TUKIO LA HIJRA

Mwenyezi Mungu anasema:- "Kama hamtamsaidia basi Mwenyezi Mungu amekwisha msaidia walipomfukuza wale waliokufuru, alipokuwa wa pili katika wawili walipokuwa wote, wawili katika pango. Alipomwambia swahibu yake; usihuzunike hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi. Ndipo Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake na akamsaidia kwa majeshi msiyoyaona" 9:40

Uchunguzi wetu katika Aya hii utahusu silabi zilizotumika katika

mfumo wa Aya hii, kwa hiyo tutajadili hapa nukta saba:

(a) Amekwisha msaidia

(b) Walipomfukuza

(c) Alipokuwa wapili katika wawili

(d) Alipomwambia swahibu yake

(e) Usihuzunike

(f) Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi

(g)Akamteremshia utulivu wake

(a) Amekwisha msaidia

lliposemwa "Mwenyezi Mungu amekwishamsaidia". Hapa pana dhamiri ya mmoja aliyesaidiwa, naye ni Mtume Muhammad (s.a.w.)

(b) Walipomfukuza

lliposemwa:- "Walipomfukuza" ni mtu mmoja aliyefukuzwa, Mtume Mohammad (s.a.w.).

(c) Alipokuwa wa pili katika wawili

lliposemwa "Alipokuwa wa pili katika wawili". Hii ni jumlatul haliyya, swahibul hali ni dhamiri katika: "AKHRAJAHU" inayomrejea Mtume Mohammad (s.a.w.). Natija inasema "Walimfukuza peke yake"

(d) Alipomwambia Swahibu yake

lliposemwa "Alipomwambia Swahibu yake" watu wengi wanafikiri kuwa Mwenyezi Mungu kulitumia tamko la "SWAHIBU" katika Aya hii ni ibara inayompa sharaf kubwa Abubakr. Ni vizuri kuliangalia tamko Ia "SWAHIBU" linavyotumiwa katika Quran: "Akamwambia Swahibu yake hali akibishana naye, mimi nina mali nyingi kuliko wewe na nguvu zaidi kwa wafuasi. Na akaingia bustani yake hali ya kujidhulumu nafsi yake, Swahibu yake akamwambia hali ya kubishana naye. Je! Umemkufuru yule aliyekuumba kwa udongo tena kwa tone Ia manii kisha akakufanya mtu kamili? 18:34-37

Mazungumzo haya yalikuwa kati ya muumini na kafiri, wakiambizana "Swahibu yangu".

(e) Usihuzunike

Iliposemwa "Usihuzunike", hapa pana Suratun Nahyi, ambayo Huzuni imepatikana kwa Abubakr ama kwa Sura ya Twaatullah au kwa Sura ya Maaswiyatullah!!

Ikiwa ni twa'atullah, basi Mtukufu Mtume (s.a.w.) hakatazi twa'a bali anaiamrisha na kuwataka Waislamu wawe watiifu.

Na ikiwa ni maasi, basi Mtume (s.a.w.) ameyakataza, Abubakr alihuzunika na Mtume (s.a.w.) akamkataza.

(f) Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi

Iliposemwa "Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi" Naam: "Hawashauriani kwa siri watatu ila Mwenyezi Mungu ni wa nne wao. Wala watano ila Mwenyezi Mungu ni wa sita wao, wala wachche kuliko hao wala zaidi ila Mwenyezi Mungu huwa pamoja nao popote walipo" 58:7

(g) Akamteremshia utulivu wake

Iliposemwa:- "Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake" ASSAKIINA (utulivu) ni jambo wanalolipata watu wema tu.

Hapa tutataja taratibu za matumizi ya tamko hili lilivyokuja katika Quran:

  1. Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha UTULIVU wake juu ya Mtume wake na juu ya waumini" 9:26
  2. "Yeye ndiye aliyeteremsha UTULIVU katika nyoyo za waumini ili waongezeke imani juu ya imani yao" 48:4
  3. Basi akateremsha UTULIVU juu yao (waumini) na akawapa ushindi wa karibu" 48:18
  4. Mwenyezi Mungu akateremsha UTULIVU wake juu ya Mtume na juu ya waumini" 48:26

Lakini katika pango tunasoma hivi "Mwenyezi Mungu akamteremshia UTULIVU wake na akamsaidia kwa majeshi msiyoyaona". Aliyeteremshiwa hapa ni Mtume Muhammad tu peke yake.