ONGEZA MAARIFA YAKO!!!

 

JE, UNAFAHAMU MADHEHEBU YA SHIA ISMAILIYA?

 

SHIA ISMAILIYYAH

 

 

 

Nalo ni kundi la Kiislamu ambalo linaamini  Uimamu wa Maimamu sita (6) watoharifu (a.s)  (yaani kuanzia Imam Ali (a.s) hadi Imam Jaafar Swadiq (a.s), kisha wanaacha Uimamu na Imam Musa Al-Kadhim (a.s)  na badala yake wanaamini Uimamu wa ndugu yake (Al-Kadhim) aitwaye Ismail bin Jaafar Al-Swadiq (a.s).

 

ISMAIL:

 

Na wameitwa “Maismailiyyah”  kwa kujinasibisha na “Ismail” Bin Jaafar
As-Swadiq (a.s), naye alikuwa  ni  mtoto wa kwanza wa Imam Jaafar, Imam alikuwa akimpenda sana, mpaka watu wakadhani kuwa yeye ndiye atakuwa Imam baada ya baba yake, lakini alikufa na kuzikwa Baqii, Madinah.  Na baba yake ( yaani Imam Jaafar (a.s) alimuhuzunikia sana na akalitangulia jeneza lake, akiwa miguu  peku na bila kuvaa joho, na akawa akiamrisha walitue jeneza lake chini kabla ya kumzika, na alikuwa akifunua uso wake na kumuangalia, ili  kuwasisitizia watu kufa kwake, ili isije dhaniwa kuwa huyu ndiye Khalifa.  Lakini pamoja na mambo yote  hayo, bado  Maismailiyyah waliendelea kuamini kuwa yeye ndiye Imam.

 

Nao wametofautiana kuhusu kifo cha Ismail. Katika uhai wa baba yake;  basi wakawa katika  makundi tofauti yafuatayo:

 

(A)        Kundi linalosema kuwa Ismail hakufa, bali baba yake alidhihirisha kwamba amekufa kwa kuogopa na kujiepusha na wale watawala waovu; na wakadai kwamba hatokufa mpaka  aitawale dunia na kuijaza uadilifu, kwa sababu yeye ndiye Al-Qaim (Al-Mahdi).

(B)         Na kundi lingine lililokiri kufa kwa Ismail kabla ya baba yake, lakini linasema kuwa Ismaili ndiye ambaye aliyeelezea kuhusu Uimamu  wa mwanae” MUHAMMAD.”

(C)         Na kundi la tatu limekubali pia kuwa alikufa kabla ya baba yake, na wakadai kuwa Imam Jaafar Swadiq alikuwa amekwisha elezea Uimamu wake (Ismail), hapo ikimaanisha kwamba Uimamu utahamia kwa kizazi chake (Ismaili hata kama yeye mwenye hatotawala kama Imam).

 

Na hivi ndivyo walivyoelekeza Uimamu kwa mtoto wake aitwaye “ Muhammad  naye ndiye Imam wa kwanza aliefichwa kwani  Imam kwao akiwa hana nguvu na uwezo juu maadui  zake basi kufichika ( hujificha) asidhihirike mbele ya watu, lakini huwepo walinganiaji  ambao huendelea kumtangaza kwa watu, ili kutimiza hoja kwa viumbe;  na akiwa na nguvu basi hujidhihirisha na kudhihirisha ujumbe wake.

 

 

Na Uimamu wa MUHAMMAD BIN ISMAIL ulihamia kwa wanae miongoni mwa maimamu waliojificha, mpaka ukafika kwa “UBAIDULLAH” aliyekuwa akifahamika kama “AL-MAHDI” naye ndiye Khalifa wa kwanza wa utawala wa FATWIMIYYAH” (296-322H) na ni wa kwanza aliyedhihirisha ujumbe wake, kisha wakafuatia watoto wake mmoja baada ya mwengine hadi ukafikia utawala kwa mjukuu wake “AL-MUSTANSIRU BILLAH  baba yake TAMIM, ambaye alikuwa ni miongoni mwa Makhalifa wa dola ya Fatwimiyyah MISRI.

 

Na alipokufa (487A.H) waligawika Maismailiyyah katika makundi mawili yafuatayo:-

 

1.                  Ismailiyyah “Nazariyyah”; ambao walidai kuwa Uimamu ulihamia kwa mwanae mustanswiru billah aitwaye “Nazaar” lakini aliuwawa na madaraka yakashikwa na watu tofauti baada yake, mpaka ulipokwisha utawala wa dola ya Maismailiyyah Nazaariyyah.  Na maismailiyyah wa aina hii ndio wafuasi wa “AGHA KHAN.

2.                  Na kundi la pili ni Ismailiyyah “Mustaaliyyah”, na hawa walidai kuwa Uimamu  ulikuwa ni “Asi-l-Qasim Ahmad”aliyejulikana kama “Al-MUSTAALIY BILLAH” japokuwa huyu hakuwa ni mtoto wa kwanza wa Al-Mustanswir billah, kisha ukahamia uimamu kwa mwanae “AL-AAMIR” bin al mustaaliy billah, kwa mwanae AT-TWIFLU-T-TWAYYIB  ambaye alijificha, ukawa umerudi mfumo wa kujificha tena, na wafuasi wake wakawa walingania ujumbe wake nchini YEMEN.

Kisha  hawa nao wakagawanyika; kundi likimsaidia AT-TWAYYIB na kundi lingine likimsapoti mwengine, na wakati huo dola la Fatwimiyyah lilikielekea ukingoni  mwake hadi lilipo kwisha katika mwaka wa 567 A.H kwa kushindwa na SALAHUDDIN AL-AYYUBI na wafuasi wake.

 

Basi akabaki At-twayyib akiwachagua walinganiaji wake  katika Yemen peke yake , kisha ukahamia ulinganio huo INDIA na wakafahamika wafuasi wa Ismailiyyah kama   “MABOHORA”

 

Na idadi  ya mabohora inakaribia MILIONI, wametawanyka katika miji mingi, wana shule Misikiti mingi na Taasisi na nyumba za  Wageni sehemu za Makkah, Madinah, Karbala, Najaf, Baghdad, Basrah, Eden, Afrika na kwengineko.

 

TAFAUTI BAINA YA ISMAILIYYAH NA ITHNA ASHARIYYAH

 

Madhehebu hizi mbili zinatafautiana katika baadhi ya mambo. Yaliyo muhimu ni haya yafuatayo.

 

1.                  Katika idadi ya Maimamu (a.s) na Maimamu wenyewe baada ya Imam Swadiq (a.s) kama tulivyoona hilo.

2.                  Masmailiyyah wameruka mipaka katika kutoa taawil ya aya  za Qur’an, Sunnah za Mtume s.a.w. kwa yale yanayoofikiana na misingi yao, ambayo hayana tamko, wala ushahidi wa kiakili wala pokeo, wala Ijmai. Ambapo Maithna ashariyyah huyaacha yale mambo ambayo maana zake haziko  wazi  limutashabihati), bila kuzitolea Ta’awil k.v zile herufi zinazoanza baadhi ya Sura (mf Alif Lam Mim).  Kama ambavyo hawatoi taawil ya aya wala hadithi isipokuwa kwa masharti  maalum.

3.                  Maismailiyyah wanatumia Usiri na kujificha, mpaka Imani yao inakua ni ngumu kufahamika kwa watafiti.  Ama maithnaashariyyah mambo yao yako wazi, hakuna uficho, wala vikwazo.

4.                  Maismailiyyah wameruka mipaka katika Usiri wao, na kutumia taqiyyah, bila kuwa na kisingizio cha Kiakili au kisheria,  kiasi ambacho huwa ni mashia pindi wawapo na mashia, masunni pindi wanapokuwa na masunni, wakristo wawapo na wakristo.  Ambapo ma ithnashariyyah  hawatumii ‘Taqiyyah” ila katika maeneo maalum, k.v. kuhofia nafsi isiangamie, au kuepusha tukio baya, na kuhofia madhara kwenye  mali.

5.                  Maismailiyyah hueneza imani zao na misingi ya madhehebu yao kwa mtindo wa hatua mbali mbali na madaraja. Na walinganiaji wao wanatofautiana madaraja yao katika kuelezea   aqida yao, kuanzia mambo madogo madogo hadi misingi mikubwa ya falsafa ambayo haifahamiki ila na baadhi ya watu wachache.

6.                   

Ama maithnaashariyyah hawana madaraja wala matabaka.

 

WAL-HAMDU LILLAHI RABBIL –ALAMIN

 

Rejea Kitabu, “ Adh’waun ‘alal firaqi wal-madhahibil islamiyyah” uk. 88-91

 

Kilichoandikwa na: “ abu Mus’ab al-Basriy”

 

Chapa ya kwanza, ya Qum Iran,  1415 A.H

 

Makala hii imetafsiriwa na Mtumishi wenu Jamali A. Kasole.

 

The .HTML version of this book is taken from
www.al-islam.org and ebooked by www.ShiaLibrary.com and www.islamkutuphanesi.com . May Allah be pleased with all.