TUKIO LA SIFFIN

Imam Ali (a.s.) baada ya kurudi kutoka Basra, alimpeleka Jariri nin Abdillah kwa Muawia kumtaka atoe kiapo cha utiifu katika serikali yake. Muawia hakukubali. Kisha Muawia alitoka na wapiganaji laki moja na ishirini elfu. Imam Ali alikwenda Siffin akiwa na wapiganaji elfu tisini.

Watu wa Sham wakauliwa sabini elfu, na watu wa Iraq wakauliwa ishirini na tano elfu akiwemo Ammar bin Yasir.

Taz: Tadhkiratul Khawas Uk. 81-82

Zubeid bin Abdukhawalan, alikuwa katika majeshi ya Muawia.

Alipoona Ammar ameuliwa na majeshi yao, akajisalimisha katika majeshi ya Imam Ali (a.s.) na alipoulizwa alisema: "Nimesikia kuwa Mtume amesema: Ammar atauliwa na kundi potovu, wakati huo Ammar atakuwa katika haki, basi yeyote ambaye hatamsaidia siku hiyo si pamoja nami". Hivyo waliomuua Ammar ni sisi basi sisi ni kundi potovu, nimeamua kujisalimisha katika kundi la amani.