Muujiza

Maji yaliongezeka na kuwa matamu katika kisima cha maji kiitwacho Baghichat ar-Rasul katika Masjid an-Nabi baada ya kuteketezwa kwa ‘Ain az-zarqa’. Maji yalipatikana kwa wingi mjini hapo na hivyo hakuna Mwislamu aliyepata shida ya kiu cha maji. Hapo awali kisima hiki kilijulikana kuwa na maji ya chumvi.

Kuzingira huku kuliendelea kwa muda wa miezi. Waislamu walikuwa wamedhalilika vya kutosha kwa matumaini kuwa Mahujjaji wa Damascus watakuja tena na hivyo kuwaokoa. Hatimaye Mahujjaji walifika, lakini kiongozi wa msafara, Ibrahim Pasha, aliwaambia, “Salimisheni mji wenu kwao,” kwa sababu yeye alikuwa hana vikosi vya kutosha vya kuweza kupigana nao.Waislamu walikuwa wanadhani kuwa Ibrahim Pasha alikuwa ameshazungumza na kuelewana na Baday na kuwa watakuwa wameahidi kuwa Waislamu hao hawatadhalilishwa wala kuteswa au kuuawa. Hapo wao waliandika barua ifuatayo kwa Sa’ud na kuituma kwa kamati kamati ya watu wanne, waitwao Muhammad Tayyar, Hasan Chawush, ‘Abd al-Qadir Ilyas na ‘Ali:

“Sisi tunatoa heshima na kutuma salaamu kwako. Tunamwomba Allah swt akufanye mshindi katika matendo yako ambayo ni kwa mujibu wa uthibitisho wake! Ewe Shaikh Sa’ud! Amir wa Mahujjaji wa Damascus alipowasili hapa na kujionea kuwa mji umezingirwa, barabara zimewekea vizuizi na maji yamekatwa na Baday. Na alijaribu kutafuta sababu ya mambo yote haya na alikuja kujua kuwa hayo ndiyo amri yako. Kama tunavyoamini kuwa wewe hauna nia ya uadui kuhusu watu wa Madina, na sisi tunadhani kuwa wewe hauna habari na matukio maovu haya yanayotokea. Sisi, viongozi wa Madina, tumekutana na kuamua kukujulisha yale tunayotendewa huku. Sisi sote kwa pamoja tumewachagua watu hawa wanne walio bora, watu watukufu na hivyo tunawatuma kwako kama wajumbe wetu. Tunamwomba Allah swt kuwa wao watarejea kwetu pamoja na habari njema za kufutufurahisha.”

Sa’ud aliwatendea vibaya kabisa hao wajumbe baada ya kusoma barua na wala hakuwa na aibu kwa kusema kuwa yeye alikuwa amewakasirikia na kuwachukia watu wa Madina.Wajumbe walimbembeleza mno kuwasamehe na huku wakijitupa hata juu ya miguu yake michafu. Lakini yeye alisema, “Mimi ninadadisi kutokana na barua yenu kuwa nyinyi hamutazitii amri zangu, kwamba hamutaikubalia dini yangu ya kweli, na kwamba nyinyi munajaribu kunidanganya kwa maneno mazuri kwa sababu nyinyi mumezidiwa na kiu, njaa na dhiki na kwamba munanibembeleza kwa nia ya kujitoa katika mambo hayo na wala hamuna nia nyingine. Kwa hakika hakuna njia nyingine isipokuwa kukubali chochote kile nikitakacho mimi. Mimi nitawafanya nyinyi muzomewe na kuteketea kabisa kama vile vilivyowafanyia watu wa Ta;if iwapo nyinyi mutajifanya kuzikubalia amri zangu wakati mutasema au kutenda visivyonipendeza.”Yeye aliwalazimisha Waislamu waache madhehebu yao.

Masharti maovu na potofu zilizotolewa na Sa’ud kwa ajili ya Waislamu wa Madina yameandikwa kwa mapana zaidi katika kitabu kiitwacho Tarikh-i-Wahhabiyan.

Wajumbe wa Madina walirudi Madina baada ya kuzikubalia amri za Sa’ud kwa ushurutisho. Wakazi wa Madina, walishtushwa mno kwa matukio hayo, na walionyesha kukubali kwao bila ya kujitakia, kwani yeyote yule aangukaye baharini humshika nyoka. Wao waliisalimisha ngome yao ya Madina kwa watu sabini wa Baday kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa sharti la saba la mapatano hayo. Moja ya masharti katika mapatano hayo ilikuwa ni kubomoa makaburi yaliyopo mjini Madina. Wao walilazimika kutimiza masharti hayo ili waepukane na mateso ya Mawahhabi. Ingawaje wao walifanya kwa shinikizo, wala si hiari zao, lakini matokeo ya matendo yao yalikuwa mabaya mno.

Hakuna jibu lililofika la barua yao ya kuomba msaada kutoka Istanbul. Wakazi wa Madina waliishi katika hali ya kuteswa na kukandamizwa kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.Ulipofika wakati ambao wao walikata tamaa kabisa wa kuwasili msaada kutoka Istanbul, wao walimwandikia barua Sa’ud ya kuomba msamaha huko Dar’iyya, iliyopelekwa na Husain Shakir na Muhammad Saghayi. Lakini Sa’ud hakuwapokea wajumbe hao kwani alikuwa amekwishapata habari kuwa wakazi wa Madina walikuwa wameomba msaada hapo awali kutoka Istanbul. Sa’ud mwenyewe aliondoka Dar’iyya pamoja jeshi kubwa mno kwenda Madina kuendeleza dhuluma na kuwatesa kuwateketeza Waislamu wa mjini humo.

Wakatili na wanavijiji wote wa majangwa ya arabia walikuwa wameshakwisha mtambua Sa’ud kama mtawala wa Najd, ambaye alikuwa akizitilia sahihi barua alizoziandika huku na huko kwa cheo “al-Imam ad-Dar’iyyat al-majdiyya wa ‘l-ahkam ‘d-da’wati ‘n-Najdiyya”.

Punde alipoingia mjini Madina, aliwaamrisha wafanyakazi na wahudumu wa makaburini hapo (Qubba) kuzibomoa kwa mikono yao. Ingawaje Waislamu wa hapo walikuwa wamekwisha bomoa maqubba mengi kwa mujibu wa sharti la tatu waliyokuwa wamepewa na Sa’ud kiasi cha miaka mitatu iliyopita, lakini wao walikuwa hawakuthubutu baadhi ya makaburi ambayo wao walikuwa wakijua kuwa zilikuwa tukufu na zilizobarikiwa. Wafanyakazi na wahudumu hao walianza kazi za kubomoa huku wakilia na kusikitika mno.Mfanyakazi na mhudumu wa kaburi la Bwana Hamza alisema kuwa yeye alikuwa ni mtu aliyezeeka na dhaifu, hivyo asingaliweza kubomoa. Sa’ud alimwamrisha mtumwa wake mwovu kubomoa. Mtu huyo alipanda juu ya Qubba kutaka kubomoa, lakini alianguka chini na kufa papo hapo, na hivyo kulimfanya Sa’ud aahirishe kubomoa kaburi hilo lakini aliondoka huku ameuondoa mlango wake.Baada ya kusimamia operesheni ya maamrisho yake maovu yenye kuteketeza, alihutubia jukwaa iliyojengwa katika mahala paitwapo Manaha.Yeye alisema kuwa wakazi wa Madina walikuwa hawtaki kumtii lakini wamekuwa wanafiq kwa uwoga wao na kwamba wanataka kuendelea na ushrikina wao kama hapo awali. Na aliongezea kusema katika sauti mbaya na ufidhuli, kuwa wale wote waliojihifadhi katika ngome mi lazima watoke nje na watoe heshima, na wale ambao watakataa kutoka nje, basi watakipata kile kiitwacho hukumu ya Mawahhabi kama ilivyotekelezwa mjini Ta’if.

Kila mtu aliogopa wakati malango ya ngome zilipofungwa na kulitolewa ilani katika kila mitaa kuwa watu wote wakusanyike mahala palipokuwa pakiitwa Manaha. Wao walidhani kuwa yale tote yatawapata waliyoyapata watu wa Ta’if, mateso na kuuawa. Wao waliagana kwa machozi pamoja na wake na watoto wao kwani walijua kuwa huo ndio ulikuwa mwisho wao.Wanawake na wanaume walikuwa wamekusanyika katika makundi mawili huku shingo zao zikiinama chini kuelekea qubba la kaburi la Mtume Muhammad s.a.w.w. Mji wa Madina haukuwahi kukumbwa na huzuni na siku nyeusi kama hiyo hapo kabla. Sa’ud alikuwa mwenye chuki dhidi ya Waislamu. Lakini Allah swt kwa baraka za Mtume Muhammad s.a.w.w.aliulinda mji mtukufu wa Madina usipakwe damu kama rangi. Baada ya kuwadhalilisha Waislamu kwa matendo na maneno maovu yaliyo kinyume na heshima, Sa’ud aliwaamrisha maharamia wake waishi katika ngome ya Madina. Yeye alimteua Hasan Chawush, mlaghai mkubwa aliyeaminiwa mno, kuwa gavana wa Madina na yeye mwenyewe alirejea Dar’iyya. Yeye alirudi Madina baada ya kutimiza Hijja huko Makkah katika msimu wake. Yeye alitoka nje ya pango lake na kwenda katika baraza lake wakati ambapo msafara wa Mahujjaji wa Damascus walipokuwa wameshaondoka kwa umbali wa siku mbili au tatu kutoka Madina. Yeye hakushtushwa na moyo wake mweusi na mgumu hata kuliko jiwe, aliwaachia maharamia wake wapore vito vya thamani, kazi za nakshi muhimu katika ukumbusho wa historia, vito vingi vilivyokuwa vimechovya katika dhahabu na kurembeshwa kwa jawhari na mawe yenye thamani na nakala zilizokuwa zimekusanywa za Quran Tukufu pamoja vitabu ambavyo vilivyokuwa havipatikani kwa urahisi, vitu vyote hivi vilikuwa vimewekwa katika jumba la kaburi la Mtume Muhammad s.a.w.w. na vilikuwa katika hazina ya Masjid an-Nabawi ambavyo vilikuwa vimetumwa kama vilivyochaguliwa na heshima kama zawadi kutoka Masultani Waislamu, makamanda, wasanii na Maulamaa kutokea sehemu zote za ulimwengu wa Kiislamu kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu moja. Moto wa uadui uliokuwa unawaka undani mwake dhidi ya Waislamu haukupoa hata baada ya matendo yake ya kuaibisha, yeye aliendelea na azma yake ya kubomoa makaburi yaliyobakia ya ma-Sahaba na Mashahidi.Yeye amejaribu sana kubomoa nyumba ya kabruri la Mtume Muhammad s.a.w.w. lakini alishindwa kwa sababu za sauti za Waislamu kupinda kitendo chake hicho, lakini aliweza kubomoa Shabakat as-Sa’ada, kwa bahati nzuri kutokugusa kuta.Yeye aliamuru kuta zizungukazo mji wa Madina zifanyiwe ukarabati.Yeye aliwakusanya wakazi wa MAdina katika Masjid an-Nabi. Alifunga milango ya Masjid na kutoa hotuba ifuatayo juu ya jukwaa:

“Enyi mliokusanyika! Nimekuiteni hapa kwa kutaka kuwapa nasiha na kuwaonyeni kuwa muzifuate amri zangu. Enyi watu wa Madina! Dini yenu ndiyo sasa imekamilika. Kuanzia sasa nyinyi ndio Waislamu.Nyinyi mmemfurahisha Allah.Kamwe musiipende dini ya potofu ya baba na mababu zenu. Wala kamwe musimwombe Allah swt awarehemu! Wao wote walikuwa kama mushrik.Na kwa hakika wote walikuwa mushrik. Mimi nimewaelezeeni vile mutakavyo mwabudu Allah katika vitabu vyangu nilivyowapa watu wenye mamalaka ya dini. Mutambue waziwazi kuwa mali yenu yote, watoto, wake na damu zenu ni mubah kwa maaskari wangu iwapo nyinyi hamutowajali watu wangu wenye mamlaka ya dini. Wao watawafungeni kwa minyororo nakuwateseni nyinyi nyote hadi kufa. Imeharamishwa katika dini ya Uwahhabi kusimama mbele ya kaburi la Mtume kwa nia ya kutoa heshima kwa kusema salat na salaam kama vile mababu zenu walivyofanya. Haiwapashi nyinyi kusimama mbele ya kaburi, lakini munaweza kupita na kusema As-salaamu ‘ala Muhammad, wakati munapokuwa mukipita. Kwa mujibu wa Ijtihad ya imam wetu Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab, heshima kiasi hiki kinamtosha Mtume”.

Sa’ud, baada ya kutoa kashfa na kauli mbayambaya ambayo sisi hatuna hima ya kuzitoa, aliamrisha milango ya Masjid as-Sa’ada ifunguliwe. Yeye alimteua mwanake ‘Abdullah kama gavana wa Madina na alirejea Dar’iyya. Baada ya hapo ‘Abdullah ibn Sa’ud hakuacha kuwatendea Waislamu wa Madina madhila na mateso ya kila aina.