(4) UDHALIMU WA MAWAHHABI KATIKA MAKKAH

Ingawaje waovu hawa waliishambulia Makkah baada ya kumwaga damu kwa wingi katika mji wa Ta’if, wao hawakuthubutu kuingia mjini Makkah kwa sababu ulikuwa ni wakati wa Hijja. Sharif Ghalib Effendi alikuwa mjini Jeddah katika kutafuta msaada wa kijeshi ili kuwakabili Mawahhabi, na huku wakazi wa Makkah walikuwa na khofu ya matukio ya maafa ya Ta’if, walituma ujumbe kwa kamanda wa Mawahhabi na walimwomba asiwatese wao. Hivyo Mawahhabi waliingia mjini Makkah katika mwezi Muharram 1218 A.H. ( 1803 ) na walizieneza imani zao za Kiwahhabi. Wao walitangaza hadharani kuwa watawaua wale wote watakao kuwa wakizuru makaburi au watakwenda Madinah kuomba mbele ya kaburi la Mtume Muhammad s.a.w.w. Baada ya siku kumi na nne wao waliushambulia mji wa Jeddah kwa kutaka kumteka nyara Shari Ghalib Effendi, ambaye aliwashambulia waporaji wa Kiwahhabi kidhahiri na kwa ujasiri kutokea ngome ya Jeddah na aliweza kuwaua wengi wao, wale waliobakia walitorokea Makkah. Walipoombwa na wakazi wa Makkah, wao walimteua ndugu yake na Sharif Ghalib Effendi, aitwaye Sharif ‘Abd al-Mu’in Effendi kama amir wa Makkah na kurudi Dar’iyya. Sharif ‘Abd al-Mu’in Effendi aliukubalia uamir kwa ajili ya kuwalinda wakazi wa Makkah kutokana na mateso ya Mawahhabi.

Sharif Ghalib Effendi alirejea Makkah pamoja na maaskari wa Jeddah na Gavana wa Jeddah, Sharif Pasha, baada ya siku thelathini na nane kuanzia pale maharamia hao waliposhindwa hapo Jeddah. Wao waliwatokomeza maharamia waliokuwa wamebakia mjini Makkah, na kwa mara nyingine tena alikuwa Amir. Maharamia hao walizishambulia vijiji vilivyozunguka mji wa Ta’if na kuwaua watu wengi mno kwa kulipiza kisasi cha Makkah. Wao walimchagua mharamia ‘Uthman al-Mudayiqi kama gavana wa Ta’if. ‘Uthman aliwakusanya maharamia wote kuuzunguka mji wa Makkah, alipata kundi kubwa mno, mwaka 1220 ( 1805). Waislamu wa Makkah kwa hakika waliathirika mno kwa mateso na njaa kwa kipindi cha miezi mingi, na hapakuwapo na hata mbwa aliyebakia kuliwa nyama yake katika siku za mwishoni mwa kuzingirwa. Sharif Ghalib Effendi alifahamu kuwa kwa wakati huo hapakuwa na suluhisho lingine lolote isipokuwa kuingia katika mkataba pamoja na maadui ili kunusuru maisha ya raia wake. Yeye aliiusalimisha mji wa Makkah kwa sharti kuwa yeye atabakia kama amir wa mji na kwamba mali na maisha ya Waislamu yatakuwa salama.

Maharamia hao waliteka miji ya Madinah na Makkah na walipora vito vya thamani kabisa duniani humu vilivyokuwa vimehifadhiwa katika Khazinat an-Nabawiyya (Hazina ya Mtume) kwa zaidi ya muda wa miaka elfu moja. Wao waliwadharau vibaya sana Waislamu kiasi kwamba hakuna maneno hata ya kuelezea. Baadaye, walirudi Dar’iyya baada ya kumteua mtu mmoj aitwaye kwa jina la Mubarak ibn Maghyan kama gavana wa mji. Wao walibakia mjini Makkah na Madinah na hawakuwaruhusu Mhujjaji wa Ahl as-Sunna kuingia Makkah kwa kipindi cha miaka saba. Wao waliifunika al-Ka’aba kwa vipande viwili vya kitambaa vyeusi vikiitwa Qailan. Wao walipiga marufuku uvutaji wa hukah na waliwatendea vibaya mno wale waliovuta. Wakazi wa Makkah na Madina hawakuwapenda hao na daima walikuwa wakijiepusha nao.

Ayyub Sabri Pasha alielezea katika juzuu ya kwanza ya kitabu chake Mirat al-Haramain, kilichochapwa katika mwaka 1301 A.H. (1883), kuhusu mateso waliyoyapata Waislamu wa Makkah kama ifuatavyo:

“Mateso waliyoyapata Waislamu katika mji mtakatifu wa Makkah na Mahujjaji, kila mwaka, ni vigumu kuyaelezea kwa undani zaidi.

“Chifu wa maharamia, Sa’ud, alikuwa akimwandikia barua za vitisho kila mara amir wa wakazi wa Makkah, Sharif Ghalib Effendi. Ingawaje Sa’ud alijaribu kuuzingira mji wa Makkah kwa mara kadhaa, lakini hakuweza kuingia mjini hadi mwaka 1218 A.H. (1802). Sharif Ghalib Effendi, pamoja na gavana wa Jeddah, waliwakusanya viongozi wa misafara ya Mahujjaji kutoka Damascus na Misri katika mwaka 1217 A.H. na kuwaambia wao kuwa maharamia walikuwa na nia ya kuushambulia mji mtukufu wa Makkah, na iwapo wao watakubali kumsaidia yeye, basi wao kwa pamojawataweza kumteka Sa’ud, chifu wa maharamia. Kwa masikitiko, ombi lake hilo halikukubaliwa. hapo, Sharif Ghalib Effendi alimteua ndugu yake Sharif ‘Abd al-Mu’in Effendi, kama amir wa Makkah, aliwatuma kwa Sa’ud ibn ‘Abd al-Aziz wanazuoni watano wa Ahl as-Sunnah, waitwao Muhammad Tahir, Sayyid Muhammad Abu Bakr, Mir Ghani, Sayyid Muhammad ‘Akkas na ‘Abd al-Hafiz al-‘Ajami kama ni kamati ya uwema na kusamehe.

“Kwa kujibu, Sa’ud alikwenda Makkah pamoja na majeshi yake. Yeye alimteua ‘Abd al-Mu’in kama ndiye Ofisa Mkuu wa jimbo na aliamrisha makaburi yote yavunjwe, kwa sababu kwa mujibu wa imani ya Mawahhabi, wakazi wa Makkah na Madina hawamwabudu Allah swt na badala yake huabudu makaburi. Wao walidai kuwa wakazi wa miji hiyo miwili watamwabudu Allah swt vile iwapasavyo kama makaburi hayo yatakuwa yamevunjwa. Kwa mujibu wa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab, Waislamu wote walikufa kama makfiri na mushrik kuanzia mwaka wa 500 A.H. (1106); Islam ya kweli na hakika uliteremshiwa yeye, na hivyo haikuruhusiwa kuwazika wale waliokuwa Mawahhabi karibu au pamoja na makaburi ya mushrik na makafiri, wakimaanishwa Waislamu.

“Sa’ud aliishambulia Jeddah kwa ajili ya kutaka kumteka Sharif Ghalib Effendi na alitaka kuiteka Jeddah. LAkini, watu wa Jeddah, bega kwa bega pamoja na majeshi ya Uthmaniyyah (Ottoman) kwa uhodari na ushupavu waliwashinda maadui wao na kuwafanya majeshi ya Sa’ud kutoroka. Sa’ud aliwakusanya wote wale waliokuwa wakitoroka na kurejea nao mjini Makkah.

“Ingawaje Sharif ‘Abd al-Mu’in Effendi alijitahidi kubakia kama rafiki wa Mawahhabi ili kuwalinda Waislamu wa Makkah wasiteswe na kuuawa na Mawahhabi wadanganyifu, lakini waovu hawa walizidisha dhuluma na udhia wa kila aina siku baada ya siku. Kwa kuona maovu ya Mawahhabi yamekithiri kupindukia kiasi, yeye alimtumia ujumbe Sharif Ghalib Effendi kuwa Sa’ud alikuwa Makkah pamoja na jeshi lake lililopiga mahema katika uwanja wa Mu’alla (makaburi ya Maqureishi )na itawezekana kumkamata Sa’ud iwapo atawashambulia hata kwa kikosi kidogo cha majeshi.

“Kwa kuupata ujumbe huo, Sharif Ghalib Effendi aliwachukua baadhi ya majeshi waliokuwa wakijulikana pamoja na Gavana wa Jeddah,Sharif Pasha, na aliwashambulia Mawahhabi wakati wa usiku. Yeye alifanikiwa kuzingira mahema yao, lakini Sa’ud aliweza kutoroka akiwa hai. Majeshi yake yalisema kuwa wao walikuwa tayari kujisalimisha iwapo watasamehewa, na ombi lao hilo lilikubaliwa. Hivyo mji mtukufu wa Makkah ulinusurika na watu makatili hawa. Ushindi huu uliwashtusha mno Mawahhabi waliokuwapo huko Ta’if, ambao nao pia walijisalimisha bila hata ya umagikaji wa damu. Mkatili ‘Uthman al-Mudayiqi alitoroka pamoja na maaskari wake kulekea katika milima ya Yemen. Sharif Ghalib Effendi alipopata habari kuwa Mawahhabi waliotoroka baada ya kushindwa wanafanya vitendo viovu vya unyanyaswaji na kupora mali za wananchi katika sehemu mbalimbali za nchi, aliwatumia ujumbe Ukoo wa bani Saqif na kuwaamuru ‘Nendeni Ta’if na muwashambulie Mawahhabi! Chukueni chochote kile mukipatacho!’ Hivyo kabila la Bani Saqif waliishambulia Ta’if kwa kulipiza kisasi juu ya waporaji, na hivyo Ta’if pia ilinusurika.

“Uthman al-Mudayiqi aliwakusanya majahili, wauaji wa vijiji vya Milima ya Yemenna, pamoja na Mawahhabi aliokuwa akikutana nao akiwa safarini, aliuzingira mji wa Makkah. Wakazi wa Makkah waliathirika kwa taabu na udhia kwa muda wa miezi mitatu. Sharif Ghalib Effendi alishindwa kuondoa hali hiyo kwani alijaribu kwa mara kumi lakini hakufanikiwa. Akiba ya chakula kilitoweka. Kulitokea mfumuko wa bei, kwani kila kitu kilikuwa ghali mno kiasi kwamba mkate uliuzwa kwa riali tano na siagi riali sita kwa kipande cha ratili 2.8, na hapo mbeleni hakuwapo mtu aliyeuza chochote. Waislamu hawakuwa na njia nyingine isipokuwa kuwala paka na mbwa, ambao nao pia walimalizika. Pia ulifika wakati ambapo iliwabidi wale manyasi na majani. Ulipofika wakati ambapo kulikuwa hakuna chochote cha kula, Mji wa Makkah ulijisalimisha kwa Sa’ud kwa sharti kwamba hatawatesa wala kuwaua wakazi wa mji huo. Sharif Ghalib Effendi hakuwa na makosa katika tukio hili, lakini asingalikuwa ameangukia katika swala kama hili lau angalikuwa ameomba kabla misaada ya washirika wake. Kwa hakika wakazi wa Makkah walimwambia Sharif Ghalib Effendi , ‘Sisi tunaweza kuendelea kuwakabili Mawahhabi hadi utakapofika msimu wa Hijja iwapo wewe utatutafutia misaada kutoka makabila tunayopendana nao, na kwa hakika tutapata ushindi pale Mahujjaji wa Msiri na Damascus watakapo kuja Kuhiji,’ Sharif Ghalib Effendi aliwaambia, ‘Mimi ningalikuwa nimefanya hivyo kabla, lakini haiyumkinika hivi sasa,’ akikiri kosa lake. Yeye pia hakutaka kujisalimisha, lakini wakazi wa Makkah walisema, ‘Ewe Amir! Bau yako Mtume Muhammad s.a.w.w. pia alifanya mikataba pamoja na maadui zake. Nawe pia, tafadhali kubaliana na maadui na ututoe sisi katika majanga haya. Wewe utakuwa ukifuata Sunnah ya Mtume Muhammad s.a.w.w. kwa kufanya hivyo. Kwa sababu Mtume Muhammad s.a.w.w. alimtuma ‘Uthman (kutoka Khudaibiya) kwa kabila la Kiqoreishi katika Makkah kwa ajili ya kufanya mkataba.’ Sharif Ghalib Effendi aliwasihi watu wajiepushe na wazo la kuingia katika mkataba pamoja na Mawahhabi na hadi mwisho alikuwa hakuingia katika mapatano. Yeye alikubali baada ya kushauriwa na kiongozi wa masuala ya dini aitwaye ‘Abd ar-Rahman wakati ambapo watu walikuwa hawawezi kustahimili shida. Kwa hakika lilikuwa ni uamuzi wa busara wa Sharif Ghalib Effendi kumsikia ‘Abd ar-Rahman na kumtumia kama mpatanishi ili kumzuia Sa’ud asiwatese na kuwaua Waislamu. Yeye vile vile alijishindia ufadhila wa wakazi wa Makkah na maaskari kwa kusema, ‘Mimi nimekubali kufanya mapatano bila ya kutaka; nilikuwa nikipanga kusubiri mpaka ufike wakati wa Hijja.’

“Baada ya kuandikiana masharti na mapatano, Sa’ud ibn ‘Abd al-Aziz aliingia mjini Makkah. Yeye aliifunika al-Ka’ba Tukufu kwa namna ya nguo iliyofanywa kwa kugandamiza manyoya ya wanyama pamoja na sherizi, e.g. ya tarbushi. Yeye alimfukuza kazi Sharif Ghalib Effendi . Alishambulia huku na huko kama Firauni na kuwatesa watu katika hali isiyostahimilika.Kwa sababu kulikuwa hakujawasili misaada yoyote kutoka “Uthmaniyya (Ottoman), Sharif Ghalib Effendi alikuwa amepata uchungu mno. Yeye alieneza tetesi kuwa sababu kuu ya kuusalimisha mji wa Makkah ilikuwa ni uzembe wa utawala wa ‘Uthmaniyyah(Ottoman Empire) na ilimshawishi Sa’ud kutowaruhusu Wamisri na Mhujjaji kutoka Damascus wasiingie Makkah ili kwamba kuwafanya ‘Uthmaniyya waanze matendo yao dhidi ya Mawahhabi.

“Mwenendo huu wa Sharif Ghalib Effendi ulimfanya Sa’ud awe katili zaidi na kuongezea mateso yake. Yeye aliwatesa na kuwaua wengi wa maulamaa wa Ahl as-Sunna na watu wengi matajiri wa mji wa Makkah.Yeye aliwatishia wale ambao hawkubainishwa kuwa wao ni Mawahhabi.Watu wake walipiga makelele masokoni na mitaani,‘Kubalini dini ya Sa’ud! Jihifadhini katika kivuli chake pana!’ Kwa hakika idadi ya watu waliokuwa wakiweza kuilinda na kuinusuru dini ilikuwa imepungua mno majangwani.

“Sharif Ghalib Effendi alipoona hali mbaya iliyojitokeza katika mazingara hayo, aliona kuwa Islam inataka kufutwa katika Hijaz na miji iliyobarikiwa kama vile ilivyokwishatokea katika miji ya majangwani, alimtumia ujumbe Sa’ud, ukisema:’Wewe hautaweza kukabiliana na majeshi ya ‘Uthmaniyya ambayo yatatumwa kutoka Istanbul iwapo utabakia kukalia mji wa Makkah baada ya msimu wa Hijja. Wewe utashikwa na kuuawa. Usibakie katika mji wa Makkah baada ya Hijja, ondoka zako!’ Kwa hakika ujumbe huu haukuleta uwema wowote bali Sa’us aliongezea ukatili na kuwatesa vibaya sana Waislamu.

“Wakati wa kipindi hiki cha uchokozi na utesaji, Sa’ud ibn ‘Abd al-Aziz alimwuliza ‘alim mmoja wa ahl as-Sunna,’Jee Muhammad (Mtume Muhammad s.a.w.w. ) yupo hai kaburini mwake? au amekufa kama tunavyoamini watu wengine wanaokufa?’ ‘Alim huyo alimjibu, ‘Yeye yu hai kwa maisha ambayo sisi hatuwezi kujua.’ Sa’ud alimwuliza swali hili kwa makusudi ili akitarajia jibu kama hilo ili aweze kumtesa na kumwua huyo ‘alim.‘Kama ni hivyo, basi tuonyeshe kama yeye yupo hai kaburini mwake ili tuweze kukuamini. Na lau utashindwa basi tutaelewa kuwa wewe ni mpinzani wa dini yangu. Iwapo utajibu visivyo sahihi, mimi nitakuua,’ alisema Sa’ud. ‘Mimi sitajaribu kukuvutia wewe kwa kukuonyesha jambo moja lisilohusiana na swala hili. Twende pamoja hadi mjini Madinah al-Munawwara na tusimame mbele ya Muwajahat as-Sa’ada. Mimi nitamtolea salaam, na iwapo yeye yu hai basi atanijibu, basi utajionea kuwa bwana wetu Mtume Muhammad s.a.w.w. yu hai kaburini mwake na kwamba husikia na kuwajibu wale wote wanaomsalimia. Iwapo hatutapata jibu la salaam yangu, basi itajulikana kuwa mimi ni mwongo. Na hivyo utaweza kuniadhibu vile utakavyo,’ alijibu yule ‘alim wa Ahl as-Sunna. Kwa kuyasikia hayo, Sa’ud alighadhabika mno na akamwachia huyo ‘alim aondoke, kwani naye pia angalikuwa kafiri na mushrik kwa mujibu wa imani zake mwenyewe iwapo angelifanya vile alivyotaka ‘alim yule.Yeye alipumbazwa kwani yeye mwenyewe alikuwa si msomi kwa kuweza kutoa majibu. Hivyo ilimbidi amwachie yule ‘alim ajindokee huru kwani asije akajiharibia jina lake.Hata hivyo wao walikuwa ni watu wenye njama mbaya, alimwamrisha askari mmoja amwue huyo ‘alim na kumpelekea habari mara moja. Lakini huyo askari wa Kiwahhabi hakupata mwanya wa kutekeleza amri hiyo, kwa baraka za Allah swt. Habari hizi mbaya kabisa zilifika katika masikio ya mwanachuoni huyo mujahid, yeye alihama Makkah akifikiri kuwa itakuwa ni wema kwake yeye kuondoka Makkah.

“Sa’ud alimtuma muuaji mmoja kwenda kumwua mujahid huyo baada ya kusikia habari za kuondoka kwake. Mwuaji huyo alisafiki usiku na mchana kutwa akidhani kuwa atajipatia thawabu nyingi mno kwa kumwua Ahl as-Sunna. Kwa bahati mbaya, mwuaji alipomfikia mujahid huyo aliyetakiwa kuuawa kwa amri ya Sa’ud, alikuwa ameshakufa kifo cha kawaida punde kabla ya kuwasili huyo mwuaji. Yeye alimfunga mnyama wa mujahid katika mti na kuodoka kwenda kunywa maji. Wakati aliporudi, akakuta ngamia peke yake bila ya maiti ya mujahid. Baada ya kurudi kwa Sa’ud, askari huyoo alimwelezea tukio lote. ‘Naam!’ Sa’ud alisema, ‘Mimi nilimwota huyo mtu akichukuliwa juu mbinguni katika Pepo miongoni mwa sauti za dhikr na tasbih. Watu wenye sura zilizokuwa ziking’ara walimwambia kuwa maiti hiyo ilikuwa ni ya mujahid yule na ilikuwa ikichukuliwa Peponi kwa sababu imani zake zipo sahihi kuhusu Mtume (Mtume Muhammad s.a.w.w. ).’ Kwa kuyasikia hayo, Mwahhabi huyo alisema, ‘Wewe ulinituma kumwua mtu kama huyu aliyebarikiwa! Na sasa wewe hautaki kurekebisha imani zako potofu ilihali umejionea baraka na rehema za Allh swt zikimfikia huyo mujahid!’. Na alimlaani Sa’ud. Yeye alitubu. Sa’ud wala hakuchukua taabu ya kumsikiliza huyo. Yeye alimteua ‘Uthman al-Mudayiqi awe gavana wa Makkah na alirudi Dar’iyya.

“Sa’ud ibn ‘Abd al-Aziz alikuwa akiishi huko Dar’iyya. Yeye vile vile alifanikiwa kuuteka mji wa Madina. Mbeleni, yeye aliondoka kwenda Makkah pamoja na wale waliokuwa wakitaka kuhiji na wale waliokuwa wakiweza kuzingumza vyema. Wale viongozi wa dini yao ya Uwahhabi walikuwa ndio katika mstari wa mbele ambao wangaliweza kuueneza na kuusifu Uwahhabi. Wao walianza kusoma na kuelezea kitabu kilichoandikwa na Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab katika Masjid al-Haram huko Makkah siku ya Ijumaa mnamo tarehe 7 ya mwezi wa Muharram, mwaka 1221 (1806). Kwa hakika Maulamaa wa Ahl as-Sunna waliwakanusha wao. Sa’ud ibn ‘Abd al-Aziz alifika baada ya siku kumi. Yeye alifanya kituo chake katika nyumba ya Sharif Ghalib Effendi katika uwanja wa Mu’alla. Yeye aliiweka kipande cha kile alichojifunika juu ya Sharif Ghalib Effendi kuonyesha urafiki. Na Sharif Ghalib Effendi aliuonyesha urafiki pia. Wote kwa pamoja walikwenda Masji al-Haram na wakafanya tawaf kuuzunguka al-Ka’aba kwa pamoja.

“Wakati huo zilifika habari kuwa msafara wa mahujjaji kutoka Damascus walikuwa wakija Makkah. Sa’ud alimtuma Mas’ud ibn Mudayiqi awaendee hao wasafiri na kuwaambia kuwa hawataruhusiwa kuingia Makkah. Mas’ud alionana na msafara huo na kuwaambia, ‘Nyinyi mulipuuzia mikataba na mapatano ya hapo awali. Sa’ud ibn ‘Abd al-‘Aziz amewatumieni amri pamoja na Salih ibn Salih kuwa nyinyi msije pamoja na majeshi yenu. Lakini tunaona kuwa mnao majeshi yenu! Hivyo kamwe hamtaweza kuingia Makkah, kwa sababu hamkutii amri’ Mkuu wa msafara huo, ’Abdullah Pasha, alimtuma Yusuf Pasha kwenda kwa Sa’ud kumwomba msamaha na idhini ya kuingia Makkah. Sa’ud alijibu, ‘Ewe Pasha! Mimi ningalikuwa nimekwishawaua nyinyi nyote kama nisingalikuwa na hofu ya Allah swt. Hebu nileteeni magunia ya sarafu za dhahabu munazozitegemea kuwagawia masikini wa haramain na wanavijiji Waarabu na mara moja muondoke zenu! Mimi ninawaharamishieni nyinyi Hijja ya mwaka huu! Yusuf pasha alizisalimisha magunia ya sarafu za dhahabu na kuondoka.

“Habari za kuzuiliwa na kufukuzwa kwa msafara wa Mahujjaji kutoka Damascus zilienea kwa kasi katika ulimwengu wa Kiislamu. Wakazi wa Makkah walilia na kusikitika mno kwani walidhani kuwa nao pia wamepigiwa marufuku kwenda ‘Arafat. Lakini siku iliyofuatia, waliruhusiwa kwenda ‘Arafat kwa masharti kuwa ilikuwa ni marufuku kwao kwenda mahfas au machela. Kila mmoja, hata mahakimu na Maulamaa, alikwenda ‘Arafat juu ya punda au ngamia. Khutba ya huko ‘Arafat ilitolewa na Mwahabbi badala ya qadhi wa Makkah. Wao walirejea Makkah baada ya kutimiza mambo ya faradhi katika Hijja.

“Sa’ud alipowasili Makkah tu alimwachisha kazi Qadhi wa Makkah, Khatib-zada Muhammad Effendi, na alimteua Mwahhabi aliyeitwa ‘Abd ar-Rahma kama Qadhi. ‘Abd ar-Rahman alimwita Muhammad Effendi, Su’ada Effendi, hakimu mkuu wa Madina, na ‘Ata’i Effendi, mwakilishi wa Masharifu huko Makkah na aliwakalisha juu ya sakafu. Yeye aliwaambia watoe heshima zao kwa Sa’ud. Maulamaa hawa walisema, La ilaha illallah wahdahu la sharika lahu kwa mujibu wa imani ya Mawahhabi na waliketi tena juu ya sakafu. Sa’ud alicheka na kusema, ‘Mimi ninawaheshimuni nyinyi pamoja na msafara wa Mahujjaji wa Damascus na kuwawekeni chini ya uangalizi wa Salih ibn Salih. Salih ni mmoja wa watu wangu wema. Mimi ninamwamini. Mimi ninawaruhusu muondoke kwenda Damascus kwa masharti kwamba mutalipa kurushi 300 kwa kila mahfa- na ngamia aliyebebeshwa mzigo na kurushi 150 kwa kila punda. Kwa hakika huu ni upendeleo mkubwa kwenu kweza kwenda Damasca kwa malipo madogo. Kwa hakika mutaweza kuondoka kwa usalama chini ya ulinzi wangu. Mahujjaji wote watasafiri katika masharti haya. Na huu ndio uadilifu wangu. Mimi nimekwisha mwandikia barua Sultan wa Wauthmaniyya Bwana Salim Khan III. Nimemwandikia kuharamishwa kujenga majengo juu ya makaburi, kufanya machinjo ya wanyama kwa ajili ya waliokufa au kuwaomba kupitia wale waliokufa.’

“Sa’ud alibakia Makkah kwa muda wa miaka minne. Muhammad ‘Ali Pasha, Gavana wa Misri, alikuja hadi Jeddah katika mwaka 1227 A.H. (1812) kwa amri ya Sultan wa 'Uthmaniyya Mahmud-i ‘Adli. Majeshi ya Misri wakishirikiana na majeshi ya Jeddah walifanikiwa kumfukuza Sa’ud kutoka Makkah baada ya vita vikali vya umagikwaji wa damu."