ALI HAKUMBAI ABUBAKR

Mwana Aisha amesema kuwa:- "Ali (a.s.) hakumbai Abubakr ila bada ya miezi sita kupita".

Abubakr alikwenda nyombani kwa Imam Ali (a.s) akawakuta Bani Hashimu wamekusanyika, Imam Ali akamwambia "Sisi haikutuzuilia kukubali ewe Abubakr, kwa kupinga heshima yako wala ubora aliokupa Mwenyezi Mungu, lakini sisi tunaamini kuwa jambo hili (la uongozi) ni letu na nyinyi mmelipokonya kwetu".

Kisha akawa anamtajia nafasi aliyonayo kwa Mtume (s.a.w.) na haki zake mpaka Abubakr akaangua kilio.

Taz: Tarikhut Tabari J. 2 Uk. 448