SAHABA

Amesema Ibn Hajar katika utangulizi kwa Kitabu chake: "Al'isaba" kuwa:

"Sahaba ni mtu aliyekutana na Mtume (s.a.w.) akamwamini na akafa katika imani hiyo. Hapa anaingia aliyeishi naye kwa muda mfupi aliyepokea kwake au hakupokea, vile vile anaingia aliyepigana pamoja naye au hakupigana, aliyemuona japo mara moja au hakumuona, kwa sababu ya matatizo fulani kama upofu".

Hata hivyo suala Ia Sahaba linagawanyika makundi mawili:

(a) Kwamba; Masahaba wote ni waadilifu, hawana makosa, huu ni msimamo wa MASUNNI

b) Kwamba; Masahaba kama watu wengine kuna walio waadilifu, na kuna wanafiki na mafasiq. Hupimwa kwa mujibu wa matendo yao, mwema atalipwa kwa wema wake na muovu ataadhibiwa kwa mabaya yake. Huu ni msimamo wa MASHIA ITHNAA'SHAR.