IMAM ALl

Imam Ali (a.s.) ni; "Ndugu ya Mtume na Wasii wake na Khalifa wake kwa Waislamu wote".

Taz: Tarikhut Tabari J.2 Uk. 63
Tarikh Ibn Athir J.2 Uk. 62
Tarikh lbn Asakir J.1 Uk. 85
Assiratul Halabiyya J.1 Uk. 311
Musnad Ahmad J.5 Uk. 41
Kanzul Ummal J.15 Uk. 115
Kifayatut Talibi Uk. 620
Mizanul Itidal J.2 Uk. 273
Majmauz Zawaid J.9 Uk. 113
Manaqib Ali Uk. 200

Maana ya "WASII" ni mtu anayesimamia kuendesha mambo ya mtu. Kwa kuwa Ali ni Wasii wa Mtume (s.a.w.) maana yake Ali atasimamia na kuendesha mambo ya Waislamu baada ya Mtume (s.a.w.).

Maana ya 'KHALIFA" ni mtu anayekuja kukaa mahala pa mtu baada yake.

Kwa kuwa Ali ni Khalifa wa Mtume (s.a.w.) manna yake Ali atashika mahala pa Mtume (s.a.w.) baada yake.

Mtume (s.a.w.) amesema: "Wewe (Ali) nafasi yako uliyonayo kwangu mimi, ni (kama) Haruna (nafasi aliyonayo) kwa Musa, isipokuwa hakuna Utume baada yangu".

Taz: Sahih Bukhari Kitabu Maghazy
Sahih Bukhari Kitabu Badi Ilkhalq
Sahih Muslim Kitbul Fadhail
Sahih Tirmidh J.5 Uk. 301
Musnad Ahmad J.3 Uk. 50
Mustadrakul Hakim J.3 Uk. 109
Ansabul Ashraf J.2 Uk. 106
Al-Isaba J.2 Uk. 507
Kifayatut Talib Uk. 281
Usudul Ghaba J.4 Uk. 26

Ujumbe uliomo katika Hadithi hii ni kwamba "Ali ni Haruna wa

Muhammad isipokuwa hakuna Utume baada yake. Haruna mbali ya kuwa ni Khalifa wa Musa, lakini pia ni Nabji, hii ndiyo manna ya Hadithi kusema kwamba: "Ali na Haruna ni kwa kila kitu isipokuwa Unabii".

Mtume (s.a.w.) amesema, "Mimi ninakuachieni vizito viwili ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea baada yangu, Quran na Ahlul Bait, viwili hivi havitaachana mpaka vitakaponifikia katika Haudh"

Taz: Tafsir Ibn Kathir J.4 Uk. 122
Tafsir Khazin J.1 Uk. 4
Tarikh Bughdad J.8 Uk. 442
Sahih Muslim J.2 Uk. 1873
Sahihut Tirmidh J.2 Uk. 308
Jamuil Usul J.1 Uk. 187
Albidayatu Wannihaya J.7 Uk. 362
Majmauz Zawaid J.9 Uk. 163
Usudul Ghaba J.2 Uk. 12
Addurrul Manthur J.2 Uk. 60

Ahlul Bait ni cha pili katika vitu viwili ambavyo Mtume (s.a.w.) ameacha katika umma huu.

lliposemwa: "Viwili hivi havitaachana mpaka vitakaponifikia katika Haudh" Maana yake, Quran na Ahlul Bait viko pamoja na vitakuwa pamoja mpaka siku ya mwisho.

Kwa maneno mengine, uongozi wa Ahlul Bait uko sambamba na uongozi wa Quran. Kwa kuwa Ali ni Imam wa kwanza katika AhIul Bait, basi Waislamu kama watashikamana naye (kwa kufuata uongozi wake) hawatapotea baada ya Mtume.