IBNU TAYMIYYAH NI NANI?

Bwana huyu alikuwa hi miongoni mwa wanachuoni wa Kihanbal, na alifariki mwaka 728 A.H. Jina lake ni Abu'l-'Abbas Ahmad bin 'Abdul-Halim, anayejulikana sana kwa jina la Ibnu Taymiyyah.

Kutokana na rai zake mbovu, na fikra zake zilizo kinyume na itikadi za Waislamu (pamoja na kuwepo tofauti ya kimadhehebu baina yao) Wanachuohi wa zama zake walikuwa wakimpinga na kutangaza vita dhidi yake, isitoshe walimhukumu kuwa hi fasiki (mharibifu wa Dini) na hasa pale alipoandika vitabu vinavyoeleza itikadi zake na akavisambaza miongonini mwa watu.

Vita vya kidini dhidi ya Ibnu Taymiyyah vilikuwa katika pande mbili muhimu:

Kwanza: Utunzi wa vitabu kupinga fikra zake potofu na kuzitengua kwa mujibu wa Qur'an na Sunna Tukufu ya Mtume [s]. Kwa mfano, tunataja baadhi ya vitabu vilivyotungwa na kutolewa dhidi ya Ibnu Taimiyyah:

1). Shifa's-Saqam Fi Ziyarati Qabril-Imam: kimeandikwa na Taqiyu'd Din Subaki.

2). Ad-Durrah Al-Mudiyyah Fi 'r-Raddi Ala Ibni Taimiyyah:

kimeandikwa na mtunzi wa kile cha kwanza.

3). Al-Maqalatu'l-Mardiyyah: kimetungwa na Qadi'l-Qudat Al-Malikiyyah Taqiyu'd-Din Abi 'Abdillah Al-Akhnai.

4) Najmu'l-Muhtadi wa Rajmul-Muqtadi, kilichoandikwa na Fakhr bin Muhammad Al-Qurashi.

5). Daf'us'h-Shubhah, kimeandikwa na Taqiyu'd-Din Al-Hisni.

6). At-Tuhfatu'l-Mukhtarah Fi'r Raddi Ala Munkiri'z-Ziyarah, kimeandikwa na Taju'd-Din.

Hivi ni baadhi ya vitabu vilivyoandikwa dhidi ya itikadi na rai mbovu za lbn Taimiyyah, na vilidhihirisha ubovu wa itikadi hizo pamoja na ubaya wake.

Upande wa pili kuhusu vita dhidi ya Ibn Taimiyyah, ni hujuma dhidi yake zilizokuwa zikifanywa na wanachuoni wa zama zake, ikiwa na pamoja na kutoa Fatwa kuwa yeye Ibn Taimiyyah hi fasiki, na wakati mwingine walimhukumu kuwa ni kafiri, pia wakiwatahadharisha watu juu ya uzushi aliouzusha katika dini tukufu ya Kiislamu.

Miongoni mwa Wanachuoni hao ni Qadi 'l-Qudat Al-Badru ibn Jama'ah wa Misri, yeye aliandikiwa suala kuhusu rai ya Ibn Taimiyyah juu ya kufanya ziyara ya kumzuru Mtume [s] kuwa haifai.

Qadi huyu aliandika jawabu lifuatalo:

"Kwa hakika kumzuru Mtume [s] ni jambo la Sunna iliyosisitizwa, na wanachuoni wameafikiana katika jambo hili; na yeyote anayeona kuwa kumzuru Mtume ni haramu, ni wajibu juu ya Wanachuoni kumkemea na kumkataza aondokane na mawazo ya aina hii; na iwapo hataachana na mawazo hayo, basi itakuwa ni lazima kumfunga na kumfedhehesha mbele za watu ili wasimfuate".

Qadi huyu wa Kishafi'i wa Misri siyo yeye peke yake aliyetoa Fatwa ya aina hii, bali Maqadhi wa Madhehebu ya Maliki na Hanbal nao walitoa Fatwa zinazofanana katika kuonyesha uovu wa Ibn Taimiyyah na wakahukumu kuwa yeye ni mpotevu.

Katika kutilia nguvu maelezo yaliyotangulia hivi punde, mwanachuoni aitwaye Adh-Dhahabi ambaye anazingatiwa kuwa miongoni mwa wanachuoni wakubwa katika Karne ya Nane Hijiriyya (alitunga vitabu vingi vya maana mno katika hadithi na wapokezi wa hadithi, na aliishi katika zama zile zile za Ibn Taimiyyah) alimuandikia Ibn Taimiyyah barua ya nasaha, akamkataza mambo yake hayo mabaya na alimfananisha (kutokana na uovu wake huo) kwa Al-Hajjaj Ath-Thaqafi katika uovu na upotevu wake.[27]

U'ipofikamwaka 728 Hijiriyya Ibn Taimiyyah alifariki katika gereza Ia Shamu, na mwanafunzi wake aitwaye Ibn Al-Qayyim akajaribu kuendeleza mwenendo wa mwalimu wake lakini hakufaulu.

Jambo la kuhuzunisha sana ni kwamba, shetani aliutega mtego wake kwa mara nyingine alipokuja Muhammad ibn AbdulWahab, hali ya kuwa amezibeba fikra za Ibn Taimiyyah zilizokuwa zimetoweka, akaafikiana yeye na kizazi cha Wasaudi kwamba, kila mmoja amsaidie mwenziwe, mmoja ashike mambo ya utawala na mwingine ashike mambo ya dini. Basi kipindi hiki upotovu ukawa umerudi na kueneza mizizi yake katika nchi ya Najdi, hivyo basi Uwahabi ukaenea katika nchi hiyo mfano wa maradhi mabaya ya Kansa katika mwili.

Watu wengi walihadaika na wakuanzisha kundi lao; inasikitisha sana kusema kwamba walitumia nembo ya Tauhidi ili kuwaua watu wa Tauhidi, na walimwaga damu za Waislamu kwa madai ya kuwapiga vita washirikina. Maelfu ya watu, wanaume na wanawake, wakubwa kwa wadogo, walijitolea muhanga dhidi ya uzushi huu.

Kwa hiyo mfarakano baina ya Waislamu ulipanuka; na likaongezeka dhehebu jipya kwenye madhehebu mengi ya Kiislamu yaliyokuwepo hapo kabla.

Na msiba huu mkubwa ulifikia kilele chake wakati miji miwili mitukufu ya Makka na Madina ilipoangukia mikononi mwa kundi hili ovu Ia Kiwahabi.

Hivyo basi, Mawahabi kutoka Najdi walijiimarisha kwa kupewa msaada na Serikali ya Uingereza ambayo kwa chuki yake dhidi ya Uislamu, sika zote ilikuwa ikikusudia kuigawa dola ya Kiislamu (iliyokuwa chini ya ukhalifa wa Kiturki), na kuifanya kuwa vijidola vidogo vidogo ambavyo vitatenganishwa na mipaka ya kijiografia.

Mawahabi walikusudia kuondoa kumbukumbu zote za Kiislamu zilizokuwepo Makka na Madina, na kuyabomoa makaburi ya Mawalli wa Mwenyezi Mungu na kukiondolea heshima kizazi cha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, pamoja na mambo mengine maovu na machafu (waliyoyatenda Mawahabi) ambayo hutetemesha nafsi ya Muislamu.

Baadhi ya wanahistoria wanasema: "Jambo la kwanza walilolifanya Mawahabi haraka haraka baada ya kuiteka Makka ni kuchukua na shoka na kuibomoa Mualla (makaburi ya Maqureish) ambapo palikuwa na qubba nyingi za watukufa wa Kiislamu.

Miongoni mwa Maqubba hayo lilikuwa ni qubba la Sayyidina Abdul-Mutalib ambaye ni babu yake Mtume [s], na qubba Ia Sayyidina Abu Talib (r.a.) ami yake Mtume, pia qubba la Bibi Khadija (r.a.) mkewe Mtume [s]. Vile vile walibomoa jengo alimozaliwa Mtume [s], na lile la Abubakr na mahala alipozaliwa Imam Ali [a], na wakabomoa Qubba la Zam-zam lililokuwa pembeni ya Al-Ka'bah; pia walifuatilia kila mahali zilipo kumbukumbu za watu wema wakazibomoa".

"Wakati wakibomoa walikuwa wakiimba na kupiga ngoma na kuyashutumu makaburi... kiasi yasemekana kwamba baadhi yao walilikojolea kaburi la Bwana Mpendwa.....!![28]

Amesema mwanachuoni mkubwa aitwaye As-Sayyid Sadru'd-Din As-Sadr (Mwenyezi Mungu amrehemu) kwamba:

"Naapa kwa 'umri wangu kwa hakika tukio la (kubomolewa makaburi ya) Baqii' huzifanya kuwa kongwe nyoyo za watoto wachanga."

"Huenda (tukio hili) likawa ndiyo mwanzo wa kufikwa na misiba (mfululizo) ikiwa (waislamu) hawatazinduliwa kutoka katika usingizi (walionao)".

"Je, hayuko Muislamu awezaye kuzichunga haki za Mtume, aliye kiongozi na muombezi wetu (kwa ajili ya Mwenyezi Mungu)?"

Amesema msha'iri mwingine:

"Wameangamia wajukuu wa Mayahudi (yaani kizazi cha Saudi) kwa matendo waliyoyatenda, hawakupata isipokuwa fedheha. Wameitweza heshima ya Mtume Muhammad kuhusu kizazi chake. Ole wao, watapata adhabu kali kwa kumuasi Mwenyezi Mungu mwenye nguvu. Wameyabomoa makaburi ya watu wema kutokana na chuki walizo nazo, kwa hakika wameangamia na wamemchukiza Mtume [s]."

Kufuatia kauli yake Mtume [s] kwamba:

"Pindi bid'ah itakapodhihiri, basi ni wajibu kwa Mwanachuoni kudhihirisha elimu yake (kupingana kukemea bid'ah hizo) na iwapo hatafanya hivyo, basi laana ya Mwenyezi Mungu imshukie mwanachuoni huyo". Kwa hiyo basi wanachuoni wengi wa Kishia na wale wa Kisunni walijitokeza (kupinga na kukemea uzushi wa Kiwahabi), kama tulivyokwisha taja hapo kabla, waliandika vitabu na kuvitawanya ili kumfedhehesha mtu huyu (Muhammad ibn Abdul Wahabi) ambaye alikuja kutekeleza malengo ya Waingereza, akiwa amevaa ngozi ya kondoo; na walizifichua siri zake kwa kuidhihirisha asili yake pia walizipinga na kuzikemea fikra zake mbaya.

Kitabu cha kwanza kutolewa dhidi ya Muhammad ibn Abdul Wahab ni "As-Sawa'iqul Ilahiyyah fi'r Raddi 'Al Wahabiyyah", kilichoandikwa na Sheikh Suleiman ambaye ni ndugu wa Muhammad Abdul Wahabi.

Kadhalika kwa upande wa Kishia, kitabu cha kwanza kutolewa dhidi ya Muhammad ibn Abdul-Wahabi ni "Man-haju 'r-Rashad" kilichoandikwa na mwanachuoni mkubwa aitwaye Sheikh Ja'far Kashif Al-Ghita' aliyefariki mwaka 1228 A.H.

Sheikh Kashif Al-Ghita' alikiandika kitabu hiki kuwa ni jawabu la barua iliyotumwa kwake na mmoja wa Maamiri wa Kisuud katika wakati huo aliyekuwa akiitwa Abdul-'Aziz ibn Su'ud.

Ndani ya kitabu hicho Sheikh Kashif Al-Ghita' ameudhihirisha wazi uwongo wa fikra za Muhammad ibn Abdul-Wahab, na amethibitisha ubatili (ubovu) wa fikra hizo kwa mujibu wa Qur'an na Sunna.

Kitabu hicho kilichapishwa katika mji mtukufu wa Najaf (Iraq) mwaka 1343.

Baadaye ulifuatia ukosoaji na kukemea itikadi za Kiwahabi katika nyakati mbali mbali, na vikatolewa vitabu mfululizo kimoja baada ya kingine mpaka katika zama zetu hizi. Na wakati huu Mawahabi wamezielekeza hujuma zao zenye hatari kubwa dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa kutumia mali zao nyingi ambazo kizazi cha Wasuud kinazipata kutokana na mauzo ya mafuta ambayo faida yake yote hurejea kwenye kizazi hiki cha Wasuud peke yao.

Watawala wavamizi wa Kisuud wametenga fungu kubwa Ia pesa zinazotokana na mauzo ya petroli kwa ajili ya kuyaeneza Madhehebu yao yaliyotoka Uingereza miongoni mwa Waislamu, na pia kuyaimarisha na kuyalinda madhehebu hayo.

Lau isingekuwa mali hizi nyingi, madhehebu haya duni yaisingeweza kabisa kudumu mpaka wakati huu. Kwa hakika wakoloni ndani ya madhehebu haya wamekipata walichokuwa wanakitafuta, nao wameyatumia kuwa ndiyo njia bora ya kuleta mgawanyiko baina ya Waislamu na kuvunja umoja wao na kuwafanya wapigane wao kwa wao.

Na Madhehebu haya yametekeleza na kutimiza malengo ya wakoloni waovu wa Kiingereza, kwani utaona kuwa yamezusha ugomvi kati ya Waislamu; imekuwa Mwislamu huyu humuona Mwislamu yule kuwa ni fasiki na mwingine naye humkufurisha. La hawla wala Quwwata Illa Billahil 'Aliyyil 'Azim.

Ewe msomaji mtukufu, kwa kweli tumekusudia katika kitabu hiki kuzichambua kwa utafiti wa kina itikadi za Kiwahabi, na tutafichua kiini chake mpaka ikudhihirikie kwamba itikadi za Waislamu zimetegemea Qur'an na Sunna tukufu, na kwamba itikadi za Kiwahabi zinakwenda kinyume cha Qur'an na Sunna ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu [s], nasi tumetumia njia ya kufupisha maelezo lakini yanayoeleweka.

[27] Takmilat As-Saif Asaqil, uk. 190.

[28] Kashful Ir-tiyabi kama alivyonakili kwa Al-Jabrati.