ANNASAI

Jina lake ni: Abu Abdur Rahman Ahmad bin Shua'ib Annasai. Alikuwa Imam wa Hadith katika zama zake, na kitabu chake ni mojawapo ya Sihahi sita zinazotegemeka sana kwa ndugu zetu Masunni. Alipoandika Kitabu: "Alkhasais" kilichotaja ubora wa Imam Ali (a.s.), Annasai anasema: "Nilipofika Damashq (Syria) na nikawaona wapinzani wengi wa Ali, nikaandika Kitabu nikitaraji kuwa watakapokisoma Mwenyezi Mungu atawaongoa"

Akaulizwa: "Kwa nini hakuandika fadhaili za Muawia"? Annasai akawajibu: "Niandike fadhla gani!! Sina ninayoijuwa isipokuwa moja tu, Mtume (s.a.w.) aliyomwambia: "Ee! Mola, usilishibishe tumbo lake". Hapo akashambuliwa na kupigwa ndani ya Msikiti, kisha akatolewa akatupwa katika kijiji cha Ramala.

Imam Annasai amekufa kwa kipigo hicho!!

Taz: Al'bidayatu Wannihaya J.11 Uk. 132
Tadhkiratul Hufadh J.1 Uk. 198