80. SURA `ABASA

Imeteremshwa Makka, ina Aya 42.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

1. Yeye aliukunja uso akapa mgongo.

2. Kwa sababu alijiwa na kipofu.

3. Ni lipi kilichokufanya wewe kujua kuwa yeye atajitakasisha,

4. Au akawaidhika ukamfaa waadhi ?

5. Ama kwa yule ajifikiriaye kuwa amejitosheleza (katika utajiri wa mali yake),

6. Na kwa huyo anamshughulikia,

7. Wala haitakuwa lawama juu yako iwapo hatajitakasa.

8. Ama yule anayekuijia kwa jitihada na moyo mnyenyekevu,

9. Na akiwa na khofu (moyoni mwake),

10. Wewe kwake huyo utamshughulikia na kumsikia

11. Sivyo ! Hakika (Quran) hii ni nasaha.

12. Basi kila apendaye atawaidhika,

13. (Yameandikwa hayo) Katika Vitabu vilivyohishimiwa.

14. Vilivyotukuzwa, vilivyotakaswa,

15. Vilivyo katika mikono ya wajumbe Malaika

16. Watukufu, watiifu wa Mwenyezi Mungu.

17. Amelaaniwa Mwanadamu ! Namna gani alivyokuwa bila shukrani ?

18. Kwa kitu gani Amemuumba ?

19. Kwa tone la manii, alimuumba, kisha akamwekea vipimo vyake.

20. Kisha akafanyia njia nyepesi.

21. Kisha akamfisha na kumfanya azikwe kaburini.

22. Kisha aendapo atamfufua.

23. La ! Hakutimiza vile alivyokuwa ameamrishwa.

24. Basi mtu na akitazama chakula chake.

25. Kuwa ndio sisi tuliomiminisha maji, mmiminiko wa nguvu

26. Kisha tukaipasua ardhi, kwa mipasuko (iliyo lazima),

27. Na tukafanya sisi kuota nafaka humo

28. Na Zabibu na mboga

29. Na Zaituni na Mitende

30. Na mabustani yenye miti mingi

31. Na matunda na malisho

32. Kwa manufaa yenu na wanyama wenu.

33. Basi itakapo kuja sauti kali iumizayo masikio (Sauti ya baragumu la kiyama)

34.. Siku ambayo mtu atakimbia ndugu yake.

35. Na mama yake na baba yake

36. Na mke wake na watoto wake

37. Kila mtu katika wao, siku hiyo atakuwa na jambo la kumshughulisha.

38. (Kutakuwepo) nyuso zing’aazo siku hiyo,

39. Zitacheka na kufurahika

40. Na (Zitakuwapo) nyuso katika siku hiyo zenye vumbi,

41. Kiza kitakuwa kimevikwa juu ya nyuso zao.

42. Hao ndio makafiri, waliokuwa wakitenda maovu.