QUR'AN IMEUMBWA

Ndugu zetu masunni wanaamini kuwa: Qur'an ni ya tangu na tangu (Qadim) Mashia Ithan Ashar wanaamini kuwa: Qur'an imeumbwa.

Kwahiyo, hapa tutachunguza kama ifuatavyo: Katika matumizi ya lugha ya kiarabu, tamko la "JAA'L".

Linapotegemezwa kwa Mwenyeezi Mungu huwa kwa maana ya "KHALQ" yaani, "KUUMBA". Na hapa tutataja baadhi ya mifano hiyo:

  1. "Wajaa'la min'ha zawjaha" yaani, "Na ameumba mkewe".
  2. "Huwalladhi jaa'la lakumul layla" yaani, "Yeye ndiye aliyewaumbia usiku".10:6
  3. "Inna jaa'lna maa'l ardhi ziinatan laha" yaani, "Kwa hakika tumeviumba vyote vilivyoko juu ya ardhi viwe mapambo yake". 18:7
  4. "Jaa'la laum min anfusikum az'wajan" yaani, "Amewaambieni wake katika jinsi yenu". 42:11
  5. "Inna jaa'lnahu Qur'anan a'rabiyyan" yaani, hakika tumeifanya (tumeiumba) Qur'an (kwa lugha ya) Kiarabu". 43:3
  6. "Khaaliqu kulli shay'in" yaani, "Muumba wa kila kitu". 6:102

Sasa, Qur'an ama iwe ni kitu au isiwe ni kitu. Kama itakuwa sikitu, basi yanini kujadili jambo ambalo halipo!! Na endapo itasemwa kuwa Qur'an ni kitu, jee! Ni kwa hoja gani Qur'an itatolewa katika umuun ya ibara hii: "Muumba wa kila kitu"? Na hapana shaka yoyote, Qur'an ni kitu, kwa hiyo: kwakuwa vitu vyote vimeumbwa (kama isemavyo Qur'an) Qur'an nayo pia imeumbwa.