Uchunguzi Juu Ya Uwahhabi

Kimeandikwa na:Sheikh Ja'far Subhani

Kimetafsiriwa na : Musabbah Shaabani Mapinda

MUHTASARI

Afrika ya Mashariki imefaidi mazingira ya amani sana kiasi cha karne mbili zilizopita. Watu wa imani na itikadi zote waliishi pamoja kwa upendo na mapenzi. Kila mmoja akishiriki kwenye shughuli za mwenzake za kijamii na za Kidini. Ukiangalia kwenye Jumuiya za Kiislamu, wote wakihudhuria kwenye Misikiti ya kila mmoja, waliungana pamoja katika Maulidi na hafla za Muharram, na kupanua ushirikiano wao katika miradi ya kila mmoja. Kama Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi alivyosema katika hotuba moja ya hadhara; "Misikiti mingi ya Waislamu wa (Madhehebu ya) Shafi'i iliyoko Zanzibar na Pemba ilijengwa na kutolewa na Shia Ithna-ashariyya"

Hatimaye Wahhabi walianza Tabligh (Mahubiri) yao hapa. Badala ya kujaribu kuwaleta mapagani au wasio waislamu kwenye boma ya Uislamu, nia yao kabisa ilikuwa na bado inakaziwa katika kuwabadilisha Mashafii wawe Mawahabi. Kwa lengo hili, hujifanya kama wao ni Masunni, na kuchanganyika pamoja na Masunni. Mawahabi hao wamepanda mbegu ya fitina na chuki kati ya Madhehebu mbali mbali za Kiislamu, na hususan kati ya Sunni na Shia. Wanazungumza dhidi ya Shia, na kusambaza vitabu na vijitabu (vya mambo ya dini) dhidi ya itikadi ya Shia ambavyo vimejaa mambo ya uwongo na uzushi. Kishawishi chao kiko wazi, kwa kuwatenganisha Masunni na Mashia, wakitumaini kupata urahisi wa kuingia katika jamii ya Sunni na Misikiti yao, ingawaje tumaini hili lingali bado kukamilishwa katika Tanzania.

Hebu tuangalie katika mzizi wa uovu wa kampeni hii. Huenda hapo nyuma katika mwaka 1979, ambapo Mapinduzi ya Ki-Islamu yalipotokea katika (nchi ya) Iran, na watawala wa Kiwahaabi wa Saudia walihadharishwa vikali mno, hata kabla ya tukio la Mapinduzi ya Kiislamu, wakati Ayatullah al-'uzma al-Khomeini (R.A.) akiwa bado Najaf (Iraq). Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Saudi Arabia, akizungumza katika hadhara moja ya Waarabu, aliuonya ulimwengu wa Waarabu kwamba kama Khomeini ataruhusiwa kuendeleza harakati zake kutoka Iraq kama hapo nyuma, sio tu kwamba utawala wa Shaha utaangushwa, lakini, hali katika eneo lote vile vile itakuwa imetibuliwa. Hivyo wakaishinikiza Iraq kuweka vikwazo juu ya Khomeini kwa hofu ya kwamba, kama juhudi zake zitafanikiwa katika Iran, zitatingisha tawala zao wenyewe zisizo imara.

Haikushangaza kwamba mara tu Mapinduzi ya Kiislamu yalipoimarika nchini Iran, hawa Wahhabi wakuanza propoganda kali yenye chuki dhidi ya Khomeini, dhidi ya Iran na dhidi ya Ushia. Kalamu za kukodisha zikuanza mchakato kutoa vitabu, makala na vijitabu (vya mambo ya dini) dhidi ya Shia. Shia waliitwa Makafiri, na pengine mtu angeuliza: Kama ni Makafiri, basi kwa nini wanapewa viza kwa ajili ya Hija na Umra? Wairani waliitwa Majus (Waabudu Moto) kwa nini? Kwa sababu kabla ya kuja kwa Uislamu waliabudu moto. Kwa hoja hii nasi hatuna haki ya kuwaita Wahhabi Mushrikuna? Kwa sababu kabla ya kuja kwa Uislamu wata wa Najd walikuwa wakiabudu Masanamu.

Baadhi ya waajiriwa wao wa ngazi za juu walikuwa ni (marehemu) Ihsan Ilahi Zaheer wa Pakistan, na Manzoor Ahmad Nu'mani na Abul Hasan Ali Nadwi wa India. Sauti itokayo kwenye vinywa vyao ni katika watakiwayo na mabwana zao kuyasema, na jambia la uzayuni lilichovywa kwenye damu ya waislamu linatumika kama kalamu yao. Kitabu kinachoandikwa dhidi ya Shia na watumwa hawa, kwa miezi michache tu kinatarujumiwa katika lugha zote kubwa za ulimwengu wa Kiislamu; na hufanywa kipatikane kila mahali, kadhalika husambazwa bure miongoni mwa Mahujaji:

Nimeandika majibu kwa kitabu kimoja kama hicho, ambacho kilichapishwa katika mwaka 1994 nchini Tanzania na Marekani kwa jina la "Wahhabi's Fitna Exposed". Kimevunja habari za uwongo wao wote na masingizio yasiyo na msingi dhidi ya Shia. Tarjuma yake ya Kiswahili (Fitina za Wahhabi Zafichuliwa) imechapishwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania, Dar es Salaam.

Bado inahisiwa haja ya kuweko kitabu katika sehemu hizi za ulimwengu ambacho kitaangalia katika mawazo yote na mafundisho ya Uwahhabi na kushughulika nayo katika mwanga wa Qur'an na Hadithi, ili kufichua uwongo na itikadi yao na mtizamo wao juu ya vita vitakatifu vya Kiislamu.

Ahlul-Bayt [a] Assembly of Tanzania, ina furaha kutoa kitabu kama hiki kwa wata wazungumzao Kiswahili. Nimechagua kwa ajili ya madhumuni haya kitabu (kitwacho) "Al-Wahhabiyah Fil-Mizan" kilichoandikwa na Mwanachuoni mashuhuri wa dini na mtunzi, aitwaye Shaykh Ja'far Subhani, Profesa wa Chuo cha dini Qum (Iran). Kitabu hiki kwa hakika (bila kupendelea) kinaangalia katika hoja zote zilizotolewa na Wahhabi na kutahini kusihi kwake kutoka kwenye Qur'an na Sunnah.

Shaykh Musabbah Shaabani Mapinda, wa Dar-es-Salaam kwa ushauri wangu amefanya tarjuma ya kitabu hiki kutoka Kiarabu kwenda kwenye Kiswahili, kinachoitwa "Uchunguzi juu ya Uwahhabi". Nimekikagua kwa utaratibu ili kuhakikisha kwamba mafuhumu ya Kiarabu kwa uaminifu na ukweli yametolewa kwenda kwenye Kiswahili.

Hiki ni kitabu cha kwanza cha "Ahlul-Bayt (A.S.) Assembly of Tanzania", na nina fahari kwa kushirikishwa katika kila hatua. Namuomba Allah Subhanahu Wa Ta'ala atoe malipo yake kwa Mtunzi, mtarjumi na wale wote ambao wamesaidia katika kuchapishwa kwake kwa njia yoyote ile.

Wa Ma Tawfeeq Illa Billah

Syed Saeed Akhtar Rizvi