MAKOSA KATIKA VITABU VYA MASUNNI

Naam bila shaka upungufu na kosa lililoko katika vitabu vya Masunni na hasa Mawahabi linarudi kwenye mambo mawili:

Jambo Kwanza:

Ni kukosa kwao maarifa mengi ya kutosha kuhusu madh-hebu ya haki, na upungufu huu walionao hauhusu zama zetu hizi tu, bali unarudi hadi kwenye karne zilizopita katika historia, na huenda sababu ya jambo hilo ni ile hali iliyokuwa ikitendwa na serikali za watu wa Jahannam yaani Banu Umayyah na wengineo katika kuwakandamiza na kuwanyima uhuru Mashia na kutokuwapa nafasi ya kubainisha itikadi zao za haki katika Mahfali na mikusanyiko ya Kielimu, ili watu waufahamu Ushia kutoka katika vinywa vya viongozi wake wasipotoshwe na uzushi wa maadui zake.

Kwa hakika historia inatuthibitishia kwamba, Madh-hebu yote yalikuwa yanauhuru wa kutoa maoni na kubainisha itikadi (zao) isipokuwa haya Madh-hebu ya haki yalikuwa yamezuwiliwa kufanya hivyo..

Naam, upepo wa uhuru kwa Mashia ulivuma katika baadhi ya nyakati ambazo hazikutosheleza kulithibitisha lengo hili.

Na kwa hali yoyote ile, kutokuyafahamu Madh-hebu ya Ushia (na wakati mwingine chuki) imekuwa ndiyo sababu ya kutengenezwa uongo na uzushi huu na kuvijaza vitabu uzushi na kuichafua shabaha ya Madh-hebu haya ya haki.

Na kwa hakika Ahmad Amin wa Misri, mwandishi wa kitabu kiitwacho "Fajrul-Islam" amekiri jambo hili baada ya kutawanya kitabu chake hicho kilichojaa uongo na uzushi dhidi ya Shia, kisha akauzuru mji wa Najaf baadhi ya wanachuoni wakamlaumu kuhusiana na kupotosha kwake na uzushi wake dhidi ya Shia, na udhuru wake mkubwa aliokuwa nao ilikuwa ni kutokuujua Ushia na uchache wa rejea.

Jambo La Pili:

Ni kuharibika kwa utaratibu wa masomo katika vyuo vya Kisunni na kubadilishwa kwa vitabu vyenye maarifa kwa undani kama vile "Kitabul-Mawaqifi na Sharhul Maqasid" (Na badala yake vikawekwa) vitabu vya kiwango cha chini visivyokuwa na uchunguzi wa kina, na jambo hilo limepelekea kushuka kwa kiwango chakufikiri na utunzi na kutoweka fikra za uchunguzi wa kina kiasi kwamba hakuna katika nchi nyingi za Kiislamu anayeweza kuvisomesha vyema vitabu hivi viwili ambavyo vimeandikwa katika karne ya nane Hijiriyyah.

Kwa sababu hii basi, siyo jambo la ajabu kumuona "Ihsan Ilahi Dhahir" kwa mfano anatangatanga hajui anachokifanya kwani hatenganishi baina ya mwito wa Uimamu na mwito wa Utume, na anaandika kitabu juu ya madh-hebu katika historia na kuvitawanya kwa kusaidiwa na mali zinazotokana na petroli ambaye inaporwa na serikali ya uvamizi ya Kiwahabi ndani ya Hijazi, na hili linafanyika hali ya kuwa inafahamika kwamba mwandishi huyu hafahamu misingi ya itikadi ya Kishia.