UCHACHE WA KUFIKIRI KWA UNDANI

Tangu zaidi ya miaka mia moja iliyopita, vita ya kifikra dhidi ya Uislamu ikiwa inawasha moto wake, na mataifa ya magharibi na mashariki yakisaidiana na vibaraka wao walioko katika nchi za Kiislamu yanafanya juhudi zao za upeo mkubwa ili kuinagamiza dini hii tukufu na kuchafua shabaha yake, haipiti wiki au mwezi isipokuwa hutolewa kitabu dhidi ya dini tukufu ya KiisIamu.

Katika hali hii yenye majonzi, hivi kweli inafaa kwa Saudia kukusanya nguvu zake na uwezo wake na matoleo yake yote ili kuupiga vita Ushia peke yake tu?!!

Na kana kwamba katika ulimwengu wa Kiislamu hakuna tatizo jingine isipokuwa Ushia?!!

Hata hivyo, lau vijitabu hivyo vingekuwa vinazungumza juu ya msingi wa mantiq na dalili tusingevipinga kwani mantiq inakubalika kwa wanachuoni wa Kishia, kwani wao huikubali au kuipinga kwa mantiq na hoja, lakini kwa bahati mbaya sana vijitabu vyao vingi utaviona vimejaa uongo, uzushi, makosa na uzandiki dhidi ya Mashia na dhidi ya wanachuoni wao wema (R.A.).

Bali utaona katika baadhi ya vitaba hivyo kuwa, havikuepukana na kumtweza na kumkosea Adabu Imamul-Muta-Qina na Amirul-Muuminina Bwana wetu na kiongozi wetu Ali [a].

Hebu chukua mfano wa hilo katika kitabu, "Ashiatu WatTashayyuu" tulichokiashiria hapo kabla, hicho ni mfano ulio wazi miongoni mwa vijitabu vyenye kupotoka, kwani utamuona mtunzi (Akinakili kutoka kwa Tabari, Ibn Kathir, Ibn Khaladun na wengineo miongoni mwa maadui wa haki) anauona Ushia kuwa ni (Dhehebu) lililozalikana kutokana na fikra ya Abdallah Bin Sabaa ambaye ni Myahudi, kisha anatolea Ushahidi aliouandika Ahmad Amin wa Misri (ndani ya kitaba kiitwacho Fajrul-Islam) dhidi ya Shia, kisha anakamilisha safari yake kutolea ushahidi makala za mustashriqin Mayahudi na Wakristo "Dauzi" na "Mul-Aer" na "Wilhazen".

Lakini hataji chochote kutoka katika vitaba vya Mashia, basi je, hii ndiyo Insaaf (Usawa)!?

Hakika wanachuoni wa Kishia wa hapo mwanzo kama vile Sheikh Saduq aliyefariki mwaka 381 A.H. na Sheikh Mufid aliyefariki mwaka 413 A.H. na wengineo, bila shaka waliziandika Aqida (Itikadi) za Kishia na kuzitawanya kwa watu nazo ni nyingi mno ndani ya maktaba na zinatoa picha ya asili ya Aqida za Kishia, basi ni vipi hazitegemei katika kuzinakili?

Je, Siyo kwamba "'Wenye nyumba ndiyo wajuao zaidi kilichomo ndani yake"?!

Je, Ahmad Amin wa Misri ambaye haujui Ushia na hautambui kama alivyokiri yeye mwenyewe ndiye ayajuaye madhehebu ya haki kuliko wanachuoni wake wema?

Na utamuona mwandishi huyu muovu wa Kiwahabi anajaribu kujitakasa makosa aliyoyafanya dhidi ya Mashia kwa kutegemea vitabu vya maadui zao anasema:

"Kwa hakika vitabu hivi (yaani vitabu vya itikadi za Kishia) ni vitabu vya propaganda za Kishia ama kwa itikadi yao halisi haikutajwa ndani ya vitabu hivi!!!

Na baya zaidi kuliko hilo ni kwamba, yeye anaileta hadithi iliyoko ndani ya 'Biharul-Anwaar" na Al-n-Waarun-Nu'maniyyah na kuizingatia kuwa ni dalili ya itiqadi ya Mashia, huku akijua kwamba hapana shaka kuwa kuna hadithi dhaifu ndani ya vitabu vya Kisunni na Kishia, hili sote tunalijua, na kutaja hadithi moja haiwi ndiyo dalili juu ya itikadi ya watu fulani (kwa namna yoyote ile) kwani wako wapokezi wengine ni dhaifu na waongo na ni Majhul hawatambulikani hali zao". Basi haiwezekani kuitegemea hadithi ila baada ya kuihakiki katika sanadi yake na wapokezi wake.

Sisi tunamuuliza Wahabi huyu mwenye kuajiriwa na wengineo mfano wake miongoni mwa wanaofadhiliwa: Je, hivi kila kilichokuja katika Tarikhut-Tabari kinazingatiwa kuwa ni sahihi bila ya shaka au ni kwamba kuyategemea hayo aliyoyaleta kunategemea uhakiki katika Isnadi yake?!

Hakika katika mambo yasiyokuwa na shaka ndani yake, ni kuwemo kwa wapokezi waongo wa wazushi ndani ya riwaya za

yake, basi Taaliq hiyo mbovu isingetoka kwake na wala asingemkosoa Sheikh Mudhafar ambaye ni mwanachuoni mkubwa.

Kishia sisi tunasema, ikiwa mwito wa Uimamu wa Ali [a] unazingatiwa kuwa ni shirki au ni kuushirikisha na utume, basi Qur'an imetangulia kulisema hilo, kwani imetoa mwito kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Ulul-Amri katika Siyaqi moja.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu "Mtiini Mwenyezi Mungu na mumtii Mtume na Ulul-Amri miongoni mwenu."

Qur'an, 4:5.

Basi kwa mujibu wa maoni ya mwandishi huyu wa Kiwahabi, ni kwamba mjumbe wa Mwenyezi Mungu [s] badala ya kulingania Tauhidi alilingania shirki na Aqida ya miungu wawili kwani aliambatanisha baina ya kuwatii Ulul Amri na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani neno Ulul Amri kwa namna yoyote ile tutakayolifasiri bila shaka litamuingiza Imam Ali [a] (Katika maana hiyo), bali yeye anastahiki zaidi kuliko wengine.

Wanahistoria na wanachuoni wa Tafsiri na hadithi wameeleza kwamba iliposhuka kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

"Na Uwaone Jamaa zako wa karibu"

Qur'an 26:214

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu [s] aliwaita jamaa zake wa karibu (nduguze, na wazee wake) kwenye karamu ya chakula nyumbani kwake, kasha akawatangazia habari ya Unabii wake na Utume wake na baada ya hapo akasema:

"Ni nani kati yenu atakayenisaidia juu ya jambo hili kwa sharti awe ndugu yangu na wasii wangu na Khalifa wangu kwenu"?

Basi hapana yeyote aliyesimama isipokua Imam Ali [a] akasema, "Mimi Ewe Mjumbe wa Mwenezi Mungu."

Mtume [s] alikariri maneno yake hayo mara ya pili na ya tatu ili awape fursa ya kuchukua uthibitisho..... Na hakuna yeyote aliyejibu isipokuwa Amir-ul-Muuminina Ali [a] basi Mtume akasema:

3. Seif Ibn Umar: Anasimulia hadithi za uongo na kuzinasibisha kwa wapokezi waaminifu. [13]

4. Yazid Al-Faq-Asii: Maj-hul kabisa (Hatambulikani hali yake kabisa) jina lake halikutajwa popote ndani ya vitabu vya "Rijal" (yaani vitabu vinavyochunguza hali za wapokezi wa hadithi).

Na inafaa kusema kwamba, Tabari anasimulia ndani ya juzuu Ia tatu, la nne na la tano katika Tarikh yake tokea mwaka wa kumi na moja A.H. mpaka mwaka wa thelathini na saba A.H. na miaka hii ni kipindi cha utawala wa Abubakr na Umar na Uthman na riwaya zote hizo zimepokelewa kutoka kwa watu hawa watano tu!! Na matokeo yake Tabari amezua matukio mengi miongoni mwa hayo na akayaeleza kama vile ipendavyo nafsi yake!! Basi Je, hii inasihi na Je, inajuzu kuzitegemea riwaya kama hizi?!

Na kinacholeta mshangao zaidi ni kwamba, riwaya za watu hawa watano ziko katika juzuu ya tatu na ya nne na ya tano tu ndani ya Tarikh Tabari, amma majuzuu mengine huwezi kuona majina yao yanatajwa wala riwaya itokayo kwao isipokuwa riwaya moja tu ndani ya juzuu ya kumi!!

Basi Je, Ujuzi wa Tarikh (Historia) alionao "Sari" na "Seif bin Umar" ulikuwa umedhibitiwa katika kipindi hiki peke yake tu, na ulikuwa unahusika na mambo ya Madh-heb peke yake?!!

Naam, yeyote mwenye kuzichunguza kwa undani riwaya za watu hawa watano atafahamu wazi kwamba riwaya hizo ni uzushi wa mtu mmoja, na kwamba ndani yake kulikuwa na lengo makhsusi.

Ni mushkeli kufikiria kuwa Tabari hakufahamu jambo hili, basi ni kwa nini Tabari ametaja yote haya?

Jawabu lake ni kwamba: Bila shaka hiyo ni hali ya kupenda na chuki vitu ambavyo humpofua mtu na kumfanya awe kiziwi!

Na kinachohuzunisha zaidi ni kwamba kundi la wanahistoria waliokuja baada ya Tabari wakanakili toka kwake na wakafuata nyayo zake na wakazileta riwaya hizi za uzushi na uongo ndani ya vitabu vyao vya historia bila ya uchunguzi wowote juu ya kusihi kwake na watu waliozisimulia na sanadi zake, wakidhani kwamba kila anachokisimulia Tabari ndiyo hasa tukio halisi na ndiyo ukweli ulivyo.

Iangalie Tarikh ya Ibn Asakir na Al-kamil ya Ibn Al-Athir, na Al-Bidayatu Wan-Nihayah ya Ibn Kathir na Tarikh ya Ibn Khaladun na nyinginezo utaona usahihi wa maneno yetu.

Hali ni hiyo hiyo kwani vitabu vya Tarikh vya sasa hivi havikusalimika na uzushi huu mbaya na Ikhtilafu inayochukiza. Lakini kwa bahati nzuri watu wa Sanadi ndani ya riwaya zilizomo katika Tarikh ya Tabari wametajwa, na hilo ni miongoni mwa mambo ambayo yanatoa nafasi ya kufahamu riwaya sahihi na kuilinganisha na riwaya dhaifu au iliyozushwa kama tulivyokuletea mfano mmoja unaoeleza jambo hilo.

Na sasa tunarudia mazungumzo juu ya Kitabu "As-Shiatu Wa At-Tashayyuu" na tunasema: "Kwa hakika kitabu kinachotegemea rejea ambazo riwaya zake ni za uzushi na wapokezi wa riwaya hizo ni waongo tena wazushi, basi kitabu hiki kitakuwa hakimiliki japo thamani ndogo, nasi sasa hivi tuko katika zama za usomi na uchunguzi.

Basi Je, hivi itasihi kwa kundi kubwa la Kiislamu Ienye hadhi kubwa katika elimu za Kiislamu na kuhuisha Sunna Tukufu ya Mtume [s] ambalo liko mstari wa mbele kuwapiga wavamizi wa Ki'Israeli, hivi kweli ni sahihi kundi hilo linasibishwe kwa Myahudi asiyejulikana kwa kutegemea Tarikh potofu ambazo umekwisha thibiti uongo wa wapokezi wake?

[13] Mizanul-Itidal, juz. 1, uk. 438, Tahdhib-but-Tahdhib. juz. 4, uk. 295