MAJIBU YETU

Katika kitabu "Asha'shaafy" na "At Talkhis" inasema Mtume (s.a.w.) amemuoa Mwana Khadija akiwa bikira.

Amesema Abulqasim Alkufy: Mtume (s.a.w.) alipomuoa Mwana Khadija (a.s.) wanawake wa kikuraishi walimkasirikia sana Mwana Khadija wakisema: Wamekuposa mabwana wa kikuraishi wenye heshima, umekataa kuolewa na yeyote kati yao, umekubali kuolewa na Muhammad, yatima wa Abu Talib Lofa hana mali!! Taz: Al' Istighatha J. 1 Uk. 70