JESHI LA USAMA

Katika mwaka wa kumi Hijjra, Mtukufu Mtume (s.a.w.) alipeleka jeshi kwenda kupigana Roma. Katika jeshi hilo Mtume aliamuru liongozwe na Usama bin Zaid akasema:- "Nenda ukapigane alikouliwa baba yako".

Uteuzi huu Masahaba haukuwapendeza, kwa hiyo walisikika wakipinga amri hiyo wakisema: "Itakuwaje mtoto mdogo huyu apewe madaraka makubwa juu yetu?

Ilipomfikia habari hii Mtume (s.a.w.) aliwaambia: "Nimesikia lawama zenu nilivyomtawalisha Usama katika jeshi hili, sioni ajabu, maana mlikwisha nilaumu zamani nilipomtawalisha baba yake kabla yake. Wallahi baba yake alikuwa ni mtu aliyefaa kushika uongozi wa jeshi hilo, kama ambavyo mtoto huyu anastahiki kabisa uongozi wa jeshi hili".

Mtume (s.a.w.) akasisitiza watu wote isipokuwa Ali, waende na jeshi Ia Usama akisema: "Andaeni jeshi la Usama, Mwenyezi Mungu amlaani atakaebaki asiende na jeshi hilo".

Taz: AI-miIalu Wannihal J.1 Uk. 20

Alipofika nje kidogo ya mji, Usama aliweka kambi ili watu wakusanyike pamoja tayari kwa msafara. Hapo Abubakar akaanza kumahawishi Usama kwamba asipeleke hilo jeshi kwa sababu haiwezekani kutoka na kumwacha Mtume (s.a.w.) akiwa hali hii ya maradhi.

Abubakar alikuwa ni mtu mzima kwa umri kuliko Usama, takriban umri wa Abubakar wakati huo si chini ya miaka hamsini, na umri wa Usama si zaidi ya miaka Kumi na Tisa.

Abubakar alitumia hila mbali mbali kwa kuendesha majadiliano kati yake na kijana mdogo Usama, baina ya jeshi liende kupigana Roma kama alivyoamuru Mtume, au lisiende kama anavyotaka Abubakar. Hali hii ilichelewesha na kuchukua muda mrefu bila ya kwenda alikoamrisha Mtume, mpaka mauti yakamfikia akafa Mtume (s.a.w.).

Mwenyezi Mungu anasema: "Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapohukumu jambo lo lote wawe na khiari katika hukumu hiyo. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotevu ulio wazi". 33:36

Amri aliyohukumu Mtume hapa ni Usama kuwa Mkuu wa jeshi litakalokwenda kupigana Roma, matoke ni kwamba; baadhi ya Waislamu hawakutii amri hiyo.

Katika Aya, iliposema: "Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotevu ulio wazi."

Hapa Abubakr na Umar wanapatikana na hatia ya kumuasi Mtume (s.a.w.), na mwenye kumuasi Mtume amemuasi Mwenyezi Mungu.