MASAHABA WAOVU

Mwenyezi Mungu anasema:

"Na wanamuapa Mwenyezi Mungu kuwa wao ni pamoja nanyi hali wao si pamoja nanyi bali wao watu wanaogopa. Kama wangelipata pa kukimbilia mapangoni au mahala pengine pa kuingia, bila shaka wangeligeukia huko hali ya kukimbia". 9:56-57

"Na wanasema: Tunatii, lakini wanapotoka mbele yako, kundi moja miongoni mwao (Masahaba) linashauriana usiku kinyume cha yale uliyoyasema. Na Mwenyezi Mungu huyaandika wanayoshauriana usiku, basi waachilie mbali na umtegemee Mwenyezi Mungu na atosha Mwenyezi Mungu kuwa mlinzi." 4:81

"Na katika mabedui wanaokaa pembezoni mwenu kuna wanafiki, na katika wenyeji wa Madina pia (wako wanafiki) wamebobea katika unafiki. (Wewe Muhammad) huwajui, sisi tunawajua, hivi karibuni tutawaadhibu mara mbili kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa". 9:101

"(Masahaba) wanapoiona biashara au mchezo wanavikimbilia, na wanakuacha umesimama (peke yako unakhutubu ukiwa na Masahaba wachache)" 62:11

Siku ya Kiama Mtume (s.a.w.) atawaona baadhi ya Masahaba waki pelekwa motoni aseme: "Sahaba wangu ataambiwa: Wewe hujui waliyoyazua baada yako, wao walirudi nyuma (ukafirini) tokea ulivyowaacha. Nitasema kama alivyosema Mja mwema, nilikuwa nikiyaona nilipokuwa nao, uliponifisha, wewe umekuwa ndiye mwangalizi wao na wewe ni shahidi juu ya kila kitu. Ikiwa utawaadhibu hao ni waja wako, na kama utawasamehe bila shaka wewe tu Mwenye ushindi Mwenye hekima".

Taz: Tafsirul Qurtubi J.6 Uk. 377
Mukhtasar Tafsir lbn Kathir J.1 Uk. 565
Zadul Masir J. 2 Uk. 465
Tafsirul Maragh J. 7 Uk. 65

Wakati wa Mtume (s.a.w.) Masahaba walikuwa wakigombana na kutukanana, na hilo halikuathir chochote heshima yao. Bali la muhimu ilikuwa kusuluhisha kati yao, na mara moja walitukanana na kupigana mbeleya Mtume (s.a.w.).

Taz: Tafsirul Qurtubi J. 16 Uk. 315
Sahihi Muslim J. 3 Uk. 1424

Mtu mmoja alimtukana Abubakr na Mtume (s.a.w.) yupo kakaa, akawa anatabasam.

Taz: Hayatus Sahaba J. 2 Uk. 414

Umar Ibn Khattab alimpiga bakora Abu Huraira mpaka akamtoa damu, kwa sababu ya ubadhirifu aliofanya Bahrain.

Taz: Tarikh Ibn Kathir J.8 Uk.113
Shaikhul Mudhira Uk. 80

Quddama bin Madh'un, ni katika Waislamu wa kwanza kwanza, amewahi kuhamia Habash na amepigana vita vya Badr na vya Uhud pamoja na Mtume (s.a.w.). Pia ni shemeji ya Umar ibn Khattab, bwana huyu alikuwa mlevi na Umar alimpiga hadd.

Taz: Al'Isaba J. 3 Uk. 228
Usudul Ghaba J.4 Uk. 198

Abdur Rahman bin Udais Al'balawiyyu, huyu alikuwapo katika Baia'tur ridhwan na alishiriki pamoja na wenziwe. Lakini, yeye ndiye aliyeuongoza msafara uliokwenda kuzingira nyumba ya Uthman bin Affan wakamuua.

Taz: Tarikhut Tabari J.3 Uk. 411
Usudul Ghaba J. 3 Uk.309

Tha'alaba bin Hatib bin Umar bin Umayya alipigana vita vya Badr na vya Uhud. Lakini alizuia zaka ya mali yake, na Mwenyezi Mungu akateremsha Aya ya kumlaumu sana.

Taz: Tafsir Ibn Kathir J.2 Uk. 388
Fat'hul Qadir J.2 Uk. 367

Al-walid bin Uqba, Mwenyezi Mungu amemwita FASIQ, soma Aya 6 ya Sura 49. Tena Sahaba huyu alikuwa mlevi, aliwekwa na Uthman bin Affan kuwa gavana wake katika Mkoa wa Kuufa.

Siku moja alilewa alfajiri na mapema akasalisha sala ya asubuhi, akapiga rakaa nne, akageuka kuwauliza: Nikuongezeni?

Taz: Tarikh Ibn Athir J.3 Uk. 53
Usudul Ghaba J.5 Uk.91
AI'bidayatu Wannihaya J.8 Uk. 216

Mwana Aisha, alisujudu sijda ya kumshukuru Mwenyezi Mungu mara alipopata habari kuwa: Imam Ali (a.s.) ameuliwa.

Taz: Maqatilut Talibina Uk. 27