UTANGULIZI

Sheikh Umar Juma Mayunga alikwenda Kenya ambako baada ya mazungumzo ya kidini, alishauriwa na Sheikh Abdallah Nasser (wa Nairobi) na Haji Ali Muhammad Jaffer (wa Mombasa) kuwa atakaporudi Dar es Salaam aonane nami kwa maelezo zaidi.

Alikuja kuonana nami, na swali lake la kwanza lilikuwa juu ya Taqiyah. Nilimpa jibu lililomtosheleza kutoka kwenye Qur'ani Tukufu na Ahadithi.

Baada ya hapo alikuwa akinitembelea mara kwa mara na mambo yote aliyokuwa akiyaelewa vibaya (kutokana na propaganda za kiovu za Wahabiyyah) aliyaelewa vipasikavyo.

Baada ya hapo aliyachambua matukio ya mwenye wakati wa mwisho wa maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mara tu baada vitabu muhimu vya historia ya Kiislam kama vile Taarikh at-Tabari, Taarikh al-Kamil na Sirah Ibn Hisham; Sura zihusikanazo na historia za vitabu vya Ahadith kama vile Sahih Bukhari, Sahih Muslim, Kanzul Ummal, n.k.

Baada ya kujifunza matukio hayo, alijifunza vitabu vya Kishia; na akavutiwa na ukweli wauzungumzao Shia.

Tangu hapo, amekuwa akizitembelea sehemu nyingi za Tanzania na Kenya. Huko Mombasa alitoa hotuba juu ya Ndoa ya Mut'a na baada ya hapo aliandika juu ya mada hiyo na kikachapishwa.

Hivi hapa, ili kuusherekea mwaka wa 1400 wa Tukio la GhadiirKhum, amekiandika kitabu ulichokishika. Nimekicheki kitabu hiki na ninathibitisha kwamba rejea zilizotajwa kitabuni humu na tafsiri zao ni sahihi.

Ninamwomba Allah Subhanahu wa Taala Akijaalie kitabu hiki kuwa njia ya hidaya kwa ajili ya watu na Amjaalie mwandishi wake Tawfiiq zaidi kuihudumia dini ya Mwenyezi Mungu kama inavyofundishwa mwenye Qur'an na Ahlul Bayt (a.s.).

Iwapo msomaji ye yote yule atataka kujua zaidi juu ya jambo lo lote lile lililotajwa kitabuni humu, anakaribishwa kumwandikia mwandishi huyu ambaye anwani yake imo kitabuni humu.

Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
Mhubiri Mkuu
Dar es Salaam
Bilal Muslim Mission of Tanzania