MAWAHABI NA QADHIA YA KUJENGEA MAKABURI YA MAWALII

Kwa mujibu wa fikra ya Mawahabi, kujengea na kuimarisha majengo juu ya makaburi ya Manabii, Mawalii na Wachamungu ni miongoni mwa mambo yasiyoweza kuvumiliwa.

Ibn Taimiyya na mwanafunzi wake Ibn Al-Qayyim, ni watu wa kwanza kutoa fatwa ya kuharamisha ujenzi huu na kwamba ni wajibu kuyabomoa majengo hayo. Ibn Al-Qayyim anasema: "Ni wajibu kuyabomoa majengo ambayo yamejengwa kwenye makaburi, na wala haifai kabisa kuyaacha japo siku moja kila itakapowezekana kuyabomoa na kuyaondoa."[29]

Katika mwaka wa 1344 A.H., baada ya watawala wa kizazi Ili kufanikisha azma yao, watawala hawa waliwauliza maswali wanachuoni wa Madina kwa kuwataka wanachuoni hao watoc fatwa inayoharamisha kujengca makaburi, na pia kufanya kila mbinu kuutakasa msimamo wa watawala wa Kisuud mbele ya mtazamo wa Waislamu wengine, na hasa katika nchi ya Hijazi. Na hii ilitokana na ukweli kwamba, Waislamu wa Hijazi (nchi ambazo zimo Makka na Madina) walikuwa na msimamo kama Waislamu wengine ulimwenguni kuhusu jambo hili, na walikuwa wakiitakidi utukufu wa Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kuwaheshumi, pia walikuwa wakikubali kuyajengea makaburi yao. Kwa hiyo 'Mawahabi wakajaribu kuingiza maovu yao kwa kulitumia vazi la Uislamu, ili wazuie shutma na lawama kutoka kwa Waislamu!!! Subhanallah!!!

Watawala wa Kisaud walimtuma Qadhi Mkuu wa Najdi Suleiman ibn Balhiid aende Madina ili akatake fatwa kwa wanachuoni wa Madina juu ya kujengea makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu.

Lakini ni lazima kueleza kwamba, maswali aliyoyauliza ibn Balhiid yalikuwa yanayo majibu ndani yake ambayo yanaafikiana na mtazamo halisi wa Kiwahabi. Hivyo basi wanachuoni hao hawakuwa na la kufanya ila kujibu kama maswali yenyewe yalivyo.

Na wanachuoni hao wa Madina hawakuwa na ushujaa au ujasiri wa kuweza kuitangaza haki kwa kutoa fatwa iliyo sahihi, hasa kwa sababu ya wao kuwa ni watu ambao riziki zao walikuwa wakizipata kupitia milango ya watawala siku zote, na walikuwa wakifahamu tangu mwanzo kwamba, kutoa fatwa kinyume cha mtazamo wa watawala kutawasababishia kutuhumiwa kuwa ni makafiri na ni washirikina, na watahukumiwa kuuawa iwapo watakataa kutubia.

Katika Mwezi wa Mfunguo Mosi Mwaka 1344 A.H., jarida liitwalo "Ummul Quraa" linalotolewa huko Makka, lilichapisha maswali na majibu kati ya Qadhi Ibn Balhiid na wanachuoni wa Madina.

Kwa hakika kuchapishwa kwa maswali hayo kulizusha zogo na kelele nyingi miongoni mwa Waislamu, Mashia na Masunni wote; kwani walikuwa wakifahamu wazi kwamba matokeo ya fatwa hii ambayo imetolewa chini ya maafikiano yenye vitisho, yatakuwa ni kubomoa Maquba na majengo yaliyojengwa kwenye makaburi ya viongozi wa Uislamu na watu watukufu katika Uislamu. Na hayo ndiyo yaliyotokea.

Na baada tu ya fatwa hii kutolewa na hao wanachuoni wa Madina wapatao kumi na tano, na ikaenea fatwa hiyo katika nchi ya Hijazi, utawala wa Kiwahabi ulianza kuyabomoa makaburi ya kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu [s], mnamo tarehe nane ya mfunguo mosi mwaka ule ule, na uliondosha kumbukumbu za kizazi cha nyumba ya Mtume [s] na Masahaba, pia walipora kila kilichokuwemo katika haram hivo tukufu yakiwemo mazulia ya thamani na vitu vingine vya thamani.

Kikundi hiki cha wakorofi kikaugeuza uwanja mtukufu wa Baqi' kuwa ardhi tupu yenye kuhuzunisha.

Katika maelezo yafuatayo tutataja sehemu ya namna maswali yalivyoulizwa na lbn Balhiid; ili ufahamu ni namna gani muulizaji alivyoyatayarisha majibu katika masuali yake na utafahamu pia kwamba lengo halikuwa kuuliza na kutaka fatwa, bali ilikuwa ni kutaka kupatikane kuungwa mkono na kuupotosha mtazamo wa Waislamu wote, na pia kuziangamiza kumbukumbu za Unabii na Utume.

Lau lengo lingekuwa ni kutaka fatwa ya kweli na kufahamu mtazamo wa uislamu, basi nini maana ya kuingiza majibu ndani ya maswali wakati wa kutaka fatwa hivo?

Bali sisi tunadhani kwamba maswali na majibu yote yalikuwa yameandaliwa tangu hapo mwanzo katika karatasi maalum, kisha karatasi hiyo ilitumwa kwa hao wanachuoni wa Madina ili kutia saini tu.

Vinginevyo haiingii akilini kuwa, eti wanachuoni wa Madina kubadilisha muelekeo wa mtazamo wao ghafla na wakatoa fatwa kuharamisha kujengea kwenye makaburi na kuwa eti ni wajibu kuyabomoa, hali ya kuwa wakifahamu kwamba, wao na wazee wao waliyokwisha pita walikuwa wakilingania kuzihifadhi kumbukumbu za Mtume, na pia wakiyazuru majengo hayo matakatifu.

Ibn Balhiid anasema katika maswali yake hayo: "Ni ipi kauli ya wanachuoni wa Madina (Mwenyezi Mungu na awazidishie fahamu na elimu) juu ya (uhalali) wa kujenga kwenye makaburi na kisha kuyafanya majengo hayo kuwa ni Misikiti, je jambo hili linafaa au hapana?" "Na iwapo haifai bali ni jambo linalokatazwa sana sana, basi je, ni wajibu kuyabomoa na kuzuia watu wasisalie mahala hapo au hapana?"

"Na kama jengo litakuwa kwenye ardhi iliyowekwa wakfu kama vile "Baqi", hali ya kuwa linazuia kuzika maiti mwingine katika nafasi iliyochukuliwa na jengo hilo, basi je kufanya hivyo itakuwa ni kupora sehemu hiyo, jambo ambalo ni wajibu kuliondosha kutokana na kuwa ni miongoni mwa dhulma dhidi ya wanaostahiki na kwamba itakuwa ni kuzuia haki yao au hapana?" Kwa kuwa maswali haya yaliulizwa hali ya kuwa wanachuoni hao wa Madina walikuwa chini ya vitisho, basi majibu yao kwa Sheikh Ibn Balhiid yakawa kama ituatavyo:

"Ama kujenga juu ya makaburi ni jambo ambalo limekatazwa kwa ijmai' kutokana na hadithi sahihi zilizokuja kukataza jambo hilo; na kwa hiyo basi wanachuoni wengi wametoa fatwa kuwa ni wajibu kuyabomoa majengo hayo wakitegemea hadithi ya Ali (r.a.) kwamba yeye alimwambia Abul-Hayyaaji, "Nakutuma kwa jambo ambalo Mtume wa Mwenyezi Mungu alinituma mimi nikalifanye, nalo ni kwamba usiliache sanamu lolote ila ulivunje, na wala usiache kaburi lolote lililonyanyuliwa ila ulisawazishe."

Sheikh An-Najdi anasema katika makala iliyochapishwa na jarida la "Ummu'l-Quraa" katika toleo lake Ia Mwezi wa Mfunguo tisa Mwaka 1345 A.H. kwamba:

"Hakika ku jenga maquba juu ya makaburi ya Mawalii ni jambo ambalo limekuwa likiendelea kuwepo tangu karne ya tano Hijiriyya."

Naam: Hii ni baadhi ya mifano ya maneno ya Mawahabi kuhusu suala la kujenga juu ya makaburi. Na utaona kwamba

mategemeo ya ushahidi wao katika kuharamisha kujengea makaburi ndani ya vitabu vyao na maandiko yao yako kwenye hoja mbili:

1. Wanadai kuna ijma'i ya wanachuoni wa Kiislamu juu ya kuharamisha jambo hilo.

2. Hadithi ya Abul-Hayyaaj aliyoipokea kwa Imam Ali [a], na zingine zinazofanana na hadithi hiyo.

Sasa hivi sisi tutazungumzia juu ya kujenga juu ya makaburi na kuyawekea paa na kusimamisha majengo kwenye makaburi hayo. Ama kuhusu suala la kuyazuru makaburi tutalizungumzia katika sehemu yake maalum "Mwenyezi Mungu apendapo".

Kwa munasaba wa lile suala la kwanza (kuwa kuna ijma'i ya wanachuoni wa Kiislamu kuharamisha kujengea makaburi) tutalizungumzia katika vipengele vitatui:

1. Je, nini mtazamo wa Qur'an katika kujenga juu ya makaburi, naje, katika Qur'an jambo hili limebainishwa wazi?

2. Je, ni kweli kwamba umma wa Kiislamu umeafikiana juu ya uharamu wa kujenga juu ya makaburi? Au kujenga huku kumekuwa kukiendelea kuwepo katika zama zote za Uislamu kuanzia wakati wa Mtume [s] na Masahaba?

3. Hadithi ya Abul-Hayyaaj inakusudia nini? Pia hadithi aliyopokea Jabir na Ummu Salamah na Na'im? Hadithi hizi ambazo Mawahabi wanatolea kama ushahidi wa mambo yao maovu.

A: MTAZAMO WA QUR'AN KATIKA KUJENGA JUU YA MAKABURI

Qur'an haikuweka wazi hukumu ya kujenga juu ya makaburi; isipokuwa inawezekana kuifahamu hukumu yake kwa kupitia baadhi ya aya tukufu ambazo zimelizungumzia jambo hili kiujumla.

Hebu fuatilia ufafanuzi ufuatao:

1). KUJENGA JUU YA MAKABURI YA MAWALII NA KUVIHESHIMU VITU VITUKUFU VYA MWENYEZI MUNGU

Hakika Qur'an Tukufu inakichukulia kitendo cha kuheshimu mambo matukufu ya Mwenyezi Mungu kuwa ni dalili ya ucha Mungu (Utawa).

Mwenyezi Mungu anasema: "Na ye yote anayeziheshimu alama za Mwenyezi Mungu, basi kufanya hivyo ni miongoni mwa uchaji wa moyo." (Qur'an, 22:32).

Sasa tunajiuliza: Nini maana ya "taadhim sha'airillah?"

Jawabu: "Sha'air" ni tamko la uwingi na umoja wake ni "Sha'irah", nalo lina maana ya dalili na alama, na wala haikuwa makusudio ya "Sha'air" katika aya hii kuwa ni alama zinazothibitisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, kwani ulimwengu wote ni dalili ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu.

Mshairi mmoja anasema:

"Katika kila kita kuna dalili inayojulisha kwamba Mwenyezi Mungu ni mmoja."

Kama ambavyo ni vema ifahamike kwamba hakuna ye yote anayesema kuwa, "kukiheshimu kila kita kilichoko ulimwenguni ni dalili ya ucha Mungu"; bali makusudio ni kuziheshimu dalili (alama) za dini ya Mwenyezi Mungu.

Na maana hii ndiyo ambayo waisemayo wafasiri wa Qur'an katika aya hii kwamba, neno "Sha'airullah", maana yake ni vitambulisho vya dini ya Mwenyezi Mungu.

Na iwapo "safa" na "Marwah" na pia ngamia anayepelekwa Mina kwa ajili ya kuchinjwa ni miongoni mwa alama za dini ya Mwenyezi Mungu, basi siyo kwa sababu nyingine bali ni kwa kuwa ni vitambulisho vya dini tukufu na mpenzi wa Mwenyezi Mungu Nabii Ibrahim [a].

Na iwapo Muzdalifah huitwa "Mash'ar" hiyo ni kwa sababu ipo miongoni mwa alama za dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; na kwamba kusimama katika Mashar hiyo ni dalili za kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Vile vile Ibada za Hija zinapoitwa kuwa ni Sha'air; basi siyo kwa sababu nyingine isipokuwa ni kwa kuwa ni alama za tauhidi na za dini tukufu.

Kwa kifupi ni kwamba, kila kile ambacho ni kitambulisho cha dini ya Mwenyezi Mungu, kukiheshimu ni katika mambo yanayomsogeza mtu katika ucha Mungu.

Hivyo basi hakuna shaka kwamba Manabii na Mawalii wa Mwenyezi Mungu, wao ndiyo alama kubwa zaidi miongoni mwa alama za dini ya Mwenyezi Mungu, kwani wao walikuwa ndiyo njia bora ya kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kuueneza miongoni mwa watu.

Hakika miongoni mwa mambo yenye kuthibiti kwa kila mtu aliyemuadilifu ni kwamba, kuwepo kwa Mtume [s] na Maimamu watukufa [a] ni katika alama na vitambulisho vya dini hii tukufu, kwa hiyo kuwaheshimu wao ni kumtukuza Mwenyezi Mungu, na ndiyo alama ya ucha Mungu.

Na hapana shaka kwamba, kuhifadhi kumbukumbu zao na kuyahifadhi makaburi yao yasiondolewe, ni moja katika aina ya kuviheshimu vitambulisho vya dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Na kwa maneno mengine, tunaweza kufahamu umihimu wa kuheshimu makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu kwa kupitia nukta mbili zifuatazo:

Kwanza: Mawalii wa Mwenyezi Mungu hasa wale ambao waliuawa kwa ajili ya kueneza dini, wao ni vitambulisho vya Mwenyezi Mungu na ni alama za dini yake.

Pili: Kujenga juu ya makaburi yao ili kudumisha utajo wao na kuishi kwa kufuata mwenendo wao wa haki ni aina ya kuonyesha kuwaheshimu na kuwatukuza.

Kwa msingi huu basi, ndiyo maana tunaona mataifa yote ulimwenguni yanatenga maeneo maalum kwa ajili ya makaburi ya watu wao mashuhuri wa kidini na kisiasa, ili kuzibakisha kumbukumbu zao zidumu kwa ajili ya wafuasi wao milele. Kwa hiyo inakuwa kana kwamba kuyahifadhi makaburi yao yasitoweke na kuharibiwa ni katika jumla ya kudumisha kumbukumbu zao na kuendelea kuwepo kwa fikra zao na miongozo yao.

Ili kuufahamu vyema ukweli huu, hapana budi tuifanyie mazingatio aya ya 36 katika Surah Al-Haj:

"Na ngamia, ngombe, mbuzi na kondoo (muwachinjao) tumekufanyieni kuwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu".

Baadhi ya Mahujaji wa Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu walikuwa wakienda hija pamoja na ngamia wao kutoka katika miji yao ili wanyama hao wapelekwe iliko Al-Kaaba - kwa madhumuni ya kuwachinja karibu na nyumba ya Mwenyezi Mungu, pia walikuwa wakiwavalisha makoja shingoni mwao ikiwa ni alama ya kutambulisha kwamba, mnyama huyo atapelekwa Makka kwa ajili ya kuchinjwa. Basi mnyama huyo huwa amewekwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hawezi kuuzwa wala kununuliwa; na kitambulisho chake katika kundi la ngamia wengine hi huko kuvalishwa hilo koja. Kwa sababu hii basi, Mwenyezi Mungu amemzingatia mnyama wa aina hii kuwa ni miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu.

Na kwa ajili hii, Uislamu umetoa hukumu ya kumheshimu mnyama huyu; hivyo basi haifai kumpanda; na ni wajibu kumkamilishia mahitaji ya chakula na kinywaji mpaka wakati wa kuchinjwa hapo karibu na Al-Kaaba.

Sasa basi, ikiwa ngamia huyu anapata heshima hii na utukufu huu kwa sababu tu amekuwa miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi utasemaje juu ya Manabii na Maimamu watukufu?

Je, Manabii na Maimamu watukufu [a] pamoja na wanachuoni na mashahidi ambao walivaa makoja ya utuinwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tangu hapo mwanzo, na walijitoa muhanga nafsi zao kuitumikia dini ya Mwenyezi Mungu, pia wakawa ni

wawakilishi wa Mwenyezi Mungu katika kuwaongoza na kuwaongoza viumbe wake; basi kwa yote haya hawatazingatiwa kuwa ni miongoni mwa vitambulishovya dini ya Mwenyezi Mungu?

Je, hivi siyo jambo la wajibu kuwatukuza na kuwapa heshima inayowastahiki wakiwa hai na baada ya kufa kwao?

Ikiwa Al-Kaaba, Safa na Marwah, Mina na Arafat (vitu ambavyo havina uhai, na ni mchanganyiko wa udongo na mawe tu vinazingatiwa kuwa ni alama za Mwenyezi Mungu, na vinastahiki heshima na utukufu unaonasibiana navyo kwa sababu tu ya kuwepo mafungamano ya vitu hivyo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi kwa nini Mawalii wa Mwenyezi Mungu ambao wao ndiyo watetezi wa dini ya Mwenyezi Mungu na walizieneza shari'ah zake wasiwe ni miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu?

Basi sisi tunawataka Mawahabi waamue wenyewe kuhusu jambo hili, na tunawauliza maswali yafuatyo:

Je, mnayo mashaka yoyote au wasiwasi wowote kwamba Manabii na Mtume ni miongoni mwa alama za dini ya Mwenyezi Mungu? Je, nafsi zenu hazioni umuhimu na kuwatukuza na kudumisha utajo wao na kushikamana na mafundisho yao?

Se, kujenga juu ya makaburi yao na kuvisafisha viwanja yalipo makaburi yao ni kuwatukuza na kuwaheshimu? Au kuyabomoa makaburi yao na kuvipuuza bila kuvisafisha viwanja walipozikwa na kuvitelekeza ndiyo kuwatukuza?!

2. KUWAPENDA AL-QURBAA

Kwa hakika Qur'an inatuamuru wazi wazi kuwapenda jamaa wa Mtume [s] na kushirikiana nao vizuri, na inasema:

"Waambie (ewe Mtume Wetu) sikuombeni malipo yoyote (katika kazi hii) isipokuwa muwapende jamaa (zangu), (42:23).

Kitu kinachoonekana wazi kwa ye yote yule ambaye Mwenyezi Mungu amemsemesha kwa usemi uliyomo katika aya hii ni kwamba, kujenga juu ya makaburi ya watu wa nyumba ya Mtume [s] ni moja katika aina za kuonyesha upendo kwao.

Desturi hii (ya kujenga juu ya makaburi ya viongozi) ni yenye kufuatwa na mataifa yote katika ulimwengu, na wote wanaizingatia hali hii kuwa ni namna mojawapo ya upendo kwa huyo aliyezikwa kwenye kaburi hilo; na ndiyo maana utaona wanawazika viongozi wao wakubwa wa kisiasa na utaalamu mbali mbali katika makanisa na sehemu mashuhuri za kuzikia, na kisha wakapanda pembeni ya makaburi hayo aina tofauti za maua na miti.

3. KUJENGEA MAKABURI KATIKA NYUMATI LILIZOPITA

 

Baadhi ya aya tukufa za Qur'an zinatufahamisha kwamba, kuyaheshimu makaburi ya waumini ni jambo ambalo lilikuwa limeenea miongoni mwa nyumati zilizotangulia kabla Uislamu haujadhihiri. Kwa mfano, zilipokuwa zimeenea habari za As-habul-kahfi (Watu wa Pangoni) miongoni mwa watu, na watu hao wakaenda kwenye hilo pango ili wakawaone hao As-habul Kahfi wenyewe, ilitokea tofauti na mabishano juu ya mahala pa maziko yao hao As-habul-Kahfi, na watu wakagawanyika makundi mawili.

Kundi moja likasema: Jengeni jengo juu yao".

Na kundi la pili likasema: "Bila shaka tutajenga Msikiti juu yao"

Hapa utaona kwamba Qur'an Tukufu inatutajia rai hizi mbili bila ya kuzikosoa; kwa hali hiyo basi inawezekana kusema kwamba lau rai hizi mbili zingekuwa hazifai, bila shaka Qur'an ingezikosoa au ingesimulia kisa cha semi mbili hizi kwa kuzipinga na kuzikemea.

Wafasiri wa Qur'an wanasema: "Mzozo kuhusu mahali walipozikwa As-habul-Kahfi, ulitokea baina ya waumini na makafiri ama makafiri wao walisema: "Jengeni jengo juu yao", na waumini nao walisema: "Tutajenga msikiti juu yao."

Ushindi waliupata waumini, kwani Mwenyezi Mungu anasema: "Wakasema wale walioshinda katika shauri lao, bila shaka tutajenga msikiti juu yao". (Qur'an, 18:21).

Msikiti ulijengwa na makaburi ya As-habul-Kahfi yakawa ni mahali panapotukuzwa na kuheshimiwa.

Hali hii inatuonyesha kwamba lengo Ia kujenga juu ya makaburi ya hao As-habul-Kahfi halikuwa jingine isipokuwa ni kuonyesha namna ya kuwatukuza Mawalii wa Mwenyezi Mungu.

Ewe msomaji mpendwa, baada ya aya tatu za Qur'an zilizotangulia hapo kabla, ni dhahiri haiwezekani kuharamisha kujengea juu ya makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu, wala hakuna karaha ya kutenda hilo kwa namna ye yote ile, isipokuwa kinachowezekana ni kulizingatia tendo la kujengea juu ya makaburi kuwa ni katika namna ya kuviheshimu vitambulisho vya dini ya Mwenyezi Mungu, na kwa kufanya hivyo ni katika kuonyesha wazi upendo wa jamaa ya Mtume [s].

4. RUHUSA YA NYUMBA MAALUM

Bila shaka Mwenyezi Mungu ametoa ruhusa ya nyumba ambazo ndani yake litatajwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mwenyezi Mungu akasema: "Katika nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha litajwe humo jina lake, humtukuza humo asubuhi na jioni watu ambao hawashughulishwi na biashara ya kuuza na kununua (wakasahau) kumkumbuka Mwenyezi Mungu (Qur'an, 24:36-37).

Katika aya hizi, ushahidi wa kufaa kujenga juu ya makaburi utakamilika kwa kubainisha mambo mawili:

La kwanza: Nini makusudio ya neno Al-Buyut (nyumba) lililomo katika aya?

La pili: Nini makusudio ya neno Ar-Raf'u pia lililoko katika aya?

Kuhusu lile neno la kwanza, kinachokusudiwa katika neno "Al-Buyut" siyo Misikiti peke yake, isipokuwa muradi wake ni misikiti na sehemu ambazo hutajwa katika sehemu hizo jina Ia Mwenyezi Mungu, sawa sawa ikiwa ni misikiti au isiwe misikiti, kama vile nyumba za Manabii na Maimamu [a] na wacha Mungu ambao haiwashughulishi biashara ya kuuza na kununua kiasi cha kuwasahaulisha kumkumbuka Mwenyezi Mungu.

Basi nyumba hizi zitazingatiwa kuwa ni miongoni mwa makusudio yanayojitokeza katika aya hiyo tukufu. Bali inawezekana kabisa kusema kwamba makusudio ya "Al-Buyuut" siyo Misikiti, kwa sababu "Al-Bait" kwa maana ya nyumba, ni jengo ambalo Iimejengwa kwa kuta nne na juu yake kuna paa.

Sasa basi ikiwa Al-Kaaba inaitwa kuwa ni nyumba ya Mwenyezi Mungu (Baitullahi), hakuna kinachosababisha iitwe hivyo ila ni kwa kuwa inalo paa.

Qur'an kwa upande wake, inazingatia neno "Al-Bait" kwa maana ya nyumba yenye paa.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

"Na isingekuwa watu watakuwa kundi moja, bila shaka tungeliwafanyia wanaomkufuru (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa Rehema, majumba yao kuwa ni yenye mapaa ya fedha".....

(Qur'an, 43:44).

Kinachofahamika katika aya hii ni kwamba nyumba "Al-Bait" huwa haiepukani na paa. Na kwa kisheria inapendekezwa Misikiti isiwe na paa na ndiyo maana unanona msikiti Mtukufu wa Makka kwa juu uko wazi haukufunikwa na paa.

Na kwa hali yoyote ile, makusudio ya "Al-Buyuut" ima yatakuwa na maana zaidi ya ile manna ya misikiti au manna yake isikusudie misikiti.

Maelezo yaliyotangulia hivi punde yamelihusu lile jambo la kwanza yaani nini makusudio ya neno "Al-Buyuut".

Na ama lile la pili ambalo ni maana ya (Ar-Raf'u), hili linawezekana kuwa na manna mbili.

Maana ya kwanza: Ni kuwa makusudio ya neno "Ar-Raf'u" (kuinua) ni kwa ile maana ya kimaada inayoonekana wazi wazi,

maana ambayo huthibitika kwa kuweka msingi (wa jengo) na kusimamisha kuta na hatimaye jengo lenyewe kusimama kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

Na (kumbukeni pale) Jbrahimu alipoziinua kuta za nyumba na Isma'il.

(Qur'an, 2:127).

Maana ya pili: Ni kuwa makusudio ya neno "Ar-Raf'u" ni kimaana (na wala siyo ya kimaada) kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na tulimuinua daraja ya juu kabisa, maana yake ni kuwa "Tulimpa daraja ya juu kabisa".

Iwapo makusudio ya Ar-Raf'u yatakuwa ni kwa ile maana ya kwanza, basi itakuwa inajulisha wazi kabisa kwamba inafaa kuyajenga na kuyaimarisha majumba ya Manabii na Mawalii wa Mwenyezi Mungu, katika zama za uhai wao na baada ya kufa kwao.

Na ni jambo linaloeleweka kwamba mahali alipozikwa Mtume [s] na mahali walimozikwa wengi wa Maimamu watukufu na Mawalii wa Mwenyezi Mungu ni katika majumba yao.

Hivyo basi, kuyajenga majumba haya na kuyahifadhi yasiharibiwe na kuondoka alama zake ni tendo linalofaa kwa mujibu wa nassi ya aya tukufu ya Qur'an; na zaidi ya hapo ni jambo lililopendekezwa litendwe.

Na kama muradi wake neno Ar-Raf'u itakuwa ni ile ya kimaana tu yaani kutukuza (kuinua daraja, cheo) matokeo yake yatakuwa ni kupatikana ruhusa ya kuyaheshimu na kuyatakuza majumba hayo na kuyahifadhi na kuyaepusha kutokana na kila kile ambacho hakistahiki heshima yake.

Na kwa hali yoyote, ile ruhusa iliyopo katika maana ya neno Ar-Raf'u, sawasawa kama itakuwa ni ile ya kimaada au ni ile ya kimaana tu, basi itakuwa haikupatikana ila kwa sababu ya kuwepo katika mahali hapo watu wema, ambao humtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu asubuhi na jioni.

Baada ya kuitaja aya hii na aya nyingine zinazofanana na hii, basi itakuwaje Mawahabi waone kuwa inafaa kuyabomoa majumba waliyokuwamo kizazi cha Mtume [s], majumba ambayo yalikuwa ni mahala ambapo Malaika wa Mwenyezi Mungu walikuwa wakishuka na pia yalikuwa ni vituo vya kumtaja Mwenyezi Mungu na kueneza dini yake na hukumu zake?

Vipi itakuwa inafaa kwa Mawahabi kubomoa makaburi matukufu ambayo ndiyo mahala pa (kuonyesha) upendo wa nyoyo za mamilioni ya waumini ambao walikuwa wakiyazuru - wake kwa waume, asubuhi na jioni, na walikuwa wakimtaja Mwenyezi Mungu katika majumba hayo, kwa kuswali, kuomba na kumtakasa?

Kwa nini basi Mawahabi wamefanya jeuri kwa kuyadharau majumba haya na kuyadhalilisha na kuyapuuza? Kwa nini wameyageuza yakawa hi mahala palipotengwa na kubaki pweke. Nyoyo za waumini wote huomboleza na kuhuzunika kutokana na kuyadharau na kuyadhalilisha majumba haya.

Kwa nini? Tena kwa nini?

Amepokea Al-Hafiz As-Suyuti kutoka kwa Anas ibn Malik na Buraidah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu [s] aliisoma kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu (isemayo) "Katika majumba ambayo Mwenyezi Mungu ameamrisha zijengwe....." Basi alisimama mtu fulani akasema: "Ni nyumba gani hizi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?"

Mtume [s] akasema: "Ni nyumba za Mitume."

Basi Abubakar akasimama na akasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, na nyumba hii ni miongoni mwa hizo?" Na aliashiria nyumba ya Ali na Fatma [a].

Mtume [s] akasema: "Ndiyo; nayo ni bora mno kuliko zingine".

B: UMMA WA KIISLAMU NA KUJENGA JUU YA MAKABURI

Uislamu ulipokuwa umeenea katika bara Arabu, na nuru yake ikaenea katika sehemu kubwa ya mashariki ya kati, makaburi ya Manabii yaliyokuwa yakifahamika yalikuwa yamejengewa na kuwekwa mapaa yaliyoyafunika.

Baadhi ya makaburi hayo yalikuwa yana Maquba imara na kuna madharih mazuri, na baadhi yake yapo mpaka leo.

Katika mji wa Makka yenyewe utaliona kaburi la Nabii Isma'il na mama yake, Hajirah, yapo katika mahala panapojulikana kama "Hijri Isma'il".

Na kadhalika Kaburi Ia Nabii Daniel liko katika mji wa Shush nchini Iran. Na makaburi ya Manabii Hud, Saleh, Yunus, Dhulkifl [a] yako nchini Iraq.

Vile vile kaburi la Nabii Ibrahim na makaburi ya wanawe kina Ishaq; Ya'qub na Yusuf [a] yako huko Baitul-Muqaddas (Jerusalem).

Na hapo kabla makaburi haya ya wana wa Ibrahim [a] yalikuwa Misri, na baadaye Nabii Musa [a] akaihamishia miili yao mitukufu huko Quds kwa amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na mpaka leo makaburi hayo bado yapo, na kila kaburi limejengwa imara na linajulikana wazi.

Na kaburi la mama Hawa (mama wa wanaadamu) liko katika mji wa Jeddah ndani ya nchi ya Hijazi, kwa mujibu wa kauli iliyo mashuhuri; na umeitwa hivyo mji huu kutokana na kuwepo kwa kaburi la mama Hawa katika sehemu hiyo.

Kaburi hili Ia mama Hawa hapo mwanzo alama zake zilikuwa zikionekana, lakini Mawahabi walipokwisha kuikalia nchi ya Hijazi waliziondosha alama zake na kufuta kabisa athari zake.

Makaburi yote haya tuliyoyataja yaliendelea kuwepo hata baada ya Waislamu kuiteka miji hiyo na waliyaona, lakini pamoja na hali hiyo hawakutenda tendo lolote la kupinga kuwepo kwa makaburi hayo na wala hawakuamrisha yabomolewe au kuharibiwa.

Basi lau ingekuwa kujenga juu ya makaburi na kuwazika wafu katika makaburi yaliyojengwa na kuwekewa mapaa ni jambo lililoharamishwa katika Uislamu, lingekuwa ni jambo la lazima kwa Waislamu hao kabla ya kufanya chochote wayabomoe makaburi hayo ambayo yapo mpaka leo katika sehemu mbali mbali nchini Iraq, Jordan na Palestina.

Pia Waislamu hao wangezuia kujengwa upya makaburi hayo kila yanapoharibika muda wote. Lakini tunachokiona ni kuwa, Waislamu hao hawakuamuru yabomolewe, bali waliendelea kuyaimarisha na kuyahifadhi muda wote wa kipindi cha karne kumi na nne.

Kwa hakika walikuwa wakifahamu kwa kupitia ufunuo wa kiakili kwamba, kuzilinda kumbukumbu za Manabii na kuzihifadhi ni miongoni mwa kuwaheshimu Manabii hao, na kwamba jambo hilo huwakuru - bisha kwa Mwenyezi Mungu na linawapatia malipo mema.

Ibn Taimiyya anasema ndani ya kitabu chake kiitwacho, As-siratul-Mustaqiim: "Quds ilipokuwa imeingia mikononi mwa Waislamu, makaburi ya Manabii yalikuwa yamo ndani ya majengo, lakini milango ya majengo hayo ilikuwa imefungwa mpaka katika karne ya nne Hijriyya."[30]

Kwa hiyo basi, lau kujengea makaburi ingekuwa ni haramu, pasingekuwa na sababu yoyote ya kuyaacha makaburi hayo kama yalivyokuwa na huku milango yake imefungwa; isipokuwa ingekuwa ni jambo la wajibu kuyabomoa mara moja, (Hata kama tukichukuwa usemi wa Ibn Taimiyya kwamba milango yake ilikuwa imefungwa mpaka karne ya nne, lakini kauli hii haina uthibitisho.)

Kwa kifupi kuyabakisha majengo hayo na Maquba yaliyojengewa kwenye makaburi muda wote huu mbele ya macho ya wanachuoni na mafaqihi wa Kiislamu, ni dalili iliyo wazi ya ruhusa ya kuyajengea makaburi katika dini ya Kiislamu.

KUMBUKUMBU ZA KIISLAMU NI DALILI YA KUENDELEZA DINI

Hapana shaka kwamba kuhifadhi kumbukumbu za Manabii na hasa zile za Nabii Muhammad [s] pamoja na kaburi Ia Mtume [s] na makaburi ya wakeze, wanawe na masahaba wake, na vile vile nyumba walizokuwa wakiishi na misikiti walimokuwa wakisali, hapana shaka kabisa kwamba mambo haya yanazo faida nyingi na yanayo matokeo mazuri.

Tunataja baadhi ya faida hizo kama ifuatavyo:

Leo hii baada ya kupita karne ishirini tangu kuzaliwa Nabii 'Isa [a] yeye na mama yake na kitabu chake cha Injili pamoja na wale wafuasi wake maalum (Hawaariyyuun) kwa mtazamo wa watu wa magharibi wamegeuka kuwa kama masimulizi yasiyo na ukweli, na baadhi ya wataalamu wanatia shaka hata kuwa je, alikuwako mtu aitwaye Masih 'Isa au mama yake aitwaye Mariyam, au kitabu chake kiitwacho lnjili. Na habari za Nabii 'Isa [a] wanazichukulia kuwa ni mazungumzo tu yasiyo na ukweli na kwamba yanafanana na ngano za Laila Majnuun.

Basi kwa nini imekuwa hivyo?

Hii ni kwa sababu hakuna athari yoyote inayoonekana kuhusu Nabii 'Isa [a].

Kwa mfano: Haifahamiki kabisa ni mahali gani Nabii 'Isa [a] alipozaliwa; na iko sehemu gani nyumba aliyokuwa akiishi, na hi mahali gani alipozikwa? (Kwa mujibu wa madai ya Wakristo kuwa Nabii 'Isa [a] aliuawa).

Kwa upande wa kitabu chake kilichoteremshwa toka mbinguni, kitabu hiki kimeingiliwa na mikono ya watu waliokigeuza na kukibadilisha na kuzua mambo mbalimbali.

Na hizi Injili nne zilizomo mikononi mwa watu hazina uhusiano wowote na Nabii 'Isa [a], na wala siyo ile Injili yake; bali hizo ni Injili za kina Matayo, Yohana, Marko na Luka.

Ndiyo maana basi, utaviona mwishoni mwake vinataja kisa cha kuuawa kwa Nabii 'Isa [a] na kuzikwa kwake.

Basi ukweli halisi ulivyo ni kuwa, lnjili hizo zimeandikwa baada ya Nabii 'Isa [a] kutoweka. Na kwa msingi huu basi wengi wa watafiti na wachunguzi wanaitakidi kwamba, Injili hizi nne ni miongoni mwa vitabu vya mafunzo tu ambayo historia yake inaanzia karnye ya pili ya masihiya.

Na lau kama vingekuwepo vitu muhimu vinavyomuhusu Nabii Isa [a] vimehifadhiwa, vingelikuwa ndiyo dalili madhubuti ya kuthibitisha kuwepo kwake, na maisha yake yalivyokuwa; na pia vingeonyesha utukufu wake, na wala kusingekuwa na nafasi ya kuzusha mashaka na maswali mengi toka kwa wataalam wenye mawazo potofu.

Ama kwa upande wa Waislamu, wao wanaukabili ulimwengu bila ya hofu na wanasema: "Enyi watu, kwa hakika kuna mtu kutoka katika ardhi ya Hijazi aliyetumwa kuja kuiongoza jamii ya wanadamu tangu miaka elfu moja na mia nne iliyopita, na ameuthibitisha ushindi wenye mafanikio katika jambo lake hilo (la dini) na hizi hapa kumbukumbu za maisha yake zimehifadhiwa kikamilifu katika miji ya Makka na Madina".

Wanaendelea kusema: "Hii hapa ndiyo nyumba alimozaliwa na hili hapa ni pango la Hiraa mahala ambapo Wahyi na ufunuo vilimshukia, na huu ndiyo Msikiti wake ambamo alikuwa akisalisha ndani yake, na hii hapa ndiyo nyumba alimozikwa na hizi ni nyumba za wanawe, wakeze, na jamaa zake, na makaburi haya ni ya kizazi chake na mawasii wake [a]."

Sasa basi, iwapo sisi tutaziondosha kumbukumbu hizi zinazojulisha kuwa Mtume [s] alikuweko, na takaondosha dalili zinazoashiria utukufu wake na ukweli wake, tutakuwa tayari tumeandaa njia kwa maadui wa UisIamu waseme yale wayatakayo dhidi yetu na Uislamu wetu.

Kwa hakika kubomoa kumbukumbu za Mtume [s] na zile za watu watukufu wa nyumba yake, siyo tu ni kuwakosea wao na kuvunja heshima yao, bali ni kufanya uadui dhahiri dhidi ya Utume wenyewe kwa nafsi yake na Mtume [s] mwenyewe na vitambulisho vya dini aliyokuja nayo.

Ujumbe wa dini ya Kiislamu ni ujumbe wa kudumu milele; na Uislamu utaendelea kuwa ndiyo dini pekee inayowafaa wanaadamu mpaka siku ya Kiyama; na vizazi vijavyo havina budi kukiri ukweli wake na kuamini utukufu wa ujumbe huu.

Na ili litimie lengo hili, ni lazima kuzihifadhi kumbukumbu za Mtume [s] ili tupige hatua mbele katika njia za kuendeleza dini hii na kuifanya ibakie milele kiasi ambacho asiwe na shaka mtu ye yote juu ya kuwepo kwa Nabii wa Uislamu [s] kama ambavyo watu wamefanya shaka kuhusu kuweko kwa Nabii 'Isa [a] (kutokana na kupotea kwa kumbukumbu zake).

Waislamu (kwa upande wao) wamelipatia umuhimu mkubwa jambo la uwekaji kumbukumbu za Nabii Muhammad [s] ikiwemo sera zake na mwenendo wake kiasi kwamba wameyasajili katika historia mambo yake madogo madogo yanayohusiana na maisha yake na athari zake za kipekee.

Wameandika pia maelezo yanayohusu pete yake na viatu vyake, mswaki wake na upanga wake, deraya yake, mkuki wake na farasi wake, ngamia wake na hata mtumishi wake na mpaka wameandika visima alivyokunywa maji na ardhi aliyoitoa wakfu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

(Waislamu) wameandika pia aina ya chakula ambacho Mtume [s] alikuwa akikipenda na zaidi ya hayo wameandika hata namna ya kutembea kwake na kula kwake na kunywa kwake na pia namna ya ndevu zake zilivyokuwa na alivyokuwa akizipaka hina na mengineyo. Na baadhi yakumbukumbu hizo bado zimebakia mpaka katika siku zetu hizi.[31]

Na kila inaporejewa historia ya Uislamu na kuichunguza hali ya miji ya Kiislamu na kumbukumbu zilizomo, inadhihirika wazi kabisa kwamba, kujenga juu ya makaburi ili kuyahifadhi yasitoweke ni jambo lililokuwa likifanyika kwa Waislamu wote katika sehemu mbali mbali za miji mikubwa ya Kiislamu, na mpaka sasa yako madhariha yaliyowekwa kwenye makaburi ya Manabii na ya watu wachamungu kiasi kwamba Waislamu wanakwenda kufanya ziyara kwenye sehemu hizo na kuomba dua.

Na Makaburi hayo yanahesabiwa (kuwa ni miongoni mwa kumbukumbu za kihistoria za Kiislamu.

Vile vile katika sehemu hizo kuna waqfu nyingi zilizowekwa ambazo kipato chake hutumika katika kuimarisha hifadhi ya kumbukumbu hizo na kusafisha mazingira yake na mengineyo.

Ukweli ulivyo ni kwamba makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu yalikuwa yamejengewa hata katika nchi ya Hijazi yenyewe, na kabla fitana hii ya Mawahabi haijaingia na kuikalia Haram ya Makka na Madina pamoja na pembezoni mwake, kulikuwa na makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu katika kila upande wa nchi ya Hijazi yamejengewa yakipata hadhi kutokana na kupewa heshima na Waislamu wote, na wala hapakuweko mwanachuoni yeyote aliyekemea kubakia kwa makaburi hayo au aliyepinga kujenga juu yake.

Wala siyo kwamba nchi ya Iran peke yake ndiyo ambayo kunapatikana makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu yaliyojengewa juu yake, bali hali hii imeenea katika nchi za Kiislamu, hasa hasa Misri, Syria, Iraq, Morocco, Tunisia na Jordan.

Katika miji hiyo kuna makaburi ya wanachuoni wakubwa wa Kiislamu yamejengewa, na Waislamu wanayatembelea kwa wingi na kusoma Qur'an wafikapo hapo, hasa Surah al-Fatiha na kumuomba Mwenyezi Mungu azipeleke thawabu za kisomo chao kwa roho za walioko kwenye makaburi hayo.

Vile vile kwenye makaburi hayo wapo wafanyakazi wanaosimamia ulinzi, huduma, usafi na hifadhi ya sehemu hizo.

Baada ya maelezo yaliyotangulia, itakuwaje ni haramu kuyajengea makaburi wakati desturi iliyokuwa ikifuatwa tangu mwanzo wa kuja Uislamu hadi leo inaendelea kutumika kitu ambacho wanachuoni wanakiita kuwa ndiyo sera ya Waislamu ambayo mizizi yake inakwenda hadi kuzifikia zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu, au zama za Maimamu watukufu wa nyumba ya Mtume [s].

Kwa hakika sera hii imesimama kwenye msingi wa ruhusa ya kujenga juu ya makaburi; bali inathibitisha umuhimu na kupendekezwa kwa jambo hili; na halikupata kupingwa na upinzani wa aina yoyote muda wote wa kuwepo kwake kitu ambacho kinaonyesha kuwa linayo asili kwa Waislamu na linafaa wakati wote, na kwamba limekuwa katika sunna zenye kufuatwa kwa Waislamu.

Mwandishi mmoja wa Kiwahabi anakiri uasili wa jambo hili alipoandika akasema:

"Jambo hili limeenea katika miji na limeenea ulimwenguni mashariki na magharibi kiasi kwamba hapana mji katika miji ya Kiislamu isipokuwa yamo makaburi na maziyara, zaidi ya hapo misikiti mingi haikosi kuwa na kaburi na ziyara; na wala haingii katika akili ya mtu kabisa kwamba jambo hili ni baya, kiasi cha ubaya nilioutaja, na kisha wanachuoni wa Kiislamu wanyamaze kimya."[32]

Ni ajabu kwamba mwandishi huyu wa Kiwahabi anakiri kuwa sera ya Waislamu inao msimamo wa kujenga juu ya makaburi ya watu wacha Mungu na kuyatukuza, lakini utamuona kuwa hakuacha uovu wake na dhamira yake mbaya, na utamuona analiona jambo hili kuwa ni baya na anawalaumu wanachuoni kwa kukaa kwao kimya na anadai kwamba kimya cha wanachuoni hao wa kale kwa muda mrefu hakiwazuwii wanachuoni wa zama hizi kulikemea jambo hilo.

Lakini jibu lake liko wazi mno. Basi ni vipi wanachuoni wanyamaze muda wote wa karne saba wasitamke chochote?

Je, wote hawa katika karne hizo zilizopita walikuwa wakilinyamazia jambo baya na wakijizuwiya kulikataza kama anavyodai Wahabi huyu?

Katika zama za Khalifa Omar bin Khattab Waislamu walipoiteka Bait-al-Muqaddas, ni kwa nini Omar hakuamrisha makaburi ya Manabii yaliyoko hapo yabomolewe? Basi je, enyi Mawahabi mwamuona Omar kwamba ni mwenye kukubaliana na washirikina?

JAWABU LA WANACHUONI WA MADINA

Jambo la ajabu katika maudhui haya ya kujenga juu ya makaburi ni lile jawabu linalonasibishwa kuwa limetoka kwa wanachuoni wa Madina, waliposema:

"Ama kujenga juu ya makaburi, ni jambo Iililokatazwa kwa ijma'i, na hii ni kutokana na hadithi sahihi zilizokuja kuzuwiya jambo hili, na kwa ajili hii wametoa fatwa wanachuoni wengi kuwa ni wajibu kuyabomoa".

Lakini ni vipi madai ya Ijma'i yatasihi katika kuharamisha kujenga juu ya makaburi, wakati VVaislamu walimzika Mtume [s] katika nyumba aliyokuwa akikaa Bibi Aisha kisha baadaye wakawazika katika nyumba hiyo hiyo Abubakar na Omar; tena karibu kabisa na Mtume kwa nia ya kupata baraka, na hatimaye walijenga ukuta uliotenganisha, sehemu moja ikawa ni makazi ya Bibi Aisha na sehemu nyingine ikawa ni makaburi ya Mtume [s] na Abubakar na Omar.

Ilipokuwa ukuta huo wa kutenganisha sehemu hizo mbili ni mfupi, uliongezwa urefu katika zama za Abdallah bin Zubair, na kisha nyumba hii yenye makaburi haya ikawa hujengwa upya kila zama na karne zinavyopita kwa ujenzi wa kitaalam ulivyo katika kila zama.

Na katika wakati wa utawala wa Banu Ummaya na Banu Abbas ujenzi wa kaburi Ia Mtume [s] ulipewa umuhimu na heshima kubwa na uliendelea kujengwa upya kwa mujibu wa utaalamu uliokuwepo katika zama zile.

Jengo Ia mwisho lililojengewa kaburi tukufu la Mtume [s] ambalo mpaka leo lipo, ni lile lililojengwa wakati wa Sultan Abdul Hamid (wa Uturki) mwaka 1270 A.H. sawa na mwaka 1869 A.D., na ujenzi huu ulimalizika kwa muda wa miaka minne.

Ewe msomaji, unaweza kurejea kitabu kiitwacho Wafa'ul-wafa cha As-samhudi, kutoka ukurasa 383 hadi ukurasa 390 ili upate maelezo kwa urefu juu ya kujengewa kaburi la Mtume [s] na kufanywa upya na kuimarishwa ujenzi wake katika historia ya Uislamu mpaka kufikia zama za huyu As-samhudi katika vitabu vya historia ya mji wa Madina.

C. HADITHI YA ABUL-HAYYAJ

Hivi sasa umefika wakati wa kuichunguza hadithi wanayoitegemea Mawahabi kuharamisha kujenga juu ya makaburi. Kabla ya yote tunaitaja hadithi yenyewe kwa sanadi aliyoipokea Muslim katika kitabu chake.

"Ametusimulia Yahya ibn Yahya, na Abubakar ibn Abi Shaiba na Zuhayr ibn Harb, Yahya ametusimulia; (na watu wawili wa mwisho wamesema): Ametusimulia Waki'i, amepokea kutoka kwa Sufyan, toka kwa Habib bin Abi Thabiti, naye kapokea kwa Abi Wa'il ambaye kapokea toka kwa Abil Hayyaj Al Asadi' amesema: "Ali ibn Abi Talib alimambia: Je, nikutume kwa jambo ambalo Mtume wa Mwenyezi Mungu alinituma kwamba, usiache sanamu yoyote ila uiondoshe wala kaburi lolote lile lililonyanyuka isipokuwa ulisawazishe".[33]

Hadithi hii Mawahabi wameifanya kuwa ndiyo dalili ya kuharamisha kujenga juu ya makaburi bila hata ya kufanya uchunguzi wowote kwa watu walioipokea na Sanadi yake.

KUIJADILI HADITHI

Kwa ujumla tunapotaka kutoa ushahidi kwa kutumia hadithi ili tutoe hukmu miongoni mwa hukmu za Mwenyezi Mungu, hapana budi hadithi hiyo itimize masharti haya mawili:

1) Kusihi kwa Sanadi: Hii ikiwa na maana kwamba, wapokezi na watu wahusikao kwenye hadithi yenyewe katika kila ngazi wawe ni waaminifu kiasi ambacho iwezekane kuwategemea katika maneno yao.

2) Ushahidi wa hadithi: Maana yake ni kwamba, matamko na sentensi zilizomo katika hadithi hiyo ziwe zimetimia katika kuelekeza makusudio yetu kwenye hadithi hiyo, kiasi waweze kuifahamu na wengine wanaofahamu vizuri lugha iliyomo katika hadithi hiyo, na wazifahamu pia kanuni zake kama tunavyozifahamu sisi na waweze kutoa matokeo tunayoweza kuyatoa.

Na kwa bahati nzuri, hadithi ya Abul-Hayyaj imekosa sharti zote mbili na hasa ile ya pili, kwani hakuna mahusiano yoyote kabisa ya kujenga juu ya makaburi katika hadithi hiyo.

UFAFANUZI WA MAMBO HAYA

(A) Ama upande wa Sanad, ndani ya hadithi hii wamo wapokezi ambao wanachuohi wa hadithi hawakuafikiana juu ya uaminifu wa wapokezi hao, tin hapa chini tunataja majina ya wapokezi waliomo katika hadithi hii ambao wanachuoni wa hadithi wamezikataa hadithi zao:

1) Waki'

2) Sufyan Ath-Thauri

3) Habib ibn Abi Thabit

4) Abu Wai'l Al-Asadi.

Wapokezi hawa wanne amewatia kasoro Al-Hafiz ibn Hajar Al-'Asqalani katika kitabu chake kiitwacho "Tahdhibut-Tahdhib, na amewataja kwa sifa ambazo zinaondoa uaminifu katika hadithi yao hii tuliyotaja hapo kabla na pia kwenye hadithi zao nyingine.

  1. Kwa upande wa huyu Waki' anapokea Al-Hafiz Al- 'Asqalani kutoka kwa Ahmad bin Hanbal (Imam wa Madhhebu ya Kihanbal) amesema: "Hakika Waki' amefanya makosa katika hadithi mia tano".[34]

    Anasema tena Al-'Asqalani akimnakili Muhammad bin Nasr Al-Marwazi "Waki' alikuwa akisimulia hadithi kwa mujibu wa maa'na yake' isitoshe hakuwa mtaalam wa lugha".[35]

  2. Na kwa upande wa "Sufyan At-Thauri" AI-'Asqalani anasema kwa kumnakili ibn Mubarak: "Sufyan alikuwa akisimulia hadithi, basi mimi nikafika kwake na yeye alikuwa anafanyia Tadlis hadithi hiyo (kufanya udanganyifu katika hadithi), basi aliponiona aliona haya (kwa tendo lake hilo).[36]
  3. Kitendo cha kudanganya katika hadithi kwa namna yo yote ile, kinajulisha kwamba yule msimulizi alikuwa hana tabia ya uadilifu na ukweli, kwa hiyo alikuwa akikifanya kitu kisicho cha kweli kionekane kuwa ni kweli, kama ilivyo maana ya tadlis katika lugha ya Kiarabu.

  4. Ama huyu "Habib ibn Abi Thabit", Al-Asqalani ameandika akimnakili Abu Habbani:
  5. "Kwa hakika Habib: Alikuwa mdanganyifu."[37]

    Na ameandika Al-Asqalani akimnakili Qat-tan: "Hakika Habib siyo mtu wa kufuatwa."

  6. Ama huyu Abu Wa'il, yeye alikuwa mpinzani wa Imam Ali [a] na ni miongoni mwa watu waliomfanyia uadui na kero Imam Ali [a].[38]

    Basi vipi atategemewa mtu kama huyo, wakati Mtume [s] amesema; "Ewe Ali, hatakupenda wewe isipokuwa mtu muumini, na hatakubughudhi isipokuwa mtu mnafiki".[39]

Na inafaa kusema kwamba mpokeaji wa hadithi ya Abul-Hayyaj hana hadithi hata moja katika sihahi zote sita isipokuwa hadithi hii tu tunayoizungumzia. Basi utasema nini kuhusu mtu ambaye hakusimulia ila Riwaya moja? Jambo hili kwa hakika linajulisha kwamba mtu huyu hakuwa mpokeaji wa hadithi, na kwa msingi huu basi kumtegemea katika hadithi yake ni jambo lenye mushkili.

Ewe msomaji mpendwa, hii ndiyo Sanad ya hadithi ya AbulHayyaj; na umefahamu udhaifu wa wapokezi wake, na kwamba wanachuoni wa hadithi hawakuafiki ukweli wa wapokezi hao.

Basi iwapo hadithi itakuwa imezungukwa na matatizo kama haya mengi haitawezekana kwa faqihi yeyote kuitegemea hadithi hiyo kwa ajili ya kufahamu hukmu ya shari'ah au kutoa fatwa.

Ama utambulisho wa hadithi hi, hautaepukana na matatizo licha ya ile Sanad yenyewe, kwani ile nukta muhimu wanayoitolea ushahidi Mawahabi ni hii ifuatayo:

"Walaa qabran mush-rifan illa Sawwaitahu".

Hapa ni lazima kutulia na kufanya mazingatio na uchunguzi kwenye maneno mawili:

1) Mushrifan

2) Sawwaitahu.

1. Tamko Al-Mushrif manna yake ni kitu kuwa juu na chenye

kunyanyuka.

Amesema katika Munjid:

Al-Mushrif minal-amakin: Al-aali Wal-mutilu ala Ghairih.

Maana yake: Mahali Mush-rif, ni pale palipo juu na pamejitokeza kuliko mahali pengine.

Naye mwenye Al-Qamus ambaye ni mpangaji bora wa utaratibu wa maana za matamko amesema:

"As-Sharaf: Al-Uluwu, Waminal-Ibili Sanaamuhu".

Yaani As-Sharafuni kuwa juu; na likitumika kwa ngamia maana yake ni nundu yake".

Kwa hiyo basi maana ya "Mushrif' ni kuwa kitu chenye muinuko (kutokeza); na hasa muinuko ulio katika umbile Ia nundu ya ngamia.

Basi hapa niwajibu pamoja na kuzirejea dalili na qarina, tufanye uchambuzi kuhusu nini lengo la neno "Al-Mush-rif" lililoko katika hadithi tunaoizimgumzia.

2. Tamko "Sawwaitahu" maana yake ni, kukifanya kitu kuwa sawa (kukisawazisha) na kurekebisha kiwe sawa sawa.

Sawwas-Shaia: Maana yake amekifanya kiwe sawasawa; husemwa: Nimesawazisha kitu kilichopinda kikasawazika, (Nimekitengeneza sawasawa).

Katika Qur'an tukufu kuna aya isemayo Al-ladhii Khalaqa Fasawwaa (Aliyeumba Akasawazisha).

Surah Al-Aalaa,aya ya 2.

Baada ya kuangalia maana ya maneno mawili tofuati, tunawajibika kufahamu nini makusudio ya maneno haya katika hadithi.

Kwa hakika hadithi hii ina mielekeo miwili, na ni lazima kuchagua mmojawapo kwa mujibu wa maana zitumikazo kwenye maneno haya pamoja na dalili nyingine.

MWELEKEO WA KWANZA

Ni kwamba Imam Ali [a] alimuamuru Abul-Hayyaj kuyabomoa makaburi yaliyoinuliwa na kuyasawazisha kabisa na ardhi.

Lakini mwelekeo huu ambao ndio wanaoushikilia Mawahabi haukubaliki kutokana na sababu nyingi.

Ya Kwanza: Neno "At-Taswiyya" katika lugha ya Kiarabu halikuja kwa manna ya kubomoa; na lau makusudio yake hapa ingekuwa ni kubomoa basi ilitakiwa hadithi hiyo isemwe hivi: "Wala Qabran Illa Sawwaitahu bil ardhi" Yaani "Wala (usiache) kaburi ila ulisawazishe na ardhi". Lakini hadithi haikuja namna hiyo.

Ya Pill: Lau kama makusudio katika hadithi yangekuwa ni kubomoa, basi ni kwa nini hakutoa fatwa mwanachuoni ye yote wa Kiislamu kuyabomoa? Zaidi ya hapo ni kwamba, kulisawazisha kaburi na ardhi ni kinyume cha sunna ya Kiislamu na mapendekezo ya kisheria; kwani inapendekezwa na sheria kaburi linyanyake kuliko ardhi, na hii ndiyo fatwa waliyoitowa mafaqihi wote wa Kiislamu kwamba kaburi liinuke kutoka katika ardhi kiasi cha shibri moja.

Katika kitabu cha Al-Fiqhu Alal-Madhaahibil-arba'ah (Fiqhi kwa mujibu wa madhehebu manne) kuna maelezo yafuatayo:

"Ni Sunna kuinua udongo juu ya kaburi kiasi cha shibri moja".[40]

Basi itapokuwa muelekeo huu wa kwanza haukubaliki itakuwa ni lazima kuifasiri hadithi hii kwa kutumia muelekeo wa pili ufuatao.

MUELEKO WA PILl

Makusudio ya neno "Tas-wiyatu l-Qabri" itakuwa ni kulisawazisha kaburi likawa sawa kwa sawa kinyume na makaburi ambayo hujengwa kwa umbile Ia samaki au nundu ya ngamia.

Kwa msingi huu hadithi itakuwa inakusudia kwamba, sehemu ya juu ya kaburi iwe imetandazwa sawa sawa, na haifai kuwa kama mgongo wa samaki au nundu ya ngamia, kama wafanyavyo baadhi ya Waislamu wa Madhehebu ya Kisunni. Maimamu wa Madhehebu ya Kisunni (isipokuwa Imam Shafi'i) wametoa fatwa kwamba inapendekezwa kulifanya kaburi kama nundu.[41]

Na kwa ajili hii basi hadithi hii inathibitisha ukweli wa fatwa ya wanachuoni wa Kishia na Kishafi'i ambao wanasema kwamba, "Inapasa kulisawazisha kaburi na kuliinua kuliko ardhi".

Muslim katika sahihi yake ameileta hadithi hii ya Abul-Hayyaj pamoja na hadithi nyingine (ambayo tutaitaja) kwenye Babul-Amri Bitas-wiyatil-Qabri, na vile vile At-Tir-midhi na An-Nasai katika Sunan zao wameileta hadithi hii kwenye hiyo hiyo

Babul-Amri Bi Tas-Wiyatil-Qabri.

Na makusudio ya Babul-Amri Bitas-wiyatil-Qabri ni (kujulisha) kwamba kaburi linatakiwa liwe ni lenye kusawazishwa, na lau ingekuwa makusudio ni kulisawazisha na ardhi basi ingekuwa lazima kuuita mlango huu kuwa ni "Babul-Amri bi TakhiriibilQuburi Wahadmiha" yaani mlango wa kuharibu na kubomoa makaburi.

Manna tuliyoieleza juu ya neno Tas-wiyah lililo ndani ya hadithi ndiyo unayoweza kuikuta katika lugha ya Kiarabu, kwani neno Tas-wiyah linapotumika kwenye kitu kama kaburi, manna yake huwa ni kwamba, hilo kaburi lisawazishwe na siyo lilinganishwe na kitu kingine kama vile ardhi.

Hebu tuangalie hadithi nyingine aliyoitaja Imam Muslim katika Sahihi yake, hadithi ambayo inayo madhumuni yale yale tuliyoyateuwa:

"Kunnaa Maa Fadhaalah Ibn Ubaid Biardhir Ruum, Biraudasi, Fatuwufiyya Sahibun lana, Faamara Fadhaalah Ibn Ubaid Biqabrihi Fasuwwiya Thumma Qaala, Samitu Rasulallahi Ya'muru Bitas-wiyatiha".

Maana Yake: Tulikuwa pamoja na Fadhaalah ibn Ubaid huko Ruum (katika sehemu iitwayo) Raudas; basi mwenzetu (mmoja) akafishwa; na Fadhaalah ibn Ubaid akaamuru lichimbwe kaburi lake (kisha tulipokwisha mzika) akalisawazisha halafu akasema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akiamuru kuyasawazisha makaburi.[42]

Kwa kifupi ufunguo wa kuifahamu hadithi liii umejificha katika tamko Ia "Sawwaitahu", na ndani yake mna uwezekano wa kupatikana maana tatu.

Pamoja na kuzifahamu dalili na Qarina hapana budi kuchagua maana moja tu. Maana hizo tatu ni hizi zifuatazo:

Ya Kwanza: Maana yake iwe ni kuyabomoa majengo yaliyojengwa juu ya kaburi.

Na maana hii ni batili kwa sababu makaburi yaliyokuwepo Madina zama hizo hayakuwa na maqubba au madharih.

Ya Pili: Iwe maana ya "Tas-wiyah" ni kulisawazisha kaburi na ardhi.

Maana hii pia haikubaliki kwa kuwa Sunna iliyothibiti inaamuru kuliinua kaburi kiasi cha shibri moja.

Ya Tatu: Maana yake iwe ni kulisawazisha kaburi na kurekebisha (likae sawa) na wala isiwe kuliinua kama ngongo wa samaki au nundu ya ngamia.

Na maana hii ndiyo maana inayokusudiwa. Kwa hiyo haina uhusiano na makusudio wanayoyatolea ushahidi Mawahabi.

Sasa hivi ndugu msomaji, hebu muangalie Al-Allamah Annawawi ambaye ndiye aliyeandika Sharhi ya Sahihi Muslim na uone ni vipi alivyoisherehesha hadithi hiyo:

Anasema: "Innas-Sunnata Annal-Qabra la Yurfa'u Anil Ardhi Kathiran wala Yusannamu, bal Yurfau Nahwa Shibrin wayusattahu."[43]

Maana Yake: Iliyo sunna ni kwamba, kaburi lisiinuliwe (muinuko) mkubwa kutoka ardhini bali liinuliwe kiasi cha shibri lizawazishwe.

Katika ibara hii inadhihiri kwamba mshereheshaji wa Sahih Muslim amefahamu maana ile ile tuliyofahamu katika hadithi hii, kwamba Imam Ali [a] alimuusia Abul-Hayyaj kuyabadilisha makaburi yenye kunyanyaliwa mno au yale yenye maumbile kama mgongo wa samaki yasawazishwe na wala hakuamuru kuyasawazisha na ardhi.

Na sisi katika kutoa maana hii ndani ya hadithi hii hatuko peke yetu bali amesema pia Al-Hafiz Al-Asqalani katika kitabu chake Irshaad as-sraari fi sharhi Sahihil-Bukhari.

Baada ya yeye kutaja kwamba iliyo sunna katika kaburi ni kulisawazisha; na kwamba haifai kuiacha sunna hii eti tu kwa sababu kufanya hivyo imekuwa ni alama ya marafidhi (anakusudia Mashia) kwani hakuna upinzani baina ya kusawazisha kaburi na hadithi ya Abul-Hayaj. Al-Hafiz Al-Asqalani anasema kama ifuatavyo:

"....Ni kwamba (katika hadithi hiyo) hapakukusudiwa kusawazishakaburi na ardhi bali alichokusudia ni kulisawazisha (yaani kuliweka sawa) na kwa hiyo tunakusanya maana za haadithi zote."

Baada ya yote haya lau ingekuwa maana ya wasia wa Imam Ali [a] kwa Abul-Hayyaaj ni kubomoa maquba na majengo yaliyojengwa kwenye makaburi, basi ni kwa nini Imam [a] hakuamuru kuyabomoa maquba ambayo yalikuwa kwenye makaburi ya Manabii katika zama zake?

Pamoja na kwamba inaeleweka kuwa yeye Imam Ali [a] alikuwa ndiyo mtawala wa nchi zote za Kiislamu na alikuwa akiyafahamu maquba yaliyojengwa kwenye makaburi ya Manabii huko Palestina, Syria, Iraq, Misri, Iran na Yemen, (lakini hakuyabomoa).

Na tukiyafumbia macho maelezo yaliyotangulia hivi punde, na tukakadiria kwamba Imam Ali [a] alimuamuru Abul-Hayyaj kuyabomoa makaburi yaliyoinuliwa na ayasawazishe kabisa na ardhi, basi ndani ya hadithi hiyo hakuna kinachojulisha wajibu wa kubomoa majengo yaliyojengwa kwenye makaburi, kwa kuwa Imam Ali [a] alisema (iwapo tutakadiria kuwa hadithi hiyo imesihi):

"Wala Qabran illa Sawwaitahu" (wala kaburi ila ulisawazishe); na wala hakusema "wala Binaan Wala Qubbatan Illa Sawwaitahuma" (yaani wala jengo wala quba isipokuwa uyabomoe). Kwa kuwa uchunguzi wetu katika maudhui haya hauhusu kaburi lenyewe, bali majengo yaliyojengwa juu ya kaburi, kwa kuwa majengo haya yaliyoko kwenye makaburi waumini huwa wanapata kivuli kwa ajili ya kusoma Qur'an, dua na kusali, basije, katika sentensi hii (wala Qabran 1lla Sawwaitahu) kuna chochote kinachojulisha kuyabomoa majengo haya na kumbukumbu ambazo zinawasaidia wenye kuzuru makaburi hayo kufanya ibada na kuwakinga kutokana na joto au baridi?

UWEZEKANO WA MAANA MBILI MWISHONI

Mwisho wa uchunguzi kuna maana mbili nyingine hatuwezi kuepuka kuzitaja ili kukamilisha maudhui hayo.

Ya Kwanza: Ni kwamba hadithi hii (ya Abul-Hayyaj na nyinginezo zinazofanana) ni ishara ya yale yaliyokuwa yamezoweleka kwa baadhi ya nyumati zilizopita ikiwa ni pamoja na kuyafanya makaburi ya wachamungu kuwa ndiyo kibla chao wakayaelekea wakati wa ibada. Watu hao pia walikuwa wakiweka picha kwenye kaburi, kwa hiyo waliacha kuelekea kibla aliyowaamuru Mwenyezi Mungu wakati wa ibada na wakayaelekea makaburi hayo.

Na kwa maana hii basi, haiwezekani kwa hadithi hii kuwa na uhusiano wowote na makaburi ya Waislamu, na wala haijapata kuonekana kwa Muislamu yeyote kuyaelekea makaburi katika swala au kuyasujudia; isipokuwa mwenendo wa Waislamu ni kuswali jirani ya makaburi bila ya kuwa yenyewe ndiyo kibla chao, bali nyuso zao zinaelekea upande iliko Al-Kaaba, nao husimamisha swala na kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu huku wakiwa karibu ya makaburi.

Na kama Waislamu wanakwenda kuzuru makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu, na wakatumia huko muda mrefu kufanya ibada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu karibu na malazi hayo matukufu, basi si kwa jingine ila ni kwa sababu ya utukufu uliyopatikana kwenye ardhi hizo kwa kuwepo watu watukufu waliozikwa mahali hapo.

Jambo hili ufafanuzi wake utakuja baadaye.

Maana ya Pili: Ni kwamba, makusudio ya kauli ya Imam Ali [a] kwa Abul-Hayyaj aliposema: "Anlaa Tada'a Timthaalan Illa Tamastahu, Wala Qabran Mushrifan Illa Sawwaitahu", makusudio yake kusema "At-Timthal" ni mapicha na masanamu, na "Al-Qabr" ni makaburi ya washirikina ambayo yalikuwa yakienziwa na kuheshimiwa na wahusika.

Kwa kifupi ni kwamba hadithi ya Abul-Hayyaj haina uhusiano wowote kabisa na kujenga juu ya makaburi, isipokuwa inahusu makaburi yaliyoinuliwa mno (kama ilivyoelezwa hapo kabla) au makaburi ya washirikina na masanamu.

Maelezo yafuatayo tunataja fatwa ya Maimamu wa Madhehebu manne ya Kisunni kuhusu kujenga juu ya makaburi.

"Yukrahu An-yubnal-qabru Bibaytin au Qubatin au Madrasatin au Masjidin."[44]

Maana Yake: Ni karaha kulijengea kaburi katika nyumba au Qubbah au chuo au msikiti.

Basi maadamu Maimamu wa Madh-hebu nne za Kisunni wameafikiana kuwa ni karaha tu kuyajengea makaburi basi ni vipi Qadhi wa Najdi anathubutu kutoa fatwa ya uharamu wa kuyajengea?

"Kwa hakika huu ni uzushi."

Tena tunajua kwamba fatwa ya ukaraha wa kujenga juu ya makaburi haitegemei dalili sahihi yo yote, na hasa itapokuwa jengo hilo linamsaidia mwenye kuzuru hapo aweze kusimamisha mambo ya faradhi ya dini na kusoma Qur'an kwenye jengo hilo.

D. HADITHI YA JABIR

Hadithi ya Jabir inafahamika kuwa ni miongoni mwa hadithi wanazozitegemea Mawahabi kuharamisha kujenga juu ya makaburi; na imepokewa hadithi hii katika Sihah na Sunan kwa matamko tofauti tofauti, na wanapatikana katika Sanadi zake zote na mapokezi yake wanapatikana watu wawili.

1. Ibnu Juraih

2. Abuz-Zubair.

Na ili kuthibitisha kusihi kwa hadithi hii itategemea kuzifahamu hali za wapokezi wake na watu wa Sanad yake.

Katika maelezo yafuatayo tutaitaja hadithi hiyo kwa matamko mbali mbali tena tofauti:

Imekuja katika Sahihi Muslim (Babun-Nahyi 'An Tajsisil-Qabri Wal-Bina'i Alaih) Hadithi ya Jabir iliyopokelewa kwa njia tatu na katika aina mbili:

1. Ametusimulia Abubakar ibn Abi Shaiba, ametusimulia Hafsu ibn Ghiyath, kutoka kwa Ibn Juraih, naye toka kwa Abuz-Zubair kutoka kwa Jabir, amesema: "Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kulipaka kaburi jasi (aina ya chokaa) na kulikalia na kujengea juu yake."

2. Amenisimulia Harun ibn Abdillah, ametusimulia Hajaaj ibn Muhammad, na amemsimulia Muhammad ibn Raafi', ametusimilia 'Abdur-Razzaq, wote hawa wamepokea toka kwa Ibn Juraih, amesema: Alinieleza Abuz-Zubair kwamba yeye alimsikia Jabir ibn Abdillah anasema, "Nilimsikia Mtume..... (kama ilivyo hadithi ya hapo awali).

3. Ametusimulia Yahya ibn Yahya, ametusimulia Isma'il ibn Ulayyah kutoka kwa Ayyub, naye toka kwa Abuz-Zubair toka kwa Jabir; amesema: Amekataza kuyapaka makaburi jasi.[45]

Na imekuja katika Sahihi Tirmidhi hadithi moja na kwa njia moja (kwenye Babu Karahiyyati Taj-sisil-Quburi Wal-Kitabati Alaiha) kama ifuatavyo:

4. Ametusimulia 'Abdur-Rahman ibn Al-Aswad, ametueleza

Muhammad ibn Rabi'ah, kiltoka kwa Ibn Juraih naye toka kwa

Abuz-Zubair kutoka kwa Jabir; amesema: Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amekataza kuyapaka jasi makaburi na kuyaandika juu yake na kuyajenga juu yake na kutembea juu yake.

Kisha baada ya kuandika hadithi hii At-Tirmidhi anaeleza kwamba imepokewa kwa al-Hasan Al-Basri na Shafi'i, kuwa wao wametoa fatwa kuruhusu kuyapaka makaburi jasi.[46]

Na katika Sahih Ibn Majah, imekuja (katika Babu Ma Ja'a fin-nahyi Anil-Bina'i Alal-Quburi Wataj-sisiha Wal-Kitabati 'alaiha) hadithi hii kwa njia mbili na aina mbili, nazo ni hizi zifuatazo:

5. Ametusimulia Azhar ibn Marwan na Muhammad ibn Ziyad, wamesema: Ametusimulia 'Abdul Warith kutoka kwa Ayyub naye toka kwa Abuz-Zubair naye toka kwa Jabir; amesema: "Amekataza Mtume wa Mwenyezi Mungn kuyapaka makaburi jasi."

6. Ametusimulia Abdallah ibn Said ametusimulia Hafsi kutoka kwa Ibn Juraih naye toka kwa Suleiman ibn Musa kutoka kwa Jabir, amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu amekataza kuandikwa chochote juu ya kaburi".[47]

Na baada ya kuitaja hadithi hii As-Sindi aliyeisherehesha anaandika akimnukuu Al-Hakim An-Nishapuri kwamba hadithi hii ni sahihi lakini haifuatwi, kwani viongozi wa Uislamu mashariki ya dunia na magharibi yake sera yao imekuwa ni ya kuandika juu ya makaburi kizazi baada ya kizazi.

Na imekuja hadithi hii katika Sahih An-nasa'i (katika Babul-Bina'I Alal-Qabri) kwa njia mbili na kwa namna mbili zifuatazo:

7. Ametueleza Yusuf ibn Sa'id amesema: Ametusimulia Hajjaj kutoka kwa Ibn Juraih amesema, amenieleza Abuz-Zubair kwamba yeye alimsikia Jabir anasema: "Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amekataza kuyapaka makaburi jasi au kujenga juu yake au yeyote yule kuyakalia."

8. Ametueleza Imran ibn Musa amesema, ametusimulia 'AbdulWarith amesema, ametusimulia Ayyub kutoka kwa Abuz-Zubair nayr kutoka kwa Jabir amesema: "Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amekataza kuyapaka jasi makaburi.[48]

Na hadithi ya Jabir imekuja katika Sunan Abi Dawuud (Juzuu ya tatu ukurasa 216), "Babul-Bina'I Alal-Qabr) kwa njia mbili na namna mbili zifuatazo:

9. Ametusimulia Ahmad ibn Hanbal, ametusimulia 'Abdur-Razzaq, ametusimulia Ibn Juraih, amenieleza Abuz-Zubair kwamba yeye amemsikia Jabir anasema, nimemsikia Mtume amekataza kukalia kaburi, na kupakwa jasi na kujenga juu yake."

10. Ametusimulia Musaddad na Uthman bin Abi Shaibah amesema: Ametusimulia Hafsu ibn Ghiyath kutoka kwa lbn Juraih naye toka kwa Sulaiman ibn Musa na kutoka kwa Abuz-Zubair kutoka kwa Jabir amenisimulia hadithi hii (iliyotajwa kabla).

Amesema Abu Daud: Amesema Uthman "au kuliongeza", na akaongeza Suleiman ibn Musa "au kuandikwa juu yake".

Ama Ahmad ibn Hanbal (Imam wa madhehebu ya Kihanbal) yeye ameipokea hadithi hii katika Musnad yake kwa namna ifuatayo:

11. Imepokewa toka kwa 'Abdur-Razzaq naye kapokea kwa Ibn Juraih: Amenieleza Abuz-Zubair kwamba yeye amemsikia Jabir ibn Abdilahi anasema: Nimemsikia Mtume akikataza mtu kukalia kaburi na kulipaka jasi na kulijenga juu yake.[49]

Haya ndiyo mapokezi yaliyopokelewa toka kwa Jabir kuhusu maudhui haya, na tumeitaja hadithi hii kwa mapokezi tofauti tofauti na Sanad zake mbali mbali.

Sasa hivi umefika wakati wa kuitafiti na kuichunguza ndani yake ili tuone je, hadithi hii inafaa kutolea ushahidi au hapana?

DALILI ZA UDHAIFU NDANI YA HADITHI HII

Hadithi hii ya Jabir ma mkusanyiko mkubwa wa nukta mbali mbali za udhaifu, kiasi kwamba nukta hizo zinaiangusha isiwezekane kuitolea hoja na kuizingatia, na haiwezekani kabisa kuitolea ushahidi kwa namna yoyote ile.

Maelezo yafuatayo tutataja nukta za udhaifu uliyomo katika hadithi hii:

Kwanza: Katika sanad zote za Hadithi hii yamo majina ya Ibn Juraih (Abdul-Malik ibn Abdul-Aziz ibn Juraih AI-Amawi) na Abuz-Zubair (Muhammad ibn Muslim Al-Asadi) kwa pamoja au likawepo Ia mmoja wao.

Tutakapofahamu mazingira ya hawa wapokezi wawili na hali zao, basi hakutakuwa na sababu ya kutaka kuwafahamu wapokezi wengine waliomo katika hadithi hii, ambao baadhi yao hawatambuliki na wengine wanaosababisha hadithi hii iwe dhaifu.

Katika kitabu kiitwacho Tahdhibut-Tahdhib cha Ibn Hajar Al-'Asqalani utasoma maoni ya wanachuoni wa Rijal (wanaotambua wapokezi wa hadithi) juu ya ibn Juraih kama ifuatavyo:

Yahya ibn Said aliulizwa kuhusu hadithi za Ibn Juraih, akasema: "Ni dhaifu;" akaambiwa: "Hata kama akisema kuwa amenieleza fulani?" Akasema, "Usihadaike; si lolote; zote ni dhaifu".[50]

Naye Ahmad ibn Hanbal amesema: "Iwapo Ibn Juraih atasema kuwa fulani amesema na fulani amesema, nami nimeambiwa, basi haya yote ni uzushi".

Maana yake ni kuwa hadithi zake hazitambuliwi au ni za uzushi.[51]

Naye Malik ibn Anas amesema: kuwa Ibn Juraih alikuwa akisenya kuni usiku (akikusanya kila kitu bila kuchagua kilicho sahihi na kisicho sahihi kama msenya kuni asenyeaye usiku hawezi kuona ni zipi kuni na wepi nyoka).

Ama Ad-Daruqutni yeye amesema: Jiepushe na tadlisi ya Ibn Juraih, kwani tadlisi yake hi mbaya sana, yeye alikuwa hafanyi tadlisi isipokuwa kwa yale aliyoyasikia toka kwa mtu Majruh. (Mpokezi ambaye ubaya wake umebainishwa).

Ibnu Hibbaan amesema: "Ibn Juraih alikuwa akidanganya katika hadithi"[52]

Ewe msomaji, nakuapia Mwenyezi Mungu, hivi kweli inafaa kuchukuwa mapokezi ya mtu huyu pamoja na kuwa wanachuoni wa hadithi wamemshutumu na kuonyesha unyonge wake?

Na je, inafaa kuacha sera ya Waislamu ya kujenga juu ya makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kuyaheshimu kwa kutegemea hadithi za mpokeaji huyu mdanganyifu?

Na je, inafaa tuwashutumu Waislamu kwa ushirikina na ukafiri na upinzani kwa kuwa wanaupenda mwenendo wa Kiislamu na wanafuata sera ya watu wema waliopita ya kujenga juu ya makaburi na kuyazuru na kuyaheshimu?

Maelezo haya yaliyopita ndiyo baadhi ya yalioandikwa kuhusu Ibn Juraih.

Ama Abuz-Zubair, msikilize lbn Hajar huyu hapa anataja kauli za wanachuoni wa Rijal wasemavyo:

"Imepokewa kutoka kwa Abdullah ibn Ahmad ibn Hanbal, naye amepokea toka kwa babaye (Imam wa Kihanbal) naye toka kwa Ayyub kwamba yeye alikuwa akimfahamu Abuz-Zubair kuwa hi mpokezi dhaifu.

Na imepokewa toka kwa Shu'bah kwamba, Abuz-Zubair alikuwa hawezi hata kuswali vizuri.

Na imepokewa tena toka kwa Shu'bah amesema: Hapakuwepo katika dunia mtu nimpendaye mno kuliko yule ajaye kisha nikamuuliza habari za Abuz-Zubair; basi nilifika Makka nikawa napokea toka kwake, ghafla nikiwa nimekaa kwake alikuja mtu na akamuuliza swali fulani, basi alimjibu lakini alizusha uongo; basi mimi nikasema: "Ewe Abuz-Zubair, unamwambia uzushi mtu Mwislamu?"

Akajibu:- "Hakika yeye amenikasirisha".

Nikasema: "Basi yeyote anayekukasirisha unamzushia? Basi kamwe sitapokea hadithi yoyote toka kwako".

Na imepokewa toka kwa Warqaa amesema: "Nilimwambia Shu'bah, vipi mbona umeziacha hadithi za Abuz-Zubair"?

Akasema: "Nilimuona akipima, na anapunguza kipimo".

Ibn Abi Hatima amesema: "Nilimwuliza baba yangu kuhusu Abuz-Zubair; akasema:

"Hadithi zake zinaandikwa lakini hazitolewi ushahidi."

Anasema tena: Na nilimwuliza Abu-zar'ah kuhusu Abuz-Zubair.

Akasema: "Watu wanapokea toka kwake".

Nikasema: "Hadithi zake hutolewa ushahidi?"

Akasema: Hutolewa ushahidi hadithi za watu waaminifu. (Akiwa na maana kuwa Abuz-Zubair siyo mwaminifu.)[53]

Naam! Ewe ndugu yangu ....... hii ndiyo hali ya Ibn Juraih na Abuz-Zubair; nao ndiyo miongoni mwa wapokezi wa hadithi ya Jabir katika Sanad zake zote. Basi, je inawezekana kutolea ushahdi hadithi ambayo ndani yake wamo wapokezi wawili hawa?

Na hapo kabla ilitangulia ishara kwamba ndani ya Sanad za hadithi hii wamo wapokezi wanyonge zaidi ya Ibn Juraih na Abuz-Zubair, kama vile Abdur-Rahman ibn Aswad anayetuhumiwa kuwa ni mwongo tena mzushi.

Basi je, inafaa kubomoa athari za watu wa nyumba ya Mtume [a] na athari za Masahaba na kuwanasibisha Waislamu kuwa wamepotea kwa muda wa karne zote kumi na nne kwa kutegemea hadithi hii dhaifu isiyokubalika?

Nukta ya Pili: Hakika hadithi ya Jabir inamvurugano sana katika matamko na matni yake, na mvurugano huu unajulisha kuwa wapokezi wa hadithi hii walikuwa hawana uwezo wa kudhibiti na kufuatilia riwaya (mapokezi), pamoja kuwa na uwezo wa kudhibiti ni moja ya masharti anayotakiwa kuwa nayo Rawii (mpokeaji).

Kwa mvurugano uliyomo kwenye hadithi hii, uaminifu unakosekana, na pia imani na mategemeo ya hadithi hii vinaondoka. Hebu endelea kuona ufafanuzi zaidi katika kuitafiti hadithi hii:

Hadithi hii ya Jabir imepokewa katika namna saba, pamoja na kuwa Mtume [s] aliitamka kwa tamko la aina moja tu.

Angalia namna hizo saba zilivyo:

1. Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kulipaka kaburi jasi na kuliegemea. Hadithi Na. 1, 2 na 9.

2. Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kulipaka kaburi jasi. Hadithi Na. 5 na 8.

3. Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kulipaka kaburi jasi na kuliandika na kujenga juu yake na kutembea juu yake. Hadithi Na. 4.

4. Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kuandika juu ya kaburi. Hadithi Na. 6.

5. Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kukaa juu ya kaburi na kulipaka jasi na kulijenga na kuliandika juu yake. Hadithi Na. 10.

6. Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kukaa juu ya kaburi na kulipaka jasi na kujenga juu yake. Hadithi Na. 11.

Hapa iko tofauti baina ya hadithi hii na ile ya kwanza, kwani ile ya kwanza imekataza kuliegemea kaburi na hii inakataza kukaa juu ya kaburi.

7. Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kukaa juu ya kaburi na kulipaka jasi na kujengea juu yake na kuliongeza na kuliandika.

Tunaona katika sura hii kumeongezwa kwenye kukaa, kupaka jasi na kujenga kuna ziada ya kuliongeza kaburi na kuandika juu yake.

Baada ya yote haya utaona kuna hitilafu katika matni za hadithi na sentensi zake, kwani katika namna ya kwanza anasema (Al-'itimadu) kuegemea, na ya tatu (Al-wat'u) kutembea, na ya tano na ya sita: (Al-qu'udu) kukaa. Hivyo basi hakuna uwezekano wa kuikubali hadithi hii na kuitegemea kwa mwanachuoni yeyote kutokana na mvurugano uliyomo.

Nukta ya Tatu: Hadithi hii iwapo itakadiriwa kuwa ni sahihi na kupuuza mvuragano uliyomo, haijulishi zaidi ya kuwa Mtume [s]

alikataza kujenga juu ya makaburi, lakini haijulishi kuwa jambo hilo ni haramu kwani kukataza (Nah-yi) kumegawanyika vigao viwili:

Kuna Nahyi Tahriim na Nahyi Karaha.

Yaani kukataza kwa kuharamisha na kukataza kwa karaha. Na hiki kigawo cha pili kimekuja mara nyingi mno katika hadithi za Mtume [s] na Maimamu watukufu [a].

Ni kweli kwamba nahyi kwa asili yake inajulisha kuharamisha na tahriim ndiyo inayothibiti kwanza mpaka ije dalili ya kugeuza uharamu na kuwa karaha, lakini wanachuoni hawakufahamu katika hadithi hiyo isipokuwa karaha tu.

Kwa mfano utamwona At-Tirmidhi ameitaja hadithi hiyo katika Sahihi yake chini ya anuani isemayo, "Karahiyyatu Taj-sisilqubur " (Ukaraha wa kupiga lipu makaburi.).

Na ushahidi uliyo wazi zaidi ni kuwa As-Sindi aliyesherehesha Sahih Ibn Majah amemnakili Al-Hakim An-Nishapuri amesema kwamba, "Hajalitumia katazo hili Mwislamu yeyote;" kwa hiyo hakulizingatia kuwa ni Nahyi Tahriim kwa dalili kuwa, sera ya Waislamu iko kwenye kuandika juu ya makaburi.

Kingine ambacho ni ushahidi vile vile kuwa Nahyi hiyo ni Nahyi karaha ni maafikiano ya madhehebu za Kiislamu kuwa inafaa kujenga juu ya kaburi isipokuwa ardhi iliyowekwa wakfu kisheria.

Anasema mashereheshaji wa Sahih Muslim alipokuwa akifafanua hadithi hii:

"Ama suala la kujenga juu ya kaburi, iwapo (ardhi) ni mali ya mjengaji basi ni karaha (kujenga) na kama ni (ardhi) ya wakfii basi ni haramu (kujenga).[54]

Katika mambo yasiyohitaji maelezo marefu ni kuwa kitu kinapokuwa karaha basi ukaraha wake huondoka kwa kuyazingatia baadhi ya mambo fulani muhimu.

Kwa mfano: Ikiwa kujenga juu ya kaburi itakuwa ni sababu ya kuhifadhi asili ya Uislamu na kudhihirisha mapenzi kwa mwenye kaburi hilo ambaye Mwenyezi Mungu amefaradhisha kumpenda au kujenga huko kutakuwa ni sababu ya kuhifadhi athari za Uislamu au itafanya wakusanyike wenye kuzuru mahali hapo chini ya jengo hilo ili wasome Qur'an na kuswali na kusoma dua, basi moja kwa moja karaha hiyo itaondoka. Si hivyo tu bali jambo hilo litakuwa ni mustahab, lenye kupendekezwa kufanywa, na litakuwa katika mlango wa kuhuyisha desturi na urithi wa dini na ni kuimarisha mambo matukufu ya Kiislamu.

KUTOLEA USHAHIDI HADITHI ZINGINE MBILI

Kwa kukamilisha uchunguzi tunataja hadithi zingine mbili ambazo Mawahabi wanazitegemea katika maudhi haya:

Amepokea lbn Majah katika Sahih yake kama ifuatavyo:

(1) Ametusimulia Muhammad ibn Yahya, ametusimulia Muhammad ibn Abdullah Ar-Riqashi ametusimulia Wahab ametusimulia Abdur-Rahman ibn Yazid ibn Jabir kutoka kwa Qasim ibn Mukhaimara, naye amepokea toka kwa Abu Sa'id: Hakika Mtume amekataza kujengwa juu ya kaburi.[55]

Na anasimulia Ahmad ibn Hanbal, hadithi ingine kwa sanadi mbili ambazo ni kama ifuatavyo:

(2) Ametusimulia Hasan, ametusimulia Ibn Lahi'a, ametusimulia Buraida ibn Abii Habib, amepokea toka kwa Na'im kijana wa Ummu-Salama, naye kapokea kutoka kwa Ummu-Salama amesema:

Amekataza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kujenga juu ya kaburi au kupakwa jasi.

Kuhusu hadithi ya kwanza, inatosha kuwa dhaifu kwa kuwa miongoni mwa wapokezi wake yumo mtu aitwaye "Wahab", ambaye hali yake haitambuliki; kwani kuna watu kumi na sababa kila mmoja wao jina lake ni "Wahab" ambao hawakupambanuliwa wala kufahamika yupi ni nani. Na kati yao wamo wazushi na waongo, na katika hadithi hii Wahab huyu hakutambulika kuwa ni yupi katika hao, kwa hiyo riwaya hii inaporomoka.

Ama hadithi ya pili inaanguka kwa kuwepo Abdallah ibn Luhay'ah katika Sanad yake.

Adh-Dhabi anasema kuhusu mtu huyu:

lbn Mu'in anasema: "(Mtu huyu) ni mdhaifu haitolewi kwake hoja.

Al-Humaydi anasema: "Imepokewa toka kwa Yahya bin Sa'idi kwamba yeye (Yahya bin Sa'id) alikuwa hamuoni kuwa ni kitu chochote.[56]

Sisi hatutajadili Sanadi ya hadithi hizi mbili, bali tutatosheka na kuonyesha nukta moja muhimu nayo ni kuwa:

Wanahistoria na wanahadithi na wanasira wameeleza kuwa mwili wa Mtume [s] umezikwa katika nyumba ya Bibi Aisha kwa maafikiano ya Masahaba.

Na kuchaguliwa kwa nyumba ya Bibi Aisha kulitimia kwa kutegemea kauli yake Mtume [s] kwamba "Kila Nabii huzikwa pale alipofia".[57]

Na sasa linakuja swali lifuatalo:

Ikiwa Mtume alikataza kujenga juu ya kaburi, basi vipi waliuzika mwili wake Mtukufu katika nyumba yenye paa, kisha wakajenga ukuta katikati ya nyumba hiyo na hivyo kulifanya kaburi tukufu la Mtume [s] kuwa ni jengo maalum wanalolikusudia waumini na Waislamu kulizuru?

Katika mambo yanayochekesha ni kauli ya mwandishi mmoja wa Mawahabi wanaopinga ukweli anaposema:

"Kilicho haramu ni kujenga juu ya kaburi na siyo kuzika ndani ya jengo, kwani walimzika Mtume ndani ya jengo na hawakujenga chochote kwenye kaburi lake.[58]

Mwandishi huyu amelazimika kuandika kauli hii ya kipumbavu kwa kuwa analiona kaburi la Mtume limejengewa jengo na Qubbah, na lau si hivyo angeharamisha pia kuzika ndani ya nyumba vile vile.

Hebu mwangalie ni vipi alivyotoa fatwa kutoka katika nafsi yake bila ya kuangalia yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ili ayaridhishe matamanio yake pamoja na mwelekeo wake potofu!!

Nasi tunamwuliza Wahabi huyu mpotovu, je, kilicho haramu ni kujenga juu ya kaburi tu lakini kubakisha jengo siyo haramu?

Au ni kwamba jengo ni haramu kulijenga na kulibakisha?

Ikiwa kilicho haramu ni jengo tu, sisi tunauliza ni kwa nini basi serekali ya mabavu ya Kisaudi kwa dhulma na uzushi ilizibomoa athari za Mtume na makaburi ya Maimamu watukufu [a] na makaburi ya Masahaba na ya watoto wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, pamoja na kuwa, kwenu ninyi Mawahabi kilicho haramu ni kujenga jengo tu, na wala siyo kulibakisha jengo lililokwisha jengwa?

Zaidi ya haya, hukmu hii muitowayo iko kinyume na fatwa ya viongozi wenu waliotangulia kama vile Ibnul Qayyim Al-Jauziyya na Ibn Taimiyya, kwani anasema Ibnul Qayyim "Ni wajibu kuyabomoa maziyara yaliyojengwa kwenye makaburi na wala haifai kuyaacha yabakie hata siku moja baada ya kuwa na uwezo wa kuyabomoa.

Kwa msingi huu basi hawezi Wahabi huyu muovu kusema kuwa ni haramu kujenga tu, ili asije akawakhalifu waliomtangulia kuingia motoni, na wala hawezi kukwepa hukmu yao ya kuharamisha kujengea na kuyabakisha.

Hapa linakuja swali lifuatalo:

Ni kwa nini Waislamu waliuzika mwili wa Mtume [s] ndani ya jengo? Ni kweli kwamba hawakujenga jengo kwenye kaburi lake isipokuwa kule kuzikwa kwake hapo kulipelekea kaburi liwe ndani ya jengo lenye paa.

Na utamwona Wahabi huyu muovu anajaribu kulikwepa swali hili na kutoa fatwa aonayo yeye badala ya vile alivyoteremshwa Mwenyezi Mungu - kama ilivyo kawaida yao Mawahabi.

Eti anasema: "Kubakisha (jengo) kuliko haramu ni lile lililojenwa kwenye kaburi, ama ikiwa jengo ndilo lililo tangulia kaburi, basi kulibakisha siyo haramu."

Angalia ni jinsi gani anatenganisha katika hukmu na kutoa fatwa aonavyo yeye ili ajitenge na msimamo wa Waislamu wa tangu zama hizo na anajaribu kuikwepa haki ambayo inampinga.

KUPINGANA KWA SERA YA WAISLAMU NA MAWAHABI

Nukta hii ambayo maelezo yake yametangulia hapo kabla, siyo pekee ambayo inayoweka wazi kutofautiana kwa Mawahabi na sera ya Waislamu kwa muda wote wa karne kumi na nne.

Bali tofauti zipo pia katika mambo mengine mengi mno. Kwa mfano: Mawahabi wanazingatia kuwa kutabaruku (kutaka baraka) kwenye athari za Mtume [s] ni haramu, wanakataza jambo hili kwa nguvu zote; wanasema "Hakika jiwe na udongo havinufaishi chochote."

Lakini utawaona Waislamu wanasongamana kwenye Hajarul-Aswad (Jiwe jeusi, lililoko kwenye Al-Kaaba) ili walibusu na kuligusa ili wapate baraka kwalo, na wanasongamana kwenye Kiswa cha Al-Kaaba (nguo inayofunikwa al-Kaaba) ili wajipanguse kwacho, na kwenye Al-Kaaba, wanavibusu vitu hivyo na kuweka mashavu yao juu yake.

Basi Waislamu wanabusu jiwe na udongo na wanatofautiana na Mawahabi ambao wanasema eti jiwe na udongo havisaidii kitu.

Vile vile Mawahabi wanakataza kujenga msikiti karibu na Makaburi ya Mawalii, wakati ambapo katika kila nchi ya Kiislamu kunapatikana misikiti iliyojengwa karibu na maziyara, hata katika ardhi ya Uhudi, palikuwepo Msikiti uliokuwa karibu na kaburi Ia Sayyidina Hamza [r.a.], lakini Mawahabi walipoikalia ardhi hiyo tukufu wakaubomoa Msikiti huo na kuifuta athari yake.

Sasa hivi utaona kaburi tukufu la Mtume [s] liko katikati ya Msikiti na Waislamu wanaswali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu katika pembe zake zote.

Kwa hakika iko mifano mingi ya jambo hili duniani. Hebu ona tofauti kubwa iliyoko baina ya Mawahabi na mwendo wa Waislamu, kitu ambacho kinajulisha kujitenga kwa Uwahabi kutoka kwenye Uislamu na kujitenga kwa Mawahabi kutoka kwa Waislamu.

KUZUA DALILI POTOFU KWA KUKWEPA KOSA

Mawahabi wametegemea kuzua hoja dhaifu zitakazowaruhusu kuyabomoa makaburi matukufu na maquba ya Maimamu watukufu [a] katika Baqii.

Miongoni mwa hoja walizozizua kuhusu jambo hili ni kwamba: "Baqii ni ardhi iliyowekwa waqfu na ni wajibu itumike kwa lengo lililokusudiwa na huyo muwekaji wa waqfu, na ni wajibu kuondosha kila kitu kitakacholazimisha kuzuia matumizi ya lile lengo, na kujenga na kusimika nguzo na kuta katika ardhi hii ni jambo linalolazimisha kuzuia matumizi ya sehemu fulani ya Baqii, kwani ardhi ya Baqii ni waqfa kwa ajili ya kuzika wafu, na ukweli ni kwamba kusimika nguzo na kuta kwa ajili ya ujenzi kunaziba sehemu ya ardhi, kwani haiwezekani kuzika chini ya nguzo na kuta, na jambo hili linasababisha kuzuia matumizi ya lengo lililokusudiwa.

Na kwa ajili hii basi ni wajibu kuondosha kila kitu kilichoko katika ardhi hii ya Baqii ikiwa ni pamoja na majengo ili iwezekane kuzika katika sehemu yote ya Baqii.

Jibu Letu: Hapana shaka kwamba aina ya ushahidi kama huu ni kutoa maamuzi bila kufikiri na ni kuukwepa ukweli halisi.

Qadhi huyu wa Kiwahabi katika fatwa yake hiyo analenga kuondoa athari za watu wa nyumba ya Mtume [s] kwa hali yoyote iwayo japo atakuwa hana dalili lakini anaamuru zivunjwe kwa nguvu na uzushi ataouzua.

Na dalili hii aliyoitoa haina chochote isipokuwa ni kuwahadaa Waislamu wa kawaida kuwa eti ametoa fatwa kwa mujibu wa hukmu aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu, na ndiyo maana utamwona anauzingatia uwanja wa Baqii kuwa ni ardhi iliyowekwa waqfu kwa ajili ya kuzikia.

Lakini dalili yao hii ni, kama zile dalili zao zingine, haifai kwa namna nyingi.

Ya Kwanza: Haikuja katika kitabu chochote miongoni mwa vitabu vya historia na hadithi habari yoyote inayoashiria kuwa ardhi ya Baqii iliwekwa waqfu, na hakuna mwana historia ye yote au mwanachuoni wa hadithi aliyebainisha jambo hili.

Angalia katika vitabu vya historia hutaona chochote kuhusu kauli hiyo; bali inawezekana kabisa kwamba ardhi ya Baqii ilikuwa ni mahali palipoachwa kwa matumizi ya watu wote kwa jumla kama ilivyo katika ardhi zingine za aina hii; na watu wa Madina walikuwa wanazika wafu wao hapo.

Na kwa maelezo haya ni wazi kuwa ardhi ya Baqii asili yake ilikuwa ni mubah (halali) kwa watu wote ambayo ilikuwa inafaa kuitumia na watu kwa matumizi mbali mbali na kwa namna yoyote.

Katika zama hizo zilizopita watu walikuwa hawapupii kumiliki ardhi tupu isiyotumika, kwani hawakuwa na uwezo wa kujenga pote ila mahala padogo. Na kadhalika watu kuhamia mjini toka vijijini lilikuwa jambo ambalo halijaanza kutokea kwa wingi. Na hapakuweko mas'ala ya ardhi, wala tatizo la watu wanaojilimbikizia ardhi au taasisi.

Kwa hiyo basi ardhi kubwa ilikuwa imeachwa bila kuwa na mwenye kuimiliki. Na ardhi namna hii ndiyo ile iitwayo katika sheria ya Kiislamu kuwa ni ardhi (Al-Mubahat na Al-Ardhil-Mawat Al-Bairah).

Kwahiyo desturi hii iliendelea katika miji na vijiji kutenga maeneo kwa ajili ya kuzikia, au pengine mtu mmoja alimzika jamaa yake mahali fulani kisha na wengine nao wakafuatia kuzika hapo bila ya kuangalia kabisa kuwa ardhi hiyo ni waqfu.

Na hii ardhi ya Baqii haiwezi kutoka kwenye desturi hii, kwani katika Hijazi yote na mji wa Madina ardhi haikuwa ni yenye thamani.

Na kutokana na kuwepo kwa ardhi isiyotumika kuuzungaka mji wa Madina, haikuwa haja kwa mtu yeyote kutenga ardhi yake ya kilimo na kuiweka waqfu kwa ajili ya kuzikia, kwani ardhi ya kilimo ilikuwa ni ndogo kinyume cha ardhi tupu isiyotumika hiyo ilikuwa ni kubwa na ni miongoni mwa ardhi iliyo halali/kwa asili yake kwa matumizi mbali mbali.

lnafaa kusema kwamba historia pia inaunga mkono ukweli huu kama asemavyo As-Samhudi katika kitabu kiitwacho "Wafaul Wafa".

"Mtu wa kwanza ambaye Mtume alimzika hapo Baqii ni Uthman bin Maz'uun na alipofariki Ibrahim mtoto wa Mtume [s], Mtume aliamuru azikwe mahali alikozikwa Uthman bin Maz'uun. Basi watu wakapapenda hapo Baqii na wakaikata miti, kisha kila kabila likachagua upande wake, na kuanzia hapo kila kabila likafahamu yalipo makaburi yao.

Uwanja wa Baqii ulikuwa na miti mingi ya gharqad, alipofariki Uthman bin Maaz'un na kuzikwa hapo Baqii, miti hiyo ikakatwa."[59]

Kutokana na maneno ya As-Samhudi inadhihiri kwamba ardhi ya Baqii ilikuwa imeachwa bila mwenye kuimiliki na iligawanywa vipande vipande baada ya kuzikwa hapo sahaba mmoja, na kikatengwa kila kipande kwa ajili ya kabila fulani miongoni mwa makabila ya nyumba za hapo Madina.

Ama eti Baqii kuwa iliwekwa wakfu huwezi kuona habari yoyote katika historia kuhusu jambo la wakfu, isipokuwa kinachofahamika katika historia ni kuwa sehemu walipozikwa Maimamu watukufu [a] katika Baqii palikuwa na nyumba ya Aqil ibn Abi Talib, na kwamba miili hiyo mitukufu ya Maimamu [a] imezikwa kwenye nyumba ambayo inarudi katika milki ya Bani Hashim.

Anasema tena As-Samhudi:

"Amezikwa Abbasi ibn Abdil-Muttalib mahala alikozikwa Fatma bint Asad bin Hashim, sehemu ambayo ndiyo yenye makaburi ya mwanzo ya Bani Hashim yaliyoko katika nyumba ya Aqil."

Na anasema tena:

Imepokewa toka kwa Said bin Muhammad bin Jubair kwamba yeye aliliona kaburi la Ibrahim mtoto wa Mtume hapo Azzawara' nayo ni nyumba ambayo baadaye ilikuwa ya Muhammad bin Zaid bin Ali .... Na kwamba Mtume alimzika Sa'd ibn Mua'adh pembeni mwa njia iliyo ubavuni mwa nyumba ya Miqidad ibn AlAswad.... nayo ndiyo nyumba iitwayo kuwa ni "Daru Ibn Aflah" mwishoni mwa Baqii na ilikuwa juu yake kuna Qubbah."[60]

Sentensi hizi zote kwa jumla zinasisitiza kwamba ardhi ya Baqii haikuwa wakfu na kwamba miili mitukufu ya Maimamu [a] ilizikwa katika nyumba zao walizokuwa wakizimiliki wenyewe.

Baada ya maelezo yaliyotangulia, je, kweli inafaa kuzibomoa athari za kizazi cha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu [s] na kuzisawazisha na ardhi eti kwa hoja kwamba hazikubaliani na wakfu?

Lau tukikubali kwa ajili ya majadiliano kwamba eti ardhi ya Baqii imewekwa wakfu, basi je kuna kitu cha kuthibitisha namna wakfu huo ulivyowekwa?

Basi huenda aliyeweka wakfu aliruhusu kusimamisha majengo na maquba juu ya makaburi ya watu watukufu wataozikwa katika ardhi hiyo.

Sisi hatujui ufafanuzi wa mambo haya, lakini tunachokifahamu ni kuwa Waislamu walijenga majengo na maquba kwenye makaburi hayo na tunawajibika kukichukuliwa kusihi kitendo hicho na kujiepusha na tuhuma na kukinasibisha kuwa ni kitendo cha maasi.

Na kwa msingi huu basi, kubomoa maquba matukufu na majengo yenye kuheshimiwa inazingatiwa kuwa ni haramu na ni kinyume kabisa cha hukmu ya sheria.

Na huyu Qadhi Ibn Balhid na wafuasi wake walikuwa wanatambua vizuri kwamba fikra ya kuifanya Baqii kuwa ni wakfu ni dalili iliyoundwa.

Na hata kama shetani asingewaundia dalili hii potofu, wangeendelea tu kuvunja athari za kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu bila kusita, kwa kuwa mara hii siyo mara yao ya kwanza kwa Mawahabi walioundwa na Waingereza, kubomoa athari za Utume na Uislamu, kwani mara yao ya kwanza ilikuwa mwaka 1221 A.H.-1801 A.D., wakati walipoikalia Madina kwa mara ya kwanza na wakayavunja majengo hayo na kumbukumbu hizo, kisha yalijengwa tena baada Mawahabi kufukuzwa kutoka Madina kutokana na nguvu za Dola ya Uthmaniyyah.

[29] Zaadul-Maad fil Hudaa Khairil-anam, uk. 661

[30] Kash-ful Irtiyab, uk. 384

[31] Tabaqat As-Sahaba cha lbn Saad: Juz. 1 uk. 360-503.

[32] Tat-hirul-iitikadi. uk. 17, Chapa ya Misri.

[33] (1) Sahih Muslim, juz. 3, Kitabul-Janaiz, uk. 612 (2) Sunan Tirmidhi, juz. 2. uk. 256, Babu Majaa fii taswiyatil-qubur. (3) Sunan an-nasaiy, juz. 4. uk. 88, Babu Taswiyatil-qubur.

[34] Tah-dhibut-Tah-dhib. juz. 11, uk. 125

[35] Tah-dhibut-Tah-dhib. juz. 11, uk. 130

[36] Tah-dhibut-Tah-dhib. juz. 4, uk. 145

[37] Tah-dhibut-Tah-dhib. juz. 2, uk. 179

[38] Sharh Nahjul-Balagha ya Ibn Abil Hadid, juz. 9, uk. 99

[39] (1) Majma'uz-zawa'id, ya Al-Haithami, Juz. 9 uk 133.(2) At-Tirmidhi katika Sahihi yake, Juz. 2 uk 301. Muslim, katika Sahihi yake, (Mlango wa Imani)

[40] Al-Fiqhu Alal-Madhaahibil-arba'ah, juz. 1, uk.420

[41] Al-Fiqhu Alal-Madhaahibil-arba'ah, juz. 1, uk. 420

[42] Sahihi Muslim, juz. 3 Kitabul Janaiz, uk. 61

[43] Sharhu Sahihi Muslim Lin-Nawai.

[44] Al-Fiqhu Alal Madhahibi-l-arba'a, juz. 1, uk. 421

[45] Sahihi Muslim kitabul janaiz Juz. 3, uk. 62

[46] . As-Sunan At-Tirmidhi Juz. 2 uk. 208 Chapa ya Maktabatus Salafiyyah

[47] Sahih Ibn Majah, juz. 1 kitabul-Janaiz uk. 473

[48] Sahih An Nasa'i juz. 4 uk. 87-88

[49] Musnad Ahmad, juz. 3, uk. 295 na 332.

[50] Tah-dhibut-Tah-dhib, juz. 6 uk. 406

[51] Tah-dhibut-Tah-dhib

[52] Tah-dhibut-Tah-dhib

[53] Tahdhibut Tahdhib, katika maelezo juu ya Abuz-Zubair.

[54] Sahih Muslim, Juz. 3 uk. 62 chapa ya Misri.

[55] Sahih Ibn Majah, Juz. 1, uk. 474.

[56] Mizanul-I'tidal, juz. 3, uk. 476.

[57] (1) Musnad Ahmad, juz. 1, uk. 72 (2) Sahih Tirmidhi, juz. 2, uk. 139 (3) Tabaqat Bin Saad, juz. 2, uk. 71 na vinginevyo.

[58] Kitabu Riyadhil-Jannat kilichoandikwa na Muqbil ibn AI-Hadi Al-wadi/chapa ya Kuwait.

[59] Wafaul-wafa juz. 2 uk. 84.

[60] Wafaul-wafa juz. 2, uk. 96.