(3) WAISLAMU WA TA’IF WAPORWA NA KUUAWA

Wakati Maulamaa wa Ahl as-Sunna walipowanyamazisha Mawahhabi katika mwaka 1210 A.H. (1796), Maulamaa wa Makkah walitayarisha waraka na kutia sahihi zao ambamo waliandika Ayah za Qur’an Tukufu pamoja na Hadith sharif kwa kuthibitisha kuwa Uwahhabi ni njia iliyo tofauti na mbali na Islam, mtego wa hila na njama zilizotengenezwa na maadui wa Islam kwa ajili ya kuuteketeza Uislam undani mwake. Mawahhabi wale watatu waliokuwa wametubu kwa upotofu wao, walihakikisha na kuthibitisha waraka huo. Nakala za azimio hilo zilitumwa katika nchi zote za Kiislamu.

Baadhi ya Mawahhabi wa Makkah walimwendea ‘Abd al-‘Aziz, mtawala huko Darr’iyya, na kumwelezea kuwa wawakilishi wao hawakuweza kuwakabili Maulamaa wa Makkah na kwamba waraka wa azimio lao kuwa Uwahhabi ulikuwa ni upotofu na njama dhidi ya Islam, zimepelekwa kila nchi ya Kiislam. ‘Abd al-‘Aziz ibn Muhammad ibn Sa’ud na wafuasi wake, waliingiwa na hasira kali kabisa dhidi ya Ahl as-Sunna, waliishambulia Makkah katika mwaka 1215. Amir wa Makkah, Sharif Ghalib ibn Musa’id ibn Sa’id Effendi, aliwakabili vikali. Damu nyingi ilimwagika pande zote mbili. Sharif Ghalib Effendi hakuwaruhusu hao kuingia Makka, lakini makabila ya Waarabu kuzunguka Makkah walikubali Uwahhabi. Baina ya Idi mbili za mwaka huo huo, Sa’ud alituma jeshi katika mji wa Ta’if. Huko wao waliwatesa na kuwachinja ovyo Waislamu wanawake na watoto wa Ta’if.

Mateso na mauaji ya Ta’if wakiwemo wanawake na watoto yalifanyika kwa amri ya adui mkubwa wa Islam, brigadia mwovu kabisa aliyekuwa akiitwa ‘Uthman al-Mudayiqi. Mtu huyu na Muhsin walikuwa wametumwa na Sharif Effendi kwenda Dar’iyya ambapo walitakiwa kuzungumzia mapatano ya awali ya kuwazuia Mawahhabi wasiizingire Madina na kutowatesa Waislamu. Lakini mnafiki huyu alikuwa ni jasusi kwa Sharif Effendi.Yeye alimhadaa mwenzake Muhsin, wakati wanaelekea Dar’iyya kuwa angeliweza kumpatia mafanikio mengi. Hao wawili walitoboa siri zao kwa Sa’ud ibn ‘Abd al-‘Aziz huko Dar’iyya. Sa’ud, alipowatambua kuwa wao walikuwa watumwa wake watiifu, aliwaweka waporaji chini ya ukamanda wao. Wao walikwenda hadi mahala paitwapo Abila karibu na Ta’if na huko wakampelekea Sharif Ghalib Effendi barua kuwa Sa’ud na wao, wasaliti hao wawili, walikuwa hawatambui uhalali wa maptano ya hapo awali na kwamba Sa’ud alikuwa akijitayarisha kuuzingira mji wa Makka. Sharif Ghalib Effendi aliwajibu katika lugha laini akiwashauri, lakini ‘Uthman mkatili, alikuwa kwa hakika adui mkubwa wa Islam, alizichana barua. Yeye aliwashambulia Waislamu waliokuwa wametumwa na Amir na kuwaghalibu.. Ilimbidi Sharif Ghalib Effendi alirudi hadi ngome ya Ta’if na kuchukua hatua za kujihami. Huyu Mwahhabi katili aliweka kambi za majeshi yake huko Malis karibu na Ta’if mwishoni mwa mwezi wa Shawwal katika mwaka 1217 A.H. (1802). Yeye vile vile alioomba msaada kutoka mkatili Amir wa Bisha, Salim ibn Shakban, ambaye alikuwa na roho katili kuliko jiwe lililojaa uadui dhidi ya Uislamu. Kulikuwapo na tawala za kifalme takriban ishirini katika majangwa na kila falme alikuwa na kikosi cha Mawahhabi mia tano zaidi ya kikosi cha Salim mwenyewe kipatacho elfu moja.

Wakazi wa Ta’if wakiongozwa na Sharif Ghalib Effendi, waliwashambulia majeshi ya Mawahhabi huko Malis. Alifanikiwa kuwaua waporaji elfu moja na mia tano wa Salim ibn Shabkan. Salim pamoja na wafuasi wake walitoroka Malis. Lakini walikusanyika na wengine na kurejea kuishambulia Malis na waliupora mji mzima. Sharif Ghalib Effendi alikwenda Jeddah kutafuta msaada wa kijeshi. Wakazi wengi wa Ta’if walikuwa wamejaa kwa khofu na walitoroka kwa kisiri siri pamoja na vitu vyao vya majumbani. Ingawaje wale wakazi wa Ta’if waliokuwa wamejisitiri katika ngome, waliweza kuwashinda majeshi madogo madogo ya Mawahhabi waliokuwa wakijaribu kuwashambulia, wao walipeperusha bendera nyeupe ya kutaka usitihwaji wa vita baina yao kwani Mawahhabi walikuwa wakimiminika majeshi mengi. Wao walikubali kujisalimisha kwa masharti kwamba maisha na heshima zao hazitadhuriwa. Ingawaje maadui pia walikuwa wamekwisha nguvu na kudhoofika kwani nao pia walipata pigo kubwa la kuuawa na wengi walitoroka kutoka majeshi yao na walidhoofika pia, akatokea mwakilishi wa wakazi wa Ta’if, ambaye alikuwa mwovu na msaliti mkubwa, ingawaje alikuwa akiwaona Mawahhabi wanatoroka kwa kukimbia hapo, aliwapigia sauti kubwa kwa kuwaambia, “Sharif Ghalib ametukimbia kwa kuogopa! Na hivyo wana-Ta’if hawana nguvu ya kukabiliana nanyi ! Wao wamenituma kuwaleteeni habarri kuwa wao wapo tayari kujisalimisha na kuisalimisha ngome nzima mikononi mwenu na wanawaombeni muwasamehe. Mimi ninawapenda Mawahhabi. tafadhalini rudini! Nyinyi mumemwaga damu nyingi kupita kiasi na haitakuwa jambo la busra kwenu nyinyi kurudi bila ya kuikamata Ta’if. Ninaapa kuwa wana-Ta’if watajisalimisha wao na ngome hiyo. Wao watakubalia chochote kile mutakacho nyinyi.” Kwa hakika lilikuwa ni kosa la Sharif Ghalib Effendi katika kuipoteza Ta’if bila maana. Iwapo angalikuwa amebakia Ta’if pamoja na Waislamu, basi isingalifika maafa hayoo. Kwa sababu waporaji ni waoga, Mawahhabi hakudhani kuwa wana-Ta’if watajisalimisha vile kirahisi. Lakini walipoona bendera ya kutaka amani juu ya ngome, walimtuma jasusi kuja kujua hali halisi iliyokuwapo ndani mwa ngome. Wana-Ta’if walimvuta ndani kwa kamba huyo mjumbe. Mjumbe huyo aliwaambia: “Kusanyeni mali zenu zote hapa na mujisalimishe kama munataka kuishi hai.” Mali zao zote zilikusanywa na kurundikwa mahala pamoja kwa msaada wa Mwislamu mmoja aliyekuwa akiitwa Ibrahim. Mjumbe huyo alisema: “kwa hakika hii haitoshi.” Aliendelea kuseam kuwa “Sisi kamwe hatuwezi kuwasameheni kwa haya tu, lazima mulete zaidi na zaidi!” Yeye aliwapa daftari na kuwaambia “orodhesheni majina ya wale wanaokataa kutoa mali zao! Wanaume wapo huru kwenda popote pale watakapo isipokuwa wanawake na watoto watafungwa kwa minyororo.” Kwa hakika wote kwa pamoja walimwomba awe mlaini mwenye huruma kidogo, basi yeye aliongeza udhalimu na uovu wake. Ibrahim, alishindwa kuvumilia zaidi ya hapo na hivyo alimpiga kifuani kwa jine na kumwua. Wakati malumbano haya yanaendelea, Mawahhabi waliishambulia na ngome hiyo na hivyo waliweza kukwepa kulengwa mizinga na risasi. Wao walibomoa milango na kufanikiwa katika kuingia ndani ya ngome. Mawahhabi waliwaua wanawake, wanaume na watoto wote waliowaona na hata kuthubutu kuwaua watoto wachanga waliokuwa katika masusu yao. Mitaa ya mji ilijaa kwa mito ya damu. Wao walishambulia kila nyumba na kupora vyote vilivyokuwamo na popte pale walichokipata, wakawa wakishambulia kama vichaa na kikatili hadi usiku ulipoingia. Wao hawakuweza kuzichukua nyumba za mawe upande wa mashariki wa ngone, hivyo walizishambulia nyumba hizo kwa risasi. Mlaghai moja wa Kiwahhabi alipiga kelele: “Sisi tunawasameheni! Munaweza kwenda popote pale mupendapo pamoja na wake na watoto wenu,” lakini wao waliyapuuzia bila kujali. Wakati huo Mawahhabi waliwakusanya watu, ambao walikuwa wakijitayarisha kuondoka na kuhama, juu ya mlima na kuzizunguka zile familia halisi wa Waislamu, ambao wamekua katika mapenzi na udugu na wengi wao walikuwa ni wanawake na watoto, na kuwaweka wakafa kwa njaa na kiu kwa muda wa siku saba, na kuwatesa mno kwa visingizio, kupiga mawe na vitisho vya aina mbalimbali. Mawahhabi walimwita mmoja baada ya mwingine na kuwapiga na kuwauliza: “Tuambieni pale mulipoficha mali zenu !” na walipiga makelele, “Siku yenu ya kufa inawadia!” kwa wale walioomba msamaha.

Ibn Shakban, baada ya kuyakamdamiza majumba hayo ya mawe kwa muda wa siku kumi na mbili bila ya kufanikiwa kuyabonyeza, aliahidi kuwa wale wote watakaotoka nje ya nyumba zao na kujisalimisha pamoja na silaha zao, basi watasamehewa. Kwa hayo, Waislamu walimwamini na kutoka nje, lakini, wakiwa wamefungwa mikono yao migongoni mwao, wao waliburutwa na Ibn Shakban hadi juu ya mlima pale ambapo walikuwapo Waislamu wengine waliokuwa wameshikiliwa. Waislamu mia tatu na sitini na saba, wakiwemo wanaume, wanawake na watoto (Allah swt awarehemu) wote kwa pamoja walichinjwa chinjwa mlimani hapo. Mawahhabi waliwaachia wanyama wao wawakanyage Waislamu hao na hatimaye kuwaacha hapo bila ya kuwazika ili waliwe na ndege wa kuwinda kwa muda wa siku kumi na sita. Wao walifanya hujuma kubwa ya kupora mali za Waislamu katika kila nyumba, na waliweza kukusanya mali nyingi mno mpaka kukutokea kama mlima mbele ya lango la ngome hiyo na walimtumia Sa’ud asilimia ishirini ya yale yaliyoporwa na iliyobakia waligawana miongoni mwao. Wadhalimu na nvua za masika zilizoa mapesa na vito vya thamani mno na hapo kulibakia kiasi cha rial za dhahabu elfu arobaini tu, katika mikono ya Ahl as-Sunna; kiasi cha rial elfu kumi ziligawiwa miongoni mwa wanawake na watoto, na vitu viliuzwa kwa bei ndogo kabisa.

Mawahhabi walizichana nakala za Qur’an tukufu na vitabu vya tafsir, Hadith na vitabu mbalimbali vya Kiislamu walivyovichukua kutoka maktaba, misikiti na majumbani mwa watu, na kuvitupa huku na huko. Wao walithubutu hata kutengenezea viatu kwa ajili miguu yao michafu vya majalada ya dhahabu ya Qur’an na vitabu vinginevyo. Kwa hakika zilikuwapo zimeandikwa Ayah tukufu za Qur’an juu ya majalada hayo. Majani (makurasa) ya Qur’an tukufu zilikuwa zimetupwa ovyo mitaani mwa mji wa Ta’if kiasi kwamba kulikuwa hakuna hata nafasi ya kuuweka mguu juu ya ardhi ya mji wa Ta’if. Ingawaje inasemekana kuwa Ibn Shakban alikuwa ametoa amri ya kutokuzichana nakala za Qur’an Tukufu, lakini hao Mawahhabi waporaji wa majangwani hawakujua Qur’an ni nini, na hivyo walizichana chana nakala zote walizozipata na kuzikanyaga kanyaga ovyo. Inajulikana kuwa ni nakala tatu tu za Qur’an Tukufu na nakala moja tu ya Sahih al-Bukhari ndizo zilizo salimika kutokana na hujuma na uporaji wa Mawahhabi katika mji mkubwa wa Ta’if.