NENO "SHIRKI" LITAKUKUTA KILA UPANDE

Bila shaka kabisa miongoni mwa maneno ambayo ni rahisi na yanatumika katika nchi ya Saudia ni neno "Shirki", na tuhuma hii huelekezwa kwa wanachuoni wengi na watu wenye heshima katika Uislamu!

Utakapokutana na watu idara ya "Al-Amri Bil Maaruf Wannahyi Anil Munkar neno utakalolisikia kila wakati ni hili neno baya na mfano wa hili, kama kwamba ndani ya kamusi zao hakuna maneno mengine isipokuwa maneno haya mabaya yenye kuchukiza tena machafu na ni kana kwamba hawana jingine la maana isipokuwa kuelekeza tuhuma hii ya shirki kwa kuwatuhumu (vibaya) wageni wa Mwenyezi Mungu na mahujaji wa nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu!!

Wakati nikiandika utangulizi huu kimenifikia kitabu kiitwacho, "As-hiatu-wa At-Tashayuu" kilichotungwa na Mpakistani mwenye chuki ambaye ni miongoni mwa wanaofadhiliwa na Mawahabi, jina lake ni Ihsan Ilahi Dharir, na kimechapishwa Saudia. Na ndani yake anazitupa tuhuma na uzushi dhidi ya Ushia, na anadai kwamba yeye anaeleza kutokana na vitabu vyao na rejea zao.

Kwa mfano, utaona katika ukurasa wa ishirini wa kitabu hicho, anataja neno la Al-Marhum Al-Ustadh Mheshimiwa Sheikh Muhammad Husein Al-Mudhaffar, kisha analisherehesha kufuatana na vile apendavyo na namna inavyompelekea nafsi yake inayoamrisha uovu.

Katika maelezo yafuatayo tunaweka mbele yako Ewe msomaji Mutukufu neno hilo pamoja na sherehe ya Wahabi huyu ili uone mwenyewe ni vipi Mawahabi waliofilisika kwa dalili wanavyotegemea maneno ya tuhuma na uzushi na uongo dhidi ya Shia. Marhum Al-Mudhaffar anasema:

"Fakanatid-Daawatu Littashayui Liabil-Hasan Alayhis Salaam Min Sahibir-Risalat Salallahu Alayhi Waalihi Wasallama Tamshi Minhu Janban Lijanbin Maad-dawat Lish-Shahadatayn."

Tafsiri Yake: Mwito kutoka kwa Mtume [s] kumfuata Abul-Hasan Ali [a] ulikuwa ukienda sambamba na mwito wa Shahada mbili.

Na maana ya maneno yake haya ni kwamba: Ushia haukuzalikana kutokana na hali ya kimazingira wala siyo Madh-hebu yaliyoanzishwa baadaye, bali ni Mah-hebu ya asili ambayo chanzo chake kinaanzia kwa Mwenyewe Mtume Muhammad [s], kwani Mtume alikuwa akilingania wau juu ya Uimamu wa Amirul-Muuminina (Ali [a]) sambamba na wito Wa Shahada mbili.

Kisha Wahabi huyu muovu anayawekea Taaliq maneno ya Sheikh Mudhaffar na anasema:

Hakika Mtume (kwa mujibu wa madai ya Mudhaffar) alikuwa akimfanya Ali kuwa ni mshirika wake katika Unabii wake na ujumbe wake"!!

Iwapo Mwandishi huyu siyo mtumwa wa matamanio yake na chuki na mwenye kufadhiliwa na Mawahabi, na iwapo ni mchunguzi wa misingi ya itikadi za Kiislamu za Kishia na misingi Tabari, nasi kwa sasa hivi hatuna lengo la kufanya ufafanuzi katika maudhui hii, lakini tunataja mfano wa jambo hilo:

Ndani ya Kitabu "As-hiatu-wa At-Tashayuu" uk. 49 mtungaji anatuhumu Ushia kwamba umepokea fikra zake kutoka kwa Abdallah bin Sabaa aliyezalikana kutoka kwa Myahudi wa Yemen, na anavyoitakidi Tabari kwamba (Abdallah bin Sabaa) alidhihirisha Uislamu na kuficha Uyahudi na mapenzi yake kwa Imam Ali aliyafanya kuwa ni kifuniko cha kueneza fikra zake.

Jambo hili hatutalitafiti kwa wakati huu.

Basi utamona mwandishi huyu wa Kiwahabi anategemea mambo aliyoyapokea Tabari kuhusu uzushi huu, Amma Sanad za riwaya ambayo Tabari anaieleza ni kama ifutavyo neon kwa neon:"Aliniandikia As-Sariyyu kutoka kwa Shuaib, kutoka kwa Seif, kutoka Atiyyah naye toka kwa Yazid Al-Faq-Asi: Abdullah bin Sabaa alikuwa Myahudi katika watu wa Sanaa...." (Vile vile ameipokea riwaya hii Ibn Khaladun Al-Magharibi na Ibn Kathir Ash-Shami na walio mfano wa Tabari miongoni mwa maadui wa Ahlul-Bait.

Sasa hivi tunaiweka riwaya hii kwenye meza ya uchunguzi wa uhakiki ili tuone, je, inajuzu kuitegemea riwaya ya wapokezi hawa amboa majina yao yametajwa hapa au haifi?

Kwa mtazamo wa haraka ndani ya vitabu vya elimu ya rijali (ambavyo vimeandikwa na wanachuoni wa Kisunni) vitatutosheleza kufahamu hali zaa wapokezi hawa.

Hebu Tazama uhakika wenyewe:

1. As-Sari sawa sawa akiwa ni As-Sari ibn Ismail Al-Kufi au As-Sari lbn A'sim aliyekufa mwaka 258 kila mmoja wao ni miongoni mwa waongo na wazushi.[10]

2. Shuaib ibn Ibrahim Al-Kufi: Maj-hul (Hatambulikani hali yake).[11]

"Hakika huyu ni ndugu yangu na ni wasii wangu na ni khalifa wangu kwenu, basi msikilizeni na mumtii.[12]

Kutokana na ukweli huu wa kihistoria Mashia wanasema kwamba, tangu siku hiyo aliyoamrishwa Mtume [s] kulingania Tauhidi na Utume, aliamuriwa pia katika siku hiyo kulingania Uimamu wa Ali [a] na ukhalifa wake baada yake, basi mwito wa imani na Utume umeambatanishwa na mwito na kuamini Uimamu.

Je, inasihi kusemwa kwamba Mashia wanaitakidi kuwa Ali [a] alikuwa mshirika wa Mtume katika Utume?" Na Je, mwito wa Ukhalifa wa Imam Ali [a] baada ya Mtume [s] kufariki maana yake ni mwito wa Unabii?

[10] Tahdhibut-Tahdhib cha Ibn Hajar, Juz. 3, uk. 46, Tarikh al-Khatib, Juz. 1, uk. 193, Mizanul-Itidal, Juz. 1, uk.37, Lisanul Mizan, Juz. 3, uk. 13

[11] Mizanul-Itidal, Juz. 1, uk. 447, Lisanul-Mizan, Juz.3, uk. 145

[12] Rejea za hadithi hii zimetajwa ndani ya vitabu vya wanahistoria na wanahadithi na wafasiri wa Qur'an, na ni hadithi maarufu kwao kwa jina la (Yaumul-Indhar na Badu'd-dawah) yaani mwaanzo wa da'awah na miongoni mwa walioipokea ni Tabari katika Tarikh yake. Juz. 2, uk. 63, chapa ya Misri.