SHIA WALIMU WA SUNNI

Kipimo cha kumpima mtu kuwa anafaa kupokea kwake mafundisho ya dini kwa salama na sahihi ni kutirnia sharti tano hizi:

(a) Uwepo uadilifu wa mapokezi, maana yake kila mpokezi katika wapokezi wake awe Mwislamu, aliye balighi, asiwe fasiq na asiwe muongo.

(b) Yakamilike mafungamano ya Sanad, maana yake kila mpokezi katika wapokezi wake awe amepokea moja kwa moja mpaka kufikilia kwa Mtume (s.a.w.).

(c) Kuwepo udhibiti wa mapokezi, yaani kila mpokezi katika wapokezi wake awe mwenye kudhibiti vyema, sawasawa iwe kwa kuhifadhi moyoni au kuhifadhi kwa maandiko.

(d) Kukosekane Shadh, yaani hadithi isiwe Shadh. Na maana ya Shadh ni: Kupinga hoja au msimamo wa walio wengi wenye kutegemeka zaidi.

(e) Kukosekana aibu, maana yake hadithi isiwe na aibu. Yaani mmoja wa wapokezi wa hadithi hiyo asijulikane na aibu yo yote.

Sharti tano hizi zinapokamilika katika hadithi, huwa hadithi hiyo ni sahihi. Na hadithi kama hizi zikikusanywa katika kitabu, hujulikana kitabu hicho kuwa ni sahihi. Ndiyo maana kwa ndugu zetu Masunni kuna vitabu viwili vilivyokusanya hadithi zilizotimiza sharti hizo. Kwa pamoja Masunni wamekubaliana kuwa: Baada ya Quran Tukufu, kitabu kilicho sahihi mno ni Bukhari na Muslim".

Taz: Sharhus Sahih Muslim J. 1 Uk. 14
Mustalahul Hadithi Uk. 36

Sasa; nitataja majina ya watu waliomo katika Sanad za hadithi zilizomo ndani ya vitabu viwili hivi (Bukhari na Muslim). Kisha msomaji atazame sharti tano tulizokwishazitaja, na watu hawa kuwamo katika Sanad za hadithi hizi sahihi.

(1) Aban bin Taghlib Alkufy. Huyu ni Shia. Imam Ahmad bin Hanbal, Yahya bin Muin, Abu Hatim na Ibn A'diyy. Hawa wamemthibitisha kuwa: "Ni mkweli anategemeka katika hadithi"

Walipoulizwa: Kwa nini kumkubalisha Shia? Na hali mtu anapimwa kwa sharti tano ndipo akubalike na Shia hapati sharti hizo! Pakajibiwa: "Kama zitakataliwa hadithi za hawa (Mashia) basi zitapotea hadithi zote za Mtume"

Taz: Mizanul Itidal J. 1 Uk. 5

Imam Muslim ametegemea hadithi zake nyingi.

(2) Ismail bin Aban Al'azdy Alkufy. Huyu ni Shia. Imam Bukhari amesoma kwake, na akamtaja kuwa: Ismail ni mkweli sana anategemeka katika hadithi.

(4) Ismail bin Abdir Rahman bin Abi Karimah Alkufy. Huyu ni Shia. Huyu ni Mfassir wa Quran, na anayejulikana sana kwa jina la ASSUDY katika tafsir mbali mbali za Kisunni.

Yeye alikuwa akimtukana Abubakr na Umar, hata hivyo amesema Imam Ahmad bin Hanbal, Ibn Addiyy, Yahya Alqattan, na Yahya bin Said kuwa: "Ismail bin Abdir Rahman ni mkweli anategemeka katika hadithi".

(5) Khalid bin Mukhlad Alkufy. Huyu ni Shia. Imam Bukhari amesoma kwake. Alikuwa akiwaalani (baadhi ya Masahaba) Imam Bukhari na Imam Muslim wametegemea hadithi nyingi kutoka kwake.

(6) Ali bin AI'juud. Huyu ni Shia. Imam Bukhari amesoma kwake, hadithi nyingi ametegemea kutoka kwa Ali bin Al'juud.

(7) Hisham bin A'mmar. Huyu ni Shia. Imam Bukhari amesoma kwake, na hadithi nyingi zilizomo katika kitabu chake amepokea kwa Hisham bin A'mmar.

(8) U'beidullah bin Musa Alkufy. Huyu ni Shia. Imam Bukhari

amesoma kwake na kupokea hadithi nyingi.

(9) Said bin Ash'wa'a. Huyu ni Shia. Imam Muslim na Imam

Bukhari wametegemea hadithi zake.

(10) Alhakam bin U'taiba Alkufy. Huyu ni Shia. Imam Bukhari na

Imam Muslim wametegemea hadithi zake nyingi.

Hapa nimeshughulikia tu kuonyesha baadhi ya watu ambao majina yao katika Sanad za Hadithi zilizomo katika Sahihi mbili, Bukhari na Muslim. Nikizingatia lile kongamano la Masunni kuwa: "Baada ya Quran Tukufu, kitabu kilicho sahihi mno ni Bukhari na Muslim".

Ni vizuri nitaje hapa tamko la Maimam wa Kisunni walioshughulika kwa undani kuchambua fani ya Hadithi kuwa: Ikiwa zitakatiliwa hadithi za Mashia, basi hadithi zote za Mtume zitapotea".

Kwa maneno mengine: "Kumtenga Shia katika Uislamu ni kufuta hadithi za Mtume, ukifuta hadithi za Mtume katika Uislamu ni kufuta Uislamu".

"NI NINI BASI BAADA YA HAKI ISOKUWA UPOTOVU?!" QURAN 10:32