SERA ZA UTAWALA BAADA YA MTUME

Ukisoma Terikh, na kisha ukafuatilia sera za utawala wa makhalifa watatu, utajua wazi kwamba mabwana hao walizuia kuandikwa Hadithi za Mtume Muhammad (s.a.w.) bali walikataza hata kuzizungumza mbele za watu. Kwa sababu walijua wazi kuwa sera za utawala wao haziendi sambamba na uongozi wa Mtume Muhammad (s.a.w.). Abubakr amekataza kuzungumza chochote juu ya Mtume (s.a.w.) na amesema: Yeyote atakaewauliza mseme: "Kati yetu sisi na nyinyi ni Qur'an, basi, halalisheni halali yake na haramisheni haramu yake".

Taz: Tadh'kiratul hufaadh J. 1 Uk. 3

Kauli hii ya Abubakr imekuja baada ya muda mfupi wa tukio la karatasi, Umar bnul Khattab alipomjibu Mtume kuwa: "Mtume anaweweseka, ipo Qur'an inatutosha", Abubakr anasema: "Kati yetu sisi na nyinyi ni Qur'an".....

Qur'an iliyo kati yetu na Abubakr inasema kuhusu wanaozuia zaka: "Na miongoni mwao wako walio mwahidi Mwenyeezi Mungu, akitupa katika fadhili zake bila shaka tutatoa sadaka na lazima tutakuwa miongoni mwa watendao mema. Lakini alipowapa katika fadhili zake, wa kayafanyia ubakhili na wakageuka, nao ndio wakengeukao. Kwa hiyo akawalipa unafiki mioyoni mwao mpaka siku ya kukutana naye, kwa sababu ya kumkhalifu Mwenyezi Mungu ahadi waliyo mwahidi, na kwa sababu walikuwa wanasema uongo". 9:75-77. Aya hizi zimeshuka kwa ajili ya Thaalaba aliyezuia zaka wakati wa Mtume (s.a.w.). Lakini pamoja na yote hayo Mtume (s.a.w.) hakumpiga wala hakumnyang'anya mali yake, ingawa Mtume yote haya alikuwa na uwezo nayo.

Ambapo suala la Malik bin Nawyira na wenzake waliodaiwa kuwa walizuia Zaka katika utawala wa Abubakr. Huo ni msimamo waliouonyesha dhidi ya utawala wa Abubakr aliyepora madaraka yasiyo kuwa yake. Kwa hiyo, kitendo cha kuzuia zaka kutoupa utawala wa Abubakr ni tafsiri halisi ya kupinga utawala huo na wala si kupinga hukumu ya faradhi ya zaka. Sasa, Abubakr yuko wapi na aya hizi aliyedai kuwa ndiyo sera yake?? Mbona amewaua watu waliozuia zaka kwa kigezo gani? Sera ya Abubakr inasema: "Kati yetu sisi na nyinyi ni Qur'an".

Qur'an inasema: "Wanaume wana sehemu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa walio wakaribia, Na wanawake wanayo sehemu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa walio wakaribia" 4:7.

Mwana Fatima bint Muhammad (s.a.w.) alipokwenda kwa Abubakr kutaka mirathi iliyoachwa na baba yake, Abubakr akakataa kumpa akidai kuwa amemsikia Mtume akisema: "Sisi Mitume haturithiwi".

Hapa Qur'an hana haja nayo, ameshika lile asilokuwa na haja nalo tokea awali, hata hivyo, Abubakr kweli maneno ya Mtume anayakubali?

MwanaAisha (Mwanawe) anasimulia tukio hili: Baba yangu alizikusanya Hadithi za Mtume (s.a.w.) ambazo zilikuwa mia tano, akakesha kucha akizigeuzageuza......kulipokucha akasema: Mwanangu! Niletee Hadithi ulizonazo, ni kampa, akazichoma moto!!

Taz: Kanzul Ummal J. 5 Uk. 237

Tadh'kiratul hufaadh J. 1 uk, 5

Je! Ni kweli Abubakr anaitegemea Qur'an tu peke yake?

Mwenyeezi Mungu anasema: "Sadaka ni kwa mafakiri tu na masikini na wanaozitumikia na waungiwao.......mioyo yao.....9:60. Iliposemwa: "Na waungiwao mioyo yao" ni wale waislamu wapya ambao ndio kwanza wanasilimu. Abubakr alipotawala, hukumu ya kifungu cha Aya hii akaifuta!!!

Taz: Tafsirut Tabari J. 10 Uk. 113