Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Kaafirun
Utangulizi:
Rudi kwenye sura
* 1. Ewe Muhammad! Sema: Enyi makafiri, mlio shikilia juu ya ukafiri wenu.
Rudi kwenye sura
* 2. Mimi simuabudu mnaye muabudu nyinyi badala ya Mwenyezi Mungu.
Rudi kwenye sura
* 3. Wala nyinyi si wenye kumuabudu huyo ambaye mimi namuabudu, naye ni Mwenyezi Mungu wa pekee.
Rudi kwenye sura
* 4. Wala mimi si mwenye kuabudu mfano wa ibada yenu, kwani nyinyi ni washirikina.
Rudi kwenye sura
* 5. Wala nyinyi si wenye kuabudu mfano wa ibada yangu, kwani hii ni Tawhidi, ibada ya Mungu Mmoja.
Rudi kwenye sura
* 6. Nyinyi mna dini yenu mnayo itakidi, na mimi nina Dini yangu aliyo niteulia Mwenyezi Mungu niishike.
Rudi kwenye sura
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani