QURAN NA AHLUL BAIT

Imepokewa kutoka kwa Sahaba Zaid bin Arqam: Amesema Mtume (s.a.w.):- "Mimi ninakuachieni vizito viwili ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea baada yangu, Quran na AhIul Bait wangu, viwili hivi havitaachana mpaka vitakaponifikia katika Haudh."

Taz: Tafsir Ibn Kathir J.4 Uk. 122
Tafsirul Khazin J.1 Uk. 4
Tarikh Bughdad J.8 Uk. 442
Sahihi Muslim J.4 Uk. 1873
Sahihi Tirmidh J.2 Uk. 308
Jamiul Usul J.1 Uk. 187
AIbidayatu Wannihaya J.7 Uk. 362
Majmauz Zawaid J.9 Uk. 163

Hadithi hii inathibitisha kuwa baada ya kuondoka Mtume watakaoshika mahala pake ni Ahlul Bait (a.s.) ambao tumekwisha waona katika tukio Ia "KISAA" na katika tukio la "MUBAHALA"

Mwenyezi Mungu ameamrisha kufuata uongozi wao aliposema: "Shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msitengane". 3:103

Tamko la kamba hapa ni AHLUL BAIT" na hapa tutaonyesha maneno ya Imam Shaafy "Na nilipowaona watu Madhehebu yao yamewapeleka katika bahari yao ya upotovu na ujinga, nikapanda kwa jina Ia Mwenyezi Mungu katika meli yenye kuokoa, nao ni watu wa nyumba ya Mtume mwisho wa Mitume. Na nikaishika kamba ya Mwenyezi Mungu nayo ni kuwatawalisha (Ahlul Bait) kama tulivyoamuriwa kushikamana na kamba, watakapo farakana katika dini makundi sabini na kidogo kama ilivyokuja katika Hadithi. Na asipatikane wa kuokoka miongoni mwao isipokuwa kundi moja, niambieni ni kundi gani hilo enyi wenye akili na maarifa je! Katika makundi yatakayoangamia mojawaponi ni lile kundi la watu wa Muhammad? Au wao ni katika kundi litakalo salimika, niambieni. Ikiwa utasema kundi la Muhammad ni katika kundi litakalookoka, basi huo ni msimamo wa kweli, na ukisema kundi hilo ni katika makundi yatayoangamia bila shaka umepotosha uadilifu, basi niachie Ali awe kiongozi wangu na kizazi chake, na wewe bakia katika mapambo ya ulimwengu."

Imam Shaafy hapa anatukumbusha tamko muhimu Ia Mtukufu Mtume (s.a.w.) aliposema: "Mfano wa Ahlul Bait wangu ni kama mfano wa Meli ya Nuhu, atakaepanda humo ataokoka, na atakaebaki nje atazama".

Taz: Manaqib Ali Uk. 132
Mustadrakus Sahihain J.2 Uk. 343
Majmauz Zawaid J.9 Uk. 168
Kanzul Ummal J.6 Uk. 216
Hilyatul Awliyaa J.4 Uk. 306

Mwenyezi Mungu anasema: "Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na Ulul'amri katika nyinyi." 4:59

Katika Aya hii kuna mambo matatu muhimu:

  1. Kumtii Mwenyezi Mungu (b) Kumtii Mtume (c) Kuwatii Ulul'amri.
  2. Kumtii Mwenyezi Mungu, maana yake ni kushika amri zake na kuacha makatazo yake. Kama ambavyo; kumtii Mtume (s.a.w.) maana yake ni kufuata uongozi wake. Katika Aya hii mwenyezi Mungu anaamrisha wa atiiwe Ulul'amri na yeyote ambaye Mwenyezi Mungu anaamrisha atiiwe lazima awe maasum (Mwenye kuhifadhiwa na makosa). Basi, lazima Ulul'amri waliotajwa katika Aya hii wawe Maasum.

    Naam; kidogo tujikumbushe lile tukio Ia "KISAA" Mwenyezi Mungu aliposema: "Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni sana sana." 33:33

    Hapa tutaangalia Nukta mbili katika Aya hii:

    (a) AR'RIJSU = Uchafu, matendo mabaya, Haramu Laana, Kufru, Adhabu.

    Taz: Al-Muujamal wasit (kamusi)

    Kwa mantik hii utaona kuwa: Ahlul Bait, Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na matendo mabaya.

    Amewaepusha haramu, hawana Iaana, wanarehema, amewaondolea kufru na adhabu.

  3. At'tuhru: Kutokuwa na uchafu wa aina yoyote.

Taz: Al-muujamal wasit (Kamusi)

Kwa hiyo; Ahlul Bait (a.s.) hawana uchafu wa aina yo yote. Natija inaonyesha kuwa: Ahlul Bait ni Watakatifu na ni Maasum.