MAPINDUZI YA KIISLAMU NA HUJUMA ZA KIWAHABI

Kwa hakika Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yameleta mshituko mkubwa katika ghuba, na kuzisononesha tawala zote zilizoko sehemu hiyo na hasa hasa zile zinazohusiana na mataifa makubwa na kuyategemea kwa kila hali, na kwa upande mwingine madola hayo ya kikoloni yanazitegemea nchi hizo na miongoni mwa tawala hizi ni ule utawala wa Kiwahabi unaotawala nchi kubwa miongoni mwa nchi za Kiislamu, nchi ambayo inasifika kwa utajiri mkubwa wa asili na inufaika kwa hali maalum ya kijiografia.

Basi ukoloni mbaya na vibaraka wake na watendaji wake wakiongozwa na waliaganiaji wa Kiwahabi wamekusudia kupinga mapinduzi ya Kiislamu na kimbunga chake kwa njia mbali mbali, miongoni mwa upinzani huo ni kuzusha wasi wasi ndani yake na kuwasha mioto ya vita dhidi yake na kulazimisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya mapinduzi hayo.

Na njama zote hizi za upinzani dhidi ya mapinduzi ziliposhindwa, wakakusudia kuleta picha mbaya ya utamaduni wa mapinduzi an kuondosha Mafhumu yake na kuuzushia uongo na kuupakazia uzushi ili kuwazuia watu kufuata muongozo wake na kumfuata kiongozi wa mapinduzi hayo.

Kwa hakika njama hii ya kiadui dhidi ya utamaduni wa mapinduzi ya Kiislamu, inabainika katika mambo yafuatayo:

1. Kueneza matangazo na magazeti aina nyingi katika nchi mbali mbali za ulimwengu ili kuzungumzia dhidi ya mapinduzi na kufanya ushawishi dhidi yake na kuonyesha sura mbaya ya utamaduni wake halisi.

2. Kuchapisha vijitabu na vitabu vingi mno kuhusu utamaduni huo kwa kupitia mikono ya watu na waandishi ambao wameuza nafsi zao na hawajali isipokuwa mlo wao na pengine vyeo vyao vya kidunia, wakiongozwa na yule muongo mkubwa ih-Sa'an ilahi dhahiri[7] ambaye ni miongoni mwa watu wanaopata mali nyingi kutoka Saudia.

Mtu huyu amesimama kidete kwa nguvu zake zote na kwa kila kile ambacho Suudia inakitoa ili kutoa picha mbaya ya taaluma ya mapinduzi miongoni mwa Waislamu.

Na huyu Bwana ni masikini kwa kila kitu hata katika madai yake kuwa anayafahamu madhhebu ya Shia Imamiyyah, basi anachanganya na kuvuruga na wala hapambanui baina ya Asili na Far-i. Wala baina ya Aqida na Riwaya, na anatoa ushahidi kwa kutumia riwaya kuwa eti ndiyo madhhebu ya Shia (yalivyo).

Yapo mengi zaidi ya hayo, katika uongo wake na uzushi wake na natija mbovu atoazo, hivyo basi sisi tutahusika naye mahala pengine ndani ya kitabu pekee.

3. Kuyaeneza Madhhebu ya Kiwahabi miongoni mwa vijana katika Eneo hilo kwa njia mbali mbali huku wakibainisha wazi kuwa Mawahabi ndiyo Waislamu na kwamba wao ndiyo wanaompwekesha Mwenyezi Mungu na ndiyo wanaoitumia Qur'an na sunna kwa usahihi, na wasiyokuwa wao wako mbali mno na hayo.

Basi kwa ajili hiyo tumeweka risala hiyo kuyabainisha madhhebu ya Kiwahabi, na kuweka bayana ndani yake upeo wa yale wayasemayo Mawahabi na upeo wa kuwa kwao mbali na Qur'an na Sunna na sera ya Waislamu.

Mwisho, tunatoa ushauri kwa wanachuoni wa Kiislamu walioko ulimwenguni kwanza, na pili kwa waandishi wa Kiwahabi, wasimamie kuitisha mkutano wa Ulimwengu wa Kiislamu, mkutano ambao utawakusanya wanachuoni wa Kiislamu kutoka vikundi vyote vya Kiislamu ili kuyachambua Mas-ala haya kwa mujibu wa Qur'an na Sunna na kuyasambaza matokeo ya mkutano huo kwa Waislamu wote ili haki iwabainikie kwa uwazi na ifuatwe, na iliyo haki ndiyo yenye haki mno kufuatwa, na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuwafikisha na ndiye msaidizi.


Jaafar Subhani
Qum Takatifu
1/Mfunguo Tano/1405
[7] Sasa hivi ni marehemu.