HISTORIA YA KIISLAM

KIME FASIRIWA NA SEYYID MUHAMMAD MAHOJ MAHDI MUSAWY

DIBAJI

Marehemu Nawwab Sheikh Ahmadd Husain Khan Bahadur, O.B.E., wa Paryawan (Bara Hin-di) katika mwaka 1920 A. D. alitunga historia ya kislam na akaipa jina Taarikh-e-Ahmadi.'

Tarehe hiyo ilikuwa namna ya pekee, kwa sababu mwandishi huyo hakutumia hata neno moja kutokana kwake; bali alinakili sehemu zenye kufaa kutokana na vitabu mbali mbali zijulikanazo na thabiti za historia, hadithi, na habari za maisha ya watu.

Maneno aliyoongeza yeye katika kitabu hiki ni (preposition) tu, meneno yenye kuunganisha kama, na , 'kwa', 'haadaye', 'tena' na kadhalika, ili kutenganisha funga la maneno.

Kitabu hiki kimepigwa chapa mara nyingi katika Bara Hindi na Pakistani.

Katika mwaka 1965A. D., tafsiri (kwa ufupi) ya sehemu ya mwanzo kitabu hiki kwa lugha ya, kingereza kimepigwa chapa Bombay na ikapewa jina "Gems of lslamic History."

Kitabu hiki chetu ni tafsiri ya "Gems of Islamic History", lakini kimesahihishwa kutokana na kile kitabu cha asili.

Kitabu hiki chaeleza matukio ya maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) lazima tujulishe hapa kwamba maalezo haya ya maisha si kinaganaga'

Msomaji ataona hakika ni kitabu chenye faida sana kwa sababu muhariri na mfasiri hawakukusudia kuthibitisha au kukanusha kitu chochote kwa kupotoa jambo la kweli la historia, kama wanavyofanya watungaji wengi siku hizi. Kitabu chetu hiki kinaonesha hasa maneno ya vitabu vya asili na kumwacha msomaji awe huru kufikiria mawazo yake binafsi.

Na kwa kuwa kitabu hiki cha pekee isio na kifani, Bilal Muslim Mission imechukuwa fursa ya kuwatunukia wa Africa mashariki ili wajipatie maandishi halisi ya wanachuoni waliotangulia wa zamani.

Natumai kitabu hiki kitapendezewa kama vilivyopendwa vitabu vyetu vingine vyambele.

S.Saeed Akhtar Rzvi

Shekh Shahabuddeen Qastalani katika kitabu chake [Mawahib-ul-adunniyah ameandika hivi,: Alipokusudia Mwenyezi Mungu kuwaomba viumbe vyake, aliichomoza Nuru ya Mtume Muhammed (s.a.w) Nuru ambayo ni tukufu ndipo akaumba dunia

Amehadithia Bwana Jabir bin Abdallah Ansari, "Nilipomwuliza Mtume Mohammad (SA.W.) ya RASUULAL-LAHI wazee wangu nakufidia, ni julishe kiumbe yupi aliumbwa mwanzo?". Akanijibu "Ey Jabir Mwenyezi Mungu aliumba nuru ya Mjumbe wake kutokana na nuru yake kabla ya kuumba chochote". Na vile vile Sayyidna Ali (A.S) ameeleza kwamba mpenzi wa Mwenyezi Mungu Mtume Muhammed (SA.W.) amesema "Mwenyezi Mungu ameumba nuru yangu miaka kumi  na nne elfu kabla ya kumuumba Nabii Adam [AS.]"

2. Mhistoria maarufu wa ki-islaam Bwana Abul-Hassan Ali bin Hussein Al-Mas'oodi katika kitabu chake maarufu cha historia kiitwacho "Murooj-udh-dhahab na Ma'adinul-jawaahir" amepokea hadithi hii kutoka kwa Imam Ali (a.s) kwamba  Mwenyezi Mungu afipotaka kuumba dunia na watu na  kila kilichomo ndani ya dunia basi kwanza kabla hakuiumba hii ardhi, kwa upekee kwa Nuru yake Jalali akaidhihirisha nuru yenye kung'aa kutokana na nuru yake na ikiwa ile nuru inatoa macheche ya nuru na mshabaha wa sura tena akakusanya zile sura akaifanya Sura moja na ikatokeza sura ya Mtume Muhammad (S.A.W.), basi hapo Mwenyazi Mungu akaikhutubia ile sura na kusema "Wewe ndiye naliyekuchagua na wewe ndiye nuru yangu kwako wewe nimewacha hazina ya uwongofu na kwa ajili yako (kwa mapanzi juu yako) mbingu nitainyanyua na ardhi (dunia) nitaitandaza na maji nitawacha yamiminike na yaende na kujaalia thawabu na adhabu. Pepo na Jahannam (Moto) kwa watii na wasiotii na nitawafanya Aali yako (AHLUL - BAYT) kuwa waongozi wa Haqi na nitawajaza kwa elimu hata wasishindwe kueleza au kuwafahamisha Umma mushkili wowote wala jambo lolote lililofichika wasishindwe kulieleza na nitawafanya wao (AHLULBAYT) wawe Hoja na Mfano juu ya viumbe vyangu na kuwa nabihisha (kuwafahimisha upekee Wahdaaniyah) wangu na Qudra yangu juu ya viumbe vyote". Baadaye Mwenyezi Mungu akachukuwa Ahadi kwa kuyakubali yote na kabla hakuchukua hiyo Ahadi  aliwajulisha viumba vyote kwa kumchagua Mtume Muhammad (SA.W.) na Aali yake kuwa ni waongozi wa Haqi na wamechagufiwa naye ili ndio iwe njia ya uadilifu na viumbe wasiwe na udhuru wowete wa kwamba hawakujua.  

3. Bwana Abul Qaasim Tabrani  (360 A.H.) katika kitabu chake

"MUJAM-lKABEER'' anahadithia kutokana na Bwana Ibn Abbas

kwamba Mtume (S.A.W.) amesema, "Mimi nilikuwa Mtume alipokuwa Adam (A.S.) katika kati ya roho na kiwiliwili (maana yake bado umbo la Nabii Adam lilikuwa halikukamilika).

4.    Bwana Ibn Atheer Juzari katika kitabu chake tareekh-ut-Kamil anaandika kwamba Abdi-Manaf (Babu wa tatu wa Mtume wetu (S.A.W.] alikuwa na watoto wawili Abdush-Shams na Heshim ambae walizaliwa mapacha kwa hali kidole cha mmoja wao kiligandana na Kipaji cha mwenziwe. Walipofanyiwa kupasuliwa mahali pale paliposhikamana ikatoka damu nyingi. Wakasema watu hii ilionyesha kwamba baina ya ukoo wao patamwagika damu nyingi. Aliposhika Bwana Hashim mahala pa baba yake Abdi-Manaf kuwa yeye mkubwa wa kabila basi Ummayah mtoto wa Abdush-Shams akaona wivu Juu yake, basi uadui baina ya watoto wa Hashim na Ummayah Ukaanzia hapa.

5.    Katika kitabu cha tafseer mashuhuri kiitwacho DURRI- MAN-SOOR CHA JALALUDDEEN SUYOOTEE imeandikwa hivi kwamba Ibn Jareer ibn Mundhir ibn Abi-Hatim, Tabrani, Ibn Mardwail na Hakim wamehadithia kwa njia sahihi mbali mbali kwamba Ali Ameeleza tafsiri ya aya hii: LAM-TARA lLAL-LADHIYNA BAD-DALUU NIA-MATAL-LAAHl KUFRA". Je, (Hukuwaona wale waliobadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kukuturu (S. 14 A.28) hivi, "Wale waliobadili dini ya Mwenyezi Mungu kwa kukufuru ni  wana (watoto) wa Umayyah na watoto wa Mugheera, ambo wenye kupita dhambi kuliko Quresh wote."

6.    Katika kitabu cha historia cha QADHI HISSEAIN IBN MUHAM­MAD DIYARBAKRI MALIKi inaoitwa TAREEK HUL KHAMEES imeandikwa hivi kwamba Mtume wetu alizaliwa mwezi (10) kumi Rabeeul Awwal, na kwa muujibu wa walivyopokea wengine tarehe ya kuzaliwa kwake ni (12) kumi na mbili RabeeuI Awwa! "na wengine wamepokea kuwa ilikuwa (17) kumi na saba RabeeuI Awwal.

7.   .SYED AHMAD ZAINE DAHLAN katika kitabu chake mashu­huri alichokiandika juu ya maisha ya Mtume wetu (S.A.W.) kinachoitwa SEERATUNNABAWEEYAH, anasema hivi; wakati wa kufa kwake Abdul Muttalib akamwusiya mwanawe Abutaalib juu ya Mtume wetu (S.A.W.), na vilevile kusema kwamba mvinyo ulikuwa haramu hata mbele ya kuja dini ya Islam (katika zama za Jaahiliyyah). Basi alivyomwusia Ahdul Muttalib mwanawe Abutaalib juu ya Mtume wetu (S.A.W.), alikuwa anampenda Mtume (S.A.W) kuliko wanawe hadi wakati wa kulala (usiku) alimlaza ubavuni mwake, na alikuwa akimlisha chakula bora kabisa.

8.   Ameeleza IBN HAJAR ASQALANI katika kitabu chake AL-ISABAH, kwa namna ya maelezo ya wanavyuoni wengi kuwa mtu wa kwanza aliyeleta imani na kukubali dini ya kiislam ni Bwana Abul-Hasan Ali bin Abitaalib. Ali alizaliwa mwaka (10) kabla ya "Bi-ithia (kabla Mfume (S.A.W.) kutangaza Utume wake). Alilelewa katika mikono ya Mtume (S.A.W.) na hawakuachana (hawakufarakiana) moisha yao yote.

9.   ABDUL MALIK IBN HISHAM katika kitabu chake alichoandika juu ya maisha ya Mtume kinachoitwa SEERATU-IBNU-HISHAM amehadithia hivi kwamba Ali ni mtu wa kwanza aliomwammi Mtume (S.A.W.) na akaukubali Uislam na yote aliyoteremshiwa Mtume: Umri wa Ali alipoikubali dini ya Uislaam ulikuwa miaka (10) kumi. Katika mabarikio aliombariki Mwenyezi Mungu Ali kulelewa Ha Mtume chini ya uongozi wake wa haqqi kabla ya kudhihirika Uislaam. Baada ya Ali Zaidi Bin Haritha kakubali Uislam na akasali na baada ya huyu Zaid Abu-Bakr kaingia katika Uislam.                              

10.Katika kitabu cha maisha ya Mtume Muhammad (S.A.W.) kiitwacho ISTEE-AB alichoandika IBN ABDUL BIR MALIKI, amesema kwamba Muhammad ibn Kaab Qarzi aliulizwa na watu, nani alioifuata dini ya Uislaam kwanza. Ali au Abu Bakr. Akajibu, "Subhaa-nallah! Ali ndiye wa kwanza kukubali Uislaam." Baadaye Ibn Abdul Bir anaeleza, "Sisi hatuna shaka kwamba Ali ndiye wa kwanza miongoni mwa hawa wawili (Ali na Abu-Bakr) kukubali Uislaam. Zaidi ya haya salman AI-Farisi, Abu Dhar, Miqdadi, Khabbab, Abu, Saeed Khudri na Zaid Bin Arqam wanashuhudia kwamba hakika Ali ni wa kwanza kukubali Uislaam na masahaba hawa wamemfadhilisha Ali juu ya masahaba wengineo."

11.Katika kitabu cha TAFSEER-I-DUURI-MANTHOOR na kafika FATHUL QADEER cha ABU ALI MUHAMMED IBN ALI SHOUKANI imeandikwa hivi kwa ushahidi wa aya ya Qur'ani, Wassaabiqoonas saabiqoon" (S. 65. A. 10-12). ibn Abi Hatim ametoa hadithi alione-na Abdullah ibn Abbas kwamba watakatifu WATATU ndio walio ikubali (walioamini" mwanzo dini ya Uislaam, JOSHUA mtoto wa Nuh alikuwa wa kwanza kumwamini Mtume MUSA. na mwenye imani alioamini mwanzo katika Al-Yaseen kuukubali utume wa Mtume Isa (Tazama S. 36, A. 20-26) na wa tatu wao ni Ali mtoto wa Abu Talib aliofungulia kukubali Utume wa Mtume wetu mtukufu.

12. IBN MARDWAIH katika maelezo yake kuhusu Aya hiyo hiyo ametoa hadithi kutokana na Ibn Abbas akisema hivi kwamba aya hii yaonyesha sifa juu ya Hizqeel mwenye kuamini kati ya watu wa Firooni (Tazama S. 40, A. 28-33), Bwana Habeeb Seremala mweye imani katika kabila ya Yaseen na Ali Ibn Abi Talib, na kila mmoja katika wao ni wa mwazo kuamini kati ya watu wao, na Ali ni bora wao kuliko wote.

13. IMAM MUHAMMAD IBN ISMA'EEL BUKHAREE katika kitabu chake TAREEKH-UL-KABEER, ametaja maneno ya Mtume wetu (S. A. W.) yaliyoelezwa na Ibn Abbas kuwa watu watatu ni "Siddeeq" hakika bila shaka Hizqeel mwamini kati ya watu wa Firaoni, Habeeb Seremala mwamini kati ya ukoo wa Yaseen na Ali IbnAbiTalib ndio wakweli.

14.    NAWAB SIDEEQ HASAN KHAN WA BHOPAL katika kitabu chake cha tafseer kiitwacho TAFSEER FAT'HUL BAYAN ameeleza hadithi kutokana na Ibn Abi Laila, na hadithi hiyo hiyo vile vile imetolewa na TAFSEER.I-DURRl MANTHOOR ya JALALU-DDEEN SUYOOTEE lakini iko tafauti ya baadhi ya maneno tu wanasema kwamba "Ni watukufu watatu tu ambao hawakukufuru au kumuasi Mwenyezi Mungu kabisa hata kiasi cha kupepesa macho na walikimbilia kuamini dini ya haki. Miognoni mwao na wa mwanzo na bora wao ni Ali Ibn Abi Talib; wa pili mwamini katika kaumu ya Firauni, na watatu wao anatokana na ukoo wa Yaseen. Na watatu hawa tu ni Sideeqs (Washuhudiao na kweli)

15.Abu Muhammad Hsain AI-Baghawi katika Tafseer Maali-mut Tanzeel, Shaikh Ala'uddeen Ali bin Moh'd AI-Baghdadi anaojulikana kwa jina Khazin Baghdadi katika kitabu chake Lubab-ut-Taweel ambacho ni mashuri na kiitwacho Tafseer Khazin, Abi Bakr Ahmad Ibn Husein Baihaqi katika kitabu chake Dalail-unNuboowwah, Jalaludeen Suyootee katika kitabu chake Jam'ul Jawani, Ala'uddeen Ali Muttaqi katika kitabu chake Kani-ul-Ummal. Abu Ja'afar Muhammad Ibn Jareer Tabari katika Tareekh ur-Rusul-wal-Mulook. Abi Sa'adat Mubaraka Ibn Atheer Al Juzeri katika Tareekh-ul-Kamil, na Isma'eel Abul fida katika Kitab-ul-Mukhtasar fi Akhbar-il-Bashar. wote hawa .wamesema hivi: kwamba Hazrat Ali amesema:— llipo-shuka aya "Waandhir Asheeratak-al-aqrabeen" (5. 26, A. 214) Mtukufu Mtume akaniita na akaniamrisha, Ee Ali Mwenyezi Mungu ameniamrisho- niwahadharishie watu wangu adhabu yake. Kwa kuona hali na tabia yao nikiwafikishia maamrisho ya Mola watapinga na kufanya yasiyofaa, basi ikanihuzunisha sana na kudhoofika, kwa hivyo nikakaa kimya nikichelewesha zaidi kutangaza maneno ya Mwenyezi Mungu basi ataishusha ghadhabu yake. Kwa hivyo Ee Ali, chukua saa (kipimo) moja mchele, na tia mguu mzima wa mbuzi (kitoweo) na bakuli kubwa la maziwa na utengeneze karamu: baadaye na

owaalike watoto wote wa Abdul-Muttalib karamu kwangu ili niwafikishie maneno ya Mwenyezi Mungu. Basi nikafanya alivyoniamrisha Mtume na watoto wa Abdul-Muttalib ambao walikuwa kiasi arubaini ambao miongoni mwao walihudhuria Ammi zake mtume, Abu-Talib. Hamza Abbas na Abu Lahab. Hapo Mtume akaniamrisha nikalete hicho chakula akachukuwa kipande cha nyama na akamyambua kwa meno tena akazitawanya pembezoni mwa sinia na akasema. "Kwa jina la Mwenyezi Mungu anzeni kula". Wote hawo waliohudhuria wakala shibe yao ingawa chakula kile na bakuli la maziwa kilikuwa cha kumshibisha mtu mmoja tu. Baadaye Mtume akataka kusema nao lakini Abu Lahab mara akadaka maneno na kusema, "Kweli rafiki yenu amekurogeni". Kwa kusikia maneno haya wote wakaondoka wakendazao, basi Mtume hakupata fursa ya kusema nao.

Siku ya pili Mtume akanitaka nitengeneze chakula na kuwaita tena, basi nikafanya vivyo hivyo wakaja wakala. walipokwisha kula hapo Mtume akawahutubia hivi. Enyi watoto wa Abdul-MutaIib, nimekuleteeni ninyi heri ya duniyani na ahera, na Mwenyezi Mungu ameniamuru nikwiteni mwende kwake (Mwabudu) yeye. Kwa hivyo nani mwenye kuitikia (kukubali) mwito wangu miongoni mwenu ili awe Waziri wangu na ndugu yangu pia?. Hapana mtu aliyeitikia. Lakini mimi (Ali) ijapokuwa nalikuwa mdogo kuliko wote katika kundi hilo nikasema, Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi niko tayari hapa kushika Wizara yako katika kazi hii. Aliposikia Mtume maneno yangu, akanipapasa shingoni kwa upole na akasema "Enyi watu wangu! Huyu Ali ni ndugu yangu, waziri wangu na mwandani wangu miongoni mwenu. Msikilizeni na mtiini huyu. Waliposikio maneno ya Mtume mara wakacheka kwa sauti na wakaondoka na huku wakamwambia Abu Talib, "Sikiliza! Umeamrishwa kumtii na kumfuata mtoto wako".                                                    

Tokeo hili vilevile limetajwa na Thomas Cartyle katika kitabu chake Heroes and Hero Worship, vile vile Gibboo katika kitabu chake cha Decline and Fall of the the Roman Empire, Devenport katika Apology for Muhammad and the Koran, na mwishoni Washington Irvin katika Muhammad and His Successors, na maelezo yake yote.                                         

16. Abul Fida katika kitabul Mukhtasar fi Akhbaril-Bashar anasema kwamba mashairi yaliyo tungwa na Abu Talib yanathibitisha yeye alileta imani na kuukubali Utume wa Muhammad moyoni. Tafsiri ya mashairi tunatoa hapa: "Ee Muhammad umeniita kuikubali dini ya Islam na sinashaka kuwa maneno unayoyasema ni kweli, madhubuti na aminifu. Na nina hakika katika kuamini kwangu kwamba dini ya Muhammad ni dini bora kuliko dini zote ulimwenguni. Naapa kwa jina la Mola! katika uhai wangu hataweza kukudhuru mtu yeyote miongoni mwa Qureish".

17. Jalaludeen Suyootee ameeleza hadithi katika Tafseer-i-Durri Manthoor inatokana na Umar na Ibn Shuaib na ushuhuda wa Ibn Mardwaih inasema hivi: Mwaka mmoja kabla ya Hijra (Mtume kuondoka Maka kwenda Madina) usiku wa mwezi 17 (kumi na saba) Rabee-ul-Awwal, Mtume alipata heshima ya kwenda Meraji. Abul Fida anaandika kwamba zipo hitilafu za rai juu ya Meraji, kama amekwenda kwa kiwiliwili chake au kama kuona ndoto ya kweli.

Watu kwa kawaida wanaamini kwamba Mtume alikwenda Meraji kwa kiwiliwili chake, lakini baadhi ya watu wanadhani kwamba ilikuwa ndoto lakini ya kweli. Ndivyo ilivyoelezwa kwamba Aisha amesema Mtume hakwenda Meraji kwa kiwiliwili chake bali Mola akafanya roho yake kwenda mbinguni usiku wa Meraji. Vile vile imehaditihiwa kuwa Muawiyah alikuwa akitakidi vivyo hivyo kwamba Meraji ilikuwa usingizi wa kweli tu. Ibn ls'haq na Ibn Jareer Tabari vile vile wametoa hadithi kutokana kwa Aisha kwamba usiku wa Mera|i kiwiliwili cha Mtume kilikuwa pale pale (kitandani) na Mwenyezi Mungu amepeleka roho yake tu juu mbinguni.

18.    Mulla Ali Qari katika kitabu chake Sharh-i-Fiqh-ul-Akbar anaandika kwamba kwenda Meraji Mtume kwa kiwiliwili chake alipokuwa yu macho na kutembea juu huko mbinguni ni kweli na yenye hakika na hadithi zimepokewa zinazothibitisha kisa cha Meraji; Kwa hiyo kila mwenye kukanusha au kutia shaka juu ya kwenda kwake Meraji basi huyo ni mkosi bali Mzushi. Kadhalika Hafiz Ahmed Fazli Ayadh AI-Qazi katika kitabu chake Shi-fa Fi Ta'areef Huqooq U Mustafa, ametia mkazo kwamba hakuna hitilafu yoyote juu ya ukweli wa kwenda Mtume Meraji na kama ilivyothibitisha Kurani. Akaendelea zaidi kueleza kwamba Abul Hamra anasema kwamba Mtume amesema, "Usiku wa Meraji nalipopita kati ya mbingu naliona juu ya ARSHI (mbingu ya mwisho juu) imeandikwa hivi: La llaha lllallahu Muhammad ur Rasool-ullah Ayyadtohu be Aleeyin". (Hakuna Mungu bali yeye Subhanan Wataala na Muhammad ni mjumbe (Rasool) wake, ambae nimemsaidiza (tegemeza na Ali). Vile vile Jalaluddeen Suyootee katika Duri-i-Manthoor ameandika hadithi iliosemwa na Ibn Adi na Ibn Askari kama walivyosikia kwa Sahaba Anas Ibn Malik kwamba Mtume alisema, "Nalipokwenda Meraji nikashuhudia juu ya kipaa cha Arshi imeandikwa "LA llaha lllallahu Muhanwnad or Rasool-llah Ayyadtuhu bi Aleeyin".

19. Ameeleza Qadhi Husein Bin Muhammad Diyarbakri Al Maliki katika kitabu chake Tareekhul Khamees kuwa  walipo afikiana makafiri wa Kikureshi kumuua Mtume Muhammad (SA.W.). akaja Jabreel (Malaika mletaji Wahy) kwa Mtume na akampasha habari juu ya hila zao na akamtaka asilale kitandani mwake bali atoke na  aende Madina.

20. Ibn Aseer Juzari ameandika katika kitabu chake Tareekh-ul-Kamil kwamba ilipoingia kiza cha usiku makafiri wakikureshi walikusanyika mlangoni mwa Mtume kwa kusudi ya kuvizia atapolala kitandani mwake ili wamshambulie na kumuua. Mtume akaona mkutano nje   na akamwamrisha AIi Ibn Abi Talib, "Lala kitandani mwangu na ujifunike toka kichwani mpaka miguuni kwa shuka langu kijani. Kuwa na hakika hayatakufikia madhara yeyote". Vile vile alimwamuru Ali awakabidhi wenye amana zao walizoziweka kwake (Mtume). Hapo Mtume akatoka nje ya nyumba yake huku anasoma aya kidogo za mwanzo wa SuraYaseen (S. 56) mpaka aya "Fa hum la Yubsiroon" na akawarushia kichwani mwa makafiri wakikureshi ukofi mmoja wa mchanga, na akashika njia ya Madina na Makureshi wasimwone.

21. Jalaludeen akaendelea na kisa hiki katika Tafseer-i-Durr Manthoor kwa ushahidi madhubuti unaotokana na Ibn Abbas kwamba Ali Ibn Abi Talib aljiifidia roho (maisha) yake juu ya Mtume na akalala kitandani mwake na kujifunika kwa shuka la Mtume. Wakati wote huo mpaka asubuhi Makureshi walioizunguka nyumba wakifikiria kwamba Mtume alilala na wakifanya mipango ya kumuua Mtume.

22.Katika Usudul Ghaba cha Ibn Aseer Juzari na Ihya-ul-Uloom cha Ghazali na Tareekhul Khamees cha Qadhi Husain al Diyarbakri imoelezwa kwamba alipolala Ali kitandani mwa Mtume, Mwenyezi Mungu aliwaambia kwa (Wahy) Jibreel na Meekaeel (Malaika watukufu, "Nimefanyiza udugu kati yenu wawili na nimejalia umri wa mmoja katika nyie kuwa zaidi kuliko mwenziwe. Kwa kufanya hivyo nani mojawapo yu tayari kufidia maisha yake kwa nduguye? Waliposikia hayo kwa Mwenyezi Mungu,' wote wawili wakakataa kumfidia maisha juu ya mwenziwe. Ndipo Mwenyeii Mungu akawaambia, "Je, hamwezi kuwa kama Ali Ibn Abi Talib? Tazameni mimi nimefanyiza udugu kati ya Mtume Muhammad (SA.W.) na Ali,na sasa Ali, amelala kitandani mwa Muhammad (S.A.W.) kwa kutaka kumfidia maisha yake kwa kuwa ndugu yake. Basi sasa nyinyi wote wawili teremkeni kwenye ardhi na nendeni mkamlinde Ali na maafa ya Makureshi. Hapo watukufu hawa wawili wa kimalaika wakateremka   na   kila   mmoja   akashika mahala pake, Jibreel kwenye kichwa cha Ali na Meekaeel kwenye  miguu ya Ali. Jibreel akanena, "Salaam na pongezi kwako. Nani kama wewe Ee mtoto wa Abu Talib! ambaye Mwenyezi Mungu amefanya fahari (kwa kitondo chako) juu ya malaika?" na alipokuwa Mtume yupo njiani kwenda Madina, Mwenyezi Mungu akamteremshia aya zifuatazo katika kumsifu Ali:

"WA MlN-AN-NASl MAN-YASHRI NAFSAHUBTIGHAA MARDHAILLAAHl WALLAHU RAOOFUN BIL-IBAAD".

(Na katika watu wauzao nafsi zao kwa kutaka radhi ya Mwenyeil Mungu; na Mwenyeii Mungu ni mpole kwa watumwa wake) (S.2.207)-

  23.    Mwandishi wa historia Mas'oodi katika kitabu Tareekh Murooj-ui-dh-Dhahab na Ma'adinul Jawahir anaandika kwamba Mtume alipowacha Maka kwenda Madina, Abu Bakr na watumwa weke Aamir bin Faheer na Abdalla bin Areeqat Daylani walifuatana naye. Abdalla Ibn Areeqat alikuwa bado hakusilimu bali welimchukuwa kuwaonyesha njia.

24.    Abul Fida katika kitabu chake Kitabul Mukhtasar fi Akhbar-'ie-Bashar ameongeza kusema kwamba Mtume alipoondoka Maka kuelekea Madina Makureshi baada ya kumkosa nyumbani mwake wakachukua khatua kubwa kumtafuta Mtume, basi Suraqa Ibn Malik alipelekwa kumfatilia Mtume, mara akafika karibu na Mtume, alipomwona tu Abu Bakr akasema, "Eee Mtume, mwenye kututafuta amefika". Mtume akajibu, "Usiogope na usihuzunike; Mwenyezi Mungu yuko na sisi". Alipokwisha sema Mtume akamwapiza Suraqa. Mara tu farasi wa Suraqa akazama mpaka tumboni ndani ya ardhi ngumu. Suraqa kwa moyo wa bidii akamwomba Mtume. Niombee niepukane na adhabu hii, na nakuahidi kwamba nitawarejesha wote wanaokutafuta 'na wenye kukufukuzia". Hapo Mtume akamwombea Dua na Suraqa akatoka katika kuzama ardhini. Pale pale akarejea na akawarejesha wale wote wanaomtafuta kila aliemkuta.Mtume akafika Madina mwezi 12 Rabeeul-Awwal mwaka.wa kwanza wa Hijra na akateremka Quba.

25.    Sheikh Zainuddeen Umar ibn al Wardi katika kitabu chake Tatimmatul Mukhtasar fi. Akhbari Bashar inaojulikana kwa jina Tareekh Ibn Alwardi anaandika kwamba baada ya kufika Mtume Quba . akatia msingi wa msikiti wa Quba ambao Mwenyezi Mungu katika Qur'ani kaitaja hivi "LA-MASJIDUN USSISA ALAT-TAQWA"

(Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa kumcha Mungu) {S.9.108). Na Sheikh Abdul Haq mwanachuon; wa Delhi mpokeaji hadithi anasema katika kitabu chake Jadhbul Quloob kwamba watu wa Quba walimwomba Mtume awajengee msikiti", bas; hapo Mtume "akawataka Masahaba watukufu mmoja wao ampande ngamia wa Mtume na azunguke naye". Mara Abu Bakr akainuka na akampanda huyo ngamia lakini ngamia hata kidogo hakutikisika wala hakuondoka. Baada ya Umar akajaribu kumpanda na mnyama asiondoke wala kutikisika. Ndipo Ali' akasimama na kwenda kumpanda mara alipotia miguu yake katika kikuku cha kupandia tu mara ngamia akanyanyuka. Mtume tena akasama, "Acha hatamu, kwani ameamrishwa na Mwenyeri Mungu azunguke". Kwa hivyo akachimba misingi ya msikiti kufuatia nyayo (alama) za   ngamia,   na   akawataka watu wa Quba wakusanye mawe. Tena akafanya alama kwa mkuki wake kuonyesha Qibla na akaweka jiwe la msingi kwa mkono wake mutukufu.

26.Nesaee ametoa hadithi katika kitabu chake Khasa'is fi fadhli Ali Ibn Abi Talib na hujulikana kitabu hicho kwa Khasaisi Nasaee, iliopokewa na Zaidi Ibn Arq-qam kwamba milango ya baadhi ya majumba ya masahaba ilifunguka ndani ya msikiti (Masjid-un-Nabi). Mtume alitoa amri milango yote ifungwe isipokuwa mlango wa nyumba ya Ali. Masahaba wakaonyesha uchungu na kutoridhaka kwa amri hiyo. Ndipo Mtume akasimama na akawahutubia. Baada ya kumsifu Mola akasema, "Kwa mujibu wa amri ya Mwenyezi Mungu nalikuamrisheni kuifunga milango yenu na Ali aiweke wazi; hoja na mabishano yenu hayatakiwi. Sikufunga wala sikufungua mlango wa mtu yeyota kwa hiari yangu. Nalifuata kama nilivyo amrishwa na Mwenyezi Mungu".

27. Abul Fida anaandika, "Basi Mtume katika Madina akaanzisha udugu kati ya Masahaba Muhajireen (wahamiaji kutoka Maka) na Ansaar (wasaidizi watu wa Madina) na akamtukuza Ali kuwa udugu naye. Abu Bakr akafanywa ndugu na Khaarijaa Bin Zaid Kadhalika Abu Ubaidah bin Jarrah akafunganishwa udugu na Sa'ad bin Ma'az, na Umar bin Khattab pamoja na Atban Bin Malik, Abdul Rahman bin Auf pamoja na Saad bin Rabee, Usman bin Affan pamoja na Aus bin Thabit, Talha bin Ubaidullah pamoja na Kaab bin Malik na Saeed bin Zaid pamoja na Ubai bin Kaab.

28.Sayyeed Nooruddeen Abul Husain Ali bin Abdllah Samhudi al Madani   ash-Shafe'i  anaandika   katika   Khulasatul  Wafa kwamba Mtume alifanyisha udugu kati ya Muhajireen na Ansaar na aliwaamuru kama kila wawili wawili (mmoja Muhajir wa pili Ansaar) waanzishe udugu kati yao; kisha Mtume akashika mkono wa Ali bin Abi Talib na akasema, "Huyu hapa ndugu yangu".

29.Na Abdul bir katika Istiaab kitabu mashuhuri kilicho andikwa na Masahaba, anasema, "Mtukufu Mtume alivyowafanya udugu kati ya Muhajireen (wafuasi wake wa Maka) katika Maka vivi hivi -alianzisha udugu kati ya Muhajireen na Ansaar katika Madina, na 'katika tukio zote mbili elimtukuza Ali kwa kumfanya ndugu yake na akasema, Wewe ndugu yangu hapa duniani na vile vile baadaye Akhera".

30. Katika Saheeh Bukhari ipo hadithi inayotokana na Aesha kwamba kasema kabla ya kuja dini ya kiislam, Makureshi siku ya Ashura (mwezi kumi Muharram, mfungo nne) walikuwa wakifunga (kuto'Kula) siku hiyo, na Mtume (S.A.W.), alipokuja Madina vile vile akifunga na akiwaambia wengine vile vile wafunge, lakini ilipofika mwezi wa Ramadhani na kwa amri ya Mwenyezi Mungu mwezi Ukawa Fardhi (lazima) Waislamu kufunga basi kufunga "siku ya Ashura akawacha (asifunge). Imepokewa kwamba Abdullah bin Mais'ood (siku ya Ashura) alikuwa akila mara Ash'as akatokea kumwona ibn Mas'ood anakula akasema, "Leo ni siku ya Ashura!" Abdallah bin Mas'ood ekasema, "Kabla mwezi wa Ramadhani haukuwa fardhi kufunga hapo siku ya Ashura ikifungwa lakini tangu kuwa lazima kufunga Ramadhani basi Ashura ikawachwa. Njoo ule pamoja nami."

31.Abdul Qasim Sulaiman ibn Ahmed Tabrani ameandika katika Mu'jami Kabeer hadithi ya Mtume iliyopokewa na Abdallah bin Mas'ood kwamba amesema "Mwenyezi Mungu ameniamrisha nimwoze Fatima na Ali". Tabrani vile vile ameeleza hadithi ya Mtume iliyopokewa na Jabir kwamba Mtume amesema hivi, Watoto na dhuria wa Mtume wote wametokana upande wa mwana' wa kiume wao lakini watoto wangu wanatokana na Ali"..Yahya Aamiri katika kitabu chake Riyadhul Mustatab anasema, Mtume alipokwisha mwoza Fatima na Ali akabashiri kwamba kuwaoza hawa (Fatima na Ali), ilikuwa imetengenezwa na Mwenyezi Mungu ambae kajaalia ukoo wangu kauweka kutoka upande wa Ali. Shaikh Abdul Haq kotika kitabu chake Madan-un-Nuboowah, ameandika hivi, "Kati ya moja katika matokeo muhimu ya mwaka wa pili (2 A.H.) ya hiijra ni kuolewa (harusi) Fatima na Ali. Anas bin Malik anahadithia kwamba, "Nalikuwa kwa Mtume mara ikamdhihirikia alama ya kuferemshiwa Mtume Wahy, nikaona na ilipokwisha tu, Mtume akasema, "Ee Anas sasa hivi Jibrili amekuja kwangu na ameniambia kwamba Mwenyezi Mungu anakuamrisha umwoze Fatima na Ali".

32.Katika Madarij-un-Nuboowah vile vile imeelezwa kwamba katika vita vya Uhud maadui walipigana vita vikali vya nguvu hata Waislam wakakimbia na wakamwacha Mtume peke yake. Mtume kwa uchungu na ghadhabu mno ilimpata ikawa linamtoka jasho na kudondoka kutoka kipajini mwake. Kwa ghafla akamwona Ali amesimama ubavuni mwake. Mtume akamuliza, "Kwa nini wewe hukukimbia pamoja na ndugu zako?" Ali akajibu, "Nikufuru (niwe kafiri) baada ya kuwa nimeshaamini? Nimeahidi kukutumikia. Nina kazi gani na watoro? Kwa bahati mara kikundi cha makafiri (maadui) wakamwelekea Mtume, hapo Mtume akamwambia.Ali huu ni wakati wa kunisaidia na kunivusha na mashambulio ya kikundi hiki na hakika akamtumikia kama ilivyombidi. Ali alipopata amri hii kwa Mtume aliwaangamiza maadui na idadi kubwa yao akawapeleka motoni.Wengine wote akawatawanya. Imeeleweka kwamba siku hiyo Ali' alipata jeraha kumi na sita (16) mwilini mwake ambayo nne katika jeraha hizo zilikuwa za kudhuru sana, hata kila mara alipopata moja katika hizo alianguka kutoka farasini mpaka chini, na mara zote nne kila alipoanguka Jibreel akamwinua chini na kumweka juu ya farasi na akasema "Ee' AIi pigana vizuri, Mwenyezi Mungu na Mtumewe wamefurahi nawe". Baadaye Jibreel akamweleza Mtume namna apiganavyo Ali na ushujaa wake. Mtume akasema, "Kwa nini Ali asijitose na kujitia hatarini roho yake kwa hali yeye ni wangu na mimi ni wake?" Pale mara Jibreel akasema, "Na mimi ni wenu wote wawili". Vile vile imehadithiwa kwamba katika vita hiyyo hivyo mlinzi wa (Janna) pepo katika kumsifu Ali alikuwa akisema "LA SAIF llA DHULFIQAR WA LA FATA ILLA ALI ALKARRAR" (Hakuna upanga bora kuliko Dhulfiqar na wala hakuna kijana Shujaa kuliko Ali mshupavu). Vile vile mpokea hadithi Abdul Haq katika kitabu chake hicho hicho amesema tukio la "Naadi-Aliyan Madhharal Ajaib" (Mwite Ali mtoa ajabu) imetokea katika vita hivi.

33.    Abu Abdullah Muhammad Ibn Abdullah maarufu kwa jina la Hakim Naishapuri katika kitabu Mustadrak na Sheikh Waleeyullah mpokea hadithi wa Delhi katika kitabu Qurratul Ainain anasema kwamba Aesha amesema kwamba Abu Bakr baba yangu amenisimulia kuwa siku ya vita vya Uhud watu walipo mkimbia Mtume na wakatawanyika, basi mimi nalikuwa mtu wa kwanza kurejea na nikamwona Mtume kwa mbali. Baadae mtu mmoja alietaka kuja mbele ya Mtume akaja nyuma yangu na akanigandamiza, nilipogeuka nikamwona kumbe Abu Ubaidah Ibn Jarrah.

34.    Jalaluddeen Suyoot katika Durri Manthoor na ibn Jareer Tabari katika Tafsir Ibn Jareer ameeleza kwamba Umar amesema "Siku ya vita vya Uhud makafiri walipowashinda Waislamu basi hapo kuivusha roho yangu nikakimbia na nikapanda jabali. Jinsi mambo yalivyokua wakati ule hata nilikuwa nikirukaruka  na   kukiuka kama mbuzi wa milimani". Fakhruddeen Raazi anaeleza katika  Tafsir Kabir kwamba Umar ni mmoja miongoni mwa wakimbizi, lakini hakukimbia mwanzoni na wala hakukimbia sana. Yeye alikimbia na mpaka akapanda Jabali. Uthman vile vile alikuwa miongoni mwa wakimbizi na alikimbia mbali sana yeye na Saad Ibn Waqas na Aqba. Akarejea baada ya Siku tatu. Ibn Atheer Juzari katika Tareekh-ul-Kamil ameongeza kusema miongoni mwa walioshindwa na kukimbia katika Waislamu alikuwa Uthman ambae alikimbia mbali mpaka mahala paitwapo Aawas   na   akakaa   huko    baada ya siku tatu akarejea kwa Mtume. Mtume akamwambia alipomwona amerejea, Hakika nyie watu mmekimbia mbali sana". Abdul Haq ameeleza zaidi katika Madarijun-nuboowah kwamba Masahaba kwa hivyo waligawanyika vikundi vinne. Kikundi kimoja kikapigana kwa ushupavu na makafiri; kikundi kingine wakapigana mpaka wakauwawa; kikundi cha tatu kikakimbia mpaka majabalini kujivusha na kikundi cha nne kikakimbia hadi mjini; Uthman alikuwa katika kikundi cha nne.

35.    Shaikh Abdul Haq anaandika katika JazbuI-Quloob kuwa "Imepokewa hadithi kwamba Mtume alisimama kwenye kaburi la Mas'ab bin Umair, mmoja katika waliouwawa katika Waislamu katika vita vya Uhud na akasoma aya ifuatayo ya Qur'an, MINAL MUMINEENA RIJAALUN SADAQOOMA'AHADULLAHA ALAIH" (na wapo miongoni mwa walioamini ambao walitimiza kama walivyomwahidi Mwenyezi Mungu. S.33.23), na akasema "Ee Mola mtumwa wako na mtume wako anashuhudia kwamba vatu hawa wameuwawa (Shaheed) kwa njia yako". Akaendelea kusema, uwazuru, mashuhadaa wa uhud waliouawa katika   Uhud) na uwasalimu mpaka ardhi na mbingu zipo. Kila mwenye kuwapa salamu anapata majibu kwao! Baadaye Mtume akaenda kwenye " makaburi ya wafia wa dini (Shuhadaa) wengine na akasema, "Hawa ni wafuasi wangu ambao siku ya Qiyama nitawashuhudia ukamilifu wa imani yao kwa Mwenyezi Mungu. Aliposikia hivyo Abu Bakar. akasema Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa nni sisi si wafuasi wako? Mtume akajibu, "Ndio wewe ni mfuasi wangu lakini siwezi kujua nini mwenendo wako baada yangu!"

36.    Ibn Aseer Juzari anaandika kwa mujibu wa Tareekh ul Kamil Baadaye Mtume akarejea Madina siku ya Ijumaa mosi. Muhammad Ibn Sa'ad Alwaqidi ameandika katika Tabaqaat - us Sahaba Wat-Tabeen, "Alipofika Mtume Madina, kawasikia wanawake wa kabila Banee Abdul Ashhal wakiwalili'a wafiwa wao waliouawa (vitani) akasema (Mtume), Ole! hakuna mtu wa kumlilia Hamza' Sahaba Sa'ad bin Ma'az akasikia masikitiko ya Mtume, na akawaendea wanawake wa kabila Banee Abdul Ashhal na akawapeleka kwake Mtume huko wakamlilia Hamza. Mtume aliposikia hivyo akawaombea Dua ya kheri na baadaye akawarejesha kwao. Tokea siku hiyo hakuna mwanamke yoyote katika Ansaar aliomlilia mfiwa wake isipokuwa amlilie Hamza kwanza.

37.    Vile vile imeelezwa katika Tabaqaat-us-Sahaba cha Sa'od Alwaqidi kwamba Jabir Ibn Abdullah amehadithia kuwa Muawiya wakati alipokuwa akitawala akataka kufanya njia ya kupitia maji kwa njia ya Uhud, wasimamiaji kazi yake wakamuarifu kwamba haitawezekana kufanya hivyo hadi mfereji upite juu ya makaburi ya wafia wa Uhud. Muawiya akawajibu na kuwaamrisha wazichimbe na kuyafufua makaburi. ilipopitishwa amri hiyo, hapo inaonekana watu wanabeba maiti. begani mwao na hao maiti wakionekana kama wamela la tu. Walipokuwa wakizichimba kaburi sururu ikaupata mguu mmoja wa Hamza, damu mbichi ikachururika kwenye jeraha. Na Shaikh Abdul Haq ametaja kutoka kitabu Shifa-ul-Asqam katika kitabu chake Jazbul Quloob kuwa alipotaka Muawiya kuijenga mfereji, akaamrisha kwamba maiti ya wafia wa Uhud waondolewe kaburini mwao na wazikwe mahala pengine. Kwa ghafula sururu ikapiga mguu mtukufu wa Hamza na damu mbichi ikachururika. Na walipokuwa wasimamizi wa Muawiya wakichimba mfereji walitangaza Madina kwamba Muawiya ameazimia kupitisha mfereji na kwamba watu wazihamishe maiti za jamaa zao.

38. Ahmed bin Hambal anahadithia katika Musnad chake kwamba Mtume amesema, "Aliflka malaika mmoja kwangu ambae kabla yake hakupata kuja. Akaniambia mwanako huyu Husein. atauawa. Ukitaka ninaweza kukuonyesha udongo wa ardhi wa mahala atapouawa. Hapo akatoa udongo na akanipa mimi".

Na Abi Muhammad Husain bin Mas'ood Baqhawi Ash Shafee anaandika katika kitabu chake Mu'jam hadithi alosimuliwa na Anas kwamba malaika mshika hesabu ya mvua, akataka kuja kuonana na Mtume alipokua chumbani mwa Ummi Salmah na akamruhusu, basi Mtume akamwambia Ummi Salmah simruhusu mtu yeyote

kuingia ndani chumbani kwake (mpaka huyo malaika akaenda zake), lakini mara Husien akatokea na akaJitia ndani na akamkumbatia Mtume. Mtume akamchukua mikononi mwake na akaanza kumbusu na kumbembeleza. Yule malaika akauliza, "unampenda sana?". Mtume akajibu, "Ndio! Malaika akasema, "Karibu wafuasi wako watamwua. Ikiwa utapenda, nikuonyeshe mahala atapouawa". Kusema hivyo akamwonyesha Mtume udongo mwekundu na Ummi Salmah akauchukua kwa Mtume na akaupiga fundo katika kitambaa chake. Kwa hivyo tangu siku ile tulikua tunasikia kwamba Husain atauwawa katika Karbala. Hadithi hii vile vile imeelezwa na Abu Hatim, Baihaqi na Abu Naeem. Hatim na Baihaqi wameipokea kwa  Ummul Fadhl ambaye amehadithia hivi:— "Siku moja nikamchukua Husein na tukenda kwa Mtume na nikamweka pajani mwako. Huku akapiga kite nalipotazama nikaona machozi yakichururika machoni mwa Mtume. Baadae Mtume akaniambia, "Ee, Ummul Fadhil Jibrili amenipe habari kuwa wafuasi wangu watamuua mwanangu huyu na amenipa udongo mwekundu wa mahaala atapouawa!" Abu Naeem ameeleza hadithi kutokas kwa Ummi Salamah kwamba alisema,"Walikuwa Hassan na Hussein wanacheza nyumbani kwangu, mara akateremka Jibriil kwa Mtume na akamwambia wafuasi wako watomwua mtoto wako Hussein baada yako! Tena akampa Mtume baadhi y udongo, baada ya kunusa ule udongo Mtume   akasema.   "Kweli,   Rasikia,  harufu ya maumivu na shida humo; Ee. Ummi Salmah, utapogeuka udongo huu kuwa mwekundu, hapo ujue mwanangu Hussein ameuawa! Ummi Salmah udongo ule akautia katika chupa.

39   Ibn Sakeen Baqhwi na Abu Naeem wanahadihtia hadithi imetokana na Anas Bin Harith ambaye amesema, "Nimemsikia Mtume akisema, "Mtoto wangu Husein atauwawa kwenye ardhi inayoitwa Karbala; kwa hivyo wataokuwa hai siku hiyo miongoni mwenu inawapasa wamsaidie". Ibn Rahwaih, Baihaqi na Abu Naeem wanaeloza kwamba Ummu Salmah amehadiuthia hivi: "Siku moja alipokuwa Mtume amelala, mara akazindukana usingizini na nikamwona amehuzunika sana na mkononi mwake amekamata udongo mwekundu na huku akiugeuza mara kwa' mara. Nikamwuliza, Ee Mtume! Ni la nini hili donge la udongo? Akanijibu, "Jibreel amenipa habari kwamba Husein atauawa katika lraqi na hili donge la udongo ni la mahala atakapouawa. Hakim katika kitabu chake Mustadrak ameandika hadithi iliyopokewa na Ibn Abbas kwamba Mwenyezi Mungu amemjulisha Mtume wake kuwa kwa kuuwawa nabi Yahya mtoto wa  nabii Zakaria nimelipiza kisasi kwa kuwauwa watu sabini elfu na nitalipiza kisasi kuwauwa watu laki moja na arbaini elfu kwa kuuawa mjukuu wako (Husein)".

40.    Katika Tareekh-ul-khamees imeandikwa kuwa AMR bin Abdiwad alikuwa shujaa maarufu miongoni mwa mashujaa wa Arabuni, na watu wakiamini kuwa sawa na wapigani elfu. Siku ya vita vya Khandaq akajitoa nje kati ya jeshi na huku amepanda farasi na kuonyesha fahari na kuruka ruka na kuita kuja kupigana vita naye. Masahaba wake Mtume walipoona vile walifadhaika na walikaa kimyaa! Utasema kama ndege wamekaa vichwani mwao (wamepigwa na bumbuwazi) kwa sababu walikuwa wanajua vizuri ushujaa wa Amr bin Abdwad. Basi Amr akaanza kupiga kelele kwa kusema, "Yupo mtu kuja kupigana na mimi? Ali akamjibu Mtume na akamwomba, "Ee Mtume unaniruhusu nende kumkabili?" Mtume akamjibu, "Kaa kitako. humjui Amr wewe". Huku Amr tena akapiga kelela na akaanza kuwadhihaki masahaba wa Mmtume, kwa kusema "Iwapi' hiyo pepo ambayo mnajidai kwamba mtu yeyote akiuwawa ataingia humo? Yupo mtu miongoni mwenu anaethubutu kuja kupigana na mimi?" Kusikia hivyo. Ali tena akasimama na akamwomba Mtume, "Ee Mtume unaniruhusu niende kupigana na huyu." Mtume akasema tena "Fohamu. kwani hujui kwamba huyu ni Amr?". Pale pale kwa mara ya tatu, Amr akaita kupigana. Ali hapo akasimama na akasema, "Ee Mtume sasa niruhusu nikapigane nae." Mtume akamwambia. "Kaa, wewe humjui huyu. Huyu ni Amr." Ali akajibu. "Ijapokuwa yeye ni Amr naomba niruhusiwe kwenda kupigana nae. Mara Mtume akamruhusu kwenda kupigana na Amr.

Katika Seeratun Nabaweeyah kisa hiki ameeleza zaidi hivi, "Mtume alipomruhusu AIi kwenda kupigana, Mtume vile vile alimpa Ali upanga wake mashuhuri unaojulikana kwa jina la Dhulfiqar na akamvalisha deraya (nguo ya pete za chuma) na akamvika kilemba chake mwenyewe Mtume, na akamwomba Mwenyezi Mungu hivi, "Ee Mola msaidie Ali mbele ya Amr. Ee Mola Ali ni ndugu yangu na binamu yangu. Usiniache peke yangu; na wewe ndiwe Mbora wa wanaorithi". (21.89) na katika hadithi nyingine imesemwa kwamba Mtume akavua kilemba chake kuelekea mbinguni na akaomba dua, "Ee Mola wangu umemwondoa kwangu Ubaidah (kauawa) katika vita vya Badr na umemchukua Hamza (kauawa) katika vita vya Uhud, sasa amebaki huyu ndugu yangu Ali kwa hivyo Bwana usiniache peke yangu, na wewe ndiwe Mbora wa wanaorithi.

41.    Mwandishi wa historia Abul Fida 'katika kitabu chake Kitabul Mukhtasar fi-Akhbaril; Bashar anaandika hivi:- Ali alipojongea mbele ya Amr kutaka kupigana naye Amr akasema, Ee mtoto wa ndugu yangu, naapa kwa Mungu mimi sitaki kukuuwa". Ali akamjibu, Lakini mimi naapa kwa Mungu nataka kukuuwa". Aliposikia haya Amr akachupa kutoka kwenye farasi wake kwa ghadhabu na akaikata miguu ya farasi kwa hasira kali. 'Kisha akaenda mbela ya Ali, na wakaanza kupigana kwa ukali. hadi mahala wapiganiapo palitifuka. Kwa ghafula Waislamu walisikia sauti ya "Allahu Akbar" na wakajua kwamba Ali ameshamuuwa Amr. Hapo vumbi ilipotuama wakamwona Ali amekaa juu ya kifua cha Amr na huku anakikata kichwa chake.

42.    Tareekh-ul Khamees ameandika kwamba Ali alipomuuwa Amr, hakutaka (kuckukua) vitu vya Amr (ijapokua siku hizo ilikuwa desturi). Kwa sababu hii alipofika dada yake Amr kwenye maiti ya ndugu yake na akaona mshindi hakuteka hata kitu kimoja bali aliwacha kila kitu alichovaa yule shujaa, ndipo akasema, "Kweli mtu aliemuuwa Amr bila shaka ni katika ukoo mkubwa". Tena akauliza nani amemuuwa Amr, na akaambiwa Ali bin Abi Talib ndie aliemuuwa. Kusikia jina hilo, hapo hapo akatunga mistari miwili ya shairi na akaisoma. Tafsiri ya mistari miwili hiyo ni hii, "Ingalikuwa Amr ameuawa na mtu mwingine si huyu aliomuuwa ningelimlilia milele, lakini hakuna shaka aliomuuwa ni mtu kamili (bilka lawama) na tangu kale akijulikana kwa "utakatifu wa mji" kwa hivyo nimepata faraja na utulizi wa moyo wangu".                   

43.    Katika kitabu Madarij-un-Nubuwwah imeelezwa kwamba siku ya vita vya Khandaq, Ali alidhihirisha na kuoneyesha ushujaa usiokuwa na mfano wa kuweza kuotea. Imepokewa hadithi kwa Mtume kwamba mapigano ya Ali siku ya vita vya Khandaq ni bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko vitendo (Amali), vya (Umma) wafuasi wangu mpaka siku ya Kiyama, na Mtume akamwombea Dua na akampa tuzo upanga wake "Dhulfiqar'.

44.    Jalaluddeen Suyootee ameandika katika Durr-Man thoor na imepokewa na Ibn Abi Hatim, Ibn Mardwaih na Asakir wanahadithia hadithi kutokana na Abdllah Ibn Mas'ood mwenyewe kwamba alikuwa "akiisoma aya hii ya Qur'an  (33.25) "Wa Kafa-laahul Mu'mineenal Qitaala bi Aliyin'. Yaani, Mwenyezi Mungu akawakifia Waislamu mapigano (Ahzab) kwa sababu ya Ali.

45.    Shaikh Abdul Haq Dahlawi katika kitabu chake Madarijun' Naboowwah anataja maneno aliyoyasema Umar wakati ukiandikwa mkataba wa Hudaibiah. Umar kasema hivi:- iliniingia shaka na wasiwasi; nikubwa moyoni mwangu siku ya mapatano ya amani ya Hudaibiah na nalikwenda upande na Mtume siku ile ambayo kabla yake sikwenda ukomo ule. Ndivyo nikaenda kwa Mtume na nikasema,

"Ati wewe si Mtume wa Mwenyazi Mungu?" Mtume akajibu. "Hakika ndie Mtume." Nikasema. "Ati sisi  si wa haki na adui wa wakosefu?" Mtume akajibu. "Ndio sisi tuko haki". Tena nikasema, "Basi kwa nini tunastahamili aibu na fedheha kama hii na kurudi na amani namna hii?" Mtume akajibu. Ewe mtoto wa Khttab! BiIa shaka mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na sifanyi jambo lolote bila ya amri ya Mola.- Yeye pekee ni msaidizi wangu na Yeye hatapoteza utumishi wangu".

46.    Katika Saheeh Bukhari ipo hadithi ambayo inasema Umar amesema, "Siku ya Hudaibiah nalimuuliza Mtume kama yeye si Mtume wa kweli. Akanijibu kwamba yaye ni Mtume na hakuna shaka yoyote juu ya jambo hilo. Tena nikamwuliza basi kwa nini tunatii na kujifanya ukosefu wa imani. Hapo Mtume akasema, "Sikia, mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na sifanyi jambo lolote kinyume cha amri yake na ni Yeye msaidizi wangu pekee'.

47.    Allama Badruddeen Abu Muhammad Mahmood Al Aini Al Hanafi katika kitabu chake (Umdatul Qari ambacho ni maelezo ya Saheeh Bukhari ameandika kwamba Umar amesama hivi'. "Siku ya Hudaibiah nailiingiwa na shaka kubwa na nikamgeukia Mtume vibaya ambavyo sikufanya hivyo kabla yake." katika Tarekh-ul-Khamees ya Duyarbakri na Durr-Manthoor ya Jalaludden Suyootee wametaja maneno ya Umar: Naapa Wallahi tangu mimi kuukubali Uislam (kusilimu) sikuwa na shaka kama siku hiyo (Hudaibiah); Kwa hivyo nalikwenda kwa Mtume nikamwuliza, "Ati wewe si Mtume wa haki? akajibu, "Bila shaka mimi ni Mtume wa haki". Nikasema, sisi si wa haki na maadui waongo? Si wafia wetu watakwenda peponi na wafia wao wataingizwa motoni?. Mtume akajibu, "Naam sisi tuko juu ya haki na wafia wetu wataingia peponi", na maadui si wa haki na wafia wao wako motoni." Tena nikasema, "Basi kwa nini tunaridhia fedheha na ila juu ya dini? (maana yake kwa nini unatia sahihi katika mkataba?). Mtume akajibu, "Mimi ni Mtume wa Mola na siwezi kuvunja amri yake na Yeye ni msaidizi na Mwongozi wangu".

48.    Diyarbakri katika Tareekh-ul-Khamees ameongeza kusema kwamba Umar mara nyingi alikuwa akisema, "Nimefanya amali na vitendo vizuri vingi kama kusali, kufunga na kutoa Sadaka kufidia ule ujinga nalioufanya siku ya Hudaibiah".

Muhammad Ibn ls'haq, katika kitabu chake mashuhuri Seerat Ibn Hisham amesimulia kwamba Umar alikuwa akisema, "Kwa yale aliyotenda Hudaibiah siku zote nikijuta na kufidia juu ya jambo lile nikisali na kufunga mfululizo".

49.    Ibn Atheer, Juzari katika Tareekh-ul-Kamil ameandika: Ilipokua mkataba bado unaandikwa. Abu Jandal Bin Suhail huku pingu miguuni ametiwa akampita Mtume. Na wakati ule kwa kuwa mkataba wa amani ukiandikwa, iliwaingia shaka ya kuogofya mioyoni mwa masahaba wa Mtume, ilifika hata hofu ya kuangamia katika upotevu; kwa vile walisikia maelezo ya ndoto ya Mtume na walikuwa na hakika ya kushinda. Suhail baba yake Abu Jandal alipomwona mwanawe ametiwa pinguni basi akamwambia Mtume, "Mambo yote kati yetu imeshaamuliwa kabla ya kuja huyu Abu Jandal". Mtume akasema, "Kweli yamesha amuliwa". Baadaye akataka kumkabidhi Abu Jandal kwa Suhail; lakini Abu Jandal akaanza kupiga makelele, "Ee waislam! Mnaanirudisha kwa Mushrikina (wenye kuamini miungu mingi) ili wanifanye (kafiri) kuharibu imani yangu?". Kwa kusikia haya, basi ile kutoafiki na fitina iliokuwa mioyoni mwao Waislamu ikachemka ikachafuka na akawa mkali zaidi. Mtume akamwambia Abu Jandal, "Subiri na usiwe na haraka. Mwenyezi Mungu atafanya njia ya kuachiliana tukuokoa wewe na marafiki zako.Kwa vile mkataba wa usuluhisho umeshatengenezwa mimi sina njia ya kutenda kinyume chake".

50.    Tokeo hili kwa jumla katika Raudhatul Ahbab cha Jamalud-deen Ataullah Bin Fadhulullah inasema hivi: Umar aliposhuhudia tokeo hilo akachupa kutoka mahala alipokuwa' na akamjia Abu Jandal na akamtaka ati astahamili na huku kwa siri akimuashiri amwue baba yake Suhhail hata ule mkataba upinduliwe, lakini Abu Jandal hakupendezewa na nia hii.

51.    Anaeleza Ibnul Wardi katika historia yake hivi:- Baadaye Mtume akarejea Madina na akabaki humo mpaka' mwanzo wa mwaka wa saba wa al-hijra (A.H.) na katika mwaka huu Mtume akawaowa Ummu-Habeebah, Maymoona na Safiya. Na mwaka huo huo Markus, gavana wa Alexandria akampelekea zawadi (Mtume) kijakazi Maria, nyumbu na farasi, Duldul. Madarij-un-Nuboowwah ametaja kwamba Mtume kajiwekea Duldul kwa ajili yake. Baada ya Mtume. Ali akimpanda farasi yule. Baadaye alikuwa akipandwa   na   Hassan mpaka farasi akafa zama za Muawiyah.

62.    Imeelezwa katika Tareekh-ul-Khamees kwamba Vita vya Khaibar ilifanyika mwaka huo huo (7 A.H.) Abul Fida anahadithia kuwa, kati ya mwezi wa Muharram (7. A.H.) Mtume alifanya safari ya kwenda Khaibar. Siku hizo Mtume alikuwa pengine huumwa na upande mmoja wa kichwa. Kwa bahati alipofika khaibar akashikwa  na kuumwa kichwa. Kwa hivyo Abu Bakr akakamata bendera  na

akapigana vita vikali lakini akarejea bila ya kushinda. Baadaye Umar akashika bendera na akapigana vikali zaidi kuliko wa kwanza lakini akarejea vile vile bila ya kushinda. Alipojua Mtume matukio haya akasema, "Wallahi kesho nitampa bendera mwana muma yule anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mwenye kupendwa nao; na ambaye thabiti katika mashambulio na si mkimbizi, na mwenye kusimama imara na kushinda". Kuyasikia haya kila mmoja katika Muhajireen (wahamaji) na Ansaar (wasaidizi) akatamani kuipata hiyo bendera. Huku Ali akafika lakini akiumwa na macho. Mtume akamwita karibu yake na akampaka mate yake machoni mwa Ali; kwa kupakwa tu hapo mara maumivu yakatoweka. ndipo Mtume akamkabidhi bendera. Ibn Hisham katika Seerat anasema kwamba Mtume kasema, "Kesho nitampa bendera yule mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na aliyewekwa kushinda vita. Yeye si wakukimbia". Kwa hiyo siku ya pili Mtume akamwita Ali ambaye wakati ule alikuwa akiumwa na macho. Mtume akampaka mate yake machoni mwa Ali na akamkabidhi bendera na akamwamuru kwenda kupigana mpaka Mwenyezi Mungu amtimilizie ushindi.

53.    Nasaee katika Kitabul khasais anasimulia hadithi kutokana na Abu Buraida ambaye amesema: "Tulipoizunguka ngome ya Khaibar, Abu Bark alipokwenda na bendera hakufaulu na akarejea bila kushinda. Siku ya pili Umar akachukuwa bendera na akaenda,lakini akarejea bila kufanikiwa patupu; na Waislamu walivumilia uchungu mwingi. Kwa hivyo Mtume alisema, "Nitamkabidhi bendera kesho mtu yule anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtumewe, na yeye anapendwa nao. Hatarejea bila ya kushinda". Tuliposikia haya, tukapitisha usiku ule kwa furaha kwa kitumainia kwamba kesho itakuwa siku ya ushindi. llipopambazuka mchana, Mtume baada ya kusali sala ya asubuhi akaja na akasimama kati yetu. Tena akaiagiza ile bendera. Wakati ule kila mmoja katika masahaba alishughulika na matumaini ya kutaraji kupata ile bendera, wakati ule ule Mtume akamwita Ali ambaye alikuwa akiumwa na macho. Mtuma akatia mate yake mikononi na akampaka machoni mwa Ali na akamkabidhi bendera". Madarijun Naboowwah  ameendelea kusema, "Baadaye Ali akaenda vitani na bendera mikononi mwake, na alipofika kwenye boma la Qamoos akasimamisha bendera juu ya kipawa (Jabali). Padri mmoja wa kiyahudi aliekuwa akichunguli kutoka kwenye boma hiyo akauliza, Ee mwenye bendera! Nani wewe? Ali akajibu, "Mimi Ali mtoto wa Abu Talib". Yule padri akawaita watu wake na akasema, "Naapa kwa taurati kweli, nyie mtashindwa". Mtu huyu hatarejea bila kushinda vita" Katika Seerat cha Ibn Hisham na vile vile katika Tareekh cha Abul fida ametaja kwamba yahudi mmoja kwenye hiyo boma akamtazama Ali na akauliza, "Wewe ni nani? Ali akaitikia. "Ali Ibn Abi Talib" Hapo yule yahudi akasema, Na apa kwa Taurati! Utatutawala sisi. Ibn atheer Juzari anaandika katika Tareekhul Kamil chake kwamba yahudi akamungalia Ali akamwuliza. "Nani wewe?" Ali akajibu. mimi Ali mtoto wa Abu Talib Aliposikia yule haya akawaambia watu wake, , "Nyinyi Mayahudi, hakika nyinyi mtashindwa". Mtungaji kitabu cha Madarijun Naboowwah anadhani, "Huenda yule Yahudi alijua vema ushujaa wa Ali na amesoma sifa zake katika Taurati",

54.    Shaikh Abdul Haq akaendelea zaidi katika kitabu chake tulichokitaja mbele, "Mtu wa kwanza alietoka kwenye boma kuja kupigana ni Harith nduguye Marhab; alichukuwa mkuki mkubwa mno ambao uzito wa ncha yake ulikuwa, kiasi cha ratili 84. Katika kushambulia kwake mara moja aliwauwa baadhi   ya   Waislamu. Baadaye Ali akatoka kupigana naye, na kwa dharuba moja akampeleka motoni (akamwua). Alipopashwa habari Marhab juu  ya kuuwawa nduguye, yeye na baadhi ya maaskari shujaa wakatoka kwenye ngome ya Khaibar, kuja kulipiza kisasi cha ndugu yake. Inasemekana kwamba Marhab alikuwa mwenye nguvu, mrefu na mkali kuliko wote miongoni mwa mashujaa wa Khaibar. na hakuwa mtu hata mmoja aliyekuwa sawa naye katika boma lake. Siku hiyo alivaa mavazi mawili ya chuma na kuning'iniza mbavuni mwake mapanga mawili kafunga vilemba viwili na kuvaa kofia ya chuma juu yake kichwani. Akenda mahali pa kupigania kwa taratibu na huku anaimba mashairi ya ushujaa wake. Hakuthubutu hata mtu mmoja miongoni mwa Waislamu kutoka kupigana naye. Hapo Ali akatangulia mbele, na huku anasoma mashairi ya ushujaa kwa kumjibu Marhab.

Marhab ndiye aliyeanza na akajaribu kumshambulia kwa upanga wake Ali. Lakini Ali akaepuka pigo hilo, na akamrejeshea pigo la hguvu kwa Dhulfiqar juu ya kichwa chaka hata ikapasua kofia ya chuma. jozi ya vilemba, na kichwa hadi kooni mwake. Katika baadhi ya hadithi inasema pigo la Dhulfiqar likampasua mpaka kwenye paja,na  wengine wamehadithia kwamba pigo lilimpasua vipande viwili mpaka tandiko la farasi na Marhab akatokomea motoni vipande viwili. Baadae Waislamu chini ya amri ya Ali wakaanza kuwaua Mayahudi. Ali pekayake aliwaua saba katika wakubwa wa jeshi la Mayahudi, ambao walijulikana kuwa   mashujaa   sana. Baadae waliobaki wakaanza kukimbia kwenye ngome,na Ali kawafuatia kati ya msukosuko huo Yahudi mmoja, kwa ghafla akapiga

Dhawruba  moja juu ya mkono wa Ali wenye ngao: ngao ikaanguka chini na Yahudi wa pili akaichukuwa na akakimbia. Hapo Ali akaghadhibika na alijiwa na nguvu ya ajabu ya kitakatifu, na mara akaichupa handaki na akaja mbele ya mlango wa boma, na katika ghadhabu ile akaung'oa mlango wa chuma upande mmoja, akaukamata kama ngao, na kuanza kupigana.

Katika Seeratu Ibnu Hisham. Tariikhul Kaamil na Tariikhi Abul fida wameeleza kwamba Abu Rafe amabadithia kuwa. "Mtume alipomkabidhi bendera na akampeleka kwenda kupigana na vikosi vya Khaibar, sisi vile vile tulimfuata. Na Ali akawa anapigana hata akafika karibu na boma Yahudi mmoja akampiga dharba moja Juu ya mkono wa Ali kwa nguvu hata ngao ikamponyoka (a.s) Mara akaung'oa mlango wa khaibar upande mmoja, na akaukamata na kuufanya ngao na akaendelea kupigana mpaka Mwenyezi Mungu akamjalia ushindi.

 Baada ya kwisha vita, Ali akavurumisha mbali ula mlango. Kwa jinsi mlango ulivyokuwa mizito hata watu wanane kati yetu hawakuweza kuugeuza kwa urahisi". Katika Musnad cha Ahmad bin Hanbal imepokewa hadithi kwa Umar kwamba alisema hivi:— Baadhi ya masahaba siku ya vita vya Khaibar walikuja kwa Mtume, na kusema habari ya watu maalum kwamba wemekufa shahidi. Akaja mwingine na akasema. hayo hayo juu ya wengine. Aliposikia haya Mtuma, akasema, "Hapana haja kabisa. Nimemwona mtu yule hasa (uliyem-taja) katika moto wa jahannam". Tena akamwamrisha Umar hivi: Ee, mtoto wa Khattab nenda ukawatangaziye watu kwamba. hataingia peponi yayote isipokuwa mwenye kuleta imani ya kweli'. Basi nikaenda na nikatangaza kama nilivyo amrishwa, kwamba   hapana mtu mwingine atake ingia peponi isipokuwa wale wenye imani ya kweli".

55.   Imeelezwa katika Madarijun Nuboowwah kwamba aliporejea Mtume katika Khaibar alipofika kwenye kituo "Sahba" baada ya kusali sala ya alasiri, Mtume akaweka kichwa chake pajani mwa Ali na akalala.katika hali ya kulala matokeo ya kutoremshiwa Wahyi ikadhihiri kwake na ikaendelea mpaka jua likachwa. Ali alikuwa bado hakusali sala ya alasiri. llipokwisha Wahyi, Mtume akamwuliza Ali, "Umesali sala yako ya alasiri?" Ali akajibu, "Sikusali, Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu". Mtume akaomba kwa Mwanyezi Mungu, "Ee .'Mola, Ali alikuwa chini ya utii wako na utii wa Mtume wako.  Inua jua tena ili aweze Ali kusali sala ya alasiri". Mwenyezi Mungu hapo hapo akaikubali Dua ya mpenzi wake Mtume, na jua likachomoza tena (baada ya kuwa limekuchwa) na ikatandaza mwangaza wake milimani na nyikani. Na watu wakashuhudia mwujiza huu wa Mtume kwa macho yao. Kwa hiyo Ali akatawadha na akasali sala ya alasiri.

56.    Abu Ja'afar al Tahawi anaandika katika Mushkil-ul-Athar. hadithi inayotokana na Asma bint Umair amesema, alipowasili Mtume kituo cha Sahba akasali sala ya adhuhuri, tena akamtuma Ali kwa kazi ya dharura, aliporejea Ali, Mtume alikuwa amekwisha sali alasiri. Mara Ali alipofika Mtume akaweka kichwa chake pajani mwa Ali na akalala mpaka jua lilipokuchwa.

Alipoamka na akaarifiwa kwamba Ali hakusali sala ya alasiri. Mtume mara akaomba dua hivi, "Mola wangu, mtuma wako mahsusi Ali amejitolea nafsi yake kwa aJili ya Mtume wako. Tafadhali rejesha jua lichomoze tena kwa ajili yake." Asma akaongeza kusema, "kwa ghafula jua likachomoza na mwangaza Wake ukatandaza juu ya ardhi na milimani Ali akatawadha na akasali sala ya alasiri. Baadaye jua likatua tena."

 Qadhi Ayadh. vile vile ameandika hadithi ya juu katika kitabu chake kiitwacho Kitabush- Shifa.

57-lmeandikwa katika Saheeh Bukhari, kwamba Mtume katika safari ya kwenda Khaibar alikataza kuoa kwa njia ya Mut'ah na kula nyama ya punda. Katika maelezo ya hadithi hiyo, Al'lama Aini katika kitabu chake cha Umdatul Qari Lisharh-i-Saheeh Bukhari ananena hivi: Kwa mujibu wa maneno ya Hafidh Abdul Bir, juu ya kwamba katika safari ya Khaibar alikataza kuoa   kwa   njia ya Mut'ah si, sahii. Suhaili vile vila amesema kwamba, hakuna hata mmoja miongoni mwa wapokeaji hadithi na waandikaji wa historia ya Mtume aliyedai kuwa Mut'ah ilipigwa marufuku katika safari ya Kbaibar. Tena Bw. Shafiee kwa kuwategemea wapokeaji hadHhi wenziwe, amemtaja Malik aliyekuwa amemsikia Ali akinena kuwa mtume wakati ule wa vita Khaibar alikataza kula nyama ya punda tu Ibnul Qaiyyim, anaeleza katika kitabu chake Zaadul Ma'ad kwamba Sufiyan bin Oyana amesema, "Mtume katika muda wa vita vya Khaibar hakukataza kuoa kwa Mut'ah, isipokuwa alikataza kula nyama ya punda". Maneno kama hayo vile vile yameelezwa na Abu Amr na Ibnu Abdul Bir katika dibaji za vitabu vyao.

58.    Mwandishi wa historia, Abul fida anaeleza: Khaibar ilishindwa vita na kutekwa katika mwezi wa safar (mfungo tano) mwaka wa saba (7 A.H.). Watu wa Khaibar wakaomba amani, Mtume akafanya sharti (a), nusu ya mazao wapewe waislamu, na Mtume wakati   wowota   akitaka   kuwafukuza   mjini anaweza. Maombi yao yalikubaliwa. Pia watu wa Fadak walikubaliwa kwa sharti lile lile.   Mapato   yote ya Khaibar yalikuwa kwa ajili ya Waislam wote kwa jumla, lakini mapato ya Fadak yalikuwa mahsusi ya Mtume. Kwa sababu Fadak ilitekwa bila ya kutumia nguvu. Anahadithia Jalaluddeen Suyuutii katika Durul-i-Manthoor kwamba Bazaar, Abu Ya'li na Ibnu Abi Hatim wamepokea hadithi kwa Abu Sa'eed Khudhri kwamba ilipoteremshwa aya ya "Wa aatidhal Qurba Haqqahu" 17.26 (Na umpe jamaa yako haki yake), Mtume akampa binti yake Fatima ardhi (milki) nzima ya Fadak. Ibnu Abbas anaeleza kwamba ilipoteremka aya ya, "Na umpe jamaa yako haki yake", Mtume akamtuza (mwanae) Fatima ile milki ya Fadak.

59.    Ibnul Wardi ameeleza kuwa baadaye ikaanza mwaka wa nane wa A.H. Katika mwaka huu. Khalid bin Walee. Amr ibnul aas na Uthman bin Talha wakaja kwa Mtume kupokea (kusilimu)  Uislam.

Hafidh Ibnu Abdul Bir anaandika katika Istee'ab na Ibnu-Atheer anataja katika Usd-ul-Ghaba kwamba hakuna uthibitisho wowote wa Khalid bin Waleed kufuatana na Mtume na kushiriki pamoja katika vita vyovyote kabla ya kutekwa Maka na Waislamu.

60.    Ibnu Atheer katika Tareekh-ul-Kamil, Ibnu Shahna katika Roudhat-ul-Manadhir na Abul Fida katika Tareekh yake wanaandika katika mwaka huu (8 A.H.) Banee Bakr wakapambana na Banee Khuza'ah. Watu wa Banee Bakr waliua baadhi ya watu wa Bani Khuza'ah. kwa vile kikundi kimoja cha Makureshi kilisaidia katika kuwaua Banee Khuza'ah, basi wao Banee kureishi wakawa wana lawama juu ya kuvunja mkataba wa ,amani wa Hudaibiah. Walijuta sana kwa kufanya vile. Ndipo kwa kutaka kurudisha na kutengeneza tena ule mkataba waliouvunja, Abu Sufyan akaja Madina. Kwanza alimpitia mwanawe wa kike Ummi Habeeba. Alipotaka kukaa juu ya tandiko la Mtume, mara Ummi Habeeba akakunja tandiko lile. Abu Sufyan akauliza, "Binti wangu,. umekunja tandiko.kwa sababu yangu?" Akamjibu hili ni tandiko takatifu la Mtume, na wewe ni mushirikina ulipoondoka kwangu? Baadaye Abu Sufyan akaenda kwa Mtume na akazungumza naye habari ya kurudisha tena ule mkataba, lakini Mtume hakumjibu kitu. Vile vile Abu Sufyan akawaendea wakubwa wa Masahaba kama Ali na Abu Bakr na akawataka kufanya tena upya mkataba wao vile vile hawakusema neno. Mwishoni Abu Sufyan akarejea Maka bila ya kufaulu muradi wake, na akawajulisha Makureshi mambo yalivyokuwa. Wakati ule Mtume akafanya mipango ya kuondoka kwenda Maka. Alitumaini kufika kabla ya Makureshi kumtazamia kufika huko. Basi kwa hivyo siku ya kumi mwezi wa Ramadhani akaondoka Madina kwenda Maka.

61.. Imeelezwa katika Saheeh Muslim hadithi innayotokana na Jabir bin Abdallah anasema, "Mwaka wa kuiteka Maka. Mtume alitoka Madina katika mwezi wa Ramadhan wakati watu wote wamefunga. Hata alipofika Mahala paitwapo KURAA GHA-MIIM', mechana kabisa, hapo Mtume akataka bakuli la maji. Baadae akapashwa habari kwamba baadhi ya wtu (waliofuatana nae) hawakufuturu, walikuwa wameendelea na saumu yao; Mtume akasema mwenye kufanya huvyo (asie fungua saumuyake) basi amefanya dhambi na uhalifu.

Ibnu Shahna anaandika katika Roudhat-ul-Manaadhir kuwa alipofika Mtume karibu ya Maka. Bwana Abbas akamleta Abu Sufyan mbele ya Mtume. Kwa heshima na usia wa ammi yake (Abba«) Mtume akampa himaya Abu Sufyan. Baadae  Mtume akasema, "Ewe Abu Sufyan, je bado hujajua Shahada, LA-ILAHA ILLALLAHU?" Abu Sufyan akajibu. "Kwa nini sivyo?" Tena Mtume akamuuliza zaidi, "Je, bado hujathibitisha kuwa mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Abu Sufyan akajibu, "Ninayo bado shaka Juu ya jambo hili". Kwa jibu hilo, Abbas akamfokea Abu Sufyan, "Kefule! juu yako wee mwenzi! Ukubali Utume wake usije ukauawa". Kwa hivyo Abu Sufyan akatoa shahada ya Mwenyezi Mungu na akaukubali Utume. Pamoja na yeye, Hakim bin Hizam na Budail bin Warqa walisilimu pia.

62.    Abdul Fida anaandika katika kitabu chake cha historia:

Baadaye Mtume akamtaka Abbas amchukue Abu Sufyan kwenye  bonde la Madheeq na amwonyeshe Jeshi la Waislamu. Abbas akasema, ee Bwana Mtume, huyu Abu Sufyan ni mwenye majivuno (anapenda kujisifu) basi mjalie Jambo moja peke yake apate kujifakharisha kwa Makureshi." Mtume akasema, "Vema, kila mwenye kukimbilia katika nyumba ya Abu Sufyan, atapata himaya yetu, na kila mwenye kukimbilia msikitini, na nyumba ya Hakim bin Hazam, au akijifungia mlango ndani ya nyumba yake pia watapata himaya yetu". Abbas akaendelea kusema, "Baadaye nikamchukua Aba Sufyani kumwonysha Jeshi la Waislam kama alivyoniamuru Mtume.  Kwa ombi la Abu Sufyan ni kuwa ninamwonyesha wakuu mashuhuri wa kila kabila katika Jeshi la Waislamu. Wakati huo huo Mtume akapitia kikosi chake cha Muhajiriina na ansaar walio vaa. mavazi ya kijani kibichi. Abu Sufyan akagutuka. "Abbas! Hakika mtoto wa ndugu yako amejipatia ufalme mkubwa kabisa!". Mimi nikamjibu "Ole wako! Huu si ufalme, bali ni Utume wa Mwenyezi Mungu"

63.   Ibn-ul-Wardi anaeleza katika kitabu chake cha historia. kwamba Maka ilitekwa Ijumaa siku ya ishirini ya mwezi wa Ramadhan.

      Pia anasema kwamba palikuwa masanamu mia tatu na sitini (360) yaligandikwa kwa risasi au bati ukutani mwa kaaba. Kila sanamu aliyopitia Mtume, alielekeza ncha ya fimbo yake akisema Ja'al-haq-qu wa-zahaqal Baa-til In-nal- Baa-Tila  kaana   Zahu-qa [17:81)". Ukweli umefika na uongo umetoweka (umekwisha ondoka) Ukweli, Uongo mwishowe huwa ndio wenye kutoweka. Basi hapo ile sanamu huanguka kichwa chini bila ya kuguswa.

         64.    Abut Fida anaeleza kwamba baada ya ushindi wa Maka, Mtume akatangaza kuhalalisha uuaji wa wanaume sita na wanawaka wanne. Wanaume walikuwa Akrama bin Abi Jahl, Hubaar bin Al'aswad, Muqis bin Sabbabah, Abdullah bin Khatal, Huwairith bin Nufail ambaye akimwudhi sana Mtume katika mashairi ya kumsimanga Mtume, na ambaye, alipopambana na Ali usiku akauawa Mwingine alikuwa Abdullah bin Sa'ad bin Abi Sarah ambaye khalifa Othman alienda kwa Mtume kumtakia msamaha. Mtume akanyamaza muda mrefu baadaye akamsamehe. Abdullah bin Sa'ad bin Abi Sarah alipopata msamaha akasilimu. Mtume baadae akasema, "Nimenyamaza kimya kwa muda mrefu huo ili mmoja wenu asimame na kumuua." Masahaba wakasema, "Kwa nini usitufanyie ishara?" Mtume akajibu, Ni vibaya Mtume kudokeza". Huyu Abdullah bin Sa'ad ambae Khalifa wa tatu alimwombea msamaha alizoea kunakili Qurani na kuibadilisha atakavyo. Baadaye akakufuru na akawa adui wa Uislam na wakati wa enzi za ukhalifa wa Uthuman akafanywa Gavana wa Misri.

Na wale wanawake wanne ambao walihalalishwa damu zao na 'Mtume, miongoni mwao ni Hind, mke wa Abu Sufyani, mama wa Muawiyah, ambae alikula ini la Hamza. Hindi mwishoni akafika kwa Mtume akaapa kukubali utii. Mtume alipomtambua hapo akaomba msamaha kwa yale aliyoyatenda, na Mtume akamsamehe.

65.    Abul Fida anahadithia: kwamba Mtume baada ya ushindi wa Maka aliwapelekea baadhi ya masahaba wakifuatana na kikosi kidogo cha askari karibu na Maka kwa makusudi ya kuwaita watu waingie Uislam (waamini) bila ya kupigwa na kuuawa watu hao. Miongoni mwa waliokwenda alikuwa Khalid bin Waleed. khalid akaenda mahali wanapoishi Bani Khuzaima. Hao Bani khuzaima walipoona jeshi la Waislam wakatoka na silaha kamili. Khalid akawataka watupe silaha na wakatii amri hii. Khalid akaamrisha wakamatwe na kufungwa mikono yao na wakauawa wote. Mtume Alipopatiwa habari ya vitendo vya Khalid mara tu akanyanyua mikono yake kuelekeza juu mbinguni, akasema. "Ee Mola wangu nayalaani na nayachukia matendo aliyoyafanya Khalid".

66.    Abdul Haq Dehlav; anaeleza katika kitabu chake Madarijun Nabuuwah kuwa walipojua watu wa Bani Khuzaima kufika kwa Khalid, walivaa silaha kwa hadhari tu. khalid akawauliza ni nani na wakajibiwa, "Sisi ni Waislamu na wafuasi wa Mtume Muhammad (SA.W.) tunasali kwa nyakati zake, tumejenga msikiti, tunaadhini na Kukimu na vile vile tunasali sala ya ljumaa kwa Jamaa". Tena Khalid akawauliza kwa nini mlitoka na silaha? Wakajibu, "kati yetu na kabila moja la Kiarabu kuna uadui, basi tukaogopa kwamba isiwe nyie katika ukoo ule ndipo tukavaa silaha" Khalidi hakukubali maelezo yao na akawataka waache silaha. Mara tu wakatupa silaha. Baadae Khalid akawaamrisha watu wake kuwafunga mikono yao kwenye mabega yao, na akawapa rafiki zake kuwalinda. Siku ya pili asubuhi, Khalid akatoa amri kuwa kila mmoja amwue mahabusu wake. Hivyo ndivyo walivyo uawa hao mahabusi ambao hawakuwa na hatia yeyote. Na hadithi nyingine inaeleza hivi, kwamba kwa amri ya Khalid watu wa Banii khuzaima walipotupa silaha, basi yeye akawaua mia moja katika kabila lile. Mmoja katika Banii Khuzaima akampelekea Mtume habari juu ya ukatili huo Mtume akaghadhibika sana, mara tatu akasema "Ee   Mola   wangu, nahuzunikia na nayalaani matendo ya Khalid".

Abul Fida akaendelea kusema: Baadae Mtume akamtuma Ali na dhahabu (pesa) kwa Banii Khuzaima na akaamuru awalipe fidia kwa wale waliouawa na kwa ajili ya mali zilizopotea. Ali akafanya kama alivyoamriwa na Mtume.

67.    Ibn-ul-Wardi anaandika: Katika mwezi wa Shawwal (mfungo  mosi) mwaka huo huo, vita vya Hunain vikapiganwa. Baada ya ushihdi wa Maka kabila la Hawazin wakiongozwa na Malik bin Auf wakakusanyika kufanya vita na Mtume. Pia kabila la Thaqif wa mji wa Taif pamoja na ukoo wa Sa'ad bin Bakr wakaungana nao. Mtuma alipoarifiwa jambo hilo akampanda farasi wake aitwaye Duldul na akawachukua askari wake kumi na mbili elfu (12,000) siku ya sita ya mwezi Shawaal (mfungo mosi) kwenda kupigana.Tirmidhi anasimulia kutokana na Abu Waqid hivi, "Alipotoka Mfume kwenda Hunain, akapita kwenye mti ambao makafiri wakiita Dhatul Anwat na wakitundika silaha zao juu yake. Masahaba wakamtaka Mtume awafanyie Dhatul Anwat sawa kama walivyokuwa nao makafiri Mtume akasema, "Subha-Nal-Lah (Utukufu na hamdi ni za Mwenyezi Mungu). matakwa yenu ni sawa na ya wafuasi wa Mtume Musa, walivyomtaka awatengenezee kitu cha kukiabudu kama miungu waliyo kuwa wakiiabudu makafiri. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu nyie mtatumia (kufuata kawaida na mila zao zote. Mfafanya yote waliyo kuwa wakiyafanya kaumu ya Musa)"

Ibn Khalladoon anasema, baadae Mtume akaondoka mahali hapo na akaingia jimbo la Hunain.

Abul-Fida ameeleza kwamba walipo pambana majeshi ya pande mbili, Waislamu wakalegea na kubabaika na wakakimbia hata mtu hakumjali mwenziwe.

Ibn-ul-Wardi anaongeza kusema, walipokimbia masahaba siku ya vita vya Hunain, Mtume akamtaka Abbas, awaite kurudi. Abbas akasema, "Vipi itawafika sauti yangu masikioni mwao? Mtume akasema, "Ni juu yako kuwaita , na juu ya Mwenyezi Mungu kuifikisha sauti yako kwenye masikio ya wakimbizi hao".

68.    Burhanuddeen Halabi Shaafi'i. katika kitabu chake Seerat-ul-Halabiya anaandika kuwa wakati ule Abu Sufiyan bin AI-Harith alikuwa amekamata hatamu ya farasi wa Mtume, na Mtume akiangalia watu wake wanavyorudi nyuma, akawa anasema, "Mnakimbilia wapi? Lakini hakuna mtu aliyekuwa akimjali Mtume. Hapo Mtume akamtaka Abbas awaite kurejea kwa kusema hivi, "Ee nyie kikundi cha wasaidazi (Ansaar), Ee watu wa Samra! (Kikundi ambacho walisha kula yamini ya utii kwa kuapa chini ya mti kiitwa Samra ambao ulijulikana sana kwa jina la Bai'at Ridhwan, lililo tajwa katika Qurani 48:18). Kiapo hicho kilikuwa siku ya suluhisho ya Hudaibia). Mnakimbilia wapi?.

Katika hadithi iliyotojwa katika Saheeh Bukhari iliyopokewa na Abu Qatada inasema hivi: Siku ya vita vya Huniein, Waislam waliposhindwa na kukimbia, mimi (binafsi) vile vile nikakimbia: kwa ghafula nikamwona Umar bin Khattab pia akiwa miongoni mwa wakimbizi. Nikamwambia, "Mambo gani yametuangukia sisi Waislam hata tunakuwa katika hali hii ya kukimbia?" Akajibu (Umar), "Ndivyo alivyotaka Mwanyezi Mungu!". Baada ya muda tukarejea kwa Mtume.

Shah Waliullah Dehlavi ameandika katika Izalat-ul-Khifa hivi:

Katika siku ya vita vya Hunein Waislamu waliposhindwa na kukimbia, Ali hakuondoka mahala pake hata kidogo. Yeye alikuwa miongoni mwa wale walio thibitisha kukaa imara mahali walipokuwa wakipigania vita.

69.   Katika kanzul Ummal ipo hadithi iliyopokewa na  Ibn Askar kutokana na Husain bin Ali inasema hivi; Wale waliosimama imara katika vita vya Hunein ambao hawakukimbia, ni Abbas. Ali bin Abi Talib, Abu Sufyan bin Al-Harthi, Aqeel bin Abi Talib. Abdallah bin Zubair, Zubair bin Awwam, na Usama bin zaid. Lakini Burhanud-deen Halabi katika kitabu chake Siiratul Halabiya anasema hadithi moja ambayo imepokewa ikisema wazi kuwa, siku ya vita vya Hunain Waislamu walipomwacha Mtume baada ya kukimbia, walibaki watu wanne tu pamoja na Mtume. Watatu katika hao walikuwa katika Hashim, yaani, Ali bin Abi Talib, Abbas na Abu Sufiyan bin Al-Harth na mmoja hakuwa katika ukoo huo naye ni Abdullah bin Mas'ood.

Abul Fida anaeleza wazi kabisa hivi: Waislamu walipokimbia ule uovu na nia mbaya ya kudhuru ya watu wa Maka ambao wakifikiria juu ya Waislamu ikadhihiri. Abu Sufiyan bin Harb akafurahia akisema "Wakimbizi hao hawatasimama mpaka wafike kwenye ukingo wa bahari".

70.    Abul Fida, akaeleza zaidi, kuwa Mtume vivyo hivyo akasimama imara mahala pake mpaka wakimbizi wakarejea, hapo vikaanza vita vikali sana baina ya Waislamu na makafiri. Wakati ule Mtume akamwambia farasi wake hivi, "Albadi, Albadi". Farasi wake Duldul aliposikia hivyo akakaa chini hadi tumbo lake likagusa ardhi Mtume akachukua ukofi mmoja wa vumbi (mchanga), akarusha upande wa makafiri. Alipofanya hivyo tu mara makafiri wakajiona kwamba wanashindwa na wakaanza kukimbia. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu aliwapa ushindi Waislamu.

Walipokimbia kabila la Thaqeef kuelekea kwao Taif. Mtume vile vile akaliongoza jeshi la Waislamu kwenda Taif. Wakimbizi wakaingia ndani ya mji na wakafunga mlango. Waislamu wakauzunguka mji (Taif) muda wa siku ishirini (20) na huku wakipigana nao kwa makombeo, mwishoni Mtume akaamuru ikatwe miti ya zabibu (mizabibu) zao. Baada ya kukatwa mizabibu Mtume akaondoka.

71.   Tirmidhi anaeleza hadithi inatokana na Jabir, kuwa katika siku za kuizunguka Taif, mara Mtume akamwita Ali faraghani na akaongea naye siri kwa muda mrefu "Watu wakaanza kusema,kuna nini! hata Mtume anazungumza muda mrefu huo siri na nduguye". Mtume aliposikia maneno hayo, akasema, "Si mimi ambae nalizungumza siri na Ali, bali Mwenyezi Mungu ndie".

72.   Imeelezwa katika Madarijun Nabuuwwah kwamba, alipo ongea Mtume siri na AIi, Umar akamwambia Mtume, "YA RASUUL-LA-LAAH (Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu unazungumza siri na Ali".) Mtume akajibu. "Mimi sizungumzi siri na Ali,  bali ni Mwenyezi Mungu".

73.    Shah Abdul Haq katika maelezo aliyoeleza katika kitabu chake Mishkat, anasema hivi, "Walaakin Allaho Antajaahu" maana yake, "Nimeamriwa na Mwenyezi Mungu". vile vile ina maana kuwa, "Si kuwa mimi niliyeanza kusema na Ali siri, bali Mwenyezi Mungu ambae humwambia siri zake Ali na 'huweka siri zake katika moyo wa Ali. Basi ikiwa ni hivyo itakuwa mimi nafuata kitendo cha Mola kumwambia Ali siri".

74.    Mas'oodi anaeleza katika Murooj-udh-dhahab, kuwa katika mwaka huu wa nane wa A.H., Mtume aliwagawia Waislamu wapya sehemu ya mali. (sehemu ile inotolewa kwa kuwapa wanaotiwa nguvu nyoyo zao Juu ya Uislamu) Miongoni mwao waislamu wapya alikua Abu Sufyan na mwanawe Muawiyah, Mwaka huo huo   akazaliwa Ibrahim mwana wa Mtume, katika tumbo la Bibi Maria.

75.    Mhistoria Ibn-ul-Wardi anasema, "Tena ukaanza mwaka wa tisa wa A.H. Mtume mwaka huu wote alikaa Madina".

Katika Madarijun Nubuwwah imeelezwa kwemba mwaka huo huo Mtume alikaa mbali na wake zake kwa muda wa mwezi mmoja. Sababu ya kufanya hivyo Mtume imeelezwa hivi katika Roudhal-ul-Ahbab. Mtu mmoja alipompelekea zawadi ya asali safi Zainab binti Jahsh (mkewe Mtume), Zainab akamwekea Mtume, kwani Mtume alikuwa akipenda sana. Basi kila alipokuwa akienda Mtume kwake alikuwa akimtengenezea Sharbati ya asali. Kwa vile kutengeneza sharbati ya asali huchukua muda, basi ilimpasa Mtume kukaa muda zaidi kwa Zainab kuliko desturi. Aisha ameeleza kwamba, "Nilipojua hayo, mimi nikafanya shauri na Hafsa, ili atapokuja kuonana nasi Mtume tumwulize iwapo amekula Maghafeer hata harufu yake mbaya tunaisikia kutoka mdomoni mwake". Basi Mtume alipokwenda kwa mmoja wao, yule bibi akasema kama walivyopanga mbele, "Je umekula maghafeer?" Mtume akajibu vikali, "La sikula maghafeer, lakini nimekunywa sharbati ya asali kwa Zainab". Basi ikiwa sivyo inaonyesha kuwa wale nyuki waliotoa asali ile walikula maghafeer Mtume akajibu, "Ikiwa ni hivyo basi sitaitumia tena ile asali. Lakini usimwambie mtu yeyote habari ya nia hii niliyoifanya". Yule mke akaahidi asiseme lolote juu ya hayo, lakini hakutimiza ahadi akaisema na siri ikatoka nje. Kwa hiyo Jibrili akateremka na aya zilizomo katika sura ya TAHREM (S. 66), zinazosema hivi:

Ewe Mtume! mbona (kwa nini) unaharimisha alichokuhalalishia Mwenyezi Mungu! Unatafuta radhi za wake zako (ndiyo maana ukafanya hivi?) Na Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye huruma. Hakika Mwenyezi Mungu kakupeni sharia ya kufungua viapo vyenu, Mwenyezi Mungu ni Mola wenu, naye ndiye ajuaye, Mwenye hekima.

 Na wakumbushe wakati Mtume alipomwambia mmoja wa wake zake jambo la siri (na yule mkewe akalitangaza). Basi (mke yule alipo itangaza siri). Mtume alinjuvya huyu bibi sehemu ya yale aliyoyasema na  akaacha sehemu nyingine. Basi alipompasha (mkewe habari hii, alisema (yule mkewe), "Nani eliyekupa habari hii?" (Mtume) akasema, "Amenipa habari hii yule aliye mjuzi wa kweli Mwenye habari ya kila jambo."

Na waliokuwa wanammtaabisha zaidi katika wake zake ni bibi Aisha na bibi Hafsa; basi Mwenyezi Mungu aliwaambia hivi, Kama nyinyi mtatubia kwa Mwenyezi Mungu, (basi inabidi mfanye upesi) kwani nyoyo zenu zimeili upande kidogo. Na kama mtasaidiana juu yake (Mtume kumwudhi kwa mambo ya nyumbani, Mwenyezi Mungu atakuwa pamoja naye juu yenu). (66: 1-4)

76.   Jalaluddiin suyuutii anaandika katika Durri Manthoor kwamba katika Saheeh Bukharii, Sahiih Muslim na Jami'a Tirmidhii imeeleza hadithi iyotokana na Ibnu Abbas kwamba anasema, '"Mimi siku zote nilitaka kumuuliza Umar, wale wanawake wawili ni nani ambao Mwenyezi Mungu amesema habari yao katika Qur'ani kwamba nyoyo zao zimepotoka' basi watubie, lakini sikupata bahati wa kumwuliza. Kwa ghafula mara moja  katika safari ya Hajji tukawa pamoja, wakati wa kurudi njiani akatokewa na haja ya kwenda chooni. Basi na mimi nikachukua kopo la maji makusudi, aliparejea kutoka chooni nilimmwagia maji mikononi, akatawadha

Hapo nikaona ni wakati mzuri wa kumuwuliza, "Ee Bwana wa wenye kuleta imani, wale wanawake wawili ni nani, ambao Mwenyezi Mungum amewaambia, "Tubuni kwani nyoyo zenu zimepotoka"? Umar akasema, "Ni ajabu kwamba wewe huwajui, wale wanawake wawili ni Aisha na Hafsa".

77. Katika Tareekh-ul-khamiis imeelezwa kuwa katika mwaka huu wa tisa A.H, mwezi wa Rajab (mfungo kumi) vita vya Tabuuk vikatokea. Hivyo Sa'ad bin Waqas amesema. "Mtume alipokuwa akienda kwenye vita vya Tabuuk, aliazimia kumwacha Ali Madina. Ali kwa makazo  na chungu, alisema, "Mbona mwaniwacha nyuma?" Mtume akasema, 'Ali huridhiki kwa kuwa wewe unao utukufu kwangu kama alivyokuwa Harun kwa Musa, isipokuwa hapana Mtume tena baada yangu?" Kwa hayo Mtume alibainisha kuwa Musa alipokuwa akienda kuchukua hukumu alimteua nduguye Haroon kuwaangalia wafuasi wake, vivyo hivyo Mtume alimwacha AIi aangalie shughuli  Zake katika Madina.

78.    Katika Roudhat-ul-Ahbal imeelezwa, 'Abu Dhar Ghaffaar-. hakuweza kufuatana na Mtume. Akaenda baada ya Mtume kuondoka. llitokea njiani kuwa ngamia wake hakuweza kuendelea na safari kwa sababu ya kuchoka mno. Kwa hivyo Abu Dhar akabeba mwenyewe mizigo yake mgongoni kwake na akaendelea mbele".

Tareekh-ul-Khamees ameendelea kueleza kwamba Mtume alipofaka kupumzika alivunja safari njiani na alikuwa amepiga kambi mara sahaba wake akamuona mtu mmoja anakuja kwa mbali. Akamwambia, "Ewe Mtume wa Mola, mtu mmoja anakuja kwa miguu peke yake". Mtume akasema, "Ndiyo, huyo ni  Abu-Dhar". :Watu wakamwangalia kwa makini na wakahakikisha kuwa alikuwa Abu-Dhar. Hapo Mtume akasema, "Mwenyezi Mungu amuhurumie Abu-Dhar. Kama anavyokuja akiwa hoi peke yake leo, vivyo hivyo atakufa peke yake".

Abul Fida amesema, "Mtume akafika Tabuuk ambako alikaa siku ishirini. Yuhanna gavana wa lla akaja kwa Mtume na walipotia sahihi mkataba alikubali kulipa jizya kwa Mtume. Baadae Mtume akarejea Madina".

79.    Nasaee anahadithia kwamba Anas amesema hivi, "Mtume alimpeleka Abu Bakar kuwafikishia watu wa Maka baadhi ya aya za mwanzo wa sura ya 'Bara'at' (S.9). baadae akamrejesha kabla hajafika na akasema, 'Hakuna mtu mwingine yeyote awezae kuhubiri sura hii, isipokuwa mtu wa  nyumbani kwangu'. Basi akamwita Ali na akamtaka kuitangaza ile sura   ijulikanayo kama "Bara'at". Huyo Nasaii pia anahadithia kwamba Ali amesema, "Mtume alimpeleka Abu Bakr na sura ya 'Bara'at kwenda kuitangaza Maka. Baadae akanipeleka nyuma yake na akaniambia "Chukua kwa Abu Bakar maandiko ya sura ya Bara'at na uende kwa watu wa Maka'. Kwa hivyo nikaondoka, njiani nikamkuta Abu Bakar na nikayachukua maandiko. Abu Bakr akarejea kwa Mtume na huzuni, akauliza, 'Ewe Mtume wa Mola! je, umeelekezwa na Mwenyezi Mungu juu yangu?" Mtume akajibu, Sivyo, bali Mola ameamuru kuwa mimi binafsi au mmoja katika watu wa nyumba yangu aitangaze sura ile. "Na katika hadithi nyengine iliyoandikwa na Nisaea pamoja na Tirmidhi pia inasema kuwa maneno yafuatayo hapa yametumiwa na Habshi bin Janada: "Mtume alisema, 'lsipokuwa Ali na mimi binafsi hakuna mtu tena awezae kuitagaza kama inavyotakikana".

80.    Abul Fida ameendelea kusema. "Miaka kumi baada ya Hijra kuanza wajumbe wa kabila zote Waarabu walifika Madina kwa Mtume, katika vikundi vikubwa na wakasilimu.

katika Raudhat-ul-Ahbal imeelezwa kwamba katika mwaka huo huo (10 A.H.), Mtume akaafikiana na Wakristo wa Najran. Waandishi wa habari za Mtume wanaeleza kwamba Mtume aliwaandikia barua Wakristo wa "Najran, kuwataka wasilimu. Wakristo wa Najran walipoipata, baada ya kushauriana wao kwa wao, wakachagua tume ya watu kumi na nne kwenda na kuleta taarifa ya uchunguzi wao juu ya maisha ya Mtume kule Madina.

    81. Katika kitabu cha Madarijun Nubuwwah imeelezwa hivi, "Mtume (S.A.W.) kawapelekea barua Wakristo wa Najran, na kawataka wasilimu. Wakashauriana wenyewe kwa wenyewe baadaye wakachagua halmashauri kumi na nne kati yao, wakawapeleka Madina kwenda kuangalia maisha na tabia ya Mtume (S.A.W.), na baadae wapeleke habari kwa watu wao. Miongoni mwa hawa halmashauri kumi na nne, watatu wao walipewa ukubwa wa mashauri yote, nao ni Abdul Maseeh ambaye akijulikana kwa Aaqib, na Sayyed na watatu wao akiitwa Abul Harith. Walipofika Madina wakabadili nguo zao za safari, na wakavaa nguo zao za hariri, na pete za dhahabu mikononi, na wakaenda msikitini 'Masjidun-Nabawi'. Wote kwa pamoja wakamwamkia (wakatoa salamu) Mtume (S.A.W.), lakini Mtume hakuijibu salamu yao, na akageuza uso wake. Baadaye wakatoka msikitini na wakamwendea Uthman bin Affaan ha Abdul Rah-man bin Auf na wakawaeleza malalamiko yao kusema, 'Mtume wenu katuletea barua na kutualika, na sasa tulipofika kwake, tukamwamkia asitujibu salamu, wala hakutusemesha; sasa mnatupa shauri gani?' Uthman na Abdur Rahman wakataka shauri kwa Ali. Ali akatoa shauri hivi. Hao wavue hizo nguo zao za hariri na pete za dhahabu, na wavae badala yake zile nguo zao za kidesturi za kipadri (Juba, joho) ndipo wafike kuonana na Mtume'. Wajumba wa Wakristo wakabadilisha mavazi kama walivyo ambiwa na baadae wakafika kwa Mtume. Mara baada ya wao kumwamkia, akawajibu na akasema, 'Naapa kwa jina la mola ambae amenifanya kuwa mjumbe wake, walipokuja hawa mara ya kwanza kwangu Shetani alikuwa amefuatana nao'. Baadaye Mtume akawataka wasilimu. Wao wakauliza, 'Nini rai yako juu ya Mtume Isa?' Mtume akajibu, Leo nyie pumzikeni hapa mjini, na baada ya mpumziko mtapata majibu ya maswali yenu yote kwangu'. Inaonyesha Mtume alikuwa akingoja 'Whayi amri ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo siku ya pili ikateremka aya hii (3:59:61) maana yake ni hii;  Bala shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; aliumbwa kwa udongo kisha akawaambia: Kuwa, basi wakawa. Hii ni haki inayotoka kwa Mola wako. Basi usiwe miongoni mwa wanaofanya shaka. Watakao kuhoji (sasa) katika haya  baada ya kukufikilia elimu  hii (na kuwafikia wao). Waambie '"Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu; na wanawake wa kwetu na wanawake wa kwenu na sisi na ninyi; kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo".

Hapo Mtume akawaita wajumbe wa Wakristo wa Najraan na akawahubiri habari yote aliyoteremshiwa kwa Mola. Lakini hao hawakukubali na wakashikilia Itikadi yao. Kwa hivyo Mtume (S.A.W.) akawaambia, "Ikiwa haya yote 'hamkubali, basi njooni tufanye "Mubaahila" (wakusanyike) pamoja, na tuapizane kuwa aliye mwongo limfike laana, na ikiwa mnataka kusimama imara katika itikadi yenu (hamtaki kusilimu) basi mkubali kutoa 'jizya" na tufanye mkataba. Wakati muda wa siku moja, wakakutana na wakashauriana na wakamtaka mkubwa wao Aaqib awape shauri. Yeye akawaambia, "Naapa kwa Mola, kuwa nyie mnajua kwamba' Muhmmad (S.A.W.) ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na amekupeni' uthibitisho dhahiri juu ya Mtume Isa, kabisa kabisa msifanye naye Mubaahala mtaangamia, ikiwa mnataka kuendelea na hiyo dini yenu. basi bora mkubali kulipa Jizya na mfanye mkataba wa suluhisho". Baadae siku ya pili watu hao wakatoka nje ya Madina kutaka kufanya Mubaahila na Mtume (S.A.W.) na huku Mtume akatoka nyumbani kwake akimbeba Husain mkononi, na kufuatana na Hasan ubavoni mwake huku  amekamata mkono wake, na nyuma yake alikuwa Fafima na nyuma yake Ali. Subhannallah! ulikuwa ni mwandamano upendezaoje! upande Mabawana wa Waislamu wamesimama, huku tayari kumwomba Mola, na huku watu wanatazama.

Baadae Mtune na Ahli Baiti wake wakasimama mbele ya wakristo, hapo akawaambia Hasa, Husein, Fatima na Ali, "Nikiomba Dua nyie wote semeni Amin kwa pamoja. Walipoona Wakiristo hawa watukufu watano na nuru zao na wakawasikia namna watavyoomba Dua ikawaingia hofu kubwa na wakaanza kutetemeka, hapo Abul Harith (ambae alikuwa na busara sana) akawaambia watu wake, "Tunashuhudia hapa watukufu hawa nuru yao, ambao wakimwomba Mwenyezi Mungu majabali yangoke mahali pake  yatang'oka, basi nakukatazeni msifanye Mubaahila nao, au mtaangamia wala hatabakia Mkristo hata mmoja ulimwenguni". Kwa hivyo wale wakamwambia Mtume Ee Abul Qaasim sisi hatutafanya Mubaahala, Mtume akawaambia basi silimu, hiyo nayo hawakukubali, basi Mtume akawaambia kaeni tayari tupigane, wakajibu sisi hatuna nguvu ya kupigana, lakini tunataka suluhisho kwa kutoa kila mwaka nguo elfu mbili ambazo bei ya kila nguo dirham arobaini (40) na katika hadithi isemayo, vilevile walikubali kutoa farasi 30, ngamia 30, nguo za chuma za vita 30, na mikuki 30. Basi kwa shuruti hizo ikawa suluhisho".

    Hakim katika kitabu chake MUSTADRAK. kapokea hadithi hii kwa njia madhubuti na sahihi kutokana na Jabir bin Abdllah Ansaari, kwamba waliposhindwa Wakristo wa Najraan na wakakataa Mubaahila, Mtume (S.A.W.) akasema, "Naapa kwa Mwenyezi Mungu ambaye mimi ni mjumbe wake, wangelifanya hao Wakristo huo Mubaahila, ungalishuka moto juu ya jangwa hilo.

   Jabir anasema juu ya tokeo hili la Mubaahila ndio aya hii imeshuka, kama tulivyo eleza nyuma. Jaabir anasema. "Katika aya hii (3:61) neno la AN-FUSA-NAA lahusika na Mtume na Ali, na neno la AB-NAA-ANA lahusika na Hasan na Husein na neno la NISAA-ANA lahusika na Fatima".

    82.   Imeelezwa katika Tareekh Tabaree kwamba katika mwake huu wa Kumi A.H., Mtume alimpeleka Ali Yemen, na kabla yake Mtume alimpeleka Khalid bin Waleed kuwataka watu wa Yemen wasilimu, lakini wakati ule mtu hakusilimu. Kwa hiyo Mtume alimpeleka baadaye Ali na alimwamrisha amuuzulu Khalid na yeyote katika wenzi wake Khalid. Basi Ali akaenda Yemen na akawasomea watu wa Yemen barua tukufu ya Mtume, mwisho kabila nzima ya Hamdan wakasilimu kwa siku moja. Ali alimpelekea habari Mtume matokeo ya kufanikiwa kwake, hapo Mtume (S.A.W.) akasema, "Salama iwashukie watu wa Hamdan". Baadaye mmoja baada ya mwingine watu wa Yemen wakasilimu. Ali alimpelekea habari tena   Mtume mafanikio yake. Mtume (S.A.W.) alifurahi mno, na hapo hapo akasujudu kumshukuru Mola kwa mafanikio hayo.

   83.    Ibnul-Wardi anaandika, "Katika mwaka huu huu Mtume alimpeleka Ali kwa Wakristo wa Najran kupokea (Jizya) kodi". AIi akatekeleza amri ya Mtume (akaenda kupokea Jizya), aliporejea akakutana na Mtume katika safari yake ya Hija ya mwisho. Mtume (SA.W.) aliondoka kutoka Maka kwa safari yake ya kuhiji mara ya mwisho siku ya mwezi ishirini na tano ya Dhil-Qa'ada (mfungo pili). Abul-Fida anaeleza Mtume aliwafundisha Waislamu namna ya kuhiji alipokuwa   safarini,   na   hapo   ikateremka aya hii: "Leo waliokufuru wamekata tamaa katika dini yenu, basi msiwaogope, bali niogopeni mimi. (5:4)

  84. Ibnu Khallakan katika kitabu chake Wafiy-Yaatul-A'yaan ameandika hivi, "Alipokuwa akirejea Mtume (S.A.W.) kutoka safari yake ya mwisho ya hija (Hij-jatul Widaa) alipofika' Ghadeer-u- Khum akamteua Ali kwa kumfanya ndugu yake na akasema, "Ali anao makamu kwangu kama alivyokuwa na makamu Haruni kwa Musa, Ee Mola mpende mwenye kumpenda Ali, na mfanye adui mwenye kumfanyia uadui Ali, msaidie mwenye kumsaidia Ali na mkatae mwenye kumkataa AIi".

     Hakim katika Mustadrak ameeleza zaidi hadithi hiyo aliopokea kwa Zaid bin Arqam, kwamba Mtume akashuka (katika safari yake ya kurudi) mahala kati ya Maka na Madina ikijulikana kwa jina la (Ghadeer-u-Khum) hapo akasali, baadaye akasimama na akawahutubia watu, hivi: kwanza akamshukuru Mola, tena akatoa mawaidha na baadaye akasema, "Enyi watu' ninawacha kati yenu vitu (mambo) viwili muhimu, Qur'ani na kizazi changu (Ahlu-bayit). Mkiyafuata (hayo mawili) hamtapotea kabisa njia ya haki". tena akaongeza kusema, "Je, mnafahamu kwamba mimi ninao uwezo na mamlaka juu ya nafsi ya kila (Mumeneen) mwenye" imani?" Wote walio hudhuria wakajibu, "Ndio unayo mamlaka". Mtume mara tatu alikariri maneno hayo hayo, na wakajibu kila mara; hapo Mtume akasema, "Sikiliza mwenye kuwa mimi nina mamlaka juu yake basi Ali pia anayo mamlaka juu yake".

85. Nasaee katika Kitabul khasais ameandika hadithi inayotokana na Zaid bin Arqam aliyoipokea Abut-Tufail, ambayo inasema hivi:

Aliporejea Mtume (SA.W.) kutoka Maka katika safari yake ya mwisho ya Hija, alitua hapo Ghadeer khum, akaamrisha itengenezwe minbari. llipokuwa mimbari tayari mtukufu Mtume akapanda mimbari, hapo akasema, "Mwenyezi Mungu ameniita (karibu nitakufa) na mimi nimeitikia mwito wa Mola. Sasa ninawaachia vitu viwili vyanye thamani sana (kwa Mwenyezi Mungu) mmoja katika hivyo ni Qur'ani tukufu na cha pili Ahlu Bait (kizazi changu. Vitu viwili hivi havita achana kabisa (duniani) mpaka vifike kwangu kwanye hodhi la Kauthar siku ya Qiyama. kwa hivyo muvitunze na kuvifuata, tazameni vipi mtatekeleza kufuata hivi vitu viwili". Baadaye Mtume akasema, ''Mwenyezi Mungu anao uwezo na mamlaka juu yangu na mimi ninayo mamlaka juu ya nafsi ya wote wenye kuleta imani, baadaye Mtume akakamata mkono wa Ali na akasena, "Tazameni, kama nilivyokuwa na mamlaka juu yenu basi huyu Ali vile vile anayo mamlaka juu yenu. Ewe Mola mpende mwenye kumpenda Ali na mfanye adui mwenye kumfanyia Ali uadui." Abut-Tufail anasema, "Naliposikia hadithi tukufu hii, nalikwenda kwa Zaid bin Arqam kumwuliza, na nikamwuliza, hivi, Je, ulimsikia Mtume kusema maneno haya?" Zaid bin Arqam akajibu, "Si mimi tu bali wote walioizunguka nimbari siku hiyo wakashuhudia kwa macho yao kwamba Mtume alikuwa akisema naneno haya na wakayasikia kwa masikio yao".

 Amehadithia Sa'ad bin Abi Waqaas kuwa, 'Tulikuwa pamoja na Mtume (katika safari yake ya mwisho) alipofika Ghadeeru Khum, akawataka watu watuwe.Kwa hivyo walotangulia wakarejeshwa na waliokuwa nyuma (bado hawakufika) wakangojewa mpaka wakawasili. Walipokwisha kusanyika wote, hapo Mtume akawauliza mara tatu hivi, "Enyi watu, nani bwana wenu?" Kila mara wakajibu watu, "Mwenyezi Mungu na Mtume wake". Kwa kusikia majibu haya kila mara, hapo Mtume aliukamata mkono wa Ali akamnyanyua juu na akasema, "Ali pia ni bwana wa wale watu ambao bwana wao Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ee Mola mpende mwenye kumpenda Ali na mfanyie uadui mwenye kumfanya Ali kawa adui wake".

    NASAEE kaendelea kueleza katika kitabu chake hicho, kwa kutaja hadithi iliyohadithiwa na Zaid bin Arqam kwa tafauti kidogo. Zaid bin Arqam anasema, - Alinyanyuka   Mtume (S.A.W.) akahutubu, kwanza kamshukuru na kumsifu Mwenyezi Mungu, baadaye akasema, "Nyie watu wangu! Hamjui kwamba mimi nina mamlaka na ubora juu ya nafsi ya kila mwenye imani? Wote wakajibu, "Ndio, sisi tunashuhudia hakika kwamba wewe unayomamlaka na ubora juu ya nafsi ya kila mwenye imani". Baadaye Mtume akamkamata Ali kwa mkono na akasema, "Ali pia ni bwana wa yule, ambaye mimi ni bwana wake".

86.    Ibnu Hajar Makki anasimulia katika kitabu chake Sawaiqul-Muhriqa hadithi ambayo imepokewa kwa njia sahihi na madhubuti na Tabrane. Inaeleza hivi: Mtume (S.A.W.) alihutubia chini ya miti mahala paitwapo Ghadeeru Khum hivi: Mwenyezi Mungu mwenye upole na ujuzi amenihubiri kwamba kila Mtume hupata umri nusu ya umri wa yule Mtume aliyetangulia. Kwa ,hivyo ninafikiri karibu nitaitwa kwenda kwa Mola na nitakubali kwenda. Sikilizeni! Huku nitaulizwa, na nyie pia (kwa upande wenu) mtaulizwa. Je, mtajibu nini? Wote waliohudhuria huko wakajibu, "Tutashuhudia kwamba Wewe ulifikisha ujumbe na ulitumia bidii yako kwa kutuongoza na kutufundisha. Mwenyezi Mungu akupe jaza njema kabisa kwa hayo yote". Baadaye Mtume akasema, "Je hamtashuhudia kwamba hakuna Mungu isipokuwa Yeye tu, na Muhammad (S.A.W.) ni mjumbe wake na Mtumewe; na Pepo na Jahannam (Moto) ni haki; na kufa na kufufuka baada ya kufa ni haki; na hakuna shaka kabisa kuwa ipo siku ya kuhukumiwa nayo ni Kiyama: na Mwenyezi Mungu atawafufua wote kutoka makaburini mwao? Wote wakajibu, "Ndio, bila shaka tunathibitisha yote haya". Tena Mtume akasema, "Ee Mola shuhudia nalivyobaini hapa. Baadaye Mtume akaendelea kusema, "Enyi watu, Mwanyezi Mungu ni Mola (bwana wangu, na mimi ni bwana wa kila mwenye imani na ninayo mamlaka na ubora juu ya nafsi zao, kwa hivyo kila mwenye kukubali kuwa ni bwana wake na ninayo mamlaka juu yake, basi Ali pia ni bwana wake na anayo mamlaka juu yake.

   Tena katika Raudhatul-Ahbaab imeelezwa kwamba, alipokuwa Mtume akirejea kutoka safari yake ya Haj-jatul-Widaa (safari ya mwisho) ya hija, alipofika kwenye kituo cha Ghadeer-u- Khum hapo akasali sala ya adhuhuri ilipoanza wakati tu,   baadaye akaelekea upande wa masahaba na akasema, "Enyi watu ati mimi ninayo mamlaka na ustahiki kwa Waislamu juu ya nafsi zao? Na katika hadithi nyingine inasema hivi kuwa Mtume alisema, "Nimeitwa kwenda kwenye maisha ya milele (kufa) na nimekubali hukumu ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo nakupeni habari kwamba ninawacha vitu viwili adhimu (bora) miongoni mwenu, moja" imetukuka zaidi kuliko nyingine, navyo ni Qur'ani na Ahlu Baiti wangu. Angalia na kuwa na hadhari kwa jinsi mtavyowatendea na vipi mtawakiria haki zao juu yenu. Na vitu viwili hivi havitawachana kabisa mpaka vifike kwenye hodhi ya Kauthar siku ya Qiyama. Baadaye akaendelea kusema, "Mwenyezi Mungu ni bwana wangu na Mwenye mamlaka juu yangu na mimi ni bwana na mwenye mamlaka juu ya wenya kuamini". Tena akaushika mkono wa Ali katika mikono yake na akasema, "Ali pia ni Bwana wa wale. ambao mimi Bwana wao. Ea Mola mpende mwenye kumpenda Ali na mfanye adui mwenye kumfanyia uadui Ali, na mwachie mbali mwenya kumwachia Ali na msaidie mwenye kumsaidia Ali, na iongoze na elekeza haki upande wowote anapoelekea na kuweko Ali".

87.   Waa-hidee katika kitabu chake Asbab-un-Nuzuul, na Suyuu-tee katika Durri-Manthoor, Shaukani katika Tafseer Fathul Qadeer na Sideeq Hasan Khan katika Fathul Bayan wameandika hadithi iliyopokelewa na Sahaba Abu Saeed AI-Khudri kwamba kasema, iliteremshwa aya hii, YAA AY-YUHAR-RASUULU. BAL-LIGH, MAA. UNZILA ILAY-KA, MIR-RAB BIKA, WA.ILL-AM TAF-AL. FAMAA, BAL-LAGH-TA, RISAA-LATAHU (5:67^. Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako; na kama hutafanya, basi hukufikisha ujumbe wake, Aya hii iliteremshwa siku ya Ghadeeru Khum kwa heshima ya Ali. Tena katika hadithi nyingine iliyoelezwa na Aini mwenye kuandika Sharh Saheeh Bukharee kafafanua aya hii, Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola, juu ya utukufu wa Ali bin Abi Talib". Basi ilipoteremshwa aya hii, Mtume akakamata mkono wa Ali na akasema, "MAN KUN,TU, MAW-LAA-HU, FA, ALIY-YUN MAW-LAA-HU". Ali pia ni bwana wa yule ambae amenikubali mimi kuwa ni bwana wake.

Naishaburi katika Tafseer Gharaibul Qur'an ametaja kwamba ya hii kwa heshima ya Ali, iliteremshwa katika Ghaderu Khum na Mtume hapo aliushika mkono wa Ali na akasema, "Mwenye kunikubali mimi ni bwana wake, basi Ali pia ni bwana wake".

Hafidh Ibnu Mardwaih na Hafidh Abu Naeem wanasimulia hadithi yaa AY-YUHAR-RASUU-LU, BALLIGH. MAA- UN-ZlLA, ILAY-KA, MIR-RAB-BIKA; Mtume (S.A.W.) akaukamato mkono w AIi, na akasema, 'AIi -ni bwana wa yule ambaye ananikubalia kuwa mimi ni bwana wake, Ewe Mola, mpende mwenye kumpenda Ali na mfanye adui mwenye kumfanya Ali kuwa ni adui wake. Baada ya kusema maneno hayo mara ikateremshwa aya hii, "AL-YAWMA, Ak-MALTU,  LAKUM DEE,NAKUM, WA'AT-MAM-TU.   ALAY-KUM, NI-MATEE, WA'RADHIIYU, LAKU-MUL, ISLAAMA- DII-NAA", (5:3) (Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu.)

 88.    Allama Ibnu Wadhih Katika kitabu chake cha tarehe kwamba, "Imepokewa kwa njia ya hadithi sahihi na madhubuti, kuwa aya hii, 'Leo nimekukamilishieni dini yenu'. Ni aya ya mwisho ya Qur'ani ilio teremshwa, na imeteremshwa siku ya maadhimisho ya Ghadeeru Khum",

Na katika lsaba cha Ibnu Hajar Asqalaani kwa Riwaya alfyopokea Baghawi na katika Kanzul-Ummal kwa Riwaya aliyopokea Ibnu Abi Shaibah na katika Abu Dawood Tiyalisi na Baihaqi wote hawa wanasimulia kwamba Ali amesema, "Siku ya Ghadeem Khum, Mtume aliviringa kilemba cheusi kichwani mwangu na ncha Za pande zote mbili kazitundika begani mwangu pande mbili.

Katika Musnad cha Ahmad Bin Hanbal imeelezwa hadithi iliyopokewa na Bara'a Bin Azib na Zaid bin Arqam, hawa rafiki wawili wanahadithia hivi. "Sisi tulifuatana na Mtume katika safari yake ya Hija ya mwisho. "Alipofika (Mtume mahala paitwapo Ghadeeru Khum, mtangazaji akatangaza, 'Ass-Salaatu Jamia', (Njooni kutanikeni kwa sala ya jamaa). Ardhi (mahala chini ya miti ikafagiwa kwa ajili ya Mtume (S.A.W.). Akasalisha sala ya adhuhuri, baadaye Mtume akakamata mkono wa Ali bin Abi Talib na akasema hivi, "Enyi watu, hamjui kwamba mimi kwa wenye kuamini ni bora kuliko nafsi zao?". Wote wakajibu bila shaka ndio. Baadaye Mtume akasema tena, "Hamjui kwamba mimi ni bora kupita nafsi ya kila mwenye

imani?". Wote wakajibu. "Ndio ilivyo Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! kwa kila mwenye imani wewe ni bora kupita nafsi yake." Tena Mtume akasema, "Ali pia ni bwana na bora kuliko nafsi ya kila mwenye imani ambaye mimi ndiye bwana na bora kupita nafsi yake. Ewe Mola mpende mwenye kumpenda Ali na mfanye adui kila mwenye kumfanyia uadui na Ali. Baadae Umar akakutana na Ali na akasema, "Pongezi kwako, Ee mwana wa Abu Talib, leo wewe umekuwa bwana wa wote wenye kuamini wanaume na wanawake".

Imeeleza katika Ma'arijun Nubuwwah kwamba siku hiyo zaidi ya masahaba, na mama wa Muminiina (wake zake Mtume) pia walimpa pongezi Ali.

89.   Muhammad Bin Salim Hanafi anasema . katika Hashia ya Sirajul Muneer Azeezi juu ya maelezo ya kitabu cha Jami Sagheer ya Suyootee kwamba Mtume alipotoa hutuba kuwa, Ali vile vile ni bwana wa yule ambaye anayenikubali mimi kuwa bwana wake, watu wakasikia yote haya, baadhi ya masahaba wakakaidi na kusema, "Haitoshi kwetu kutoa shahada, kusali na kutoa zaka kwa kawaida, hata ukamnyanyua na kumfanya bwana na kumpa ubora juu yetu? Mambo haya yanatokana kwako binafsi au ni amri uliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu?" Mtume akajibu, "Naapa kwa Yule ambae hayupo wakuabudiwa isipokuwa Yeye, kwamba hii ni amri ya Mola".

Katika Tafseer ya THA'labi, NooruI-Absaar, Seeratul Hala-biyah na Mustadrak wote hawa wanaeleza kwamba, Mtume aliporejea Madina baadaye mtu mmoja jina lake Haris mtoto wa No'man Fihri alipohadithiwa kisa cha Ghadeeru Khum alikataa kabisa kukiri kuwa Ali awe bwana wake na akabishana na Mtume juu ya jambo hilo na akasema, Ewe Mola ikiwa ni kweli Mtume amefanya haya kwa amri yako, basi teremsha mawe kutoka mbinguni (adhabu) juu ya Muhammadi au tupe adabu sisi (ikiwa Mtume kweli) hapo hapo ikateremka jiwe kubwa kutoka mbinguni na likamwangukia na hapo hapo akafa, kama hapo kale ilivyoteremshwa majiwe juu ya jeshi la Abraha na wakafa wao wote kwa mafendo yao. Ziliteremshwa aya hizi kwa kisa cha Harith bin No'man: SA'ALA. SAA-ILUN BI-ADHA-A-BIN WAAKI-IN LIL-KAA FIREENA LAY.

SALAHUU DAA.FIUN.(70: 1-2} (70:1-2) "Mwulizaji kaomba adhabu isioepukika kuwaangukia wasio amini.

Al'lama Nuurudden Halabi Shafii katika kitabu chake Seeratul Halabiya anaeleza tokeo hili, limetokea siku ya mwezi kumi na nane Dhil-Hijja (mfungo tatu) ambao siku hiyo Marafidee (shia) wanaifurahikia na ni Idi yao.

90.    Katika Tareekh Abul Fida imeandikwa kuwa baada ya kurejea Mtume katika safari yake ya "Hi'ja ya Mwisho", Mtume akakaa Madina mpaka mwaka wa kumi (A.H.) ukamalizika, na ikaanza Muharram (mfungo nne) wa mwaka kumi na moja (A.H.) mpaka mwezi huo ukamalizika, na ukangia mwezi wa Safar (mfungo tano) katika siku za mwisho wa mwezi Mtume akawa mgonjwa, hapo Mtume akawaita wake zake wote katika nyumba ya mke wake Maimoona (ambapo wakati ule akikaa huko)   na   akawataka waridhiane akae kwa mmoja kati yao wakati wa ugonjwa. Wake wote wakakubali akae kwa Aesha.                  

Ibnu Jareer Tabaree katika kitabu chake cha historia ameeleza hadithi inayatokana na Aesha na kupokewa na Ubaidullah kwamba Aesha amesema, "Mtume katika hali ile ile ya ugonjwa kwa msaada wa Fadhl bin Abbas na mtu mmoja mwingine, kwa Jinsi alivyokuwa dhaifu miguu ikifanya alama juu ya ardhi kwa kukokota na kichwani amefunga   kitambaa   wakaingia   kwangu. Ubaidullah anasema. "Nikamhadithia hadithi hii Abdalla bin Abbas

akasema, unamjua yule mtu wa pili aliyefuatana na Mtume, ambae Aisha hakutaja jina lake ni nani." Nikamjibu simjui, Ibnu Abbas akasema yule alikuwa Ali bin Abi Talib ambaye Aesha hakumtaja kwa jina kwa kuwa Aesha alikuwa hawezi (hapendezewi) kumtaja Ali kwa mambo ya kheri".

91. Abul Fida anaeleza, "Alipotoka Mtume, nyumbani kwenda msikitini kwa msaada wa Fadhl bin Abbas na Ali bin Abi Talib, kwanza akakaa juu ya mimbari, baada ya kumsifu Mwenyezi Mungu akasema, "Enyi watu! na aje mbele yangu, yule ambaye nalipata kumpiga migongoni mwake, au nimechukua mali yake, wote waje kuchukua kisasi na mali yao kwangu".

Ibnu Jareer Tabaree ameongeza kusema, "Baadaye Mtume akasema, "Enyi watu! kila mwenye kuwa na hofu juu ya nafsi yake kuhusu jambo lolote, asimame na aseme ili nipate kumwombea kwa Mola; mtu mmoja aliposikia hivyo akainuka na akasema, Ewe Mtume mimi ni msema uwongo, na nafanya maovu na na lala usingizi sana. Mtume akamwombea hivi, Ee Mola mfanye aseme kweli, mpe Imani, na mwondolee usingizi wa kulala sana. Baadaye akasimama mtu mwingine akasema, Ewe Mtume! mimi msema uwongo, na vile vile ni mnafiki, Umar alipoyasikia maneno haya akasimama na kusema Ewe umejifedhehesha! Mtume akajibu vikali, Ewe mwana wa Khattab! Fedheha ya duniani ni bora na inavumilika kuliko fedheha ya Akhera. Ewe Mola mruzuku ukweli na Imani. (Tokeo hili katika Raudhatul-Ahbab, na Madarijun Nubuuwwah vile vile limetajwa).

   Abul Fida amepokea hadithi kwa Aesha anasema, "Baadaye ' Mtume akaja kushinda kwangu, wakati ule Mtume kaniona nikiugua kichwa na huku napiga kelele, Ee kichwa changu! Kwa kwa vile Mtume alipoona vile hali yangu akasema, "Wallaahi, ewe Aesha, inafaa mimi niseme kichwa changu! kwa vile kichwa kinaniuma. tena Mtume akasema, "Ee Aesha utakuwa na hasara gani ukifa wewe kabla yangu? Mimi nitasimamia mazishi yako yote, na baada ya kukuvalisha sanda nitakusalia kisha nikuzike. Naliposikia hayo kwa Mtume nikasema, "Nadhani ukishanizika na kurejea nyumbani, utakuwa unastarehe na wake zako wengine huku kwangu".

92.   Ibnul Wardi anaandika katika kitabu chake cha historia hivi:

Vakati wa ugonjwa wake Mtume, kaamrisha litayarishwe jeshi chini ya uongozi wa Usama bin Zaid, mmoja katika watumwa wake na kashikilia kwa ngovu waondoke upesi.

Abdul Haq Muhaddith Dehlavi katika kitabu chake Madaari- jun Nuboowwah ameeleza, "Baadaye siku ya pili ijapokuwa ugonjwa ulimzidi na hali yake ilikuwa mbaya, Mtume mwenyewe akafunga bendera ya jeshi na akamkabidhi Usama na akasema, "Nenda kwa

jina la Mwenyezi Mungu na pigana na Makafiri kwa jina la Mola, Usama akatoka nje ya Madina pamoja na ile bendera na huko akamkabidhi mikononi mwa Buraida Bin AI-Khusaib na akamteua kuwa ni mshika bendera wake. Alipowacha Madina akatua kwenye kijiji kiitwacho JARF, ambacho kipo karibu na mji wa Madina mahala hapo jeshi wakakusanyika. Mtume vile vile aliamrisha masahaba wote, hata wakubwa wao kama Abu Bakr, Umar Othuman, Saad bin Abi Waqaas, Abu Ubaidah binil-jarrah na  wengineo lazima wamfuate na waingie katika jeshi la Usama, isipokuwa Ali kaambiwa asiende. Baadhi ya masahaba wakaona ari na vigumu kuwa mtumwa awaongoze "Muhajiriina na Ansaar" basi wakaanza kunung'unika na kulaumu. llipomfikia habari hii Mtume alihuzunika na, ingawa Mtume alikuwa na homa na kuumwa kichwa, akatoka nyumbani na hamaki, akapanda mimbari na akatangaza, Enyi watu nini mnasema kwa vile nimemfanya Usama kuwa mkubwa wa jeshi juu yenu? Mnasema kama mlivyosema nilipo mteua baba yake ama kuwa mkubwa wa jeshi katika vita vya Moota. Wallahi, Usama anastahiki kuwa mkuu wa jeshi na vile vile baba yake alistahili kuwa mkubwa wa jeshi".

Shahrastanee katika kitabu chake Al-Milal Wan Nihal na Nawab Siddeeq Hasan Khan katika kitabu  chaka   Hujajul karaamah ameeleza  kwamba Mtume  kawaamrisha   Masaka ba,"Fanyeni haraka kuungana na jeshi la Usama. Mwenyezi Mungu amlaani asiye ungana na jeshi la Usama".

93.    Katika Madarijun Nuboowah imeelezwa: Baadaye kwa amri ya Mtume, Usama akaenda kwenye kambi, na akawaamrisha jeshi kuondoka. Alipokuwa karibu Usama kumpanda farasi wake, mama yake akamletea habari kwamba Mtume anaumwa sana amekaribia mauti. Kusikia habari hiyo Usama na baadhi ya masahaba watukufu wakarejea. Abu Bakr na Umar walikuweko Madina tangu hapo, walikuwa bado hawakwenda kuungana na lile jeshi.

94.    Ibnu Jareer Tabaree katika kitabu chake cha historia inayoitwa Tareekhu Rusul Wal Mulook, ameandika hadithi tukufu ndogo ndogo zilizopokewa na Ibnu Abbas zinazosema hivi: Mtume alipokuwa katika hali mbaya ya ugonjwa wake, akatoa amri, Mleteni AIi kwangu". Aisha akasema, Bora itakuwa umwite Abu Bakr. Na Hafsa akasema, "Itakuwa bora umwite Umar." Kwa muda mchache tu wote wawili hao wakahudhuria hapo. Mtume akasema, "Nendeni zenu wote wawlli, nitakuiteni mwenyewe nikikutakeni"., Baadae wakaenda zao.

95.    Ibnu Khaladoon katika kitabu chake cha historia anaeleza, "Mtume alipopata hujambo kidogo, akatoka nyumbani na akaenda msikitini. Wakati ule Abu Bakr alikuwa akisalisha Alipohisi kwamba Mtume amefika akarudi nyuma kwenya mahala pake. Mtume akamwachia asimame mahala alipo, na yeye Mtume binafsi akaanza kusalisha kwa kupaza sauti katika sala. Abu Bakr alikuwa akimfuata Mtume. na watu wakimfuata Abu Bakr."

Zaidi ya hayo katika Roudhatul Ahbab na Madarijun Nuboowwah imeelezwa kwamba Abu Bakr alikuwa akimfuata Mtume na wengine wakimfuata Abu Bakr, maana yake kwa kutamka Takbiratu Abu Bakr, (kujulisha watu) watu wakimfuata sala ya Mtume.

96.   Tabranee ameeleza hadithi inaotokana na Umar kwamba wakati wa ugonjwa wake Mtume alisema, "Nileteeni kidau cha wino na karatasi ili nikuandikieni hati namna hiyo ambayo (mkifuata) hamtapotea (hamtaongozwa vibaya) baada yangu. (Kwa kuwa hata mtu mmoja hakutimiliza maombi ya Mtume) Umati wa wanawake nyuma ya pazia wakapiga kelele, 'Hamsikii Mtume anayo sema?' Umar akasema kuwajibu wake zake Mtume. 'Nyie ni kama wale wanawake waliomshawishi Mtume Yusufu. Mnalia kuwa Mtume mgonjwa, na anapokuwa mzima mnamkamata roho (mnamhangaisha). Mtume akajibu vikali, 'Usiwahoji wanawake hao, wao ni bora zaidi kuliko nyie".

    Katika Saheeh Muslim imetajwa hadithi inayotokana na Ibnu Abbas inayosema hivi Alipokuwa Mtume  akiumwa sana Umar   Ibnu   Khattab   na   masahaba   wengine   waliwepo kwa Mtume. Mtume akasemai, "Niachilieni nikuandikieni hati kwa kuusia wasiyah) ili msipotee baada yangu". Umar akasema Mtu huyu anasema kwa kuwewaseka, tunayo Qur'an na inatutosheleza". Matamko hayo ya Umar yakaleta mgogoro kati ya wale waliokuwa huko. Baadhi yao wakisema amri ya Mtume lazima ifuatwe kwa kumwacha awaandikie atakayo kwa ajili ya uzuri wetu. Wengine waka wafikiana na Umar. Ghasia na mgogoro ulipozidi Mtume akasema, "Ondokeni mbele yangu ('Tokeni nje)". Kwa sababu hiyo Ibnu Abbas alikuwa akisema, "Hakika lilikuwa tukio lenya huzuni na mashaka tena iliposimama mgogoro na ubishano kumzuwia Mtume kuandika Usia wake wa baadaye kufuatwa na umma."

Saeed Ibnu Jubair anahadithia kama ilivyo andikwa katika Sahihi Bukharee kuwa ibnu Abbas alisema, "Alhamisi ile ilikuwa siku yenye huzuni na msiba", na huku akilia sana hadi changarawe zilizokuwepo hapo alipokaa zikalowa na machozi yake. Baadaye akaendelea kusema, siku ya Alhamisi ugonjwa, ukamzidi Mtume na siku hiyo Mtume akasema, "Nipeni vitu vya kuandikia ili nipate kukuandikieni hati ambayo baadaye hamtapotea katika uovu kabisa". Kwa kuomba hivyo Mtume mgogoro na mabishano kati ya waliohudhuria kwake ukaanza (ingawa mbele ya Mtume kugombana hakufai). Wakasema Mtume ameweweseka. Hapo Mtume akapiga kelele, "Tokeni nje kwangu,mimi ni mzima kuliko ninyi".

Katika Musnad cha Ahmad bin Hambal na Saheeh Muslim imeelezwa hadithi iliyo simuliwa na Saeed bin Jubair hivi: Kwamba Ibnu Abbas kila akiikumbuka siku hiyo ya Alhamisi akisema, Ole siku ya Alhamisi, na akalia namna hii hadi machozi yakamiminika juu ya mashavu yake kama mtungo wa lulu ukiteremka, tena (Ibnu Abbas) akasema siku ya Alhamisi ni siku ile ambayo Mtume akataka kwa wale waliohudhuria kwake wamletee karatasi na vitu vya kuandikia ili aandike hati (kama wasia) wasije baada yake wakapotea katika upotevu. Hapo wakasema, "Mtume anaweweseka".

Shahabudiin Khaffaji katika kitabu chake Naseemur-Riyaadh alichoandika maelezo juu ya kitabu cha Shifa cha Qadhi Ayadh anasimulia hivi: Imepokelewa hadithi (tukio) hilo kwa njia nyingine hivi, "Kwamba msemaji wa tamko la kuwa Mtume anaweweseka ni Umar".

Shahrastanii katika kitabu chake cha Milal wan Nihal anasimulia kuwa mabishano na hitilafu ya mawazo iliotokea mwanzo katika siku za ugonjwa wa Mtume ilikuwa ile alioeleza Bwana Bukhari katika kitabu chako SahihiBukhari aliyo ipokea kwa njia sahihi na thabitl kutokana na Ibnu Abbas alihadithia hivi: Ulipozidi ugonjwa wa Mtume, hapo Mtume akasema, "Nipeni kidau cha wino na karatasi ili nikuandikieni (wasiya) hati ambayo (kwa kufuata) hamtapotea baada yangu". Aliposikia Umar hivyo akasema, "Mtume ugonjwa umezidi ndio maana anasema maneno kama haya. Kitabu cha Mwenyezi Mungu kinatutoshea". Kwa kusema hivyo Umar, makelele na fujo ikazuka hapo Mtume akasema, 'Tokeni nje kwangu". Haikufalieni kufanya makelele na ugomvi mbele yangu". Kwa tukio hilo ndio sababu ya kulalamika na kuhuzunika Ibnu Abbas na  kusema. "Msiba mkubwa na jambo liletalo huzuni siku ulipozuka ugomvi na hitilafu kati yetu hata ikazuwilika Mtume kutuandikia wasia".

97.    Imeelezwa katika Roudhatul-Ahbaab kwamba Mtume akamwambia binti wake Fatima awalete wanawe kwake, Fatima (a.s) akawaleta wanawe Hasan na Husein (A.S.) kwa Mtume (SA.W) walipofika tu, wakamwamkia Babu yao na wakakaa ubavuni pake. Walipoona vile hali ya Babu yao wakaanza kulia. walilia sana na kwa kilio chao kila aliyekuwepo hapo akalia. Hasan akaweka uso wake juu ya uso wa Mtume, na Husein akaweka kichwa chake juu ya kifua cha Mtume na Mtume akafunua macho na akawabusu wajukuu wake hapo akaamuru na kuusia watu wawapende na kuwa heshimu mabwana hawa. Katika hadithi nyingine inasema hivi: Masahaba waliohudhuria hapo, walipowaona Hasan na Hussein kulia vile, wao pia wakaanza kulia kwa sauti kubwa hata Mtume hakujiweza kujizuia na Yeye akalia kwa kilio chao. Baadaye akaamrisha hivi, "Mwiteni ndugu yangu mpenzi Ali". Ali akafika na akakaa karibu na kichwa cha Mtume. Mtume aliponyanyua kichwa chake Ali akasogea ubavuni pake na akakamata kichwa cha Mtume na akaweka pajani mwake. Tena Mtume akasema. "Ee Ali, nimekopa kiasi maalum cha pesa kwa Yahudi fulani kwa ajili ya matumizi ya kutayarisha Jeshi la usama. Fahamu ulipe. Ee Ali, wewe ni mtu wa kwanza atayefika kwangu kwenye Hodhi ya Kauthar (siku ya Qiyama). Utapata taabu sana baada ya kifo changu. Lazima uvumilie kwa upole na ukiwaona watu wamehiari tamaa mbaya ya hii dunia, basi wewe chagua Akhera".

Imeelezwa katika Madarijun Nuboowwah kwamba alipofariki dunia Mtume, Fatima yakamtoka machozi ghafla na huku anasema. Ole! baba yangu, umepokea mwaliko wa Mwenyezi Mungu. Ah baba! umehiari njia ya Peponi. Ee baba! sasa Jibrili ataleta maneno

ya Mwenyezi Mungu kwa nani? Ea Mola chukua roho yangu kwa roho ya Mtume. Ea Mola usininyime mazuri ya mpenzi wako, na siku ya Qiyama usinikoseshe''Shafaat" yake.

Vile vile katika kitabu hicho na katika kitabu cha Raudhatul Ahbaab imeelezwa kwamba baada ya Mtume kufariki  dunia, hakupata mtu kumwona Fatima anacheka.

98.    Ibnu Saad anaandika katika kitabu chake Tabaqaat kwamba Ali bin Husain (A.S.) amehadithia kwamba "Wakati wa kufariki Mtume dunia, kichwa cha Mtume (S.A.W.) kilikuwa juu ya paja la Ali. Katika kitabu hicho vile vile imeelezwa kwamba Abu Ghatfan amesimulia kuwa, "Nalimuliza Ibnu Abbas, 'Uliona juu ya paja la Ali kilikuwi kichwa cha Mtume wakati wake wa mwisho alipofariki dunia?' Ibnu Abbas akasema. 'Alipofariki dunia Mtume kichwa chake kilikuwa kimeegemea kwenye kifua cha Ali', Mimi nikasema, Lakini Ur'wah amenisimulia kutokana na Aesha kwamba Aesha amesema kuwa Mtume amefariki dunia pajani mwake".

Abdullah Ibnu Abbas akasema. "Wewe hufahamu Wallaahi Mtume alipofariki dunia kilikuwa kichwa chake kimeegemea kwenye kifua cha Ali, na yeye ndiye aliyemuosha".

Imeelezwa katika Khasais Nasaii hadithi iliyo simuliwa na Ummu Salma amesema, "Wallahi mtu aliyekuwa karibu sana na Mtume siku ambayo Mtume amefariki dunia alikuwa Ali. Siku ambayo amefariki dunia Mtume, asubuhi mapema Mtume akamwita Ali alipokuwa amemtuma ujumbe nje, mara tatu alikuwa akiuliza Ali kabla hakurudi. Walakini Ali akafika kabla ya kuchomoza Jua siku hiyo. Kwa hivyo tukajua kwamba Mtume anamazungumzo ya siri na Ali basi sote tukatoka nje. Mimi nilikuwa mtu wa mwisho kutoka humo, na nikakaa nyuma ya mlango, na mimi nalikuwa karibu na mlango kuliko wake zake Mtume. Kwa hivyo nikamwona Ali kakiinamisha kichwa chake kwa Mtume, na Mtume akawa anamnong'oneza siri sikioni mwake (kwa muda). Basi Ali pekea ndiye mtu aliekuwa karibu na Mtume mpaka kufariki".

Zaidi ya hayo Hakim ameeleza katika Mustadrak kwamba Mtume (SA.W.) akaendelea kuongea siri na Ali mpaka wakati wa kufa. Tena Mtume akavuta pumzi ya mwisho na  akafariki.

99. Ibnu Wardi anaeleza katika kitabu chake cha Tarikh kwamba watu walioshiriki kutangeneza Mazishi (kumwosha) ya Mtume walikuwa Ali, Abba', Fadhl. Qathm. Usama bin Zaid na Shaqraan mtumwa wake Mtume. Abbas, Fadhl na Qadhm wakaugeuza mwili

mfukufu, Usama na Shaqraan wakitia maji na Ali akimkogesha Mtume.

Tareekh-ul-Khamiis ameongeza kusema kuwa, Abbas, Fadhl na Qathm walikuwa wakigeuza kiwiliwili cha Mtume, na Usama na Shaqraan wakitia maji. Wote hawa walifunga kitambaa machoni.

  Ibnu Sa'ad katika Tabaqaat anaeleza hadithi inayotokana na Ali kwamba amesema hivi, "Mtume ameniamuru na kuusia kwamba asimwachilie mtu yeyote kuniogesha bila yeye tu kama si hivyo atakayemkogesha bila Ali atapofuka macho".

100.    Abdul-Bir katika kitabu chake Istii'ab anaeleza hadithi inayotokana na Abdulla Ibnu Abbas kwamba amesema hivi. "Ali anazo heshima na sifa njema za pekee ambazo mtu yeyote kati yetu hana sifa hizo isipokuwa yeye. (I) Yeye ni mtu wa kwanza miongoni mwa Waarabu kusali sala pamoja na Mtume. (2) Katika vita vyote, yeye ndiye mshika bendera ya Mtume. (3) Walipokimbia masahaba wote vitani na wakamwacha Mtume pekee Ali ndiye aliesimama imara ubavuni mwa Mtume kumhami. (4) Ali ni pekee aliyemwosha (kiwiliwili) Mtume na kumlaza Mtume kaburini mwake.

101.    Abul Fida na Ibn-ulwardi wote wawili wameandika kwamba Mtume alifariki dunia siku ya juma tatu na alizikwa siku ya pili yake (Jumanne). Na katika hadithi moja inasema kwamba (Mtume) alizikwa usiku wa kuamkia Jumatano, na hii ndio sahihi na inakubaliwa zaidi. Vile vile wengine wamesema kuwa hakuzikwa ila siku tatu baada ya kufa kwake.

Katika Tareekh-ul-Khamis imeelezwa kwamba amesema Muhammad bin ls'haaq. "Mtume (S.A.W.) amefariki dunia siku ya Juma tatu na alizikiwa usiku wa kuamkia Jumatano.

Mpokea- hadithi Abdul Haq Dehlavi anaeleza katika kitabu chake cha MA' THABATA BIS-SUN-NAH kwamba Fatima (binti wa Mtume) akazoa baadhi ya udongo wa kaburi la Mtume na huku anaunusa na kusema maneno haya kwa mashairi: "Atakaenusa udongo wa kaburi la Mtume, hatanusa maishani mwake manukato yeyote. Ole! Baada ya kufariki yeye nimefikiwa na msiba namna hiyo ambayo ungeliufikia mchana ungebadilika kuwa giza kama usiku." (Ole! Baada ya kufariki yeye umeniangukia msiba namna hiyo, hata ungelianguka juu ya mchana ungebadilika giza na kuwa usiku).

Ibnu Sa'ad katika Tabaqat ameeleza kwamba Muhammad bin Qasi amesema, "Mtumeamefariki  siku ya Jumatatu, mwezi pili Rabiul Awwal" 11 A.H Lakini Aesha anasema kwamba Mtume amefariki jumatatu mwezi kumi na 12 Rabiul Awwal"

Abul Fida amekadiria umri wake (Mtume) anaandika. 'Ijapokuwa ipo hitilafu juu ya shauri ya umri wa Mtume walakini kwa kutegemea hadithi sahihi inaonyesha Mtume aliishi miaka sitini na tatu.

102. Katika Saheeh Bukhari imeelezwa hadithi inayotokana na UM-MUL-MUMINIIN Maymoona kwamba amesema. "Mtume alikuwa akisali na kusujudu juu ya KHUMRA. allama Muhammad Tahir Fatmi katika kitabu chake MAJ'MA BIHARUL ANWAAR anasema ni kitu kile ambacho SHIA mpaka leo wanasujudia wakisali katika Sajdah. (kipande kidogo cha mkeka uliosukwa kwa makuti ya mtende).

Tirmidhi katika kitabu chake Jaame ametaja hadithi inayotokana na Abu Saeed Khudri kwamba Mtume alikuwa akisali juu ya mkeka. lmeongezwa kuelewa katika Saheeh Bukharee hadithi inayotokana na Ibnu Abbas kwamba tulikuwa tukitambua sala imemalizika (wakati akitoa takbira Allahu Akbar).

103.    Imeelezwa katika kitibu cha JADH-BUL.QULOOB kwamba zaidi katika majumba ya Mutme yalikuwa namna ya majumba ya Waarabu ya makuti ya mtende na yamefunikwa na blanketi ya manyoya ya ngamia. Vile vile blanketi lilitundikwa kwenye milango tababu ya sitara. Na katika kila nyumba palikuwa chumba kimoja mahsusi. Mahali hapo ilikuwa chumba cha Fatima, na katika ukuta kati ya chumba cha Aesha na Fatima palikuwa dirisha, na kutoka dirisha hiyo Mtume alikuwa akiingia kwa Fatima na akiuliza hali yake Fatima na wenawe Hasan na Husein. Mara moja nusu ya usiku Aesha akaja kwenye hiyo dirisha na akajibizana na Fatima ukali. Fatima akamwomba baba yake aifungo hiyo dirisha. Tena katika kitabu hicho hicho imeelezwa hadithi iliyopokewa na Tabrani inasema hivi: Mtume alifanya kawaida akirejea kutoka katika safari, kwanza alikuwa akienda msikitina na akisali rakaa mbili, baadae akimpitia kumtazama na kumwuliza hali binti yake. Mwishoni alikuwa akienda kwenye vyumba vya wake zake na akikaa hapo kwa muda. Na katika kitabu hicho hicho imeelezwa kuwa ilikuwa desturi ya Mtume anapotoka nyumbani husimama penye mlango na akawaambia Ali, Fatima na Hasannayni (wanawao) AS-SALAAMU ALAYKUM AH-LAL-BAYT IN-NAMAA YU-REE-DUL-LAA-HU LI-YUDH-HIBA AN-KU-MUR-RIJSA AH-LALBAY-TI WAYU-TAH-HIRA-KUM TAT-HEE-RA.

      "Amani na salama juu yenu, Enyi watu wa nyumba yangu. Mwenyezi Mungu amekusudia (ameazimia) kuweka mbali na nyie kila namna ya uovu na uchafu, na amekutakaseni utakaso wa utakatifu kama inavyotakikana" (33:56)

104.   Imeelezwa katika Saheeh Bukharee kwamba Aesha amesema kuwa sikuwa na husuda na kuona wivu kwa wake wenzangu (wa Mtume) kama nilivyokuwa nikimhusudu Khadija ingawa sikumwona, lakini kwa vile Mtume mara nyingi alikuwa akimtaja, na pengine akichinja mnyama alikuwa akiwapelekea nyama rafiki zake Khadija, kwa hivyo sikuweza kukaa kimya na nikimwambia Mtume, "Kwani hakutokea humu duniani mtu kama Khadija! Tena Mtume akijibu, "Ndio yeye alikuwa namna hiyo, alikuwa namna hiyo, na kizazi changu chote kinatokana na yeye".

Vile vile kitika kitabu cha Siiratul Halabiya imeelezwa kwamba Aesha amesema hivi:

Sikupata kamwe kumwonea wivu au kumhusudu mwanamke yeyote kama nilivyokuwa nikimhusudu na kumwonea wivu Khadija (wema na uzuri wake) mara nikamchukiza kusema. "Kwa nini daima huwa unamsifu yule kizee kibogoyo kwa sababu Mwenyezi Mungu amekupa mke bora kuliko yeye? Hapo Mtume alighadhibika na kukasirika sana na akasema, "Naapa kwa   jina   la   Mola hakunipa mke bora kuliko yeye. Khadija kaniamini wakati watu hawakunisadiki, na Mwenyezi Mungu amenibarikia kizazi changu kutokana na yeye tu.

105.    Imeebzwa katika Mawahib-uI-Ladunniyah dhahiri na kukubaliwa na wote kuwaidadi ya wake wa Mtume wetu ilikuwa kumi na moja nao ni hawa (I) KHADIJA Bint khuwailid (2) Aesha Bint Abu Bakr (3)Hafsa Bint Umar-Bin AI-Khattab (4) UMMU Habeeba Bint Abu Sufiyan (5)Ummu Salma Bint Abi Umayyah (6) Sauda Bint Zum'a (7) Zainab Bint Juhsh (8) Maimoona Bint AI-Harith (9) Zainab Bint Khuzaimah (10) Juwaira Bint Al Harith na (II) Safiyyah Bint Hayy Bin Akhtab.

Jalaluddeen, Suyuutii ameandika katika kitabu chake cha Tafsiir Durr-i-Manthoor hadithi iliyopokewa na Ibnu Abi Hatim (33:5 na 53) inasema "Wake zake Mtume ni Mama wa walioamini kwa sababu imekatazwa na Mwenyezi Mungu kuwa kila mwenye kuamini (Mwislamu) kumwoa mmoja wapo wa mke wa Mtume alio waacha (Mtume) katika uhai wake au kuowa mmojawapo baada ya kufariki Mtume dunia, imeharimishwa katika Qur'ani tukufu.

Katika Umdatul Qaree ambayo ni Sherehe ya kitabu cha Sheeh Bukharee imeelezwa kwamba Aesha alisema, "Wake wa Mtume ni Mama wa walioamini wanaume tu si wanawake".

Katika Tafseer Durr-u-Manthoor cha Suyootee imeandikwa hadithi aliyo ipokea kwa Baihaqi inayotokana na Aesha inasema hivi: Aesha amesem kwamba siku moja mwanamke mmoja akamwita Aesha, "Ee Mama!, mara Aesha akamwambia, "Sisi wake wa Mtume ni Mama wa wanaume si wa wanawake". Ipo hadith iliyopokewa na Ibnu Sa'ad, Abdur-Raazzaq na Abd bin Hameed kwamba Qatada alisema, "Talha bin Ubaidullah amewaambia watu kwamba atamuoa Aesha akishafariki dunia Mtume. Ndipo aya hii katika Qur'an ikateremka (33:53) Haijuzu na haikufalii nyinyi kumuudhi Mtume kwa vyovyote wala si halali kuwaoa wake zake baada yake kabisa".