U L A W I T I

           DHAMBI   KUU

                                                     YAMEANDIKWA NA:

                            AYATULLAH  SYED DASTAGHIB SHIRAZI (a.r.)

  

                                                    YAMETARJUMIWA NA:

                                                  AMIRALY  M.  H.  DATOO

                                                     BUKOBA - TANZANIA

 

                                                       YALIYOMO

Ulawiti ni kufr (ukafiri).......................................... 3

Mlawiti  miongoni mwa watu wa Mtume Lut a.s.................. 5

Ulawiti ni tendo la kuaibisha............................................................. 6

Kumtazama kijana  mtazamo wa ashiki au uzinifu............ 7

Busu ya kiashiki na  hatamu ya Motoni........................................ 7

Kulala pamoja kwa watu wawili wa jinsia moja............... 8

Adhabu za Ulawiti......................................................................................... 8

Je kwa nini ulawiti unaadhibiwa kwa kifo ?........................... 9

Moto haukumchoma aliyefanya Tawba................................... 11

Mambo ya kuzingatia............................................................................... 13

Mama, Dada na Binti wa Mlawiti...................................................... 13

Madondoo kutoka kitabu cha NDOA KATIKA ISLAM .......... 13

Ulawiti wa kila aina................................................................................. 13

Zinaa....................................................................................................................... 14

Fatwa za Mujtahid kuhusiana na ulawiti............................... 15

 


Mojawapo ya madhambi ambayo imechambuliwa kama ndilo dhambi kuu ni ulawiti[1] au kuingiliana jinsia moja.  Hivyo imethibitishwa na al-Imam as- Sadique a.s.  na Al-Imam Ali ar-Ridha a.s. Kwa hakika dhambi hili ni kubwa hata kuzidi dhambi la zinaa. Madhambi na adhabu  yake ni zaidi ya zinaa. Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Al-Kafi :

 

“Kuingiza mwanzoni mwa mkundu ni dhambi kubwa kabisa hata kuliko kuingizia katika kuma. Kwa hakika Allah swt ameangamiza ummah mzima wa Mtume Lut a.s. kwa sababu wao walijiingiza katika laana ya ulawiti. Allah swt kamwe hakumteketeza hata mtu mmoja kwa dhambi la zinaa.”

 

Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Wasa’il al-Shiah :

“Mtu yeyote anayetenda ulawiti pamoja na kijana wa kiume atapatwa na janabah (uchafu) ambao hautaweza kutakasishwa hata kwa maji ya dunia nzima. Allah swt atamghadhabikia na kumlaani vikali. (Yaani Allah swt atazichukua rehema na baraka kutoka kwake na kumlipa Motoni i.e. Jahannam). Kwa hakika ni mahala pabaya kabisa !  Pepo (Jannah) zitakuwa zimemkasirikia mno. Na mtu ambaye anakubali kulawitiwa kwa nyuma, basi Allah swt  humweka ukingoni mwa Jahannam (motoni penye moto mkali kabisa) na atamweka huko hadi hapo atakapo maliza kuwahoji watu wote. Hapo ndipo atakapo mwamrisha kuwekwa Motoni. Atapitia adhabu moja baada ya pili hadi kuzimaliza adhabu zote za Jahannam na hadi atakapofikia daraja la chini kabisa. Na kamwe hataweza kutoka hapo.”

 

Ulawiti ni kufr (ukafiri)

 

Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Al-Kafi

“Ulawiti ni moja ya Madhambi Makuu na inaadhibu pale mtu mmoja anapompanda mtu  bila ya kumwingilia. Na iwapo atamwingilia kwa nyuma basi hiyo itakuwa ni kufr (ukafiri).”

 

Hivyo inamaanisha kuwa mtu ambaye anachukulia ulawiti kuwa imehalalishwa basi huyo ni kafiri moja kwa moja, kwa sababu moja ya masharti ya imani ni kusema na kuamini kuwa ulawiti ni haramu katika dini ya Islam.  Na yeyote ambaye haamini masharti na matakwa ya Dini ya Islam, anakuwa kafiri. Lakini mtu anapotenda kosa hili la ulawiti huku akijua kuwa ni haraam basi anastahili kuadhibiwa kama adhabu za kukufuru, nayo ni daima.

 

Hudhaifa ibn Mansur anasema :

“Mimi nilimwuliza  al-Imam as- Sadique a.s. kuhusu Dhambi Kuu.

 

Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Wasa’il al-Shiah :

“Kubana kwa sehemu za kiume baina ya mapaja mawili kwa njia isiyoruhusiwa.”

 

Nikamwuliza tena, “Je ni mtu gani anayetenda dhambi la ulawiti ?”

Al-Imam as- Sadique a.s. alinijibu : “Yule ambaye amekufuru kwa Allah swt kwa yale aliyoteremshiwa Mtume Muhammad s.a.w.w. (Qur’an tukufu ).”

 

Amenakiliwa akisema al-Imam as- Sadique a.s. kwa kumjibu Abu Basir kuhusu Ayah ya Al-Qur’an Tukufu, Sura Hud, 11, Ayah 82  isemayo :

‘ Basi ilipofika amri yetu, Sisi tuliibinua (mji) juu chinii, na kuwateremshia mvua ya mawe magumu ya udongo uliopikwa, tabaka juu ya tabaka.

 

 Al-Imam as- Sadique a.s. alimjibu:

“Yupo mtu ambaye anaiaga hii dunia huku akisadiki kuwa ulawiti ni halali, lakini Allah swt anampiga kwa jiwe moja ambalo liliwadondokaea watu wa Mtume Lut a.s.[2]

 

Imeripotia katika Wasa’il al-Shiah kuwa mtu yeyote ambaye anachukulia ulawiti kuwa ni tendo la kihalali na hutenda mara kwa mara bila hata ya kufanya Tawba  [3]  ; wakati wa kufa kwake, Allah swt  humpiga jiwe moja ambalo yalitupiwa watu wa Mtume Lut a.s.  na ambayo yaliuangamiza umma mzima. Kifo chake kitakuwa kimetokana na kipigo hicho cha jiwe, lakini watu watakuwa hawalioni  (hilo jiwe).            Tafsir-i-Qummi

 

Walivyoadhibiwa umma wa Mtume Lut a.s.

 

Qur’an tukufu  imeelezea aina tatu za adhabu zilizoteremshiwa umma wa Mtume Lut a.s. .

1.       Sauti kubwa ya kutisha na mayowe ya kusikitisha na makubwa mno

2.       Kupigwa kwa kutupiwa mawe juu yao

3.       Kupindua ardhi juu chini

 

Baada ya kutaja adhabu hiyo ya tatu, imeelezwa katika Sura Hud, 11 : 83 

     ‘(Mawe hayo ya udongo uliopikwa) yalikuwa yametiwa alama (za adhabu) za Mola wako; Na wala haipo (maangamizo ya miji) mbali kutoka wadhalimu (wengine kama hawa watu wa umma huu wanaofanya machafu haya)’

 

Aya hii ni dalilisho kuwa aina hii ya adhabu inaweza kuwateremkia wale wote ambao wanatenda matendo kama haya ya ulawiti katika zama zetu hizi.

 

Mtumwa aliyemwua bwana wake

 

Wakati wa ‘Umar, mtumwa mmoja alimwua bwana wake. Wakati mtumwa huyo alipokiri kosa lake mbele ya ‘Umar, aliamrishwa kuuawa.

 

Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alimwuliza mtumwa huyo swali :”Je ni kwa nini umemwua bwana wako ?”

 

Mtumwa alijibu:  “Bwana wangu alinishurutisha katika kunilawiti.

 

Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. aliwauliza warithi wa marehemu: “Je nyinyi mumeshamzika ?”

 

Nao walijibu kuwa “ndipo tunapotokea sasa hivi.”

 

Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alimshauri ‘Umar kuwa amweke mtumwa huyo katika mahabusu kwa muda wa siku tatu na kuwashauri jamaa za marehemu warudi hapo baada ya siku tatu kupita.

 

Mlawiti atahesabiwa miongoni mwa watu wa Mtume Lut a.s.

 

Baada ya kupita siku tatu, Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. pamoja na ‘Umar na wajamaa zake walikwenda hadi kaburini. Walipofika huko Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. aliwauliza : “Je hili ni kaburi la mtu wenu ?”  “Naam !” walijibu.

 

Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. aliwaamrisha kulichimba kaburi hilo. Kwa kushangaza, maiti ya huyo bwana wa mtumwa haikuwamo na ilikuwa imepotea.   Kwa hayo Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alisema :

 

“Allahu Akbar ! Mimi nimemsikia Mtume Muhammad s.a.w.w. akisema kuwa : “ Yeyote katika Ummah wangu akitenda tendo la watu wa Mtume Lut a.s. na akifa bila ya kufanya Tawba basi maiti yake haitabakia kaburini zaidi ya siku tatu. Ardhi itamnyonya ndani yake na atafikishwa mahali walipo watu (walawiti) wa ummah wa Mtume Lut a.s.  Mahala ambapo maisha yao yaliangamizwa na kuteketezwa. Na kwa hayo mtu huyo atahesabiwa kuwa yu mmoja miongoni mwao (watu wa Mtume Lut a.s.).”                         (Kitab Muallim-uz-Zalfa)

 

Ulawiti ni tendo la kuaibisha

 

Imam ‘Ali ar-Ridha a.s. amesema : katika  Fiqh-i-Ridha

“Jiepusheni na ulawiti na zinaa, na huu ulawiti ni chafu na mbaya kabisa  kuliko zinaa. Madhambi haya mawili ndiyo vyanzo vya mabaya sabini na mbili ya humu duniani na Aakhera.”

 

Qur’an tukufu imetumia neno ‘utovu wa adabu, uchafu’ kwa ajili ya zinaa kwa njia ambayo imetumika vile vile kwa ajili ya ulawiti. Twaambiwa katika Surah A’araf, 7, : Ayah 80 - 81

‘Na (Sisi tulimpeleka) Lut, wakati alipowaambia watu wake:”Je ! Mwatenda jambo chafu ambalo halikutendwa na yeyote kabla yenu katika ulimwengu.’

 

“Nyinyi mnawaendea wanaume kwa hamu (ya kufanyiana uchimvi) badala ya wanawake; Ama nyinyi ni watu wafujaji.’

 

Je inawezekana nini kuwa uchafu zaidi ya mwanamme kuwa mbadhirifu wa mbegu zake za kiume (manii) kwa njia ambayo Allah swt ameharamisha badala ya kuzipandikiza katika tumbo la mwanamke ambapo ndiko kunakohakikisha kuendelezwa kwa binadamu.

 

Ulawiti  umeshutumiwa katika Surah Hud, Ankabut, Qamar,Najm na katika Surah za A’araf ili watu waweze kuonywa ili wajiepushe na tendo ovu kabisa la kumdhalilisha mwanadamu. Allah swt ameharamisha tendo hili kwa ukali sana.

 

Kumtazama kijana wa kiume kwa mtazamo wa ashiki au uzinifu

 

Kumtazama kijana mdogo wa kiume kwa macho ya ashiki au uzinifu ni Haraam kabisa, hususan kijana ambaye bado hajaota nywele za usoni mwake. Madhara na adhabu za mtazamo wa ashiki au uzinifu vinazungumziwa kwa mapana na marefu katika mudhui yanayozungumzia zanaa.  Vile vile Mtume Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Wasa’il al-Shiah :

“Jiepusheni na kuwatazama kwa macho ya ashiki au uzinifu vijana wa matajiri na watumwa, hususan wale ambao hawajaota hata ndevu. Kwa sababu uchokozi unaofanywa kwa mitazamo ya aina hiyo ni mbaya kabisa kuliko uchokozi wa kuwatazama hivyo wasichana wadogo walio katika hijabu.”

 

Ni wajibu wa kila Mwislamu kudhibiti macho yake yasikae yanapenda kuangalia kila kitu na wajiepushe na kila kitu kilicho chafu na kuaibisha.

 

Busu ya kiashiki na  hatamu ya Motoni

 

Ni haraam kumbusu kijana wa kiume kwa kuashiki.  Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika  Al-Kafi kwa kumnakili Mtume Muhammad s.a.w.w. :

“Iwapo mtu atambusu kijana wa kiume kwa kuwa ashiki, basi Siku ya Hukumu (Siku ya Qiyama) , Allah swt atamfunga mdomoni mwa mtu huyo hatamu ya moto.”

 

Al-Imam ar-Ridha a.s. amesema katika Fiqh-i-Ridha :

“Wakati mtu anapombusu kijana wa kiume kwa kuwa ashiki (mapenzi au nyege) basi Malaika wa mbinguni na Malaika ardhini , Malaika wa Rehema na Malaika wa adhabu  wote kwa pamoja humlaani huyo mtu. Na allah swt humtolea hukumu yake kwenda Motoni (Jahannam). Loh ! mahala pakutisha mno.”

 

Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Mustadrakul Wasail :

“Allah swt  atamwadhibu Motoni (Jahannam) kwa maelfu ya miaka mtu ambaye anambusu kijana wa kiume kwa ashiki au matamanio ya mapenzi.”

 

Iwapo mashahidi wawili watatoa ushahidi wa kumwona mtu akimbusu kijana mdogo kwa kuwa na ashiki, basi mtuhumiwa anaweza kuadhibiwa viboko thelethini hadi tisini kama vile atakavyoamua Qadhi. Hukumu hii inatolewa kwa mujibu wa Sharia za Kiislamu.

 

Riwaya zinasisitiza kuwa wale wanaotenda maovu kama haya vile vile waadhibiwe kama wazinifu, yaani wachapwe viboko mia moja. Hata hivyo kama wanawake wawili watatuhumiwa, basi Qadhi atawahukumu viboko chini ya mia moja kwa ajili yao.

 

Kulala pamoja kwa watu wawili wa jinsia moja

 

Wanazuoni wanasema kuwa wanaume wawili kulala pamoja chini ya blanketi moja bila mavazi kunawapa adhabu kwa mujibu wa Sharia za Kiislamu, navyo pia ni miongoni mwa madhambi makuu.

 

Hivyo ni Sunnah kutokulala kwa watu wawili pamoja, hata kama watakuwa wamevaa nguo zao. Isipokuwa kwa mume na mke waliohalalishwa kwa ndoa, Islam inaharamisha kwa watu wawili wanaoweza kutofautisha baina ya sahihi na kosa, kulala pamoja au chini ya blanket au shuka moja.  Vivyo hivyo, uharamisho huu pia unawahusu mtu na dada yake.

 

Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika  Wasa’il al-Shiah :

“Tengenezeni vitanda vya kulalia tofauti  kwa ajili ya watoto wenu wanaozidi umri wa miaka kumi. Ndugu wawili wa kiume au ndugu wawili wasichana au ndugu na dada yake wasilazwe pamoja katika kitanda kimoja."

 

Hivyo tumeona kuwa Uislamu umetushauri kuwa mtu na dada yake wasilale kwa kukaribiana na wanapojifunika blanketi au shuka, basi kila mmoja wao atumie ya kwake (wasishirikiane shuka au blanketi moja tu kwa watu wawili).

 

Adhabu za Ulawiti

 

Kwa kuwa ulawiti ni dhambi kubwa hata kuliko zinaa na maovu yake ni mabaya sana, kwa hivyo na adhabu yake pia lazima iwe kali zaidi kuliko adhabu za zinaa kwa mujibu wa sharia za Kiislam. Islam imetoa hukumu kali kabisa yaani mlawiti  na aliyelawitiwa wote kwa pamoja wauawe iwapo ni watu watu wakubwa na wenye akili timamu. Mwenye kutenda akatwe kichwa kwa upanga au auawe kwa kupigwa mawe au achomwe moto akiwa hai au atupwe kutoka mwinuko huku mikono na miguu yake ikiwa imefungwa. Hizi ndizo njia zilizopo za kumwadhibu mtuhumiwa, lakini ni uamuzi wa hakimu wa kuchagua ni aina gani ya adhabu itekelezwe. Vivyo hivyo Qadhi ndiye atakayetoa uamuzi wa aina ya adhabu gani ya kifo itumike kwa ajili ya  mtendewa (aliyelawitiwa).

 

Kwa mujibu wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. , mtu aliyetenda dhambi kama hili, mwili wake uchomwe moto hata baada ya kuuawa kwa njia nyingine. Yaani akishauawa kwa adhabu atakayoiamua Qadhi, basi baada ya kuuawa mwili wake uchomwe moto.

 

Kama ilivyo katika kesi ya zinaa, ulawiti pia unathibitishwa kwa njia mojawapo kati ya mbili.. Ya kwanza ni kwamba, washiriki wote wawili au mmoja wao akikiri mara nne mbele ya Qadhi. Iwapo yeye atakiri kosa lake chini ya mara nne, basi hataweza kuhukumiwa adhabu iliyohalalishwa. Basi hapo yeye ataonywa vikali kabisa na kutishwa kwa misingi kuwa kamwe hatarudia tena.  Baadhi ya Mujtahid wanaamini kuwa kukiri kwa mtuhumiwa kwa mara nne kufanyike katika nyakati mbalimbali. Vile vile inabidi mtuhumiwa awe ni mtu mzima, mwenye akili timamu, huru (asiwe mtumwa) na mwenye hiari zake.  Hata kama yeye atakiri kwa mara nne, kwa mtu mwenye umri mdogo, basi huyo atakaripiwa kwa tendo alilolifanya ili kwamba asirudie kulitenda tena. Vivyo hivyo ni kwa ajili ya mfungwa na mwenda wazimu (asiye na akili timamu).  Mbali na haya, iwapo mtu atakuwa amelazimishwa katika dhambi kama hili na hakuwa na uwezo wa kujiepusha nayo, basi huyo hataadhibiwa.

 

Njia ya pili ya kuthibitisha dhambi la ulawiti ni kwa watu waadilifu wanne wakiona kwa macho yao tendo hilo likifanyika na wakatoa ushahidi wao unaolingana (hautofautiani katika maelezo). Iwapo mashahidi watakuwa pungufu ya wanne, basi ushahidi wao hautakubalika na hivyo adhabu kwa mtuhumiwa wa ulawiti hautatekelezwa. Iwapo watu pungufu ya wanne ndio walioona tendo hili, basi wasitoe ushahidi wao. Na iwapo wao watatoa ushahidi, basi wao watakuwa mustahiki wa adhabu za qadhaf. [4]  Sura hii inazungumziwa vyema katika vitabu vya Fiqh-i. Iwapo mtuhumiwa atatubu mbele ya mashahidi wanne, basi hataadhibiwa na hivyo adhabu ya kifo haitatekelezwa kwa hivyo hatauawa.  Kukiri kwa watuhumiwa  au ushahidi utakaotolewa lazima uthibitishe kuwa uume (mboo) ulikuwa umeingia ndani ya mkundu, na hapo tu ndipo kutakapoweza kutolewa na kutekelezwa adhabu ya kifo.

 

Iwapo wanaume wawili watatokwa na shahawa tu bila ya kuingiliana  mkunduni (kwa kuminyaminya mboro baina ya mapaja mawili ya mtu mwenzake au kusugua matakoni ) basi kwa hayo adhabu yake itakuwa ni viboko mia moja kwa kila mmoja wao.

 

Je kwa nini ulawiti unaadhibiwa kwa kifo ?

 

Watu ambao hawana heshima na haya kiasi cha kuingia katika kutenda uchafu mkubwa wa kupotosha katika maingiliano mbele ya watu, ni sawa na ugonjwa wa kansa katika jamii yenye maadili mema na utamaduni mzuri.  Iwapo hao wataachiliwa kubakia hai, basi wao hawatasita kueneza uchimvi huu hadi hapo kuna hatari ya jamii nzima kukumbwa na uchimvi huu.  Na haya ndiyo yaliyowakumba watu wa Mtume Lut a.s..  Kwanza, Shaitani alimtanguliza mtu mmoja kutenda uchimvi huu na baadaye aliwaita watu wengine katika uchafu huu wa ulawiti. Hatimaye, dhambi hili lilifikia sehemu kubwa kabisa kiasi kwamba katika umma wa Mtume Lut a.s. mtu yeyote aliweza kuthubutu kumpanda mtu mwingine mbele ya watu bila hata ya kuona aibu (kama vile tuwaonavyo mbwa wakipandana hata mabarabarani mbele ya watu) na wanawake walikuwa wanaingiliana wao kwa wao, kwa hayo yote yalipokithiri basi Allah swt aliwalaani hawa watu na kuwaangamiza.

 

Ulawiti ni dhambi kubwa na baya kabisa kiasi kwamba iwapo mtu hatafanya Tawba na kusali kwa ajili ya kusamehewa,  basi hugeuka kuwa kama yule ambaye amemkana Allah swt, yaani amekuwa kafiri. Yeye atakuwa mustahiki wa adhabu za milele za Allah swt kama mkafiri.  Hivyo hakuna njia nyingine iliyo bora kwa watu kama hawa waliokufuru, isipokuwa kuwaua  na kuwachoma moto.

 

Kama inavyoelezwa katika swala la zinaa kuwa katika Islam zipo adhabu kali kabisa kwa matendo machafu, lakini hayakosi rehema na huruma za Allah swt.  Vile vile inaelezwa kuwa Islam imeweka Shariah kali si kutaka kuwaadhibu  wahalifu lakini ni kuwashtua na kuwarekebisha wale wazembe na wapuuzaji.  Ingawaje imeweka adhabu ya kifo kwa madhambi kama ya ulawiti, lakini ni lazima itekelezwe kwa masharti ya mashahidi wanne ambao watatoa shahada ya kuwa tendo hilo limetendwa mbele yao (na kwamba shahada zao zisitofautiane, zote ziwe sawa).  Kwa hakika ulegevu na huruma za Shariah za Kiislamu zinaonekana bayana hapa. Iwapo mtu ataonyesha adabu ya kutotenda uchimvi kama huu mbele ya watu na khofu ya kuuawa, Islam haiwaruhusu watu wenzake kumwadhibu. Vile vile iwapo mtuhumiwa akifanya tawba mbele ya mashahidi wanne waliokuwa wametoa ushahidi, basi hawezi tena kuuawa. Lakini iwapo ushahidi utakuwa umekamilika, basi adhabu haiwezi kupunguzwa na mtuhumiwa lazima auawe.

 

Hadi hapo kukiri kwa mtuhumiwa kunapohusika, Shariah za dini zinahusiana na swala la zinaa. Mtuhumiwa lazima akiri mara nne. Na ni lazima kuwa akiri katika maneno yaliyo wazi na bayana na wala asizungumze kama anayedanganya au asiyekumbuka kumbuka vyema. Qadhi lazima ahakikishe kuwa huyo mhalifu ni mtu mzima.  Wala kusiwe kunafanyika kwa mzaha kwa yale asiyoyatenda kwa hakika. Mambo yote haya na kukiri anapewa mhalifu. Kutoka kwa amri za Allah swt ili mhalifu aweze kupata fursa ya kujiokoa na adhabu hiyo ya kifo. Hatimae iwapo kweli mhalifu anastahili kuadhibiwa adhabu ya kifo kwa mujibu wa Shariah za Islam, basi adhabu hiyo ya kifo kitakuwa ni fundisho kwa wengine. Madhumuni ya Islam ni kuitengeneza na kuirekebisha jamii  iondokane na iepukane na maovu yanayoteketeza na kuangamiza jamii, na wala si kutaka kuwaadhibu tu wahalifu, bali na kuijenga jamii bora iliyo safi na sawa ili sisi wanaadamu tuishi vyema humu duniani na kujipatia yaliyo bora kabisa huko Aakhera.

 

Mhalifu anakiri na kupewa adhabu alizoamrisha Allah swt humu duniani kwa hivyo atakuwa ametakasika na hataadhibiwa tena huko Aakhera. Hata hivyo litakuwa jambo la busara iwapo mhalifu hataitoboa siri ya dhambi alilolitenda na badala yake aiweke kesi yake mbele ya Allah swt. Yeye inambidi afanye Tawba, alie na kuendelea kumwomba Allah swt kwa kupita kiasi ili aweze kusamehewa kwa Baraka Zake. Insha Allah, Allah swt atamsamehe.  Hata hivyo mtu haimbidi kutosheka na kuomba tu kwa hayo, bali akiwa anatarajia msamaha wa Allah swt inambidi awe mnyenyekevu na mchamungu mwema wa Allah swt ili asamehewe haraka iwezekanavyo na kwa hakika ataweza kujipatia nafasi bora kabisa mbele ya Allah swt kuliko hata alivyokuwa hapo kabla.

 

Hapa mwishoni tunakuleteeni hadith ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. aliyoisema :

“Mtu yeyote anayestahili kuuawa mara mbili kwa kupigwa mawe basi huyo ni mlawiti.”

 

Dini zote zinaafikiana kuwa ulawiti ni lazima udhibitiwe ipasavyo na isiachiwe ikatapakaa kwani si kwamba binadamu atadhalilika kiroho na kwa magonjwa tu bali hata kuangamia na kupotea mbali. Kijana aliyelawitiwa, hupoteza uume wake. Ulawiti huichukua jamii katika kina kirefu cha hasara kubwa. Kwa hivyo ni faradhi kwa waume kwa wake kuoa na kutimiza haja na matamanio yao ya kujamiiana katika hali iliyo bora na ambayo ipo katika mipaka ya Sharia na kwa njia za kibinadamu. Kwa hayo tutaweza kuhakikisha kuendelea na kuwa vyema kwa binadamu.

 

Moto haukumchoma aliyefanya Tawba

 

Ipo riwaya kutoka kwa  al-Imam as- Sadique a.s. katika  Al-Kafi (mlango unaozungumzia adhabu) kuwa:

Siku moja Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa ameketi pamoja na Sahaba wake ambapo mtu mmoja alimwijia na kusema : " Ya Amir al-Muminiin ! Mimi nimetenda tendo la ulawiti pamoja na kijana wa kiume, tafadhali sana naomba unitakase (yaani uniadhibu Shariah za Dini).” Kwa kuyasikia hayo Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alimwambia “Ondoka, nenda zako nyumbani, labda umeghafilika.”

 

Siku ya pili mtu huyo huyo alirudi tena kwa Imam a.s.  na alikiri kosa lake na kuomba aadhibiwe.  Tena Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alimwambia :”Nenda zako nyumbani, labda kwa sasa hivi wewe haupo katika fahamu zako kamili.”

 

Mtu huyo akaondoka na akajapo kurudi kwa mara ya tatu na kurudia kukiri dhambi alilolitenda na kuomba adhabu ili atakasike.

 

Na liporudi kwa mara ya nne na kurudia hayo hayo, hapo Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alisema:

“Mtume Muhammad s.a.w.w. ameelezea njia njia tatu kuhusiana na sura kama hizi zinapojitokeza, wewe unaweza kuchagua kifo mojawapo – kwa kufungwa miguu na mikono ukatupwa kutoka mchongoma, ukatwe kichwa au uchomwe moto ukiwa hai.”

 

Mhalifu huyo akasema, “Ewe Ali a.s., je ni adhabu ipi iliyo kali katika zote hizo ?”  Imam a.s. alimjibu : “Kuchomwa moto ukiwa hai.”  Akajibu :”Kwa hivyo mimi ndivyo ninaichagua adhabu hii ya kifo changu.” 

 

Kwa ruhusa ya Imam Ali a.s. aliinuka na kusali raka’a mbili na akasema “Ewe Allah swt ! Mimi nilitenda dhambi ambalo Wewe walijua vyema na mimi nikawa na khofu ya dhambi hili moyoni mwangu, mimi nimejileta mbele ya Khalifa halisi wa Mtume Muhammad s.a.w.w.  ili aweze kunitakasa. Yeye naye amenipa chaguo tatu za kifo. Na mimi ninachagua kifo kile ambacho ni kali zaidi kuliko zilizobakia.  Hivyo Ewe Allah swt ! Mimi ninakuomba kuikubalia adhabu hii kama ni fidia ya dhambi langu na wala usinichome kwa moto wa Jahannam, moto ambao umewashwa na Wewe.”

 

Kwa kusema hayo aliinuka akilia na akajitumbukiza katika shimo kulimokuwapo ukiwaka moto kwa ajili yake.  Yeye alikuwa ameketi katika moto uliokuwa umemzunguka pande zote.  Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alianza kuangua kilio, kwa kuyaona haya Sahaba wengine pia waliangua kilio.

 

Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alisema : “Inuka, ewe uliyesababisha Malaika wa Mbinguni na ardhini walie. Allah swt kwa hakika amekubali Tawba yako. Inuka na kamwe usiikaribie hilo dhambi ulilokuwa umelitenda.”

 

Na hivyo ndivyo ilivyokuwa, mtu alitoka nje ya moto uliokuwa ukiwaka akiwa salama u salimini bila hata ya mikwaruzo ya aina yoyote ile. 

 

Hivyo moto haukumchoma aliyefanya Tawba.

 

Mambo ya kuzingatia

 

Imekubalika miongoni mwa Mujtahid kuwa iwapo mtu atakiri mara nne na akafanya Tawba  kabla ya kutekelezwa hukumu juu yake, basi Qadhi anayoruhusa ama ampitishie amri ya kuuawa au amsamehe. Ripoti hiyo ya hapo juu pia inatudalilishia kuwa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. hakujitolea hukumu wala kumlazimisha au kumshawishi akiri.  Hata hivyo, hukumu haitaweza kufutwa baada ya ushahidi wa mashahidi wanne waadilifu.

 

Mama, Dada na Binti wa Mlawiti

 

Ni lazima ujilikane wazi wazi kuwa mwanamme yeyote anayemlawiti kijana wa kiume (anamwingilia mkunduni), basi wafuatao watakuwa wame haramishwa kwake : mama wa kijana huyo, dada na binti yake huyo kijana kwa maisha yake yote.  Yaani, mtu huyu (mlawiti) kamwe hataweza kumwoa mama yake, au dada au binti ya huyo kijana.

 

Madondoo kutoka kitabu cha NDOA KATIKA ISLAM [5]

 

1.       Watu wengi wanachukulia mambo ya kishetani katika kusuhubiana huku wakipuuza njia aliyoihalalisha Allah swt. Wao wanaingilia  njia ya  nyuma i.e. panapopitia choo kwa kisingizio cha kupata raha zaidi kumbe kunakujitumbukiza katika hatari ya kuweza kuambukizwa magonjwa hatari kabisa kwa sababu hiyo ni nafasi ya kupitia uchafu mtupu uliojaa magonjwa ya kila aina. Kwa msomaji ni ushauri wangu kuwa aonane na mganga ili aweze kupata ukweli na uhakika wa swala hili ili aweze kuelewa vyema falsafa ya Islam katika swala hili.

 

1.      Ulawiti wa kila aina

Kwa  mujibu wa Shariah za Kiislam, ulawiti na wanawake kuingiliana wenyewe kwa wenyewe ni matendo ya Ghunah-i-Kabira na hivyo kiviwekea adhabu kali mno hapa duniani na Aakhera. Iwapo kutapatikana watu wakifanya hivyo, basi wote wachinjwe. Hapo Hakim-i-Sharah (Hakimu wa Kidini) anaweza kutoa amri ya ya kuchinjwa kwa panga, kufungwa mikono na miguu na hatimaye kutupwa kutoka juu, au kuchomwa moto, kupigwa mawe hadi kufa au kuangushiwa ukuta. Vile vile anaweza kutoa adhabu zingine  pamoja na kuchomwa moto.

 

Ulawiti baina ya mwanamke mmoja na mwanamke mwingine pia inachukuliwa na Shariah kuwa ni dhambi kubwa kabisa kama vile ilivyo ulawiti baina ya wanaume. Iwapo wanawake wenye kutenda hivyo ni wenye akili na fahamu timamu,basi wapigwe viboko mia moja kila mmoja. Adhabu hii imewekwa kwa ajili ya wanawake wote wale walioolewa na wasioolewa.

 

Iwapo mwanamke atapatikana na makosa kama haya kwa mara ya nne,basi atachinjwa. Na iwapo mwanamke atakapopatikana na kosa kama hili,na akakiri na kutubu,basi Imam anaweza kumsamehe au kumpangia adhabu.Vile vile Naibu wa Imam  anayo mamlaka kama haya. Lakini siku hizi hakuna ad­habu kama hizi.

 

3. Zinaa

Kama vile Uislamu unavyolaani pombe vile vile inalaani vikali sana zinaa, kwa uchache ninawaletea mazungumzo na Hadithi juu ya suala hili.

 

Allah swt ametuamrisha katika Quran kuwa siku ya Qiyama mwenye kutenda zinaa ataadhibiwa mara dufu na daima atakaa katika moto wa Jahannam.

 

Imeelezwa katika kitabu Tafsir-i-Safi  kuwa miongoni mwa chemichemi za Jahannam moja inaitwa Asam ambamo badala ya maji inatiririka shaba iliyoyeyushwa.  Maumivu ya chemichemi hizi inazidi hata adhabu za ahera na adhabu za Jahannam. Wale watakaotupwa katika chemichemi hii inayotokota ni wale ambao wanamwabudu mtu mwingine mbali na Allah swt, na wale ambao wamewaua wale watu ambao wameharamishwa kuuawa na wale watu watendao zinaa.

 

Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema: "Allah swt ameweka adhabu sita kwa wale watendao zinaa ambapo adhabu za aina tatu wanazipata humu humu duniani na zinazobakia hizo tatu wanazipata huko Akhera. 

Adhabu hizo zilizowekewa humu duniani ni:-

1.  Wanapoteza nuru 

2.  Wanakuwa maskini

3.  Maisha yao yanakuwa mafupi.

 

Adhabu tatu zilizowekewa Akhera ni:-

1.  Allah swt atakuwa amewakasirikia mno

2.  Watahesabiwa siku ya Qiyama kwa Sharia kali

3.  Wataishi milele Jahannam.

 

Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema: "Manukato ya Jannat yataweza kusikika hadi umbali wa miaka. Hata hivyo yule mtoto ambaye amekanushwa na wazazi yaani wazazi wamesema sio mtoto wao tena, na mtu yule ambaye haonyeshi huruma kwa jamaa zake na yule mtu mzee anafanya zinaa, hao ndio watu hawataweza kusikia manukato ya Jannat."

 

Kuna Hadithi isemayo kuwa mwenye kufanya zinaa na mwenye kufanya Ulawiti watakuwa wakinuka kama nyama ya mizoga siku ya Qiyama hadi watakapoingizwa Jahannam.  Na kwa kweli watu wataudhika na kud­hurika kwa harufu zao hizo mbaya. Na wala hakuna matendo yao mema yeyote yatakayokubalika na kwamba matendo yao yote hayo yatakuwa yametupiliwa mbali.Watapigiliwa misumari katika masanduku ya maiti.  Watakuwa wamepewa adhabu kubwa kweli kweli kiasi kwamba iwapo mishipa yao watafungwa watu laki nne wote watakufa kwa kuathirika na adhabu watakuwa wakipata watu kama hao.Na watu kama hao ndio watakaopata adhabu kubwa kabisa katika wakazi wa Jahannam.

 

Mtu yeyote iwapo ni mtumwa au mtu mwingine yeyote afanyapo zinaa na Mwislamu, Myahudi, Mkristo, au mwanamke mwingine, Allah swt atamfungulia milango laki tano katika kaburi ambamo wataingia nyoka, nge na miale ya mioto ambavyo vyote hivyo vitakuwa vikimuadhibu na kumteketeza humo hadi siku ya Qiyama wakati watu wote watakapokuwa wamekusanyika siku ya Qiyama, watu kama hawa watakuwa wakitoa harufu mbaya katika sehemu zao za siri, kiasi kwamba watu wengine wote watakuwa wakiona udhia, na harufu hii itaendelea kutoka hadi watakapoingizwa Jahannam. 

 

Fatwa za Mujtahid kuhusiana na ulawiti

 

(2413)  Iwapo mwanamme aliyebaleghe atafanya Ulawiti na kijana wa kiume, basi mama, dada na binti wa mtoto huyo atakuwa haramu kwa ajili yake. Na Sharia kama hii itatumika wakati ambapo mtu ambaye amelawitiwa ni mwanamme mtu mzima, au wakati mtu anayelawiti ni kijana ambaye hajabaleghe.  Lakini iwapo mtu atakuwa na shaka iwapo kikofia cha uume wa mwanamme  umeingia katika sehemu za choo au haikuingia, basi katika sura hiyo mwanamke katika kikundi cha hapo juu hawatakuwa haramu kwa ajili yake.

 

(2414)  Iwapo mwanamme atamuoa mama au dada wa kijana mvulana, na akamulawiti huyo mvulana baada ya ndoa kwa misingi ya tahadhari hao watakuwa ni haramu kwa ajili yake.

 

 

                                T A M A T I           Walhamdulillaah.

 

VITABU VILIVYOKUSANYWA NA KUTARJUMIWA NA

AMIRALY  M. H.  DATOO  - P.O. Box  838 - BUKOBA TANZANIA

                      Datooam@hotmail.com

 

1.    UHARAMISHO WA  KAMARI KATIKA ISLAM

2.    UHARAMISHO WA  VILEO KATIKA ISLAM

3.    UHARAMISHO WA  ULAWITI KATIKA ISLAM

4.    UHARAMISHO WA  KUSEMA UONGO KATIKA ISLAM

5.    UHARAMISHO WA   RIBA’ KATIKA ISLAM

6.    TAJWID ILIYORAHISISHWA

7.    BWANA ABU TALIB a.s. MADHULUMU WA HISTORIA

8.    FADHAIL ZA IMAM ALI IBN ABI TALIB a.s.

9.    HUKUMU ZILIZOTOLEWA NA IMAM ALI IBN ABI TALIB a.s.

10. MSAFARA WA IMAM HUSAYN IBN ALI a.s. MADINA – KARBALA

11. DALILI ZA QIYAMA NA KUDHIHIRI KWA IMAM MAHDI a.s.

12. KITABU CHA TAJWID

13. NDOA KATIKA ISLAM

14. MAKALA MCHANGANYIKO  No. 1

15. MAKALA MCHANGANYIKO  No. 2

16. KESI YA FADAK

17. UWAHHABI – ASILI NA KUENEA KWAKE

18. TAWBA

19. TADHWIN AL-HADITH

20. HEKAYA ZA BAHLUL

21. SHADA LA MAUA KUTOKA BUSTANI YA AHADITH

22. TAFSIRI YA JUZUU’ ‘AMMA

23. HIARI NA SHURUTISHO KATIKA ISLAM

24. WAANDISHI MASHIA KATIKA SAHIH NA SUNAN ZA AHL SUNNA

25.  USINGIZI NA NDOTO

26. MAJINA KWA AJILI YA WATOTO WAISLAMU

27. USAMEHEVU KATIKA ISLAM

28. QURBAA - MAPENZI YA WANANYUMBA YA MTUME S.A.W.W.



[1]  Ulawiti ni tendo la mtu mmoja kumpanda na kumwingilia mtu mwingine

   kwa kupitia sehemu za choo kubwa yaani mkundu. Dhambi hili limegusiwa

   katika hatua nne:1) kumtazama kwa nia yenye shahawa yaani ni mbaya

   2)kumgusa au kumbusu kwa nia mbaya 3) kumpanda nyuma bila ya

    kumwingilia  4) kumwingilia kwa nyuma ambayo ni ukafiri moja kwa moja

   (kufr)

[2]  Msomaji anashauriwa kukisoma vyema kijitabu nilichokitayarisha mimi kinachozungumzia Ummah wa Mtume Lut a.s. kwa makini kwani kinazungumzia vyema juu ya hali ilivyokuwa na ilivyokuja kuharibika na mafunzo tuyapatayo  kwa kukisoma kisa hicho. Kama hukipati basi wasiliana kwa anwani yangu iliniweze kukusaidia.

[3] Msomaji unashauriwa kukisoma kitabu juu ya maudhui haya ya Tawba

  kwani kinazungumzia kwa marefu na mapana maudhui haya.

  Nilikitayarisha mimi Kitabu hiki ingawaje bado hakijachapwa lakini

  kinaweza kupatikana kwa sasa hivi au mbeleni kidogo katika mtandao wa

  kompyuta, popote pale ulipo humu duniani, kwa anwani ifuatayo; 

  http://www.al-islam.org/kiswahili Hapo utapata hazina kubwa.

[4] Qadhaf ni kumsingizia mwanamme au mwanamke mwema kwa tuhuma za

  zinaa au ulawiti.

[5]  Kitabu hiki  nilikitayarisha mimi na kimetolewa na kuchapwa na Bilal

    Muslim Mission of Tanzania  P.O.Box 20033 DSm . bilal@raha.com na vile vile kinapatikana katika ‘wavuni (internet) http://www.al-islam.org/kiswahili