KUTOA AU KUOMBA SADAKA

 

Kimeandikwa na:SHEIKH HURRI ‘AAMILI 


YALIYOMO

YALIYOMO 2

MANENO MAWILI 5

TUJIELIMISHE KUHUSU ILIMU NA MENGINEYO … 6

1. MAIMAMU WA SHIA KATIKA UANDIKAJI NA UENEZAJI WA HADITH 6

2. MASHIA NA UANDISHI WA HADITH: 10

3.  HISTORIA YA UANDISHI WA HADITH KATIKA SUNNI: 15

4.      SABABU ZA UCHELEWESHO KATIKA UANDISHI WA 21

HADITH: 21

HADITHI NI NINI ? 22

SHI’AH NA HADITH 24

MTUNZI NA HABARI ZAKE. 30

UTAMBULISHO WA MA’SUMIIN A.S. 33

KATIKA AHADITH: KUNIYYAT  NA  ALQAAB 33

ALQAAB. 35

MWENYE KURIPOTI AHADITH AWEJE? 36

AINA ZA AHADITH 38
1. HADITH SAHIH 38

2. HADITH HASAN 38

3. MUTAWATH-THAQ 38

4. DHAIF 38

HADITH ZILIZOGHUSHIWA 39

SIFA ZA KUZITAMBUA HADITH 45

ZAKA NA SADAKA HUONGEZA NEEMA 46

SADAKA   NA   MISAADA: 56

MADONDOO JUU YA SADAKA 64

 

 

1. ISISITIZWE KUTOA SADAKA KWA WENYE SHIDA, MASIKINI NA MADENI 652. KUSAIDIA FAMILIA YA WAISLAMU WENYE SHIDA NI AFADHALI KULIKO KWENDA HIJJA ZILIZO SUNNAH NA KUWAFANYA HURU WATUMWA 69

3. KUWATOLEA WAGONJWA SADAKA NI SUNNAH 70

4. MTOE SADAKA KWA NIABA YA WATOTO WENU NA WATOTO WENU WATOE SADAKA KWA MIKONO YAO HATA KAMA ITAKUWA KIDOGO KIASI GANI. 71

5. MTOE SADAKA KWA MIKONO YENU WENYEWE  hUSUSANI WANANYUMBA WATOE SADAKA KWA MIKONO YAO NA WANAYEMPA WAMWOMBE AWAOMBEE DUA NJEMA. 73

6. KUTOA SADAKA KILA MARA NA KWA WINGI NI SUNNAH 74

7. KATIKA KUTOA SADAKA HATA KIASI KIDOGO  CHOCHOTE KILE NI SUNNAH 75

8. KILA SIKU ASUBUHI MTOE SADAKA NA MNUIE 78

9. KAMA KUNA HOFU YA KUJA KWA BALAA AMA KWA KUTOKEZEA UBAYA WOWOTE AU KWA SABABU YA UGONJWA NA HOFU YOYOTE BASI TOENI SADAKA. 80

10. MNAPOKUWA NA HOFU YA KUPATA HATARI KATIKA MALI, BASI MTOE SADAKA NA KAMA HAMPATI YULE ALIYEMUSTAHIKI, BASI MFANYE NIA SEHEMU HIYO MUITENGE NA MALI YENU. 82

11. WAOMBAJI WANATAKIWA WARIDHIKE KWA KILE WANACHOPATA NI SUNNAH, KUWAONGEZEA WALE WALIORIDHIKA NA KUTOWAJALI WALE WASIORIDHIKA. 84

 

12. ASUBUHI NA MAPEMA NA USIKU UNAPOINGIA NA SAA ZINAZOKUWA MBAYA UANPOTOKA NJE BASI MTOE sadaqah. 85

13. NI VYEMA KUTOA SADAKA KIFICHOFICHO KULIKO KIDHAHIRI. 87

14. KUTOA SADAKA USIKU NI SUNNAH 91

15. MUJIPATIE FADHILA KWA KUTOA Sadaka  KATIKA SIKU TUKUFU NA MWEZI WA RAMADHANI. 95

16. JE SADAQAH  ITOLEWE WAKATI GANI? 96

17. MSIMRUDISHE ANAYE KUJA KUOMBA USIKU 98

18. KATIKA IBADA ZOTE ZA SUNNAH  SADAKA  INAONGOZA. 99

19. AINA ZA SADAQAH. 100

20. KUWASAIDIA MAJAMAA NA NDUGU KUNA THAWABU ZAIDI. 102

21. IWAPO MWOMBAJI HAUMJUI MPE Sadaka  KIDOGO ILI AWEZE KUWA NA HURUMA NA MAADUI  WA AHLUL BAYT a.s. WASIPEWE Sadaka 104

22. KUMRUDISHA MASIKINI NI KARAHA HATA KAMA USTAHIKI WAKE UTAKUWA MASHAKANI, LAKINI LAZIMA APEWE CHOCHOTE, NA KAMA HAKUNA CHOCHOTE CHA KUMPA BASI UNAWEZA KUMWONDOA KWA MANENO MAZURI NA MATAMU. 107

23. BAADA YA KUMSAIDIA MASIKINI MARA TATU UNAWEZA KUMWAMBIA AONDOKE. 111

24. HAWEZI KURUDISHA Sadaka NA BAADA YA KUMTOA MTUMWA KAMA Sadaka  HUWEZI KUMCHUKUA TENA KATIKA MILIKI YAKO. 112

25. NI SUNNAH KUWAAMBIA WAOMBAJI WAWAOMBEENI DUA NA VILE VILE NI SUNNAH KWA MWOMBAJI PIA KUWAOMBEA DUA WANAO WASAIDIA. 114

 

 

26. KUSAIDIA KUWAFIKISHIA SADAQAH WANAO HITAJI NI SUNNAH. 116

27. KUTOA KATIKA MALI YAKO KWA AJILI YA KUMSAIDIA MUUMIN NI SUNNAH. 117

28. MTU AMBAYE AMEISHA TIMIZA MAHITAJI YA WATOTO WAKE NA NDUGU NA JAMAA ZAKE BASI INAMBIDI AJITAABISHE NAFSI YAKE KWA KUWAHUDUMIA WANGINE, HATA KAMA HUDUMA HIYO

ITAKUWA NI BURE LAKINI NI SUNNAH. 121

29. NI SUNNAH KUUBUSU MKONO WAKO MWENYEWE BAADA YA KUTOA SADAQAH NA KUKINUSA KITU NA KUKIBUSU KITU AMBACHO UNAKITOLEA SADAQAH. 126

30. KATIKA KUTOA SADAQAH NI SUNNAH KUKOPA NA KUMLIPA MARADUFU ALIYEKUKOPA WAKATI WA KUTOA SADAQAH. 129

31. NI HARAMU KUOMBA KAMA HAKUNA HAJA. 131

32. MAOVU YA KUOMBA HATA KAMA ITAKUWA NI KIJITI AU MAJI. 133

33. KUOMBA KATIKATI YA UMATI WA WATU SI VYEMA KABISA. 139

34. NI KARAHA (MAKRUH) KUDHIHIRISHA SHIDA NA UOMBAJI. 140

35. KURUHUSIWA KUMWAMBIA SHIDA ZAKO MUUMIN NA NDUGU PALE INAPOTOKEA. 142

36. KUISHI NA WATU KWA WEMA NI SUNNAH NA KUTOKUWA NA TABIA YA KUWAOMBA OMBA WALA KUWA NA TAMAA KWA YALE WALIYO NAYO. 144

37. SI VYEMA KUMSEMA MTU BAADA YA KUMSAIDIA AU KUMSEMA YULE ULIYEMPA SADAQAH. 147

38. MTU ANAPOTOA KITU KUSAIDIA BASI HAIRUHUSIWI KUMWAMBIA KUWA UMETOA ZAIDI KUPITA KIASI. 150

39. KUMSAIDIA MTU KABLA HAJAOMBA NA KUMSAIDIA KATIKA HALI YA KUTOKUJULIKANA NI NANI ANAYESAIDIA NI SUNNAH. 151

 

40. NI SUNNAH KUENDELEZA NA KUTUNZA MSAADA NA UKARIMU NA KUENDELEAZA MOYO WA KUTOA. 153

41. KUHURUMIA NA KUSAIDIA NI SUNNAH NA HUKUMU ZINAZOHUSIANA NAZO. 154

42. NI SUNNAH KUWAWIA WANA NYUMBA WAKO KWA WEMA KABLA YA KUTOA SADAQAH KWA WATU WA NJE. 155

43. NI KARAHA KUKWEPA NJIA WANAYOPITA MASKINI. NI SUNNAH KUTOKEZEA MBELE YA WAOMBAJI NA KUWASAIDIA KITOSHELEVU KWA KUTOA SADAQAH. 158

44. NI SUNNAH KUTOA KITU CHOCHOTE KILA SIKU KATIKA NJIA YA ALLAH SWT. 159

45. KUTOA SADAQAH NI SUNNAH LAKINI KUSAIDIA KUTOA MSAADA KWA KUTEGEMEANA NA WADHIFA WA MTU NI FARADHI. 160

46. SADAQAH KUTOLEWA KUTOKA MALI ILIYO HALALI NA HAIRUHUSIWI KUTOA SADAQAH KUTOKA MALI ILIYO HARAMU. 161

47. KULISHA CHAKULA NI SUNNAH. 165

48. MTOE SADAQAH KUTOKA VILE VITU MNAVYOVIPENDA SANA. 167

49. IMESISITIZWA MNO KUWANYWESHA MAJI WANAADAMU NA WANYAMA HATA KAMA HAPO KUTAKUWA NA MAJI MENGI MNO. 168

50. NI SUNNAH KUWATENDEA MEMA WAUMIN NA KUWATIMIZIA MAHITAJI YAO KWA UWEZO ALIONAO MTU NA KUWA NA UHUSIANO MWEMA PAMOJA NA MASHIAH WENZAKE. 170

51. INARUHUSIWA KUTOA SADAQAH KATIKA HALI YA rUKU’U, BALI NI SUNNAH. 173

52. KUGAWA NUSU YA MALI KATIKA SADAQAH NI SUNNAH. 177

MAREJEO YA SADAKA KATIKA QUR’ANI TUKUFU 178

VITABU VILIVYOKUSANYWA NA KUTARJUMIWA NA 181

 

 

 

 

The .HTML version of this book is taken from
www.al-islam.org and ebooked by www.ShiaLibrary.com and www.islamkutuphanesi.com . May Allah be pleased with all.

Kimekusanywa na kutarjumiwa na

AMIRALY  M.  H.  DATOO

BUKOBA – TANZANIA   


 

 


 

MANENO MAWILI

 

Bismillahir Rahmanir Rahiim

Natanguliza kumshukuru Allah swt pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ma-Imamu a.s. walionijaalia Tawfiqi ya kuweza kuwaleteeni mbele yeni kitabu hiki.

 

Mimi nimekitarujumu kitabu Dhambi Kuu la kutokulipa Zaka, Khums na Sadaka katika Kiswahili na wakati nikiwa nikiifanya kazi hiyo, niliona itakuwa afadhali iwapo Sadaka pia nitakitayarishia kitabu chake. Na hivyo ndicho hiki kipo mikononi mwenu.

 

Kwa hakika sisi tunakuwa daima tukitoa sadaka lakini hatujui habari zaidi kuhusu Sadaka na hivyo nimevutiwa na kazi aliyokuwa ameifanya Marehemu Mullah Asghar M.M.Ja’afer, aliyekuwa Mwenyekiti wa World Federation of Khoja Shi’a Ithna-Ashery Muslim Communities, na hivyo nimekitarjumu katika Kiswahili.

 

Kitabu hiki cha Sadaka ni sehemu ya Kitabu kiitwacho Wasa’il as-Shi’a mlango wa Kitabuz - Zakaat  cha Sheikh Hurri ‘Aamili.

 

Vile vile kumeongezewa habari za Elimul Hadith na Majma’ul Hadith kutokea juhudi zilizofanywa na Maulama wa Kishi’a.

 

Ni matumaini yangu kuwa kitabu hiki kitatufaidisha sote na tutakuwa na moyo zaidi wa kutoa Sadaka.

 

 

Amiraly M.H.Datoo         6/5/2002   -   23 Safar 1423

P. O. Box  838

BUKOBA- Tanzania

 

datooam@hotmail.com

 

 


TUJIELIMISHE KUHUSU ILIMU NA MENGINEYO …

 

MAIMAMU WA SHIA KATIKA UANDIKAJI NA UENEZAJI WA HADITH

 

Katika sehemu hii, twategemea kuzungumzia kwa mukhtasari msimamo wa Shia kuhusu uandikaji wa Hadith kutokea mwanzoni.  Itaonekana kuwa ni kinyume na msimamo wa wengine kuhusu swala hili.  Msimamo wa Kishia ulisisitiza mno juu ya uandikaji wa Hadith zikisaidia uhifadhi wake wakati ambapo Maulamaa mashuhuri wa Kisunni, hata kufikia mwanzoni mwa karne ya 3A.H./9 A.D. walikuwa wakipinga uandikaji wa Hadith.  Ni baada ya uandikaji wa Hadith ulipokuwa dhahiri hao wanaopinga walipoanza kwenda kinyume na Hadith walizokuwa wamezitoa wakipinga uandishi na uenezaji wake na hapo wakaanza kuziandika.

 

Alba ibn al-Ahmad ananakili kuwa mara moja Ali ibn Abi Talib a.s. wakati akitoa Hotuba juu ya mimbar, alibainisha: "Je, ni nani atakayeinunua elimu kwa Dirhamu moja?"  Al-Harith ibn al-A' war alinunua karatasi yenye thamani ya Dirhamu moja na kumwijia Imam Ali ibn Abi Talib a.s. na kuandika kiasi cha kutosha cha elimu juu yake.[1] Riwaya hii inatuonyesha vile Imam a.s. alivyokuwa akisisitiza juu ya uandikaji.

 

Imam Hassan ibn Ali ibn Abi Talib a.s. ameripotiwa akiwashauri watoto wake kama ifuatavyo:-

"Nyinyi sasa ni watoto wa Ummah ambao katika maisha ya mbeleni mtakuwa wakubwa wao.  Jielimisheni Elimu; na yeyote yule miongoni mwenu atakayeweza kuhifadhi (kukariri) elimu (yaani Hadith), basi aiandike na kuiweka nyumbani mwake."[2]

 

Imeripotiwa kuwa Hujr ibn Adi, mmoja wa Sahaba wa Mtume s.a.w.w. na Imam Ali ibn Abi Talib a.s., aliziandika Hadith za Imam Ali ibn Abi Talib a.s. katika kitabu na kuzirejea pale alipohitaji msaada wa mwongozo katika masuala mbalimbali [3] Mifano hii inadhihirisha umuhimu aliokuwa ameuambatanisha Imam Ali ibn Abi Talib a.s., watoto wake na Sahaba wake katika uandikaji wa Hadith.  Mifano miwili ifuatayo itaonyesha dhahiri vile Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alivyokuwa akisisitiza umuhimu wa Hadith na kuzihifadhi.

 

Umar ibn Ali anaripoti kuwa mtu mmoja alimwuliza Imam Ali ibn Abi Talib a.s. ni vipi kuwa yeye (i.e. Ali) aliweza kunakili na kusimulia Hadith nyingi za Mtume s.a.w.w. kuliko Sahaba wengineo.  Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alijibu: "Hii ni kwa sababu daima nilipokuwa nikimwuliza swali Mtume s.a.w.w., alikuwa akinijibu maswali yangu.  Na pale nilipokuwa nikiwa kimya, basi Mtume s.a.w.w. alianzisha mazungumzo mwenyewe." [4]

 

Ali ibn Hawshab anaripoti kutoka Makhul, mwanachuo kutokea Syria, kuwa Mtume s.a.w.w. aliisoma Ayah ya Qur'an, Surah Al-Haqqah,69, Ayah  12)

 Ili tuyafanye hayo  kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi

 

Na hapo alimwambia Imam Ali ibn Abi Talib a.s. "Mimi nimemwomba Allah swt kuwa masikio hayo yawe ni yako."  Baadaye Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alisema:  "Mimi kamwe sikusahau Hadith yoyote au chochote kile kilichosikilizwa na sikio langu kikisemwa na Mtume s.a.w.w. [5]

 

Umar ibn al-Harith anasema: 

"Wakati mmoja Ali  a.s. aliuelekeza uso wake kuelekea mbinguni na kuurudisha chini akisema:"Mwenyezi Mungu na Mtume wake s.a.w.w. wamesema kweli." "Je, kilikuwa nini?"  Kikundi cha watu kiliuliza.  Imam Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alisema: "Mimi ni mpiganaji wa vita na vita vinarithishia mtu ulaghai. Vivyo hivyo, ninaweza kukubali iwapo nitaporomoka kutokea mbinguni kwa ajili ya kunaswa na ndege kuliko kumsingizia uwongo Mtume wa Allah swt. Kwa hivyo fuateni chochote kile mukisikiacho kikitoka kwangu........" [6]

 

Kauli juu ya uandishi wa Hadith pia zimenakiliwa kutoka Maimamu wengine.

Al-Imam al-Sadiq a.s. alisema:

"Andikeni na kuieneza elimu yenu miongoni mwa ndugu zenu, na iwapo mtafariki basi watoto wenu watarithi vitabu vyenu.  Itafika siku ambapo patatokea machafuko na hapatakuwapo na mtu wa kumfanya rafiki na wala hapatakuwa na chochote cha kuweza kutegemewa isipokuwa ni vitabu tu....[7]

 

Al-Imam al-Sadiq a.s. pia amenakiliwa kwa kusema:  "Hifadheni vitabu vyenu kwani mutakuja kuvihitaji hivyo siku moja."  Vile vile ameripotiwa akisema kuwa nguvu za moyo na kuhifadhi akilini inategemea mno juu ya maandishi.[8]

 

Abu Basir anaripoti kuwa aliambiwa na Imam al-Sadiq a.s.: "Baadhi ya watu waliotoka Basrah walikuwa wakija na kuniuliza kuhusu Hadith na waliziandika.  Je, kwa nini nawe hauziandiki?"  Na aliongezea kusema, "Elewa wazi wazi kuwa wewe kamwe hautaweza kuhifadhi Hadith bila ya kuiandika."[9]

 

Idadi kubwa ya mapokezi yanaonyesha kuwa Maimamu a.s. walikuwa navyo vitabu na maandishi ambavyo walirithi kutoka vizazi vilivyowatangulia.[10]

 

Katika riwaya nyingine Imam Ali ibn Abi Talib a.s. ameripotiwa akiwa amesema:  "Ikamateni elimu (kwa kuiandika),"  ambavyo aliirejea mara mbili [11] Imeripotiwa kutoka Ja'bir kuwa Abu Hanifa alikuwa akimwita al-Imam al-Sadiq a.s. "Kutubi" (yaani mwenye vitabu) kwa sababu ya kutumia mno vitabu, na Imam a.s. alifurahishwa kwa jina kama hilo.  [12]

 

Vile vile imeripotiwa kuwa al-Imam Muhammad ibn Ali al-Baqir a.s. ameziandika Hadith za Mtume s.a.w.w. ambazo zilikuwa zikinakiliwa na Jaabir ibn Abdullah Ansaari. [13]  

 

(Ingawaje taarifa hii inaonyesha kuwa siyo ya ukweli kwani Jaabir alikuwa ameshakwisha kufariki wakati Imam a.s. alikuwa na umri wa miaka mitano tu, labda inawezekana kuwa Hadith ziliandikwa na mjumbe).


MASHIA NA UANDISHI WA HADITH:

 

Kwa kuwa riwaya (desturi) ya uandishi wa Hadith ilikuwapo miongoni mwa Shia tangia mwanzoni, wao walikuwa wanaongoza katika uandishi wa Hadith na Fiqh. Dr. Shawqi Dayf anaandika:

"Mwelekeo na umuhimu wa Mashia katika uandishi wa Fiqh umekuja daima ni madhubuti mno. Sababu nyuma yake ilikuwa ni imani yao katika Maimamu wao ambao walikuwa ni kiongozi wao (haad) na wakiwa wameo ngozwa na Allah swt (mahdi) na fatawa zao zimekuwa zimeshikamana. Kwa hivyo, wao walipatiwa uzito na umuhimu katika misemo ya Imam Ali ibn Abi Talib a.s. Na kwa sababu hiyo, mkusanyiko wa kwanza ulifanywa na Mashia, ulifanywa na Sulaym ibn Qays al-Hilali, katika zama za al-Hajjaj." [14]

 

Al-Allamah al-Sayyid Sharaf al-Din anaandika:

“Imam Imam Ali ibn Abi Talib a.s. na wafuasi wake walitilia mkazo na kufuatilia swala la uandishi kuanzia mwanzo kabisa.  Jambo la kwanza kabisa lililotiliwa mkazo na kufuatiwa na Imam Ali ibn Abi Talib a.s. ilikuwa ni kuiandika Quran nzima, ambayo aliifanya baada ya kifo cha Mtume s.a.w.w. kwa kuiandika kimpangilio wa ufunulio wa Aya za Qurani.Katika Qurani hiyo pia alikuwa ameonyesha ni aya zipi zilizokuwa 'amm au khass, mutlaq au muqayyad, muhkam au mutashabih. Baada ya kukamilisha hayo, aliendelea na kazi ya ukusanyaji wa kitabu kwa ajili ya Fatimah, ambacho kilikuwa kikijulikana kwa vizazi vyao kama Sahifat Fatimah. Baada ya hayo, aliandika kitabu juu ya diyat (fidia) ambacho kilijulikana kama Sahifah.  Ibn Sa'id amenakili hivyo katika musnad kutoka kwa Imam Ali ibn Abi Talib a.s. mwishoni mwa kazi yake mashuhuri al-Jami.'  Mtunzi mwingine wa Kishia ni Abu Rafi, ambaye alikusanya maandiko yakiitwa kitab al-Sunan wa al-ahkam wa al-qadhaya. [15]

 

Marehemu Sayyid Hassan al-Sadr anaandika kuwa Abu Rafi, aliyekuwa mawla wa Mtume s.a.w.w. ndiye aliyekuwa wa kwanza miongoni mwa Mashia kwa kukikusanya kitabu. [16]  al-Najashi katika Fihrist ameelezea kuwa Abu Rafi alikuwa ni mtunzi katika kizazi cha kwanza cha Mashia.  Mfuasi wa Imam Ali ibn Abi Talib a.s. Abu Rafi alishiriki katika vita vya Imam Ali ibn Abi Talib a.s. na alikuwa ni mwangalizi wa hazina ya Serikali huko Kufah. Kitabu chake kilichokuwa kikiitwa Kitab al-Sunan wa al-ahkam wa al-qadhaya, ambacho kilikuwa kimeanza kwa sura izungumziayo Salat, kufuatiwa na sura juu ya Saumu, Hajj, Zakat, kutolewa kutoka kwa Imam Ali ibn Abi Talib a.s. katika Kufah, Kitabu hiki kilinakiliwa na Zayb ibn Muhammad ibn Ja'afer ibn al-Mubarak katika nyakati za al-Najashi.

 

Ali ibn Abi Rafi, mwana wa Abu Rafi, aliye tabi't na Mshia khalisi ameweza vile vile kukusanya kitabu kilichokuwa na sura mbali mbali juu ya mambo ya Sheria kama vile wudhuu, Salaat, n.k.  [17]

 

Kama ilivyoelezwa hapo awali, abu Hanifa alimwita al-Imam al-Sadiq a.s. kutubi (akisema 'innahu kutubi' ) sifa ambayo ilimtambulisha na wengineo.  Wakati Imam a.s. aliposikia kuhusu hayo, alicheka na kusema,  "...... lakini kila alichokisema kuwa kwangu suhufi ni kweli; mimi nimesoma suhuf (vitabu) vya mababu zangu." [18] Riwaya hii inaonyesha kwa wazi wazi kuwa Imam a.s. alikuwanavyo vitabu fulani ambavyo alipewa na mababu zake, na hiki kilikuwa ni kipindi ambacho Ahl al-Sunnah walikuwa hawakutilia mkazo katika uandishi wa Hadith.

 

Miongoni mwa mapokezi ambayo inatuonyesha kuwa ma-Imam a.s. walikuwa navyo vitabu kama hivyo, ni mojawapo iliyoripotiwa na Muhammad ibn 'Udhafir al-Sayrafi anasema:

"Mimi nilikuwa pamoja na al-Hakam ibn Utaybah na tulimtembelea al-Imam al-Baquir a.s. Al-Hakam alimwuliza swali Imam a.s. Abu Ja'afer a.s. alikuwa akimstahi sana. Wao walitofautiana juu ya swala fulani na hapo Abu Ja'afer alisema: "Mwanangu (mtoto wake), inuka na ukilete kitabu cha Imam Ali ibn Abi Talib a.s. Huyo mtoto alimletea kitabu kikubwa, ambacho Imam a.s. alikifungua, na kulipitishia macho hadi kulipata swala walilokuwa wakilizungumzia. Na hapo Abu Ja'afer a.s. alisema:  "Haya ni maandishi ya Imam Ali ibn Abi Talib a.s. na yaliyosemwa na Mtume s.a.w.w..........."[19]

 

Katika riwaya nyingineyo ameripotiwa Imam al-Baquir a.s. akisema: "Katika kitabu cha Imam Ali ibn Abi Talib a.s. nimepaona ambapo Mtume s.a.w.w. akisema: 'Wakati zakat itakapokuwa hailipwi, basi baraka itapotea kutoka ardhi."  [20]

 

Vile vile ipo imeripotiwa kuwa Imam al-Sadiq a.s. amesema:

Baba yangu alisema: 

"Mimi nimesoma katika kitabu cha Imam Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa Mtume s.a.w.w. ameandika mkataba baina ya Muhajirun na Ansar na watu wengineo wa Yathrib ambao waliungana naye, ikisemwa humo hivi:  "Jirani ni sawa na mtu mwenyewe; asitendewe visivyo haki au kutendewa madhambi. Utukufu wa jirani wa mtu ni sawa na ule utukufu wa mama yake." [21]

 

Katika riwaya nyingine al-Imam al-Sadiq a.s. amesema:

Imeelezwa katika kitabu cha Imam Ali ibn Abi Talib a.s.

"Mfano wa dunia ni sawa na mfano wa nyoka: ngozi yake nyororo mno, lakini ndani yake ni sumu kali mno. Mtu aliye mwenye busara hujiweka naye mbali, lakini jahili anafanya kila aina ya jitihada ya kutaka kuikaribia." [22]

 

Kwa mujibu wa riwaya nyingineyo, habari ifuatayo imetoka katika kitab adab Amir al-Muminiin:

Mtu yeyote asijaribu kurejea katika mithali katika masuala ya Din, kwani amri ya Allah swt haiwezi kutambuliwa kwa mithali.  Watatokezea watu ambao watakuwa wakirejea katika mithali, na hao watakuwa na uadui pamoja na Din. [23]

 

Zurarah anaripoti:

Nilimwuliza al-Imam al-Baquir a.s. kuhusu hisa ya babu katika urithi.  Imam a.s. alijibu: "Sijawahi kumwona mtu yeyote yule akilisemea swali hili bila ya kuongezea mawazo yake ya kibinafsi, isipokuwa Amir al-Muminiin Ali ibn Abi Talib a.s.." Mimi nilimwuliza: "Na jee alisema nini?" Imam a.s. alinijibu: "Njoo kesho, mimi nitakusomea kutoka kitabuni." Mimi nilisema, "Mimi niwe fidia juu yako, naomba uiseme katika mtungo wa Hadith kwani Hadith zako ni afadhali kwangu kuliko kukisoma kitabu." Imam a.s. alisema: "Tafadhali usikilize kile nilichokuambia. Njoo kesho na mimi nitakusomea kutoka kitabu hicho." Siku ya pili mimi nilimwendea Imam a.s. wakati wa adhuhuri. Jaafer ibn Muhammad mwanae Imam a.s. alinikaribia na Imam a.s. alimwambia kunisomea kitabu hicho........[24]

 

Katika riwaya nyingine, Imam al-Sadiq a.s. anasema: 

"Ipo imeelezwa katika Kitabu cha Imam Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa mtu anywaye pombe na mwenye kumsaidia aliyelewa (muskir) basi wote wanastahili kuadhibiwa, ambavyo ni sawa katika sura zote mbili." [25]

 

Muhammad ibn Muslim, Sahaba wa Imam al-Baquir a.s. asema:

 "Abu Jaafer alinisomea kitabu kitab al-faraidh, ambacho yalikuwemo yaliyosemwa na mtume s.a.w.w. na kuandikwa na Imam Ali ibn Abi Talib a.s.." [26]

 

Habari zote zilizotajwa hapo juu, ambazo ni chache sana kutokea riwaya nyingi mno kama hizo, zinatudalilisha kuwa desturi ya Mashia ya kuandika Hadith imetangulia mawaidha ya ma-Imam a.s. kwa sahaba wao kuhusu uandishi wa Hadith.  Ilikuwa ni desturi ambayo ilianzia katika zama za Mtume Mtukufu s.a.w.w. na ilikuwa imeanzishwa na Imam Ali ibn Abi Talib a.s. Zipo Hadith, nyingi katika desturi ya Mashia ambazo zimetimiza kanuni za tawatur, na vile vile yapo marejeo katika Sunni ambazo zinathibitisha na kushuhudia Hadith kama hizo.

 

Mambo yote hayo yanakuelekeza katika uimara na uhakikisho wa usahihi wa Hadith zilizonakiliwa na Mashia.  Hii ni kwa sababu pamoja na kuendelea na maongozo ya Maimamu a.s. hadi kufikia katikati ya karne 3 A.H./9 A.D., Hadith za Mashia zilitoa watunzi wengi mno na ambao maandishi yao kuanzia kipindi cha al-Imam al-Sadiq a.s. yamekuwa kwa hakika ni katika idadi kubwa sana.  Iwapo mtu ataweza kutupia macho Rijal al-Najashi, basi huyo ataweza kuona kuwa wafuasi wa Imam a.s. wametupatia kazi kubwa ambazo zimetumika kama misingi ya Fiqh katika Ushia.

 

Ukweli ni kwamba, Mashia idadi yao ndogo kwa upande mmoja na maisha ya hatari waliyokuwa wakiishi kwa upande wa pili ambayo iliwazuia watu waovu na wenye kuvizia majukumu kuingia katika Ushia pamoja na umuhimu uliosisitizwa na Maimamu a.s. na wafuasi wao katika uandishi, ndivyo vilivyoleta matokeo ya utajiri na usahihi wa Fiqh ya Kishia.  Haya ndiyo faida ambazo hazikupatikana kwa Ahl al-Sunnah kwani, kwanza, wingi wa idadi yao, pili, kwa kuwa madhehebu ya Sunni ndiyo iliyokuwa Dini ya utawala wa Dola, na tatu, kwa sababu ya ukosefu wa Hadith zilizoandikwa kwa Waislam kwa ujumla kuyafuatilia yale yanayotokana na ukweli wa misingi ya kihistoria.

 


HISTORIA YA UANDISHI WA HADITH KATIKA SUNNI:

 

Kazi zote zilizopo hadi leo zinazohusu Hadith zilikuwa zimekusanywa katika kipindi cha karne 2 A.H./8 A.D. au katika karne ya 3 A.H./9 A.D.  Historia inatuonyesha kuwa katika kukaribia karne ya 2 A.H.  kulitokezea idadi ndogo ya Muhaddithun ambao walianza kuziandika Hadith, ingawaje hazikuwa na mpangilio.  Baadaye mkusanyiko huu mdogo ulikuwa kiini cha kazi zote kubwa.  Hata hivyo wingi wa Hadith zilizopo sasa kwa kukusanywa, zilienezwa kwa desturi ya kutamkwa (kusemwa), na wakati zilipokuja kuandikwa vitabuni, zilikuwa hazikuwahi kuandikwa popote kabla yake.

 

Ucheleweshwaji katika kuandikwa kwa Hadith ni swala mojawapo muhimu katika historia ya Hadith.  Umuhimu wake ni wa ukweli kwamba kucheleweshwa huu kuliathiri hasa kuhusu utunzi na idadi ya Hadith pamoja na uwepesi wao wa kuzushwa (zikaongezwa na kupunguzwa na hatimaye zikawa ni zile zilizo na uongo) na matatizo mengi mengineyo yanayohusiana.

 

Jambo la umuhimu huu katika swala hili linawahusu wale ambao ndio waliokuwa wamesababisha ucheleweshwaji huo wa kuandikwa kwa Hadith.  Mwelekeo wao ulikuja kama ni mfano kwa ajili ya wengine katika kutoziandika Hadith.  Katika sehemu yetu hii, tutaweza kuchambua makusudio yao na athari za mwenendo wao wa aina hiyo juu ya Hadith.

 

Kila kinachoweza kukusanywa kwa shida katika Historia ni kwamba baadhi ya Makhalifa walizuia uandikaji wa Hadith kwa sababu fulani fulani.  Baada yao kikundi cha Sahaba na Tabiun waliwafuata katika swala hili.  Kwa mujibu wa msemo "Watu hufuata dini ya wafalme wao,"  wao walijiepusha na uandikaji wa Hadith kwa kukubali na kuridhia kwa kuharamishwa hivyo.

 

Wao walizihifadhi Hadith za Mtume s.a.w.w. kwa kuzikariri tu (kwa kuzihifadhi akilini mwao tu).  Kama vile tutakavyoona hapo mbeleni, wao nyakati zinginezo walijaribu kurejea katika kuziandika, ili kuyateketeza maandishi yao katika kipindi cha mwisho wa maisha yao, kama kwamba maandishi hayo yaliwasaidia wao tu katika kuhifadhi kwao.  Kumbukumbu hizo za Hadith zilizokuwa zimeandikwa hazikutumiwa kwa kutaka kuzihifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo.  Ni jambo la kuvutia sana kuona kuwa kupigwa marufuku wa uandikaji wa Hadith katika Sunni ulitolewa na watawala wao; na vile vile ile amri ya kuziandika Hadith pia zilitolewa na watawala wao.

 

Al-Zuhri anasema:

"Sisi tulikuwa tukichukia mno uandishi wa elimu, hadi hapo wakuu wetu walipotulazimisha kuyaandika hayo.  Hapo baadaye tulikuja kugundua kuwa hapakuwapo na yeyote miongoni mwa Waislam waliopinga."

 

Al-Zuhri anaendelea kusema:

"Wafalme waliniambia kuandika elimu ('ilm, i.e. Hadith) kwa ajili yao.  Baada ya kuwaandikia kwa muda fulani, mimi nilishikwa na aibu mbele ya Allah swt; (mimi nilijiuliza):  Je, kwa nini nimejitayarisha kwa ajili ya kuwaandikia wafalme na wala si kwa ajili ya watu wengineo!?" [27]

 

Ni dhahiri, kama vile itakavyokuja kuonekana kwamba Hadith hazikuwa ni kweli kwa ajili ya Sahaba na Tabiun wote.  Wengi wao na akiwemo Ali ibn Abi Talib a.s. waliziandika Hadith na vile vile waliwaambia wengine kufanya hivyo.  Wengine walianza kuziandika Hadith wakati sheria zilizowekwa na Makhalifa juu ya kutoziandika Hadith zilipobadilishwa na amri ya Kikhalifa kutoka kuziandika Hadith.[28]

 

'Umar ibn Abd al-Aziz (101 A.H./719 A.D.) ndiye aliyekuwa Khalifa wa kwanza kuamrisha wanazuoni wa miji mbalimbali kuziandika Hadith na kumpelekea huyo Khalifa maandishi yote. [29] Imeripotiwa kuwa Khalifa alimwandikia Muraah ibn Kathir akimwomba amwandikie Hadith za Mtume s.a.w.w. [30]  Vile vile yeye alimwandikia Abu Bakr ibn Muhammad Hazm: "Andika Hadith yoyote ile ya mtume s.a.w.w. uliyonayo na kunitumia na chochote kile kilichonakiliwa kutoka kwa Umar, kwa sababu ninayo hofu kuwa utafika wakati ambapo Hadith zitakuwa zimetoweka."  [31] Yeye pia aliwaandikia watu wa Madinah akiwataka wamwandikie chochote kile kilichobakia cha Hadith za Mtume s.a.w.w. [32]

 

Ripoti hizi zinaonyesha wazi wazi kuwa uandikaji wa Hadith haukuwa jambo lenye umuhimu hadi wakati huo, hata hivyo, haimaanishi kuwa hapakuwepo na Hadith zilizokuwa zimeandikwa hadi wakati huo.

 

Pamoja na kifo cha Umar ibn Abd al-Aziz kazi hii haikufuatiliwa na Makhalifa waliofuata, na kwa mara nyingine tena uandikaji wa Hadith uliangukia katika kusahauliwa.  Kukariri (kuhifadhi katika akili) ndiyo iliyokuwa njia iliyobakia.

 

Hadith za kusemwa mdomoni tu  (bila ya maandiko) ndiyo iliyokuwa njia ya uenezaji wakati ambao Sunni walirithi kutoka vizazi vyao vilivyowatangulia, ilisababisha upinzani mkubwa mno katika kuziandika Hadith. Sisi twaweza  kuelewa vyema hali hii wakati tutakapokuja kujua kuwa baadhi ya Muhaddithun walichukizwa mno na uandishi wa Hadith hadi kufikia mwishoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D.  Kauli za wanahistoria kuhusiana na ukusanyaji wa Hadith hapo mwanzoni zinaelezea hayo hayo.

 

Abd al- Razzaq anaelezea kuwa mtu wa kwanza kuzikusanya Hadith alikuwa Abd al-Malik ibn Jurayj, aliyejulikana kama Ibn Jurayj (150 A.H./767 A.D.)  Vile vile Abd al-Rahman Al-Awzai (88-157 A.H./707-773 A.D.) alikuwa ni miongoni mwa wale walioanza kuzikusanya Hadith.[33]

 

Al-Dhahabi anaandika kuwa, katika kipindi hiki ndipo Wanazuoni wa Kiislamu walianza kuandika Hadith, Fiqh na tafsiri katika mwaka 143 A.H./760 A.D.  Wafuatao ndio waliokuwa wakiongoza katika kazi hizo nao ni Ibn Jurayj katika mji wa Makkah, Malik (179 A.H./795 A.D.) huko Madinah, al-Anzai katika Syria, Said ibn Abi Urwah (156 A.H./783 A.D.) huko Basrah, Muammar huko Yemen, Sufyan al-Thawri (156 A.H./783 A.D.) huko Kufah.  Kabla ya kipindi hicho, hata hivyo, Muhaddithun waliongoza wakiripoti Hadith kutokea kukariri au kutokea kwa waliotegemewa lakini zilikuwa ni mikusanyo isiyokuwa na mipangilio.[34]

 

Mahali pengine yeye ni mbainifu zaidi wakati asemapo: "Ibn Jurayj na Ibn Abi Urwah walikuwa ni miongoni mwa watu wa kwanza katika ukusanyaji wa Hadith na Muammar ibn Rashid alikuwa ni wa kwanza miongoni mwao huko Yemen." [35]  Ipo habari iliyoripotiwa na Abd al-Aziz ibn Muhammad al-Darwardi kuwa mtu wa kwanza kukusanya elimu alikuwa Ibn Shihab al-Zuhri. [36]  Ibn Shihab al-Zuhr (124 A.H./742 A.D.) mwenyewe anaripotiwa akiwa amesema: "Umar ibn Abd al-Aziz alituamrisha kuzikusanya Hadith za Mtume s.a.w.w.  Kufuatiwa hayo sisi tuliandika katika sura ya kitabu, na kupeleka nakala ya kitabu hicho katika sehemu zote za utawala wake." [37]

 

Ni dhahiri, ingawaje Hadith zilikuwa zikikusanywa kwa kiasi fulani katika siku hizo, kazi ya ukusanyaji ilianza kuzorota kwa sababu ya upingamizi uliofuatia kifo cha Umar ibn Abd al-Aziz, na vile anavyosema al-Dhahabi, kazi hiyo ya ukusanyaji wa Hadith uliahirishwa au kuachwa kwa kipindi cha nusu karne.

 

Ibn Hajar anasema:

“Kazi ya ukusanyaji na upangaji (tabwib) wa Hadith ulianza katika miaka ya mwishoni mwa kipindi cha tabi'un, yaani ni kwamba, wakati ambapo Wanazuoni wa Kiislam walipokuwa wameenea katika miji.  Wa kwanza katika ukusanyaji wa Hadith walikuwa ni Rabi ibn Subayh na Sa'id ibn Abi Urwah......hadi wakuu miongoni mwa Wanazuoni wa tabaka la tatu walipokusanya ahkam. [38]

 

Al-Dhahabi pia anaelezea kitu kama hicho. [39] Kutokana na taarifa hizo inaweza kudadisiwa kuwa ukusanyaji wa Hadith uliotokezea katika sehemu mbili:  Sehemu ya kwanza ni mkusanyiko usio kamilifu mwanzoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. na sehemu ya pili ni ukusanyaji uangalifu katika sehemu yake ya pili.  Hajji Khalifah anakubaliana na haya pale asemapo:

 

“Wakati Islam ilipoenea katika sehemu mbalimbali, na miji ya Islam ilipopanuka, tabi'un walisambaa mote humo.  Baada ya muda, mkuu wao alipofariki dunia na hivyo ndivyo ilivyokuwa imekuja kuathiri ukusanyaji wa Hadith.  Wanazuoni walianza kuhisi haja ya kuziandika Hadith na kuzihifadhi kwa njia ya kuziandika.  Katika maisha yangu, lilikuwa ni jambo la maana la kuziandika Hadith, kwa sababu kukariri tu kuna uwezekano mkubwa wa kuweza kuja kupoteza fahamu au kuzipotoa.  Baada yao, kulitokezea kipindi cha wataalamu wa Hadith kama Ibn Jurayj na Malik ibn Anas.  Inasemekana kuwa mtu wa kwanza katika kukusanya Hadith alikuwa Rabi ibn Subay wa Basrah.  Baada yahuyo, zoezi kama hili lilikuwa ni la kawaida. [40]

 

Kutokana na taarifa hizo, tunaweza kumalizia kuwa, kotekote, kulikuwapo na vipindi vitatu katika mpitilio wa Hadith za kutamkwa.  Kipindi cha kwanza kilichukua/kilidumu mwanzoni hadi mwishoni mwa karne ya 1 A.H. /7 A.D. katika kipindi hiki uandishi wa Hadith haukuwapo wala haukujaribiwa isipokuwa tu katika hali chache ambapo Sahaba walijaribu kuziandika kwa kwenda kinyume na amri ya Makhalifa. Katika kipindi cha pili, kuanzia mwanzoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. hadi kwa kufikia katikati, kulitokezea uandishi  na ukusanyaji wa Hadith katika hali isiyokuwa kamilifu na pia mambo yaliyoandikwa yaliweza kukusanywa. Katika kipindi cha tatu, kilichoanzia katikati ya karne ya 2 A.H./8 A.D., uangalifu mkubwa ulielekezwa katika ukusanyaji na uandikaji wa Hadith ikiwa ni shughuli muhimu kimsingi.  Vitabu vichache mno vilivyoandikwa katika kipindi hiki vinaweza kupatikana na baadhi ya mikusanyiko ya zamani sana pia vinaweza kupatikana na baadhi ya mikusanyiko ya zamani sana pia vinaweza kupatikana- kama vile musannaf Ibn Abi Shaybah, musannaf ya Abd al-Razzaq na Muwatta ya Malik ibn Anas yalikuwa yameanzishwa katika sehemu ya pili ya karne ya 2 A.H./8 A.D.

 

Kwa mujibu wa ripoti ya al-Dhahab, musnad ya kwanza ilikusanywa na Nu'aym ibn Hammad. [41]  Yahya al-Hamani [42] huko Kufah na al-Musd [43] huko Basrah nao ndio waliokuwa wa kwanza miongoni mwa Wanazuoni wa miji hii katika kukusanya musnad.

 


SABABU ZA UCHELEWESHO KATIKA UANDISHI WA HADITH:

 Inafahamika vyema kabisa kuwa Mtume s.a.w.w., kuanzia mwanzoni kabisa mwa Utume wake, aliupatia umuhimu zaidi kuhusu uandishi wa Qurani. Kimatokeo Qurani ikawa ipo mbali na makosa au mabadiliko (tahrif).   Hata hivyo, katika hali ya Hadith kwa mujibu wa imani yetu mbali na ruhusa au amri ya Mtume s.a.w.w. kwa kuhusiana na uandishi wa Hadith na mbali na ukweli kwamba Hadith zilikuwa zimeandikwa katika zama za uhai wa Mtume s.a.w.w. , sio kwamba tu kuwa haukupewa umuhimu kwa kazi, pia iliweza hata kupingwa.  Upingamizi huo ulisababisha matatizo mengi kuhusiana na Hadith, ambayo tutayaona hapo mbeleni.

 

Uchelewesho huo wa kuziandika Hadith na matokeo yenye hatari yalifanya kikundi kimoja kumtupia lawama na 'udhubillah Mtume s.a.w.w. Wao walitambua wazi kuwa upingamizi wa uandishi wa Hadith iwapo itatokea kwa Mtume s.a.w.w. , basi haitaweza kulaumiwa, kwani Mtume s.a.w.w. hawezi kulaumiwa; hata hivyo, iwapo wataielezea kwa wengine basi itatoboa udhaifu wao.  Kwa hivyo, walimwelekezea Mtume s.a.w.w. kuwa ndiye aliyekataza kuandikwa kwa Hadith.

 


HADITHI NI NINI ?

 

Mawaidha na Nasiha maneno aliyoyazungumza Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Hadith kwa kifupi, maneno yoyote yaliyotoka mdomoni kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mbali na ayah za Qur'an Tukufu, ama yale aliyoyatenda kuonyesha, hayo yote ni Hadith. Vile vile maneno na matendo yote ya Ma’asumin a.s. pia ni Hadith yaani yataingizwa katika Hadith. Kutokana na Hadith sisi tunaweza tukajua na kufuatilia na kutekeleza mambo ambayo ni usuliFuru’, Sunnah na faradhi.

 

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kwa maisha yake yote alikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  Hivyo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. popote pale alipokuwa akiwapa watu nasiha na mawaidha katika mambo mbalimbali na kuwaongoza katika masuala mbalimbali basi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. daima alikuwa akinufaika na hayo yaliyokuwa yakisemwa na kutendwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na ndivyo alivyosema “Sisi ndio dalili za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na vile vile ndio Sahaba wake halisi, na sisi ndio ufunguo wa hazina yake ya ilimu na mlango wa mji wake wa ilimu[44] alioutangaza Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na mtu yeyote hawezi kuingia katika nyumba au mji isipokuwa kwa kupitia mlango wake.”

 

Kwa kiapo cha Allah swt ! Mimi nina ilimu na ma’arifa ya Utume na maneno ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  Sisi Ahlul Bayt a.s. ni milango ya hekima na kwa hakika sisi ndio tunayo nuru ya hukumu za Allah swt. (Nahjul Balagha).

 

Katika historia tunapata habari kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ndio aliyekuwa mtu ambaye amekusanya na kuwa na hazina kubwa ya Hadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  Tumepata kuona kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. yeye daima alikuwa akiziandika Hadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kuzielewa na kuzikariri vyema kabisa. Na kwa amri ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ndipo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alitayarisha kitabu kimoja ambamo kumeandikwa Hadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Sunnah zake, na kitabu hicho kinaitwa Sahifat Jami’a na kitabu kingine kinaitwa Kitabul Faraidh, ambamo katika vitabu hivyo vyote viwili kumeandikwa Ahkam za Sharia.  Vitabu hivyo vimenakiliwa katika vitabu vingine mfano Sahih Buhari amenakili kwenye kitabu chake ambao ni upande wa Masunni. Na upande wa Mashi’ah Ma’ulamaa wa Kishi’ah Sheikh Sadduq a.r. amenakili katika kitabu kinachoitwa Manla yahdharulfaqih na Sheikh Tusi a.r. kinachoitwa Tahdhib na Thiqqatul Islam Quleyni r.a amenakili katika Al Kafi.

 


SHI’AH NA HADITH

 

Kwa hakika Mashiah wana mchango mkubwa sana katika uandishi wa Hadith na katika hali ambayo ni sahihi. Na wa kwanza kabisa ni mchango Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ambao hauna kifani wala usioelezeka, je litakuwa ni kosa gani iwapo wafuasi wake watamfuata yeye katika kuzidumisha na kuzihifadhi sirat na sunnah za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.? Katika historia vile vile tunapata mambo yaliyowazi kabisa kuwa kulikuwa na baadhi ya Ma-sahaba wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambao walikuwa wakikataa kabisa kusiandikwe Hadith kwa sababu ya visingizio kuwa vilikuwa vikigongana na ayah za Qur'an Tukufu. Na wapo Ma-Sahaba wengine pia wameadhibiwa vifungo na adhabu mbalimbali kwa ajili ya kunakili na kusambaza Hadith za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  Kwa hakika Ibn Hajar anaandika katika Futuh al-Bari utangulizi wake jambo moja la kustaajabisha, kuwa yeye anasema,

“Mwanzoni mwa Waislam kulikuwa na utata katika uandishi wa Hadith, kwa sababu baadhi yao walikuwa wanasema kuwa ni karaha kuziandika. Na katika wale waliokuwa wakisema kuwa ni makuruh alikuwepo ‘Umar bin Al Khattab, Ibn Masoud na Abu Sai’d Al Khudhri. Na katika upande wa pili ambao walikuwa wakieneza Hadith kwa usahihi walikuwa ni Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., mtoto wake Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. na vile vile Anas alikuwapo.  Na kwa hakika Mashi’ah wamekuwa mbele katika kueneza Hadith zilizokuwa sahihi na miongoni mwao nawaletea majina yao:

 

1.   Mtumwa wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliyekuwa akiitwa Abu Rafi’, na ambaye alikuwa miongoni mwa wale Waislam wa mwanzoni kabisa.

Bwana ‘Abbas mjomba wake Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ndiye aliyekuwa amempa zawadi huyo, na wakati huyo mtumwa alipo mpa habari Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa mjomba wake huyo Bwana ‘Abbas ameukubalia Uislam, basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa kusikia hiyo habari njema alimfanya huru huyo mtumwa kwa sababu ya kuleta habari hizo njema. Katika fadhila zake tunaona kuwa yeye alifanya Hijra mara mbili, na amesali katika Qibla zote mbili na amefanya Bay’a ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mara mbili.

 

Na vile vile ameshiriki katika vita vya Jihad vingi sana pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., na baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. yeye hakumwacha Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na daima alikuwa naye pamoja. Alikwenda na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. hadi Kufa, Nchini Iraq na alishiriki naye katika vita vitukufu vyote vilivyotokea na alikuwa ni mtu mmoja aliyekuwa akiaminiwa sana na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kiasi kwamba yeye alikuwa akitunza Baitul Maal pia. Yeye alifariki akiwa na umri wa miaka themanini na tano. Na yeye ni miongoni mwa Rawi wa Kishi’ah [45] wanaoaminiwa na kusadikiwa, naye ameandika kitabu kimoja ambamo ameandika riwaya za Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kinachoitwa Kitabu Sunan Wal-ahkam Wal-Qadhaya. Katika vitabu vya ‘ilmul Rijal kitabu hiki ni muhimu sana na chenye faida kubwa sana.

 

2.   Bwana Salman Muhammad (Al Farsi) ambaye baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliandika habari za Jasliq kwa niaba ya Mfalme wa Roma

 

3.   Asbagh bin Nabata, aliandika usia wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alioumfanyia Bwana Malik Ashtar, vile vile aliandika Nasiha alizomfanyia mtoto wake Muhammad. Asbagh bin Nabata alikuwa ni mmoja wa Ma-Sahaba wa karibu sana wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.

 

4.   Suleim bin Kais Al Hilali yeye ameandika kitabu chenye Ahadith ambacho kinatumika mpaka sasa hivi na kwa mara ya mwisho kilikuwa kimechapwa huko Najaf Al Ashraf, nchini Iraq. Hadith zake zimetokana na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mwenyewe na vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ; Miqdad, Salman, Abudhar na wapenzi wa Ahlul Bayt a.s.

 

5.   Mitham al-Tammaar yeye alikuwa mmoja wa Ma-Sahaba mashuhuri na mshupavu wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. yeye naye ameandika kitabu ambacho Sheikh Sadduq amekitumia katika ‘Aamali na vile vile Tabari ametumia katika Basharatul Mustafa.

 

6.   Zaid bin Wahab Aljahni ambaye ametunga kitabu kimoja ambamo ameandika hotuba zote za Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alizokuwa akizitoa siku za Ijumaa na Idi, kwa hakika ameufanyia ‘umma huu ihsani kubwa sana. Ibn Hajar na Ma’ulamaa wengine wanasema kuwa huyu bwana Zaid bin Wahab Thiqqah na wanampa Ukuu. Yeye amefariki katika mwaka takribani 96 Hijriyyah.

 

7.   Mkusanyiko mkubwa kabisa wa semi na Dua za Ma’sumin a.s. yanayojulikana kama Sahifa al-Kamila na vile vile inajulikana kama Zaburi Al Muhammad. Kitabu hicho kimekuwa tangia uhai wa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. na humo kumeandikwa semi zao n.k. ambayo yalikuwa yamesimamiwa kikamilifu na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ndiye aliyefanya mpango huo.

 

8.   Jabir bin Yazid bin Al Harith Al Jaufi, yeye ameziandika yaani yeye katika nuru ya ahadith za Masumin a.s. ameandika Tafsiri, vita vya Jamal, Siffin, na Naherwaan, na vile vile ameandika kuuawa kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s.  Yeye amefariki katika mwaka 128 Hijriyyah.

 

9.   Bwana Abu Hamza Thumali (aliyefariki mwaka 150 Hijriyyah) alikuwa mmoja Sahabi mashuhuri mwaminifu kabisa wa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. na Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. na ameweza kutunga kitabu kiitwacho Annawadir Wa-Dhuhud. Vile vile amefanya tafsiri ya Qur'an Tukufu pia.

 

10. Vile vile miongoni ma Ma-Sahaba wa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. na Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. alikuwa akiitwa Muhammad bin Keis Al Bijalli ambaye ameandika kitabu kiitwacho Qadhaya Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.

 

11. Aban bin Taghlib (aliyefariki mwaka 141 Hijriyyah) ni kwamba wote wanaafikiana kuwa yeye ameishi katika zama za Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s., Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., na Hadith zao alizozileta huyu Aban bin Taghlib zinasemwa kuwa ni Asili. Yaani inamaanisha kuwa Hadith zake hizo yeye alizoziandika zimetoka moja kwa moja kutoka kwa Maimamu a.s. na si kwa kupitia watu wengine walizozisikia inamaanisha kuwa ni yeye mwenye amezisikia hizo.

 

12. Takriban waliosomea ilimu ya Hadith ilifikia elfu nne au na zaidi kuanzia katika zama za Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Siku moja Hassan bin Ali Alwashakhi yeye alikutana na wale watu waliokuwa wakizoea kuzisema Hadith si chini ya mia tisa katika Masji Al-Kufa, na wengi wa wale waliokuwa wakizisema hizo Hadith walikuwa wakisema tumeambiwa Hadith hii na Ja’afar bin Muhammad yaani zilikuwa ni Hadith asili ambazo huyo mtu amezisikia moja kwa moja kutoka kwa Maimamu a.s.

 

13. Ibn Nadhir katika kitabu chake Fahrist amemwandikia yule Yunusu bin ‘Abdul Rahman na habari zake kuwa ni mtu mmoja mwaminifu na mwenye kutegemewa kabisa ambaye miongoni mwa Ma-Sahaba wa Al Imam Musa al-Kadhim a.s. na Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. Kwa hakika kitabu hiki ni chenye manufaa sana kiitwacho Jawamiul Aasar.

 

14. Ibn Nadiim katika kitabu chake Fahrist amewaandika watoto wawili wa Sa’id bin Himad ambao ni Hussein na Hassan na vile vile ameandika habari zao pia, kuwa hawa watu walikuwa ni hodari kabisa katika ‘ilimu ya Hadith, Fiq-h na Manaqib. Hao wote walikuwa wana kitabu walichokitunga juu ya Hadith na walikuwa ni miongoni mwa Ma-Sahaba wa Al Imam Muhammad Taqi Al Jawad a.s. na Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s.

 

15. Fadhl Bin Shaazan Nishapouri (aliyefariki 260 Hijriyyah) yeye amewahi kuwa Sahaba wa Maimam watatu a.s. ambao ni, Al Imam Muhammad at-Taqi a.s., Al Imam 'Ali an-Naqi a.s. na Al Imam Hassan al-'Askari a.s.  Naye ameandika vitabu vitatu:

·         Cha kwanza Kitabul Faraidh Al Akbar,

·         cha pili Kitabu Faraidh Al Awsat,

·         cha tatu Kitabu Faraidh Al-Asghar  ambacho ni mashuhuri.

 

16. Na baada ya hapo hii kazi ya ukusanyaji na uandishi wa Hadith ulikuwa umeendelezwa na Ma-Sahaba na wazee na wameweza kuleta kazi nne zilizo kubwa kabisa. Kazi hizo nne ambazo mpaka leo zinajulikana kwa jina la mashuhuri Kutub Al-‘Arbi’a yaani inajulikana kwa jina la vitabu vinne. Kitabu Cha kwanza kabisa ni Al Kafi, ambacho kimetayarishwa na kuandikwa na Thiqqatul Islam Al Quleyni a.r. (amefariki mwaka 329 Hijriyyah) katika kitabu hiki zipo Hadith takribani elfu kumi na sita.  Vile vile kuna kitabu kingine kinachoitwa Man la haydharul faqih ambacho kimeandikwa na Bwana Abu Ja’afer As-Sadduq humo takribani Hadith elfu sita zinapatikana. Vile vile kulikuwa na kitabu chake kingine kijulikanacho kwa jina Madinatul ‘Ilm ambacho Shahid a.r. amekizungumzia.

 

Na kwa kutokana na fitina za zama hizi kitabu hiki hakipo yaani hakipatikani  Na Sheikh Sadduq a.r. katika mwaka 381 Hijriyyah.

 

      Vile vile tunapata vitabu viwili mashuhuri na vyenye faida sana ambavyo vinavyoitwa Tahdhibul Ahkam na kingine Al-Istibsaar vyote vikiwa vya Sheikh Taifah Bwana Ja’afer Muhammad bin Hassan Tusi (aliyefariki mwaka 460 Hijriyyah).  Kwa kuunganisha vitabu vyote viwili zipo Ahadith elfu kumi na nane zilizo andikwa.

     

Kwa hakika katika zama zote hizi ilimu hii ya Hadith na katika nuru ya Ayah za Qur'an Tukufu na Sunnah ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ‘ummah umeweza kuwatambua na kuwafuata Ahlul Bayt a.s. na kuweza kujipatia ma’arifa yao na Ma-Sahaba. Katika kila zama kazi zilikuwa zikifanyika kwa kiwango fulani katika kuendeleza jitihada hizi za Hadith lakini katika mwaka wa 11 Hijriyyah kulifanywa kazi moja kwa kiasi kikubwa sana cha kutungwa kwa kitabu kiitwacho Bihal Al Anwar ambacho kilitungwa na Muhaqqiq ‘Allama Majlisi a.r. (aliyefariki 1111 Hijriyyah), kitabu hicho ambacho kilikusanya Hadith kwa wingi. Kwa hakika kitabu hiki kimoja yaani Bihal Al Anwar sisi hatujakipa heshima kiasi inavyotakiwa na wala sisi hatujafaidika nacho kiasi tunachotakiwa kufaidika nacho. Bihal Al Anwar ni kitabu ambacho Hadith ambazo hazikuandikwa katika Kutub Al-‘Arbi’a basi hizo Hadith zinapatikana katika kitabu hiki cha Bihar Al Anwar. Kwa hakika kitabu hiki kina Juzuu ishirini na sita lakini katika Jamhuri ya Kiislam ya Iran na Beirut wamejaribu kukipanga katika vitabu vidogo zaidi ambavyo vimefikia Juzuu mia moja na kumi, ambavyo hata mimi ninavyo. Katika zama hizi vitabu hivyo na vingine vingi vinapatikana kwa urahisi katika CD za compyuta ambavyo mtu hana haja ya kujitwisha vitabu hivyo na inakuwa rhisi kutafuta masuala atakayo.

 

Kwa hakika Maulamaa wamefaidika sana na Hadith zilizo andikwa katika Bihar Al Anwar na vile vile inadhihirisha vile wanavyoonyesha kuisifu na kuiheshimu kazi hiyo na hapa nimejaribu kuwaletea baadhi ya majina yao ambao wamekuwa katika zama zake hizo na mmoja miongoni mwao kama Marhum ‘Allamah Majilisi alipewa ruhusa ya kunakili yaani ‘ijaza ya riwaya.

 

1.   Muhammad bin Hassan Hurri ‘Aamili aliyefariki mwaka 1104 na mwandishi wa kitabu kinachoitwa Wasa’il as-Shi’ah, nacho kimechapwa si chini ya Juzuu ishirini.

 

2.   Mullah Muhsin Faiz Khashani aliyefariki 1091 na ambaye ni mwandishi wa Al-wafi  Kitabu hiki kina Juzuu kumi na nne kinazungumzia juu ya Usul, Furu’, Sunan, na Ahkam.

 

3.   Mulam ‘Abdullah bin Nurullah Bahrani mwandishi wa kitibu kiitwacho Al Awalim kitabu hiki kiko katika Juzuu mia moja. 

 

4.   Sheikh Muhammad Ridha bin Abdul Latif Tabrizi, aliyefariki mwaka 1158 na ni mwandishi wa kitabu kiitwacho As-Shifa’.

 

 


MTUNZI NA HABARI ZAKE.

 

Kitabu hiki cha sadaqah  ambacho kipo kwa mikononi mwenu, Hadith zake zimetolewa kutoka Wasa’il as-Shi’ah na tunaona vyema kuwaleteeni habari chache kuhusu kitabu na mtunzi wake.

 

Sheikh Hurri ‘Aamili baada ya jitihada zake nyingine kwa muda wa miaka ishirini mfululizo amekigawa kitabu hicho katika sehemu sita katika fani mbalimbali na kuzigawia Hadith kimpangilio mzuri kabisa kwa na hakika anastahili pongezi kubwa sana kwa jitihada zake zote katika kuzipanga Hadith kimpangilio mnavyouona katika kitabu hiki pia.

 

Mwandishi wa Al-Mizaan fi Tafsir al-Qur'an yaani As-Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai kuhusu Wasa’il as-Shi’ah anaandika :

Kwa hakika kitendo hicho ni kipeo cha hali ya juu kabisa katika maswala ya Fiq-h na Mafuqahaa na Mujtahidiin wanakitegemea sana. Wao katika kutoa waftwah zao wanakitumia na kukitegemea sana na kitabu hiki ambacho kinawafaidisha na hawana shaka na hawana shaka yoyote kwenye kitabu hiki. Mambo yote ambayo yameisha zungumzwa humu kwa hakika yana mapana yake, kwa hakika kutokana na zama zao hizo mpangilio na utaratibu uliotumika kunasaidia na wenye manufaa sana.  Kwa hakika inatubidi sisi tujali na kutekeleza na kuipa muhimu sana matamshi na maneno matakatifu yaliyozungumzwa na watu watukufu kabisa.

 

Sheikh Hurri Aamili alikuwa ni mwandishi yaani ni mtu mwenye habari, na ni mmoja wa waandishi wa vitabu vinne vya kutegemewa kabisa ambavyo vimeisha kwisha kuelezwa hapo nyuma.  Kwa hakika katika zama zetu hizi kuna pengo kubwa sana la ma’ulamaa kama hao ambalo haliwezi kuzibwa kwa hakika athari ya mapengo hayo yanaonekana katika zama zetu na zile zitakazo kuja kwa sababu mapango yamebakia wazi yanaongezeka na maulamaa wengi wametumia kazi ya Bwana Hurri ‘Aamili kama vile Said Abul Qasim Al-Khui ametumia katika Mu’jamur Rijaal na kumtaja kuwa Bwana Sheikh ‘Aamili alikuwa ni mtu wa maswala ya habari pia.  Hivyo hivyo hali kadhalika Sheikh ‘Aamili alizaliwa katika Jabal ‘Aamil kijiji kimoja kijulikanacho kama Mashgharah (Mwezi wa Rajab mwaka 1033 Hijriyyah) na amefariki na amezikwa Mashhad al-Muqaddas katika mwaka 1104 Hijriyyah.

 

Katika sehemu mwisho ya Wasa’il as-Shi’ah ‘Aamili anaandika kuhusu Alama Majlisi a.r. anaandika kuwa: Yeye ni mwisho katika wale waliokuwa wamenipa idhini, nami nilimpa idhini.

 

Mbali na kitabu cha Wasa’il as-Shi’ah, Sheikh ‘Aamili ameandika vitabu vingine ishirini na sita ambavyo vingi vyake vina Juzuu mbalimbali. Kwa hakika mwanga wake huo mkubwa alioutoa kwa ajili ya madhehebu ya Ahlul Bayt a.s. ni mkubwa sana na wenye kustahili kusifiwa na kupewa heshima zote.

 

Tunaomba Allah swt awajaalie kila la heri Ma’ulamaa wakubwa waliojitolea mhanga kuinusuru dini hii tukufu ya Islam.

 

Kwa hakika kitabu hiki cha sadaka  ni sehemu moja tu ndogo au tunaweza kusema ni sura mojawapo katika Juzuu ishirini za Wasa’il as-Shi’ah katika sura inayoitwa Kitabu cha Zakah. Mkiangalia kazi yake yote hiyo kwa hakika hamtakuwa na la kusema. Na surah hii inaitwa Kitabu cha Sadaka  ambacho kinazunguzia mambo juu ya sadaka na humo zipo surah hamsini na nne sasa mfikirie kama yeye kwa swala moja dogo hili amechukua kwa hakika uzito mkubwa kama huo je mfikirie kazi yote hiyo itakuwa imechukua uzito gani?

 

Kwa hiyo ndugu msomaji sababu ya kupenda kuchukua maudhui haya ni mambo mawili,

  • Kwanza kabisa ni kuweza kuwadhihirishia  na kuwaonyesha mchango wa Ma’ulamaa wa Kishi’ah katika ilimu hii ya Hadith na
  • vile vile kuteketeza uvumi kuwa Mashi’ah wanaikubali Qur'an Tukufu lakini hawakubali na hawana Hadith zozote wao na kwa hakika hilo ndilo litakalo kuwa jibu letu.

 

Kwa hakika ukiweza kuangalia utaona kuwa ilimu ya Hadith imehifadhiwa na kuendelezwa na hii Madrssah ya Ahlul Bayt a.s. ambapo kwa wengine jambo hili halikupewa uzito wala tahadhari ya aina yoyote ile. Leo ukiangalia katika ulimwengu wa Masunni utaona kuwa vitabu vyao vilivyopo wamshukuru ‘Umar ibn ‘Abdul Aziz na kama akiwa kiongozi mtawala asingetia msisitizo katika swala hili basi hawa watu ambao wamejitenga na Ahlul Bayt a.s. wangekuwa hawana chochote, hazina yao ingekuwa tupu kabisa.

 

Vile vile mtarjumu wa kitabu hiki ambaye yeye ametokea ‘Umma huu na amesomea, hivyo ameona afadhali kuwa kazi aifanye ili aweze kuleta mbele ya umma huu na kwa ajili ya manufaa ya wana-‘umma huo kwa hivyo itasaidia pia kumtaarufisha mwandishi wa kitabu hiki.

 

Sote kwa pamoja tunaomba kwa Allah swt nguvu zetu na jitihada zetu hizi azikubalie. Iwapo kumetokezea au kumebakia kasoro zozote katika kutarjumu basi tunamwomba Allah swt atusamehe na ninawaomba Wanazuoni na wenye Ilimu wajaribu kusaidia turekebishe kwa sababu katika kukitarjumu kitabu hiki hapakuwapo na matayarisho kamili kuanzia awali.

 

Na kazi hii imefanywa kwa nia njema kwa matarajio kuwa itatumika kwa nia njema na itafaa kutukupeleka mahala pema. Inshallah.

 

Naomba kazi yangu hii niiweke mbele kwa idhini ya Allah swt.

 

Na kuiweka mbele ya Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s. iwe ni kama zawadi kwake.

 


UTAMBULISHO WA MA’SUMIIN A.S.

KATIKA AHADITH: KUNIYYAT  NA  ALQAAB

 

Mara nyingi tunaposoma vitabu vya riwaya tunapata majina mengine yaliyotofauti na majina ya asili.  Hivyo tunaona katika Ahadith kuwa Ma’asumiin a.s. wanatambulishwa kwa majina yanayoitwa Kuniyyat au Iaqab, kwa mfano: Qala Abul Hasan ( yaani amesema Abul Hasan ) au Qala Abu ‘Abdillah (yaani amesema  Abu ‘Abdillah) n.k. na hapo ndipo tunakuwa hatuelewi ni Ma’sum a.s. yupi ambaye amesema hayo.

 

Waarabu wanayo desturi ya kuwaita wazee wao si kwa majina yao bali kwa majina mengineyo yaan Kuniyyat au Alqaab.  Hivyo inatubidi tupate ufafanuzi zaidi kuhusu majina hayo yanayotumiwa kwa ajili ya Ma’sumiin a.s zaidi ya mara moja.  Na hivyo Maulamaa wetu wametuelewesha ilivyo sahihi kabisa.

 

Wakati wa kujaribu kufafanua juu ya Laqab au Kuniyyat kunatiliwa maanani kuhusu maneno na maana ya Hadith, zama za kusemwa na habari za wale wanaoziripoti, ndipo hapo panapoweza kutambuliwa kwa Alqaab au Kuniyyat katika Hadith hiyo kunatambulishwa Ma’sumiin a.s. yupi.

 

Hivyo kuelezea hayo na mengineyo, maelezo yafuatayo yatasaidia kutoa mwanga katika swala hili kwa ujumla:

 

1.  ABUL QASIM Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Mtume Muhammad s.a.w.w. na Imam al-Mahdi a.s. Iwapo  kutaripotiwa riwaya kuwa Abul Qasim tu, basi ijulikane kuwa ni Imam al-Mahdi a.f

 

2.  ABU MUHAMMAD  Zipo Hadith chache mno zinazojulikana kuwa Imam Hasan a.s. Hata hivyo hiyo ndiyo Kuniyyat yake.

 

3.  ABU ‘ABDILLAH  Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam Hussein a.s na vile vile inatumika kwa ajili ya Imam Ja’afer as-Sadiq a.s.

 

4.  ABUL HASAN

Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. , Imam Musa ibn Ja’afer a.s., Imam Ali ibn Musa al-Ridha a.s. na Imam Ali an-Naqi a.s. Iwapo kutakuwapo na Abul Hasan tu katika riwaya, basi kutatambuliwa Imam Musa ibn Ja’afer a.s. Na iwapo kutaandikwa Abul Hasan Thani (Abul Hasn wa pili) basi kutakuwa kumefanywa ishara ka Imam Ali ar-Ridha a.s. na pale panapoandikwa Abul Hasan Thalith (Abul Hasan wa tatu) basi tujue kuwa kunamaanishwa Imam Ali an-Naqi a.s.

 

5.  ABU MUHAMMAD

Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam  Hasan a.s., Imam Zaynul Aabediin a.s na Imam Hasan al-‘Askari a.s. lakini iwapo kutaandikwa riwaya kwa Abu Muhammad tu tutatambua kuwa riwaya hiyo ni kutoka Imam Hasan al-‘Askari kwa sababu riwaya za Imam Zaynul Aabediin a.s. zinatajwa kwa jina lake tu, bali zipo riwaya chache mno tu kwa Kuniyyat yake.

 

6.  ABU IBRAHIM  Katika Hadith Kuniyyat hii inatumika hasa kwa ajili ya Imam Musa ibn Ja’afer a.s.

 

7.  ABU IS-HAQ Kuniyyat hii inatumika kwa kumtambulisha Imam Ja’afer as-Sadiq a.s.

 

8.  ABU JA’AFER

Kuniyyat hii inatumika kwa ajili ya Imam Muhammad al-Baquir a.s. na Imam Muhammad Taqi a.s

 

Lakini iwapo kutakuwapo na Abu Ja’afer tu au Abu Ja’afer Awwal, (Abu Ja'afer wa kwanza) basi ijulikane kunamaanishwa kwa Imam Muhhammad al-Baquir a.s.

 

Na iwapo kutaandikwa Abu Ja'afer Thani (Abu Ja'afer wa pili) basi kutambuliwe kuwa ni Imam Jawad a.s.

 

Kwa mara chache mno Abul Hasan inatumika kwa ajili ya Imam Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. lakini mahala pengi mno kunatumika Kuniyyat yake mahsusi ya Abul Hassanain.

 


ALQAAB.

Wakati pale utakapoona riwaya zinanakiliwa kutoka kwa ‘Aalim, Sheikh Faqih au ‘Abdi Salih, basi mutambue kuwa kunamaanishwa kwa   

Al Imam Musa al-Kadhim a.s.

 

Vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anajulikana kwa alqaab zifuatazo: Sheikh , Abu ‘Abdillah, Faqih na ‘Aalim.

 

‘Allamah Majlisi a.r. anasema kuwa mahala pengi mno katika riwaya kunapotajwa Faqih basi kunamaanishwa kwa Imam ‘Ali an-Naqi a.s. na kwa mara chache mno kunatumika Jawallaij kwa ajili ya Imam Hasan al-‘Askari a.s na Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s.

 

Naqi, Mazii, Sahibul ‘Askar na Hajul kunamaanisha Imam Hasna al-‘Askari a.s.

 

Sahib na Sahibuddaar zinatumika makhsusi kwa ajili ya Imam al-Mahdi a.s. Lakini Sahibun Nahiyah inapokuja, basi kwa mara nyingine hutumika kwa ajili ya Imam ‘Ali an-Naqi a.s. au Imam Hasan al-‘Askari a.s. ‘Allamah Majlisi anasema kuwa mara nyingine katika Ahadith hutumika maneno Ghaib, ‘Alil au Gharim basi inatubidi kuelewa Imam al-Mahdi a.s.

 

Iwapo kutakuwapo bi ahadihima (kwa mojawapo) basi itatubidi tuelewe kuwa ni ishara kwa Imam Muammad al-Baquir a.s. au Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.

 

Na iwapo tutakuwa bi ‘Askariyyen, tuelewe kuwa ni Imam Ali an-Naqi a.s. na Imam Hasan al-‘Askari a.s.

 

Vile vile iwapo tutaona bi Kadhimain basi kunamaanishwa Imam Musa al-Kadhim a.s. na Imam Mahammad at-Taqi a.s.

 

Kwa mukhtasari, zipo alqaab nyingi ambazo zinajulikana kimakhsusi kwa ajili ya Ma’sumiin a.s. kama vile Amir al-Muuminiin, Mujtaba Shahid, Zaynul Aabediin, Baquir, Sadiq, Kadhim, Ridha, Jawad, Hadi, ‘Askari, na Sahib uz Zamaan (salaam ziwe juu yao wote).

 


MWENYE KURIPOTI AHADITH AWEJE?

Kwa hakika somo hili ni kubwa na lenye kwenda kwa undani zaidi, lakini kwa ajili ya wasomaji, tunawaleteeni habari hizi kwa kifupi ili kuwafaidisha.

 

Katika lugha ya Kiarabu, mtu anayeripoti riwaya huitwa Rawi na sifa zake zimeelezwa na kubainishwa na Ma’ulamaa walio mabingwa wa ilimu ya Ahadith:

 

1. Rawi lazima awe mtu mwenye akili na fahamu timamu. Riwaya zozote zitakazotolewa katika hali ya  kuwehuka au kurukwa na fahamu, basi hazitathaminika au kukubalika.

 

2. Ni lazima Rawi awe amebaleghe na Mukallaf, yaani shariah za Dini ziwe zimeshakwisha kuwa faradhi juu yake. Hapa inawajumuisha vijana na watoto na wale wote ambao bado hawajabaleghe lakini wanaweza kutofautisha baina ya wema na ubaya. Aina hii ya vijana hao huitwa Mumayyiz na hivyo riwaya zao zinapotimika masharti mengineyo, huweza kukubalika na kusadikika.

 

3. Ni lazima Rawi awe Mwislamu.  Riwaya za mtu asiye Mwislamu haziwezi kuaminiwa au kusadikiwa.

 

4. Rawi lazima awe ni Mwislamu mfuasi wa Madhehebu ya Sh’iah Ithna-Asheria.  Lakini iwapo kutakuwa na riwaya kutokea Mwislamu mfuasi wa Madhehebu mengine, basi kwa uzito wa dalili zinginezo na kufanya uchunguzi iwapo huyo Rawi ni mtu aaminiwaye katika historia.

 

5. Uadilifu wa Rawi pia ni sharti mojawapo, yaani asiwe akifanya madhambi makuu (Kabair Dhamb)[46] na wala asiwe akirudiarudia madhambi madogo madogo (Dhamb-i-Saghirah).

 

   Sheikh Tusi a.r. ametilia mkazo swala hili kwa kuelezea kuwa kuna tofauti katika uadilifu wa Rawi na mtoa ushahidi.  Iwapo Rawi ni fasiki na iwapo itathibitika kuwa yeye katika riwaya yake na habari zake ni mkweli bila ya udanganyifu, basi riwaya yake inaweza kufuatwa.

 

6. Rawi asiwe msahaulivu, bali awe ni mtu mwenye kukumbuka vyema na udhibiti wake, (yaani haimaanishi kuwa Rawi asiwe akisahau kama mtu wa kawaida) yaani Rawi anapotaka kuelezea riwaya au Hadith, basi asiwe na mushkeli wa kuikumbuka.

 


AINA ZA AHADITH

Sayyid Ibn Taus a.r. (amefariki 673 Hijriyyah) na ‘Allamah Hilli a.r. (amefariki 726 Hijriyyah) kwa juhudi zao, wao wamefanikiwa kutuletea kanuni nne kuu zijulikanazo usul-i-‘arbi’ah ambazo ni kama zifuatazo:

 

1. HADITH SAHIH

    Rawi wote lazima wawe waaminifu na Shia Ithna-Asheri na riwaya hizo ziwe zikifika hadi kwa Ma’sumiin a.s.

 

2. HADITH HASAN

   Riwaya ambazo Rawi wake ni Mashiah na ambapo hapakufanywa uchunguzi wowote juu ya uadilifu wao.

   Hadith kama hizo zinajulikana kama hasan kwa sababu Rawi amepokelewa kwa misingi ya husn-dhan yaani kwa dhana njema.

 

3. MUTAWATH-THAQ

   Yaani Rawi wote wawe wakiaminiwa lakini miongoni mwao si wote ambao ni Mashiah.

 

4. DHAIF

   Ni riwaya zile ambazo hazina sifa hata mojawapo za hapo juu.

 

   Tanbih lipo jambo moja la kuzingatia, kuwa Ma’ulamaa wanakubaliana na Hadith zilizo Sahih, Hasan na Muwath-thiq.  Ama kuhusu Hadith zilizo dhaif ni kwamba iwapo atayamkinika kuwa Rawi hao si watu wa kutegemewa lakini maelezo na maana yake ni sawa na maana ile ya Ma’sumiin a.s. na katika sura hii, itaweza kukubalika, na wakati Ma’ulamaa wanaozisimulia basi nia yao huwa juu ya Hadith, bali huwa ni kutoa ushahidi tu.


HADITH ZILIZOGHUSHIWA

Kwa mujibu wa kanuni hizi nne, mmefahamu kuwa Hadith inapoangukia kuwa dhaifu haimaanishi kuwa ni Hadith ya uongo, yenye mfululizo dhaifu, na kwa dalili zinginezo na kwa nyenzo zinginezo inaweza kuthibitika kuwa Hadith hiyo inaweza kukubalika, Lakini inapokuwa imekosewa kabisa basi huitwa Kidhb (uongo) au Iftira’ (tuhuma).  Yaani utaratibu uliotumiwa wa kuwanasibisha Ma’sumiin a.s. haupo wenye ukweli, bali tunaweza kusema kuwa ni tuhuma.  Hadith hizo ni uzushi mtupu.  Katika historia ya ilimu ya Hadith, utaratibu huu mmoja ni tatizo kubwa mno kuling’amua iwapo Hadith hii ni uzushi au la.

 

Sayyid Murtadha ‘Alamal Hudaa a.r. anasema:

“Zipo baadhi ya sehemu za Hadith katika Mashia na Waislamu wote kwa ujumla ambazo zimejazwa makosa na uzushi ambazo zinatufanya kuzichukulia kuwa ni Hadith za uongo.  Katika Hadith hizo kuna mambo fulanifulani ambazo kwa hakika si rahisi kukubalika kiakili na ni pingamizi mtupu.  Kwa mfano imani juu ya jabr (ushurutisho) yaani mwanadamu ameshurutishwa na Allah swt katika matendo ya madhambi na uasi, au siku ya Qiyamah Allah swt ataonekana n.k. na hivyo inamaanisha kuwa kunahitajika uchuguzi na utafiti mkubwa katika kuthibitisha ukweli wa usahihi wa Hadith kama hizo.”

 

Imam Ali a.s. amesema: “Mtume Muhammad s.a.w.w. alisema

“Enyi watu, kumekithiri mno kuninasibishia mambo ya uzushi, hivyo mutambue kuwa mtu yeyote kwa makusudi ataninasabisha na uongo au uzushi wowote, basi hakuna mahala pale pengine isipokuwa ni Jahannam tu.”

 

Katika zama hizi ni lazima kufahamu ‘Ilmul Hadith na Rijal yaani kujua habari za wale wenye kuleta riwaya.  Kazi hii ni ya wale mabingwa katika fani hii na wala si ya wale wenye ilimu kidogo ambao wamejua Kiajemi na Kiarabu kidogo hivyo wakaanza kuwapotosha watu.

 

Sasa tuangalie ni kwa sababu gani kumetokezea haja ya kutaka kuzichuja Ahadith na tuwaangalie watu mbalimbali ambao wamefanya juhudi za kuingiza uongo na uzushi na tuhuma katika Ahadith.

(1).  Baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  kulizuka mgogoro kuhusu ukhalifa ambapo kulitokezea makundi mawili.  Kundi moja likidai kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa amekwisha elezea ni nani atakaye kuwa Khalifa baada yake na kundi la pili likaanza kuzua Hadith kuwa swala hilo liachiwe ‘ummah wa Kiislamu kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema kuwa ukhalifa baada yake hautatokana na Bani Hashim (uzushi mtupu).

 

(2). Wakati Uthman alipouawa, basi Ma’uwiya bin abi Sufiyan kwa hila zake alitupa tuhuma za mauaji yalilengwa kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. Hapo kuliibuka Hadith za kuzuliwa katika kuwatukuza Bani Umayyah, umadhulumu wa Uthman na hukumu juu ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.  katika mauaji ya Uthman.  Si hayo tu, bali Hadith zile zilizokuwa zikielezea fadhila za Imam Ali a.s. pia zilianza kubadilishwa na kupotoshwa.  Mfano, ipo ayah ya Qur’an tukufu: ‘wa minanaasi manyashrii nafsahubtighaa mardhatillah’ Aya hii inatoa shuhuda ya tukio lililotokea katika usiku wa Hijrah ambapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s.  alijitolea nafsi yake kwa ajili ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Kwa amri za Mu’awiyah, Hadith hii ikageuzwa kuwa imeteremka kwa ajili ya Ibn Muljim kwa sababu yeye alikuwa ameiweka nafsi yake hatarini katika kumwua Imam Ali a.s.

 

(3).  Makhariji walizua Hadith chungumzima kuhusu akida zao na Waislamu kwa ujumla pia walizizua  Hadith nyingi mno katika upinzani wao

(4).   Ma’ulamaa wa Kiislamu walianza kuzua na kutumia hizo Ahadith katika kuzieleza na kuziendeleza fikra, nadhiri na akida zao.  Mu’tazila, Tasawwuf, Gulat na Ash-Ari na wengineo wote wakaanza kuzua Hadith katika kueneza imani zao.  Iwapo utabahatika kukisoma kitabu kiitwacho Ihyaul Ulumiddiin basi ndipo utakapokuja kujua hali halisi ya uovu huu wa kuzua Ahadith za kiuongo dhidi ya Ma’sumiin a.s. ambazo kwa hakika hazikubaliki kuwa zimesemwa nao.  Kwa kutoa mfano, tunawaleteeni chache ili muweze kuziangalia:

(a).   Ahmad bin Mansur anasema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Baina mikono miwili ya Allah swt kuna maandiko fulani ambamo kuna majina ya wale watu ambao wanaitikadi kuhusu kuwapo kwa uso na kuonekana kwa Allah swt siku ya Qiyama.  Na Malaika wanaona fakhari kwa majina hayo!

(b).  Mamun bin Ahmad Harwi anamnakili Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akisema:

“Kuna mtu mmoja katika ‘Ummah wangu ambaye ni hatari hata kuliko Shaytani, na jina lake ni Muhammad bin Idris (yaani Imam Sahfi’i) na vile vile kuna mtu mwingine ambaye yuko sawa na nuru kwa ‘Ummah wangu, na jina lake ni Abu Hanifa.”

 

Tanbii: Mwandishi wa Lisanul Mizaan anaandika kuwa sababu kubwa ya kuizua Hadith hii ni kwamba huko Khurasan, wafuasi wa Imam Shafi’I walikuwa wengi.

(c). Ahmad bin Nasr anasema kuwa siku moja alimwota Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika ndoto akimwambia;

“Itakuwa wema kwako kumtii Shafi’i kwani anatokana nami na Allah swt yu radhi naye”

(d). Kwa hakika jambo lakusikitisha mno ni kwamba hawa wataalamu wa kuzua (wazushi) ni watu ambao wameilimika vyema katika masomo ya Qur’an na Hadith.  Mafunzo ya Qur’an hayakuwa yenye maana kwao bali wametilia mkazo masilahi na ulafi wa dunia hii.

 

Ayatullah al-Khui r.a. anaandika katika kitabu chake Al-Bayan fi tafsiril Qur’an, Uk. 28 kuwa kuna rundo kubwa kabisa la riwaya za uongo na zilizozuliwa, ambamo hawa wazushi wamechukua tahadhari kuwa kusije kukapunguzwa fadhila za Qur’an, basi wamezua Hadith zao binafsi; na wamezirembesha kwa fadhila mbalimbali kiasi kwamba zinapopimwa kwa kauli za Allah swt zinajulikana kuwa ni za uongo mtupu. Mfano Abu Ismah Faraj bin Abi Maryam al-Maruzi, Muhammad bin Akasha al-Kirmani, Ahmad bin Abdillah Juibarri na wengineo wengi.

 

Wakati mtu mmoja alipomwuliza Abu Ismah kuwa amezitoa wapi Hadith chungu mzima kutokea kwa Ikramah na Ibn ‘Abbas kuhusu fadhila za Sura moja moja za Qur’an tukufu ?  Alianza kusema: “Mimi niliona kuwa watu wameanza kuipa mgongo hiyo Qur’an na badala yake wanajishughulisha mno na fiqhi ya Abu Hanifa, watu wamejishughulisha kuisoma Maghazi  ya Muhammad bin Is-Haq, basi mimi nimezusha Hadith hizo juu ya Qur’an kwa kutaka furaha ya Allah swt ………….!

(e).  Wakati kulikuwapo utawala wa Bani ‘Abbas, basi Ma’ulamaa wenye tamaa ya dunia walizizusha Ahadith nyingi mno katika kuelezea fadhila za watawala hao.  Katika Tarikhul Khulafa anaandika as-Sayyuti:

“Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema kuwa yeye alipoona kuwa Bani Marwan wanachezea Mimbar yangu, basi hapo mimi nilisikitishwa mno.  Na hapo baadaye nikaona Bani ‘Abbas pia wanachezea, na kwa hayo mimi nilifurahishwa  mno.”

 

Abu Hurairah ananakiliwa riwaya moja kuwa siku moja Mtume Muhammad s.a.w.w. alitoka nje, na hapo alikutana na Baba mkubwa ‘Abbas, na alimwambia: “Ewe Abul Fadhl ! Je nikupe habari njema ?

 

‘Abbas alisema:

“Naam, Ewe Mtume wa Allah swt !” Ndipo Mtume Muhammad s.a.w.w. aliposema: “Allah swt ameitengeneza swala hili (yaani Dini hii ya Islam) kwangu na kuishia kwa ‘Ummah wangu.” Na akaendelea kusema: “Wakati kizazi chako kitakapoishi Iraq, watakuwa na usukani huu wa Islam kwa muda mpaka atakapodhihiri Mtume Isa a.s. na kumkabidhi.”

 

Tanbihi: Ni jambo la kushangaza mno kuwa huyu huyu as-Suyuti ameandika kitabu kimoja juu ya masuala ya uzushi kiitwacho Al-Lulil mansukh (Lulu bandia) na amewatahadharisha Waislamu kujitahadharisha na Hadith kama hizo za uzushi, pamoja na hayo yeye mwenyewe amenakili riwaya nyingi mno zilizo bandia na Ahadith zilizo zuliwa na hivyo ameshiriki kikamilifu katika kuifikishia Islam jeraha kubwa.

 

(f).  Baadhi ya makafiri na maadui wa Islamu wamekuwa wakiishi miongoni mwa Waislamu na kujihusisha katka harakati za kueneza sumu hii miongoni mwa Waislamu kwa hila na njama mbalimbali.  Wao ili kutaka kutimiza mikakati yao hiyo ya kueneza upotofu, wamekuwa wakijishughulisha na uzushi wa Ahadith za Mtume Muhammad s.a.w.w. na Ma’sumiin a.s. na walikuwa wakizileta mbele ya watu. Ibn Abil Awjah amekiri mwenyewe kuwa yeye ameingiza kiasi cha Ahadith zipatazo elfu nne zilizozuliwa miongoni mwa Ahadith zilizo za kweli. ( ! )

 

(g).  Katika kipindi cha mwanzo cha Islam, watu walikuwa na shauku kubwa ya kusikiliza visa na masimulizi mbalimbali na katika hali hii kuliibuka wasimulizi wengi wa masimulizi kama hayo na hivyo wao walikuwa wakifanya kila jitihada za kukusanya habari na porojo za kila aina na walikuwa wakiongezea chumvi na pilipili ili kwamba mazungumzo yao yalete ladha nzuri na kuwavutia watu.  Matokeo yakawa ni kwamba Mayahudi walikuwa wamezusha visa na hadithi nyingi kuhusu mitume yao, hivyo mazushi hayo yakapata soko kubwa miongoni mwa Waislamu, na rundo kubwa hili linajulikana kwa jina la Israiliyyaat [47] Hadith zilizozushwa juu ya Mitume a.s. inapatikana katika Tarikhul Ambiya’ na hususan katika tafisiri za Ayah ambazo zinazungumzia habari za Mitume a.s.

 

Ibn Jawzi anaandika kuwa Imam Ahmad bin Hambal na Yahya bin Mu’in walikuwa wakisali Msikitini na wasimuliaji wakaja wakatandika mikeka yao tayari kuanza masimulizi yao mbele ya halaiki kubwa ya mashabeki wao.

 

Wasimulizi wakiendelea na masimulizi yao, wakasema: “Mimi binafsi nimemsikia Ahmad bin Hambal na Yahya bin Mu’in kuwa wao wamewasikia Rawi fulani fulani kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: “Mtu yeyote atakaye sema La ilaha Illallaah basi Allah swt atamwumba ndege mmoja ambaye mdomo wake utakuwa wa dhahabu na macho ya marjaan………”  Hivyo wao walizielezea habari za ndege huyo, na kama tukianza kuziandika tutaandika kurasa ishirini zinginezo.

 

Kwa hakika watu walipoyasikia haya walianza kuyumba na kwa kutoa shukurani zao walianza kuwatupia mapesa hao wasimulizi, nao walibakia kimya kwa muda zaidi kidogo ili waendelee kupata zawadi zaidi, na hapo ndipo Yahya bin Mu’in alipojitokeza na kumwita aje mbele yake.  Msimulizi alikuja mbio mbio hapo mbele kwa kutarajia kupata zawadi nono, ndipo Yahya alipomwuliza: “Je habari zote hizi zisizo na miguu umeyatoa wapi?” Akajibu: “Nimemsikia Yahya bin Mu’in na Ahmad bin Hambal.”

 

Yahya na Ahmad bin Hambal walishikwa na bumbuwazi na walibakia wakitazamana, na hapo ndipo Yahya kwa hasira alimgeukia msimulizi na kumwambia: “Je hauoni aibu? Wewe umethubutuje kuzusha uongo dhidi yetu ilhali tukiwa mbele yako ? Jina langu ni Yahya bin Mu’in na huyu ndiye Ahmad bin Hambal.”

 

Yule msimulizi alianza kusema: “Mimi daima nimekuwa nikisikia kuwa Yahya bin Mu’in ni mtu mpumbavu na mjinga kabisa, na kwa hakika nimepata uthibitisho huo leo hii, kwa hakika ni ajabu kubwa !.  Je dunia hii nzima ina Yahya bin Mu’in na Ahmad bin Hambal nyie wawili tu na wala haina wengine?  Kwa kusema ukweli mimi nimewanakili riwaya mbalimbali Yahya bin Mu’in sabini na Ahmad bin Hanbal sabini.” Kwa kusema hayo msimulizi alijiondokea zake.

 

(h).  Kulizuliwa Ahadith nyingi mno katika kutukuza makabila na Miji ya Kiislamu. Tazameni mfano mmoja.  Imeripotiwa kuwa al-Imam ar-Ridha a.s. amesema kuwa Mji mtukufu wa Qum umeitwa hivyo kwa sababu hapo ndipo Safina ya Mtume Nuh a.s. iliposimama baada ya kuisha kwa tufani.  (Katika lugha ya Kiarabu neno Qum linamaanisha kusimama).

 

(i).   Katika zama za Makhalifa watu walikuwa wakijishughulisha mno katika kuzusha Hadith za uongo au kuzigeuza maana ili waweze kupata zawadi, hongo au kutukuzwa miongoni mwa watu.  Katika zama za Mahdi ‘Abbasi ambaye alikuwa khalifa wa Bani ‘Abbas, aliijiwa na mtu mmoja aitwaye Ghiyas Bin Ibrahim ambaye aliwakuta njiwa wengi mno katika kasri ya khalifa, na kwa hayo alisema: “Ipo riwaya kutokea Mtume Muhammad s.a.w.w. kuwa imeruhusiwa mashindano matatu tu yaani ngamia, farasi na njiwa.”

 

Kwa hayo, khalifa alimpa zawadi na wakati alipokuwa akiondoka, khalifa alimwambia:

“Mimi nashuhudia kuwa huyu aliyetupa mgongo amemnasibishia Mtume Muhammad s.a.w.w. uongo.”

 

 


SIFA ZA KUZITAMBUA HADITH

Ili kuweza kuzitambua ni Hadith za aina gani zilizo za uongo, Ma’ulamaa wetu wametupatia dalili ambazo zitakazotujulisha usahihi na ukweli wa Hadith hizo na masharti ni kwamba mtu yeyote asijitumbukize katka kuzieneza na kuzisherehesha Hadith hadi hapo atakapoweza kuthibitisha kuwa zinastahili hivyo.  Hapa tunawaleteeni kwa mukhtasari:

 

(1). Habari zilizoelezwa katika Hadith zisiwe zikipingana na Ayah za Qur’an tukufu, yaani zisipingane na maamrisho ya Allah swt.  Angalieni kuwa mara nyingi ‘Aam, khaas, mutlaq, muqayyad – kwa kutokujua mambo haya watu wanafikia uamuzi wa kusema kuwa Hadith fulani inakwenda kinyume na Ahadith, kunaleta hatari kubwa ya kupotosha maana sahihi ya Hadith.

 

(2). Hadith kamwe isiwe kinyume na akili bali iwe kwa mujibu wa akili.

 

(3). Iwapo Hadith itakuwa ni salama kwa Dini na Madhehebu, basi ipokelewe.

 

(4). Kwa kuitambua Hadith mambo yafuatayo yanatosha:

(a). Ujue lugha ya Kiarabu na kanuni zake kwa ukamilifu,

(b). Zaidi ya hayo inabidi Lisan-i-Suduur yaani kujua maarifa na ubalagha wa lugha ya Ma’sumiin a.s.

(c).Inabidi kuwa mjuzi wa historia ya Kiislamu na sirah za Ma’sumiin a.s.

(d). Ni lazima ajue Madhehebu na mwanzo wao na kuzijua itikadi zao kwa vyema.

(e). Itabidi mtu huyo awe amejiepusha na ta’assub yaani chuki za aina yoyote ile kwani hapo ndipo hapo atakapoweza kushughulikia bila ya upendeleo au ushawishi wa aina yoyote ile.

                                                           

 

 


ZAKA NA SADAKA HUONGEZA NEEMA

 

Faida kuu mojawapo ya kutoa Zaka ni kuongezeka kwa neema na baraka ya mali yetu iwapo itatolewa kwa kuzingatia kanuni na ustaarabu wa kutoa hivyo, na ni kinyume na mawazo na mipango ya ki-Shaytani, kwani mabakhili hufikiria daima kuwa kwa kutoa mali yao kwa ajili ya misaada na Sadaka na Zaka, basi mali yao hupungua na hivyo wanaweza kuwa masikini na kwa hakika hayo ndiyo mawazo na upotofu wa Shaytani.

 

Amesema Allah swt katika Quran: Surah al –Baqarah, Ayah 28 : “Allah swt huongezea katika Sadaka” yaani huongezea baraka humu duniani na vile vile kutakuwapo na malipo mengine huko Aakhera

Na amesema Allah swt katika Quran: Surah al – Saba,34, Ayah 39 :

‘Chochote kile mtakachokitoa (katika njia yake), basi Atawalipeni (humu humu duniani) malipo yake, Naye ni Mbora wa wanao ruzuku.’

 

Amesema Allah swt katika Quran: Surah al –Rum, 30,  Ayah 39 :

‘Na mnachokitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Allah swt . Lakini mnachokitoa kwa Zaka kwa kutaka radhi ya Allah swt, basi hao ndio watakaozidishiwa.’

 

Katika Ayah hizo, tumeona kuwa kuongezeka zaidi mno na vile vile Baraka pia itakuwamo, vyote kwa pamoja. Katika kusisitiza hayo, zipo riwayah nyingi mno.

 

Amesema Bi. Fatimah az-Zahra a.s. bintie Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika hotuba aliyoitoa kuzungumzia Fadak katika Bihar al-Anwaar, J.8, Uk 109 :

 “Kwa ajili ya kujitakasa na dhambi la Shirk, Allah swt ametufaradhishia kuikamilisha imani yetu ( yaani mtu yeyote anayetaka kujitakasisha na unajisi basi inambidi kuleta imani kwa moyo wake kamilifu), na Sala inamwepusha na magonjwa ya kiburi na kujifakharisha, na Zaka inamwepusha mtu kwa magonjwa ya ubahili ili mwanadamu awe mkarimu na mpenda kutoa kwa ajili ya mema ili atakasike) na hii pia ndiyo sababu kuu katika kujiongezea riziki .”

 

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. ameripotiwa akisema katika Al-Kafi:

“Yeyote yule anayetumia kutoka mali yake katika njia ya kheri, basi Allah swt anamlipa mema humu duniani na kumwongezea katika malipo yake.”

 

Vile vile ameripotiwa akisema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s.  katika Wasa’il as-Shiah : Mlango Sadaka, Hadith 19, J.6, Uk. 259 :

“Tafuteni riziki yenu kwa kutoa Sadaka.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa katika Kitab ‘Uddatud-Da’i kuwa  alimwuliza mtoto wake :”Je nyumbani kuna kiasi gani kwa ajili ya matumizi ?”

 

Naye alimjibu : “Zipo Dinar arobaini tu.” 

Imam a.s. alimwambia “Dinar zote hizo zigawe Sadaka.”

 

Kwa hayo mtoto wake alimwambia Imam a.s. “Ewe Baba ! Mbali na Dinar hizi arobaini, hatutabakia na akiba yoyote.”

 

Imam a.s. alimwambia : “Nakuambia kuwa zitoe Dinar zote Sadaka kwani ni Allah swt tu ndiye atakayetuongezea kwa hayo. Je wewe hauelwei kuwa kila kitu kina ufunguo wake ? Na ufunguo wa riziki ni Sadaka ( kutolea mema ).”

 

Kwa hayo, mtoto wake aliyekuwa akiitwa Muhammad, alizitoa Sadaka Dinar hizo na hazikupita siku kumi, Imam a.s. alitumiwa Dinar elfu nne. Hapo Imam a.s. alimwambia mwanae : “Ewe Mwanangu ! Sisi tulitoa Dinar arobaini tu na Allah swt ametupa Dinar elfu nne badala yake.”

 

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. amesema katika Nahjul Balagha kuwa :

“Mtu anapokuwa masikini au mwenye shida basi fanyeni biashara pamoja na Allah swt kwa kutoa Sadaka.”

 

Al Imam ‘Ali ar Ridha  a.s. alimwambia mfanyakazi wake : “Je leo umeshagawa chochote katika njia ya Allah swt .”  Mfanyakazi huyo, “La, bado sijagawa.”  Kwa kuyasikia hayo Imam a.s. alimjibu, “ Sasa kama haukufanya hivyo, basi Allah swt atatulipa nini badala ya tendo letu ? Hivyo hatutapata baraka wala neema yoyote kutoka kwa Allah swt . Tukitoa chochote ndipo Allah swt atatulipa kwa wingi badala yake.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameelezea Hadith katika Al-kafi, Kitab ad-Du’a, J. 2, Uk.595  moja kwa kutokea Ayah Fahuwa Yukhlifuhu (yaani chochote kile kinachotolewa katika njia ya Allah swt , basi hulipa malipo yake kwa haraka sana ). Na Hadith yenyewe ni :

“Je utadhaniaje kuwa Allah swt anakiuka ahadi aliyoitoa ?”

 

Basi mwandishi  akajibu : “La ! Sivyo hivyo.”

 

Ndipo Imam a.s. alimwuliza : “Sasa je kwanini wewe haupati malipo yako kwa yale unayoyatoa na kugawa ?”

 

Naye akajibu, “ Kwa hakika mimi sijui sababu zake.”

 

Imam a.s. alimjibu, “Iwapo miongoni mwenu yeyote atakayekuwa akiipata riziki yake kwa njia zilizo halali, na kama ataitumia hata Dirham moja katika njia zilizo halali, basi lazima mtapata malipo yake na kwa wingi zaidi.  Na iwapo mkiona kuwa hamkupata chochote katika malipo yenu basi mutambue kuwa mali hiyo ilichumwa kwa njia zilizo haramu au ilitolewa na kutumiwa katika njia iliyoharamishwa.”

 

Kuhusiana na swala hili zipo Ayah na riwayah nyingi mno, lakini tunatua hapa. Marehemu Nouri katika kitabu chake Kalimah at-Tayyibah amezungumzia mengi na kwa mapana na undani zaidi kuhusu kutoa Sadaka katika njia ya Allah swt  na amedondoa hekaya takriban arobaini ambamo ‘Alim Rabbani Akhwand Mullah Fath ‘Ali amenakili kisa cha jamaa yake ategemewae ambaye amesema,

“Mwaka mmoja ambapo hali ya ughali ilikuwa imekithiri, nilikuwa na kipande kimoja cha ardhi ambapo nilikuwa nimepanda Shayiri na ikatokea kuwa shamba langu hilo likawa na mavuno mengi mno kuliko mashamba mengineyo. Kwa kuwa hali ilikuwa ni mbaya kwa watu wengineo, hivyo tamaa ya kujitafutia faida zaidi katika mazingara hayo niliyatoa kutoka nafsi yangu. Hivyo mimi nilikwenda moja kwa moja Msikitini na kutangaza kuwa mazao yote yaliyo shambani mwangu nimeyaacha kwa masharti kwamba yeyote mwenye shida tu ndiye aende kuchukua na masikini na mafukara waende kuchukua kwa ajili ya chakula cha familia zao. Wote wachukue kiasi wanachokihitaji. Hivyo masikini na mafukara na wenye shida walikuwa wakichukua mavuno kutoka shambani mwangu huku wakisubiri mavuno yao kukomaa. Kwa hakika nafsi yangu ilikuwa imetulia vyema kabisa kwani sikuwa na wasiwasi kwani nilikuwa nimeshajitenga navyo.

 

Wakulima wadogowadogo wote walipovuna mazao yao, nami nikavuna kutoka mashamba yangu mengineo na nikawaambia wafanyakazi wangu waende katika shamba ambalo nilikuwa nimeligawa kuwasaidia wenye shida wakati huo, wakaangalie kama kumebakia chochote ili waweze kuvuna.

 

Kwa hakika hao walipokwenda shambani humo walikuta shamba zima limejaa Shayiri kupita kiasi na baada ya kuvuna na kusafisha nilikuta kuwa nimepata mavuno mara dufu kuliko mashamba yangu mengineyo. Ingawaje humo watu wote walikuwa wakivuna kwa ajili ya chakula chao na familia zao, ilitakiwa kuwa tupu kumbe Allah swt amerudishia mavuno tena mara dufu.

 

Vile vile sisi tulikuwa tukipanda mwaka mmoja na kuipumzisha ardhi mwaka mmoja, lakini shamba hilo halikuhitaji kupumzishwa wala kuwekewa mbolea na badala yake nimekuwa nikilima na kupanda nafaka kila mwaka na nilikuwa nikipata mavuno mara dufu kila msimu.

 

Mimi kwa hakika nilistaajabishwa mno kuona hayo na nikajiuliza isije hiki kipande cha ardhi kikawa ni kitu kingine na mavuno yanapokuwa tayari, hupata mavuno mengi kabisa kuliko mashamba mengine yangu na ya watu wengineo.

 

Mbali na hayo, Merehemu amenakiliwa kuwa :

‘Yeye alikuwa na shamba moja la mizabibu kandoni mwa barabara na kwa mara ya kwanza kulipozaa zabibu katika matawi yake, alimwammuru mtunza shamba wake kuwa zabibu zote zilizopo kando ya barabara aziache kwa ajili wapitao njia. Hivyo kila mpita njia alichuma na kula zabibu zilizokuwa hapo na wengine hata walichukua pamoja nao. Msimu ulipokwa ukiisha aliwaamuru wafanyakazi wake waende kuangalia kama kulibakia zabibu zilizokuwa zimefichika nyuma ya majani au pembeni. Lakini jambo la kustaajabisha ni kwamba, wafanyakazi waliporudi, walikuwa wamevuna zabibu mara dufu ya mashamba yake mengineyo pamoja na kwamba kila mpita njia alikuwa akichuma zabibu hapo.’

 

Vile vile imenakiliwa kuwa :

‘Kila msimu alipokuwa akivuna ngano na kuzisafisha, alikuwa akizileta nyumbani kwake na hapo ndipo alipokuwa akitoa Zaka yake. Lakini safari moja alipovuna na kusafisha, akiwa akielekea nyumbani kwake aliwaza kuwa inambidi alipe Zaka haraka iwezekanavyo, kwani si vyema kuchelewesha ulipaji wa Zaka. Ni ukweli kwamba ngano ipo tayari na mafukaraa na masikini pia wapo. Hivyo aliwajulisha mara moja mafukaraa na masikini waje kuchukua ngano, na hivyo akapiga mahisabu yake na kuwagawia sehemu yao na hivyo sehemu iliyobakia aliileta nyumbani kwake na kujaza madebe makubwa makubwa na alikuwa akijua ujazo wao. Lakini alikuja kuangalia hapo baadaye akakuta kuwa idadi ya ngano imeongezeka mara dufu pamoja na kwamba alikuwa amepunguza kwa ajili ya kuwagawia mafukaraa na masikini.Na hivyo alikuta idadi ya ngano ipo pale pale kabla ya kutoa Zaka.’

 

Katika kitabu kilichotajwa, Alhaj Mahdi Sultan Abadi amenakili kuwa :

‘Mwaka mmoja mimi nilipovuna mavuno, nilipima uzito wa ngano na nikatoa na kuigawa Zaka yake. Na nafaka hizo zilibakia mahala hapo hapo kwa muda wa mwezi mmoja ambapo wanyama pamoja na mapanya walikuwa wakila humo. Na nilipokuja kurudia kupima uzito wake nikakuta kuwa uzito wa ngano ulikuwa vile vile kama siku ya kwanza yaani kiasi nilichokitoa Zaka na kilicholiwa na wanyama na mapanya hakikupungua hata chembe kidogo.’

 


SADAKA   NA   MISAADA: 

 

WANANYUMBA WANAOSTAHIKI MALIPO

Wanaostahiki malipo ni mke ( wa ndoa ya kudumu ) mtiifu na watoto wake na watoto wa watoto wake na vile inavyoendelea kuteremka chini na ambao wanahitaji msaada, basi ni faradhi. Vile vile baba na mama na babu mzaa baba na mama mzaa mama na vile itakavyoendelea juu na iwapo wanahitaji msaada wake na watu wengineo basi na kwa kiasi cha uwezo wake kama anao na iwapo hatawapa basi atatazamwa miongoni mwa watu kama qata’ rahmi . Na jambo hili limezungumziwa katika makala mengine.

 

1. SADAKA ZILIZO SUNNAH

Zipo aina nyingi za malipo yaliyo Sunnah. Katika Ayah na riwayah nyingi mno kumesisitizwa mno kuwa Sadaka itolewe hususan katika siku ya Ijumaa, Siku ya ‘Arafah, katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani itolewe kwa makhususi ya majirani, majamaa n.k. Vile vile Sadaka ni dawa ya ugonjwa, huondoa balaa, huleta riziki, huzidisha mali na huepusha vifo vya kutisha kama kuungua moto, kuzama maji  na kuwazuia Majinni na kwamba huondoa balaa sabini. Kila utakavyotoa Sadaka zaidi basi matokeo yake pia yatakuwa ni mazuri zaidi. Wala haina kiwango kidogo, kiasi chochote mtu atakachokitoa kitatosha walau hata kama atatoa kokwa moja ya tende basi nayo itatosha !

 

2. ZAWADI

Ni kitu ambacho mtu mmoja anampa mtu mwingine kwa ajili ya kuongezea urafiki ama awe masikini au tajiri. Na iwapo hivyo itakuwa kwa nia ya kutaka furaha ya Allah swt, basi itakuwa ni ‘ibada bora kabisa.

 

Imeripotiwa kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. katika Al-Kafi J.5, Uk. 144  kuwa :

“Iwapo mimi nitapenda kumpatia kitu rafiki yangu basi mimi nitampa zawadi kwani ninaipenda zaidi kuliko Sadaka.”

 

3. UGENI NA UKARIMU

Zipo riwayah nyingi mno kuhusu kuwakarimu wageni na kamba hiyo ndiyo tabia njema ya Mitume a.s. Ipo riwayah moja kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. kwa muda wa siku saba hakupata mgeni nyumbani kwake basi alisema huku akilia :

“Nasikitika mno na ninakhofu kuwa isije Allah swt akaniondolea rehema na baraka zake.”

 

4. HAKI ILIYO MAALUMU NA ISIYO MAALUM

Inatubidi sisi tuwe tumepanga viwango maalumu vya kila siku au kila wiki au kila mwezi katika mali zetu kwa ajili ya wale wenye shida na kwa ajili ya majamaa zetu ili kukidhi mahitaji yao.

 

Amesema Allah swt katika Quran: Surah al- Ma’arij, 70  , Ayah 24 – 25 :

Na ambao katika mali yao iko haki maalumu.

Na mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba…

 

Al Imam Musa bin Ja’afer a.s. amepokelewa riwayah kuwa  :

“Katika ukoo wa Bani Israil kulikuwa na mtu mwema ambaye alikuwa na mke aliye mwema pia. Siku moja aliota ndoto ambamo aliambiwa kuwa Allah swt amempangia kiasi fulani cha umri wake ambapo nusu ya umri huo utapita katika raha na mustarehe wakati nusu ya umri uliobakia utapita katika shida na dhiki na umasikini.

 

Hivyo Allah swt amekupa fursa wewe kuchagua iwapo utapenda kupitisha umri wako wa nusu ya awali ya raha na mustarehe na baadaye dhiki na umasikini ? Hivyo chagua mojawapo. Kwa hayo mtu huyo alijibu kuwa : ‘Mimi ninaye mke wangu aliye mwema na hushirikiana naye katika maswala yote, hivyo nitapenda kupewa muda wa kuweza kuongea naye kabla sijatoa uamuzi wa chaguo langu.’

 

Mke wake alimshauri mumewe kuukubalia umri ule wenye neema uwe ndio wa kuanzia kwani: ‘Inawezekana Allah swt anataka kututeremshia neema na baraka zake hivyo tukaongoka.’

 

Hivyo usiku uliofuatia, bwana huyo aliulizwa jibu alilolifikia katika uamuzi wake. Naye akajibu : ‘Mimi ninataka kuupitisha nusu ya umri wangu katika neema, raha na mustarehe.’ Kwa hayo akajibiwa kuwa hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa mujibu wa chaguo lake.

 

 Kuanzia hapo yeye alijaaliwa kila aina ya raha na akawa tajiri mkubwa mwenye mali na milki nyingi.

 

Katika kutajirika huku, mke wake akamwambia, ‘Ewe Bwanangu! Usiwasahau kuwasaidia na kukidhi haja za majamaa zetu na mafukara na masikini na uwe na uhusiano mwema pamoja nao. Na uwazawadie watu fulani fulani wakiwemo majirani na marafiki, zawadi mbalimbali.’

 

Mtu huyo alizingatia na kutekeleza ushauri uliokuwa umetolewa na mke wake. Na hivyo alifungua milango ya kugawa mali yake katika masuala hayo hadi ulipofika wakati wa kuisha kwa nusu ya umri wake wa awali.

 

Kuisha huku kwa nusu ya kwanza ya umri wake, aliota ndoto tena ambamo aliambiwa kuwa : ‘Kwa kutokana na uwema wako wa kuwasaidia wenye shida na dhiki imekuwa kipaumbele kwako, basi Allah swt amekubadilishia sehemu hii ya pili kuwa katika raha na mustarehe kama ilivyo sasa.’”

 

 5.  HAKI YA UVUNAJI

Wakati wa mavuno kwa kiwango kile ambacho bado Zaka haijapigiwa hisabu, inagawiwa kwa kuchota mkono moja kwa wapita njia kama vile alivyosema Allah swt katika Quran: Surah al –Al-An-‘Aam 6, Ayah 141 :

Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisiyo tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana. Kileni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.

 

Katika aina za Sadaka, aina hizi mbili za Sadaka ni Sunnah kwani Ayah ya Qur'an Tukufu pamoja na riwayah nyingi zimezungumzia na kusisitiza na ndio maana zimezungumziwa mbalimbali.

 

 

6.  KUKOPA MADENI

Yaani kuwakopa Waislamu ambao wanashida ya kukopa deni ili kukidhi masuala yao. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Al-Kafi :

“Katika mlango wa Jannat kumeandikwa ‘Yapo mema kumi kwa mtoa Sadaka na mema kumi na nane kwa mkopeshaji madeni.’”

 

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika  Al-Wafi :

“Wakati Mumin mmoja anapomkopesha Mumin mwenzake deni kwa ajili ya kutaka ridhaa ya Allah swt , basi Allah swt anamhisabia deni hilo katika Sadaka hadi kuja kulipwa kwake.”

 

Kila mara mtu atakapokuwa akimpa muhula mdaiwa wake kulipa deni lake, basi Allah swt atakuwa akimwandikia kuwa ametoa Sadaka kiasi hicho kwani yeye alikuwa na haki kamili ya kufanya na kulazimisha malipo lakini hakutumia nguvu kudai na badala yake amemwongezea muda mdaiwa wake, hivyo inamaanisha kuwa amemkopa mara mbili katika mali hiyo. Hivyo mtu huyo anakuwa mustahiki wa kupata thawabu za kutoa Sadaka kwa mara ya pili.

 

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa akisema kuwa :

“Kwa kupuuzia ‘Ma’un’ (mambo ya nyumbani ) ambayo Allah swt ameahidi katika Qur'an Tukufu adhabu, basi si Zaka inayozungumziwa, bali ni kuwasaidia kwa kuwakopa wale wenye shida na wenye shida wanapokuja kuazima vitu vya nyumbani, basi inabidi  kuwa azima vitu vya nyumbani.”

 

Abu Basir amemwambia Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa

“Majirani zetu wanapokuja kuazima vyombo au vitu vingine vya nyumbani, na tunapo waazima basi huvunja vunja na kuviharibu vitu vyetu na hivyo sisi tunalazimika kuwakatalia kwa misingi hiyo, sasa je kuwakatalia huku ni dhambi ?”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu :

“Iwapo watu hao wanatabia kama hiyo, basi si dhambi kuwanyima.”

 

Kuwakopa Waislamu ambao wanashida ya kukopa deni ili kukidhi masuala yao. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Al-Kafi :

“Katika mlango wa Jannat kumeandikwa ‘Yapo mema kumi kwa mtoa Sadaka na mema kumi na nane kwa mkopeshaji madeni.’”

 

7.  KUWAPA MUDA WADAIWA AU KUWASAMEHE MADENI

 

Inabidi kuwapa muda au kuwasamehe madeni wale ambao hawana uwezo wa kuyalipa madeni hayo. Na kuhusiana na swala hili Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema :

“Iwapo mtu anataka asidhalilishwe Siku ambayo hakuna mwingine wa kuwaokoa isipokuwa Allah swt , basi inambidi awape muda wa kulipa madeni wadaiwa wake au kuwasamehe madeni yao.”

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema :

“Yeyote yule atakayempa muda wa kulipa madeni ambaye hana uwezo wa kulipa ( basi kwa ajili yake ) thawabu zake mbele ya Allah swt  ni sawa na thawabu za kutoa Sadaka kila siku kwa kiasi hicho hadi atakapolipwa.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliambiwa kuwa :

“’Abdur Rahmaan bin Sababah anamdai deni marehemu mmoja, nasi twamwambia yeye kuwa amsamehe lakini yeye anakataa kata kata kumsamehe deni lake.”

 

Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akasema :

“Ole wake, je haelewi kuwa iwapo atamsamehe marehemu deni lake basi Allah swt atamlipa Dirham kumi kwa kila Dirham yake moja. Na iwapo hatamsamehe basi atalipwa Dirham moja kwa Dirham yake moja.”

 

8.  KUSAIDIA MAVAZI NA UKARIMU

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J.2,Uk. 204 :

“Mtu yeyote atakayemsaidia Mumin kwa mavazi wakati wa baridi au joto basi Allah swt atamjaalia mavazi ya Jannat (Peponi au Paradiso ) na atampunguzia shida kali wakati wa kutoa roho yake (wakati anapokufa ) na atampanulia kaburi lake na Siku ya Qiyamah atakapotoka nje ya kaburi lake atakuwa akitoka katika hali ya furaha kwa kuonana na Malaika.”

Vile vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-kafi, J.2, Uk.205 :

“Iwapo Mwislamu yeyote atamsaidia mtu asiye na mavazi kwa mavazi au aliye na dhiki ya mali, akasaidiwa ( nyumba,mali n.k ) basi Allah swt anamwekea Malaika elfu saba hadi Siku ya Qiyama kwa ajili ya kumwombea maghfirah kwa kila dhambi lake.”

 

9.  HISHIMA NA TAADHIMA NA KUJIHIFADHI

Ili kujihifadhi na shari na dhuluma na udhalilisho wa madhalimu kutolewe mali kwa misaada. Imeripotiwa kuwa bora ya kutoa mali kwa kusaidia ni kule ambamo kunalindwa hadhi na heshima ya mtu.

 

10.  MEMA YA KUDUMU

Kutumia mali kwa ajili ya mema ya kudumu na kwa faida ya watu, kwa mfano kujenga Misikiti au Madrassah, daraja, barabara, kupanda miti, vyoo, kuchimba mito, visima vya maji au kuchapisha vitabu vya dini  n.k. ambavyo daima huwafaidisha watu kwa muda mrefu na hivyo mwenye kujitolea kufanya vitu hivi pia huendelea kupata thawabu zake milele.

 

Merehemu Haji Nouri (r.a.) katika Dar-us-Salaam anamnakili Sheikh mkongwe na ‘A’alam Rabbani Sheikh ‘Abdul Hussein Tehrani ( r.a. ) kuwa :

“Mirza Nabi Khan ambaye alikuwa ni mtu makhsusi katika zama za Muhammad Shah Qajar, hadi alipofariki alikuwa mashuhuri katika kutenda maovu.

 

Usiku mmoja mimi niliota kuwa nipo ninatembelea Bustani mojawapo na kuangalia majumba ya Jannat  ( Peponi au Paradiso ) na ninaye mtu mmoja ambaye ananiongoza na kunionesha na kunielezea habari mbalimbali. Basi tulifika mahala ambapo mtu huyo aliniambia kuwa hapa kuna maskani ya Mirza Nabi Khan na iwapo utapenda kumtembelea, basi yeye yupo ameketi hapo, mtu huyo alikuwa akinitolea ishara pa mahala hapo.

 

Mimi nilipoangalia kwa makini nikaona kuwa ameketi peke yake na aliponiona akanifanyia ishara kuwa nipande juu na nilipomfikia na kumkaribia, aliinuka na kunisalimia na kunikaribisha na kunikalisha sebuleni naye aliketi vile alivyokuwa akiketi humu duniani kwa tabia zake zile zile. Mimi kwa hakika nilikuwa nimeshikwa na bumbuwazi kwa hali aliyokuwa nayo.

 

Yeye aliweza kung’amua yale niliyokuwa nikiyawazia, na hivyo akaanza kuniambia kuwa, ‘Ewe Sheikh ! Bila shaka umeshtushwa na kustaajabishwa kwa kuniona katika hali hii hapa Jannat  (Peponi) kwani matendo yangu yalikuwa maovu na yaliyokuwa yakistahili adhabu wakati bado nikiwa duniani, kwa hakika hivyo ndivyo ilivyokuwa hapo awali huko katika mji wa Taliqan, nilikuwa na machimbo ya chumvi ambapo kodi yake nilikuwa nikiituma Najaf  kila mwaka kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s. pamoja na wanayumba ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  Na kwa hakika Allah swt alipendezewa na tendo langu hili na kwa malipo yake amenipatia maskani pamoja bustani hizi.’

 

Sheikh Marehemu Haji Nouri anasema kuwa, ‘Mimi niliamka na kutoka katika ndoto hiyo ya kushangaza na kustaajabisha. Na ndoto yangu hiyo niliielezea kwa wanafunzi wangu darasani. Katika darasa hilo kulikuwapo na mwanafunzi mtoto wa Mullah Muti’i  Taliqani, ambaye alithibitisha kuwa hayo yalikuwa maneno ya kweli kuwa huyo alikuwa na machimbo ya chumvi huko Taliqan na kodi yake ipatayo kiasi cha Tuman mia moja ( Sarafu ya jamhuri ya Kiislamu ya Iran ) na kiasi hicho alikuwa akikituma Najaf na mzazi wangu ndiye aliyekuwa akiichukua pesa hizo kwa ajili ya kuandaa maombolezo hayo ya kila mwaka ya Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s.

 

Marehemu Sheikh aliyekuwa mwalimu alikuwa hajui iwapo huyo alikuwa akihusiana na Taliqan na akifanyisha maombolezi kila mwaka huko Najaf.’

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema , katika Al-Wafi, al-Kafi na kunakiliwa pia katika Tahdhiib :

“Baada ya kufariki kwa mtu, huongoka  kwa mambo matatu

Sadaka ambayo aliitoa humu duniani na ambayo inaendelea baada yake,Sunnah ambayo aliitekeleza kwa mfano Adhan ambayo baada ya kifo chake ingali ikiendelea, Kuacha mtoto mwenye tabia na mienendo mizuri ambaye atakuwa akimwombea dua na usamehevu kwa ajili yake ( na akifanya mema kwa niaba ya baba yake, kama inavyoelezwa katika vitabu vingine.

 

 


MADONDOO JUU YA SADAKA

 

Hapa nitapenda kuzungumzia machache kuhusu Sadaka

  • Sadaka inalipia madeni na kuongezea neema kwetu,
  • Sadaka inatuepusha na mauti katika hali mbaya
  • Siku ya Qiyama kutakuwa na jua na joto kali mno, lakini Mumin atakuwa katika kivuli, nacho ni Sadaka aliyokuwa akiitoa.
  • Toeni Sadaka asubuhi na mapema, ili balaa na matatizo yasiwafikieni katika siku nzima.
  • Muwatibu wagonjwa wenu kwa kutoa Sadaka
  • Kutoa Sadaka ni afadhali kuliko kumnunua mtumwa na kumfanya huru
  • Mtu mmoja alifiwa na watoto wawili, alibakia mmoja. Akashauriwa kutoa Sadaka. Toeni Sadaka kwa mikono yenu wenyewe kwani hamtakufa kifo kibaya na balaa zaidi ya 70 zitaepukwa na kujiepusha na mitego 70 ya Shaitani, kwani Shaitani yupo anasema, “Usitoe Sadaka.” Je tutamwitikia Shaitani ?
  • Toeni Sadaka hata kama ni tonge moja ya tende na kama hiyo pia hamuwezi basi toeni punje moja ya tende.
  • Sadaka inatuepusha na balaa 70 ambamo kuna magonjwa, madhara ya moto, kuzama maji, kuangukiwa na kufunikwa na majumba yanayoporomoka na kubomoka na kutokuwa masikini,
  • Unapokuwa na hofu ya kuibiwa, kuungua moto n.k. bali toa Sadaka.

 

 

 


1. ISISITIZWE KUTOA SADAKA KWA WENYE SHIDA, MASIKINI NA MADENI

 

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa :

“Sadaka inalipia madeni na inaongezea katika barakah.”

 

2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwayah kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa :

“ Sadaka inamwepusha mtu na ajali mbaya.”

 

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa:

“Mtu yeyote yule aliye mja wa Allah swt akiwa Mumin akatoa Sadaka, basi Allah swt baada ya kifo chake huyo mtu huwaweka vyema na kuwasaidia wananyumba yake katika hali njema.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akaendelea kusema :

“Faida ya kutoa Sadaka ni kwamba inamsaidia kulipia madeni na viile vile kuongezea katika baraka.”

 

4. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Kusaidia na kutoa sadaka vyote hivyo vinaondoa umasikini na hurefusha umri wa mtu. Na yule anayetoa huweza kuepukana na aina sabini za ajali mbaya.

 

5. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika kuelezea tafsiri ya aya, ya Qur'an Tukufu, Sura Al-Layl, 92 , Ayah ya 5 na 6 :

Ama mwenye kutoa na akamcha Mungu,

Na akaliwafiki lilio jema.

 

ndipo amesema kuwa;

Allah swt ndivyo anavyo walipa wale watendao mema, kwa mema yao mara kumi, au hata mara laki moja na hata zaidi ya hapo.

 

Na vile vile amesema kuwa: anayetoa katika njia ya Allah swt basi Allah swt humjaalia kila aina ya tawfiqi katika kazi hiyo ya khairi.”

 

6.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amemnakili Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa

“Mtu yeyote yule ambaye anamwamimi Allah swt kuwa atamlipa na atamwongezea zaidi ya kile anacho kitoa basi huyo mtu kwa moyo mkunjufu na bila aina ya ubakhili wowote atatoa sadaka na misaada kwa wingi kabisa.”

 

7. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amemnakili Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa

“Siku ya Qiyama ardhi itakuwa imepata moto kupita kiasi na mumin watakuwa katika kivuli na kivuli hicho itakuwa ni kile alicho kuwa akitoa Sadaka.”

 

8. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwayah moja kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akisema kuwa:

“Enyi watu! Toeni sadaka bila shaka sadaka inaongezea katika mali yenu, na hivyo mtoe sadaka na Allah swt atawarehemu.”

 

9. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa katika Kitab ‘Uddatud-Da’i kuwa  alimwuliza mtoto wake :

“Je nyumbani kuna kiasi gani kwa ajili ya matumizi ?”

 

Naye alimjibu : “Zipo Dinar arobaini tu.” 

 

Imam a.s. alimwambia “Dinar zote hizo zigawe Sadaka.”

 

Kwa hayo mtoto wake alimwambia Imam a.s.

 “Ewe Baba ! Mbali na Dinar hizi arobaini, hatutabakia na akiba yoyote.”

 

Imam a.s. alimwambia :

“Nakuambia kuwa zitoe Dinar zote Sadaka kwani ni Allah swt tu ndiye atakayetuongezea kwa hayo. Je wewe hauelwei kuwa kila kitu kina ufunguo wake ? Na ufunguo wa riziki ni Sadaka ( kutolea mema ).”

 

Kwa hayo, mtoto wake aliyekuwa akiitwa Muhammad, alizitoa Sadaka Dinar hizo na hazikupita siku kumi, Imam a.s. alitumiwa Dinar elfu nne. Hapo Imam a.s. alimwambia mwanae :

“Ewe Mwanangu ! Sisi tulitoa Dinar arobaini tu na Allah swt ametupa Dinar elfu nne badala yake.”

 

10. Al Imam Musa al-Kadhim a.s. amesema kuwa:

“ Toeni sadaka mjipatie riziki.”

 

11. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“ Toeni sadaka mjiongezee riziki yenu. Bila shaka anayeamini kuwa Allah swt hulipa mambo yote. Basi yeye huwapa sadaka masikini kwa kupita kiasi. Allah swt humjaalia riziki kwa njia mbalimbali kwa  kile huyu mtu akitoacho katika mali yake.”

 

12. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa  Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. siku moja alitoa Dinar moja kama Sadaka na hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia :

“Ya Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.! Je unaelewa kuwa pale mtu anapotoa Sadaka kwa mkono wake mwenyewe basi hujiepusha na mitego ya mashetani sabini, na kila shetani husema, ‘Ewe fulani, usitoe sadaka kamwe.’”

 

Akaendelea kusema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

Ya Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.! Kile utoacho Sadaka kabla hakijaingia katika mkono wa yule anayeomba, kwanza hupitia katika mkono wa Allah swt.

 

Na baada ya hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisoma aya hii ifuatayo ambayo iko katika Qur'an, Surah Tawbah,9, Ayah  104.

Je hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anapokea toba ya waja wake, na anazikubali sadaqah , na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba na Mwenye kurehemu?

 

13. Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. amenakili riwayah kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akisema kuwa :

“Kuwa na akida ya Tawhid ni nusu ya sehemu ya dini, enyi watu!  Toeni Sadaka ili mpate riziki zaidi”.

 

14. Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s.  ametoa riwayah kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa :

 “Kuwa mali halisi ya mtu ni ile ambayo yeye ametolea sadaka.”

 

15. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa:

“Toeni Sadaka asubuhi na mapema ili balaa zisiwafikieni katika siku nzima.”

 

16. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwayah kutoka Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa:

“Sadaka ni kinga dhidi ya moto wa Jahannam .”

 

17. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akisema:

“ Enyi watu muwatibu wagonjwa wenu kwa kutoa Sadaka.”

 

18. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. katika Nahjul Balagha amesema kuwa:

“Mnapoona riziki yenu inapungua na kuwa finyo basi muwe mkitoa sadaka ndivyo mtakuwa mkifanya biashara na Allah swt.”

 

19. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“ Imani ya muumini inakuwa na sifa nne za lazima,

1.      Awe na tabia njema,

2.      Awe mkarimu na mwepesi wa kutoa

3.      Asizungumze zaidi ya yale yanayo takikana (hazungumzi mambo ovyo ovyo)

4.      Hutumia kile kiasi kinacho takiwa ,siyo mfujaji ( anaotoa katika njia ya Allah swt ).

 

 


2. KUSAIDIA FAMILIA YA WAISLAMU WENYE SHIDA NI AFADHALI KULIKO KWENDA HIJJA ZILIZO SUNNAH NA KUWAFANYA HURU WATUMWA

 

1. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa:

“Iwapo mimi nitakwenda Hijja moja basi afadhali niwafanye huru watumwa kumi, lakini iwapo mimi nitajichukulia jukumu la kuwalisha familia ya Waislamu ambao wanashida ya chakula na ambao wanaishi kwa njaa nikawamalizia shida zao, nikawavalisha nguo wale ambao hawana nguo, na nikawarudishia heshima yao miongoni mwa watu, basi mimi ninaona jambo hili ni afadhali na bora zaidi kuliko hata kwenda kuhiji Hijja sabini.”

 

2.  Al Imam Musa al-Kadhim a.s. aliijiwa na mtu mmoja na aliyeuliza,

“Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Mimi ninazo pesa na utajiri je ni jambo gani afadhali nitoe sadaka au nimnunue mtumwa na kumfanya huru?”

 

 Kwa hayo Al Imam Musa al-Kadhim a.s.  alimjibu kuwa:

“Kuwa mimi ninaonelea kuwa kutoa Sadaka ni afadhali zaidi.”

 

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Siku moja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza Maimuna binti Harun, Je Kijakazi wako amekuwaje? Akasema Maimuna kwa hayo alimjibu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., ‘Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Mimi nimemfanya huru.’

 

 Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia “Iwapo kama wewe ungelichukua jukumu la kumlisha, kumtunza, kumsaidia na kumwonea huruma basi ingekuwa afadhali zaidi.”

 

 


3. KUWATOLEA WAGONJWA SADAKA NI SUNNAH

 

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Muwatibu wagonjwa wenu kwa Sadaka, na muzuie maafa kwa kuomba dua na kutoa sadaka muongezee riziki zenu zipanuke, na kwamba Sadaka inawaepusheni na mitego ya mashetani sabini.”

 

2.  Siku moja walikuja wagonjwa wakilalamikia magonjwa yao mbele ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., naye akawaambia;

“Nendeni mtoe Sadaka kwa ajili ya magonjwa yenu na mtapona, iwapo mtu atatoa Sadaka kwa kile akitumiacho kwa  siku dharura wake, basi Allah swt huahirisha hata kifo chake na vile vile humwepusha na ajali mbaya.”

 

 


4. MTOE SADAKA KWA NIABA YA WATOTO WENU NA WATOTO WENU WATOE SADAKA KWA MIKONO YAO HATA KAMA ITAKUWA KIDOGO KIASI GANI.

 

1. Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. aliulizwa na Sahaba mmoja  :

“Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Mimi watoto wangu wawili wamefariki na amebakia mtoto wangu mdogo.”

 

Kwa hayo Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. kamwambia:

“Basi toa Sadaka kwa niaba ya mtoto wako huyo.”

 

 Na siku moja Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. alipomtembelea huyo mtu akamwambia,

“Mwambie mtoto wako huyo atoe Sadaka kwa mkono wake walau kiasi kidogo chochote kile au hata kama kitakuwa ni kipande kidogo tu. Utambue wazi kuwa kiasi chochote kile hata kikiwa kiasi gani kama kitatolewa kwa roho safi  basi mbele ya Allah huwa ni kipenzi, kwani Allah swt ameelezea kuwa: Qur’an Tukufu, Surah Az-Zilzalah,99, Ayah7 - 8

Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona !

Na anaye tenda chembe ya uovu atauona !

 

Vile viel Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. alimwelezea kuwa:

“Allah swt amesema katika Qur’an Tukufu, Surah Al-Balad,90, Ayah11 - 16

Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.

Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani ?

Kumkomboa mtumwa;

Au kumlisha siku ya njaa

Yatima aliye jamaa,

Au masikini aliye vumbini

 

“Hivyo ewe Sahabi  uelewe kuwa Allah swt anaelewa wazi wazi kuwa si watu wote wenye uwezo wa kuwanunua na wenye kufanya huru watumwa hivyo yeye ameweka thawabu hizo hizo kwa wale watakao toa Sadaka au watakao walisha yatima na masikini.”

 

2. Al Imam Musa al-Kadhim a.s. alijiwa mtu mmoja mbele yake na kuelezea habari za mtoto wake, na kwa hayo Al Imam akamjibu :

Toa Sadaka kwa niaba yake.”

 

Na mtu huyo akajibu kuwa

“Sasa mtoto wake amekuwa na umri  yaani amekuwa kijana.”

 

Basi Al Imam Musa al-Kadhim a.s. alimwambia kuwa

“Mtoto wako atoe Sadaka kwa mkono wake, hata kama itakuwa ni kipande cha mkate, na hapo ndipo Al Imam Musa al-Kadhim a.s. alisema riwayah ya Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. kuwa:

“Katika Israil alikuwa mtu mmoja aliyekuwa akimpenda mno mtoto wake, na akaona katika ndoto yake anaanmbiwa kuwa, mtoto wako huyo umpendaye mno atakufa usiku wa ndoa yake. Kulipowadia usiku wa arusi baba mzazi wa mtoto huyo, usiku kucha akawa katika wasiwasi na hakupata usingizi na kamwe hakupata raha usiku huo.

 

Na kulipo pambazuka asubuhi na mtoto alipotoka chumbani mwake akiwa hai basi baba yeke alimwuliza

 ‘Ewe mwanangu! Je katika usiku huu wako wa kuamukia leo umefanya mema yoyote?’

 

 Kwa  hayo mtoto akajibu

“Ewe baba yangu! hakuna jambo la maana sana lililotendeka, bali alitokezea masikini mmoja akaja mlangoni kuomba chakula, alikuwa na njaa na kile chakula walichokuwa wameniwekea, mimi nikampa chakula chote huyo mtu aliyekuja kuomba.’

 

 Kwa hayo baba yake akasema

“Kwa sababu hii tu ndiyo Allah swt amekuondoshea balaa kubwa iliyokuwa ikupate wewe usiku huo.”

 

 


5. MTOE SADAKA KWA MIKONO YENU WENYEWE  hUSUSANI WANANYUMBA WATOE SADAKA KWA MIKONO YAO NA WANAYEMPA WAMWOMBE AWAOMBEE DUA NJEMA.

 

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa:

“Kwa kutoa Sadaka kwa mkono wako mwenyewe basi unajiepusha na ajali mbaya, unajiepusha na balaa na maafa sabini na mitego ya mashetani sabini na ambamo kila shetani yuko anakwambia ‘ewe fulani!  Usitoe Sadaka kamwe.”

 

2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Mgonjwa atoe Sadaka kwa mkono wake mwenyewe na anayempa amwambie amwombee dua”.

 

3.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika hadith zake amesema kuwa:

“Mkono uliye juu yaani mtoaji ni afahali kuliko mkono ule ulio chini yake, yaani mpokeaji.”

 

4. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa:

“Kuna aina tatu ya mikono wa

·         kwanza ni mkono ule wa Allah swt  ambao uko juu kabisa na kwa hakika neema zote ni za Allah swt,

·         mkono wa pili ni ule mkono wa yule mtu anaye toa, ambaye anatoa katika njia ya Allah swt na

·         mkono wa tatu ni wa yule anaye pokea ambao mkono uliochini wa yule anayetoa. Kwa hivyo enyi watu chochote kile kinachobakia miongoni mwenu mtoe katika njia ya Allah swt  na musikalifishe nafisi zenu”.

 

 


6. KUTOA SADAKA KILA MARA NA KWA WINGI NI SUNNAH

 

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.  amesema kuwa:

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa amemfanyia usia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.; Ewe Ali! Ninakufanyia usia wa mambo mema machache na uyakumbuke vyema.

 

Ewe Allah swt umsaidie Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. Baada ya hapo wakati akifanya usia, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema: Ama kuhusiana na sadaka tafadhali usiwe na mnunguniko wowote. Utoe kiasi kwamba mpaka uhisi kwamba wewe umefuja mali yako, lakini utambue wazi kuwa hiyo sio ufujaji bali hiyo umetoa katika njia ya Allah swt.”

 

 


7. KATIKA KUTOA SADAKA HATA KIASI KIDOGO  CHOCHOTE KILE NI SUNNAH

 

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa kuna riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa

“Toeni Sadaka, angalau hata kwa sa’  ya tende, na kama sa’ moja hiyo hamnayo basi mtoe tende kwa kiganja kimoja na hata kama hivyo haitawezekana basi mtoe tende kiasi chochote kile na kama hivyo haitawezekana basi mtoe angalau kokwa moja ya tende, na kama hivyo pia haitawezekana basi yule masikini aliyekuja kuwaomba mumwambie maneno mazuri na matamu na maneno matakatifu katika kumwelezea kuwa hakuna chochote, na hayo pia ni sadaka.

 

Kwa sababu isitokee Siku ya Qiyama kwamba Allah swt atakapo kuuliza hesabu ya neema alizokujaalia akakuambia

‘Ewe mja! Mimi nilikupa mambo chungu nzima, sasa hebu angalia nafsini mwako je kwa kutumia neema hizo wewe umejiandalia nini?’

 

Na hapo wewe utaangalia sehemu zote nne za dunia na utajawa na masikitiko, na utakuta hakuna jambo lolote lile litakalo kuokoa dhidi ya adhabu za Allah swt.”

 

2. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa:

“Mtoe tende kiasi fulani kwani itawaokoa na moto wa Jahannam , mpanue riziki zenu na mteremshiwe riziki nyingi kwa kutoa Sadaka na kupitia dua mziondoe balaa na shida zenu.”

 

Mkumbuke kuwa kwa kutoa Sadaka hamtapungukiwa katika mali yenu. Na miongoni mwa jamaa zenu wanapokuwa na shida muwasaidiapo hiyo siyo Sadaka bali hiyo ni wajibu wenu.”

 

3. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa:

“Kulikuwa na mja mmoja aliyekuwa akifanya ibada ya Allah swt kwa umri wake wa miaka  themanini.

 

Siku moja alimwona mwanamuke mmoja mzuri aliyekuwa akipendeza naye akawa ameingia katika mtego wake.  Yeye alitimiza matamanio yake visivyo halali na mara akatokezea Malakul mauti (malaika anayetoa roho). Ulimi wake ulifunga kuongea na jasho lilianza kumtoka na kutokwa kwa roho na mara hapo alipita masikini akiomba.

 

Basi mtu huyu ambaye alikuwa katika hali ya kukata roho alimwambia yule masikini kwa ishara kuwa mahala fulani kuna mkate hivyo auchukue hivyo aweze kula huyo masikini, na masikini huyo alivyoelekezwa akauchukua mkate akaondoka zake.

 

Kwa hiyo ikatokea kwamba Allah swt aliibatilisha ibada zake za miaka themanini kwa sababu ya kuzini na ikatokea kwamba Allah swt akamsamehe madhambi yake yote kwa sababu ya kutoa Sadaka kwa moyo mkunjufu.”

 

4. Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s.  amesema kuwa;

“ Katika zama za Bani Israil kuliwahi kutokea baa la njaa ambao uliendelea kwa muda wa miaka mingi. 

 

Katika wakati huo ikatokezea kwamba bibi kizee mmoja akiwa amekabwa na njaa hali ya juu alikuwa ameketi akiwa na kipande kidogo cha mkate huku akitaka kukila kipande hicho, mara akasikia mlangoni sauti ikisema ya masikini aliyekuwa amekuja kuomba:

‘Ewe mja wa Allah swt! Mimi nakufa kwa njaa naomba unisaidie, bibi kizee huyo akajiambia kwa hakika Sadaka ndiyo wakati huu muafaka wa kutoa, na kile alichokuwa akila akakitoa haraka akampa huyo aliyekuwa akiomba.

 

Bibi kizee huyo alikuwa na mtoto mmoja aliyekuwa amekwenda porini na ghafla kule alishambuliwa na mnyama. Kwa kusikia sauti ya mtoto wake huyo bibi kizee ikimwita, alikimbia kumfukuza mnyama huyo na kwa muujiza wa Allah swt  ni kwamba,  Allah swt alimtuma Malaika Jibrail a.s kwenda kumwokoa mtoto huyo katika mdomo na mabano ya mnyama wa huyo muuwaji, na Malaika Jibraili a.s. akamwambia ‘Ewe bibi kizee ! Je umefurahi sasa? Kwa kile ulichokitoa sadaka basi Allah swt naye amekulipa mema yake.”

 

 

5. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa:

“ Mfanye mema katika hali ya shida na ufakiri, na wema huo ni Sadaka.

 

Toeni Sadaka kama itakuwa ni kiasi gani kwa udogo wake. Mnaweza kutoa kiasi cha tende mkajiokoa na  Jahannam. Kwa hakika udogo huo siyo hoja na Allah swt ataulea udogo huo kama kwamba nyie mnavyo walea watoto wadogo wanaonyonya maziwa, na siku ya Qiyama wakati mema yenu hayo  ( mliyokuwa mkisema ni madogo) yatakapoletwa mbele yenu mtaona kuwa ni sawasawa na ukubwa wa milima mikubwa sana.”

 

6.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameseama kuwa Allah swt anasema kuwa :

“Hakuna kitu kingine mbali na Sadaka ambacho mtu anaweza kumpatia mtu mwingine kidhahiri, na kwa hakika mimi ndiye wakili wake musitahiki, na mimi ninayepokea kwa mikono Sadaka hiyo halafu hata ikiwa kama ni tende kidogo haidhuru mimi ndiye ninaitunza, kama vile mwanadamu anavyowatunza watoto wake.

 

Siku ya Qiyama huyo mtoa Sadaka atastaajabishwa mno kwa Sadaka zake ndogo alizokuwa akitoa zimekuwa kubwa kama milima ya Uhud, milima mikubwa sana.”

 

 


8. KILA SIKU ASUBUHI MTOE SADAKA NA MNUIE

 

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa: 

“Toeni Sadaka asubuhi na mapema kwa sababu kunaondoa balaa kwa siku nzima.”

 

2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Kwa kutoa Sadaka asubuhi na mapema basi mtoa Sadaka huepukana na kila aina ya matatizo na mabaya yote kwa siku nzima.”

 

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Toeni Sadaka asubuhi, na kwa mapenzi kabisa, mwenyewe kutoa Sadaka amebahatika. Basi humwomba Allah swt amani kutokana na balaa zote zilizoko ardhini na mbinguni, na kwa hakika Allah swt humjaalia hivyo kwa sababu ya kutoa Sadaka.” 

 

4. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anaelezea kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwusia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa:

“Ewe Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.! Sadaka huondoa balaa ambazo lazima zitatokezea, na kwa kutenda mema pamoja na ndugu na majamaa kunarefusha umri.

 

Ya Ali! Iwapo jamaa na ndugu ni watu wenye shida, basi kuwapa Sadaka  hao haitakuwa ni Sadaka.

 

Ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.! Kusema maneno bila vitendo ni ya bure hayana maana, na Sadaka  bila kuwa na nia nayo haiwi Sadaka.”

 

5. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa: Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza mtu mmoja

“Je leo umefunga Saumu?”

 

Mtu huyo alijibu

“La hapana! Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.”

 

 Tena Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza:

“Je leo umeshawahi kumtembelea aliye mgonjwa?”

 

 Naye akajibu:

“Hapana! Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.”

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  aliendelea kumwuliza naye aliendelea kumjibu hapana hakufanya hivyo.

 

Mwishoni Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.aliendelea kumwuliza:

“Je umemlisha masikini yeyote?”

 

 Naye akajibu: “Hapana Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.!”  

 

Na hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipomwambia huyo mtu :

“Nenda kwa wananyumba wako, nenda ukawatendee  na uwe nao kwa  mema na uwawie wema, basi hayo ndiyo yatakuwa Sadaka  yako kwao.”

 

 


9. KAMA KUNA HOFU YA KUJA KWA BALAA AMA KWA KUTOKEZEA UBAYA WOWOTE AU KWA SABABU YA UGONJWA NA HOFU YOYOTE BASI TOENI SADAKA.

 

 

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripoti riwayah kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambaye ameseama:

“kwa baraka za Sadaka Allah swt humwondolea mwenye kutoa Sadaka balaa sabini, ambamo kuna magonjwa, madhara yatokanayo na moto, kuzama maji, kufunikwa na majumba mpaka kufa na atamwepusha ili asiwehuke au asiwe mwehu.”

 

2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripoti riwayah kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa: 

Ili kutaka kuepukana na shari za madhalimu basi toeni Sadaka.”

 

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anaelezea kuwa: Siku moja Myaudi mmoja likuwa akienda kukata miti porini na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwangalia na kuwaambia Ma-Sahaba wake :

 “Myahudi huyu leo ataumwa na nyoka na kifo chake kitasababishwa na sumu ya nyoka. Myahudi huyo kama kawaida yake alikata kuni na alijitwisha kichwani mwake na akarud akiwa salama.

 

Na tena Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipomwona Myahudi huyo akamwambia ateremshe mzigo wa kuni huo na auweke chini. Na Myahudi akafanya hivyo alivyoambiwa, na katika mzigo huo wa kuni wakaona kuna nyoka mweusi mwenye sumu kali sana huku akiuma kuni.

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza Myahudi yule,’Je wewe leo umefanya jambo gani?’

 

 Myaudi huyo akasema: Mimi nimekata kuni na kuzifunga tu, lakini wakati nilivyokuwa nikirudi nilibakiwa na vipande viwili vya mkate na kipande kimoja mimi nikala na kipande kimoja nikampa masikini Sadaka.

 

 Hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema kwa kiapo cha Allah swt ni kwa sababu ya Sadaka  ndiko balaa hii imekuondokea, kwa hakika Sadaka humwepusha mtu na ajali mbaya.”

 

4. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. siku moja alikuwa pamoja na Ma-sahaba wake katika Masjid Nabawi, na upande mmoja wa ukuta ukaanguka chini. Kulikuwa na mtu mmoja hapo ambaye aliponea chupu chupu tu, kulianguka kizingiti kizito karibu na muguu wake. Lakini yeye bahati nzuri hakupata udhuru wowote.

 

Hapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. aliwaambia Ma-sahaba wake, hebu mwulizeni huyu mtu leo amefanya matendo gani? Na wakati alipoulizwa huyo mtu akasema:

“Mimi nilipotoka nyumbani mwangu leo nilikuwa na kokwa chache za  tende. Na kukatokezea na masikini mmoja akaniomba basi mimi nikampa kama Sadaka .

 

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. akajibu

“Basi kwa sababu hiyo tu leo, Allah swt amekuepusha na balaa hii ambayo ingekumaliza.”

 

5. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. siku mmoja alimwambia Sahabi wake Mayassari kuwa:

“Ewe Mayassari je wajua kuwa wewe umeisha fikiwa na mauti mara nyingi, lakini Allah swt amekuongezea umri wako zaidi kwa sababu ya wewe kuwa mkarimu na kuwajali jamaa na ndugu zako umewawia wema ndio maanake umri wako umezidi.”

 

 

 


10. MNAPOKUWA NA HOFU YA KUPATA HATARI KATIKA MALI, BASI MTOE SADAKA NA KAMA HAMPATI YULE ALIYEMUSTAHIKI, BASI MFANYE NIA SEHEMU HIYO MUITENGE NA MALI YENU.

 

1. Al Imam Hasan al-'Askary a.s. anasema kuwa:

“ Wakati mmoja Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akiwa pamoja na wenzake walikuwa safari na wenzake hao walikuwa na mali nyingi sana. Na njiani wakapata habari kuwa wako majambazi wanaowapora matajiri mali zao. Kwa kusikia hayo hao matajiri walianza kutetemeka na wakaingiwa na hofu na wakaanza kumwuuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. je tufanyeje sasa?

 

Na kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akawajibu:

‘Mkabidhini mali yenu yule ambaye ataweza kuifadhi mali yenu, na kwa kweli ataitunza sana na baada la kupungua hata itazidi pia, sio hayo tu na pale mutakapokuingiwa na shida ya mali yenu basi yeye kila siku atawarudishia pamoja na nyongeza yake. ‘

 

Kwa kusikia hayo hao wenzake aliokuwa nao katika safari wakamwuliza :

“Je ni nani huyo?”

 

 Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akawajibu:

“Yeye ni miliki wa malimwengu zote Allah swt.”

 

 Basi hao wenzake wakamwuliza je tunaweza kumkabidhi vipi mali zetu hizi? Hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akawaambia: Toeni Sadaka  muwape wale wanaostahiki. Kwa kusikia hayo wakauliza ewe mjukuu wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Hapa tulipo tutawatoa wapi hawa masikini na mafakiri tutawatafuta wapi? Basi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. aliwajibu: munuie kuwa  sehemu moja ya mali yenu mtatoa Sadaka basi na msiwe na wasiwasi Allah swt atailinda mali yenu yote.

 

 

“Wale waliokuwa naye pamoja safarini walinuia hivyo kama vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alivyowaambi,a na Imam a.s. akawaambia sasa nyie mko katika amani ya Allah swt, na wakiwa wanaendelea na safari majambazi hao walikumbana nao na kwa kudura za Allah swt wao wakawapita salama usalimini bila ya kudhurika na kusumbuliwa, hadi wakafika mwisho wa safari yao.

 

Waliopofika tu mwisho wa safari yao wao wakatoa sehemu moja walizokuwa wamenuia kama Sadaka na sehemu iliyo bakia walifanyia biashara yao, na Allah swt akawajaalia baraka kiasi kwamba wakapata faida hata zaidi ya mara kumi.” 

 

 


11. WAOMBAJI WANATAKIWA WARIDHIKE KWA KILE WANACHOPATA NI SUNNAH, KUWAONGEZEA WALE WALIORIDHIKA NA KUTOWAJALI WALE WASIORIDHIKA.

 

1. Siku moja Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alikuwa Mina pamoja na Ma-sahaba wake wakila zabibu. Mara akatokezea mtu mmoja na akaomba. Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kwa mkono wake akachukua fungu moja la zabibu akampa basi huyo akakataa kupokea, akisema “mimi sitaki zabibu hizi bali ninataka pesa tasilimu kama zipo ndio nichukue”.

 

Basi kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwambia “Allah swt atakuzidishia” na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. hakumpa chochote, baada ya muda si muda huyo mwombaji tena akarudi kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. na akamwambia Imam a.s. “Nipe zile zabibu ulizokuwa ukitaka kunipa.” Na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwambia Allah swt atakutafutia njia yake, pamoja na hayo Imam a.s. hakumpa chochote.

 

Wakati bado wakiwa wamekaa akatokezea mtu mwingine kuja kuomba, na Imam a.s. alitoa mbegu tatu tu za zabibu akampa huyo mwombaji. Mwombaji huyo alianza kumshukuru Allah swt kwa kumjaalia riziki hiyo na akaonyesha shukurani kwa ujumla. Kwa kusikia hayo Imam a.s. alichota mikono ya zabibu miwili akampa na hapo tena huyo mwombaji akaendelea kumshukuru Allah swt zaidi na zaidi. Kwa kusikia hayo tena Imam a.s. akamwambia mtumwa wake kama tuna pesa zozote zile tulizo nazo kwetu mpe huyo. Na huyo mfanyakazi wa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kwa amri yake alimpa Dirham Ishirini alizokuwa nazo. Mwombaji akiwa anachukua Dirham akasema: ‘Ewe Allah swt! Nakushukuru mno sana na hakuna mwingine wa kushirkishwa nawe. Kwa kusikia hayo Imam a.s. nguo aliyokuwa amejifunika akampa huyo mwombaji na huyo mwombaji baada ya kuivaa na kujifunika na hiyo nguo akamshukuru Allah swt ambaye amemjaalia nguo ya kujifunika. ‘Ewe Aba ‘Abdillah! Allah swt akulipe kila la heri. Na baada ya kusema hayo akaondoka zake. Kwa kuona haya Ma-sahaba wakamwambia Imam a.s. kuwa kila alivyoendelea yeye kumsifu Allah swt ndivyo wewe ulivyoendelea kumpa na kama asinge omba kwa kutaja jina la Al Imam a.s. lazima angeendelea kumpa chochote zaidi ya hayo.”


12. ASUBUHI NA MAPEMA NA USIKU UNAPOINGIA NA SAA ZINAZOKUWA MBAYA UANPOTOKA NJE BASI MTOE sadaqah.

 

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“ Mimi nilinunua ardhi pamoja na mtu mmoja. Mtu huyo huyo alikuwa ni mnujumi, kwa hiyo yeye kila alipokuwa akipiga mahesabu yake na elimu ya nyota yake aliyokuwa nayo alikuwa akiangalia saa nzuri ndipo alipokuwa akienda shambani mwake, nami bila kujali kama saa mbaya nilikuwa nikienda shambani mwangu, na sisi tulipokuwa tayari basi ardhi au sehemu yangu ikawa na faida zaidi kuliko sehemu yake.

 

Kwa hivyo yeye bila kusita katika  hali ya kustaajabisha aliniambia mimi sijawahi kuona kama hivi. Mimi kila saa zilizokuwa nzuri nilikuwa nikija shambani mwangu. Na wewe bila kujali saa nzuri au mbaya ulikuwa ukija kwenye shamba lako. Sasa itakuwaje mimi nipate hasara au kasoro?

 

 Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamjibu ngoja nikwambie hadithi moja ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliyesema kuwa:

‘Mtu yeyote anayetaka Allah swt amwepushe na maovu na mabaya ya siku nzima basi yeye aianze siku yake kwa kutoa Sadaka, na yeyote anayetaka ajiepushe na balaa na maovu ya usiku basi yeye usiku unapoingia atoe Sadaka na ujue kwamba mimi daima ninapotoka nyumbani mwangu huwa ninatoa Sadaka. Kwa hivyo kufanya biashara na Allah swt hivi afadhali zaidi kuliko elimu yako ya nyota na kupiga ramli.”

 

2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema :

“Mtoe Sadaka  usiku kwa sababu huiondoa ghadhabu ya Allah swt, husamehe madhambi mazito, na hukusababishia hesabu zako siku ya Qiyamah zikaenda vizuri. Kutoa Sadaka  katika siku kunaiongezea mali yako na kuilinda na kunaufanya umri wako uwe mrefu.”

 

 

 

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“ Kwa kutoa Sadaka  yaani kunapokucha kunayeyusha madhambi kama vile chumvi inavyoyeyuka katika maji. Na kunapotolewa Sadaka usiku basi kunaondoa ghadhabu za Allah swt.”

 

4. Ibn ‘Abbas amesema kuwa: Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu, Sura Al-Baqarah,2, Ayah 274  

Wale wanao toa mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhaahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika

 

“Aya hiyo imeteremshwa makhsusi kwa ajili ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kwa sababu yeye alikuwa anazo Dinar chache ambazo wakati wa usiku yaani baadhi ya Dinar hizo wakati wa usiku na baadhi wakati wa mchana na zinginezo katika hali ya siri na zinginezo zikiwa ni dhahiri alizokuwa akitoa Sadaka katika njia ya Allah swt.”

 

 


13. NI VYEMA KUTOA SADAKA KIFICHOFICHO KULIKO KIDHAHIRI.

 

1. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akisema kuwa:

“Kwa kutoa Sadaka  kifichoficho ghadhabu za Allah swt hupoa.” 

 

2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Sadaka inayotolewa kidhahiri basi kuliko hiyo Sadaka  inayotolewa kifichoficho ni afadhali zaidi.”

 

3. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. siku moja alisema kuwa:

“Mambo yanayomfikisha mtu moja kwa moja kwa Allah swt kama kipitio au (Wasila) ni imani. Na baada yake ni kuwatendea mema ndugu na majamaa zake mtu, ambaye inaongezea baraka katika mali yake na umri wake ukawa  mrefu na Sadaka inayotolewa kifichoficho inamfanya huyo mtu asamehewe madhambi yake, na madhambi aliyokuwa yamemgadhabisha  Allah swt kwa sababu ya kutomtii, yanabadilishwa kuwa mema na baadaye ni tabia njema na uwema, mambo ambayo yanaepusha ajali mbaya na inamfanya huru mtu katika makucha ya udhalilisho.”

 

4. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Kwa kutoa Sadaka  kidhahiri kunaondoa aina sabini za balaa lakini kwa kutoa Sadaka  kifichoficho kunamfanya mtu anusurike  na ghadhabu za Allah swt.”

 

5. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s.   amesema kuwa:

“Baba yake Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. kila siku usiku alikuwa akitoka nyumbani pamoja na kifurushi cha fedha mgongoni mwake na mara nyingine alikuwa akichukua kufurushi cha vyakula na alikuwa akiwaendea wale wenye shida na dhiki.

 

Wakati akiwapelekea misaada hii majumbani mwao Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa akiufunika uso wake ili wasiweze kumtambua ni nani huyu anayewafikishia misaada mpaka majumbani mwao.

 

Wakati Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alipofariki ndipo hapo ikajulikana hawa wanaosaidiwa wenye shida hawapati misaada waliyokuwa wakipata, ndipo hapo wakajua kuwa aliyekuwa anawasaidia mpaka milangoni mwao alikuwa si mtu mwingine bali ni Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s . vile vile wakati Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alipolazwa wakati wa kuoshwa baada ya kufariki kulionekana mabegani mwake na mgongoni mwake alama zilikuwa zikionyesha kuwa alikuwa akibeba mizigo mizito kwa muda mrefu.

 

Na katika kipindi kimoja cha baridi kali sana yeye alikuwa amejifunika nguo ambayo ilikuwa inamsaidia asiisikie makali ya baridi wakati alikuwa ametoka nje ya nyumba anakwenda mahala fulani. Njiani alikutana na mtu ambaye alimwomba nguo hiyo ili naye aweze kujistiri na kujizuia dhidi ya makali ya baridi iliyokuwapo. Kwa maombi hayo Al Imam Zaynul 'Aabediin a.s. alimpa hiyo nguo naye akabaki bila nguo ya kujifunika au  kujuzuia na baridi.  Vile vile Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa kila mwaka akijifunika nguo ya kujizuia baridi na kipindi kilipokwisha alikuwa akiiuza na fedha zake zote zilizokuwa zikipatikana alikuwa akitumia katika kuwasaidia wenye kuhitaji misaada.”

 

Vile vile Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. alisema kuwa:

“Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s.  alikuwa akiwasaidia na kuwalisha na kuwatunza familia zaidi ya mia moja katika mji wa Madina. Na alipokuwa akikaa kula mayatima, wazee, wagonjwa na masikini walikuwa wakikaa kula naye pamoja na Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s., na vile vile alikuwa akiwafungia vyakula kwa ajili ya kuwachukulia wale waliokuwa majumbani mwao au kama baba ni mzee alikuja kula huko basi alifungiwa chakula awapelekee mke na watoto zake nyumbani.

 

Vile vile yeye yasemekana kuwa  alikuwa hakai kula pamoja na mama yake juu ya meza moja ya chakula na watu walipomwambia ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. wewe ni kigezo cha tabia njema na mfano bora katika Waislamu! Je kwanini hukai pamoja na  mama yako katika kula chakula?.

 

Al Imam Zaynul 'Aabediin a.s.  aliwajibu kuwa

“Mimi sikai na mama yangu kwa sababu yawezekana mama yangu akiangalia chakula moja labda akataka kuchukua na wakati huo mkono wangu ukawa mrefu kwenda kuchukua chakula hiki itakuwa kweli hiyo ni kitovu cha nidhamu na ndivyo maana yake ninajiepusha kukosa nidhamu mbele ya mama yangu.”

 

6. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa:

“Mtu anapotoa Sadaka  ya chakula kwa ajili ya kuwapa masikini na mafakiri basi mujue kuwa aina hiyo ya Sadaka  huondoa ufakiri na humwepusha mtu na kumuondolea ufakiri, na kuurefusha umri wake na humwepusha na aina sabini za vifo vya kutisha (ajali mbalimbali).”

 

7. Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Siku ya Qiyamah wakati kutakuwa na jua kali lichomalo basi watu aina saba watakuwa wamepewa kivuli na Allah swt na mmoja wao ni yule anayetoa Sadaka ya vyakula kiasi kwamba mkono wa kushoto haupati habari kuwa mkono wa kulia umetoa Sadaka.”

 

8. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa:

“Enyi Waislamu! Je niwaambieni mambo matano ambayo kwa hakika ni mema, maneno hayo yanawapelekeni hadi Jannat.?  

 

Ma-Sahabah wakajibu

“Naam lazima tuambie ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Naomba utuongoze.”

 

Kwa hayo Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. akasema:

“Mnapopatwa na misiba basi lazima ufanye subira na mujaribu kuficha, mutoe Sadaka kiasi kwamba mkono wa kulia unapotoa mkono wa kushoto usipate habari, muwatende mema wazazi wenu, na kwa hakika katika mambo hayo ndiyo kuna furaha ya Allah swt na kila mara mwezavyo kusema semeni La Haula wala Quwwata illa billahil ‘Aliyil ‘Adhiim  kwa hakika hiyo ni  hazina moja kubwa katika hazina za Jannat, na vile vile katika nyoyo zenu muwe na mapenzi ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja na Ahlul Bayt a.s.

 


14. KUTOA SADAKA USIKU NI SUNNAH

 

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. daima ilikuwa akitoka usiku katika kiza huku amejitwisha mafurushi ya mapesa na vyakula kwa ajili ya kwenda kugawa kwa masikini katika mji wa Madina, alikuwa akiwafikishia misaada waitaji walipokuwa. Na siku ambayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliaga dunia, watu wakaona misaada imesimama na watu hawakufikiwa na misaada hiyo ndipo walipokuja kujua kuwa misaada hiyo ilikuwa ikiletwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ambaye daima alikuwa akificha uso wake ili watu wasijue kuwa ni yeye anayewafikishia misaada hiyo.

 

2. Mu’alla ibn Khuns anasema kuwa:

“Usiku mmoja kulikuwa kukinyesha manyunyu ya mvua, nikamwona Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akielekea katika makazi ya Banu Sai’d nami nikajaribu kumfuata nyuma kisirisiri na mara nikasikia katika giza kizito hicho kama kitu kimedondoka na nikamsikia Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akisema:

‘Ya Allah swt! Ninaomba vitu hivi nivipate tena.’

 

Na hapo mimi nikatokezea karibu ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.,  nikatoa salamu. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. baada ya kuitikia salamu akaniambea je wewe ni Mua’alla ?

 

Nami nikamjibu :

‘Ndiyo ewe Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ! Niwe fidia juu yako.

 

Hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akaniambia:

‘Naomba uniokotee vitu hapo chini unisaidie.”

 

 Mu’alla anasema mimi katika giza kizito hicho nikaanza kupapasa aridhini na nikakuta kumbe ni vipande vya mikate na wakati ninamkabidhi Imam a.s mikate  nilivyo viokota katika giza  kali nilihisi kifurushi alichokuwa nacho migongoni mwake kilikuwa kizito mno na hivyo nilimwomba Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Lakini hakukubali  nimsaidie kubeba kifurushi hicho.”

 

 

Lakini Imam a.s alikataa akaniambia

“Ninapendelea kuubeba uzito huu mimi mwenyewe kwa sababu huu ndiyo utakao kuwa ufanisi wangu katika siku ya Qiyamah na bora kwangu na hivyo unaweza kuja nami katika safari hii.”

 

Tulipokaribia katika makazi ya Banu Sa’id, Imam a.s. alikwenda kwa kila mmoja ambaye ni mwenye shida akamwekea mikate miwili na akarudi. Na wakati huo akaniambia kwa kutoa Sadaka usiku kunatuliza ghadhabu za Allah swt, na Allah swt usamehe madhambi makubwa, na kusahilisha hesabu katika siku ya Qiyamah.”

 

3. Zuhri anasema kuwa: 

“Siku moja wakati wa baridi kali mno na ukungu ulikuwa umejaa mwingi mno mimi nilimwona Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. akiwa amejitwisha kifurushi kikubwa cha chakula na mzigo mkubwa wa kuni.

 

Nami sikusita nikamwambia ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Je nini haya?’

 

Imam a.s akanijibu nina nia mpango wa safari, na hivyo ndivyo ninavyojitayarisha kwa ajili ya mahitaji yangu.

 

 Zuhri akasema:

‘Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Mimi nakupa mfanyakazi wangu ambaye atakusaidia kukubebea mizigo yako hiyo mizito.”

 

Al Imam Zaynul 'Aabediin a.s. alimkatalia nami nikamwambia,

“Basi nipe mimi mwenyewe nikupunguzie kukusaidia kukupunguzia huu mizigo. Kwa hayo Imam a.s. akajibu, lakini kwa kufanya hivyo mimi sitakuwa nimetoka katika wajibu wa kufika mwisho wa safari yangu vile inipasavyo kufika, kwa hiyo naomba uendelea na shughuli zako uniache peke yangu.”

 

Zuhri anasema:

“Baada ya kufika siku chache mimi nilipomwona Imam a.s nikamwambia,

“Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Mimi sioni kama wewe ulikwenda safari yoyote ile.”

 

Imam a.s akamjibu:

“Naam ! Vile uchukuliavyo sivyo. Muradi wangu ulikuwa ni safari ya Aakhera. Mimi nilikuwa nikijitayarisha kwa ajili ya safari ya Mauti. Kumbuka kwamba kujikumbusha na kujitayarisha kwa mauti basi mambo mawili ni muhim, kwanza kujiepusha na yaliyo haramishwa na pili ni kutoa muhanga wa mali katika njia ya Allah swt.”

 

4. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. katika baadhi ya misemo yake anasema.:

·         “Toeni Sadaka  kwa basabu kunatuliza ghadhabu za Allah swt .

 

·         Toeni Sadaka  katika njia ya Allah swt mngejariwa kwa sababu ya riziki muliyojaaliwa na Allah swt kwa kufanya hivyo nyinyi mtahesabiwa katka wale wanaopigana katika njia ya Allah swt.

 

·         Yeyote yule ambaye ana imani kamili kuwa Allah swt hulipiza kile kinachopendwa na Mumin basi huyo mtu lazima ataitia  nafsi yake katika shida na kwa kufanya mema.

 

·         Muwatibu wagonjwa wenu kwa Sadaka .

 

·         Muilinde na  muihifadhi na kulinda mali yenu kwa kutao zaka[48].  

 

·         Urekebishe matumizi na mahitaji ya maisha yenu ili mweze kupima vyema.

 

·         Kuwaza na mawazo ni nusu ya uzee unaoletwa nawe.

 

·         Mwenye matumizi yenye mahesabu yaani anayebana matumizi kamwe hawezi kuwa mwenye shida na dhiki.

 

·         Kumsaidia yule ni mtu ambaye anaheshima na mkuu na kumsaidia yule ambaye ana madeni haya maneno mawili hayana kifani yoyote.

 

·         Kila jambo lina mazao yake, kwa hiyo mazao ya mema  na  kuwa na nia  katika  kutumia mali au chochote katika njia ya Allah na kwa ajili ya Allah swt basi mazao yake ni kwamba kufanya haraka kutekeleza azma hiyo na kamwe usifanye kucheleweshwa.

 

·         Muongezee na mupanue riziki yenu kwa kutoa Sadaka, kabla hamjaijiwa na balaa, mwombe dua na kwa hakika mtaweza kujiepusha  nayo na  kujiokoa nayo.

 

 


15. MUJIPATIE FADHILA KWA KUTOA Sadaka  KATIKA SIKU TUKUFU NA MWEZI WA RAMADHANI.

 

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Kutoa Sadaka  siku ya Ijumaa kuna thawabu na  fadhila kubwa sana.”

 

2. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Msimkatalie masikini anayeomba siku ya ‘Arafah. Lazima mpeni chochote kile.”

 

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Mtu yeyote atakaye kuwa ametoa Sadaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, basi yeye atakuwa ameepukana na balaa za aina sabini.”

 

 


16. JE SADAQAH  ITOLEWE WAKATI GANI?

 

1. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa ameulizwa na mmoja wa Ma-Sahaba wake,

“Ewe Mtume wa Allah swt! Ni Sadaka  ipo iliyo bora kabisa  kuliko zote!”

 

Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alijibu,

“Sadaka  iliyo bora ni ile ya wakati ule ambapo mtoa Sadaka  yuko salama u salimini, mwenye afya kamili na anayeishi maisha mema bila wasiwasi, na ambaye anauogopa umasikini.

 

Na wala msicheleweshe kiasi kwamba mpaka kwamba mwisho wa maisha yenu yameisha wafikia shingoni, na hapo ndiyo mnaanza kutoa usia kuwa kiasi fulani mpe masikini fulani na fulani mpe kiasi fulani na kadhalika. Kama tunaelewa kuwa mtu fulani kweli ni mstahiki wa msaada au Sadaka sasa kwa nini tusubiri mapaka sisi tunataka kufa ndiyo basi tuseme msaidieni wakati shida alikuwa nayo tangu hapo zamani?”

 

2.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliombwa na mtu mmoja kuwa ampatie nasiha, na hivyo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwambia:

“Tayarisha matayarisho yako ya safari, na matayarisho yako hayo yatume kabla wewe hujaenda safari. Jifanyie matendo yako mwenyewe yaani kama unataka kufanya mema uyatende mema kabisa katika uhai wako na mambo yoyote yale ambayo  unayoona yanafaida kwako uyatende wewe mwenyewe na wala usiwatupie wengine kama unaweza kujitimizia wewe mwenyewe.[49]

 

3.  Kwa kuzungumzia swala tulilozungumziwa hapo No. 2  hapo juu siku moja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa amekwenda katika ghala la mtu mmoja ambaye alikuwa amefanya usia kuwa baada ya kifo chake maghala yake yote yaliyokuwa yamejaa kwa tende yagawiwe Sadaka  kwa masikini. Na baada ya kifo chache ikatekelezwa usia wake na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipokwenda kule baada ya kufagia akakuta kokwa moja ya tende imebakia mguuni mwake basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akainama akalichukua kokwa hilo la tende moja  akasema:

Kama mtu huyu katika uhai wake angelikuwa amegawa kokwa hii moja ya tende basi angepata thawabu zaidi  kuliko hata  mlima mkubwa kabisa wa Uhud.”

 

 


17. MSIMRUDISHE ANAYE KUJA KUOMBA USIKU

 

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwayah kutoka kwa mababu zake a.s. kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akisema:

“Pale anapokuja mtu yeyote usiku kugonga mlango kwa nia ya kuomba msaada, basi msimvunje moyo, msaidieni na hasa inapokuwa mwombaji aliyekuja ni mwanaume.”

 


18. KATIKA IBADA ZOTE ZA SUNNAH  SADAKA  INAONGOZA.

 

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Allah swt kwa kila kazi amemweka mweka-hazina ambaye anaweka mahesabu yake isipokuwa Sadaka, ambaye mahesabu yake na utunzaji wake anaweka Allah swt mwenyewe. Baba yangu mzazi wakati alipokuwa akimpa chochote mwombaji alikuwa akikichukua tena na alikuwa akiubusu mkono wa  huyo mwombaji, na alikuwa akiunusa kwa hamu sana, na ndipo baadaye alipokuwa akimrudishia na kumpa kitu hicho hicho.”

 

2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema:

“Allah swt amesema  kuwa mimi nimewateua mawakili kwa kila jambo na ambao ndio wanaosimamia na kuweka ripoti zake isipokuwa Sadaka ambayo mimi mwenyewe ndiye ninayetunza habari zake.”

 


19. AINA ZA SADAQAH.  

 

1. Mu’alla bin Khunais amesema kuwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alikwenda katika makazi ya Banu Sa’id na wale wote waliokuwa na shida aliwawekea mikate na kuondoka zake. Hapo mimi nilimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.:

Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu :

“La! Hawa kama wangekuwa marafiki na wapenzi wetu na wafuasi wetu basi ningewaongezea kiasi cha punje ya chumvi”. [50]

 

Hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliponielezea kwa uwazi zaidi kwamba siku moja Mtume ‘Isa bin Maryam a.s. alikuwa akipita ufuoni mwa bahari, na akatoa mkate kidogo kutoka kifurushi chake akatupa baharini. Baadhi ya wale aliokuwa nao wakamwuliza!

“Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Je umefanya nini bwana? Nini maana ya kutupa mikate baharini?

 

Mtume Isa a.s akawajibu:

“Katika bahari kuna viumbe vya Allah swt na iwapo kutatokezea na viumbe vyovyote vitakavyo kula humo kutokana na nilichowatupia basi kwa hakika katika ufalme wa Allah swt nitakuwa na thawabu nyingi mno.”

 

2. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s.  amesema:

“Pozeni nyoyo zenu kwa sababu ya kiu kali kwani Allah swt hupendezewa sana na tendo hilo. Kwa hakika amebahatika yule mtu ambaye anawamalizia kiu wanyama kwani yeye siku ya Qiyamah  atapata msaada mkubwa sana atakapokuwa katika hali ya kiu.”

 

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alikuwa akifunga safari baina ya Makkah na Madina, akaona kuwa kulikuwa na mtu mmoja aliyejitupa chini ya mti mmoja. Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwamwambia mtu mmoja aliyekuwa naye, aende akamwulize hali yake, inawezekana labda alikuwa na kiu kali. Mtu huyo alipomwendea huyo mtu aliyekuwa amelala chini ya mti na kumwuliza hali yake basi ikajulikana kuwa mtu huyo alikuwa na kiu ya maji. Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimnywesha maji na akaondoka  kuendelea na safari yao. Yule aliyekuwa naye safarini akasema,

“Ewe  mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. !  Huyu mtu alikuwa ni Mnasara, watu kama hawa pia tunaweza kuwasaidia na kuwapa Sadaka?”

 

 Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamjibu

“Naam ! Katika mazingira kama haya inawezekana.”

 

4. Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa pamoja na wafuasi wake nao katika safari, na waliketi kwa ajili ya kula chakula. Na akatokezea swala mmoja ambaye alikuwa akitafuta chakula, Imam a.s. akamwambia huyo

‘Swala njoo karibu, njoo ule nasi! Usiwe na wasiwasi utulie na ujue hapa kwetu hautakuwa na hofu yoyote, upo katika usalama.”

Kwa kusikia hayo Swala huyo alimsogelea Imam a.s. na alikula pamoja nao.

 

5. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa Siku moja baba yake alikuwa pamoja na wenzake katika bustani yake na walipoketi  kula  chakula na  mara akatokezea Swala mmoja aliyekaribia.

 

Hapo Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. . ambaye ni baba yake na  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. akasema:

“Ewe Swala, jina langu mimi ni Al Imam Zaynul 'Aabediin bin Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  na mama yangu Bi Fatima az-Zahra a.s., njoo ushiriki nasi katika kula. Na Allah swt kiasi alichokuwa amemjaalia cha chakula  huyo Swala alikula.”

 

6. Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  amesema:

“Hakuna mtu yeyote mwingine isipokuwa ni Mwislamu tu anayeweza kuchinja wanyama wenu wa dhabihu siku ya Iddi na  Sadaka, na unapotoa Sadaka  katika kutoa humo lazima wapewe Waislamu tu. Na unapotoa Sadaka  katika mali zinginezo unaweza kuwapa Kafir Zimmi  ambao wenye kuhitaji misaada hiyo.”

 

 


20. KUWASAIDIA MAJAMAA NA NDUGU KUNA THAWABU ZAIDI. 

 

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripoti riwayah moja kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa mtu mmoja alimwuliza Mutume s.a.w.w. :

“Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Je ni Sadaka  ipi iliyo bora kabisa?”

 

Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alijibu:

“Sadaka  ile ambayo watakayo pewa wale jamaa na ndugu ambao hata kama alikuwa amekorofishana nao au amegombana nao au hawana uhusiano nao kwa sababu ya magomvi.”

 

2. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Iwapo wewe unatoa kumi kwa ajili ya Sadaka , basi ili kuwasaidia Mumin toa kumi na nane na yule ambaye hawezi kabisa msaidie kwa ishiririni na kwa ajili ya kuwasaidia jamaaa na ndugu kwa wema  utoe ishirini na nne.”

 

3. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema Riwayah kutokea  kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  kuwa amesema:

“Mtu yeyote atakaye wasaidia jamaa na ndugu zake katika kwenda Kuhijji au ‘Umra, basi Mtume Allah swt atamjaalia thawbu za Hijja mbili na ‘Umra mbili, na yoyote yule atakayemsaidia ndugu yake Mumin basi Allah swt atamlipa kusiko na kifani.”

 

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameseama kuwa:

“Iwapo mtu atawasaidia jamaa au ndugu zake ambao wana shida ni muhtaji basi hiyo siyo Sadaka.”

 

5. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwayah moja ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akisema:

“Kwa mtu yeyote yule ambaye atakwenda mwenyewe kwenda kumsaidia jamaa au ndugu yake mwenye shida na kutoa kitu chochote kwenye mali yake na kumsaidia  basi Allah swt atamjaalia ujira wa mashahidi mia moja na kwa kila hatua atakayotembea atamwandikia mema elfu arobaini,  na kiasi hicho hicho cha maovu yake yatasamehewa. Na vile vile kiasi hicho hicho ataongezewa daraja lake mbele ya Allah swt na atamwandikwa miongoni mwa wale waja wake halisi waliofanya ibada yao kwa uhalisi kwa muda wa miaka mia moja.”

 

6. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., aliulizwa na mtu mmoja :

“Ewe Mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Je yeyote yule anayekuja kuomba mlangoni anastahili kupewa Sadaka au badala yake tuwape jamaa na ndugu zetu Sadaka  hiyo?”

 

Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliwajibu :

“Kwa hakika kuwapelekea msaada Sadaka  jamaa  na ndugu wa mtu zina thawabu nyingi zaidi.”

 

7. Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s. aliandikiwa barua na mtu mmoja akimwuliza

“Iwapo mtu anaweza kunuia  kuwa mimi katika mali yangu nitatoa sehemu fulani ya mali nitamsaidia mtu fulani na katika kipindi hicho iwapo atakuja kujua kuna mtu katika ndugu na jamaa zake ambaye ni kweli anashida na anahitaji msaada wake basi je huyo mtu anaweza kubadilisha nia yake ya kumsaidia jamaa yake badala ya kumpa mtu aliyekuwa amenuia hapo kabla?”

 

Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s. akamjibu kuwa:

“Utaangalia ukaribu wa watu hao na yule aliye karibu nawe katika madhehebu umpatie na lau kama wote wawili kama watakuwa wanatokana na dhehebu  moja tu basi kwa mujibu wa kauli ya Al Imam Musa al-Kadhim a.s. kuwa kugawanywe kati kati yaani watu wote wawili wapewe nusu kwa nusu, kwa sababu iwapo kutakuwa na jamaa na ndugu ambao wana shida na taabu basi huwezi kutoa Sadaka  na kuwapa wengine. Na kwa hakika kwa kufanya hivyo utakuwa umepata thawabu na fadhila za Sadaka.”

 


21. IWAPO MWOMBAJI HAUMJUI MPE Sadaka  KIDOGO ILI AWEZE KUWA NA HURUMA NA MAADUI  WA AHLUL BAYT a.s. WASIPEWE Sadaka  

 

1. Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s. aliandikiwa barua na mtu mmoja akimwuliza kuwa:

“Je inawezekana mimi nikatoa Zaka au Sadaka  kutoka mali yangu nikampa mtu ambaye si jamaa wala ndugu yangu?”

 

 Na kwa hayo Imam a.s. alimjibu:

“Usimpe Zaka au Sadaka  mtu yeyote mwingine  isipokuwa wenzako na majamaa zako.”

 

2. Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s. aliulizwa:

“Je inawezekana kumpa Sadaka  Nasibi (maadui wa Ahlul Bayt a.s. )?”

 Imam a.s akamjibu kuwa:

“Musiwape Sadaka  wala Zaka maadui wa Ahlul Bayt a.s. na ikiwezekana hata maji pia msiwape.”

 

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliulizwa kuwa:

“Je inaruhusiwa kumlisha mtu kama humwelewi kuwa ni Mwislamu au si Mwislamu?”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akajibu kuwa :

“Mtu ambaye humwelewi na kama huelewi chochote kuhusu urafiki au adui, basi yeye unaweza kumpa. Kwa sababu Allah swt anasema tuwatendee watu mema. Lakini yule aliye mpingamizi wa haki au ambaye anaelekea kuhusu upotofu na madhambi au anayewachukua watu kuelekea upotovu na madhambi, huyo msimpe.”

 

4. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliulizwa kuwa:

“Mara nyingi tunaona masikini wanaokuja kuaomba, lakini sisi tunakuwa hatuwafahamu, Je watu kama hawa tunaweza kuwapa?”

 

 

 

 

 Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliwajibu

“Kama wewe moyoni mwako utaingiwa na huruma  kwa ajili ya mtu huyo basi unaweza kumpa, ingawaje hata kama si kamili lakini hata kidogo itafaa.”

 

5. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Kidhahiri wapo waombaji wengi ambao (wengi wanatoka vijijini na maeneo karibu ya mji ) hivyo nyie muwape Sadaka watoto, wanawake, wagonjwa, wadhaifu na wazee.”

 

6. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Mnapoijiwa na masikini kwa ajili ya kuomba ambao ni wazee kabisa na wanawake na watoto na wasichana wadogo basi muwasaidie Sadaka na vile vile muwasaidie Sadaka  wale mnaoijiwa huruma mioyoni mwenu.”

 

7. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliulizwa kuwa:

“Mijini mwetu wanakuja waombaji wengi sana kutoka vijiji na vitongoji ambavyo viko karibu na mji ambamo humo wamechanganyikana Mayahudi,Manasara, Wakristo na hata Majusi (Wanaohabudu moto) sasa katika sura hii je tunaweza kuwasaidia Sadaka ?”

 

Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alijibu :

“Naam ! Mnaweza kuwapa.”

 

8. Al Imam 'Ali an-Naqi a.s. aliandikiwa barua na humo akaulizwa:

“Je tunaweza kuwasaidia wale masikini waliopo mitaani ambao hatujui dini na wala Madhehebu zao?”

 

Kwa hayo Al Imam 'Ali an-Naqi a.s. aliwajibu:

Kama mtaweza kuwatambua wale maadui na wenye chuki na Ahlul Bayt a.s. na mukiwasaidia basi Allah swt hatakulipeni chochote  ama wale ambao nyie hamuelewi Madhehebu yao basi hakuna matatizo yoyote katika kuwapa Sadaka.  Na muwasaidie masikini wale wowote wanaoomba kama mtaingiwa na huruma mioyoni mwenu. Hata kama hamtaweza kuwaelewa dini na madhehebu zao… Insha-Allah hakuna tatizo lolote katika  kutoa Sadaka  katika sura kama hizi.”

 

9. Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimwambia muhudumu wake:

“Yeyote yule anayekuja kuomba nyumbani kwake basi asimruhusu akaondoka hadi pale ahakikishe kuwa amemlisha chakula, hususan siku ya Ijumaa.”

 

Mwandishi anasema kuwa mimi nilimwambia Imam,

“Ewe mjukuu wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Kila mwombaji huwa si msitahiki.”

 

Kwa hayo Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alinijibu

“Ninaogopa kuwa inawezekana mwombaji akawa msitahiki lakini mimi nikamfukuza, isije tukapata matatizo na dhiki iliyo mpata Mtume Ya’aqub a.s na nyumba yake.”

 

 


22. KUMRUDISHA MASIKINI NI KARAHA HATA KAMA USTAHIKI WAKE UTAKUWA MASHAKANI, LAKINI LAZIMA APEWE CHOCHOTE, NA KAMA HAKUNA CHOCHOTE CHA KUMPA BASI UNAWEZA KUMWONDOA KWA MANENO MAZURI NA MATAMU.

 

1. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Msimvunje moyo mwombaji hata kama atakuwa amekuja kuomba katika usafiri wa farasi.”

 

2. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Iwapo mtoaji atakuwa anajua wema na fadhila za kutoa Sadaka  basi kamwe hatamrudisha mtu yeyote bila ya kumpa kitu chochote.”

 

3. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Kamwe msiwarudishe mikono mitupu waombaji. Iwapo waombaji wengine wasingekuwa waongo na wadanganyifu basi kamwe wengine wasingerudipo.”

 

4. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  kamwe hakumrudisha masikini yeyote aliyemwomba asaidiwe Sadaka. Na kama Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa hana chochote cha kumpa basi alikuwa akimwambia kwa lugha tamu Allah swt atakujaalia Insha-Allah.”

 

5. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Mtume Ibrahimu a.s. daima amekuwa akiwahudumia na kuwakarimu wageni, na pale alipokuwa hakuwapata wageni wowote wale, basi alikuwa akifunga mlango wake na akitoka kwenda kuwatafuta wageni.”

 

Na katika hadithi hiyo hiyo tunapata wakati mmoja Malaika Jibrail alimwijia Mtume Ibrahim a.s. na kumwambia :

“Allah swt amenituma safari hii kwa mja wake mmoja ambaye ameweka marafiki Wake kama ni Khalil Wake.”

 

Kwa hayo Mtume Ibrahim a.s. akaingiwa na shauku ya kutaka kumjua na akasema :

“Tafadhali sana naomba unitambulishe huyo umzungumzaye, nami nitapenda kwenda mbele yake.”

 

Jibrail a.s. akasema :

“Ewe Khalil (rafiki)! Ndiwe wewe tu !”

 

Basi Mtume Ibrahim a.s. akamwambia :

“Ewe Jibrail a.s. ! Je kwanini umenifanyia hivyo ?”

 

Hapo Malaika Jibrail a.s. akamjibu :

“Kwa sababu wewe kamwe haujamnyooshea mkono yeyote, na wewe daima haujawahi kumkatalia yeyote aliyekuja kukuomba.”

 

6. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema sema kuwa Mtume Allah swt alikuwa akisema

“Kamwe msimrudishe mikono tupu mwombaji. Hata kama mtakuwa katika hali ya ugumu kiasi gani.

 

7. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa Mtume Musa a.s. wakati alipokuwa akimlilia Allah swt, Allah swt alimwambia :

“Ewe Musa hata kwa ukimpa kidogo mpe ili utunze heshima ya mwombaji,  na kama hicho pia hauna basi kwa maneno matamu na kauli nzuri umwambie na kumwomba msamaha. Kwa sababu miongoni mwa waombaji mara nyingine si lazima atokane na binadamu au Majini bali anakuwa ni Malaika wa Rehema. Kwa hiyo Malaika huyo ndiye anaye wajaribu watu na kile nilicho kushauri ndiyo ujaribu kutegemea kupata jibu lake na huwa anawaombeamo kwa hivyo, ewe mwana wa Imran  angalia vile tabia yako itakavyo kuwa”.    

 

8. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa riwaya kuwa siku moja mtu mmoja alikuja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuomba kwa hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliwaangalia Ma-Sahaba wake  na kuwaambia,

“Enyi Ma-Sahaba wangu ! Msaidieni.”

 

Na mmoja katika Ma-Sahaba wake akamsaidia kifaa cha dhahabu. Aliyekuja kuomba akasema

“Je leo ni --  yako?”

 

Yule Sahaba wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akajibu :

Naam ndiyo maana yake”.

 

Yule mwombaji akasema:

Mimi nimekubalia hivyo. Mimi si Jini wala si binadamu; bali mimi ni Malaika niliyetumwa na Allah swt nije nikujaribu na kwa hakika nimekuona wewe miongoni mwa watu wenye kushukuru neema za Allah swt. Mungu akujaalie kila la heri.”

 

9. Sa’ad bin Musayyab anasema kuwa Siku moja wakati wa swala ya asubuhi yeye alikuwa pamoja na Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s., akatokezea mwombaji mmoja na wakati huo Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. akasema:

“Mpeni huyo mwombaji---- kumbukeni kuwa---kamwe msimwondoe mwombaji  katika hali ya kuhuzunika yaani msimwondoe mwombaji bila kumpa chochote”.

 

10. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ananakili riwaya kutoka baba yake mzazi a.s. kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa:        

“Mruhusu mwombaji aondoke hata kwa kidogo na kwa  mapenzi na kwa huruma pia. Kwa sababu mara nyingi anayekuja kuomba huwa si kutoka binadamu au Majini bali huwa ni njia moja kwa kuwajaribia nyie kwa ajili ya kuwaongezea neema.”

 

11. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Nahjul Balagha :

“Masikini anapokuja kwenu basi anakuwa ni mjumbe wa Allah swt na yeyote yule atakaye muudhi na atakayemhudhunisha basi atakuwa amemhudhunisha Allah swt na yeyote yule atakaye kuwa amempa chochote basi ajue kuwa amempa Allah swt”.

 

12. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anaripoti kutoka kwa wazazi wake a.s ambao wamesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Wakati ‘Ummah wangu utakapogeuza uso au utakapo wageuzia uso wale wanao hitaji msaada wao na watakapoanza kutembea kwa maringo basi wakati huo Allah swt atasema: kwa kiapo cha utukufu na ukuu wangu hawa watu watakomeshana wao kwa wao na hivyo ndivyo nitakavyo waonjesha adhabu yao.”

 

 


23. BAADA YA KUMSAIDIA MASIKINI MARA TATU UNAWEZA KUMWAMBIA AONDOKE.

 

1. Walid bin Sahib anasema kuwa:

“Siku moja mimi nilikuwa kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. na hapo akatokezea mwombaji mmoja. Imam a.s alimpa chochote huyo mwombaji na akatokezea mwombaji wa pili naye akapewa chochote. Hivyo hivyo akatokezea mwombaji wa nne basi Al Imam a.s akamwambia Allah atakusaidia upate zaidi njia yako atakupanulia. Na baada ya hapo Imam a.s akasema iwapo mtu atakuwa na Dirham takriban elfu thelathini au arobaini, na akanuia akawa na mpango wa kuzitumia zote ambazo kimatokeo hatabakiwa na chochote basi mtu kama huyo atawekwa miongoni kwa wale watu ambao Allah swt huzitupiliambali dua zao.”

 

Kwa hayo mimi nikasema

“Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Je ni makundi gani ya watu hawa watatu?

 

Kwa hayo Imam a.s akajibu

“Mmoja wao ni yule ambaye ana mapesa na mali na baada ya kutumia vyote anaomba ‘ewe Mola wangu naomba unipe riziki’. Basi  hapo Allah swt anamjibu  ‘Je mimi sikukupanulia njia na kukuwekea sababu za wewe kujiwekea riziki yako?”

 

2. Ali ibn Hamza anasema kuwa:

“Mimi nilimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. swali kuwa yeye amesikika akisema mwalishe watatu---- na kama mnataka kuwapa chochote zaidi muwape ama sivyo nyie mmeshatimiza haki ya siku yenu hiyo”.

 


24. HAWEZI KURUDISHA Sadaka NA BAADA YA KUMTOA MTUMWA KAMA Sadaka  HUWEZI KUMCHUKUA TENA KATIKA MILIKI YAKO.

 

 

1. Walid bin Sabih daima alikuwa akisema kuwa:

“Mtu yeyote anayetoa Sadaka  na iwapo Sadaka  hiyo itakubaliwa au Sadaka  hiyo itarudishwa basi yule mtoa Sadaka  haruhusiwi kuila au kuitumia tena hiyo Sadaka  kwa ajili yake. Na badala yake hana njia yoyote isipokuwa aigawe Sadaka    kwa mtu mwingine. Hatakuwa na ruhusa kwa vyovyote vile vya kuitumia hiyo Sadaka  isipokuwa Sadaka  itatolewa tena Sadaka  kwa mtu mwingine. Vile vile mfano wake inachukuliwa kuwa mtu anapomfanya huru mtumwa katika njia ya Allah swt na kwa ajili ya kutaka furaha ya Allah swt basi kamwe hawezi kumchukua tena yule mtuma(aliyefanywa huru) akamfanya  mtumwa wake. Na baada ya kumfanya huru mtumwa na mtumwa atakapo rudi kwake basi hawezi kumweka vile alivyokuwa amemweka mwanzoni kabla ya kumfanya huru katika njia ya Allah swt. Na vivyo hivyo ndivyo swala hizi zinausiana na Sadaka pia.”

 

2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.  amesema:

“Yeyote yule atakayekuwa ametoa Sadaka  na iwapo Sadaka  hiyo itamrejea yeye tena basi yeye mwenyewe hataweza kuitumia wala hataweza kuiuza, kwa sababu kitu hicho kilishatolewa katika njia ya Allah swt na kwa ajili ya ridhaa ya Allah swt na hivyo hakuna kitakachoweza kushirikishwa katika swala hilo, na mfano wake pia ni sawa na ule wa kumfanya huru mtumwa hivyo hataweza kurudishwa tena katika utumwa.”

 

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema

“Iwapo mtu atanuia kutoa Sadaka kwa ajili ya mtu fulani anayeuhitaji msaada huo na wakati huo akapata kujua kuwa mtu huyo ameshaondoka, basi hawezi kuirudisha na kuichanganya hiyo mali katika mali yake na badala yake itambidi amgawie mtu mwingine.”

                                  

4.  Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa: Kuna mtu alimwuliza iwapo mtu alimfanya huru mtumwa bado ambaye hajafikia umri wa kubalehe je sheria inasemaje?

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu

“Hakuna tatizo lolote ndani yake lakini sheria itakayotumika hapo ni kama ile ya kutoa Sadaka  (yaani baada ya kumfanya huru mara moja hauwezi kumrudisha katika utumwa tena).”

 

 

 


25. NI SUNNAH KUWAAMBIA WAOMBAJI WAWAOMBEENI DUA NA VILE VILE NI SUNNAH KWA MWOMBAJI PIA KUWAOMBEA DUA WANAO WASAIDIA.

 

1.      Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. amesema:

“Dua ya mtu msiidharau au kusema kuwa haifai chochote. Mara nyingi dua muliyoombewa na Mayahudi au Manasara hukubaliwa. Ingawaje inawezekana kwa dua aliyo jiombea yeye mwenyewe haiwezi kukubalika.”

 

2.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Wakati mnapo wasaidia waombaji, muwaombe wawaombeeni dua hata kama dua zao wenyewe hazikubaliki kwa ajili yao wenyewe, mradi kuna uwezekano mkubwa kwa dua zao kwa ajili yenu zikakubalika.”

 

3.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakiliwa na Abu Basir riwaya moja kuwa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Wakati mtu anapomsaidia fakiri mwenye shida sana asiye na uwezo, na pale fakiri huyo anapomwombea dua, basi dua hiyo lazima inakubaliwa na Allah swt.”

 

4.      Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Wakati mnapowapa chochote waombaji; basi muwaombe wawaombeeni dua, kwa sababu inawezekana kwa sababu ya udanganyifu na ulaghai wake dua zake zenyewe kwa ajili yake zisikubaliwe lakini kwa ajili yenu dua zake zitakubaliwa.”

 

5.      Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s.:

“Alikuwa akimwambia mfanyakazi wake, zuia kwa punde kidogo sadaka, ili mwombaji amalize kuomba dua.”

 

6.      Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. Na vile vile amesema:

“Dua ya fakiri na mwombaji kamwe hairudishwi au haitupiliwi mbali.”

 

7.      Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. amemwamrisha mfanyakazi wake kuwa:

“Wakati unapowapa chochote waombaji basi muwaambie wawe wakituombea heri.”

 

8.      Al-Imam a.s. amesema:

“Wakati muwapapo chochote masikini na waombaji basi muwe mukiwaomba wawaombeeni dua kwa sababu wanapo waombeeni dua kwa ajili yenu dua zao hukubalika na inawezekana dua zao kwa ajili yao wenyewe hazikubaliki.”

 

 

 


26. KUSAIDIA KUWAFIKISHIA SADAQAH WANAO HITAJI NI SUNNAH.

 

1.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

   “Iwapo mtu atapewa msaada ikapitia mikono themanini hadi ikamfikia aliye

    mustahiki basi kila mkono utapata haki sawa sawa ya malipo.”

 

2.      Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Bora ya sadaka zote ni ile ambayo binaadamu baada ya kujitimizia mahitaji yake kwa moyo mkunjufu anatoa sadaka.”

 

3.      Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Yule atakaye fikisha msaada katika hali nzuri kwa mwenye kustahiki basi huyo mfikishaji wa sadaka atapata thawabu sawa kama za yule atakaye toa sadaka yake – hata kama katika kufikisha msaada huo kwa anayestahiki itachukua mikono elfu arobaini basi wote watapata malipo sawa kabisa kwani Allah swt hana upungufu wala kasoro ya aina yoyote ile, na wale watu wanaofanya Taqwa na kutenda mema basi laiti kama mungeweza kuelewa uhakika wa swala hili.”

 

4.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Watoaji ni wa aina tatu

·         kwanza ni Allah swt mwenyewe ambaye anatoa kwa ajili ya malimwengu zote.

·          Pili ni yule mwenye mali na

·         tatu ni yule msaada unaopitishwa katika mikono yake au ni mtu ambaye anafikisha misaada hiyo.”

 

5.      Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amenakiliwa riwaya na Abu Basir kuwa amesema:

“Watoaji ni wa aina tatu wa

·        kwanza kabisa ni Allah swt,

·         wa pili ni yule ambaye anatoa kutoka mali yake na

·        tatu ni yule anayefikisha kama msaidizi katika kufikisha msaada huo kwa mustahiki.”

 


27. KUTOA KATIKA MALI YAKO KWA AJILI YA KUMSAIDIA MUUMIN NI SUNNAH.

1.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Allah swt amefaradhisha kwa waja wake kwa kusisitiza kuwa kama yafuatavyo,

·         kwanza uadilifu na mapenzi yake pamoja na muumini mwenzake kama vile ajipendeavyo yeye kwa ajili yake ndivyo ampendee muumini mwenzake.

·         pili awe ameweka hisa fulani au kiasi fulani katika mali yake kwa ajili ya kutaka kumsaidia muumin ndugu  mwenzake. Na

·          tatu kumukumbuka Allah swt katika kila hali na hapa haimaanishi kuwa kwa kumsifu Allah swt peke yake au kwa kutoa uradi (tasbihi) bali hapa kuna maanisho ya kuwa kufanywe kwa kimatendo kabisa yale yaliyoelezwa katika dini yakiwa ni sehemu ya imani ya mtu.”

 

4.      Aban ibn Taghlib anasema kuwa Siku moja yeye alimwomba Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amwelezee haki za muumini mmoja juu ya muumini mwingine. Kwa hayo Imam a.s. alimjibu :

“Ewe Aban! Achana nayo, usini shurutishe kukujibu ulicho uliza.

 

Nami nikamwambia :

 “Ewe Mola wangu niwe fidia kwako.”

 

Na baada ya hapo niliendelea kumsisitiza Imam a.s. anielezee na ndipo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alipoanza kuniambia :

“Haki ya muumini mwenzako juu yako ni kwamba nusu ya mali yako iwe ni mali yake.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akagundua kuwa rangi ya sura yangu imebadilika na akaniambia,

 “Ewe Aban je huna habari kuwa Allah swt ameelezea habari za wale watu ambao wamezipenda nafsi za watu wengine kuliko hata nafsi zao?”

 

 

Nami nikamujibu

“Bila shaka, niwe fidia juu yako.”

 

Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akaendelea kujibu,

“Kwa hivyo nyie toeni nusu ya mali yenu muwape ndugu zenu muumini, na kwa hayo pia haitamaanisha kuwa nyie mmethibitisha mapenzi yenu kikamilifu, kwa sababu bado mko mnalingana. Kujitolea mhanga na kufikia kiwango hicho itathibitika pale ambapo hata katika nusu ya mali mliyobakia nayo mkatoa mkawagawia muumini ndugu zenu.”

 

4.      Muhammad bin  Ajlan anasema kuwa yeye alikuwa pamoja na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. na mara akatokezea mtu mbele yao akatoa salamu, na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwuliza

“Je ndugu uliowaacha huko nyuma hali zao ziko je?”

 

Basi huyo aliyekuja akawasifu na akatoa sifa zao na akaelezea kuhusu hali zao zilivyokuwa. Kwa hayo Imam a.s. akauliza :

“Je matajiri miongoni mwao wanawatunzaje wagonjwa wao?”

 

Basi huyo mtu akajibu :

“Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. !  Kidogo tu.”

 

Na Imam a.s. akamwuliza

“Je hao matajiri wanaonana mara ngapi na masikini?

 

Basi huyo mtu akajibu :

“Mara chache tu.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwuliza

 “Je hao matajiri wanawasaidia kwa mikono yao hao masikini?

 

Kwa hayo huyo mtu akasema

“Ewe Mawla !  Wewe unaniuliza mambo ambayo katika utamaduni wetu upo mchache sana.”

 

 

Kwa hayo Imam a.s. alimujibu

“Je wao watajidhaniaje kuwa wao ni Mashi’a wetu?”

 

4.      Abu Ismail anasema kuwa:Yeye alimwambia Al Imam Muhammad al-Baquir a.s.,

“Ewe Maula niwe fidia juu yako! Kwa sasa hivi huko kuna Mashia wengi.”

 

Kwa hayo Imam a.s. akajibu:

 “Je wanawasaidia na kuwahurumia mafakiri na wenye shida? Je wale wanao watendea mabaya sasa watu hao wema waliofanyiwa mabaya wanawasamehe hao wabaya walio watendea mabaya? Je wanasaidiana miongoni mwao katika kamari ? [51]

 

Kwa hayo yote mimi nikajibu :

 “Hapana sivyo hivyo.”

 

Hapo Imam a.s. akasema :

“Kwa hakika hao sio Mashia wetu. Basi mjue wazi kuwa Mashia wetu mienendo yao na desturi na utamaduni wao ni kama vile nilivyoelezea hapo.”

 

15.               Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. siku moja alimwuliza Sa’id bin Hassan,

“Je inawezekana miongoni mwenu kuwa muumini mmoja akatia mkono katika mfukoni mwa muumini wa pili na akajitolea kiasi cha fedha alizo na shida nazo bila ya kusita au kuogopa na muumini yule aliyetiliwa mkono mfukoni mwake asimzuie?”

 

Said bin Hassan akamjibu

“Ewe Mawla! Kwa hakika mimi sina habari na jambo kama hili.”

 

Kwa hayo Imam a.s. akamwambia

“Kwa hakika hakuna chochote.”

 

Hapo mimi nikamwambia Imam a.s. :

“Je hii inamaanisha kuwa sisi tumeisha teketea na kuangamia?”

 

Imam a.s. kwa hayo akamujibu :

“Sivyo hivyo, miongoni mwenu udugu na upendo bado haujaingia nafsini mwenu.”

 

Na katika maswala ya dua imesha zungumziwa hadithi moja ambamo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema zipo aina tatu za dua ambazo kwa kufika kwa Allah swt hakuna mtu anayeweza kuzizuia. Miongoni mwake moja ni

·         dua ya muumini anayemwombea muumini mwenzake na ambaye ametoa msaada kutoka mali yake kwa ajili ya ridhaa ya Allah swt na Ma’asumiin a.s. Na pili ni

·         dua kwa ajili ya muumini mwenzake ambaye pamoja na uwezo wake anaomba hivyo na ambaye baada ya kujua shida na dhiki kali ya muumini mwenzake hakuipuuzia bali amemsaidia.”

 

 


28. MTU AMBAYE AMEISHA TIMIZA MAHITAJI YA WATOTO WAKE NA NDUGU NA JAMAA ZAKE BASI INAMBIDI AJITAABISHE NAFSI YAKE KWA KUWAHUDUMIA WANGINE, HATA KAMA HUDUMA HIYO ITAKUWA NI BURE LAKINI NI SUNNAH.

 

1.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliulizwa na mtu mmoja :

“Ewe Mawla! Je ni mtu gani mwenzi wako aliyebora kabisa?”

 

 Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alijibu,

“Ni wale ambao wanawawia na kuwafanyia mema ndugu zao katika imani katika hali ya raha,starehe na shida.”

 

Na aliendelea kueleza kuwa

“Ewe Jamil, yeyote yule aliye nacho kingi basi kutenda kwake mema ni rahisi sana. Kwani Allah swt amewasifu wale walio nacho kidogo na huku wanafanya mema.

Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Hashri, 59, Ayah 9,

Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.

 

2.      Jamil bin Darraj anasema kuwa:

“Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alitukusanyisha na kutuambia

“Miongoni mwenu bora kabisa ni yule ambaye ni mkarimu na mtenda mema kwa wenzake na mwovu kabisa ni yule ambaye ni bahili na anawawia wengine kwa hali hiyo na bora ya matendo ni kule kutendeana mema pamoja na ndugu zenu na vile vile kuwatimizia haja na mahitaji yao na kwa hakika matendo haya yanamuudhi na kumvunja nguvu Shaitan na kunamwepusha mtu asiingie Jahannam na badala yake aingizwe Jannat. Ewe Jamil! Naomba uwafikishie habari hizi muumin halisi.”

 

3.      Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimfanyia usia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kwa kumwambia:

“Ewe Ali! Nina ku-usia mambo matatu ambayo kwa hakika yanathibitisha imani.

  • Moja ni kwamba wakati wa shida na dhiki kutoa mali au chochote na kuitumia katika njia ya Allah swt
  •  pili kuwawia waadilifu watu
  • tatu ni kuwapa elimu wale wanao tafuta elimu kama wanataka kujifunza elimu.”

 

4.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwaya moja kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambaye amesema:

“Bora ya sadaka ni ile ambayo inatolewa bila ya kuwa na shida yoyote na inatolewa kwa furaha.”

 

Mwandishi anasema hadithi hii inawahusu wale ambao wana watoto, familia na ndugu na majamaa. Yeye anakuwa na majukumu ya kuwauliza na kuwatimizia haja hawa watu wanaomtegemea yeye na hivyo baada ya kumalizana nao anatoa sadaka kwa furaha.

 

5.      Sama’a anasema kuwa:

“Siku moja alimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.,

“Iwapo mtu atakuwa na chakula cha kumtosha siku moja, je anaweza kumsaidia yule mtu mwingine ambaye hana chochote? Au tuseme kama mtu ana chakula cha kuweza kumsaidia mwezi mmoja anaweza kuwasaidia wengine ambao hawana kiasi hicho au yeye hana zaidi bali ana kiasi kile tu cha kumtosha yeye,na hivyo hawezi kumsaidia mwingine basi mtu kama huyo atakuwa amelaumiwa na kushutumiwa?”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamjibu,

“Katika suala hili yapo mambo mawili, miongoni mwenu kuna watu ambao wao wanawasaidia na kuwapenda wengine zaidi kuliko nafsi zao na ambapo Allah swt amesema katika Qur’an Tukufu, Surah A-Hashr, 59, Ayah 9 :

Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala wahaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa , bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.

 

Na jambo la pili ni kwamba yule ambaye ana kiasi kile tu ambacho kinamtosha yeye tu, basi mtu kama huyo hayuko katika lawama.

 

Naam, mkono ulio juu uko afadhali kuliko mkono uliopo chini (yaani yule anayempa mtu mkono wa juu na yule anayepokea ni mkono wa chini)na daima wakati wa kutoa lazima aanzie na wale ambao kwa hakika wako chini ya utunzaji wake (anawajibika kuwatunza na kuwasaidia na kuwatimizia mahitaji yao).”

 

6.      Al Imam Musa al-Kadhim a.s. aliambiwa na ‘Ali bin Sued Assinani:  “Ewe Mawla! Naomba unifanyie usia”.

 

 Kwa hayo Imam a.s. alimwambia

“Fanya Taqwa. Na umwogope Allah swt”.

 

Na hapo Imam a.s. alinyamaza kimya, basi yeye akasema :

“Ewe Imam a.s.! Nina shida kubwa sana. Mimi nimeshindwa kabisa sina uwezo wowote, yaani fikiria kwamba sina nguo yoyote juu ya mwili wangu iwapo fulani ibn fulani asingenivulia nguo zake akanipa na kunivalisha mimi.”

 

Katika kumjibu Al Imam Musa al-Kadhim a.s. alimujibu,

“Funga saumu na utoe sadaka.”

 

Naye kwa kunyenyekea alisema:

“Je nitoe katika yale ambayo mimi ninasaidiwa na watu? Na nitoe kiasi gani kutoka humo?”

 

Al Imam Musa al-Kadhim a.s. alimjibu

 “Chochote kile Allah swt anachokufikishia katika riziki yako toa humo sadaka, kwa kufanya hivyo acha nafsi yako ivumilie kidogo kwa ajili ya kuwatolea wengine walio na shida pia.”

 

7.      Abu basir ananakili riwaya moja ama kutoka kwa Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. au Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Yeye aliuliza, bora ya sadaka zote ni ipi?”

Imam a.s. akamujibu,

“Sadaka bora ni kutoka ile mali ambayo mtu hana nyingi (kitu ambacho unacho kidogo au cha kukutosheleza tu wewe, unatoa humo sadaka), je wewe huna habari

Allah swt amesema katika Qur’an Tukufu, Surah A-Hashr, 59, Ayah 9 :

Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala wahaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa , bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.

 

8.      Hakika hadithi moja ndefu Masufi walileta dalili moja mbele ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Allah swt amesema katika Qur’an Tukufu, Surah A-Hashr, 59, Ayah 9 :

Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala wahaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa , bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.

 

Imam a.s. aliwajibu

“Kwa ayah hiyo ni ufafanuzi ambavyo watendaji walikuwa wakitenda kama Allah swt alikuwa ameruhusu. Hakuna aliye wazuia hao, na ujira wao pia upo kwa Allah swt, lakini hiyo ni amri ya Allah swt ambayo ni kinyume na matendo yao.

 

Na sababu ya kufanya hivyo ni kwamba Allah swt anamwonea huruma muumin ili huyo muumin asiweze kuwaletea shida na kuwadhuru nafsi za wananyumba katika familia yao watoto – dhaifu na watoto wadogo, wote walio dhaifu, na ambao hawawezi kustahimili njaa, wazee waume kwa wanawake.

 

Iwapo mimi nitakuwa na kipande kimoja cha mkate na nikagawa sadaka, basi wale wote wanaonitegemea mie wataangamia na kuteketea.

 

Ndyio maana Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, iwapo mtu atakuwa na kokwa tano za tende au mikate mitano au Dinar tano au Dirham tano na yeye anataka kuzitumia zote, basi itakuwa ni vyema kabisa iwapo yeye azitumie kwa ajili ya wazazi wake, na baadaye kwa ajili yake mwenyewe na watoto wake na tabaka la tatu kwa ajili ya ndugu na jamaa zake ambao wana shida na wanahitaji msaada wake, na baada ya hapo awasaidie majirani ambao ni mafakiri, na mwishoni kabisa atumie kwa ajili ya kuwasaidia wengineo katika njia ya Allah swt.

 

Na baadaye akaendelea kusema kuwa siku moja ilitokea mtu mmoja kutokea Ansaar alifariki(kufa). Kwa mujibu wa usia wake yeye alikuwa na watumwa watano au sita ambao wote walifanywa (kwa mujibu wa usia huo) huru na wakaondoka zao na huko nyuma familia yake hakuwaachia chochote watoto wadogo wadogo na wana nyumba yake wote wakawa ni muhtaji, wakawa wao sasa wanategemea misaada kutoka wengine ilhali huyu bwana alikuwa na watumwa watano au sita.

 

Na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipojulishwa habari hizo alisikitika mno na akasema,

“Laiti kama nyie mngelikuwa mmenijulisheni kabla kuwa mtu huyo amewafanya watoto na wenye nyumba yake kuwa muhtaji (ni watu wenye kuhitaji misaada na sadaka) basi mimi kamwe nisingelikubali mtu huyu azikwe katika makaburi ya Waislam.’

 

Hlafu anaedelea kusema kuwa wazee wetu wamenakili riwaya kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa mtoaji sadaka inambidi kwanza awatimizie mahitaji ya wale wanao mtegemea yeye; na wale ndugu na jamaa walio wakaribu zaidi ndio awape kwanza (yaani wazazi, mke, watoto na ndugu zake na majamaa wanaofuatia wa karibu zaidi) na baada ya hapo majamaa na ndugu wenye uhusiano wenye ujamaa nao wa mbali ndio wapewe”.

 


29. NI SUNNAH KUUBUSU MKONO WAKO MWENYEWE BAADA YA KUTOA SADAQAH NA KUKINUSA KITU NA KUKIBUSU KITU AMBACHO UNAKITOLEA SADAQAH.

 

1.      Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. Amenakiliwa hadithi yake moja isemayo kuwa:

“Wakati muwapapo sadaka masikini muwaombe wawaombeeni dua, na akaendelea kusema, baadaye kuubusu mkono wa yule uliyemsaidia (uliyempa sadaka) kwa sababu sadaka unayoitoa kwanza inakwenda katika mikono ya Allah swt ndipo inapoingia katika mikono ya mwombaji.

 

Kama vile Allah swt anavyosema katika Qur’an Tukufu, Surah Tawba, 9, Ayah 104

Je hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anapokea toba ya waja wake, na anazikubali sadaqah , na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba na Mwenye kurehemu?

 

2.      Ahmad bin Fahad anaandika katika kitabu chake kuwa:

“ Al Imam Zaynul 'Abediin bin Hussein bin 'Ali bin Abi Talib a.s. wakati wa kutoa sadaka alikuwa akiubusu mkono wake mwenyewe, na mtu mmoja alimwuuliza sababu ya kufanya hivyo na Al Imam Zaynul 'Abediin bin Hussein bin 'Ali bin Abi Talib a.s. alimjibu,

“Kwa sababu kufanya hivyo ni kwamba sadaka kwanza inakwenda katika mkono wa Allah swt ndipo baadaye huishia katika mkono wa mwombaji.”

 

3.      Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Sadaka inayotolewa na muumin kwa hakika inafika mikononi mwa Allah swt na baadaye ndio anapewa aliye mwombaji. Na akaendelea kuelezea ayah ya Qur’an Tukufu, Surah Tawba, 9, Ayah 104.

Je hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anapokea toba ya waja wake, na anazikubali sadaqah , na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba na Mwenye kurehemu?

 

4.      Jabir Al J’ufi amenakili riwaya kutoka Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. kuwa  Al Imam Amir al-Muuminiin ‘Ali bin Abi Talib a.s. amesema kuwa:

“Siku moja nilitoa sadaka ya Dinar moja, hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akaniambia,

“Je unajua sadaka inapotolewa na mkono wa muumin kabla yake yeye anakuwa amejitoa nje ya mitego ya masheitani sabini? Na kabla ya yule mwombaji hajapokea hiyo sadaka inakwenda katika mikono ya Allah swt?

 

Allah swt anatuambia katika Qur’an Tukufu, Surah Tawba, 9, Ayah 104.

Je hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anapokea toba ya waja wake, na anazikubali sadaqah , na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba na Mwenye kurehemu?

 

5.      Mu’alla bin Hunais ananakili riwaya moja kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa amesema:

“Kila kitu Allah swt amekiwekea mtunza hesabu wake, isipokuwa sadaka tu, kwamba yeye ndyeo mwenyewe anayeishughulikia. Na baba yangu a.s. alipokuwa akimpa masikini au mwombaji sadaka yoyote, alikuwa akiichukua tena akawa akiinusa na kuibusu na tena alikuwa akimrudishia mwombaji mikononi mwake kwa heshima na adabu.

 

Kwa sababu sadaka anayopewa mwombaji kwanza inakuwa imepitia katika mikono ya Allah swt ndipo inapoishia katika mikono ya yule anayeomba. Kwa hiyo mimi pia nimependelea kukibusu kitu kile ambacho kimeshaingia katika mikono ya Allah swt ndipo kikaenda katika mkono wa mwombaji!”

 

6.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Kwa kila kitu isipokuwa sadaka tu Allah swt amemweka Malaika kutunza habari zake – na sadaka ameiweka katika usimamizi wake mwenyewe.”

 

7.      Muhammad bin Muslim ameripoti riwaya moja ama kutokea Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. au Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

         “Al Imam Zaynul 'Abediin bin Hussein bin 'Ali bin Abi Talib a.s. kila alipokuwa akimpatia sadaka mwombaji basi alikuwa akiibusu mikono ya mwombaji huyo. Na alitokezea mtu akauliza sababu ya kufanya hivyo naye akajibu kwa sababu inatoka kwenye mikono ya Allah swt na inaingia katika mikono ya mwanadamu huyo mwombaji.”

 


30. KATIKA KUTOA SADAQAH NI SUNNAH KUKOPA NA KUMLIPA MARADUFU ALIYEKUKOPA WAKATI WA KUTOA SADAQAH.

1.      Siku moja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliijiwa na mtu mmoja ambaye akasema:

“Je kuna yeyote yule atakayeweza kunisaidia kwa kunikopa? Mmoja katika

Ma-Ansaar akainuka na kusema :

‘Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Mimi nina uwezo wa kumkopesha”.

 

Basi kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwambia:

“Mpe mifuko minne ya tende huyu mwombaji. Kwa kusikia hayo huyo Ansaar akampa mwombaji kama vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alivyomwagiza”.

 

Baada ya kupita muda ,huyo Ansaar alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa kufanya madai ya mifuko minne ya tende aliyokuwa amemkopesha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambayo Mtume alimpa mtu sadaka, basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwambia Inshaallah basi nitakutimizia. Na ikafika mara tatu huyu mtu akawa anakuja kuomba alipwe deni lake na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kila mara alikuwa akimwambia Inshaallah nitafanikishia tu.

 

Mwishoni huyo mtu akashidwa kusubiri na katika hali hiyo akasema,

“Ewe Mtume wa Allah swt! Inshaallah, nimeisikia mara nyingi vya kutosha.!”

 

Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akacheka na kuwageukia na Ma-Sahaba na kuwauliza,

“Je kuna yeyote miongoni mwenu ambaye anaweza kunikopesha?”

 

Basi mtu mmoja akainuka na kusema,

“Ewe Mtume wa Allah swt! Naomba ukope kwangu”

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa hayo akamwambia

“Je una kiasi gani?”

 

Na huyu katika kumjibu akamwambia

“Kiasi chochote utakacho kihitaji wewe.”

 

Hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwambia

“Mpe mifuko minane huyu Ansaari.”

 

Huyo Ansaar akasema

“Ewe Mtume wa Allah swt! Mimi nilikukopa mifuko minne tu, sasa kwa nini  unanirudishia mifuko minane?”

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamjibu

“Mifuko minne ninakulipa na mifuko minne zaidi ninakuongezea zawadi kwa ajili yako.”

 

2.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema :

“Kwa hakika sadaka inayotolewa kwa moyo mkunjufu inalipia deni, na inaleta mfululizo wa baraka.”

 

 


31. NI HARAMU KUOMBA KAMA HAKUNA HAJA.

 

1.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Mtu yeyote atakayeomba chochote bila ya kuwa na dharura yake, basi Allah  swt  atamfanya awe muhtaji kwa maswala hayo kabla ya kufa kwake, na kwa sababu ya kuomba kwake huku kusikostahiki, yeye ataadhibiwa na kutupwa Jahannam [52].”

 

2.   Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Kwa Allah swt amekula kiapo kuwa mtu yeyote bila ya kuwa na shida au dharura kama atamwomba mtu amsaidie, basi kuomba kwake huko kutamfanya yeye lazima siku moja awe mwombaji.”

 

3.   Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa akisema:

“Enyi watu mfuate na kutekeleza nasiha za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., kama alivyosema:

“Iwapo mtu yeyote atajifungulia milango ya kuomba, basi Allah swt atamfungulia milango ya ufukara na umaskini.”

 

4.   Muhammad ibn Muslim ananakili riwaya kutoka kwa Al Imam Muhammad

      al- Baquir a.s. kuwa amesema:

“Ewe Muhammad! Iwapo waombaji wangelielewa mabaya katika kuomba, basi kamwe wasingeweka mikono yao mbele ya wengine; na iwapo mtoaji angezijuafaida na mema basi kamwe asingeuzuia mkono wake katika kutoa sadaka na misaada. Na vile vile Imam a.s.akaendelea kusema, bila shaka yule ambaye ana mali na uwezo na huku anaendelea kuwa mwombaji basi siku ya Qiyama atafika mbele  ya Allah swt huku uso wake ukiwa umejeruhiwa.” 

 

5.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Mtu yeyote ambaye ana maslahi ya vyakula vya kujitosheleza kwa muda wa siku tatu na pamoja na hayo anaendelea kuomba basi mtu huyo siku ya Qiyama atakuja mbele ya Allah swt huku uso wake utakuwa hauna nyama.”

 

6.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Bila ya kuwa na dhiki na shida mwenye kula kwa kuomba basi ni sawa na mtu anayekunywa pombe.”

 

7.   Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Mimi kwa kiapo cha Allah swt ninasema kuwa ni ukweli kabisa kuwa yeyote atakayeilisha nafsi yake kwa kujifungulia milango ya kuomba, basi Allah swt lazima atamfungulia milango ya ufukara na umaskini”

 

8.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Mtu yeyote anayejifungulia mlango wa kuomba, wakati anao uwezo wa kujilisha mwenyewe basi Allah swt atamfungulia milango sabini ya ufukara na umaskini, kiasi kwamba hakuna yeyote atakayeweza kuufunga hata mlango wake mdogo kabisa.”

 

9.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Mtu yeyote ambaye ataunyoosha mkono wake kwa kuomba huku ana chakujitosheleza kwa siku moja pia, basi huyo mtu atahesabiwa miongoni mwa wafujaji.”

 

10.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Siku ya Qiyama Allah swt hatawaangalia watu wa aina tatu na wala hatawatakasisha na watu kama hawa watapewa adhabu kali kabisa.

·         Kwanza ni mwanaume yule ambaye anafanya ulawiti,

·         mwanamke yule ambaye hakubakia na haya yoyote na

·         tatu ambaye pamoja na kuwa na mali bado anaendelea kuomba kwa watu.”

 


32. MAOVU YA KUOMBA HATA KAMA ITAKUWA NI KIJITI AU MAJI.

1.   Muhammad bin Muslim ameripoti riwaya kutoka kwa Al Imam Muhammad

      al-Baquir a.s. kuwa amesema:

“Ewe Muhammad ! Kama mwombaji (laiti) angelijua kuwa katika kuomba maovu mangapi yamejificha ndani yake, basi kamwe asingenyoosha mikono yake katika

kuomba.”

 

2.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

 “Ole wenu ! Kamwe msiwanyooshee watu mikono yenu kwa ajili ya kuwaomba kwani itawadhalilisheni duniani, na mtakuwa mkijitafutia dhiki na shida na siku ya Qiyama mtasimamishwa katika mazingara magumu kujibu mahesabu yake.”

 

3.   Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Mikono iko aina tatu,

·         kwanza ni mkono ulio juu kabisa ambao ni wa Allah swt.

·         Mkono wa pili ni ule ambao ni wa mtoaji na

·         wa tatu ni wa yule wa mpokeaji ambao ni wa chini kabisa.

 

Kila ikiwezekana mjaribu kujiepusha na kuomba, kwa sababu hiyo itakuwa ni vizuizi katika riziki yenu hapo mbeleni.

 

Iwapo mtu atapenda kuinusuru na kuihifadhi na kuilinda heshim na aibu yake basi anaweza kujichumia na kujitafutia riziki yake mwenyewe kwani kunakuwapo na pazia mbele ya riziki..

 

Kwa kiapo cha Allah swt ambaye roho yangu iko mikononi mwake, iwapo mtu akienda msituni ambapo akakata kuni na siku hiyo hiyo akaziuza au kubadilishana kwa tende na sehemu moja ya tende hizo akajiwekea yeye kumalizia shida zake na sehemu mbili akizigawa katika kuwasaidia wengine katika njia ya Allah swt, basi kwa hakika matendo yake haya ni bora na afadhali kabisa kuliko kunyoosha mikono yake mbele ya watu kwa ajili ya kuomba, kwani pengine wao watampa kidogo au chochote na wengine watamdanganya na kumdharau au na hata kumdhalilisha.”

 

4.   Abu Basir ameripoti riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliijiwa na baadhi ya watu kutoka makabila ya Ansaar ambao baada ya kutoa salamu waliketi, na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliwajibu salamu yao.

 

Wao wakasema ewe Mtume wa Allah swt sisi tuna ombi letu moja. Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akawaambia wamwambie. Nao wakasema ni haja yetu moja kubwa kabisa. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa kusikia hayo akasema nawaombeni mniambie ili niweze kujua. Wao wakaanza kusema, ombi letu ni kwamba tunakuomba wewe uchukue dhamana yetu ya ya kuingia Jannat (Peponi).

 

Kwa kusika hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikiinamisha kichwa chake, na kutumia vidole vyake alianza kama kuchimba ardhini kwa vidole vyake. Muda si muda akainua kichwa chake juu na kusema

“Ninaweza kuwapa dhamana hiyo kwa masharti kwamba kamwe katika mazingira yoyote yale nyie hamtamwomba mtu yeyote kitu chochote.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa hao watu hali yao ilikuwa mbaya kabisa kiasi kwamba katika safari hata kama fimbo yao ilikuwa ikidondoka basi wao walikuwa hawamwombi mtu yeyote msaada na hivyo walikuwa wakiteremka chini kutoka wanyama wao na wakijiinulia fimbo zao na walipokuwa wakikaa juu ya meza kwa chakula, wao walikuwa hawawaombi wenzao maji. Bali walikuwa wakienda wenyewe pale penye maji na walikuwa wakiyanywa.”

 

5.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Allah swt anamrehemu yule mja wake ambaye amebakia katika heshima utoharifu na katika desturi zake njema, na ambaye amejiokoa na hakuomba kwa hakika kuomba kunaleta udhalilisho duniani, na uelewe wazi kuwa watu humu duniani kamwe hawataweza kummalizia shida zake zote. Na hapo baadaye Imam a.s. akaelezea kisa kimoja kwa kifupi cha Hatim:

Wakati nafsi za watu zinapo kata tamaa kwa watu basi hapo kwa hakika yanaingia katika shida na taabu kubwa, na kwa uhakika tamaa ndio ufakiri mkubwa na tamaa ndiyo ufukara mkubwa.”

 

6.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kwa kupitia Ma-Imamu a.s. ameripoti riwaya kuwa:

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwusia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.,

“Ewe Ali ! Ni rahisi kabisa kuutia mkono wako katika mdomo wa nyoka mkubwa kuliko kumyooshea mkono yule ambaye alikuwa hayupo duniani na akaja akazaliwa baadaye.”

 

Na akamwambia Abu Dhar:

“Ewe Aba Dhar! Ole wako kamwe usiombe kwa sababu ni udhalilisho na unakaribisha shida na taabu. Na vile vile siku ya Qiyama utatakiwa utoe mahesabu yake makubwa na marefu. Na akaendelea kusema “Ewe Aba Dhar! Kamwe usifungue kiganja chako kwa ajili ya kuomba. Naam, unyooshe mikono yako kwa Allah swt kwa kumshukuru kwa ile riziki aliyokupa.”

 

7.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Msiwe miongoni mwa watu wasio wajali watu, msiwe kama watu wenye kuwa na dhiki na shida kama maji mnayoyatema baada ya kupiga mswaki mnavyo sukutua.”

 

8.   Katika kitabu Thawabul A’amal imeandikwa riwaya ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ambaye amesema:

“Allah swt anamrehemu yule mtu ambaye ameweka desturi na tabia zake kitakatifu na amejizuia kwa njia zote asiombe kwa watu. Kwa hakika kuomba ni kudhalilika na kujidhalilisha duniani na hakuna duniani wale watu watakaoweza kumtimizia haja yake.”

 

9.   Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. amesema:

“Allah swt amemfanya Mtume Ibrahim a.s. kuwa Khalil wake (Rafiki wake) kwa sababu yeye kamwe hakulitupilia mbali jambo ambalo alimwomba yeye na yeye mwenyewe kamwe hakumnyooshea mtu yeyote mikono yake isipokuwa kwa Allah swt.”

 

10. Imeripotiwa riwaya kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa:

“Allah swt bila shaka anawachukia sana wale watu ambao hawana aibu ni mchafu (mwili na kiroho), na vile vile mtu yule ambaye amejigundisha kwa watu kwa tabia zake za kuomba omba.”

 

11. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Msiwaombe ndugu zenu mahitaji yenu, isitokee kwamba wao wakakataa kukutimizia maombi yako, na nyie mkachukia na mkaingia katika kukufuru.”

 

12. Bwana Salman Al-Farsi r.a. anasema kuwa :

“Mpenzi wangu Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amefanya usia na kusisitiza kabisa kuwa, mimi nisipuuzie mambo saba.

·         Ya kwanza yeyote yule aliye mkubwa kuliko mimi nisimtupie macho yangu, bali nimtupie macho yule ambaye yuko chini yangu;

·         niwe na mapenzi na maskini na

·         niwe karibu nao,

·         niseme ukweli daima hata kama utakuwa mchungu,

·         niwatendee mema na kuwahurumia ndugu na majamaa zangu, hata kama yule nimfanyiaye hayo atanigeuzia mgongo,

·         kamwe nisiunyooshe mkono wangu mbele ya watu kuwaomba na vile vile ameniusia kuwa

·         daima niwe nikisema La Haula Wala Quwwata Illa bilahil ‘Aliyyil ‘Adhiim kwani hiyo ni hazina mojawapo katika hazina za Jannat.”

 

13. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. Nahaj-ul-Balagha anasema:

“Muwe mkiziachia matamanio na mahitajio yenu kuliko kuwaomba waovu na wasio stahiki. Na akaendelea kusema na utakatifu na utukufu ni sifa moja ya kupendeza ya mafakiri, na hakika urembo wa shida na dhiki ni kushukuru.”

 

14.  Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. amesema:

“Ujue kuwa uso wako unaong’ara kwa heshima na adabu, na wewe wakati unapokwenda kuomba na ukarefusha mikono yako kwa ajili ya kuomba basi heshima na adabu hiyo inayeyuka na kuanza kudondoka kutoka usoni mwako. Sasa ni kuangalia uyeyukaji huo unamdondokea nani ndio wewe unatakiwa ujue uangalie na ujue.”

 

15.  Ibn Fahad ameripoti riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Shi’a wetu hata kama watakuwa wakifa kwa njaa basi kamwe wakati wowote ule hawatainyoosha mikono yao kwa mbele ya watu kwa ajili ya kuomba.”

 

16.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Mtu yeyote anayenyoosha mkono wake na kufungua kiganja chake kwa ajili ya kuomba, basi ushahidi wake utupiliwe mbali.”

 

17.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Iwapo mwombaji angelikuwa akijua yale majukumu na wajibu walio nao katika kufanya hivyo, basi kamwe asingeomba chochote kwa mtu yeyote. Na vile vile na kutokumpa mwombaji pia kuna majukumu na wajibu mkubwa sana iwapo watu wangelijua basi kamwe wasingeli wakatalia kuwasaidia watu.”

 

18.  Siku moja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliwaambia Ma-Sahaba wake:

“Ni kwa nini hamfanyi bay’a yangu (utiifu wangu)?”

 

Basi Ma-Sahaba wakamjibu:

“Ewe Mtume wa Allah swt! Sisi tumeshakwisha kufanya bay’a yako tangu mwanzoni. Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema, mfanye bay’a katika swala ambalo mle kiapo kuwa nyinyi kamwe hamtanyoosha mikono yenu kwa wengine kwa ajili ya kuomba. Na baada ya kula viapo hivyo ikaonekana mandhari tofauti kabisa miongoni mwa Ma-Sahaba kiasi kwamba hata mtu alipokuwa akidondosha mkongojo wake basi alikuwa akiteremka kutoka usafiri wake wa mnyama kama ngamia n.k. kuteremka chini na kujiokotea mkonojo wake, na kamwe alikuwa hamwambii mtu mwingine amwokotee na kumpa hiyo bakora yake iliyoanguka”

 

 

19.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Iwapo mtu atakwenda mbio mbio msituni akakata kuni na mzigo huo akauchukua kuja nao kwa hiyo atakuwa ametunza heshima na hadhi yake, basi jambo hilo ni afadhali kuliko udhalilisho wa kuomba.”

 

20.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Yeyote yule aliyetuomba sisi tunampa na yeyote yule aliyetoa na yeyote yule aliye shukuru basi Allah swt atamfanya awe tajiri.”

 

21.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Kwa kuwaomba watu mahitajio yako ni kuteketeza na kuangamiza heshima yako ni sawa na kuteketeza na kuangamiza heshima yako, na vile vile ustahi wako pia unamalizika. Na kwa hakika kile walichonacho wao utajiri wao inambidi mtu akate tamaa asitegemee chochote yaani asiwe na tamaa ya aina yoyote na hakika hii ndio inayo hesabika kuwa ni heshima kubwa ya muumin. Kumbukeni kuwa tamaa ni ufakiri wa aina mojawapo.”

 

22.  Ja’bir amenakili riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa amesema:

“Allah swt ameweka karaha kwa wale wanao omba kwa kung’angania na kwa kufuatilia.”

 

 


33. KUOMBA KATIKATI YA UMATI WA WATU SI VYEMA KABISA.

 

1.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Enyi watu! Msiombe wakati watu wanapokuwa katika makundi, isitokee kwamba kwa sababu ya ubahili wao ikawawia nyie machungu.”

 

 


34. NI KARAHA (MAKRUH) KUDHIHIRISHA SHIDA NA UOMBAJI.

 

1.      Mufadhdhal bin Kais bin Rumman anasema kuwa:

“Yeye siku moja alikuwa katika huduma ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., na mimi nikamdokezea kidogo kuhusu matatizo niliyokuwa nayo. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwambia kijakazi wake:

Naomba ule mfuko. Na akaniambia Abu Ja’afar (Manthur) amenitumia hizi Dinar mia nne kwa ajili ya msaada, hivyo chukua wewe. Na uende ukamalize shida na dhiki uliyo nayo.”

 

Nami nikamwambia:

“Hapana! Kwa kiapo cha Allah swt mimi niwe fidia juu yako – mimi sina nia hivyo – mimi nilikuwa natarajia kuwa wewe uniombee dua kwa Allah swt ili shida na dhiki niliyonayo isiniwie ngumu bali iwe nyepesi.”

 

 Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akasema,

“Pamoja na mimi kukuombea dua, kamwe usiwaambie mbele ya umati wa watu shida zako kwani kwa kufanya hivyo wewe utapoteza heshima na hadhi yako.”

 

2.      Harith Hamdani anasema kuwa yeye amesikia hadithi ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kutokea kwa Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. kuwa:

“Maombi ni amana za Allah swt katika vifua vya watu na yeyote yule atakayeficha siri hiyo basi atapata thawabu za ibada.”

 

3.      Kulayni anasema kuwa Bwana Luqman alikuwa akimpa mafunzo mwanake kwa kumwambia:

“Ewe mwanangu, mimi nimeisha kunywa dawa na magamba yaliyo chungu kabisa, lakini mbele ya shida na dhiki hakuna kitu kinachozidi uchungu wake. Iwapo wewe utapitia katika hali kama hiyo, basi kamwe usiseme maombi yako mbele ya watu, kwa sababu wewe katika macho yao utaanguka heshima na taadhima yako, na watu hao hawawezi kukufaidisha chochote na badala yake nakuomba umwombe yule ambaye anakujaribu kwa mitihani ya aina hiyo, na bila shaka ni yeye tu anayeweza kukuondolea matatizo na dhiki iliyokukabili, hivyo umwombe yeye tu (Allah swt). Yeye ni nani duniani ambaye amemwomba Allah swt na akarudi mikono mitupu, na yupo ambaye aliweka matarajio na matumaini yake kwa Allah swt na akajikuta ametoka mtupu?”

 

4.      Imeripotiwa kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa amesema:

“Ewe 'Ali! Allah swt ameweka ni amana miongoni mwa waja wake katika hali ya shida na ufukara, na yeyote yule atakayeweza kuificha hiyo amana basi ajue kuwa yeye ni mtu ambaye amedumisha ‘ibada na anapata fadhila za wale walio dumisha ‘ibada na wanao funga saumu, lakini yeyote yule ambaye anaitoboa na kuitangaza hiyo amana ya Allah swt kwa kudhihirisha na kufanya bayana siri ya shida na ufukara wake kwa wengine, na hao watu baada ya kumsikiliza hawamsaidii basi mjue kuwa huyo mtu kwa hakika wamemuua. Mauaji haya sio kwa upanga au kwa mkuki bali ameuawa kimoyo.”

 

5.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripoti riwaya kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa amesema:

“Enyi wenye shida na masikini! Tunzeni heshima zenu na mpeni Allah swt furaha ya mioyo zenu ili kwamba Allah swt awalipe mema kwa ufukara na shida zinazo wakabili na kama nyie hamtafanya (isije mkakufuru na kuvuka mipaka kwa sababu ya kukosa subira na hikima) hivyo basi mtambue kuwa mtapata adhabu na gadhabu za Allah swt.”

 

 


35. KURUHUSIWA KUMWAMBIA SHIDA ZAKO MUUMIN NA NDUGU PALE INAPOTOKEA.

 

1.      Imenakiliwa riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Itakapo tokea miongoni mwenu mtu akazingirwa kabisa kwa hali mbaya, basi inambidi awajulishe jamaa na ndugu zake na asiiweke nafsi yake katika shida.”

 

2.      Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. amesema katika Nahaj –ul – Balagha kuwa:

“Mtu yeyote atakayemwambia mahitaji yake dharura zake kwa muumin basi ajue kuwa ameweka habari zake hizo kwa Allah swt, na yeyote yule atakayeleta dharura na mahitajio yake kwa kafiri basi ajue kuwa amekwenda kinyume na maamrisho ya Allah swt.”

 

3.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Katika hali tatu tu ndipo kunapo ruhusiwa kuomba ama sivyo hairuhusiwi.

·         Kwanza katika kujinusuru mtu mwenyewe,

·         kujinusuru na hasara kubwa kabisa ya mali na

·         tatu iwapo kwa kutokuomba kutakuja kumpatia udhalilisho wa hali ya juu sana. Yaani mtu katika vitu hivyo vitatu kujiokoa na hali hizo tatu mtu anaweza kuomba msaada kwa wengine.”

 

4.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa:

“Mtu mmoja alimwijia Al Imam Hassan ibn 'Ali bin Abi Talib a.s. na kuomba chochote: Kwa hayo Imam a.s. akamwambia haistahiki kuomba isipokuwepo hizo sura tatu.

·               Kwanza ama kuzuia umwagikaji wa damu,

·               ama mtu akiwa na shida ya hali ya juu kabisa au

·               kujizuia kuja kudhalilika vibaya sana.

 

Sasa hebu wewe niambie wewe upo katika sura ipi kati ya hizi tatu? 

 

Yeye akasema ‘Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Katika sura tatu ulizozitaja ipo mojawapo. Basi bila kusita kwa haraka sana Al Imam Hassan ibn 'Ali bin Abi Talib a.s. akamtolea dinar elfu hamsini na kumpa, na  Al Imam Hussein ibn 'Ali bin Abi Talib a.s. akampa dinar elfu arobaini na tisa  na ‘Abdulah bin Ja’afar akampa dinar elfu arobaini na nane.”

 


36. KUISHI NA WATU KWA WEMA NI SUNNAH NA KUTOKUWA NA TABIA YA KUWAOMBA OMBA WALA KUWA NA TAMAA KWA YALE WALIYO NAYO.

 

1.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Heshima ya muumin ni kule kuamka kwa ajili ya sala za usiku, na vile vile heshima yake ni kule kutokuwa mwombaji wa watu.”

 

2.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwaya kutoka kwa Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. kuwa amesema:

“Wewe lazima uwe na moyo wa kuishi vyema na watu na kuwaheshimu na kutosheka nao. Na kuishi nao vyema ni kule kuongea nao kwa upole na utamu na uwe na uso wenye tabasamu na uishi nao vile kwamba kila wakuonapo uwe ukionyesha furaha usoni mwako na hivyo utakuwa umejiwekea heshima katika jamii.”

 

3.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema:

“Iwapo kutatokezea miongoni mwenu anayemtegemea Allah swt azikubalie kila dua zake anazoziomba basi awe akiishi na watu wote kwa wema na kamwe asimtegemee mtu yeyote isipokuwa Allah swt peke yake na atakapo jiona kuwa yeye kwa hakika anao moyo kama huo basi atambue wazi kuwa chochote kile atakachomwomba Allah swt atampatia na kumjaalia.”

 

4.      Al Imam Zaynul 'Abediin bin Hussein bin 'Ali ibn Abi Talib a.s. anasema kuwa:

“Iwapo mtu atataka wema wote kwa ajili yake ni kwamba yeye ajiepushe mbali na tamaa za kila aina ya kutamani yale waliyonayo watu, na kama yeye ana matamanio yoyote au maombi yoyote basi asiwategemee hawa watu bali zote azielekeze kwa moyo mkunjufu na halisi kwa Allah swt na lazima Allah swt atazikubalia dua na maombi yake na atamtimizia.”

 

5.      Abul A’ala bin A’ayan anasema kuwa mimi nimemusikia Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akisema:

“Enyi watu nyie mtajidhuru pale mtakapo peleka maombi yenu na mahitaji yenu kwa watu, na kwa hakika inafukuzia mbali heshima na adabu. Mkae na watu katika hali ya kuridhika na kuwa na uhusiano nao mzuri na kwa hakika hiyo ndiyo kwa ajili ya usalama. Kwa hakika tamaa yenu ndiyo dalili ya ufakiri wenu.”

 

6.      Ahmad bin Muhammad bin Abi Nassr anasema kuwa yeye siku moja alimwambia Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. :

“Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Ninaomba uniandikie barua moja kwa Ismail bin Daud, ili kwamba niweze kupata chochote kutoka kwake. Kwa hayo Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. akamwambia iwapo mimi kitu unachokitaka au cha kukutosheleza wewe ningekuwa nimekukataa, ndipo ningekuandikia, ama sivyo uchukue kile nilicho nacho mimi kwangu na ukitegemee hicho.”

 

7.      Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Kwa hakika yale waliyonayo watu katika uwezo wao na kuridhika nayo ndimo humo kuna heshima ya muumin ya imani yake, je nyie hamjaisikia kauli ya Hatim?  Hatim alisema kuwa pale mtakapoona nafsi zenu zimevutiwa kwa mali za watu wengine basi muelewe kuwa shida na taabu ziko zinawakaribia, na kwa hakika tamaa ni ufakiri ulio dhahiri.”

 

8.      Abdullah Bin Sinan anasema kuwa yeye amemsikia Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akisema:

“Kwa ajili ya muumin mapendezi ya dunia na akhera yako katika mambo matatu.

·         Kwanza ni sala katika sehemu ya mwisho wa usiku,

·         kutokuvutiwa na kutokuwa na husuda na mali na miliki wanayomiliki watu wengine na

·         kuwa mwaminifu na mtiifu kwa ukamilifu wa Ahlul Bayt a.s. na mapenzi yao.”

 

9.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Alikuwapo mtu mmoja mbele ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na akamwuliza, ‘Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! naomba unionyeshe unieleze jambo moja nilifanye jambo ambalo Allah swt atakuwa radhi pamoja nami. Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimujibu:

Udumishe amani na upendo katika utamaduni wa dunia, jambo ambalo kimatokeo utapata mapenzi ya Allah swt na usiwe na kijicho na wivu wala tamaa kwa mali na miliki za watu jambo ambalo litahifadhi heshima yako machoni na mioyoni mwao.”

 

10.  Ja’bir bin Yazid ananakili riwaya kutoka kwa Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. kuwa amesema:

“Usiwe na wivu choyo wala tamaa kwa mali za watu kwa hakika ni jambo jema kabisa kwa kuitakasisha nafsi yako kuliko hata kutoa mhanga wa mali. Vile vile wakati wa shida na dhiki fanya subira. Kuhifadhi heshima yako na utakatifu wako, mambo haya ni afadhali hata kuliko kugawa mali kwa watu. Kwa hakika kuwa na imani kamili juu ya Allah swt na kutotaka kutovutiwa kutokuwa na wivu au kijicho au tamaa kwa mali waliyonayo watu wengine ndio hayo mambo yaliyo bora kabisa katika maisha ya mwanadamu.”

 

 


37. SI VYEMA KUMSEMA MTU BAADA YA KUMSAIDIA AU KUMSEMA YULE ULIYEMPA SADAQAH.

 

1.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akisema:

“Allah swt amechukia hafurahishwi na sifa sita na vile vile mimi sizifurahii hizo sifa sita na ndio nimefanya usia kwa mawasii na waumini wote kuwa vitu hivyo sita wajiepushe navyo na mojawapo ni kule baada ya kutoa sadaka mtu akaanza kumsema na kuvisema.”

 

a.    Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Baada ya kutenda mema mtu atakapovizungumzia hayo basi atayateketeza mema yake yote.”

 

3.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwaya kutoka kwa Mtume Muhammad

      Mustafa s.a.w.w. kuwa:

“Allah swt hakupendezewa na mambo sita na mimi vile vile katika kizazi changu Maimam wote sikupenda kutokezee sifa hizo, na vile vile Maimam pia nimewahusia kuwa wasizipende sifa hizo ziwepo katika muumin. Hivyo kila muumin anabidi ajiepushe na sifa hizo. Katika sifa hizo sita mojawapo ni ile baada ya kumfanyia mtu wema mtu anaanza kuyazungumzia huku na pale.”

 

4.      Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. anasema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Allah swt hapendi sifa sita na hizo sifa sita mimi sikupendezewa kwa ajili ya mawasii watakao nifuata na waumini wote watakaonifuatia.

·        Kwanza kusali isivyo kwa makini,

·        pili katika hali ya saumu kujamiiana na mwanamke,

·        tatu baada ya kutoa sadaka kutangaza na kuonyesha.

·        Nne kuingia msikitini katika hali ya Janaba,

·        kuwa na shauku ya kutaka kujua mambo ya watu majumbani mwao kunatendeka na kunaendelea nini, na

·        sita kucheka makaburini mtu anapokuwa baina ya makaburi mawili.”

 

5.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kwa mamlaka yake amenakili riwaya kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa:

“Mtu yeyote atakaye msaidia muumin ndugu yake na baadaye akaja akamwambia kuhusu wema huo akausema basi Allah swt hulirudisha tendo hilo halikubalii. Basi mtoaji atabakia na uzito juu yake na kwa lile jema alilolitenda hana malipo yoyote kutoka kwa Allah swt.”

 

Na Imam a.s. aliendelea kusema: “Kwa sababu Allah swt anasema kuwa yeye ameiharamisha Jannat kwa ajili ya yule anayesema baada ya kutenda tendo jema na bahili na mchonganishi.

 

Muelewa wazi kuwa yule mtoa sadaka, hata anayetoa kiasi cha Dirham moja, basi Allah swt humlipa zaidi ya ukubwa wa mlima wa Uhud kwa neema za Jannat na yeyote yule atakaye saidia kufikisha hiyo sadaka kwa yule ambaye anahitaji basi Allah swt atamlipa mema hayo hayo, na kamwe hakutakuwa na punguzo lolote katika neema za Allah swt kwa ajili ya wote hao.”

 

6.      Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika hotuba yake alisema:

“Yeyote yule atakaye tenda wema na kuwawia wema ndugu wenzake, na akaanza kutanganza mema aliyoyafanya basi matendo ya watu kama hawa yatatupiliwa mbali na hayatakuwa na maana yeyote.

 

Allah swt amewaharamishia Jannat watu wafuatao:

·         Kwanza ni wale wanao tangaza mema waliyowafanyia watu wenzao, na

·         Wale wanaowapotosha watu wengine,

·         wafitini,

·         wanywaji wa pombe,

·         wale wanao tafuta makosa ya watu na aibu za watu,

·         wale wenye tabia mbaya,

·         wale walio makatili kwa wenzao na vile vile

·         wale watu wanao watuhumu watu wengine kwa tuhuma za kuwazushia maovu.”

 

7.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwaya kutoka kwa mababu zake kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Allah swt amewazuieni nyinyi kwa matendo maovu takriban ishirini na manne na mojawapo ni jambo lile ambalo baada ya kutoa sadaka mtoaji anamwambia maneno aliyempatia.”

 

8. Bwana Abu Zahar Al Ghafar amenakili riwaya kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa:

“Kuna aina tatu ya watu ambao Allah swt kamwe hatazungumza nao siku ya Qiyama.

·         Kwanza ni yule mtu ambaye hatoi kitu chochote bila ya kumsema au kumwambia yule anayempa, na

·         pili ni yule ambaye hachukui jukumu wala haoni umuhimu wa kuficha zehemu zake za siri na wa

·         tatu ni yule ambaye anauza mali yake na kutaka faida kupindukia kiasi.”

 

9.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Mtu yeyote baada ya kumsaidia muumin atamuudhi kwa kumwambia au kwa kumsengenya kiasi kwamba roho yake ikaumia basi Allah swt huibatilisha sadaka na wema kama huo.”

 

10.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Aina tatu ya watu kamwe hawataingia Jannat.

·         Moja ni yule ambaye wazazi wake wamemfanya Aak, wa

·         pili mnywaji wa pombe (daima anakunywa pombe) na

·         tatu ni yule baada ya kufanya mema huanza kusema na kutangaza.”

 

 


38. MTU ANAPOTOA KITU KUSAIDIA BASI HAIRUHUSIWI KUMWAMBIA KUWA UMETOA ZAIDI KUPITA KIASI.

 

1.      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. siku moja alimtumia mifuko mitano za Tende za Baqi’ (Jannatul Baqi’, ipo Madina ). Mtu huyo alikuwa muhtaji mwenye shida na daima alikuwa akitegemea msaada kutoka kwa Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s., na kamwe alikuwa harefushi mikono yake kwa wengine kwa ajili ya kuomba kwa watu wengineo. Mtu mmoja alipo yaona hayo basi alimwambia Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s.:

 

“Kwa kiapo cha Allah swt, huyu mtu hajakuomba chochote wewe kwa hivyo badala ya kumpa mifuko mitano mfuko mmoja tu ulikuwa ukitosha, na kwa hayo Al Imam 'Ali bin Abi Talib a.s. akamwambia:

 

“Allah swt asiongezee idadi ya muumin kama wewe humu duniani!  Wewe mtu wa ajabu sana, mimi ndiye ninayempa lakini ubahili unaufanya wewe!  Kumbuka kuwa mtu mwenye shida na anaye kutegemea wewe hakuombi, Je ni haki kuwa mwenye shida asipoomba basi asisaidiwe mpaka lazima aombe? Basi hapa inaonyesha heshima yake. Uso ule ambao unawekwa juu ya udongo kwa ajili ya ibada ya Allah swt katika hali ya sujuda itakuwa basi mimi nimeubadilisha ule sura badala ya kumwangukia Allah swt utakuwa umeniangukia mimi ! Na jambo ambalo silitaki mimi na wala silifanyi hivyo.”

 

Mtu ambaye hathamini hajali shida za muumini wengineo itakuwaje ategemee Jannat wakati huku yeye mwenyewe anafanya ubahili katika mali yake? !

 

Yule asemaye daima “Ewe Allah swt wasamehe madhambi yao yote waume kwa wanawake Waislam” kwa hakika mtu kama huyu huwa anategemea Jannat tu je ni uadilifu gani kwa kusema tu kwa mdomo kuwaombea mema watu ambapo wao hawawafai watu wengine wanapokuwa na shida na dhiki huku wakiwa wanafanya ubahili kwa mali zao?”

 


39. KUMSAIDIA MTU KABLA HAJAOMBA NA KUMSAIDIA KATIKA HALI YA KUTOKUJULIKANA NI NANI ANAYESAIDIA NI SUNNAH.

 

1.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Kwa hakika uwema ni ule ambao mtu anamsaidia mtu kabla hajaombwa, na kumpa baada ya kujua hali yake inamaanisha umempa baada ya kujua hivyo. Inawezekana maskini huyo mtu usiku kucha akawa anatapatapa iwapo atafanikiwa au hatafanikiwa, huku akiwa amejawa mawazo niende kwa nani nisiende kwa nani, na hatimaye moyo ukiwa unadunda mwili ukiwa unatetemeka na akiwa amejawa na aibu kubwa anatokezea mbele yako.”

 

2.  Yas’ab bin Hamza anasema kuwa:

“Mimi siku moja nilikuwa pamoja na Al Imam Musa al-Kadhim a.s., watu walikuwa wamekaa huku wamemzunguka, yaani watu wengi walikuwapo. Watu walikuwa wakiulizia masuala ya halali na haramu, na mara tukaona akaingia mtu mmoja mrefu na akaanza kusema, “Iwe salamu juu yako ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Mimi ni mpenzi na mfuasi wako wewe na baba na mababu zako, na hivi nimerudi kutoka Hijja Tukufu. Mimi nimeibiwa mali yangu yote na hivyo sitaweza kufika nchini kwangu (yaani nyumbani). Mimi naomba nisaidiwe sadaka kiasi kwamba niweze kufika nyumbani kwangu, na mimi nitakapo rudi katika mji wangu kiasi hicho cha fedha nitakitoa nigawe katika kuwasaidia wengine kama sadaka.

 

Imam a.s. akamwambia:

“Naomba ukae kidogo upumzike, Allah swt akurehemu. Na Imam a.s. aliendelea na mazungumzo yake pamoja na umati uliokuwa pale katika kuulizana na kueleweshana kuhusu maswala mbalimbali. Hatimaye mimi Khaysama na Suleiman Al-Ja’afari ndio tuliokuwa tumebakia na hapo Imam a.s. kwa kuniangalia mimi akasema:

“Je unaniruhusu mimi niende chumbani kwangu?”

 

Suleiman akasema

“Allah swt aiendeleze amri yako”.

 

Hapo Imam a.s. aliinuka na kuelekea katika  chumba chake a baada ya muda si muda akatoka nje akafunga mlango na mwenyewe akasimama nyuma ya mlango na akatoa mkono tu nje huku akisema, je huyo msafiri kutoka Khurasan yuko wapi?”

 

Hapo mimi nikamjibu:

“Ya Imam a.s.! Mimi niko hapa.”

Na kwa hayo Imam a.s. akamwambia”

“Nimekupa hizi Dinar mia mbili ambazo zitakusaidia wewe katika gharama na matumizi ya safari yako na vile vile napenda nikujulishe kuwa hakuna haja tena ya hizi pesa kuzitolea sadaka  ufikapo nyumbani kwako, asante na unaweza kuendelea na safari yako na itakuwa vyema tusitazamane nyuso. Msafiri huyo akachukua hizo pesa na kuondoka zake.”

 

Seleiman Al-Ja’afar akauliza:

“Niwe fidia juu yako ewe Mwana wa Mtume s.a.w.w.! Kwa hakika wewe umefanya wema na ihsani mkubwa sana wenye huruma, lakini pamoja na hayo kwa nini umejificha?”

 

Kwa hayo Imam a.s. akamjibu

“Hakuna sababu nyingine ila sikutaka kuona uso wa mwombaji ukiwa umeingiwa na aibu na unyonge sababu ya kuomba. Je wewe hujaisikia hadith ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambamo amesema, kwa yeyote yule anayeficha wema hulipwa thawabu za Hijja sabini na yeyote yule baada ya kutenda maasi na madhambi anatangaza basi daima hubakia dhalili. Na yeyote yule anayeficha madhambi na maovu basi Allah swt humsamehe.”

 

 


40. NI SUNNAH KUENDELEZA NA KUTUNZA MSAADA NA UKARIMU NA KUENDELEAZA MOYO WA KUTOA.

 

1.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Jambo jema kabisa linalonisaidia mimi katika kufanya wema katika kuwasaidia ni mkono ambao unawafikishia na mkono mwingine unashirikiana naye. Na kwa hakika hao wanaokuja kuomba wanakuja na maombi yao ndipo wanapokuwa karibu nami zaidi. Kwa hakika nimeona kuwa wale wanao sahau waliyoyatenda mema kabla na baada ya kuurudisha mkono wao nyuma huonekana kuwa wao wanaanza kuyasahau mema yote. Kwa hakika moyo wangu kamwe haukuniruhusu kuwafukuza na kuwakatalia waombaji. Na baada ya hapo Imam a.s. alisoma mashairi ifuatayo:

 

Wakati unapokuijia mtihani kwako kwa heshima zako pia inabidi uombe,

Basi uende kwa mtu mmoja aliye mkuu na aliye Sharifu kwa ajili ya kuomba kwake.

Kwa hakika, huyo mtu Sharifu na mkuu atakapokusaidia basi humo ndani hakutakuwa na maonyesho wala masengenyo, na badala yake ndani kutakuwa na unyenyekevu na kuhuzunika pamoja nawe.

 

Kumbuka wakati utakapotaka kupima katika mzani uombaji na utoaji sadaka  na mema basi utaona sahani ya mzani ya uombaji utakuwa daima ni mzito kuliko nyingine yote.”

 

2.  Warram bin Abi Faras ameandika riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Wenye imani dalili zao ni nne,

·         kwanza nyuso zao huwa zina bashasha,

·         ndimi zao zinakuwa zenye ukarimu na mapenzi,

·         nyoyo zao zinakuwa zimejaa huruma, na

·         wanakuwa na mkono wenye kutoa mkono unaopendelea kutoa sadaka  na misaada nk.”

 

 


41. KUHURUMIA NA KUSAIDIA NI SUNNAH NA HUKUMU ZINAZOHUSIANA NAZO.

 

1.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa Mtume Muhammad Mustafa

     s.a.w.w. alikuwa akisema:

“Kila kila aina ya wema na huruma ni sadaka.”

 

2.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akizungumzia neno Ma’arufu katika Qur’an

     Tukufu, Surah Nisah, 4, Ayah 114:

Hakuna heri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipokuwa kwa yule anaye amrisha kutoa sadaqah, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayokwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja mpa ujira mkubwa.

 

 Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Kwa ma’arufu kuna maanisha kule mtu kutimiza wajibu wake aliofaradhishiwa.”

 

 


42. NI SUNNAH KUWAWIA WANA NYUMBA WAKO KWA WEMA KABLA YA KUTOA SADAQAH KWA WATU WA NJE.

 

1.  Siku moja Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliwasaidia waombaji watatu na wa nne

     alipokuja hakumpa chochote. Na hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akasema:

“Iwapo mtu atakuwa na Dirham elfu thelathini au arobaini na zote akazigawa kwa kusaidia au sadaka  bila ya kubakiza chochote kwa ajili ya wana nyumba wake basi huyo mtu atakuwa mmoja miongoni mwa watu watatu ambao dua zao hazikubaliwi na Allah swt. Na katika watu hawa watatu: mmoja ni yule ambaye bila kutimiza wajibu wake anagawa mali yote kama sadaka  au kusaidia, na baada ya hapo anakaa akiomba dua:

“Ewe Allah swt naomba unipe riziki.”

Basi hapo atajibiwa, “Je mimi nilikuwa sikukufanyia njia ya kujipatia riziki?”

 

2.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Bora ya sadaka  zote ni ile kufanya wakati mtu anapofanya katika hali unapokuwa sawa.”

 

3.  Hisham bin Al Muthanna anasema:

“Kuna mtu mmoja alimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuhusu tafsiri ya ayah Surah An Am, 6, Ayah 141.

Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisio tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu,

“Katika Ansaar alikuwako mtu mmoja (aliwapa jina lao) ambaye alikuwa ana shamba. Pale mazao yake yalipokuwa yakiwa tayari yeye alikuwa akigawa yote katika sadaka, na alikuwa hawapi chochote watoto na wana nyumba yake; na kwa tendo lake hili Allah swt alikuwa akimhesabia yeye kama ni mfujaji na mbadhirifu.”

 

4.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Baada ya mtu kujitolea kile kiasi alicho na dharura nacho kwa mujibu wa mahitaji yake na baadaye katika kiasi kinachobaki akitoa sadaka basi hiyo sadaka  ni bora kabisa.”

 

5.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema:

“Mojawapo katika Nasiha na Mawaidha ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ilikuwa ni kila aina ya wema ni sadaka  mojawapo, na sadaka  iliyo bora kabisa ni pale kutoa wakati mtu ameshajitimizia wajibu wake na ametosheka, na mkumbuke kuwa muwape wale ambao kwao nyie mnawajibika kuwatimizia mahitaji yao.

 

Mkono wa mtoaji ni afadhali kuliko mkono wa mpokeaji. Kwa hakika mtu ambaye anachuma kwa uwezo wake na kutumia kwa ajili yake na kuwatimiza mahitaji yao basi Allah swt kamwe hatamlaumu.”

 

6.  Mtu mmoja alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kumlalamikia

     kuhusu njaa:

“Basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimtuma mmoja wa wake zake naye alipowaendea wakamwambia kuwa wao walikuwahawana chochote isipokuwa maji ya kunywa tu, na kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwambia, je kuna yeyote yule atakaye mchukua mtu huyu kuwa mgeni wake kwa usiku huo?”

 

Na kwa hayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. akasema,

“Ewe Mtume wa Allah swt ! Mimi nakubali kumchukua huyu kama mgeni wangu kwa usiku wa leo.” Na walipofika nyumbani kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. , Imam a.s. alimwuliza Bi. Fatimah az-Zahra a.s. “Je nyumbani kuna chakula chochote?”

 

Kwa kusikia hayo Bi. Fatimah az-Zahra a.s. akasema, tuna chakula kiasi cha kuwalisha watoto wetu tu lakini na mgeni pia ana haki yake.”

 

Na hapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. akasema

“Wewe walaze watoto, na uizime taa.”

 

Asubuhi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alipokuja mbele ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwelezea kisa kilivyotokea na wakati bado akiwa anaelezea kisa hicho ayah ifuatayo iliteremshwa Surah Al Hashri, 59, ayah 9. :

Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.

 

 


43. NI KARAHA KUKWEPA NJIA WANAYOPITA MASKINI. NI SUNNAH KUTOKEZEA MBELE YA WAOMBAJI NA KUWASAIDIA KITOSHELEVU KWA KUTOA SADAQAH.

 

1.  Muhammad bin Yaqub Kuleiyni amenakili riwaya kutoka Abu Nasar kuwa yeye amesoma barua ambayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimwandikia Abu  Ja’afar (Mutawakili, mtawala wa Ki Abbasi). Humo kulikuwa kumeandikwa:

“Ewe Abu Ja’afar ! nimepata habari kuwa wewe unapotoka nje wakati umekaa juu ya usafiri wako basi wafanyakazi wako wanakutoa nje kwa kupitia mlango mdogo, ili kwamba yule ambaye ana shida na mwenye kuuhitaji msaada wako asiweze kufaidika hivyo.

 

Mimi kwa kiapo cha haki yangu ninakusihi kuwa kutoka kwako na kuingia kwako uwe kupitia mlango mkubwa na uwe na wingi wa dhahabu, fedha na mali ili atakapo tokezea mbele yako mwombaji mwenye shida uweze kumsaidia. Wajomba zako wanapokuomba uwape Dinar hamsini na wake zao wanapokuomba uwape Dinar ishirini na tano na usiwape chini ya hapo kama utawapa zaidi basi hilo ni shauri lako.

 

Na hii nakuambia kwa sababu iwapo wewe utafuata hivyo basi Allah swt atakuwia wema, hivyo utumie na usiwe na shaka katika ahadi na neema za Allah swt mmiliki wa malimwengu yote.”

 

 


44. NI SUNNAH KUTOA KITU CHOCHOTE KILA SIKU KATIKA NJIA YA ALLAH SWT.

 

1.  Safwan anasema kuwa siku moja Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. alimwuliza mmoja wa wahudumu wake:

“Je leo mmetoa chochote katika njia ya Allah swt ?”

 

Naye alijibu hapana, leo sijatoa chochote bado.”

 

Kwa hayo Imam a.s. alisema

“Sasa usipotoa hivyo unategemea Allah swt atupe baraka kwa misingi gani? Lazima utoe kwa njia ya Allah swt hata kama itakuwa ni Dirham moja.”

 

 


45. KUTOA SADAQAH NI SUNNAH LAKINI KUSAIDIA KUTOA MSAADA KWA KUTEGEMEANA NA WADHIFA WA MTU NI FARADHI.

 

1.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa Ayah ya Qur'an Surah Al-Hajj, 22 , Ayah 28:

Ili washuhudie manufaa yao na walitaje juna la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya nyama haoa alio waruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri.

 

“Allah swt katika ayah hii anamaanisha kuwalisha wale walio na shida na kuwasaidia, ambapo wao kwa heshima zao wenyewe hawajitokezi nje mbele ya watu kuomba.”

 

2.  Isack bin Ammar amenakili riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Utafika wakati mmoja ambapo waombaji wanaorefusha mikono yao kwa watu watakuwa wakiishi kwa starehe na wale watakao kaa kimya kwa kutunza heshima zao watakuwa wakifa kwa shida zitakazo kuwa zikiwakabili.

 

Kwa hayo mimi nikamwuliza Imam a.s.,

“Ewe Maula ! Je yakitokea hayo katika zama za uhai wangu mimi nifanyeje?”

 

Kwa hayo Imam a.s akamjibu,

“Kwa hakika kile ulichonacho wewe uwasaidie hao watu kwa hali na mali na kwa hata cheo chako ulicho nacho na kwa wadhifa wako ulio nao uwasaidie ipasavyo.”

 

 


46. SADAQAH KUTOLEWA KUTOKA MALI ILIYO HALALI NA HAIRUHUSIWI KUTOA SADAQAH KUTOKA MALI ILIYO HARAMU.

 

1.  Abu Basir anasema kuwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliitolea maelezo Ayah ya Qur'an Tukufu Surah Al Baqara, 2, ayah 267  isemayo

Enyi malio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa.

 

Amesema kuwa:

“Zama kabla ya Islam watu walikuwa wamejilimbikizia mali iliyopatikana kwa njia zisizo halali (kwa njia zilizo haramu) na baada ya wao kusilimu, walikuwa wakidhani kuwa kwa kutoa mali iliyo patikana kwa njia haramu, watakuwa wametakasisha mali yao iliyo halali, kwa hivyo Allah swt alitoa amri kuwa sadaka  itolewe kutoka mali iliyo halali tu.”

 

2.  Kwa kuzungumzia ayah hiyo ya juu Shahab amenakili riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Ambamo amesema kulikuwa na kaumu moja ambayo walikuwa na mali nyingi iliyo chafu  (iliyopatikana kwa njia za haramu ). Wakati wao walipoukubalia Islam walianza kuchukizwa na malimbikizo yao hayo machafu na wakataka kutoa kwa njia za sadaka. Allah swt aliwaonya kwa kuwaambia kuwa sadaka  hutolewa kutokea mali iliyo halali tu.”

3.  Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Iwapo watu watachuma au watajipatia mali kwa mujibu wa hukumu za Allah swt na wakaitumia kinyume na hukumu za Allah swt au iwapo watachuma kwa njia zilizo kinyume na hukumu za Allah swt na wakazitumia kwa mujibu wa hukumu za Allah swt; katika hali zote mbili Allah swt hazikubalii.

 

Katika kutaka kukubaliwa sharti ni kwamba mapato hayo yawe yamepatikana kwa njia zilizo halali na zitumiwe katika njia zilizo halali vile vile.”

 

4.  Halabi anasema kuwa mtu mmoja alimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuhusiana na ayah hii katika Qur'an Tukufu Surah Al Baqarah, 2, ayah 267:

Enyi malio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa.

 

Na hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akasema:

“Wapo baadhi ya watu ambao baada ya kuingia katika Uislam bado wameendelea kubakia na mali iliyopatikana kwa njia zisizo halali. Na humo kulikuwa na mmoja ambaye kwa makusudi alianza kutoa sadaka kutoa mali hiyo isiyo halali. Na Allah swt alimzuia kufanya hivyo yaani sadaka  haiwezi kutolewa isipokuwa kutokea mali iliyotokana kwa njia halali.”

 

5.  Katika Ma’anil Akhbar Al Imam Hassan al-'Askari a.s. kwa kupitia sanad amenakili riwaya moja kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa amesema:

“Wale ambao wanajiona utukufu na wakubwa na ambao wanatenda matendo kwa mujibu wa nafsi zao, mfano wake ni wa yule mtu ambaye mimi nilisikia watu wakimsifu sana na kumheshimu sana, na hivyo mimi nikawa na shauku ya kutaka kuonana na mtu huyo lakini katika hali ambayo yeye hataweza kunitambua. Siku moja mimi nilimwona alikuwa amezingirwa na watu. Baada ya muda mchache kupita mimi nikamwona yeye ametoka humo na akawa anaondoka, basi mimi nilimfuata nyuma yake.

 

Tulipita katika duka la muuza mikate, huyo mtu kwa kuficha macho yake na kificho ficho akaiba mikate miwili. Kwa hakika mimi nilistaajabishwa mno, na nikadhani kuwa labda wao wana maelewano fulani kabla ya tukio hilo.

 

Tukaendelea mbele yeye akamghafilisha mfanya biashara huyo na akaiba makomamanga mawili humo. Na hapa pia nikafikiria kwa labda wao watakuwa na maelewano kama hayo kabla ya kutokea tukio hili, nikiwa hapo nikaingiwa na wazo kuwa je iwapo watakuwa na maelewano kama hayo basi kwa nini achomoe vitu kimafichoficho?

 

Basi mimi niliendelea kumfuata nyuma yake, tukafika njiani akamwona mtu mmoja mgonjwa basi huyo akasimama kwa mgonjwa huyo na akatoa ile mikate miwili na hayo makomamanga mawili, akampa huyo mgonjwa.

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamwuliza huyo mtu kulikuwa na dharura gani kwa kufanya hivyo. Mtu huyo kwa kuniona mimi akasema je wewe ni Ja’afar bin Muhammad ? Nami nikamjibu naam, basi yeye hapo akaanza kusema nasikitika sana kwa kutokujitambulisha kwako hapo kuja kukufikishia faida (kwa sababu Imam a.s. alikuwa hakujionyesha kuwa yeye ni Imam bali alikuwa amejiweka kama yeye ni mtu wa kawaida)

Imam a.s. akamwambia kwa hakika matendo yako hayo yana aibisha.

 

Basi yeye akasema kuwa Allah swt anasema katika Qur'an Tukufu Surah An A’Am, 6, Ayah 160:

Afanyae wema atalipwa mfano wake mara kumi. Na afanyae ubaya hatalipwa ila sawa nao tu. Na wao hawatadhulumiwa.

 

Ama kwa mujibu wa ayah ya Qur'an Tukufu mimi nimeiba mikate miwili hivyo nimetenda madhambi mawili na nimeiba makomamanga mawili hivyo nimetenda madhambi wawili na kwa ujumla nimetenda madhambi manne.

 

Na pale mimi nilipompa mgonjwa sadaka  mimi kwa kila wema nimepata malipo kumi ya thawabu hivyo jumla nimepata malipo ya thawabu arobaini. Na kutoka arobaini ukitoa nne ninayo mema thelathini na sita bado.”

 

Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamjibu:

“Mama yako akae kwenye kilio chako! Wewe kwa hakika umeitoa maana isivyo ya Ayah za Qur'an Tukufu. Je wewe huelewi ayah ya Qur'an Tukufu isemayo Surah Al Maida, 5,  Ayah ya 30:

Basi nafsi yake ikampelekea kumuuwa nduguye, akamuuwa na akawa miongoni mwa wenye kukhasirika.

 

Kwa mujibu wa ayah hiyo wewe umeiba mikate miwili umetenda madhambi mawili na kwa kuiba makomamanga mawili umetenda madhambi mawili mengine na hivyo jumla umetenda madhambi manne, na pale ulipotoa hiyo mali yaani mikate na makomamanga, kama sadaka  bila idhini ya mwenye mali basi umetenda madhambi mengine manne. Kwa hivyo umetenda madhambi nane kwa pamoja. Sasa wewe unafikiria mema hayo arobaini yametoka wapi?”

 

Kwa hakika mtu huyo aliduwaa, akimwangalia Imam a.s. na akajiondokea zake.

 

Baada ya hapo Imam a.s. akasema kwa kujitolea maana potofu ya ayah za Qur'an Tukufu vile isivyo sahihi ndio matokeo yake haya na vile vile kuwapotosha watu wengine pia.”

 

7.  Katika tafsiri Ayyashi Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amenakiliwa akitoa tafsiri ya ayah Surah Al Baqarah, 2, ayah ya 267:

Enyi malio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa.

 

Imam a.s. akaelezea:

“Miongoni mwa watu kulikuwa kumelimbikwa mali iliyopatikana kwa riba na njia zingine zisizo za halali, basi wao walinuia kutoa sadaka  humo, na ndipo Allah swt alipowakataza kufanya hivyo (kutoa sadaka  kutoka mali iliyopatikana kwa njia za haramu hairuhusiwa).”

 


47. KULISHA CHAKULA NI SUNNAH.

 

1.  Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. ameripoti riwaya kutoka kwa Al Imam Ja'afer  as-Sadiq a.s. kuwa amesema:

“Katika vitu vya kuleta uokovu mojawapo ni kuwalisha chakula wale wenye kuwa na shida na dhiki, na pili mtu awe ni mwanzilishi awe ni mwanzo wa kutoa salamu na vile vile wakati watu wamelala usingizi mtu anaamka kwa ajili ya kusali na kufanya ‘ibada.”

 

2.  Muhammad  Yakub amenakili kutoka ‘Ali bin Ibrahim ambaye naye amenakili kutoka Muhammad bin ‘Isa bin ‘Ubaid ambaye naye amenakili kutoka Ahmad bin Muhammad naye amenakili kutoka ibn Fazzal Ma’aruf naye kutokea Tha’alaba bin Maymun ambaye naye pia amenakili riwaya hiyo kutoka kwa Zararah, kuwa Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa:

“Allah swt hupendezewa mno kulishwa chakula wale wenye dhiki na shida na njaa, na vile vile hupendezewa kutolewa kwa dhabihu (qurbani).”

 

3.   Hisham bin Hakam amenakili riwaya kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Tendo lililo bora na la kipenzi mbele ya Allah swt ni kule kumlisha muumin mwenye njaa mpaka akashiba, ama kummalizia shida aliyonayo au kumlipia deni lake.”

 

4.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:

“Siku moja waliletwa wafungwa ambao walikwisha kutolewa hukumu ya kuuawa mbele ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Basi ikatokea kwamba mmoja wa wafungwa hao alipoletwa mbele ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Malaika Jibrail a.s. akaja akamwambia Mtume :”Ewe Mtume wa Allah swt ! Huyu mtu adhabu yake iahirishwe kwa leo.  Na wengine waliendelea kuletwa na hukumu zikapitishwa na hatimaye wakauawa. Na mwisho yule mtu aliporudishwa mbele ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na tena Malaika Jibrail a.s. akatokezea akamwambia:

 

“Ewe Mtume wa Allah swt ! Allah swt anakusalimia na huyu mtu huwa anawalisha wale wenye kuwa na shida, na mkarimu kwa wageni, mwenye kusubiri wakati wa shida na dhiki, anayechukulia majukumu na wajibu wa watu wengine kwa kuwasaidia.”

 

Basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia huyo mtu kuwa Malaika Jibrail a.s. amekuja na kumwambia habari hizo, na hivyo yeye alikuwa akimfanya yeye awe huru. 

 

Kwa kujibu huyo mtu akasema:

“Je Allah swt, mola wako amependezewa na matendo yangu hayo?”

 

Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwambia, “Naam! Na kwa hakika mtu huyo papo hapo aliisoma Kalimah ya Shahada na akaukubalia Uislam na akawa Mwislam  papo hapo; na akasama:

“Kwa kiapo cha Allah swt ambaye amekutuma wewe katika haki, mimi kamwe sijamrudisha mtu yeyote akiwa amehuzunika yaani bila kusaidiwa kutoka mali na miliki yangu.”

 

5.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anamnakili baba yake Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. kuwa amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Kisu kinapita haraka sana katika shingo ya mnyama lakini kwa kasi zaidi ya kisu ni kile chakula anacholishwa yule mwenye kuhitaji na dhiki.(hivyo malipo yake ni kasi zaidi kwa Allah swt )”

 

 


48. MTOE SADAQAH KUTOKA VILE VITU MNAVYOVIPENDA SANA.

 

1.   Al-Kuleyni anaandika riwaya kuwa Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. :

“Ilikuwa ni tabia yake kuwa alikuwa kila alipokuwa akikaa kula alikuwa ana beseni moja ambamo alikuwa akiweka kila aina chakula iliyokuwa mbele yake kidogo kidogo na alikuwa akitoa hukumu kuwa beseni hiyo ipelekwe kugawiwa kwa wenye shida na muhitaji. Na hapo akasoma ayah ya Qur'an Tukufu ifuatayo: Surah Al Balad,  90,  ayah 11:

Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.

 

Na baadaye akasema Allah swt anaelewa wazi wazi kuwa katika uwezo wa kila mtu kumfanya huru mtumwa kwa hiyo na hivi ndivyo alivyofungua njia ya kumfikisha mtu hadi kuingia Jannat.”

 

2.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. katika Sadaka alizokuwa akitoa alikuwa akitoa sukari pia.

Kwa hivyo kulitokea mtu mmoja akamwuliza, Yabna Rasulallah! Kwa nini unatoa sukari? Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alijibu:

“Mimi ninapenda sana sukari, na ninapenda kuwa niwe nikitoa Sadaka  kwa kile kitu ninachokipenda sana katika njia ya Allah swt.”

 


49. IMESISITIZWA MNO KUWANYWESHA MAJI WANAADAMU NA WANYAMA HATA KAMA HAPO KUTAKUWA NA MAJI MENGI MNO.

 

1.   Al-Kuleyni amemnakili Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ambaye naye amemnakili

      Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. riwaya kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Siku ya Qiyama tendo jema kabisa malipo yake watapewa wale watu ambao wamefanya wema katika kugawa maji.”

 

Riwaya hiyo hiyo Sheikh Sadduq a.s. ameielezea pia.

 

2.   Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Sadaka  iliyo bora kabisa ni ile ya kuutuliza moyo unaowaka kwa kiu cha maji.”

 

3.   Ali ibn Ibrahim amenakili riwaya kutoka kwa baba yake kuwa

      Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:

“Pale panapokuwa na maji na mtu akatoa Sadaka ya kuwagawia watu maji basi Allah swt humjaalia thawabu za kumfanya huru mtumwa mmoja, na pale ambapo hakuna maji kabisa na mtu akatoa Sadaka ya kugawa maji basi Allah swt humhuisha mtu mmoja na kwa hakika mtu anayemhuisha mtu mmoja ni sawa sawa na kuhuisha ulimwengu mzima.”

 

Riwaya hii vile vile  Sheikh as-Saduq ameinakili.

 

4.   Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa:

“Siku moja alikuja Mwarabu mmoja kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kumwambia:

“Ewe Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.! Naomba unionyeshe tendo ambalo litaniingiza mimi peponi. Kwa kusikia hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema: Chukua Mashk (chombo cha kujazia maji iliyokuwa ikitumika katika zama hizo na ilikuwa ikitengenezwa kwa ngozi) na uwapelekee maji hayo familia ambayo ipo inateseka kwa kukosa maji na kiu kinawasumbua sana kiasi kwamba watakapo pata maji hayo watayanywa kwa haraka sana. Basi uelewe kuwa wewe utaipata Jannat kabla hata maji hayo hayajaisha au Mashk yako hiyo haijatoboka.”

 

5.   Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Bila shaka, Allah swt anafurahishwa mno kwa kuona mtu anawanywesha maji wanaadamu au wanyama ambao kwa joto au kiu kali kabisa kinacho wasumbua hao na Allah swt siku ya Qiyama atamjaalia kivuli. Na kwa hakika hakutakuwa na kivuli kingine chochote isipokuwa kile kilichotolewa na Allah swt tu.”

 

6.   Ibn Abbas anasema kuwa mtu mmoja katika kutaka kumhurumia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema:

“Ewe Mtume wa Allah swt! Je ni tendo gani lile nifanye mimi ili niweze kuwa mustahiki wa kuingia Jannat?”

 

Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwambia:

“Nunua Mashk moja mpya na uwe ukiwanywesha watu maji kutoka humo, hadi Mashk yako hiyo itakapofika hatua ya kuja kutoboka (yaani itakapo chakaa au kuzeeka). Basi kwa tendo hili kwa hakika ndilo litakalo kufikisha wewe Jannat.”

 

7.   Abu Hamza Thumali amenakili riwaya kutoka kwa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s.  kuwa amesema:

“Yeyote yule atakaye mlisha na kumshibisha muumin ambaye ana njaa basi Allah swt siku ya Qiyama atamlisha matunda ya Jannat, na yeyote yule atakaye tuliza kiu cha muumin ambaye ana kiu basi Allah swt siku ya Qiyama atamnywesha maji ambayo yamepigwa lakiri. Na yeyote yule atakaye mvalisha mavazi nguo muumin ambaye kwa hakika ana shida basi Allah swt siku ya Qiyama atamvalisha mavazi kijani ya Jannat.”

 

 


50. NI SUNNAH KUWATENDEA MEMA WAUMIN NA KUWATIMIZIA MAHITAJI YAO KWA UWEZO ALIONAO MTU NA KUWA NA UHUSIANO MWEMA PAMOJA NA MASHIAH WENZAKE.

 

1.   Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. amesema:

“Yeyote yule ambaye hakubahatika kutufanyia sisi wema basi ni wajibu wake kuwafanyia mema na kuwatimizia mahitaji ya marafiki zetu.  Na yeyote yule ambaye hakubahatika kudhuru makaburi yetu basi adhuru makaburi ya wafuasi na marafiki zetu.”

 

2.   Muhammad bin Ali bin Hussein Jamil amenakili riwaya moja kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:

“Miongoni mwenu mtu aliye bora kabisa ni yule mwenye moyo mkarimu yaani mwenye moyo wa kutoa na mtu mwovu kabisa ni yule ambaye ni bahili. Na usafi wa imani dalili yake ni kwamba huwawia kwa wema muumin wenzake na kuwatimizia dharura na mahitajio yao. Bila shaka yeyote yule anayewafanyia hisani ndugu zake katika imani basi ndiye mpenzi wa Allah swt kwa sababu katika kufanya wema huko kuna mambo mengi yanayomzuia mtu asiingie katika mitego ya Sheitani na vile vile asiingie Jahannam, na kwa matokeo yake ndiye mtu anayeingia Jannat.”

 

Baada ya hapo Imam a.s. alimwambia Jamil, “Ewe Jamil! Habari hizi uwafikishie wenzako.

 

Kwa hayo mimi nikasema, “Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Niwe fidia juu yako. Je ni watu gani hao?”

 

Imam a.s. akasema: “Hao ni wale ambao wanawafanyia wema ndugu zao katika imani wakati wa shida huwa pamoja nao na vile vile wakati wa furaha pia huwa nao.”

 

3.   Sheikh Sadduq a.s. amenakili riwaya kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ambaye amesema kuwa:

“Yeyote yule ambaye hakupata fursa kufanya wema nasi, basi awafanyie wema wapenzi na wafuasi wetu basi atapata thawabu za kutufanyia wema sisi. Na vile vile ambaye hakubahatika kutuzuru sisi katika uhai wetu na uhai wake basi awazuru wapenzi na wafuasi wetu, basi atapata thawabu kama za kutuzuru sisi.”

 

4.   Safwan Al-Jammal anasema kuwa siku moja Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimwambia Mu’alla bin Hunais:

“Ewe Mu’alla! Uwe wa Allah swt, ili Allah swt aweze kukutunza na kukuhifadhi.

 

Kwa hayo Mu’alla alianza kusema:

“Je hivyo inawezekanaje?”

 

Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamjibu, uwe na hofu ya Allah swt, uwe daima ukimwona yeye katika mawazo yako, kwa hiyo yeye atakifanaya kila kitu kiwe kikikuogopa wewe, na vile vile kitakuwa kikikuwazia wewe na kukujali wewe. Ewe Mu’alla ili kujipatia mapenzi ya Allah swt lazima uwatendee watu matendo mema, na utambue wazi wazi kuwa Allah swt anapendezewa sana na moyo wa ukarimu na huchukizwa sana na ubahili na huwa na uadui nao.

 

Angalia !  Wewe kama utaniomba chochote na mwisho wake wewe ukaaza kufanya mapenzi nami, na badala yake mimi nitafurahishwa sana iwapo wewe hautaniomba chochote na hautapata chochote kutoka kwangu na baada ya hayo wewe bado ukawa na mapenzi nami.

 

Na kwa hakika ukiniuliza mema yote naweza kuyafanya kwa ajili yako basi ukweli ni kwamba sifa zote ni za Allah swt kwa sababu yeye amekupitishia neema yake kwa mikono yangu mimi nimekuwa ni kipitishio tu kwa ajili yako kwa hiyo yeye ndiye anayestahiki sifa zote.”

 

5.   Ali ibn Ibrahim anaandika katika tafsiri yake kuwa mtu mmoja alitokezea katika kikao cha Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. na humo akaanza kuwazungumzia matajiri na mara akaanza kuwasema vibaya na kuwatukana.

 

Kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimwambia, “Nyamaza!”

Wale mafukara ambao wanawajali ndugu na jamaa zao na kuwawia wema wenzao, Allah swt huwapa ujira mzuri sana, kwa sababu Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu: Surah Sabaa, 34, ayah 37:

Na si mali yenu wala watoto wenu watakao kukaribisheni kwetu muwe karibu, isipo kuwa aliye amini na akatenda mema. Hao basi watapata malipo maradufu kwa walio yafanya. Nao watakuwa salama katika maghorofa.

 

 


51. INARUHUSIWA KUTOA SADAQAH KATIKA HALI YA rUKU’U, BALI NI SUNNAH.

 

1.   Sheikh Quleyni amenakili riwaya kutoka kwa Ahmad bin ‘Isa kuwa Allah swt amesema katika Qur’an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake  na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea.

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa kwa neno ‘Innama’ inamaanisha kuwa katika kazi zenu au shughuli zenu zote, mwenye kuwa na haki zaidi kuliko yeyote juu ya nafsi zenu na mali zenu ni Allah swt, baada yake ni Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na baada yake ni, Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na hadi kufikia Qiyama Maimamu a.s. kutokea kizazi chake.

 

Qur’an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake  na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea.

 

Kisa katika ayah hii ni kwamba Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa akisali sala ya Dhuhuri, alipomalizia raka’a ya pili tu akatokezea mwombaji. Siku hiyo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa amevaa  Khullah yenye thamani ya Dirham elfu moja ambayo alikuwa amepewa zawadi na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  Na Imam a.s. alipokuwa katika hali ya Ruku’u, kulitokezea maskini mmoja ambaye akasema, “Ewe Walii wa Allah swt na muumin halisi, iwe salamu juu yako, naomba unipe mimi maskini sadaka yoyote. Kwa hayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. aliinamisha chini Hulla na kwa ishara akamwambia huyo maskini aichukue.”

 

Kwa tukio hili ndipo Allah swt alipoteremsha ayah hii kwa ajili yake na kwa ajili ya kizazi chake na kuonyesha fadhila na kufuzu kwao. Fadhila zao kuwa wanagawa sadaka  hata kama watakuwa katika hali ya Rukuu.

 

Kwa hakika imekuja kujulikana kuwa yule maskini aliyekuja kuomba alikuwa si mtu bali alikuwa ni Malaika ambaye alikuja kuomba, na vile vile katika kizazi kizima cha Maimam a.s. pia tumeona mara nyingi sana Malaika huwa wanakuja kuomba katika sura ya maskini.

 

2.   Katika kitabu kiitwacho Ihtijaj humo Tabarasi amenakili riwaya kutoka Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ameelezea kuhusu ayah hiyo kuwa:

“Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. katika hali ya sala akiwa katika Ruku’u alitimiza wajibu wake na akatoa Zaka na Allah swt ndipo alipoiteremsha hiyo ayah na makusudio yake yalikuwa ni kupata ridhaa ya Allah swt.”

 

3.   Ali bin Ibrahim katika kitabu chake Tafsir ananakili riwaya kutoka kwa baba yake Ma’arifat Safwan kuwa Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema:

“Siku moja Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipokuwa amekaa pamoja na ‘Abdullah bin Salam kulikuwa na kikundi cha Mayahudi pia. Na wakati huo ikateremshwa ayah ya Qur’an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake  na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea.

 

Baada ya hapo mara Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akatoka nje haraka na akaelekea msikitini na huko njiani alikutana na mwombaji mmoja na hivyo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza:

“Je kuna mtu aliyeweza kukusaidia?”

 

Basi huyo mwombaji akasema,

“Naam, kuna mtu anayesali msikitini humo ndiye aliyenisaidia.”

 

Na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alivyoukaribia msikiti akamwona huyo mtu si mwingine bali ni Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.

 

Na riwaya hii vile vile imenakiliwa na Abu Hamza ambaye ameandika katika Tafsir Ayyashi.

 

4.   Muhammad bin Ali bin Hussein katika kitabu cha Amali amenakili riwaya kutoka Abul Ja’rud Ma’rifat kuwa Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amenakiliwa riwaya kuwa amezungumzia kuhusu ayah

Qur’an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake  na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea.

 

Kama ifuatavyo:

“Katika Mayahudi ambaye mnafiki mmoja alipoukubalia Uislam akaanza kuiga:

“Ewe Mtume wa Allah swt! Je ni nani Wasii na Khalifa wako? Na nani huyo atakaye kuwa Walii baada yako?”

 

Ndipo hapo ayah hiyo ilipoteremshwa na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akawaambia inukeni, basi hao wote wakainuka na wakaanza kuelekea msikitini. Walipofika msikitini wakakutana na maskini mmoja akitoka nje na hivyo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwuuliza, “Je kuna mtu yeyote aliyekupa chochote ?” Huyo akasema “Kwa nini isiwe hivyo pete hii je niliyoipata?” Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema,”Je ni nani aliyekupa?”

 

Huyo mwombaji akasema “Huyo mtu ambaye bado anasali.”

 

Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema

“Je alipokupa hiyo pete alikuwa katika hali gani?”

 

Huyo mwombaji akasema alikuwa katika hali ya Ruku’u. Na hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipopaaza sauti ya Takbira yaani Allahu Akbar na wale wote waliokuwepo pamoja naye nao pia walitoa Takbira kwa nguvu na sauti na hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ndipo alipowaambia wote:

“Mtambue wazi kuwa baada yangu Walii ni huyu Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. na wa si mwingine”

 

Karta anasema kuwa

“Kwa mujibu wa riwaya zilizopatikana kuwa katika sala moja aliitoa Hullah, na katika sala ya pili alitoa pete basi inadhihirika kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. anatoa sadaka katika hali ya sala zaidi ya mara moja ndivyo inavyothibitika kwa mujibu wa riwaya zinazopatikana.”

 

5.   Ayyashi katika Tafsir yake ananakili riwaya moja kutokea kwa mwana wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kwa Ammar Yasir amesema:

“Siku moja Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alipokuwa akisali sala ya Sunnah aliahirisha tendo moja kiasi kwamba mpaka akavua pete yake kwa ajili ya kumpa aliyekuja kuomba. Na pale Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipokuja basi alimwelezea hivyo. Na wakati huwo iliteremshwaayah yake hadi kufikia :

Qur’an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake  na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea.

 

Basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alitusomea ayah hiyo na akasema,

“Yeyote yule ambaye mimi ni Mawla wake basi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ni Mawla wake. Ewe Allah swt! Uwe na mapenzi na yule ambaye anawapenda wao, na uwe na uadui na yule ambaye anafanya uadui pamoja nao.”

 

 


52. KUGAWA NUSU YA MALI KATIKA SADAQAH NI SUNNAH.

 

1.   Halabi anasema kuwa yeye alipomwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. basi Imam a.s. akamjibu:

“Naam kabisa! Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. aligawa nusu ya mali yake katika njia ya Allah swt – hadi kwamba nguo kwa nguo, Dinar kwa Dinar, alivigawa vyote katika njia ya Allah swt, na alikwenda Hija ishirini kwa kutembea na miguu.”

 

 

MWISHO.

 


MAREJEO YA SADAKA KATIKA QUR’ANI TUKUFU

 

Na

MAUDHUI

SURAH : AYAH

1

‘Ibada katika Sadaka

2:261; 2:262; 2:265; 2:272; 9:99; 76:9; 90:6

2

‘Ibada na Sadaka

22:35

3

Asili ya Sadaka

4:78; 4:79

4

Athari za Sadaka

2:177; 2:261; 2:268; 2:271; 3:92; 3:180; 5:12; 32:16; 47:36; 51:19 57:7; 57:10; 57:11; 57:24; 68:17; 69:34; 70:35; 90:17; 92:21

5

Baraka zitokanazo na Sadaka

30:39

6

Biashara na Sadaka

34:39

7

Faida za Sadaka

9:103

8

Habari watoao  Sadaka

22:37

9

Hishima katika Sadaka

2:148

10

Imani baada ya Sadaka

41:6

11

Imani na Sadaka

32:16

12

Kanuni za Sadaka

2:177; 6:141; 9:104

13

Kasoro katika kutoa Sadaka

17:29

14

Kuachwa kwa Sadaka

3:180; 4:39; 68:17; 74:43

15

Kuepusha Sadaka

63:10

16

Kunyenyekea katika Sadaka

3:92

17

Kusikitika kuhusu Sadaka

90:4; 90:6

18

Kusita katika Sadaka

2:195; 2:254; 2:268; 9:67; 63:10

19

Kutumia mali katika Sadaka

2:215; 2:245; 17:29; 23:57; 23:100; 24:33; 47:36; 47:37; 47:38; 57:11; 63:10; 68:19; 

20

Kuwa na moyo kwa Sadaka

2:177

21

Lipeni Sadaka kutokea mbao

22:28; 22:36

22

Mabaya katika Sadaka

2:262; 2:264

23

Mabedui na Sadaka

9:98

24

Mafanikio ya Sadaka

90:10

25

Majamaa wapewe Sadaka

2:177; 2:215

6

Makatazo kutoka Sadaka

63:7

27

Malengo ya Sadaka

3:117

28

Malipo ya Sadaka

35:32

29

Malipo ya Sadaka

56:18

30

Mambo mapya katika Sadaka

57:10

31

Manufaa ya Sadaka

2:195; 2:272

32

Masharti ya Sadaka

76:9

33

Masikini wapewe Sadaka

2:215; 51:19

34

Masikitiko juu ya Sadaka

90:6

35

Matumizi ya Sadaka

2:273

36

Mumin na Sadaka

27:3

37

Mwelekeo katika Sadaka

2:148

38

Nia katika Sadaka

92:19

39

Njia za Sadaka

11:31

40

Nyayo za Sadaka

9:103; 51:19; 58:12

41

Ongezeko kufuatia Sadaka

30:39

42

Sadaka bora kabisa

2:273

43

Sadaka itokanayo na urithi

89:19

44

Sadaka kwa kupiga magoti

5:55

45

Sadaka watoao makafiri

6:136

46

Sadaka watoao Wanafiki

9:53; 9:54

47

Sadaka ya Allah swt

2:195; 2:245; 3:17; 30:38; 42:38; 56:18; 63:7; 63:10; 64:16; 64:17; 65:7; 73:20; 92:18;

48

Sadaka za makafiri

6:136

49

Swala la Sadaka

2:215

50

Taratibu ya Sadaka

2:215

51

Uchoyo katika Sadaka

47:37; 53:34; 57:10; 57:24; 68:17; 68:19; 68:28; 69:34; 89:17

52

Ufujaji katika kutoa Sadaka

17:29

53

Uhakika wa Sadaka

2:261; 2:265; 5:12; 90:4; 90:6

54

Umuhimu wa Sadaka

2:196; 2:277; 14:31; 28:54; 30:38; 35:29

55

Umuhimu wa Sadaka

6:141

56

Unafiki katika Sadaka

2:264; 2:266; 2:270; 4:38; 4:39

57

Upotevu au Sadaka ?

34:39

58

Ushawishi katika Sadaka

2:245; 3:180; 4:40

59

Utaratibu wa Sadaka

3:92

60

Uthamini wa Sadaka

9:104

61

Utumiaji wa Sadaka

2:273

62

Uwajibu katika Sadaka

2:262; 2:263; 2:264; 2:266; 90:6

63

Uwastani katika Sadaka

2:195; 25:67

64

Uwema katika Sadaka

2:177

65

Vipangimizi katika Sadaka

2:268

66

Vipimo vya Sadaka

2:219

67

Wakati wa Sadaka

2:274

68

Wanafiki na Sadaka

63:7

69

Wayahudi na Sadaka

5:12

70

Sadaka za wana wa Israil

2:83

71

Sadaka za Mayahudi

2:43

72

Utaratibu wa Sadaka

9:104

 

 


VITABU VILIVYOKUSANYWA NA KUTARJUMIWA NA

AMIRALY  M. H.  DATOO  - P.O. Box  838

BUKOBA TANZANIA

e-mail : datooam@hotmail.com

Na unaweza kuvipata katika Internet katika :

http://www.al-islam.org/kiswahili

 

1.    UHARAMISHO WA KAMARI

2.    UHARAMISHO WA RIBA

3.    UHARAMISHO WA ULEVI

4.    UHARAMISHO WA ULAWITI

5.    UHARAMISHO WA  ZINAA

6.    UHARAMISHO WA UWONGO  (juzuu ya kwanza )

7.    UHARAMISHO WA UWONGO  (juzuu ya pili )

8.    USAMEHEVU KATIKA ISLAM

9.    TAJWID ILIYORAHISISHWA

10. KITABU CHA TAJWID

11. KESI YA FADAK

12. TAWBA

13. BWANA ABU TALIB a.s. MADHULUMU WA HISTORIA

14. FADHAIL ZA IMAM ALI IBN ABI TALIB a.s.

15. TADHWIN AL-HADITH

16. TAFSIRI YA JUZUU’ ‘AMMA

17. HUKUMU ZILIZOTOLEWA NA IMAM ALI IBN ABI TALIB a.s.

18. MSAFARA WA AL-IMAM HUSSEIN IBN ‘ALI IBN ABI TALIB A.S MADINA – KARBALA

19. DALILI ZA QIYAMA NA KUDHIHIRI KWA IMAM MAHDI a.s.

20. NDOA KATIKA ISLAM

21. MAKALA MCHANGANYIKO  No. 1

22. MAKALA MCHANGANYIKO  No. 2

23. UWAHHABI – ASILI NA KUENEA KWAKE

24. HEKAYA ZA BAHLUL

25. SHADA LA MAUA KUTOKA BUSTANI YA AHADITH

26. HIARI NA SHURUTISHO KATIKA ISLAM

27. WAANDISHI MASHIA KATIKA SAHIH NA SUNNAHN ZA AHL SUNNA

28. USINGIZI NA NDOTO

29. MAJINA KWA AJILI YA WATOTO WAISLAMU

30. QURBAA - MAPENZI YA WANANYUMBA YA MTUME S.A.W.W.

31. TUSIUPOTEZE WAKATI

32. DHAMBI KUU LA KUTOKULIPA ZAKA, KHUMS NA SADAKA

33. JANNAT NA JAHANNAM

34. MASIMULIZI YA HADITH KUTOKA QUR’AN

35. SADAKA

36.  FAHISTI YA AYAH ZA QUR’AN TUKUFU KIMAUDHUI

 



[1] *Tabaqat al-Kubra , j. 6, uk.168,; Taqyid al-'ilm , uk. 89,90; Kanz al-‘ummal, j. 10, uk. 156; Rabi’

    al-Abrar, j.. 3 , uk. 294

[2] Bihar al- Anwar, vol. 2 uk. 152; al- Taratib al - idariyyah vol. 2, uk. 246; Sunan al - Darimi, vol 1, uk.

   130; Ilal al - Hadith, vol. 2, uk. 438; Taqiyyad al - Ilm, uk. 91; Jami’bayan al - ‘ilm, uk.99; Kanz

    jumat al - Imam al - Hasan min Tarikh Dimashq, uk. 167.

[3] Al - Tabaqat all- Kubra, vol. 6 uk.220.

[4] Ansab al - ashraf, vol. 2 uk.98; na Hadith no. 1980 kutokea maisha ya Imam Ali (a.s.) katika Tarikh

  Dimashq Historia ya Damascus); Bihar al- Anwar, vol.2 uk. 230; al - Fadhail ya Ibn Hanbal, Hadith

   no. 222.

[5] Ansab al - Ashraf, vol. 1, uk. 121; Tarikh Dameshq, vol. 38, uk. 202; Hilyat al - awliya, vol. 1, uk. 67;

   Shawahid al - tanzil, Hadith no. 1009.

[6] Ansab al - Ashraf, vol. 2, uk. 145.

[7] Bihar al - Anwar, vol. 2 uk. 50 kutoke  ashf al - Mahajjah.

[8] Bihar al - Anwar, vol. 2, uk. 152.

[9] Bihar al - Anwar, vol. 2, uk 153.

[10] Kwa ajili ya kutaka kuelezwa zaidi juu ya Hadith zizungumziazo swala hili urejea Makatib al –

   Rasul, vol. 1, uk. 71 na 89 iliyoandikwa na Ali Ahmad Miyanji.

[11] Taqyid al - ilm, uk. 89.

[12] Rawdhat al - Jannat, vol. 8, uk. 169.

[13] Taqyid al - Ilm, uk. 104.

[14] Tarikh al - adab al - ‘ Arabi, “al -’ Asr al - Islami”, uk. 453, ambapo masimulizi kama hayo hayo

   yametolewa na Mustafa Abd al - Razzaq; rejea  Tamhid li - tarikh al - falsafah al - Islamiyyah,

   uk.202,203.

[15] Al-Muraja’at , uk. 305,306, iliyochapishwa na al-’Alami,Beirut.

[16] Ta’asis al-Shiah li-ulum al-Islam, uk.280, iliyochapishwa na al-Alami, Beiru.

[17] Rijal al-Najishi, uk.3,4, iliyochapiswa Qum.

[18] Qamus al-Rijal, chini ya maisha ya Muhammad ibn Abd Allah ibn al-Hassan;Rawdhat al Jannat

     vol. 8,uk. 169.

[19] Rijal al-Najashi,uk. 3,4, iliyochapishwa Qum.

[20] Fur’ al - Kafi, vol.2, uk.666; kwa mifano mingine rejea  Fur al-Kafi, vol.7 uk.77.

[21] Wasa’il al-Shiah, sura juu ya Zakati; rejea Makatib al-Rasul vol. 1, uk.73.

[22] Was’il Shiah, sura juu ya  Jihad (vita vitukufu); Makatib al-Rasul, uk.176.

[23] Wasa’il al-Shiah, sura juu ya Qadha.

[24] Furu al-Kafi, vol.7, uk 94.

[25] Was’il al-Shiah, sura juu ya al - Hudud.

[26] Furu al - Kafi, Vol. 7. uk.98.

[27] Al-Tabaqat all-kubra, vol 2. uk. 389; al-Musnaf ya Abd al-Razzaq, vol. 1, uk. 285; Taqyid al-Ilm. uk

    107.

[28] Jami’bayan al-Ilm, vol.1, uk.92.

[29] Al-Musannaf ya Abd-Razzaq, vol.7, uk.337.

[30] Al-Tabaqat al-Kubra, vol.7, uk 447.

[31] Sunan al-Darimi, vol.1,uk.126; Taqyid al-Ilm uk. 105,106.

[32] Sunan al Darimi, vol.1. uk. 126; Akbhar Isbahan, vol 1, uk. 312; Tadhrib al-rawi, uk. 90  ya al-

    Siyuti..

[33] Al-Jarh wa al-ta’dil, vol. 1, uk.184.

[34] Tarik al-Khulafaa, uk. 261 ya al-Suyuti.

[35] Tadhkirat al-Huffadh, vol. 1, uk. 169,170,191,203.

[36] Jami’bayan al-Ilm, vol. 1, uk.88,91.

[37] Jami’bayan al-Ilm, vol. 1, uk.92.

[38] Muqaddamata Fath al-Bari, uk.4,5.

[39] Tadhkirat al-Huffadh, vol.1, uk.160.

[40] Kashf al -zunun, vol. uk. 237.

[41] Tadhkirat al-huffadh, vol. 1, uk.419.

[42] Ibid., vol.uk. 423 (kama hapo 44)

[43] Tadhkirat al-huffadh, vol.1, uk.423; Tadrib al-rawi uk. 88,89.

[44] Ipo Hadith ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa “Mimi ni mji wa elimu na Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ni mlango wake” na vile vile amesema “Mimi ni hazina ya elimu na Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ni ufnguo wake.” Na zipo Hadith nyingi kama hizo.

[45] Nimetarjumu orodha ya Rawi 100 wa Kishi’ah wanaojuikana na walio ma’arufu katika vitabu vya Ahl as-Sunnah. Kwani wengi wa Masunni wanadai kuwa Mashi’ah ni Rafidhi  (walio asi ) na wengine majaheli kuthubutu kusema kuwa Mashi’ah ni Makafiri. Hivyo itakuwa vyema iwapo utapata makala hayo ukayasoma.

[46]  Mimi ninetarjumu baadhi ya vitabu ,kama inavyoonekana katika fahiristi hapo nyuma ya kitabu hiki, zinazozungumzia madhambi mbalimbali.

[47] Msomaji anaombwa kujaribu kusoma kitabu nilichokitarjumu katika lugha ya Kiswahili kwa jina la Tadhwin al-Hadith (Uchunguzi juu ya ukusanyaji na uandishi wa Hadith) ambamo swala hili limezungumzwa kwa marefu na mapana.

[48] Ndugu msomaji kitabu hiki kinazungumzia mambo ya sadaqah  na kuna kitabu kimoja nimekitarjumu katika lugha ya kiswahili kinachozungumzia dhambi kuu, kutokulipa zaka na sadaqah. Kwa hiyo ili kutaka kusema habari zaidi kuhusu zaka naomba usome kitabu hicho hutapata kulipa mambo marefu na mapana juu ya zaka.

[49] Mara nyingi sisi hatufanyi mambo mema hatutoi Sadaka, hatusali hatufungi saumu na tunafanya usia wakati wa kufa tunategemea tuache usia kwamba kazi fulani nilikuwa nataka kuifanya mtoto wangu aifanye, Sadaka fulani nilikuwa nataka kuitoa mtoto wangu aitoe, siku fulani sikusali mtoto wangu anisalie, saumu sikufunga mtoto wangu anifungie saumu zangu nk. Kwa hakika mambo kama hayo hayana dhamana kuwa yatatimizwa hivyo unaweza kukosa wewe vyote na ukawa  umestahiki wa ghadhabu na adhabu za Allah swt siku ya Qiyamah.

 

[50] Yaani Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alikuwa anamaanisha hapa kuwa angewaongezeapo kidogo.

[51] Nimekitarjumu kitabu juu ya kamari :  Katika Islam Uharamisho wa Kamari. Na kimechapwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania, DSM, Box 200333

[52] Nimekitarjumu kitabu juu ya Jannat (Peponi ) na Jahannam (Motoni)