MAJIBU YETU

Tamko la "AZZIYADAH" katika sura ya kumi aya ya ishirini na sita ni: MUB'HAM halionyeshi chochote kuhusu kuona. Kwa hiyo, huwezi kwa tamko hilo kuthibitisha kuwa Mwenyeezi Mungu anaonekana. Bali lililothibiti waziwazi ni hivi asemavyo Mwenyeezi Mungu kuwa, "Maono hayamfikii bali yeye anayafikia "Maono", 6:103. Kwahiyo, zile hadithi zisemazo kuwa Mwenyeezi Mungu anaonekana ni batili kwa sababu zinapinga Aya. Mwenyeezi Mungu anakataa kuwa: "Maono hayamfikii" na maono ni zaidi kuliko macho!!