(6) WAUTHMANIYYA WAKOMBOA MIJI

Katika miaka hiyo, Serikali ya Wauthmaniyya ilikuwa imeshughulika na masuala ya nje na ilikuwa ikijaribu kuuzima moto wa upinzani uliochochowa na chama chenye utaratibu maalum wa siri (freemasons). Wakati ukatili na mateso ya Sa’ud kwa ajili ya Waislamu yalipofikia hali isiyohimilika katika mwaka 1226 A.H. (1811), Khalifa wa Waislamu, Sultan Mahmud Khan ‘Adli II, alimwandikia barua Gavana wa Misri, Muhammad ‘Ali Pasha, awaadhibu hao mahamia. Kwa kupata barua hiyo, Muhammad ‘Ali Pasha alituma majeshi yake kutokea Misri katika mwezi mtukufu wa Ramadhani chini ya ukamanda wa mwanake Tosun Pasha. Tosun Pasha aliikomboa mji wa Yanbu, bandari ya Madina, lakini alishindwa katika vita vikali baina ya sehemu ya bonde la Safra na mpitio wa Judaida wakati akiwa anaendelea Madina katika siku za mwanzoni mwa mwezi wa Dhul Hijja, mwaka wa 1226 A.H. Ingawaje Tason Pasha mwenyewe alikuwa hakudhurika lakini Waislamu wengi wa ‘Uthmaniyya walikuwa mashahidi. Muhammad ‘Ali Pasha alipopata habari hizi alihuzunika sana kwa bahati mbaya hiyo na hivyo alitokeza na jeshi kubwa la maaskari wenye silaha nzito nzito pamoja na mizinga kumi na nane, mabunduki makubwa tatu na silaha nyingi zinginezo. Wao walipita bonde la Safra na mpitio wa Judaida katika mwezi wa Sha’ban 1227 A.H. (1812). Wao walizikomboa vijiji vingi bila ya kupigana katika mwezi mtukufu wa Ramadhan. Muhammad ‘Ali Pasha, kama vile alivyokuwa ameshauriwa na Sharif Ghalib Effendi, alitenda kwa busara kabisa katika kujipatia ushindi kwa kugawa riali 118,000 kwa vijiji ambazo zimejisalimisha kwa ajili ya mapesa. Iwapo Tosun Pasha angekuwa amemtaka ushauri Sharif Ghalib Effendi kama vile alivyofanya baba yake, basi bila shaka asingaliweza kupoteza jeshi lake kubwa kiasi hicho. Sharif Ghalib Effendi alikuwa amir wa mji wa Makkah kama alivyokuwa ameteuliwa na Mawahhabi; lakini moyoni mwake alikuwa na nia ya kuja kuikomboa Makkah kutoka makucha ya maharamia wa Kiwahhabi. Muhammad ‘Ali Pasha piia alifanikiwa kuikomboa Madina bila ya umwagaji wa damu mwishoni mwa mwezi wa Dhul Qa’da. Habari hizi za ushindi zilitumwa Misri ili ziweze kufikishwa kwa Khalifa. Watu wa Misri walisherehekea ushindi huo kwa siku tatu (usiku na mchana) na habari hizo zilienezwa katika nchi zote za Kiislamu. Muhammad ‘Ali Pasha alituma kikosi kwenda Makkah kwa kupitia Jeddah. Kikosi hicho kiliwasili huko Jeddah mwanzoni mwa mwezi wa Muharram 1228 A.H. na kuelekea mji wa Makkah. Wao waliingia kwa urahisi mjini Makkah kwa msaada wa mpango wa siri uliotolewa na Sharif Ghalib Effendi. Wakati huo maharamia wa Kiwahhabi pamoja na viongozi wao walikuwwa wamekwishautoroka mji wa Makkah pale walipopata fununu zakikosi cha Wauthmaniyya walipokuwa wakiukaribia mji huo.

Sa’ud ibn ‘Abd al-Aziz alirejea katika pango lake la uchochezi, Dar’iyya, katika mwaka 1227 A.H., baada ya kumaliza Hijja na kuzuru Ta’if ambapo damu nyingi mno ya Waislamu ilikuwa imemwagwa. Kwa hakika alishtushwa mno punde alipowasili Dar'iyya kwa kusikia kuwa miji ya Makkah na Madina imekombolewa na majeshi ya 'Uthmaniyya. Katika siku hizo hizo, majeshi ya 'Uthmaniyya yalishambulia mji wa Ta’if lakini hawkukumbana na upinzani wowote, kwani nduli wa Ta’if, ‘Uthman al-Mudayiqi pamoja na maaskari wake walikuwa wamekwisha toroka kwa hafu ya kushindwa na kushikwa. Habari hizo nzuri ziliwasilishwa mbele ya Khalifa wa Waislamu huko Istanbul, Sultan Mahmud Khan ‘Adli, ambaye alifurahishwa mno na alimshukuru kwa moyo wake wote Allah swt kwa baraka zake.Yeye alimtumia salaam za pongezi na shukrani na mazawadi mengi gavana huyo Muhammad ‘Ali Pasha na alimwamuru aende Hijaz tena kwa ajili ya kukagua na kuwadhibiti vyema hao maharamia wa Kiwahhabi.

Muhammad ‘Ali Pasha akiitii amri ya Sultan Mahmud Khan, aliondoka Misri kuelekea Hijaz. Wakati huo, Sharif Ghalib Effendi alikuwa Ta’if pamoja na maaskari wa 'Uthmaniyya ,wakimsaka mkatili ‘Uthman aliyejaa damu ya Waislamu waliouawa kwa mikono yake. Baada ya mipangilio ya utafutaji sahihi, ‘Uthman alipatikana na kukamatwa na kupelekwa Misri na baadaye Istanbul. Muhammad ‘Ali Pasha alipowasili Makkah alimpeleka Sharif Ghalib Effendi kwenda Istanbul na kumteua ndugu yake Yahya ibn Mas’ud Effendi kuwa amir wa Makkah. Katika mwezi Muharram 1229 A.H. Mubarak ibn Maghyam, haramia mwingine alikamatwa na kutumwa Itanbul. Maharamia hawa wawili, kwa hakika walikuwa wamemwaga damu ya Waislamu kwa mamilioni, na wakaadhibiwa adhabu waliyostahiki na wakatembezwa katika mitaa ya Istanbul ili watu wawaone na kuwajua. Sharif Ghalib Effendi ambaye alitumikia cheo cha amir kwa muda wa miaka 26 alikaribishwa kwa makaribisho makubwa na yaliyojaa kwa mapenzi, na alipelekwa Salonika ambapo alipumzika hadi alipofariki katika mwaka 1231 ( 1815 ). Qubba ya kaburi lake liko Salonika na ipo wazi kwa wale wafanyao ziyara.

Kikosi kilkuwa kimetumwa kusafisha mahala mbali hadi Yemen baada ya kuwafagia maharamia nje ya miji mitukufu ya Hijaz. Muhammad ‘Ali Pasha alikwenda kukisaidia kikosi hiki pamoja na maaskari wake na aliisafisha wilaya nzima. Yeye alirejea Makkah na kuishi huko hadi Rajab 1230, wakati alipomteua mwanake Hasan Pasha kuwa gavana wa Makkah na alirudi Misri. Sa’ud ibn ‘Abd al-‘Aziz alikufa katika mwaka 1231 na mwanake, ‘Abdullah ibn Sa’ud alimrithi yeye. Muhammad ‘Ali Pasha alimtuma mwanake Ibrahim Pasha pamoja na kikosi dhidi ya ‘Abdullah ibn Sa’ud. ‘Abdullah alikuwa ametiliana saini na Tosun Pasha kuwa yeye atakuwa mttifu kwa 'Uthmaniyya iwapo yeye atapewa ugavana wa Dar’iyya, lakini Muhammad ‘Ali Pasha alikataa kuutabua mkataba huo. Ibrahim Pasha aliondoka Misri mwishoni mwa mwaka 1231 na aliwasili Dar’iyya mwanzoni mwa 1232. ‘Abdullah ibn Sa’ud alipambana na Ibrahim Pasha kwa vikosi vyake vyote, lakini alishindwa na kukamatwa baada ya kutokea vita vikali vya kumwagika damu katika mwezi wa Dhul Qa’ada 1233 A.H. (1818). Habari nzuri za kufurahisha za ushindi zilipokelewa huko Misri kwa maelfu ya sauti za mizinga kutokea boma na kulikuwapo na sherehe kwa muda wa mcha na usiku saba mdululizo. Mitaa yote ilijaa kwa mabendera. Takbir na qasida zilisikika kutokea minara.

(7) KAZI ZILIZOFANYIKA BAADA YA UKOMBOZI