UBORA WA SAHABA KWA ITIKADI ZA SUNNI

"Bora ya umati wangu ni karne yangu kisha wanaofuatia, kisha watakaofuata, kisha watakuja watu viapo vyao vitakuwa mbelembele kuliko kuonyehsa ushahidi wao. Na watatoa ushahidi kabla ya kuombwa hilo."[1]

"Msiwatukane Masahaba wangu, Wallahi laiti atatoa dhahabu mmoja wenu iliyo kubwa kama mlima wa Uhud, hawezi kufikia ubora wao"[2]

"Nilimuuliza Mola wangu kuhusu Masahaba wangu watakao khitilafiana baada yangu Mwenyezi Mungu akaniambia: Ewe Muhammad, Sahaba wako kwangu mimi ni kama nyota zilizoko juu, baadhi yake zinang'aa sana kuliko zingine. Basi atakafuata lolote walilonalo katika khitilafu zao, huyo kwangu mimi yuko katika uongofu"[3]

"Mwenyezi Mungu amenichagulia mimi na akachagua Masahaba wangu, akawafanya (baadhi yao) wakwe zangu (baadhi yao) Ansar wangu, na katika Zama za mwisho watatokea watu watawadharau. Sikilizeni msiwaoze wala msioe kwao, sikilizeni msisali nao wala msiwasalie (wakifa) imewashukia laana"[4]

[1] Mara baada ya kufariki Mtume (s.a.w.) Masahaba wengi walikimbilia kwenye ukumbi wa Bani Saida. Baada ya mabishano makali na kushutumiana, hatimae Abubakr akachaguliwa kwa taabu. Kwa kitendo hiki Abubakr na Umar hawakumzika Mtume (s.a.w.).

Ilipokuwa tarehe kumi na nane mfungo tatu mwaka thalathini na tano Hijria Uthman bin Affan aliuliwa na Masahaba.

Taz: Tarikhut Tabari J.3 U.K 411.

Katika mwaka wa arobaini Imam Ali (a.s.) akauliwa. Kisha Muawia katika mwaka wa arobaini na moja aliamrisha watu wote wamlaani Imam Ali.

Taz: Tarikhut Tabari J.4 Uk. 188

[2] Kwa sababu hii Muawia akaanza kumlaani Imam Ali (a.s.) mpaka alipokuja Umar Abdul Azizi.

[3] Mtume (s.a.w.) alisema kumwambia Ammar bin Yasir: "Utauliwa na kundi potovu".

Taz: Sahih Bukhari Kitabul Jihad

Sahihut Tirimidhi J.5 Uk. 333

Mustadrakul Hakim J. 2 Uk. 148

Tarikh Ibn Athir J. 3 Uk. 310

Ammar ameuliwa katika vita vya Siffin akiwa upande wa Imam Ali.

Kwa hiyo basi, inaonyesha kuwa watu waliosimama dhidi ya Imam Ali walikuwa watu wa motoni, ambao walikuwa: Muawia na Masahaba wengine. Lakini hapa tunaambiwa kuwa wote hawa ni wema, waliokuwa upande wa Imam Ali (a.s.) na pia waliokuwa dhidi yake wote wema!!

[4] Inajulikana kuwa: Kuwaua Masahaba kama Ammar bin Yasir, au kuwapiga, kama Abdullah bin Masuud (ambaye Uthman bin Affan aliamuru Abdullah bin Zam'a ampige Abdullah bin Masuud; Abdullah bin Zam'a alimpigiza chini Abdullah bin Masuud mpaka ukavunjika ubavu mmoja). Au kuwafukuza Madina kama Abudharri yote hayo si kitu, lakini kuwadharau ni dhambi.