(5) MAWAHHABI HUKO MADINA

Sulaiman Khan, Khalifa wa sabini na tano wa Ahl as-Sunna na Sultan wa kumi wa Wauthmaniyya, alijenga kuta kuuzunguka mji mtukufu wa Madina; mji ambao haukudhurika kwa mashambulizi ya aina zozote za majambazi kwa muda wa miaka 274 kwa sababu za kuta zake kuwa madhubuti, na Waislamu wa hapo waliishi kwa amani na raha hadi ulipofika mwaka 1222 A.H. (1807) wakati walipoangukia kama windo mikononi mwa Sa’ud.

Sa’ud aliwatuma waporaji aliowakusanya kutoka vijiji kwenda Madina baada ya kuiteka Makkah na vijiji vilivyozunguka. Yeye aliwateua ndugu wawili waitwao Baday na Nadi kama makamanda wa vikosi hivyo vya waporaji. Wao walipora vijiji kila walipokwenda na kuwaua Waislamu wengi mno. Vijiji vingi mno kuelekea madina vilichomwa moto na kuteketezwa kabisa. Waislamu waliokuwa na msimamo wa haki kama Maulamaa wa Ahl as-Sunna, waliporwa kila kitu na hatimaye kuuawa. Kwa hakika hali ya uporoja na uteketezwaji wa vijiji kuelekea Madina hauwezi kufanyiwa makisio, hali ilipindukia kiasi. Vijiji vya karibu na Madina vilijisalimisha kwa Mawahhabi kwa hofu ya kuporwa, kuteswa na kuuawa. Na hivyo wote walikuwa ni watumwa na manamba wa Sa’ud. Sa’ud aliwaandikia barua Waislamu wa Madina kwa kumtumia Salih ibn Salih:

Mimi ninaanza kwa jina la Mmiliki wa Siku ya Malipo. Nadhani inafahamika miongoni mwa Maulamaa, maofisa na wafanya biashara wa Madina kuwa amani na raha inapatikana kwa wale tu ambao wanajipatia muongozo.Enyi watu wa Madina! Ninawaiteni katika dini ya haki Ayah ya 19 na 85 ya Surah al-Imran inasema: ‘Bila shaka dini (ya haki) mbele ya Allah ni Uislam. Na anayetaka dini isiyokuwa basi haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye hasara!’ Mimi nataka mujue hisia zangu kuhusu nyinyi. Mimi ninawapendeni na ninayo imani n awatu wa Madina. Mimi ninataka kuja kuishi pamoja nanyi katika mji wa Rasulullah.Mimi sitawateseni wala kuwadahalilisha iwapo nyinyi mutanisikiliza na kuzitii amri zangu. Watu wa Makkah wamekuwa wakifaidika na fadhila na huruma zangu tangu nilipoingia mjini humo. Mimi ninawatakeni nyinyi nyote muwe Waislamu kwa upya. Hapo mutasalimika na udhalilisho, mateso na hata mauti iwapo tu mutazitii amri zangu. Allah swt atawalinda na mimi nitakuwa mlinzi wenu. Mimi ninawatumieni barua hii pamoja na mtu nimthaminiaye mimi, naye ni Salih ibn Salih. Someni vyema na mufanye maamuzi yenu pamoja naye.! Kile atakachokisema yeye ndicho nikisemacho mimi.”

Kwa hakika wakazi wa Madinah walishtushwa mno kwa barua hiyo. Hivi karibuni wao walikuwa wamesikia mateso na mauaji yaliyowakumba wakazi wa Ta’if wakiwemo wanawake na watoto na hivyo walikuwa wamejaa kwa hofu. Wao hawakuwa na la kusema ndiyo au hapana kwa barua ya Sa’ud ibn ‘Abd al-’Aziz. Vile vile hawakutaka kusalimisha maisha yao wala dini yao.

Kwa kuona hakuna majibu ya barua, kiongozi wa mahramia, Baday mwovu kabisa, aliishambulia mji wa Yanbu, bandari ya Madina. Baada ya kuiteka Yanbu, aliizingira Madina na aliishambuli mara kwa mara kuta za lango la ‘Anbariyya. Ikatokea kuwa siku hiyo Mahujjaji kutoka Damascua walikuja pamoja na kiongozi wao ‘Abdullah Pasha. Pale alipoona mji umezingirwa, Mahujjaji na maaskari walipigana vita vikali dhidi ya maharamia wa Kiwahhabi. Kiasi cha maharamia mia mbili waliuawa katika mapigano ya umwagikaji damu yaliyodumu masaa mawili, waliobakia walifanikiwa kutoroka.

Waislamu wa Madina walikaa katika raha na amani hadi pale ‘Abdullah Pasha alipokuwapo Madina kutimiza faradhi zake za Hijja, lakini Baday aliuzingira tena mji wa Madina baada ya kuondoka Mahujjaji wa Damascus. Yeye aliteka Quba, Awali na Qurban na alijenga maboma mawili ya ng’ombe katika eneo hilo. Yeye aliweka vizuizi katika barabara zote ziendazo Madina na aliteketeza chemchemi iliyokuwa ikiitwa ‘Ain az-zarqa’.Hivyo Waislamu walikuwa hawana chakula wala maji.