KIASI CHENYE MAKOSA

Tunakwenda sambamba na mwandishi huyu wa Kiwahabi katika kitabu chake kisichokuwa na maana, na tunamuona anamkosoa Imam Ali ibn Abi-Talib [a] kwa njia ya kutaka kufahamu na kuuliza sababu za kufanya haraka kumuuzulu Muawiyah mara tu Imam Ali [a] alipotawalia (Ukhalifa) na anajiuliza anasema: Kwa nini, kwa nini?

Bila shaka kilichompelekea kupinga ni kule kumlinganisha kwake Imam Ali [a] na watawala wenye kujali maslahi ambao hawafikiri isipokua maslahi yao binafsi na kuyatanguliza kuliko hukumu za sheria na wajibu aliowajibisha Mwenyezi Mungu, bali huupinda upande wa sheria kwa lengo la kulinda uongozi na utawala wao, basi kwa mujibu wao "lengo lao in kujisafishia wasiIa."

Fikra hii potofu ndiyo iliyomfanya mwandishi huyo wa Kiwahabi ampinge kiongozi wa wachamungu (ali [a]) kwa njia ya kuuliza na kutaka kufahamu. Naam, lau Imam Ali [a] angekuwa kama watawala wengine wanaojali maslahi yao, basi upinzani wa Wahabi huyu ungekuja hapa na angetakiwa awaache watu wapotofu na mafasid kama vile Muawiyah na mfano wake waendelee kuwatawala Waislamu kama zipendavyo nafsi zao za kishetani, lakini Imam Ali [a] siyo kiongozi wa aina hiyo ya watawala hao sivyo kabisa. Kwa hakika ni kiongozi mwenye Ikhlas, kwani anasema (Imam Ali [a]) akimjibu Mughira ibn Shu'bah na walio kama Mughira "Mimi sitaki Mwenyezi Mungu anione ni mwenye kuwafanya wanaopotosha kuwa ni wasaidizi (wangu)".[14]

Ewe msomaji mpendwa: Mpaka hapa tunafupisha maneno, na tunachokitarajia ni kwamba jibu hili la haraka tulilolileta limekuwekea wazi msimamo wa huyu Wahabi mwenye chuki dhidi ya kizazi cha Mtume Muhammad [s] na wafuasi wao na (na vile vile limekuwekea wazi) kufilisika kwake (Wahabi huyu) katika maarifa ya Dini na Itikadi za haki za Kiislamu na kukosea kwake na upotofu wake alioufanya kwa makusudi na riwaya zake za nongo. Nao wanachuoni wa dini na wanachuoni wa sheria ya haki watazishughulikia hujuma hizi mbaya za Kiwahabi, nasi tunataraji hivi karibuni apendapo Mwenyezi Mungu, litatolewa jawabu thabiti dhidi ya uzushi wa Wahabi huyu mpotofu mwenye kupotosha.

[14] Kitabu Waqiatis-Sifin uk. 58 Chapa ya Misri.