(2) MISHENI YA KWANZA YA MAWAHHABI

'Abd al- Aziz ibn Muhammad , ambaye amewaua kikatili Wailsamu wengi kupita kiasi kwa kuueneza Uwahhabi, aliwatuma Mawahhabi watatu kwenda Makkah katika mwaka 1210 A.H. (1795). Maulamaa wa Ahl as-Sunna walikabiliana nao kwa kuwatolea Ayah za Qur’an Tukufu na Hadith sharifu kiasi kwamba Mawahhabi hao wawakilishi hawakuweza kujibu vyovyote vile. Wao hawakuwa na lolote lile la kuzungumzia isipokuwa kukubaliana na ukweli mtupu uliojitokeza mbele yao. Hao wawakilishi wa ki-Wahhabi waliandika ilani ndefu mno na kuzitia sahihi zao kuwa Ahl as-Sunna wapo katika njia ya haki na kweli na kwamba wao watatu walikuwa katika njia iliyopotoka, njia ya wendawazimu. Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba kiongozi wao ‘Abd al-Aziz hakukuyatia maneno ya viongozi wake wa kidini yenye nasiha kwake masikioni mwake kwani yeye alichokuwa akikitaka ni matakwa yake ya kisiasa na alikuwa amekwishaufanya roho yake kwa ajili ya uchifu. Yeye aliongezea kuwatesa Waislamu siku baada ya siku nyuma ya pazia la kidini. Kwa hakika Waislamu waliangamizwa na kuteketezwa kwa uwezo wake wote.

Mawahhabi hao watatu waliweka hoja ishirini za kuwashawishi Waislamu wakazi wa Makkah. Hoja zao hizo ishirini zimegawanyika katika makundi hayo matatu tuliyoyazungumzia. Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alisema kuwa ni Ijtihad ya Imam Ahmad ibn Hanbal, kuwa ibada ni sehemu ya imani. Hatahivyo, Ijtehad zote za Imam Ahmad ibn Hanbal zilikuwa zimerekodiwa katika vitabu na Maulamaa wa Makkah walikuwa wakizijua zote, hivyo wao waliweza kwa urahisi mno kuwashawishi Mawahhabi hao watatu kuwa shutuma za Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab zilikuwa za uongo na potofu.

Mawahhabi hao watatu walikuwa na uhakika kuwa imani ya Maulamaa wa Ahl as-Sunna yalikuwa ni sahihi nao hata walithubutu kusema: “Waislamu wa Makkah wanazuru makaburi ya Mtume Muhammad s.a.w.w., ‘Abdullah ibn Abbas na Mahjub ( Mahjub Sayyid ‘Abd ar-Rahman, alikuwa ni ‘Alim mashuhuri katika zama zake, alifariki katika mwaka 1204 A.H. (1790) na alizikwa katika makaburi ya Mu’alla (makaburi ya Maqureishi) ) na huwa wakisema: ‘Ewe Rasul - Allah !’ au ‘Ewe Ibn ‘Abbas!’ au ‘Ewe Mahjub!’ Hatahivyo, kwa mujibu wa ijtihad ya Imam wetu Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab, wale wasemao ‘La ilaha Illallah Muhammadun Rasulullah,’ lakini wanawaomba watu wengine hugeuka kuwa makafiri. Hivyo ni halali kuwaua na kuzichukua mali zao zote.” Maulamaa wa Ahl as-Sunna waliwajibu: “Kuzuru makaburi ya waja wapenzi wa Allah swt kwa ajili ya kuwafanya tawassul au kuwaomba watuombee, haimaanishi kuwa wao wanaabudiwa. Wao wanapowazuru, hapakuwi na nia ya kuwaabudu bali ni kwa madhumuni ya kumwomba Allah swt wawe wasila, yaani, kuwapitia na kuwafanya watetezi.” Na wao walitoa hoja zao kwa vithibitisho kuwa imeruhusiwa na vile vile ni muhimu kuwachukua hao kama ndio sababu.

Zipo dalili na uthibitisho mwingi wa uhalali wa kuzuru makaburi ya Awliya' kwa ajili ya kuwafanya wasila au kuwaomba wawe wasila wakati wa kumwomba Allah swt hoja zetu: Ayah ya 35 ya Surah al-Maidah inasema, “Enyi Waumini ! Mwogopeni Allah natafuteni Wasila wa kunifikia Mimi !” Vitabu vyote vya tafsiri vinaandika chochote au yeyote apendwaye au akubaliwaye na Allah swt huwa wasila. Ayah ya 80 ya Sura an-Nisa’ inasema: “Yeyote amtiiaye Rasul basi amemtii Allah.” Hii ni sababu kwa nini wasila katika Ayah iliyotangulia ni Rasulullah kwa mujibu wa maulamaa’ wengi wa Kiislam. Kwa hivyo, inaruhusiwa kufanya wasila wa Mitume a.s. na warithi wao – Awliya' na waja halisi Waislamu – na kujaribu kumkaribia Allah swt kwa kuwapitia hao. Iwapo ingalikuwa ni ukafiri au ushirikina kwa kuwataja au kuwaomba, wale ambao husali basi wote kwa pamoja watakuwa makafiri; basi Mawahhabi pia watakuwa makafiri kwa mujibu wa taarifa ya hapo juu – kama ilivyonakiliwa fatwa ya Muhammad ibn Sulaiman, kwani kila Mwislamu anatuma salaam juu ya Rasulullah na dua kwa ajili ya mtukufu Mtume s.a.w.w. katika kila sala kwa kusoma”As-salaamu ‘alaika ayyuhan Nabiyyu wa rahmat-Allah.”

Zipo faida nyingi mno kwa kuzuru makaburi na kumwomba Allah swt kwa kuwafanya Awliya' kama wasila. Kwa sababu Hadith iliyotolewa na Ibn ‘Askari na kunakiliwa katika Kunuz ad-daqaiq inasema, “Mwislamu ni kioo cha Mwislamu ndugu yake.”Tunaelewa kutokana na Hadith hiyo kuwa roho ya Mwislamu mmoja ni kioo cha Mwislamu mwingine. Hivyo zinaonekana ndani mwao. Uwema unatoka kutoka roho ya walii kuingia katika moyo wa yule mtu ambaye anayemfikiria na kuwa wasila wake wakati wa kulizuru kaburi la wali huyo. Roho iliyo dhaifu inapata nguvu. Huu ni mfano wa vyombo viliwi vinavyounganishwa kwa bomba. Roho iliyo na nguvu au cheo cha juu ndiyo inayopungukiwa. Iwapo roho ya yule aliye kaburini itakuwa dhaifu basi roho ya aliyemzuru itakuwa imeudhika.Na hii ndiyo sababu kuu ya kuharamishwa kuzuru makaburi hapo katika kipindi cha mwanzoni cha Islam, kwa sababu makaburi hayo yalikuwa ni ya watu wale waliotoka katika kipindi cha ujahili wakati huo. Baada ya muda ilitolewa ruhusa kuzuru makaburi kwa sababu palikuwa pamezikwa Waislamu. Mtu atakuwa akifikiria Mtume Muhammad s.a.w.w. au wali atakapokuwa akizuru kaburi lake. Ipo Hadith sharifu isemayo: “Allah swt huonyesha rehema wakati waja Wake watukufu wanapofikiriwa.” Hivyo imeeleweka kutokana na Hadith hii vile vile kuwa Allah swt humpelekea rehema mtu anayezuru makaburi, na Yeye huzikubalia sala za waja Wake wale ambao huteremshiwa rehema Zake.Hivyo kusema kidhahiri kuwa:“Makaburi yasitembelewe. Awliya' hawawezi kuchukuliwa kama wasila,” ni maoni yanayotakiwa kupuuzwa. Ipo Hadith tukufu isemayo: “Yeyote yule anayezuru kaburi langu baada ya kutimiza faradhi za Hijja basi atakuwa kama ametembelea mimi pale nilipokuwa hai,” inakanusha imani hii katika misingi yake na hivyo kuonyesha umuhimu wa kuzuru makaburi. Hadith hii imetolewa kutoka Kunuz ad-daqa’iq.

Mawahhabi nao wanaleta mbele Hadith: “Wanalaaniwa wale wanawake ambao huzuru makaburi na wale wafanyao sala makaburini na wale ambao huwasha mishumaa juu ya makaburi,” kama kisingizio cha kubomoa makaburi ya shakhsiyyah watukufu. Wao vile vile wandai kuwa mambo kama hayo hayakuwapo katika zama za Mtume Muhammad s.a.w.w. na wanatoa Hadith ifuatayo, “Mambo ambayo hayapo katika zama zetu lakini yataletwa mbeleni na wala musiyanasabishe kwetu.” Wawakilishi wa Mawahhabi walikubaliana na Maulamaa wa Ahl as-Sunna kwa sababu majibu ya dai lao la pili yalikanusha madai yao.