KHADIJA ALIOLEWA NA YEYOTE KABLA YA MTUME?

Inasemekana kuwa: Mtume (s.a.w.) hakuoa mke yeyote aliye bikira isipokuwa Mwana Aisha tu. Wanasema kuwa: "Mwana Khadija kabla ya kuolewa na Mtume (s.a.w.) alikwisha olewa na waume wawili kabla ya Mtume Muhammad (s.a.w.) na amepata watoto wawili.

Tutataja kidogo hapa baadhi ya hoja zinazosemwa juu ya Mwana Khadija kuhusu watoto aliopata kwa waume wengine kabla ya Mtume Muhammad (s.a.w.) ni kama ifuatavyo:

Wanasema: Shahidi wa kwanza katika Uislamu ni mtoto wa Mwana Khadija aitwae Harithi bin Abi Hala, alipata shahada pale Mtume (s.a.w.) alipotangaza Uislamu hadharani.

Taz: Al' Isaba J. 1 Uk. 293

Al'Awaail J. 1 Uk. 311-312

Lakini, hoja hii inaangushwa na riwaya ya Qatada inayosema kuwa: Shahidi wa kwanza katika Uislamu ni Sumayya, mama yake Ammar bin Yasir.

Taz: Al' Isaba J. 4 Uk. 335

Imepokewa kuwa: Mwana Khadija (a.s) alikuwa na nduguye akiitwa Hala, aliolewa na mtu mmoja katika Koo ya Al'Makhzumi, akazaa mtoto wa kike jina lake Hala, Kisha aliachika akaolewa na mtu mmoja katika Koo ya At'Tamim aitwaye Abu Hindi, akamzalia mtoto jina lake Hind. Huyu Abu Hindi, alikuwa na mke mwingine ambaye alimzalia watoto wawili: Zaynab na Ruqayya. Hatimae Abu Hindi na mkewe wa pili walikufa,akabakia Bi Hala ndugu ya Mwana Khadija, pamoja na watoto wawili: Zaynab na Ruqayya. Yule mtoto wake wa kuzaa: Hind, alikwenda kwa jamaa za mumewe. Ndipo Mwana Khadija alipowakusanya wote akawa nao, Bi Hala na watoto wawili walioachwa na mama yao: Zaynab na Ruqayya. Mwana Khadija alipoolewa na Mtume (s.a.w.) Bi Hala alifishwa, wakabaki Zaynab na Ruqayya wakilelewa na Mtume (s.a.w.). Katika mila za Kiarabu, walikuwa wakiamini kuwa mtoto wa kufikia ni mtoto wako halisi, kwa hiyo, watoto hawa wakapewa ubinti wa Mtume (s.a.w.) (Zaynab binti Muhammad na Ruqayya binti Muhammad).

Taz: As' Sahihu Minsiiratin Nabi J. I Uk. 123