TUKIO LA JAMAL

Jamal: Ni ngamia. Inaposemwa: Tukio la Ngamia, maana yake; yule ngamia aliyempanda Mwana Aisha akaenda nae katika uwanja wa Basra.

Katika mwaka wa thelathini na sita Hijria, Talha na Zubeir walimuomba ruhusa Imam Ali kwenda Makka kwa ajili ya Umra. Walipokuwa njiani wakakutana na Mwana Aisha akawauliza habari za Uthman, wakamwambia kuwa Uthman ameuliwa. Mwana Aisha akasema "Muuweni na'athala hakika amekufuru".

Taz: Tarikh Ibn Athir J.3 Uk. 206
Lisanul Arab J.14 Uk. 193
Assiratul Halabiyya J.2 Uk. 286

Na'athala: Maana yake; Myahudi mmoja aliyekuwa akushi Madina, ambaye alikuwa na manywele mwili mzima. Mwana Aisha anamfananisha Uthman na myahudi yule.

Imam Ali (a.s.) aliposhika uongozi, Mwana Aisha alitoka akilia na huku akisema "Uthman ameuliwa kwa dhulma" Ammar bin Yasir akamuuliza:

"Ni vipi wewe jana ulikuwa ukimlaani na leo hii unamlilia".

Taz: Ansabul Ashraf J.5 Uk 75
Tarikh Ibn Asakir J.7 Uk. 319

Mwana Aisha alipokuwa njiani kuelekea Basra alifika mahala akabwekewa na mbwa wengi. Mwana Aisha alishtuka akauliza hapo ni mahala gani? Akaambiwa: "Ni Hauab" Mwana Aisha akalalamika sana akataka arudishwe nyumbani, jamaa wakamgomea. Alipoulizwa kwa nini kulalamika hivyo akajibu: "Nimemsikia Mtume (s.a.w.) akituambia: Nani katika nyinyi atabwekewa mbwa wa Hauab"?

Imam Ali (a.s.) alipigana na majeshi yakiongozwa na Mwana Aisha, Talha, na Zubeir watu kiasi elfu kumi walikufa katika vita hivyo.

Taz. Tarikhut Tabari J.3 Uk. 543

Baada ya kumalizika vita, Imam Ali (a.s.) alimpeleka Abdullah lbn Abbas kwa Mwana Aisha kumuamuru amrudishe Madina. Akapanga kikosi cha wapiganaji thelathini akiwamo ndugu yake Abdur Rahman bin Abi Bakr. Na mabibi watukufu wa Basra ishirini, waliovalia sare za jeshi la Ali pamoja na silaha. Akawausia kuwa; "Wasimuonyeshe Mwana Aisha kuwa wao ni wanawake".

Imam Ali akaamuru mara moja jeshi hilo kumrudisha Mwana Aisha Madina.

Tukio Ia Jamal, Mwana Aisha hakulisahau maishani mwake, na kila alipolikumbuka alikuwa akijuta akisema: "Laiti ningelikuwa uchafu uliotupwa".

Taz: Tadhkiratul Khawas Uk. 81