UTANGULIZI

Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwafikisha mara nyingine kukamilisha kuandika kitabu hiki, baada ya kitabu chetu:- "Mut'a ndoa sahihi."

Mambo yanayoweza kuamsha misimamo ya watu na kuleta msukumo mpya katika kumwandaa binadamu ili apige hatua mbele, ni kujua habari za watukufu wao waliotangulia. Kwa sababu kujua habari za watangulizi wetu ni mizani ya kutupimia sisi tunaokuja baada yao.

Katika kitabu hiki, nimetaja mambo ambayo ingawa yanajulikna na wengi, lakini ni mageni katika kusema. Wanaoyajua kuwa ni kweli si kidogo, lakini wengi wanaogopa kuyasema au wametiliwa itikadi potovu kuwa hayafai kusema. Bila shaka yakionekana katika kitabu hiki itakuwa dhambi kubwa kwao. Sisi nasi tunaamini kuwa Haki ni lazima isemwe, sawa sawa itawaridhi watu au haitawaridhi.

"NA LAU HAKI INGEFUATA MAPENZI YAO BASI MBINGU NA NCHI ZINGEHARIBIKA." 23:71

Ninawashukuru wote waliokipitia Kitabu hiki kukisahihisha, na wakanipa maoni yao yenye thamani kubwa. Mwenyezi Mungu awalipe malipo mema duniani na akhera.

OMARI JUMAA MAYUNGA