumu ambayo hata shirika la mashirika ya watu lingeona kwamba ni mazito zaidi mno. Tangu ile Hijja ya Muago mnamo Machi 632, alifanya kazi takriban bila kupumzika. Kazi ngumu mfululizo na ugumu maishani mwote vilichukua hesabu yake, na akaugua. Maradhi haya yalikuwa yawe ya kufisha. Ingawa alijisikia udhaifu hata kabla maradhi hayajaanza, hakuuruhusu udhaifu huo kuingilia kati kazi zake kama Mtume wa Allah (s.a.w.). na kama kiongozi mkuu wa Waislamu.

Ule "wakati unaofaa" uliosubiriwa kwa muda mrefu unaelekea kuwa umewadia mwishoni. Mtume (s.a.w.) aliandaa na kuanzisha jeshi jipya kufanya uvamizi wa mpaka wa Syria. Hadhi ya Uislamu ilikuwa imevunjwa katika vita vya Muutah, na wakati ulikuwa umefika wa kuirudisha upya. Kuongoza jeshi hilo, Mtume (s.a.w.) alimchagua Usamah, kijana wa miaka 18, mtoto wa Zayd bin Haritha, shahidi wa Muutah. Wote baba na mwana walikuwa vipenzi wakubwa wa Mtume. Lakini hakuwafanya kuwa majenerali kwa ajili ya upen-deleo; aliwafanya majenerali kwa sababu walifuzu kwa uwezo wao wa kusimamia watu wengine, na kuwaongoza kwenye vita.

Mnamo mwezi 18 Safar ya mwaka 11 A.H., Muhammad Mustafa aliweka bendera ya Uislamu mikononi mwa Usamah, akamweleza kwa kifupi malengo ya pambano hilo, na akampa maelekezo juu ya jinsi atakavyoliendesha. Kisha ndipo akawaamuru maswahaba wake wote, isipokuwa Ali na watu wengine wa Bani Hashim, kupiga ripoti kikazi kwa Usamah, na kuwajibika chini yake. Masahaba hawa walijumuisha watu wazima, watu matajiri sana, na watu wenye nguvu sana wa Maquraishi kama vile Abu Bakr, Umar, Abdur Rahman bin Auf, Abu Ubaida ibn al-Jarrah, Sa'ad bin Waqqas, Talha, Zubayr, Khalid bin Walid, na wengine wengi. Mtume (s.a.w.) alimuamuru Usamah kuondoka haraka mbele ya maswahaba hao na jeshi kuelekea kwenye kituo chake.

268

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Sir William Muir

Katika siku ya Jumatano iliyofuata, Muhammad alishikwa na maumivu ya kichwa makali na homa; lakini yalipita. Asubuhi iliyofuata alijikuta amepona kabisa kuweza kufunga kwa mkono wake mwenyewe kwenye mlingoti wa bendera, ile bendera kwa ajili ya jeshi. Aliikabidhi kwa Usamah pamoja na maneno haya: 'Pigana chini ya bendera hii kwa jina la Allah (s.w.t.) na kwa njia Yake. Hivyo utawashinda na kuwaua wale watu ambao hawamuamini Allah (s.w.t.)' Kisha kambi ikawekwa hapo Jurf; na kundi lote la wapiganaji, bila ya kumuondoa hata Abu Bakr na Umar, waliitwa kuji-unga nayo.

(The Life of Muhammad, London, 1877)

Muhammad Husein Haykal

Waislamu hawakukaa kwa muda mrefu hapo Madina kufuatia kurudi kwao kutoka kwenye Hija ya Muago huko Makka. Mtume (s.a.w.) aliamuru mara moja ukusanya-ji wa jeshi kubwa na akaliamrisha kwenda al-Sham. Alituma pamoja na jeshi hilo idadi ya wazee wa Kiislam, wale Muhajirina wa mwanzo, miongoni mwao ambamo Abu Bakr na Umar walikuwemo. Alitoa uongozi wa jeshi hilo kwa Usamah ibn Ziyad ibn Haritha,

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Mtume (s.a.w.) alilitaka jeshi hilo kuondoka Madina mara moja. Lakini ni ajabu kwamba jeshi hilo halikuonyesha shauku ya kumuitika yeye. Badala ya utii, Mtume (s.a.w.) aliku-tana na upinzani - kutoka kwa baadhi ya maswahaba wake! Tokea wakati huo na kuende-lea, Mtume (s.a.w.) ilimbidi apambane na matatizo mawili; moja lilikuwa ni kuvuka katika maradhi yake na jingine ni kushinda ule upinzani wa jeshi lake. Zile siku chache za mwisho za maisha yake hapa duniani zilitawaliwa na pambano hili lenye ncha-mbili.

Wale watu wakubwa wa Ki-Quraishi walichukia sana kule kunyanyuliwa kwa mvulana wa miaka 18 juu yao wote, na kwamba pia, mtoto, sio wa nasaba bora ya Quraishi, bali wa mtu aliyekuwa mtumwa kabla! Kwa hiyo, badala ya kuripoti kwake kikazi, wengi miongoni mwao wakaanza kutoroka na kuchelewesha muda kwa makusudi. Wengine miongoni mwao walikuwa hawakuridhika kabisa na uchaguzi wa Usamah kama jenerali wao kiasi kwamba walionyesha waziwazi kutoridhika kwao.

R.V.C. Bodley

...Wakongwe hawakulipenda lile wazo la kuwashambulia wale Warumi ambao walikuwa bado wanaogofya na mvulana, ambaye alikuwa na uzoefu mdogo wa kivi-ta, kama kiongozi wao. Muhammad alikuwa, hata hivyo, hashitushwi na malalamiko hayo. Alikuwa anaanzisha kigezo, kilichotazamwa tangu hapo miongoni mwa

269

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Waislamu, kwamba umri na hadhi katika jamii hakusababishi kufanya majenerali wazuri. Alikuwa akijenga ndani yao ujumbe wa demokrasia ambao walikuwa wau-peleke duniani kote. Bila ya kujadili ule uteuzi alimuita Usamah Msikitini na kumk-abidhi bendera ya Uislamu pamoja na kumnasihi namna ya kuiletea heshima.

(The Messenger, New York. 1946)

Kuteuliwa kwa Usamah kama jenerali hakukuwa, hata hivyo, ndio sababu pekee ya kwa nini baadhi ya maswahaba hawakupenda kwenda Syria. Kulikuwa na baadhi ya sababu nyingine pia za kwa nini waliamini ilikuwa ni muhimu sana kwao kubakia Madina, bila kutilia maanani amri za Mtume wa Allah (s.a.w.) Usamah alimuuliza Mtume (s.a.w.) kama haingekuwa bora kuahirisha ule uvamizi wa Syria mpaka atakapopona homa yake. Lakini Mtume (s.a.w.) alisema: "La. Nakutaka wewe uondoke muda huu huu."

Usamah alikwenda kwenye kambi yake huko Jurf lakini wachache wa maswahaba waliku-ja kuripoti kwa ajili ya kazi. Walijua kwamba ugonjwa wa Mtume (s.a.w.) umeleta "wasi-wasi" juu ya Umma (jamii), na waliona kwamba ni "hatari" kuondoka Madina kwa wakati kama huu ingawa waliona ni "salama" kudharau amri zake. Waliweka ile kanuni ya dha-habu ya "Usalama Kwanza" mbele ya amri za Mtume wa Allah (s.a.w.)

Mtume (s.a.w.) alikuwa na homa na maumivu makali ya kichwa lakini alimudu kwenda Msikitini, na kuhutubia ule mkusanyiko pale ambao ulijumuisha wengi wa waliochelewa nyuma, hivi:

"Enyi Waarabu! Mmekuwa wanyonge kwa sababu nimemteua Usamah kama jenerali wenu, na mnaleta maswali kama anazo sifa za kuwaongozeni ninyi kwenye vita. Ninajua ninyi ni watu wale wale mlioleta swali hili hili kuhusu baba yake. Wallahi, Usamah ana sifa za kuwa jenerali wenu kama vile baba yake alivyokuwa na sifa za kuwa jenerali. Sasa tiini amri zake na muende."

Betty Kelen

Mara baada ya ile Hijja ya Muago, pamoja na nia yake kuongezeka kasi zaidi kuelekea kaskazini kana kwamba katika kumfikisha mwisho, Muhammad aliandaa jeshi jipya la kupigana ugenini kwenda Syria, akimuweka mtoto wa Zayd, Usamah, kuliongoza - dhidi ya ushauri wa baadhi ya majenerali wake, kwa vile Usamah alikuwa na miaka ishirini tu. Muhammad aliwaambia kwa ukali, 'Mnamkemea yeye kama mlivyomkemea baba yake, lakini yeye anastahili zaidi uongozi kama baba yake alivyokuwa.'

Hakutaka tena kupoteza muda kutetea utendaji wake. Aliiweka bendera yake kwenye mikono ya Usamah na akamtuma kwenda kwenye uwanja wa kukusanyikia, lakini

270

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

mabishano yale yaliendelea kumchoma moyo hata hivyo.

(Muhammad, Messenger of God)

Wakati wowote Mtume (s.a.w.) alipopata nafuu kidogo kutokana na homa na kichwa chake, aliwauliza wale waliokuwepo kama jeshi la Usamah limeondoka kwenda Syria. Aliendelea kuwahimiza, 'Pelekeni jeshi la Usamah mara moja.'

Wapiganaji wa kawaida wa jeshi hilo waliitika amri za Mtume, na wakapiga ripoti kikazi kwa mkuu wa kikosi huko Jurflakini wengi wa maswahaba wakubwa hawakufanya hivyo. Wengine miongoni mwao walisita humo mjini; wengine, chini ya msukumo wa Mtume (s.a.w.) kwa muda wote, walikwenda Jurf lakini wakarudi. Walibaki wakisafiri kati ya kambi na mjini. Wengine wao walikuja mjini kuchukua vitu ambavyo vilikuwa vinakosekana kwenye zana, na wengine walitaka kusikia habari. Bado wengine walirudi "kujulia hali ya afya ya Mtume." Walikuwepo pia wale maswahaba ambao hawakwenda Jurf kabisa. Walibakia pale mjini kwa sababu ya "mapenzi" yao kwa Mtume (s.a.w.) kwa vile walikuwa hawakuwa na ule "moyo" wa kumuacha yeye katika wakati ambapo anaumwa vibaya sana.

Lakini haya malalamiko ya "mapenzi" na "wasiwasi" kwa ajili ya ustawi wake hayakumpendeza Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Kigezo cha kuthibitisha mapenzi yao kwake kilikuwa ni utii wao kwenye amri zake. Aliwaamuru kuondoka kwenda Syria lakini hawakwenda. Walimuasi yeye wakati wa siku zake za mwisho wa maisha yake.

Betty Kelen

Maradhi yake Mtume (s.a.w.) yalizidi, lakini alijaribu kuyatupilia mbali kwa ajili ya Usama, kwani vile habari za ugonjwa wa Muhammad zilivyoenea kote, huyu kijana alikuwa akipata muda mgumu kukusanya vikosi vyake. Watu wengine waliokuwa wamejiunga naye, walikuwa wakirejea Madina, na kwa uhakika hakuna waliokuwa wanabakia.

(Muhammad, Messenger of God)

Mwishowe, lisilopingika likatokea. Muhammad, Mtume (s.a.w.) wa mwisho wa Allah (s.a.w.) katika dunia hii, akafa. Juhudi yake ya kuwatoa maswahaba zake nje ya Madina, zikafika mwisho, pamoja na muonekano wa "ushindi" kwa maswahaba. Hawakupiga ripoti kikazi kwa Usamah na jeshi halikwenda kwenye pambano - wakati wa maisha yake!

Kwa Waislamu, kila amri ya Muhammad ni amri ya Allah (s.w.t.) Mwenyewe kwa sababu yeye ndiye Mfasiri wa amri hizo, wa Mapenzi na Makusudio ya Allah (s.w.t.) Uasi kwa Muhammad ni uasi kwa Allah (s.w.t.) Mwenyewe. Kwa hiyo, wale watu waliomuasi yeye

271

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

(Muhammad) walipata ghadhabu za Allah (s.w.t.)

Vita vya Muutah vilipiganwa mnamo mwaka 629 A.D., na kuishia kwenye kushindwa kwa Waislamu. Mtume (s.a.w.) alitaka kufuta lile doa la kushindwa. Lakini haikuwa mpaka miaka mitatu baadae - mnamo mwaka 632 A.D. - ambapo alimuamuru Usamah kuvamia mpaka wa Syria katika ufidiaji wa yale maafa ya Muutah.

Upangiliaji wa muda wa msafara wa Usamah unazua msongamano wa maswali. Kwa nini Mtume (s.a.w.) asitume msafara wake wa kuadhibu huko Syria katika muda wowote wakati ile miaka mitatu ya kati? Kwa nini alichagua muda kabla tu ya kifo chake mwenyewe kuutuma msafara huo? Kwa nini, ghafla tu, ilikuja kuwa muhimu sana juu yake kuwatuma maswahaba wake na wapiganaji nje ya Madina?

Kama ilivyoonyeshwa kabla, baada ya ile Hijja ya Muago, afya ya Mtume (s.a.w.) ilianza kuonyesha dalili za mfadhaiko. Miezi miwili baadae, hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi, na siku kadhaa baadae, akafa.

Pia, kama ilivyoonyeshwa kabla, Mtume (s.a.w.) aliwaambia Waislamu katika zaidi ya tukio moja kwamba hakuwa na muda mrefu zaidi wa kuishi katika dunia hii. Tabari, yule mwanahistoria, amemnukuu Abdullah ibn Abbas akisema: (kama miezi miwili baada ya ile Hija ya Muago) "Mtume wa Allah (s.w.t.) alituambia kwamba huenda angekufa ndani ya muda wa mwezi mmoja." (Ta 'rikh Tabari, juz.2, uk. 435).

Pia imesimuliwa kwamba usiku mmoja Mtume (s.a.w.) alikwenda kwenye uwanja wa makaburi ya Al-Baqi, akifuatana na mtu wa nyumbani. Baada ya kuwaombea wafu, alimwambia huyo mwenzie: "Wao (wale wafu) wako kwenye hali nzuri kuliko wale ambao wako hai. Hivi punde maovu mapya mengi sana yatatokea, na kila moja litakuwa lenye kuogofya na kutisha sana kuliko lile lililolitangulia."

Kwa upande mmoja Mtume wa Allah (s.a.w.) alikuwa akitabiri kifo chake mwenyewe, na alikuwa pia akitabiri kutokea kwa maovu mapya na kuzuka kwa vurugu mpya; na kwa upande mwingine akiwashawishi Masahaba zake kuondoka Madina na kwenda Syria!

Kuzingatia kukaribia kwa kifo chake yeye mwenyewe, ni lipi la muhimu sana kwa Mtume (s.a.w.) kufanya: kutafuta kulipiza kisasi kwa ajili ya kifo cha rafiki yake ambaye aliuawa miaka mitatu iliyopita kwenye mpaka wa mbali au kulinda Nchi ya Madina na umma wa Kiislam kutokana na hatari ambazo, alisema, zilikuwa zijitokeze karibuni?

Jibu la wazi kwa swali hili ni kwamba kama kisasi cha kifo cha Zayd kingeweza kusubiri kwa miaka mitatu, kingeweza kusubiri zaidi kidogo, na kwamba usalama wa Nchi na ule wa umma, ulikuwa ni wa muhimu zaidi sana kuliko kitu chochote kingine. Kwa hiyo,

272

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mtume (s.a.w.) alipashwa kulipanga jeshi hilo ndani ya, na kuizunguka Madina, badala ya kulituma nje ya nchi.

Lakini inaonekana kwamba Mtume (s.a.w.) mwenyewe hakuweza kukubaliana na tathmi-ni hiyo. Hakukiona chochote chenye umuhimu zaidi kuliko kutuma maswahaba zake kwenda Syria nje ya Arabia yenyewe. Alipogundua kwamba wanapuuza amri zake, akawalaani. Shahristani, yule mwanahistoria, ameandika katika kitabu chake, Kitab al-Milal wan-Nihal (uk.8): "Mtume wa Allah (s.a.w.) alisema: 'Jeshi la Usama lazima lion-doke mara moja. Allah (s.w.t.) awalaani wale watu ambao hawaendi pamoja naye.'"

Ilikuwa ni mara yake ya kwanza katika uhai wake ambapo Muhammad Mustafa, Mtume (s.a.w.) wa Rehma na aliye Rehma kwa ulimwengu wote, alipomlaani mtu yoyote. Kabla ya hili, alikuwa hajawahi kamwe kumlaani mtu yoyote - sio hata wale maadui zake wenye msimamo mkali kabisa kama Abu Jahl na Abu Sufyan. Hakuwalaani watu wa Taif pale walipompiga mawe na kumfukuza nje ya mji wao. Pia, huko nyuma, kama mtu yeyote alikuwa hawezi kwenda vitani, hakumlazimisha kwenda, na alimwacha abakie nyumbani. Lakini katika suala la jeshi la Usamah, hakutaka kusikia sababu zozote au visingizio kuto-ka kwa mtu yeyote kwa kushindwa kwake kwenda na jeshi hilo. Amri yake kwa maswahaba zake ilikuwa ni isiyobadilika, isiyoyumba na yenye mkazo.

Katika dakika za mwisho za maisha yake, mtu hupenda kwamba ndugu zake wote na marafiki wawe karibu naye. Anapenda na kutegemea kwamba baada ya kifo chake, watashiriki katika mazishi yake; watamuombea, na watailiwaza familia yake. Lakini kinyume na kanuni zote za mwenendo huu katika wakati kama huu, Muhammad Mustafa alikuwa akifanya kila aliloliweza kuwaondoa maswahaba na marafiki zake kutoka Madina. Hakumtaka yeyote kati yao kubaki pamoja naye. Waislamu wa Sunni wanadai kwamba Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Uislamu, hakuchagua mrithi wake mwenyewe, na alili-acha suala la kuchagua kiongozi wa Umma kwa maswahaba zake. Kama wako sahihi katika madai yao, basi ile amri ya Mtume (s.a.w.) kwa maswahaba kuondoka Madina na kwenda Syria, kunaleta tatizo lenye ugumu sana kwao.

Ni dhahiri kwamba Mtume (s.a.w.) alikuwa afariki. Yeye mwenyewe amesema hivyo mara kwa mara. Muda ulikuwa umewadia, kwa hiyo, kwa maswahaba zake kukusanya vichwa vyao pamoja na kutafuta sehemu mpya ya mamlaka. Lakini Mtume (s.a.w.) alikuwa ana-sisitiza kwamba waende mamia ya maili mbali na yeye - na kutoka Madina. Kama aliwata-ka wao kuchagua au kuteua mrithi wake kupitia "ushauri wao wa makubaliano," angeweza yeye kuwaamuru wao kuondoka Madina? Tena, yeye mwenyewe aliuonya umma kwamba ulikuwa unatishiwa na hatari mpya kubwa kubwa. Asingeweza kwa hiyo, kuwataka maswahaba zake kubakia Madina, na kuukinga umma kutokana na hatari hizo kubwa? Hata hivyo, ni nani angeukinga umma wa Muhammad kutokana na hatari hizo kama sio maswahaba zake wenyewe?

273

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kwa vile Mtume (s.a.w.) alijua kwamba atakufa, asingetayarisha kamwe na kuandaa jeshi la Usamah. Badala yake, angependekeza kwa maswahaba zake kwamba wanapashwa kutengeneza mkakati, kwa ushauri wa makubaliano, kuzuia yale maovu mapya na hatari ambazo tayari zimetishia kwenye upeo wa macho ya Madina.

Lakini Muhammad Mustafa hakufanya hivi. Yeye, kwa kweli, alifanya kinyume chake tu. Aliwaamuru maswahaba zake kutoka nje ya Madina, na kamwe hajawahi kuwa na mkato kwao hivyo kama alivyokuwa safari hii. Je, inaweza kuwa na maana kwamba walikuwa ni maswahaba wenyewe ambao aliwaona kama watunzi wa maovu na hatari mpya zinazo-tishia umma wake?

Kwa kweli, usalama na wokovu wa Waislamu ulilala kwenye utii wao usio na kuuliza kwenye amri za Mtume (s.a.w.) wao. Pale walipomuasi yeye, waliufungua mlango wa maovu yote, vurugu na hatari.

Katika mazingira yalimotokea matukio ya wakati huo, inaonekana kwamba Muhammad Mustafa alikuwa na sababu muhimu sana za kuchelewesha jeshi la Usamah mpaka dakika za mwisho. Alikwisha kutangaza wazi, kwa usahihi kabisa na kwa kurudia rudia kwamba Ali ibn Abi Talib atakujakuwa mrithi wake. Lakini alikuwa pia anatambua kuwepo kwa hisia za kichinichini za upinzani wa maswahaba zake kwa Ali.

Mtume (s.a.w.) pia alijua kwamba kile kikundi kilichokuwa kinampinga Ali, kilikuwa na nguvu sana na chenye hadhari sana. Kwa hiyo, aliwaza kwamba kama wakati wa kifo chake, watu wa kikundi hiki kinachozungumziwa, watakuwa nje ya Madina, yeye (Ali) atamrithi bila ya kadhia yoyote. Lengo hasa la Mtume, katika kuandaa jeshi la Usamah, kwa hiyo, lilikuwa ni kuwatuma wale watu mbali kutoka Madina, ambao wangempa Ali changamoto katika kupanda kwake kwenye kiti cha ukhalifa. Alitegemea kwamba katika kutokuwepo kwa maswahaba hapo Madina, Ali angekipanda kiti, na watakaporudi, wangemkuta yeye imara kabisa katika usimamizi wa serikali.

Jeshi la Usamah, kwa hiyo, lilikuwa ni utangulizi wa kuhamisha madaraka kutoka kwa Muhammad kwenda kwa mrithi wake, Ali ibn Abi Talib.

Lakini maswahaba hawakuwa waondoke Madina. Kule kubakia Madina, walimpinga Mtume (s.a.w.) mwenyewe, na pia walizipuuza laana zake. Walijua kwamba kama Ali mara atakapopanda kwenye hicho kiti, basi wao (maswahaba) watakuwa wamefungiwa nje ya "makasri ya madaraka" daima dumu, na walikuwa, kwa sababu hii, wazuie kupanda kwa Ali kwenye kiti hicho kwa gharama zote. Hawakuwa na nia ya kufungiwa nje ya "makasri ya madaraka"

Mambo yafuatayo yawekwe akilini na msomaji kwa ajili ya kutathmini upya kwa tukio

274

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kwenye mfululizo wa matukio ya jeshi la Usamah:

1. Vita vya Muutah vilipiganwa mnamo A.D.629. Wakati wa kiangazi cha mwaka A.D.632, mpaka wa Syria ulikuwa tulivu na shwari, na hapakuwa na tishio lolote, la kweli au la kuhisiwa, la uvamizi wa Madina kutokea kaskazini. Kwa kweli, hakukuwa hata na tetesi la shambulizi juu ya Madina au Hijazi kutoka kwa yeyote yule. Na bado, Muhammad Mustafa alikuwa akionyesha shauku kubwa ya kupeleka jeshi lake huko Syria.

2.   Jeshi la Usamah liliandaliwa, inavyoonekana, ili kurudisha hamasa ya Waislamu baada ya kushindwa kwao katika vita vya Muutah, na kuwaadhibu wale watu waliomuua baba yake, Zayd bin Haritha. Mtume (s.a.w.) alimtwisha Usamah kazi ya kulipiza kisasi kutoka kwa wauaji wa baba yake. Sasa Ja'afar bin Abi Talib, Shahidi mwenye Mbawa (at-Tair) wa Uislamu, na kaka mkubwa wa Ali, naye pia aliuawa kwenye vita hivyo hivyo. Lakini Mtume (s.a.w.) hakumtuma Ali au mtu mwingine yoyote wa ukoo wa Bani Hashim pamoja na jeshi hilo. Aliwabakisha wao wote pamo-ja naye hapo Madina.

3.   Mbali na maradhi yake makali, Mtume (s.a.w.) alikuwa akilihimiza jeshi hilo kwenda Syria. Yeye kwa hasira aliutupilia mbali ule wasiwasi uliotangazwa wa baadhi ya Masahaba zake juu ya hali yake, na akawaamuru kwenda pamoja na Usamah mara moja.

4.   Usamah bin Zayd bin Haritha alikuwa ndio mkuu wa jeshi wa wale maswahaba wa Mtume (s.a.w.) ambao walikuwa wazee wa kutosha kuwa babu zake kama vile Abu Bakr, Umar, Uthman, Abu Ubaidah bin al-Jarrah, Abdur Rahman bin Auf, na wengine wengi. Mtume (s.a.w.) kwa hiyo alikuwa akiikazia kanuni, kabla tu ya kifo chake, kwamba Waislamu wasiwe wa kumfikiria mtu kustahili uongozi kwa sababu tu alikuwa mtu mzima.

5.   Kama mtu mwenye sifa zinazostahili anakuwepo wa kuwa kiongozi, basi mtu asiye na sifa hizo asimuondoe mahali pake. Masahaba walitoa vipingamizi kwenye uongozi wa Usamah juu ya msingi huu. Mtume (s.a.w.) alikubali kwamba yule tu mwenye sifa zinazostahili ndiye anayepaswa kupewa madaraka makubwa. Lakini alisisitiza kwamba Usamah alikuwa anastahili zaidi kuliko wale watu wote walioamriwa kuwa chini yake, licha ya ujana wake mdogo.

6.   Waislamu wa Sunni wanasema kwamba Mtume (s.a.w.) "alishauriana" na maswahaba zake, na hili liliifanya serikali yake kuwa ya "kidemokrasia." Ni kweli kwamba "alishauriana" nao mara chache katika masuala madogo lakini yeye mwenyewe ali-fanya maamuzi bila kuwahusisha wao. Pale Hudaybiyah, Umar bin al-Khattab alion-

275

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

goza upinzani kwake alipokuwa akijadili masharti ya amani pamoja na wapagani. Alipuuza upinzani wake, akaendelea na kusaini mkataba nao. Baadae, mafaqihi wa Sunni walieleza kwamba Mtume (s.a.w.) alipuuza upingaji wa Umar kwa sababu alikuwa (yeye Mtume) akitenda chini ya amri ya Mbinguni. Wako sahihi. Lakini kuteuliwa kwa Usamah kama mkuu wa jeshi hakukuwa na uhusiano wowote na amri za Mbinguni na Mtume (s.a.w.) alikuwa huru kutangua amri zake wakati anapokabili-wa na upinzani kutoka kwa maswahaba. Bali alikataa hata kuzungumza nao juu ya suala hilo seuze "kutaka ushauri" wao juu ya suala hilo.

7.  Amri za Mtume (s.a.w.) kwa maswahaba zake kuwa jeshini chini ya Usamah, na kuon-doka Madina kwenda Syria, zilikuwa wazi sana. Lakini hawakuondoka Madina, na akafa. Wao, kwa hiyo, waliijua dhamiri yao ambayo ilikuwa ni kuwepo kimwili hasa pale Madina wakati wa kifo chake.

8.   Masahaba wale wa Mtume (s.a.w.) ambao aliwaamuru kupiga ripoti kikazi kwa Usamah - mkuu wao - walikuwa wakimdharau wakati alikuwa bado yu hai. Ikiwa waliweza kutojali amri zake na matakwa yake katika uhai wake, wanaweza kama kawaida, kutojali amri na matakwa yake katika suala la mrithi wake baada ya kifo chake. Waliweka tamaa na maslahi yao binafsi mbele ya amri na matakwa ya Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliyebarikiwa.

276

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Abu Bakr kama kiongozi katika Swala

Wanahistoria wa Sunni wanadai kwamba wakati Muhammad Mustafa alipokuwa hawezi kuhudhuria kwenye Swala za jamaa kwa sababu ya maradhi yake, alimuamuru Abu Bakr kuongoza Swala za jamaa, na wanalitanguliza hili kama "ushahidi" kwamba alimtaka yeye Abu Bakr kuwa ndio mrithi wake.

Kuna matoleo mbalimbali ya Hadith hii yaliyopo hadi sasa. Kwa mujibu wa mojawapo, Bilali alikuja kumuuliza Mtume (s.a.w.) kama ataongoza Swala, naye akasema: "La, mwambie Abu Bakr aongoze Swala."

Kuna toleo la pili ambamo wakati wa Swala, Mtume (s.a.w.) alimuuliza mtu mmoja, Abdullah bin Zama'a alikokuwa Abu Bakr. Ibn Zama'a alitoka nje kwenda kumwita Abu Bakr lakini hakumpata. Bali alimpata Umar, na akamwambia aongoze Swala. Lakini pale Umar alipotamka takbir (Allah-u-Akbar), Mtume (s.a.w.) alimsikia, naye akasema: "Hapana! Hapana! Allah (s.w.t.) na waumini wanakataa hiyo. Mwambie Abu Bakr aongoze Swala hiyo."

Kufuatana na Hadith ya tatu, Mtume (s.a.w.) aliwauliza wale waliokuwa karibu naye kama wakati wa Swala ulikuwa umekwishafika. Wakasema umefika, ndipo akawataka wamwambie Abu Bakr aongoze hiyo Swala ya jamaa. Lakini mkewe, Aisha, akasema kwamba baba yake alikuwa mtu mwenye huruma sana, na kama ataona nafasi yake (Mtume) pale Msikitini iko wazi, yeye (Abu Bakr) atalia sana, na hakuna atakayeweza kusikia sauti yake. Lakini Mtume (s.a.w.) alisisitiza kwamba Abu Bakr asimame kama kiongozi wa Swala.

Zipo Hadith nyingine pia kama hizi katika vitabu vya historia na maudhui yao zote ni kwamba Abu Bakr aliongoza jamaa katika Swala wakati wa siku za mwisho za Mtume (s.a.w.) duniani hapa.

Muhammad ibn Ishaq

Ibn Shihab alisema, Abdullah ibn Abu Bakr bin Abdur Rahman bin al-Harith bin Hisham aliniambia kutoka kwa baba yake kutoka kwa Abdullah bin Zama'a bin al-Aswad bin al-Muttalib bin Asad kwamba wakati Mtume (s.a.w.) alipokuwa mgonjwa sana na mimi pamoja na idadi fulani ya Waislamu tulikuwa pamoja naye, Bilali alimwita kwa ajili ya Sala, na akatuambia kuwa tumuamuru mtu maarufu aongoze hiyo Swala. Hivyo nilitoka nje na hapo alikuwepo Umar na watu, Abu Bakr hakuwe-

277

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

po pale. Nilimwambia Umar asimame na kuongoza Swala, alifanya hivyo, na alipose-ma Allah-u-Akbar, Mtume (s.a.w.) akasikia sauti yake, kwani alikuwa na sauti yenye nguvu sana, na akauliza alikokuwa Abu Bakr, akisema mara mbili zaidi, "Allah (s.w.t.) na Waislamu wanakataa hiyo," Kwa hiyo nikatumwa kwa Abu Bakr na aliku-ja baada ya Umar amekwisha maliza Swala ile naye akaongoza. Umar akaniuliza ni nini nilichokifanya hasa, akisema, "Pale uliponiambia niongoze Swala, nilidhani kwamba Mtume (s.a.w.) amekupa amri kwa jambo hilo; lakini kwa hilo nisingeweza kufanya hivyo." Nilijibu kwamba hakunituma kufanya hivyo, bali pale nilipokuwa sikuweza kumpata Abu Bakr nilidhani kwamba yeye (Umar) alikuwa anastahili zaidi ya wale waliokuwepo kuongoza Swala.

(The Life of the Messenger of God)

Yaliyopita ni maelezo ya mwanzoni kabisa yaliyopo hadi sasa ya Hadith kwamba Abu Bakr aliongoza Swala. Msimulizi wake alikuwa ni Abdullah bin Zama'a. Yeye mwenyewe anasema kwamba Mtume (s.a.w.) alimtuma yeye kumwambia mtu maarufu ambayo ina maana mtu yoyote, aongoze Swala, na hakumtaja makhsusi Abu Bakr. Hata baadae, wakati Mtume (s.a.w.) alipomkataza Umar kuongoza Swala, hakumuamuru Abu Bakr kuchukua nafasi yake. Aliuliza tu alikokuwa Abu Bakr.

Abdullah bin Zama'a alidhani kwamba Umar alikuwa ndiye "mwenye kustahili zaidi" kuongoza Swala lakini Mtume wa Allah (s.a.w.) hakukubaliana naye.

Sir William Muir

Imesimuliwa kwamba katika tukio moja Abu Bakr alitokea kutokuwepo wakati adhana ya Swala ilipopigwa na Bilali, na kwamba Umar akiwa amepokea, kama alivyoamini kimakosa, amri ya Muhammad kuongoza katika nafasi yake, alisimama pale Msikitini, na katika sauti yake nzito akaanzisha Takbir, "Mungu ni Mkubwa!" kwa matayarisho ya Swala. Muhammad akisikia hili kwa bahati tu kutoka nyumbani kwake, alikemea kwa kutumia nguvu, "Hapana! Hapana! Allah (s.w.t.) na kundi zima la waumini wanakataza hilo! Si mwingine bali Abu Bakr! Asiongoze Swala mtu mwingine bali yeye tu."

(The Life of Muhammad, London. 1877)

Kama ilivyoelezwa hapo juu, kwa mujibu wa wanahistoria wa Sunni, lengo la Mtume (s.a.w.) katika kumuamuru Abu Bakr kuongoza Swala lilikuwa ni "kumtangaza" yeye kama mrithi wake.

Inawezekana kabisa kwamba Abu Bakr aliongoza Waislamu katika Swala katika wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Ambacho, hata hivyo, kisichoelewaka ni kama alifanya hivyo kwa amri ya Mtume, au, angalau kwa idhini yake ya kimyakimya. Dai la kwamba Abu Bakr aliongoza Swala kwa amri ya Mtume (s.a.w.) linaleta maswali kwa

278

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

sababu alikuwa afisa mdogo katika jeshi la Usamah, na Mtume (s.a.w.) alikuwa amemua-muru yeye kuondoka Madina na kupiga ripoti kwa Mkuu wake wa Kikosi huko Jurf ambavyo, inavyoonekana, kamwe hakufanya hivyo.

Hata kama ikichukuliwa kwamba Mtume (s.a.w.) alimuamuru Abu Bakr kusimama kama Imamu (kiongozi wa Swala), bado haieleweki kama ni vipi ilikuwa ni "kuidhinishwa" kwa ugombea wake wa urithi. Hata hivyo, Abu Bakr mwenyewe, Umar bin al-Khattab, na Abu Ubaidah ibn al-Jarrah, wote watatu walikwisha tumika chini ya Amr bin Al-As katika vita vya Dhat es-Salasil, na waliswali Swala zao nyuma yake kwa majuma mengi tu. Amr bin Al-Aas aliliweka wazi kwao wote watatu kwamba yeye alikuwa ndiye bosi wao sio tu katika jeshi bali pia kama kiongozi katika ibada za kidini.

Kama ilivyokwisha kuelezwa, Waislamu wa Sunni wanashikilia kwamba Mtume (s.a.w.) alimchagua Abu Bakr kuongoza Swala ya jamaa kabla tu ya kufa kwake kwa sababu alim-taka yeye awe ndiye khalifa wake.

Ibn Hajar Makki, mwanahistoria wa Sunni, anasema katika kitabu chake, Tathiir al-Janan (uk.40):

"Abu Bakr aliwaongoza Waislamu katika Swala (kwa amri ya Mtume). Hii, kwa hiyo, ni ijma (makubaliano) ya wanazuoni wote kwamba ukhalifa wake ulikuwa kwa agizo la Mtume."

Lakini Masunni haohao pia wanalichukulia wazo la kwamba kuwaongoza Waislamu wengine kwenye Swala hakutunukii heshima yoyote juu ya muongozaji mwenyewe, na kwamba sio lazima kwa mtu kuwa na "sifa stahilivu" kusimama kama Imamu (kiongozi wa Swala). Kwa kuhusiana na hili, wananukuu "Hadith" ifuatayo ya Mtume wa Uislamu (s.a.w.) iliyosimuliwa na Abu Hurayra:

"Swala ni wajibu wa lazima juu yenu, na unaweza kuiswali nyuma ya mwislamu yoyote hata kama ni fasiq (hata kama anatenda madhambi makubwa)."

Kwa mujibu wa "Hadith" hii mtu fasiq (mtenda madhambi) anastahili vilevile kuwa Imam wa Swala kama mtakatifu; katika suala la kusimama kama Imam, mwenye dhambi na mtakatifu wanakuwa na usawa!

John Alden Williams

Na kuwasikiliza na kuwatii Maimam na Ma-Amirul-Mu'minin (ni lazima) - Yeyote yule aliyeupata Ukhalifa, ama awe mchaji au fisadi, ama watu walikubaliana naye na wanamfurahia au kama aliwashambulia kwa upanga mpaka akawa Khalifa na akait-

279

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

wa "Amirul-Mu'minin." Kwenda kwenye vita tukufu (jihad) kunafaa pamoja na mchaji au kamanda fisadi mpaka siku ya Qiyamah; mtu hamuachi yeye. Ugawaji wa ngawira za vita na kutoa adhabu zilizoagizwa na Sheria ni kwa Maimam. Haiwi kwa mtu yeyote kuwashutumu au kushindana nao. Kukabidhi pesa za Zaka kwao (kwa ajili ya ugawaji) inaruhusiwa na inafaa; yeyote anayewalipa wao atakuwa ametimiza wajibu wake iwe huyo Imam alikuwa mcha-mungu au fasiq. Swala ya mkusanyiko nyuma ya Imam na wale anaowaongoza ni halali na kamili; rakaa zote. Yeyote atakayezirudia ni mzushi, anayeitelekeza Hadith na kupinga Sunnah. Hakuna lazima kabisa katika Swala yake ya Ijumaa, kama haamini kuswali na Maimam, wawe wowote wale, wazuri au wabaya; iliyo Sunnah ni kuswali rakaa mbili nao na kulichukulia jambo hilo kuwa limekwisha. Katika hilo usiache shaka yoyote katika kifua chako.

(Some Essential Hanbali Doctrines from a Credal Statement in Themes of Islamic Civilization, p.31, 1971)

Kwa mujibu wa fatwa ya Hanbali iliyonukuliwa hapo juu, yeyote na kila mtu anaweza kuwaongoza Waislamu katika Swala. Abu Hurayra na Abu Sufyan wanazo sifa zinazostahili sana kuweza kuwa viongozi wa Swala kama Abu Bakr.

Dhana hii iliundwa na vizazi vya baadae vya Waislamu. Mtu mmoja ambaye hakuishiriki pamoja nao, alikuwa ni Muhammad Mustafa, Mfasiri wa Ujumbe wa Mwisho wa Allah kwa wanadamu. Alimuona Umar bin al-Khattab kuwa "hana sifa zinazostahili" kuongoza Waislamu kwenye Swala, na akamkataza kufanya hivyo.

Waislamu wa Shia wanaichukulia kama ilivyokuwa ni ya uongo, ile "Hadith" ambayo Abu Hurayra ameihusisha kwa Mtume wa Uislamu (s.a.w.) kwamba ni halali kuswali nyuma ya mtu yoyote, hata aliye fasiq. Wao wanasema kwamba Imam (kiongozi wa Swala) lazima awe:

Ni Mwislamu

Mwanaume

Mtu mzima

Mwenye akili timamu

Mkweli (Muadilifu)

Mjuzi Mtu mwenye heshima nzuri, yaani, mtu anayefahamika kuwa na tabia nzuri.

Hadithi ya kwamba Abu Bakr aliwaongoza Waislamu katika Swala katika uhai wa Mtume, ama ni ya kweli au ya uongo. Kama ni ya kweli, basi ina maana kwamba alitekeleza wajibu

280

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ambao kwa kulingana na Abu Hurayra na mafaqihi na wanachuoni wa Ki-Sunni, mtu yey-ote na kila mtu mwingine alikuwa na sifa zinazostahili kufanya, na haikumfanya yeye kuwa "maalum" kwa namna yoyote ile; kama ni ya uongo, basi ina maana kwamba hakuongoza mkutano wowote kabisa wa Sala wakati Mtume (s.a.w.) alipokuwa bado yu hai.

Lakini kama Hadith hii ni ya kweli, basi pia ina maana kwamba Swala yoyote inayoswali-wa nyuma ya Umar ibn al-Khattab, ni halali. Mtume (s.a.w.) alisema kwamba Allah (s.w.t.) Mwenyewe hakutaka Umar kusimama kama kiongozi wa Swala. Kung'ang'ania kwa Umar juu ya kuwaongoza Waislamu katika Swala, kabla au baada ya kifo cha Mtume, kusingeweza pengine kuzifanya Swala zile kuwa zisizokubalika zaidi kwa Allah (s.w.t.)!

281

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Wosia Usioandikwa wa Mtume wa Allah (s.a.w.w)

Uislamu ulikuwa ndio sababu kamili ya kuwepo kwa Muhammad Mustafa, Mtume mtuku-fu wa Allah (s.a.w.w). Alitumwa duniani hapa kuja kueneza Uislamu. Ili kusambaza ujumbe wa Uislamu, ilimbidi kupambana dhidi ya vipingamizi vigumu lakini alivishinda. Aliufanya Uislamu uweze kuwepo kwa kutumia makafara makubwa ambayo aliyatoa kwa ajili yake. Mfumo wa Uislamu na utaratibu wa manufaa yake vilikuwa kwake ni kama bus-tani ambayo ameikuza kwa damu ya wapenzi wake mwenyewe.

Ni nini kinachoweza kuwa na mantiki zaidi kuliko kufikiria kwamba Muhammad angeta-ka kuchukua hatua ambazo zingeweza kuhakikisha usalama na uhai wa Uislamu kwa wakati wote? Ni nini kingekuwa cha kawaida zaidi kwake kuliko kutaka kwamba kuona Uislamu unakuwa haudhuriki? Yeye, kwa hiyo, alifikiria juu ya kulinda maslahi ya baadae ya Uislamu, kwa kadiri ilivyokuwa kwenye mamlaka yake kufanya hivyo, kwa kuandika mirathi na wosia wake.

Hivi mwislamu anaweza kufikiria kwamba Muhammad Mustafa angeweza kupuuza wajibu muhimu kama wa kuandika mirathi kwa ajili ya umma wake? Mirathi, wosia wa Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.w) wenye kueleza kwa uwazi, utaratibu na uamuzi wake wa mwisho, amri zake kuhusiana na uhamishaji wa mamlaka kwa mrithi wake, lilikuwa ni jambo la lazima kabisa la uimarishaji wa Uislamu. Kwa hiyo, kabla tu ya kifo chake, aliwaamuru wale maswahaba waliokuwa karibu yake kumletea kalamu, karatasi na wino ili aweze kuamuru hati kwa ajili ya umma ambayo itaulinda kutokana na kupotea, na itauzuia kutokana na kugawanyika.

Lilikuwa ni ombi la maana sana la mtu aliyekuwa kwenye kitanda chake cha mauti, na ambaye angeweza kufa wakati wo wote.

Lakini alikutana na ukaidi!

Lilikuwepo kundi la maswahaba wake ambalo halikumtaka yeye aandike wosia wake. Imam Bukhari anaandika katika juzuu ya 1 ya Sahih yake: Umar akasema, 'Mtume wa Allah (s.a.w.w) amezidiwa na maumivu. Hatuhitaji wosia wowote. Tayari tunacho Kitabu cha Allah (s.w.t.) na kinatutosha Kitabu cha Allah.' (uk.25)

Bukhari ameandika tukio hilo hilo katika Juz.11 ya Sahih yake katika maneno yafuatayo:

282

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

"Mtume wa Allah (s.w.t.) akasema: 'Nileteeni kipande cha karatasi. Nitawaandikieni kitu juu yake ambacho kitawazuieni kutokana na kupotea.' Lakini wale watu waliokuwepo pale, wakaanza kubishana miongoni mwao wenyewe. Baadhi yao wakasema kwamba Mtume wa Allah (s.w.t.) alikuwa anaweweseka." (uk. 121)

Hapa Bukhari amejaribu kuficha kutambulikana kwa Umar nyuma ya pazia la maneno baadhi yao.

Lakini Sheikh Shihab-ud-Din Khaffaji, mwanahistoria wa ki-Sunni, amekosa aibu katika suala hili, na anasema:

"Umar akasema: 'Mtume wa Allah anaropoka.'"

(Nasim-ur-Riyadh, Juz. 1V, uk. 278)

Kwa mwislamu kusingizia kwamba Mtume wa Mwisho wa Allah (s.a.w.w) na Adhimu sana alikuwa "anaweweseka" ilikuwa ni kauli ya uovu kabisa na ya kizembe. Inawezekana kweli kwamba Mletaji na Mfasiri wa Ujumbe wa Mwisho wa Allah (s.a.w.w) kwa wanadamu, angeweza kuwa "mzungumzaji wa kuweweseka?" Na tena, ni kipi kili-chokuwa hakina maana au bila mantiki au la kulaumika katika ombi lake la kumuacha aandike wosia wake?

Maoni ya Umar yasiyo na sababu yalisababisha mabishano miongoni mwa wale maswa-haba ambao walikuwepo pale chumbani kwa Mtume. Wachache kati yao walisema kwamba walipaswa kumtii Bwana wao, na kumletea kalamu, karatasi na wino. Lakini wale wengine ambao walikuwa wengi, walimuunga mkono Umar na wakamnyima vile vifaa vya kuandikia. Mabishano yakawa makali sana kiasi kwamba ilimbidi Mtume (s.a.w.) kuwaamuru watoke chumbani kwake, na wamuache peke yake.

Bukhari anaandika zaidi katika Sahih yake:

"Wakati Mtume (s.a.w.) maradhi yake yalipochukua hatua mbaya, alisema, 'Nileteeni karatasi ili niweze kuwaandikieni wosia ambao utakuzuieni kutokana na kupotea baada ya kifo changu.' Umar bin al-Khattab akasema, 'Hapana. Haya ni mazungum-zo yasiyokuwa na maana. Kitabu cha Allah (s.w.t.) kinatutosha' Mtu mwingine akasema: 'Ni lazima tulete karatasi,' mpaka kukawa na mabishano, na Mtume (s.a.w.) akasema: 'Ondokeni hapa.'"

Kumdharau Mtume wa Allah (s.a.w.w) kwa Umar kumekingamiza msafara wa Mtume (s.a.w.) kwenye makundi mawili. Ilikuwa dhahiri kutoka wakati huu kwamba utengano uli-inua kichwa chake katika umma wa Kiislamu.

283

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Yumkini ilikuwa mara ya mwisho ambapo Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.w) na Mtawala wa Waislamu, alieleza haja yoyote mbele ya maswahaba zake. Lakini walimdha-rau. Alishituka lakini pengine hakushangazwa na ukaidi wao. Haikuwa ni mara ya kwan-za kumfanyia ukaidi yeye. Jeshi la Usamah liliwafichua.

Sir William Muir

Wakati huu, akimtambua Umar, na watu wengine maarufu mle chumbani, yeye Muhammad alisema kwa sauti: 'Nileteeni hapa wino na karatasi, ili niweze kuwaandikieni maandishi yatakayokuzuieni msipotee daima.' Umar akasema, 'Anaweweseka huyo. Kwani Qur'an haitutoshi sisi?'

(The Life of Muhammad, London, 1877)

Muhammad Husein Haykal

Akiwa bado yuko kwenye mashambulizi makali ya homa, na amezungukwa na wageni, Muhammad aliomba kwamba aletewa kalamu na wino na karatasi. Alisema kwamba angetoa imla ya kitu kwa faida ya wafuasi wake, akiwahakikishia wao kwamba kama watashikamana nacho, hawatapotea kamwe. Baadhi ya watu waliokuwepo walifikiri kwamba kwa vile Mtume - Rehema na amani ziwe juu yake - alikuwa mgonjwa sana na kwa vile Waislamu tayari walikuwa wanayo Qur'an, hakuna maandishi zaidi yaliyokuwa na lazima. Imesimuliwa kwamba wazo hilo lilikuwa ni la Umar. Watu waliokuwepo pale wakahitilafiana miongoni mwao wenyewe, wengine wakitaka kuleta vifaa vya kuandikia na kuandika kile Mtume (s.a.w.) atakacho amuru, na wengine wakidhani kwamba maandishi yoyote ya ziada mbali na yale ya Kitabu cha Allah (s.w.t.) yatakuwa yamezidi kiasi. Muhammad akawaambia waondoke, akisema, 'Msigombane mbele yangu.' Ibn Abbas alihofia kwamba Muhammad anaweza kupoteza kitu muhimu kama hawakumletea vile vifaa vya kuandikia lakini Umar alisimama imara kwenye uamuzi wake ambao aliuege-meza juu ya maneno ya Allah (s.w.t.) Mwenyewe ndani ya Kitabu Chake: "Ndani ya Kitabu, Hatukuacha kitu chochote."

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Katika makala yenye kichwa cha Iqbal and Islamic Polity, iliyochapishwa katika toleo la mwezi wa April 1964 la gazeti la kila mwezi la Muslim News International, la Karachi, Pakistani, mwandishi, Jamilud-Din Ahmad anasema:

"...Swali linalozikabili nchi za Kiislamu ni, kama sheria ya Kiislamu ina uwezo wa mabadiliko - swali ambalo litahitaji juhudi kubwa za kisomi na lina uhakika wa kujibiwa kwa kukubali; alimradi ulimwengu wa Kiislamu ukabiliane nalo katika msi-mamo wa Umar - akili ya kwanza ya ukosoaji na huru katika Uislamu, ambaye, kati-

284

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ka dakika za mwisho za Mtume, alikuwa na moyo kuthubutu kutamka maneno haya ya ajabu: 'Kinatutosha Kitabu cha Allah (s.w.t.)'"

Mwandishi aliyetajwa hapo juu inavyoonekana anajivunia sana "moyo wa kijasiri" wa Umar.

Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.w) alikuwa kwenye kitanda cha mauti yake, na huen-da hakuwa na masaa mengi ya kuishi. Ilikuwa ni wakati huu ambapo Umar alichagua kuonyesha moyo wake wa kijasiri. Pale Hudaybiyya, Muhammad Mustafa alimtuma kupeleka ujumbe kwa Maquraishi huko Makka lakini alikataa kwenda kwa kutoa dharura kwamba kwa vile hakuna hata mtu mmoja katika mji ule wa kumlinda yeye, wangemuua. Pia wakati Mkataba wa Hudaybiyya ulipotiwa saini, Umar aliongozwa, na "mapenzi" yake juu ya Uislamu kumkaidi Mtume wa Allah (s.a.w.w) na sasa wakati Mtume (s.a.w.) alipokuwa anakufa, "mapenzi" yale yale yakajithibitisha kwa mara nyingine tena, na yakamlazimisha yeye kumzuia Mtume (s.a.w.) kuamuru maandishi yoyote ambayo "yangedhoofisha mamlaka ya Kitabu cha Allah (s.w.t.)!"

Kama Umar alichochewa kumkaidi Muhammad Mustafa kwa sababu hii, basi ina maana yeye Umar aliamini kwamba Muhammad alikuwa ayape changamoto mamlaka ya Qur'an. Lakini Umar alijuaje kwamba Muhammad angeyapa changamoto mamlaka ya Qur'an? Kama Mtume (s.a.w.) angekuwa ameamuru kuandikwa kwa wosia ule, maneno yake machache ya mwanzo yangeonyesha, bila ya shaka yoyote, kama alikuwa, kwa maneno ya Umar, "anaweweseka" na alikuwa "anaropoka"

Labda haikuingia akilini mwa Jamilud-Din Ahmad kwamba Umar alikuwa anapambanisha akili yake ya "ukosoaji na yenye kujitegemea" dhidi ya Qur'an Tukufu ambayo inasema: Imeagizwa, mmoja wenu anapofikiwa na mauti, Kama akiacha mali, afanye wosia kwa wazazi wake na jamaa zake, kwa namna nzuri inayopendeza. Ni wajibu haya kwa wacha-mungu. (Sura ya 2; Ay a ya 180)

Lakini inawezekana kwamba Umar alichochewa kutomtii Mtume (s.a.w.) sio kwa woga wake kwamba Mtume, katika dakika zake za mwisho za maisha yake, angetangua kazi aliyoifanya katika uhai wake, kwa kupuuza mamlaka ya Qur'an; bali kwa dhana yake kwamba yeye Mtume (s.a.w.) angeweka kwa maandishi kile alichokisema mapema kule Ghadir-Khum mbele ya mkusanyiko wa mahujaji, akimteua Ali ibn Abi Talib kama mrithi wake. Umar alikuwa amzuie bila kujali gharama. Wosia uliobeba muhuri na saini ya Mtume, unaomtaja Ali kama mkuu wa baadae wa Dola la Kiislam utakuwa ni hati ambayo itauweka ukhalifa mbali na wagombea wengine wote wa ukhalifa huo. Mtume (s.a.w.) alifahamu fika kuhusu nia za maswahaba wake wakuu kuhusiana na urithi wa Ali kama kiongozi mkuu wa utawala wa Kiislamu. Vile alivyoendelea kuwa mnyonge wa dhahiri, waliendelea kuonekana kuwa washupavu zaidi katika kumkaidi yeye. Jeshi la

285

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Usamah bado lilikuwa limening'iniza moto. Katika kuchukia kabisa, Mtume (s.a.w.) aliomba laana ya Allah (s.w.t.) juu ya wale watu ambao hawakupiga ripoti kikazi kwa Usamah lakini hawakusogea. Na walikuwa hawakushituka kabisa wakati walipowaambia watoke nje ya chumba chake.

Mwislamu wa siku hizi anaweza kuona ni jambo la ajabu sana kwamba sahaba yeyote wa Mtume wa Uislamu anaweza kuhusisha amri zake na "kuweweseka." Lakini upo ulingan-isho wa ki-Qur'an kwa tabia kama hiyo. Inaonekana kwamba wale maswahaba wa Muhammad, Mtume wa Waarabu, waliosema kwamba alikuwa "anaweweseka," walikuwa na watangulizi wao wenyewe katika ndugu zake Yusuf, Mtume wa Bani-Israil. Ndugu zake Yusuf walisema kwamba Yakoub, baba yao ambaye pia alikuwa Mtume, alikuwa "anaweweseka." Walidhani kwamba wao ndio walikuwa "watanashati" ambapo yeye hakuwa. Qur'an imewanukuu kama ifuatavyo:

Usahihi-36.jpg

Pale waliposema: "Hakika Yusufu na nduguye wanapendwa sana na baba yetu kuliko sisi: Hali sisi ni kikundi chenye nguvu! Hakika baba yetu yumo katika upotofu wa dhahiri. (kich-wani mwake) Muueni Yusufu au mtupeni nchi ya mbali (isiyojulikana), Ili uso wa baba yenu ukueleekeeni ninyi. (na kutakuwa na muda wa kutosha) Na baada ya haya mtakuwa watu wema. (Sura ya 12; Aya ya 8 na 9)

Maoni ya Mtarjuma - (wa Kiingereza)

Wale ndugu kumi sio tu waliwaonea wivu na kuwachukia ndugu zao wadogo Yusufu na Bin-yamin (Benjamin). Walimdharau na kumfedhehesha baba yao kama mjinga asiye na akili - katika upungufu wake wa akili kutokana na uzee. Kwa kweli Yakoub alikuwa na busara ya kuona kwamba watoto wake wadogo na wasio na makosa wal-itaka ulinzi na kufahamu umashuhuri wa kiroho wa Yusufu. Lakini busara yake, kwao ilikuwa ni upumbavu au wenda wazimu au upunguani, kwa sababu iligusa mapenzi-binafsi yao, kama ukweli mara nyingi unavyofanya. Na walitegemea mabavu ya idadi yao - ndugu kumi vibonge dhidi ya mzee Yakoub, kijana Yusufu, na mtoto Bin-yamin.

(A. Yusufu Ali)

286

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kuelezea mstari wa mwisho wa Aya ya pili, iliyonukuliwa hapo juu, mfasiri anaendelea kusema kwamba:

Wao (ndugu zake Yusufu) wanasema kwa kejeli, "Kwanza tumuondoe Yusufu. Itakuwa ni muda wa kutosha kisha tujifanye kuwa 'wema' kama yeye, au tutubie uovu wetu baada ya kuwa tumepata manufaa yake yote katika vitu vya kimaada."

Hapa mwanafunzi wa historia anaweza akauliza swali: Kwa nini Muhammad asiamuru kuandikwa wosia wake baadae, baada ya kushindwa kwake kwa awali; kwa kweli, zilikuwepo nyakati ambapo maswahaba walikusanyika tena kumuona yeye, na angeweza kuwasomea wosia wake wakati huo.

Tunaweza kuchukulia kwamba Muhammad angeweza kuamuru kuandikwa wosia wake katika muda wa baadae lakini ni nini kilichokuwepo cha kumzuia Umar na wafuasi wake kudai kwamba uliamriwa katika hali ya "kuweweseka" na ulikuwa "wa kipuuzi," na ulikuwa, kwa hiyo, usiokubalika kwa umma. Muhammad alikuwa hajasikia chochote kibaya zaidi tangu zama za Abu Jahl, na alikuwa hana hamu ya kulisikia tena, hususan akiwa yuko kwenye kitanda cha mauti yake. Yeye, kwa hiyo, aliliacha kabisa jambo hilo.

Hila ya Umar ingefanya kazi hata kama Muhammad angeamuru kuandikwa kwa wosia wake. Kuiongeza ufanisi tabia ya Umar, watetezi wake wanasema kwamba dini ilikuwa imekamilishwa na kutimilishwa, na wosia, kwa hiyo, haukuwa na lazima. Ni kweli kwamba dini ilikuwa imekamilika na kutimia lakini haikuwa na maana kwamba na umma ulikuwa timilifu, na kwamba ungeweza kuachana na mwongozo kwa vile haukuwa kwenye hatari yoyote ya kukengeuka kutoka kwenye njia ya Haki. Umma ungeweza kupo-toka kutoka kwenye unyofu, na umefanya hivyo. Vita vyote vya wenyewe kwa wenyewe, mifarakano na utengano katika Uislamu, vilisababishwa na upotofu.

Kwa umma kuthibitisha kwamba wosia kama ule haukuwa lazima, ni kujitwalia madaraka makubwa sana wenyewe. Ulipaswa kuliacha jambo hili kwenye uamuzi wa mtu ambaye Allah (s.w.t.) amemchagua kuwa Mtume Wake kwa wanadamu. Yeye peke yake ndiye ali-jua kama wosia ulikuwa na lazima au la. Ni haki gani waliyonayo umma ya kuzuia uhuru wa kutenda wa Mwakilishi wa Allah (s.a.w.) kwenye dunia hii?

Ukaidi wa Umar kwa Muhammad, ambapo Muhammad alikuwa tayari yuko kwenye mlan-go wa mauti, ni moja kati ya matukio ya kutisha sana katika historia ya Uislamu, na haku-na kiwango cha upendezeshaji cha wanahistoria kinachoweza kuliondoa kijanja. Tukio hilo hilo lilikuwa pia ndio utangulizi wa makabiliano yaliyopatikana baina ya maswahaba na watu wa nyumba yake Mtume.

287

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Wake zake Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.w.t)

MKE WA KWANZA WA MUHAMMAD ALIKUWA NI KHADIJA. Walioana huko Makka na wakaishi kwa robo karne ya mapenzi na furaha pamoja - mpaka kifo chake. Wakati Khadija alipokuwa hai, Muhammad hakuoa mwanamke mwingine.

Baada ya kifo cha Khadija, Muhammad akaoa wanawake wengi wengine lakini hakuna mmoja kati yao ambaye angeweza kamwe kuchukua nafasi ile ile katika moyo wake kama aliyokuwa nayo Khadija. Wakati alipokufa, ile furaha yake kamili, ya maisha ya ndoa, pia iliondoka pamoja naye. Mpaka mwisho wa maisha yake, alikumbuka mengi juu yake, na akamkumbuka kwa mapenzi, upendo na shukrani.

Mwanamke wa kwanza Muhammad aliyemuoa baada ya kifo cha Khadija, alikuwa ni Sawdah binti Zama'a, mjane ambaye mumewe alikufa huko Abyssinia.

Mke wa tatu wa Mtume (s.a.w.) alikuwa ni Aisha, binti ya Abu Bakr. inasemekana kaole-wa huko Makka lakini alikwenda nyumbani kwa mumewe huko Madina.

Mtume (s.a.w.) mara nyingi alijaribu kupata mahusiano mema na ukoo au kabila kwa kuoa mmoja wa wanawake zake. Kumuoa kwake Ummu Habiba binti ya Abu Sufyan, na Safiya binti ya Akhtab, kulikuwa ni ndoa kama hizo.

Mmoja wa wake za Mtume (s.a.w.) alikuwa ni Hafsa binti ya Umar ibn al-Khattab. Mumewe aliuawa katika vita vya Badri, na baba yake alikuwa na shauku ya mume mpya kwa ajili yake. Alimposesha kwa marafiki zake wa moyoni, kwanza kwa Uthman bin Affan, na kisha kwa Abu Bakr. Wote walisikitikia kukosa uwezo kwao wa kumuoa.

Umar alidhalilika kwa kule kukataliwa kwa binti yake hata na marafiki zake mwenyewe, na akalalamika kwa Mtume (s.a.w.) kuhusu hilo. Mtume, ili kutuliza uchungu wa moyo wa Umar, akasema kwamba madhali hakuna mtu mwingine aliyemtaka binti yake, yeye atam-chukua harimu yake mwenyewe.

Ukimuacha Khadija, wake wengine wote wa Mtume (s.a.w.) walibakia bila mtoto. Gavana wa Misri alikuwa amemtumia mtumwa wa kike Mkibti aliyeitwa Maria. Aliingia kwenye harimu yake, na akamzalia mtoto wa kiume ambaye alimwita Ibrahim.

Kuzaliwa kwa mtoto wa kiume kulimpa Maria umuhimu wa kipekee, kwenye maudhi

288

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

makubwa na uchungu wa mioyo wa wake wenzie. Mtume (s.a.w.) alitoa mapenzi makub-wa juu ya kijana mdogo huyo, na alitumia masaa mengi pamoja naye, akimbeba mikononi mwake. Lakini kwa bahati mbaya, kijana huyo hakuishi muda mrefu, na akafa katika mwaka ule wa kuzaliwa kwake.

D. S. Margoliouth

Miaka yake (Muhammad) ya mwisho ilichangamshwa na kwa muda kwa kuzaliwa kwa mtoto wa kiume na kimada/suria wake (sic - hili sio kweli) wa ki-Kibti - Maria, ambaye alimkubali kama ni wake, na ambaye alimwita kwa jina la muasisi wa kud-haniwa (sic - japo si kweli) wa dini yake, Ibrahim. Kimada/suria huyo (sic) akiwa ni chanzo cha wivu mkali wa wake zake wengi wasiokuwa na watoto, tukio hili la bahati liliwasababishia uchungu wa moyo mkali sana; ambao kwa kweli ulipunguzwa kwa haraka na kifo cha mtoto huyo (ambaye aliishi kwa miezi kumi na moja tu).

(Muhammad and the Rise of Islam, London, 1931) Muhammad Husein Haykal

Kwa kuzaa mtoto, hadhi ya Maria ilipanda katika taadhima ya Muhammad; yeye sasa alimuona kama mke huru, hasa, anayefurahia nafasi yenye fadhila kubwa.

Ilikuwa ni kawaida kwamba mabadiliko haya yangechochea sio wivu kidogo mion-goni mwa wake zake wengine waliokuwa wagumba. Ilikuwa ni kawaida pia kwamba heshima na upendo wa Mtume (s.a.w.) kwa mtoto huyo aliyezaliwa na mama yake viliongezea wivu huo. Zaidi ya hayo, Muhammad kwa ukarimu kabisa alimzawadia Salma, mke wa Abu Rafi, kwa jukumu lake kama mkunga. Alisherehekea uzazi huo kwa kutoa kipima cha nafaka kwa mafukara wote wa Madina. Alimkabidhi huyu mtoto aliyezaliwa hivi karibuni kwenye malezi ya Ummu Sayf, mama wa kunyonye-sha, ambaye alikuwa akimiliki mbuzi saba, ambao maziwa yake alikuwa Ayaweke kwenye haki ya matumizi ya huyu mtoto mchanga. Kila siku Muhammad alitembe-lea nyumba ya Maria ili akaone ule uso mwangavu wa mwanae na kujihakikishia yeye mwenyewe maendeleo ya afya ya mtoto huyo na ukuaji wake. Yote hii ili-chochea wivu mkali miongoni mwa wake zake wagumba. Swali lilikuwa, ni kwa muda mrefu kiasi gani wake zake hawa wangekuwa na uwezo wa kuvumilia mateso Haya ya kila siku.

Siku moja, pamoja na tabia za fahari ya mababa wapya, Mtume (s.a.w.) aliingia chumbani kwa Aisha pamoja na yule mtoto mikononi mwake, ili amuonyeshe kwa Aisha. Alimuonyesha yeye kufanana kwake kukubwa na mwanae. Aisha akamtazama yule mtoto na akasema kwamba hakuona kufanana kokote kule. Wakati Mtume

289

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

(s.a.w.) aliposema jinsi mtoto anavyokua, Aisha akajibu kwa chukichuki kwamba mtoto yeyote akipewa kiwango cha maziwa kama alichokuwa anapewa yeye angekua na ukubwa tu na mwenye nguvu kama yeye. Kwa kweli, kuzaliwa kwa Ibrahim kulileta maumivu mengi sana kwa wake za Mtume (s.a.w.) kiasi kwamba wengine wao wangekwenda kwa majibu makali zaidi ya haya na sawa na haya. Ilifikia kiasi kwamba Wahy wenyewe ulilazimika kutamka shutuma maalum. Bila shaka, jambo zima liliacha chapa katika maisha ya Mtume (s.a.w.) na vilevile katika historia ya Uislamu

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Wakati mmoja, Hafsa anasemekana kuwa "alimshitukiza" mumewe akiwa na Maria, na akaieleza "siri" hii kwa Aisha. Wake wengine wa Mtume (s.a.w.) waliisikia habari hii kuto-ka kwa Aisha. Kulikuwa na umbeya mwingi na uropokaji kuhusu tukio hili. Hatimae, Qur'an Tukufu ilibidi iingilie kati kwa karipio kwa mabibi wawili hao katika Aya ifuatayo:

Usahihi-37.jpg

"Kama ninyi wawili hamkutubia kwa Allah, basi nyoyo zenu zimekwisha kuelekea huko; laki-ni kama mtasaidiana dhidi yake (Mtume), hakika Allah ndiye mlinzi wake,na Jibrilu, na wau-mini wema na zaidi ya hayo, Malaika pia watamsaidia." (Sura ya 66; Aya ya 4)

Maelezo ya Mfasiri

"Nyumba ya Mtume (s.a.w.) haikuwa sawa na nyumba zingine. Wake bora wa Mtume (s.a.w.) walitegemewa kuwa na tabia njema ya hali ya juu na ukimya kuliko wanawake wa kawaida, kwani walikuwa na kazi ya hali ya juu ya kutekeleza. Lakini walikuwa binadamu hata hivyo, na walikuwa wenye kupatwa na udhaifu wa jinsia yao, na wakati mwingine walishindwa."

"Ujinga wa Aisha wakati mmoja ulisababisha matatizo magumu sana: akili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) ilipata uchungu sana, na aliacha ujamaa na wake zake kwa muda fulani. Binti ya Umar, Hafsa, alikuwa pia wakati mwingine mwepesi wa kutu-mia vibaya nafasi yake, na pale wawili hawa walipoungana katika ushauri wa kisiri, na kuzungumzia mambo na kupeana siri, walisababisha huzuni kubwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w)."

(A.Yusufu Ali)

Wengi wa wafasiri na watarjuma wa Qur'an wamelitafsiri neno la Kiarabu Saghat linalo-tokea kwenye Aya ya 4 ya Sura ya 66, iliyonukuliwa hapo juu, kama "kuelekea." Tarjuma yao inasomeka kama ifuatavyo:

290

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mioyo yenu imekwisha kuelekea.

Kuelekea kwenye nini? "Mioyo yenu imekwisha kuelekea," ni tafsiri isiyo na maana kati-ka muktadha huu. Tafsiri sahihi ya neno Saghat ni "imepotoka," M. Abul Ala Mauduudi ametoa tafsiri sahihi ya Aya hii ambayo ni kama ifuatavyo:

"Kama nyie (wanawake) wote mtatubia kwa Allah, (ni bora kwenu), kwani mioyo yenu imepotoka kutoka kwenye njia ya haki, na kama mtasaidiana dhidi ya Mtume, basi mjue kwamba Allah ndiye Mlinzi wake, na baada Yake ni Jibril na waumini wema na Malaika ndio wenzake na walinzi wake..."

(Tafhiim-ul-Qur'an, Juz. 6, Lahore, Pakistani, tarjuma ya Kiingereza ya Muhammad Akbar Muradpuri na Abdul Aziz Kamal, chapa ya pili, Mei 1987)

Wakati Hafsa "alipomshitukiza" Muhammad akiwa pamoja na Maria, alipaswa ati kutoa ahadi kwa Hafsa kwamba yeye hatakutana Maria tena. Hili, kwa kweli, limekatazwa. Mke mmoja hakuwa na haki kuzuia uhuru wa mumewe kukutana na wake zake wengine. Jaribio kama hilo kwa upande wa mke mmoja lingekuwa kinyume sio tu na sheria za Kiislamu bali pia na desturi za Arabia, wakati wote, kabla na baada ya Uislamu.

Sir William Muir

Katika suala la Zainabu, Muhammad (s.a.w.) alitoa ujumbe kutoka Mbinguni ambao ulikataza ahadi yake ya kutengana na Maria, ukamkemea Hafsa na Aisha kwa ukaidi wao, na ukadokezea juu uwezekano wa wake zake wote kuachwa kwa mwenendo wa uasi sana kwake mwenyewe. Kisha akajiondoa kwenye ujamaa nao, na kwa mwezi mzima akaishi peke yake pamoja na Maria. Umar na Abu Bakr walifedheheka sana kwa kutengwa kwa mabinti zao kwa ajili ya kimada duni (ingawa sio kweli) na wakahuzunikia umbeya wa mwenendo mzima.

(The Life of Muhammad, London, 1877)

Kutoka kwenye hayo yaliyotangulia inaweza kuonekana kwamba maisha ya nyumbani ya Mtume (s.a.w.), baada ya kifo cha Khadija, hayakuonyesha ufasaha wowote. Wengi wa wake zake walikuwa ni wanawake wenye wivu, na "ajali" ya kwanza ya wivu wao ilikuwa ni amani ya nyumba yake.

D. S. Margoliouth

Kukaa kwa wake katika harimu ya Mtume (s.a.w.) kulikuwa kufupi, kutokana na kutostahili kwa tabia; katika moja au zaidi ya masuala, wale wageni walifundishwa na wale wake za Mtume (s.a.w.) wenye wivu kanuni ambazo, walipozitamka bila

291

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kujua maana, zilimfanya Mtume (s.a.w.) kuwafukuza papo hapo. Mmoja alifukuzwa kwa kutangaza katika kufa kwa yule mtoto mchanga Ibrahim kwamba baba yake angekuwa ni Mtume, asingeweza kufa - matumizi ya ajabu ya uwezo wa fikira..

(Muhammad and the Rise of Islam, London, 1931)

Ilikuwa ni mazoea ya Mtume (s.a.w.), mara kwa mara, kuondoka nyumbani kwake usiku na kwenda kutembelea makaburi ya Baqii kuwaombea marehemu waliozikwa pale. Kabla tu ya maradhi yake ya mwisho, aliyatembelea makaburi hayo mara nyingine tena, labda kwa mara ya mwisho, na akakaa hapo na kuwaombea marehemu hao mpaka usiku wa manane. Baadhi ya wanahistoria wanasema kwamba ilikuwa ni katika safari hii kwamba alipatwa na homa ya baridi, na ilikuwa ndio mwanzo wa maradhi yake makali. Aisha anasemekana kumfuata katika moja ya safari hizi.

D. S. Margoliouth

Wakati wa usiku wa manane, inavyosemekana, Mtume (s.a.w.) alikwenda kwenye uwanja wa makaburi unaoitwa al-Baqii, na akaomba msamaha kwa ajili ya wale marehemu waliozikwa pale. Hili kwa hakika alilifanya hapo kabla; Aisha safari moja alimfuata yeye kama mpelelezi alipotoka wakati wa usiku, kwa kumdhania yeye kwamba amedhamiria mapenzi fulani; lakini alikokuwa akienda, aligundua, ilikuwa ni makaburini. (kutoka Musnad ya Imam Ahmad Hanbal, juz. Iv, uk. 221).

(Muhammad and the Rise of Islam, London, 1931)

Wanawake aliowaoa Mtume (s.a.w.) baada ya kifo cha Khadija, walikuwa tofauti sana na yeye (Khadija) kwa tabia na mwenendo. Khadija alikuwa amempa mumewe msaada thabiti na usio na mbwembwe katika uenezaji wa Uislamu, na alijitolea muhanga utajiri wake wote mkubwa kwa ajili ya lengo hilo. Kujitolea muhanga kwake kulimshusha mpaka kwenye hali ya ufukara lakini hakulalamika kwa mumewe kuhusu kukosa kitu chochote. Ndoa yake ilikuwa na utajiri katika baraka za upendo na urafiki wa mumewe, na katika furaha isiyo na kikomo.

Muhammad Mustafa mwenyewe aliishi maisha ya kawaida kabisa. Hata pale alipokuwa ndio mtawala wa Arabia nzima, alikuwa bado ni mwenye kujihini kama alivyokuwa huko Makka kabla ya kuhama kwake kwenda Madina. Aisha mwenyewe anasema hana kum-bukumbu kama mumewe aliwahi kula chakula cha ridhaa ya moyo wake mara mbili kwa siku moja.

Wakati ngawira za vita au mapato ya dola yalipokuja, Mtume (s.a.w.) aliyagawanya mion-goni mwa Waislamu. Wake zake waligundua kwamba hata wale wanawake masikini kabisa hapo Madina walikuwa kwa hivyo wakawa matajiri lakini sio wao. Ilijitokeza kwao

292

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kwamba hawakupaswa wakoseshwe ukarimu mkubwa wa mume wao. Hata hivyo, wao hawakuzoea kuishi maisha ya kujihini kiasi hicho kama alivyokuwa yeye. Walilijadili suala hili miongoni mwao wao wenyewe, na wote wakakubaliana kwamba walipaswa kupata sehemu katika vile vitu vizuri na halali - sawa na wale wanawake wengine wa Madina.

Wake za Mtume, kwa hiyo, wakawasilisha madai yao kwake. Walikuwa na kauli moja katika kudai posho kubwa ya kujikimu kutoka kwake. Wawili wao, yaani, Aisha na Hafsa, wal-isimama kama "wazungumzaji" wao. Walipokuwa wakisisitiza madai yao kwake, Abu Bakr na Umar wakaja kumuona Mtume (s.a.w.) kwa shughuli fulani za kibinafsi au za

umma.

Mtume (s.a.w.) alikaa kimya, akiwa amezungukwa na wake zake. Pale Abu Bakr na Umar walipogundua yale yanayopikwa, walikasirika sana, na wakawalaumu kwa ukali kabisa mabinti zao kwa kudai pesa zaidi kutoka kwa mume wao.

Muhammad Husein Haykal

Abu Bakr alimuinukia binti yake Aisha na kumvuta nywele zake na vivyo hivyo Umar akamfanyia binti yake, Hafsa. Wote Abu Bakr na Umar wakawaambia binti zao: "Mnathubutu kumuomba Mtume wa Allah (s.a.w.) kile ambacho hawezi kumudu kukitoa?" Wao wakajibu: "Hapana, Wallahi hatumuombi yeye kitu kama hicho."

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Hatimae jambo hilo lilikomeshwa pale iliposhushwa Aya mpya kwa sababu hii, na ambayo inasomeka kama ifuatavyo:

Usahihi-38.jpg

Ewe Mtume! Waambie wake zako: "Ikiwa mnataka maisha ya dunia hii na mapambo yake, basi njooni, nitakulipeni kitokea nyumba, na kukuacheni kwa njia nzuri. Na ikiwa mnampenda Allah na Mtume Wake, na nyumba ya Akhera, Basi Allah amewaandalia wafanyao mema, miongoni mwenu, malipo makubwa. (Sura ya 33; Aya ya 28 na 29)

293

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Maelezo ya Mfasiri:-

Nafasi ya wake za Mtume (s.a.w.) haikuwa sawa na ile ya wake wa kawaida. Walikuwa na kazi na wajibu maalum... wake wote katika nafasi yao ya juu walipaswa kufanya kazi na kusaidia kama akina-mama wa umma. Yao hayakuwa ni maisha ya kutulia, kama yale ya masuria, ama kwa anasa zao wenyewe au anasa za mume wao. Wanaambiwa hapa kwamba walikuwa na sehemu katika Kaya Tukufu (ya Mtume) kama walipenda starehe na mapambo ya dunia tu. Kama hali ilikuwa ni hiyo, wangeweza kuachwa na kukimiwa vya kutosha, na zaidi.

(A.Yusufu Ali)

Qur'an Tukufu iliwapa nafasi wake za Mtume, yaani, ama walikuwa wamchague Allah (s.w.t.) na Mtume Wake (s.a.w.), na kuishi maisha ya kujinyima na kujitoa muhanga; au wangeweza kuchagua anasa, starehe na mapambo ya dunia hii ambavyo kwa suala hilo ingewalazimu kuachana na mume wao daima. Fursa hiyo ilikuwa ya dhahiri, na wake hao walikuwa na uhuru wa kuchagua.

Aisha, Hafsa na mabibi wengine saba walilitafakari jambo hilo, na kisha wakaamua kusamehe burudani na starehe za dunia hii, na kubaki katika nyumba ya Mtume (s.a.w.) kama wake zake.

Wakati Muhammad Mustafa (rehema na amani juu yake na Ahlul-Bait wake) alipokufa mwaka 632, alikuwa na wake tisa katika harimu yake. Aisha aliishi kwa nusu karne baada yake, na mke aliyeishi zaidi ya wake wengine wa Mtume, alikuwa ni Maimuna. Yeye, ilivyokuwa, alikuwa ndiye mwanamke wa mwisho aliyemuoa.

294

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kifo cha Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.w.t.)

MALENGO YA MAISHA YA MUHAMMAD MUSTAFA (s.a.w.), kama Mtume wa Mwisho wa Allah (s.w.t.) katika dunia hii yalikuwa:

•   Kuangamiza ibada ya masanamu na ushirikina;

•   Kutangaza rasmi Tauhidi ya Muumba;

•   Kufikisha Ujumbe wa Muumba kwa wanadamu;

•   Kukamilisha mfumo wa dini na sheria;

•   Kutakasa nafsi za wanaume na wanawake;

•   Kukomesha dhulma, uovu na ujinga;

•   Kuanzisha mfumo wa amani pamoja na haki;

•   Kuunda chombo katika namna ya hali ya kisiasa kwa ajili ya utambuzi wa malengo hayo yote yaliyopita, na chombo ambacho kitadumisha mwendo wa kazi yake.

Ndani ya ile miaka 23 ya kazi yake kama Mtume wa Allah, Muhammad (s.a.w.) alikuwa amefanikisha malengo yote Haya, na kisha ilianza kuonekana kama ilivyo kwa wanadamu wengine wote, yeye pia ilimbidui aondoke kwenye dunia hii. Kama ilivyoelezwa hapo kabla, alipokea taarifa hii kwa mara ya kwanza pale Suratun-Nasr (msaada), Sura ya 110 ya Qur'an Tukufu, iliyonukuliwa mapema katika kitabu hiki, iliposhushwa kwake.

Muhammad Mustafa alitumia maisha yake yote katika Swala na ucha-mungu lakini baada ya kuteremshwa kwa Nasr kuzama kwake katika kumuabudu Muumba wake kukawa kukubwa zaidi kuliko hapo kabla, katika kujiandaa kukutana Naye.

Mtume (s.a.w.) mwenyewe alidokeza, angalau katika matukio haya mawili kwamba kifo chake hakikuwa mbali sana naye:

1. Katika hotuba yake ya Hij a ya Muago pale Arafat siku ya Ijumaa, mwezi 9 Dhil-Hajj, mwaka wa 10 H.A., alisema: "Labda, hii ndio Hija yangu ya

295

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

mwisho." Katika kumalizia hotuba yake, aliuliza swali kwa mahujaji, yaani, "Mtakapoulizwa na Mola wenu kuhusu kazi yangu, majibu yenu yatakuwa yapi?" Mahujaji wakajibu kwa sauti moja: "Ulifikisha ujumbe wa Allah (s.w.t.) kwetu, na ulitimiza wajibu wako." Alipolisikia jibu hili, alitazama kuelekea Mbinguni, na akasema: "Ewe Allah! kuwa shahidi kwamba nimetekeleza wajibu wangu."

2. Wakati wa "kutawazwa" kwa Ali ibn Abi Talib pale Ghadir-Khumm, mnamo mwezi 18 Dhil-Hajj, 10 H.A., Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.a.w.w) alizungumzia tena kifo chake kilichokuwa kinakaribia kwa kusema: "Mimi pia ni mwanadamu, na ninaweza kuitwa mbele ya Mola wangu wakati wowote."

Makumi ya maelfu ya Waislamu waliyasikia matangazo haya ya Mtume wao (s.a.w.), na wote walijua kwamba hatakuwa nao kwa muda mrefu zaidi. Yeye mwenyewe alijua kwamba alikuwa amekamilisha kazi yake ambayo Mola wake alimkabidhi, na alikuwa, kwa hiyo, na shauku ya kukutana Naye.

Mtume (s.a.w.) alitumia nyakati zake za kila usiku pamoja na wake zake mbalimbali kwa zamu. Mnamo mwezi 19 Safar ya mwaka wa 11 H.A., ilikuwa ni zamu yake kulala kwenye chumba cha Aisha. Usiku, alitembelea viwanja vya makaburi vya Baqii akiwa pamoja na mtumishi wake, Abu Muwayhiba, ambaye baadae alisimulia kwamba:

"Mtume (s.a.w.) alisimama katikati ya makaburi na akayahutubia kwa maneno yafu-atayo: 'Amani iwe juu yenu ninyi mlioko kwenye makaburi haya. Mumebarikiwa katika hali yenu ya sasa ambamo mmejitokeza kutokea kwenye hali ambamo watu wanaishi katika dunia. Mashambulizi ya kuangamiza yanashuka moja baada ya jingine kama mawimbi ya giza, kila moja bay a zaidi ya yale yaliyotangulia.'"

Muhammad Husein Haykal anasema kwamba yale maradhi "makali" ya Mtume (s.a.w.) yalianza asubuhi iliyofuatia ule usiku ambao alitembelea uwanja wa makaburi, yaani, mnamo mwezi 20 Safar. Yeye anaendelea kusema:

Ilikuwa ni hapo kwamba watu waliingiwa na wasiwasi na lile jeshi la Usamah halikuondoka. Kweli, ile Hadith ya Abu Muwayhibah inatiliwa shaka na wanahisto-ria wengi ambao wanaamini kwamba maradhi ya Muhammad (s.a.w.) yasingeweza kuwa ndio sababu pekee ambayo ilizuia hilo jeshi kutoondoka kwenda al-Sham, kwamba sababu nyingine ilikuwa ni kule kutoridhika kwa wengi, pamoja na idadi ya Muhajirina wakubwa na Ansari, kuhusiana na uongozi wa jeshi hilo.

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

296

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Tukio lifuatalo linaelekea kuwa limetokea asubuhi ya mwezi 20 ya Safar:

Sir William Muir

Usiku mmoja Mtume (s.a.w.) alitembelea kwenye viwanja vya makaburi nje ya viun-ga vya mji. Huko alichukua muda mrefu akiwa amezama katika tafakari na kuwaombea marehemu. Wakati wa asubuhi, akipita kwenye mlango wa Aisha, ambaye alikuwa anaugua kutokana na maumivu makali ya kichwa, alimsikia aki-lalamika (kupiga kite): kichwa changu! oh, kichwa changu! Akaingi ndani na akase-ma: "Hapana, Aisha, kwa hakika mimi ndio ningekuwa na haja ya kulia - kichwa changu kichwa changu!" Kisha kwa mwelekeo wa upole: "Lakini usingependa wewe kuchukuliwa wakati nikiwa bado hai; ili niweze kukuswalia wewe, na kukusetiri wewe, Aisha, katika sanda yako, hivyo nikupeleke wewe kaburini?"

"Hilo litokee kwa mwingine," alimaka Aisha, "na sio kwangu mimi!" kimzaha akaongeza: "Ah, hilo ndilo unalolitaka wewe! Hakika, naweza kukuota wewe, baada ya kwisha kunifanyia yote haya na kunizika mimi, unarudi moja kwa moja nyumbani kwangu, na kutumia jioni hiyo hiyo kwa kucheza mahali pangu na mke mwingine!"

Mtume (s.a.w.) akatabasamu kwa mzaha wa Aisha, lakini maradhi yalizidi kumsonga kwa nguvu kuweza kutoa jibu katika mwelekeo huo huo.

(The Life of Muhammad, London, 1877) Betty Kelen

Yeye (Mtume) aliomba usiku kucha (kwenye makaburi ya Baqii) na akarudi nyumbani kwake, akiingia kwenye nyumba ya Aisha, ambaye alikuwa anaumwa na kichwa, na alipomuona Mtume (s.a.w.) alikunja uso wake na akasema, "Oh! kichwa changu!"

"Hapana, Aisha," alisema Mtume (s.a.w.), "ni oh! kichwa changu mimi!" Akaketi chini kwa nguvu, kichwa chake kikimgonga, maumivu yakibana viungo vyake muhimu, sasa akasema: "Hivi inakuhuzunisha kujifikiria wewe mwenyewe kufa kabla yangu, ili kwamba niweze kukusetiri kwenye sanda na kukuzika wewe?"

Alikuwa anaonekana kama mgonjwa wa kufa, lakini Aisha, ambaye aliamini kwamba alikuwa kwa hali yoyote ile amefika mwisho wa njia yake ya ndoa za kidiploma-sia, alimpa jibu la kisirani: "Hapana. Kwa sababu naweza pia kufikiria kuja kwako wewe moja kwa moja kutoka makaburini kusherehekea usiku wa harusi."

(Muhammad, The Messenger of God)

297

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Muhammad Husein Haykal

Asubuhi iliyofuata, Muhammad (s.a.w.) alimkuta Aisha, mke wake, akilalamikia maumivu ya kichwa, na akiwa ameshikilia kichwa chake kati ya mikono miwili, huku akiugulia, "oh! kichwa changu!" Yeye mwenyewe akiwa na maumvu ya kichwa, Muhammad (s.a.w.) alijibu, "Lakini hasa, Ewe Aisha, ni kichwa changu mimi!" Hata hivyo, maumivu hayakuwa makali sana kiasi cha kumlaza kitandani, kumzuia kazi zake za kila siku, au kumzuia yeye kuongea na wake zake na hata kutaniana nao. Aisha alivyoendelea kulalamika kuhusu kichwa chake, Muhammad (s.a.w.) alimwambia: "Haitakuwa vibaya hata hivyo, Ewe Aisha, kama ingekuwa ufe kabla yangu mimi. Kwani nitaweza hapo kukuswalia na kuhudhuria mazishi yako." Lakini hili liliamsha tu harara za Aisha mwenye ujana, ambaye alijibu: "Wacha hayo yawe majaaliwa mema ya mtu mwingine na sio mimi. Kama hilo litanitokea mimi, utakuwa una wake zako wengine utakaokuwa pamoja nao."

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Mtume (s.a.w.) hakutoa jibu lolote kwa dhihaka ya Aisha, na akaegemea kwenye ukuta. Pale maumivu yalipopungua, alinyanyuka na akawatembelea wake zake wengine kama alivyokuwa akifanya siku zote. Siku ya mwezi 24 Safar, alikuwa kwenye nyumba ya mke wake, Maimuna, alipopata shambulizi la ghafla la maumivu makali ya kichwa na homa. Inasemekana kwamba aliwaita wake zake wote na akawaomba wamhudumie kwenye chumba cha Aisha. Walikubali kufanya hivyo.

Mtume (s.a.w.) alikuwa amechoka sana kiasi cha kushindwa kutembea mwenyewe. Kwa hiyo, Ali alimsaidia kwa upande mmoja, na Abbas, ami yake, upande mwingine, na wal-imsindikiza kutoka kwenye chumba cha Maimuna kwenda kwenye chumba cha Aisha. Alikaa kwenye chumba cha Aisha mpaka kifo chake siku chache baadae.

Lakini licha ya homa na udhaifu wake, Mtume (s.a.w.) alikwenda Msikitini kila mara alipoweza, na akawaongoza Waislamu kwenye Swala. Siku ya mwezi 26 Safar, anase-mekana kujisikia vizuri kidogo, na alikwenda Msikitini akisaidiwa na Ali na Abbas. Aliongoza Swala ya zuhr, na baada ya Swala, akaongea na mkusanyiko wa waumini.

Hii ilikuwa ndio hotuba ya mwisho ya Mtume wa Uislamu, na ndani yake alitoa dokezo moja zaidi lililifichikana la kifo chake kilichokuwa kinakaribia. Wanahistoria wa Sunni wanasema kwamba Abu Bakr ambaye alikuwepo katika hadhara hiyo, alielewa kile Mtume (s.a.w.) alichokisema, na akaanza kulia kwani alikuwa na moyo wa huruma sana. Mtume (s.a.w.) alimwona akilia na akajaribu kumliwaza, na kisha akigeukia ule mkusanyiko, akasema:

298

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

"Namshukuru sana Abu Bakr zaidi kuliko mtu mwingine yoyote kwa msaada wake wa hali na mali, na kwa usuhuba wake. Kama katika umma huu, ingekuwa kamwe nichague mtu kama rafiki, ningeweza kumchagua yeye. Lakini sio lazima kwa sababu udugu wa Kiislamu ni kifungu imara zaidi kuliko kingine, na kinatutosha sisi sote. Na kumbukeni kwamba milango yote inayofungukia Msikitini, lazima ifungwe isipokuwa mlango wa nyumba ya Abu Bakr."

Mtume (s.a.w.) aliwaonya Waislamu wasije wakarudia kwenye kuabudu masanamu, na kukumbuka kwamba wao walikuwa wenye kumuabudu Mungu Mmoja, na akaongeza:

"Kitu kimoja ambacho kamwe msije mkakifanya, ni kuabudu kaburi langu. Yale mataifa ya siku zilizopita ambayo yaliabudu makaburi ya mitume yao, walipatwa na ghadhabu ya Mola, na waliangamizwa. Jihadharini, msije mkawafuata wao."

Mapema siku hiyo ilitolewa taarifa kwa Mtume (s.a.w.) kwamba Ma-Ansari walikuwa na huzuni kubwa sana kwa sababu ya maradhi yake. Ulikuwa, kwahiyo wakati muafaka wa kuwaambia Muhajirina kuhusu Ma-Ansari na huduma yao kubwa kwa Uislamu. Akasema:

"Msije mkasahau hata mara moja kile walichokufanyieni Ansari. Wamekupeni makazi na hifadhi. Walichangia nyumba zao na mkate wao pamoja nanyi. Ingawa hawakuwa matajiri, walitanguliza mahitaji yenu mbele kuliko yao. Wao ni 'wakfia' wangu kwenu. Watu wengine wataongezeka kwa idadi lakini wao watapungua tu. Yote yaliyokuwa wajibu kwa Ansari, wameyatimiza kwa uaminifu kabisa, na sasa ni zamu yenu kutimiza wajibu wenu kwao."

Ansari pia walikuwepo mle ndani ya Msikiti, na walikuwa wakijaribu kuzuia vilio vyao vya kikweukweu. Akiongea nao, Mtume (s.a.w.) akasema:

"Enyi Ansari! Baada ya kifo changu mtakabiliwa na huzuni nyingi na matatizo."

Wakamuuliza: "Ewe Mtume wa Allah! una ushauri gani kwetu? Itatupasa tufanyeje zitakapofika hizo nyakati ngumu?"

Yeye akasema: "Msiache ustahimilivu wenu, na wekeni imani zenu kwa Allah (s.w.t.) wakati wote."

Ule msafara wa kijeshi wa kwenda Syria bado ulikuwa umesimama. Mtume (s.a.w.) ali-washutumu maswahaba zake kwa kutojali maadili kwao katika kupiga ripoti kikazi kwa jenerali wao, na akawaamuru kwa mara nyingine kuondoka hapo mjini papo hapo. Alikatisha kuongea kwa muda kidogo, na kisha akaomba laana ya Allah (s.w.t.) juu ya watu wale wote watakaodharau amri yake ya kwenda Syria.

299

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hotuba yake ikaisha. Mtume (s.a.w.) alishuka kwenye mimbari na kurudi chumbani kwake. Alijihisi kuzimia kutokana na ile juhudi ya kuongea, na hakwenda pale Msikitini tena. Ilikuwa ndio mara ya mwisho kuonekana hadharani.

Sehemu ya kwanza ya hotuba yake ambayo inahusiana na Abu Bakr, inaelekea ni ya uongo, na inaonekana kuwa imeongezwa. Kama ilivyokwisha kuonyeshwa, Abu Bakr alikuwa chini ya amri ya kujiunga na jeshi la Usamah lakini inawezekana kwamba Mtume (s.a.w.) alipuuza kushindwa kwake kuripoti kikazi. Mtume (s.a.w.) anaweza pia kuwa ali-tambua mchango wake wa mali kwa Uislamu. Aliwakomboa watumwa wengi huko Makka, na alitoa mali yake yote kuandaa msafara wa Tabuk.

Hadithi ya kwamba Mtume (s.a.w.) aliamuru milango yote iliyokuwa ndani ya Msikiti ifungwe isipokuwa mlango wa chumba cha Abu Bakr, ni Hadith ya kubuni ya dhahiri pia. Abu Bakr aliishi katika kitongoji cha Madina kilichokuwa kikiitwa Sunh. Hakuwa akiishi hapo mjini, na hakuwa na chumba ambacho mlango wake ulifungukia Msikitini.

Mtume (s.a.w.) pia alisema katika hotuba yake kwamba kama ingekuwa amchague mtu yoyote kuwa rafiki, angemchagua Abu Bakr.

Kama hotuba hii vile ilivyosimuliwa, ni sahihi, basi ina maana kwamba Mtume (s.a.w.) ali-tangaza hadharani kwamba hakutaka kumfanya Abu Bakr kuwa rafiki. Kama kauli yake itafafanuliwa, itasomeka hivi: "Kama ingekuwa nichague rafiki, ningemchagua Abu Bakr. Lakini sitamchagua. Sisi wote ni wahusika wa udugu wa Kiislam wa ulimwengu mzima, na hilo linatutosha sisi sote."

Hata hivyo, kulikuwepo na nini cha kumzuia Muhammad Mustafa kumchagua Abu Bakr kama rafiki? Hakuna! Malaika Mkuu Jibril hakuja kutoka mbinguni kumwambia asimch-ague Abu Bakr kama rafiki, wala hakuwepo yeyote duniani hapa aliyetishia kumfanyia madhara yoyote kama angemchagua yeye (Abu Bakr) kuwa rafiki.

Kwa vile huku kulikuwa ni kuonekana kwa mara ya mwisho hadharani kwa Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.a.w.w) na kwa vile, kwa mujibu ya madai ya Sunni, alimpen-da sana Abu Bakr, alipaswa kuitumia nafasi hii, sio tu kwa kumtangaza yeye kama rafiki bali pia na kumtangaza yeye kama khalifa (mrithi) wake. Kama angefanya hivyo, angeweza mtu yoyote kumpinga? Lakini kwa sababu moja au nyingi za ajabu, hakufanya hili wala lile. (Muhammad hakumchagua Abu Bakr kama rafiki wala hakumfanya yeye kuwa mrithi wake). "Mapenzi" yake kwa Abu Bakr yalipaswa kupata maelezo, lakini hayakupata; "kukosekana" kwa ajabu sana kwa upande wake katika wakati muhimu kabisa.

300

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Tarehe 27 ya Safar, Mtume (s.a.w.) alijihisi mnyonge sana kuweza kusimama na kuswali. Wanahistoria wa Sunni wanasema kwamba ilikuwa ni kuanzia tarehe hii kwamba alimua-muru Abu Bakr kuongoza Waislamu katika Sala. Yeye mwenyewe, wanasema, alibakia amekaa na akafanya vitendo vya Swala.

Bukhari, mkusanyaji wa Hadithi (maneno ya Mtume), anasimulia tukio lifuatalo katika Sahih yake:

"Mnamo mwezi 28 Safar, Abbas ibn Abdul Muttalib alikuja kumuona Ali, na akase ma: 'Wallahi, Muhammad karibuni atakufa. Ninaweza kulijua hilo kutokana na kuonekana kwa nyuso za watoto wa Abdul Muttalib wanapotaka kufa. Mimi, kwa hiyo, nashauri kwamba uzungumze naye na umuulize yeye kuhusu suala la urithi (ushikamakamu) wake.' Lakini Ali akasema: 'Hapana. Sio katika hali aliyonayo sasa hivi. Mimi sipendi kulileta suala hilo."

Wanahistoria wa Kishia wanaikataa kabisa "Hadith" hii. Wao wanasema kwamba Mtume (s.a.w.) alikuwa ametangaza, sio mara moja, bali mara nyingi tu kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi wake na mtawala wa Waislamu wote. Kama Waarabu hawakuwa wamkubali kama bwana wao hata baada ya matangazo mengi, tangazo moja zaidi lingekuwa vigumu kuweza kufanya mabadiliko. Mtume, kwa kweli, alifanya jaribio la kuandika wosia wake pale alipoitisha kalamu, karatasi na wino lakini alikutana na dharau. Na Ali hakutaka mtu yoyote aonyeshe "moyo wake wa kujasiri" kwa kukemea kwamba Mtume wa Allah (s.a.w.w) alikuwa "akiropoka." Kusikia hiyo kauli ya tusi kungeweza tu kuharakisha kifo cha bwana wake kutokana na mshituko.

Kama Hadith hii ni ya kweli, inaelekeza tu kwenye upendo wa Ali kwa bwana wake, na kupenda kusaidia kwake kumkinga kutokana na kila mshituko.

Waislamu wa Kishia pia wanasema kwamba Abbas mwenyewe angeweza kulichukua suala hilo la kujadili na Mtume (s.a.w.) ambaye alikuwa ni mpwa wake. Mtume (s.a.w.) alikuwa mchangamfu, na mwenye kuweza kufikiwa hata na wageni. Kulikuweko na nini, kwa hiyo, kwa Abbas, cha kuwa na mashaka nacho?

Masahaba waliweza kuona kwamba Mtume (s.a.w.) hatapona kutokana na homa yake na maumivu ya kichwa. Mara alipokuwa amezuiliwa kwenye kitanda cha mauti yake, wengi wao walijihisi kwamba walikuwa "salama" kama wangeacha kumtii yeye. Kwa hiyo, lolote alilofanya katika kuwashinikiza wao katika kwenda Syria, wao hawakwenda, na msafara wa Usamah kamwe haukutimizwa - katika uhai wake!

Wakati wa mchana, Muhammad Mustafa alimwita Ali, na akamwambia: "Kwangu mimi ni mwisho wa safari. Nitakapokufa, wewe uoshe mwili wangu, uuvishe sanda, na uushushe

301

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kaburini. Ninadaiwa pesa na watu fulani na fulani, miongoni mwao Myahudi mmoja alin-ipa mkopo wa kutayarishia jeshi la Usamah. Lipa madeni haya kwao wote pamoja na huyo Myahudi." Kisha akaivua pete aliyokuwa amevaa, akampa Ali, na akamuomba aivae ambapo aliivaa. Na pia alimpa yeye (Ali) upanga wake, mkuki, deraya na silaha nyingine-zo.

Jumatatu, Rabi al-Awwal 1, 11 H.A.

Jumatatu, mwezi 1 Rabi al-Awwal ya 11Hijiria ilikuwa ndio siku ya mwisho ya Muhammad ibn Abdullah (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.w.t.) katika dunia hii. Kulikuwa na nyakati ambapo alijisikia nafuu kidogo lakini wakati mwingine, alikuwa dhahiri kwenye maumivu makali. Aisha, mke wake, anasimulia ifuatavyo:

"Jinsi siku ilivyosogea kuelekea mchana, Fatima Zahra, binti yake Mtume wa Allah (s.a.w.w) alikuja kumuona Mtume. Alimkaribisha na kumwambia akae kandoni mwake. Kisha akamwambia kitu ambacho sikuweza kusikia lakini alianza kulia. Alipoyaona machozi ya binti yake, alimwambia kitu kingine ambacho pia sikuweza kusikia lakini yeye alianza kutabasamu. Yeye alifanana sana na baba yake katika mwenendo, tabia na Sura."

Muda baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.), Aisha alimuuliza Fatima ni kitu gani ambacho baba yake alimwambia yeye ambacho kwanza kilimfanya alie na kisha kikamfanya atabasamu.

Fatima akasema: "Kwanza baba yangu aliniambia kwamba alikuwa anakaribia kufa. Nilipolisikia hili, nilianza kulia. Kisha akanijulisha kwamba mimi ndio nitakayekuwa wa kwanza kabisa kukutana naye huko mbinguni, nalo pia, ni hivi karibuni tu. Nilipolisikia hili, nilifurahi sana, na nikatabasamu."

Washington Irving

Mtoto pekee wa Muhammad aliyekuwa amebakia, Fatima, mke wa Ali, alikuja sasa kumuona yeye Muhammad. Aisha alizoea kusema kwamba hajawahi kumuona mtu yoyote anayefanana na Mtume (s.a.w.) zaidi katika uzuri wa moyo kama huyu binti yake. Alimshuhulikia siku zote kwa upendo wa heshima. Alipokuja kwake, alizoea kusimama, kumfuata, kumshika mkono na kuubusu, na humkalisha kwenye sehemu yake mwenyewe Mtume. Kukutana kwao katika safari hii kunasimuliwa hivyo na Aisha, katika Hadith zilizohifadhiwa na Abulfida.

"Karibu mwanangu," alisema Mtume, na akamfanya akae karibu naye. Kisha akanong'ona kitu fulani katika sikio lake, ambacho kwacho alilia. Katika kutambua huzuni yake, alinong'ona kitu kingine zaidi, na sura yake ikan'gara kwa furaha.

302

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

"Hii ina maana gani?" nilimuuliza Fatima. "Mtume (s.a.w.) anakuheshimu wewe kwa dalili ya mategemeo ambayo hajayaonyesha juu ya yeyote kati ya wake zake." "Siwezi kutoa siri ya Mtume wa Allah (s.a.w.w)" alijibu Fatima. Hata hivyo, baada ya kifo chake, alisema kwamba kwanza alimtangazia kifo chake kilichokuwa kinakaribia; lakini alipomwona yeye analia alimtuliza kwa kumhakikishia kwamba angemfuata baada ya muda mfupi na kuwa Malkia wa peponi."

(The Life of Muhammad)

Kuelekea mchana ule Mtume (s.a.w.) alikuwa na hali ya kutotulia. Aliulowesha uso wake mara kwa mara kwa maji baridi kutoka kwenye gudulia lililokuwa karibu yake. Alipomuona katika maumivu kama hayo, Fatima alilia: "Oh mateso ya baba yangu!" Mtume (s.a.w.) alijaribu tena kumliwaza, na akasema: "Baada ya siku hii ya leo, baba yako hatakuwepo kwenye mateso tena." Na akaongeza: "Wakati nikifa, sema, "Sisi wote ni wa Allah na Kwake ndio marejeo yetu."

Sasa, kupumua kwake kukawa sio kwa kawaida, na alisikika akinong'ona kitu. Ibn Saad anasema katika Tabaqaat yake kwamba Mtume (s.a.w.) alikuwa akisema: "Ninachokitafuta sasa ni kuwa pamoja na Allah (s.w.t.)" Haya yalikuwa ndio maneno yake ya mwisho.

Muhammad (s.a.w.) alisikika akiyarudia maneno haya mara tatu, na kisha akanyamaza kimya - daima! Muhammad, Mtume wa Mwisho wa Allah (s.a.w.w) kwenye dunia hii, akafariki.

Aisha anasema: "Niliweka mto chini ya kichwa chake, na nikafunika kichwa chake na shuka. Kisha nikasimama pamoja na wanawake wengine, na wote tukaanza kulia, tukipi-ga vifua na vichwa vyetu, na kujipiga makofi kwenye nyuso zetu."

Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.w.t.) alifariki siku ya Jumatatu ya kwanza ya Rabi al-Awwal ya mwaka wa kumi na moja Hijiria wakati wa mchana. Alikuwa ameishi kwa miaka 63 iliyopungua siku nane tu.

Wanahistoria wa Ki-Sunni wanasema kwamba Mtume (s.a.w.) alifariki, sio kwenye tarehe mosi bali mnamo tarehe 12 Rabi al-Awwal. Waislamu wa Shia wanasema kwamba alifariki, sio kwenye mwezi mosi ya Rabi al-Awwal bali siku moja mapema zaidi, yaani mwezi 28 Safar.

Makubaliano ya wanahistoria wa kisasa wa Magharibi, ni kwamba, Mtume (s.a.w.) alifariki mnamo tarehe 8 Juni, 632. Tarehe nane ya Juni, kwa bahati, pia ndio siku ya kuzaliwa kwake.

303

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mazishi ya Mtume (s.a.w.)

Mwili wa Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.) ulioshwa siku ya Jumanne. Ni watu sita tu waliokuwapo kwenye huduma hii ya mazishi. Nao walikuwa ni:

Ali ibn Abi Talib

Abbas ibn Abdul Muttalib

Fadhl ibn Abbas

Qathm ibn Abbas

Usamah ibn Zayd bin Haritha

Aus bin Khuli Ansari

Usamah, mkuu wa jeshi la kwenda Syria, alikuwa yuko Jurf, akiwa bado anawangojea maswahaba. Baadhi yao walimpelekea habari kwamba Mtume (s.a.w.) alikuwa anafariki, na kwamba angepaswa arudi Madina. Alirudi, na muda kidogo baadae, bwana wake aka-fariki.

Ali aliuosha mwili wa Mtume (s.a.w.) wakati Usamah akiwa anammwagia maji. Wakati mwili ulipokwaisha kuoshwa, Ali aliufunika na sanda, na akauswalia. Kisha yeye akatoka nje, na akawaambia Waislamu waliokuwa ndani ya Msikiti, waende chumbani na kuswali Swala ya maiti. Bani Hashim walikuwa wa kwanza kumswalia, na kisha Muhajirina na Ansari wakatekeleza wajibu huu.

Hapo Madina, palikuwa na wachimba-kaburi wawili. Walikuwa ni Abu Ubaida bin al-Jarrah na Abu Talha Zayd bin Sahl. Waliitwa wote lakini ni huyu wa mwisho tu ndiye aliyepatikana. Alikuja na akalichimba kaburi. Ali aliingia mle kaburini ili kulisawazisha vizuri. Kisha akaunyanyua mwili kutoka pale chini, na akauteremsha taratibu ndani ya kaburi, akisaidiwa na ami yake na binamu zake. Kaburi kisha likafunikwa kwa udongo, na Ali akanyunyizia maji juu yake.

Wakati Ali na watu wengine wa Bani Hashim walipokuwa wanashuhulika na mazishi ya Mtume wa Uislamu (s.a.w.), Abu Bakr, Umar, Abu Ubaidah bin al-Jarrah, na wengineo, walikuwa wanashughulika huko Saqifah wakicheza bahati na sibu ya madai ya ukhalifa. Abu Bakr, ilivyotokea, alikuwa ndiye mgombea aliyeshinda. Alipokuwa amepokea viapo vya utii vya Ansari hapo Saqifah, yeye na marafiki zake walirudi kwenye Msikiti wa Mtume (s.a.w.w.). Ndipo akapanda kwenye minmbari ya Mtume (s.a.w.) kupokea viapo kama hivyo kutoka kwa watu wengine. Siku ya Jumatatu jioni, na kutwa nzima ya Jumanne, watu walikuwa wanakuja Msikitini kuchukua kiapo cha utii kwake. Kuchukua kiapo kulikwisha baadae sana usiku wa Jumanne, na ilikuwa ni Jumatano tu ambapo huyu khalifa mpya alipopata muda wa kugeuzia mawazo yake kwa bwana wake aliyekwisha fariki, na kufanya Swala ya maiti kaburini pake.

304

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.a.w.) kiongozi wa Waislamu wote, na Rehma kuu ya wanadamu, hakupata mazishi ya kitaifa. Kiasi kidogo tu cha watu - ndugu zake wa karibu - walimfanyia mazishi. Wengi wa wale waliodai kwamba walikuwa ni maswahaba na rafiki zake, walimtelekeza wakati wa saa yake ya kufa. Kutokuwepo kwao kwenye mazishi yake kulikuwa ndio kuvurugika kukubwa kabisa kwa mipango kwenye mazishi yake.

Ibn Saad anasema katika Tabaqaat yake kwamba Ali ibn Abi Talib aliyalipa madeni yote ya Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Uislamu. Alimtuma mpiga-mbiu mjini kote Madina, na wakati wa msimu wa Hijja, alituma mpiga-mbiu huko Makka, kutangaza kwamba yeye Ali angelipa madeni yote ya Muhammad (s.a.w.), na kwamba yeyote ambaye alikuwa na madai, aende kwake kulipwa. Aliwalipa wadai bila ya kuwauliza maswali yoyote na bila ya kutaka uthibitisho kwamba Muhammad (s.a.w.) alikuwa anadaiwa na wao kitu cho-chote, na hili alikuwa akilifanya mpaka mwisho wa siku zake.

305

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hisia za Familia na za Masahaba wa

Muhammad Mustafa (s.a.w.)

juu ya Kifo chake

WATU WA FAMILIA YA MUHAMMAD MUSTAFA (s.a.w.) walikuwa wamesongwa na wimbi kubwa la huzuni kwa kifo chake. Binti yake, Fatima Zahrah, alikuwa ndiye "Nuru ya macho yake." Lakini sasa macho yale yalikuwa yamefumbwa daima; yasingeweza kum-salimia yeye na watoto wake tena. Wala asingeweza kusikia kutoka midomoni mwake ile sauti ya upendo na upole ikimkaribisha nyumbani; walinyamazishwa daima. Kwake yeye alikuwa ni baba, ni "mama," Malaika mlezi, na Rehma ya Allah (s.w.t.) juu ya ardhi. Kwake yeye, alikuwa ndio kitovu cha uhai wenyewe.

Kwa Muhammad (s.a.w.), binti yake, Fatima, na familia yake, walikuwa ndio mfano hal-isi wa mapenzi yake yote, upendo wake, shangwe zake na furaha zake. Alimradi wakati alipokuwa hai, alimtendea kwa heshima kubwa mno, na alimuonyesha tofauti ambayo inastahili tu kwa Malkia. Lakini kwake yeye, alikuwa ni zaidi kabisa kuliko malkia. Kati ya watu wote aliowajua yeye Mtume (s.a.w.) yeye (Fatima) alikuwa wa kwanza na wa mbele kabisa katika moyo wake.

Sasa Fatima alikuwa na haja moja tu - kukutana na baba yake huko mbinguni. Aliitambua haja hii mapema - majuma kumi tu baada ya kifo chake. Kifo chake (Fatima) kilimuacha mume wake na watoto wake kuvumilia sio moja bali huzuni mbili.

Hasan na Husein (a.s) walikuwa ni wajukuu wa Muhammad Mustafa (s.a.w.). Walikuwa ni vipenzi vyake. Walikaa mapajani mwake wakati alipokuwa yuko Msikitini au nyumbani, na walipanda mabegani mwake alipokuwa akitembea nje. Mapaja yake yalikuwa ndio "pepo" yao, na mabega yake yalikuwa ndio "vipando" vyao. Sasa ile "pepo" na "vipando" vilikuwa vimewapotea daima. Macho yao, yakiwa na utando wa machozi, yalimsaka bila mafanikio, babu yao mpendwa kila mahali. Mimbari yake na baraza ya Msikiti wake vilikuwa sasa viko tupu, na kuta zake nzio zenyewe zilionekana kuwa katika maombole-zo. Msikiti wake ulikuwa kama koa ambamo lulu yake imekwisha toka. Vilio vya maom-boleza na malalamiko ya watoto hawa wadogo wawili vilirudi kutoka kwenye kuta za Msikiti wake katika mwangwi wenye majonzi.

Watoto wote wawili waliingiliwa na hisia ngeni, zisizoeleweka na za wasiwasi, na wal-ishikwa na hofu zisizo yakini na zisizotajika. Walikuwa ni wadogo sana kuweza kupam-banua hisia hizi au kuelewa hofu hizi; lakini hata hivyo walihisi hiyo hisia mpya ya kukosa usalama ambayo iliwasumbua wao wote. Kwa mara ya kwanza katika miaka michache

306

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

waliyoishi, waliwindwa na hali isiyo na usalama. Babu yao alikuwa, kwao wao, ni dalili na ishara ya usalama, na sasa alikuwa ameondoka.

Kwa Ali, kifo cha Muhammad (s.a.w.) kilikuwa ni msiba mkubwa katika maisha. Dunia yake ilikuwa imemzunguka Muhammad (s.a.w.) tangu alipozaliwa. Muhammad (s.a.w.w) alikuwa ndio kitovu na mzingo wa dunia yake. Kutoka kwenye dunia ile, Muhammad alikuwa ametoweka, na sasa Ali hakujua namna atakavyoishughulikia. Alijihisi kama ame-funguliwa kutoka kwenye minyororo yake, na maisha ghafla yalionekana kupoteza sababu yake ya kuwepo, kwa ajili yake yeye.

Ali alikuwa ndio roho ya Uislamu. Tabia yake ilikuwa adhimu sana na haiba yake ilikuwa haiwezi kulinganishikika. Lakini alikuwa ametegemea juu ya Muhammad (s.a.w.) awe kama kichocheo cha roho na haiba yake kukua. Alikuwa na kila sifa ya uwezekano ambao ulimfanya yeye kuwa wa muhimu sana kwa Uislamu lakini zimechukua ustadi wa ajabu wa Muhammad (s.a.w.) kuzifanya zijulikane.

Na sasa wakati akiwa na umri wa miaka 32, wakati akiwa kwenye ujana wa maisha yake, wakati akiwa kwenye ufanisi wa nguvu zake, na wakati akiwa angeweza kutoa zaidi kwa Uislamu na kwa dunia yote, zaidi kuliko alivyokwishatoa, Muhammad (s.a.w.) akafariki. Kifo cha Muhammad (s.a.w.) kilikuwa ni kipingamizi kwa Ali ambacho hakuweza kukom-boka kutokana nacho kwa maisha yake yote yaliyobakia.

Hisia za Fatima Zahrah, Hasan, Husein na Ali (a.s), kwa kifo cha Muhammad (s.a.w.) zilikuwa za kawaida na za kutibika. Wote watano waliunda jamii ya familia, iliyoungan-ishwa katika mapenzi yao, na utii wao kwa Allah (s.w.t.), Muhammad (s.a.w.) alikuwa ndio "mhimili" wa jamii hii ndogo. Kwa kifo chake, "jamii" hii ilivunjika, ikiwaacha watu wengine wa familia hiyo wakiwa wamekanganyikiwa kabisa. Labda hawakujua kwa wakati ule, ingawa walikuwa waje kujua punde tu, kwamba kifo cha Muhammad (s.a.w.) kimeashiria tu mlolongo mzima wa mishtuko na huzuni mpya kwao. Tokea hapo na kuen-delea, walikuwa wawe kwenye hali ya "kuzingirwa" na huzuni. Kila siku mpya ilikuwa ilete mshituko mpya, na huzuni mpya. Lakini kwa kupitia msukosuko huu wa majanga na misiba, imani yao katika rehema za Allah (s.w.t.) na katika ushindi bora wa haki na ukweli, ulibakia imara kama jiwe, na ya kudumu. Matumaini yao ya kupata radhi za Allah (s.w.t.) yalizidi kuongezeka nguvu zaidi daima kwa kila wimbi jipya la mshituko na huzuni.

Ili kuhimili mshituko wa kifo cha Muhammad (s.a.w.), watu wa familia yake walitafuta na kupata msaada kutoka kwenye kile Chanzo Kimoja ambacho hakishindwi kamwe - Rehma za Allah (s.w.t.) zisizo na mipaka.

307

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kifo cha Muhammad Mustafa (s.a.w.) na Umma wake

Waislamu waliwajibika kwa Muhammad (s.a.w.) kwa kiapo cha namna mbili; kwanza katika wadhifa wake kama Mtume wa Allah (s.w.t.); na pili katika wadhifa wake kama Mtawala wa Arabia. Hakuna ambaye angeweza kuzuia uwajibikaji na utiifu kwake katika wadhifa wowote ule, na akabakia kuwa bado ni mwislamu.

Katika mwenendo wake kama Mtume wa Allah (s.w.t.) Muhammad (s.a.w.) amewapatia wokovu kutoka kwenye fedheha ya kuabudu masanamu, na alikuwa amewafundisha kumuabudu Mungu Mmoja; na katika mwenendo wake kama Mtawala wa Arabia, alikuwa amewaletea ukombozi kutokana na machafuko ya kisiasa na vita vya maangamizi. Alikuwa amewapa sheria na taratibu. Alikuwa pia amewapa ukombozi kutokana na maadili ya vurugu, umasikini wa kiuchumi na utamaduni usiofaa. Alikuwa amewafanya kuwa matajiri na waliostaarabika, na alikuwa amewafanya kuwa taifa kubwa. Kwa kifupi, alikuwa ndio mfadhili wao mkubwa kabisa. Cha mwisho kabisa ambacho wangeweza kumfanyia kilikuwa ni kumpatia utii na upendo wao. Utii na upendo kwa Muhammad (s.a.w.) ulikuwa uwe ndio kigezo cha imani ya Waislamu katika kazi yake - katika Uislamu!

Walikuwepo wale Waislamu, wengi wao wakitokana na watu wa kawaida, ambao walimpa Muhammad (s.a.w.) upendo wao na hakuna ambaye angeweza kukataa kwamba upendo wao ulikuwa ni halisi. Wakati alipofariki, walipatwa na majonzi; walivunjika mioyo, na kwao wao ule Msikiti, mji na dunia yote ilionekana iliyotelekezwa.

Lakini hisia za maswahaba wakubwa wa Muhammad (s.a.w.) kwenye kifo chake, zilikuwa tofauti. Wakati Muhammad (s.a.w.) alipofariki, maswahaba wake wakuu hawakushtushwa na kifo chake. Kama kifo chake kiliwahuzunisha, wao hawakuonyesha kuhuzunika kokote. Kitu kimoja ambacho hawakukifanya, kilikuwa ni kutokutoa rambirambi zao kwa ile familia iliyoondokewa. Hakuna hata mmoja miongoni mwao aliyekuja na kuwaambia: "Enyi watu wa Nyumba ya Muhammad, tunachangia pamoja nanyi huzuni yenu kwa kifo chake. Kifo chake ni pengo sio kwenu tu bali kwetu sisi sote."

Katika wakati ambapo huruma inatarajiwa hata kutoka kwa wageni, kwa kweli, hata kwa maadui, haisadikiki lakini ni kweli kwamba Masahaba wa Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.w.t.) waliinyima familia yake mwenyewe. Waliiacha familia yake kuomboleza kifo chake yenyewe.

308

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Muhammad Mustafa (s.a.w.) na Urithi Wake

KAMA KIONGOZI, MUHAMMAD (s.a.w.) ALIKUWA KATIKA TABAKA LA WALE MASHUHURI KABISA - katika dunia nzima. Alijaaliwa na uwelewa wa kustaajabisha, uwezo wa kuona mbali na kipaji cha siasa. Katika miaka yake kumi ya mwisho ya uhai wake, alitakiwa afanye maamuzi muhimu sana katika historia ya Uislamu. Maamuzi yale yaliwagusa sio Waislamu tu au Waarabu bali wanadamu wote. Alikuwa pia anatambua kwamba vitendo vyake na maamuzi yake vingegusa vitendo na maamuzi ya kila kizazi cha Waislamu mpaka mwisho wa wakati wenyewe.

Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.w.t.) kwa hiyo, hakufanya uamuzi wowote, haid-huru uwe wa kawaida kiasi gani, kwa msingi wa kusudi maalum; wala kufanya maamuzi kwa utaratibu wa "kubahatisha." Maamuzi yake yote yalikuwa ni ya kujaaliwa. Yalikuwa ni vigezo kwa umma wa Kiislam (taifa au jamii) kwa wakati wote. Ilikuwa ni pamoja na ujuzi na ufahamu huu kwamba alisema au kutenda kitu chochote na kila kitu.

Muhammad (s.a.w.) alifanikiwa, baada ya mapambano marefu na ya kikatili dhidi ya waabudu masanamu na washirikina wa Arabuni, katika kuanzisha Ufalme wa Mbinguni Duniani ili umma wake uweze kuja kuishi kwa amani na usalama, kupendwa na kuonewa wivu na wanadamu waliobakia. Ufalme wa Mbinguni Duniani ulikuwa ndio kazi ya maisha ya Muhammad (s.a.w.). Alijua kwamba yeye ni binadamu, na atakuja kufa siku moja, lakini kazi yake, kama ilivyounganishwa kwenye huo "Ufalme" ingeishi. Alijua kwamba baada ya kifo chake, mtu mwingine tena angeendeleza ile kazi aliyoianzisha yeye. Alijua pia kwamba umakamu (urithi wa kazi yake) uliopangwa vizuri ndio nanga ya utulivu. Alijua yote haya na mengi zaidi ya haya. Hakuna mwislamu ambaye angeweza kamwe kuthubutu kudhania kwamba Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.w.t.) hakuyajua yote haya vizuri zaidi kuliko mtu mwingine yeyote.

Urithi wa Muhammad (s.a.w.) ulikuwa pia ni jambo la kunong'onwa sana miongoni mwa Waislamu wengi. Swali moja ambalo lilitawala sana katika akili za wengi wao, hususan baada ya kutekwa Makka, lilikuwa, ni nani atakayemrithi yeye kama Mkuu mpya wa Dola ya Madina, baada ya kufa kwake.

Swali hili linatoa nafasi kwa jibu moja tu, yaani, mwislamu bora zaidi! Mrithi wa Muhammad (s.a.w.) anapaswa kuwa, sio mtu wa daraja la pili, bali tunda bora kabisa la Uislamu; mtu ambaye Uislamu wenyewe utamkubali kwa fahari kama "chombo cha kipaji."

"Chombo cha kipaji" kama hicho kilikuwa ni Ali ibn Abi Talib, Muhammad (s.a.w.) "alim-

309

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

gundua" yeye mapema maishani; alimuandaa na alimteua yeye kama mrithi wake, hivyo kuhakikisha ukabidhi wa mamlaka wa amani na utaratibu. Alikuwa na hamu kubwa sana ya kuzuia kushindania madaraka miongoni mwa maswahaba wake baada ya kifo chake yeye mwenyewe.

Lakini, kwa bahati mbaya, mpango huu haukufanikiwa, na urithishaji, baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.) haukuwa wa amani na wa utaratibu. Kulikuwa na kushindania madaraka kukali miongoni mwa maswahaba zake ambamo baadhi ya wagombea wapya wa madaraka walifanikiwa katika kukamata Dola ya Madina. Kufanikiwa kwao kuliashiria mwisho wa ghafla wa Utawala wa Mbinguni Duniani, na kuliashiria, wakati huohuo, kuzaliwa kwa Dola ya Kiislam - Dola iliyoongozwa na watu ambao walikuwa Waislamu. Utawala wa Mbinguni Duniani au Dola ya Kiislam haikudumu muda mrefu baada ya kifo cha Mtume. Kifo cha Taifa la Kiislamu, likiwa bado katika uchanga wake, kinaweza kuamsha udadisi wa mwanafunzi wa historia. Anaweza kushangaa ni kwa nini liliishi kwa muda mfupi kiasi hicho, na jinsi ilivyowezekana kwa hawa wagombea wapya kupindua mpango uliofanywa na Mtume (s.a.w.) mwenyewe kwa ajili ya ukabidhianaji wa amani na utaratibu wa madaraka, na kulazimisha kukubalika kwa mpango wao wenyewe juu ya umma wa Waislamu.

Lifuatalo ni jaribio la kujibu swali hili

Wagombea wapya wa madaraka hawakuunga mkono ule mpango uliofanywa na Mtume (s.a.w.) wa kukabidhi madaraka. Wao na wafuasi wao walikuwa na ajizi nyingi za kuuhusu, na walikuwa wamekusudia kukamata Dola ya Madina wao wenyewe. Kwa ajili hii, walikuwa wamekwishapanga mkakati wa hali ya juu na walikuwa wameingia katika kazi ya kuutekeleza hata kabla ya kifo cha Mtume (s.a.w.).

Hila kuu katika mkakati wa hawa wagombea wa madaraka ulikuwa ni kueneza ile taarifa ya uongo kwamba si Kitabu cha Allah (s.w.t.) kilichoelezea maoni yoyote juu ya jambo la uongozi wa umma wa Waislamu, wala Mtume wa Allah (s.a.w.w). kuchagua mtu yeyote kama mrithi wake. Waliwaza kwamba kama Waislamu wakiamini dai kama hilo kuwa la kweli, basi watachukulia kwamba Mtume (s.a.w.) aliiacha kazi ya kutafuta kiongozi wa baadae wa serikali yake kwa umma wenyewe, na katika umma huo, kwa kweli, kila mtu alikuwa huru kuingia kwenye orodha na kunyakua madaraka mwenyewe, kama angeweza.

Dr. Hamid-ud-Din:

"Qur'an Tukufu haikutaja kitu chochote kuhusu namna ya kuchagua khalifa. Hadithi za kutegemewa za Mtume (s.a.w.) nazo pia ziko kimya kuhusiana na hili. Kutokana na hili, mtu anaweza kuchukua uamuzi kwamba Shari 'ah (Sheria Tukufu) imeliacha jambo hili kwenye mapendekezo ya Umma wenyewe ili uweze kuchagua viongozi wao kulingana na mahitaji yao wenyewe, na kulingana na hali itakayokuwepo wakati

310

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

huo."

(History of Islam by Dr. Hamid-ud-Din, M.A.{Honors}, Punjab; M.A.{Delhi};

PH.D.[Harvard University, U.S.A.}, Published by Ferozesons Limited,

Publishers,Karachi,Pakistan,page 188, 4thedition, 4th printing, 1971)

Hila hii ilipata mafanikio ya kushangaza, na ina maisha marefu ya kustaajabisha. Ilitumika wakati huo na inatumika siku hizi.Huko nyuma ilikuwa ikitumika huko Mashariki tu; sasa inatumika kote Mashariki na Magharibi. Wachache huko Mashariki na hakuna yeyote huko Magharibi walioshindana nayo. Mafanikio yake yanathibitishwa na ushahidi wa wanahis-toria wafuatao:

Marshall G.S. Hodgson:

"Qur'an haikutoa, kwa mfano hasa, mambo ya kisiasa yanayoweza kutokea kwa kifo cha Mtume (s.a.w.)"

(The Venture of Islam, Vol1, 1974)

Dr. Muhamed Hamidullah:

"Ukweli kwamba zimekuwepo tofauti za maoni, katika kifo cha Mtume (s.a.w.), unaonyesha kwamba hakuacha maelekezo ya wazi na sahihi kuhusu kurithiwa kwake."

(Introduction to Islam, Kuwait, 1977)

Francesco Gabrieli:

"Muhammad (s.a.w.) alifariki, baada ya kuugua kwa muda mfupi, mnamo tarehe 8 Juni, 632. Hakuweka au hakuweza kuweka ushahidi wa kisiasa na hakumteua mtu aliyekuwa anastahili sana kumrithi yeye."

(The Arabs, A Compact History, New York, 1963)

G. E. Von Grunebaum:

"Mtume (s.a.w.) alifariki mnamo tarehe 8 Juni, 632. Hakufanya maandalizi kwa ajili ya mtu atakayemrithi."

(Classical Islam - A History 600 - 1258) John B. Christopher:

"Tatizo la haraka sana lililoikabili Jumuiya changa ya Madola ya Kiislamu lilikuwa ni urithi kwenye uongozi wa umma pale Muhammad (s.a.w.) alipofariki; tatizo hili lilikutwa na kuanzishwa kwa ukhalifa.

311

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kwa sababu Muhammad (s.a.w.) hakufanya maandalizi kwa ajili ya mtu atakayem-rithi, ile jumuiya ya Kiislam iliyoathirika ikageukia nyuma kwenye vigezo vya kika-bila vya kuchagua Sheikh mpya mara tu baada ya Mtume (s.a.w.) alipofariki."

(The Islamic Tradition, Introduction, New York)

Bernard Lewis:

"Katika asili zake, ile taasisi kubwa ya Kiislam ya ukhalifa ilikuwa ni ushitukizaji wa ghafla. Kifo cha Mtume (s.a.w.), bila ya urithishaji uliopangwa, kilihimiza mgogoro kwenye jumuiya changa ya Kiislamu."

(The Legacy of Islam - Politics and War - 1974)

George Stewart:

"Kuipitia upya historia, mtu anasita na kushangaa ni vipi ukhalifa umetokea kuwepo. Muhammad (s.a.w.) hakuacha usia wowote; hakumteua mtu yoyote kufuata katika nyayo zake, hakukaimu kwa yeyote mamlaka ya kiroho, na hakutoa funguo za Utawala wa Mbinguni kwa mtu ambaye ni Mtume..."

(George Stewart katika makala yake, Is the Caliph a Pope? iliyochapishwa katika kitabu, The Traditional Near East, kilichohaririwa na Stewart Robinson, na kuchapishwa na Prentice-Hall, Inc., N.J., 1966)

Robert Frost wakati fulani alisema: "Nadharia, kama ukiishikilia kwa nguvu ya kutosha na kwa muda mrefu wa kutosha, inapata kuthaminiwa kama kanuni ya imani." Maelezo haya yanaweza kubadilishwa kidogo yasomeke kama ifuatavyo: "Uongo, kama ukiushikilia kwa nguvu ya kutosha na kwa muda mrefu wa kutosha, unapata kuthaminiwa kama kanuni ya imani."

Wingi usio na idadi, wa wanahistoria wa Uislamu, wamedai kwamba Mtume (s.a.w.) hakumtaja bay ana mtu yeyote kama kiongozi wa baadae wa Dola ya Madina baada ya kifo chake yeye mwenyewe. Kwao wao, na kwa wengine wengi, dai hili limekuwa ni kanuni ya imani sasa.

Lakini sio kwa Waislamu wa Shia. Wao wanatetea kwamba Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.w.t.) alitangaza kwa kurudiarudia na kwa msimamo ulio wazi kabisa kwamba Ali alikuwa ndio mshikamakamu wake na kiongozi wa Waislamu wote.

Muhammad (s.a.w.) alionyesha uelekeo kwa ajili ya umma wake, na aliwaonya wao wasiukengeuke baada ya kifo chake. Lakini umma ulikengeuka hata hivyo, na

312

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ukengeukaji huu umewafikisha, kwa kujua au kwa kutojua, kwenye kufufua mila ya kipagani.

Baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.), baadhi ya maswahaba walikusanyika kwenye ukumbi wa nje ya Madina uliokuwa ukiitwa Saqifah, na wakamchagua Abu Bakr kama kiongozi wa Waislamu. Hapakuwa na kigezo katika Uislamu kwa ajili ya uch-aguzi kama huo, lakini kilikuwepo kigezo kwa ajili hiyo katika asasi za kisiasa za nyakati kabla ya Uislamu.

Wanahistoria watatu wa wakati mmoja wa Pakistani wanaandika katika historia zao

History of the Islamic Caliphate kama ifuatavyo:

"Baada ya kifo cha Muhammad (s.a.w.), tatizo muhimu na gumu sana ambalo Waislamu ilibidi wakabiliane nalo, lilikuwa lile la kuchagua khalifa. Qur'an iko kimya juu ya jambo hili, na Mtume (s.a.w.) pia hakusema lolote juu yake. Katika nyakati za kabla ya Uislamu, desturi ya Waarabu ilikuwa ni kuchagua wakuu wao kwa wingi wa kura. (Kwa kushindwa kupata kigezo kingine) kanuni hiyo hiyo ilifu-atwa katika kumchagua Abu Bakr."

(History of the Islamic Caliphate (Urdu), Lahore, Pakistan. Professor M. Iqbal, M.A., L.L.B.; Dr. Peer Muhammad Hasan, M. S., Ph. D.; Professor M. Ikram Butt, M.S.)

Kwa mujibu wa wanahistoria hao watatu waliotajwa hapo juu, kazi muhimu kabisa mbele ya Waislamu wakati wa kifo cha Mtume (s.a.w.) ilikuwa ni kutafuta kiongozi, kwa vile Mtume (s.a.w.) aliwaacha bila kiongozi. Kukosekana kwa kigezo katika Uislamu wenyewe kwa ajili ya kutafutia kiongozi, walilazimika kuchukua mila ya kipagani, na wakamchagua Abu Bakr kama kiongozi wao mpya.

Mtindo huu wa kutafuta kiongozi kwa ajili ya Waislamu ulikuwa haukubaliani na busara za Uislamu. Ulikuwa, kwa hiyo, ni upotofu, kama ilivyokwisha tajwa. Upotofu huu umezingatiwa na Mustashirki wengi; miongoni mwao ni:

R. A. Nicholson:

"Kwamba Muhammad (s.a.w.) hakuacha mtoto wa kiume ilikuwa labda haikuwa na maana zaidi kuliko kupuuza kwake au kukataa kuteua mrithi. Waarabu walikuwa ni wageni na mtiririko wa kurithiana katika mamlaka ya kifalme, ambapo wazo hilo lilikuwa halijaingia bado la mtawala mkazi mwenye haki ya ki-Mungu katika famil-ia ya Mtume (s.a.w.). Ilikuwa inakubaliana kwa kinaganaga na mazoea ya Waarabu kwamba jamii ya Waislamu ichague kiongozi wake yenyewe, kama vile katika siku za upagani kabila lilichagua kiongozi wake lenyewe. "

(A Literary History of the Arabs)

313

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Profesa Nicholson anasema kwamba: "Waarabu walikuwa ni wageni na mtiririko wa kurithiana katika mamlaka ya kifalme. Anaweza akawa sawa. Waarabu, hata hivyo, walikuwa hawana uzoefu na vitu vingine vingi kama vile imani katika Tauhidi ya Allah (s.w.t.) na walikuwa na uzoefu mkubwa na masanamu yao ya mawe na miti; waliambatana nayo kwa ushupavu, na wengi wao wakafa kwa ajili yao."

Hata hivyo, ule "ugeni" wa Waarabu kwenye mtiririko wa kurithiana katika mamlaka ya kifalme haukudumu kwa muda mrefu; ulidhihirisha kuwepo kwa muda mfupi sana. Kwa kweli, huo "ugeni" wao ulidumu kwa chini ya miaka thelathini (kutoka 632 hadi 661). Baada ya ile miaka thelathini ya ugeni na kanuni ya mtiririko wa kurithiana wa mamlaka ya kifalme, wakaja kuwa na ujuzi sana nayo, na ujuzi wao mpya umedumu mpaka kufika kwenye nyakati zetu wenyewe.

Kwa kuwa "wageni" na utaratibu wa mtiririko wa kurithiana wa mamlaka ya kifalme, Waarabu walikuwa wanapapasa gizani, ambapo ghafla wakajikwaa kwenye mfano kutoka kwenye zama zao wenyewe za kabla ya Uislamu, kutoka kwenye siku zile walipokuwa waabudu masanamu, na wakaudaka. Walisisimka kwamba walikuwa wamepata "wokovu."

Francesco Gabrieli:

"Kwa kuchaguliwa kwa Abu Bakr kanuni ilianzishwa kwamba Ukhalifa au Uimam (Uimam katika suala hili ni kisawe cha khalifa) ulikuwa ubakie kwenye lile kabila la Makka la Quraishi ambalo Muhammad alitokana nalo. Lakini wakati huohuo mwe-nendo wa uwezo wa uchaguzi wa nafasi hiyo uliidhinishwa, kama ule wa bwana au kwa kukataa madai ya kurithiana ya familia ya Mtume (s.a.w.) (Ahlul Bait) inay-owakilishwa na Ali."

(The Arabs, A Compact History, 1963)

Francesco Gabrieli anasema kwamba: "kwa kuchaguliwa kwa Abu Bakr, utaratibu ulianzishwa kwamba Ukhalifa utabakia katika lile kabila la Makka la Quraishi. Lakini hasemi ni nani aliyeanzisha "utarattibu" huu. Je, anayo idhini ya Qur'an au Hadith za Mtume (s.a.w.) za kuiunga mkono? Haina. Kwa kweli, ulikuwa ni "utaratibu" wenye kusu-di maalum uliotekelezwa na wale watu ambao walitaka kujitwalia Ukhalifa au Uimamu kwa wao wenyewe. Waliuona "utaratibu" huu ni wenye kufaa sana kwa sababu uliwaweze-sha wao kuikamata serikali ya Muhammad (s.a.w.w), na kuing'ag'ania wakati wakiwazuia watoto wake kutokana nayo. Lakini kivitendo kama ulivyo "utaratibu" huu, unayo idhini yake, sio ndani ya Qur'an bali katika "jamii ya kipagani," kama ilivyoonyeshwa na mwanahistoria huyu mwenyewe."

314

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Bernard Lewis:

"Mgogoro wa kwanza katika Uislamu ulikuja wakati wa kifo cha Mtume (s.a.w.) mwaka 632. Muhammad (s.a.w.w) hajawahi kudai kuwa zaidi ya mwanadamu anayekufa - tofauti sana juu ya wengine kwa sababu alikuwa Mtume wa Allah na mwenye kuleta neno la Allah (s.w.t.) bali mwenyewe sio kama Mungu wala asiyeku-fa. Alikuwa, hata hivyo, hakuacha maagizo ya wazi juu ya nani alikuwa amrithi yeye kama kiongozi wa Jumuiya ya Kiislamu na mtawala wa Dola changa ya Kiislamu, na Waislamu walikuwa na ujuzi wa kisiasa mdogo sana wa Arabia ya kabla ya Uislamu wa kuwaongoza wao. Baada ya mabishano kiasi na kipindi kifupi cha mvutano wa hatari, walikubaliana kumteua Abu Bakr, mmoja wa waliosilimu mwanzoni kabisa na mwenye kuheshimiwa sana, kama khalifa, naibu, wa Mtume (s.a.w.) - hivyo kuunda, takriban bila ya kutegemea, ile taasisi kubwa ya kihistoria ya Ukhalifa.

(The Assassins, 1968)

Kama ilivyoelezwa mapema, ile taarifa ya uongo kwamba Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.a.w.w) hakuacha maagizo yoyote juu ya ni nani alikuwa amrithi kama kiongozi wa Jumuiya ya Kiislam, imekuwa ni Kanuni ya Imani kwa wengi wa wanahistoria, wa zamani na wa sasa, Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Mtu labda anaweza kuwapuuza hao wanahistoria wa Kisunni kwa kung'ang'ania kwenye "kanuni ya imani" hii lakini ni ajabu kwamba wanazuoni wa safu kama hiyo na sifa kama Nicholson na Bernard Lewis hawakufanya chochote zaidi katika vitabu vyao juu ya Uislamu kuliko kuandika tena mtin-do usiobadilika wa historia ambao "ulirithishwa" kwao na wanahistoria wa mabaraza ya Damascus na Baghdad ya karne za mbeleni. Bernard Lewis, hata hivyo, amekiri, kama Nicholson na Gabrieli, kwamba wale Waislamu ambao walimchagua Abu Bakr kama khalifa wao, walikuwa na ujuzi wa kisiasa mdogo sana wa Arabia ya kabla ya Uislamu wa kuwaongoza

Bernard Lewis anaendelea kusema kwamba ile taasisi kubwa ya kihistoria ya Ukhalifa ilizaliwa "takriban bila ya kutegemewa."

Taasisi muhimu sana ya kisiasa ya Uislamu - Ukhalifa - ilizaliwa kwa hiyo "takriban bila ya kutegemewa!"

315

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

George Stewart:

"Cheo cha Ukhalifa kilikuja kuwepo sio kwa mpango wa makusudi au katika busara ya kuganga yajayo, bali takriban kutokana na kama ajali... Ukhalifa uliumbwa kutokana na ajali za ghasia za zama hizo ambazo zilifanya uzaliwe."

(The Traditional Near East, 1966) Akiandika kuhusu jamii ya Kiarabu ya kabla ya Uislamu, Profesa John Esposito, anasema:

"Kikundi cha familia kadhaa zinazohusiana kilitengeneza ukoo. Mkusanyiko wa koo kadha uliunda kabila. Makabila yaliongozwa na chifu (shaykh) ambaye alichaguliwa kwa makubaliano ya watu wa sawa na yeye - yaani, wakuu wa koo au familia zina-zoongoza."

(Islam - the Straight Path, 1991, uk. 5)

Katika kitabu hicho hicho (na mlango huo huo), Profesa Esposito anaendelea kusema -

katika ukurasa wa 16:

"..Jamii iliyoegemea kwenye ushirikishwaji wa kikabila na sheria na desturi ya kika-bila iliyotungwa na watu ilibadilishwa kuwa jamii iliyounganishwa kidini (umma wa Kiislamu) uliotawaliwa na sheria ya Allah (s.w.t.)"

(Abu Bakr alichaguliwa na kuwa mkuu (sheikh) kwa "makubaliano ya mamwinyi - yaani wakuu wa koo au familia zinazoongoza." Ilikuwa ni ile "sheria na desturi ya kikabila iliyotungwa na watu" iliyompa mamlaka. Kitu kimoja ambacho hakikutekelezwa katika kuch-aguliwa kwake, ni "sheria ya Allah (s.w.t.)")

Wanahistoria wote waliotajwa hapo juu wanakubaliana katika kueleza kwamba:

1.  Muhammad Mtume wa Allah (s.a.w.), hakutoa maagizo yoyote kwa umma wake kuhusiani na mwenendo wa serikali ya baadae ya Kiislam, na hakumteua mtu yoyote kuwa kiongozi wake baada ya kifo chake yeye mwenyewe. Katika suala la ushikamakamu, hakuwa na msimamo wa wazi wa sera.

2.  Wakati Muhammad alipokufa, Waislamu walilazimika watafute kiongozi mpya wa jumuiya hiyo. Kwa kukosa muongozo na kigezo, hawakuwa na chaguo bali kurudia nyuma kwenye taasisi na desturi za kisiasa za Zama za Ujahilia ili kupata kiongozi, na Abu Bakr akawa ndio chaguo lao.

316

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kama wanahistoria hawa wako sawa, basi ni kosa baya kupita kiasi kwa upande wa Qur'an Tukufu na Mfasiri na Mtangazaji wake, Muhammad (s.a.w.), kuacha kuwaelimisha Waislamu katika jambo la kuchagua viongozi wao.

Lakini halikuwepo na lisingeweza kuwepo kosa baya kupita kiasi kama hilo kwa upande wa ama Qur'an au Muhammad (s.a.w.). Qur'an imeeleza, kwa maneno ya wazi na makali, ni zipi sifa za kiongozi aliyeteuliwa na Allah (s.w.t.) na Muhammad (s.a.w.) aliuambia umma, kwa maneno ya kufahamika kirahisi na makali, ni nani mwenye sifa hizo. (Suala hili limeshughulikiwa katika mlango mwingine).

Wakati huu, hata hivyo, Abu Bakr alichaguliwa kuwa khalifa wa Waislamu. Amri ya Allah (s.w.t.) haikutekelezwa katika kuchaguliwa kwake. Kuchaguliwa kwake, kwa hiyo, kunazua maswali ya msingi, kama:

1.   Matakwa ya Allah (s.w.t.) na Mtume Wake (s.a.w.) hayakuonekana popote katika uchaguzi wa Abu Bakr. Kwa vile alichaguliwa na baadhi ya maswahaba wa Mtume (s.a.w.), alikuwa ni mwakilishi wao au mwakilishi wa Waislamu. Mtume (s.a.w.) peke yake angechagua mrithi wake, na hakumchagua Abu Bakr. Je, bado Abu Bakr anaweza kuitwa mrithi wa Mtume wa Allah?

2.  Wajibu mkubwa katika mfumo wa jamii yoyote unatekelezwa na serikali au hasa, na kiongozi wa serikali hiyo. Qur'an inashikilia kwamba yenyewe ni pana na haikuacha kitu chochote cha muhimu. Lakini mashabiki wa Abu Bakr wanasema kwamba Qur'an haikuwaambia Waislamu namna ya kumpata kiongozi wa serikali yao. Kama wako sawa, sasa basi, je, tunaweza kudai mbele ya wasiokuwa Waislamu kwamba Qur'an ni mkusanyiko wa sheria ulio kamili na sahihi, na haikusahau jambo lolote muhimu la maisha ya mwanadamu kulifikiria?

3.  Kama Muhammad Mustafa (s.a.w.) mwenyewe hakuwaongoza Waislamu katika nadharia na utendaji wa serikali, basi, je, tunaweza kudai mbele ya wasiokuwa Waislamu kwamba yeye ni mfano bora kwa wanadamu wote katika kila kitu?

4.  Hivi mafundisho ya Muhammad (s.a.w.) yalikuwa pungufu na yasiyotosheleza kiasi hicho kwamba mara tu baada ya alipokufa, wafuasi wake walilazimika kutekeleza desturi, vigezo na mila za kipagani? Na kwa kuwa walifanya hivyo, je, hakuacha mwenendo wake kuwa wakutiliwa mashaka?

Ukweli ni kwamba Qur'an Tukufu ni kanuni pana na timilifu ya maisha. Lakini watakaopata uongofu ndani yake, ni wale tu watakaoutafuta. Hakuna ushahidi kwamba uongofu kutoka kwenye Qur'an ulitafutwa katika uchaguzi wa Abu Bakr. "Utaratibu"

317

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

uliotekelezwa katika uchaguzi wake ulitolewa kutoka kwenye uzoefu wa kisiasa wa Arabia ya kipagani. Uongozi wake uliegemea kwenye desturi iliyochimbuliwa kwenye mamlaka ya kikabila ya kabla ya Uislamu.

Kama vile Qur'an ilivyo kanuni timilifu ya maisha, Muhammad Mustafa (s.a.w.), Mletaji na Mfasiri wake, ndiye mfano bora kwa wanadamu. Alijua kwamba alikuwa anapaswa kutii sheria zilezile za uhai na umauti kama walivyokuwa binadamu wengine. Alikuwa pia amejaaliwa na hisia za historia, na alijua ni nini kilitokea wakati viongozi wakubwa walipofariki. Kitu kimoja ambacho asingeweza kukifanya, ni kuwaacha watu wake kuwa wapinzani kwa mara nyingine tena kama walivyokuwa katika Zama za Ujahiliya. Kitu kimoja ambacho kisingeweza, na hakikuweza kumtoka kwenye uangalifu wake, kilikuwa ni taratibu ya urithi katika Ufalme wa Mbingnii Duniani.

Abu Bakr alichaguliwa katika ukumbi wa Saqifah kama kiongozi wa serikali ya Waislamu kwa msaada wa Umar bin al-Khattab. Kwa hiyo, serikali yake, na vilevile serikali za warithi wake wawili - Umar na Uthman - wote watatu, walikuwa ni "matokeo" ya Saqifah. Nitazitaja serikali zao kama serikali za Saqifah ili kuzitofautisha na serikali ya Ali ibn Abi Talib ambayo haikuwa matokeo ya Saqifah. Serikali ya Ali ilikuwa ni ule Ufalme wa Mbinguni Duniani (uliorudishwa).

318

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Nadharia ya Kisunni juu ya Serikali

Wale waislamu wanaotangaza kwamba wanafuata sunnah (kauli na vitendo) ya Muhammad Mustafa (s.a.w.) Mtume wa Uislamu, na maswahaba zake, wanaitwa Ahl-us-Sunnah wal-Jama'at au Sunni. Wao pia wanajiita wenyewe Waislamu "wenye imani hal-isi", na wanafanya idadi kubwa ya Waislamu duniani.

Waislamu wa Sunni wanaamini kwamba Mtume wa Uislamu (s.a.w.) hakumteua mtu yey-ote kama mrithi wake, na yeye (yamkini) alichukulia kwamba baada ya kifo chake, Waislamu watajitafutia kiongozi wao wenyewe. Wanaendelea kusema kwamba Mtume (s.a.w.) wala hakuwaeleza wafuasi wake ni jinsi gani wangepaswa kuchagua viongozi wao wa baadae au ni sifa gani ambazo viongozi hao lazima wawe nazo. Hivyo, kwa kukosa vyote, kigezo na mwongozo katika jambo la kutafuta viongozi wao, maswahaba hao hawakuwa na chaguo bali kuchukua njia ya ufaraguzi (yaani, nje ya kanuni za Uislamu).

Lakini ufaraguzi sio busara, kama ilivyotarajiwa, ilitokea kuwa njia potovu hasa ya kuta-futia viongozi wa umma wa Kiislam. Katika mfano mmoja maswahaba walimpata kiongozi kupitia kilichochukuliwa kama uchaguzi. Katika mfano mwingine, yule aliyeko madarakani wa kwanza (ambaye alichaguliwa), akateua na kumuweka mrithi wake mwenyewe. Katika mfano wa tatu, yule mwenye madaraka wa pili (ambaye aliteuliwa), akateua kamati ya watu sita na akawapa jukumu la kuchagua mmoja kati yao wenyewe kama kiongozi wa baadae wa umma wa Kiislam.

Huyu kiongozi wa tatu, aliyechaguliwa hivyo, aliuawa katikati ya vurugu na machafuko, na umma ukaachwa bila kiongozi. Masahaba hapo wakageukia kwenye familia ya Mtume wao (s.a.w.), na wakamuomba mmoja wa watu wake kuchukua uongozi wa serikali ya Waislamu, na kwa sababu hiyo kuuokoa kutokana na kuvunjika na kuvurugika.

Huyu mwenye madaraka wa nne alikuwa bado anawatawala Waislamu wakati mgombea mwingine wa uongozi alipoibukia huko Syria. Aliipuuza ile shera ya uchaguzi, akapinga mamlaka halali ya Waislamu kwa kutekeleza utaratibu wa mabavu, na akafanikiwa katika kuikamata serikali. Kitendo chake kilifanya idadi ya "taratibu" za kutafuta viongozi wa umma wa Kiislam kuwa nne, ndio kusema.

1. Uchaguzi

Abu Bakr alichaguliwa kuwa khalifa (mrithi wa Mtume) kwa wingi wa kura ndani ya Saqifah. (Ali ibn Abi Talib, wa nne kwenye mamlaka, alichaguliwa pia kuwa khalifa kwa wingi wa Muhajirina na Ansari waliokuwepo Madina wakati wa kifo cha khalifa wa tatu)

319

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

2. Uteuzi

Umar aliteuliwa na Abu Bakr kama mrithi wake.

3. Uteuzi wa matajiri wenye mamlaka

Uthman alichaguliwa kuwa khalifa na kamati ya watu sita iliyoteuliwa na Umar.

4. Kukamatwa kwa serikali kwa mabavu yasio na aibu

Muawiya bin Abu Sufyan aliikamata serikali ya Waislamu kwa nguvu za kijeshi.

Waislamu wa Sunni wanaziona hizi "taratibu" zote nne kama ni za halali na zenye nguvu. Kwa mwenendo huu, mifano "halali" minne tofauti ya kutafuta kiongozi wa umma wa Kiislam ikaja kuwepo.

Hapa hakuna budi ielezwe kwamba ingawa Waislamu wa Sunni wameupa kila mmoja wa mifano hii minne tofauti ya kutafutia viongozi kwa ajili ya umma "hadhi" ya "kanuni", hakuna hata mmoja kati yao uliopatikana kutoka kwenye Kitabu cha Allah (s.w.t.) (Qur'an), au kwenye Kitabu cha Mtume (Hadith). Yote ilipatikana kutoka kwenye kadhia zilizotokea baada ya kifo cha Mtume wa Uislamu (s.a.w.).

Katika historia ya nchi yoyote ile, utengenezaji wa katiba ndio hatua ya kwanza kuelekea kwenye ujenzi wa taifa. Hiyo katiba ndio sheria-mama ya nchi. Ndio mfumo wa msingi wa mamlaka ya umma. Inaonyesha na kufafanua wajibu, kazi na madaraka ya serikali. Maamuzi yote makubwa yanayogusa maslahi ya taifa yanafanywa kwa kuzingatia kanuni zake. Chochote kinachokubaliana nayo, kinachukuliwa kwamba ni halali na chenye nguvu; ambacho hakikubaliani, kinaachwa kama kisicho cha kikatiba.

H. A. R. Gibb:

"Sheria inaitangulia nchi, kote kimantiki na katika misingi ya wakati; na nchi inakuwepo kwa madhumuni mamoja tu ya kuilinda na kuitekeleza sheria."

(Law in the Middle East)

Nadharia ya Sunni juu ya serikali inasumbuliwa na kioja kilichojengwa ndani kwa ndani. Kama taratibu, sera na vitendo vya viongozi wa kisiasa vinapaswa kufuata kanuni za katiba; lakini hawafanyi hivyo. Badala yake, ni katiba inayofuata matukio yatokanayo na maamuzi na vitendo vya viongozi wa kisiasa. Kwa maneno mengine, sio katiba inayoen-desha serikali; badala yake ni serikali, yaani, ni viongozi wa kisiasa wanaoongoza serikali ndio ambao "wanaiendesha" hiyo katiba.

320

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kwa kweli, hakuna kitu kama nadharia ya Sunni juu ya serikali. Wakati wowote tukio jipya lilipotokea, mafaqihi wa Kisunni walitengeneza "nadharia" au "kanuni" mpya ili kuipa mantiki. Kwa njia hii wameingiza nadharia yao ya serikali yenye tabia ya kigeugeu na wa kuendana na matukio ambayo kwa kweli ni ya ajabu kabisa.

Nadharia na utendaji wa serikali ya Kisunni imechunguzwa na kuchambuliwa na wanafun-zi wengi wa maendeleo ya kisiasa ya Kiislamu, wote, wa zamani na wa sasa, Waislamu na wasiokuwa Waislamu.

Mwandishi wa Sharh-Mawaqif, mwandishi wa jadi wa Kiarabu, anaamini kwamba vitu vinavyohitajika kwa mgombea wa uongozi, ni uwezo wake wa kutwaa na kushikilia madaraka. Anasema:

"Anapokufa Imam na mtu mwenye sifa muhimu anakidai cheo hicho (bila ya kiapo cha utii, yaani Bay 'a kuchukuliwa kwake, na bila kuteuliwa kwake kurithi), madai yake ya ukhalifa yatakubalika, alimradi tu mamlaka yake yanadhibiti watu; na ni dhahiri hali itakuwa ni hiyohiyo wakati huyo khalifa mpya akitokea kuwa mbumbum-bu au muovu. Na hali kadhalika ikiwa khalifa kwa njia hii amejiimarisha kwa nguvu kubwa na baadae anashindwa na mtu mwingine, yule khalifa aliyeshindwa ataon-doshwa madarakani na yule mshindi atatambuliwa kama Imam au Khalifa."

Mchambuzi mwingine wa nyakati za jadi, Taftazani, ana maoni kwamba kiongozi anaweza kuwa dhalimu au anaweza kuwa mwovu; anakuwa hata hivyo ni mtawala halali wa Waislamu. Anaandika katika kitabu chake, Sharh-Agha 'id-Nasafi hivi:

"Imam hana haki ya kuondolewa madarakani kwa sababu ya kuwa kwake mkukan-damizaji na asiyemcha Mungu."

Stewart Robinson amemnukuu Imam Ghazzali, katika kitabu chake, The Traditional Near East, kwamba anasema:

"Sultani mfanya-maovu na mkatili ni lazima atiiwe."

Wachambuzi wa kisasa wa maoni ya kisiasa ya Kiislam pia wameona kutokuwiana katika nadharia ya Sunni ya serikali. Ufuatao ni ushahidi wa wachache wao:

H. A. R. Gibb:

"Nadharia ya Kisunni juu ya serikali ilikuwa, kwa kweli, ni kuongeza ufanisi historia ya jamii. Bila ya vigezo, hakuna nadharia, na mfumo wote wa kuvutia wa tafsiri ya vyanzo vyake, ni utetezi tu baada ya matukio (post eventum?), wa vigezo ambavyo

vimeidhinishwa kwa ijma."

(Studies on the Civilization if Islam, 1962)

321

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Bernard Lewis:

Hitilafu hii kati ya nadharia na vitendo - kati ya maagizo ya kiungwana ya sheria na mambo ya kikatili ya serikali - imewasababisha baadhi ya wanazuoni kuukataa mfumo mzima wa kisiasa na kikatiba wa mafaqih wa jadi wa Kiislam kuwa ni muun-do wa kinadharia na wa bandia, kwa ulivyohusiana kidogo sana na ukweli kama haki za raia zilivyohifadhiwa sana katika katiba za udikteta wa kisasa. Ulinganishaji umetiwa chumvi sana na sio wa haki. Mafaqih wakubwa wa zama za kati za Uislamu hawakuwa wapumbavu wala wapotoshaji - wala wasiojua ukweli, wala wakaidi wa kuulinda huo ukweli. Kinyume chake, walisikitishwa na wasiwasi mkubwa wa kidi-ni, uliotokea hasa kutokana na kutambua kwao lile pengo kati ya mafundisho mema ya Uislamu na zile desturi za mataifa ya Kiislam. Tatizo la waandishi wa kifaqih juu ya serikali lilikuwa zito kuliko lile lililoletwa na tabia ya mtawala mmoja au mwingine. Lilihusu mwelekeo uliochukuliwa na jamii ya Kiislamu kwa jumla tangu siku zile za Mtume (s.a.w.) - mwelekeo ambao umeiongoza jamii hiyo mbali sana kutoka kwenye mambo ya kimaadili na kisiasa ya Uislamu uliobashiriwa. Bado kutil-ia shaka uhalali wa mfumo wa serikali ambao chini yake Waislamu waliishi, kulikuwa ni kupinga imani ya asili ya umma wa Kiislam, hali ambayo haikubaliki kwa ulamaa wa Kisunni, ambao ufafanuzi wao hasa wa imani ya asili unaegemea kwenye vigezo na utendaji wa jamii (ya Kiislamu). Faqih alilazimika kwa hiyo, kwa kiwango fulani, kutetea utaratibu uliopo, ili kuthibitisha imani na mfumo wa Sunni dhidi ya madai kwamba wamepotoka na wamewaingiza Waislamu kwenye hali ya dhambi."

(The chapter on Politics and War published in the volume, Legacy of Islam, 1974)

G. E. Von Grunebaum:

"Katika kuwasilisha wajibu wa khalifa, mtu anahisi juhudi za mashaka za mwandishi za kulinganisha ile kazi kamilifu na mambo duni ya kipindi chake. Sheria imeweka kanuni zisizobadilishika, bila kufikiria kuongezeka kwa kukosa uwezo kwa mtawala wa Waumini katika kutekeleza hata zile kazi zake za wastani kabisa. Hivyo nadharia inalazimika kukubaliana, na kuenea kwa dhana ya uchaguzi kuingiza uchaguzi wa mpiga kura mmoja mwenye mpaka - kwa maneno mengine, kuidhinisha ile hali hal-isi ambamo khalifa anachaguliwa na mtangulizi wake au kiongozi wa kijeshi anayetokea kuwa katika madaraka. Hata uwezekano wa wingi wa viongozi wa jamii itabidi ukubaliwe. Na katika zama zingine na ustaarabu mwingine, nadharia ya mam-laka inakuja kuwa silaha katika kupigania mamlaka."

(Islam, London, 1969)

322

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

John Alden Williams:

"Kauli wakilishi ya namna wanasheria wa Kiislam wa mwishoni mwa kipindi cha kati walivyoyaona matatizo ya madaraka na uongozi wa Kiislam inaonyeshwa na mtu wa Syria wa wakati mmoja na Ibn Taymiya (na ambaye Hanbal kwa kawaida hawakukubaliana naye). Ibn Jama'a (kafa 1333) ambaye alikuwa mmoja wa watu-mishi wakubwa wa utawala wa kidini wa Mamluki, na Qadhi Mkuu wa Cairo kwa mara mbili. Ingawa alikuwa mfuasi wa Shafi'i, kama al-Mawardi, ni maoni ya Ibn Jama'a yanayokubaliana na yale ya Ahmad ibn Hanbal katika maelezo ya kiimani yanayopatikana kwenye mfumo wa imani: Imam aliyeko madarakani atiiwe bila kujali ni vipi ameingia madarakani pale. Katika mgongano kati ya umoja na haki, umoja wa umma lazima uwe na kipaumbele. Kwa nyongeza, yeyote atakayeshika madaraka yenye nguvu katika sehemu yoyote ile lazima atambuliwe na Imamu, kama hana namna yoyote ya kumuondoa. Kwa kifupi, watawala lazima wachukuliwe kana kwamba walikuwa safi, kama wako hivyo au la; haja ya Jamii kulindwa kutokana na makosa iliihitajia. Yalikuwa ni maoni ya kimantiki lakini Ibn Taymiya alihisi kwamba ilikuwa muflisi kimaadili."

(From Imam and Legality. From Emancipated Judgment in the Governance of Muslims. Cha Ibn

Jama'a (d. 1333 A.D.),Al- Ahkam fi Tadbir Ahl al-Islam).

Uimamu uko wa namna mbili: ule wa uchaguzi, na ule wa kunyang'anya. Uimamu wa kuchaguliwa unathibitishwa kwa njia mbili, na Uimamu wa kunyang'anya, kwa njia ya tatu. Njia ya kwanza katika Uimamu wa kuchaguliwa ni kwa kiapo cha wale wenye mamlaka kufungua na kufunga. Njia ya pili ni kwa Imamu kuchaguliwa kama mrithi na yule aliyekuwa mbele yake.

Na kwa njia ya tatu, kukubalika kwa mnyang'anyi kunafanywa halali, inatekelezwa kwa kumshinda mwenye kutumia nguvu halisi, na kama hakuna Imamu kwa wakati huo, na mtu akajiweka mwenyewe ambaye vinginevyo hana sifa ya cheo hicho, na anawashinda watu kwa nguvu zake na kwa majeshi yake bila uchaguzi wowote au kuteuliwa kwenye urithi, basi kukubalika kwake ni halali na mtu analazimika kumtii yeye, ili umoja wa Waislamu uhakikishwe na wanaongea kwa sauti moja. Haina tofauti kama ni mbumbumbu au ni dhalimu, kwa mujibu wa maoni yaliyo sahihi kabisa, na kisha mwingini anainukia na kumshinda yule wa kwanza kwa nguvu zake na majeshi, na yule wa kwanza anaondoswa madarakani, kisha yule wa pili anakuwa ndiye Imamu, kwa ajili, kama tulivyosema, ya ustawi wa Waislamu na umoja wao wa kujieleza. Kwa sababu hii, mtoto wa Umar alisema katika vita vya Harra: "Tuko pamoja na yule mwenye kushinda" (uk. 91).

Kwa kweli, Umma ulikabidhi mambo yake kwa Khalifa, na ulimuomba yeye awe mtawala kamili kabisa. Mbali na swali la kama hii kwa kawaida sio mikingamo -

323

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

maelezo yanayopingana yenyewe, hapakuwa na chombo cha uhakika cha kumchagu-lia yeye au kuhakikisha urithishaji wa amani wa mamlaka yake, na aghalabu au hata kwa desturi watu waliingia kwenye mamlaka kwa njia za kikatili, ambazo zimekatali-wa na sheria. Ulikuwa ni ukweli wa kuhuzunisha kwamba katika mataifa mengi, isipokuwa yale machache kama ufalme wa ukhalifa wa Uthmaniah (Ottoman Empire) na wa Mongolia ambao walifanikiwa katika kuanzisha kanuni ya kurithiana, "hakuna kitu chochote kilichomfaa mtu kwa ajili ya madaraka kama silika za kijinai."

(Themes of Islamic Civilization, 1971, University of California Press, Berkeley)

Mafaqih na wana fikra wa Sunni walikuwa na uwezo wa kufanya marekebisho na maafikiano yasiyokwisha. Walikuwa tayari kuwakubali kama watawala halali, sio tu wale madhalimu na wanyang'anyi wa Kiislamu bali pia hata wasiokuwa Waislamu.

Bernard Lewis:

"Mengi yameandikwa kuhusu Vita vya Kidini juu ya Ulaya. Kidogo hasa kimeandik-wa kuhusu matokeo ya hivi na mapambano mengine yanayofanana na hayo katika nchi za Kiislamu. Kwa mara ya kwanza tangu mwanzo, Waislamu walilazimika kwa kushindwa kijeshi kuachia maeneo makubwa ya nchi ya zamani ya Kiislamu kwa watawala wa Kikristo, na kuacha idadi kubwa ya Waislamu chini ya utawala wa Kikristo. Mambo yote yalikubalika kwa utulivu wa ajabu. Kote Magharibi na Mashariki, watawala wa Kiislamu walikuwa tayari kujihusisha na majirani zao wapya, na hata ikibidi kufanya ushirikiano nao dhidi ya ndugu zao Waislamu - kama wajibu wa Sheria Tukufu - ya kunyenyekea kwa madhalimu, kulikuwa rahisi kuipan-ua hoja hiyo ya kuwahusisha wasiokuwa waumini.'Ambaye madaraka yake yameshinda lazima atiiwe,' alimradi tu kwamba anawaruhusu Waislamu kutekeleza dini yao na kuitii Sheria Tukufu. Eneo la mtawala kama huyo linaweza kuwa pia kuchukuliwa kama sehemu ya Nyumba ya Uislamu."

(Politics and War, kwenye kitabu, Legacy of Islam).

Kifupi na kiini cha uchambuzi huo uliopita ni kwamba nadharia ya Sunni ya kiserikali inaruhusu utaratibu mmoja tu, yaani, mabavu ya kikatili. Takriban mafaqih na wana fikra wote wa Sunni wametoa baraka zao kwenye "utaratibu" huu. Kama utaratibu, mabavu ya kikatili yamekuwa ndio kawaida pekee ya nadharia ya Sunni ya kiserikali tangu Mu'awiyah atwae ukhalifa mnamo A.D. 661. Ina maana kwamba kama mtu anaweza kuhuisha, katika Ufalme wa Mbingnii katika ardhi, sehemu yoyote, ile sheria ya zamani inayojulikana kama "Mwenye Nguvu Mpishe," basi ndiye mtawala wa haki wa umma wa Kiislam. Serikali haina nadharia ya muundo au chombo zaidi ya mabavu ya kidhalimu. Amri za Allah (s.w.t.) zilizohifadhiwa ndani ya Qur'an Tukufu, matakwa, vigezo na amri

324

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

za Mtume Wake (s.a.w.w), na mfumo mzima wa maadili, vyote havifai. Haishangazi sana labda, msimamo huu wa mafaqih wa Sunni unaendelea kuwepo katika nyakati hizi za kisasa. Baraza la Ukhalifa likikutana huko Cairo, Misri, mnamo 1926, lili-weka utaratibu kwamba mwislamu anaweza kihalali kuwa khalifa kama atazatiti madai yake kwa ushindi, hata kama hatatimiza lolote kati ya masharti mengine yanayotakiwa na wanasheria (mafaqih).

Katika uchambuzi wake uliotolewa hapo juu, Dr. Williams amemnukuu Abdullah mtoto wa Umar bin al-Khattab (khalifa wa pili) akisema kwamba yeye (Abdullah) yupo pamoja na mwenye kushinda yoyote yule atakayekuwa. Huyu Abdullah alijulikana kwa uchamungu wake na moyo wa dini na ujuzi. Alitumia au alijaribu kutumia muda wake mwingi akiwa pamoja na Mtume (s.a.w.) kiasi alivyoweza, na kama yeye Abdullah akisema lolote, lilikuwa (na bado) linachukuliwa kama jambo la kuaminika katika mfumo mzima wa Sunni. Inashangaza kwamba hakufikiria kwamba katika mgogoro wowote kati ya watu wawili tofauti au vikundi viwili, suala la haki na batili halikuwa na uhusiano wowote. Kitu cha muhimu pekee kilikuwa ni kushinda. Kwa mujibu wake yeye, yoyote anayeshinda, anayo haki. Kama jambazi anafanikiwa katika kuwaua washindani wake wote na akawa ndiye mshindi wa dhahiri katika kugombania madaraka, basi mantiki ya mafanikio itamfanya yeye kuwa ndio mtu bora kwa nafasi hiyo muhimu na ya juu kabisa katika ulimwengu wa Kiislamu. Anachotakiwa kufanya kuthibitisha kwamba yeye ndiye mgombea mwenye sifa zinazostahili kabisa kwa kiti cha ukhalifa, ni kudhihirisha kwamba anaweza kukitwaa kwa mabavu ya kikatili, na kama atafanya hivyo, kitakuwa ni chake - hakuna sifa katika Uislamu kama mabavu ya kikatili!

Mafaqih, wana-fikra na wachambuzi wa kisiasa wa Sunni wameonyesha msimamo wa kushangaza katika ufafanuzi wao, katika kutetea ile kanuni ya kwamba utii lazima utolewe kwa yeyote aliye na mamlaka mikononi mwake. Hii labda ndio sababu kwa nini utii wa kimyakimya kwa mtawala umekuwepo, kwa maneno ya Elie Kedourie, "desturi ya kisiasa ya kutawala katika Uislamu," na sababu ya kwa nini heshima ya ziada ya Waislamu ime-tolewa kwa ajili ya jambo lililokwisha fanywa na kuhitimishwa; — "mwenendo wake usio na makosa kwenye historia ya Uislamu."

Waislamu wa Shia wanaipuuza nadharia ya Sunni juu ya serikali kwa kukosa kwake muafaka wa kimaadili na kukosa kwake msimamo. Wanasema kwamba kanuni lazima iwe ima ni sahihi au ima lazima itakuwa ya makosa, na kigezo pekee cha kuthibitishia uasili wake kama ni wa kweli au wa uongo ni Qur'an Tukufu. Waislamu wa dunia nzima wanaweza kwa kukubaliana kabisa kuifanya kuwa sheria lakini kama inapingana na Qur'an, haiwezi kuwa ya Kiislamu. Chanzo cha makubaliano ya kimaadili katika Uislamu ni Qur'an, na sio "wingi."

325

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Waislamu wa Shia pia wanasema kwamba lazima pawepo na msimamo katika utekeleza-ji wa Sheria au kanuni. Lakini kama haipo, na "sheria" mpya au "kanuni" mpya inabidi itu-mike kutosheleza kila hali mpya, basi itakuwa isiitwe sera, bali manufaa. Kama ilivy-oelezwa hapo juu, msimamo pekee katika nadharia ya Sunni ya serikali inapatikana kukubaliwa kusiko na sifa, na mafaqih na wanazuoni wa Sunni, kwa "kanuni" kwamba nguvu ndio usuluhishi wa dunia hii, na Waislamu, kwa hiyo, lazima waisujudie (kama hes-hima). Hata Imam Ghazali anasema kwamba "kanuni" hii lazima iungwe mkono kwa sababu ni amri kwa Waislamu ya Qur'an Tukufu yenyewe.

Imam Ghazali ni mmoja wa watu wenye heshima kubwa katika ulimwengu wa Kiislam. Anaonekana kwa ujumla kama mwana-theologia mkubwa sana wa Uislamu wa Sunni. Wanazuoni wa Kisunni wamefika mbali kiasi cha kudai kwamba kama mtu yeyote angeweza kuwa Mtume baada ya Muhammad Mustafa (s.a.w.), angekuwa Ghazali. Na bado, aliwashauri Waislamu kuridhia kimyakimya kwenye mamlaka ya mtu mmoja ya dik-teta au kiongozi wa kijeshi kwa sababu (alisema kwamba) wajibu wao wa kutii mamlaka yaliyopo umeegemea kwenye kitabu cha Qur'an chenyewe: "Mtiini Allah, Mtume Wake na wale wenye mamlaka juu yenu." Inashangaza kwamba mtu kama Imam Ghazali hakuweza kufanya chochote ila kuidhinisha tafsiri isiyo na asili kabisa ya Aya hii.

Qur'an Tukufu, kwa bahati, ni ngeni kwa nadharia zote hizi za serikali na kanuni za vyama vya kisiasa zilizogunduliwa, zilizoelezwa kwa ufasaha na kuwekwa katika mpango wa wazi na wengi wa Waislamu, na hii kwa sababu rahisi, yaani, inayo nadharia yake yenyewe ya serikali na falsafa yake yenyewe ya kisiasa. Haina, kwa hiyo, haja yoyote na nadharia ngeni au falsafa ya serikali.

Falsafa ya kisiasa ya Qur'an imeshughulikiwa katika mlango mwingine katika kitabu hiki.

326

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kugombea Madaraka - 1

Waislamu wa Sunni wanadai kwamba maswahaba wote wa Muhammad Mustafa Mtume wa Allah (s.a.w.) aliyebarikiwa, walikuwa ni mifano ya mwendo wa kuigwa, na kwamba hawakuguswa na uroho wa pesa, tamaa ya madaraka wala malengo yoyote ya kidunia. Wanasema pia kwamba maswahaba wote walipendana wenyewe na kwamba mahusiano yao hayakuchafuliwa na ubeuzi wala husuda.

Hilo, kwa bahati mbaya, liko mbali na ukweli wenyewe ulivyo. Tungependa iwe hivyo lakini ushahidi wa historia hauungi mkono dhana kama hiyo, na mambo ya kikatili yanauchanilia mbali uongo na ufasaha wa usemaji wa wapenzi wa maswahaba waliotu-rithisha sisi. Mpenzi wao mwenye msimamo mkali kabisa hawezi kukataa kwamba kugombea madaraka miongoni mwao kuliibuka hata kabla ya mwili wa Mtume (s.a.w.) haujafanyiwa mazishi. Ushahidi wa historia, kwa hiyo, ungetufanyia uwezekano wa kufanya uchambuzi wenye ukweli zaidi wa tabia ya maswahaba wa Mtume (s.a.w.), na nafasi zao mbalimbali katika historia ya Kiislamu.

Ingekuwa, kwa kweli, ni vigumu kibinadamu kwa maswahaba wote wa Mtume (s.a.w.) kufanana kwa kila hali. Hakuna watu wawili wanaoonyesha mwenendo wa tabia unao-fanana kwenye matukio na mazingira ya nje yao. Kuukubali Uislamu, na usahaba wa Mtume wake (s.a.w.) hakukulazimisha kutakasika silika za kila Mwarabu. Walikuwa ni kundi lililochanganyika. Baada ya kusilimu, baadhi yao walifikia viwango vya juu; wengine walibakia palepale walipokuwa.

Ugumu wa kutathmini nafasi ya sahaba wa Mtume (s.a.w.) umeambatana na upotovu wa tafsiri yake. Kulingana na fasiri moja, mwislamu yeyote aliyemuona Mtume wa Uislamu, alikuwa ni sahaba wake. Waislamu wengi sana walimwona katika miaka 23 ya ujumbe wake kama Mtume wa Allah, na wote hao, kwa hiyo, walikuwa "maswahaba" zake. Lakini Waislamu wa Shia hawaikubali tafsiri hii. Wanasema kwamba cheo cha sahaba kilikuwa ni kitu ambacho Muhammad (s.a.w.) pekee aliweza kukitoa kwa mtu fulani. Kama hakufanya hivyo, basi haikuwa kwa wengine kudai heshima hii.

Waislamu wa Sunni wananukuu "Hadith" ya Mtume (s.a.w.) ambayo anadaiwa kwamba alisema: "Masahaba wangu wote ni kama nyota. Yeyote mtakayetafuta uongofu kwake, mtaupata." Anasemekana pia kwamba alisema: "Masahaba wangu wote ni wema, wenye haki na wakweli."

Kama Hadith hizi ni sahihi, na maswahaba wote wa Mtume (s.a.w.) ni kweli wao ni "nyota," basi kwa ajabu sana, kwa kushangaza sana, moja ya nyota zenyewe; kwa kweli, moja ya nyota yenye kung'ara sana katika kundi zima la nyota la maswahaba, ilionyesha mashaka makubwa juu yao. Nyota husika yenyewe ni Umar ibn al-Khattab, khalifa wa pili wa Waislamu. Sio alionyesha tu kwamba hakukubaliana na Hadith hizi mbili na nyingine

327

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

zinazofanana nazo; bali alizikataa pia. Wakati wa ukhalifa wake mwenyewe, aliwaamuru hao maswahaba wa Mtume (s.a.w.) - hao nyota - kubakia Madina au wasiondoke Madina bila ruksa yake. Yeye kwa hiyo alizuia uhuru wao wa kutembea, na walilichukia sharti hili. Lakini alichukuwa madhila ya kuwaeleza kwamba alikuwa anafanya hivyo kwa maslahi yao wenyewe!

Kuhusu suala hili, Dr. Taha Husein anaandika katika kitabu chake, Al-Fitnatul-Kubra (Mageuzi Makubwa), kilichochapishwa mwaka 1959 na Dar-ul-Ma'arif, Cairo, Misri: Umar alikuwa na sera kuhusiana na Muhajirina wakubwa na Ansari. Walikuwa mion-goni mwa watu wa awali kabisa kuukubali Uislamu, na waliheshimiwa sana na Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Wakati wa uhai wake, aliwaweka wengi wao katika uon-gozi wa mambo muhimu. Umar pia alishauriana nao katika mambo ya maslahi ya jamii, na yeye pia aliwafanya wengi wao kuwa maswahaba na washauri wake. Hata hivyo, alihofia fitna juu yao, na pia alihofia fitna kutoka kwao. Kwa hiyo, aliwazuia hapo Madina, na hawakuweza kutoka nje ya Madina bila ya ruksa yake. Hakuwaruhusu kwenda kwenye zile nchi zilizotekwa isipokuwa pale tu alipowaamu-ru kwenda. Alihofia kwamba watu katika nchi zile "wangewatukuza" wao (kwa sababu ya hadhi yao kama maswahaba wa Mtume (s.a.w.)), na akahofia kwamba hili litaongoza hao (maswahaba) kwenye vishawishi. Aliyaogopa pia matokeo ya "kutukuzwa" huku kwa maswahaba, kwa ajili ya serikali. Hapana shaka kwamba kuzuiwa huku kulichukiwa na wengi wa maswahaba hao, hususan na wale Muhajirina miongoni mwao.

Itakuwa vema tu kama tutaichunguza kwa kuikosoa hii sera ya Umar kuhusiana na kundi hili mashuhuri miongoni mwa maswahaba. Wakati alipowaamuru kubakia Madina, labda alikuwa sawa katika sera yake. Kwa nini tusiviite vitu kwa majina yao halisi? Au, bora zaidi, kwa nini tusiifasiri ile sababu iliyomshawishi Umar kuwazuia maswahaba hapo Madina, kwa istilahi za kisasa? Umar aliogopa kwamba hao maswahaba, kama watakwenda huko kwenye majimbo, wataweza kunywea kwenye vishawishi vya kutumia uwezo na hadhi zao!

Kama matukio yaliyofuata baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.) yatatazamwa katika mazingi-ra yake ya kibinadamu, itatoa kinga ya kuhimili mshituko kwa wale wanaotegemea maswahaba kuwa Malaika, lakini wawaone ni wamoja, watu wa kawaida. Kama wengi wa maswahaba walijionyesha wenyewe kama watu wanaoendeshwa na tamaa na maslahi binafsi baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.), ilikuwa ni kwa sababu wakati wa uhai wake hawakuwa na matumaini wala fursa ya kuwatambua wao. Lakini mara tu baada ya kufari-ki kwake,walijihisi kwamba walikuwa huru kuandama malengo yao wenyewe katika maisha.

Mtazamo wa kimapokezi wa Sunni kwenye ukadiriaji wa nafasi ya maswahaba umekuwa kile Thomas Fleming alichokiita "mtazamo wa mng'aro wa dhahabu." Mtazamo huu unamwelezea kila mmoja wa maswahaba kama muungano wa shujaa-mtakatifu na mwenye kipaji. Lakini uelezaji huu sio wa kweli kwa maisha, na kwa sababu sio wa kweli,

328

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

unawatoa kwenye kitovu cha kuonekana vizuri. Maoni yenye ukweli zaidi yangekuwa kwamba hao maswahaba walikuwa binadamu kama watu wengine wote, na kwamba wao pia wangeweza kunywea kwenye vishawishi vya kunufaika na fursa au mamlaka yaliyoko mikononi mwao.

Lord Action, mwanahistoria maarufu wa Uingereza, na mwenyewe akiwa mfuasi wa Katoliki, wakati mmoja alitoa onyo lifuatalo kwa wale watu ambao walitoa visingizio kwa ajili ya matendo maovu kupindukia ya Mapapa wa Ufufuko Mpya wa Kanisa Katoliki:

"Siwezi kukubali sheria zenu za kanisa kwamba tuwahukumu Papa na Mfalme tofau-ti na watu wengine, kwa ufidhuli wa upendeleo kwamba hawakufanya kosa lolote...madaraka yanaelekeza kwenye maovu, na mamlaka kamili hupotosha kikamilifu.. Hakuna uasi mbaya kuliko ule ambao ofisi inamtakasa mbebaji wake."

Qur'an Tukufu imetoa sifa nzito kwa wale Waislamu waliothibitisha wao wenyewe kus-tahiki usahaba wa Muhammad (s.a.w.). Lakini pia imewaonyesha wale wale miongoni mwao ambao hawakustahili usahaba huo. Aya nyingi zilishuka katika kuwakosoa kwao.

Sifa za maswahaba wengi wa Mtume (s.a.w.) zilichafuliwa na husuda. Kinyongo chao kwa kuchaguliwa kwa Usamah bin Zayd bin Haritha kama Kamanda Mkuu wa msafara wa Syria, kilikuwa ni udhihirisho wa wazi wa husuda hii. Katika miaka ya baadae, chuki hiyo hiyo ilisababisha kuuawa kwa khalifa mmoja, na ikasababisha maasi dhidi ya mwingine.Si wengi miongoni mwa maswahaba waliofanya jitihada za makusudi kuzuia chuki zao kwa maslahi makubwa ya Uislamu, na ya umma wa Mtume (s.a.w.).

Migogoro ya maswahaba ina muda mrefu tangu iingie kwenye historia. Iwezekane, kwa hiyo, kwa mwislamu wa kisasa kuamka juu ya misimamo ya jazba ya kizamani, na waan-galie kwa makini ule "utendaji wa zamani" wa wao wote. Inaweza ikawa vigumu lakini inawezekana kufanya hivyo ikiwa madhumuni ya kujitolea kwake sio watu bali ni ukweli tu. Kilicho muhimu hata hivyo, ni kuelewa na sio hisia!

Muhammad Mustafa (s.a.w.), alikwisha "mtawaza" rasmi Ali ibn Abi Talib kama mrithi wake huko Ghadir- Khum, na alikwisha mtangaza kama kiongozi wa baadae wa Waislamu wote. Walikuwepo maswahaba wachache waliokuwa wanatambua kwamba vitendo vya Mtume (s.a.w.) vilikuwa havina shaka. Waliamini kwamba vitendo vyake vyote vilikuwa ni msukumo kutoka mbingnii, na kwamba havikuchochewa na ukabila wowote. Walijua kwamba ikiwa amemnyanyua Ali kama Kiongozi Mkuu wa Dola ya Kiislamu, ilikuwa ni kwa sababu Ali alikuwa na sifa zote muhimu kwa ajili ya madaraka kama hayo.

Lakini kulikuwa na kikundi kingine cha maswahaba ambacho kiliamini kwamba Mtume (s.a.w.) hakuwa huru kabisa kutokana na hisia za asabiyya (mshikamano wa kikabila; aina ya utaifa wa kikabila; "kabila langu, liwe sawa au na makosa;" mapenzi ya moyo wa ukoo). Waliyahusisha matangazo na kauli zake zinazoonyesha ubora wa Ali, kwenye asabiyya yake. Utawala wa Ali haukukubalika kwao. Walijiona wao wenyewe ni wenye

329

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

sifa nzuri tu kuweza kuongoza Dola changa ya Madina kama Ali, na walitambua kwamba ili kuiendesha hasa, walipaswa kuchukua hatua kabla muda haujapita sana.

Kulikuwa na njia moja tu kwa watu wa kundi hili ya kufanikisha lengo lao, nayo ilikuwa ni kuiteka Dola ya Madina katika muda muafaka. Wakiwa na shabaha hii mawazoni mwao, walianza kutangaza imani yao wenyewe, yaani, kwamba Utume na ukhalifa havipaswi kuchanganyika katika nyumba hiyo hiyo. Hakukuwa na njia yoyote ya wao kuuondoa Utume kwenye nyumba ya Muhammad (s.a.w.) bali labda ilikuwa inawezekana kuuondoa ukhalifa humo.

Waliamua kujaribu. Kampeni hiyo ilifunguliwa na Umar bin al-Khattab. Yeye alikuwa ndiye kiongozi wa kikundi hicho kilichotaka kuteka serikali. Kwenye kumbukumbu yapo mahojiano mafupi aliyowahi kufanya, wakati wa utawala wake, na Abdullah ibn Abbas, ambamo alisema kwamba kwa vile Mtume (s.a.w.) alikuwa ni wa ukoo wa Bani Hashim, "Waarabu" hawakupenda lile wazo la kwamba na khalifa pia awe ni mtu wa ukoo huo huo. Mahojiano hayo yalikwenda kama ifuatavyo:

Umar: Ninaelewa kwamba Waarabu walikuwa hawakutaka kwamba ninyi (Bani Hashim) muwe ndio viongozi wao.

Abdullah ibn Abbas: Kwa nini?

Umar: Kwa sababu hawakulipenda lile jambo la kwamba mamlaka yote ya kiroho na kidunia yawe ni haki ya pekee ya Bani Hashim kwa wakati wote.

Abbas Mahmoud Al-Akkad, mwanahistoria wa kisasa wa Misri, anasema katika kitabu chake, 'Abqariyyat al-Imam Ali, kilichochapishwa Cairo mnamo mwaka 1970:

Umar aliielezea sababu katika kauli ifuatayo, kwa nini baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.), Ali hakuweza kuwa mrithi wake:

"Maquraishi walichagua khalifa kutokana na hiari yao wenyewe. Hawakuwa tayari kuona kwamba Utume na Ukhalifa vyote viwe ni mali ya Bani Hashim."

Maquraishi hawa ambao walisukumwa na tamaa yao ya kutwaa serikali ya Muhammad (s.a.w.), waliunda mpango uliofanywa kwa uangalifu sana, kwa ajili ya azma hii, wasiache chochote cha kuhatarisha.

Bukhari, Abu Daud na Tirmidhi (wakusanyaji wa Hadith) wamemnukuu Abdullah Ibn Umar bin al-Khattab akisema:

Katika wakati wa Mtume (s.a.w.) tulikuwa tumezoea kusema kwamba watu bora katika umma ni Abu Bakr, Umar na Uthman."

(The Virtues of the Ten Companions - cha Mahmud Said Tantawi wa The Council of

Islamic Affairs, Cairo, Egypt, 1976) John Alden Williams

330

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

"Ahmad bin Hanbal amesema: "Wabora wa umma huu - baada ya Mtume (s.a.w.) -ni Abu Bakr al-Siddiq, kisha Umar ibn al-Khattab, kisha Uthman ibn Affan. Tunatoa upendeleo kwa wale watatu (juu ya Ali) kama maswahaba wa Mtume (s.a.w.) walivy-owapendelea. Hawahitilafiani katika hilo. Kisha baada ya wale watatu wanakuja wale Wapiga Kura Watano (Ashab as-Shura) walioteuliwa na Umar alipokuwa anafariki: Ali ibn Abi Talib, Zubayr, Talha, Abd al-Rahman ibn Auf, na Sa'd ibn Abi Waqqas. Wote hao walifaa kwa ukhalifa, na kila mmoja wao alikuwa Imam. Katika hili tunakwenda kwa mujibu wa Hadith ya mtoto wa Umar:

Wakati Mtume wa Allah alipokuwa hai - rehma juu yake na amani - na maswahaba zake wakiwa bado wapo, tulikuwa tukiwahesabu kwanza Abu Bakr, kisha Umar, kisha Uthman, na kisha tukanyamaza kimya."

(Baadhi ya Mafundisho Muhimu ya Hanbali kutoka kwenye Maelezo ya Kanuni za Imani).

(Themes of Islamic Civilization, 1971)

Maelezo ya Abdullah ibn Umar ni uthibitisho kwamba njama za kumnyanyua Abu Bakr, Umar, na Uthman juu ya Ali, zilianzishwa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.) mwenyewe, kwa matarajio, na matayarisho kwa ajili ya nyakati za mbele. Maquraishi walikwisha kua-mua kabla ni nani watakuwa viongozi wa umma baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.), na kwa mpangilio gani.

Wakati Mtume wa Allah (s.a.w.w) alipofariki, Abu Bakr hakuwepo Madina; alikuwa nyumbani kwake huko Sunh, kitongoji cha Madina. Lakini Umar alikuwepo kwenye tukio hilo. Alichomoa upanga wake na akaanza kupiga kelele:

"Wanafiki wanasema kwamba Mtume wa Allah (s.a.w.w) amekufa. Lakini hakufa. Yuko hai. Amekwenda, kama Musa alivyokwenda, kumuona Mola Wake, na atarudi baada ya siku arobaini. Kama mtu yeyote atasema kwamba amekufa, nitamuua." Waislamu wengi waliingiwa na wasiwasi walipomsikia Umar akijitapa kwa hasira. Kwa kupunga upanga wake, na kwa kutishia kuua, alifanikiwa katika kuwanyamazisha watu. Baadhi yao walifikiri kwamba anaweza akawa anasema kweli, na Mtume (s.a.w.) anaweza akawa hakufariki. Baadhi ya wengine walianza kunong'onezana na kujiuliza kama Mtume (s.a.w.) alikuwa amefariki kweli. Lakini wakati huo Abu Bakr aliwasili pale Msikitini na akasoma Aya ifuatayo ya Qur'an Tukufu mbele ya umati wa Waislamu:

Usahihi-39.jpg

"Hakuwa Muhammad ila ni Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake Mitume. Je, akifa au akauawa ndio mtageuka mrudie ya nyuma? Na atakayerudi nyuma huyo hatamdhuru kitu Allah. Na Allah atawalipa wanaomshukuru."(SW« 3; Aya ya 144)

331

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Waislamu walipoisikia Aya hii, waliridhika kwamba Muhammad Mtume wa Allah (s.a.w.), alikuwa tayari amekwishafariki, na haukubakia wasiwasi wowote juu ya hilo kwenye akili ya mtu yoyote.

Kama ilivyoonyeshwa kabla, Umar hakumwacha Muhammad Mustafa (s.a.w.) aandike mirathi na wosia wake wa mwisho akihofia kwamba atamtaja Ali kama mrithi wake. Kisha Mtume (s.a.w.) akafariki. Lakini katika ule muda kati ya kufa kwa Mtume (s.a.w.) na kuwasili kwa Abu Bakr, Umar alikuwa bado ana hofu wasije wale Waislamu waliokuwe-po pale Msikitini, wakamtambua Ali kama kiongozi wao. Ili kuwahi kuvuruga uwezekano huu, alichomoa upanga wake, na akaanza kupiga makelele kwamba Muhammad (s.a.w.) hakufa bali alikuwa hai ili isijetokea kwa mtu yeyote kwamba kiongozi mpya wa umma anapaswa kuchaguliwa. Umar alikuwa anamaanisha kwa njia hii kwamba wakati Mtume (s.a.w.) akiwa bado yuko hai, ni nani atahitaji mrithi; baada ya kuwa warithi wote walikuwa ni kwa ajili ya wafu na sio kwa waliohai! Wanasiasa wengi, wakati wote kabla na tangu ya Umar, wameficha taarifa za kifo cha mfalme au mkuu wa nchi kwa wananchi mpaka mrithi wake awe amekwisha chaguliwa.

Kifo cha Mtume (s.a.w.) kilikuwa ni kweli. Lakini Umar angemuua mtu kama angeueleza ukweli huo? Angemuua mtu kwa kusema ukweli? Hivi ni dhambi mtu kusema kwamba mtu aliyekufa amekufa, na adhabu ya kusema hivyo ilikuwa ni kifo?

Kuwathibitishia Waislamu kwamba Muhammad (s.a.w.) alikuwa hajafariki, Umar akaleta mfano kama wa Musa. Lakini mfano huo uliingiwa na dosari ya dhahiri. Bani Israil wal-imwona Musa akiondoka sehemu waliyokuwa mpaka alipopotea machoni mwao. Lakini mwili wa Muhammad Mustafa (s.a.w.) ulikuwa umelala chumbani kwake, na haukuondo-ka machoni mwa mtu yeyote. Waislamu, pamoja na Umar mwenyewe, waliweza kuuona, na kuugusa, na kuuhisi kwamba ni wa baridi na usio na uhai.

Mwandishi wa Kihindi wa wasifa wa Umar, M. Shibli, na wengineo wanasema kwamba yeye (Umar) alikuwa akitishia kuwauwa Waislamu kwa kutokana na mapenzi yake juu ya Muhammad (s.a.w.). Alikuwa, wanavyosema, katika hali ya mshituko. Na alikuwa anashindwa kushikamana na ukweli! Umar alikuwa kati ya miaka ya hamsini wakati Mtume (s.a.w.) alipofariki.

Je, inawezekana kwamba hajawahi kumuona mtu yoyote akifariki, na alikuwa hajui kufa kuna maana gani?

Ukweli unaotisha ni kwamba Umar alikuwa akijifanya tu. Kujifaragua kwake kulikuwa ni pazia la nia yake halisi. Kusisitiza kwake kwamba Muhammad (s.a.w.) alikuwa hajafa, kulikuwa ni moja kati ya mfululizo wa mbinu kuficha mahali maalum pa mamlaka na uon-gozi kwenye macho ya watu. Wakati fulani alikuwa tayari kumuua mtu yeyote kwa kuse-

332

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ma kwamba Mtume (s.a.w.) amekufa lakini muda mfupi unaofuatia tu, pale Abu Bakr alipotokea, na kusoma Aya kutoka kwenye Qur'an, akawa mbadilikaji wa mara moja kwenye wazo la kwamba yeye Mtume (s.a.w.) alikuwa ni binadamu, anaweza kufa, na amekufa kweli. Alikiri pia kutokujua kwake Qur'an, na akasema kwamba imeonekana kwake kama ni mara ya kwanza kuisikia ile Aya ambayo Abu Bakr alimsomea yeye na Waislamu wengine ndani ya Msikiti.

Kuwasili kwa Abu Bakr kulimtuliza Umar, na akili zake zote zikamrudia kabisa. Kisha akakimbilia, pamoja na Abu Bakr, kwenda Saqifah, kutoa madai ya ukhalifa, na kuuteka kabla ya Maansari kuweza kuuteka. Mazishi ya mwili wa Mtume (s.a.w.) yalikuwa ni kitu wanachoweza kuwaachia watu wa familia yake mwenyewe.

Njama za Umar za kuthibitisha kwamba Muhammad Mustafa (s.a.w.) alikuwa hai, zilivun-jika ghafla. Alikuwa na uwezo, hatimae, wa kuweza kukubaliana na ukweli! Kanuni ya sheria ya zamani ya Kirumi ni kwamba suppressio veri ni sawa na suggestio falsi. Hii ina maana kwamba kuficha ukweli ni sawa na kueneza uongo!

Mwanzoni, katika mlango huu, nilinukuu kifungu kutoka kwenye kitabu, Al-Fitnatul-Kubra au mageuzi makubwa, cha Dr. Talha Husein, kuhusu kizuizi kilichowekwa na Umar bin al-Khattab, khalifa wa pili wa Waislamu, juu ya uhuru wa kutembea wa Muhajirina.

Umar aliwakataza Muhajirina kuondoka Madina bila ya idhini yake. Lakini walikuwa ni akina nani hawa Muhajirina ambao walikatazwa kuondoka Madina? Muhajirina wote walikuwa wameondoka Madina - ukiwaacha wawili tu, yaani, Uthman bin Affan na Ali ibn Abi Talib!

Kwa vile Uthman alikuwa na uwezo mdogo wa utekaji au uongozi, angeweza kuwa amekaa Madina kwa hiari yake, Umar, kwa hiyo, ilimbidi aitekeleze sheria hii kwa ajili ya Ali pekee.

Umar hakuweza kutamka wazi kwamba kati ya Muhajirina wote, Ali peke yake haruhusi-wi kuondoka Madina. Ni kwa sababu gani Umar angeweza kumkataza Ali kuondoka Madina? Inavyoonekana hakuna. Yeye, kwa hiyo, ilimbidi atumie istilahi ya jumla ya "Muhajirina" kuzuia uhuru wa Ali wa kutembea.

Hata hivyo, alikuwa ni Ali, kama akiwa yeyote, ambaye asingeshawishika kutumia sauti yake juu ya jeshi, kama hicho ndicho Umar alichokuwa akikiogopa.

333

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kugombea Madaraka - 2

Mkutano wa Ansari ndani ya Saqifah

Mnamo A.D.622, ansari walimkaribisha muhammad (s.a.w.w.), mtume wa Allah (s.a.w.w) aliyebarikiwa, huko Madina, na walimkubali kama kiongozi wao wa kiroho na kidunia. Waislamu wengine wa Makka, yaani Muhajirina, pia walihamia Madina, na Ansari wakawakaribisha kwa mikono miwili. Walishirikiana nao majumba yao na chakula chao. Katika nyakati nyingi, waliwanyima watoto wao wenyewe chakula ambacho walikitoa kwa Muhajirina wenye njaa.

Muhammad (s.a.w.) aliifanya Madina kuwa makao makuu ya Uislamu, na kwa wakati huo, mji huo ukaanza kuchukua sifa bainifu za dola. Jinsi muda ulivyoendelea, ule mji mdogo dola ulikua na kuwa serikali imara yenye vyanzo vyake vya mapato, hazina yake, jeshi, mfumo wa sheria na utawala na vyombo vya kidiplomasia.

Ilikuwa haikwepeki kwamba itakuja kutokea kwa Ansari (na Waislamu wengine) kwamba siku itafika ambapo Muhammad (s.a.w.), mwanzilishi wa Dola ya Madina, atakuja kuwaa-ga na atakuja kuiaga dunia hii. Uwezekano huu uliwakabili pamoja na maswali mapya au hasa magumu kama vile:

1.  Kifo cha Muhammad Mustafa (s.a.w.) kitakuwa na athari gani kwa Dola changa ya Madina na kwa umma wa Kiislam?

2.  Ni nani atakayemrithi Muhammad (s.a.w.) kama kiongozi mpya wa Dola ya Madina wakati atakapofariki?

3.  Ni ipi itakayokuwa hali ya Ansari baada ya kifo cha Muhammad (s.a.w.)? Huyo kiongozi mpya atakuwa maridhawa tu na muadilifu kama alivyo

yeye?

4.  Hivi Ansari wataendelea kuwa mabwana katika nchi yao wenyewe - Madina -baada ya kifo cha Muhammad (s.a.w.)?

Ansari walikuwa wamesikia ile hotuba ya Mtume. wa Allah (s.a.w.w) pale Ghadir-Khum akimteua Ali kama mrithi wake, na waliuunga mkono kwa moyo wote utaratibu huu. Lakini pia waliuhisi ule mkondo wa kichinichini wa uadui wa Muhajirina kwa Ali, na hawakuwa na hakika kama urithi wake utakuwa salama au kama utafanyika kamwe. Ilikuwa ni dhahiri kabisa kwao kwamba kulikuwa na upinzani mkubwa, miongoni mwa Muhajirina, juu ya urithi wake, na kwamba, miongoni mwao, alikuwa yu peke yake. Mara

334

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

tu Ansari walipoupata ukweli huu, walianza kujishughulikia wao wenyewe. Ilikuwa ni kwa sababu hii ndipo wakajikusanya ndani ya Saqifah.

Mtu anaweza akakipuuza kitendo hiki cha Ansari hata kama mtu hatakisifu kwa sababu wazo kubwa sana katika akili zao, kufuatia kifo cha bwana wao, Muhammad (s.a.w.), lilikuwa ni la kujilinda. Ingawa walipaswa kuahirisha mkusanyiko wao wa kisiasa mpaka baada ya mazishi ya mwili wa bwana wao, kwa wakati huo ilijitokeza kwao kwamba walipaswa kushughulika mara moja, vinginevyo watakuwa wamechelewa sana.

Kama ilivyoelezwa kabla, Ansari walikuwa wametoa hifadhi kwa Uislamu katika wakati ambapo hali yake ilikuwa nyonge sana. Kwa ajili ya Uislamu, wamewafanya Waarabu wote kuwa maadui zao. Kwa ajili ya Uislamu, wamejidharaulisha mbele ya Arabia yote. Katika kila vita ya Kiislam, walijitoa wenyewe kwa heshima kabisa. Wengi wa vijana wao wameuawa kwenye vita hivi. (Katika vita vya Uhud, Waislamu 75 waliuawa; kati yao wanne walikuwa Muhajirina, na waliobakia wote walikuwa Ansari). Walionyesha mapen-zi yao kwa Uislamu na utii wao kwa Mtume (s.a.w.) katika kila sehemu.

Ansari walijua kwamba Ukhalifa ulikuwa ni haki ya Ali lakini walijua pia kuhusu "azimio" la Waarabu la kuuondoa ukhalifa nje ya nyumba ya Mtume (s.a.w.). Tafsiri yao juu ya "azimio" hili lilikuwa kwamba Muhajirina hawatamuachia Ali akifikie kiti cha ukhalifa.

Lakini kama sio Ali, basi ni nani mwingine atakayekuwa mrithi wa Muhammad (s.a.w.)? Jibu pekee la wazi kwa swali hili lilikuwa: Ni Muhajirina mwingine. Lakini Muhajirina yeyote mwingine mbali na Ali alikuwa hakubaliki kwao - kwa Maansari. Wao, kwa hiyo, waliamua kuweka mgombea wao wa uongozi wa umma. Hata hivyo, ilikuwa ni msaada wao, uliokuwa sababu, na sio msaada wa Muhajirina, ambao uliofanya Uislamu kuwepo.

Wasiwasi wa Ansari ni wenye kueleweka vizuri sana. Kwao wao, matarajio ya Dola ya Madina kuangukia kwenye mikono ya Bani Umayya, maadui wa jadi wa Allah (s.w.t.) na Mtume Wake (s.a.w.), ambao sasa wamekuwa Waislamu, yalikuwa ya kuchukiza sana. Wao (Ansari) walikuwa wamewaua wengi wao katika vita vya Kiislam. Kama Dola ya Madina ambayo iliimarika kwa msaada wao, ikawa kamwe imetekwa na watoto wa wale wapagani ambao wao Ansari waliwaua, watawatendea vipi hao Ansari, lilikuwa ndio swali lisilotamkika lililo ndani ya moyo wa kila Ansari. Matukio yalithibitisha kwamba hofu yao haikuzalika kutokana na ndoto yoyote ile.

Bani Umayya walipigana kwa chuki sana dhidi ya Uislamu na Mtume Wake. Wakati Mtume (s.a.w.) alipoiteka Makka, wao "walisilimu" kwa sababu hakukuwa na chochote cha kufanya tena. Kama ilivyoelezwa kabla, Mtume (s.a.w.) hakuwapa kamwe nafasi yoyote ya madaraka ingawa aliwapa sehemu kubwa kutoka kwenye ngawira ya vita ya Hunayn. Kwa upande wake yeye, ilikuwa ni kitendo cha ishara ya mapatano lakini

335

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

haikupunguza uadui wao kwa Uislamu.

Lakini Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.w.t.) hakuwa amekufa kwa muda mrefu wakati Abu Bakr alipowainua hawa maadui wa jadi wa Uislamu, na maadui wa kiukoo wa Mtume wake (s.a.w.), kwenye vyeo vikubwa ndani ya jeshi. Alimfanya Yazid, mtoto wa Abu Sufyan, kuwa jenerali katika jeshi lake. Wakati Syria ilipotekwa, Umar ambaye alim-rithi Abu Bakr kama khalifa, alimfanya huyo Yazid kuwa gavana wa kwanza huko. Yazid alikufa miaka michache baadae ambapo Umar akamfanya mdogo wake, Mu'awiyyah, kuwa gavana mpya wa Syria. Kana kwamba alikuwa hajafanya ya kutosha kwa Bani Umayya, Umar, akiwa kwenye kitanda cha mauti yake, aliitengeneza hali katika namna ambayo ilihakikisha urithi wa Uthman, Bani Umayya mwingine. Katika ukhalifa wa Uthman, watu wa ukoo wake, Bani Umayya, walikuwa wakitawala kila jimbo katika himaya hiyo na walikuwa wakiongoza kila idara katika jeshi.

Ansari walihofia pia kwamba kama Muhajirina wataitwaa Dola ya Madina, basi wao (Muhajirina) wataidhalilisha misaada yao Ansari kwa Uislamu, na watawashusha kutekeleza wajibu, kama utakuwepo wowote, mdogo sana ndani ya Uislamu.

Kwa kujaaliwa na ujuzi wa kubashiri hali ya mambo kama walivyokuwa, Ansari walifanya uchambuzi sahihi na wa kweli wa hali hiyo. Mkusanyiko wao pale Saqifah ulikuwa moja kwa moja ni wa asili ya kujilinda. Ulichochewa na hisia tu za kupona. Lakini kwa bahati mbaya, waling'ang'ania husuda yao wenyewe. Husuda yao ilisababisha malengo yao yasi-fanikiwe. Tabaka zao za kikabila - Aus na Khazraji - zilitiliana shaka, na ilikuwa ni shaka hii ambayo iliwafichua kwa Muhajirina.

Kama ilivyokwisha kuelezwa, kitendo kile cha Ansari cha kukusanyika pale Saqifah kinaleta wasiwasi, lakini hisia yao ilikuwa na maana. Matukio ya baadae yalithibitisha vyakulitosha kwamba walikuwa sahihi na walikuwa na sababu ya kuhoji nia za Muhajirina juu yao. Miongoni mwa Muhajirina, mlinzi pekee wa maslahi yao alikuwa ni Ali ibn Abi Talib. Lakini pale Maquraishi walipofanikiwa katika kumpinga asiingie madarakani, wal-ifanikiwa pia katika kuwateremsha hadhi hao Ansari mpaka kwenye hali ya watu wa kawaida tu.

Muhammad (s.a.w.) alipokufa, na urithi wa Ali kuzuiwa, Ansari walikoma kuwa mabwana nyumbani kwao wenyewe - Madina!

336

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kugombea Madaraka - 3

Saqifah Banu Sa'ida

Bukhari amemnukuu Umar bin al-Khattab akisema:

"Wakati yeye (Mtume (s.a.w.) alipofariki, Maansari walitupinga sisi. Walijikusanya ndani ya Saqifah Banu Sa'ida. Ali, Zubayr na marafiki zao pia walitupinga."

Ni nini hicho ambacho Umar na marafiki zake walichokuwa wakikifanya, na ambacho Maansari walikipinga?

Wakati Mtume (s.a.w.) alipofariki, Maansari, siku zote wakiwa wepesi kuhisi mikondo ya kichinichini ya kisiasa, na wenye hofu na tamaa na dhamira za Muhajirina, walijikusanya katika ukumbi nje ya Madina unaoitwa Saqifah, na walimwambia Saad ibn Ubada, kion-gozi wao, kile walichokijua juu ya mipango ya Muhajirina. Saad alikuwa mgonjwa na akamwambia mwanae, Qays, kwamba yeye alikuwa hakujihisi kuwa na nguvu za kutosha kuhutubia huo mkutano, na kwamba atamweleza alichotaka kukisema, na yeye Qays akakirudie kwa waliohudhuria.

Saad akaongea na mwanae, naye akafikisha maana yake kwa Ansari.

Hotuba ya Saad

"Enyi kundi la Ansari! Mnao umuhimu katika Uislamu ambao hakuna mtu anayeweza kuukataa, na hili peke yake linakufanyeni ninyi kuwa kitu maalum katika Arabia yote. Mtume wa Allah (s.a.w) alihubiri Uislamu miongoni mwa watu wake mwenyewe kwa miaka 13 na ni wachache wao tu walioukubali ujumbe wake. Walikuwa wanyonge sana kiasi kwamba walikuwa hawana uwezo wa kumlinda yeye au kutetea Uislamu. Allah (s.w.t.) katika baraka Zake alipendelea kuweka heshima ya kumlinda Muhammad (s.a.w.) juu yenu. Alikuchagueni ninyi mbali na watu wengine kutoa hifadhi kwa Mtume Wake na Waislamu wengine kutoka Makka. Aliridhia kuuimarisha Uislamu kupitia kwenu ili kwamba mpigane na maadui wa dini Yake. Mmemlinda Mtume Wake kutokana na maadui zake mpaka ujumbe wa Uislamu ukaenea katika Arabia yote. Kupitia panga zenu ameiteka Arabia kwa ajili ya Uislamu, na ilikuwa ni kwa kupitia panga zenu kwamba wapagani wote walishindwa. Kisha wakati ukafika ambapo Mtume wa Allah (s.a.w) aliiaga dunia hii; alikuwa radhi juu yenu alipokuwa akienda mbele za Mola wake. Kwa hiyo, baada ya kifo chake, ni haki yenu kuitawala Arabia."

337

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ansari walionyesha makubaliano ya pamoja na Saad, na wakaongeza kwamba kwa maoni yao, hapakuwepo na mtu aliyestahili zaidi yake kuwa mtawala wa Waislamu wote.

Ilikuwa ni wakati huu ambapo Abu Bakr, Umar na Abu Ubaidah ibn al-Jarrah, waliwasili ndani ya Saqifah. Pale Ansari walipowaona, mmoja wao - Thabit bin Qays - akasimama na kuwaambia kama ifuatavyo:

"Sisi ni waja wa Mungu, na ni wanusuru wa Mtume Wake (s.a.w.). Na ninyi, wakim-bizi kutoka Makka, ni watu wachache tu. Lakini tunajua kwamba mnataka kuiteka Dola ya Madina, na mnataka kutuondoa sisi humo."

(Tabari na Ibn Athir)

Hii ni kauli yenye kufichua. Ina maana kwamba Muhajirina walikuwa wanapanga mipan-go ya kupora mamlaka, na ule mkusanyiko wa Ansari mle Saqifah ulikuwa ni jibu tu la mwanzo wa jambo lao.

Wakati Thabit bin Qays alipofanya ufichuzi huu, hakuna hata mmoja kati ya Muhajirina hawa watatu aliyempinga. Umar anasema kwamba pale Thabit bin Qays alipokaa chini, yeye alisimama na kuongea kitu kinachofaa. "Nilikuwa nimeandaa hotuba nzuri sana niki-tarajia tu jambo kama hili," alisema. (Tarikh-ul- Khulafa).

Huku ni kukubali kwa Umar mwenyewe kwamba alikuwa amefanya maandalizi yaliy-ochanganuliwa kabla kukabiliana na dharura yoyote ile. Lakini Abu Bakr alimzuia, na yeye mwenyewe akasimama kuwahutubia Ansari.

Alisema:

"Hakuna shaka kwamba Allah (s.w.t.) alimtuma Muhammad (s.a.w.) na Imani ya kweli na nuru ya dini Yake. Yeye (Muhammad) kwa hiyo, aliwaita watu kwenye dini ya Allah (s.w.t.) Tulikuwa wa kwanza kuitikia wito wake. Tulikuwa wa kwanza kuukubali Uislamu. Yeyote aliyesilimu baada yetu sisi, alifuata kutangulia kwetu. Zaidi ya hayo, sisi tuna uhusiano na Mtume wa Allah (s.a.w.w), na sisi ndio wenye sharafu kubwa zaidi ya Waarabu wote kwa damu na nchi. Hakuna kabila lisilotambua mamlaka ya Maquraishi, na nyie, Maansari, ndio mliotoa hifadhi na mliosaidia. Nyinyi ni ndugu zetu katika imani. Tunawapenda na kuwathamini ninyi kuliko watu wengine. Lakini viongozi lazima wawe wanatoka kwa Maquraishi. Sisi tutakuwa ndio watawala na nyie mtakuwa mawaziri. Msione wivu juu yetu. Mmetusaidia sisi huko nyuma, na sasa hampaswi kuwa wa kwanza kutupinga sisi. Ninawaombeni mtoe viapo vyenu vya utii kwa mmoja wa hawa watu wawili, Umar au Abu Ubaidah. Nimewateua wote wawili kwa sababu hii; wote wanastahili heshima hii, na wote wana sifa zinazafaa kwa cheo cha Amir."

338

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Muhammad Husein Haikal:

"Umar na Abu Bakr walikuja kwenye uwanja wa Saqifah. Wakifuatiwa na idadi ya Muhajirina, walikalia viti vyao katika mkutano huo. Mara, mzungumzaji akasimama na kuwahutubia Ansari kama ifuatavyo: "Sifa zote na shukrani ni zake Allah (s.w.t.) Sisi ni Ansari, yaani Wasaidizi wa Allah (s.w.t.) na sisi ni jeshi la Uislamu. Ninyi, Muhajirina, ni watu wachache tu katika jeshi hilo. Hata hivyo, mnajaribu kutun-yang'anya sisi haki yetu ya uongozi."

Kwa kweli, kwa Ansari, lilikuwa ni lalamiko la siku nyingi, hata katika wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.). Sasa pale Umar alipolisikia tena, alichukia sana, na alikuwa tayari kulikomesha kwa upanga kama ikibidi kuwa lazima. Lakini Abu Bakr alimzuia na akamuomba kuwa muungwana. Yeye kisha akawageukia Ansari na akasema: "Enyi Ansari! Tunayo jadi na kizazi kitukufu sana. Sisi ndio tunaoheshimiwa sana na kutukuzwa mno na vilevile ndio tulio wengi sana katika kundi lolote ndani ya Arabia. Zaidi ya hayo, sisi ndio ndugu wa damu wa karibu sana wa Mtume (s.a.w.). Qur'an yenyewe imetoa upendeleo kwetu sisi. Kwani ni Allah (s.w.t.) Mwenyewe - Yeye ashukuriwe na atukuzwe - Ambaye amesema, Wa kwanza kabisa walikuwa ni Muhajirina, kisha Ansari, na kisha wale waliowafuata hay a makundi mawili katika wema na uadilifu. Sisi ndio wa kwanza kuhama kwa ajili ya Allah (s.w.t.) na ninyi ni Ansari, yaani, Wenye kunusuru. Hata hivyo, ninyi ni ndugu zetu katika imani, wen-zetu katika vita, na wanusuru wetu dhidi ya maadui. Yote mazuri mliyodai juu yenu ni ya kweli, kwani ninyi ndio wabora zaidi wa wanadamu. Lakini Waarabu hawataukubali uongozi wa kabila lolote isipokuwa la Quraishi. Kwa hiyo, sisi tutakuwa ndio viongozi, na nyie mtakuwa mawaziri wetu." Kufikia hapa Ansari mmoja akasimama na akasema: "Kila uamuzi utategemea juu yetu sisi. Na uamuzi wetu sisi ni kwamba mnaweza kuwa na kiongozi wenu; sisi tutakuwa na wa kwetu." Lakini Abu Bakr akasema kwamba kiongozi wa Waislamu lazima atokane na Quraish, na mawaziri kutokana na Ansari. Kufikia hapa aliishika mikono ya Umar na Abu Ubaidah na akasema: "Yeyote kati ya hawa watu wawili anazo sifa za kuwa kiongozi wa Waislamu. Chagueni mmoja kati yao."

(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Lakini Umar alisimama na akasema kwa kupinga: "Ewe Abu Bakr, sio sahihi kwa mtu yeyote kupewa nafasi ya kwanza juu yako we we kwa sababu we we ndio mbora wetu sisi sote.Wewe ulikuwa 'sahaba wa kwenye pango,' na wewe ndiye 'wa pili katika wawili.' Na kuna yeyote aliyesahau kwamba Mtume (s.a.w.) alikuamuru kuongoza Swala wakati alipokuwa mgonjwa? Kwa hiyo, wewe ndiye mtu anayestahili zaidi kuwa mrithi wake."

339

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ansari mwingine alisimama kuwajibu Abu Bakr na Umar, na akasema: "Tunatambua kutangulia kwenu katika Uislamu na sifa zenu nyingine, na tunawapenda pia. Lakini tunao wasiwasi kwamba baada yako, watu wengine wataitwaa serikali, na hawatakuwa wema na waadilifu kwetu. Kwa hiyo, tunashauri kwamba wawepo watawala wawili, mmoja Muhajir na mwingine Ansari (huu ulikuwa ufichuaji mbaya wa kwanza upande wa Ansari wa udhaifu wao wenyewe). Kama huyo Muhajir akifariki, nafasi yake ichukuliwe na Muhajir, na kama huyo Ansari akifariki, nafasi yake ichukuliwe na Ansari mwingine. Kama mkiukubali mpango huu, tutakupeni kiapo chetu cha utii. Huu ndio utaratibu mzuri ambao unaweza kufanywa kwa sababu kama Quraishi anakuwa ndio kiongozi pekee wa dola, Ansari wataishi kwa hofu, na kama Ansari anakuwa Khalifa, Maquraishi wangeishi kwa hofu."

Abu Bakr akazungumza kujibu hivi:

"Allah (s.w.t.) alimtuma Muhammad (s.a.w.) na Kitabu Chake kwa wanadamu. Wakati huo kila mmoja alikuwa akiabudu masanamu. Muhammad alipowaambia wayabomoe masana-mu hayo, wao walilichukia hilo. Hawakutaka kuyatelekeza. Kwa hiyo, Allah (s.w.t.) akawachagua Muhajirina kushuhudia Utume wa Muhammad (s.a.w.). Waarabu waliobakia waliwatukana na kuwatesa Muhajirin, lakini walikuwa imara katika msaada wao kwake. Walikuwa wa kwanza kumuabudu Allah (s.w.t.) na walikuwa wa kwanza kumtii Mtume Wake. Wana uhusiano naye, na wao ni ndugu zake. Kwa hiyo, wao peke yao wanastahili kuwa warithi wake, na hakuna mtu atakayewapinga katika hili isipokuwa madhalimu.

Nanyi, Enyi Ansari! Ni watu ambao ubora wenu haukanushiki. Hakuna mtu anayeweza kuishinda nafasi yenu ya juu katika Uislamu. Allah (s.w.t.) aliwafanyeni ninyi kuwa wanusuru wa dini Yake na Mtume Wake. Na ilikuwa ni kuelekea kwenu ambako alihamia. Kwa hiyo, cheo chenu katika Uislamu ni cha juu kabisa baada ya Muhajirin. Tunakupendeni na kukutukuzeni ninyi. Lakini inastahili tu kwamba vion-gozi watoke kwa Muhajirin na mawaziri kutoka kwa Ansari. Chochote tukachoki-fanya, tutakifanya kwa kushauriana nanyi."

Mzungumzaji aliyefuatia alikuwa ni Hubab ibn al-Mundhir wa Madina. Alisema:

"Enyi kundi la Ansari! Watu hawa (Muhajirin) wapo chini ya ulinzi wenu. Hawana mamlaka yoyote ya kuwapinga ninyi. Macho ya Waarabu wote yanakutazameni ninyi, na mnao utanguliaji ule ule katika Uislamu kama walionao. Wallah wao (Muhajirin) kamwe hawakuthubutu kumuabudu Allah (s.w.t.) hadharani mpaka mlipowapa hifadhi katika mji wenu. Hakuna mahali ambapo Swala iliswaliwa wazi-wazi isipokuwa kwenye mji wenu. Waabudu masanamu na washirikina hawakushind-wa ila kwa panga zenu. Kwa hiyo, uongozi ni haki yenu na wala sio yao. Lakini kama hawatakubaliana na hili, basi pawepo na viongozi wawili, mmoja kutoka kila kimoja kati ya vikundi hivi viwili."

340

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Umar alijibu hotuba ya Hubab ibn al-Mundhir kwa kusema: "Haiwezekani kwamba pawepo na wafalme wawili katika falme moja. Waarabu hawataukubali utawala wa mtu yeyote ambaye si wa kabila la Quraishi kwa vile Mtume wa Allah (s.w.t.) mwenyewe alikuwa mtu wa kabila hilo. Khalifa wa Waislamu kwa hiyo, lazima awe ni mtu wa kabila lile lile kama Mtume mwenyewe. Ule ukweli kwamba yeye alikuwa ni Quraish unakamilisha kabisa hoja yote. Sisi ni Maquraishi, na hakuna mtu yeyote atakayeweza kubishana nasi katika wajibu wetu wa uongozi."

Hubab ibn al-Mundhir akasema tena:

"Enyi Ansari! Msimsikilize mtu huyu na wenzie. Ukhalifa ni haki yenu. Uchukueni. Kama hawakubaliani na haki hii, wafukuzeni ndani ya mji wenu. Kisha mnachagua kiongozi kutoka miongoni mwenu wenyewe. Kile mlichokipata kwa panga zenu, msikitoe hicho kwa watu hawa, na kama mtu yoyote ananipinga mimi hivi sasa, nita-mnyamazisha kwa upanga wangu."

Abu Ubaidah ibn al-Jarrah ndipo akasimama, na akasema:

"Enyi kundi la Ansari! Mlikuwa wa kwanza kumsaidia Mtume wa Allah, na kutoa hifadhi kwa dini yake. Je, mtakuwa ninyi wa kwanza sasa kusababisha msambaratiko katika dini ile?"

Mzungumzaji aliyefuatia alikuwa ni Ansari mwingine, ambaye ni Bashir bin Saad. Alijua kwamba Ansari walikuwa wamedhamiria kumchagua Saad ibn Ubada kama kiongozi wa umma wa Kiislam. Alikuwa na chuki na Saad na hakupenda kumuona yeye akiwa mtawala wa Arabia. Kwa hiyo, alichokisema ndani ya Saqifah kili-chochewa, sio na mapenzi na Abu Bakr au wale Muhajirin bali na chuki yake juu ya Saad. Alisema:

"Enyi kundi la Ansari! Bila shaka tuna kipaumbele katika Uislamu, na katika vita vya Kiislam. Lakini kwa vile ni hivyo, tusilazimike kuwa wabinafsi. Nia yetu iwe tu ni kutafuta radhi za Allah (s.w.t.) na kumtii Mtume Wake (s.a.w.). Huduma zetu kwa Uislamu zilikuwa ni kwa ajili ya Allah (s.w.t.) na sio kwa ajili ya manufaa ya dunia, na Yeye atakulipeni kwa ajili hiyo. Kwa hiyo, tusijaribu kuwekeza juu ya huduma hizo sasa. Mtume wa Allah (s.a.w) alitokana na kabila la Quraishi; kwa hiyo, ni haki kwamba warithi wake wawe pia wanatokana na kabila hilohilo. Wanastahili kuwa warithi wake. Ukhalifa ni haki yao na sio yetu, na tusiwapinge katika jambo hili. Kwa hiyo, muogopeni Allah (s.w.t.) na msijaribu kuchukua kisichokuwa chenu."

Hotuba hii ya Bashir bin Saad ilimtia hamasa Abu Bakr ya kusimama mara nyingine tena na kusema:

"Kama nilivyosema kabla, viongozi wawe wanatokana na Quraishi. Kwa hiyo, Enyi Ansari! msisababishe mgawanyiko miongoni mwa Waislamu. Ni ushauri wangu

341

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kwenu kwamba mtoe kiapo cha utii kwa mmoja kati ya watu wawili hawa walioko hapa, Umar na Abu Ubaidah bin al-Jarrah. Wote wawili ni Maquraishi wanaostahili."

Lakini Umar akamwingilia kati akisema, "Inawezekanaje kwamba mtu mwingine yeyote apokee kiapo cha utii wakati wewe upo miongoni mwetu. Wewe ndiye mtu mzima zaidi katika Quraishi, na umetumia muda mwingi zaidi pamoja na Mtume (s.a.w.) kuliko yeyote kati yetu. Kwa hiyo, mtu yeyote asijiweke mwenyewe mbele yako. Nyoosha mkono wako ili nikupe kiapo changu cha utii." Umar aliushika mkono wa Abu Bakr, na akauweka mkono wake juu yake kama ishara ya kiapo. Alikuwa, kwa kitendo hiki, amemthibitisha Abu Bakr kama khalifa. Abu Ubaidah bin al-Jarrah na Bashir bin Saad Ansari pia wakatokea mbele, wakaweka mikono yao juu ya mkono wa Abu Bakr, kiapo chao kwake.

Bashir bin Saad Ansari alikuwa akionyesha shauku sana katika kutoa kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Hubab ibn al-Mundhir aliyekuwa anamtazama, akasema kwa sauti kubwa:

"Ewe Bashir! Wewe ni msaliti kwa watu wako mwenyewe. Tunajua ni kwa nini uliru-ka mbele kuchukua kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Wewe unamchukia Saad ibn Ubadah, wewe haini mnyonge. Ni jinsi gani unavyochukia kumuona yeye akiwa Amir wa Waislamu."

Ilikuwa ni katika wakati huu wa maamuzi ya hatma ambapo wengi wa watu wa mak-abila ya Kibedui ambao waliishi kati ya Madina na Makka walijitokeza uwanjani. Walikuwa na uadui na Ansari, na walikuwa wameingia hapo mjini waliposikia habari za kifo cha Mtume wa Allah (s.a.w.w) Walipong'amua kile kinachopikwa pale Madina, walijitawanya karibu na Saqifah. Kutokeza kwao kwa ghafla kuliongeza nguvu nyingi sana kwenye hamasa ya Abu Bakr na Umar; na kwa wakati huo huo, kulitia mawimbi juu ya uhakika wa Ansari. Watu hawa wa makabila walikuwa wote wana silaha. Kwa kutokea kwao, nguvu ya ushawishi katika ule mjadala mrefu kati ya Muhajirin na Ansari, ikaenda kwa Muhajirin.

G .E . Von Grunebaum:

"Katika kipindi cha vurugu Ansari hatimae walishawishika kutong'ang'ania juu ya urithi kwenda kwa mmoja wa watu wao wenyewe wala juu ya watawala wawili wa Sahaba na Msaidizi, na kwa kiasi fulani chini ya shinikizo kutoka kwa Mabedui ambao walikuwa wanamiminika kuingia ndani ya mji huo, walikubali kufanya heshi-ma kwa Abu Bakr."

(Classical Islam - A History 600 - 1258)

342

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Umar alisema baadae kwamba mpaka walipotokea wale watu wa makabila, alikuwa na mashaka makubwa kuhusu matokeo ya ule mjadala na Ansari. Kutokea kwao katika muda muafaka, na matumizi yao ya shinikizo juu ya Ansari, kulihakikisha makubaliano ya hawa Ansari katika kufika kwa Abu Bakr kwenye kiti.

Hila ya Bashir ilishinda. Aliihujumu ile nia ya - kupigana ya Ansari. Malalamiko ya Saad ibn Ubada na Hubab ibn al-Mundhir hayakuwa na mafanikio yoyote. Wakati Umar, Abu Ubaidah na Bashir walipotoa kiapo cha utii kwa Abu Bakr, wengine wote walifuata kama kondoo. Ansari walikuwa wameshindwa mapambano!

Ufumbuzi wa mafanikio ya Abu Bakr katika kuchaguliwa khalifa hapo Saqifah ulikuwa ni ule uadui wa pamoja wa yale makabila mawili ya Madina ya Aus na Khazraj. Yote yalikuwa yamepigana "Vita vya Miaka Mia Moja" vya wenyewe kwa wenyewe, na walikuwa wamesimamisha uhasama wao kwa sababu tu ya kuchoka kwao kimwili.

G .E . Von Grunebaum:

"Hawa Aus na Khazraj walikuwa hali ya kuendelea katika vita vya msituni dhidi yao kwa vizazi na vizazi. Ugomvi wao ulifikia kwenye kilele cha kumwaga damu mnamo mwaka 617 katika "Vita vya Bu'ath," ambavyo baada yake wahusika wakuu walicho-ka sana kiasi kwamba ilififia mpaka kwenye mapatano ya kusimamisha vita, yaki-ingiliwa tu na vitendo vya kisasi vya mara kwa mara.

(Classical Islam - A History 600 - 1258)

Vita vya mwisho vikubwa kati ya Aus na Khazraj vilikuwa vimepiganwa miaka minne tu kabla ya kutokea kwa Mtume (s.a.w.) hapo Madina kama Mpatanishi. Mara tu wote walipomkubali yeye kama kiongozi wao, walikubaliana pia kuridhia kwenye maamuzi yake katika migogoro yao yote, na walifanya makubaliano ya kusitisha mapambano kwenye vita vyao visivyokwisha. Lakini mara tu yule Mpatanishi na hakimu alipokufa, chuki zao za zamani, hofu na wasiwasi viliwaka moto tena. Pale viongozi wa Aus walipoona kwamba Khazraj walikuwa wamemtoa Saad ibn Ubada - Mkhazraji - kama mgombea wa ukhalifa, walifikiria kwamba kama atachaguliwa kuwa khalifa, basi wao -Aus - watashushwa mpaka kwenye hadhi ya utwana kwa wakati wote. Maslahi yao, waliona, yatalindwa vema kama kiongozi wa umma angekuwa ni Muhajir kutoka Makka badala ya Khazraj wa Madina. Wao kwa hiyo, wakaharakisha kumhakikishia Abu Bakr kwamba walikuwa watiifu kwake kabla Khazraj hawajaweza kumtangaza Saad ibn Ubadah kama mkuu mpya wa Madina. Ilikuwa kwa hiyo ni Aus wa Madina ambao walikuwa hasa wamesaidia katika kupatikana kwa mafanikio ya Abu Bakr katika kuchaguliwa kwake kama khalifa. Vipengele vingine, kama vile usaliti wa Bashir bin Saad, mwenyewe akiwa Khazraj, kwa kabila lake mwenyewe, la Khazraj; na uingiliaji wa watu wa kabila la Kibedui katika wakati mgumu, pia vilichangia mafanikio ya Abu Bakr.

343

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Maxime Rodinson:

"Watu wa Madina, hususan wale wa kabila la Khazraj, walihisi kwamba Wahamiaji wa Kiquraishi ambao walikuwa wamekuja pamoja na Muhammad (s.a.w.) ambao walikuwa siku zote wakiwaonea wivu, sasa watajaribu kudai uongozi juu yao wenyewe. Mtume (s.a.w.) alikuwa amekufa. Hapakuwa na sababu tena ya kuendelea kuwatii hawa wageni. Waliitisha mkutano katika ukumbi wa moja kati ya koo zao -Banu Sa 'ida, kuzungumzia njia bora ya kulinda maslahi yao. Walichoshauri kufanya kilikuwa ni kuchagua mmoja wa watu wao maarufu, Sa'd ibn Ubadah, kama Kiongozi mpya wa Madina.

Abi Bakr alikuwa katika nyumba ya Muhammad (s.a.w.), alidokezwa juu ya hili na akakimbilia kwenye sehemu hiyo pamoja na wanasiasa wenzie, Umar na Abu Ubaidah. Waliungana humo njiani na kiongozi mwingine wa kabila jingine la Madina, la Aus, mahasimu wa Khazraj. Jambo la mwisho kabisa walilotaka lilikuwa ni kuona madaraka yakiwa kwenye mikono ya Khazraj. Mitaani humo msisimko ulikuwa unaenea kwa watu wa makabila mengine ya Madina, ambao walikuwa hawana tamaa ya kushika nafasi ya ukibaraka katika mchezo wowote wa madaraka ambao ulikuwa karibu uanze. Usiku ulipoingia, kila mtu alikuwa amesahau ule mwili (wa Mtume (s.a.w.)) uliokuwa bado umelala katika kibanda kidogo cha Aishah (ingawa - la kibanda - si sahihi).

Majadiliano yaliyoendelea kwa mwanga wa tochi na taa za mafuta, yalikuwa marefu, makali na yenye rabsha. Mtu mmoja wa Madina alishauri kwamba wangechaguliwa viongozi wawili, mmoja Quraishi na mmoja wa Madina. Watu wengi walitambua kwamba hiyo itakuwa ni njia ya kukaribisha ugomvi na balaa juu ya jamii. Kila mmoja alikuwa anapiga kelele kwa wakati mmoja; wangeweza hata kufikia kupi-gana."

(Muhammad, tafsiri ya Ann Carter, 1971)

Walifikia kupigana. Saad ibn Ubadah alimkamata Umar kwenye ndevu zake. Umar ali-tishia kumuua yeye kama angeng'oa unywele mmoja toka kwenye ndevu zake. Umar akamwambia Hubab ibn al-Mundhir: "Allah akuuwe wewe," naye huyu akamwambia: "Allah akuuwe wewe."

Hubab ibn al-Mundhir alifanya juhudi kubwa kuokoa hali hiyo. Alipojaribu kuwazuia Ansari kutoa kiapo cha utii kwa Abu Bakr, kundi moja likamvamia, likampokonya upan-ga wake, na likamsogeza pembeni. Walikuwa ni Mabedui wanaowaunga mkono Muhajirin. Hubab alikosa upanga wake lakini bado alizipiga nyuso za wakazi wa Madina ambao walikuwa wakitoa kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Aliwalaani na kusema: "Enyi Ansari! Naweza kuona kwa macho yangu mwenyewe kwamba watoto wenu wanaomba chakula kwenye milango ya nyumba za hawa watu wa Makka lakini badala ya kupata chakula wanapigwa kwenye meno na watu hawa, na wanafukuzwa."

344

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Abu Bakr akamuuliza Hubab: "Unawazia hofu kama hizo kutoka kwangu mimi?" Akasema: "La. Sio kutoka kwako bali kutoka kwa wale watakaokuja baada yako." Akijaribu kumhakikishia, Abu Bakr akasema: "Kama hilo likitokea, mnaweza wakati wote kukana kiapo chenu kwa makhalifa wenu." Yeye kwa uchungu akajibu kwa ukali sana: "Itakuwa tumekwisha kuchelewa sana wakati huo, na haitasaidia chochote."

Ulikuwa ni mkutano huu wa fujo, wa kiajabu ajabu na usio na mpangilio, wa ndani ya ukumbi wa Saqifah ambao ulimchagua Abu Bakr kama khalifa. Ansari hawakuridhika sana na kuchaguliwa kwake. Wao kwa hali yoyote ile, hawakuteua mtu anayestahiki-sana. Umar kwa ustadi sana aliliweka kando suala la sifa-stahilifu, na kamwe hakuliruhusu liibuke ndani ya mjadala huo. Suala la sifa za mgombea lilifunikwa chini ya wingu la ufasaha wa kukwepa kwepa.

Saad ibn Ubadah, kiongozi wa Khazraj, na "mshindi wa pili" ndani ya Saqifah ambamo mbinu-zote-zinakubaliwa na huru kwa watu wote, alikuwa mmoja wa wale watu ambao walikataa kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Alimwambia Abu Bakr: "Ewe Abu Bakr! Kama nisingekuwa kwenye hali hii ya kutokujiweza kwa sababu ya maradhi yanayonid-hoofisha, ningekurudisheni Makka wewe na marafiki zako, kwa ndugu zenu wenyewe." Saad kisha akawaomba marafiki zake wamtoe nje ya Saqifah. Kwa muda fulani Abu Bakr hakumuingilia yeye, na kisha siku moja akamtumia ujumbe akimtaka aje kutoa kiapo cha utii. Saad akakataa. Umar akamshinikiza Abu Bakr achukue kiapo chake kwa nguvu. Lakini Bashir bin Saad Ansari akaingilia kati kwa kusema: "Saad akiwa amekwisha kataa, kamwe hatokupeni kiapo chake cha utii. Kama mkimlazimisha yeye, inaweza kusababisha umwagaji wa damu, na watu wa Khazraj wote watasimama pamoja naye dhidi yako. Kwa maoni yangu mimi, haitakuwa busara kulazimisha jambo hili. Yeye, hata hivyo, ni mtu mmoja tu, na akiachwa alivyo, hawezi kufanya madhara yoyote kwa namna yoyote ile."

Wale watu wote waliokuwepo kwenye lile baraza la khalifa, waliyaunga mkono maoni ya Bashir, na Saad aliachwa kwa amani. Alipona maradhi yake, na miaka mitatu baadae, aka-hama kwenda Syria.

Maandishi ya hotuba zilizotolewa pale Saqifah, na maelezo juu ya matukio yaliyotokea pale, yamechukuliwa kutoka kwenye vitabu vifuatavyo:

1.  Tarikh - Tabari

2.  Tarikh al-Kamil - Ibn Athir

3. Kitab-al-Imama was-Siyasa - Ibn Qutayba Dinwari

4.  Siraat-ul-Halabiyya - Halaby

345

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kugombea Madaraka 4

Wakati Abu Bakr alipokubaliwa kuwa khalifa pale saqifah, yeye, Umar bin al-Khattab na Abu Ubaidah bin al-Jarrah walirudi kwenye Msikiti wa Mtume (s.a.w.). Ndani ya Msikiti mlikuwa na watu wengi, miongoni mwao, watu wa ukoo wa Bani Umayya; Saad bin Abi Waqqas; Abdur Rahman bin Auf; na baadhi ya Muhajirina wengine.

Alipowaona wamekutana faragha kwenye kundi moja. Umar alisema kwa sauti: "Abu Bakr amechaguliwa kuwa khalifa wa Waislamu. Sasa nyie wote hapa mpeni kiapo cha utii. Ansari, Abu Ubaidah na mimi tayari tumekwisha fanya hivyo."

Bani Umayya waliokuwepo mle ndani ya Msikiti walikuwa wa kwanza kuitika mwito wa Umar, na kuchukua kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Saad ibn Abi Waqqas, Abdur Rahman bin Auf na wengineo waliwafuatia hao, na wakachukua kiapo cha utii kwa Abu Bakr.

Takriban "mamwinyi" wote walichukua kiapo cha utii kwa Abu Bakr siku ya Jumatatu. Wale "watu wa kawaida" hawakujua kuhusu kuchaguliwa kwa Abu Bakr bado. Walikuja pale Msikitini siku ya Jumanne. Kutwa nzima walikuwa wakija na kuingia na kutoka nje ya Msikiti, na Abu Bakr alikuwa akishughulika kupokea viapo vyao vya utii kwake. Ilikuwa tu siku ya Jumatano ambapo hatimae alikuwa huru kushughulikia mambo mengine.

Wakati huohuo, muda wote wa kinyang'anyiro kikali cha madaraka ndani ya Saqifah, na baadae, Ali ibn Abi Talib na watu Bani Hashim, walikuwa wakishughulikia mazishi ya Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.). Pale Mtume alipokuwa amekwishafanyiwa mazishi, Ali na Bani Hashim walirudi majumbani kwao.

Watu wengi hapo Madina walikuwa wamekwisha kuchukua kiapo cha utii kwa Abu Bakr lakini walikuwepo wengine ambao walikuwa bado. Muhimu sana miongoni mwao wote alikuwa ni Ali ibn Abi Talib, kiongozi mpya wa ukoo wa Bani Hashim. Khalifa mpya na washauri wake waliamini kwamba ilikuwa ni muhimu sana kwamba Ali achukue kiapo cha utii sawa na watu wengine. Wao, kwa hiyo, walituma aitwe kutoka nyumbani kwake lakini alikataa kuja. Kukataa kwake kulimkasirisha Umar. Mapema kidogo, alikuwa mtu mwenye kuathiri uteuzi, lakini sasa amekuwa Mtendaji Mkuu wa serikali mpya ya Saqifah. Yeye, kwa hiyo, alikwenda pamoja na wasindikizaji wenye silaha kutekeleza amri za serikali, na akatishia kuichoma nyumba ya binti ya Muhammad Mtume wa Allah (s.a.w.), kama Ali asingekuja kwenye baraza kuchukua kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Mtu mmoja alikumbusha kwamba nyumba ile ilikuwa ni mali ya binti ya Mtume (s.a.w.), hivyo Umar angewezaje kuichoma. Lakini Umar akasema haidhuru kama nyumba hiyo ilikuwa ni ya mtoto wa Mtume (s.a.w.). Kilichokuwa na umuhimu hasa, alisisitiza, ni kiapo cha utii

346

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ambacho Ali alipaswa akichukue. Edward Gibbon:

"Bani Hashim peke yao walikataa kiapo cha utii (kwa Abu Bakr); na kiongozi wao (Ali), katika nyumba yake mwenyewe, alidumisha zaidi ya miezi sita (ingawa sio kweli), kimya kizito na cha upweke, bila ya kupatiliza vitisho vya Umar, ambaye ali-jaribu kuyachoma kwa moto makazi ya binti ya Mtume (s.a.w.)."

(The Decline and Fall of the Roman Empire)

Hata mtu kama Shibli, mwandishi wa wasifu wa Umar, na mmoja wa washabiki wake wakubwa sana, amelazimika kukubali kwamba "Umar alikuwa mtu mwenye hasira mbaya sana, na haishangazi kabisa kama alifanya jaribio la kuchoma moto nyumba ya binti ya Mtume (s.a.w.)." - (Al-Faruuq)

Uzuri ulioje, utamu ulioje, na ujasiri ulioje wa Umar kujaribu kuchoma nyumba ya Fatima Zahra! Siku tatu baada ya kifo cha Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Mwisho wa Allah (s.a.w.w) kwa wanadamu, Umar alifika mlangoni mwa nyumba ya Fatima Zahra. Kundi lingine la wachomaji moto mali wa maksudi lilikuwa pamoja naye, na alidai kiapo cha utii cha Ali kwa Abu Bakr.

Uonyeshaji huu wa "ushujaa" lazima utakuwa "umemfurahisha" sana Allah (s.w.t.) hasa, pale mtu anapokumbuka kwamba mbali na Ali na Fatima, walikuwemo pia ndani ya nyumba yao, watoto wao wadogo wanne - wajukuu wa Muhammad Mustafa (s.a.w.). Walipishana kwa umri kutoka miaka miwili hadi nane. Watoto hao lazima watakuwa "wal-isisimka" kusikia sauti ya Umar. Kwao wao, lazima alikuwa kama mfano wa "Santa Claus," (Baba Chrismas) - Santa Claus huyo wa jangwani, akiwa amesimama mlangoni mwa nyumba yao akiwa na "zawadi" ya moto kwa ajili yao. "Zawadi" yake, huenda atakuwa amewaeleza, ilikuwa na nguvu ya kubadili zile kuta za kijivu zisizovutia za nyumba yao ndogo kuwa ndimi za moto zinazoruka na kualika alika zenye rangi nyingi.

Kipi tena angewafanyia hao ili "kuwaliwaza" na "kuwafariji" baada ya kifo cha babu yao, Muhammad (s.a.w.), ambaye alikuwa akiwapenda sana? Hivi wamekwishawahi kamwe kuona kioja cha "fataki" yenye kumeremeta kupita kiasi kama hicho anachoweza kuwaonyesha punde hivi tu kama baba yao, Ali ibn Abi Talib, hakuchukua kiapo cha utii kwa Abu Bakr?

Kwa wakati huu, Zubayr ibn al-Awam alikuwa pia pamoja na Ali. Mke wake alikuwa mmoja wa mabinti wa Abu Bakr lakini mama yake yeye alikuwa ni Safiyah bint Abdul Muttalib, shangazi yake Muhammad (s.a.w.) na Ali. Yeye, kwa hiyo, alidai kwamba na

347

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

yeye pia alikuwa mtu wa ukoo wa Bani Hashim. Umar alimuamuru kuchukua kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Lakini alikataa na kutishia kutumia upanga wake kama atasumbuliwa sana. Umar aliwakemea vibaraka wake wanyakue upanga wake. Walifanikiwa katika kumzidi nguvu. Alinyang'anywa silaha, na akapelekwa kwenye baraza la baba-mkwe wake. Ilikuwa ni katika hali hii kwamba alitoa kiapo chake cha utii kwake.

Umar alijaribu kupata nguvu kwa vitisho, kufoka - kwa kiburi, na udanganyifu. Zamani, mtu alikuwa anaweza kutaja udanganyifu wake lakini sasa ilikuwa haiwezekani kufanya hivyo. Pamoja na Zubayr kumalizwa hivyo, Umar aligeuzia mazingatio yake kwa Ali, na alipelekwa kule kwenye baraza. Humo ndani ya baraza, Umar alirudia dai lake la kiapo lakini Ali akasema:

"Mimi ni mtumwa wa Allah (s.w.t.) na ni ndugu yake Muhammad, Mtume Wake. Mtumwa wa Allah (s.w.t.) hawezi kuwa mtumwa wa mtu mwingine yeyote. Kama mmefanikiwa katika kuiteka serikali ya Muhammad (s.a.w.) kwa sababu ninyi, kama ulivyosema, ninyi mpo karibu zaidi kwake kuliko Ansari, basi mimi ni mdogo wake, na ni nani miongoni mwenu ambaye anaweza kudai kuwa karibu naye zaidi kuliko mimi? Waislamu wote wanapaswa kunipa mimi viapo vyao, na sio mtu mwingine yeyote. Mnainyang'anya familia ya marehemu bwana wenu haki yao. Mliwashawishi Ansari kwa hoja kwamba Mtume wa Allah (s.a.w.w) alikuwa ni mmoja wenu, na hakuwa mmoja wao, na waliuachia ukhalifa kwenu. Sasa naitumia hoja hiyo hiyo -hoja yenu - ambayo mliitumia dhidi ya Ansari. Sisi ndio warithi wa Mtume wa Allah (s.a.w.w) katika uhai wake na baada ya kifo chake. Kama mnauamini ujumbe wake, na kama mmeukubali Uislamu kwa uaminifu, basi msizichukue kwa nguvu haki zetu."

Umar alimjibu hivi:

"Wewe ni mtumwa wa Allah (s.w.t.) lakini sio ndugu yake Mtume Wake (s.a.w.). Kwa hali yoyote, itakubidi utoe kiapo cha utii kwa Abu Bakr, na hatutakuachia hapa mpaka umefanya hivyo."

Ali akasema:

"Ewe Umar! Kama unatetea suala la Abu Bakr kwa shauku kubwa namna hiyo, hilo linaeleweka. Leo unamfanya mfalme ili kwamba kesho akufanye wewe kuwa mfalme. Mimi sitafanya kile unachonitaka nifanye, na sitampa kiapo changu."

Abu Ubaidah ibn al-Jarrah alikuwa mwanachama wa "kundi la watu watatu" (troika), na kwa hiyo, alikuwa wakili mkali wa serikali ya Saqifah. Yeye pia alifanya jaribio la kumshawishi Ali kuitambua ile serikali mpya, na kuchukua kiapo cha utii kwa kiongozi wake. Alisema:

"Ewe binamu ya Mtume (s.a.w.)! wewe ni mdogo kuliko watu hawa. Wao ni wakub-

348

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

wa sana kuliko wewe na wanao uzoefu mkubwa kuliko ulionao wewe. Inakubidi uchukue kiapo cha utii kwa Abu Bakr sasa hivi, na kisha, siku isiyo na jina, zamu yako inaweza kuja pia. Unastahili kuwa kiongozi wa Waislamu kwa sababu ya utan-guliaji wako kwenye Uislamu, ushujaa wako, ujuzi wako, elimu yako, na utumishi wako kwenye Uislamu. Na kisha wewe ni mkwe wa Mtume wetu."

Ali alimjibu kama ifuatavyo:

"Enyi Muhajirin! Msiyatoe madaraka na mamlaka ya Mtume wa Allah (s.a.w.w) nje ya nyumba yake kwenda kwenye majumba yenu. Wallahi, urithi wa Muhammad (s.a.w.) ni haki yetu sisi. Yeye mwenyewe alitoa tamko hili, na sio mara moja bali mara nyingi tu. Hivi yupo mtu kati yenu ambaye ana ujuzi mzuri na uelewa wa Qur'an kuliko nilionao mimi? Yupo yeyote miongoni mwenu ambaye anayo elimu nzuri ya vitendo na Hadith za Mtume wa Allah (s.a.w.w) kuliko niliyonayo mimi? Yupo yeyote kati yenu ambaye anaweza kuiendesha serikali yake vyema kuliko mimi niwezavyo? Kama yupo, mtajeni, na mimi nitamstahi yeye. Lakini hayupo. Ni mimi tu niwezaye kutoa amani ya kweli, ustawi na haki ya kweli kwa Waislamu wote. Kwa hiyo msiangukie kwenye vishawishi vyenu, na msiweke tamaa na mapenzi yenu wenyewe mbele ya amri za Allah (s.w.t.) na Mtume Wake (s.a.w.). Na kama mkifanya hivyo, mtapotoka kwenye Haki, na mtaangukia kwenye Upotovu."

Bashir bin Saad, yule yule aliyekuwa Ansari wa kwanza kuchukua kiapo cha utii kwa Abu Bakr ndani ya Saqifah, alikatisha hotuba ya Ali, na akasema:

"Ewe Ali! Kama ungetuambia hayo kabla, sisi tusingekuwa tumempa kiapo cha utii mtu yeyote badala yako wewe."

Ali akamwambia:

"Wewe ulikuwa huyajui yote haya? Unachojaribu kushauri ni kwamba kama vile wote nyie mlivyomtelekeza Mtume wa Allah (s.a.w.w) mara tu alipofariki, mimi pia ningemtelekeza, na mimi pia ningeingia Saqifah kugombea ukhalifa pamoja nanyi? Hili nisingeweza kulifanya. Kufanya hivyo kusingestahili kabisa kwangu mimi. Nisingeweza kumtoroka Mtume wa Allah (s.a.w) katika kufa kwake kama nisivyomtoroka wakati wa uhai wake."

Baada ya maelezo haya, Ali alitoka kwenye baraza ya Abu Bakr iliyokuwa imeendeshwa kwenye Msikiti wa Mtume (s.a.w.). Hizo ndizo zilikuwa mbinu za kuchaguliwa kwa Abu Bakr kama khalifa wa Waislamu - mfululizo wa ufaraguzi wa kuwa tayari kufanya lolote, na mara nyingi wenye misukosuko. Wakati wa kuchukua viapo kwa faragha ndani ya Saqifah, na vile vya hadhara ndani ya

349

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Msikiti wa Mtume (s.a.w.), kulipokamilika, Abu Bakr, khalifa mpya, akatoa hotuba yake ya uzinduzi. Baada ya kumshukuru Allah (s.w.t.) na kumtukuza, alisema:

"Enyi Waislamu! wale kati yenu waliokuwa wakimwabudu Muhammad, basi nawa-jue kwamba amekufa; lakini wale kati yenu waliokuwa wakimwabudu Allah (s.w.t.) nawajue kwamba Yeye yuko Hai, na hatakufa kamwe.

Enyi Waislamu! Ingawa mmenichagua mimi kama kiongozi wenu, mimi sio mbora sana miongoni mwenu. Kama mtu mwingine angechukua dhima ya mzigo huu ambao mmenitwisha mimi, ingekuwa bora sana kwangu. Kama mnanitegemea niwatawale kama vile tu Mtume wa Allah (s.a.w) alivyofanya, basi lazima niwaambie kwamba hiyo haiwezekani. Mtume (s.a.w.) alipokea Wahy kutoka Mbingnii, na alikuwa asiyetekosea (maasum) ambapo mimi ni mtu wa kawaida tu. Mimi sio bora kuliko ninyi. Kwa hiyo, kama mkiniona ninakwenda katika njia iliyonyooka, nifuateni; lakini kama mnaniona nikiikengeuka, nishutumuni. Kama nikifanya sawa, niungeni mkono; kama nikifanya makosa, nisahihisheni. Nitiini mimi pale tu nitakapokuwa ninamtii Allah (s.w.t.) na Mtume Wake (s.a.w.). Lakini kama mkiniona ninawakiuka wao, nanyi pia mniepuke.

Mnayo Qur'an pamoja nanyi, na imekamilika. Mtume wa Allah (s.a.w) amekuonyesheni kwa maagizo na kwa mifano pia namna ya kujiweka nyie wenyewe katika maisha haya. Mwenye nguvu zaidi miongoni mwenu ni yule anayemuogopa Allah (s.w.t.) Mdhaifu sana miongoni mwenu mbele ya macho yangu ni yule mwenye-dhambi. Taifa linaloacha jihadi, linapoteza hadhi yake. Salini Swala zenu kwa wakati makhsusi, na msizikose. Allah (s.w.t.) awe na huruma juu yenu, na Akusameheni ninyi wote."

Hotuba ya khalifa mpya ilikuwa ni ya maelezo ya malalamiko-binafsi kweli, porojo lisilo na dhamira maalum, isiyotia moyo au umaizi. Kauli ya mwanzo, hata hivyo, ilikuwa na maana. Aliwaambia Waarabu kwamba kama walikuwa wakimuabudu Muhammad (s.a.w.), amekufa! Hivi kuna Waarabu wowote waliomuabudu Muhammad? Kwa miaka 23, Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.a.w) aliyebarikiwa, alikuwa akilifundisha somo la Tauhid (Mungu mmoja) liingie kwenye vichwa vya Waarabu. Ikiwa baada ya juhudi kubwa namna hiyo, walianza kumuabudu yeye badala ya kumuabudu Allah (s.w.t.) basi kazi yake yote kama Mtume, lazima iamuliwe kwamba ilishindwa kabisa.

Lakini ujumbe wa Muhammad (s.a.w.) haukuwa kazi bure. Waislamu walimuabudu Allah (s.w.t.) na hawakumuabudu Muhammad. Wao, kwa hakika, walirudia mara nyingi kwa siku kwamba Muhammad alikuwa ni mtumwa wa Allah (s.w.t.) na Abu Bakr alilijua hili. Hivyo ni kwa nini aliona umuhimu kuwaambia kwamba kama walikuwa wakimuabudu Muhammad, amekufa?

350

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kauli ya Abu Bakr ilikuwa ni hila ya ujanja. Muhammad (s.a.w.) ndio kwanza amefariki, na ilikuwa ni kawaida kwa Waislamu kuwa na huruma kwa watu wa familia yake kwa kuondokewa kwao kukubwa. Lakini Abu Bakr alikuwa na hofu na huruma hii. Aliiona ni ya hatari kwa usalama wake binafsi juu ya ufalme. Kipindi cha maombolezo rasmi kingeweza kuwa cha hatari pia kwake. Yeye, kwa hiyo, alilinganisha maombolezo juu ya kifo cha Muhammad (s.a.w.) na "kumuabudu" Muhammad (s.a.w.), na ni nini kinachoweza kuwa cha kulaumika katika Uislamu kama "kumuabudu" Muhammad - mwanadamu -badala ya kumuabudu Allah (s.w.t.)!

Abu Bakr, kwa njia hii, aligeuza azma ya umma wa Kiislamu mbali na huruma yoyote ambayo ungeweza kuihisi kwa familia inayohuzunika ya Muhammad (s.a.w.).

Waarabu hawakuabudu kitu chochote vizuri zaidi kuliko vipande vya mawe au miti; Muhammad (s.a.w.) aliwafanya wawe wanaomuabudu Allah (s.w.t.) - Muumba mmoja na Mola wa Ulimwengu. Waarabu walikuwa ni wachunga kondoo au maharamia; Muhammad (s.a.w.) akawafanya wafalme na washindi. Waarabu walikuwa washenzi na wajinga; Muhammad (s.a.w) akawafanya taifa lililostaarabika zaidi duniani. Alikuwa ni mfadhili mkubwa sio tu kwa Waarabu wa wakati wake mwenyewe bali kwa wanadamu wote kwa wakati wote. Mtu kama huyo alipofariki, Waarabu, Waislamu, ambao walikuwa wafaidika-ji wa kazi yake kwao, walipaswa kupondwa na huzuni. Lakini cha kushangaza, kushtusha na kisichopingika, hawakuwa hivyo! Ingawa walikuwa wamepoteza baraka kubwa sana ambayo Allah (s.w.t.) alishusha kwao - kupitia Mpendwa Wake Mwenyewe, Muhammad - hawakuonyesha hisia zozote za hasara hata kidogo.

Haikujitokeza kwa umma wa Kiislamu kwamba Muhammad (s.a.w.) alikuwa ni mwon-gozaji wake, na kiongozi wake sio tu katika maisha bali hata katika kifo, alipaswa kupata mazishi ya kitaifa, na palipaswa kuwa na kipindi cha maombolezo rasmi kwa ajili yake.

Umma wa Kiislamu ni dhahiri uliona kwamba kuomboleza kwa ajili ya kifo cha Muhammad (s.a.w.), na kumfanyia mazishi, zilikuwa ni kazi ambazo ni vema kuachiwa kwa watu wa familia yake mwenyewe. Watu wa familia yake waliomboleza kwa ajili yake, na walimfanyia mazishi.

351

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Tahakiki ya Saqifah

Muhammad ibn Ishaq, mwandishi wa wasifa wa Mtume wa Uislamu, anaandika katika Siirah yake - (Maisha ya Mtume wa Allah):

Umar alisema: "Na tazama! wao Ansari walikuwa wanajaribu kutuondoa sisi kutoka kwenye asili yetu na kupora mamlaka kutoka kwetu. Alipomaliza (Ansari mmoja) hotuba yake, nilitaka kuzungumza, kwani nilikuwa nimeandaa hotuba kichwani mwangu ambayo ilinifurahisha sana. Nilitaka kuitoa mbele ya Abu Bakr na nilikuwa ninajaribu kulainisha makali yake fulani; lakini Abu Bakr akasema, 'Taratibu Umar,' Sikutaka nimuudhi na kwa hiyo akazungumza yeye. Alikuwa ni mtu mwenye maari-fa na heshima kubwa kuliko mimi, na Wallahi, hakuacha hata neno moja ambalo nilikuwa nimelifikiri na aliisema kwa namna yake isiyo na kifani, vizuri zaidi kuliko ambavyo ningeweza kufanya mimi.

Yeye (Abu Bakr) alisema: 'Mazuri yote mliyoyasema juu yenu wenyewe (Ansari) yanastahiki. Lakini Waarabu watayakubali tu mamlaka yaliyo katika kabila la Quraishi, wao wakiwa ndio wabora wa Waarabu kwa damu na nchi. Nawapeni mmoja kati ya watu wawili hawa: mkubalini yule mnayempenda.' Baada ya kuyasema hayo aliukamata mkono wangu na ule wa Abu Ubaidah ibn al-Jarrah ..."

Muhammad Mtume wa Allah (s.a.w.w), hakuwa amekufa kwa zaidi ya saa moja bado, pale Abu Bakr alipofufua ule ufidhuli wa Nyakati za Ujahilia kwa kudai mbele ya Ansari kwamba Quraishi, kabila ambalo yeye anatokana nalo, lilikuwa "zuri" kuliko au "bora" kwao Ansari "kwa damu na nchi!"

Abu Bakr alijuaje kuhusu "ubora" huu wa Quraishi? Qur'an na Mletaji wake, Muhammad (s.a.w.), hawajasema kamwe kwamba kabila la Quraishi lilikuwa na "ubora" kwa yeyote yule au kwamba lina ubora wowote kamwe. Kwa kweli, lilikuwa ni kabila la Quraishi ambao walikuwa ndio wasiokata tamaa kati ya waabudu masanamu wote wa Arabia. Waliyashikilia masanamu yao na walipigana na Muhammad (s.a.w.) na Uislamu, kwa hasira za kinyama, kwa zaidi ya miaka ishirini. Ansari, kwa upande mwingine, waliukubali Uislamu kwa hiari na bila ya kusita.

"Ubora" wa Quraishi ambao Abu Bakr alitambia hapo Saqifah, mbele ya Ansari, ulikuwa ni dhamira ya kabla ya Uislamu ambayo aliifufua ili kutia nguvu madai yake ya ukhalifa.

Siku chache tu kabla, Umar alizuia kalamu, karatasi na wino kwa Muhammad (s.a.w.) wakati yeye (Muhammad) alipokuwa kwenye kitanda chake cha umauti, na alitaka kuandi-ka wosia wake. Wosia, Umar alisema, haukuwa na haja kwa sababu "kinatutosha Kitabu cha Allah." Lakini kule Saqifah, yeye na Abu Bakr walikisahau Kitabu hicho, ambacho kwa mujibu wake hicho, ubora unazingatiwa sio kwa damu na nchi bali kwa ucha-mungu. Katika Kitabu hicho, hiki ndicho tunachokisoma:

352

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Usahihi-40.jpg

Hakika aliye mbora kati yenu mbele ya Allah ni yule mcha-mungu zaidi kati yenu. (Sura ya 49, Aya ya 13)

Mbele ya Allah (s.w.t.) wabora ni wale watu tu ambao wana tabia njema, ambao wanamuo-gopa Allah (s.w.t.) na wanaompenda. Lakini kitu kimoja ambacho Abu Bakr na Umar hawakukitangaza mle Saqifah ni Kitabu cha Allah (s.w.t.). Kabla ya kuingia Saqifah, walikuwa wamesahau kwamba mwili wa Mtume wa Allah (s.a.w) ulikuwa unasubiri maziko; na baada ya kuingia, wakasahau Kitabu cha Allah (s.w.t.) - "sadfa" ya kushangaza ya usahaulifu!

Dr. Muhammad Hamidullah:

"Qur'an imekataa ubora wowote kutokana na lugha, rangi au mifano yoyote ya asili isiyoepukika, na inatambua ubora pekee wa watu ulioegemea kwenye ucha-mungu."

(Introduction to Islam, Kuwait, 1971)

Madai ya Abu Bakr juu ya ubora wa Quraishi kwa misingi ya damu na nchi, yalikuwa ni dalili ya kwanza ya kuzuka tena kwa upagani katika Uislamu!

Sir John Glubb:

"Juu ya matukio yaliyofuatia kifo cha Mtume wa Uislamu:

Hii ghasia kali ilikuwa wala haijakwisha pale mtu alipoharakishia kwa Abu Bakr kumjulisha kwamba watu wa Madina walikuwa wanakusanyika kwenye ukumbi wa wageni wa ukoo wa Bani Sa'idah, wakishauriana kumchagua Saad ibn Ubadah, kion-gozi wa kabila la Khazraj, kama mrithi wao kwa Mtume (s.a.w.)."

Muhammad alikuwa hajafa kwa zaidi ya saa moja kabla ugombea madaraka kutishia kuuingiza Uislamu kwenye makundi ya uadui. Abu Bakr mpole na mkimya, Umar ibn al-Khattab mkali waliondoka kwa haraka kwenda kukabiliana na changamoto hiyo mpya. Walifuatana na yule mwerevu na mpole Abu Ubaidah, mmoja wa wafuasi wa awali, ambaye tutasikia mengi zaidi juu yake baadae.

Miaka kumi kabla, Maansari walimkaribisha Mtume (s.a.w.) yule aliyeteseka, kwenye

353

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

majumba yao na wakawa wamempa ulinzi, lakini Muhammad (s.a.w.) kidogokidogo aliku-ja kupata umaarufu na nguvu, na alikuwa amezungukwa na ndugu zake mwenyewe wa Quraishi (hii si kweli). Watu wa Madina, badala ya kuwa walinzi wa Waislamu, walijiku-ta kwenye nafasi ya chini kabisa kwenye mji wao wenyewe. Shutuma zilizimwa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.), lakini alikuwa hata hajafa pale makabila ya Aus na Khazraj yalipoamua kuutupilia mbali utawala wa Quraishi. "Wao wawe na kiongozi wao wenyewe," walipiga makelele watu wa Madina. "Na kuhusu sisi, tutakuwa na kiongozi kutokana na sisi wenyewe." Kwa mara nyingine tena, Abu Bakr, mtu dhaifu mwenye umbo dogo wa miaka sitini mwenye kuinama kidogo, alikabiliwa na tukio la ghasia za kusisimua. Alilikabili kwa utulivu wa dhahiri. "Enyi watu wa Madina," alisema, "Mazuri yote ambayo mmeyasema juu yenu, yanastahili. Lakini Waarabu hawatakubali kiongozi ila atokanaye na Quraishi."

"Hapana! Hapana! Hiyo sio kweli! Kiongozi kutoka kwetu na mwingine kutoka kwenu." Ukumbi ulijaa makelele, jambo hilo lilibaki kwenye mashaka,uhasama ulizi-di tu kuongezeka.

"Hivyo sivyo," alijibu Abu Bakr kwa uimara. "Sisi ndio wabora wa Waarabu. Hapa ninawapeni fursa ya kuchagua watu wawili hawa; mchagueni yule mtakayempa kiapo chenu cha utii," na akawanyooshea mkono maswahiba wake wawili, Umar na Abu Ubaidah, wote Maquraishi.

(The Great Arab Conquest, 1967)

Sir John Glubb amefanya rejea kwenye "ghasia kali" iliyofuatia mara tu baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.). Ni kweli kwamba kulikuwa na vurugu na ghasia nyingi. Lakini sehemu yake kubwa ilianzishwa na umuhimu wa hali halisi. Mara tu Abu Bakr alipowasili kwenye tukio, alimhakikishia kila mtu kwamba Mtume (s.a.w.) alikuwa amefariki na vurugu ikafikia mwisho. Vurugu ilidumishwa kwa kiasi ilivyokuwa inahitajika lakini sasa ilikuwa haihitajiki tena.

Ansari walikuwa wanayaangalia matukio hayo. Ilionekana kwao kwamba kukataa kwa Muhajirina kuandamana na jeshi la Usamah kwenda Syria; kukataa kwao kutoa kalamu, karatasi na wino kwa Mtume (s.a.w.) wakati alipokuwa kwenye kitanda chake cha umauti na akiwa alitaka kuandika wosia wake; na sasa kukataa kifo chake, kote kulikuwa ni sehemu ya mkakati mkubwa wa kuutoa ukhalifa nje ya nyumba yake. Waliridhika pia kwamba Muhajirina walikuwa wakimpuuza Mtume (s.a.w.) wakati wa uhai wake, hawakukubali kamwe Ali achukue nafasi yake kwenye utawala. Wao, kwa hiyo, waliamua kuchagua kiongozi wao wenyewe.

Lakini Ansari walizidiwa ujanja na Muhajirina. Ansari hawakuwa na mfumo wa ujasusi unaowafanyia kazi, lakini Muhajirina walikuwa nao. Yule mtu aliyemjulisha Abu Bakr na Umar kile Ansari walichokuwa wakikifanya, alikuwa mwenyewe ni Aus wa Madina.

354

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kama ilivyokwisha elezwa tayari, alitoa sauti kali kwa Khazraj.

Kwa kweli mpelelezi huyu alikutana na Umar na akamjulisha juu ya ule mkutano wa Ansari kule Saqifah. Abu Bakr alikuwa ndani ya chumba cha Mtume (s.a.w.). Umar alimwita nje. Alitoka nje na wote wawili wakatoka mbio kuelekea Saqifah. Walimchukua pia Abu Ubaidah pamoja nao. Waliunda "kamati ya watu watatu" ya wenye athari juu ya uchaguzi wa kiongozi.

Ansari mle Saqifah hawakuwa wakila njama dhidi ya Abu Bakr au Umar au dhidi ya mtu yeyote yule. Walikuwa wakijadili jambo lililogusa Uislamu na Waislamu wote. Kuwasili kwa hii "kamati ya watu watatu" katika mkutano wao, kuliwashitusha Khazraj lakini kukawafurahisha Aus. Hawa Aus sasa walipata matumaini ya kuwakwamisha maadui zao - Khazraj - kwa msaada wa hii "kamati ya watu watatu."

Sir John Glubb anasema kwamba Abu Bakr na Umar "walitoka kwa haraka kukabiliana na changamoto hii mpya." Inakuwaje kwamba Abu Bakr na Umar wao tu ndio walikuwa wak-abiliane na changamoto ambayo ilikuwa "inatishia" sio wao tu, bali umma mzima wa Kiislam? Ni nani aliyewapa mamlaka ya kukabiliana na "changamoto" hii? Hata hivyo, kwa wakati huu, wao walikuwa ni kama mtu mwingine yoyote wa jamii hiyo. Na vipi hawakumuamini mtu mwingine kwenye "faragha" yao kana kwamba walikuwa kwenye kazi maalum ya siri?

Mwanahistoria huyu anasema tena kwamba watu wa Madina walijikuta kwenye nafasi ya chini kabisa katika mji wao wenyewe wa nyumbani. Hiyo ni kweli lakini haikutokea wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.). Yeye aliwafanya Ansari kana kwamba walikuwa wafalme, na walikuwa na nafasi ya kwanza moyoni mwake. Lakini mara tu alipofariki, kila kitu kikabadilika upande wao, na walikoma kuwa mabwana katika majumba yao wenyewe.

Muhammad Husein Haykal:

"Ni ya kukasirisha kwa kiasi gani zaidi ambako mandari hii fupi lazima imekuwa kwa Muhammad (s.a.w.) ambapo kwa wakati huo huo alikuwa akabiliane na mambo yenye umuhimu mkubwa sana kama jeshi la Usamah lililokwisha hamasishwa na hatma ya Ansari inayotishiwa na pia ya umma wa Waarabu uliounganishwa pamoja hivi karibuni na dini ya Kiislam?"

(The Life of Muhammad)

Sehemu yenye msisitizo ya swali hili ni siri kubwa mno. Inaelekea kwamba kulikuwa na utambulisho wa tishio hilo. Wote, Mtume (s.a.w.) mwenyewe na marafiki zake Ansari, walikuwa na wasiwasi wa kutokea kwa uovu fulani ambao ulining'inia kama wingu juu yao. Lakini ni nani anayeweza kuwatishia Ansari na kwa sababu gani?

355

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Katika mfuatano wa matukio hayo, ilikuwa wazi kuona kwamba watu pekee wanaoweza kuwatishia Ansari walikuwa ni wale wageni wao wenyewe wa zamani kutoka Makka -Muhajirina. Hakuna wengine mbali na Muhajirina, katika peninsula yote ya Arabia, aliyekuwa katika hali ya kutoa tishio kwenye usalama wa Ansari.

Aus na Khazraj walikuwa na chuki na kushukiana wenyewe kwa wenyewe. Walikuwa, kwa hiyo, rahisi kuhujumiwa na maadui zao. Na kwa vile viongozi wao walikuwa wanau-tambua unyonge huu miongoni mwa watu wao, walikuwa wako katika kujihami mle Saqifah. Na pale mmoja wa viongozi wao alipowaambia Muhajirina: "Tutachagua viongozi wawili - mmoja kutoka kwetu na mmoja kutoka kwenu," ilikuwa ni dhahiri kwamba alikuwa anazungumza kwa hali ya unyonge, sio umadhubuti. Kwa kule kupendekeza utawala wa pamoja, Ansari walikuwa wamefichua udhaifu wao wenyewe kwa wapinzani wao.

Clausewitz aliandika kwamba nchi inaweza kupuguzwa nguvu na athari za ugomvi wa ndani. Na chama pia kinaweza kupunguzwa nguvu na athari kama hizo hizo. Kimsingi ilikuwa ni athari hizo za ugomvi wa ndani ndizo zilizowashinda Ansari. Wao walikuwa wamechukua hatua potovu mbaya sana. Saad ibn Ubadah alikuwa amewatahadharisha kwamba walikuwa wanadhihirisha unyonge wao wenyewe kwa wapinzani wao lakini madhara yaliyotendeka hayawezi kubadilishwa hasa kwa vile Aus waliamini kwamba Muhajirina watakuwa waadilifu zaidi kwao kuliko Saad ibn Ubadah wa Khazraj.

Katika mjadala huo wa kusisimua, mkali na mrefu humo Saqifah, Abu Bakr aliwaambia Ansari, miongoni mwa mambo mengine, kwamba Waarabu hawatamkubali kiongozi ambaye hatokani na Quraishi. Lakini angeweza kuwa karibu sana na ukweli kama angekuwa amesema kwamba kiongozi asiyetokana na Quraishi hatakubalika kwake yeye binafsi, kwa Umar na kwa Muhajirin wengine wachache. Hata hivyo, yeye alijuaje kwamba Waarabu hawatakubali uongozi wa asiyekuwa Quraishi? Je, hayo makabila ya Waarabu yalituma ujumbe kwake kumueleza kwamba hawatamtambua Ansari yeyote kama kiongozi? Abu Bakr aliwajumuisha Waarabu wote kwa Muhajirina wachache ambao walitaka kujitwalia madaraka wenyewe.

John Alden William:

"Machimbuko ya Ukhalifa - Uimamu yamekuwa ni maswali yenye wasiwasi sana katika historia ya Kiislamu. Kundi lenye watu wengi, la Sunni, limeacha nyaraka zinazoelekea kuashiria kwamba ukhalifa ulikuja kuwepo kwa ghafla, na kama jibu kwa kifo cha Mtume (s.a.w.) mwaka 632. Alimradi Mtume (s.a.w.) alipokuwa hai, alikuwa ndio kiongozi safi - mwenye kuingilika, mpole, mwenye upendo wa ubaba, mpiganaji na hakimu, na "daima muadilifu" kwa watu wake. Sasa amekufa bila kutarajiwa. Wakiwa wanakabiliwa na pengo hili, na bila mrithi juu yake (sic), umma

356

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ulianza kugawanyika kwenye makundi ya makabila yake. Kwa hatua za haraka, Abu Bakr na Umar, walifanikiwa kufanya mmoja wao wenyewe kukubaliwa na wote kama mtawala. Maelezo ya kina ya matukio ya Umar, katika zamu yake alipokuwa mtawala, ni kama yafuatayo:

"Ninakaribia kuwaambieni kitu ambacho Allah (s.w.t.) amependa kwamba niweze kukisema. Yeyote yule anayekielewa na kukitii, naakichukue pamoja naye popote anapokwenda. Nimesikia kuwa mtu mmoja amesema kwamba, " kama Umar angek-ufa, ningemkaribisha fulani (yaani Ali) - (Mhariri). Mtu yeyote asijidanganye mwenyewe kwa kusema kwamba kule kukubaliwa kwa Abu Bakr kulikuwa ni jambo ambalo halikufikiriwa kwanza, ambalo (wakati huo) lilikuwa limeidhinishwa. Kwa hakika ilikuwa hivyo, lakini Allah (s.w.t.) aliepusha uovu wake. Hakuna yeyote mion-goni mwenu ambaye kwake watu watajitiisha wenyewe kama walivyofanya kwa Abu Bakr. Yeyote atakayemkubali mtu kama mtawala bila kushauriana na Waislamu, ukubalikanaji kama huo hauna uhalali kwa yeyote kati yao ... (wote) wapo katika hatari ya kuuawa. Kilichotokea ni kwamba pale Allah (s.w.t.) alipomchukua Mtume Wake, Ansari (watu wa Madina) walitupinga na wakakusanyika pamoja na wakuu wao katika ukumbi (wa Saqifah) wa Banu Saidah, na Ali na Zubayr na marafiki zao wakajiondoa kutoka kwetu (kuandaa mwili wa Mtume (s.a.w) kwa ajili ya mazishi -Mhariri) ambapo Muhajirina (wahamiaji kutoka Makka) walijikusanya kwa Abu Bakr.

Nilimuambia Abu Bakr kwamba ili tubadili tuende kwa ndugu zetu Ansari kwenye ukumbi wa Bani Saidah. Katikati yao alikuwepo (kiongozi wao) Sa'ad Ibn Ubadah ambaye alikuwa mgonjwa. Mzungumzaji wao ndipo akaendelea: Sisi ni wenye kum-nusuru Allah na ni kikosi cha jeshi la Uislamu. Ninyi, Enyi Muhajirina ni katika familia yetu na kikundi cha watu wenu walikuja kufanya makazi.

Na tazama! Walikuwa wanajaribu kutukata kutoka kwenye asili yetu (katika kabila ya Mtume - Mhariri) na kutupokonya mamlaka. Nilitaka kuzungumza, lakini Abu Bakr akasema, taratibu, Umar. Sikutaka ni muudhi, hivyo alizungumza kwa namna yake isiyo na kifan, vizuri zaidi kuliko ambavyo ningefanya mimi. Alisema. 'Mazuri yote mliyoyasema kuhusu ninyi wenyewe yanastahiki. Lakini Waarabu watAyatambua mamlaka katika makabila hili tu la Quraishi, wao wakiwa ndio Waarabu bora zaidi kwa damu na nchi.

Ninakupeni mmoja kati ya watu wawili hawa: mkubalini yule mumpendaye'. Baada ya kusema hayo aliukamata mkono wangu na ule wa Abu Ubaidah Ibn al-Jarrah (ambaye alifuatana nasi)."

(Themes of Islamic civilization 1971)

357

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kwa hatua za haraka, Dr. Williams anasema, Abu Bakr na Umar, walifanikiwa katika kupa-ta mmoja wao kukubalika kama mtawala. Kwa kweli kwa hatua za haraka Abu Bakr na Umar walifanikiwa katika kuwafanya wote wawili kukubalika kama watawala. Hatua zao za haraka pia zilihakikisha kwamba Ali (na Ansar) watawekwa nje ya baraza la siri la utawala. Humo Saqifa, madaraka na mamlaka yaliingia kwenye mikono yao, na hapo yalikuwa yadumu. Hata baada ya kufa kwao, watawala wa baadaye walikuwa wawe ni watu walioandaliwa tu na wao wenyewe. Huu ulikuwa ndio ustadi mkubwa wao mkakati wa mkuu. "Hatua za haraka" zilizaa malipo ya mwisho mazuri ya kushangaza juu yao!

Wazo muhimu la hotuba za Abu Bakr ndani ya Saqifah lilikuwani ubabaishaji. Ilikuwa pia ni moja ya siri za mafanikio yake. Ingawa alikuwa mgombea wa ukhalifa na alikuwa mwanachama wa upinzani kwa Ansari, alijitokeza kwao kama asiyetaka, asiye mfuasi, mtu wa tatu. Kama angeingia Saqifah kama mgombea au kama msemaji wa muhajirina, upinzani wa Ansari ungekuwa mgumu. Lakini aliwaambia:

"Ninakupeni mmoja kati ya watu wawili hawa - Umar na Abu Ubaydah. Mkubalini mmojawapo kama kiongozi wenu.."

Abu Bakr aliwasifu Ansari na akatambua utumishi wao mkubwa kwa Uislamu lakini juu ya yote, kwa kufanikiwa kujifanya kuwa huru na asiyependelea, alifanikiwa katika kuwapoza. Kuhusu Muhajirina alisema kwamba walikuwa na nafasi ya kwanza katika kuukubali Uislamu, na kwamba walikuwa wa kabila la Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Ansari, kwa kweli, hawangeweza kuyakataa madai haya. Aliendelea kuliimarisha suala la Muhajirina kwa kunukuu mbele yao Hadith ya Mtume (s.a.w.) ambayo ndani yake anadai-wa kusema:

"Viongozi watakuwa kutokana na Quraishi."

Kama nipe nikupe ya kumtambua yeye kama Amir (khalifa), Abu Bakr alipendekeza kuwafanya Ansari kwua mawaziri wake. lakini pendekezo hili lilikuwa ni kitulizo tu kwa Ansari. Kamwe hawakuwa mawaziri au washauri au chochote katika Serikali ya Saqifah. Katika kuyaeleza kwa mukhtasari matukio ya Saqifah, Umar alilalamika kwamba Ansari walikuwa "wanajaribu kuwaondoa kutoka kwenye asili zao."

Ni asili zipi hizo ambazo Ansari walikwua wakijaribu kumuondoa Umar, na kwa namna gani? Kauli hii haina usahihi. Katika ukweli wa mambo, hivi haikuwa ni Umar ambaye aliyekuwa akijaribu kuwaondoa Ansari kutoka kwenye asili zao?

Kila mara, ilionekana kwamba Umar alipotewa na kumbukumbu. Kulikuwa na nyakati ambapo alisahau amri za Allah (s.w.t.) kama zilivyoshuka kwenye Qur'an Tukufu. Kama yeye mwenyewe alivyokiri; na kulikwa pia na wakati ambapo alisahau matamko na maele-zo ya Mtume wa Allah (s.a.w). Hivyo inaonekana kwamba yeye hakuwa na kumbukum-

358

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

bu ya matukio mawili katika uhai wa Mtume (s.a.w.), moja likihusiana na ule Mkataba wa Pili wa Aghaba (A.D. 622), na hilo jingine likihusiana na vita vya Hunayn (A.D. 630), na yote yalihusiana na Ansari.

Katika Mkataba wa Pili wa Aghaba, Abul Haitham wa Yathrib (Madina ya baadae), alimuuliza Muhammad Mustafa (s.a.w.) swali lifuatalo:

"Ewe Mtume wa Allah! Kitakuja kutokea nini wakati Uislamu utakapokuwa imara;

je utaondoka tena Yathrib na kurejea Makka, na kuifanya ndio Makao yako Makuu?"

"Kamwe," ndio lilikuwa jibu la dhahiri la Mtume wa Allah (s.a.w). kwa Abul Haithum na wenziwe. "kuanzia siku hii ya leo, damu yenu ni damu yangu, na damu yangu ni damu yenu. Kamwe sitawaacheni ninyi, na ninyi na mimi tutakuwa hatuten-ganishiki," aliwahakikishia.

Wakati ulifika ambapo Uislamu ulikuwa imara na hai na Muhammad Mustafa (s.a.w.) alikumbuka ahadi yake kwa Ansari. Aliifanya Madina - mji wao - makao makuu ya Uislamu. Muhammad (s.a.w.) hakuwahi kamwe kuwaambia Muhajirina kwamba damu yake ni damu yao au damu yao ni damu yake. Ilikuwa, kwa hiyo, ni Umar aliyekuwa aki-jaribu kuwakata Ansari kutoka kwenye asili zao, na sio vinginevyo. Kadhia ya pili ilitokea mara tu baada ya vita vya Hunain. Mtume (s.a.w.) aliwaamuru Ansari kukusanyika katika hema huko Jirana, na walipokusanyika, aliwahutubia kama ifuatavyo:

"...Mimi sitawaacheni ninyi kamwe. Kama wanadamu wote wakienda upande mmoja, na watu wa Madina wakaenda upande mwingine, mimi nitakwenda njia waliyokwenda watu wa Madina Allah (s.w.t.) aliridhie juu yao, na awabariki, na watoto wao na watoto wa watoto wao daima."

Muhammad-Mtume wa Allah (s.a.w) aliwambia Ansari kwamba yeye angekwenda njia yao hata kama dunia yote iliyobakia wakienda njia nyingine. Katika kuwapinga na kuwashinda hawa Ansari, mtu anaweza kuona ni njia ipi waliyokwenda Muhajirina. Muhammad (s.a.w.) na Ansari walikuwa wamechagua upande mmoja wa kusafiria. Lakini mle Saqifah, Muhajirina walichagua upande uliopotoka juu yao wenyewe!

Umar pia alikamata "Mamlaka" ambayo, alisema, Ansari walikuwa wakijaribu "Kutunyang'anya." Kauli hii tena inakosa Mashiko. Ni "mamlaka" gani ambayo Umar alikuwa akiyazungumzia juu yake? Na ni " mamlaka" gani aliyokuwa nayo hata hivyo? Ni nani aliyempa hayo mamlaka ambayo Ansari walikuwa wakijaribu kuyapora kutoka kwake? Na kwa nini aliingia Saqifah? Hivi hakuingia pale kupora mamlaka kutoka kwa Ansari?

Ule mkutano ndani yaukumbi wa Saqifah ulikuwa na jambo moja tu katika " ajenda" yake, nalo lilikuwa ni "mamlaka." Ilikuwa ni Abu Bakr na Umar waliofanikiwa katika kuyashika mamlaka yale. Mara yalipokuwa mikononi mwake, Umar angeweza kuwa mkosoaji na angeweza kumudu kuwakemea Ansari kwa kujaribu kwao kumuondoa kutoka kwenye

359

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

"asili" yake, na kwa kujaribu kupora "mamlaka" kutoka kwake.

Kama ilivyoelezwa kabla, wakati Mtume (s.a.w.) alipofariki, Abu Bakr hakuwepo pale Msikitini. Alikuwa yuko Sunh, mbali kidogo kutoka Madina. Kutokuwepo kwake kulim-tia Umar kwenye fadhaa kubwa. Alipunga upanga hewani na kutishia kumuua yeyote ambaye angesema kwamba Mtume amefariki. Hii hali ya karibu-kupagawa ilisababishwa na hofu wasije wale Waislamu mle Msikitini wakampa Bay 'ah (kiapo cha utii) Ali ibn Abi Talib, na wakamtambua yeye kama mtawala wao. Lakini akiwa hajui ni wakati gani Abu Bakr atatokea, yeye alimgeukia Abu Ubaidah, na akamwambia: "Ewe Abu Ubaidah! Nyoosha mkono wako, na nitakupa kiapo changu cha utii ili uweze kuwa Amir wa Waislamu. Nimemsikia Mtume wa Allah (s.w.t.) akisema kwamba wewe ndiye Amiin (mwaminifu) wa Umma huu."

Lakini Abu Ubaidah akakataa kupokea kiapo cha Umar, na akamuonya akisema:

"Maajabu gani ya dunia hii, Ewe Umar, uweze kunipa mimi Ukahalifa ambapo mtu kama Abu Bakr yupo miongoni mwetu? Umesahau kwamba yeye ndiye "Sidiq" na ni wa pili kati ya wawili wakati wote kwa pamoja walipokuwa ndani ya pango."

Jibu la Abu Ubaida lilimucha Umar hana la kusema. Yeye akaonekana "mwenye kupa-gawa" tena, akitishia kumuua yeyote ambaye angesema kwamba Mtume alikuwa amefariki, na akabakia katika hali hiyo mpaka Abu Bakr alipokuja. Abu Bakr alipokuja, yeye (Umar) mara moja akapona " mpangao " wake.

Baadae kidogo, ile "kamati ya watu watatu" ya Abu Bakr, Umar na Abu Ubaidah ilitum-bukia ndani ya Saqifah. Humo Abu Bakr aliwashawishi Ansar kutoa kiapo chao cha utii kwa Abu Ubaidah au kwa Umar. Katika muda chini ya saa moja, Abu Ubaidah ibn al-Jarrah, mchimba kaburi wa Madina, alikuwa amekwishapokea pendekezo la kuwa mtawala wa Arabia mara mbili - kwanza kutoka kwa Umar na kisha kutoka kwa Abu Bakr. Yeye lazima iwe alikuwa mtu wa kusifika sana kuweza kupendekezwa, sio na mtu mmoja tu, bali na wenye athari juu ya uchaguzi wawili!

Kwa kweli, mbali na ukweli kwamba alikuwa ni mfuasi wa awali wa Uislamu, Abu Ubaidah hakuwa na kingine chochote cha kuonyesha. Kuhusu yeye, yule mwanahistoria wa Kiingereza, Sir William Muir, anaandika katika kitabu chake The life of Muhammad hivi:

"Hapakuwa na chochote katika yaliyotangulia ya Abu Ubaidah cha kukubaliana na madai ya ukhalifa. Alitajwa hivi hivi tu na Abu Bakr kwa kuwa kwake Quraishi mwingine pekee aliyekuwepo."

Sir William Muir yu sahihi katika kuonyesha kwamba hakuna chochote katika yaliyotangulia ya Abu Ubaidah cha kuweza kukubaliana na madai ya Ukhalifa. Lakini basi, kulikuwa na kitu gani katika yaliyotangulia ya Umar mwenyewe cha kukubaliana na madai

360

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kama hayo? Ni lini na wapi alipojidhihirisha yeye mwenyewe katika kuutumikia Uislamu, ama kwenye medani ya vita au kwenye baraza?

Hapa mwanahistoria huyu anaonyesha mshangao kwamba Abu Bakr angeweza kupen-dekeza ukhalifa kwa Abu Ubaidah, mtu asiyekuwa na chochote katika habari zake zilizo-pita. Lakini huenda hakutambua kwamba katika hali iliyoko kwenye uchunguzi, suala la mambo yaliyopita ya mgombea wa ukhalfia, halikuwa na uhusiano wowote. Hawa wenye sauti katika uchaguzi wangependekeza ukhalifa kwa mtu yeyote miongoni mwa Muhajirina alimradi tu kwamba mtu huyo hakuwa ni Ali ibn Abi Talib au mtu mwingine wa ukoo wa Muhammad Mustafa Mtume wa Allah (s.a.w.).

Sir, William Muir anasema kwamba Abu Bakr alimtaja Abu Ubaidah kwa sababu tu ndiye alikwua Quraishi pekee aliyekuwepo. Hapa tena amesema kweli. Haina budi, hata hivyo, ikubmukwe akilini kwamba Abu Bakr na Umar walikuwa wamehusika na kazi muhimu sana ya kuteua Kiongozi Mkuu wa Ufalme wa Mbingnii juu ya Ardhi. Mtu anaweza kuuliza kama wangeweza kuwa wabahatishaji kama walivyokuwa. Na ni nini kingetokea kama badala ya Abu Ubaidah, Quraishi mwingine, Abu Sufyan - angekuwepo pale? Hivi Abu Bakr angependekeza ukhalifa kwake? Kweli kabisa, angeweza. Hata hivyo Abu Sufyan hakuwa mtu wa kabila la Quraishi tu bali pia alikuwa mmoja wa wakuu ambapo sio Abu Ubaidah wala Umar wala hata yeye mwenyewe walikuwa wakuu.

Umar na Abu Bakr walikuwa wakizunguka wakipendekeza utawala wa Arabia kwa mtu wa "kustahiki" lakini je utawala huu ulikuwa ni mali ya mtu ambao wangeweza kuuweka juu ya mtu yeyote waliyetokea kumpenda? Kama ulikuwa, basi ni nani aliyewapa? Hata hivyo, wao hawakuurithi. Kama haikuwa hivyo, basi walikuwa na haki gani kuutoa kwa mtu yeyote? Walikuwa wakizunguuka kupendekeza kitu ambacho sio chao. Kama hawakuja kukimiliki kwa njia za haki, kisheria, kwa njia iliyokubaliwa na Allah (s.w.t.), basi walikuwa wanamiliki kitu ambacho ni wazi kabisa wamekipora.

Kugombea uongozi, baada ya kifo cha Muhammad (s.a.w.) kulikuwa wazi tu kwa watu wa kabila la Quraishi, na sio kwa mwislamu mwingine yeyote. Abu Bakr, Umar na Abu Ubaidah - ile "kamati ya watu watatu" walitengeneza kanuni za ugombea huo, na kanuni hizo zilikuwa zenye kubadilika. Sasa Bani Hashim walikuwa pia ni ukoo wa Kiquraishi, na wao pia walikuwa watolewe katika ugombea madaraka. Lakini vipi? Hili lilileta tatizo kwa kamati ya watu watatu. Kamati hii iliweza kuliepuka tatizo hilo kwa werevu ambao ni muhimu kuswalia katika jangwa. Ilitangaza kwa ukweli kwamba ukoo wa Bani Hashim ulitoa Mtume kwa ajili ya Waarabu - heshima kubwa sana juu yao na kwamba walipaswa kuridhika nayo; na kuhusu warithi wake, haitakuwa kwa maslahi ya Umma kama Bani Hashim watawatoa wao pia; kwa hiyo, koo mbali na Bani Hashim zingepaswa kuwatoa wao.

Koo hizo zingekuwa zipi, ilikuwa ni juu ya "kamati ya watu watatu" kuamua. Zile koo ambazo hawa watu wa " kamati ya watu watatu" wenyewe wanazotoka, zitakuwa, bila

361

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

shaka ndio za kwanza.

Hivyo kile kilichothubutu kuwa chombo chenye thamani sana kwa kabila la Quraishi, yaani kuwemo kwa Muhammad (s.a.w.) Mtume, ndani yake kulithibitika kuwa ni "Madaraka" makubwa mno kwa ukoo wa Bani Hashim. Hawa Bani Hashim "waliondole-wa" kwenye kushiriki katika kugombea mamlaka kwa sababu tu Muhammad alitokana na wao!

Umar alifanya mgeuko wa nyuzi 180 humo Saqifah. Kabla ya kuingia Saqifah, alikuwa akitoa ubashiri kwamba kama ile familia iliyotoa mtume, ingekuwa pia itoe mrithi wake, "Waarabu" wataasi dhidi yao. Lakini alipokabiliana na Ansari mle Saqifah, alitabiri kwamba "Waarabu" hawatakubali uongozi wa mtu kama hakuwa wa kabila ambalo Mtume mwenyewe anatokana nalo. Yeye na Abu Bakr waliweka madai ya ukhalifa kwa misingi ya kwamba wao wote walikuwa watu wa kabila moja na Muhammad (s.a.w.) ambapo wao Ansari hawakuwa.

Al-Marehemu Maulana Abu Ala Maududi wa Pakistani ametoa sifa za juu sana kupin-dukia, juu ya Maquraishi. Anasema kwamba watu wa kabila la Quraishi ni watu wenye vipaji na uwezo wa kipekee, na walitoa viongozi wote wa Waislamu. Kuyafanya madai yake yasadikike, amenukuu maelezo yenye kudai ubora wao, ambayo anasema, yalitolewa na Mtume (s.a.w.) na Ali ibn Abi Talib.

Lakini inawezekana kabisa kwamba Ansari wangeweza kutoa viongozi wakuu kama hao hao, au kwa kweli hata wakubwa zaidi kuliko Maquraishi waliotoa. Lakini "kamati ya mtu watatu" waliwapigia turufu kuwazuia wasiingie mle Saqifah na umma wa Kiislam haukuweza kufaidika na ustadi wao wa uongozi.

Usahihi wa maelezo yanayowasifia Maquraishi ambayo Maududi ameyahusisha kwa Ali, yanatia wasiwasi. Ali angepata machache sana ya kusifia katika Quraishi. Alikuwa hajafikia hata umri wa miaka kumi na nne walipofanya jaribio la kwanza la kumzuia Muhammad (s.a.w.). Ali alikabiliana na upinzani wao. Upanga wake siku zote ulikuwa uki-tiririka damu yao ya kipagani au ya watetezi wa upagani. Yeye na wao walikuwa katika makabiliano ya kudumu maisha kati yao.

Waislamu wa Shia wanapingana na kanuni ya uchaguzi wa kiongozi kwa misingi ya kujit-walia au "kutangulia" tu. Kwa mujibu wao, mapendekezo, yanayodhibiti katika kuchagua kiongozi lazima yasiwe ni uhusiano wake na Quraishi au umri wake, bali tabia yake, uadil-ifu wake, uwezo na uzoefu. Tabia inakuja ya kwanza. Jinsi gani kiongozi wa Waislamu anavyofanya aeleweke mwenyewe kwenye maisha - sio tu kwa jukumu hili au lile, sio kwa muda huo, bali kwa kudumu na kwa upeo wa ufahamu.

362

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Uchaguzi wa kiongozi unahitaji uchunguzi wa hali ya juu unaofikia mbali zaidi ya tabia za kimaadili. Hata hivyo, uongozi wa Waislamu (ukhalifa) sio zawadi katika mashindano ya maadili. Kiongozi (khalifa) lazima awe mtu, sio tu mwenye tabia njema na uadilifu bali pia mwenye uwezo wa dhahiri na uzoefu mkubwa. Kwa maneno mengine, uteuzi wa mgombea bora, - bora katika kila hali ya istilahi hiyo; wa juu katika uadilifu binafsi bali pia mtu mwenye uwezo ambao umeonyeshwa, kuthibitishwa - sio mara moja au mbili bali kwa mara nyingi lazima iwe ndio kanuni. Na kwa kweli lazima awe na ile sifa ya ziada bali ya lazima na tena adimu iitwayo taqwa.

Hao wateuzi; kama kipo chombo kama hicho, wanao wajibu juu ya uchanguzi wa makini na kamilifu wa sifa zote za ustahilifu, na maelezo binafsi ya siku za nyuma ya mtu ambaye ataweza kuwa mgombea wa nafasi hiyo ya juu sana katika Uislamu. Lazima wapime uwezo wake, maamuzi, uhuru na muonekano wa utulivu wake kwa masharti ya kama ndiye mtu ambaye wanaweza kwa makini sana kumuidhinisha kama anayeweza kuwa khalifa.

Kama tulivyokwishaona, tabia na uwezo wa mgombea au wagombea wa ukhalifa haviku-jadiliwa mle Saqifah. Yalikuwa ni mambo "yasiyohusika". ufasaha wa Muhajiri na Ansari ulizalisha swali moja tu, yaani, je, kiongozi wa Waislamu, awe Muhajirin au Ansari?

Ansari walikubali kushindwa mle Saqifah walipokabiliwa na werevu wa wapinzani wao, Muhajirina, kwamba ukahifa wa umma wa Kiislam ulikuwa ni "haki" pekee ya Quraishi kwa sababu Muhammad (s.a.w.) mwenyewe alikuwa ni Quraishi!

363

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

SAQIFAH NA MANTIKI YA HISTORIA

Katika utangulizi wa kitabu hiki, nilimtahadharisha msomaji juu ya tabia na wepesi wa Mustashriq wengi, kukubali, bila kuangalia undani wake, mengi ya maelezo ya uongo na madai ya uongo ambayo yaliingizwa kwenye mzunguko, zamani sana, na wale wanahis-toria ambao walikuwa kwenye "orodha ya malipo" ya Serikali ya Damascus na Baghdad - zote zikiwa warithi wa Serikali ya Saqifah. Kwa mfano kuna makubaliano miongoni mwao kwamba Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) hakuchagua mrithi wake mwenyewe wala hakuwaambia Waislamuu namna wanavyopaswa kuchagua viongozi wao kwa ajili ya Serikali ambayo aliianzisha, na alifariki akiacha kila kitu, dhahiri kabisa, kwenye mashauri yao na hiari zao.

Baadhi ya mifano ya kukubali kusiko na udadisi kwa Mustashriq juu ya dai hili, ilitoka katika Sura ya 45. Ufuatao ni mfano mwingine zaidi.

"Muhamamd alifariki hapo Madina mnamo tarehe 8, Juni, 632, bila ya kuacha maagizo kwa ajili ya Serikali ya baadae ya jamii ya Waislamu."

Habari hii inatokea kwenye makala yenye kichwa cha habari Caliphate, kwenye ukurasa wa 643, juzuu ya 4, chapa ya 14 ya 1973 ya Encyclopedia Britannica. Ni kipande cha propaganda cha dhahiri lakini hiyo Encyclopedia Britannica, kile kienezaji kikuu cha elimu, kimeikubali. Ni taarifa ya uongo ya kihistoria yenye kugawa mno katika Uislamu, lakini cha ajabu, inapita bila kupingwa, karne baada ya karne.

Hawa Mustashirki wanaweza wasilete pingamizi kwenye huu uongozi wa muda mrefu unaokubalika kwenye mila na desturi, lakini hata hivyo unazua maswali fulani ya msingi. Maswali hayo ambayo yanahusiana na maadili ya Uislamu na falsafa ya kisiasa ya Muhamamd Mtume wa Allah (s.a.w.) yameorodheshwa hapo chini. Yote yanasimama kwenye dhana ya kwamba Muhamamd (s.a.w.) haku...(rudia haku.J hakuteua mrithi wake mwenyewe wala hakutoa maagizo yoyote kwa maswahaba zake kwa ajili ya serikali ya baadae ya umma wa Kiislam. Kwa hiyo, wakati alipofariki, Umma wake ulijikuta wenyewe katika hali ya mfadhaiko mkubwa kabisa.

1. Je, Muhammad (s.a.w.) Mtume wa Allah (s.w.t.) na Muasisi wa Serikali ya Madina, alijiona binafsi ni mwenye uwezo wa kuchagua mrithi wake mwenyewe au la?

364

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

2.    Kipi kingefaa, ni sababu za kubuni juu ya kushindwa kwa Muhammad (s.a.w.) kuteua mrithi wake mwenyewe?

3.    Kwa vile Muhamamd (s.a.w.) hakuteua mrithi wake mwenyewe, je, aliik-abidhi jamii ya Waislamu jukumu hilo la kuchagua au kuteua kiongozi wao wenyewe?

4.    Kwa vile jamii ya Kiislamu ilikosa mwongozo juu ya kuteua kiongozi, je maswahaba wa Muhamamad, kwa ridhaa yao ya pamoja, na kabla ya kuweka kiongozi (au hata baada ya kuweka kiongozi) waliandaa orodha ya masharti au miongozo ambayo wao waliishika (baadaye)?

5.  Upi ulikuwa msimamo na mwenendo wa maswahaba wakubwa wa Muhamamd (s.a.w.) juu ya uongozi wa jamii ya Waislamu baada ya kifo chake?

6.  Upi ulikuwa mwenendo (Sunnah) wa Muhamamd (s.a.w.) kuhusiana na uteuzi na uwekaji wa watumishi?

7.   Ni ipi Fatwa ya Qur'an juu ya mwenendo (sunnah) wa Muhamamd

8.    Muhamamd (s.a.w) alifanya nini hasa kuhusu kurithiwa kwake?

9.     Ni nini hasa kilichotokea baada ya kifo cha Muhammad (s.a.w)?

10.  Je, swala la urithi lina umuhimu gani katika historia kwa jumla? Jaribio limefanyika katika kujibu maswali haya kama ifuatavyo:

Swali la 1

Je, Muhammad Mtume wa Allah (s.a.w.), na muasisi wa Serikali ya Madina, aliona binaf-si yeye ni mwenye uwezo wa kuchagua mrithi wake mwenyewe au la?

Jibu

Hakuna hata mtu mmoja ambaye angefikiria, kati ya Waislamu wote, kwamba Muhamamd hakuwa na uwezo na kumuweka mrithi wake mwenyewe. Mwislamu hawezi kudhania kwamba Mtume (s.a.w.w) alikosa uwezo wa kuteua mrithi kwa ajili yake mwenyewe.

Waarabu walikuwa ni kizazi chenye sifa mbaya ya kiburi, cha wajinga, wenye ghasia na wasio na sheria. Muhamamd (s.a.w.) alizieneza sheria za Allah (s.w.t.) miongoni mwao, na

365

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

akawalazimisha kuziheshimu na kuzitii sheria hizo. Aliunda taasisi ya kisiasa iliyoitwa Dola au Serikali ya Madina. Katika Dola hiyo, madaraka yake yalikuwa hayana mpaka. Aliwachagua watumishi wake wote, wa kiraia na kijeshi. Aliweza kumuweka mtumishi au kumfukuza, bila kufuata msingi maalum, na bila ya kutoa sababu zozote kwa mtu yeyote kwa kufanya hivyo.

Mwelekeo wa tabia (sunnah) ya Muhammad (s.a.w.) ilikuwa thabiti na ya kudumu daima. Alikuwa kwa kweli, ni mwaminifu kiasi kwamba alikuwa takriban ni "mwenye kutabiri-ka." Waislamu wote walijua kwamba angeteua na kuweka watu wenye uwezo katika nafasi zote muhimu, na pia walijua kwamba angefanya hivyo bila kushauriana nao. Wala haku-toa mamlaka kwa maswahaba wake wo wote ya kuweka watumishi. Muhammad Mtume wa Allah (s.a.w.). pekee ndiye alikuwa na uwezo wa kuteua na kuweka mrithi wake mwenyewe, na hakuna yeyote ambaye angemfanyia hivyo badala yake.

Swali la 2

Kipi kingefaa, ni sababu za kubuni juu ya kushindwa kwa Muhamamad (s.a.w.) kuteua mrithi wake mwenyewe?

Jibu

Kama Muhammad (s.a.w.) angekufa bila ya kuchagua mrithi na atakayemfuata baada yake, anajiweka kwenye lawama ya kutotekeleza wajibu. Yeyote anayedai kwamba yeye hakuchagua mrithi wake, anashauri kwamba alikiacha chombo dhaifu cha Uislamu kwenye bahari iliyochafuka bila ya dira, bila ya usukani, bila ya nanga na bila ya Nahodha, na kukiacha kabisa kwenye huruma ya upepo na mawimbi. Ni kudhania kwamba hakuwa mwangalifu wa maslahi muhimu kabisa ya umma wa Kiislamu na kwamba alikuwa amezembea kwenye ustawi wa vizazi vya Waislamu, vitakavyokuja baadae. "Uzembe" kama huo kwa upande wake ungeweza kuwa na sababu tatu zinazowezekana, yaani:

a) Watu wote wa Umma wa Kiislamu wamekuwa wenye ufahamu mkubwa, wenye heki-ma, wacha-mungu na wenye kumpenda Allah (s.w.t.) na kila mmoja wao alikuwa amepa-ta elimu kamili ya tafsiri ya Qur'an. Vile vile kila mmoja alikuwa analingana, katika kila hali na kila mtu mwingine. Ilikuwa haiwezekani kwa shetani kumshawishi au kumpoteza yeyote kati yao. Kwa hiyo, Muhammad (s.a.w.) angeweza kuacha wajibu wa kuteua na kuchagua mrithi wake kwenye fursa ya kubahatisha. Angeweza kufarijika kwa kudhani kwamba yeyote yule atakayefanywa kiongozi wa jamii hiyo kwa mkondo wa matukio, atakuwa ni mtu sahihi, na Serikali ya Madina na jumuiya ya waumini vyote vingeweza kuwekwa chini ya uangalizi wake.

Lakini hivyo sivyo ilivyokuwa na isingeweza kuwa hivyo. Haiwezekani hata kwa watu wawili kulingana katika uwezo, tabia na desturi. Muhammad (s.a.w.) alijua kwamba

366

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Waarabu wote waliokubali Uislamu, sio lazima kuwa walikuwa wote ni Waislamu waaminifu. Miongoni mwao, ilikuwemo idadi kubwa ya "wanafiki" au "Waislamu wachache." Kuwepo kwao pale Madina kunashuhudiwa na Qur'an yenyewe. Waliukubali Uislamu kwa nje tu bali moyoni walikuwa wapagani. Walikuwa ndio maadui wa Muhamamd, wa Uislamu, na wa Dola aliyokuwa ameianzisha. Walifanya "safu ya tano" ya upagani hapo Madina, tayari kutumia fursa ya kwanza ya kuudhoofisha Uislamu. Kama Muhammad (s.a.w.) angekuwa aiache Dola hii mpya bila ya kiongozi, kwa kweli angeiwe-ka mkononi mwa hawa wahujumu wa kiitikadi, silaha zenyewe hasa ambazo kwazo watauangamizia.

Muhammad aliyajua yote haya, na alifariki, sio ghafla, bali baada ya maradhi ya muda mrefu, yeye alikuwa na muda wa kutosha kushughulikia mambo muhimu ya Dola, lenye umuhimu zaidi likiwa ni uteuzi wa usimamishaji wa mrithi wake mwenyewe. Kitu kimo-ja ambacho asingeweza kukifanya, kilikuwa ni kuitelekeza serikali yake, ambayo ilikuwa ni Ufalme wa Mbinguni Duniani, kwenye uangalizi wa mpenda fursa asiyejulikana au mpenda vituko mwenye majigambo.

b) Muhammad (s.a.w.) hakuupenda hasa Uislamu. Alitiwa shauku tu na malengo yake binafsi. Alitaka kuiweka peninsula yote ya Arabia chini ya mamlaka yake, na Uislamu ulikuwa ndio njia ya ambayo alifanikiwa nayo katika kufanya hivyo. Lakini mara alipo-timiza lengo lake hakujali kwamba baada ya kufa kwake, ile serikali ambayo ameianzisha, ilikuwa imara au ilichanguka. Hakujali kama, baada ya kifo chake, Waarabu walibakia waaminifu kwa Uislamu ama walirejea kwenye uabudu masanamu na ushenzi.

Ni nini kitakachokuwa cha kipumbavu zaidi kuliko kudhania kwamba Muhammad (s.a.w.) hakuupenda Uislamu? Akiwa Makka, alivumilia mateso, njaa, kiu, kunyimwa, ufidhuli na uhamisho, yote hayo kwa ajili ya Uislamu. Wakati alipokuwa Madina alitakiwa kutoa mihanga mikubwa zaidi kwa ajili ya Uislamu. Wawili wa ami zake, binamu zake watatu, watoto wa kufikia wawili na ndugu mmoja wa kunyonya, na marafiki wengi waliuawa katika kuutetea Uislamu. Kwa wakati upasao, akawa mkuu wa Madina lakini hakuna cho-chote kilichobadilisha mtindo wa maisha yake. Watu wengi wa jumuiya hiyo mpya walikuwa mafukara, naye aliwalisha. Aliwalisha chakula chake yeye mwenyewe kiasi kwamba mara nyingi, yeye na wanawe walilazimika kukaa na njaa. Hii iliendelea mwaka baada ya mwaka. Alifanya makafara yote haya na mengine yasiyo na idadi kwa ajili tu ya kuufanya Uislamu uweze kuwepo na uwe na nguvu.

Hapo Makka, Maquraishi walimuahidi Muhammad madaraka, utajiri na vivutio kama angeiacha kazi yake kama Mtume wa Uislamu. Lakini alivipiga mateke vyote hivyo. Katika kuvipiga mateke hivyo, alikuwa akiipiga mateke "tamaa." Labda haikumjia kwamba kulikuwa na kitu kama tamaa. Kiini hasa cha kazi yake kwa ajili ya Uislamu kilikuwa ni mapenzi yake tu juu yake. Mapenzi haya yalimchukua kutoka mwanzo hadi mwisho.

367

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Alikuwa na "tamaa" moja tu katika maisha, nayo ilikuwa ni kuona Uislamu unakuwa ni wa kudumu. Aliitimiza "tamaa" hiyo kwani tunajua kwamba Uislamu ni wakudumu milele.

C) Muhammad (s.a.w.) hakuteua mrithi wake kwa sababu alikuwa anaogopa upinzani.

Muhammad (s.a.w.) alikuwa haijui kabisa hofu. Aliushinda upagani katika wakati ambapo yeye alikuwa peke yake katika dunia nzima, na kwamba dunia yote ilikuwa imejaa uhasama dhidi yake. Upagani ulitumia nguvu zake zote ili kumvunja lakini ulishindwa. Yeye aliuvunja. Kwa kutumia ujasiri wake binafsi, alipata ushindi juu ya dunia nzima. Katika mawili kati ya mapambano ya Uislamu, Waislamu walishindwa, na walikimbia kutoka kwenye medani ya vita. Lakini yeye alisimama imara na hakukimbia, na kwa kweli, alikuwa ni kiungo cha kukusanyikia watoro wa vita. Utulivu wake wa akili ulihuisha ule ushupavu wa Waislamu, na wakarudi vitani.

Baada ya vita ya Hunain, Arabia yote ilikuwa chini ya miguu ya Muhammad (s.a.w.), na hakuna kabila au muungano wa makabila ambao uliweza kushindana na nguvu zake. Nguvu zake, ndani ya peninsula, zilikuwa kubwa. Suala la yeye kuogopa upinzani wa mtu yoyote, kwa hiyo haliji.

Swali la 3

Kwa vile Muhammad (s.a.w.w.) hakuteua mrithi wake mwenyewe, je, aliikabidhi jamii ya Waislamu jukumu hilo la kuteua na kuchagua kiongozi wao wenyewe?

Jibu

Kuteua Mtendaji Mkuu wa umma wa waumini lilikuwa ni jambo muhimu. Muhammad (s.a.w.) alitambua umuhimu wake. Lakini kwa sababu zisizojulikana, alijizuia kumteua. Sababu pekee inayowezekana kwamba hakumteua inaweza kuwa kwamba aliuachia umma jukumu hilo.

Lakini si Abu Bakr na Umar wala wanahistoria wa baadae wa Sunni, ambao wametoa dai hili kamwe. Hawajadai, kwa mfano, kwamba Muhammad Mustafa (s.a.w.) alisema: "Enyi Waislamu! Sipendi nijichagulie mrithi wangu mwenyewe,"

au "Siwezi kujichagulia mrithi wangu mwenyewe,"

au

"Sina uwezo wa kuchagua mrithi wangu mwenyewe. Kwa vile sina uwezo huo, ninakuachieni ninyi wajibu huo. Nitakapofariki, mnateua na kuchagua kiongozi wenu wenyewe."

Hakuna hata mtu mmoja aliyejaribu kuhusisha kauli kama hiyo kwa Muhammad Mustafa (s.a.w.). Muhammad Mustafa (s.a.w.) hakuwapa maswahaba zake mamlaka ya kuteua hata

368

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

mtumishi mdogo seuze kwa kiongozi mkuu wa baadae wa Dola ya Kiislamu! Swali la 4

Kwa vile jamii ya Kiislamu ilikosa mwongozo juu ya kuteua kiongozi, je, maswahaba wa Muhammad (s.a.w.), kwa ridhaa yao ya pamoja, na kabla ya kuweka kiongozi (au hata baada ya kuchagua kiongozi) waliandaa orodha ya masharti au mwongozo ambao wal-iushika (baadae)?

Jibu

Masahaba wa Muhammad (s.a.w.) hawakuandaa, katika wakati wowote, mfumo wa masharti wa kuwaongoza katika kuchagua kiongozi. Katika jambo hili, walishika kanuni ya kuangalia manufaa yao. Kwanza waliteua kiongozi, na kisha wakaunda "masharti" au "kanuni" kwa ajili ya uchaguzi wake. Waislamu "walichagua" wale makhalifa wa kwanza "walioongoka" wanne. Uteuzi wa kila mmoja wao ulisababisha kugunduliwa kwa "masharti" mapya au "kanuni" mpya. Hizi "kanuni" nne ziliunganishwa ipasavyo katika fikra za kisiasa za Waislamu.

Lakini mara khalifa mpya akaingia madarakani huko Syria. Kuibuka kwake kulisababisha kugunduliwa kwa "kanuni" mpya ijulikanayo kama " mwenye nguvu mpishe." "Kanuni" hii ilizifanya zile "kanuni" nne za kwanza kuwa zisizotumika tena. Kutoka wakati huu, ukhalifa ukawa uwe ni tuzo ya mgombea aliyeweza kutumia nguvu ya kinyama kwa ukatili zaidi kuliko wapinzani wake. "Kanuni" hii imepata ukubalikanaji wa kimataifa miongoni mwa Waislamu katika historia yao yote ndefu .

Swali la 5

Upi ulikuwa msimamo na mwenendo wa maswahaba wakubwa wa Muhammad (s.a.w.) juu ya uongozi wa jamii yaWaislamu baada ya kifo chake?

Jibu

Waislamu wa Sunni wanasema kwamba Abu Bakr na Umar ndio walikuwa maswahaba wakuu wa Muhammad Mustafa (s.a.w.). Walikuwa ni wote hao, maswahaba wakuu, ambao walitwaa Dola ya Madina katika wakati ambapo Ali na watu wote wa Bani Hashim walikuwa wakishughulika na mazishi yake.

Mara tu Mtume (s.a.w.) alipofariki, maswahaba zake wakubwa walikusanyika katika Ukumbi wa Saqifah kudai uongozi wa umma. Uongozi huu, kwa maoni yao, ulikuwa ni muhimu sana kiasi kwamba hawakuweza kutulia hata kumzika bwana na mfadhili wao aliyefariki. Kushindania madaraka kwa wazi kuliibuka kwa dakika chache tu za kifo cha

369

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Mtume (s.a.w.). Zamakhshari, mmoja wa wanazuoni na wanahistoria wa kuaminika wa Sunni, anaandika kuhusiana na hili, hivi:

"Yalikuwa ni makubaliano ya maswahaba wote kwamba baada ya kifo cha Mtume ili-wabidi wateue mrithi wake mara moja. Waliamini kwamba kufanya hivyo ilikuwa ni muhimu zaidi kuliko hata kushughulikia mazishi ya bwana wao. Ulikuwa ni umuhimu huu ambao ulimchochea Abu Bakr na Umar kuhutubia ule mkusanyiko wa Waislamu. Abu Bakr alisema: 'Enyi watu! hebu nisikilizeni. Wale kati yenu waliokuwa wakimuabudu Muhammad, nawajue ya kwamba amekufa; lakini wale waliokuwa wakimuabudu Allah, nawajue kwamba Yuko hai, na kamwe hatakufa. Kwa vile Muhammad amekufa, inawabidi sasa muamue ni nani atakayekuwa kion-gozi wenu wa baadae.' Wakasema: 'Umesema kweli; ni lazima tuwe na kiongozi mpya.' Sisi Sunni na Mu'tazili, tunaamini kwamba umma wa Waislamu ni lazima kwa wakati wote usikae bila ya kiongozi. Mantiki peke yake inaamuru hivi. Pia, Mtume wa Allah (s.a.w). alitekeleza sheria, na alitangaza rasmi amri kuhusu kuulin-da Uislamu, na ulinzi wa Madina na ulinzi wa Arabia. Baada ya kifo chake, anapaswa awepo mtu wa kutekeleza sheria zake, na kutekeleza amri zake."

Kutokana na ushahidi huu uliopita, ni dhahiri kwamba maswahaba wa Mtume (s.a.w.) walitambua ilivyokuwa muhimu kwa umma kupata kiongozi. Walijua kwamba kama hapakuwa na mtu wa kutekeleza sheria na amri alizozitangaza, umma wake ungeangukia kwenye vurugu.

Hali hiyo imejawa na kejeli. Masahaba waliridhika kwamba ilikuwa ni muhimu sana kwa umma wa Waislamu kuwa na mtendaji mkuu lakini kulikuwa na mtu mmoja ambaye hakuamini kwamba ilikuwa muhimu, naye alikuwa ni Muhammad (s.a.w.)! Ingawaje kama angeamini hivyo, angeupatia umma huo mtendaji mkuu. Alikuwa ndiye mtu pekee ambaye haikujitokeza kwake kwamba palipaswa kuwa na mtu wa kutekeleza zile sheria na amri ambazo yeye mwenyewe alikuwa amezitangaza rasmi.

Hao maswahaba wakubwa hawakuhudhuria mazishi yake. Kwao wao, kilichokuwa na umuhimu zaidi kuliko kuhudhuria mazishi ya bwana wao, kilikuwa ni kupata kiongozi mpya. Tatizo hili lilikuwa gumu sana lakini "walilitatua" kwa kumchagua mmoja kati yao, yaani, Abu Bakr, kama kiongozi mpya wa Waislamu.

Miaka miwili baadae, Abu Bakr alikuwa amelala akifariki. Juu ya kitanda chake cha mauti, alimteua Umar kuwa mrithi wake, na kiongozi wa Waislamu. Katika kumteua Umar kama mrithi wake, hakujua tu kwamba alikuwa anatekeleza wajibu wake muhimu sana bali ali-tambua kwamba kama hakufanya hivyo, atakuwa mwenye kuulizwa mbele za Allah kwa kushindwa kwake kufanya hivyo.

370

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

"Asmah, mke wa Abu Bakr, anasema kwamba wakati mume wake alipokuwa kwenye kitanda chake cha mauti, Talha alikuja kumuona, naye akasema: 'Ewe Abu Bakr! umem-fanya Umar kuwa amir wa Waislamu, na unajua kabisa kwamba alikuwa dhalimu mno wakati ulipokuwa khalifa. Bali sasa kwa vile atakuwa na uhuru wa kufanya atakalo, sijui ni vipi atakavyowaonea Waislamu. Baada ya muda mfupi utafariki, na utajikuta mwenyewe mbele ya Allah (s.w.t.) Katika muda huo utatakiwa kumueleza Yeye juu ya matendo yako. Je, umeandaa tayari majibu yako?' Abu Bakr akakaa juu ya kitanda hicho, na akasema: 'Ewe Talha! je, unajaribu kunitisha mimi? Sasa sikiliza, kwamba pale nitakapokutana na Mola wangu, nitasema kwamba nilimchagua mtu aliye bora kama amir wa umma wa Waislamu.'

Abu Bakr aliongeza kwamba elimu na uzoefu wake juu umma ya Umar vilimthibitishia yeye kwamba hakuna mtu katika wa Waislamu ambaye angeweza kuubeba uzito wa ukhal-ifa vizuri zaidi kama ambavyo yeye (Umar) angeweza. Alikuwa, kwa hiyo, na imani kwamba majibu yake yatamridhisha Allah (s.w.t.)

Abu Bakr alijua kwamba atakuja kujitetea mwenyewe katika Mahakama ya Allah (s.w.t.) kwa kumteua Umar kama mtawala wa Waislamu. Aliridhika kwamba asingeweza kumch-agua mtu mwingine bora zaidi kuliko Umar kuwa mrithi wake. Na wasiwasi wa Talha juu ya kuwajibika kwa Abu Bakr mbele Allah, unaonyesha tu uangalifu wake kuhusu wajibu wake wa "kuamrisha wengine kufanya mema na kukataza maovu."

Kejeli tena! Masahaba wote walikuwa waabudu-masanamu kabla ya Muhammad Mtume wa Allah (s.a.w.), aliyebarikiwa, hajawasilimisha kwenye Uislamu. Sasa, wao kama Waislamu wa dhati, walikuwa wanatambua kwamba walikuwa ni wenye kuwajibika kwa Allah (s.w.t.) kuhusu wajibu wao wa kuchagua mrithi wake. Lakini cha ajabu, na cha kushangaza, alikuwepo mtu mmoja ambaye ni dhahiri hakuwa na ufahamu kwamba, siku moja, yeye pia atakuja kusimama katika Mahakama ya Allah (s.w.t.), na kuulizwa kuhusu wajibu wake wa kuchagua mrithi wake. Yeye alikuwa ni Muhammad (s.a.w.), Mtume Wake Mwenyewe Allah (s.w.t.)! Waislamu wanaamini kwamba Abu Bakr alikuwa tayari kutetea kitendo chake cha kuchagua mrithi wake, kwa majibu ambayo alijua, yatamridhisha Allah (s.w.t.) Je, wanaamini pia kwamba Muhammad, Mtume wao, alikuwa tayari kutetea kushindwa kwake kuteua mrithi wake mwenyewe, kwa majibu ambayo Allah (s.w.t.) atapata kuridhika nayo?

Baada ya kifo cha Abu Bakr, mrithi wake, Umar ibn al-Khattab, alitawala kama khalifa kwa miaka kumi. Katika miaka ya mwisho ya uhai wake, alionekana mara kwa mara akiwa katika lindi la mawazo. Kila alipoulizwa na marafiki zake, kama alikuwa akifikiria juu ya nini, alisema: "Sijui nifanye nini kwa umma wa Muhammad, na jinsi ya kuteua amir atakayeuongoza baada ya kufa kwangu."

371

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Ni wazi kwamba Umar aliona kuteua mrithi wake lilikuwa ni jambo la umuhimu mkubwa sana kwa jinsi alivyotumia muda wake mwingi na akili kwenye suala hilo.

Wasiwasi wa Umar kuhusu uongozi wa umma baada ya kifo chake mwenyewe, ulichangi-wa na Aisha, mjane wa Mtume (s.a.w.). Tabari, mwanahistoria huyu, anasimulia yafuatayo kuhusiana na hili:

"Wakati Umar alipokuwa anafariki, alimtuma mwanae kwa Aisha kuomba ruksa ya kuzik-wa karibu na Mtume na Abu Bakr. Aisha akasema: 'Kwa furaha kubwa,' kisha akaongeza: 'Nitolee Salam zangu kwa baba yako, na mwambie kwamba asije akawaacha Waislamu bila ya kiongozi vinginevyo kutakuwa na vurugu baada ya kifo chake.'"

Aisha alionyesha wasiwasi mkubwa sana juu ya ustawi wa Waislamu kama vile tu ambavyo angepaswa kufanya. Wakati Umar alipokuwa anafariki, alimshauri asiuache umma bila ya kiongozi, ama sivyo, alionya, ghasia zitafuatia kifo chake. Inashangaza kwamba Aisha hakuwahi kumshauri mume wake mwenyewe kuteua kiongozi kwa ajili ya Waislamu, na hakumuonya kwamba ghasia zitafuatia kifo chake kama angewaacha bila ya kiongozi.

Lakiini Aisha, binti ya Abu Bakr, alikuwa na sababu nzuri tu ya kuwa na "makini" na mume wake, na hakulileta kwenye mjadala pamoja naye, suala la uteuzi wa mrithi, wakati wowote.

Swali la 6

Upi ulikuwa mwenendo (sunnah) wa Muhammad (s.a.w.) kuhusiana na uteuzi na uwekaji wa watumishi?

Jibu

Katika miaka kumi ya mwisho ya maisha yake, Muhammad (s.a.w.) aliandaa misafara ya kijeshi zaidi ya themanini. Aliwatuma wengi wao chini ya amri ya kiongozi fulani; mingine aliiongoza yeye binafsi.

Wakati wowote Muhammad (s.a.w.) alipotuma msafara nje, aliteua mmoja wa maswahaba zake kama kapteni wake. Aliwaamuru wale wapiganaji wa kawaida kumtii yeye, na akam-fanya huyo kapteni kuwajibika kwake yeye mwenyewe Mtume. Pale msafara uliporudi Madina, alimhoji yule kapteni ili kupata taarifa. Haikuwahi kutokea kwamba aliwaambia watu wa msafara au kikosi cha upelelezi kwamba walipaswa kuchagua au kuteua kapteni wao wenyewe.

Katika kadhia ambapo Muhammad (s.a.w.) alipokuwa akiongoza mwenyewe msafara nje ya Madina, aliteua gavana wa mji huo, na akamfanya mwenye mamlaka ya kusimamia she-ria na maagizo wakati wa kutokuwepo kwake yeye mwenyewe. Hakuwahi kuwaambia raia

372

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kwamba katika kipindi ambacho hatakuwepo, ilikuwa ni wajibu wao kujichagulia au kuji-teulia gavana wao wenyewe.

Katika mwaka 630 ambapo Muhammad (s.a.w.) aliiteka Makka, na kuijumuisha kwenye ile Dola mpya, aliteua mtawala kwa ajili ya mji ule, na alifanya hivyo bila ya kushauriana ama na watu wa Makka au na maswahaba zake mwenyewe.

Montgomery Watt:

"Kiasi cha madaraka ya utawala wa Muhammad katika miaka yake miwili au mitatu ya mwisho kinadhihirishwa na uteuzi wake wa "wakala" kusimama badala yake katika maeneo mbalimbali, na kwa hakika na suala zima la uteuzi wa nafasi za utawala. Tokea mwanzoni Muhammad aliteua watu kufanya shughuli mbalimbali ambazo yeye alihusika nazo. Hivyo aliteua makamanda wa misafara ambapo yeye hakuwepo binafsi. Uteuzi mwingine wa kawaida tangu nyakati za awali kabisa ulikuwa ni ule wa Kaimu hapo Madina wakati Muhammad alipokuwa hayupo hapo mjini."

(Muhammad at Madina, 1966) Maxime Rodinson:

"Yeye (Mtume) ama aliteua kiongozi au alichukua mamlaka mwenyewe. Anaelekea kuwa alikuwa na kipaji cha kijeshi kama alichokuwa nacho kwenye mikakati ya kisi-asa. Alikabidhi baadhi ya shughuli zake kwa watu ambao walikuwa kama mawakala wake binafsi. Wakati wowote, kwa mfano, alipoondoka Madina, alikuwa akiacha mwakilishi nyuma yake.

(Muhammad, kilichotafsiriwa na Anne Carter, 1971)

Hiyo ilikuwa ndio sera na mwenendo wa Muhammad Mtume wa Allah (s.a.w.), katika kuteua na kuweka watumishi wake, na kamwe haukuwa na ukengeukaji ndani yake kwa wakati wowote.

Swali la 7

Ni ipi Fatwa ya Qur'an juu ya mwenendo (sunnah) wa Muhammad (s.a.w.)?

Jibu

Kwa mujibu wa Qur'an, vitendo vya Muhammad ni vitendo vya Allah (s.w.t.) Mwenyewe. Msomaji mwislamu anatakiwa atafakari juu ya maana ya Aya zifuatazo za Qur'an Tukufu:

373

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Usahihi-41.jpg

Wakati ulipotupa (ukufi wa mchanga), Sio wewe uliyetupa, bali ni Allah Aliyetupa...(Sura ya 8; Aya ya 17)

Usahihi-42.jpg

Bila shaka wanaofungamana nawe,kwa hakika wanafungamana na Allah;Mkono wa Allah uko juu ya mikono yao:basi anayevunja ahadi yake, anavunja kwa kuidhulumu nafsi yake, na anayetekeleza alimuahidi Allah,Allah atamlipa ujira mkubwa. (Sura ya 48; Aya ya 10)

Waislamu wote wanaamini kwamba chochote alichokisema au kukitenda Muhammad (s.a.w.), kilikuwa ni wahyi kutoka Mbinguni. Kwa maneno mengine, alikuwa ni chombo ambacho amri za Mbinguni zilitekelezwa kupitia kwake.

Kama ilivyoelezwa kabla, Muhammad Mtume wa Allah (s.a.w) hakuchangia pamoja na mtu yeyote yule mwingine mamlaka yake ya kuteua gavana kwa ajili ya mji, au jemadari kwa ajili ya msafara wa kijeshi. Yeye na yeye peke yake aliyatekeleza tokea mwanzo hadi mwisho. La muhimu zaidi kuliko uteuzi wa gavana au jemadari, ilikuwa ni uteuzi wa mrithi wake mwenyewe, na mkuu wa baadae wa umma wa Waislamu. Hakukuwa na sababu ya kuigeuka sera na mwenendo wake mwenyewe, na kuuacha umma wake wote bila ya kiongozi. Tabia yake ilikuwa yenye msimamo thabiti, na ufuatao ni ushahidi wa Qur'an Tukufu:

Usahihi-43.jpg

"Hutapata mabadiliko katika mtindo wa Allah (wa utendaji), hutapata mageuko katika mwendo wa Allah (wa utendaji). Sura ya 35; Aya ya 43)

Huo (ulikuwa) ndio mwendo wa Allah (ulithubutu) uliokwisha pita zamani:

Usahihi-44.jpg

Wala hutapata mabadiliko katika mwendo wa Allah (uliothubutu). (Sura ya 48; Aya ya 23)

374

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Hakukuwa na mabadiliko katika mwenendo wa Mtume wa Allah (s.a.w.w). Hakuwatelekeza Waislamu ili waje kuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Alimteua binamu yake Ali ibn Abi Talib, kuwa mrithi wake, na kiongozi mkuu wa baadae wa umma wa Waislamu. Alimtambulisha Ali kwa umma huo kama mtawala wa baadae, katika Karamu ya Dhu ’l- 'Ashiira, mara tu baada ya tangazo la kwanza, hadharani la ujumbe wake kama Mtume wa Mwisho na Mkuu kabisa wa Allah (s.w.t.) ulimwenguni.

Swali la 8

Muhammad (s.a.w.) alifanya nini hasa kuhusu kurithiwa kwake?

Jibu

Muhammad aliunda Dola mpya - Dola ya Kiislamu. Katika kuunda Dola hiyo ya Kiislamu, lengo lake lilikuwa ni kuanzisha Ufalme wa Mbinguni Duniani. Hili alilifanya kwa msaada na ushirikiano wa binamu yake, Ali ibn Abi Talib. Alimchagua Ali miongoni mwa maswahaba zake wote, kumfuatia yeye, kama mkuu wa Dola ya Kiislam, na kama Mtawala wa Waislamu wote.

Kumteua Ali kama mrithi wake, Muhammad hakusubiri mpaka alipokuwa ameiunda hasa hiyo Dola ya Kiislam, na kuiimarisha kama ufalme wa mbinguni na duniani. Alimtangaza Ali kuwa mrithi wake katika wakati ambapo Dola hiyo haijawa na uhai wo wote. Alimtangaza Ali kuwa mrithi wake katika wakati uleule alipotangaza kwamba Allah (s.w.t.) amemtuma yeye kama Mtume Wake wa Mwisho kwa wanadamu.

Muhammad (s.a.w.) alimtaja Ali ibn Abi Talib kama mrithi wake kwenye Karamu ya Dhu ’l- 'Ashiira huko Makka wakati yeye Ali akiwa na umri wa miaka kumi na tatu tu; na alitumia muda wa uhai wake wote kumuandaa yeye kwa ajili majukumu mazito yaliyokuwa mbele yake.

Miaka ishirini baadae, katika bonde kubwa la Khum, karibu na Ghadiir, Muhammad (s.a.w.) alifanya matengenezo ya mwisho katika kazi yake aliualika umma wake, kwenye mkusanyiko mkubwa, kukutana na mkuu wao wa baadae. Kwa kufanya hivyo, alifuata amri ya Mbinguni iliyohifadhiwa katika Aya ya 70 ya Sura ya tano ya Qur'an Tukufu; na alitimiza wajibu wake juu ya umma wake. Umma wake ulikuwa na haki ya kujua ni nani atakaye uongoza baada ya kifo chake (yeye Muhammad).

Muhammad Mustafa (s.a.w.) hakumteua Ali kuwa mrithi wake kwa kufafanua au kutafsiri tu sheria za Kiislam. Alimteua Ali kuwa mrithi wake kwa kuzitenda na kuzitekeleza she-ria hizo. Kwa maneno mengine, alimteua Ali kuongoza serikali ya Kiislam.

Kama kuna sheria, lazima awepo mtu wa kuidumisha - katika dola ya mji wa Madina -

375

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kama kwingineko. Kitendo pekee cha kupitisha sheria hakina maana yoyote. Yenyewe peke yake, sheria haiwezi kuhakikisha usalama, ustawi na furaha ya mwanadamu. Baada ya sheria kupitishwa, ni muhimu pia kuunda nguvu ya utendaji, ya kuitekeleza. Kama sheria haiwezi kudumishwa, haiwi ni chochote zaidi ya kipande cha karatasi. Kama serikali inakosa mamlaka ya utendaji, haiwezi hata kuitwa ni serikali. Kwa hiyo, pale Uislamu ulipopitisha sheria, uliunda pia mamlaka ya utendaji.

Katika wakati wa Muhammad Mtume wa Allah (s.a.w.), sheria hazikuwa zikifafanuliwa na kutangazwa rasmi tu; zilidumishwa na kutekelezwa pia. Yeye alizidumisha na kuzitekeleza.

Muhammad (s.a.w.) alimteua Ali kudumisha sheria za Kiislamu, na kutekeleza amri za Allah kama zilivyoshushwa kwake ndani ya Qur'an. Alimteua Ali kushika mamlaka ya utendaji juu ya Waislamu, baada ya kifo chake yeye mwenyewe.

Swali la 9

Ni nini hasa kilichotokea baada ya kifo cha Muhammad (s.a.w.)?

Jibu

Baada ya kifo cha Muhammad Mustafa, aliyebarikiwa, Ansari walijikusanya katika banda la Saqifah ili kuchagua kiongozi. Abu Bakr, Umar na Abu Ubaidah - Muhajirina hawa watatu - waliwatembelea. Waliwaambia hao Ansari kwamba kwa vile Muhammad (s.a.w.) hakuteua mrithi wake, iliwabidi wachagua mtu wa kujaza nafasi hiyo. Kitendo chao, walisema, hakikuwa tu ni halali bali pia kilikuwa ni muhimu sana, ikiwa ni kwa kuuokoa umma kutokana na vurugu na ghasia.

Hawa Muhajirina watatu waliingia kwenye majadiliano makali na Ansari mle Saqifah. Mada ya mjadala huo ilikuwa: ' Je, mrithi wa Muhammad (s.a.w.) na mtawala wa Waislamu awe ni Muhajir (wa Makka) au Ansari (wa Madina).' Wasemaji wakali waliijadili mada hii vya kuchosha.

Ingawa kulikuwa na mambo mengine muhimu ambayo hayakuwa kwa jumla yasiyohusi-ka kwenye mjadala huo, kama vile matakwa ya Allah (s.w.t.) na Mtume Wake (s.a.w.), sifa zilizohitajika kwa mgombea au wagombea kwenye nafasi iliyowazi ya mtawala wa Arabia, na maslahi ya Uislamu na umma wa Waislamu, hayo hayakujadiliwa. Masuala haya hayakuwemo kwenye "ajenda" za mkutano huo mle Saqifah. Wasemaji hao, kwa hiyo, hawakutoka nje ya mada yao.

Hatimaye, kwa ustadi, uvumilivu na kwa maarifa, hawa Muhajirina watatu walilisuluhisha kwa mapatano tatizo hili, au, kiasi, walitunga "papo kwa papo" ufumbuzi wake.

376

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Francesco Gabrieli:

"Katika lile baraza la vurugu lililofanyika kwenye makao makuu ya Banu Sa'idah hapo Madina, Umar, takriban kama kwa kushitukiza, alimuweka Abu Bakr kama khalifa au mrithi wa Mjumbe wa Allah. Kama matukio mengi na asasi nyingi, ukhal-ifa ulizaliwa katika ufaraguzi.

(The Arabs - A Compact History, 1963)

Ukhalifa au uongozi wa umma wa Waislamu ndio taasisi muhimu sana ya kisiasa katika Uislamu wote.

Kwa kweli, kuweko hasa kwa Uislamu kunategemea juu ya khalifa au kiongozi wa umma. Kwa hiyo, haisadikiki kwamba uliachwa si kwenye ubora wowote bali ufaraguzi! Itakuwa haishangazi kwamba ulimwengu wa Kiislamu umekuwa mara kwa mara umefunikizwa kwenye damu juu ya suala la urithi na uongozi.

Vita, mapambano ya wenyewe kwa wenyewe, mapinduzi, migogoro, uchochezi na ghasia zimekuwa haziepukiki wakati umma ulipochagua ufaraguzi mle Saqifah, badala ya kielele-zo cha ki-ungu na "mpango" wa majaaliwa wa Muhammad Mustafa (s.a.w.), kwa ajili ya upokezanaji wa utaratibu mzuri na wa amani wa mamlaka kutoka kwake mwenyewe kwenda kwa mrithi wake.

Watetezi wa Saqifah wanasema kwamba kitendo cha Umar kilichochewa na shauku yake ya kuzuia uongozi wa umma kutokana na kuwa daima mali ya familia moja - hasa, famil-ia ya Muhammad Mustafa (s.a.w.). Wanasema kwamba ukiritimba kama huo wa mamlaka ungeweza kuwa ni "janga" kwa Uislamu. Hoja hii ambayo ni ngumu kueleweka, ya wanahistoria wa Sunni imekuwa ni kipokeo cha kawaida na kisichoeleweka cha siku-za-baadae kinachoimba maangamizi. Lakini hakuna hata mmoja kati yao ambaye amewahi kueleza ni kivipi.

Kama baada ya kifo cha Muhammad (s.a.w.) utawala wa Waislamu ungegeuka kuwa "mali" ya familia yake mwenyewe, hivi Waarabu wangeukana Uislamu, na kurudi kwenye uabudu masanamu? Au Waajemi na/au Warumi wangeivamia na kuiteka Arabia na kuwaangamiza Waislamu wote?

Katika mawazo ya Abu Bakr na Umar, kulikuwa na njia moja tu ya "kuuokoa" umma wa Muhammad (s.a.w.) kutokana na "janga," na hiyo ilikuwa ni kwa kuikataa familia yake kwenye uchaguzi, na kwa kujitwalia serikali yake wao wenyewe!

Umar alikuwa na shauku kwamba ukhalifa usije ukawa ni wa kurithiana katika ukoo

377

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

mmoja wowote ule, na kwamba unapaswa kubaki ukizunguka miongoni mwa Waislamu ili kwamba "kila kijana wa Kiarabu aweze kuwa na bahati ya kuwa khalifa." Hata hivyo, licha ya ndoto na tahadhari juu ya mambo ya baadae ya Umar, ukhalifa ulikuja kuwa wa kurithi-ana ndani ya miaka kumi na sita ya baada ya kifo chake mwenyewe.

Lakini ulikuwa wa kurithiana siyo katika familia ya Muhammad (s.a.w.) bali katika famil-ia ya maadui zake wakuu - wale watetezi wa upagani wa Makka - wale watoto wa Abu Sufyan na Hinda. Hivyo ndoto za Umar hazikuendelea zaidi ya miaka kumi na sita labda kama lilikuwa ni lengo lake kwamba ukhalifa uje kuwa wa kurithiana katika nyumba ya Abu Sufyan. Kama ilikuwa hivyo, basi lazima ikubalike kwamba yeye alikuwa ni mtu wa ajabu kweli kutokana na ndoto zake.

Abu Bakr na Umar walifanikisha muujiza wa ufaraguzi mle Saqifah.

Akizungumzia juu ya machafuko kufuatia kifo cha Muhammad (s.a.w.), na akitoa sababu zake za kwa nini binamu yake, Ali, alikataliwa katika kugombea ukhalifa, Sir John Glubb anaandika hivi:

"Waarabu hawakuwa tayari kamwe kutoa heshima kwenye fahari, daraja, au fursa za kurithiana au vyeo.

(The Great Arab Conquests, 1963)

Uchambuzi huu, wa mwanahistoria huyu, wa tabia ya Kiarabu, unakwenda kinyume na ushahidi wa historia. Watawala wa kale wa Uturuki (Seljukes), Mamluki, na watawala wa Uthmainia (Ottoman Turks) waliwatawala Waarabu kwa karne nyingi. Waarabu waliwatii kama kondoo. Wao, kwa kweli, waliukubali ule usemi usio na uthibitisho wa kwamba Waturuki wawe wanaamrisha, na wao Waarabu wawe ni wenye kutii.

Hakuna yeyote anayeweza kusema ni kwa muda mrefu kiasi gani zaidi huo utawala wa Kituruki juu ya ardhi za Waarabu ungechukua kama Waingereza na Wafaransa wasingeusi-mamisha.

Katika kusalimu amri kwao kwa jumla na kwa kinyonge kwa Waturuki, Waarabu walikuwa wakitoa heshima kabisa kwenye "fahari, daraja au fursa za kurithiana au vyeo." Kwa karne nyingi Waturuki walizitawala nchi za Kiarabu kwa ukali, na hakuna aliyewahi kusikia manung'uniko japo madogo sana ya upinzani kutoka kwa Waarabu.

Kwa hakika, Waarabu hawana tofauti na watu wengine ikiwa ni pamoja na Waingereza, ambao na mwanahistoria huyu mwenyewe anatokana nao. Kama wengine wanatoa heshima kwenye fahari, daraja, au fursa na vyeo, Waarabu nao wanatoa heshima kwavyo. Haieleweki ni kwa nini Sir John Glubb ana shauku ya kufanya mambo ya kutukuzwa sana

378

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

kwa Waarabu!

Mwandishi huyo huyo anaendelea kusema:

"(Utawala wa) Kurithiana hakukukubaliwa na Waarabu kama msingi wa kufaa wa kupokezana mamlaka. Katika uteuzi wa wakuu wa kawaida, mgombea aliyefaa zaidi, wa familia inayotawala kwa kawaida ndiye aliyechaguliwa. Katika uteuzi wa khalifa, chaguo la kawaida kabisa, na lile ambalo katika nadharia ndilo lilifanywa katika kadhia za wale wanne wa kwanza, lilikuwa ni lile la kiongozi wa Kiislam anayefaa zaidi.

Kwa vitendo ugumu wa kuteua mgombea safi na hatari inayojitokeza ya vita vya wenyewe kwa wenyewe mara nyingi ulisababisha matumizi ya haki ya kurithi kwa mtoto wa kwanza katika falme za Kiislamu za baadae.

Waarabu, hata hivyo, kamwe hawakuutwaa ule utaratibu wa urithi wa moja kwa moja wa mtoto mkubwa."

(The Great Arab Conquests, 1963)

Mwanahistoria huyu, inavyoelekea, kwa mara nyingine tena, yuko kinyume na mambo. Pale anaposema kwamba kurithiana kamwe hakukukubaliwa na Waarabu kama msingi unaofaa wa kupokezana mamlaka, anapaswa kuweka wazi, kwamba Waarabu anaowazungumzia, walitokana na kizazi cha wakati wa Mtume (s.a.w.) mwenyewe, na sio na wale waliokuja baada yake. Ndani ya miaka thelethini ya kifo cha Mtume (s.a.w.), Waarabu hao hao walikuwa wakinyenyekea kwa miguuni kwa yule khalifa wa Syria, na waliukubali urithianaji kama msingi unaofaa wa kupokezana mamlaka bila haya. Sio kwamba walimkubali tu Yazid, mtoto wa Mu'awiyah, kama khalifa wao halali, bali kwa miaka 600 iliyofuatia, yaani, mpaka kukomeshwa kwa ukhalifa wenyewe mnamo mwaka 1258, hawakuwahi kuuliza swali kuhusu haki ya mtoto wa khalifa kumrithi baba yake.

Geoffrey Lewis:

"Kwa khalifa wa tano, yule mwenye nguvu sana Mu 'awiyah (661 -680), cheo hicho (ukhalifa) kilikuwa ni cha kurithiana kiukoo. Utawala wake wa Bani Umayya ulichukuliwa nafasi yake na ule wa Bani Abbas mnamo mwaka 750."

(Turkey, 1965)

Dr. Hamid-ud-Din:

" Kuanzia wakati wa Mu'awiyah, kiti cha ukhalifa kilikuwa ni haki ya kurithiwa ya Bani Umayya. Kila khalifa alimteua mwanae au ndugu mwingine yoyote kama mrithi wake, na Waislamu kwa unyenyekevu kabisa walimkubali kama khalifa wao, nao

379

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

hawakuuliza maswali."

(History of Islam, 1971, uk. 364 kilichotolewa na Ferozsons Ltd,

Karachi na Lahore, Pakistan).

Waarabu pekee ambao hawakukubali urithianaji wa kiukoo kama msingi wa kupokezana mamlaka, walikuwa ni maswahaba wa Muhammad (s.a.w.) mwenyewe. Sababu yao ya kutokubali urithianaji kama msingi wa kupokezana mamlaka, ilikuwa ni mtazamo wa heki-ma. Kama wangekubali urithianaji wa kiukoo kama msingi wa kupokezana mamlaka, basi kungekuwa hakuna njia ya wao kuwa makhalifa.

Katika nadharia ya Shia juu ya serikali, urithianaji wa kiukoo hauchukuliwi kama msingi wa kupokezana mamlaka. Kwa mujibu wa nadharia ya Shia, haki ya kuchagua mrithi wake mwenyewe, ilihusika pekee kwa Muhammad Mustafa (s.a.w.), na sio kwa maswahaba zake; na yeye alimchagua Ali. Na hakumchagua Ali kwa sababu ya udugu, bali kwa sababu ilikuwa ni amri ya Allah (s.w.t.) kwake yeye kufanya hivyo.

Pale Waarabu walipokataa kukubali kule kuteuliwa na Muhammad Mustafa (s.a.w.) kwa Ali ibn Abi Talib kama mrithi wake, hawakuwa kwa hakika wakitetea "kanuni." Kukataa kwao kulikuwa ni mwanzo tu wa kuondoa kituo maalum cha madaraka na mamlaka kuto-ka kwenye nyumba ya Muhammad (s.a.w.). Mara tu "kanuni" ilipotimiza lengo lao, wao -Waarabu - walikuwa wa kwanza kuitelekeza.

Laura Veccia Vaglieri:

"Kuelekea mwishoni mwa utawala wake, Mu'awiyah, akitumia ustadi wake wote wa kidiplomasia, alimudu kuwashawishi wale watu mashuhuri wa himaya hiyo kumtam-bua mwanae Yazid kama mrithi kwenye utawala, bila kuigusa ile kanuni kwamba hes-hima kuu lazima itolewe katika muda wa kurithi. Kwa njia hii alipata muafaka. Kinadharia, hiari ya wachaguzi iliheshimiwa, kwa vile ilikubalika kwamba wanaweza kumkataa yule mrithi aliyeteuliwa na mkuu anayetawala (kwa kweli, ni watu mashuhuri wanne au watano tu waliokataa kuridhia ombi la Mu'awiyah), lakini kwa hali halisi hii ilidokeza kufutwa kwa mfumo wa uchaguzi, ambao ulikuwa ndio chan-zo cha matatizo mengi huko nyuma, na ilianzisha urithianaji wa kiukoo.

Mageuzi ya Mu'awiyah yalifuatwa na makhalifa wote waliokuja baada yake, na yali-wawezesha Bani Umayya kushikilia madaraka kwa miaka 90, na Bani Abbas kwa karne tano."

(Cambridge History of Islam, 1970)

Mu'awiyah alipuuza ile "kanuni" ya uchaguzi ambayo haikuwa ni chochote zaidi ya kichekesho hata hivyo.

Hata hivyo, katika shughuli yote hii iliyopinda ya "kuchagua" au "kupendekeza" au

380

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

"kuteua" mtawala wa Waislamu, kulikuwa na "kanuni" mmoja iliyokuwa ikifanya kazi. ilikuwa ni ile "kanuni" ya kuwaondoa watu wa familia ya Muhammad Mustafa Mtume wa Allah (s.a.w.) aliyebarikiwa, kutoka kwenye mahali maalum pa madaraka na mamlaka. Saqifah, kwa kweli, ilikuwa ni vuguvugu ya nguzo imara, iliyounganishwa na kuchanganyika ya maswahaba wakubwa na wasaidizi wao ya kuwaondoa Bani Hashim kutoka kwenye serikali ya Kiislam. Kama ungekuwepo msimamo thabiti wowote ama kati-ka matendo ya makhalifa watatu wa kwanza, au, mwingine wa maswahaba, au wa Bani Umayya na Bani Abbas, ulikuwa ni katika kuitumia "kanuni" hii. Katika jambo hili, yalikuwepo makubaliano miongoni mwao wote. Ilikuwa ndio asili na kiungo muhimu cha sera yao wote iliyopangwa na kuratibiwa. Hata kwa zile falme ambazo zilikuwa zifuatie za Bani Umayya na Bani Abbas, ishara za Saqifah zilikuwa na nguvu, dhahiri na bayana. Walifuata masharti, kwa uaminifu, takriban kwa ushabiki uliokithiri ya "sera" iliyoundwa kwenye ukumbi wa Saqifah. Kiini cha sera ile kilikuwa ni uadui wa wazi kwa Ali ibn Abi Talib, binamu wa kwanza wa Muhammad (s.a.w.), na kwa Bani Hashim, ukoo wa Muhammad (s.a.w.).

Swali la 10

Je, suala la urithi lina umuhimu gani katika historia kwa jumla?

Jibu

Suala la kurithisha au kuhamisha madaraka kutoka kwa mwenye cheo mmoja kwenda kwa mwingine, limekuwa moja ya matatizo magumu na yenye mzozo ya historia ya mwanadamu. Katika kadhia nyingi, tatizo hili limetatuliwa katika juhudi ambamo mbinu zote zinakubalika, na madaraka yamekuwa ni tunzo la yule aliyekatili zaidi kati ya wag-ombea. Ukweli kwamba taifa lina serikali ya kikatiba, hakuihakikishii kwamba itakingika kutokana na ugombaniaji wa madaraka. Ugombeaji wa Stalin na Trotsky baada ya kifo cha Lenin mnamo 1924, na kuuawa kwa Beria baada ya kifo cha Stalin mnamo 1953, ni miwili kati ya mifano mingi kutoka kwenye historia ya sasa.

Kwenye matukio yasiyo na idadi ndani ya historia, suala la urithi limechokonoa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambamo wanaume na wanawake wasio na idadi wameangamia. Wengi wetu tunaweza kushawishika kujigamba kwamba tumepitia zama hizo za kikatili ambamo maelfu ya wanaume na wanawake waliuawa kabla suala la ni nani atakayekuwa mtawala halijafumbuliwa. Lakini hakuna sababu ya kutojali. Kugombea madaraka kunaweza kuibuka mahali popote wakati wowote bila kukwepa tu baadae kama ilivy-otokea huko nyuma. Harakati za kichini chini huenda zinatokota wakati wote lakini kwa hakika zinakuja kuchemka wakati kiongozi wa nchi atakapofariki.

Geoffrey Blainey:

"Uchunguzi wa sababu zinazofanana kwenye vita nyingi za karne ya kumi na nane unaonyesha ishara moja ya wazi. Kifo cha mfalme kilikuwa mara nyingi ndio dalili ya vita. Kiungo kinawakilishwa kwenye majina maarufu yaliyotolewa kwenye vita

381

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

nne muhimu. Kwa namna hii kulikuwa na Vita ya urithi wa Hispania, na vita ya urithi wa Uholanzi, na zilifuatiwa na vya urithi wa Australia na kisha wa Bavaria Majina yao kiushawishi yanamaanisha kwamba suala la nani afuatie kwenye kiti kilichokuwa wazi lilikuwa ndio chanzo kikuu cha vita hizo.

Vita hizi nne za urithi hazikuwa ndio vita pekee ambazo zilitanguliwa na kushawishi-wa na kifo cha mtawala. Mnamo mwaka 1700, watawala wa Saxony, Denmark na Urusi waliingia vitani dhidi ya Sweden ambayo mtawala wake kijana, Charles X11, hajakaa muda mrefu kwenye madaraka. Katika mwaka wa 1741 vikosi vya Sweden vilivamia Urusi, ambayo mfalme wake wa kabla ya mapinduzi, alikuwa na umri wa mwaka mmoja. Mnamo 1786 kifo cha Frederick Mkuu wa Prussia aliandaa njia ya mapambano ya Austri-Russia dhidi ya Uturuki katika mwaka uliofuata. Na mnamo Machi, 1792 kifo cha Mfalme Leopold II huko Vienna kilikuwa ni moja ya matukio yaliyoashiria Tangazo la Ufaransa la vita dhidi ya Austria katika mwezi uliofuatia.

Katika vita zote nane za karne ya kumi na nane ziliashiriwa na kushawishiwa na kifo cha mfalme; na vita hizo zilianzisha nyingi ya vita kubwa za karne hiyo. Wala vita hivyo vya kukesha na mgonjwa anayekaribia kufa havikukoma kabisa baada ya 1800. Hivyo vita mbili kati ya Prussia na Denmark zilitanguliwa na vifo vya wafalme wa Kidenishi, vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani vilifuatia kifo cha raisi mnamo 1861, Vita Vikuu vya Kwanza vilitanguliwa na kuuawa kwa mrithi wa Austria."

(The Causes of War, 1973)

Kugombea madaraka ni tabia ya kudumu ya historia ya mwanadamu. Huko nyuma, kwa mara nyingi kifo cha mfalme kilikuwa ni ishara ya maasi katika nchi yake mwenyewe. Kama alikuwa ameikamata nchi pamoja kwa uongozi madhubuti, kifo chake kilichukuli-wa kama ni fursa ya kuishambulia serikali kuu, na kudai uhuru wa jimbo lenye upinzani. Mara nyingine, kifo cha mfalme kilikuwa ni kukaribisha majirani wenye tamaa kuivamia nchi yake kwa matumaini kwamba huyo kiongozi mpya, kwa kukosa uzoefu, hatakuwa na uwezo wa kutoa upinzani wenye nguvu kwao, na watajitwalia nchi mpya wenyewe.

Historia ya tawala za Kiislamu imeloweshwa katika damu za Waislamu. Huko nyuma, wakati wowote mfalme au sultani alipofariki, wanae na ndugu zake walirukiana makooni kuchinjana. Wakati mwingine wadogo na hata watoto wachanga hawakuachwa kama walikuwa kwenye nasaba ya moja kwa moja kutoka kwa mtawala, na kwa hiyo, walikuwa wenye uwezekano wakuwa vyanzo vya matatizo. Wakati wa kifo cha mtawala, kuenea kwa vita na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe, na maasi katika majimbo, vilionekana kuwa ni kawaida.

Wanahistoria wengi wa kisasa ambao wamesoma nadharia ya kisiasa ya Uislamu na uwezekano wake, na wamejaribu kuanisha sababu na athari, wameihusisha migogoro ya

382

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

ndani ya Uislamu na vita vya "kushindwa" kwa Muhammad Mustafa (s.a.w.) kuteua mrithi wake mwenyewe. Kuna dokezo lililofichwa au mifano yenye shaka katika vitabu vyao kwamba "alihusika" nazo. Lakini baadhi ya mifano mingine haikufichika au kuwa na shaka kiasi hicho.

Edward Jurji:

"Hali ya kivita, iliyokuwepo kati ya Mtume na ndugu zake, ilifikia kikomo katika ushindi kamili wa majeshi ya Kiislam uliofikishwa kileleni na kuingia kwa ushindi kwa Muhammad katika mji alimozaliwa kwa kubomoa kumbukumbu za uabudu masanamu. Ingawa kazi yake ilibakia ya Kiutume, Muhammad alikuwa ameongeza kuja kutumia upanga wa kiongozi wa kijeshi na kusimamia mambo ya dola ya kisi-asa yenye hima, akitambua wajibu wa dola hiyo katika historia. Kifo chake kilipo-tokea tarehe 8 Juni, 632, alirithisha kwa wafuasi wake urithi wa dini-na-siasa daima ulioelemewa na kusumbuliwa kwa karne nyingi na jukumu la kupata khalifa (mrithi) anayekubalika kujaza nafasi ya juu kabisa katika Uislamu. Ukhalifa (urithi) kama jambo, lililokuzwa na kimya cha kuchosha cha Mtume juu ya suala la ni nani angem-fuatia, lilikuwa ni mzizi wa uovu mwingi, na balaa la ndani kubwa la Uislamu, chan-zo cha mipasuko na mifarakano, na urithi wa kuhuzunisha wa machozi na damu."

(The Great Religions of the Modern World, 1953)

Kwa mujibu wa mwanahistoria huyu, kilikuwa ni "kimya kinachochosha cha Mtume (s.a.w.) juu ya suala la, ni nani angemfuatia yeye, ambalo lilikuwa "mzizi wa uovu mwingi, balaa kubwa ya ndani ya Uislamu, chanzo cha mipasuko na mifarakano, na urithi wa kuhuzunisha wa machozi na damu."

Hivi huu ndio "urithi" ambao Muhammad (s.a.w.) aliouachia umma wake? Ikiwa Waislamu wa sasa wanaamini kile kioja cha Saqifah kwamba hakuteua mrithi wake mwenyewe, basi watakubaliana na uamuzi wa mwanahistoria huyu. Lakini kama watakubaliana na uamuzi huu, itawabidi wapingane na Qur'an Tukufu ambayo imemuita Muhammad ni "rehma kwa ulimwengu mzima."

Sir John Glubb:

"Mtume alifariki bila ya kuacha maagizo yoyote kuhusiana na mrithi. Ilipofahamika tu kwamba amefariki, watu wa Madina walikusanyika pamoja na wakaamua kuch-agua mkuu wao wenyewe. Upinzani wa wadai wa ukhalifa ulisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Waislamu visivyokwisha, ambavyo labda vingeweza kuepukwa kama Muhammad angeweka sheria kwa ajili ya urithi (ushika makamu)."

(A Short History of the Arab Peoples, 1969)

383

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Kama Waislamu wa sasa, baada ya kusoma fatwa hii ya mwanahistoria, bado wanashikil-ia kwamba Mtume wao hakuchagua mrithi wake mwenyewe, basi lazima wakiri kwamba vile vita vyote vya umwagaji damu vya wenyewe kwa wenyewe vya historia yao, vilikuwa ni "zawadi" yao kutoka kwake - kutoka kwake yeye ambaye alikuwa ndiye mfano wa rehema. Je, vita, hususan vya wenyewe kwa wenyewe, ni laana au ni baraka? Kama ni laana - na hakuna laana kubwa katika dunia kuliko vita - hivi wataamini kwamba Mtume wao alikuwa ndiye mletaji kwao Uislamu - wa amani?

Kwa kweli, moja ya malengo ya Muhammad (s.a.w.), kama Mtume wa Allah (s.a.w.w), lilikuwa ni kufuta vita, na kurudisha amani ya kweli ulimwenguni. Vita ndio laana kubwa kabisa, na amani ni moja ya baraka kuu za Allah (s.w.t.) Yeye alikuwa ni Mtume wa Amani. Kwa kweli, harakati aliyoianzisha, yenyewe iliitwa Amani au Uislamu. Kama Mwislam anaamini kwamba Muhammad alikuwa mchocheaji wa vita na umwagaji damu, atakoma kuwa mwislamu.

Sasa chaguo mbele ya mwislamu ni rahisi: ama anaamini kwamba Muhammad

haku..(narudia) hakuteua mrithi wake mwenyewe, au anaamini kwamba alifanya hivyo.

Kama anaamini kwamba Muhammad (s.a.w.) hakuteua, basi itamaanisha kwamba alileta huzuni na misiba yote iliyopita na ya baadae juu ya umma wa Waislamu. Imani kama hiyo itakuwa, kwa kweli, ni "ukosoaji" wa kimya kimya wa mwislamu, kumkosoa Muhammad kwa "kosa la kutofanya vizuri" kazi yake. Lakini ajiulize yeye mwenyewe kama anaweza "kumkosoa" yule Mtume wa Mwisho na Mkuu kabisa wa Allah (s.w.t.) na bado akawa ni mwislamu!

Kama mwislamu wa wakati huu anaamini kwamba Muhammad (s.a.w.) aliteua mrithi wake mwenyewe, basi lazima akiri kwamba ule mkutano uliofanyika pale Saqifah ulikuwa "hauna mamlaka" kwa sababu ulifanywa kwa ukaidi wa amri za Allah (s.w.t.) na Mtume Wake (s.a.w.). Maovu yote, mabalaa ya ndani ya Uislamu, mipasuko na mifarakano, ule urithi wa huzuni wa damu na machozi, na vita vya wenyewe kwa wenyewe visivyo na kikomo vya Waislamu, vilikuwa na chanzo chao mle Saqifah.

Uislamu umetoa uhuru wa chaguo kwa Waislamu wote. Kwa upande mmoja wanao uamuzi wa majaaliwa wa Muhammad (s.a.w.); na kwa upande mwingine, kuna ule uamuzi uliofanywa kwenye ukumbi wa Saqifah. Wanaweza kuchagua wowote wanaoutaka.

Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.a.w.w) na mfasiri wa Qur'an, alikuwa ndiye mwenye ujuzi zaidi kati ya wanadamu. Sio tu kwamba alikuwa na ujuzi wa historia, na ujuzi wa sababu za kuibuka, kupungua nguvu na kuanguka kwa mataifa, alikuwa pia na ujuzi na ufahamu wa asili ya mwanadamu. Mikondo ya historia yote ilikuwa yenye kuju-likana kwake. Kwa sababu alikuwa amejaaliwa na ujuzi kama huo, hakuliacha suala la urithi kwenye nafasi ya kubahatisha. Alikuwa ameanza utekelezaji wa ratiba ya kujenga upya jamii ya wanadamu, na alikuwa ameanzisha Ufalme wa Mbingnii juu ya Ardhi. Na

384

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

alijua kwamba hataishi milele.

Muhammad (s.a.w.) alijua kwamba atakufa lakini ujumbe wake utaishi. Ujumbe wake uli-hitajia kuendelezwa. Kuendelezwa kulikuwa ni muhimu sana kwa mafanikio ya ujumbe wake, na chochote kilikuwa kisiukatishe, sio hata kifo chake mwenyewe. Kwa hiyo ili kutoa mwendelezo kwenye kazi yake, alimchagua Ali ambaye ingawa bado mdogo kwa miaka, alikuwa ndio mfano halisi wa sifa zote za uongozi katika Uislamu. Muhammad (s.a.w.) alitoa tamko la majaaliwa katika karamu ya Dhu ’l- 'Ashiira kwamba Ali alikuwa ni waziri wake, mshikamakamu na mrithi wake. Lakini pia alikuwa amefanya uchunguzi wa maisha na uchambuzi yakinifu wa tabia na uwezo wa Ali, na akammwona yeye ni asiyelin-ganishika.

Ali alikuwa wa namna ya kipekee. Alikuwa ni mtu mwenye-uwezo zaidi katika Uislamu!

Hata kama hakuna ushahidi wa kihistoria unaoweza kupatikana kwamba Muhammad (s.a.w.) aliteua mrithi wake mwenyewe, bado inawezekana kufanya tafsiri chache kutoka kwenye tabia na mwenendo wake. Alikuwa mwangalifu, mwenye hadhari na makini wa iti-faki katika maisha ya ndani na ya nje. Busara, kuona mbali na upangaji makini uliainisha kazi yake. Madai ya kwamba hakuuambia umma wake ni nani atakayeuongoza katika vita na amani, na ni nani atakayeuelekeza katika dharura nyingine za maisha, ni kinyume kabisa na tabia yake.

Muhammad (s.a.w.) alikuwa ndiye mwalimu wa Waislamu. Aliwafundisha kila walichok-ijua. Juu ya elimu ya Uislamu, hakuwaficha chochote kile. Kudai kwamba aliwaficha taar-ifa yenye muhimu sana kwao, yaani, jina la mtu ambaye atashika usukani wa chombo cha Uislamu, baada ya kifo chake yeye mwenyewe, kunashindana na kanuni zote za maarifa ya kawaida na mantiki.

Itakumbukwa kwamba wakati Muhammad Mustafa (s.a.w.) alipokuwa yuko Makka, wakazi wa Makka walileta fedha na vitu vyao vya thamani kwake kwa ajili ya kuvihifad-hi - kabla na baada alipoanza kuutangaza Uislamu kwa sababu walimuamini. Uaminifu na ukweli wake vilikuwa havina shaka yoyote.

Katika mwaka 622 A.D. Muhammad Mustafa (s.a.w.) alihama kutoka Makka na kwenda Madina. Kabla ya kuondoka Makka, alimfanya Ali mwenye-mamlaka kwa ajili ya kurud-isha amana zote kwa wenyewe (wapagani) - wenyewe wale wale waliokuwa na uchu wa kumuua yeye kwa kutangaza Uislamu. Lakini amana ni kitu kitakatifu, na lazima kiheshimiwe na kila mtu, hususan na Mtume wa Allah!

"Amana zinaweza kuelezewa au kutekelezwa. Amana za kuelezwa ni zile ambapo mali imekabidhiwa au kazi inatolewa na mtu kwa mtu mwingine anayemwamini, kuitekeleza ama mara moja au katika dharura nyinginezo maalum, kama vile kifo.

385

Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu

Amana za kutekelezwa zinatokea kwenye madaraka, au nafasi, au fursa; kwa mfano, mfalme anashika falme yake kwa dhamana kutoka kwa Allah kwa ajili ya watu wake."

(A. Yusuf Ali, Mtarjumu na Mfasiri wa Qur 'an Tukufu).

Baada ya kuondoka kwa Muhammad kutoka Makka, Ali alirudisha amana zote kwa wenyewe.

Lakini kwa Muhammad (s.a.w.) hakukuwa na "amana" kubwa zaidi kuliko Uislamu. Allah (s.w.t.) aliweka juu yake wajibu wa kufikisha amana hii kwa wanadamu wote. Kwa hiyo, kabla ya kifo chake, ilimlazimu kumfanya mtu kuwa na dhamana ya kusimamia "amana" hii.

Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Uislamu, alimfanya Ali mwenye-mamlaka ya kusimamia "amana" hii; na kwa usemi wake wa kisiasa - Serikali ya Madina.

Dhamana bora ya usalama wa Dola ambayo Muhammad (s.a.w.) alikuwa ameianzisha, ilikuwa ni katika kuwafahamisha Waislamu ni nani atakayekuwa kiongozi wao baada ya kifo chake yeye mwenyewe. Usalama wa Dola hiyo utakuwa, kwa kweli, umehatarishwa vibaya kama angeshindwa kuwajulisha wafuasi wake ni nani atakayemfuatia yeye kama Mtendaji Mkuu.

Hakuna mwislamu ambaye angethubutu kudhania kwamba Muhammad Mtume wa Allah (s.a.w.), angesema au kufanya kitu chochote chenye madhara kwenye maslahi ya Uislamu. Wala ambaye angethubutu kudhania kwamba Muhammad (s.a.w.) angesema au kufanya kitu kisicho na mantiki.

Kuchukulia kwamba Muhammad (s.a.w.) hakuteua mr