MAWAHABI NA MSIMAMO WAO KWA UNDANI KATIKA QADHIYYAH ZA TAUHID.

Cha ajabu, (na midhali uhai utona maajabu zaidi) in kwamba, Uwahabi unatokana na fikia ya Sheikh mpotofu aitwaye Ibn Taimiyyah ambaye ametuarifisha maana ya Tauhidi katika kitabu chake aliposema: "Hakika Mwenyezi Mungu yuko juu ya mbingu yake kwenye arshi yake, yuko juu ya viumbe wake".[1]

Na amesema tena: "Mola wete hushuka mpaka kwenye mbingu ya dunia kila siku inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku kisha husema; Nani ataniomba (saa hizi) nami nitamkubalia (maombi yake) nani ataniomba nami nitampa, ni nani atanitaka msamaha nami nitamsamehe".[2]

Haya ndiyo maarifa ya mtu huyo (Ibn Taimiyyah) na huku ndiko kumtakasa kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu na (yote haya aliyoyasema) inajulisha wazi kabisa kuwa yeye anaitakidi kuwa Mwenyezi Mungu anao mwili na anapatikana upande fulani. Na (huyu Ibn Taimiyyah) amesema hayo kutokana na kung'ang'ania kwake dhahiri ya aya na hadithi za Mtume bila ya kuzitafiti kwa undani aya zilizokuja kuhusu maudhui hiyo, na bila ya kufanya uhakiki katika isnadi za hadithi na madhumuni yake.

Basi iwapo haya ndiyo maoni ya mwalimu (wa Mawahabi) basi itakuwaje hali ya watu wanaoramba vikombe vyake na wanakaa katika meza zake kama kina Ibn Al-Qayyim na Muhammad bin Abdul-Wahhab. Na cha ajabu ni kwamba, hawa nao wanataka wawe ni waalimu wa Tauhidi na walinganiaji wa Tauhid. Na Mwenyezi Mungu amrehemu mshairi aliyesema: "Katika maajabu ya duniani ni kwamba, mwenye ugonjwa wa manjano anadai kuwa ni mganga na mwenye macho mabovu awe mwenye kutengeneza dawa ya macho na kipofu awe mnajimu, na msomaji wetu wa Qur'an awe Mturuki na Khatibu wetu awe Muhindi, basi njooni tulie na tupige vifuajuu ya Uislamu, (Tuulilie kwa msiba uliyoufika).

Hii ndiyo itikadi ya jamaa hawa kuhusu Mwenyezi Mungu, basi iwapo tutataka kuzipima fikra hizi, basi tunawajibika kulinganisha kati ya maelezo hayo na yale yaliyopokelewa kutoka kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume [s] kuhusu makusudio hayo (ya Tauhid), kisha tuone ni lipi kati ya makundi haya mawili lenye haki ya kufuatwa.

Je, ni yule amsifuye Mwenyezi Mungu kwamba, yeye ana mwili na anakaa upande fulani na kuteremka mpaka mbingu ya dunia, (ndiye wa kufuatwa) au yule amsifuye Mwenyezi Mungu kwa kusema:

"Shukurani zote anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye hawafikii kikamilifu sifa zake wenye kuzisema, wala hawazidhibiti neema zake wenye kuhesabu, na wala hawatekelezi ipasavyo haki yake wenye kujitahidi, Mwenyezi Mungu ambaye fikra hazimfikii hate ziende umbali kiasi gani, wala akili hazimfikii japo ziende ndani kiasi gani, ambaye sifa zake hazina mpaka, wala hakuna maneno yatakayoeleza sifa zake kikamilifu. Na yeye hana wakati uliohesabiwa wala muda uliopangwa, mwenye kumsifu Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa fikra zake atakuwa kamfanyia mwenza, na mwenye kumfanyia mwenza atakuwa kanifanya wawili na mwenye kumfanya wawili basi atakuwa kamgawa. Na mwenye kumgawa hakumjua, na asiyemjua atamuashiria na mwenye kumuashiria atakuwa kamuwekea mipaka, na mwenye kumuwekea mipaka atakuwa kamfanya kuwa zaidi ya mmoja, na atakayeuliza yuko katika kitu gani, basi yeye atakuwa kamuweka ndani ya kitu, na atakayemuuliza kuwa yuko juu ya kitu gani, basi yeye atapafanya mahala pengine pote kuwa Mwenyezi Mungu hayupo. Yeye yupo lakini si kwamba hapo kabla hakuwepo. Yupo pamoja na kila kitu, lakini si kwa kuambatana naye yu mbali na kila kitu lakini si kwa kuondoka.[3]

(Ndugu msomaji), utakapolinganisha yale yaliyonakiliwa kutoka kwa As-Habul-Hadithi kuhusu Tauhidi ya Mwenyezi Mungu na kumtakasa kwake utastaajabu, kwani Imam Al-Ash-Ari amenakili toka kwao kwamba, maana ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika kuomba ni kuwa: Maovu ya waja anayaumba Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa matendo ya waja anayeyaumba ni Mwenyezi Mungu na waja hawawezi kufanya chochote.[4]

Bila shaka ibn Taimiyyah na wale walioko kama yeye wanajisifu wenyewe kuwa ni Ahlul-hadithi na wanaitafsiri Tauhidi inayohusu kuumba kwa maana hii. Basi Je, baada ya hali hii itawezekanaje kwao (kina ibn Taimiyyah) kumtakasa Mwenyezi Mungu kutokana na dhulma na ujeuri na kuvuka mipaka. Basi iwapo Mwenyezi Mungu ndiye anayeumba maovu ya waja, na waja hao wakawa hawana walichokifanya katika maovu hayo, si kwa uwezo wao wala kwa kuiga basi ni kwa nini Mwenyezi Mungu awaadhibu?

Je, hali hii siyo miongoni mwa kauli za msemaji fulani aliposema:

"Amefanya makosa mwingine nami ninaadhbiwa."

Nawe unatambua kwamba Tauhid inayohusu kuumba haimaanishi kama walivyoileza Ahlul-Hadithi, na kabla na baada yao (waliyasema kama hayo) Jabriyyah na ibn Taimiyyah na wafuasi wake.

Bali maana yake ni kwamba: Muumba mwenye kujitosheleza na mtendaji asiyehitaji kitu chochote ni yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu. Lakini wako watendaji wanaotenda kwa idhini yake na wanaumba kwa amri yake na husimama na kukaa kwa uwezo wake na nguvu zake, hivyo basi mtu analo jukumu lake kutokana na matendo yake na kazi zake: "Kila nafsi itafungika kwa yale iliyoyatenda".

Qur'an, 74:38

Notes:

[1] Maj-mu'a 'Tur-Rasailil-Kubra, cha Ibn Taimiyyah,Al-A'qidatul-Wasitiyah uk. 401.

[2] Rejea iliyotangulia uk. 309.

[3] Nahjul-Balagha Khutba ya Kwanza.

[4] Maqa'latul-Islamiyyin uk. 321.