MAJIBU YETU

  1. Mwana Aisha wakati wa tukio hilo alikuwa hajaolewa na Mtume, bali yaelekea hata kuzaliwa alikuwa bado!!
  2. Mwenyeezi Mungu anasema: "Utukufu ni wa yeye ambaye alimpeleka Mja wake usiku, kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa mbali" 17:1. lliposemwa: "ASRAA BIA'BDIHI" tamko la "A'BD" hutumiwa kwa roho na kiwiliwili pamoja. Kwa hiyo, Mtume (s.a.w.) alikkwenda mwenyewe akiwa macho.
  3.  

  4. Kama Israa ingelikuwa kwa njozi, basi kusingekuwako na upinzani mkubwa hivyo, na watu wasingeritarddi.
  5. Taz: Tafsir ibn Kathir J. 3 Uk. 24

    Tarikhul Khamisi J. 3 Uk. 308

    Almuswannaf J. 5 Uk. 327

  6. Kama Israa ingelikuwa kwa njozi, basi Abu Talib na Bani Hashim wasingetoka kumtafuta, kwa sababu Bani Hashim walitoka kumtafuta siku hiyo.

Taz: Assahihu Minsiiratin Nabii J. 1 Uk. 276