RIWAYA KUHUSU SWALA

Imepokewa kwa Mwana Aisha kuwa, Mtume (s.a.w.) alipougua maradhi aliyofia, aliamrisha kuwa: Abubakr aslishe watu, mimi (Aisha) nikasema, Abubakr ni mtu mpole sana, atakaposimama mahala pako atashindwa (kusalisha) Mtume akaamuru: Abubakr asalishe. Nikasema kama nilivyosema kwanza, Mtume akakasirika akasema: Nyinyi ni watu wa Yusuf. Mara Mtume akahisi woga moyoni mwake, akatoka akichechemea kwa kushikiliwa na watu wawili (Ali na Abbas) alipofika Msikitini, Abubakr akarudi nyuma ya safu ya kwanza. Mtume akakaa kuongoza swala, Abubakr akawa anafuata sala ya Mtume (s.a.w.) na Waislamu wakawa wanapokea kwa Abubakr."

Taz: Tarikhut Tabari J.2 Uk. 439
Afatu As'habil Hadithi Uk. 13-30

Hapa pana mambo matano yanahitaji kuangaliwa:

(a) Abubakr ni katika watu walioamriwa na Mtume kutoka pamoja na jeshi Ia Usama bin Zaid. Kwa hiyo basi, amma Abubakr aliwenda pamoja na jeshi hilo, na kwa hivyo hakusalisha maana hakuwepo. Amma alikuwapo mjini, kwa hivyo alipinga amri ya Mtume (s.a.w.) na kwa hivyo Abubakr amelaaniwa.

(b) Mtume (s.a.w.) alipougua maradhi aliyofia, alikuwa ndani ya nyumba ya Mwana Aisha, Mtume alisema: "Niitieni Ali" Aisha akajibu: "Laiti ungemwitisha Abubakr" Hafsa (mtoto wa Umar) akasema: "Laiti ungemwitisha Umar" (kila mmoja akamwita baba yake) wakakusanyika mbele ya Mtume. Alipowaona Mtume akawaambia "Ondokeni nikikuhitajini nitakuiteni".

Taz: Tarikhut Tabari J.3 Uk. 439.

(c) Mtume (s.a.w.) alipowaambia Aisha na Hafsa, "Nyinyi ni watu wa Yusufu" hapa inaonyesha kuwa amri ya kusalisha Abubakr si ya Mtume (s.a.w.), hali ya kisa cha wanawake waliomtaka Nabii Yusufu (a.s.) na yeye akajizia, na kisa cha Aisha na Hafsa kuwatanguliza mbele baba zao ni jambo lililofanana.

(d) Mtume (s.a.w.) alitoka akichechemea taabani na watu wawili wamemshikilia, Abubakr akapisha mahala hapo, na Mtume (s.a.w.) akashika mwenyewe kusalisha. Ni jambo gani lililomlazimisha kutoka akiwa hali hii, ikiwa yeye ndiye aliye amuru Abubakr asalishe? Jambo gani lililomsonga asalishe watu hali amekea chini kwa taabu na dhiki kubwa?

(e) Kuonyesha dalili zote hizi, haina maana kuwa: kama itasihi kuwa Abubakr amesalisha, basi itapasisha Abubakr kushika uongozi baada ya kuondoka (kufa) Mtume (s.a.w.). Hii haina maana, kwa sababu nafsi ya kusimama mbele na kusalisha watu si jambo lenye kima na thamani tukufu ambalo litampasisha kupata kila apitae mbele na kusalisha watu!!

Kwa mujibu wa Hadithi za ndugu zetu Masunni, inasema kuwa:Mtume (s.a.w.) amesema, "Salini nyuma ya kila mwema na muovu". Na kwa msingi huu Madhihabi ya Imam Shaafy na Imam Ahmad na wengine wamepasisha Mwislamu asali nyuma ya ye yote japokuwa Fasiq.

Taz: Assunanu Walmubtadiatu Uk. 182

Lakini pia tukiliangalia kwa wema suala hili tunaona kuwa: Mtume (s.a.w.) alipokuwa akitoka kwenda vitani, nyuma alikuwa akiweka mtu wakushika mahala pake katika masuala mbalimbali, ikiwa ni pamojana kusalisha.