MAJIBU YETU

Kwanza, ni muhimu kuangalia maana ya tamko la "ARRU-UYA" yaani "KUONA". Taqriban tamko hili linatumika katika nyanja zifuatazo,

(a) Kuona kwa mboni za macho.

(b) Kuona kwa dhana.

(c) Kuona kwa yaqin.

Sasa: Inaposemwa: Mwenyeezi Mungu anaonekana, ni kwa kupitia kigezo gani kati ya vigezo vilivyotajwa hapo juu au chochote kingine. Ikiwa kuwepo kwa kitu ni sharti ya kuonekana, ni nani basi aliyethibitisha mpaka sasa kuwa ameiona Roho, Akili, Nguvu, Sauti, na kadhalika?!

Kuhusu aya zilizosomwa kuthibitisha kuwa Mwenyeezi Mungu anaonekana, majibu yake ni kama ifuatavyo:

  1. Nabii Musa (a.s.) alikuwa akijua vyema kuwa Mwenyeezi Mungu haonekani duniani wala huko akhera. Wala hilo ombi lake hakukusudia kuomba jambo lisilo wezekana, isipokuwa Nabii Musa hapa ametumia uslub (njia) ya kukomesha madai ya watu wake ambao waling'ang'ania kumtaka awaonyeshe Mwenyeezi Mungu waziwazi kama tunavyo soma katika Qur'an: "Ewe Musa, hatutakuamini mpaka tumuone Mwenyeezi Mungu waziwazi". 2:55
  2. Kwahiyo, Nabii Musa (a.s.) alitaka kumaliza ubishi wao, akatumia ibara kati yake na Mola wake ili afute kabisa matumaini ya ombi la watu wake. Qarina ya nukta hii ni pale aliposema Mwenyeezi Mungu kuwa:

    "Hakika walimuomba Musa makubwa kuliko hayo, na wakasema: Utuonyeshe Mungu wazi wazi." 4:153

  3. Iliposemwa: "FASAWFA TARAANI" yaani "UTANIONA" ibara hii imetanguliwa na tamko la: "LAN TARAANI" yaani, "HUTANIONA ABADANI" silabi ya "LAN" imekuja katika "NAFYU TAABID" "HUTANIONA ABADAN" matumaini ya kumuona Mwenyeezi Mungu hayako aslan, kwa mujibu wa maweko ya silabi na matumizi yake yaliyokuja katika Aya hii.
  4. Iliposemwa: "ILA RABBIHA NADHIRA". yaani, ZIKINGOJA MALIPO KWA MOLA WAO" na wala si ZIKITAZAMA KWA MOLA WAO, hiyo ni tasfiri ya kimakosa kama tutakavyoonyesha. Ku'unganishwa silabi ya "ILA" na silabi ya "NADHAR" hapa kunafidisha maana yaa "KUNGOJEA"

Tutaonyesha mfano hapa kuthibitisha hilo kama ifuatavyo: katika kitabu: Lisanul A'rab juzu ya saba ukurasa 72 imeandikwa hivi:- "INNAMAA NANDHURU ILA LLAHI THUMMA ILAYKA" akafafanua hapo hapo: "INNAMAA ATAWAQQAU FADHLALLAHI THUMMA FADHLAK" Maana ya msitari wa kwanza "Kwa hakika tunangojea fadhila za Mwenyeezi Mungu, kisha fadhila zako" katika msitari wa pili, alikusudia kufafanua ibara isemayo: "NANDHURU ILA LLAHI" akasema;

"ATAWAQQAU FADHLA LLAHI" yaani, "Ninangojea Fadhila za Mwenyeezi Mungu". Hivi ndivyo yalivyo matumizi ya silabi ya "ILA" inapokutana na silabi ya "NADHAR" mara nyingi.