POTE LENYE KUOKOKA

Amesema Mtukufu Mtume (s.a.w.) "Watafarakana umma wangu makundi sabini na tatu, kundi moja tu kati ya hayo litaokoka, na yaliyobaki yatatiwa motoni. Ali akauliza: "Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu! Kundi gani litakalookoka? Mtume (s.a.w.) akajibu: "Wewe na watu wako".

Taz: Ithbatul Hudat J. 2 Uk. 260

Mfarakano kwa mara ya kwanza ulitokea kwa Waislamu pale tu alipofariki Mtume Muhammad (s.a.w.). Mtume (s.a.w.) kabla ya kufariki dunia, aliweka sera kamili ya uongozi katika Uislamu. Iliposhuka Aya: "Hakika wale walioamini na wakatenda mema, basi hao ndio wema kushinda viumbe vyote" 98:7. Mtume (s.a.w.) akamwambia Ali: "Wewe Ali na kundi (pote) lako".

Taz: Tafsirut Tabari J. 30 Uk. 171

Mtume (s.a.w.) amesema: "Ali yu pamoja na Qur'an, na Qur'an ipamoja na Mi, hawataachana mpaka wanifikie katika Haudh".

Taz: Faidhul Qadir J. 4 Uk. 358

Musnad Ahmad J. 5 Uk. 31

Alfat'hul Kabir J. 2 Uk.21

Tarikhul Khulafai Uk. 174

Majmauz Zawaid J. 9 Uk. 134

Kifanyatut Talibi Uk. 399

Asnal matalibi Uk 136

Mtume (s.a.w) amesema: "Mimi ninakuachieni vizito viwili ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea baada yangu, Qur'an na Ahlul Bayt wangu, viwili hivi havitaachana mpaka vitakaponifikia katika Haudh".

Taz: Tafsir ibn Kathir J. 4 Uk. 122

Tafsir ul Kazin J. 1 Uk. 4

Tarikhu Bughdad J. 8 Uk. 442

Sahihi Muslim J. 4 Uk. 1873

Jamiul Usul J. 1 Uk. 187

Albidayatu Wannihaya J. 7 Uk. 362

Majmauz Zawaid J. 9 Uk. 163

Musnad Ahmad J. 2 Uk. 17-26

Al Mustadrak J. 4 Uk. 109

Imam Ali (a.s.) mmoja katika Ahlul Bayt wa Mtume (s.a.w.) tazama pale iliposhuka Ayatut Tat'hir: "Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni sana sana" 33:33. Na mke wa Mtume (s.a.w.) (Ummu Salama) alipotaka kuingia katika nguo hiyo Mtume akamzuia!!

Taz: Sahihi Muslim J. 4 Uk. 127

Sahihi Tirmidhi J. 4 Uk. 304

Alkhasais Uk. 4

Tarikh Bughdad J. 9 Uk. 126

Al' Isaba J. 1 Uk. 27

Usudul Ghaba J. 5 Uk. 521

Al Mustadrak J. 2 Uk. 416

Tafsirut Tabari J. 22 Uk. 5-7

Tafsirul Khazin J. 5 Uk. 259

Addurrul Manthur J. 5 Uk. 198