UTANGULIZI WA CHAPA YA KWANZA KUHUSU MAWAHABI NA ITIKADI ZAO

Shukurani zote Anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye ni Mtangu na hapana kitu kilichokuwepo kabla yake, naye ndiye wa mwisho hapana baada yake chochote. Na yeye ni dhahiri hapana kilicho dhahiri kuliko yeye, naye ni batin hapana kilicho Batin kuliko yeye.

Na Sala na Salamu zimshukie Mtume wake na mbora wa viumbe wake ambaye alimtuma katika kipindi ambacho watu walikuwa ndani ya upotevu wakihangaika na wamezama ndani ya Fitna, na wametekwa na matamanio yao na wamepotoshwa na ujeuri na akili zao zimepotoshwa na Ujahili uliopita kiasi, wakihangaika katika mambo yaliyovurugika na balaa linalotokana na ujinga, basi Mtume [s] akatoa nasaha kwa upeo, akaitengeneza njia na akalingania kwa hekima na mawaidha mazuri.

Mwenyezi Mungu alimtuma kuitimiza ahadi yake na kukamilisha Utume wake. Alichukua ahadi yake toka kwa Manabii na alama zilikuwa Mashuhuri na mazazi yake yalikuwa matukufu hali ya kuwa walimwengu katika zama hizo wakiwa na mila tofauti tofauti, na fikra mbali mbali na ni vikundi vingi wakiwemo wanaomshabihisha Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake au walikuwa wakifanya kufuru na shiriki katika jina lake au wakimuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu akawaongoa kupitia kwa Mtume [s] kutoka kwenye upotovu na akawaokoa kutokana na ujinga kwa njia yake na ni nguzo ya dini yake.

Na Rehma za (Mwenyezi Mungu) zimshukie Mtume na kizazi chake (watu) ambao ndiyo wa ndani wake na ni tegemeo la dini yake na ni chombo cha elimu yake, na ni rejea ya hekima zake na ni hazina ya vitabu vyake.

Kwao wao Mwenyezi Mungu aliimarisha dini yake, na ni watu ambao Mwenyezi Mungu amewaondoshea uchafu na kuwatakasa mno.

Na (Pia) ziwashukie Masahaba wake ambao waliisoma Qur'an na wakazitumia hukmu zake na wakazizingatia faradhi kisha wakazisimamisha. Waliihuyisha Sunna na kuuwa Bid'a, walilinganiwa kwenye jihadi wakaitika, na walimuamini kiongozi wao (ambaye ni Mtume [s], kisha wakamfuata. Wamekutana na Mwenyezi Mungu na akawalipa ujira wao, na amewapa makazi ya amani baada ya khofu waliyokuwa nayo, waliendelea katika njia ya Dini na wakaifuata haki, Rehma ziwashukie daima milele muda wote wa kudumu mbingu na ardhi.

Amma baad, bila shaka umma wa Kiislamu tangu mwanzoni umeshikamana juu ya Tauhudi katika nyanja zake mbali mbali, ukaafikiana juu ya kuipwekesha dhati ya Mwenyezi Mungu na kwamba, yeye ni mmoja hana mshirika wake na ni mpweke hana mfano.

Kama ambavyo umeafikiana ya kwamba, yeye ni uumba na hapana muumba asiyekuwa yeye.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Je, kuna muumba asiyekuwa Mwenyezi Mungu"

Qur'an, 35:3

Na Amesema tena:

"Waambie, Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa kila kitu"

Qur'an, 13:16.

Vile vile umekubaliana juu ya Tauhidi yake katika Rububiya yake na kwamba hapana Mola wala mwenye kusimamiya (mambo yao) asiyekuwa yeye.

Amesema Mwenyezi Mungu:

Yeye ndiye anayesimamia mambo yote hakuna muombezi ila baada ya idnini yake, huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu basi muabuduni yeye, Je, hamna kumbukumbu?

Pia wamekubaliana kempwekesha Mwenyezi Mungu katika Ibada na kwamba, yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola ambaye anastahiki kuabudiwa na hukuna wa kuabudiwa asiyekuwa Yeye.

Mwenyezi Mungu Amesema:

"Waambie, Enyi mliopewa Kitabu, njooni kwenye neno lililo sawa kati yetu na ninyi ya kwamba, tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, na wala tusimshirikishe na chochote, wala baadhi yeta tusiwafanye kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu".

Qur 'an, 3:64

Bali hizi ndizo nukta ambazo zenye kuafikiana baina ya sheria zote za mbinguni, na yote haya yanaonekana kuwa ni miongoni mwa mambo ya kipekee kwa baadhi ya wafuasi wa sheria zilizopita. Basi mtazamo uliyo kinyume na misingi hii ni miongoni mwa vitendo vya uchafuzi na kupotosha vinavyotokana na wanachuoni, Watawa na Makasisi (wao).