MASAHABA WEMA

Mwenyezi Mungu anasema:

"Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewawia radhi waumini walipofu ngamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo mioyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao na akawalipa ushindi wa karibu" 48:18

"Na waIiotangulia wa kwanza katika wahajiri na Ansar na wale waliofuata kwa ihsani. Mwenyezi Mungu amewaridhia nao pia wameridhia na amewaandalia bustani zipitazo mito chini yao, kukaa humo milele huku ndiko kufaulu kukubwa" 9:100

"Ni kwa mafukara waliohama, ambao walifukuzwa katika nyumba zao na mali zao wakitafuta fadhila za Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hao ndio wa kweli. Na wale waliofanya maskani na kushika imani kabla ya hao, wanawapenda waliohamia kwao wala hawapati dhiki mioyoni mwao kwa hayo waliopewa. Na wanawapendelea kuliko nafsi zao ingawa wenyewe wana hali duni, na aepushwae na ubahili wa nafsi yake basi hao ndio wenye kufaulu". 59:8-9