MWENGE WA HAKI

MAJADILIANO KATI YA MA'MUNI NA WANACHUONI KUHUSU SIFA ZA ALl BIN ABI TALIB [a]

 

DIBAJI YA TOLEO LA KWANZA

 

Kitabu hiki ni tafsiri ya mazungumzo kati ya Khalifa mashuhuri wa Kiislamu aitwaye Ma'mun Ar-Rashid na wanachuoni arobaini wa Kiislamu wenye elimu ya juu kabisa zamahizo. Jambo waliojadiliana ni ubora wa Seyyidna Ali bin Abi Talib [a] juu ya Masahaba wengine wa Mtume Mtukufu [s].

 

Mazungumzo hayo yameandikwa na Bw. Abu Umar Ahmad bin Mohammad bin Abdi Rabbih Al-Undulusi (246 A.H. -327 A.H) katika kitabu chake mashuhuri Al Iqdul ­Fareed. Mwanachuoni huyu Bw. Ibnu Abdi Rabbih alikuwa mashuhuri sana, na alikuwa mwenye elimu ya Lugha na alikuwa mtunga mashairi pia. Tangu hapo zamani watu walitambua na kujua thamani na kutunuka kwa kitabu chake hicho, hata wakawa wanapenda mno hata walijifunga kwa kukitalii na kudondoa mule na wakazitumia katika kutungia vitabu vyao na kuzungumzia katika hutuba zao. Na kilipigwa chapa mara nyingi sana kuanzia mwaka 1292 A.H. hadi 1384 A.H. miaka sita mbele.

 

Nakala tunayo katika Maktaba yetu hapo Dar es Sa­laam, imepigwa chapa Cairo (Misri) katika mwaka 1384 A.H (1965 A.D) baada yakuangaliwa na kusahihishwa na wanachuoni watatu.

 

Mazungumzo hayo yameandikwa katika Juzuu ya tano, kuanzia uk. 92 hadi uk. 101, chini ya anwani:

 

(Majadiliano ya Ma'mun na Wanachuoni kuhusu ubora wa Ali R.A).

 

Mwanachuoni mashuhuri wa Ki-Sunni aitwaye Allama Shibli Numanii (India) ameandika mawazo yake juu ya majadiliano hayo hivi:

 

­"Mazungumzo mashuhuri ya Ma'muni ambayo yamethibitisha kwamba Bw. Ali bin Abi Talib alikuwa bora kuliko Masahaba wote na hakika majadiliano hayo yalikuwa yenye nguvu sana. Yahya bin Aktham na wanachuoni arobaini waliokuwa hodari wa zama hizo ndio waliokuwa wapinzani kwa dai hilo, na Ma'muni alikuwa peke yake. Wakati yalipoanza majadiliano hayo waliruhusiwa wazijibu hoja za Ma'muni bila ya hofu, bila ya kufikiria kwamba wanajadiliana na mfalme wao. Majadiliano hayo yalianza asubuhi hadi alasiri, pande zote mbili wakijadiliana vikali. Lakini juu ya hayo kwa kweli kila mara mshindi alikuwa Ma'muni. Majadiliano hayo yote yameandikwa katika kitabu Al-Iqdul Fareed, na kusema kweli ufunuo wa fikra, uhodari wa akili, na ujuzi wa elimu, ufasaha, na nguvu ya maelezo ya Ma’muni ni jambo la kustaajabisha sana.”

 

Tafsiri ya majadiliano haya ilipigwa chapa hapo zamani katika lugha ya Urdu mara nyingi na Idara ya Islah; katika mji wa Khujwa, Saran (India).

 

Hivi karibuni tafsiri yake kwa Kiingereza imepigwa chapa na M/s. Peer Mohamed Ibrahim Trust, Karachi (Pakistan).

 

Kwa ushauri wangu mshiriki wangu Agha Seyyid Muhammad Mahdi Shushtari, ameifasiri kwa lugha ya Kiswahili; katika mwaka 1967; na sasa kwa manufaa ya watu wa Afrika ya Mashariki tunaipiga chapa.

 

Nafikiri ni wajibu kutaja hapa kwamba siku hizi ndugu zetu wa Kisunni wanaamini kuwa ubora wa Khulafau Rashideen ni kwa mujibu wa Ukhalifa wao; kwa mfano Bw. Abu Bakr ni bora kuliko wote, baadaye Bw. Umar bin Khattabu, baadaye Bw. Uthmani, tena Bw. Ali bin Abi Talib. Lakini itikadi na imani ya namna hiyo haitegemeani na hadithi za Mtukufu Mtume [s]; na pia palikuwa na mzozo na hitilafu kubwa kati ya Masahaba na Tabein juu ya jambo hilo.

 

Imeandikwa katika Sharh-e-Maqasid cha Bw. Saad-ud ­Deen Taftazani hivi:­

 

(Kumfadhilisha mmoja juu ya mwenziwe ni jambo la uchunguzi (mawazo ya mwanachuoni tu); halina uthibitisho usiopingika.

 

Na Sayyid Sharif Ali bin Mohammad Jurjani (916 A.H) ameandika katika kitabu chake Sharh-e-Mawaquif:

 

­(Jua kwamba jambo la ubora ni jambo ambalo hakuwezekani kupatikana yakinisho na uthabiti).

 

Na kwa sababu hiyo wanachuoni wa mbele wakihitilifiana kuhusu madhumuni hayo:­

 

(1) Kikundi kimoja waliitakidi kwamba Khulafau Rashideen ubora wao juu ya wenziwe hufuata kwa mujibu wa utaratibu wa ukhalifa wao, kama tulivyoeleza nyuma.

 

(2) Kikundi kingine waliitakidi kwamba Bw. Abu Bakr alikuwa bora, tena baadaye Bw. Umar. Baada ya hawa wawili hawakuweza kuamua kuwa Bw. Ali ni bora au Bw. Uthmani. Hii ni itikadi ya Imam Malik, Imam Abu Hanifa, Yahya bin Said Qattan na wengineo.

 

(3) Kikundi cha tatu wanaitakidi kwamba Bw. Ali alikuwa bora kuliko Bw Uthman. Katika kikundi hiki wamo kina Sufyan Thauri, Abu Bakr Khuzaima, Imam Abdalla Yafei, Imam Hakim na Abdullah bin Khattab.

 

(4) Kikundi cha kutosha waliitakidi kwamba Bw. Ali bin Abi Talib ni bora kuliko wote licha ya Bw. Abu Bakr. Ameandika Allama Ibn Abdil Barr katika kitabu chake "Istiaab".

 

“Vile vile wamehitilafiana wakubwa wa dini wa mbele kuhusu ubora wa Bw. Ali na Bw. Abu Bakr." Tena akaendelea kuandika hivi:

 

(Salman, Abu Dhar, Miqdad, Ammar Khabbab, Jabir Hudhaifa, Abu Saeed Al Khudri, Zaid bin Arqam (Masahaba) wote hao wamesema, “Wa mwanzo kabisa mwenye kuikubali dini ya Islamu ni Bw. Ali bin Talib" na Masahaba hao wanamfadhilisha Bw. Ali juu ya wote").

 

Nimetoa maelezo haya hasa kueleza kwamba imani ya kawaida ya ndugu zetu wa Kisunni siku hizi si itikadi ambayo imekubaliwa na wakubwa wa dini wote.

 

Imam Ghazali ameeleza hivi:­

 

(Hakika ya ubora ni uliyoko kwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala; na ambaye hawezi kuujua isipokuwa Mtukufu Mtume [s] peke yake).

 

Ni dhahiri kuwa njia ya pekee kujua ubora (kufadhilika zaidi) kwa Mwenyezi Mungu ni kwa njia ya hadithi za Mtukufu Mtume [s]; kuziangalia kwa uwangalifu zile Hadithi zenye nguvu, na zenye kukubaliwa na aghlabu ya Madhehebu ya Kiislamu.

 

Juu ya jambo hilo marehemu Bw. Ubaidullah Amritsari ameandika katika kitabu chake kiitwacho Ar-Jahul Matalib (Uk. 122) ifuatayo.

 

"Kuhusu hadithi za sifa na utukufu wa Bw. Ali bin Abi Talib zilizopokelewa na wanachuoni wa Kisunni Allama Ibn Abdil Barr katika kitabu chake kiitwacho 'Istiaab Fi Maarifatil As-habi' anaandika hivi: “Wamesema kina Al-Imam Ahmad bin Hanbal, Ismail bin Ishaki Al-Kadhi, Ahmad bin Ali bin Shuaib An-Nasai, na Abu Ali An Nisapuri:

 

Hazikupokewa hadithi kwa sanadi njema kuhusu fadhila za sahaba yeyote kwa wingi, kama zilivyopokewa kuhusu fadhila ya Bw. Ali bin Abi Talib (R.A).

 

"Licha ya hayo, tukiangalia zile sifa zenye kuhusika na yeye tu kwa wingi wa thawabu alizonazo, hapo utamuona bila shaka kwamba yeye (Ali) ni bora kuliko wote baada ya Mtume [s]".

 

Mtungaji huyo (yeye binafsi alikuwa Sunni) ameeleza kwa urefu habari hiyo katika kitabu chake hicho tulichokitaja, katika mlango wa tatu (kutoka Uk. 103 hadi Uk. 516).

 

Bilal Musim Mission ya Tanzania inawashukuru Messrs. Peer Mohamed Ebrahim Trust ilioko Karachi (Pakistan) kwa kukipiga chapa kitabu hiki kwa ujira mdogo, hata tukaweza kukiuza kwa bei ya chini kama hiyo.

 

            P. 0. Box 20033            Seyyid Saeed Akhtar Rizvi

            Dar-es-Salaam  Chief Missionary

            Tanzania           Bilal Muslim Mission of

            4 Julal, 1971      Tanzania

 

DIBAJI YA TOLEO LA PILl

 

Kwa vile toleo la kwanza lilipendwa mno na wasomaji, sasa tunachapisha toleo la pili.

 

Tunawashukuru Waislamu wenzetu kwa kuisaidia Jumuiya hii kwa msaada unaotuwezesha kukiuza kitabu hiki kwa bei rahisi. Mwenyezi Mungu awape jaza ya kheri katika dunia na Akhera. Amin.

 

Dar es Salaam  Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

26 Januari, 1978.           Chief Missionary

 

MAELEZO YA MAJADILIANO KATI YA MA'MUNI NA WANACHUONI KUHUSU SIFA ZA ALl BIN ABI TALIB

 

Is-haq bin Ibrahim bin Ismail bin Hamad bin Zayd amesimulia kwamba siku moja Yahya bin Aktham Qadhil ­Qudhat (Kadhi mkubwa) alinitumizia mimi na baadhi ya sahibu zangu katika wanachuoni, kusema, "Kuwa Ameerul Mumineen ameniamrisha kesho alfajiri niwachukue watu arobaini, wote wawe Faqeeh wenye elimu ya kutosha, wanachuoni wa Fiqhi wawe na uwezo wa kufahamu wanachoambiwa na kujibu vizuri", basi wataje hao ambao unadhani kama watafaa kwa yale anayoyataka Ameerul Mumineen." Tukamtajia idadi maalum na yeye pia akawataja idadi maalum, hata wakatimia arobaini (40) kiasi alichotaka, na wakaandikwa majina yao, na akaamrisha kuamka mapema alfajiri, na akawatumizia wasiohudhuria kuwaamrisha wahudhuriye kwake. Sote tulioalikwa tukafika kwake kabla ya mapambazuko ya alfajiri, tukamkuta amevaa nguo zake amekaa tayari anatungoja; akampanda mnyama wake nasi pia tukapanda tukaenda hata tukafika mlangoni mwa jumba la mfalme; mara tukamkuta mtumishi amesimama. Alipotuona tu akasema "Ewe baba wa Muhammad; Ameerul Mumineen anakungoja", tukapelekwa ndani; tukaambiwa tusali (sala ya asubuhi) tukasali, hata bado hatujamaliza akaja mjumbe akasema, "Ingieni ndani, tukaingia, mara tukamkuta Ameerul Mumineen amekaa kwenye firashi (tandiko) lake, na amevaa nguo za kifalme (amevaa nguo nyeusi, amejitanda na shuka ya kijani, na amevaa kilemba). Sote tukasimama mbele yake tukamwamkia; na yeye akaitikia Salamu, na akatuamrisha kukaa.

 

Julipokwisha sote kukaa kwa uzuri, yeye (Ma'mun) akateremka kwenye tandiko lake, akavua kilemba na shuka aliojitandia, na akavaa kofia ya kidasturi. Baadaye akaja upande wetu akasema, "Nimefanya vile (kuvua yale mavazi) ili ninyi pia mfanye vivyo hivyo na mkae kienyeji." Lakini viatu hatukuvua, tena yeye (Ma'mun) akanyosha miguu yake, na baadaye akatuambia tuvuwe kofia na viatu na shuka ya kujitandia. Sisi tukasita kufanya hivyo. Basi Yahya akatuambia tufuate tulivyoamrishwa na Ameerul Mumineen. Tukaona ajabu basi tukaenda tukavua viatu, shuka na kofia na tukarejea mahali petu.

 

Tulipokwisha kaa sawa hapo, Mfalme Ma'mun akatuambia kwamba ametuita kwa ajili ya majadiliano, kwa hivyo mwenye kushikwa na choo kidogo au kikubwa na aende, kwani akiwa hakwenda haja atakuwa hana raha kukaa, kusema na kufahamu. Basi mwenye kushikwa na haja, basi kile pale choo (akaonyesha kwa mkono). Tukamshukuru.

 

Baadaye akatoa swali kuhusu fiqha (kanuni za Kiislamu) na akasema, "Ewe Abaa Muhammad! jibu wewe, na baadaye wajibu wengine (watoe ufafanuzi wao). Yahya akajibu na wengine mmoja baada ya mmoja tukajibu na kutoa fafanuzi, hali yeye (Ma'mun) kimya anasikiliza macho chini; hata yalipokwisha maneno, akaelekea kwa Yahya akasema, "Ewe Abaa Muhammad, jibu lako lilikuwa sahihi, lakini hukutumia ukweli katika hoja zako." Baadaye alikuwa akiwajibu kila mmoja na kukataa hoja zao na wengine akazikubali hoja zao hadi wote tukesha. Baadaye akasema, "Mimi sikukwiteni mje hapa kwa ajiIi ya jambo hili tulilozungumza, lakini nalipenda kufanya hivyo ili mchangamuke na muwe huru bila ya wasiwasi katika mazungumzo; hasa lengo langu kukwiteni ninyi hapa tujadiliane kwa yale ninayoitakidi na ninayoamini.

 

Tukasema basi na afanye Ameerul Mumineen, Mwenyezi Mungu amuafikishe.”

 

Ma’mun: Imani yangu ni kwamba baada ya Mtume Hazrat Ali bin Abi Talib ni bora kuliko watu wote, na yeye ndiye mwenye kustahili, na Ukhalifa ni haki yake, mnasemaje?

 

Allama: Sioni uthabiti wowote juu ya haya uliyoyasema. Kwa sababu gani H. Ali akawa bora na mwenye kustahili Ukhalifa kuliko wote baada ya Mtume [s]?

 

Ma’mun: Hebu kwanza niambie kwa kitu gani mtu akawa bora kuliko mwenzake, na kwa sababu gani husemwa fulani ni bora kuliko fulani?

 

Allama: Kwa vitendo vyake vizuri.

 

Ma’mun: Hakika kweli, sasa niambie kama ikiwa mtu mmoja katika zama za Mtume [s] kwa vitendo vyake akawa bora kuliko wote, lakini baada ya Mtume [s] watu wengine wakatokea wenye kutenda vitendo vizuri zaidi kuliko vitendo vyake, je, hawa watu watakuwa sawa na yeye?

 

Allama: (Akababaika kulijibu swali hili na akaanza kufikiri; hapo Ma'mun akamwambia).

 

Ma'mun: Nina hakika kwamba hutaweza kusema ndio, kwani mimi ninaweza kukuonyesha zama hizi hizi, wapo watu ambao kuliko hao wanapigana jihadi, wanahiji (Hija), wanafunga saumu, wanasali na wanatenda mambo mengi mengine ya kheri. Basi kwa hivyo watu wa zama zetu hizi pia watakuwa bora kuliko masahaba.

 

Allama: Bila shaka, aliyekuwa bora katika zama za Mtume [s], mtu mwingine yeyote hataweza kuupata au kuufikia ubora huo wakati mwingine wowote hata kama amefanyaje.

 

Ma'mun: Vizuri kabisa, sasa hebu watazame masahaba watukufu wa Mtume, Tabieen, Muhad-ditheen (wapokeao Hadithi) na wale wanavyuoni ambao ndio mnawakubali kuwa ni viongozi wenu wa dini; basi angalia zile daraja za juu za Hadithi walizozipokea katika sifa ya H.Ali wanahadithia. Baadaye hadithi hizi na hadithi zile za wema wa H. Abu Bakr mlizozipokea ninyi mzilinganishe; ikiwa hadithi zote hizo ni sawa na H. Ali, basi bila shaka ninyi mnaweza kudai kwamba H. Abu Bakr alikuwa bora kuliko H.Ali. Wallahi si hivyo tu, nasema hata mkizikusanya hadithi za wema wa H. Abu Bakr na H. Umar wote wawili pia; na mkazilinganisha na za H. Ali tu, na zikiwa sawa na za H. Ali peke yake, hapo kwa furaha H. Abu Bakr na H. Umar mwakubali kuwa ni bora kuliko H. Ali. La, naapa yamini! hata mkizikusanya hadithi za wema wa H. Abu Bakr na H. Umar na H. Uthman na mkazilinganisha hadithi za watatu hao na kwa jumla zikawa sawa na za H. Ali peke yake, basi ninyi pasipo taabu mabwana watatu hao muwaridhie kuwa bora. Sivyo wallahi! hata "Ashara Mubash-shara (wale masahaba wapenzi kumi ambao Mtume ameshuhudia kwamba ni watu wa peponi) mkiwachukua wote hawa mkizikusanya sifa zao kwa umoja na mkilinganisha hizo sifa zao na sifa za H. Ali peke yake hapo ninyi mnayo haki ya kusema kuwa ni bora kuliko H. Ali. Lakini haiyumkiniki kabisa, kwa sababu sifa za H Ali zimezidi sifa za H. Abu Bakr; Umar, Uthman, sio hivyo tu bali zimezidi za hao Ashara- Mubashara pia. Vizuri, Ee Is-haq hebu sasa eleza; tangu Mtume [s] alipodhihirisha utume wake wakati ule amali bora kuliko yote ilikuwa nini?

 

AlIama: Kuamini kwa moyo safi na ukamilifu.

 

Ma'mun: Kamini dini ya lslamu kwa kutangulia mbele ya watu wote si amali bora kabisa?

 

Allama: Kwa nini isiwe hivyo? Bila shaka ni bora.

 

Ma’mun: Isome Aya hii katika Qur’ani (56:10&11) “Was-saabiqun as-Saabiqun Ulaikal – muqar- raabuuun" (Na waliyotangulia kabisa katika heri hao ndio walioko mbele. Hao ndio vipenzi zaidi kuliko wote (Kwa Mwenyezi Mungu ). Hapa Mwenyezi Mungu amewakusudia wale ambao katika kuamini Uislamu walikuwa mbele kwa haraka. Je! mnamjua mtu, ambaye aliamini mbele kuliko H. Ali?

 

Allama: Bwana, H, Ali ameamini utotoni wakati ambapo haikumlazimu sheria juu yake, lakini H. Abu Bakr alikuwa mzee na akaukubali Uislamu ambapo kila kitu cha sheria kilikuwa wajib juu yake.

 

Ma'mun: Nataka kwanza uniambie ni nani wa kwanza wa mbele kuukubali Uislamu, baadaye tutajadiliana ju uzee au utoto.

 

Allama: Bila shaka mbele kuliko H. Abu Bakr ameamini H. Ali lakini alikuwamtoto.[1]

 

Ma'mun: Kweli H. Ali utotoni ameamini; sasa tufikiwa kuwa yapo mambo mawili, la kwanza ni kuwa H. Ali ameamini kwa kuwa Mtume amemwambia aamini; Ia kwamba Mwenyezi Mungu amemwongoza kwa "ILHAM” Ali auamini Uislamu; sasa niambie ni njia gani ni mnaikubali?

 

Allama: (Anahadithia kama swali hili la Ma'n lilinibabaisha mno, na nikafikiri sana mwishowe sikuweza kumjibu, hapo Khalifa mwenyewe akasema.)

 

Ma'mun: Is-haq! ninyi  hamwezi hamtakubali kusema kwamba H. Ali aliletewa "Ilham" (ameongozwa na Mola) kwa sababu mkikubali hivyo itakuwa ninyi daraja ya H.Ali mmeitukuza kuliko ya Mtume, kwani Mtume kwa kuletewa “Ilham" (Uongozi) na Mwenyezi Mungu hakuujua Uislamu, bali Mwenyezi Mungu alimpeleka Jibrili kwa Mtume.

 

Allama: Bila shaka H. Ali hakushushiwa Ilham, bali Mtume binafsi alimwita na akamtaka auamini Uislamu.

 

Ma’ mun: Kadhia hii itakuwa hali mojawapo ya mbiIi: Mtume kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu amemwambia H. Ali kuukubali Uislamu (Kuamini), au Mtume kwa matamanio yake mwenyewe tu amemtaka H. Ali aamini.

 

Allama anasema, swali hili Ia Khalifa Mamun vile vile Iilimfadhaisha na akafikiri amjibu nini. Hakuweza kumjibu basi hapo Khalifa mwenyewe akasema.

 

Ma’mun: Ee, Is-haq, ninyi hamwezi kumtuhumu na kumsingizia Mtume [s] kwamba yeye hufanya kitu cho chote kwa matamanio yake, kwani mkisema hivyo itakuwa ninyi mnamghadhibisha Mwenyezi Mungu ambaye alimwamrisha Mtume wake awaambie watu hivi, "Wamaa Yantiqu Anil-hawaa, In huwa illaa Wahyun Yuuhaa” (53: 3&4) (Hatamki neno lolote kwa matamanio yake; ila kama anavyoamrishwa na Mwenyezi Mungu).

 

Allama: Bila shaka Mtume hakufanya hivyo kwa matamanio yake binafsi bali kwa amri ya Mwenyezi Mungu alimwambia H. Ali aamini.

 

Ma'mun: Ni ajabu mno! Hii ndio shani ya Mwenyezi Mungu! kuwaambia Mitume wake kumtaka mtu ambaye si halali (si wajibu juu yake) kumwambia kufanya jambo?

 

AIIama: Ma-adhallah! Toba! sivyo hivyo kabisa.

 

Ma’mun: Wewe ulivyosema kwamba H. Ali ameamini utotoni, ambapo wakati ule haikumjuzia kuamrisha cho chote, basi kwa kusema kwenu hivi ni maana yake kwamba Mtume amewaita watoto kuamini jambo lililokuwa si uwezo wao. Na ikiwa wale watoto kwa kutakwa na Mtume wangeamini, je,nini hukumu ya mtoto mmojawapo baadaye akikufuru utotoni, hatapewa adhabu ya kukufuru kwake? Je, isingemjuzia Mtume kuwaamrisha jambo lolote? Mwaridhia kumsingizia Mtume kwamba amefanya mambo kama haya?

 

Allama: Toba! sivyo kabisa.

 

Ma’mun: Nafahamu kwamba madhumuni ya maneno yako ni kuwa, hiyo ilikuwa sharafa mahsusi ya H. Ali, hata iwe H. Ali kwa cheo (Sharafa) hicho na fadhila hii (ambayo imezidi zote) awe bora kuliko wote. Ndio sababu watu wote wazijue sifa na vyeo vyake vyote. Kinyume chake ikiwa Mwnyezi Mungu alimwamuru Mtume kuwataka kwa jumla kila mtoto aamini, basi Mtume kama alivyomtaka H. Ali waamini, angewataka watoto vile vile waamini.

 

Allama: Bila shaka bwana! uliyoyasema yote ni kweli.

 

Ma'mun: Je, Mtume alipata kuwaambia watoto wa jamaa zake mmojawapo kuamini? Makusudio ya kuuliza kwangu hivi, ni kwamba msije mkasema kuwa H. Ali alikuwa Bin Ammi wa Mtume ndipo akamtaka aamini kama alivyowataka watoto wa jamaa zake wengine waamini; basi ikiwa ndivyo hivyo, hapatakuwa na sifa wala kufadhilika kwa H. Ali mahsusi yake.

 

Allama: Sijui mimi kama Mtume alipata au hakupata kumwamkia mtoto yeyote.

 

Ma'mun: Ee, Is-haq: unadhani wewe kwamba kesho Kiyama, Mwenyezi Mungu atakuuliza kuhusu mambo usiyoyajua?

 

Allama: La, jambo nisilolijua kwa nini niulizwe?

 

Ma'mun: Kwa hiyo, jambo ambalo Mwenyezi Mungu ametuondolea takalifu yake, kwa nini unalitaja? (itapokuwa hujui) kwamba Mtume (s.a.w) alipata kumwambia mtoto mmoja yeyote katika ukoo (jamaa) wake kukubali Uislamu, basi kuna dharura gani ya kudhania? Sema kwa mujibu wa elimu yako, kwamba Mtume hakumwambia mtoto mwingine yeyote. Hiki ni cheo kilicho mahsusi cha H. Ali. Niambie sasa, baada ya mtu kuamini jambo (amali) gani bora ili kuitenda?

 

Allama: Kufanya jihadi (kupigana) katika njia ya Mwenyezi Mungu.

 

Ma’mun: Hakika, ni kweli, jinsi H. Ali alivyopigana na kuweka ukumbusho wa uhodari na ushujaa wake, Je, yupo sahaba mwingine ambaye amefanya hivyo?

 

Allama: Vita gani na wakati gani?

 

Ma'mun: Chukuwa wakati wo wote, au vita vyo vyote utakavyopenda kutaja (Wakati wo wote au vita vyo vyote sahaba yeyote amepigana na kufanya kazi kama H. Ali?

 

Allama: Na tutazame vita vya Badr.

 

Ma'mun: Ndio hasa tazama humu. Mimi vile vile ninavipenda vita hivi. Katika vita vya Badr pia (ambavyo vilikuwa katika mwaka wa pili, A.H., mwezi wa Ramadhani) mambo aliyoyafanya H. Ali na mambo waliyoyafanya masahaba wengine si tofauti sana? Hebu sema katika vita hivi watu wangapi wameuawa?

 

Allama: Zaidi ya sitini.

 

Ma'mun: Katika hao sitini H. Ali peke yake kawauwa wangapi?

 

Allama: Mimi sijui.

 

Ma'mun: Basi nisikie mimi, ishirini na tatu au chache yake ishirini na mbili, na arobaini waliobaki katika makafiri wameuwawa na Waislamu wengine.[2]

 

Allama: Bwana angalia vile vile haya, kuwa H. Abu Bakr Radhiyallah, alikuwa amekaa katika Jukwaa (AREESH) pamoja na Mtume.

 

Ma'mun: Hapana shaka alikuwa! Lakini kule akifanya nini? (kwani huku akimuua adui? Au akipigana na adui?).

 

Allama: Alikuwa amekaa na akifikiria njia ya kushinda vita.

 

Ma'mun: Inasikitisha mtu kama wewe kusema hivyo! Niambie yeye akifikiri hayo mbali na Mtume, au pamoja na Mtume? Ikiwa walikuwa pamoja basi yaonyesha kwamba Mtume alimfanya kushirikiana katika fikra zake? Katika mambo haya matatu ni jambo lipi unalikubali?

 

Allama: Ma'ahallah hakushiriki katika fikra, wala hakuwa mshiriki wake wala Mtume (s.a.w) hakuhitajia fikra zake.

 

Ma'mun: Ikiwa si hivyo basi hapo kwenye jukwaa amekaa akifanya nini? Ikiwa katika vita ya Badri hakutenda jambo lolote ila kukaa jukwani tu, basi itakuwa vipi yule ambaye katika kumhifadhi Mtume, kajitumbukiza vitani, na kupigana kwa upanga roho mikononi asiwe bora kuliko yule aliyekaa kwenye jukwaa raha mstarehe?

 

Allama: Bwana Jihadi (vita) jeshi zima Ia Kiislamu lilikuwa likipigana. H. Ali ajikuwa na halisi gani?

 

Ma'mun: Ndio hii ni kweli kwamba wote walikuwa wakipigana, lakini je yupi bora? Yule aliyekuwa anapigana na kumhifashi Mtume; au yule aliyekaa naye kwa utulivu na amani? Kwani wewe aya hii katika Qur'ani hukusoma ambayo inasema:

 

"La yas-tawil qaa-iduuna minal-mu’mineena ghayru ulidh-dha-rari wal-mujaa hiduu-na fi sabee-lil-Laahi biamwaa-lihim wa-an-fusi-him, Fadh-dha-lal-laa-huI mujaa-hideena biam-waa-lihim wa-an-fusi-him alal qaa­idee-na darjah; wa-kul lan wa-adal-laa- hul hus-naa; wa fadh-dha-lal laa-hul mujaa hidee-na al-qaa-ideena ajran adhee-ma (4:95)."

 

(Hawawi sawa Waislamu wanaokaa wasiende vitani, isipokuwa wenye udhuru (Hawawi sawa) na wale wapiganao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na kwa nafasi zao. Mwenyezi Mungu amewafadhilisha katika cheo wale wapiganao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na kwa nafsi zao kuliko wakaao (wasiende kupigana) Ingawa. Mwenyezi Mungu amewaahidi wote (Kupata) wema, lakini Mwenyezi Mungu amewafadhilisha kwa ujira mkuu wale wapiganao kuliko wakaao).[3]

 

Allama: Lakini H. Abu Baki na Umar pia walikuwa vitani (kwa sababu ya nia hiyo walikuja vitani).

 

Ma'mun: Basi kwa hivyo, H. Abu Bakr na Umar (ambayo walikuja) itakuwa wanao ufadhili juu ya wale wasioenda kabisa vitani, ndiyo au siyo?

 

Allama: Hapana budi ndiyo.

 

Ma'mun: Basi kwa sababu hiyo, bwana mkubwa yule ambaye roho yake aliweka hatarini, na akapigana na maadui, vile vile atakuwa bora kuliko H. Abu Bakr na Umar (kwa sababu wawili hawa ijapokuwa walifika vitani, lakini hawakufanya kitu, bali walikaa tu kwa utulivu).

 

Allama: Ndiyo maneno yako kweli.

 

Ma'mun: Sina shaka, Qur’ani unasoma?

 

Ailama: Ndiyo bwana ninasma.

 

Ma’mun: Hebu isome sura ya ‘Hal-Ataa’ ambayo ndani yake Mwenyezi Mungu anasema, "Hal Ata Alal Insani Hiynum Minad Dahri Lam Shay-am-Madh-kuura”. (hakika ulimfika mtu wakati Fulani wa dahari ambapo hakuwa kitu kinchotajwa).

 

Allama Is-haq anasema nikaanza kuisoma hiyo sura, lakini nalipofika kwenye kuanzia aya hii: Yashrabuna Min Ka’sin Kana Mizaa-Juha ka-fuura mpaka Wayut-Imuunat-ta-ama Ala Hub-bihi Misky-Naw-waya-tiyamaw-wa-asiyra. (…Watakunywa katika kikombe kilichochanganyika na kafuri… Na huwalisha chakula maskini na yatima na mfunguwa kwa mapenzi yake. Qur’ani 76:5,8) Ma’mun akauliza akasema:

 

­Ma'mun: Ngoja kidogo, hebu nifahamishe aya hizi,

zimeshushwa katika shani ya nani?

 

Allama: Katika ukubwa na cheo cha H. Ali.

 

Ma'mun: Kwa njia ipi maneno haya yamekufikia kwamba H. Ali alipokuwa akiwapa chakula maskini, yatima na mfungwa, na huku kwa ulimi wake akisema hivi: Innamaa Nut-Imukum Liwaj-Hillah (Tunakulisheni nyie kwa ajili ya kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukrani!). Ikiwa si hivyo, na bila shaka sivyo; basi inathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu akijua nia ya H. Ali, na baadhi yake Mwenyezi Mungu Mwenyewe ametambulisha na kudhihirisha kwa kusema vile, "sisi tunakulisheni kwa ajili ya kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu tu". Hebu sasa, niambie jinsi Mwenyezi Mungu kwa sifa hii ya H. Ali aliyomsifu. Unaweza kumtaja sahaba mmojawapo ambaye alikuwa amefanya jambo fulani, na Mwenyezi Mungu juu ya nia yake, badala yake akatia maneno yake na akaileta kwa namna ya aya?

 

Allama: H. Ali bila shaka hakuyasema kwa ulimi wake haya 'ln-namaa Nut-Imukum Liwaj-hil-laah', wala hakuna sahaba yeyote sifa kama hii kuteremshiwa katika Qur’ani.[4]

 

Ma'mun: Ndiyo unasema kweli, na sababu yake ni hii, kwamba Mwenyezi Mungu anajua tabia na nia ya vitendo vya H. Ali, kwamba H. Ali kila jambo alifanyalo huwa kwa ajili ya kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu tu, hana makusudio mengine. Ewe Is-haq, hebu sasa niambie wewe unashuhudia na kukiri au la, kwamba Ashra Mubash-shara ni watu wa peponi?

 

Allama: Bila shaka! Na mimi vile vile ninashuhudia pia.

 

Ma'mun: Je sasa, ikiwa mtu kasema hivi: "Naapa kwa Mwenyezi Mungu sijui hadithi hiyo ni kweli au uwongo, na pia sijui kwamba Mtume (s.a.w) amehadithia hiyo hadithi au Ia." Je, mwenye kusema hayo yote, utamfikiri kuwa ni kafiri?

 

Allama: Ma’adhallah kabisa siyo!

 

Ma'mun: Hebu sasa tutazame ikiwa mtu, yule yule akisema, "Mimi sina hakika kwamba sura ya ‘Hal Ata’ ni maneno ya Qur'ani (Mwenyezi Mungu) au siyo, basi huyo atakuwa kafiri au sivyo?

 

Basi nini tofauti na sababu ya maneno haya mawili? Tofauti hii ipo, kuwa fadhili ya H. Ali Qur'ani ni ushuhuda wake, ambao mwenye kukanusha huwa kafiri; na fadhili ya masahaba ni maneno ya hadithi ambayo huwa kila namna sahihi au si sahihi, na akiyakanusha imani imekwisha; Vema, je Ee ls-haq wewe unahadithia hadithi za Mtume?

 

Allama: Ndiyo bwana, ninafanya hadithi.

 

Ma'mun: Unaijua hadithi ya 'TAYR' (ndege)?

 

Allama: Ndiyo bwana.

 

Ma'mun: Hebu hadithia.

 

Allama ls-haq anaeleza, mimi nikaisoma hadithi ambao ni hii, Siku moja Mtume alipokaa kula nyama ya ndege ya kukaanga (aliyoletewa zawadi) akaomba, "Ee Mola Wangu, mlete kwangu mtu yule ambaye kwako wewe ni mpenzi (Mahbubi) na umpendaye zaidi kuliko watu wote, aje hapa kula nami. Mara tu baada ya kumalizika dua yake Mtume, H. Ali akapelekwa kwa Mtume, na akakaa kula naye. Hii inaonyesha na inathibitisha kwamba Ali anapendwa kuliko wote; na hadithi hii ndiyo inaitwa hadithi yaTAYR (ndege). Baadaye Ma'mun akasema.

 

Ma'mun: Ewe ls-haq, mpaka hivi sasa, nalikuwa nikikufikiri kwamba wewe si adui wa jambo Ia haki, lakini sasa imenidhihirikia kuwa wewe ni adui wa haki. Je, unayo yakini kwamba hadithi hii lazima kuwa ni kweli?

 

Allama: Bila shaka, ninayo yakini, kwani hadithi hii imepokewa na wanavyuoni wakubwa, ambao mtu yeyote hawezi kuwapinga.[5]

 

Ma'mun: Sasa hebu sema, unaweza kufikiri kamba mtu yeyote mwenye imani na yakini juu ya hadithi hii, anaweza kufikiria kwamba katika umati wa Mtume, yupo mtu bora kuliko H. Ali?

 

Kama bado anafikri kuwa yupo aliye bora kuliko H. Ali basi katika mambo matatu haya lazima jambo moja alikubali.

 

(1) Aseme kwamba Mwenyezi Mungu hakukubali ombi (Dua) la Mtume.

 

(2) Au akubali baada ya kuwepo mtu bora kuliko wote, Mwenyezi Mungu alimpenda asiye bora (H. Ali).

 

(3) Au aitakidi kwamba Mwenyezi Mungu hapambanui aliye bora na asiye bora (kwa sababu ya lile ombi (Dua) la Mtume, Mwenyezi Mungu amempeleka H. Ali tu).

 

Kafika mambo matatu haya jambo lipi unalolikubali?

 

Allama Is-haq anaeleza kwamba kusikia maneno haya ya nguvu ya Ma'mun akili "ikaniruka na nikababaika nikawa sina la kumjibu." Hapo Ma'mun akasema:

 

Ma'mun: Ewe Is-haq, huwezi kulichagua na kulikubali hata moja katika mambo matatu haya kwani (utakufuru na imani itakutoka na) nitakufanya ukiri, pasipo haya labda utafute njia ya nne.

 

Allama: Bwana akilini mwangu halifafanuki jambo jingine lolote. Lakini naweza kusema hivi tu, kwa vyo vyote H. Abu Bakr pia hakukosa sifa yo yote?

 

Ma'mun: Mimi siwezi kukanusha haya, kwa sababu ikiwa hana sifa yoyote, basi itakuwa ni upuzi kusema H. Ali ni bora kuliko H. Abu Bakr. (kwani mtu bora anaambiwa yule ambaye anazo sifa zaidi kuliko wengine maana yake asiye bora anazo sifa kidogo na aliye bora anazo sifa zaidi kuliko wote); lakini wakati huu umekumbuka yake?

 

Kisa cha “GHARI”: H. ABU BAKR
KUFUATANA NA MTUME

 

Allama: Kufuatana na H. Abu Bakr kwenye Pango (Ghari) na maelezo ya aya ya Ghari ambayo Mwenyezi Mungu amesema katika Qur'ani; "THANI-YATH-NAYNI," (Mtume) alipokuwa wa pili wa wawili, walipokuwa wote wawili katika pango; (Mtume) anapomwambia sahibu yake; Usihuzunike, kwa yakini Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi." (Qur'an 9:40)

 

Hebu angalia katika aya hii Mwenyezi Mungu, amemtaja H. Abu Bakr kuwa 'Sahib' (mwenzi) wa Mtume kwani hiyo fadhili ya H. Abu Bakr ni ndogo au kama kawaida tu?

 

Ma'mun: Ewe Is-haq, mimi sitakusumbua wala sitakupeleka njia ya shida (bali kwa kila namna ya msaada nitakupa, ili utumie uwezo na maarifa yako yote katika majadiliano haya; na nguvu zako zote uzitumie mpaka uridhike). Bila shaka katika aya hii Mwenyezi Mungu alimtaja H. Abu Bakr kuwa ni Mwenzi wa Mtume. Lakini (Humu fadhili gani inathibitisha, au sifa gani imo humo?). Kwa kuwa ninaona Mwenyezi Mungu katika Qur'ani, amemwita Kafiri pia Mwenzi ambaye alifuatana na mtu mmoja mwenye kupendwa na Mwenyezi Mungu, basi katika Qur'ani ameeleza hivi, "Faqaala lahu Sahibuhu, Wahuwa Yuhaawiruhu.' Basi akamwambia mwenzake na hali ya kuwa akibishana naye, "Je, unakufuru (na unakanusha neema za) yule aliyekuumba kwa udongo, tena kwa tone la manii, kisha akakufanya mtu kamili? (Qur'ani, 18:37)

 

Allama: Lakini bwana, yule Mwenzi aliyetajwa katika aya hii alikuwa kafiri na H. Abu Bakr alikuwa Mwislamu.

 

Ma'mun: Mimi ndiyo nasema hayo hayo, kwamba ikiwa inajuzu kwa Mwenyezi Mungu, Kafiri mmoja aliyefuatana na mpenzi wake mmoja kumwita sahib (Mwenzi); basi vile vile inajuzu Mwislamu aliyefuatana na Mtume wake amwite Mwenzi (Sahib), lakini kwa kumwita hivyo (Mwenzi) yule mtu hawezi kuwa bora kuliko Waislamu wote.

 

Allama: Bwana, aya hii ya Ghari (pango) ni tukufu sana kwa sababu Mwenyezi Mungu anasema, "Alikuwa na Mwenziwe wa pili yake peke yao." Wakati ule walipokuwa wote wawili katika pango; (Mtume) anapomwambia Sahib yake, "Usihuzunike, kwa yakini Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi.

 

Ma'mun: Ewe, Is-haq, naona nisipokusaidia kukufikisha kwenye ufafanuzi hutakubali jambo lolote. Hebu sasa nieleze huzuni ya H. Abu Bakr ilikuwa katika hali ya ghadhabu au utulivu? (alipokuwa na furaha akahuzunika au alipokuwa na ghadhabu?)

 

Allama: Huzuni hiyo alimhuzunikia Mtume, alimfikiria kwamba asije (Mtume) akapatwa na msiba (taabu) ye yote.

 

Ma'mun: Haya sio majibu ya swali langu. Eleza huzuni ya H. Abu Bakr ilikuwa ya nini? Kutaka ridhaa ya Mwenyezi Mungu au ilikuwa huzuni hii kinyume chake kumghadhibisha Mwenyezi Mungu?

 

Allama: Alihuzunika 'lillahi' kutaka ridhaa ya Mwenyezi Mungu (huzuni ya H. Abu Bakr pale ni kumfurahisha Mwenyezi Mungu).

 

Ma’mun: Kwa mujibu haya, inathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ametupelekea Mtume yule ambaye anawakataza viumbe kufanya jambo yenye kumridhisha na kumfurahisha Mwenyezi Mungu?

 

Allama: Ma’adhallahi! (vipi itakuwa hivi?)

 

Ma’mun: Kwani wewe sasa hivi hukusema kwamba kuhuzunika kwa H. Abu Bakr kulikuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

 

Allama: Bila shaka nilisema.

 

Ma'mun: Basi mbona Qur’an inseam kwamba Mtume amemwambia Sahib wake H. Abu Bakr, ‘LA TAHZAN’ (Usihuzunike); amemkataza asihuzunike. Lakini yeye huzuni yake ilikuwa ‘LIL-LAHI’ minajili ya Mwenyezi Mungu, hatimaye inaonyesha kwamba Mtume (s.a.w.) amemzuwia H. Abu Bakr kupata furaha na ridhaa ya Mwenyezi Mungu!

 

Allama: Ma’adhallah (La haula, makosa gani nimefanya!)

 

Ma’mun: Ewe, Is-haq, mimi ninajadiliana nawe kwa urahisi na utaratibu, ili labda uongoke na ufuate njia ya haki na uwache opotovu (batili) kwani nakuona mara kwa mara unasema AU-DHUL-BIL-LAHI. Hebu nifahamishe Mwenyezi Mungu katika Qur’ani amesema hivi: FA ANZALA-LAHU SAKI-NATA-HUU-ALAYHI. (Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake). Hapa amekusudiwa Mtume (s.a.w.) au H. Abu Bakr?

 

Allama: Hakukusudiwa H. Abu Bakr bali Mtume ndiye aliyekusudiwa.

 

Ma'mun: Vizuri kabisa. Na tutazame aya hii katika Qur’ani inasema hivi: WA YAWMA HUNAYNIN' mpaka mwisho wa aya hii. (Bila shaka Mwenyezi Mungu amekunusuruni katika mapigano mengi, na siku ya Hunaini (pia); ambayo wengi wenu ilikupandisheni kichwa lakini haukufaeni chochote, an ardhi ikiwa finyu juu yenu; ingawa ilikuwa yenye wasaa, kisha mkageuka mkarudi nyuma; (mkakimbia). Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu wake juu ya Mtume wake na juu ya Walioamini) (9:25&26). Hebu eleza katika aya hii Mumineen (walioamini) wamekusudiwa nani?

 

Allama: Bwana! hakika sijui.

 

Ma'mun: Katika vita vya Hunain Waislamu wote walikimbia na kumwacha Mtume peke yake, ispokuwa watu saba katika ukoo wa Bani Hashim ndio walikaa thabiti na imara. Miongoni mwa watu saba hawa mmoja alikuwa H. Ali ambaye kwa upanga wake akimhifadhi Mtume; na wa pili H. Abbas ambaye alikamata hatamu ya nyumbu wa Mtume, wengine watano waliobaki walimzunguka Mtume, ili makafiri wasimjie (Mtume). Ikaendelea hali hii mpaka Mwenyezi Mungu akampa uwezo na akashinda. Kwa hiyo katika aya hii neno la Mumineen wamekusudiwa hasa hawa wawili H. Ali, H. Abbas na wale Bani Hashim ambao wakati ule wa dhiki walikuwa na Mtume. Hebu niambie nani bora kati ya mabwana (H. Ali na H. Abbas, na wenziwao) wakati ule walikuwa na Mtume; na wale waliokimbia kujivusha nafsi zao ambao bila shaka Mwenyezi Mungu hakuwakuta hapo hata awateremshie juu yao utulivu?[6]

 

Allama: Bila shaka, ninayo yakini kwamba mabwana wale ni bora, ambao Mwenyezi Mungu amewateremshia utulivu juu yao.

 

KISA CHA KUJITOLEA H. Ali ROHO YAKE, USIKU WA KUHAMA MTUME MAKKA

 

Ma'mun:            Hebu kidogo nieleze kuwa yule mwenzi ambaye alikuwa na Mtume (s.a.w) katika pango, au bwana yule ambaye alijitolea roho yake na kumhifadhi Mutme, na akalala mahala pa Mtume hadi akaweza kuhama; bora yupi?

 

Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume (s.a.w) amtake H. Ali alale mahala pake kwa kujiweka hatarini roho yake iii amwokoe (Mtume). Basi Mtume alipomfikishia maneno ya Mola; Ali akali, Mtume akamwuliza, "unalia nini, unalia kuogopa mauti?" H. Ali akajibu, "Siyo bwana. Naapa kwa jina Ia Mwenyezi Mungu silii kwa haya, bali ninao wasiwasi kuhusu wewe, kwamba kwa kuhama utaingia taabuni. Je, nikilala mahala pako wewe roho yako itasalimika?" Mtume (s.a.w.) akasema, "Bila shaka itasalimika." Hapo H. Ali akafurahi na akasema, Bwana kwa hiyo basi nina hofu gani? Mimi mzima wako ni tayari, kwa utulivu mno, bila wasiwasi, na kwa furaha nitafidia roho yangu ili nikusalimishe." Baadaye akaenda kulala mahala pa Mtume (s.a.w) na akajifunika shuka Ia Mtume lenye rangi ya kijani kibichi, akalala kwa raha kabisa. Punde baadaye makafiri wa Kikureshi wakafika na wakaizunguka nyumba kwa kumfikira H. Ali kuwa ndiye Mtume aliyelala; hapakuwa na shaka kwa mtu hata mmoja katika wao. Kabla ya hapo Makureshi walikwisha kata shauri kwamba katika kila kabila mtu mmoja atampiga Mtume pigo moja kwa upanga, wote kwa mara moja. Madhumuni ya kufanya hivyo ni kuwa Bani Hashim wasiweze kuchukuwa kisasi kwa kabila fulani tu, ijapokuwa H. Ali alikuwa akisikia na akijua mashauri yao yote yakifanywa kuwa tayari kumwua, hakukunja uso hata kidogo, wala kuingiwa na wasiwasi, bali kwa utulivu kamili akalala kwa kujitolea. Kinyume cha hayo H. Abu Bakr (kwa neno dogo tu) kule pangoni akaingiwa na hofu na akalia na kubabaika. Huku H. Ali kwa utulivu kamili bila hofu wala wasiwasi akalala vivyo hivyo muda mrefu. Kwa (Toleo na mhanga) huo wa H. Ali Mwenyezi Mungu (alifurahiwa) akawapeleka malaika wake watukufu ambao mpaka asubuhi walimlinda. Asubuhi alipoondoka hapo alipolala pahala pa Mtume, makafiri wa kikureshi wakawa wanamtazama na wakasema, "Ala ulikuwa wewe umelala? Basi Mtume yako wapi?" Na Ali akawajibu "Ninajuwaje Mtume aliko?” Ndipo wale wakasema "Ewe Ali, inaonyesha tangu usiku, ulijifanya adui wa roho yako (kwa kulala juu ya mahala hapa) na ukamwokoa Mtume wenu. Kwa ufupi hivyo mpaka kufa kwake H. Ali katika kila jambo alithibitisha utukufu wake juu ya watu wote, na utukufu wake na fadhila yake unazidi. Hakuna utukufu kama H. Ali.[7]

 

MABISHANO JUU YA KISA CHA GHADEER

 

Ma'mun: Ewe, Is-Haq, sasa niambie hadithi ya Ghadeer, Je, mnasimulia?

 

Allama: Ndiyo bwana.

 

Ma'mun: Hebu eleza kidogo.

 

Allam'a Is-haq anasema, "Nikieleza kisa cha ghadeer mbele ya Ma'mun. Baadaye Ma'mun akasema:

 

Ma'mun: Ewe Is-haq! Hebu sema, waweza kuingia akilini mwako maneno haya, kwamba kwa jinsi ilivyombidi H. Abu Bakr kuiamini na kuifuata hadithi inayomhusu H. Ali itampasa H. Ali vile vile hadithi inayowahusu H. Abu Bakr na Umar kuifuata? (Yaani Mwenyezi Mungu alifanya farashi (lazima) juu ya H. Abu Bakr na Umar kwa kuwa wamekubali kwamba H. Ali ndiye bwana na mwongozi wao, lakini haikuwa lazima bali hata haikumjuzia H. Ali kuwakubali H. Abu Bakr na Umar kuwa mabwana wake).

 

Allama: Bwana!  Watu wanasema kwamba sababu ya kisa hiki ni Zayd bin Haritha, kwani kati yake na H. Ali ilikuwa baadhi ya kutopatana: ambao juu ya hayo akaacha usuhba (urafiki) na H. Ali. Kwa hiyo Mtume akasema, "Mwenye kuamini mimi ni bwana (rafiki) wake, basi Ali vile vile bwana (rafiki) wake. Ee, Mwenyezi Mungu, Mpende ampendaye Ali; na mfanye adui mwenye kumfanya Ali adui yake."

 

Ma'mun: Kwanza nieleze mtume amesema hadithi hii wakati gani? Hakusema wakati alipokuwa akirudi kwenye hija yake ya mwisho, (alipofika Ghadeer-e-khum) wakati ule ndiyo?

 

Allama: Ndiyo wakati ule ndiyo akasema.

 

Ma'mun: Ikiwa muda mrefu kabla ya kisa cha Ghadeer-e-Khum huyo Zayd bin Haritha ameshakuwa Shaheed (ameuawa) basi vipi nyie mnasingizia kuwa kisa cha Ghadeer ni sababu ya kutopatana na Zayd? (Kwa sababu Wahistoria wote kwa ujumla wanaafikiana kwamba katika vita vya MUTAH ambavyo vilikuwa katika mwaka wa nane (A.H.) ndiyo Zayd kawa Shaheed (ameuawa), ambacho ni kisa mashuhuri. Na kisa cha Ghadeer kimekuwa mwezi kumi na nane (Mfungo tatu) Zilhaj, mwaka wa kumi wa A.H. Hebu sasa niambia, ikiwa mtoto mmoja wako aliyefikia umri wamiaka kumi na tano (15) ukamwona anamwambia watu hivi, "kila aliyekuwa rafiki yangu, basi yule vile vile atakuwa rafiki wa binamu wangu, Enyi watu kumbukeni maneno haya vizuri na msije mkayasahau." Je, wewe hutaona vibaya, kwa vile mwanawo kuwaambia watu maneno ya upuuzi kama hayo, ambayo yanajulikana na kila mtu, na hapana aliyeyakataa?

 

Allama: Shahidi Mungu, nasmea hakuna budi nitaona vibaya.

 

Ma'mun: Basi, haya! Maneno ambayo hupendi haa mwanao ayaseme, basi vipi utampenda Mtume? (Yaania mtume (s.a.w) alikuwa anajua kwamba aliyekuwa rafiki yake, basi vile vile ni rafiki wa H. Ali, au tuseme anayependa Mtume, hakuna shaka anampenda H. Ali vile vile. Kwa hivyo, kitu gani kilimfanya mtume kufanya bidii na usimamizi wote ule na kuwapa habari masahaba na Waislamu? hapana budi itakulazimu kukiri na kusema kwamba shabaha na lengo Ia Mtume ni kuwafahamisha kwamba mwenye kumkubali yeye kuwa ni bwana na mwongozi wake, basi vile vile amemkubali H. Ali kuwa ni bwana na mwongozi wake)[8]

 

Nina majonzi kuona hali yenu hiyo. Msiwe watumwa wa wanavyuoni wenu, na hawo waongozi wenu wa dini msiwafikiri kuwa miungu wenu. Kwa hakika ninyi mnalelewa kwamba Mwenyezi Mungu katika Qur’ani amesema: "Ittakhadhuu - Ahbaa-rahum.' (wamefanya wanavyuoni wa na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu, (9:31). Ijapokuwa (Mayahudi na Manasara) hawakusali sala za waongozi wa dini yao, wala hawakufunga wala hawakuitikadi kwamba waongozi wa dini yao hakika ni miungu wao; lakini kila waliyoyasema hawo wanavyuoni wao, waliyakubali bila ya kutumia akili yao (na ndivyo Mwenyezi Mungu akasema hivyo).

 

Majadiliano juu ya hadithi ya manzilat (cheo).

 

Ma'mun: Ewe Is-haq, je, hadithi hii vile vile mnahadithia, kwamba Mtume (s.a.w.) alisema, " YA ALl ANTA MIN-NI BIMAN ZILATI HARUUNA MIN MUSA." (Yaani, Ee, Ali wewe kwangu, una cheo na darja kama alivyokuwa nayo Bw. Harun kwa H. Musa).

 

Allama: Bwana, mimi pia hadithi hiyo nimesikia, isitoshe haya nimewasikia wenye kuikubali na wenye kuipinga hiyo hadithi.

 

Ma'mun: Wewe, miongoni mwa hawo wanavyuoni kikundi kipi unakiamini na kukitegemea, katika wale wenye kuikubali hadithi hii au wale wenye kuipinga?

 

Allama: Nawasadiki na kuwaamini wale wanaoikubali hiyo.

 

Ma'mun: Inaaminika kwamba Mtume (s.a.w) amesema hadithi hiyo kwa mzaha na mchezo tu?  

 

Allama: Ma’adhallah! Sivyo hivyo.

 

Ma'mun: Hujui kuwa Bwana Harun alikuwa ndugu halisi wa Mtume Musa?

    

Allama: Najua bila shaka.

 

Ma'mun: Je, hii sivyo kuwa Bwana Harun alikuwa Mtume na H. Ali hakuwa Mtume?

 

Allama: Hapana shaka ndivyo.

 

Ma’mun: Basi sasa, tumekwisha yakinisha kwamba H. Ali hakuwa ndugu halisi wa Mtume.

 

Allama: Hapana shaka ndivyo.

 

Ma'mun: Basi sasa, tumekwisha yakinisha kwamba H. Ali hakuwa ndugu halisi wa Mtume, walahakuwa Mtume. Sifa zote hizo mbili hata moja hakuwa nayo. Sembuse Bwana Haruun alikuwa nayo sifa zote mbili. (Yakini katika sifa hizi mbili H. Ali hakumshabih Bwana Harun kabisa). Kwa hivyo usemi wa Mtume, "ANTA MIN-NI BIMAN-ZILAT HARUUNA MINI MUSA," (Ee Ali wewe kwangu una daraja na cheo ambacho Bwana Haruun alikuwa nacho kwa Mtume Musa), una maana gani? (Sasa H. Ali alikuwa na sifa na cheo kipi ambacho kamsabihi Bwana Haruun hata Mtume akasema hadithi hiyo?).

 

Allama: Hadithi hiyo si kitu, kwa sababu Mtume kayasema maneno haya katika kumfurahisha H. Ali tu, hakuwa na shabaha zingine, na kwa sababu ya kufanya vile ni kuwa Wanafiki (Munafiqeen) walivumisha kwamba Mtume kwa vile moyoni alikwa hakuridhika naye ndipo akamwacha huko Madina.

 

Ma'mun: Kwa hivyo imethibiti kwamba Mtume juu ya jambo la upuuzi (uvumi) kataka kumfurahisha H. Ali tu.

 

Allama anasema "Kwa suala gumu hilo nikafadhaika na nikafikiri niseme nini? Lakini haikunijia akilini majibu yeyote, basi hapo Ma'mun akasema:

 

Ma'mun: Ewe Is-haq, kwa namna Mtume katika hadithi hiyo amemshabihisha H. Ali na H. Haruun, namna hiyo hiyo maneno wazi wazi hapo katika Qur’ani.

 

Allama: (Kwa kuona ajabu sana) Bwana maneno gani?

 

Ma'mun: Kwa maneno ya Mtume Musa, Mwenyezi Mungu katika Qur’ani amesema, "Qala Musa li Akhi-hi Haruun ikhlufni fi Qawmi wa'aslih walaa tat-tabi Sabiylal ­muf-sideen. (Musa akamwambia ndugu yake, Harun: "Shika mahali pangu katika (kuwaendesha) watu wangu na usuluhishe wala usifuate njia ya Waharibifu 7:142).

 

Allama: Bwana! haya vile vile angalia kuwa mtume Musa alipokuwa anakwenda kuomba kwenye jabali ya TUUR ndipo akamfanya kiongozi nduguye H. Haruun juu ya umma wake, na wakati ule H. Musa alikuwa hai, vile vile Mtume wetu akamfanya H. Ali kuwa kiongozi wa umma, wakati ule tu alipokuwa akienda kwenye vita vya TABUUK, wakati wa uhai wake. (Vita vya Tabuuk vilikuwa akatika mwaka wa tisa A.H)

 

Ma'mun: Toba! Unasema nini? Sivyo hivyo kamwe, hebu sema wewe mwenyewe Mtume Musa alipomfanya H. Haruun khalifa kushika mahala pake, alipokuwa akienda kwenye Tuur; je alimchukua mtu yeyote katika wafuasi wake kwenda naye huko?

 

Allama: Hakuna.

 

Ma'mun: Kwa hiyo, je, haioneshi; kwamba Mtume Musa kamfanya H. Haruun kuwa ni Khalifa wa Umma wake wote?

 

Allama: Bila shaka, alikuwa khalifa juu ya umma wote.

 

Ma'mun: Lakini alipokwenda Mtume (s.a.w) kwenda kwenye vita vya Tabuuk; bila ya watoto, wanawake, na baadhi ya Waislamu dhaifu (wasio na afya) aliwawacha watu (wasio hao) wengine Madina? Basi vipi yaweza kusemekana kwamba tokeo hili ni kama la H. Musa? (Yaani ya Mtume Musa alikwenda kwenye jabali ya Tuur peke yaje lakini Mtume wetu (s.a.w) alipokwenda Tabuuk, alikwenda na masahaba na wasaidizi wake; H. Musa kauacha Umma wote nyuma, lakini Mtume wetu isipokuwa Waislamu dhaifu, wanawake na watoto, waliobaki aliwachukuwa wote; kwa hivyo kuna faraka ya ardhi na mbingu, basi utalishabihisha vipi tokeo la mtume na H. Ali na tokeo la nabii Musa na H. Haruun? Wazo moja linanijia akilini mwangu juu ya hadithi hii, na wazo hilo linatokana na Qur’ani, na ni uthibitisho wa nguvu juu ya jambo hili; nalo ni kuwa Mtume amemfanya H. Ali (Wakati wa uhai wake na baada ya kufa kwake) Khalifa halisi juu ya waislamu wote (yaani isiyo na kiasi wala mipaka). Mtu yeyote hawezi kuupinga uthibitisho huu wala kujibu dalili hii; wala hakuna mtu kabla ya mimi aliyeleta na kuonyesha dalili hiyo, bali na amini kwamba Mwenyezi Mungu kwa fadhili zake mahsusi juu yangu kaniwazisha uthibitisho huo.

 

Allama: Bwana, uthibitisho gani?

 

Ma'mun: Ni haya maneno ya nabi Musa ambaye Mwenyezi Mungu ameyataja katika Qur’ani hivi; Waj-Aliy Wazi-ran (mpaka mwisho wa aya; sura 20, Aya 29-35). "Na unijalie waziri (msaidizi) katika jamaa zangu, ndugu yangu Haruun umfanye awe ndiye waziri kwangu) nitie nguvu kwa ndugu yangu huyu, na umshirikishe katika kazi (hii), ili tukutukuze sana na tukutaje kwa wingi. Hakika wewe unatuona." Vile vile mtume wetu  mtukufu (s.a.w) amesema kwamba; Ee, Ali wewe uko kwangu mwenye daraja na cheo kama alivyokuwa H. Haruun kwa Mtume Musa, kuwa wewe ni Waziri wangu na vile vile ndugu yangu, ambao kwa wewe nimepata nguvu, na kukufanya kuwa mshiriki katika kazi zangu, ili tumtukuze sana, na tufanye atajwe sana kote. Je, sasa yuko mtu mwenye uwezo wa kueleza au kufasiri hadithi hii kwa vingine hata yasije maneno (hadithi) ya Mtume ya kubatilika au kuwa isiofaa ya upuuzi.

 

Allama anasema hivyo hivyo majadiliano ya nguvu kwa muda mkubwa yakaendelea kwa urefu hata ikafika alasiri, hapo Qadhi Qudhat (Qadhi mkuu) Yahya bin Aktham akasema:[9]

 

Qadhi Yahya bin Aktham: Bwana, hakika leo kwa wenye kutaka haki (ukweli) na kheri umewafungulia na kuthibitisha Siraatul Mustaqeem (Njia iliyonyooka ya kweli) na bila shaka umedhihirisha haki kwa dalili zenye nguvu hata hataweza mtu yeyote kuzijibu.

 

Allama Is-haq anasema, "Alipokwisha kuyasikia Ma'mun maneno ya Qadhi Yahya, basi akaelekea kwetu na akasema hivi: “Je nyie mnasema nini? Sisi sote kwa pamoja tukasema, "Sisi vile vile tunawaafiki nyie bwana, na yote mliyoyasema ni ya haki na kweli."

 

Ma’mun: Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu isingekuwa Mtume (s.a.w) ametuamuru kukubali maneno ya watu na kuisadiki; basi kabisa kamwe nisingeyakubali maneno yenu haya (kwa sababu mpaka hivi sasa hamkubali moyoni kuwa H. Ali Khalifa (waziri) Bila Fasi wa Mtume (bila kuwa kati mtu mwingine) Kwani sasa mnafikiri mbele yangu tu).

 

Ee, Mola wangu mimi nimewanasihi na kufanya kutimiza wajibu wangu wa 'Amr Bil Maaruf’ kama inavyotakikana. Ewe Mola wangu, wajibu wa kudhihirisha na kufikisha haki na ukweli nimeshaufanya na mzigo huo nimeshautua, Ee Mola wangu, kwa ajili ya mapenzi ya H. Ali na ubashiri wake, unipe uwezo wa kukukaribia; na ninaifuata madhehebu hii.



[1] Ukitaka kujua zaidi vitazame vitabu vifuatavyo:

 

(a)     Musnad kitabu cha Imam Ahmad Hanbal, Juzuu ya kwanza Uk. 99,141, 209, 331, 373 na katia juzuu ya nne Uk. 368, 370, 371  na katika juzuu ya tano Uk. 26.

(b)     Sunan Ibn Majah. MIango 11 Uk. 12.

(c)     Sunan Tirmidhi kitabu cha 46 Mlango wa Ishrini (20).

(d)     Mustadrak kitabu cha Hakim Nishapoori, juzuu ya tatu, Uk. 136

(e)     Jalaalud-Deen Suyooti, katika Tareekhul Khulafaa Uk. 113.

(f)      Musnad Abi Daaud At-Tiyaalisi juzuu ya kwanza, Uk. 26, hadithi ya 188 na juzuu ya tatu Uk. 93, hadithi ya 678.

(g)     Tareekh Muroojudh-dhahab cha Masudy, juzuu ya kwanza. Uk 307.

(h)     Tareekh AbiI-Fida, juzuu ya kwanza, Uk. 116.

(i)       Kanzul Ummal, juzuu ya sita Uk. 156 hadithi ya 2610.

(j)      Al-Istiab cha Ibn Abdil Barr, Uk. 470 na 786.

 

Viko vitabu vingi vingine vya kuthibitisha hiyo lakini kwa muhi tumevitaja hivyo tu.

 

[2] Na kama iIivyoandikwa katika Habibussiyar kwamba H. Ali peke yake amewauwa makafiri 36. Na kama ukitaka kujua zaidi vitazame vitabu vifuatavyo:

 

(a)                 Tareekhul Kaamil kitabu cha lbn Atheer. Juzuu ya pili uk. 44 na 47.

(b)                 Tareekhul Khamees 32 kitabu cha Diyaar Bakri, juzuu ya kwanza Uk. 418, 426, 427.

(c)                 Mataalibus Suul ya Talha Ash Shafii na

(d)                 Mohamed Yusuf I – Kunji katika kitabu chake Kifaayatu-Taalib. Viko vitabu vingi vingine vya kuthibitisha hiyo lakini kwa muhtasari tumeviyaja hivyo tu.

(e)                 

[3] Ukitaka kujua zaidi vitazame vitabu vifuatavyo:

 

a.         Tareekhul Khamees juzuu ya kwanza, Uk. 427 na 429

a.         Tareekhul Kaamil, juzuu ya pili Uk. 47

b.         Saheeh Bukhari, juzuu ya kumi na sita Uk. 12.

 

Viko vitabu vingi vingine vya kuthibitisha hiyo lakini kwa muhtasari tumevitaja hivyo tu.

 

[4] Ukitaka kujua zaidi vitazame vitabu vifuatavyo:

 

(a)     Zamakshari katika tafseer yake KASH_SHAF juzuu ya pili uk. 511 na 512.

(b)     Waahidi katika kitabu cha “ASBABBUN NUZUUL”

(c)     Zaynul-fata fi tafseer Hal-Ata kitabu cha al-Hafidh Abu Muhamed al-Asimi.

(d)     Ibn Jareer Tabaree katika kitabu chake “Al-Kifayah”.

(e)     Thaalabi katika tafseer yake ya Al-Kashf wal-Bayaan.

(f)      Ishaaq al-Hamawiy katika kitabu chake “Farayidus-Simtain.”

 

Viko vitabu vingi vingine vya kuthibitisha hayo lakini kwa muhtasari tumevitaja hivyo tu.

 

[5] Ukitaka kujua zaidi vitazame vitabu vifuatavyo:­

 

(a)       SunanTirmidhi ya BwanaTirmidhi

(b)       Kitaabul Khasais cha Bwana Nasai, hadithi ya tisa.

(c)       Abu Jaffer Ibn Jariir Tabari ameandika kitabu kimoja kizima juu ya kisa hiki.

(d)       Muhammad Ibn Abdi Rabbih katika kitabu chake Al-Iqdul Fareed.

(e)       Kitabul Ilal cha Bwana Dar Qutni

(f)        Mustadrak cha Haakim, Juzuu ya Tatu uk. 130,131,132.

(g)       Jaamiul Usool ya Ibn Atheer Juzary

(h)       Usdul Ghaaba ya Bwana IbnuI Atheer Juzary.

(i)        Mishkaatul Masabeeh ya Al-Khateeb Attab Rizi, uk. 564.

(j)        Lisaanul Meezan ya Ibn Hajar Asqalani.

 

Viko vitabu vingi vingine vya kuthibitisha hiyo lakini kwa muhtasari tumeandika hivyo tu.

 

[6] Ukitaka kujua zaidi vitazame vitabu vifuatavyo:­

 

(a)                 Tareekhul Umam ya Ibn Jareer Tabari, juzuu ya tatu Uk. 128.

(b)                 Tareekhul Kaamil ya Ibn Atheer Juzary ,juzuu ya pili Uk. 100.

(c)                 Seeratun Nabi ya Ibnu Hishaam, juzuu ya nne, Uk. 72.

(d)                 Tareekh abul Fida, juzuu ya Kwanza, Uk. 146.

(e)                 Saheeh Bukhari, juzuu ya tatu, Uk. 45

(f)                  Kanzul Ummal, juzuu ya tano, Uk. 304 na 306, hadithi ya 5597, 5598, 5608.

(g)                 Musnad Imam Ahmad Hanbal, juzuu ya kwanza Uk. 207 na 453 na juzuu ya nne, Uk. 281,04.

(h)                 Seeratul Halbiya, juzuu ya tatu Uk. 125.

(i)                   Tareekhul Khamees ya Diyar Bakri, juzuu ya pili Uk. 89 na 11.

 

Vipo vitabu vingi vingine vya kuthibitisha hiyo lakini kwa muhtasari tumevitaja hivyo tu.

 

[7] Ukitaka kujua zaidi vitame vitabu vifuatavyo:­

 

(a)                 Tareekhul Khamees juzuu ya kwanza Uk. 367.

(b)                 Ibn Jaree Tabaree katika kitabu chake tareekhul umam, juzuu ya pili, Uk. 244.

(c)                 Ibn Hisham katika kitabu chake Seeratun Nabi, juzuu ya pili Uk. 94.

(d)                 Abul Fida katika Tareekh, juzuu ya kwanza Uk. 133.

(e)                 Ibn Atheer katika Tareekh, juzuu ya pili, Uk. 38

(f)                  Ibn Khalduun katika tareekh , juzuu ya pili, Uk. 15

(g)                 Al-Hakim katika Mustadrak juzuu ya tatu, Uk. 133

(h)                 Suyootee katika Durre Manthoor, juzuu ya tatu, Uk. 180.

(i)                   Imam Hanbal katika Musnad, juzuu ya kwanza, Uk 331 na 348.

 

Viko vitabu vingi vingine vya kuthibitisha hivyo lakini kwa muhtasari tumeandika hivyo tu.

 

[8] Ukitaka kujua zaidi vitazame vitabu vifuatavyo:­

 

(a)     Imam Hanbal katika Musnad, Juzuu ya nne, Uk. 372.

(b)     Ibn Katheer katika Tarehe yake al-Bidaya wa-Nihay, juzuu ya tano uk. 208/214, anaeleza kwamba Bwana Abul Maali Juwayni anahadithia kuwa, “Naliona kwa mfunga kitabu, kitabu kilichoandikwa hadithi ya Mtume na jina la kitabu hicho ni ‘kitabu cha ishirini na naen kuhusu hadithi hii ya man kuntu Mawla Fa Aliy-yun Mawla’ na tutaanza kitabu cha ishirini na tisa.”  

(c)     Ibn Jareer Tabari katika Tarehe yake.

(d)     Sibt ibn Jawzi katika tadhkira Khawasul-Umma, mlango wa pili Uk. 18

(e)     Sheikh Ahmad bin aI-Fadhil Bakatheer katika Waseelatul Maal.

(f)      Suyooty katika AZHAARUL MUTANAATHIRA, NA Durri Manthoor, juzuu ya pili, Uk. 293/294.

(g)     Hakim katika Mustadrak, juzuu ya tatu, Uk. 110/111.

(h)     Imam Ghazali katika Sirrul Alameen.

(i)       Imam Nasai katika Khasais Alawiya.

(j)      Muhamad bin Isa Tirmidhi katika kiabu chake cha Sunan.

 

Viko vitabu vingi vingine vya kuthibitisha hiya lakini kwa muhtasari tumeandika hivyo tu.

[9] Ukitaka kujua zaidi vitazame vitabu vifuatavyo:

(a)                 Seeratun Nabi ya Ibn Hisham.

(b)                 (b) Tabaqaat ibn Saad juzuu ya tatu, Uk 14.

(c)                 Musnad ibn Hanbal, juzuu ya kwanza, Uk. 170 hadi 331, juzuu ya tatu, Uk. 32 na 338, juzuu ya sita, Uk. 369 na 438.

(d)                 Saheeh Bukhari, Juzuu ya pili, Uk. 200 mlango wa sifi za Ali ibn Abi Talib.

(e)                 Saheeh Muslim, juzuu ya saba, Uk. 120

(f)                  Sunan lbn Maajah, Juzuu ya kwanza Uk. 55.

(g)                 Sunan Tirmidhi.

(h)                 Khasis ya Ahmad bin Shueb nasai.

(i)                   Tareekhul Umam ya Ibn Jareer Tabai, juzuu ya tatu Uk. 144

(j)                  Hakim katika Mustadrak, juzuu ya tatu, Uk. 109 na 133.

(k)                 Ibn Abdul Bir katika Isteeb, juzuu ya pili, Uk. 473.

(l)                   Ibnil Baghazili katika Kitabul Manaaquib.

 

Viko vitabu vingi vingine vya kuthibitisha hivyo lakini kwa muhtasari tumeandika hivyo tu.

 

The .HTML version of this book is taken from
www.al-islam.org and ebooked by www.ShiaLibrary.com and www.islamkutuphanesi.com . May Allah be pleased with all.