ABUBAKR AMTEUA UMAR

Abubakr alipokuwa mgonjwa taabani alimwitisha Uthmani bin Affan ili aandike wasia juu ya Umar binil Khattab, akamwambia:

"Andika Bismillahir Rahmanir Rahimi, hili ni agizo la Abubakr bin abi Quhafa kwa Waislamu wote" mara Abubakr akazimia Uthman akaendelea kuandika: "Amma baada ya haya, nimekutawalisheni Umar bnil Khattab na sikuacha kukupendeleeni kheri". Kisha Abubakr akazimuka, akauliza: Umeandika nini? Uthmani akassomea yale aliyoyaandika, Abubakr akashangilia sana kisha akasema Uliogopa kuwa khitilafu ingetokea kama ningezimia moja kwa moja? Uthmani akajibu:

"Ndiyo Abubakr akasema Mwenyezi Mungu akulipe wema". Umar akashika mahala pa Abubakr.

Taz: Tarikhut Tabari J.2 Uk. 618
Tarikh Ibn Athir J.2 Uk. 292

Katika tukio la Ghadir Khum, vitabu vya tarikh vimeonyesha kuwa Umar alitoa BAIA kwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s.). Na katika kumbukumbu ya tarikh vile vile vitabu kama vile: ASSUNANU WALMUBTADIA'TU ukurasa wa pili, inasimuliwa kuwa: Katika zama za Mtume (s.a.w.) Waislamu wawili waligombana wakaenda kwa Mtume kuamuliwa. Mtume (s.a.w.) baada ya kusikiliza ugomvi baina yao, mmoja akamtia makosa na wa pili akampa haki. Yule aliyeonekana na makosa mbele ya Mtume (s.a.w.) akakafaa kukubali makosa yake, kwa hiyo akashauri kesi yao ipelekwe kwa Abubakr. Wakaenda kwa Abubakr, wakamhadithia namna kesi yao ilivyosikilizwa na kuhukumiwa na Mtume (s.a.w.), Abubakr akasema: Sina zaidi ya alivyohukumu Mtume (s.a.w.).

Hapo vile vile ikashindikana, wakaamua kwenda kwa Umar binil Khattab, wakamhadithia walivyoanzia kwa Mtume kisha kwa Abubakr. Umar akachomoa upanga akakata kichwa cha aliyekataa kutii hukumu ya Mtume (s.a.w.). Pale pale Mwenyezi Mungu akateremsha Aya ya 65 ya Sura ya 4 kuwa: "Naapa kwa Mola wako, hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye hakimu wao katika yale waliyohitilafiana kati yao, kisha wasione dhiki katika nyoyo zao kwa hukumu uliyotoa na wanyenyekee sana sana".

Ikiwa Umar amekata kichwa cha mtu aliyekataa kutti hukumu ya Mtume, kisha Mwenyezi Mungu akambariki kwa kitendo hicho.

(a) Kwa nini Umar hakukata kichwa cha Abubakr aliyekwenda kinyume na Aya ya 67 ya Sura ya 5 ambayo imeshuka kwa ajili ya kumtawalisha Imam Ali bin Abi Talib (a.s.).

Kitendo ambacho kilihudhuriwa na zaidi ya Waislamu laki moja, akiwamo Abubakr na yeye mwenyewe Umar?

(b) Na; kwa nini Umar hakukatwa kichwa kwa kuipinga Aya 67 ya Sura ya 5 ambaye alionekana hadharani akitoa BAIA kwa Imam Ali (a.s.) kuwa ndiye Imam wake baada ya kuondoka Mtume?