Meza ya Uchunguzi

Kimeandikwa na : Omar Jumaa Mayunga

PONGEZI

"Enyi waumini, mkimcha Mwenyezi Mungu atakuongozeni njia ya haki na atawafutieni makosa yenu na atakusameheni". 8:29

Uchamungu ni moja ya pambo Ienye thamani kwa binadamu na nikipimo cha haki na batili na kila ambacho kinamfanya mwanadamu kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, kwani uchamungu ni vazi zuri Ienye thamani kila ataelivaa, hupata ukunjufu wa moyo na hima ya kutafuta haki hadi kufikia kikomo na kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, kando ya neema zake, zikitiririka bila ya hesabu.

Katika ulimwengu huo ambao umejaa ibilisi wenye rangi tofauti, wakiwa na mitego tofauti ili kuwanasa wanadamu kwa vishawishi vipotovu na kuwatowa katika misingi ya haki na ya ukweli na yenye mwelekeo wa tawhid.

Wale ambao waliofahamu hila za ibilisi na wakakana kudhalilishwa kwa kufuata vishawishi vyake, kwa hakika hawa ni katika waongofu.

Jambo lakusikitisha, kwamba kwa upande mwingine makafiri wanahila zao, nara zao zaweza kuwa ni uchamungu na wakafanya vitendo viovu wakiona ni vyakumridhisha Mwenyezi Mungu, hali ya kughafilika kwamba huo ni upotovu na ni chanzo cha kuangamia, lakini Mwenyezi Mungu amewaahidi wale wamchae kuwaonyesha njia ya haki.

Kitengo cha Utamaduni Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, unayo furaha ya kuchapisha kitabu, kwa jina: (MEZA YA UCHUNGUZI) kimeandikwa na mtafiti wa haki, si mwingine nae ni Sheikh Omar Juma Mayunga, mwandishi wa kitabu hiki amepata misuko suko mingi mpaka kufikia upeo wa haki, yeye ni mfano wa kuigwa kwani wengi bado wanayumba yumba katika kutafuta ukweli. Kwani haki ni lulu yenye thamani hupatikana kwa juhudi, ongeza uchamungu.

Kwani uchamungu ni taa yenye kung'arisha njia ya haki, na wale ambao si wachamungu wakiitafuta haki hawaiyoni.

Sheikh Omar Jumaa Mayunga katika kitabu chake ametowa dalili za Qur'an na Sunna za Mtume (SAW), ongeza tajruba zake katika kuitafuta haki na Uislam wa kweli ulioletwa na Mtume Muhammad (SAW) akisaidiwa na nuru ya uchamungu ameweza kufikia chemchem ya chimbuko la haki.

Tukiacha kupendelea katika itikadi na matamanio ya nafsi na wasi wasi wa ibilisi, tukiangalia kwa jicho la haki kitabu hiki kinaweza kuwa muamuzi na sababu ya kupata kheri za dunia na akhera.

Kitengo cha Utamaduni kinasisitiza kuwa yote yaliyoandikwa katika kitabu hiki ni yake Muandishi, Kitengo cha Utamaduni kimesaidia kuchapa copy 10,000 tunawaombea Mungu wote wanaotafuta haki na Uislamu wa kweli.

Mustaffa Najarian Zadeh
Mkurugenzi wa Kitengo cha Utamaduni,
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Dar es Salaam - Tanzania